Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live

Aibu! Vunja Jungu yamtokea Puani Njemba…Anaswa akila URODA na Mke wa Mpangaji wake GESTI

$
0
0
Vunja jungu! Saa kadhaa kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali ameibua sekeseke kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti), kisa kikidaiwa ni mchepuko akihusishwa na mke wa mpangaji wake, Ijumaa Wikienda lina kisa na mkasa.

Wakati ikirandaranda mitaani kutega mingo, Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilipokea mchongo kuwa kuna timbwili kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar ambapo walifika eneo la tukio na kushuhudia kasheshe hilo la aina yake.

OFM ilimshuhudia mzee huyo akichomolewa kutoka chumbani huku damu zikimvuja baada ya kula kichapo kutoka kwa jamaa na ndugu wa mwanaume aliyedai kuwa jamaa huyo alikuwa anamsumbua mkewe.

Kwa mujibu wa mashuhuda, kabla ya jamaa hao kuingia chumbani humo kwanza walivunja mlango wa chumba hicho baada ya kupata idhini kutoka kwa msimamizi wa gesti hiyo kufuatia  baba mwenye nyumba huyo kukahidi kuwafungulia mlango ili wamchukue mke wa ndugu yao aliyedaiwa kuwa ndani na mzee huyo.

Walidai kwamba mzee huyo ambaye ni baba mwenye nyumba, alikuwa akimtolea udenda mke huyo wa mpagaji wake ambaye ni jirani yake huku akimsumbua mara kwa mara kwa simu na ujumbe mfupi wa SMS.

Ilidaiwa kwamba kufuatia usumbufu huo, mke huyo alimweleza mumewe lakini mumewe hakuamini kama kweli baba mwenye nyumba alikuwa  akimtaka mke wake kimapenzi.
Ilisemekana kuwa mume huyo alimweleza mkewe ili aamini kweli baba mwenye nyumba alipania kumtaka basi amkubali ili amkute naye gesti amkomeshe kwa tabia hiyo ya baadhi ya wenye nyumba ambao huwataka wake wa wapangaji wake.

“Nilimwambia mke wangu amkubali kwa sababu nilikuwa na nia ya kukomesha tabia yake ya kutongoza wake wa wapangaji wake, akamwita Buguruni ndipo nikawapigia ninyi waandishi wa habari ili mje mchukue ushahidi,” alisema mume huyo.

Baada ya kukutwa gesti humo, mzee huyo aliomba msamaha kwa mpangaji wake huyo na kuahidi kulipa fidia ambapo aliwaandikia cheki feki kisha akakimbilia Kituo cha Polisi cha Buguruni na kufungua shauri kuwa alitekwa, akapigwa kisha akapelekwa gesti.

Shauri hilo ambalo liliandikishwa kwa jalada namba BUG/RB 6182/2014- utekaji. Mzee huyo alidai kutekwa na mpangaji wake huyo na kumpeleka nje ya mji kisha kumpiga ili kuua soo.
Hadi gazeti hili linaanua jamvi kituoni hapo, polisi walikuwa wakichunguza ili ukweli ujulikane.

CREDIT: GPL

Aliye Kuwa Akizuia Magari Yasikanyage Maiti Barabarani Nae Agongwa na Gari na Kufariki Hapo Hapo

$
0
0
WATU wawili wamefariki dunia jijini Dar es Salaam juzi akiwamo Emmanuel Ndahani (39) mkazi wa Kibamba, aliyegongwa na gari na kufariki dunia alipokuwa akiweka alama za matawi kuzuia gari zisikanyage maiti.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema Ndahani aligongwa na gari isiyofahamika kwa kuwa lilikimbia baada ya ajali hiyo.
Alisema Ndahani alikuwa akitaka kuzuia magari yasiukanyage mwili wa Onesmo Yarimunda aliyefariki dunia baada ya kugongwa na basi la Prince Muro alipokuwa akivuka barabara.

Kamanda Wambura, alisema Yarimunda (36), mkazi wa Kibaha aligongwa na basi hilo aina ya Scania, juzi, saa 3 usiku maeneo ya Kibamba.
Maiti zimehifadhiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha. Dereva wa basi la Muro, Boniface Chuwa (36) mkazi wa Kibaha anashikiliwa na polisi.

Bongo Billionaire Le Mutuz Aopoa Kifaa cha Uganda Billionaire Zari ?

$
0
0
Bongo Billionaire Le Mutuz Aopoa Kifaa cha Uganda Billionaire Zari 
Really? Bilionaire

Jina la Diamond Laandikwa Kwenye Hollywood Walk of Fame

$
0
0

Diamond yupo jijini Los Angeles Kuhudhuria utoaji wa tuzo za BET jpil trh 29..na moja ya kitu ambacho itakua ni arama na kumbukumbu kubwa kwake,ni jinalake kuandikwa kwenye sakafu ya HOLLYWOOD WAKE OF FAME ambapo anakuwa mtanzania wa kwanza katika historia pale huandikwa majina ya watu maarufu/mashuhuri duniani kama heshima..mmoja ya mastaa ambao majina yao yameandikwa pale ni bruce wills,michael jackson ,JBieber na wengine wengi..Hongera My big boss,ni heshima kwako na sisi pia ..na Mungu ajalie kesho ushinde.

Mtangazaji Regina Mwalekwa Aikimbia Clouds FM, Apata Deal la Nguvu Redio Kubwa

$
0
0
Leo Asubuhi Mtangazaji wa Clouds FM Mwanadada Regina Mwalekwa Ametangaza wazi kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM kuwa anaacha kazi rasmi katika kituo hicho alichofanya kwa muda mrefu, Regina Mwalekwa aliwashukuru Watangazaji na Mabosi wa Kituo cha Clouds kwa Kumlea Vizuri katika kipindi chote alichokuwa hapo.
Regina Mwalekwa hakusita kusema sababu ya Kuacha kazi kituo hicho ambapo alisema amepata kazi katika Shirika la Utangazaji la BBC.

Uzuri Wooote...Kilichonitumua ni Harufu Mbaya ya Ikulu

$
0
0
Washkaji wote chuo walikuwa wanamtolea macho huyu dada,alikuwa ni mzuri sana,yaani kwa ukubwa na shape ya makalio yake alibandikwa jina la ''MARKING SCHEME''..yaani makalio yake yanasahihisha makalio yote ya madem wa chuo,niliimpata kirahisi..hata nisiseme nilimpata,alinipata kirahisi sababu sikumtongoza,alijileta mwenyewe na kwa kasi ya hatari mpaka nikastuka,siku zikaenda ikafika day ndo gem inapigwa sasa,lita nini sana tu,sasa ile naanza piga issue,mazee..hiyo harufu!nlijikausha nkapiga kimoja lakini harufu mikononi iliisha after two days,nikaanza mpotezea na hata ham naye ikaisha,wadau wakaanza sema nimetoswa...ilhali nlichokutana nacho nakijua mwenyewe,kweli vingine vione kwa nje tu,huko ndani ni balaaa!

Hii ni listi mpya ya Forbes ya most powerful celebrities na pesa walizoingiza kwa mwaka

$
0
0
Forbes mtandao unaoaminika kwa kutoa list mbalimbali za uhakika hivi sasa wametoa list ya most powerful celebrities pamoja na pesa walizoingiza tangu June 2013 hadi June 2014.
Beyonce amefanikiwa kunaa namba moja akimuacha mume wake nafasi tano nyuma ambaye yupo namba 6. Top 10 ina watu maarufu kama LeBron James,Oprah,Rihanna,Jay Z,Katy Perry na wengine,
Hii ndiyo list ya top 10 na pesa walizoingiza kwa muda wa miezi 12
1) Beyonce: $115million
2)LeBron James – $72million
3)Dr. Dre – $620million
4)Oprah Winfrey- $82million
5) Ellen DeGeneres – $70million
6)Jay Z – $60million
7)Floyd Mayweather- $105million
8)Rihanna – $48million
9)Katy Perry- $40million
10)Robert Downey Jnr – $75million.
Note : Hii ni list ya most powerful celebrities na sio most richest celebrities.

Msajili: Mbowe, Dk Slaa Hawana Sifa Kugombea Uongozi Tena Chadema Baada ya Kipengele cha Ukomo wa Uongozi Kuondolewa Kinyemela

$
0
0
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa hawana sifa za kugombea tena uongozi wa chama hicho kwa kuwa wanabanwa na katiba yao.

Akizungumza jana ofisini kwake baada ya kuzungumza na Mbowe, Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza alisema walipata malalamiko na kuyafanyia kazi, ikiwa ni pamoja na kupitia kumbukumbu walizonazo na kubaini kuwa kipengele cha ukomo wa uongozi kiliondolewa kinyemela katika katiba ya chama hicho.

Alisema kwa kawaida vyama vyote vinapofanya mikutano huwapelekea muhtasari, hivyo Chadema nacho kiliwapelekea kumbukumbu ya Mkutano Mkuu wa mwaka 2006, lakini hakuna sehemu yoyote iliyoondoa ukomo wa uongozi.

“Hivyo, hawa tayari wana vipindi viwili, wakichaguliwa katika uchaguzi unaokuja hatutawatambua. Wakitaka wabadili katiba kwa njia halali ambayo ni ya mkutano mkuu na si vinginevyo,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mbowe alisema hakuwa tayari kulizungumzia, akieleza kwamba amefika kwenye ofisi hiyo ya Msajili kwa masuala mengine.

“ Siwezi kulizungumzia suala hilo kwa sasa, likifikishwa kwenye Kamati Kuu ndipo nitalielezea,” alisema Mbowe.

Baadaye Ofisa wa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema kwamba Msajili alimwita Mbowe ili kumshawishi asaidie wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) warejee katika Bunge la Katiba.

“Mwenyekiti alibainisha kuwa msimamo wa Ukawa upo wazi kwamba hawatarudi katika Bunge hilo hadi pale maoni ya wananchi yatakapoanza kujadiliwa na msimamo huo hautabadilika,” alisema Makene akimkariri Mbowe.

Makene alisema baada ya kutoa msimamo huo, hakuna maongezi mengine yaliyoendelea baina ya Mbowe na Msajili.

Alipoulizwa iwapo Msajili alionyesha nia pia ya kuushawishi upande wa pili wanaotaka serikali mbili, Makene alisema hawezi kufahamu, japo kwa nafasi yake, Mutungi ana uwezo wa kufanya hivyo.

Alipoulizwa iwapo Msajili pia alizungumzia suala la ukomo wa uongozi linalodaiwa kubadilishwa kinyemela, alisema: “Kuhusu hilo Chadema tunafuatilia kwa kina taarifa zinazozagaa zikionyesha correspondence (barua) zinazotoka kwa Msajili wa Vyama juu ya Chadema na tutakapokamilisha tutatoa taarifa.”

Gazeti hili jana lilichapisha taarifa iliyonukuu barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chadema, ikieleza kuwa kipengele hicho katika Ibara ya 6.3.2 (C) kiliondolewa kwenye katiba bila idhini ya mkutano mkuu wa chama hicho.

Jaji Mutungi alisisitiza kuwa mkuu wa chama hicho ndiye wenye mamlaka ya kurekebisha katiba, hivyo baada ya kupitia muhtasari wa Mkutano Mkuu wa mwaka 2006 suala la kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi halikuonyesha kujadiliwa katika mkutano huo.

Hata hivyo, akizungumza kwa simu juzi, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema kipengele hicho kiliondolewa kwa vikao vya chama ambavyo ni wilaya na mkoa.

Hoja hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na ambaye sasa si mwanachama wa chama hicho

UCHAGUZI MKUU SIMBA: Aveva apata ushindi wa kimbunga

$
0
0

Evans Aveva ameula baada ya kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa klabu ya Simba katika uchaguzi mkuu uliofanyika juzi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Aveva alipata ushindi huo wa mithili ya kimbunga baada ya kupata kura 1845 na kumgaragaza mpinzani wake Andrew Tupa aliyepata kura 387 huku kura sita zikiharibika.

Katika nafasi ya Makamu wa Rais, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 1043 huku Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ akipata kura 413 na Swedy Mkwabi akipata kura 300.

Awali, aliyekuwa mgombea Urais wa klabu hiyo, Michael Wambura alizuiwa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba kuingia kwenye Ukumbi.

Wambura, alienguliwa kwanza kwa kuwa amesimamishwa uanachama na baadaye kwa kukiuka taratibu za uchaguzi, alishindwa kupiga kura kutokana na uamuzi wa kumzuia kuingia ukumbini.

Kwa mujibu wa wasimamizi waliokuwa wakihakiki uhalali wa wanachama kwenye uchaguzi huo, jina la Wambura halikuwapo katika orodha ya wanachama wanaostahili kupiga kura.

Wambura kama walivyokuwa wanachama wengine, walifika katika eneo la uchaguzi kwa ajili ya kukamilisha haki hiyo ya kikatiba, lakini alionekana kushangazwa na uamuzi huo wa kuzuiwa kupiga kura.

Jibu alilopewa lilimfanya kuondoka maeneo hayo kwa hasira majira ya saa 4:00 asubuhi. Wakati hayo yakitokea, wafuasi wake walionekana kukasirishwa na kitendo hicho na kutaka kufanya fujo, hata hivyo askari waliokuwapo maeneo hayo walizima jitihada hizo.

Katika mkutano huo wa uchaguzi ulioanza rasmi saa 5:00 asubuhi, lilipomalizika zoezi la wagombea kujinadi, zoezi la kupiga kura liliibua vurugu nzito kutokana na wanachama wengine kukosa karatasi za kupigia kura kwa nafasi za rais na makamu wake.

Hali hiyo ilichangiwa na wanachama kushindwa kuwa na utulivu. Hata hivyo, baada ya muda zoezi hilo liliendelea kukiwa  na utulivu mdogo katika zoezi hilo la kupiga kura lililoanza saa 9:00 alasiri na kura kuhesabiwa saa 11:00 jioni.

BABY MADAHA: Siolewi kwa kufuata Mkumbo…Pesa Ndiyo Kila Kitu Kwangu

$
0
0

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amesema anaishi katika staili ya kivyake hivyo kamwe hawezi kuolewa kwa kufuata mkumbo kama ilivyo kwa wasanii wengine.

Akipiga stori na mwandishi wetu, Baby Madaha alikiri kuwa ana mchumba ambaye ni Joh Kairuki, anampenda sana ila katika suala la kufunga ndoa bado yupoyupo sana kwa sababu haolewi kwa kufuata mkumbo kwani amejifunza kupitia kwa walioolewa na kuachika.

Nitaolewa nitakapokuwa tayari siyo kwa kufuata mkumbo vinginevyo bora nibakie hivihivi kwa sababu pesa kwangu ndiyo kila kitu, mambo mengine yanafuata,” alisema.

Henry kilewo 'Hebu Msajili wa Vyama Tumia Akili Yako Acha Kukubali Udhalilishaji Unaofanya Kwa Kupitia CCM"

$
0
0
Nimesikitika sana siku ya leo kwakuona taarifa juu ya msajili na chama changu cha chadema, hivi msajili umekubali kuitumikia akili yako kwa kuiweka mfukoni ili uisaidie ccm 2015? Kama katiba ya 2006 inakasoro katika kifungu ulichokitaja, inamaana na sisi viongozi wa chadema tuliyochaguliwa 2009 hatupo kihalali ? Pamoja na wabunge, madiwani na wenyeviti wa mitaa?
Hebu msajili tumia akili yako acha kukubali udhalilishaji unaofanya kwa kupitia ccm... Ni hivi huwezi kuzuia mabadiliko hata kidogo tena ukituuzi zaidi maandamano ya wakati huu tutayafanyia nyumbani kwako kudai haki yetu.
1. Mwaka 2006 CHADEMA haikufanya marekebisho ya ibara au katiba, iliandika katiba mpya!
2. Msajili wa Vyama vya Siasa hana authority juu ya katiba yetu bali sisi wenyewe!
Henry kilewo
Katibu wa chadema mkoa wa kinondoni
Na kanda maalum ya Dar es salaam

DIAMOND PLATNUMZ...Has Really Changed This Game na Anastahili HESHIMA Kama Balozi...HATE IT OR LOVE IT

$
0
0
TUMHESHIMU HUYU MTU:NALETA HOJA TASHTITI ALFAJIRI NA.MAPEMA
Nazidi kuchimba na najiuliza tu maswali...Walisema anatumia Ndumba...Je,Ndumba inavuka bahari??
TUTAZAME HISTORIA KIDOGO
MWAKA 2011 tuzo ya BET ya African Act ilitua mikononi mwa D"BANJ na 2FACE IDIBIA(Shared) wakiwa wameshindana na wakali wafuatao:
1.ANGELIQUE KIDJO-Mnaojua Muziki huyu amewahi kuwa GRAMMY WINNER...lakini HAKUCHUKUA!
2.FALLY IPUPA-HAKUCHUKUA
3.TEARGAS kutoka SA-HAWAKUCHUKUA
4.D"BLACK-Ghana-HAKUCHUKUA
Mwaka 2012 tuzo ikaenda kwa watu wawili tena,WIZKID na SARKODIE na waliofeli kuchukua ni CAMP MULLA(Kenya),2FACE IDIBIA,ICE PRINCE ZAMANI(Nigeria),LIRA(SA), na MOKOBE(Mali)
Mwaka 2013 tuzo ikaenda kwa ICE PRINCE ZAMANI(wengi wetu hata hatumjui kudadeki),ikiwa ni his SECOND NOMINATION, 2YEARS IN A ROW,na alishindanishwa na vichwa kama 2FACE IDIBIA(Nigeria),TOYA DELAZY na DONALD(SA),R2BEES(Ghana) na RADIO AND WEASAL(Uganda)
Mwaka huu,DIAMOND ameshindanishwa na vichwa kama MAFIKIZOLO(SA) ambao ni washindi wa Tuzo 8 kwenye SAMA mwaka huu na wamepafomu live BET mwaka huu,SARKODIE(Ghana) ambaye ameshashinda BET mwaka juzi ila MWAKA HUU KAFELI...TIWA SAVAGE(Nigeria) na DAVIDO ambaye ni mara ya kwanza kuwa nominated na AMESHINDA
Kama SARKODIE,Rapa maarufu afrika nzima,na mshindi waTuzo hii ya BET mwaka 2012 alongside WIZKID AMEFELI na amekubali kushindwa SISI NI NANI???
HEBU IMAGINE...
No PSQUARE hata kwenye kushiriki
No IYANYA hata kwenye kushiriki
No WIZKID(Winner 2012) hata kushiriki
No JOSE CHAMELIONE mkongweeee
No DON JAZZY(kama humjui Google)
No DBANJ...Jamani!
DIAMOND...has really changed this game na anastahili HESHIMA kama Balozi...HATE IT OR LOVE IT...Tuzo hii SI RAHISI kuipata maana hata hao MAGWIJI wa Muziki huu WANAFELI PIA sembuse DIAMOND ambaye hii ni 1st time Nomination??Ice Prince alikosa 2012 akaichukua 2013...Diamond also CAN!
Naruhusu Hoja kama bado kuna mamluki wanaobwabwaja bila hoja..ASANTE!
-Seth

Tid Amtukana Ray C 'Bitch Leave Me Alone' ni Baada ya Ray C Kumuomba Wazungumze

$
0
0
Harakati za Rehema Chalamila aka Ray C kukiokoa kizazi cha Tanzania katika janga la matumizi ya madawa ya kulevya si rahisi kama unavyodhani.

itihada za kutaka kumuokoa muimbaji mwenzie, TID anayedaiwa kuwa mtumiaji mzuri wa ‘ngada’ zimegonga mwamba na kujikuta akiambulia matusi mazito. Picha lilianza baada ya TID kuweka picha Instagram ya wimbo wake Asha uliorudiwa tena na Lamar katika mradi wake wa ‘Refix’ na kuandika: Listen to this mix….once again from @lamarfishcrab.


Ray C alicomment chini ya picha hiyo: Come let’s talk Tid ur the best musician in east Africa pls lets talk @tidmnyama.” Pamoja na Ray C kutofafanuwa anataka waongee kuhusu jambo gani, TID alitafsiri ujumbe huo moja kwa moja kuwa Rehema anataka kumhubiria story zake za ‘Methadone’.

Bi*ch leave me alone am not ur type also I don’t need shit from you,ur mistake is yours nakuomba can u jus f*ck off,help ur boyfriend,I have never liked you,full stop,” aliandika TID.

Majibu ya TID yaliwashangaza followers wake wa Instagram waliojiuliza kipi hasa cha kumfanya ajibu kwa matusi kama hayo kwa ujumbe ambao pengine haukuwa na maana aliyoifikiria yeye.

Ray c anataka kuongea nae ili aache madawa nyie mnashabikia uozo @rayc1982 usife moyo my dada mkazanie ataacha tu anajishaua na matus ni maunga anayovua hayo huna lolote unataka kusaidia uache maunga yako eti back off ny*o back off my foot unajifanya mnyama mnyama gan anakula sembe bwege ww @tidmnyama,” aliandika mmoja.

Hv wew tid huo usela mavi utaacha lini wew teja utakufa na maunga hayo acha kujishauwa @rayc1982 anataka kuongea na wew unajishauwa ili uonekane wa maan hv hujui unajimaliza taratibu na kujishushia hadhi yako unadhani leo umepunguza mashabik wangapi huna akili kweli unga umekutenda pole sana rayc sio type yako wew tid kwa kipi ss rayc akushobokee mbn huna hy hadhi yakuwa na mrembo km rayc fyuuuuuu ……………ms**ge kweli wew na this time nahis wew unamfollow langa ny*ko weeeeeeeeetena ukome kumshobokea rayc tutakupanga teja hilooooooooooo nautaf**wa mk**d hapo stereo kutwa uko chini ya mwembe unabembea macho km chura mnyama gani wew kenge tu mnyama teja mxiiiiiiuuuuuu,” yalisomeka maoni mengine.

Oscar de la Hoya kaulizwa live kwenye ESPN kuhusu addiction na kakubali anapata matibabu sasa hivi. Nani asiejua tid ni teja?!? Whether public or privately. @tidmnyama needs #help. What can tid give @rayc1982 apart from pills to pop?! He is a fucking junk who needs #help. #Methadone will do. Alcohol. Drugs won’t make you Real! Real is God. Hardworking. Responsibilities. You have a kid tid who looks up to you.. Tyson. Eminem.. Our own @rayc1982 all had addition but they knew it was wrong and rectified their mistakes,” yalisomeka mengine.

Kwanini Diamond Alimuacha Wema Sepetu Tuzo za BET?

$
0
0
Kama unakumbuka vizuri kwenye tuzo za MTVMAMA...Msanii diamond aliongozana na KIJIJI..yani ni kundi kubwa la watu, kuanzia kina tale, Fella, Aunt Ezekiel, na wengine kibao akiwepo mama la mama yani Wema Sepetu:
BUT hizi za BET naona kijana amepunguza timu na hadi mama la mama amepigwa chini yani hajaibuka nae...Ukizingatia kwamba kupitia SOSHO MIDIA, Wema Sepetu alishaleta mbwembwe za kuwenda kwenye tuzo hizo na kuonana na ndugu zake wanaoishi huko marekani....

Sasa tunajiuliza je, jamaa aliona ni gundu kwenda nae (siunajua mambo ya kiswahili tena)? au nauli?
Hehehe yetu macho moshi tumeshauona.....Kabla sijakuacha ujiulize nawewe...Kingine tena hiki hapa....Tofauti na MTV Wema sasa hadi sasa  hivi (muda huu naposti hii kitu)hajasema chochote kwenye mitandao ya kijamii kumtia moyo MUPENZI WAKE

Watangazaji watanzania mjifunze kutoka kwa Regina Mwalekwa

$
0
0
Kwanza Hongera Kwa Kupata Kazi Mpya BBC
Yaani hakuna watu wananikera kusikiliza kama hawa vijana ambao wanajiita "wanavipaji" vya utangazaji na mbaya zaidi hawana taaluma ila wanaishi kwa kudra za Mungu tu.Ebu angalia ubunifu na weledi alionao Regina Mwalekwa kwenye utangazaji na hata ubunifu wa vipindi vyenye maudhui ya kuelimisha na si kukaraisha msikilizaji.

Leo hii mpaka nawashangaa TCRA kwa kushindwa kuchukua hatua kwenye radio za hawa watu ambao wanajiita ni radio ya watu kama vile radio zingine ni za mapaka vile.

Kipindi cha mida ya saa fulani za asubuhi mpaka muda wa maakuli,yaani hiki kipindi mimi ningekuwa nina mamlaka huko TCRA ningekifungia kabisa.

Sikatai kuna maswala wanazungumzaga yanagusa jamii ndio,lakini sio kipindi ambacho unaweza sema kina caliber ya ushindani katika tuzo za kimataifa na ndio maana wanakosa hata tuzo za TASWA sijui zile!

Mimi sio mwandishi lakini nadhani hakuna ethic inayomtaka mwanahabari kuongea mambo ya ajabu katika radio ya umma nkimaanisha inayosikilizwa na watu wengi na wa rika mbalimbali.. 

Yani radio hyo ya Mikocheni yenye vijana wanaovaa milegezo ndio watangazaji ambao maneno machafu midomoni mwao ni kama sala kitu ambacho kilimtofautisha sana dada Regina na vijana hawa,lakini pia kwakuwa Regina alitambua kuwa radio ya vijana wanahitaji kufahamu lugha adhimu ya kiswahili aliamua kuwa na segment ya angalau neno moja kila siku ili vijana waelewe walau matumizi ya maneno.

Ila la kheri Regina na kama hao mabinti na vijana wanaosema "wanavipaji" watashindwa kujiendeleza kielimu wakiendelea kubweteka kwakuwa bosi anawapa vocha na wanajulikana na vijana basi Mungu awasaidie lakini wataishia hapa hapa na hawatakaa wapate exposure katika maeneo mengine.
By Bomouwa Via JF

E. Mbasha kwa Nini Hukujibidisha Upate Hela Zako?

$
0
0
Pole kwa yaliyokukuta but cha kujiuliza pamoja na kuwa kwenye game zaid ya miaka 10 (kwa ufadhili wa Flora) iweje leo unalia lia tu kwenye media kuwa Flora kakuacha? 

Kwani huna kisomo, nguvu na maarifa ya kukufanya upate hela na ujitegemee? Acha kulia lia na media eti umeporwa mke. La muhimu jipange uanze upya na ukipata pesa ama Flora au mwanamke yeyote atakuja mwenyewe (bila kutongoza) otherwise usipojibidisha na kufanya kazi unaweza kuandika historia mbaya (Cameron).

We mwanaume pambana.

Mwanaume kama hujui kutunza utaishia kuitaga shemeji

$
0
0
Sasa leo nataka niseme kitu kimoja kwenu wanaume,

Mwanamke mzuri anahitaji pesa jamani,usitegemee utampata mwanamke mzuri kwa sasa hivi kama hauna mkwanja mrefu,hilo sahau kabisa,

Vinginevyo utaishia kuwaita mashemeji tu kwa hiyo wakati ukimtamani mdada mrembo ujue hadi unamuona mrembo ni pesa hizo.

Unakuta mkaka unawasiliana nae wiki nzima,unamjib text,akipiga unaongea nae fresh haha unashindwa kutuma tigo pesa hata elfu 30 useme jiunge bando?

Wallah mie nasemaje kama huna pesa au hujui kutunza usinisumbue kabisa coz hatutoendana
Unataka meeting na mie hutumi hata laki 1 ya saloon licha ya mafuta ya kukufata inahuuu
Badilikeni basi.

Touching Story:Mchungaji wa Kanisa Aamua Kumuoa Kahaba

$
0
0
Hili ni simulizi la  kweli linalomhusu mwanamke  mmoja ambaye alikuwa ni kahaba  wa makahaba......

Mwanamke  huyu  alijitambua  vyema  na  kukiri  ndani ya  nafsi yake kuwa hawezi  kuolewa  na maname  yoyote  yule  maana  jamii yote ilikuwa inamtambua  kwa uchangudoa  wake......

Kwa hiyo , ili kurahisisha mambo na  kuifanya  biashara  yake  iimarike, mwanadada  huyu aliamua  kwenda hospitali kukitoa  kizazi chake.Hakutaka  tena  usumbufu wa kutoa  mimba  au kufikiria kondomu......
Bonyeza Read more kusoma Story yote:

Tangu wakati  ule biashara  yake  iliimarika na wateja  walizidi kumiminika.Baada  ya miaka  kadhaa, Upako  wa  mwenyezi mungu  ulimfikia kupitia kwa mtumishi  mmoja  wa  mungu ambaye  alifanikiwa  kumfanya  aokoke  na  kuwa mtumishi mzuri  kanisani.....

Siku moja, mchungaji  mmoja alimwita na  kumwambia  kuwa:
"Dada yangu, Mwenyezi mungu  amenena  na  mimi na  kunifunulia  kuwa  wewe  ndo mke  wangu wa ndoa, hivyo naomba tuoane.."

Mwanamke huyu alitabasamu na kusema:
 "Kaka  yangu, Mungu hajakwambia lolote, lasivyo, utakuwa  hujamsikia vizuri.Naomba  uniache tu maana  sina  mpango wowote wa  kuolewa"

Yule  mchungaji  aliendelea kushikilia  msimamo wake  na  kudai kuwa :

"Mungu  amenifunulia,wewe  ndo  mke wangu"

Mwanamke  huyu  aliendelea  kuyapuuza  maneno hayo na ndipo sakata  hilo  lilipomfikia  Askofu  wa  kanisa  hilo.....

Wakiwa mbele  ya mchungaji,Mwanamke huyu  alifunguka  kwa  uwazi mbele  ya askofu  na  kudai kuwa kabla ya kuokoka yeye  alikuwa  ni kahaba  wa  makahaba....

Askofu naye alifunguka  na  kudai kuwa :"Sioni sababu ya kuumiza kichwa  kwa  mambo yaliyopita.Mungu  humsamehe  mwanadamu  kwa  kuzifuta  dhambi zake  zote za  nyuma  na  kumfanya  awe  mpya..!!!"

Mwanamke huyu  alifunguka  tena na kudai kuwa:
"Baba  askofu, mimi  nilishatoa kizazi changu  wakati nikiwa  kahaba, kwa hiyo  sitaweza    kuzaa  tena"
Askofu  aliishiwa  pumzi baada  ya kusikia hivyo.Hakuweza tena  kusema  kuhusu  kusahau ya  nyuma.Ilibidi amgeukie yule mchungaji  na  kumwamba:

"Vipi, bado  kuna maono yoyote  toka  kwa mwenyezi mungu?"

Mchungaji alijibu  ,"Ndio, huyu ndo mke wangu.."


 Askofu  ilibidi  awaombee kwa  sala  maalumu.Hatimaye ndoa  ikafungwa......Baada  ya  miezi  michache  tu, huyu mwanamke  alibeba  mimba.Yeye  pamoja  na mumewe waliongozana pamoja kwenda  hospitalini, tena  kwa  yule  yule doctor  aliyekitoa  kile  kizazi......

Daktari  alipomuona  alifurahi  akidhani kuwa pengine  mteja  wake  kamletea  mteja mwingine.....Doctor  hakuamini  masikio  yake baada  ya kuambiwa kuwa  huyu  mwanamke ni mjamzito na  amekuja  kujiandikisha  clinic....
Hakika Mungu ni  Muweza wa  yote....

Aliyekuwa Mume wa Dida Edzen Afunguka Sababu za Kuachana na Kupeana Talaka

$
0
0

Baada ya ndoa ya Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM, Khadija Shaibu 'Dida' kudaiwa kuvunjika, mumewe anayepiga mzigo TV1, Ezden Jumanne amefunguka mengi kuhusu sababu za kuvunjika ndoa hiyo.

Mzee wa Upako Anthony Lusekelo Adai Kuteswa na Misukule

$
0
0
 MBALI na Askofu wa Kanisa la Full Gosple Bible Fellowship, Zacharia Kakobe kuteswa na misukule inayodaiwa kufufuliwa na baadhi ya makanisa ya kiroho nchini, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ (pichani) naye ameibuka na kucharukia suala hilohilo.

Akizungumza na Uwazi juzi, Mzee wa Upako alisema suala la misukule linamtesa sana na kwamba anapingana na kufufuliwa kwao na baadhi ya wachungaji wa makanisa mbalimbali wanaojigamba kufufua misukule wakati si kweli na ni utapeli mtupu.

MZEE WA UPAKO ANAFUNGUKA:
“Kuna baadhi ya viongozi wa makanisa ya kioroho (bila kutaja majina)  wanadanganya  watu kuwa wanatoa misukule, si  ukweli kabisa ni uongo. Wanatafuta  namna ya kula sadaka za waumini wao kwa kuonekana wanaweza sana mambo ya kiroho,” alisema Mzee wa Upako na kuongeza:

“Hawa wachungaji wanatuchafua sana sisi tunaosimamia Neno la Mungu, wanaharibu Kanisa la Mungu kwa kudanganya waumini wao kwa sababu ya pesa tu. Hebu fikiria kuna wengine wanatoa hadi  shilingi 400,000 kwa mtu ili akubali kufanywa msukule feki na baadaye aombewe kanisani tena nimesikia wanatengenezewa hati za kifo kuonesha kuwa kweli watu hao walifariki dunia wakati si kweli, wamwogope Mungu.

“Huo ni usanii ndani ya Kanisa la Mungu. Nasema naumizwa sana na wachungaji wa namna hii, nateseka sana na hili jambo. Ninayo mpaka CD za mahubiri za  baadhi ya viongozi wa makanisa wanaodanganya kuwafufua misukule lakini kwa busara siwezi kuwataja ila wanajijua kwa sababu hata dhamira zao zinawashuhudia.”

TURUDI KWA KAKOBE
Akikazia zaidi, Askofu Kakobe alisema, anayedai ana uwezo wa kufufua misukule ni muongo na kwamba atakuwa anaabudu shetani.

“Mwenye uwezo wa kufufua ni Yesu Kristo pekee na alifanya hivyo kwa sababu ya utukufu wa Mungu na si vinginevyo, si  binadamu wa kawaida ambaye amepewa upako wa Mungu anadanganya watu kuwa anao uwezo wa kumtoa  mtu ambaye alichukuliwa msukule,” alisema Askofu Kakobe huku akisisitiza kwamba mtumishi yeyote wa Mungu anaweza kufanya muujiza huo kwa utukufu wa Mungu lakini si kwa sababu ya kuonesha yeye anaweza.
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live




Latest Images