Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Mahakama Imewahukumu Kwenda Jela Miaka Mitatu Waliokuwa Maofisa wa TAN-TRADE

$
0
0
Mahakama Imewahukumu Kwenda Jela Miaka Mitatu Waliokuwa Maofisa wa TANTRADE
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh5 milioni kwa kila kosa waliokuwa Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Samweli Mvingira na Naibu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala,  Judith Msuya baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia Serikali hasara.

Hata hivyo, mshtakiwa Judith Msuya ambaye alikuwa ni Naibu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Mamlaka hiyo (Tan Trade) amelipa faini hiyo na kuepuka kifungo cha miaka mitatu jela.
Washtakiwa kwa pamoja wametiwa hatiani katika mashtaka manne kati ya matano walioshtakiwa nayo mahakamani hapo  likiwemo la kutumia madaraka yao vibaya kwa kuagiza gari lililotumika kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma iliyosababisha AL Hamadi Motors FZD kupata faida ya Sh34. 89 milioni.

Katika kesi hiyo, washtakiwa walikuwa watatu akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tan Trade ambaye alifariki dunia wakati shahidi wa kwanza alipotoa ushahidi wake.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema ameridhishwa na mashahidi wa upande wa Jamhuri ambao wameweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.
“Nimewatia hatiani washtakiwa  hawa kwa makosa manne ya kutumia madaraka vibaya, hivyo kosa la kwanza hadi la nne mtalipa faini ya Sh 5milioni kwa kila kosa au kwenda jela miaka mitatu kwa kila kosa na shtaka la tano nawaachia huru kwa sababu Jamhuri imeshindwa kuthibitisha shtaka hili,” amesema Hakimu Mkeha.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wanadaiwa kuwa kati ya Septemba 2007 na Julai 2008, Makao Makuu ya TanTrade wilaya ya Temeke walitumia madaraka yao vibaya kwa kuagiza gari lililotumika kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma iliyosababisha AL Hamadi Motors FZD kupata faida ya Sh34.89 milioni.

Katika shtaka la pili, tarehe hiyo na mahali hapo, washtakiwa kwa kutumia madaraka yao vibaya, walinunua gari iliyotumika kwa lengo la kumnufaisha Humer Stars kiasi cha Sh32.77 milioni.
Katika shtaka la tatu, washtakiwa wanadaiwa bila kufuata utaratibu wa kushindanisha zabuni waliagiza gari iliyotumika na kusababisha AL Hamad kupata faida ya Sh34.89 milioni huku shtaka la nne watuhumiwa walinunua gari bila kufuata utaratibu wa zabuni.
Shtaka la tano, ambalo washtakiwa waliachiwa huru baada ya Jamhuri kushindwa kuthibitisha shtaka, washtakiwa walidaiwa kutumia madaraka yao vibaya, uzembe na kumsababishia mwajiri wao hasara ya Sh49.145 milioni.

Afariki Kwa Mganga wa Kienyeji Wakati Akiongezwa Nguvu za Kiume

$
0
0
Afariki Kwa Mganga wa Kienyeji Wakati Akiongezwa Nguvu za Kiume
MWANAUME anayefahamika kwa jina la Joseph Sahni (60), mkazi wa Kijiji cha Nzonza Kata ya Salawe Shinyanga Vijijini, amefariki dunia akiwa nyumbani kwa mganga wa kienyeji wakati akipatiwa matibabu ya nguvu za kiume.

Alikutwa na mauti baada ya kuwekewa dawa aina ya unga kwenye tundu la sehemu zake za siri, kisha kusukumiziwa kwa kupampiwa na pampu ya baiskeli, hivyo kupoteza maisha.

Tukio hilo lilitokea Jumapili saa 10:00 jioni, ambapo Sahni baada ya kupatiwa matibabu hayo, alianza kutokwa damu nyingi sehemu zake za siri kisha kuishiwa nguvu na kupoteza maisha.

Akizungumzia tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Simon Haule, alisema Jeshi lake linamshikilia mtuhumiwa mganga huyo wa kienyeji, Robert Mkoma, kwa tuhuma za mauaji, na baadaye atafikishwa mahakamani baada ya taratibu kukamilika.

“Natoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuacha tabia ya kuendekeza kukimbilia kwa waganga wa kienyeji kutafuta tiba, waende kwenye vituo vya afya au hospitali kufanyiwa uangalizi na kupewa matibabu sahihi,” alisema Kamanda Haule.

Katika tukio lingine, Jeshi hilo linamsaka Masesa Sesaguli, mkazi wa Kijiji cha Mwakolongwa Tarafa ya Itwangi Shinyanga Vijijini, kwa tuhuma za kumuua binti yake, Nshoma Masesa (16), aliyekuwa akisoma kidato cha pili Buhongwa jijini Mwanza, baada ya kuacha masomo na kwenda kuolewa wilayani Kahama.

Kamanda Haule alisema baada ya binti huyo kutafutwa na kurejeshwa nyumbani kwao, ndipo baba yake alianza kumpiga kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili hadi kuishiwa nguvu na kupoteza maisha.

Kamanda Haule alisema baada ya mauaji hayo, mwanaume huyo alitorokea kusikojulikana.

Kamanda Haule aliwaasa wanafunzi wa kike kujikita zaidi kupenda masomo, ili kutimiza malengo yao, na kuacha tabia ya kujiingiza kwenye masuala ya mapenzi katika umri mdogo, ambayo yamekuwa yakiwaharibia mwelekeo wa maisha yao.

Kampuni Tatu za Nje Ikiwemo Acacia Chanzo cha Kushuka Mauzo DSE

$
0
0
Kampuni Tatu za Nje Ikiwemo Acacia Zimechangia Kushuka Mauzo DSE
 Kampuni tatu za nje zimechangia kushuka kwa mauzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa Sh50 bilioni.

Taarifa ya DSE inazitaja kampuni ambazo hisa zake zimeongoza kushuka kuwa ni Uchumi Supermarket (USL) kwa asilimia 22, Shirika la Ndege la Kenya (KA) asilimia 16 na Acacia kwa asilimia tisa.

Mauzo ya soko hilo kwa kipindi cha wiki moja yameshuka kutoka Sh53 bilioni mpaka Sh3 bilioni baada ya hisa 800,000 za kampuni za ndani kuuzwa kati ya Septemba 25 hadi Septemba 29.

Wiki iliyoishia Septemba 22, jumla ya mauzo ilikuwa Sh53 bilioni, lakini wiki iliyoishia Septemba 29 yalikuwa Sh3 bilioni.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, USL ilianza wiki ikiuza hisa kwa Sh90 lakini ikamaliza kwa Sh70 wakati KA ilianza na Sh120 na ikahitimisha kwa Sh100. Hisa za Acacia ambayo inaendelea na mazungumzo na Serikali baada ya kuzuiwa kusafirisha mchanga wa madini zilikuwa zinauzwa Sh5,480 mwanzo mwa wiki hiyo lakini zilishuka mpaka Sh4,980.

Bei ya hisa za Acacia zimepungua kutoka Sh12,500 kabla ya zuio hilo, Machi mwaka huu. Wakati suala la mchanga likiitesa Acacia, maduka ya Uchumi yanakabiliwa na madeni ya bidhaa inazoletewa kiasi cha Serikali ya Kenya inakotoka kuahidi kuisaidia kuyalipa.

Ofisa Masoko Mwandamizi wa DSE, Mary Kinabo alisema kupungua kwa hisa zilizouzwa kutoka milioni nne hadi 800,000 kumechangia kuporomoka kwa mapato hayo.

Hata ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa sokoni hapo umepungua kwa Sh115 bilioni. “Wiki iliyoishia Septemba 23 ulikuwa Sh20.5 trilioni lakini Septemba 29 ulikuwa Sh20.3 trilioni,” alisema Kinabo.

Hata hivyo, ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umeongezeka kwa Sh71 milioni kutoka Sh9.6 trilioni hadi Sh9.7 trilioni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa za Kampuni ya Sigara (TCC) iliongoza kwa kwa asilimia 66 ikifuatiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa asilimia 27 na Benki ya CRDB asilimia mbili.

   

Pcha:Yaliyojiri Usiku wa Private Party ya Diamond

$
0
0
Pcha:Yaliyojiri Usiku wa Private Party ya Diamond
Usiku wa kumkia leo ndiyo kilele cha kuhitimisha siku nne za kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa C.E.O wa WCB, Diamond Platnumz ambapo private party  imefanyika katika hotel ya Hyatt Rency na kuhudhuriwa na mastaa kadhaa pamoja na watu wake wa karibu.



Kabla ya sherehe hiyo Diamond ametoa msaada wenye thamani ya shilingi  milioni nne katika hospitali ya Amani iliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo ndiyo alizaliwa miaka kadhaa iliyopita.
Manager wa Diamond(kulia) Sallam akifurahia jambo na Diamond kwenye birthday dinner party
Diamond akiwa na mlinzi wake
Diamond akiwa na wageni waalikwa






Hamisa Mobetto Achukizwa na Ujumbe wa Idriss ,Auchukulia Kama Kejeli /Dharau.... Ujumbe Huo Umesomeka hivi

$
0
0

Hamisa Mobetto Achukizwa na Ujumbe wa Idriss ,auchukulia Kama kejeli /dharau.... Ujumbe Huo Umesomeka hivi :
.
By Idriss Sultan - Dear Diamond nimekaa nikawaza sanaaaaa ila nimemaliza na jibu nimepata, kama kaka au mshkaji wako nimeona kuna vituo vingi sana vya watoto wasio na uwezo wa kujisomesha na hata chakula hakitoshi, nimeona kuna vijana wengi hawana ajira, nimeona kuna wengi hawajui wataamkaje kesho. Kwa sasa wewe unaweza kuwasaidia sanaaaa. Utakua unajiuliza hii 500 ya nini ila nimegundua nikikupa hii 500 ntakua nimeokoa maisha ya watu wengi sana. HII 500 NUNUA CONDOM ILI HIZO ELF 70 TUWE TUNATOA MISAADA NA RAV 4 ZITAPELEKA MCHELE ORPHANAGE.

Rais Museveni Atimiza Ahadi Utafiti Mafuta Tanzania...

$
0
0
RAIS Yoweri Museveni wa Uganda ametekeleza ahadi aliyoiweka Agosti 5, mwaka huu kwa Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi bandari ya Chongoleani, jijini Tanga, Tanzania

Wakati wa uzinduzi huo, Rais Magufuli alimuomba Rais Museveni wataalamu waliogundua mafuta katika Ziwa Abert nchini Uganda kushirikiana na wataalamu wa Tanzania katika utafiti wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na Eyasi nchini. “Rais Museveni wa Uganda alitumia wataalamu wake ambao aliwapeleka kusoma na kisha kufanya utafiti huo na hatimaye kugundua mafuta.

Kwa maana hiyo, Tanzania tutawatumia hawa watalaamu wa Uganda katika kufanya utafiti wa mafuta Ziwa Tanganyika na Eyasi,” alisema Rais Magufuli siku hiyo. Takwimu za awali zinaonesha kwamba maeneo hayo yana kiwango kikubwa cha mafuta. Katika mkutano huo, Rais Museveni wakati akizungumza alionesha nia ya kuileta timu hiyo Tanzania huku naye akitaka gesi asili kufikishwa Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, timu hiyo ya wataalamu ambayo ilifika nchini jana na kufanya mazungumzo wizarani hapo, sasa inaelekea Ziwa Eyasi kwa siku mbili kabla ya kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo zaidi. Kufika kwa timu hiyo ya watu sita ikiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Uganda, Robert Kasande kunaamsha upya mchakato wa kutafuta mafuta katika Ziwa Tanganyika na Eyasi, ambako tayari kuna utafiti kadhaa zimeshafanywa kuanzia miaka ya 1950.

“Tumefika hapa na tupo tayari kubadilishana uzoefu ambapo utalenga katika kuangalia tafiti zilizowahi kufanyika nyuma, kutembelea maeneo husika na kuweka mikakati ya namna bora ya kufanya utafiti kwa ubora wa hali ya juu kwa kushirikiana na Tanzania,” alisema Kasande. Katika kikao hicho cha utambulisho kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani, walikuwepo pia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Pallangyo na wataalamu kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).

Rais Magufuli amekuwa katika harakati za kutaka kuhakikisha kuwa rasilimali ya mafuta inagunduliwa na kuanza kuleta manufaa kwa wananchi. Dk Kalemani akizungumza katika kikao hicho, alisema; “Sisi kama Tanzania tupo tayari kubadilishana uzoefu na wataalamu wa Uganda kwenye utafiti wa mafuta na kuanza kazi mara moja; hata hivyo pia tupo tayari kubadilishana nao uzoefu kwenye masuala ya gesi kwa kuwa tuna utaalamu huo, lengo likiwa ni kuimarisha sekta hizi za mafuta na gesi kwa nchi zote mbili.”

Ameongeza kwa kuwa Tanzania ina uzoefu mkubwa kwenye utafiti wa gesi asilia, wapo tayari kutuma wataalamu nchini Uganda kushirikiana kwenye utafiti wa gesi nchini Uganda. ZIWA EYASI Hili ni ziwa la magadi ambalo mito yake huishia katika ziwa hilo. Kijiografia ziwa hilo lipo kwenye ukanda wa Bonde la Ufa upande wa mashariki chini ya beseni la Serengeti, Kusini mwa Hifadhi ya Serengeti na kusini magharibi mwa Kreta ya Ngorongoro.

Mito mikubwa inayoingia maji katika ziwa hili ni mto Sibiti na Mto Baray. Maeneo haya ni nyumbani kwa makabila ya Datooga na Hadzabe na eneo maarufu la korongo. Ziwa hili lipo magharibi mwa Ziwa Manyara kiasi cha kilometa 155 magharibi mwa Arusha likiwa na ukubwa wa maili za mraba 400 sawa na kilometa za mraba 1,050. Katika historia takribani miaka mitatu iliyopita, Tanzania ilifanya mazungumzo na kampuni za Total na BP ya kutafuta mafuta katika ziwa hilo.

Kampuni nyingine zinazotafuta mafuta nchini kutoka Norway ni Statoil, Kampuni ya Brazil ya Petrobras, Kampuni ya Uholanzi ya Shell, BG Group na Exxon Mobil. Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, Profesa Sospeter Muhongo alisema Total wameonesha nia ya kutafuta mafuta katika Ziwa Eyasi na hivyo kuongeza ushindani. Mei 2015, kampuni ya China ya usakaji mafuta ya CNOOC Ltd na kampuni ya gesi ya Urusi ya Gazprom pia ziliwasilisha zabuni za vitalu vinne kati ya nane vilivyopo.

UTAFITI WA ANGA Aidha, Novemba 2015 dalili za kuwapo kwa mafuta zilikuwa dhahiri kwa Mkoa wa Arusha baada ya TPDC kufanya utafiti wa anga katika maeneo ya Ziwa Eyasi na Natron. Utafiti huo umeshafanyika mara mbili ambapo mara ya pili ulifanyika katika eneo la Eyasi Wembere na Mandawa eneo ambalo wataalamu wa Uganda watakwenda kulichungulia. Utafiti huo ulikamilika katikati ya Januari 2016 kwa gharama ya Sh bilioni 14 zikiwa ni fedha za Serikali ya Tanzania.

Kupatikana kwa mafuta nchini Kenya na Uganda katika ukanda wa Bonde la Ufa, unafanya kuwepo na imani kubwa kwamba Ziwa Eyasi litakuwa na nafasi ya kuwa na mafuta pia. Upimaji wa eneo hilo kwa kutumia ndege maalumu ulifanyika katika umbali wa kilomita 23,000. Utafiti huo ulifanywa huku ndege hiyo ikiwa katika umbali wa meta 80 hadi 100 kutoka usawa wa bahari katika spidi ya kilometa 220 kwa saa.

ZIWA TANGANYIKA Katika Ziwa Tanganyika, Kampuni ya Beach Energy ilishasema kwamba ziwa hilo lina uwezekano mkubwa wa kuwa na mafuta. Hata hivyo, eneo ambalo lilionekana dhahiri ni eneo la nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Hata hivyo, Beach Energy wamesema kwamba upo uwezekano mkubwa wa ziwa hilo kuwa na mafuta kiasi cha mapipa kadri ya milioni 200.

Taarifa hizi za kuwepo kwa mafuta ni za zamani hata kabla ya mafuta ya Ziwa Albert kuonekana katika miaka ya 2000 hivyo inakuwa ni kitu kipya kuanza kuthibitisha uwapo wa mafuta katika maeneo hayo. Mwaka 2008, DRC na Tanzania ilitiliana saini mkataba wa kufanya uchunguzi kwa pamoja, lakini kwa mujibu wa taarifa katika mitandao, mkataba huo haukutekelezwa. Maeneo ya DRC uwepo wa mafuta unaonekana kutokana na mafuta hayo kujitokeza wazi.

Ester Bulaya Afunguka Kilichojiri Akiwa Mahabusu Mpaka Kupoza Fhamu na Kulazwa

$
0
0
Ester Bulaya Afunguka Kilichojiri Akiwa Mahabusu Mpaka Kupoza Fhamu na Kulazwa
Mbunge wa Bunda mjini kupitia CHADEMA, Ester Amos Bulaya, kwa mara ya kwanza ameelezea kile kilichojiri akiwa mahabusu mpaka kupelekea kupoteza fahamu na kulazwa.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Ester Bulaya amesema sababu ya kukamatwa kwake ilikuwa kwa kosa la kwenda kutoa misaada kwenye shule iliyopo kwenye jimbo la mbunge mwenzake wa CHADEMA John Heche.

Ester Bulaya ameendelea kusimulia kwamba baada ya kumkamata akawaambia kwamba ana tatizo la pumu, hivyo wasimuweke kwenye mazingira ambayo yanaweza yakamletea matatizo kiafya, lakini wakamuingiza mahabusu bila kujali afya yake, na baada ya muda hali ikaanza kubadilika, na ndipo mahabusu wenzake aliokuwa nao ndani wakaanza kupiga kelele wakiwa ndani ili polisi waje wasaidie.

Chuo Kikuu cha Nairobi Chafungwa Kwa Muda Usijulikana

$
0
0
Chuo Kikuu cha Nairobi Chafungwa Kwa Muda Usijulikana
Chuo Kikuu cha Nairobi kimefungwa kwa muda usiojulikana.

Wanafunzi chuoni hapo waliamriwa ifikapo saa tatu asubuhi leo Jumanne wawe wameondoka chuoni hapo.

Uamuzi huo umefikiwa na Seneti ya chuo kutokana na suala la kiusalama.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Umma wa chuo hicho, John Orindi amesema, "Tutatangaza ni lini chuo kitafunguliwa.”

Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na maandamano yaliyofanyika wiki iliyopita ambayo yalisababisha wanafunzi 27 kujeruhiwa.


Nissan Yazindua Kiti cha Gari Chenye Uwezo wa Kutambua Jasho la Binadamu

$
0
0
Nissan Yazindua Kiti cha Gari Chenye Uwezo wa Kutambua Jasho la Binadamu
Nissan imeuzindua kiti cha gari chenye uwezo wa katambua jasho la binadamu ambacho kampuni hiyo inasema kuwa kitasaidia kupunguza ajali za barabarani.
Teknolojia hiyo inayojulikana kama Soak, hubadlisha rangi ikiwa itatambua kuwa dereva atakuwa ameishiwa maji mwilini.
Utafiti wa walia uliofanywa na taasisi za European Hydration Institute na Loughborough University uligundua kuwa madereva wanaoishiwa na maji mwilini huwa na makosa mengi sawa na madereva walevi.
Nissan yaunda magari mapya yanayotumia umeme
China katika mipango ya kupiga marufuku magari yanayotumia mafuta
Ngozi hiyo ya kiti iliyoundwa na kampuni moja nchini Uholanzi pia itawekwa kwenye usukani wa gari na viti vya mbele vya gari .
"Hii ni sehemu ya mpango mzima ambao sio tu wa kufuatilia tu gari bali pia dereva." alisema Prof Peter Wells.

Lema Aiweka Mtegoni TAKUKURU

$
0
0
Lema Aiweka Mtegoni TAKUKURU
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amesema kwamba jambo la kupeleka  ushahidi Takukuru tatizo siyo rushwa kutumika bali ni mambo mengine makubwa yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali ikiwepo kuchoma shule kwa ajili ya kujipatia madaraka.

Akifanya mahojiano na EATV, Lema amesema kwamba kupitia video walizorekodi kuna video inamuonyesha diwani aliyenunuliwa akizungumzia kuwa aliyekuwa akichoma moto shule za Arusha ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda.

"Kwangu kuchomwa shule moto ni jambo la muhimu kuliko Rushwa iliyotumika kununua madiwani Arusha. Hii inahusisha watoto kuungua na mauti. Ikifika mahali watu tunataka madaraka kwa kiasi hicho inakuwa hatari. Sijasema amefanya lakini najaribu kufikiria kama ni Lema ningekuwa nimeonekana nikitoa rushwa kwa ajili ya kununua madiwani au balozi sijui Mkurugenzi wa Takukuru angechukuaje hatua kuhusu mimi. Nachotaka ni kuona haki na sheria inachukuliwa" amesema Lema.

Ameongeza kwamba, hata kama baada ya kukabidhi ushahidi wao hatua stahiki zisipochukuliwa kwa watuhumiwa anaamini tayari wao kama viongozi waliofanikisha shughuli hiyo watakuwa wamekwisha timiza majukumu yao na kuwataka kila mwenye nafasi ya kufichua maovu afanye

"Wenye mamlaka wakiona kwamba siyo jambo la msingi na wakaamua kupuuza sisi htutakuwa na la kufabnya isipokuwa tunawaachia wao na sisi tutakuwa tumekamilisha wajibu. Tunaamini  ipo siku na hiyo siku ipo karibu sana hao wananchi wanaonekana kuwa ni wapuuzi watakuwa ni watu wenye akili sana" Lema ameongeza.

Kijana wa Azam U-20 Apata Shavu Kuchezea Kikosi cha Kwanza cha Timu Hiyo

$
0
0
Kijana  wa Azam U-20 Apata Shavu  Kuchezea Kikosi cha Kwanza cha Timu Hiyo
Kocha mkuu wa Azam FC Aristica Cioaba amesema ataendelea kutoa nafasi kwa vijana watakaoonyesha uwezo wa kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari leo kocha huyo ameanza kwa kusifu kiwango kilichooneshwa na kinda wa timu ya vijana ya Azam FC (Azam U-20), Paul Peter kwenye mchezo dhidi ya Singida United uliopigwa wikiendi iliyopita.

“Paul (Peter) ni mshambuliaji mzuri kijana, licha ya uchanga wake haikunipa shida mimi kama kocha kuweza kumpa nafasi kwenye mechi iliyopita”, amesema Cioba.
Muromania huyo ameongeza kuwa kama alivyompa nafasi Paul Peter ataendelea kutoa nafasi kwa vijana wengine ambao wanaonesha uwezo wa kutoka timu za vijana za Azam FC.

Paul Peter alipandishwa kwenye kikosi hicho Jumanne iliyopita, nakutumia siku nne tu kufanya mazoezi na kikosi cha wakubwa kabla ya Jumamosi kufunga bao la kusawazisha na Azam FC kuvuna pointi moja dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Merezaga Atoa Agizo Kwa Wakuu wa Magereza

$
0
0

Kamishna Jenerali wa Merezaga Atoa Agizo Kwa Wakuu wa Magereza
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dk Juma Malewa amewaagiza wakuu wa magereza nchini kutumia rasilimali zilizopo kwenye maeneo ya vituo vyao vya kazi ili kukabiliana na changamoto zilizopo, ikiwemo kupunguza uhaba wa nyumba za askari.

Ametoa kauli hiyo baada ya kukagua Gereza la Mkuza lililopo Picha ya Ndege wilayani Kibaha akiwa ziarani kujionea changamoto zilizopo.

Dk Malewa amesema jana Jumatatu kuwa changamoto zilizopo katika gereza hilo ni uchache wa nyumba za askari na zilizopo zimechakaa hivyo kuhitaji ukarabati.

“Nitoe wito kwa askari waweze kutumia rasilimali zilizopo ili kukabiliana na hali hiyo wakati Serikali ikiendelea na jitihada za kuzitatua," amesema.

Amesema wanaweza kufyatua matofali na kuyachoma na wale ambao kuna miti kwenye maeneo yao wanaweza kutengeneza mbao ili kujenga nyumba za kuishi askari za gharama nafuu.

Kutokana na umuhimu wa askari wa Jeshi hilo, amesema Serikali imeendelea kuweka mikakati ya kuboresha makazi.

Amesema hivi karibuni Rais John Magufuli ametoa fedha zitakazotumika kujenga nyumba za askari zipatazo 300 katika Gereza la Ukonga.

Dk Malewa amesema nyumba zingine tano zitakazokuwa na uwezo wa kuishi askari 60 zinatarajiwa kuzinduliwa mkoani Arusha.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Pwani, Boidy Mwambingu amesema wameshaanza ujenzi wa nyumba mbili za askari katika Gereza la Bagamoyo na pia wanaendelea na ujenzi wa zahanati ya Gereza la Mkuza.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alimuomba Dk Malewa kuangalia uwezekano wa kutenga bajeti ya kutosha na hasa kwa ajili ya kulipia bili za maji na umeme kwenye majengo ya Magereza kuepusha taasisi hiyo muhimu kukatiwa huduma hizo.

Rais Magufuli Afunguka Kuhusu Bombardier

$
0
0
Rais Magufuli Afunguka Kuhusu Bombardier
Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kuzungumzia juu ya ndege za Tanzania sita zilizonunuliwa na serikali ikiwepo Bombardier Q 400-Dash ambayo inashikiliwa nchini Canada na kusema ndege hizo zitawasili nchini mwakani 2018.

Rais Magufuli amesema hayo alipokuwa kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) ambao uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, Rais Magufuli amesisitiza kuwa Tanzania inakosa watalii wengi kutokana na kukosa ndege.

"Tumenunua ndege sita ndege mbili zimeshawasili Tanzania, lakini ndege zingine ikiwepo Bombardier zitawasilia mwakani 2018 mwanzoni tunafanya haya kwa ajili ya kutengeneza Tanzania mpya, nchi ambazo zina ndege zake idadi ya watalii wanaoingia kwenye nchi hiyo ni kubwa zaidi, nchi yetu ni ya pili kwa kuwa na vivutio vingi duniani lakini idadi ya watalii wanaoingia ni ndogo kutokana na kukosa ndege zetu" alisema Rais Magufuli 

Serikali ilikiri ndege mpya aina ya Bombardier Q-400 Dash 8 iliyonunuliwa na serikali ambayo ilipaswa kuingia nchini toka mwezi Julai lakini ikashindikana kufika kutokana na kudaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd iliyozuia ndege aina ya bombardier Q400-Dash 8 iliyonunuliwa na Tanzania nchini Canada.

Mtoto Aliyefungiwa Chumbani kwa Miezi Sita Aanza Matibabu

$
0
0
Mtoto Aliyefungiwa Chumbani kwa Miezi Sita Aanza Matibabu
Mtoto Mariam John (12), mkazi wa Nyamongo wilayani hapa aliyekuwa amefungiwa ndani kwa zaidi ya miezi sita, ameanza kupata matibabu baada ya kuokolewa, huku mzazi wake akijitetea kuwa uwezo wa kumhudumia ndio uliochangia.

Mariam aliokolewa na Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu cha Masanga kilichopo wilayani hapa baada ya wazazi kumfungia ndani kutokana na ugonjwa wa degedege huku akiwa na tatizo la akili.

Mzazi wa mtoto huyo, Paulina John alisema kuwa mwanaye alianza kuugua ugonjwa huo tangu Januari 2017 na kuvimba mwili wote, na wakati huo mama huyo alikuwa na mtoto mwingine aliyekuwa anaumwa hivyo alishindwa kuwahudumia wote kwa pamoja.

Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe alisema wanamshikilia mama huyo huku akiendelea kumhudumia mwanaye hadi atakapopata nafuu ndipo atakapofunguliwa mashtaka ya kumficha na kumnyima chakula.

Hata hivyo, kamanda huyo alisema baba wa mtoto huyo alikimbia kusikojulikana kukwepa mkono wa sheria, lakini wanamsaka ili naye ajibu tuhuma hizo.

Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu Masanga ambacho pia kinatoa huduma za afya, Stella Mgaya alisema kwa sasa mtoto huyo ameanza kuonyesha matumaini ya kuimarika kiafya.

Msimamizi wa kituo hicho, Julius Joshua alisema mtoto huyo alipokewa kituoni hapo Septemba 26 akiwa na hali mbaya na hakuwa na uwezo wa kukaa wala kuona vizuri kutokana na kudhoofika mwili na alipopimwa aligundulika kuwa na utapiamlo uliopitiliza.

“Tulipompima uzito siku hiyo alikutwa na kilo 12, lakini baada ya kukaa hapa kituoni kwa siku chache amepimwa na kukutwa amefikisha kilo 16, hilo ni jambo la kufurahisha,” alisema Joshua.

Alisema walipata taarifa za mtoto huyo kutoka kwa majirani kwamba amefungiwa ndani.

Meneja wa kituo hicho, Valerian Mgani alisema baada ya mtoto huyo kufikishwa walimwanzishia chakula lishe ili kumpa nguvu na kuujenga mwili ambapo kwa sasa mtoto huyo anaweza kukaa na kuona vizuri.

Mimba ya Mwanafunzi Yamfikisha Mahakamani Mtendaji

$
0
0
Ofisa Mtendaji  Afikishwa Mahakamani Tuhu
 Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ihulike wilayani Bukombe, Lucas Maganga amefikishwa katika mahakama ya wilaya kwa tuhuma ya rushwa.

Akimsomea shtaka hilo mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Gabriel Kurwijila, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wa wilaya hiyo, Kelvin Murusuri alidai Maganga alitenda kosa hilo Julai kwa tarehe na nyakati tofauti.

Alidai kuwa baada ya mshtakiwa kupata taarifa za ujauzito wa mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Ihulike, alizikutanisha familia mbili za upande wa msichana na mvulana aliyempa ujauzito kisha akizishawishi zielewane.

Aliendelea kuiambia mahakama kuwa baada ya ushawishi huo, Stephano Maliyatabu ambaye ni mzazi wa mvulana alitoa Sh950,000, kati ya fedha hizo mtendaji alipewa Sh450,000 na nyingine alipewa mzazi wa msichana huyo. Hata hivyo, mshtakiwa alikana shtaka hilo na upande wa mashtaka ulidai uchunguzi umekamilika. Mshtakiwa alikosa wadhamini wawili waliopaswa kusaini dhamana ya Sh3 milioni kila mmoja na hivyo kukosa dhamana. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 12.

Klabu ya Yanga Yaomba Msaada

$
0
0
Klabu ya Yanga Yaomba Msaada
Klabu ya soka ya Yanga imerudi tena kwa wanachama wake mara hii ikiwa ni kuhitaji ushirikiano kwenye ujenzi wa uwanja wa Kaunda ambao utatumika kwenye mazoezi ya timu hiyo.

Msemaji wa Yanga Dismas Ten amesema Yanga inawaomba wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kupeleka vifusi kwenye uwanja huo ili kusaidia zoezi la ujenzi linaloendelea.

“Zoezi la ujenzi wa uwanja wetu linaendelea ambapo tumeanza na hatua ya kumwaga vifusi, wanachama wanaleta na tunaomba wengine wazidi kuleta, mtu yeyote anayejua kifusi kinapatikana wapi anaweza kuleta”, amesema Ten.

Yanga imepanga kuuboresha uwanja wa Kaunda uliopo makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es sala

Ushaidi Kesi ya Uhujumu Uchumi ya Vigogo wa Tanesko

$
0
0
Ushaidi Kesi ya Uhujumu Uchumi ya Vigogo wa Tanesko
Usikilizaji wa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili watumishi watano wa zamani wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na msambazaji kutoka kampuni ya M/S Young Dong Electronic Co. Ltd utaanza Novemba 2 na 3 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) washtakiwa wanadaiwa kuisababisha Serikali hasara ya Sh275 milioni.

Washtakiwa hao ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Robert Shemhilu; Ofisa Ugavi, Harun Mattambo; Mkurugenzi wa Fedha, Lusekelo Kasanga; mwanasheria, Godson Makia na msambazaji, Martin Simba.

Usikilizaji wa ushahidi wa upande wa mashtaka unatarajiwa kuanza Novemba 2 na 3 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka mawili ya uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya madaraka, hivyo kusababisha hasara ya Sh275 milioni.

Upande wa mashtaka unawakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Vitalis Peter.

Wanadaiwa kati ya Januari na

Desemba 2011 katika ofisi za Tanesco, Ubungo washtakiwa wakiwa waajiriwa wa shirika hilo walitumia madaraka yao vibaya kufanikisha malipo kwa msambazaji Martin Simba bila kufanya uhakiki.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo kinyume cha kifungu cha 35 cha Sheria ya Ununuzi wa Umma namba 21 ya 2014 kitendo ambacho kilisababisha msambazaji huyo kupata faida.

Inadaiwa kati ya Januari na Desemba, mwaka 2011 katika ofisi za Tanesco, Ubungo washtakiwa wakiwa waajiriwa wa shirika hilo pamoja na msambazaji huyo waliisababishia Serikali hasara ya Sh275 milioni. Washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Makumbusho ya Olduvai Gorge Yamezinduliwa

$
0
0

Makumbusho ya Olduvai Gorge Yamezinduliwa
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amezindua makumbusho ya Olduvai Gorge, ambako ni chimbuko la historia ya binadamu.

Amesema makumbusho hayo ni kielelezo cha maisha na ustaarabu wa binadamu ambao unaelezea maisha ya vizazi vilivyopita.

“Makumbusho haya pia yatasaidia kujua sisi ni nani na tumetoka wapi,” amesema.

Amesema ujenzi wa makumbusho hayo utasaidia kuvutia watalii na wanasayansi wa masuala ya mambo kale duniani.

Samia amesema eneo la Ngorongoro lina historia kubwa ya maisha ya zamadamu ikibainika miaka 3 milioni iliyopita walikuwepo walioishi kwa kutembelea miguu miwili.

Amesema eneo la Ngorongoro kumebainika miaka 2.7 milioni iliyopita binadamu walianza kutumia zana za mawe katika kula nyama na kuwinda.

“Hapa ni chimbuko la historia ya zamadamu, Serikali itaendelea kulihifadhi na kulitunza eneo hili,” amesema.

Makamu wa Rais ameishukuru Jumuiya ya Ulaya kwa kutoa fedha kugharimia ujenzi wa makumbusho hayo na miundombinu yake.

Makamu wa Rais ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuwa na mkakati wa kutangaza makumbusho hayo ndani na nje ya nchi ili kuvutia zaidi watalii.

Pia, amewaomba wananchi wa Ngorongoro kuendelea kuhifadhi eneo hilo ikiwemo kutopeleka mifugo eneo la Creta. Amesema Serikali inajitahidi kuwaondolea kero zao likiwemo tatizo la maji.

Awali, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema eneo la Ngorongoro ni la urithi wa dunia, hivyo wizara kwa kushirikiana na mamlaka wataendelea kulihifadhi na kulitunza.

Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, anayeshughulikia huduma za jamii, Asangye Bangu amesema ujenzi wa makumbusho hayo utasaidia kuongeza watalii.

Ametoa wito kwa mawakala wa utalii kuwapeleka watalii eneo la Olduvai Gorge  ili kuongeza mapato kwa manufaa ya Taifa.

Meneja wa idara ya urithi wa tamaduni katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mhandisi Joseph Mwankunda amesema ujenzi wa eneo hilo umegharimu Sh1.7 bilioni.

Amesema makumbusho hayo ni ya kisasa zaidi duniani na wanatarajia yatadumu kwa zaidi ya miaka 50.

Meneja miradi katika Jumuiya ya Ulaya, Alexa Haden amesema jumuiya ya Ulaya imetoa fedha katika mradi huo kutokana na kuthamini mchango wa mambo ya kale.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge wa Ngorongoro, William ole Nasha ameomba mafanikio ya mradi huo kugusa maisha ya wananchi wanaoishi ndani ya mamlaka hiyo wanaokabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa maji.

Nyumba za Wabunge wa Upinzani Zashambuliwa Uganda

$
0
0
Nyumba za wabunge wa upinzani zashambuliwa Uganda
Vitu vinavyokisiwa kuwa guruneti vimetumiwa kushambulia nyumba za wabunge wawili wa upinzani nchini Uganda, mmoja wao akiwa ni mwanamuziki ambaye sasa ni mbunge Bobi Wine, kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini humo.

Polisi sasa wanachunuza mashambulizi kwenye nyumba za Bobi Wine ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi, anayewakilisha eneo la Kyaddondo West na Allan Ssewanya ambaye ni mbunge wa Makindye West.

Mashambulizi hayo yalifanyika mapema Jumanne.
Wiki iliyopita shambulizi liliripotiwa kwenye nyumba na mbunge mwingine Moses Kasibante ambaye ni mbunge wa Rubaga North.

Wabunge watwangana makonde Uganda
Mwanamuziki Bobi Wine akamatwa Uganda
Kwenye ujumbe kupitia mtandao wa Facebook, Bobi Wine alisema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa nyumbani kwake

Amesema amekuwa akipokea vitisho vya kuuliwa karibu kila siku.
Gazeti la New Vision lilisema kuwa wabunge ambao nyumba zao zilishambuliwa ni badhi ya wale waliotimuliwa bungeni kufuatia ghasia wakati wa mijadala kuhusu kuondolewa kwa umri wa kuwania urais.

Wataalamu Bingwa wa Dawa za Usingizi Afrika Mashariki Wakuta na Dar

$
0
0
Wataalamu Bingwa wa Dawa za Usingizi Afrika Mashariki Wakuta na Dar
Wataalamu bingwa wa dawa za usingizi Afrika Mashariki wamekutana katika Kitengo cha Mifupa (MOI) kwa ajili ya mafunzo ya siku nne yanayotolewa na Chuo Kikuu cha Afya Kwa Zulu Natal kwa kushirikiana na Chama cha madaktari wa Dawa za Usingizi nchini(Sata).

Mafunzo hayo ambayo kwa mara ya kwanza yanafanyika nchini Tanzania,  yanaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye pia ni daktari bingwa wa dawa za usingizi,  Mpoki Ulisubisya.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumanne,  Dk Ulisubisya amesema mafunzo hayo yatasaidia uwezo wa madaktari bingwa kushughulikia magonjwa ya ajali kwa watoto.

Amesema mafunzo hayo yametayarishwa na Sata kwa kushirikiana na kampuni ya kuuza dawa za usingizi Abbvie,  ili kusaidia madaktari bingwa wa upasuaji kupata uelewa wa ni jinsi gani ya kuhudumia upasuaji wa usingizi.

Amesema kampuni hiyo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa upande wa mabingwa wa usingizi nchini na imeweza kupeleka wataalamu kwenda kupewa mafunzo Kwa Zulu Natal nchini Afrika Kusini ambao wana kila kitu cha kujifunzia hivyo kumwezesha mtaalamu kufanya mafunzo kwa vitendo.

"Vifaa au midoli hii ya kufundishia ni salama zaidi ikilinganishwa na kufanya mafunzo kwa vitendo kutumia binadamu, kwani faida ya kutumia hii hata kama ukikosea huwezi kusababisha madhara yoyote kiafya," amesema Dk Ulisubisya.

Kwa upande wake daktari bingwa wa dawa za usingizi kwa watoto kutoka Hospitali ya Taifa Rwanda, Dk Rosemary Mukunzi amesema mafunzo hayo ni ya kwanza kutolewa Afrika Mashariki lakini yamekuwa yakitolewa Kusini mwa Jangwa la Sahara, "ni mafunzo muhimu kwa wataalamu wa dawa za usingizi kwani ni sekta nyeti na muhimu, hata hivyo duniani wataalamu wake ni wachache.”
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images