Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Shilingi Mil 60 Kumaliza Mgogoro wa Flora Mbasha, Vikao Vyafanyika Siku Tatu, Flora Akataa Ndoa Mara Tano

$
0
0

Stori: Haruni Sanchawa na Shakoor Jongo

HABARI zilizotua kwenye meza ya Uwazi juzi zinadai kuwa familia mbili, ya Emmanuel na Flora Mbasha zimeweka kikao kwa siku tatu mfululizo kutaka kuinusuru ndoa ya wawili hao lakini imeshindikana huku pembeni ikidaiwa kwamba ili mambo yakae sawa lazima Mbasha alipe shilingi milioni 60.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, kikao hicho kiliitishwa na baba wa Mbasha kwa kushirikiana na ndugu wengine wa pande zote mbili.

“Mbasha na mke wake, Flora walikutanishwa sehemu fulani jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupatanishwa. Kikao kilikuwa kizito, wakubwa wa familia zote walikuwepo lakini Flora alikataa mara tano kurudi kwenye ndoa yake.

UWAZI LAPIGA HODI NYUMBANI KWA MBASHA
Juzi Jumapili, Uwazi lilitia timu nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga jijini Dar na kubahatika kuzungumza na baba na mama wa Mbasha bila kumpata Mbasha mwenyewe.

Mzee huyo aliyejitambulisha kwa jina la Maneno alikiri kuwepo kwa kikao kwa muda wa siku tatu tofauti lakini akasema mambo yalishindikana.

“Mimi nilikuja Dar kutokea Dodoma wiki moja iliyopita baada ya kupata wito wa mwanangu kuhusu mgogoro wa ndoa. Nilipofika hapa, sikumkuta Flora, nyumba ilikuwa tupu.

“Kikao kiliitishwa na pande zote mbili, akiwemo Mchungaji Gwajima ambaye alionekana kusuluhisha mgogoro wao lakini dalili za Flora hazikuonesha kuwa tayari kurudi kwenye ndoa yake,” alisema mzee huyo.

KUNA MKONO WA MTU
Mzee Maneno aliendelea kusema: “Mimi kama mtu mzima, nilichokiona katika ndoa ya mwanangu kuna mkono wa mtu. Ila sasa ametumia mbinu kubwa sana kumrubuni Flora na yeye kakubali kurubunika.”

MAMA MZAZI NAYE
Kwa upande wake, mama mzazi wa Mbasha, Zulfa Maneno alisema kwake ni masikitiko makubwa kwa sababu mtoto wake alishakuwa na jina kubwa kimataifa na mkewe pia.

Alisema: “Mimi kwenye kikao nilipomwona Flora anakataa ndoa yake mara tano, kila akiulizwa anasema hataki kurudi mpaka mara tano, nikajua hakuna ndoa.

“Ninachojua, mgogoro huo wa ndoa ulitengenezwa kwa makusudi kabisa ili ndoa ivunjike. Ila kama aliamua kumwacha mwanangu angefanya hivyo kwa amani na si visa kama hivi.”  
Kuhusu kutakiwa shilingi milioni sitini ili Flora arejee kwenye ndoa yake, wazazi hao walisema hawajui kitu labda kama yanasemwa pembeni.

KULIKUWA NA MGOGORO

Habari zaidi zinadai kwamba, fedha zinazotakiwa kulipwa ni kwa sababu, ndoa hiyo ilikumbwa na mgogoro kabla ya kuibuka kwa madai ya Mbasha kumbaka shemeji yake.
Flora aliwahi kufungukia hilo kwamba, kabla ya kutokea kwa madai ya ubakaji, alitibuana na Mbasha na akaamua kuondoka nyumbani kwenda kuishi hotelini. 

DALILI MBAYA
Kuna madai kwamba, siku ambayo Mbasha alikwenda kujisalimisha polisi (Juni 16, 2014), Flora alipigiwa simu kujulishwa lakini hakutokea kituoni.

Ikazidi kuelezwa kwamba, siku Mbasha anapelekwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar kujibu madai ya ubakaji, pia Flora alijulishwa lakini hakutokea mahakamani hapo.

Mbali na kupelekwa mahakamani, habari za uhakika zinasema hata pale Mbasha alipokosa dhamana na kupelekwa kwenye Gereza la Keko, Flora alijulishwa, lakini hakufanya lolote.

“Je, kwa hayo yote ni kweli Flora anaipenda ndoa yake? Si jibu lipo wazi kwamba  hakuna ndoa.” alisema mtu mmoja aliye karibu na familia hiyo.

MBASHA BAADA YA KUTOKA JELA
Ushahidi wa majirani umeweka bayana kwamba, Mbasha alipotoka gerezani na kufika nyumbani kwake, Tabata-Kimanga, Dar, walimfuata na kuangua kilio mbele yake huku wakimpa pole kwa mkasa mzima.

Baadhi ya majirani waliozungumza na Uwazi juzi, walisema kuwa siku hiyo nyumbani kwa Mbasha kulikuwa na dalili zote za kuwepo kwa msiba kwani vilio vilitawala.

MADAI
Mbasha, alipandishwa mahakamani Juni 17, mwaka huu kwa madai ya kumbaka mara mbili shemeji yake (jina tunalo).

Siku hiyo alikosa dhamana na kupelekwa Gereza la Keko ambapo Alhamisi ya Juni 19, mwaka huu alirudishwa tena mahakamani hapo kwa ajili ya dhamana. Kesi yake itaanza kusikilizwa Julai 17, mwaka huu huku ikielezwa kuwa upelelezi umekamilika.
GPL

Umemuona mtoto wa Nakaaya? picha na alichomuimbia viko hapa

$
0
0
Ni longtime kidogo ulikua hujamsikia Nakaaya na hii ni kwa sababu alikua na break ya uzazi akiwa ndio amejifungua mtoto wake wa kwanza nyumbani kwao Arusha.
Mwimbaji huyu ambae ujazo wa jina lake uliongezeka baada ya kutoa ile single ya ‘Mr. Politician’ sasa hivi anamiliki mawimbi na single yake mpya inaitwa ‘blessing’ aliyoifanya Noizmekah Arusha.
Nakaaya ameamua kuifanya hii single mpya kama dedication kwa mtoto huyu aitwae Kai kuonyesha ni jinsi gani amemgusa moyoni, vilevile kumpa ahadi ambayo ni mama pekee anaiweza.

Dr. Slaa: Wakorofi CHADEMA ni Wajinga

$
0
0
Ni kauli nzito iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema Dr. W. Slaa baada ya kushutumiwa pamoja na Mwenyekiti wake juu ya uvujaji wa mamilioni ya chama hicho.

Ametoa kauli hiyo na kusema wasome katiba vizuri.

- Wenyewe wahoji matumizi ya Ruzuku, kususia Bunge la Katiba
- Wadai Mbowe amejilipa milioni 700/= za chama kinyemela
- Washinikiza kuitishwa Mkutano wa Baraza kuu kuwahoji

Source: Raia Tanzania

Jirani zetu Kenya Wanazidiwa Nguvu na Alshaabab, Tanzania iko wapi?

$
0
0
Ni muda sasa jirani wetu Kenya wanapata mashambulizi kutoka kikundi cha magaidi wa alshaabab.

Karibu kila siku mashambulizi ya mabomu ya kutegwa na risasi hutokea ktk miji ya Nairobi na Mombasa huku ikiua ndugu zetu wakenya.

Ni alshaabab wanaojipambanua kuwa wanahusika na mauaji hayo ukizingatia alshaabab waliwahi kusema;

"Kenya imeingiza majeshi somalia, hivyo itajuta kuingiza majeshi somalia, tutaishambulia kenya".... "Tofauti yetu na Kenya ni kuwa, Wakenya wao wanakuja kupigana vita Somalia huku wakiogopa kufa, sisi tunapigana vita huku tukiwa hatuogopi kufa.."

Nimetafakari sana hatua ambayo watanzania tumechukulia wenzetu wa kenya kushambuliwa na wahuni wa alshaab huku tukiwa kimya tu. kwa nini nasi tusipeleke jeshi letu Somalia kama walivyopeleka wenzetu wa KENYA na UGANDA?

Hivi alshaabab wakipata nguvu wakishuka wakatake over Mombasa, je pwani yetu itakuwa salama? Tanzania itakuwa salama?

ALSHAABAB WAKIONA WANAIWEZA KENYA, MAJIRANI HATUTOKUWA SALAMA HATA

Kitale Akanusha Kuwa na Mahusiano na Vj Penny

$
0
0
Msanii wa filamu za vichekesho, Kitale, ambae kwa sasa anatambulika zaidi kwa jina la ‘Mkude Simba’ amekanusha kuwa hajawai kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Vj Penny ambae aliwai kuwa mpenzi wa zamani wa Diamond.

Kitale akizungumza Global TV hivi karibuni ,amekanusha uvumi huo, ambao uliambatana na picha ambazo zinaonyesha Penny wakati akimbusu Kitale.

“Penny mimi sina mahusiano nae yoyote, siyo kweli sina mahusiano nae , mimi nina ndoa yangu na nina mke wangu na nina mtoto, naiheshimu ndoa yangu”Alisema Kitale.

Lulu akana kushirikishwa na Mapacha, ‘I swear sina idea na huku kushirikishwa’

$
0
0
Kundi la Mapacha jana (June 23) wametambulisha ngoma yao mpya baada ya ukimya wao wa muda mrefu, wimbo ambao wamedai wamemshirikisha muigizaji wa Bongo Movie Elizabeth Michael aka Lulu. Lakini Lulu leo amekana kushirikishwa katika wimbo huo kwa kusema kuwa hana taarifa zozote wala haujui wimbo huo.


Hiki ndicho alichokiandika Instagram:



Mwe mwe mwe…!Mbona mnaninyasanyasa…’in Senga’s voice’
I swear sina idea na Huku kushirikishwa….au kuna Elizabeth Michael’Lulu’ mwingine!????
Dah…hebu mliosikia hyo nyimbo labda mniambieMana nashirikishwa ki miujiza jmn”.

Wimbo mpya wa Mapacha unaoitwa ‘Time For The Money’ umetengenezwa na Tudd Thomas.

TBS yakamata Shehena ya Nguo za Ndani za Mitumba

$
0
0
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekamata shehena ya marobota ya nguo za ndani za mitumba ambazo thamani yake haijajulikana kwa kuwa zimechangaywa na nguo za watoto.

Mkaguzi wa TBS, Donald Manyama alisema wamefanikiwa kukamata nguo hizo juzi bandarini zikiwa kwenye kontena mbili ambapo walilazimika kuongozana na wahusika ambao ni Kampuni ya Dema ili kuufanyia ukaguzi zaidi mzigo huo.

“Katika ukaguzi wetu , tumebaini kwamba marobota haya yanaonekana kama ni nguo za watoto lakini ndani kuna nguo nyingi za ndani za kike na za kiume za wakubwa na watoto za mitumba ambazo zimepigwa marufuku kuingizwa au kuuzwa nchini,” alisema.

Akiwa katika ghala za kampuni hiyo eneo la Mwenge, Dar es Salaam, Manyama alisema kazi ya kuzichambua na kuzitenganisha inaendelea ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.

Mfanyabiashara Mussa Kassim wa Kampuni ya Dema katika utetezi wake amedai  kusikitishwa kwake na hali hiyo hasa kwa kuwa wao waliagiza nguo za watoto na siyo za ndani kama ilivyotokea.

“Mitumba hii sisi tunaiagiza kutoka Ujerumani. Hatukuagiza nguo za ndani kwa kuwa siyo kusudio letu wakati Serikali imepiga marufuku. Nafikiri zimechangaywa kwa bahati mbaya,” alisema Kassim.

BATULI: Sijawahi Kula Hela ya Mume wa Mtu..Mwili Wangu Si Mtaji Kwangu

$
0
0
Staa  wa  kike  anayefanya  vizuri  katika  tasnia  ya  fillamu Yobnesh Yusuph ‘Batuli’   amefunguka  na  kudai  kuwa  hajawahi  kula  hela  ya  mume  wa  mtu  na  kama  watu  wanamhisi  hivyo  basi  watakuwa  wanakosea  sana…..

Batuli  alitoa  kauli  hiyo  ili  kuwathibitishia  mashabiki  wake  juu  ya  kauli  mbovu  za  watu  kuwa  urembo  wake  unategemea  mtaji  wa  mwili  wake  ambapo  amewajibu  kwa  kusema  kuwa    urembo  na  uzuri  wake  unatokana  na  matunda  ya  kazi  yake  ya  sanaa  na  kimsingi  anautumia  huko   kwa  kuwa  haoni  faida  ya  kula  hela  ya  mwanaume  kwani  hajaifanyia  kazi.

Amini  kuwa  naendesha  maisha  yangu  kwa  misingi  ya  kazi  zangu, inawezekana  wapo  wanawake  wanaoishi mjini  kwa  kutegemea  mtaji  wa  miili  yao  na  si  sanaa.

Kwa  upande  wangu  hata  Mungu  ananiona  kuwa  kile  ninachokipata  kupitia  sanaa  ndicho  ninachokitumia  kwenye  matumizi  yangu,” alisema  Batuli

Baby Madaha : 'Wema Sepetu Tuachie Na Sisi Huyo Diamond Tumfaidi '

$
0
0
Star wa filamu na muziki wa Bongoflava Baby Madaha anadaiwa kuwewesekea penzi la Diamond Platnumz na kumtaka Wema Sepetu awaachie na wao Diamond a.k.a Sukari ya warembo ili wafaidi kama anavyojiachia.

Chanzo kimoja kilicho karibu na Baby Madaha ambacho pia kinafanya juu chini kuwika katika filamu kwa masharti ya kutotajwa jina lake kikizungumza na Swahiliworldplanet wiki iliyopita kilisema kuwa:

Nawapa habari, Baby Madaha anamtaka Diamond hata kule kumponda kwenye media sio kwa dhati ni njia ya kumshawishi amtongoze. 

“Sikia nikwambie, katika Kill Awards (mwaka huu) Madaha alikuwa na lengo la kumbusu Diamond kwa stage lakini  alikuwa anamhofia Wema na Team Wema wangeweza kuja juu ikawa habari mpya…

“Anamtaka ila anashindwa tu kusema wazi, unajua Wema anambana sana Diamond, anataka Wema amwachie” kilisema chanzo hicho huku kikisisitiza kuwa kisitajwe jina lake .

Umeipata Hii ? Kajala Kakimbia Nchini…Chanzo ni Bifu Kati Yake na Wema Sepetu

$
0
0
Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amefunguka kuwa yuko Bongo kwa kuwa ndipo nyumbani kwao lakini hana hamu ya kuendelea kuishi nchini kutokana na kuzushiwa mambo kila kukicha.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko wikiendi iliyopita, mwigizaji huyo alisema anapenda awe na maisha ya furaha na wanawake wenziye kwa kubadilishana mawazo ya hapa na pale lakini kwa sasa hana upendo huo kwa kuwa kuna watu wanaishi kwa kutegemea bifu.

Unajua inauma sana, unaenda klabu unamkuta mtu ambaye huko nyuma alikuwa shoga’ko, kula, kuvaa na kila aina ya ushirikiano mnapeana, sasa mnakuja kugombana, kiukweli roho huwa inauma ndiyo maana nashindwa hata kwenda klabu kuepusha mengi, nasubiria viza yangu itoke nisepe zangu China,” alisema Kajala.

Kwa muda mrefu kumekuwa na ugomvi usiokwisha kati ya Kajala na mwigizaji mwenzake, Wema  Sepetu.

Walio Muua Sista wa Kanisa la Roma Walipora Kiasi Hichi cha Fedha..Soma Mchezo Mzima Ulivyokuwa

$
0
0
Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam imesema majambazi waliohusika na mauaji ya Sista wa Kanisa Katoliki, Clencensia Kapuli wamepora kiasi cha Sh20 milioni na nyaraka mbalimbali.

Tukio la kupigwa risasi sista huyo lilitokea juzi saa 8 mchana eneo la Riverside Ubungo, Dar es Salaam na dereva , Patrick Mwarabu alikatwa kidole gumba kwa risasi.

Sista Kapuli wa Shirika la Mtakatifu Maria wa Parokia ya Mtakatifu Gaudence Makoka jijini hapa alikuwa Mhasibu wa Parokia hiyo ambayo inamiliki Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anwarite na Chuo cha Ufundi Stadi Makoka.

Kamanda wa Kanda hiyo alisema Kamishna Suleiman Kova alisema jeshi hilo limetangaza msako wa kuwatafuta na kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo.

Kova alisema marehemu akiwa ameongozana na wenzake ambaye ni Sista Brigita Mbaga na dereva aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Hilux walikuwa wakitoka Benki ya CRDB, Tawi la Mlimani City kuchukua fedha.

Alisema walipofika eneo la Ubungo Kibangu ili kulipa deni la chakula katika duka la Thomas Francis ndipo walitokea majambazi wawili wakiwa na pikipiki ambayo haikusomeka namba.

Alisema kati ya majambazi hao mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG wakampiga risasi ya kidole gumba cha mkono wa kulia dereva wa gari hilo kisha sista huyo alipigwa risasi ya kifua na kuporwa fedha hizo Sh20 milioni.

Kova alisema jeshi hilo limebaini kuwa matukio ya ujambazi hasa unaohusiana na wananchi kuporwa kiasi kikubwa cha fedha unaanzia benki na huwafuatilia wanapoingia na kutoka.

“Ni muhimu kwa benki kuwahimiza wateja wao kutochukua kiasi kikubwa cha pesa kiholela kwani ni rahisi kuporwa na watu wasio na nia njema,” alisema Kova.

Alisema benki ziwahimize wateja wao kutumia njia mbadala za kusafirisha pesa nyingi kama vile kwa hundi, kufanya miamala bila kadi na matumizi ya kadi za ATM.

Kova alizishauri benki nchini zianzishe vitengo vya ushauri kwa wateja ili wanapokuwa na fedha nyingi wasindikizwe na polisi.

Je Kuna Ugonjwa wa Hamu ya Kufanya Mapenzi Au ni Kujiendekeza..Hawezi lala Bila ya Kupata Dozi

$
0
0

Wakati nasoma sekondari kuna dada alikua hadi anazimia mara adondoke yaani tabu tupu.

AKIPELEKWA HOSPT MADAKTARI WANATUULIZA je ana mpenzi?( maana tulikua tunatoka sehemu moja hivyo tulikua tunamsindikiza) japo tulikua bodin

kwa uoga tulisema HANA lakini alikua nao na akigombana na one of them ndo anaumwa

na kujaamiiina ilikua kawaida sana kwake 

Sasa basi juzi nikaambiwa mtu flani muacheni tu awe hata na watoto maana hawezi lala bila kujamiina

SASA NIKABAKI NA SWALI JE HUO NI UGONJWA au nikujiendekeza?

AVEVA: Nipeni Simba Niinyooshe Yanga

$
0
0

WANACHAMA wa klabu ya Simba Jumapili ya wiki hii watachagua viongozi wapya wa klabu hiyo katika ngazi ya urais, makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo watakaopewa dhamana ya uongozi kwa miaka minne ijayo.

Mmoja wa wagombea urais wa klabu hiyo, Evans Aveva alizungumza na Mwanaspoti na kutoa sera zake endapo atafanikiwa kuingia madarakani.

“Sera yangu kuu ni kuleta umoja ndani ya klabu ya Simba, sitaki kuona Mwanasimba anajitofautisha na mwenzake kisa ametoka kwenye kundi fulani, sisi sote nia yetu ni moja hivyo nitajitahidi kwenye uongozi wangu kuhakikisha tunakuwa na umoja.

“Sera yangu ya pili ni kutaka Simba icheze mpira, tumedhalilika sana, wapenzi wa klabu yetu wamefedheheshwa sana na matokeo mabovu ya klabu yetu hivyo mimi nimepanga kurejesha heshima hiyo, nataka klabu yetu icheze soka safi na la kisasa.

“Katika kulifanikisha hilo nitahakikisha kuwa nafanya usajili wa kikosi imara, wachezaji wanakuwa na mazingira mazuri ya kazi, naboresha mishahara yao na masilahi yao mengine ili waweze kuweka akili yao kwenye mchezo,” anasema Aveva.

“Nitaangalia wachezaji wazawa zaidi kwa sasa, kwa wachezaji wa kimataifa nitahakikisha tumefanya skauti za maana ili kuepuka kusajili wachezaji wenye uwezo wa chini, tunataka kuhakikisha Simba inakuwa na wachezaji wenye hadhi ya kucheza kwenye klabu yetu na siyo kuokota okota tu.”

“Mbali na hilo nitaziunganisha kamati ya usajili na ile ya ufundi, tunatakiwa tuwe na taasisi moja kubwa ambayo itatuletea wachezaji wa maana, nimepanga kuona wanakuwa na maskauti wa usajili wa ndani na nje ya nchi, wa ndani watatazama mechi zote za Ligi Kuu na kutuletea mapendekezo ya maana.”

Kuongeza pato la klabu

“Kwa sasa tunashindwa hata kuuza jezi za klabu yetu kutokana na mwenendo mbovu wa timu, nitaweka nguvu kubwa kwenye heshima ya soka uwanjani na hiyo ndiyo itasaidia kukuza kipato chetu.

“Watu wataingia kwa wingi kuitazama Simba, watu watanunua jezi za Simba, pia nitajitahidi kushirikiana na viongozi wenzangu kuona namna ya kuanzisha bidhaa nyingine za klabu kama vile vikombe, kalamu skafu na kadhalika,” anasema Aveva.

“Kikubwa ninachoamini ni kuwa kuiwezesha Simba kucheza mpira, wadhamini watakuja wenyewe tu, kwa mfano mpaka sasa wadhamini watatu wameonyesha nia ya kuingia udhamini na sisi iwapo nitaingia madarakani, wameonyesha kuniamini hivyo tukicheza kwa kiwango cha juu itakuwa zaidi ya hapo.”

Aveva anaongeza kuwa atahakikisha kuwa idara ya masoko atayaoiunda itasimamia na kukuza mauzo ya bidhaa za klabu hiyo pamoja na kubuni njia nyingine za mapato za klabu hiyo ikiwemo namna ya kuboresha jengo la klabu hiyo lililopo eneo la Kariakoo, Dar es Salam.

Baba Mbasha: Ni Ukweli Usio Pingika Kuwa Flora Alichoka Kuishi na Mwanangu (Video)

$
0
0
Baba mzazi wa Emmanuel Mbasha, Mzee Maneno amefunguka kuwa mwimbaji wa Injili Flora Mbasha alichoka kukaa na mwanaye ndiyo maana mgogoro wao umefika hatua hii. Tazama Video Hapa:

Lupita Nyong’o Athibitisha Kuwa na Hhusiano wa Kimapenzi na Rapa Huyu.

$
0
0
Lupita amezidi kuchukua headlines za vyombo mbalimbali vya habari tangu afanikiwe kuchukua tuzo za Oscar na kutajwa kama mwanamke mrembo zaidi duniani, sasa amethibitisha kuhusu upande wake wa mahusiano kuwa ni kweli ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki K’naan kutoka Somalia.

Mara ya kwanza Lupita alikuwa akihusishwa na Michael Fassbender na Jared Leto lakini mwigizaji huyo amekita mizizi yake ya kimapenzi kwa rapa K’naan na wanafuraha na mahusiano yao.
Wapenzi hao mara kadhaa wamekuwa wakionekana katika maeneo mbalimbali wakiwa pamoja lakini hawakuwa wakiweka wazi nini kinaendelea kati yao na kufanya watu wahisi tu juu ya uhusiano wao.

Stori ni kwamba katika jarida la hivi karibuni la Vogue ambalo Lupita ametokea kwenye ukurasa wa mbele amethibitisha kweli ana uhusiano wa kimapenzi na K’naan na anampenda sana.
K’naan ni mzaliwa wa Somalia na ameingia katika umaarufu baada ya kuimba wimbo rasmi wa kombe la dunia kwa mwaka 2010 wa “Wavin’ Flag”.

Ushahidi wa Suarez Kumng’ata Mchezaji Mwingine Mechi ya Italy vs Uruguay

$
0
0
Kwa mara nyingine katika kipindi cha maisha yake ya soka, Luis Suarez ameingia tena kwenye headlines kwa kumng’ata mchezaji mwenzie uwanjani.
Kwenye mchezo wa mwisho wa makundi kati ya Uruguay vs Italy, zikiwa zimebakia dakika 9 mchezo kuisha ulitokea utata mkubwa wakati Suarez na Chiellini walipokumbana katika maeneo ya penalti

Beki huyo wa Italia alilalamika wakati kwa refa kwamba alikuwa ameng’atwa na akajaribu kumwonyesha alama.
Wakati wachezaji wa Italia walipokuwa wakiendelea kulalamika, Uruguay wakapata kona.
Suarez alipiga pasi nzuri naye Godin akafunga bao hilo la ushindi.
Mpaka unamalizika Uruguay walikuwa washindi, na kuungana na Costa Rica kwenda hatua ya 16 ya michuano hiyo.
Wakati huo huo Italy iliungana na England iliyomaliza mechi zake za makundi kwa kutoka sare ya 0-0 na costa Rica – kufungasha virago kurudi nyumbani zikishindwa kufuzu kwenda hatua ya pili.
Uruguay sasa itacheza na Colombia wakati Costa Rica ikikutana na Ugiriki kwenye hatua ya 16 bora.

AGIZO: Mikutano ya Nape yapigwa ‘stop’

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ameonja chungu ya uamuzi wa Serikali wa kusitisha mikutano ya hadhara katika mikoa ya Lindi na Mtwara baada ya kushindwa kufungua mashina ya chama hicho mjini Mtwara.

Nape ambaye alikuwa mkoani Mtwara kwa ziara ya siku moja, alijikuta akiishia kuwakabidhi bendera za chama hicho viongozi wa matawi ili wakazipandishe wenyewe kimyakimya.

Akizungumzia hatua hiyo, Nape alisema amri hiyo ya kusitisha mikutano imekuwa kikwazo na inadidimiza demokrasia katika mikoa hiyo, hivyo Serikali inapaswa kuibadili ili kuruhusu iendelee kufanyika. Mashina ya chama hicho ambayo yalitarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa wiki ni Shapriya, Coco Beach na Kwajionee.

“Ni kweli ilikuwa twende kuzindua kwenye maeneo yenu lakini… lipo agizo ambalo lilitolewa na Serikali kuzuia mikutano katika mikoa hii, kupitia kwenu ipo haja ya kufungua mikutano ili demokrasia ipanuke zaidi,” alisema Nape na kuongeza:

“Amri hii kwa mtazamo wangu inabaka demokrasia, lazima mikutano iruhusiwe kama hali ni mbaya, kazi ya Serikali ni kulinda huo usalama… nitakwenda kushauriana nao ili mikutano ifunguliwe, sidhani kama masikio yanaweza kuzidi kichwa.”

Akizungumzia hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maisha Maganga alisema Serikali haijatengua agizo hilo.

“Kama Lulu Akikubali Kuolewa Nitatulia Nae na Kuanzisha Familia…..Anajua Kutafuta Hela Hata kwa Muonekano ni Mkali.”

$
0
0
Ammy Nando na Lulu walitengeneza vichwa vya habari mara kadhaa wakihisiwa kuwa na uhusiano wa mapenzi. Hata hivyo wawili hao kwa nyakati tofauti waliueleza uhusiano wao kuwa ni wa kirafiki.

Lakini Nando bado anamuangalia Lulu kwa jicho la tatu kama wife material.

Nando amefunguka yote katika kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm kinachoongozwa na Maryam Kitosi, Edson Mkisi Jr na DJ RGuy.

Amesema Lulu ni rafiki yake, lakini ni msichana ambaye anamzimia kwa kuwa anajua kutafuta pesa japo ana umri mdogo.

“Lulu ni mwanaharakati, ni mdogo lakini she knows how to get money.” Amesema Nando.

Aongeza kuwa kutokana na sifa alizonazo za kutafuta pesa pamoja na uzuri wake, atakapokuwa na mpango wa kuolewa yeye yuko tayari kutulia nae.

“Kama Lulu akikubali kuolewa, me I settle down….nitatulia kwa Lulu kama akikubali kuolewa…..hata kwa muonekano ni mkali.” Alisikika Nando kupitia 100.5 Times Fm.

Hivi karibuni Lulu alisema kuwa hana uhusiano wa mapenzi na Nando na ana mpenzi wake mwingine.

Nando pia alieleza uhusiano wake na Dayna Nyange na kudai kuwa ni rafiki yake tu na wanashirikiana katika video ya wimbo wake mpya, “nitauza sura mle ndani.”

Baada ya kupata hayo maelezo kutoka kwa Nando, naomba nikwambie kitu kingine muhimu.

Tuzo Za Watu zitatolewa June 27 Mwezi huu Serena Hotel, tunaomba kwa moyo mkunjufu, mpigie kura Maryam Kitosi kama mtangazaji anaependwa, andika TZW1 MARYAM kwenda 15678.

Pia kipigie kura kipindi cha Hatuta Tatu kama kipindi cha radio kinachopendwa andika TZW2 HATUA TATU kwenda 15678. Asante.

Picha ya Lupita Yawanyamazisha Waliomkosoa Kuwa kisura wa Kampuni yenye Bidhaa za Kujichubua

$
0
0
Baada ya kutoka tangazo kuwa Lupita Nyong’o atakuwa kisura wa kwanza mweusi kwenye bidhaa ya Lancome, wengi walianza kumkosoa kwa uamuzi wake kwa kuwa kampuni hiyo ina bidhaa za kujichubua ngozi.

Hata hivyo, picha ya kwanza ya kampeni ya Lupita kwa bidhaa tofauti za kampuni hiyo zimewanyamazisha walioanzisha mgogoro huo. Lupita ameitangaza Tiente Idole Ultra 24H.

Sasa kampuni hiyo imetangaza ngozi nzuri ya mrembo Lupita Nyong’o bila kuwa na dalili za kujichumbua. Huenda ikawashawishi wateja wao kuachana na mpango wa kujichubua kwa kuwa black is beauty.

Mapacha Wamjibu Lulu Baada ya Kukana Kuimba Kwenye Wimbo wao, 'Ametudharau Sana'

$
0
0
Baada ya Elizabeth Michael kukana kushirikishwa na kundi la mapacha kwenye wimbo wao mpya ‘Time For The Money’. Kundi la Mapacha limeeleza jinsi lilivyoipokea taarifa hiyo.

Akiongea na tovuti ya Times Fm, Kulwa wa Mapacha amesema kitendo alichokifanya Lulu ni dharau kubwa kwao na kwamba inawezekana ameona hataki kusikika kwenye wimbo waliofanya wao.

“Sisi tuliamua kumtaja kwa respect kwa kuwa tulipenda alichofanya kwenye ile beat ambayo sisi tuliamua kuiimbia kwa kutumia chorus yake. Lakini yeye ameamua kutu-disrespect. Sasa sisi tumeamua hata kama wimbo huo ukipata tuzo basi yeye hatutamtaja...ametudharau.”Alisema Kulwa.

Aliongeza kuwa hivi sasa wameamua kulifuta jina la Lulu na kwamba hata wimbo huo utakapokuwa unapigwa asitajwe kabisa.

“Sasa hivi tunasimama kama Magenge peke yetu. Tumeachana na masuala ya Lulu, hatutamtaja

na tunafuta jina lake kabisa sasa hivi tunabaki Magenge tu.”

Tulipomuuliza kwa nini hawakuwasiliana nae awali angalau kumshukuru kwa chorus aliyowafanyia ili wapate mrejesho mapema. Alisema wao hawajawahi kuonana nae wala kuwasiliana nae hata siku moja.

“Tungewasiliana nae vipi, si unajua hawa watoto unaweza kuwapigia simu wakaacha hata kupokea..si unajua mwanangu. Sisi tungempata wapi sasa. Tud yeye alituambia ni Lulu na sauti yake kweli ni yeye. Sasa kama anakataa bana tunaachana nae."

Baada ya Mapacha kutambulisha wimbo wao na taarifa kumfikia Lulu leo, aliandika kwenye Instagram kwa mshangao mkubwa.

Mwe mwe mwe...!Mbona mnaninyasanyasa...'in Senga's voice'

 I swear sina idea na Huku kushirikishwa....au kuna Elizabeth Michael'Lulu' mwingine!????

 Dah...hebu mliosikia hyo nyimbo labda mniambieMana nashirikishwa ki miujiza jmn.”
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images