Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

CUF Ya Lipumba Yaikana CUF.

$
0
0
Chama cha Wananchi(CUF), upande wa Profesa  Ibrahim Lipumba kimesema kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi wa madiwani uliopangwa kufanyika Novemba 26 lakini kimesisitiza kutoshirikiana na Ukawa.

Hii ni mara ya kwanza kwa chama hicho kuweka msimamo wake katika uchaguzi tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambapo CUF ilikuwa miongoni mwa vyama viliunda umoja huo kwa kuweka wagombea waliokubaliana.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya amesema jana  Jumamosi jijini kuwa chama hicho hakioni sababu yoyote ya kushirikiana na vyama vingine kwenye uchaguzi huo ambao unahusisha halmashauri 34.

“CUF tunashiriki kwenye uchaguzi huu lakini hatututegemei kushirikiana na umoja wowote ule, sisi hatuitambui Ukawa lakini tunajua kuna chama kama Chadema, CUF na vyama vingine,” alisema Kambaya wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni.

Alisema chama hicho kimejipanga vilivyo kuelekea kwenye uchaguzi huo na kwamba ili kuwaletea maendeleo wananchi wa maeneo hayo kunahitajika kuwa na viongozi wenye utulivu wa akili.

“Sisi tuko tayari kuelekea kwenye uchaguzi huo bila kuhusishwa na chama kingine chochote tunaamini tutafanya vizuri,” alisema.

Awali, mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho, Jafari Mneko aliwataka wana CUF kujitokeza kwa wingi katika kinyang’anyiro hicho. Amesema chama chake kimepokea taarifa kutoka ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikiwaarifu kuhusu uchaguzi huo.

“Tumepata barua kutoka tume ambayo imetueleza kuhusu tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo na sisi tumeanza kujiandaa na ndiyo maana tunawaomba wanachama wetu wanaohisi wana uwezo wajitokeze kuomba nafasi na baadaye viongozi wa chama watachuja majina yao,” alisema.

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo alionya kile alichokiita mali ya chama kutumika kinyume na sheria na akawataka wanachama kutetea maslahi ya chama chao.

“Kuanzia sasa hatutapenda kuona mali ya chama kama mihuri, bendera ikiendelea kuchezewa ovyo, tunawataka wanachama kuzingatia katiba ya chama ibara ya 12 ambayo inamtaka kila mwanachama kulinda katiba na imani ya chama,” alisema.

Kauli Tatu za Nape Nnauye Mwezi Huu

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mtama, Mh Nape Nnauye toka umeanza mwezi Oktoba, 2017  ametoa kauli zake tatu ambapo katika kauli ya kwanza alikuwa amelenga kuwapa ujasiri vijana na Watanzania kiujumla kuchukua hatua katika mambo fulani fulani.


Nape Nnauye alitumia mtandao wake wa twitter kuyasema hayo na kuwambia kuwa unapoona umekosa matumaini juu ya jambo fulani hupaswi kusita kufanya maamuzi huku ukimuamini Mungu kwani yeye hutoa njia.

"Mwenyezi Mungu hufanya njia pasipokuwa na njia! Amini na chukua hatua" alisema Nape Nnauye 
Aidha Mbunge huyo alizidi kuwasisitiza Watanzania na kuwataka kuwa na busara katika mambo yao hata mambo yanapokwenda ndivyo sivyo aliwataka kutumia busara zaidi
"Taulo likianguka, hatua ya kwanza chutama, ndio busara aaaakh" alisema Nape Nnauye 

Mbali na hili Nape Nnauye alimalizia kwa kauli hii
"Usipande miba kwenye njia yangu maana unaweza kesho kuja kwangu ukiwa peku! Weka akiba" 

Serikali itabidi ikope Kulipa Mishahara - Zitto Kabwe

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi  ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kutoa sababu kwanini mapato ya serikali yameshuka na kusema serikali inapaswa kutazama upya utendaji wake vinginevyo itabidi ikope ili kulipa mishahara kwa watumishi.

Zitto Kabwe amesema kuwa kwa miezi ya Julai na Agosti mwaka huu mapato ya serikali yalishuka mpaka shilingi 600 bilioni na kusema ni maporomoko makubwa hivyo madhara yake ni makubwa.
"Ni mporomoko mkubwa Sana na sio jambo la kushangilia hata kidogo. Madhara ya kushuka kwa mapato ni makubwa kwani mishahara ya watumishi wa Umma peke yake ni Shilingi 570 bilioni Kwa mwezi" alisema Zitto Kabwe

Aidha kiongozi huyo ameelezea sababu kubwa iliyopelekea mapato ya nchi kushuka 
"Mzee Harry Kitilya alipata kuniambia mwaka 2013 " Mwenyekiti, TRA inatoza kodi kutoka kwenye shughuli za biashara zinazozalisha mapato na sio kutoka kwenye biashara tu ". Kitilya alikuwa na maana kuwa kama hakuna shughuli za biashara ( business transactions), huwezi kutoza kodi. Maelezo haya yanaeleza kwanini mapato ya serikali yameshuka. Shughuli za biashara zimeshuka sana nchini na hivyo kupelekea kuporomoka Kwa mapato" alisema Zitto Kabwe

Zitto Kabwe aliendelea kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili la kuporomoka kwa mapato ya serikali
"Kodi inayoingiza mapato mengi Serikalini ni PAYE ( kutoka mishahara ya wafanyakazi). Kitabu cha mapato ya serikali kuu cha mwaka 2016/17 kinaonyesha kuwa wafanyakazi wote wa sekta ya Umma na sekta binafsi walichangia jumla ya shilingi trilioni 3 kwenye mapato yote ya Serikali. Hivi karibuni tumeshuhudia makampuni yakipunguza wafanyakazi na mengine kufungwa. Pia Serikali yenyewe ilipunguza watumishi iliyowaita hewa na wenye vyeti feki. Hivyo eneo kubwa la kodi ya PAYE limeathirika" alisisitiza Zitto Kabwe

Mbali na hilo Zitto Kabwe aliitaka serikali kutazama upya utendaji wake ili kuweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji nchini na kudai kama serikali haiatafanya hivyo itafika mahali itabidi ikope pesa ili kulipa mishahara ya watumishi mbalimbali.

Godbless Lema: Hakuna Jipya Baraza la Mawaziri

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa baraza jipya la mawaziri lililotangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli halina jipya kwani sura zilizobaki ni zile zile.

Ameyasema kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Twitter, ambapo amesema kuwa ameona mabadiliko ya baraza la Rais Magufuli lakini bado fikra ni zile zile na watu ni wale wale na kudai katiba mpya ndio suluhisho la vyote.

“Nimeona Mabadiliko ya baraza la JPM. Watu ni wale wale, fikra zile zile. Katiba Mpya yenye fikra mpya ndio tumaini kwa mabadiliko sahihi ya nchi na watanzania kwa ujumla,”ameandika Lema

IGP Sirro: Mjadala wa Tundu Lissu kupigwa risasi ufungwe mara moja

$
0
0
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro ametaka mjadala kuhusu kupigwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ufungwe mara moja.

Agizo hilo amelitoa leo akiwa ziarani jijini Mbeya wakati akizungumza na vikosi vya ulinzi na usalama ambapo amewaonya wanasiasa kuacha kuuendeleza na waliachie jeshi lifanye kazi yake.

Kuhusu madai yaliyotolewa hivi karibuni na familia ya mbunge huyo kuwa jeshi hilo halina dhamira ya dhati ya kufanya uchunguzi, IGP Sirro amesema hana cha kuwajibu kwa kuwa hataki malumbano na familia hiyo.


Chanzo: Azam Tv

Biko Waja na Biko Sports....Karibu Jamvini

$
0
0
Karibu BIKOSPORTS karibu JAMVINI.
Jeff lea na Maulid Kitenge washatandika majamvi yao tayari.
Dnmark wanakutana na Romania ,Slovenia  watakuwa Dimbani na Scotland,Egypt wakipambana na Congo huku Poland vs Montenegro.Tandika wa kwako sasa kupitia www.bikosports.co.tz kwa Odds za kijanja tena bila ya kujisajili.
#KaribuJamvini
#ChezaKuanziaJero
#FastPlayFastPay

Wanaume Wananichukulia Tofauti na Nilivyo...Siko Hivyo Jamani

$
0
0

Naombeni mchango wa mawazo, imetokea wanaume wananiambia ati wananiogopa, mie ni mbabe, najiamini sana na wengine huenda mbali kwa kusema mwanamke wa dizain yako sioi.

Kwakweli sipo hivyo na huwa naumia sana mtu anaponitamkia hayo. Nasikitika mana sielewi ni kitu gani na kutongozwa na waume za watu kumezidi il a sio na singles?

Tafadhalini wanajamii naimani kuna watu wanaofahamu vizuri psychology wanishauri jamani.

Asanteni kwa kunijibu bila kejeli

Je Wajua Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Madogo ya Kiume?

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WA NA MAUMBILE MADOGO?Tatizo hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia ,hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wenzao,kwakawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6_8 vinginevyo mtu huyu ana matatizo.Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo baadhi ni,upungufu wa vichocheo (hornes) za gestrojen ambapo mwanaume anapobalehe vichocheo hivi (hormones)huchochea ujuaji wa uume.chango ambalo hushambulia nerve ambapo huharibu kabisa ukuaji wa uume,Punyeto ambayo huasili misuli ya uume,pia ngiri ambayo huleta maumivu ya tumbo kuunguluma na kujaa gesi,korodani moja kuvimba,kutopata choo vizuri,sababu hizi na nyinginezo hufanya uume kulegea na kisinyaa nakuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu zakiume (hamu ya tendo landoa hupungua au kuisha kabisa).NSUMBU,Nidawa inayozalisha hormones za gestrogene na kufanya uume kukua na kuongezeka mara dufu.NZAGI,Ni dawa ya kurudisha nguvu za kiume ,hutia hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha nakuponya kabisa tatizo hilo. Pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk 15 nakuendelea kwa tendo la kwanza.kumbuka dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji.Natunatibu kisukari,bp,ngiri,miguu kuwaka moto,namengine mengi.WASILIANA OSTADHI JUMA KWA SIMU NO,0784002216 AU 0769597778.

Hizi Hapa Aina Nne za Wanawake Michepuko…..

$
0
0

1.MCHEPUKO LAMI: Huu ni ule ambao hauombi pesa, katulia hana mapepe, uwe naye au usiwe naye maisha yake yanaendelea tu.

2. MCHEPUKO VUMBI: Huu ni ule wa vibomu!! mara ooohhh sina pesa, naomba vocha, sijui simu imekufa, oooh mara nipo saluni nadaiwa elf thelathin, naomba nauli…..n.k! Na hii ndio noma maana njia kuu lazima washtuke mana mchepuko vumbi unachafua na unasumbua full time.

3. MCHEPUKO KOKOTO: Huu ni mkali zaidi ya njia kuu maana kila mara huuliza upo wapi, Uko na nani, why hupokei simu yangu? Kama uko kwako naomba utoke nje tuongee kidogo na leo uwe na mimi tu…Yaani tabu tupu!

4: MCHEPUKO MATOPE: Yaani huu usiombe hata kukutana nao maana wenyewe ndio funga kazi.. Huu bana unajua kuchuna hasa ila pale unapoupa pesa na wenyewe unaenda kuzihonga zote kwa mchepuko wake mwingine yaani hatari tupu

Dr Kashililah Asema Rais Hajakosea Uteuzi wa Mrithi wake

$
0
0

 Katibu wa Bunge wa zamani, Dk Thomas Kashililah amesema, Rais John Magufuli hakufanya kosa katika uteuzi wa Katibu wa Bunge.

Rais Magufuli jana Jumamosi alimteua Steven Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge, uteuzi ambao umeibua hoja kwamba sheria haikufuatwa.

Dk Kashililah akizungumza na mwananchi leo Jumapili, amesema kwa mujibu wa ibara ya 87(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano  mamlaka ya uteuzi haikufanya kosa licha ya sheria ya Bunge kuelekeza utaratibu.

Amesema, “Mamlaka ya uteuzi iko sahihi… unajua sheria haiko juu ya Katiba na Katiba iko juu ya sheria, hivyo Rais akiamua anaweza kufanya hilo, sheria haiwezi kumzuia,” amesema Dk Kashililah akisisitiza ibara ya 87 iko wazi.

Ibara hiyo inasomeka: “Kutakuwa na Katibu wa Bunge ambaye atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye madaraka ya juu katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.”

Dk Kashililah amesema: “Kama aliyeteuliwa angekuwa hayuko kwenye madaraka ya juu hapo sawa, lakini huyu aliyeteuliwa (Kagaigai) ni mtu senior kabisa serikalini na ana vigezo hivyo… kuna watu wanapotosha ukweli.”

ACT Wazalendo yapinga Uteuzi Katibu wa Bunge

$
0
0
Chama cha ACT Wazalendo kimeeleza kusikitishwa na uteuzi wa Rais John Magufuli wa Katibu wa Bunge.

ACT katika taarifa yake leo Jumapili, imesema Rais ameamua kuyaweka pembeni matakwa ya sheria yanayoongoza mchakato wa uteuzi wa Katibu wa Bunge na kuamua kujichagulia apendavyo.

“Kutokana na unyeti wa nafasi ya Katibu wa Bunge, na kwa minajili ya kuweka 'check and balance' pamoja na kulinda uhuru wa Bunge, kwenye mchakato wa uteuzi wa nafasi husika, sheria imeweka utaratibu wa kufuatwa kwenye uteuzi wa Katibu wa Bunge,” imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Ado Shaibu ambaye ni katibu wa itikadi, mawasiliano na uenezi wa ACT Wazalendo.

Amesema mbali na Rais kuwa na mamlaka ya kumteua Katibu wa Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 87 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, anapaswa kuzingatia utaratibu uliowekwa na Sheria ya Utawala wa Bunge ya mwaka 2015.

Kwa mujibu wa kifungu cha 7(3) cha sheria hiyo, Rais atateua jina moja kutoka miongoni mwa majina matatu yaliyopendekezwa na Tume ya Huduma za Bunge.

Shaibu amesema jambo hilo si la hiari bali ni sharti la lazima la sheria ambalo Rais analazimika kulifuata.

Ndiyo maana kifungu husika kinasema, “The Commision shall recommend three names. (Tume ni lazima ipendekeze majina matatu)”.

ACT imesema wajumbe wa Tume ya Huduma za Bunge kwa taarifa ambazo chama hicho kinazo, hakuna kikao chochote kilichoketi na kupendekeza majina kwa Rais kwa ajili ya uteuzi wa Katibu wa Bunge.

Chama hicho kimesema uteuzi huo ni ushahidi wa wazi wa kudharauliwa mhimili wa Bunge.

“Ni matumaini yetu kuwa Bunge na watu wote wanaopenda uhuru na uimara wa Bunge watasimama imara kuupinga uteuzi huu ambao ni kinyume cha sheria,” amesema.



ACT imesema iwapo Rais hatatengua uteuzi huo na kufuata utaratibu uliowekwa na sheria za nchi, kitalifikisha suala hilo mahakamani ili kupata ufafanuzi wa Mahakama.

“Ni wakati muafaka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndiye mwenye dhamana ya kuishauri Serikali kwenye masuala ya k

Siri ya Rais Magufuli kumpa Angellah Kairuki Wizara ya Madini

$
0
0
Hizi inawezekana kabisa ndizo sababu kwanini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua na kumpa Angellah Kairuki Wizara mpya ya Madini.

1. Kutokana na kumudu vilivyo katika Ofisi aliekuwepo awali yaani Wizara -Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala bora.

2. Kutokana na Mh Kairuki kubuni mbinu mbalimbali za kuangalia upya mifumo ya ajira kwa kubuni uhakiki wa vyeti, uhakiki wa mifumo ya mishahara, ubunifu wa kupata taarifa za wafanyakazi halali na uhalali wa wafanyakazi waliopo na wale waliopo katika payroll yaani 'hewa' hali iliopelekea serikali kuokoa mabilioni ya shilingi.

Hiki ndicho kilichomsukuma kwa utashi na kwa imani alionayo kwa Mh Angellah Kairuki ndipo Mh Rais John Pombe Joseph Magufuli kumteua katika Wizara hii mpya ya Madini na Wizara ngumu iliowashinda wengi Ma- Dr na Ma- Professa hii itapelekea Angellah Kairuki ahakiki tena aina, na idadi ya migodi yote nchini kutokana na ubunifu na uaminifu alionao Mama huyu

Julius Mtatiro Adokeza Alichoteta na Tundu Lissu

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, (CUF) Julius Mtatiro ambaye yupo nchini Kenya amesema kuwa leo Oktoba 8, 2017 amepata bahati ya kumuona Mbunge Tundu Lissu hospitali na kusema kuwa Lissu ni mtu asiyeogopa na mwenye maono makubwa.

Mtatiro anasema kwa muda ambao ameweza kukaa na Lissu hospitali amemwagiza kuwaambia Watanzania kuwa atarudi akiwa mzima na kuendelea na mapambano maradufu zaidi katika kupigania haki.

"Mtatiro nenda kawaambie kuwa nitarudi nikiwa mzima na tutaendelea na mapambano maradufu zaidi, faraja muhimu nayohitaji kutoka kwa Watanzania hivi sasa ni kuendeleza mapambano ya kudai haki na kupambana na udikteta, tusikubali nchi yetu iharibiwe na kikundi cha watu wanaoogopa kukosolewa" alisema Mtatiro

Aidha Mtatiro anasema kumuona Mbunge Tundu Lissu hospitali ni kitu ambacho kimezidi kumjenga zaidi na kumpa mafunzo makubwa katika maisha ya kila siku na katika siasa

"Mimi binafsi kama Mtatiro, kumuona Lissu kumenijenga zaidi, kumenifundisha kuwa ukipigwa risasi hata 100 kwa sababu ya kuwa mkosoaji wa watawala yapo mambo mawili yatatokea, aidha utapona kama Lissu au utakufa kama ilivyowatokea wapigania haki wengi. Uki-survive kama Lissu jambo moja litatokea, utaungana na wananchi wote kupigania haki kwa nguvu kubwa zaidi. Ukiuawa kwa risasi kama wapigania haki wengi jambo moja kubwa litatokea, kifo chako kitapandikiza mbegu kubwa ya ukombozi, kifo chako kitaliamsha taifa kupigania haki na kupambana na madikteta wajinga" alisisitiza Mtatiro 

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 na kisha baada ya hapo alipelekwa nchini Kenya jijini Nairobi kwa matibabu zaidi ambapo mpaka sasa yuko Kenya kwa matibabu.

Chadema iwe Serious Sasa na Ulinzi wa Viongozi Wao, Kibatala Apewe Ulinzi Sasa

$
0
0


Sitapenda kuandika mengi ila Chadema ilizembea sana kutokumpa ulinzi mtu aliyekuwa anaandamwa kama Lisu.

Wote tumeshuhudia system ya ulinzi ya Askofu Gwajima kuanzia kwenye stage mpaka escort yake pale hakuna cha Nissan nyeupe ya kutia puwa unless iwe imetangazwa vita ndio unaweza kumvamia Gwajima kijeshi, lakini yeye binafsi ametimiza wajibu wake wa kujilinda na the rest ni mamlaka ya Mungu.

Ni uzembe wa hali ya juu mmeufanya Chadema tusingependa hili lijirudie otherwise hao Red bregade wenu ni wa kazi gani?

Nyumba ya Kibatala kwa sasa ifungwe mifumo yote ya kiulinzi ya kielectroni na simu za viongozi wenu ambao ni threat kwa watu fulani muwape satellite phone kwa ajili ya mawasiliano muhimu. Nilisikitika sana kusikia mawasiliano ya Lisu yalikuwa yanaingiliwa huu ni uzembe wa hali juu sana, hata Mange anawazidi akili.

Nakaribisha na wenye utaalam wa kiusalama wa kisasa tuwape ushauri Chadema.

By Matola/JF

Aina Kumi Za Waume Ambao Wake Zao Wanakereka Kuwa Nao

$
0
0
Kila ndoa inachangamoto zake na maana halisi ya ndoa ni ule uwezo wa wanandoa kuvumiliana katika changamoto hizo. Kuna changamoto za kimungu ambazo wanandoa hawawezi kuziepuka lakini kuna zile za kiuanadamua mbazo nyingi ni za kimakusudi na mtu huamua tu kuwa hivyo. Katika kuangalia ndoa leo nimeona nichambue aina kumi za waume ambao wake zao wanakereka kuwa nao;

(1) Wanaojione Kama Wafalume (King Husband); HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea.

(2) Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband); Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake.

(3) Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband); Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya misngi, mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke.

(4) Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband); Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.

(5) Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband); Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wekea zao.

(6) Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol Husband); Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vizawadi, wanajua udhauifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wanawake, hawajali tena.

(7) Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband); Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwa na mke akifanya kosaa kidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu zake, mbona flani alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo. Kwakifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa.

(8) Mume Mtalii (Visiting Husband); Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto.

(9) Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband); Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia huhisi wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke.

(10) Mwanaume Mbahili (Miserly Husband); Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha naataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake.

Hiyo nji baadhi tu ya aina ya wanaume ambao wanawake wengi wasingependa kuwa nao. Kama mwanaume upo hivyo jua mke wako hafurahii na anavumilia tu. Ndoa ni furaha amua kubadilika na usimfanye mke wako kuishi na wewe kwa kujilazimisha. Kama ni mume jiulize uko namba ngapi hapo na kama ni mke mezea namba ya mumeo na jua hauko peke yako

Uteuzi wa Rais Magufuli Kupingwa Mahakamani

$
0
0

Chama cha ACT Wazalendo kupitia kwa Katibu wa Itikadi, Mawasialiano na Uenezi, Ado Shaibu kimesema kuwa kitakwenda mahakamani kupata ufafanuzi wa kina kuhusu kile walichodai ni kukiukwa kwa sheria katika uteuzi wa Katibu wa Bunge uliofanywa na Rais jana Oktoba 7, 2017.

Katika taarifa iliyotoleo leo na chama hicho, imeeleza kwamba, “Kama Rais hatatengua uteuzi huu na kufuata utaratibu uliowekwa na sheria za nchi, ACT Wazalendo kitalifikisha suala hili mahakamani ili kupata ufafanuzi wa mahakama.”

Wakati akitangaza mabadiliko katika baraza la mawaziri, Rais Magufuli alitangaza pia kumteua Stephen Kigaigai kuwa Katibu wa Bunge, na kwamba katibu aliyekuwepo, Dk. Thomas Kashililah atapangiwa kazi nyingine.

ACT Wazalendo wamesema uteuzi huo ni kinyume na sheria kwa sababu, mbali na Rais kuwa na mamlaka ya kumteua Katibu wa Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 87 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anapaswa kuzingatia utaratibu uliowekwa na Sheria ya Utawala wa Bunge – The National Assembly (Admintration Act), 2015. Kwa mujibu wa Kifungu cha 7(3) cha Sheria hiyo, Rais atateua jina moja kutoka miongoni mwa majina matatu yaliyopendekezwa na Tume ya Huduma za Bunge.

Kwa mujibu wa ACT wamesema, hakuna kikao chochote cha Tume ya Bunge kilichoketi na kupendekeza majina kwa Rais kwa ajili ya uteuzi wa Katibu wa Bunge. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wajumbe wote wa Tume ya Huduma za Bunge waliohojiwa na vyombo vya habari wamethibitisha pia kutofanyika kwa kikao hicho.

“ACT Wazalendo tunaona kuwa uteuzi huu si tu ni mwendelezo wa Rais kufanya maamuzi bila kuzingatia sheria za nchi bali ni ushahidi mwingine wa wazi wa kudharau mhimili wa Bunge,” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha, chama hicho kimemtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndiye mwenye dhamana ya kuishauri serikali kwenye masuala ya kisheria kuwajibika, lakini pia wakamataka mwanasheria mkuu kujiuzulu endapo ushauri wake kwa serikali hauthaminiwi.

“Inawezekana Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa woga au uzembe, hamshauri Rais ipasavyo au Rais hafuati ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Katika yote mawili, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kama anataka kulinda heshima yake binafsi na ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hana budi KUJIUZULU.”

Uteuzi Katibu wa Bunge Kaa la moto..Magazeti ya Leo Jumatatu

$
0
0

























Uteuzi Katibu wa Bunge Kaa la moto..Magazeti ya Leo Jumatatu

Je Una Upungufu wa Nguvu za Kiume, Kukosa Hamu ya Tendo, Kufika Kileleni Haraka na Kushindwa Kurudia Tendo?

$
0
0
JE, UNA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KUKOSA HAMU YA TENDO, KUFIKA KILELENI HARAKA NA KUSHINDWA KURUDIA TENDO AU MAUMBILE MADOGO YA UUME?
       Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana duniani kote. Kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume husababishwa na mambo mengi kama KISUKARI, UNENE ULIOPITILIZA, KUJICHUA  (MASTER BLASHION), HOMONI kushindwa kufanya kazi ipasavyo n.k.
     Upungufu wa nguvu husababisha tendo la ndoa kutokufanyika kwa kujiamini na kwa usahihi na hivyo kusababisha ndoa na mahusiano kuvunjika.
      BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa
☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni
☆Uume kusinyaa katikati ya tendo
☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.
     Kwa kutumia mimea na matunda @markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL:- kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6 hadi 7  @150,000/=
3.VigRX CREAM:- ni gely iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile kwa wastani wa inch 6.5 hadi 8 na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200,000/=
4.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150,000/=
5.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni @130,000/=
      BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA NA ZIMETHIBITISHWA KIAFYA.
    KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WETU WA INSTAGRAM :-
      @markson_beauty_pr
     
    Wasiliana nasi Popote ulipo duniani kwa (+255)
           0767447444 na
              0714335378

        UTAPATA HUDUMA
    NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.

Nigeria yaiongoza Afrika kuingia Kombe la Dunia

$
0
0
Timu ya Taifa ya Nigeria imekuwa ya kwanza kutoka barani Afrika kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi baada ya kufanya vyema kwenye michezo yake.

Katika ushiriki wao mara 6 kwenye Kombe la Dunia tangu mwaka 1994, 1998 na 2014 waliishia raundi ya pili, huku mwaka 2002 na 2010 waliishia hatua ya makundi.

Taifa jingine lililojikatia tiketi hiyo mapema ni Costa Rica ikiwa ni mara yao ya tano kushiriki Kombe la Dunia.



Faida ya Kufanya Mazoezi ya Kutembea

$
0
0
Suala la mazoezi kwa karne ya sasa ni a maisha ya watu  kila siku, hii ni kutokana na  kuwa mazoezi ni kitu muhinu sana katika  maisha ya binadamu ili ajilinde na  magonjwa nyemelezi.



Zipo faida nyingi za kufanya mazoezi ila hizi ni chache kwa mazoezi ya kutembea.

1. Mazoezi ya kutembea husaidia kupunguza uzito wa mtu. Sio vibaya ukitembea kwa dk 60(sawa saa 1) kila siku, Unaweza ukaamua utembee mchana ana jioni.

2. Mazoezi ya kutembea husaidia kupunguza mafuta mwilini. Kitendo cha kutembea kinahusisha mwili mzima na baadhi ya viungo vya binadamu hivyo husaidia kutoa mafuta katika mwili.

3. Vile vile mazoezi ya kutembea huwa ni msaada mkubwa kwa watu walio na tatizo la shinikizo la damu.

4. Zoezi la kutembea kwa miguu husaidia kupunguza msongo wa mawazo(stress). Endapo unakuwa na mawzo ukitumia mazoezi haya husaidi kupunguza hii ni kutokana na kuwa mazoezi haya yanakupa nafasi ya kutazama vitu kadhaa njiani na pia aakili inakuwa inapata mawzo mapya.

Zipo faida byingi za mazoezi haya ila tumia dakka 60 kila siku kwa kuafanya mazoezi ya kutembea kwani kutasaidia mambo kadhaa ikiwemo kuimarisha mifupa.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live


Latest Images