Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Haya Ndiyo Maneno ya Nape kwa Tundu Lissu 'Mjomba Tunashukuru Mungu kwa Tabasamu Usiseme Mengi Tulia Mjomba Upone Kabisa '

$
0
0
Haya Ndiyo Maneno ya Nape kwa Tundu Lissu 'Mjomba Tunashukuru Mungu kwa Tabasamu Usiseme Mengi Tulia Mjomba Upone Kabisa '
Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye amefunguka na kusema amefurahi kumuona Tundu Lissu akiwa katika furaha na tabasamu na kumuomba kwa sasa asiseme lolote mpaka pale atakapona kabisaa.

Nape Nnauye amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema tabasamu la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa kwenye hospitali jijini Nairobi linatoa matumaini makubwa.
"Mjomba tunamshukuru Mungu kwa tabasamu hili la matumaini!Nakuombea afya iimarike kabla hujasema mengi! Tulia mjomba upone kabisa kwanza" alisema Nape Nnauye

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma nyumbani kwake na baadaye alipelekwa jijini Nairobi kwa matibabu zaidi ambapo mpka sasa anapatiwa matibabu huko.


Obama na Bush Wakosoa Uongozi wa Trump

$
0
0
Obama na Bush Wakosoa Uongozi wa Trump
Marais wawili wa zamani nchini Marekani wameonyesha wasiwasi wao kuhusu hali ya kisiasa nchini humo bila kumtaja rais Donald Trump kwa jina.
Barrack Obama aliwataka wapiga kura kukataa kile alichokitaja kuwa siasa za kuwagawanya watu mbali na siasa za hofu.
Alikuwa akimfanyia kampeni mgombea wa chama cha Democrat anayewania wadhfa wa gavana wa jimbo la New Jersey.
Matamshi yake yanajiri saa chache baada ya mtangulizi wake George W. Bush kukosoa unyanyasaji na chuki katika maisha ya kawaida ya raia Marekani.
Katika hotuba, alisema chuki dhidi ya wale wanaokupinga zimeongezwa nguvu huku maadili ya kiraia yakisahaulika.
Bwana Trump ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa mtangulizi wake bado hajatoa tamko lolote.
Marais wa zamani nchini Marekani kwa kawaida huwa nadra kutoa maoni yao kuhusu hali ya kisiasa na ilionekana kuwa makosa makubwa kwa rais aliyetangulia kumkosoa mrithi wake katika ikulu ya Whitehouse.
lakini maadili na viwango vya tabia ambazo awali zilikuwa zikifuatwa sasa zimesahaulika katika mazingira ya kisiasa ya wakati huu.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni za chama cha Democrat , mjini New Jersy, Obama alisema kuwa Wamarekani wanapaswa kutuma ujumbe kwa ulimwengu kwamba tunakataa siasa za kugawanywa na siasa za hofu.
Aliongezea: Kile ambacho hatufai kuendelea nacho ni kuwa na siasa za zamani za kugawanyana ambazo zimekuwepo nyakati za wali.
Siasa tunazoziona sasa tulidhani zimepitwa na wakati, hiyo ni kurudi miaka 50 nyuma.Ni karne ya 21 sio 19. jamani!.

Mwanamke Adakwa Baada ya Kuiba Watoto Watatu

$
0
0
Mwanamke Adakwa Baada ya Kuiba Watoto Watatu
Mama mmoja aliyetambulika kwa jina la Asia Ismali alimaarufu kama Apendeki Katembo Rashid mwenye umri wa miaka 37 raia wa Congo anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuiba watoto watatu Nyamagana Mwanza.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi la polisi linamshikilia mama huyo kwa tuhuma za kuiba watoto watatu, wawili wakiwa na umri wa miaka mitatu na mmoja akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu.

Leo Mashahidi Watatu Kutoa Ushahidi Kesi ya Lulu ya Kuua Bila Kukusudia

$
0
0
Leo Mashahidi Watatu Kutoa Ushahidi Kesi ya Lulu ya  Kuua Bila Kukusudia
MSANII wa Filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo Ijumaa, Oktoba 20, amefika katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuendelea kusikiliza kesi inayomkabili ya kusababisha kifo cha aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba bila kukusudia.
Jana mahakamani hapo, Mdogo wa Kanumba, Seth alitoa ushahidi wake akiieleza mahakama kwamba anachofahamu yeye ni kuwa palikuwa na mgogoro kati ya Lulu na Kanumba aliousikia ambapo Lulu alikuwa akiongea kwa simu na mwanaume mwingine hali iliyozua ugomvi huo na Kanumba.
Leo mashahidi watatu wanatarajiwa kutoa ushahidi wao kwenye kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Sam Rumanyika.

Korea Kaskazini Yaionya Australia Kutoshirikiana na Marekani

$
0
0
Korea Kaskazini Yaionya Australia Kutoshirikiana na Marekani
Serikali ya Australia imesema kuwa imepokea stakhabadhi kutoka Korea Kaskazini ikiitaka Canbera kutojihusisha na utawala wa rais Trump.
Barua hiyo imeshutumu onyo la Marekani kwamba itaiangamiza Korea Kaskazini iwapo italazimika kujilinda.
Waziri mkuu wa Australia PM Malcolm Turnbull amesema kuwa barua hiyo pia ilimwa kwa mataifa mengine.
Amesema inaonyesha kuwa shinikizo za kidiplomasia dhidi ya Korea Kaskzini zimeanza kufanya kazi, licha ya barua hiyo kuwa na ufyozi na malalamishi ya kawaida ya taifa hilo.
Barua hiyo yenye ukurasa mmoja ilitumwa kupitia ubalozi wa Korea Kaskazini nchini Indonesia na inadaiwa kutoka kwa kamati ya maswala ya kigeni ya Korea Kaskazini.
Imezitaka serikali nyengine kujitenga na hatua zisizokuwa na heshima za rais Trump ikisisitiza kuwa Marekani inaweza kusababisha janga kubwa la kinyuklia.
Bwana Turnbull amesema kuwa Korea Kaskazini ndio inayosababisha wasiwasi kwa kutishia kuyashambulia mataifa ya Japan, Korea Kusini na Marekani kwa kutumia silaha za kinyuklia.
''Wametuma barua hizi kwa mataifa mengi , kama barua iliosambazwa'', alisema Bwana Turnbull kwa kituo kimoja cha redio 3AW.
Waziri wa maswala ya kigeni Julie Bishop aliitaja barua hiyo kuwa hatua isiokuwa ya kawaida ya Korea Kaskazini.
Baadaye bwana Turnbull alionekana kutojali umuhimu wake akiifananisha na ufyozi na malalamishi kuhusu Donald Trump unaotolewa na Korea Kaskazini.
Hatahivyo wote wanakubaliana kwamba huenda ni ishara kwamba shinikizo za kimataifa dhidi ya taifa hilo zimeanza kuzaa matunda na kuwa na matumaini kwamba kutakuwa na majadiliana ya kimataifa.
Siku ya Jumamosi Pyonyang iliionya Australia kwamba haitaweza kuzuia janga iwapo itashirikiana na sera za Marekani dhidi ya utawala wa Kim Jong Un.
Korea Kaskazini imekiuka makubaliano ya kimataifa katika miezi ya hivi karibuni kupitia kufanyia majaribio kombora lake la kinyuklia mbali na kurusha makombora mawili juu ya anga ya taifa la Japan.
Marekani imejibu kwa vitisho vya kijeshi , lakini waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson anasisitiza kuwa bwana Trump yuko tayari kuutatua mgogoro huo kupitia diplomasia.

Ebitoke Akubali Yaishe kwa Ben Pol 'Mapenzi ni Hisia Siwezi Nikakosa Furaha Nimeamua Nimuache'

$
0
0
Ebitoke Akubali Yaishe kwa Ben Pol 'Mapenzi ni Hisia Siwezi Nikakosa Furaha Nimeamua Nimuache'
 Mchekeshaji wa kundi la Timamu Africa, Ebitoke amesema ameamua kumuacha Ben Pol aliyekuwa akidaiwa kuwa mpenzi wake kipindi cha nyuma.

Kauli ya Ebitoke inakuja mara baada ya drama za hapa na pale hivi karibuni kuwa wawili hao wamezinguana licha ya wao kutopenda kuliweka hilo wazi. Akizungumza na Papaso ya TBC Fm Ebitoke amesema kutokana na ubize wa Ben Pol na malengo yake ameamua kumuacha.

“Unajua mapenzi ni hisia, nahisi nilikuwa kama namlazimisha lakini nimegundua siwezi nikakosa furaha nikashindwa kufanya baadhi ya malengo yangu, kwa hiyo nimeamua kumuacha afanye maisha yake, ameniacha na mimi nimemuacha tu, nimeamua kutulia nifanye mambo yangu” amesema Ebitoke.

Katika hatua nyingine amesema kwa sasa hawezi kuja kumtangaza mpenzi wake hadharani na kitu alichojifunza ni kukaa kimya katika maisha ya kimahusiano.

Nafasi za Ajira zilizotangazwa Leo Ijumaa

Je Wajua Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Madogo ya Kiume?

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WA NA MAUMBILE MADOGO?
Tatizo hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia ,hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wenzao,kwakawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6_8 vinginevyo mtu huyu ana matatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo baadhi ni,upungufu wa vichocheo (hornes) za gestrojen ambapo mwanaume anapobalehe vichocheo hivi (hormones)huchochea ujuaji wa uume.chango ambalo hushambulia nerve ambapo huharibu kabisa ukuaji wa uume, Punyeto ambayo huasili misuli ya uume,pia ngiri ambayo huleta maumivu ya tumbo kuunguluma na kujaa gesi,korodani moja kuvimba,kutopata choo vizuri,sababu hizi na nyinginezo hufanya uume kulegea na kisinyaa nakuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu zakiume (hamu ya tendo landoa hupungua au kuisha kabisa).NSUMBU,Nidawa inayozalisha hormones za gestrogene na kufanya uume kukua na kuongezeka mara dufu.NZAGI,Ni dawa ya kurudisha nguvu za kiume ,hutia hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha nakuponya kabisa tatizo hilo. Pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk 15 nakuendelea kwa tendo la kwanza.kumbuka dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji.Natunatibu kisukari,bp,ngiri,miguu kuwaka moto,namengine mengi.

WASILIANA OSTADHI JUMA KWA SIMU NO,0784002216 AU 0769597778

Juma Nature Awachana Wasanii Wanaotumia Nyimbo za Wasanii Wakongwe Awataka Kuomba Kibali kwa Wahusika

$
0
0
Juma Nature Awachana Wasanii Wanaotumia Nyimbo za Wasanii Wakongwe Awataka Kuomba Kibali kwa Wahusika
Msanii Juma Nature ambaye ni mkongwe kwenye game ya bongo fleva, amewataka wasanii wachanga kufuata sheria pale wanapotaka kutumia nyimbo za wasanii wakongwe jukwaani, ikiwemo kuomba kibali kwa muhusika na ikiwezekana amlipe fedha

Juma Nature ameyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Radio, na kueleza kwamba msanii mchanga kuimba nyimbo za msanii mkongwe jukwaani sio jambo baya na inaonyesha heshima, lakini ni vyema wakawa na makubalino maalum kabla hajafanya hivyo kuepusha migogoro.

Matokeo ya Mitihani ya Darasa la Saba Yatangazwa na NECTA

$
0
0
Matokeo ya Mitihani ya Darasa la Saba Yatangazwa na NECTA
Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba leo Oktoba 20,2017.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 au zaidi kati ya alama 250 wanazopaswa kupata.

Dk Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 na wavulana ni 321,015 sawa na asilimia 74.80 .

http://www.necta.go.tz/matokeo/2017/psle/psle.htm

Amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76.

Dk Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 70.36, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.40.

Katibu Mtendaji huyo amesema ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Hisabati umepanda kwa asilimia kati ya 4.25 na asilimia 10.05 kulinganishwa na mwaka 2016.

"Kwa masomo ya Sayansi na maarifa ya jamii ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 3.56 na asilimia 13.97 kulinganisha na mwaka 2016.

"Watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili ambalo ufaulu ni asilimia 86.86 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Kiingereza, lenye ufaulu wa asilimia 40.30," amesema Dk Msonde.

Katibu Mtendaji, Dk Msonde amezitaja shule 10 bora kitaifa kuwa ni St Peter iliyopo Kagera, St Severine  (Kagera), Alliance (Mwanza), Sir John (Tanga), Palikas  (Shinyanga), Mwanga (Kagera), Hazina (Dar es Salaam), St Anne Marie (Dar es Salaam), Rweikiza (Kagera) na Martin Luther (Dodoma).

Amezitaja shule 10 ambazo hazikufanya vizuri kuwa ni Nyahaa ya Singida, Bosha (Tanga), Ntalasha (Tabora), Kishangazi (Tanga), Mntamba (Singida), Ikolo (Singida), Kamwala (Songwe), Kibutuka (Lindi), Mkulumuzi (Tanga) na Kitwai A (Manyara).

Aliitaja mikoa iliyoongoza kitaifa kuwa ni Dar es Salaam, Geita, Kagera, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Mwanza, Katavi na Tabora.

Dk Msonde amesema mikoa iliyofanya vibaya ni Singida, Tanga, Tabora, Songwe, Lindi na Manyara.

Nassari Ashangazwa Kuwaona Ofisini Viongozi Waliotumia Kununua Madiwani

$
0
0
Nassari Ashangazwa Kuwaona Ofisini Viongozi Waliotumia Kununua Madiwani
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amesema kuwa bado anashangaa kuendelea kuwaona ofisini viongozi ambao aliowataja kwenye ushahidi wa kutumia rushwa kununua madiwani wa Chadema mkoani Arusha kwani watakuwa na nafasi kubwa ya kuharibu ushahidi huo.

Mh. Nassari amesema kwamba hofu yake kwa viongozi hao ni kwamba watakuwa na nafasi kubwa ya kuuharibu ushahidi huo kwa kuwa bado wamekalia madaraka hivyo wanaweza kufanya lolote kuhakikisha ushahidi ulioneshwa unaharibika ikiwa ni pamoja na upelelezi kufanyika kwa mashaka.

"Kinachonishikisha ni kuendelea kuwaona viongozi wale bado wapo ofisini. Huko nyuma tumeona watu wakiwajibika kisiasa pale wanapopata tuhuma kuhusu rushwa, huwa wanawajibika au kuwajibshwa. Hapa naona inakuwa ngumu kidogo kuhusu upelelezi wa kesi hii kufanyika . Mfano tunaona sehemu kwenye video Mkurugenzi anasikika akieleza ni namna gani ataelekeza wale madiwani waanze kulipwa kidogo kidogo lakini bado yupo ofisini hii inanisikitisha kwani upelelezi unakuwa na mashaka kidogo" Nassari

Aidha Nassari amesema ameshangazwa na kauli ya Mkurugenzi wa Takukuru, Valentino Mlowola kwamba yeye anaingilia upelelezi wao na kudai kwamba anachoamini yeye ni kwamba hajavunja sheria wala hajaingilia upelelezi wao kwani anachokifanya ni kuutaarifu umma kila hatua anayokua anaifanya.

Nassari ameongeza kwamba kauli zinazotolewa na Mlowola kama zina lengo la kumtia hofu basi kwake hofu hiyo anaamini haitafanya kazi kwake kwani kama ni kuzungumza na wanahabari wakati akiwa anapeleka ushahidi hataacha kwani huwa hazungumzii ushahidi alioubeba bali huwa anazungumzia hatua anazopiga.

Pamoja na hayo Nassari amesema hawezi kuzungumza kama haki itapatikana au la bali anachoamini Takukuru ni taasisi inayojitegemea hivyo hawataona haya kutenda haki ili ijulikane wateule wa rais wana hatia au vinginevyo.

Mpinzani Mkuu wa Uganda Kizza Besigye Akamatwa na Polisi

$
0
0
Mpinzani Mkuu wa Uganda Kizza Besigye Akamatwa na Polisi
Mpinzani mkuu wa Uganda na kiongozi wa Forum for Democratic Change (FDC) Dk Kizza Besigye amekamatwa.

Wengine waliokamatwa pamoja na Dk Besigye, ni mgombea urais wa FDC Patrick Amuriat na katibu wa uhamasishaji Ingrid Turinawe. Wote walikamatwa jana jioni walipokuwa katika kijiji cha Burambira, tarafa ya Bubaare, Rubanda walipokuwa njiani wakielekea wilaya ya Kabale wakitokea Rukungiri.

Kamanda wa polisi wa mkoa Denis Namuwoza amesema Besigye anasakwa Rukungiri ambako inadaiwa alitenda makossa kadhaa ya uhalifu Jumatano. “Anatafutwa Rukungiri kwa kutishia kumuua ofisa wa polisi na kuandaa mkutano haramu,” amesema Namuwoza.

Ameongeza kwamba Besigye aliamuru watu kuwarushia mawe maofisa wa polisi ambao walikwenda kutawanya wafuasi wa FDC waliokusanyika kumsikiliza Amuriat aliyekuwemo wilayani kuomba kura.

Walipoondoka kuelekea Kabale saa 11:00 jioni walikutana na kizuizi cha polisi barabarani katika eneo la Burambira, kilomita nne kutoka mjini Kabale. Amuriat aliposhuka kwenye gari ili kuzungumza na polisi alikamatwa na kuingizwa kwenye gari la polisi. Kadhalika polisi walizingira gari walilokuwa wakisafiria Besigye na Turinawe.

Wanasiasa hao bado walikuwa wanashikiliwa na polisi hadi saa 1:00 usiku wakati habari hii inaandikwa.

“Bado tunamshawishi ashuke kwenye gari ili tumpeleke Rukungiri,” amesema Namuwoza

Shaidi Ashindwa Kujua Kilichosababisha Kifo cha Kaka Yake

$
0
0
Mdogo wa Kanumba Hajui Kilichosababisha Kifo cha Kaka Yake
Wakati kesi ya mauaji ya mcheza filamu maarufu nchini, Steven Kanumba ikianza kuunguruma, shahidi wa upande wa mashtaka ameileza mahakama kuwa hajui aliyesababisha kifo cha msanii huyo.

Katika kesi hiyo iliyoanza jana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, Elizabeth Michael Kimemeta, ambaye pia ni msanii wa filamu akijulikana zaidi kama Lulu , ameshtakiwa kwa kosa la kumuua Kanumba bila ya kukusudia.

Lulu, ambaye yuko nje kwa dhamana, anadaiwa kufanya kosa hilo eneo la Sinza Vatican wakiwa nyumbani kwa Kanumba Aprili 7, 2012.

Aliposomewa maelezo ya awali mwaka 2014, Lulu alikana kuhusika na mauaji hayo, jambo ambalo liliilazimu upande wa mashtaka kuita mashahidi kuthibitisha shtaka hilo dhidi ya mshtakiwa.

Kwa mara nyingine, jana msaanii huyo aliposomewa shtaka hilo alikana kuhusika, ndipo upande wa mashtaka ukamuita shahidi wake wa kwanza kwa upande wake, Seth Bosco (30) ambaye ni mdogo wa marehemu Kanumba.

Shahidi huyo aliieleza mahakama kuwa alikuwa akiishi pamoja na Kanumba Sinza Vatican na kwamba siku ya tukio kaka yake na mshtakiwa ambaye alikuwa ni mpenzi wake, walifika nyumbani saa 6:00 usiku.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Faraja George, shahidi huyo alidai kuwa akiwa chumbani kwake alisikia kelele za ugomvi baina ya Kanumba na Lulu na kwamba baada ya muda Lulu alitoka na kumueleza kuwa Kanumba ameanguka.

Aliongeza kuwa alikwenda chumbani akamkuta Kanumba akiwa katika hali ya kukosa hewa, ndipo akamfuata daktari wao, kisha wakampeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili. Baada ya kuchunguzwa ikabainika kuwa alikuwa ameshafariki dunia.

Hata hivyo, alipoulizwa na moja wa wazee wa Baraza, Rajabu Mlawa baada ya kutoa ushahidi wake, kama anajua aliyesabisha kifo cha msanii huyo, shahidi huyo alisema hajui.

Mzee wa Baraza: Katika kumchunguza kwako marehemu baada ya tukio hilo, ulibaini kwamba marehemu alipata madhara gani?

Shahidi: Madhara niliyoyabaini ni kukosa pumzi

Mzee wa Baraza: Hayo madhara ya kukosa pumzi yalisababishwa na ugomvi ule?

Shahidi: Kwa hilo mimi siwezi kujua nini kilisabisha kukosa pumzi.

Mzee wa Baraza: Umesema kuwa ulipokwenda chumbani kwa marehemu ulimkuta ameanguka akiwa ameegemea ukutani, unajua ni nani alisababisha tukio la kuanguka?

Shahidi: Siwezi kujua ni nani aliyesababisha kwa sababu mimi sikuwemo mle ndani

Wakati akihojiwa na wakili wa mshtakiwa, Peter Kibatala, kama alikuwepo wakati sampuli za mwili wa marehemu zikichukuliwa kwa ajili ya vipimo vya maabara, kama ilivyoandikwa kwenye maelezo yake, alisema hakuwepo.

“Mimi sikuwepo wakati wa kuchukua sampuli za mwili wa marehemu. Alikuwapo ndugu yangu mwingine, mimi nilikuwepo kwenye mostmortem (taarifa ya kitabibu ya chanzo cha kifo) ya kawaida.”

Wakili Kibatala: Kwa hiyo aliyeandika hapa alikuwa akibuni?

Shahidi: Siwezi kusema kuwa alikuwa akibuni, labda kama ungemuuliza mwenyewe.

Wakili: Katika maelezo yako Polisi ambayo uliyaandika muda mfupi tu wakati wa tukio, kuna mahali ulipoeleza polisi kwamba ulipokwenda kumfuata Dk Paplas ulimwambia mshtakiwa abaki na marehemu?

Shahidi: Hakuna mahali ambapo kuna kipengele nilipomweleza polisi kuwa nilimuacha Elizabeth Michael na marehemu (Baada ya kusoma maelezo yake)

Hata hivyo, alipoulizwa tena na Wakili wa Serikali, George kuhusu kuwepo kwa tofauti ndogondogo katika maelezo yake aliyoyaandika polisi na yale aliyoyatoa kwenye ushahidi wake mahakamani, shahidi huyo alieleza kuwa yeye alikuwa akihojiwa tu na aliyekuwa akiandika ni askari.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Sam Rumanyika iliahirishwa na itaendelea tena leo kwa mashahidi wengine wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao.

Awali Wakili George aliieleza mahakama kuwa alitegemea kuwa na mashahidi wawili jana, akiwemo Dk Kageiya, lakini wakati wakifanya mazungumzo na shahidi huyo, aliwaeleza kuwa hajisikii vizuri na kuomba atoe ushahidi wake kesho.

Pia Wakili George aliileza mahakama kuwa wataomba kuongeza shahidi mwingine ili wafikie watano.

Afisa Mkuu wa Tume ya Uchaguzi Kenya Ezra Chiloba Ajiondoa

$
0
0
Afisa Mkuu wa Tume ya Uchaguzi Kenya Ezra Chiloba Ajiondoa
Afisa mkuu mtendaji wa tume ya uchaguzi nchini Kenya Ezra Chiloba anatarajiwa kuchukuwa likizo ya wiki tatu na hatoshiriki katika uchaguzi wa marejeo wa Alhamisi.
Kulingana na duru katika tume hiyo ya IEBC bwana Chiloba alifanya uamuzi huo wa kibinafsi wa kutoshiriki ili kujenga upya imani ya washikadau ambao wamelalamika kuhusu maafisa wa tume hiyo.
Afisa huyo amekuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka muungano wa upinzani Nasa kujiuzulu, huku mgombea wa urais wa muungano huo Raila Odinga akiitisha maandamano ya kumlazimisha kuondoka pamoja na maafisa wengine ikiwatuhumu kwa kusimamia vibaya uchaguzi wa Agosti 8 ambapo rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi.
Matokeo ya uchaguzi huo hatahivyo yalifutiliwa mbali na mahakama ya juu ambayo iliamua kwamba haukufanyika kulingana na sheria.
Bwana Chiloba anachukua likizo baada ya mwenyekiti wa tume hiyo wafula Chebukati kutaka maafisa waliotajwa baada ya uchaguzi huo kufutiliwa mbali kung'atuka.

Mahakama ya juu ilisema kuwa haikupata ushahidi kuhusu makosa yaliofanywa na maafisa lakini wanasiasa wamelalamika na kuishutumu tume hiyo kwa kujaribu kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo mbali na wizi wa kura.
Uamuzi huo wa kuchukua likizo ulijadiliwa na mwenyekiti na bwana Chiloba anaamini kwamba kutokuwepo kwake hakutaathiri maandalizi ya tume hiyo kusimamia uchaguzi ulio huru na haki .

Umoja wa Mataifa Umesitisha Shughuli Zake Zote Nchini Kenya Kuhofia Uchaguzi

$
0
0
Umoja wa Mataifa Umesitisha Shughuli Zake  Zote Nchini Kenya
Umoja wa Mataifa (UN) umesitisha shughuli zake zote nchini Kenya katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26.

Taarifa iliyotolewa Ijumaa na Msaidizi wa Katibu mkuu kanda ya Afrika Mashariki, Peter Drennan imesema umoja huo utasitisha kwa muda programu zake zote ambazo hazikuwa muhimu sana.

“Baada ya kufanya tathmini ya hali ya usalama nchini Kenya, ofisa mteule (DO) kwa ushauri kutoka Timu ya Usimamizi wa Usalama, ameshauri kusitishwa kwa warsha, mikutano, semina na makongamano na jumbe mbalimbali zisizo za lazima nchini Kenya walau kwa wiki moja kabla na wiki moja baada ya uchaguzi wa marudio kwa kura ya urais,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

“Ninakubaliana na ushauri wa DO na mamlaka husika kusitishwa kwa programu hizo ambazo hazina ulazima kuanzia leo Oktoba 19 hadi Novemba 2.”

Jana Alhamisi serikali ilitangaza kwamba Alhamisi ya Oktoba 26 itakuwa siku ya mapumziko kwa ajili ya kuruhusu wananchi kushiriki uchaguzi wa marudio.

Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani, Fred Matiang’i alitangaza kwamba siku hiyo imeandikwa katika Gazeti la Serikali kwamba itakuwa siku ya mapumziko kuwezesha Wakenya kushiriki kwa uhuru uchaguzi huo.

Tangazo hilo limekuja katikati ya mnyukano wa kisiasa na kuiweka uchaguzi huo katika hatihati ya kufanyika.

Jumatano, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati alielezea kukerwa kwake katika maandalizi ya uchaguzi wa marudio na akatangaza wazi kuwa hawezi kuhakikisha uchaguzi wa kuaminika.

Chekubati alisema kutokana na kupanda sana kwa hofu ya kisiasa nchini, alipendekeza Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wakutane kwa mazungumzo kabla ya uchaguzi huo

Kocha Kagera Sugari Asema Timu Yake Bado Inatafuta Ushindi

$
0
0
Kocha Kagera Sugari  Asema Timu Yake Bado Inatafuta Ushindi
Kocha wa klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara Meck Mexime amesema timu yao bado inatafuta ushindi.

Meck ameyasema hayo leo kuelekea mchezo wa raundi ya 7 dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.
“Kikubwa sisi tunatafuta ushindi kwasababu hatujaupata tangu ligi ianze, hivyo tumejiandaa kutafuta ushindi na pointi tatu”, amesema Meck Mexime.
Mexime ambaye ni mchezaji na kocha wa zamani wa timu ya Mtibwa Sugar ameshindwa kuonesha makali ya msimu uliopita tangu ligi ya msimu wa 2017/18 ianze ambapo hajafanikiwa kupata ushindi kwenye mechi Sita za mwanzo.

Hadi sasa Kagera Sugar inaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 2. Wakata Miwa hao wa Kaitaba wamepoteza mechi 4 na kutoa sare mechi mbili. Wakati Mwadui wanashika nafasi ya 12 ikiwa na alama 6 baada ya michezo Sita.

Install Application ya MCHAMBUZI Kwenye Simu yako Kusoma Habari na Matamko ya Wanasiasa Kila Siku

$
0
0
Maswala ya Siasa na Matamko ya kila siku ya Wanasiasa Hakikisha Umedownload App ya Mchambuzi Kwenye simu yako
BonyezaHAPA

Kama we ni Mpenzi wa Habari za Siasa Usipitwe na Hii Application ya Mchambuzi..... 
Bonyeza HAPAKudownload kwenye Simu yako


JE Una Upungufu wa Nguvu za Kiume, Kukosa Hamu ya Tendo, Kufika Kileleni Haraka na Kushindwa Kurudia Tendo ?

$
0
0
JE, UNA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KUKOSA HAMU YA TENDO, KUFIKA KILELENI HARAKA NA KUSHINDWA KURUDIA TENDO AU MAUMBILE MADOGO YA UUME?
       Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana duniani kote. Kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume husababishwa na mambo mengi kama KISUKARI, UNENE ULIOPITILIZA, KUJICHUA  (MASTER BLASHION), HOMONI kushindwa kufanya kazi ipasavyo n.k.
     Upungufu wa nguvu husababisha tendo la ndoa kutokufanyika kwa kujiamini na kwa usahihi na hivyo kusababisha ndoa na mahusiano kuvunjika.
      BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa
☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni
☆Uume kusinyaa katikati ya tendo
☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.
     Kwa kutumia mimea na matunda @markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL:- kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6 hadi 7  @150,000/=
3.VigRX CREAM:- ni gely iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile kwa wastani wa inch 6.5 hadi 8 na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200,000/=
4.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150,000/=
5.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni @130,000/=

      BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA NA ZIMETHIBITISHWA KIAFYA.
    KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WETU WA 
  ulipo duniani kwa (+255)
          0767447444 na
              0714335378
        UTAPATA HUDUMA
    NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.

   

Mkuu wa Kanisa la KKKT Frederick Shoo Asimulia Sauti ya Lissu Ilivyomtoa Machozi

$
0
0
Mkuu wa Kanisa la KKKT Frederick Shoo Asimulia Sauti ya Lissu Ilivyomtoa Machozi
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo amesimulia alivyobubujikwa machozi baada ya kusikia sauti ya Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu.

Dk Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, amesema hayo baada ya Jumatano Oktoba 18,2017 Lissu kutoa salamu akiwashukuru Watanzania kupitia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7,2017 mjini Dodoma.

Sauti ya Lissu katika video hiyo ilikuwa ni ya kwanza kusikika tangu apelekwe jijini Nairobi Septemba 7.  Alisikika akiwashukuru madaktari wa Nairobi na Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa kuokoa maisha yake.

Pia, amewashukuru viongozi wa dini na wananchi kwa kumuombea, na taasisi za kitaaluma  ndani na nje ya nchi ikiwemo TLS ambazo zilionyesha mshikamano mkubwa.

Akizungumza na Mwananchi, Askofu Shoo amesema alijikuta akitokwa machozi aliposikia sauti ya Lissu, akisema kupona kwake ni onyo kwa wale waliohusika.

 “Ninazidi kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyomuokoa na anavyozidi kumpa uponyaji. Kupona kwa Lissu ni jibu la Mungu na onyo kwa wale wote waliohusika. Mungu amesema hapana,” amesema.

Askofu Shoo amesema, “Mwenye masikio na asikie. Uhai wa mwanadamu ni kitu cha kuheshimu. Tusijaribiwe kujichukulia madaraka ya kuondoa uhai wa mtu hata kama uwezo tunao kwa maana Mungu hataki na wala hataacha kumwadhibu yeye aondoaye uhai wa ndugu yake kwa hiana.”

Shaidi wa Pili Aeleza Alivyokuta Panga Chumbani mwa Kanumba

$
0
0
Shaidi wa Pili Aeleza Alivyokuta Panga Chumbani mwa Kanumba
KESI inayomkabili muigizaji wa kike, Elizabeth Michael ‘Lulu’,  leo Ijumaa, Oktoba 20, imeendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo shahidi wa pili upande wa Jamhuri ametoa ushahidi wake.

Shahidi huyo aliyekuwa daktari wa familia ya marehemu Steven Kanumba ameeleza kuwa siku ya tukio alifuatwa na mdogo wa Kanumba, Seth Bosco kwenda nyumbani kumpima ambapo alifika na kumpima shinikizo la damu na sukari.

Aidha mpelelezi ACP Ester Zephania kutoka Kituo cha Polisi Oyster Bay ambaye alikwenda kumkamata Lulu na kufanya uchunguzi wa tukio hilo, naye ametoa ushahidi wake.
Baada ya ofisa huyo kueleza hatua zote walizozifanya pia ameieleza mahakama kwamba walikuta mchirizi wa rangi nyeusi kwenye ukuta wa chumba cha Kanumba na panga lililokuwa chini ya uvungu wa kitanda.

Mbali na hayo pia ameieleza mahakama kwamba baada ya kuandika fomu ya PF3 kwa watu waliofika polisi kutoa taarifa ambao ni Seth  na datktari wa familia hiyo.
Kilichofuata ni namna ya kumkamata mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano ambapo shahidi wa pili (daktari) ndiye aliandaa mtego siku ya Aprili 7, 2012 na kufanikiwa kumkamata Lulu maeneo ya Bamaga-Mwenge na kupelekwa kituo cha Polisi Oyster Bay, Kinondoni.

Walipofika huko ACP Ester ameieleza mahakama kwamba Lulu alipelekwa kwa Ofisa Mkuu wa Upelelezi ambaye alimtaja kwa jina la Wambura na baada ya mahojiano afande Ester aliletewa taarifa  kwamba Lulu alikuwa akijisikia maumivu na hivyo alipelekwa hospitalini.
Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Jaji Sam Rumanyika baada ya mashahidi hao kutoa ushahidi  na itaendelea kusikiliza ushahidi wa nne Oktoba 23 mwaka huu.
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images