Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

TMA Yafunguka Kuhusu Matalajio ya Hali ya Hewa Leo Katika Baadhi ya Maeneo

$
0
0
TMA Yafunguka Kuhusu Matalajio ya Hali ya Hewa Leo
Matarajio ya hali ya hewa leo tarehe 26/10/2017 kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA)





Washauri wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Wamesema Lulu Ameua Bila Kukusudia Hukumu Yake Kujulikana Novemba 13

$
0
0
Washauri wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Wamesema Lulu Ameua Bila Kukusudia Hukumu Yake Kujulikana Novemba 13
Kesi inayomkabili Elizabeth Michael ambaye ni muigizaji wa filamu bongo ya kuua bila kukusudia, inatarajiwa kufikia hatma yake baada ya Mahakama kusema kuwa hukumu itatolewa Novemba 13, 2017.

Kesi hiyo ambayo imesikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, imesema imemkuta Elizabeth Michael na hatia ya kumuua bila kukusudia muigizaji mwenzake Steven Kanumba ambaye alikuwa mpenzi wake, baada ya kusikiliza maoni ya Baraza la Wazee hii Leo.
Wazee hao ambao walikuwa watatu, kila mmoja alitoa maoni yake na kusema kwamba muigizaji huyo ana hatia ya kuua bila kukusudia, kwani marehemu alikuwa na mwili mkubwa zaidi ya mshtakiwa.
Kabla ya  wazee kutoa maoni, Jaji Rumanyika ambaye ndiye anayeendesha kesi hiyo, alisoma maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili na kusema kwamba ushahidi upande wa mashtaka umejikita katika ushahidi wa kimazingira kwa kuwa Lulu ndiye mtu wa mwisho kuwa na Kanumba, kisha kusikiliza maoni hayo ya Baraza la Wazee.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Novemba 13, ambapo hukumu yake itasomwa

Huyu Hapa Muigizaji wa Filamu Adai Kunyanyaswa Kijinsia na George Bush

$
0
0
Huyu Hapa Muigizaji wa Filamu Adai Kunyanyaswa Kijinsia na George Bush
Aliyekuwa rais wa Marekani George Bush ameomba msamaha kwa dhiki aliyosababisha baada ya muigizaji mmoja kumtuhumu wa kumnyanyasa kijinsia.
Heather Lind alisema kuwa rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 93 alimshika kutoka nyuma akiwa katika kiti chake cha magurudumo na kutamka ''mzaha mchafu'' wakati wakijiandaa kupiga picha.
Bi Lind alitoa madai hayo katika mtandao wa Instagram katika chapisho ambalo limefutwa.
Msemaji wa Bush alisema kuwa kisa hicho kilikuwa jaribio la ucheshi.
''Rais Bush alikuwa hawezi chini ya hali yoyote ile na kwa makusudi kumsababishia mtu dhiki na ameomba msamaha iwapo kitendo chake cha kuzua ucheshi kilimkosea bi Lind'', taarifa iliosambazwa kwa vyombo vya habari ilisema.

Bwana Bush alihudumu katika kipindi cha miaka mitano kutoka 1989 hadi 1993 na ni babake George W Bush ambaye alihudumu mihula miwili kati ya 2001 hadi 2009.
Mzee huyo anaugua ugonjwa wa kutetemeka.

King Majuto Atoa ya Moyoni kwa Wasanii wa Bongo Movie

$
0
0
King Majuto Atoa ya Moyoni kwa Wasanii wa Bongo Movie
Msanii mkongwe wa filamu Bongo, King Majuto amewataka wasanii ambao wapo katika tasnia hiyo kufanya kazi zenye ubora ili kufikia mafanikio kama yake.

Muigizaji huyu ambaye alitangaza kustaafu kuigiza ameiambia Azam Tv kuwa kwa sasa hivi wasanii wanapendwa na serikili inawatambua hivyo watumie fursa hiyo kufanya kazi.

“Kwa hiyo msichoke, fanyeni jitihada, tengenezeni michezo yenye busara, tengenezeni michezo inayoeleweka msifanye ilimradi tu na heshimuni bodi ya filamu ili mfanye kazi nzuri” amesema King Majuto.

Chanzo Bongo5

Yanga Wawatega Mashabiki Wake Kuhusu Manji 'Shujaa Amerudi, Shujaa Yupo Nyumbani'

$
0
0
Yanga Wawatega Mashabiki Wake Kuhusu Manji 'Shujaa Amerudi, Shujaa Yupo Nyumbani'
Mashabiki wa klabu ya soka ya Yanga wamebaki kwenye sintofahamu endapo mwenyekiti wao wa zamani Yusuf Manji amerejea kwenye madaraka yake au la.

Kupitia ukurasa rasmi wa klabu hiyo kwenye mtandao wa Instagram  imewekwa picha yenye utata ikielezea kuanza kuuzwa kwa jarida la klabu hiyo linaloitwa ‘Yanga Magazine’,wakati ukurasa wa pili wa Jarida hilo ukiwa na ujumbe unaoashiria kurejea kwa Manji ndani ya Yanga.
Katika ukurasa huo wa pili wa Jarida hilo yameandikwa maneno haya “SHUJAA AMERUDI SHUJAA YUPO NYUMBANI” huku yakipambwa na picha ya mfanya biashara huyo ambaye alijiuzulu cheo hicho miezi kadhaa iliyopita.

Kama hiyo haitoshi inaonekana kuna Makala ambayo ina maelezo ya maneno hayo japo yametiwa kivuli kiasi kwamba hayawezi kusomeka kwa urahisi. Swali linabaki kuwa Je, kuelekea pambano la watani wa Jadi Yanga na Simba siku ya jumamosi huenda Manji akatangaza kurejea kuiongoza Yanga?
Yanga na Simba zitakutana kwenye mechi ya raundi ya nane siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Hadi sasa timu hizo zinalingana pointi kila mmoja akiwa na 15 baada ya mechi saba huku Simba ikiongoza kwa tofauti ya mabao.

Odinga la Kuliamsha Dude Kesho Kuibadirisha Hali ya Kenya

$
0
0
Odinga la Kuliamsha Dude Kesho Kuibadirisha Hali ya Kenya
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya chini ya mwamvuli wa NASA, Raila Odinga ametangaza amefunguka na kusema kuwa kuanzia siku ya kesho Ijumaa Oktoba 27, 2017 hali haitakuwa kawaida nchini humo na kudai mambo yatabadilika kabisaa.

Odinga ambaye anapinga uchuguzi wa Rais ambao unaendelea leo nchini humo amesema kuwa kwanza watasusia bidhaa na huduma zote za kampuni zinazonufaisha udikteta nchini humo na kwenda mbali kuwa muungano wa NASA sasa utajulikana kama Muungano wa Kitaifa wa mageuzi. 
"Kuanzia Ijumaa Oktoba 27, hali haitakuwa kawaida. Mambo yatabadilika kabisa, tutaleta pamoja makundi yote ya utetezi nchini kuhakikisha uchaguzi wa urais unaandaliwa upya kwa njia ya uwazi, haki na usawa katika siku 90. Tutasusia bidhaa na huduma zote za kampuni zinazonufaisha udikteta, tutaanzisha kampeni za kitaifa za kupinga mamlaka haramu ya serikali na kukaidi mashirika yake" alisema Odinga
Mbali na hilo Odinga amewataka wanachama na wapenzi wa NASA kutojihusisha na jambo lolote linalohusu Jubileee ikiwa pamoja na kushiriki uchaguzi wa leo na kusema zipo njia nyingi za kumuuwa panya.

Tanesco Yafunguka Tatizo la Kukatika Umeme Ghafla

$
0
0
Tanesco Yafunguka Tatizo la Kukatika Umeme Ghafla
Tunaomba radhi wateja wetu
Imetokea hitilafu gridi ya taifa na kusababisha umeme eneo lote la Dar es Salaam na baadhi ya mikoa kukosa umeme.

Tatizo hili linashughulikiwa na umeme utarudi baada ya muda mfupi

=======

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUTOKEA KWA HITILAFU KATIKA GRIDI YA TAIFA​

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake waliounganishwa katika Mikoa iliyo katika Gridi ya Taifa kuwa majira ya Saa 12:30 imetokea hitilafu kwenye Gridi ya Taifa na kusababisha Mikoa hiyo kukosa umeme.

Jitihada zimefanyika ili kurejesha umeme na baadhi ya Mikoa imeshaanza kupata huduma ya umeme

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi.

TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

25/10/2017

=======
UPDATE: Oktoba 26, 2017

Tunapenda kuwataarifu Wateja wetu waliounganishwa katika Mikoa iliyo katika Gridi ya Taifa kuwa leo Alhamisi Oktoba 26, 2017 majira ya Saa 12:03 Asubuhi imetokea hitilafu tena kwenye Gridi ya Taifa na kusabisha Mikoa hiyo kukosa umeme.

Mafundi wanafanya jitihada usiku na mchana ili kuhakikisha hali hii haijirudii na umeme unarejea katika hali ya kawaida kwa haraka

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi...

TANESCO

Pata Muonekano wa Shape Bomba na Rangi ya Ngozi Kwa Kutumua Products za Natural Beauty

$
0
0
OFFER SPECIAL
NATURAL BEAUTY ndiyo kampuni pekee inayotoa bidhaa ORIGINAL zenye GARANTII NA RISITI
Sasa ni wakati wako wa kupendeza na bidhaa hizi zisizo na kemikali wala madhara kwa mtumiaji.
       Pata bidhaa hizi upate matokeo mazuri kwa haraka na uhakika zaidi. Bidhaa zetu zote zimetengenezwa kwa mimea na matunda.

          BIDHAA ZETU:-
 
1.Kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @150,000/=
2.Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa:-
(a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200,000/=
(b)Vidonge  @180,000/=
(c)BOTCHO 10× ya kupaka @170,000/=
3.Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:-
 (1)Mafuta  @150,000/=
(11)Vidonge @170,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
5.Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a)SHARK POWER gely ya kupaka @150,000/=
(b)Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu hata kwa wenye kisukari @150,000/=
(C) VigRX CREAM- Ni dawa mpya ya kuongeza maumbile hadi nchi 7.5 inapatikana kwa @200,000/=
(C)Handsome up original ni kifaa kinachoongeza maumbile kwa %99 size uipendayo  @250,000/=
6.Kuondoa mvi milele zisiludi tena @150,000/=
7.Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula  @150,000/=
8.Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @150,000/=
(b)Mkanda wa kawaida @150,000/=
(c)Micro-computer belt wa umeme @200,000/=
9.Kupunguza  maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @150,000/=
10.Kushepu miguu (CHUPA YA BIA) na kuondoa vigimbi @150,000/=
11.Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @150,000/=
12.Kurudisha usichana  (bikra) @150,000/=
        Wasiliana nasi :- (+255)
             0759029968 au.     
                0659618585
  TAHADHARI: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa NATURAL BEAUTY pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
👉🏻Ili kuona bidhaa zaidi na shuhuda za waliotumia bidhaa zetu. ...............
     Follow us on instagram  @natural2162
@natural2162
@natural2162

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Octoba 27

$
0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Octoba 27

Sababu Zilizowafanya Wazee wa Baraza Wamtie Hatiani Lulu Michael

$
0
0
Wazee wa baraza wameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwa mwigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu amehusika kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Wakitoa maoni yao jana baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, wazee hao walieleza kuwa Lulu ndiye aliyesababisha kifo cha mpenzi wake huyo wakati wa ugomvi baina yao usiku wa Aprili 7, 2012.

Wakizungumza mmoja baada ya mwingine, wazee Omary Panzi, Sarah Lugoma na Rajabu Mlawa, walihusisha tukio la Kanumba kujibamiza kichwa ukutani na kusukumwa na mshtakiwa.

“Kutokana na sababu na uainishi wa kesi (ushahidi) wa pande zote, mimi kwa upande wangu nimeridhika kuwa Elizabeth (Lulu) ameua bila kukusudia,” alisema mzee Mlawa na kuongeza: “Katika ugomvi, inawezekana hekaheka za kujinusuru, alitumia nguvu kumsukuma Kanumba na kuanguka ukutani. Hivyo, kwa maoni yangu kosa la kuua bila kukusudia kwa Elizabeth limethibitika.”

Akitoa maoni yake, Sarah Lugoma alisema Kanumba alifariki dunia kutokana na ugomvi baina yake na mpenzi wake (Lulu) kwa kuwa ndani kulikuwa giza, Kanumba aliteleza wakati wa ugomvi huo akaanguka.

“Hivyo mshtakiwa aliua bila kukusudia,” alisisitiza Lugoma wakati akihitimisha maoni yake.

Mzee mwingine, Panzi alisema Kanumba aliteleza na kuanguka wakati wa ugomvi huo, mshtakiwa ndiye aliyehusika na kifo chake kwa kuua bila kukusudia.

Hata hivyo, maoni ya wazee hao wa baraza siyo hukumu halisi ya Mahakama bali yanayotokana na mtazamo wao tu katika hali ya kawaida nje ya sheria kwa namna walivyousikiliza ushahidi wa pande zote.

Hivyo, kumtia hatiani mshtakiwa huyo hakumaanishi kuwa tayari ana hatia kwa kuwa maoni hayo hayamfungi jaji katika hukumu yake ambaye huongozwa na sheria husika.

Kwa hiyo, hatima ya msanii huyo kama ana hatia au la itabainishwa na Mahakama Novemba 13 wakati Jaji Sam Rumanyika anayesikiliza kesi hiyo atakapotoa hukumu.

Jaji Rumanyika aliwakumbusha wazee hao muhtasari wa ushahidi uliotolewa na pande zote kabla ya kutoa maoni yao.

Jaji Rumanyika akieleza kwa ufupi kilichozungumzwa na kila shahidi wa pande zote, alitoa mwongozo kwa wazee hao pamoja na mambo mengine, kutoa maoni yao bila kuongozwa na huruma wala kuogopa chochote.

“Mnalo jukumu la kutoa maoni yenu bila kuongozwa na huruma wala vitisho. Mnatakiwa kutoa maoni yenu kwa mujibu wa ushahidi mliousikia,” alisema Jaji Rumanyika.

Aliwaeleza kuwa kama walivyosikia ushahidi wa upande wa mashtaka kuwa umejikita kwenye ushahidi wa kimazingira, mshtakiwa ndiye aliyekuwa mtu wa mwisho kuwa na Kanumba.

Alisema ushahidi wa kimazingira lazima uwe ni vipande ambavyo ni mnyororo (muunganiko) unaomhusisha mshtakiwa kuwa ndiye ametenda kosa.

“Kama mkiona kuwa mshtakiwa ametoa maelezo ya kutosheleza basi mnaweza kusema hana hatia, lakini kama mna maoni tofauti pia mtaniambia,” alisema Jaji Rumanyika na kuongeza:

“Mkiona kuwa kifo hicho kilitokana na ugomvi, basi shtaka lake huwa ni la kuua bila kukusudia, mkishawishika kwa vyovyote na kwa namna yoyote ile mshtakiwa hakuhusika na kifo hiki msisite pia kunipa maoni yenu.”

Mwanamuziki Shilole Achoshwa na Mapenzi ya Viben Ten

$
0
0
MWANAMUZIKI anayefanya vizuri kwenye miondoko ya Mduara, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefunguka kuwa, mambo ya mapenzi ameyaweka kando hivyo watu aliokuwa akitembea nao ‘vi-ben ten’ sasa basi.

Akigonga stori na Star Mix, Shilole alisema kuwa, akiyaweka mapenzi mbele mara nyingi hayamzalishii matunda yoyote lakini akikazana katika kazi inamletea mafanikio makubwa.

“Jamani kwa usawa huu mtu usipobadilika na kuangalia kitu cha maana ni shida sana, mimi mambo ya mapenzi sijui vi-ben tena sasa hivi yanisubirie kwanza, nifanye kazi zangu ili nipate maendeleo sio mapenzi wanafaidi mashabiki wa Instagram kukuangalia maisha yako,” alisema Shilole.

NA IMELDA MTEMA

Kesi ya Lulu Michael Yamnyima Muna Love Usingizi..

$
0
0
MSANII wa filamu na mjasiriamali, Rose Alphonce ‘Muna’ amesema kuwa, anapitia katika kipindi kigumu sana cha kumuuguza mtoto wake lakini muda huohuo kukosa usingizi kutokana na kesi inayoendelea ya mdogo wake wa hiari, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Akizungumza na Star Mix, Muna ambaye tangu kesi ya Lulu imeanza kusikilizwa hakosi kuwa naye mahakamani alisema, amekuwa kwenye kipindi kigumu kwa kuwa takribani miezi miwili anamuuguza mtoto wake mguu wenye majeraha lakini pia hapati usingizi kwa ajili ya kesi ya Lulu.

“Yaani najiona kabisa kama huu mwaka ni wangu, maana pale Muhimbili walishanizoea kabisa, nimekaa muda mrefu nikimuuguza mwanangu mguu lakini ukiachana na hilo nahangaika na upande wa pili ishu ya Lulu mpaka nachanganyikiwa,” alisema Muna.

STORI: IMELDA MTEMA

Mwakyembe Amteua Alberto Msando kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki.

$
0
0
Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amemchagua Mwanasheria na mdau wa masuala ya Sanaa Alberto Msando kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki.

Katika tarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara Bi Leah Kihimbi kuhusu uteuzi huo wa Msando imesema kwamba uteuzi huo umetokana na vikao vilivyofanywa na wadau wa sanaa pamoja Mh. Waziri Mwakyembe.

Kwa upande wa Alberto Msando ambaye amepatiwa nafasi hiyo na serikali ameahidi kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria za nchi zinalinda haki za wasanii na kuhakikisha wasanii wanafaidika na kazi zao.

Msando ameandika  "Ulaya na Marekani wasanii wengi sio masikini. Hapa kwetu wasanii wengi ni majina tu. Wengi wanaishi maisha ya 'naomba nitoe niko vibaya'. ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria zetu zinalinda haki za wasanii".

Ameongeza "Harrison Mwakyembe tutafanya kazi uliyotutuma"

Msando mara nyingi amekuwa mbele katika kuwasaidia wasanii kwenye masuala yanayohitaji msaada wa kisheria.

Install Application ya MCHAMBUZI Kwenye Simu yako Kusoma Matamko ya Wanasiasa Kila Siku

$
0
0
Maswala ya Siasa na Matamko ya kila siku ya Wanasiasa Hakikisha Umedownload App ya Mchambuzi Kwenye simu yako

Bonyeza HAPA

Kama we ni Mpenzi wa Habari za Siasa Usipitwe na Hii Application ya Mchambuzi..... Bonyeza HAPA Kudownload kwenye Simu yako


Ayler Atoa Sababu ya Kuchukua Waume za Watu

$
0
0
Ayler Atoa Sababu ya Kuchukua Waume za Watu
Msanii Ayler amesema kwa sasa hatothubutu kumuweka wazi mwanaume wake kwani wanawake wengi ni wezi wa wanaume.

Akiongea kwenye Back Stage ya Bongo Fleva Top 20 ya East Africa Radio, amesema wanawake wengi siku hizi ni wezi na wa waume za watu, na kwamba hiyo imetokana na wanaume kuwa wachache na wengine kupoteza sifa ya kuwa wanaume.

Ayler amesema wanawake wanapenda kufanya hivyo ili kupata mteremko kwa wanaume ambao tayari wana maisha yao, kwani kila mwanaume ambaye tayari ana familia, mara nyingi hutekeleza majukumu yake ipasavyo, na ndio kitu wanawake wote duniani huangalia.

Huu Hapa Uteuzi wa Rais Magufuli kwa Viongozi Mbalimbali

$
0
0
Huu Hapa Uteuzi wa Rais Magufuli kwa Viongozi Mbalimbali
Rais  Dkt. John Pombe Magufuli leo Oktoba 26, 2017 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali katika serikali wakiwepo Makatibu Wakuu, Wakuu wa mikoa na kumteua Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania mstaafu (IGP) Ernest Mangu kuwa balozi.

Akizungumza kwa niaba ya Rais, Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Balozi John William Herbert Kijazi amesema kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi huo ili kukamilisha safu ya watendaji ambao watalisaidia Baraza lake jipya la Mawaziri ambalo amelifanyia marekebisho siku za karibuni.
Miongoni mwa watu ambao wameteuliwa kuchukua nafasi hizo ni mabalozi wawili ambao vituo vyao vya kazi vitakuja kutangazwa baadaye akiwepo aliyewakuwa IGP Ernest Mangu  pamoja na  Azizi Mlima.

Joti Kimeeleweka Anatarajia Kufunga Ndoa Hivi Karibuni

$
0
0
Jot Kimeeleweka Anatarajia Kufunga Ndoa Hivi Karibuni
Mchekeshaji mkongwe Bongo, Joti hatimaye ameamua kuachana na utani wa kudai anaoa na kuamua kufanya kweli kwa kudhihirisha yupo serious kidogo kwa jambo la mahusiano kwa kutarajia kuvuta jiko hivi karibuni.

Joti ambaye anafahamika kwa kufanya matangazo mengi ikiwemo ya kufunga ndoa , aliambatana na  watu wake wa karibu  katika sendoff  yake  iliyofanyika siku ya jana( Alhamisi) akiwa na mchekeshaji Seki.

Mchekeshaji huyo mwenye dili kibao town anatarajia kufunga ndoa rasmi  hivi karibuni na atakuwa ameingia kwenye orodha ya mastaa wa Bongo waliopo  katika ndoa kama Babuu wa Kitaa, Mx Carter, Kenedy The Remedy, Professa Jay, ZamaradI Mketema na Frola Mbasha.
chanzo Bongo5

Lema Afunguka Asema 'Dau Kubwa Latengwa Nassari kununuliwa'

$
0
0
Lema Afunguka Asema 'Dau Kubwa Latengwa Nassari kununuliwa'
Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA) Goodless Lema amefunguka na kusema kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti ametangaza kuwa anadau kubwa la kuweza kununua madiwani wengine 20  pia anadau kubwa kwa ajili ya Mbunge Joshua Nassari.

Lema amesema kuwa kitendo alichofanya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti ni wazi amethibitisha kuwa hata madiwani wa awali ni kweli waliwanunua hivyo amewataka TAKUKURU kuchukua hatua kwa kauli anazotoa diwani huyo.
"DC ambaye alitoa rushwa amethibitisha mwenyewe kuwa alitoa rushwa na DC amesema bado anafungu kubwa kununua zaidi ya madiwani 20 na anasema anadau kubwa kwa ajili ya Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Mhe. Nassari kwa hiyo kama Mlowola  Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU alikuwa anatafuta ushahidi basi DC mwenyewe ameshampa ushahidi lakini nina uhakika Mlowola hatachukua hatua yoyote dhidi ya DC kwa sababu DC huyu huu ujasiri alionao anajua unatoka wapi" alisema Godbless Lema
Lema anasema kwa hali ya kawaida kiongozi hawezi kutoa kauli kama hiyo kwenye jambo ambalo ni nyeti kama hilo la ununuzi wa madiwani na kiongozi huyo akaendelea kubaki madarakani mpaka sasa. Aidha Lema amesema kitendo alichokifanya Mnyeti ni dhihaka kubwa na dharau ya juu sana kwa Umma.

Korea Kaskazini Yaiwachilia Huru Meli ya Uvuvi ya Korea Kusini

$
0
0
Korea Kaskazini Yaiwachilia Huru Meli ya Uvuvi ya Korea Kusini
Korea Kaskazini inasema kuwa itaiachilia meli ya uvuvi ya Korea Kusini ilioikamata siku sita zilizopita kwa kuingia katika himaya yake kinyume cha sheria, chombo cha habari kimesema.
Meli hiyo na wafanyikazi wake itaachiliwa katika mpaka wa kijeshi katika bahari ya mashariki kulingana na chombo cha habari cha KCNA.
Uamuzi huo ulitolewa baada ya wafanyikazi hao kuomba msamaha kwa kufanya makosa hayo, kiliongezea.
Hatua hiyo inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi katika eneo hilo huku pande zote mbili zikifanya mizururu ya mazoiezi ya kijeshi.
Korea Kaskazini imesema kuachiliwa kwa meli hiyo ya uvuvi, baadaye siku ya Ijumaa inafuatia hatua ya kukiri makosa kwa wale waliokuwa wakiabiri chombo hicho ambao walitaka serikali ya Korea Kaskazini kuwavumilia.
Uchunguzi, kulingana na Korea Kaskazini, ulithibitisha kuwa wavuvi hao waliingia maji ya taifa lake siku ya Jumamosi.
Msemaji wa serikali ya Korea Kusini alisema ni afueni kwamba wavuvi hao watarudi kulingana na chombo cha habari cha reuters

Nitapambana Vilivyo kwa Ajili ya Kutetea Haki ya Mwanamke na Watoto - Jokate

$
0
0
Nitapambana Vilivyo kwa Ajili ya Kutetea Haki ya Mwanamke na Watoto - Jokate
MWANAMITINDO maarufu Bongo, Jokate Mwegelo amesema kuwa, atahakikisha anapambana vilivyo kwa ajili ya kutetea haki ya mwanamke pamoja na watoto kwa ujumla.

Akizungumza na Star Mix, Jokate alisema, kuna umuhimu sana kila mmoja mwenye nafasi kwenye jamii atambue nafasi ya mwanamke kwani wao ndio wenye nafasi kubwa kwenye jamii na pia kukazania kuwapa elimu.

“Unajua watu wengi wanajisahau kuhusu mwanamke na watoto lakini kwa upande wangu naona thamani kubwa sana ya mwanamke hasa akipatiwa elimu bora na kupewa nafasi nyingi za kuongoza huku watoto wakipewa haki inayostahili,” alisema Jokate.
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images