Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Siku Yangu ya Kujifungua Nitakuwa 'Live' Instagram Yangu- Maimatha

$
0
0
Siku Yangu ya Kujifungua Nitakuwa 'Live' Instagram Yangu- Maimatha
MTANGAZAJI maarufu wa televisheni Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’ ambaye hivi sasa ni mjamzito, amesema atapenda siku yake ya kujifungua ikifi ka, awe mubashara katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram.

Tofauti na alivyozoeleka kuwa ni mtu wa ‘viwanja’, siku hizi Mai haonekani tena akijichanganya kama zamani na badala yake amkuwa mtulivu nyumbani.

“Ni kweli, nina ujauzito na unanisumbua sana ndiyo maana sionekani siku hizi, siwezi kusema una umri gani ila ninapenda kujifi cha hivi hadi nitakapojifungua na ninapenda siku hiyo nikiwa ninajifungua, niwe live kwenye Instagram,” alisema Mai ambaye mtangazaji wa AzamTV

Watumiaji wa Twitter Kuongeza Idadi ya Maneno

$
0
0
Watumiaji wa Twitter Kuongeza Idadi ya Maneno
Mtandao wa kijamii wa Twitter umetangaza jaribio lake la kongeza idadi ya maneno ya ujumbe ambayo mtu anaweza kuandika kwenye mtandao huo kwa mara moja hadi kufikia 280 ambayo ni mara mbili ya kiwango cha idadi ya maneno yaliyopo kwa sasa.
Mtandao huu ambao umekuwa na idadi ya zaidi watumiaji milioni mia tatu,umekuwa ukikabiliwa na changamoto ya ukuaji na hivyo inatafuta namna mbalimbali za kukuza wigo wa watumiaji.
Kundi dogo la watumiaji wa mtandao huo watahusishwa katika jaribio hilo la kuongeza idadi ya maneno ya kuandika.
Kampuni hiyo imesema hiyo ni hatua ya kutatua moja ya changamoto ambayo imekuwa ikiwasumbua watumiaji wengi

Uhasama wa Kenyatta na Mhakama Wazidi Kupamba Moto

$
0
0
Uhasama wa Kenyatta na Mhakama Wazidi Kupamba Moto
Uchaguzi mpya wa urais Kenya ulioitishwa baada ya maamuzi ya Mahakama ya Juu sasa utafanywa Oktoba 26, siku tano kabla ya kipindi cha siku 60 kilichowekwa na mahakama hiyo.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC), Wafula Chebukati ametangaza uamuzi huo umechukuliwa ili kuhakikisha tume hiyo inajitayarisha vilivyo kutokana na hukumu kamili na Mahakama ya Katiba iliyotolewa Jumatano iliyopita.

Tume ya Uchaguzi imeibadilisha tarehe iliyoiweka awali, Oktoba 17, na imeiomba Serikali iipatie Sh12.2 za Kenya ili kuendesha uchaguzi huo baada ya matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8, ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa kuwa mshindi, kubatilishwa.

Katika uamuzi wake juu ya madai yaliowasilishwa na mgombea wa Muungano wa Nasa, Raila Odinga, Mahakama iligundua uchaguzi huo haukuwa huru na haki, pia ulikuwa kinyume na Katiba na sheria.

Rais Uhuru Kenyatta ameilaumu Mahakama hiyo kwa kutoa uamuzi uliomzuia kuapishwa kuwa rais kwa muhula wa pili na akatishia kwamba mamlaka ya majaji yatachunguzwa upya baada ya yeye kushinda uchaguzi wa marudio.

Jaji mmoja katika jopo la walioisikiliza kesi hiyo, aliulinganisha mwenendo mzima wa uchaguzi uliopita kuwa kama gari la daladala lisilojali sheria za barabarani.

Mahakama ilisema uchaguzi wa Agosti 8 ulikuwa haujahakikiwa, na kwamba IEBC ilishindwa, ilidharau na kukataa kuendesha uchaguzi mzuri na ulio wazi, kama ilivyotakiwa na Katiba.

Kwa hivyo kulikuwa hakuna njia nyingine isipokuwa kuyabatilisha matokeo. Moja kati ya mifano muhimu: kukosekana kuandikwa matokeo ndani ya fomu za karatasi kutoka karibu vituo 11,000 kati ya zaidi ya vituo vya uchaguzi 44,000 nchini kote, na kuingizwa kwa njia ya kielektroniki katika kompyuta ya Tume. Jambo hilo halijafanywa.

Zile fomu zilizotumwa, kwa mfano, hazijawa na mhuri rasmi, nyingine zilikuwa hazijatiwa saini sawa na nyingine hazijawa na nambari au alama rasmi, hivyo kuweko wasiwasi kama fomu hizo ni za halali.

Tume ya Uchaguzi, licha ya kuamriwa na Mahakama ya Katiba, ilikataa kuachia mfumo wake wa kielektroniki kuchunguzwa, kwa hivyo wengi wa majaji walilazimika kuukubali mtazamo wa upinzani kwamba mfumo wa kompyuta wa Tume ya IEBC uliingiliwa na kuchakachuliwa.

Japokuwa Mahakama ilisema haijaweza kupata ushahidi wa moja kwa moja ni maofisa gani wakuu wa IEBC waliochakachua na kusababisha dosari zilizotajwa, hata hivyo, upinzani umesisitiza kwamba hautaweza kushiriki katika uchaguzi ujao pindi watu wanaoshukiwa kuhusika na uchafuzi uliopita hawatawekwa kando katika kusimamia uchaguzi ujao.

Jambo hilo linapingwa na chama tawala cha Jubilee cha Rais Kenyatta, kikisema Tume ya Uchaguzi ni huru na isiingiliwe katika shughuli zake za kuteua watu gani wa kusimamia uchaguzi na taratibu zitakazofuatwa katika mchuano huo.

Itakumbukwa kwamba mwaka 2007 Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanywa Durban nchini Afrika Kusini ulipitisha itifaki ili iingizwe ndani ya Azimio la Hati ya Afrika ya Haki za Binadamu na ikatajwa kwamba ni muhimu kuhakikisha kuna utawala bora kupitia njia ya wananchi kushiriki.

Ilisisitizwa kwamba chaguzi ndio msingi wa Serikali yeyote inayowakilisha wananchi na ni ufunguo wa mwenendo wa kidemokrasi. Ilitajwa kwamba chaguzi lazima ziendeshwe kwa njia iliyo huru na ya haki, chini ya Katiba za kidemokrasi, chini ya mfumo wa kugawa madaraka baina ya mihimili mitatu ya utawala, Serikali, Bunge na Mahakama – hasa kuhakikisha uhuru wa Mahakama.

Itifaki hiyo ilisema lazima ihakikishwe kwamba chaguzi si tu lazima ziwe huru na za haki, lakini lazima zionekane dhahiri kuwa ni huru na za haki mbele ya walimwengu.

Kuweko tume huru siku hizi kunaonekana kuwa ni hatua muhimu ya kujenga tabia ya uhuru na kutopendelea upande wowote pamoja na kupata vilevile imani ya wapiga kura na ya vyama vya kisiasa vinavyoshiriki katika chaguzi zenyewe.

Swali ni kama IEBC itaweza kufanya uchaguzi safi, ikijulikana kwamba Mahakama ya Juu ya Kenya imesema haitasita kuchukua tena msimamo kama iliouchukua pindi makosa yaliyofanyika hapo kabla yatarejewa. Kikatiba, kwa vyovyote vile, tarehe ya mwisho ya kufanywa uchaguzi mpya ni Oktoba 30. Kama Tume ya Uchaguzi itaweza kumaliza matayarisho yote hadi siku ya uchaguzi Oktoba 26 ni suala la kusubiri. Lakini, endapo uchaguzi kwa namna yeyote vile hautaweza kufanywa hadi Oktoba 30, basi Kenya itaingia katika mzozo wa kikatiba.

Rais wa sasa atabakia madarakani hadi pale rais mpya atakapochaguliwa na kuapishwa. Lakini, kuna wataalamu wengine wanaohoji kwamba pindi siku 60 za rais wa sasa za kujishikiza zikimalizika na hakuna rais mpya aliyechaguliwa na kuapishwa, basi spika wa bunge atakamata wadhifa huo wa kuwa kaimu rais hadi pale rais mpya atakapochaguliwa na kuapishwa.

Na ikiwa spika hatakamata nafasi hiyo ya kujishikiza, basi atafuata Jaji Mkuu. Na hapo kitakuwako kiroja cha mambo kwani itakuwa ni zamu ya David Maraga, Jaji Mkuu aliyebatilisha kuchaguliwa kwa rais wa sasa kukamata nafasi hiyo.

Hiyo ndio maana Uhuru Kenyatta anadai kwamba uamuzi wa Mahakama Kuu ya Katiba wa Septemba Mosi yalikuwa mapinduzi yaliofanywa na Mahakama kuupindua uamuzi wa wananchi wa Agosti 8.

Jumanne iliyopita Jaji Maraga mbele ya waandishi wa habari alilaumu juu ya vitisho vinavyoelekezwa kwa Mahakama, tangu pale ulipotangazwa uamuzi wa kuyabatilisha matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8.

Vitisho hivyo vilianza pale Rais Kenyatta alipoiita “Mahakama ya Maraga na wakora wenzake.” na kutishia kuisafisha pale atakapochaguliwa tena kuwa rais.

Tamko hilo liliwachochea wafuasi wa Kenyatta kwenda barabarani na pia kuongeza sumu kupitia mitandao ya kijamii. Maraga alitaja vitisho dhidi ya wafanyakazi wa Mahakama na kusema kwamba mkuu wa polisi, Joseph Boinnet, hajawapa ulinzi wa kutosha.

Kwa mshangao aliongeza kusema: “Tuko tayari kulipia gharama ya juu kabisa ili kuilinda katiba ya nchi.”

Wakati wa joto hili la kisiasa, Kenyatta na Odinga inabidi wajiandae na kampeni ngumu ya uchaguzi, kuranda tena kila kona ya nchi kuomba kura.

Duru ijayo ya uchaguzi huenda ikawa chafu zaidi kuliko ile iliyopita, hofu ya kutokea machafuko bado ipo. Kinyume na uchaguzi wa Agosti, huu hautaingiza kugombea ubunge, useneta, ugavana, uwakilishi wa wanawake au kuwa mjumbe wa baraza la mkoa (County).

Hivyo vishindo huenda vikapungua, lakini kuna hatari kwamba nguvu zote na mori wote ukaelekezwa katika mabishano ya watu wawili, Kenyatta na Odinga.

Hali hiyo ina hatari zake, hasa uhasama wa kikabila, jambo ambalo si geni katika siasa za Kenya.

Bulembo Abadiri Gia Angani Aamua Kujiondoa Kwenya Uchaguzi

$
0
0
Bulembo Abadiri Gia Angani Aamua Kujiondoa Kwenya Uchaguzi
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Alhaji Abdallah Bulembo amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi hiyo kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Novemba mwaka huu.
 .
Bulembo alikuwa ni miongoni mwa makada 49 wa CCM waliochukua fomu za kuwania uenyekiti wa taifa akitaka kutetea nafasi yake, lakini sasa ameamua kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho.

Kwa kauli yake anasema; “Uamuzi huu nimeufikia baada ya kuona kwamba katika kinyang’anyiro hiki kwenye nafasi ya uenyekiti tulijitokeza wagombea 49. Sasa nina uhakika baada ya kujitoa mimi katika 48 waliobaki lazima atapatikana CCM ambaye viatu vyangu vitamtosha,”

Mwenyekiti huyo anayemaliza muda wake akasema kuwa ameamua kutogombea sio kwa shinikizo lolote kwa kuwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi ndani ya chama hakuna sehemu yoyote inayomzuia kuwania uongozi.

Akasema kuwa anafurahi kwamba anaiacha Jumuiya hiyo ikiwa bora kuliko alivyoikuta, akisema, kwamba sasa hadhi ya shule za jumuiya hiyo imepanda kitaaluma, na pia jumuiya imeweza kulipa asilimia 68 ya madeni aliyokuta ikidaiwa.

Hayo ndiyo yalikuwa maelezo ya Bulembo wakati akitangaza hatua yake ya kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho wiki iliyopita alipokutana na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari, jijini Dar es Salaam.

Ni kweli juhudi ambazo Bulembo amezifanya, ili kuhakikisha jumuiya hiyo inarudi kwenye hadhi kama ilivyokuwa zamani ni kubwa, hivyo mwenyekiti mpya atayechaguliwa ni vyema aendeleze pale Bulembo alipoishia.

Siyo siri kwamba amejitahidi kufanya mchakato wa kurejesha mali za jumuiya hiyo, ambazo zilikuwa zinamilikiwa na baadhi ya watu ikiwamo Shule ya Sekondari Kaole ya mjini Bagamoyo mkoani Pwani ingawa alikumbana na changamoto nyingi.

Mbali na hayo, baadhi ya shule zilishindwa kulipa mishahara ya watumishi kwa wakati muafaka hali iliyodhoofisha utendaji kazi katika jumuiya husika hadi ikafikia kuwapo uvumi wa kurudishwa shule hizo mikononi mwa serikali, lakini akawa ameziimarisha kufuatia baadhi kuendeshwa kama mali ya mtu binafsi.

Kwa maelezo zaidi ya Bulembo ni kwamba katika uongozi wake aliikuta akaunti ya jumuiya ikiwa haina kitu, lakini sasa ina fedha ambayo ataikabidhi baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa viongozi wa taifa.

Aidha, akasema kuwa chini ya uongozi wake amefanikiwa kupima viwanja 56,000 vya jumuiya ya wazazi na hivyo kuiweka katika mazingira mazuri zaidi ya kimaendeleo.

Lakini mbali na hayo, Jumuiya hiyo pia iliwahi kukunjua makucha na kuwatangazia mafisadi waliovamia viwanja vyake kuvisalimisha mara moja vinginevyo wangenyang'anywa kwa nguvu.

Kwamba kamwe mali zake haziwezi kuendelea kuwa `shamba la bibi.'

Kwa mtazamo wangu nikiuangalia uongozi wake ninaona kwamba hata kama hakufanikiwa kurejesha mali zote mikononi mwa jumuiya, lakini juhudi zake zilionekana.

Hizo ni pamoja na kukemea vitendo vyote vyenye lengo la kuivuruga jumuiya hiyo.

Hivyo wakati huu ambapo jumuiya inajiandaa kufanya uchaguzi ni vyema kiongozi ajaye aanzie pale Bulembo alipoishia, ili kuendeleza mapambano ya kukomboa mali za jumuiya, ambazo bado ziko mikononi mwa watu wachache.

Ninajua wapo makada wengi wa CCM waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ambao baadhi yao ni Dk. Edmund Mndolwa, Mtiti Butiku, Daud Manoti, James Ouma, Simon Rubugu, David Msuya, Vitus Lipagile, Japheti Kasiri, Maliki Maruru na Paul Chacha.

Wengine ni mwenyekiti wa zamani wa jumuiya hiyo, Abiud Maregesi, Burton Kihaka, Jafari Kunambi, George Busungu, James Albert, George Nangale, Malila Malila, Semmy Kiondo, Levina Lemomo, Dk. Walter Nko, John Lema na Israel Salufu.

Wapo pia Frey Msekeni, Ali Makwilo, Manfred Lioto, Swalehe Katala, Dk. Damas Kashegu, Richard Lugandu, Jacob Mzuri, Nicholas Haule, Deogratius Magongwe, Kanuth Ndagine, Geofrey Sanga, Fatma Kasenga, Adam Malima, Charles Maguye, Mohamed Mgoli na Abednego Range.

Kwa hali hiyo ni muhimu wanachama kuwapima na kuchagua kiongozi atakayeendeleza alikoishia Bulembo.

Novemba mwaka 2012, Jumuiya hii ya Wazazi ilifanya uchaguzi wa viongozi wake wa taifa na kumchagua Alhaji Bulembo kushika nafasi hiyo ambayo sasa ameona awaachie makada wengine wa CCM.

Nakumbuka katika uchaguzi Bulembo alipata kura 673 akifuatiwa na Martha Mlata aliyepata kura 107, huku John Barongo, ambaye kwa sasa ni marehemu akiwa amepata kura 51.

Baada ya ushindi huo wapo baadhi ya watu waliandika kwenye mitandao ya kijamii wakibeza uwezo wa Bulembo na kudai kuwa hana lolote na hawezi kuisaidia jumuiya hiyo wala CCM kupiga hatua.

Lakini sio siri kwamba amefanya makubwa hadi kufikia kuvalishwa vazi aina ya Mpuzu la heshima kwa kabila la Waha na kutawazwa kuwa kiongozi anayeheshimika, alipokuwa katika ziara ya kichama mkoani Kigoma.

Mwenyekiti huyo amefanya kazi kubwa ikiwamo kuimarisha jumuiya kama ambavyo alieleza alipozungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kujitoa kuwania nafasi hiyo na pia ameingiza wanachama wapya ndani ya CCM.

Juni 10 mwaka huu alihitimisha ziara yake ya kichama akiwa amefanikiwa kutembelea mikoa saba na jumla ya wilaya 47 za mikoa husika, ziara ambayo ilianza Mei 26 mwaka huu akiwa 'amezoa' wanachama wapya 376.

Jumuiya ya Wazazi ya CCM, ambayo awali ilikuwa ikijulikana kama Tanzania Parents Association (TAPA) ilianzishwa mwaka 1955 na sasa ina umri wa miaka 62 ikiwa imeongozwa na makada mbalimbali wa chama hicho.

Baadhi ya makada hao ni Idd Simba, Abiud Maregesi, Athman Mhina na Bulembo, ambaye sasa ametangaza kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi hiyo na kuwaachia wengine

Real Madrid Yaibuka na Ushindi Mnono wa Magoli 3-1 Dhidi ya Dortmund

$
0
0
 Real Madrid Yaibuka na Ushindi Mnono wa Magoli 3-1 Dhidi ya Dortmund
Usiku wa September 26 2017 michezo nane ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018 ilichezwa barani Ulaya, moja kati ya mchezo wa kuvutia ulikuwa ni mchezo kati ya Borussia Dortmund dhidi ya Real Madrid ya Hispania ambao walikuwa ugenini.

Real Madrid leo wakiwa ugenini wamefanikiwa kupata ushindi wa pili wa Champions League wa magoli 3-1 dhidi ya wenyeji wao Borussia Dortmund ya Ujerumani, magoli ya Real Madrid yalifungwa na Gareth Bale dakika ya 18 na Cristiano Ronaldo aliyefunga magoli mawili dakika ya 50 na dakika ya 79.

Kufunga magoli mawili kwa Ronaldo kunamfanya kuzifunga timu za Ujerumani kwa mara ya 25 akicheza dhidi yao kwa mechi 21, hata hivyo usiku huo umemfanya Ronaldo kufikisha jumla ya game 400 akiichezea Real Madrid akiwa kafunga jumla ya magoli 411, assist 111 na amefunga jumla ya hat-trick ya 42.


Wanawake Ruhsa Kuendesha Magari Saudia

$
0
0
Wanawake Ruhsa Kuendesha Magari Saudia
Mfalme Salman wa Saudi Arabia ametoa idhini ya wanawake kuendesha magari, hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa. Uamuzi huu umefikiwa kutokana na harakati za muda mrefu kwa makundi ya wanawake na haki za bindamu kushinikiza wanawake waruhusiwe kuendesha magari.
Kwa muda mrefu Saudi Arabia imekuwa nchi pekee Duniani kuwazuia wanawake kuendesha magari. Abdallah al-Mouallimi Mwakilishi wa umoja wa mataifa kutoka Saudia ametangaza habari hizi umoja wa huko umoja mataifa.
"Ndugu Mwenyekiti, Mabibi na mabwana. Najua mtapenda kujua jambo hili kwamba dakika chache zilizopita Mfalme amepitisha sharia inayowapa idhini,wanawake nchini Saudia kuendesha magari.Hii ni historia mpya leo kwa jamii ya Saudia,kwa wanaume na wanawake.Na kwa sasa tunaweza kusema kitu angalau.'' Abdallah al-Mouallimi.
Akizungumza na waandishi wa msemaji wa idara ya Marekani,Bi.Heather Nauert amelezea kupokea kwa furaha tangazo hilo.
"Tuna wanafuraha kusikia jambo hilo,kwamba wanawake wa Saudia sasa wanaruhusiwa kuendesha magari,kwa hapa Marekani tunafurahia jambo hilo,na kuona ni hatua kubwa na mwelekeo mzuri kwa taifa hilo'' Heather Nauert.
Mwanaharakati wa Saudi Arabia aliyewahi wekwa kizuizini kwa siku 73 kutokana na kupinga wanawake kuzuiwa kuendesha magari, ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter akisema 'Thank you God', yaani asante Mungu.
Sheria hii inaanza kufanya kazi mwezi june mwaka ujao, na kwa sasa wizara itatakiwa kuandaa ripoti maalumu kuhusiana na jambo hilo.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumanne

$
0
0

Pendeza na Kessy Products: Badili Muonekano Wako na Kuweka Mwili Wako Sawa Bila Madhara yoyote

$
0
0
PENDEZA NA KESSY PRODUCT: BADILI MUONEKANO WAKO NA KUWEKA MWILI WAKO SAW KWA PRODUCT ZA ASILI ZISIZO NA MADHARA YEYOTE WALA KEMIKALI, MATOKEO NI KWAARAKA


1) KUTOA MVI SUGU PIA ZA KUZALIWA NAZO _80,000/
2) KUREFUSH NYWELE  KUZIJAZA NA KUZUIAKUKATIKA 90,000/
3) TENGENEZA SHEPU YAKO KUWA NA UMBO ZURI (HIPS & BATKS)KUNADAWA AINA TATU (@)KUPAK (B) KUNYWA (C)VIDONGE_130,000/
  4)ONDOA NYAMA UZEMBE MIKONONI, KIUNONI KUPAK _90,000/
5)TOA  KITAMBI KABISA(@) KUPAK 10O,000/ (B)VIDONGE/SLIMING MAJAN 130,000/
6) PUNGUZA MWILI MZIMA KUANZIA KILO UNAZOITAJI WEWE
@) DAW YA MAJIN NA VIDONGE_130,000/
7)PUNGUZA MAZIWA NA YASIMAME KAMA MWANZO _80,000/
8) PIA UNA KUONGEZA MAZIWA SAIZI UNAYOHITAJI WEWE_80,000/
9)ONGEZA UNENE WA MWILI MZIMA_100,000/
10) ONDOA MICHIRIZI ILIYO SHINDIKANA_90,000/
11) TOA MAKOVU, CHUNUSI, WEUSI KWENY MAPAJA KIKWAPAN_90,000/
13) KUWA MWEUPE WAKUPENDEZA(@) VIDOGO(WHITE SOLUTION)_130,000/(B)MAFUTA YAKUPAK 100,000/
14)TOA NDEVU VINYWELEO MILINI _90,000/
15/ ONGEZA NGUVU ZA KIUME (@)JELI_80,000/(B)VIDONGE MAX MAN_ 100,000/
16) ENGEZA MAUMBIL YA KIUME
@) (HANDSOME UP) MASHINE _200,000/
@) JELI NA VIDONG VYA SHARK_120,000/
17) RUDISHA HAMU YA TENDO NA KUCHELEWA KUFIKA KILELE_90,000/
18) RUDISH(BIKRA) 100,000/
19)ONDOA MAFUTA USONI _90,000/
20) ONDOA MIKUNJO USON_70,000/
(21) ENGEZA  MGUU_80,000/

 TUNAPATIKAN DAR W SALAAM: NAKWA MIKOAN KOTE UTAPATA PIGA CM

(+255) 0719955528
0756259180
0785371237

@dr_kessy_product
Delivery  POPOTE ULIPO

Mbunge wa CCM Amuombea Maji Tundu Lissu Jimboni Kwake

$
0
0
Na Mathias Canal, Singida

Pamoja na Changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi katika Jimbo la Singida Mashariki Wilayani Ikungi Mkoani Singida lakini uhaba wa upatikanaji wa huduma ya maji ni kikwazo kikubwa kwa wananchi kwani wanatumia umbali na muda mrefu
kutafuta maji.

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu ametoa ombi hilo mbele ya Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe wakati akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Ikungi kwenye kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu.

Kingu alisema kuwa Jimbo lake lina changamoto ya maji ambayo kwa kiasi kikubwa serikali inaendeleza juhudi za kuzitatua, huku akisema kuwa katika Jimbo jirani la Singida Mashariki linaloongozwa na, Tundu Lissu hali ni mbaya zaidi katika upatikanaji wa miundombinu ya maji kwa wananchi wake.

Alisema kuwa hivi karibuni alipita katika jimbo hilo na kujionea adha inayowakumba wananchi jambo ambalo lilimfanya kujipanga kuwaombea maji wananchi hao katika kipindi cha Bunge lijalo.

Alisema kuwa wananchi hao wamebaki wakiwa utadhani hawana muwakilishi wa Jimbo kwa kipindi cha miaka 10 jambo ambalo linafanya kuteseka na huduma za utafutaji maji kwa kutumia muda mwingi na umbali mrefu.

Aidha, Mhe Kingu alisema kuwa pamoja na changamoto ya upatikanaji wa maji Katika Jimbo la Singida Mashariki lakini pia jimbo hilo linakumbwa na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu ambayo ni pamoja na uhaba wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, maabara, matundu ya vyoo na mabweni.

Hata hivyo alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kwa kuanzisha mkakati wa pamoja wa kuanzisha Mfuko wa Elimu Ikungi utakaowashirikisha wananchi pamoja na wadau wa elimu kuchukua hatua madhubuti ili kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto na hatimaye kuwafanya wanafunzi waweze kuongeza ufaulu.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe ameanza ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Singida ambapo atatembelea na kukagua Miradi ya Maji na vyanzo vya uboreshaji upatikanaji wa maji.

MWISHO

Vijana Wakimya Wanabahati Sana ya Kupendwa na Wasichana

$
0
0
Nimekuja kugundua wanawake hawapendi sana mwanaume mjuaji. Kuna watu wakimya sana hata akilewa yeye huwa anatabasamu tu, basi wewe utaongeeaaa, utapiga storiii na kujifanya kila kitu unajua lakini utashangaa mwisho wa siku aliyeenda kugegeda ni jamaa aliyekua hajachangia hata sentesi moja kwenye kiringe.

Na wala huwezi jua amemtongoza huyo msichana saa ngapi, nimejaribu hii kitu imenishinda aisee, yaani Safari zikishafika tatu tu, yaani naongea mpaka mishipa ya kichwa inanitoka.

Kwa kweli ukimya ni kipaji.

Kutana na Mtabibu wa Asili Allan Shariffu Musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH shariffu musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na shariffu musa Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 629793352 au watsap
+255 679119679

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE.

Martini Kadinda Amtaja Mpenzi Wke Kwa Mara ya Kwanza

$
0
0
Martini Kadinda Amtaja Mpenzi Wke Kwa Mara ya Kwanza
Mbunifu wa mavazi wa hapa bongo ambaye ameshawahi kujinyakulia tuzo mbali mbali kwa ubora wa kazi zake, kwa mara ya kwanza ameweka wazi mahusiano yake ya kimapenzi ambayo yalikuwa siri kwa kipindi kirefu.

Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Martin Kadinda amesema kwa sasa yuko kwenye mahusiano na binti mmoja ambaye ni mjasiriamali mkubwa na kuahidi wadau wake muda muafaka ukifika watarajie kumfahamu kwa sura.

Uhamiaji Yaagiza Kambi za Wakimbizi Zifungwe

$
0
0
Uhamiaji Yaagiza Kambi za Wakimbizi Zifungwe
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Anna Makakala amewasili wilayani Ngara na kuagiza kambi za wakimbizi za muda zifungwe kwa wanaotoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Amesema wageni watakaoingia wasiitwe wakimbizi bali watakuwa ni wahamiaji haramu.

Dk Makakala amesema leo Jumatano kuwa, Mkoa wa Kagera unapakana na Uganda, Rwanda na Burundi, hivyo wananchi wasioe raia wa kigeni kinyume cha utaratibu. Amesema ni lazima hati ya ukaazi ilipiwe

Kamishna Jenerali Makakala ameahidi kuongeza watumishi wa Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera.

Pia, ameiomba Serikali kutoa vifaa vya usafiri.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Michael Mntenjele alisema kuna watu 223 wanaoomba hifadhi kutoka Burundi na DRC ambao wanapokewa katika kambi ya Rumasi wilayani hapa.

Amesema changamoto iliyopo ni maeneo ya mipaka kuwa wazi na kutokuwepo askari wa kutosha kudhibiti raia wa kigeni ambao huingia kufanya kazi kwa Watanzania na baadhi hupata makazi na wengine kuolewa.

Pia, amesema vigingi vya mipaka vilivyowekwa tangu wakati wa ukoloni na vingine vya mwaka 2014 vinaingia kwenye mashamba ya wananchi.

Mkuu wa wilaya amesema walioolewa au kuoa wanakabiliwa na changamoto ya kukosa Dola 50 za Marekani za kulipia hati ya ufuasi.

Niki wa Pili Awatolea Uvivu Dogo Janja, Young Dee Awataka Washindane Kimuziki na Si Maisha Yao Binafsi

$
0
0
Niki wa Pili Awatolea Uvivu Dogo Janja, Young Dee Awataka Washindane Kimuziki na Si Maisha Yao Binafsi
Msanii kutoka kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili ameingilia kati ugomvi wa Dogo Janja na Young Dee na kusema kwamba wanapaswa kushindana kimuziki na siyo kushambuliana katika maisha yao binafsi kwani jambo hilo linaweza kuja kuwaletea madhara kwa baadae

Nikki wa Pili amesema hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kupita siku kadhaa tokea Dogo Janja kutoa kauli yake ya kukataa kufananishwa na Young Dee kwa madai ni 'mteja wa unga' jambo ambalo lilizua makelele mengi kwa mashabiki wa wasanii hao pamoja na meneja wake Young Dee.

"Mimi naona kuna tatizo hapo, kwa sababu wameanza kuhusisha maisha yao binafsi, kwa hiyo ningefurahi kuona wanashindana kimuziki zaidi. Maana unapokuwa maarufu ukiongea kitu ujue kinaishi kwa kipindi kirefu na hakiwezi kufutika kiurahisi, kwa hiyo ni vizuri kuchagua maneno ya kutumia", amesema Nikki wa Pili.

Mtazame hapa Nikki wa Pili akifunguka mengine zaidi kuhusu ugomvi baina ya Dongo Janja na Young Dee

Dudu Baya Amshukia Vikali Mwanaye Anayedaiwa Amekataa shule

$
0
0
Dudu Baya Amshukia Vikali Mwanaye Anayedaiwa Amekataa shule
Msanii mkongwe wa muziki Bongo, Dudu Baya amefunguka maneno mazito dhidi ya mwanaye Wille ambaye anadai amekataa shule.

 Dudu Baya amesema mtoto huyo amekataa shule na kuanza muziki kwa kificho na amekuwa akikutana na baadhi ya wasanii kama Dully Sykes Coco Beach na kuwaeleza dhamira yake ya kuanza muziki lakini hajawahi kumuambia suala hilo.

Dudu Baya ameendelea kusema Wille amekuwa hivyo baada ya kuamia kwa mama yake na kuonya kuwa aendelee na anayofanya ila yeye hawezi kumtafuta.

“Mungu mwenyewe alisema mtoto mwenye busara na hekima humfurahisha babaye lakini na toto jinga, shenzi na pumbavu ni mzigo kwa mama,” Dudu Baya

“Mara nyingi watoto wa namna hii, vibaka, wezi, chagudoa, mashoga wanakaaga sana na mama zao lakini baba yoyote mtoto wa namna hiyo hawezi kukaa naye, huwa wanaitimua ndio maana mtoto anaweza kuwa kibaka mwizi akapelekwa jela baba yake asiende kumuangali lakini mama yake akaenda,” ameongeza.

Dudu Baya amemaliza kwa kusema yeye hamtafuti Wille kwani ni kijana mkubwa mwenye umri wa kati ya miaka 16/17.

Msigwa Afunguka Namna Wakenya Wanavyoshangaa Hadhi za Wabunge wa Tanzania

$
0
0
Msigwa Afunguka Namna Wakenya Wanavyoshangaa Hadhi za Wabunge wa Tanzania
Tangu mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliposhambuliwa kwa risasi akiwa mjini Dodoma Septemba 7, kumekuwa na malumbano makali kati ya viongozi wa Chadema, Bunge na Serikali.

Mzozo ulianzia Hospitali ya Mkoa wa Dodoma wakati Lissu akipatiwa huduma ya kwanza. Serikali ilitaka apelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), lakini viongozi wa Chadema walitaka akatibiwe Nairobi, Kenya, jambo lililotekelezwa kwa kuchangishana fedha za kukodisha ndege na kugharamia matibabu.

Malumbano hayo yameendelea kuchukua sura mpya kila siku, huku kila upande ukivutia kwake, kunyoosheana vidole na kujitetea kwa kila namna.

Miongoni mwa viongozi wa Chadema aliyeshiriki kumsaidia Lissu tangu hospitalini hadi Nairobi ni Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa ambaye amerudi nchini hivi karibuni.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu, Msigwa anasimulia hatua kwa hatua kuhusu misukosuko ya tukio hilo na safari ya kwenda Nairobi ilivyokuwa. Endelea

Swali: Tumesikia mambo mengi kuhusu mkasa uliompata Tundu Lissu hivi karibuni. Kwa kuwa wewe ulikuwapo tangu Dodoma na sasa umetoka Nairobi, hebu tueleze hali ilikuwaje wakati huo na sasa ikoje?

Jibu: Nataka tu niwaambie Watanzania kwamba Tundu Lissu wetu aliumizwa sana katika jaribio la kuchukua uhai wake. Watu wasichukulie kama ni jambo dogo, ni jambo kubwa lililoharibu hata akili za watu tuliokuwa karibu naye.

Mimi ambaye nilikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwa naye, nikafika mahali nikaona risasi siiogopi tena kwa maumivu aliyokuwa nayo. Nisingependa kama Taifa tufikie huko, yaani tusiogope risasi.

Hali aliyokuwa nayo hata alipofika Nairobi, madaktari walishangaa kuona Lissu akiwa hai kwa sababu alipoteza damu nyingi sana. Lakini, niwashukuru sana madaktari wa Hospitali ya Dodoma kwa huduma waliyotoa kufanya Lissu tufike Nairobi.

Swali: Hali ilikuwaje baada ya kupata ndege na kuanza safari ya Dodoma.

Jibu: Kwenye ndege nako tulipata shida kidogo, kuna wakati kitanda kilifyatuka. Mimi nikawa nashikilia, Mwenyekiti kuna hewa ya Oxygen alikuwa anashikilia ambayo ilikuwa imetoboka, kwa hiyo muda mrefu mimi nimeshikilia kitanda, madaktari wale nao wameshikilia.

INATOKA UK 15

Height (kimo) ya ndege nayo ilikuwa ndogo na (Lissu) alikuwa apewe dawa za usingizi, inakuwa siyo rahisi, hewa na maji ilikuwa inashindwa kufika vizuri.

Kwa hiyo kisaikolojia unaathirika kwa kuona mateso aliyopata. Lakini, tulifika Nairobi vizuri wametupokea wakaanza kushughulika naye, mpaka mambo yakaenda vizuri. Lakini, niseme mwenzetu ameumizwa sana.

Leo (Jumatano) ndiyo nimeondoka Nairobi na nilipata nafasi ya kumuaga, anaendelea kupata operesheni za hapa na pale. Isingependeza kuingia kwa undani kwa ajili ya kulinda privacy (faragha) ya mgonjwa. Lissu anaendelea vizuri, yuko critical lakini stable, kiasi kwamba anaanza kupata vitu vya majimaji.

Swali: Awali Serikali ilishauri Lissu atibiwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kwa nini ninyi mling’ang’ania kwenda Nairobi?

Jibu: Tulipomwondoa hapa, hatukusema kuwa madaktari wetu hawawezi, sababu kubwa ni security (usalama). Hata hivyo, ni ukweli usiopingika kuwa hospitali ya Muhimbili haina tofauti na hospitali ya Jomo Kenyatta kule Kenya ambayo nayo ni ya Serikali, lakini hospitali tuliyompeleka siyo ya umma, ina gharama kubwa lakini ina huduma kubwa.

Huduma zinazidiana. Ukienda Afrika Kusini, ukienda Ulaya au Marekani, kuna utofauti. Kama tutalazimika kwenda nje baada ya kushauriana na madaktari, lazima tutumie ndege ua kubeba wagonjwa, haitakuwa chini ya Dola 250,000. Hiyo ni mikakati tunayofanya.

Pamoja na maombi, kilichosaidia pale ni kwamba wenzetu Nairobi wana vifaa vya kisasa ambavyo vinacheki maeneo mengi sana. Kwa hiyo utaona lile jopo la madaktari 10, wengine ni wa mifupa, wengine wa saikolojia, wengine wa ndani ya tumbo na maeneo mengine, wote wanakaa kumhudumia.

Sasa tulikuwa tunashangaa, tuna wataalamu wengi hapo Muhimbili, lakini hatuna vifaa vya kutosha na madaktari kimekuwa kilio chao kikubwa. Lissu yuko katika hali ya dharura, unasema tufuate utaratibu, kwamba aende Dar es Salaam, madaktari wakae kwanza.

Alipofika Nairobi, kila kitu kilisimama, tulikuta pameandaliwa vizuri kwenda hospitali. Maana yake si kwamba wanaanza tu kuunga mifupa. Wakafanya vizuri, sasa ndiyo wakasema wanampeleka kwenye chumba cha upasuaji.

Swali: Pengine huo ndiyo utaratibu wenu wa matibabu bungeni au Serikali, kwa nini msingeufuata?

Jibu: Kwa kweli huduma ya kwanza aliyoipata Dodoma ilikuwa nzuri sana. Sasa ndiyo useme tufuate utaratibu? Ni mawazo ambayo naweza kusema yalikuwa ya kijinga.

Nadhani ni maneno katika kitabu cha No longer at ease, mwandishi anasema kuku akienda porini akakamatwa na mbweha, akiwa kwenye kinywa cha mbweha, huanzi kumkemea kuku kwamba kwa nini ulikwenda porini, unamtoa kwanza kisha unamwambia usiwe unakwenda porini utaangamia.

Sasa Lissu yuko kwenye hatari ya kupoteza uhai, watu wanasema tufuate utaratibu? Hata Kenya wanatushangaa wabunge wa Tanzania, kwamba Watanzania tuna bima inayofanya kazi tu ndani, wanasema ninyi VIP wa aina gani?

Wanashangaa Wakenya. Wakati wa Anna Makinda tulikuwa na bima ya Jubilee, lakini sasa hii ni ya ndani. Tunafikiria bora tukate bima ya binafsi, kwa sababu hatuko salama.

Ukiangalia wenzetu Kenya, mbunge analindwa na Serikali, walinzi zaidi ya wanne ambao wako full armed (wenye silaha), lakini na nyumbani wako wawili, kwa sababu huyu ni mbunge anayeisimamia Serikali, anakosoa. Halafu mtu anakwambia uende Muhimbili.

Swali: Hivi karibuni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Serikali iko tayari kumtibu Lissu mahali popote duniani kama familia yake itaomba, kwa nini msiombe?

Jibu: Sisi hatuhitaji kuiomba Serikali, inawajibika kumtibu Mbunge. Bunge linawajibika kumtibu Mbunge, lakini kwa sababu Spika ametishwa, Bunge halifuati utaratibu. Hebu tufikirie, kosa la Lissu ni nini katika nchi tukiwa wakweli?

Tunasimama kwenye jukwaa, tukamate kipaza sauti, tunawaambia Serikali imekesea moja, mbili, tatu… tunawaambia bombardier (ndege ya Serikali) imekamatwa, wawekezaji wanaondoka, sisi tunaisaidia Serikali, sisi ni marafiki.

Serikali inapaswa iwalinde hawa watu wanaoisaidia Serikali.

Swali: Ile kauli yako kwa Spika Job Ndugai kuhusu nani aliyelipia ndege huoni kwamba ilikuwa mapema mno kuitoa?

Jibu: Ulikuwa ni wakati mwafaka kwa sababu niliona Spika analeta utani kwenye masuala ya msingi. Ni kweli yule bwana alisaidia sana wakati tunatafuta ndege, kwa sababu ile ndege iliyoletwa ilikuwa haiwezi na ilibidi tutafute ‘jet’.

Ni kweli yule bwana (Turki) alitusaidia lakini hakulipa. Sasa Spika anasema amelipa wakati hakulipa. Kama amelipa kwa nini watuletee sisi invoice? Nasema hivyo kwa sababu niko kwenye Tume ya Bunge.

Spika hana uwezo wa kuliendesha Bunge, ndiyo maana nimesema, akitaka anifukuze hata kesho. Kimsingi Tanzania hatuna Bunge huru. Kwa mimi ambaye nimetoka Kenya, ukiangalia jinsi wenzetu wanavyofanya kazi kwa uhuru, jinsi vyombo vya habari vinavyofanya kazi, utafikiri uko Ulaya, kweli.

Jana nimeona watu wameandamana mpaka mahakamani, japo walizidisha kugonga milango ya mahakama, lakini polisi waliwaacha. Kesho wataandamana Nasa yataisha. Watakuwa na Uhuru pale watamkosoa, mambo yanaendelea. Watu wamewekeza vizuri, kuna uchumi mzuri.

Sasa hapa, huko mitaani watu mnateta na hii hali msidhani kwamba kuna mtu atakuja kuwabadilishia hapa Tanzania, ni sisi wenyewe. Tuwe huru, Msigwa niwe na uwezo wa kukosolewa na kila mtu akosolewe.

Kwa hiyo kauli yangu ilikuja wakati mwafaka na nina maanisha, niko tayari kufukuzwa bungeni, kwa sababu Spika asidhani kwamba hatuwezi kuishi bila kuwa wabunge. Siyo kwamba uanasiasa wangu utakoma kwa sababu siko ndani ya Bunge.

Wala asidhani kwamba tutakosa hela, mimi kwa sasa nina miaka 52, hapo bungeni si nina miaka saba tu? Miaka yote hiyo nilikuwa naishije? Kwa hiyo haitatufanya tunyamaze.

Swali: Kwa nini mnaoikosoa Serikali halafu mnalalamika kwamba haiwajali katika suala hili?

Jibu: Wana hiari ya kuja, maana yake kupigwa risasi siyo jambo la mchezo, unakufa kabisa. Sisi ndiyo tunapigwa risasi. Sasa hizo ni hisia tu, wangekuja kumuona wakafukuzwa hiyo ingekuwa kweli.

Kweli mtu kama Lissu ni mtu wa Rais John Magufuli kutoa masikitiko yake kwenye Twitter?

Angekuwa Mbunge wa CCM wange tweet kama hivyo? Ni mtu wa ku-tweet masikitiko yake hivyo? Ni mtu ambaye mpaka leo hakuna hata mtu aliyekamatwa? Magari yametajwa yanaeleweka.

Pale anapokaa Lissu ni karibu na anapokaa Naibu Spika anayelindwa na askari wenye silaha, wanakaa viongozi, mawaziri.

Tuliwauliza waendesha bodaboda wakasema, pale mliofika mnapajua, walizuia njia ile ya Dodoma Klabu 84 na huku (kwenye tukio), walipomaliza mipango yao walifungua.

Swali: Kwa hiyo kuna watu mnawahisi?

Jibu: Sisi tunaihisi Serikali.

Swali: Lakini si mtu moja kwa moja?

Jibu: Nimesema, hivi wakitaka kujua kama mimi niko hapa, hawatajua? Kwa sababu wale watu waliokwenda pale walikuwa wanawasiliana na kuna mnara pale. Hiyo ni akili ya kitoto tu. Ukicheki mawasiliano lazima utawajua. Kilichomwokoa Lissu ni kwa sababu hakushuka kwenye gari.

Swali: Kuhusu dereva wa Lissu, mbona mmempeleka Nairobi wakati anatafutwa na polisi?

Jibu: Wao walisema amekimbia, ngoja niulize swali, polisi wamekuja hospitali saa mbili baada ya tukio. Mimi nilikuwa mbunge wa kwanza kufika hospitali, nilifungua kwa nguvu kwenye huduma ya kwanza, baadaye wakaja kina Mbowe (Freeman) na Selasini (Joseph), hata waandishi wa habari walichelewa.

Nilikuwa mtu wa pili kupata taarifa, nikaendesha gari mwenyewe mpaka kufika pale ndani. Shughuli zote zimekwisha, polisi wamekuja baada ya saa mbili.

Pili, hata kwenye tukio la Lissu kupigwa risasi, walikuja baadaye sana.

Mahakama: Jalada la Kesi ya Aveva, Kaburu Bado Lipo kwa DPP

$
0
0
Mahakama: Jalada la Kesi ya Aveva, Kaburu Bado Lipo kwa DPP
Jumatano September 27, 2017, Upande wa Mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi ya utakatishaji fedha na kughushi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ bado lipo kwa DPP.

Wakili wa Serikali, Vitalis Peter amemweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa lakini jalada la kesi bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Aidha, amedai kuwa DPP ataangalia kama ameridhishwa na kesi hiyo ama ala, ambapo watasubiri kama uchunguzi umekamilika.

Baada ya kuelezwa hayo, Wakili wa utetezi, Evidius Mtawala kwa sababu ya taratibu zinazoendelea ni za kiofisi wanatumai jalada litaharakishwa.

Kutokana na hatua hiyo Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi October 4, 2017.

Evans Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha Dola za kimarekani 300,000.

Meya Wa Ubungo Kuzungumza Shauri Lake la Vyeti Feki Dhidi ya Makonda Kesho

$
0
0
Meya Wa Ubungo Kuzungumza Shauri Lake la Vyeti Feki Dhidi ya Makonda Kesho
Meya wa Ubungo (Chadema), Boniface Jacob ameeleza kuwa kesho atafika katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma kuzungumzia shauri lake la vyeti dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano, Jacob amesema wiki iliyopita amepokea barua kutoka sekretarieti wakimtaarifu kwamba wiki hii ndiyo wanalifanyia kazi shauri lake.

“Wananitaka kwamba baadhi ya mambo niliyoyaongea wananitaka na mimi nipeleke vielelezo vya ufafanuzi lakini kimsingi ni mambo mapya, yaani kana kwamba mtuhumiwa wangu mambo ya vyeti amekiri, amekubali.”

Jacob amesema akitoka kwenye mahojiano hayo na Sekretarieti ya Maadili ataongea na vyombo vya habari juu ya shauri hilo kuhusu kugushi vyeti na malalamiko mengine manne.

Mbali na hilo amesema atazungumzia vishawishi na vitisho katika kulimaliza shauri hilo lisiendelee.

“Kutoridhika na mwenendo wa shauri hilo linavyofanywa kwa kuchelewa na usiri mkubwa sana.”

Ofisi Nyingine za Mawakili Zavunjwa na Kuporwa Vifaa

$
0
0
Ofisi Nyingine za Mawakili Zavunjwa na Kuporwa Vifaa
Wiki mbili baada ya ofisi za mawakili ya Prime Attorneys jijini Dar es Salaam kuvamiwa usiku wa manane na watu wasiojulikana, ofisi nyingine ya mawakili imefanyiwa uhalifu wa aina hiyo mjini hapa.

Katika uvamizi wa ofisi za mawakili za Prime Attoneys ambao pia wanamteta mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji, wezi waliiba sefu ya fedha na nyaraka baada ya kumfunga kamba mlinzi.

Mmoja wa mawakili wa kampuni hiyo, Hudson Ndusyepo alisema katika uvamizi wa ofisi hizo zilizopo kwenye jengo la Prime House, Mtaa wa Tambaza, Upanga nyaraka za mfanyabiashara huyo hazikuibwa.

Wakati uvamizi wa ofisi hizo ukiacha utata, watu wasiojulikana walivunja na kuiba mali mbalimbali katika ofisi mbili za mawakili jijini Arusha tukio ambalo limeibua hali ya hofu na sintofahamu kwa baadhi ya mawakili.

Ofisi zilizovamiwa ni za Ideal Chambers iliyopo jengo la Blue Rock na Equality Attorneys yenye maskani yake katika jengo la Said Kondo zote zikiwa katikati ya jiji.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo alithibitisha kwa kifupi kuvamiwa kwa ofisi hizo akisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa matukio hayo.

Wakili Edmund Mgemela wa kampuni ya Equality Attornerys alielezea kuwa tukio hilo lilitokea mwezi uliopita ambapo mara baada ya kuwasili asubuhi alikuta mlango wa ofisi ukiwa wazi na umevunjwa.

Mgemela alisema baada ya kuingia ndani alikuta baadhi ya nyaya za kompyuta ofisini zimenyofolewa, baadhi ya nyaraka zimechukuliwa sanjari na suti ambazo huzihifadhi ofisini kwake pia hazikuzikuta.

Hatahivyo, alisema kwamba aliripoti tukio hilo polisi na kupewa RB namba 790/2017 akiamini wahusika walikuwa na nia ovu kwa kuwa ndani ya jengo analofanyia shughuli zake kuna ofisi mbalimbali ambazo hazikuguswa siku ya tukio. “Mpaka sasa sielewi kama ni visasi au la, lakini ninachoweza kusema ni kwamba hawa watu walikuwa na nia ovu haiwezekani ndani ya jengo hili kuna ofisi nyingi wazipite zote kuanzia ghorofa ya kwanza mpaka wafike ya tatu kwangu na kuvunja,” alisema Mgemela.

Wakili kutoka Ideal Chambers, Robert Akileti alisema uvamizi katika ofisi yao ulifanywa Agosti 10 ambapo watu hao walivunja mchana alipokuwa ameenda kupata mlo.

Akileti alisema kuwa aliporejea ofisini kuendelea na shughuli zake alikuta mlango wa ofisi umevunjwa na kompyuta tatu mpakato (laptop)zimeibiwa kitendo ambacho kiliwapa hofu na mpaka sasa hawaelewi watu hao walikuwa na nia gani.

Uzushi Ambao Umesambaa Kuhusu Wanawake wa Zanzibar na Ubikira Wao

$
0
0
Uzushi Ambao Umesambaa Kuhusu Wanawake wa Zanzibar na Ubikira Wao
Nimegundua kuna uzushi ambao umesambaa sana hasa huku Tanzania bara juu ya wanawake wa Zanzibar, hivyo mimi nimeamua kuja kuweka ukweli wote hapa.

Kuna mada ilipostiwa juzi hapa JF, kuhusu mikoa ya Tz na wanawake bikra waliopo katika mikoa hiyo ambao wamefikisha umri wa miaka 25. katika ile list wanawake wa Zanzibar waliongoza ( pemba 45%, na unguja 43%) huku wa Dar es salaam wakishika mkia kwa 3%.

Sasa baada ya kupitia comments za watu, nikaona kuwa wengi wanasema kuwa wanwake wa Zanzibar wapo bikra kwa sababu wanafanya mapenzi kinyume na maumbile kabla ya ndoa.

Hii dhana siyo ya kweli kabisa, ni uzushi tu uliosambaa kwa kasi ya 4G. halafu nimegundua kuwa wengi wanao sambaza uzushi huu hata zenji hawajawahi kufika.

Nakubali kuwa jamii yoyote lazima watakuwepo "wahuni", hivyo sikatai kuwa baadhi yao kuwa wanafanya hivyo vitendo. ila ni wachache sana ( less than 0.01% ) kitu ambacho si haki kuki generalize kwa population nzima.

Hivyo basi msiwachafue wanawake wa Zanzibar kwa vitu ambavyo sio vya kweli.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images