Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live

Dogo Janja Ajawa na Kigugumizi Kuthibitisha Ukweli wa Ndoa Yake na Iren Uwoya

$
0
0
Dogo Janja Ajawa na Kigugumizi Kuthibitisha Ukweli wa Ndoa Yake
Wakati taarifa zikiendelea kusambaa kuhusu Dogo Janja kufunga ndoa na muigizaji Irene Uwoya, msanii huyo ameshindwa kuweka ukweli wa jambo hilo.

Dogo Janja ambaye kwa sasa anafanya vizuri ngoma ‘Ngarenaro’ ameiambia Planet Bongo ya East Africa Radio kwa sasa hayupo Dar es Salaam ila atakaporojea atalizungumzia hilo.

“Nitakuambia tu wala usijali, nikirudi mjini, nipo mitaa ya Bagamoyo, nikitoka naenda Zanzibar, nikitoka nitakupa exclusive” amesema.

Siku ya Jumamosi October 28, 2017 ndipo taarifa zilianza kudai wawili hao kufunga ndoa lakini hakukuwa na ushahidi wowote zaidi ya picha walizoweka katika mtandao wa Instagram ingawa watu karibu na Dogo Janja wamekuwa wakieleza ni kweli.

Zitto Kabwe ni Kama Harmorapa Anatafuta Kiki - Mwakibinga

$
0
0
Zitto Kabwe Anatafuta Kiki Kama Harmorapa- Mwakibinga

KIJANA kutoka Kundi la Vijana Wazalendo nchini, James Mwakibinga, amekuja juu na kumshukia kiongozi wa Chama cha Act- Wazalendo, Zitto Kabwe na kusema anatafuta kiki kama Harmorapa kwa kupingana na kasi ya Rais Dk .John Pombe Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi uliofanyika katika madini nchini.

Mwakibinga amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa mambo yanayofanywa na kiongozi huyo siyo ya kizalendo na hayafai kufumbiwa macho na mtu yoyote mwenye akili na mwenye dhamira ya kweli kwenye taifa lake.

“Nadiliki kusema kuwa game changer amebadilisha mchezo hivyo wanasiasa wanashindwa kufanya kazi katika majimbo yao na kazi yao imekuwa kufanya upotoshaji  juu ya kazi zilizofanywa na Rais Dk John Pombe Magufuli hasa katika swala zima la kuokoa mali za Watanzania katika sekta ya madini,” amesema Mwakibinga.

Amesema Zito anatakiwa kufanya siasa za kistaarabu na kuacha kupayuka tu kwani hii ni miaka miwili bado mitatu hivyo zama hizi zimebadilika hakuna utaratibu tena wa mashirika kuwahonga viongozi wa kisiasa.

Mwakibinga amesema kuwa vijana wazalendo wako nyuma yake watamlinda na kusimamia misingi yote ya kulinda rasilimali za wananchi zisiendelee kuibwa.

Hivi Ndivyo Kenyata Alivyotangazwa Mshindi wa Urais Kenya Akiwa na Kura 7.5m

$
0
0
Hivi Ndivyo Kenyata Alivyotangazwa  wa Urais Kenya Akiwa na Kura 7.5m
Rais Uhuru Kenyatta ametangazwa mshindi wa urais wa marudio nchini Kenya akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati amesema kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96.
Kwa Picha: Uchaguzi wa marudio Kenya
Bw Chebukati amesema jumla ya wapiga kura 7,616,217 kati ya jumla ya wapiga kura 19.6 milioni ambao wamejiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo walishiriki uchaguzi huo wa Alhamisi wiki iliyopita.

Rais Kenyatta, akihutubu baada ya kutangazwa mshindi, amewashukuru waliompigia kura.
Amesema uchaguzi uliomalizika ni ishara ya uthabiti wa demokrasia na uthabiti wa taasisi za Kenya pamoja na Wakenya wenyewe.
"Agosti 8, na sitachoka, Wakenya walirauka kupiga kura. Na siku hiyo walinichagua bila shaka. Ushindi wangu ulipopingwa Mahakama ya Juu, kwenye hukumu, mahakama haikupinga ushindi wangu wa 54%. Takwimu hazikupingwa. Kilichokosolewa ni utaratibu uliopelekea ushindi wangu," amesema.

Bw Odinga alikuwa ametarajiwa kutangaza mwelekeo kwa wafuasi wake baada ya tangazo la matokeo kufanywa na Bw Chebukati.
Taarifa zinasema ameamua kufanya hivyo hapo kesho.
Matokeo kamili ya wagombea wote kama yalivyotangazwa na Bw Chebukati
MgombeaChamaKuraAsilimia
Uhuru KenyattaJubilee7,483,89598.28
Raila Odinga (Alisusia)ODM73,2280.96
Mohamed Abduba DidaARK14,1070.19
Japheth Kavinga KaluyuMgombea wa kujitegemea8,2610.11
Michael Wainaina MwauraMgombea wa kujitegemea6,0070.08
Joseph Nthiga NyagahMgombea wa kujitegemea5,5540.07
John Ekuru AukotThirdway Alliance21,3330.28
Cyrus JirongoUDP3,8320.05
Bw Chebukati amesema anaamini uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
Mwenyekiti huyo amesema mambo aliyosema yalihitajika kufanyika kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki yalitimizwa.

Amesema walitaka kuhakikisha kila kitu kilikuwa sawa.
"Hata tulibadilisha tarehe kutoka 17 hadi 26 Oktoba kuhakikisha tuna muda wa kutosha," amesema.
Kadhalika, amesema alikuwa na kundi la kusimamia mradi wa uchaguzi wa urais kuondoa majukumu kutoka kwa makamishna ambao walituhumiwa na baadhi ya wadau.
"Naweza kusema kwa uhakika, kwamba 26 Oktoba kabla ya uchaguzi kuanza, nilikuwa nimeridhika kwamba tulikuwa tumefanya kila kitu kuhakikisha kila Mkenya angetekeleza haki yake kikatiba," amesema.

"Na haki hii mtu anafaa kuitekeleza bila kutishiwa au kuzuiwa."
Bw Chebukati anasema alishangaa kwamba watu waliotafuta wa kushambulia walimwendea yeye.
Hata hivyo, anasema ndani ya tume nao walimwogopa.
"Hatutaweza kufurahisa kila mtu. Nimedumisha na kuheshimu sheria, kama mwanasheria ziwezi kuvunja sheria niliyojitolea kuilinda," amesema.

Matokeo yalivyokuwa uchaguzi wa tarehe 8 Agosti ambao ulifutwa na Mahakama ya Juu
MgombeaChamaKuraAsilimia
Uhuru KenyattaJubilee8,203,29054.27
Raila OdingaODM6,762,22444.74
Mohamed Abduba DidaARK38,0930.25
Japheth Kavinga KaluyuMgombea wa kujitegemea16,4820.08
Michael Wainaina MwauraMgombea wa kujitegemea13,2570.09
Joseph Nthiga NyagahMgombea wa kujitegemea42,2590.28
John Ekuru AukotThirdway Alliance27,3110.18
Cyrus JirongoUDP11,7050.08

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumanne

$
0
0

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..



JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.

Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 622588038au 0679119679 au +255 764318107
NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Profesa Jay Atupa Dongo Hili “Mkimaliza Hoja Yenu Mfu ya Ufisadi Muwatimue Mapema Msisubiri Waondoke Wenyewe"

$
0
0
Profesa Jay Atupa Dongo Hili  “Mkimaliza Hoja Yenu Mfu ya Ufisadi Muwatimue Mapema Msisubiri Waondoke Wenyewe"
Mbunge wa Jimbo la Mikumi Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ametoa ujumbe unaoonekana kama ushauri kwa vyama vya siasa huku ukilenga matukio ya hivi karibuni ya wanasiasa kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine.

Katika Ukurasa wake wa mtandao wa Twitter Profesa Jay ameandika “Mkimaliza hiyo HOJA yenu Mfu ya UFISADI, leteni tuhuma za wote waliobaki huko na Muwatimue mapema msisubiri waondoke wenyewe... TUMEELEWANA”?
Ujumbe huu wa Profesa Jay umekuja ikiwa ni chini ya saa 24 toka Mbunge wa Singida Kaskazini kupitia CCM, Lazaro Nyalandu ajiuzulu Ubunge pamoja na nyadhifa zingine ndani ya chama ikiwemo kujivua uanachama.
Kwa upande mwingine ujumbe huo umechukuliwa kama jibu kwa Chama cha Mapinduzi ambacho kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kilijibu suala la Nyalandu kuhama kwa hoja ya kuwa ni miongoni mwa wanachama wengi wasio waadilifu ambao wameamua kuondoka kabla ya Panga kuwafikia.
Hata hivyo Profesa Jay amegoma kufafanua undani wa ujumbe huo iwapo umelenga kupuuza hoja hiyo ya Ufisadi. Awali Profesa Jay aliandika ujumbe wa kumpongeza Nyalandu kwa uamzi wake na kumkaribisha Chadema. “Hongera sana my brother Lazaro Nyalandu kwa Ujasiri na kusimamia kile unachokiamini!! KARIBU SANA KIUMENI SPEAK YOUR MIND”, aliandika Profesa Jay.

Nafikiria Kuachia Wimbo wa Mwisho Baada ya Hapo Nitakuwa Nimestaafu Rasmi Muziki- Jokate

$
0
0
Nafikiria Kuachia Wimbo wa Mwisho Baada ya Hapo Nitakuwa Nimestaafu Rasmi Muziki- Jokate
MWANAMITINDO na msanii wa Bongo Fleva, Jokate Mwegelo amefunguka kuwa, ‘soon’ ataachana na muziki huo, bila kutaja sababu ya kufanya hivyo.
Jokate aliiambia Full Shangwe kuwa, anajipanga kuachia wimbo mmoja wa mwisho kisha anaachana kabisa na Bongo Fleva.
“Nafikiria kutoa wimbo moja wa mwisho, halafu baada ya hapo nitakuwa nimestaafu kufanya muziki, sina sababu ya msingi ila ni maamuzi yangu tu,” alisisitiza Jokate.

Mwakibolwa: Zitto Kabwe Ahojiwa Akituhumiwa Kufanya Makosa ya Uchochezi

$
0
0
Mwakibolwa: Zitto Kabwe Ahojiwa Akituhumiwa Kufanya Makosa ya Uchochezi
Baada ya kukamatwa kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe, Timu ya mawakili wa chama hicho kimeeleza kuwa kiongozi huyo amekamatwa na polisi na anahojiwa akituhumiwa kufanya makosa ya uchochezi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Wa Sheria wa Chama hicho, Stephen Mwakibolwa, imesema kuwa juzi, Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani.

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe, amekamatwa na polisi na kuhojiwa akituhumiwa kufanya makosa ya Uchochezi juzi, Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Maneno hayo ni yafuatayo:

1. Wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.

2. Wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.

Zitto Kabwe amekamatwa leo asubuhi na kupelekwa katika kituo cha polisi Chango’mbe.

Joti Awajibu Waliomsema Kufunga Ndoa na Kiduku

$
0
0
Joti Awajibu Waliomsema Kufunga Ndoa na  Kiduku
Jumamosi iliyopita ilikua harusi ya Mchekeshaji maarufu Tanzania Lucas Muhavile maarufu kama Joti ambapo gumzo lilikua pia nywele zake alizonyoa kwa staili ya kiduku na kuingia nacho Kanisani jambo ambalo lilifanya baadhi ya watu kuongea sana kwenye mitandao.

Joti kwenye Exclusive Interview ambapo amewajibu waliomsema kuhusu kiduku chake, >>> “Sidhani kama kuna sheria au kuna maandiko yameandika kwamba ukinyoa hivi hutakiwi kufunga ndoa, hii sanasana iko kwenye maadili tu“

“Nilimuomba Padri na akanielewa na kuniambia wewe ni Msanii tunajua cha kufanya usisuke tu, fumua hizo nywele ziwe tu kawaida zibanebane vizuri”

Ali Kiba Akataa Kuitwa Mungu wa Bongo Fleva 'Naomba Msiniite Hivyo Siwezi Kuwa Hivyo'

$
0
0
Ali Kiba Akataa Kuitwa Mungu wa Bongo Fleva 'Naomba Msiniite Hivyo Siwezi Kuwa Hivyo'
Jinsi mashabiki wa soka wanavyochizika muda mwingine, ndivyo hivyo hata katika muziki. Kitu hiki kimemtokea shabiki mmoja wa Alikiba kitu kilichopelekea kumuita msanii huyo ‘Mungu wa Bongo Flava’.

Hata hivyo kilikuwa ni kitu ambacho hakikumpendeza Alikiba, ndipo alipoamua kumjibu shabiki huyo ambaye anatumia jina la Kibasalu katika mtandao wa Instagram;

Officialalikiba @kibasalu naomba msiniite hivyo siwezi kuwa wala siwezi kukubali imani yetu haturuhusu kujiita au kuitwa na mtu yoyote ule jina la MUUMBA.

Comment hiyo ya Alikiba inakuja mara baada ya shabiki huyo kwenda kwenye moja ya picha za msanii huyo katika mtandao wa Instagram na kuandika, ‘Bongo flaver god’.

Mtandao wa WhatsApp Waruhusu Kufuta Ujumbe,Picha Uliotuma kwa Mtu Usiyemkusudia

$
0
0
Mtandao wa WhatsApp Waruhusu Kufuta Ujumbe,Picha kwa Mtu Usiyemkusudis
Ilishawahi kukutokea kutuma ujumbe, picha au video au documenti yeyote kwa mtu usiyemkusudia kwa bahati mbaya kupitia programu ya WhatsApp? kama huwa unapatwa na matatizo hayo sahau kabisa kwani tayari programu hiyo imeshaongeza sehemu ya kufuta jumbe hizo.

WhatsApp is rolling out the Delete for Everyone (Recall) feature for all users! 🎉https://t.co/3bnbgxtPvU

— WABetaInfo (@WABetaInfo) October 26, 2017

WhatsApp tayari imezindua huduma hiyo ambayo imeongezwa kwenye programu kwa jina ‘Delete For Everyone’ ambapo mtumaji wa ujumbe, picha au video atachagua kufuta kwake au kwa mtu aliyemtumia kimakosa.



Kwa sasa huduma hiyo inapatikana kwa watumiaji wote wa iOS na Android kama bado basi cha kufanya update programu yako ya WhatsApp ili uanze kutumia.

Hii inakuwa hatua nyingine ya maboresho ya programu hiyo baada ya kutangaza kuongeza sehemu ya Live Chart  ndani ya mwaka huu.

Mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu WhatsApp Inc walitangaza kuwa wataleta mabadiliko makubwa manne ndani ya mwaka huu ambayo yataifanya programu ya WhatsApp kuwa ya kisasa zaidi.

Twambie wewe mtumiaji wa programu pendwa ya WhatsApp umeyapokeaji mabadiliko haya.

Miili 9 Iliyokatwakatwa Yapatikana Kwenye Nyumba Tokyo Japan

$
0
0
Miili 9 Iliyokatwakatwa Yapatikana Kwenye Nyumba Tokyo Japan
Polisi nchini Japan wamemkamata mwanamume mmoja baada ya kupata viungo vya miili tisa katika nyumba yake iliyo Zama huko Tokyo.
Polisi walipata vichwa viwili kwenye jokovu nje ya nyumba ya mshukiwa kwa jina Takahiro shiraishi, wakati wakichunguza kutoweka kwa mwanamke mmoja.
Pia walipata viungo vya watu saba kwenye majokovu yaliyo ndani ya nyumba yake.

Mtu huyo wa umri wa miaka 27 anashtakiwa kuwa ndiye alitupa miili hiyo.
Polisi walikuwa wamepata miili ya wanawake 8 na mwanamume mmoja, mingine tayari ikiwa imeanza kuoza.
"Niliwaua na nikaifanyia kazi miili yao ili kuficha ushahidi," shirika la habari la NHK lilimnukuu akisema.
Jirani wake alisema kuwa alikuwa ameanza kuhisi harufu mbaya kutoka kwa nyumba yake tangu Bw. Shiraishi ahamie nyumba hiyo mwezi Agosti.
Polisi walifanya ugunduzi huo walipokuwa wakimtafuta mwanamke wa umri wa miaka 23 ambaye amekuwa hajulikani aliko tangu tare 21 mwezi Oktoba.
Wachunguzi waligundua kuwa Bw. Shiraishi amekuwa akiwasiliana na mwanamke huyo baada ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa alikuwa anataka kujiua.

Breaking News: Zitto Kabwe Aachiwa kwa Dhamana Akamatwa Tena

$
0
0
Breaking News: Zitto Kabwe Aachiwa kwa Dhamana Akamatwa Tena
Saa chache baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kukamatwa na Jeshi la Polisi  na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Chang’ombe Dar es salaam, aliachiwa kwa dhamana lakini amekamatwa tena na kupelekwa kituo cha Polisi cha Kamata kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Katibu na itikadi na uenezi wa ACT WAZALENDO amesema “baada ya kukamatwa tena amepelekwa kwenye kituo cha Polisi Kamata, hatufahamu ni sababu gani zilizofanya akakamatwa tena, tuna tafsiri kama Chama mwenendo wa sasa wa kumshughulikia Zitto ni kujaribu kumnyamazisha“

Ni Sawa Kutumia Mswaki Mmoja na Mpenzi Wako?

$
0
0
Ni Sawa Kutumia Mswaki Mmoja na Mpenzi Wako?
Jamani usiombe mapenzi yakakunogea utatamani ugandane na mpenzi wako kila mahala.

Katika kona kona za mapenzi mapenzi leo nimekuta na hii kitu.

Mara nyingi watu wanapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi huwa wanaaminiana kupita kiasi hata kama hawakuwahi kuchunguza afya zao.

Hali hii hupelekea wapenzi kuchangia vitu mbali mbali kama nyembe, mswaki,mkasi hata wengine hufikia hatua ya kuchangia pichuu! "ukivaa BOXER yangu na vaa KIBINI yako"

Hapa leo nitahitaji tuongelea kitu kimoja.

Mswaki,hivi ni sahihi wapenzi kuchangia mswaki?

Na kiafya iko vipi, hakuna magojwa yoyote yanayoweka kutokea kwa kuchangia mswaki?

Au matumaini yetu yako juu ya zile dawa za meno tupe Mtazamo wako.

Ndikumana Aibuka na Kujibu Mapigo Baada ya Iren Uwoya Kuolewa

$
0
0
Ndikumana Aibuka na Kujibu Mapigo Baada ya Iren Uwoya Kuolewa
Aliyekuwa mume halali wa muigizaji wa filamu bongo Irene Uwoya, mcheza soka kutoka nchini Burundi Hamad Ndikumana, ameonyesha kujibu mapigo baada ya mwenza wake kuonekana kuolewa, kwa kupost picha akiwa na mwanamke mwengine.

Kwenye ukurasa wake wa instagram Ndikumana amepost picha hizo, huku akiandika ujumbe kama ambao unaonekana ni kurusha vijembe kwa mwenza wake huyo, ambaye hivi karibuni alimuandikia waraka kuanika yale aliyokuwa akithubutu kuyafanya, na kusema yuko tayari kutoa talaka.
Wawili hao walitfunga ndoa takatifu katika kanisa la Mtakatifu Joseph la Jijini Dar es salaam, na kutengana baada ya muda mfupi wa ndoa yao, huku kukiwa na tetesi kuwa hakuna maelewano baina yao.



Nyarandu Amechukua Uamuzi Sahihi Amethibitisha CCM si Chama Tena- Peter Msigwa

$
0
0
Nyarandu Amechukua Uamuzi Sahihi Amethibitisha CCM si Chama Tena- Peter Msigwa
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Msigwa amefunguka na kumpongeza Lazaro Nyalandu na kumwambia kuwa amechukua uamuzi sahihi kuachana na chama hicho na kusema amewaonyesha watanzania mambo saba muhimu.

Msigwa amesema kitendo cha Nyalandu jana kuamua kuachana na Chama Cha Mapinduzi ni wazi kuwa amethibitisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) si chama tena bali kimekuwa chini ya dola na hakina uwezo wa kuikosoa serikali tena. Msigwa aliainisha mambo hayo saba kama ifuatavyo
1. Nyalandu umethibitisha kwamba CCM sio Chama Cha siasa tena. CCM iko chini ya miguu ya dola na haina uwezo wa kuikosoa serikali tena
2. CCM imepoteza mwelekeo wake. Imeshindwa kusimamia uchumi, siasa na uongozi wa nchi
3. Misingi ya nchi yetu imebomolewa chini ya utawala wa CCM na umeitisha mwito wa kila mmoja wetu kuijenga upya misingi ya nchi yetu
4. Tanzania imekithiri ukiukwaji wa haki za binadamu , dhulma na kutekwa na serikali mhimili wa bunge pamoja mahakama.
5. Watanzania wapate fursa ya kuchagua itikadi wanayoona inafaa na sio kutishiwa na kulazimishwa.
6. Mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini yatapatikana kwa mfumo wa demokrasia na Uhuru wa mawazo.
7. Mwisho umeonesha umuhimu wa kupata Katiba Mpya kwa sasa katika Nchi yetu
Mbali na hilo Mbunge Msigwa alimaliza na kusema kuwa "Kuishi nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inawezekana"

Ongezeko la Walaji wa Nyama ya Mbwa Lazua Taharuki Nchini China

$
0
0
Ongezeko la Walaji wa Nyama ya Mbwa Nchini China Lazua Taharuki Mitaani
Serikali nchini China kupitia wizara yake ya Afya ya Wanyama na Ukaguzi imedai kuwa ongezeko la walaji wa nyama ya mbwa nchini humo kumepelekea ongezeko la kesi za watu kupotelewa na mbwa kuongezeka.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na shirika la Change.Org nchini China kwa mwaka zaidi ya mbwa milioni 20 huchinjwa kwa kitoweo ambapo inakadiliwa kuwa mbwa milioni 2 huchinjwa kwa mwezi ikiwa ni ongezeko la asilimia 15 ukilinganisha na mwaka 2015.

Serikali ya China tayari imeanzisha msako wa kukagua leseni za bucha zinazotoa huduma ya kuuza nyama ya mbwa ili kubaini ukubwa wa ongezeko la bucha zinazofanya kazi bila kibali maalumu.

Wiki iliyopita maafisa usalama nchini humo walikamata lori lenye mbwa 200 wakisafirishwa bila kibali maalumu na tayari mbwa hao wameshapata wenyewe.

Taarifa hiyo imekuja baada ya maafisa usalama nchini humo kueleza kuwa kuna ongezeko la kesi za watu wakiripoti kila siku kupotelewa na mbwa majumbani kwao.

Tayari wanaharakati nchini China wameungana na nchi nyingine kulaani utumiaji wa nyama ya mbwa kama kitoweo huku wakidai kuwa sio unanyanyasaji wa Wanyama.

Nchini China baadhi ya watu hutumia nyama ya Mbwa kama kitoweo kama sehemu ya utamaduni wao.

Wakati hayo yanajiri, jana mtandao wa kupambana na ulaji wa nyama ya mbwa duniani wa Fight Dog Meat umeripoti kuwa nchini China kuna watu wanawauwa mbwa hao kwa kuwachoma kwa moto wa gesi hadi kufa na kuwafanya vitoweo.

Hata hivyo tayari wanaharakati wameanza kupiga vita tamasha kubwa la ulaji nyama ya mbwa la  The Yulin Dog Meat Festival linalofanyika mjini Yulin nchini China kila mwaka ambapo inakadiliwa zaidi ya mbwa elfu 10 huchinjwa.

Mahakama Yamkuta na Kesi ya Kujibu 'Scopion' Atakiwa Kujitetea Novemba 14

$
0
0
Mahakama Yamkuta na Kesi ya Kujibu 'Scopion' Atakiwa Kujitetea Novemba 14
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemkuta na kesi ya kujibu mshtakiwa Salum Njwete maarufu kama Scorpion anaekabiliwa na kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi ambae aliingia kwenye vichwa vya habari baada ya kumtoboa mtu macho.

Hatua hiyo inatokana na Hakimu Mkazi Flora Haule kusema kuwa amepitia ushahidi wa upande wa mashtaka na kujiridhisha na kuona mshtakiwa Njwete ana kesi ya kujibu.

Hakimu Haule amesema kwa sababu hizo, Mshtakiwa anapaswa kutoa utetezi kwa njia atakazopenda kama kwa kiapo ama bila kiapo ambapo baada ya kueleza hayo, Mshtakiwa Njwete alisema kuwa atajitetea mwenyewe kwa njia ya kiapo lakini pia atakuwa na mashahidi wawili ambao walitumiwa kama Mashahidi wa upande wa mashtaka jambo ambalo Hakimu Haule amelikataa na kusema atafute mashahidi wengine au ajitetee mwenyewe.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Njwete anaetetewa na wakili Juma Nassoro anaidaiwa Septemba 6, 2016 saa 4 usiku maeneo ya Buguruni Ilala Dar es Salaam, aliiba cheni ya Silva yenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000 na simu ya mkononi pamoja na fedha taslimu Sh 330,000 vyote vikiwa na thamani ya Sh 474,000 mali ya Said Mrisho Said.

Pia anadaiwa kabla na baada ya kutekeleza tukio hilo, Mtuhumiwa huyo alimchoma Mrisho sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo machoni, tumboni na mabegani ili kurahisisha kupata mali hizo.

Hakimu Haule ameahirisha kesi hiyo hadi November 14, 2017 kwa ajili ya Njwete kuanza kujitetea.

Video: Ado Afunguka Kuhusu Kukamatwa Zitto Asema Utawala Haiwezi Kumzima Zitto

$
0
0
Video: Ado Afunguka Kuhusu Kukamatwa Zitto Asema Utawala Haiwezi Kumzima Zitto
Katibu mwenezi wa ACT Wazalendo Taifa, Bwana Ado Shaibu amefunguka na kusema kuwa utawala pamoja na jeshi la polisi linapomkamata kiongozi wa chama chao, ndugu Zitto Kabwe ni kujaribu kutaka kumtisha jambo ambalo wao wanasema haliwezekani.

Ado Shaibu amesema kuwa utawala wa awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli unaminya sana Demokrasia na haki za kiraia pamoja na kuminya sauti zinazotetea haki za raia na Demokrasia.

Akili The Brain Apata Shavu Specious Afrika

$
0
0
Akili The Brain Apata Shavu Specious Afrika
MSANII aliyewahi kutamba na vibao vingi kwa staili ya Bhangra, Akil The Brain leo hii amelamba dili katika lebo ya muziki ya Specious Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Akil aliyewahi tamba na vibao kama Regina na Bongo Bhangra alisema huu ni mwanzao wa kuleta mapinduzi na kwamba alikuwa kimya tangu 2013 na sasa amerudi upya.

“Najiona kama nimezaliwa upya. Wote mnanifahamu kwa jinsi nilivyo kwenye kuimba. Nimerudi na mapinduzi mapya katika muziki. Nawapongeza Specious Afrika kwa kuniweka kundini tena,” alisema Akil.

Naye mkurugenzi wa Specios Afrika ambaye pia ni msanii, prodyuza na mtangazaji, Hennesseyy alisema kuwa, baada ya kufanikisha Specious sehemu mbalimbali ikiwemo Amerika sasa ni zamu ya Afrika.

“Tumejipanga, tumesoma muziki wa Tanzania na kuona unafaa kufanya kitu cha kitofauti kwa hiyo niwaambie tu waandishi wa habari Specious Afrika inarudi kivingine na mtarajie kuona mambo mengi.

“Tayari tuna msanii Elly Da Bway na Akil The Brain na tunategemea kutanuka zaidi ya hapa. Elly Da Bway ameshaachia nyimbo mbili mpaka sasa, wa kwanza ni Boss na sasa ameachia Sura ambao umeshaanza kutikisa. Akil naye yupo mbioni kuachia,” alisema Hennessey.
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live




Latest Images