Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Mashehe: Ndoa ya Dogo Janja, Irene Uwoya ni Batili na Hata Kama Walikuwa Wanafanya Filamu Wamekiuka Dini ya Kiislam

$
0
0
Mashehe: Ndoa ya Dogo Janja, Irene Uwoya ni Batili na Hata Kama Walikuwa Wanafanya Filamu Wamekiuka Dini ya Kiislam
WAKATI sakata la ‘ndoa’ ya msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ na mwigizaji Irene Pancras Uwoya likizidi kupamba moto, mashehe mbalimbali wameibuka na kutoa sababu zinazodhihirisha kuwa ndoa hiyo ni batili, Ijumaa Wikienda linakupakulia ubuyu wa motomoto.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Ijumaa Wikienda, mashehe watatu wa misikiti tofauti jijini Dar, walioomba hifadhi ya majina, walimkosoa Uwoya na Dogo Janja kwa kuonesha kwamba walichokifanya si sahihi.

NI BATILI
Mashehe hao walisema kuwa, ndoa hiyo ni batili kutokana na jinsi ilivyofungwa, lakini pia hata kama walikuwa wanafanya filamu, bado walikiuka taratibu za Dini ya Kiislam.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mmoja wa mashehe hao alianika sababu tano (5) zinazodhihirisha kwamba ndoa hiyo ni batili;
SABABU YA KWANZA (MATITI NJE)
Alisema kuwa, katika picha mbalimbali zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha Uwoya akiwa amevaa gauni la harusi, zinamuonesha akiwa matiti nje, jambo ambalo halijawahi kutokea kwa bibi harusi wa Kiislam kuacha nje maumbile hayo nyeti ya mwanamke yanayopaswa kusitiriwa mbele ya kadamnasi.
“Dini yetu hairuhusu kabisa mwanamke kuacha matiti wazi wakati wa kumfungisha ndoa,” alisema shehe huyo.

SABABU YA PILI (KUACHA KICHWA WAZI)
Shehe huyo aliitaja sababu ya pili kuwa, ni kitendo cha Uwoya kuonekana akiwa amevaa ‘less wigi’ huku akiwa ameacha kichwa wazi, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa dini hiyo wakati alidai kwamba, alibadili dini na kuwa Muislam kisha kupewa jina la Sheila.
“Unaanzaje kufungishwa ndoa ukiwa na liwigi lako kichwani? Pale panaonesha kabisa hata kama walikuwa wanafanya filamu, basi walishindwa kujielimisha kisawasawa,” alisema shehe huyo.

SABABU YA TATU (TATUU)
Shehe huyo alisema kitendo cha mrembo huyo kuonekana kwenye picha hizo za ndoa akiwa na tatuu mbalimbali mwilini ikiwemo ile ya msalaba alijichora mgongoni kwa juu, kilizidi kuwakera zaidi watu kwamba wawili hao hawakuwa ‘serious’ katika kile walichokuwa wakikifanya kwani hakuna shehe anayeweza kukubali kuwafungisha ndoa watu wakiwa katika mwonekano huo.
 
“Ule ni mzaha kabisa walikuwa wanafanya, mtoto wa kike umejichora tatuu halafu tena zinaonekana wazi kabisa halafu shehe aridhie tu mfunge ndoa? Utani ule,” alisema shehe huyo kwa ukali.

SABABU YA NNE (CHETI)
Kama hiyo haitoshi, shehe huyo alikwenda mbali zaidi kwa kusema, ndoa hiyo inakosa uhalali kwani hata kama ni kiki kama vile alivyokiri Uwoya kwamba ni filamu, hairuhusiwi kufanyia mchezo vyeti vya ndoa kwa kuwa viko kimahesabu na huwa vinapelekwa BAKWATA kwa ajili ya kumbukumbu ya ndoa zilizofungwa.
 
SABABU YA TANO (KUFUNGA NDOA SEHEMU MOJA)
Shehe huyo alimaliza na sababu ya tano kwa kusema, wawili hao wanaonekana wakifunga ndoa sehemu moja, tofauti na taratibu za ndoa nyingine za Kiislam kwani mwanaume huanza kufungishwa ndoa nje akiwa amezungukwa na wanaume wenzake huku bibi harusi akiwa chumbani, lakini kwao ilikuwa ni tofauti.
“Hapo ndipo utagundua kabisa kwamba hakuna ndoa pale. Unaanzaje kumfungisha halafu eti wote wanasaini cheti cha ndoa hapohapo pamoja, haipo hiyo Kiislam,” alisema shehe huyo na kuongeza:
“Licha ya hivyo, wazazi wa pande zote nimeambiwa hawakuwepo na walioshika nafasi hizo ni wasanii wenzao, jambo ambalo linaonesha kabisa siyo ndoa halali.”

MSIKIE MTABIRI MAARUFU
Akizungumzia ndoa hiyo mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya alipigilia msumari kuwa ndoa hiyo ni batili kwani kwa utaratibu wa Dini ya Kiislam, bibi harusi hawezi kukaa nusu utupu yaani matiti nje kama ilivyokuwa kwa Uwoya.
Aidha, alisema kuwa, utaratibu uliotumika siyo sawasawa na kama ni kiki, basi Dogo Janja atakuwa amemkufuru Mungu na ipo siku Mungu atamwadhibu maana ndoa ni jambo takatifu, lakini amelifanyia utani na kuwadanganya watu kuwa ameoa.
“Yaani atakuwa amemkufuru Mungu kama ndiyo hizo kiki zao wanazozifanya. Kuna mambo ya kufanyia mzaha, lakini si suala kama hili linalogusa imani,” alisema Maalim.
Chanzo Global Publishers

Nyalandu Kufikishwa Kwenye Mikono ya Sheria

$
0
0
Nyalandu Kufikishwa Kwenye Mikono ya Sheria
Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Hamisi Kigwangalla amesema viongozi wote waliohusika na rushwa kwenye wizara hiyo watafikishwa kwenye mkono wa sheria.

Waziri ameyasema hayo alipotembelea hifadhi ya Serengeti katika pori tengefu la Loliondo ambapo amesema kuna kikundi ndani ya wizara kimekuwa kikiendesha vitendo vya rushwa kikihusisha wakurugenzi na mawaziri waliomtangulia.
“Ninafahamu kuwa kuna ugawaji wa vitalu kinyume na sheria ambao nimeusitisha na nitafuatilia vitalu alivyogawa waziri Nyalandu kinyume na sheria na mkurugenzi aliyekuwepo nitawachukulia hatua”, amesema Kigwangalla.

Kigwangalla amesema kuwa atafukua mafaili yote na kuwaondoa mmoja baada ya mwingine na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wote waliohusika na vitendo hivyo ikiwemo kuwauza wanyama hai nje ya nchi.
“Siwezi kuendelea kufanya kazi mpaka nisafishwe hii nyumba kwasababu ni chafu nitaisafisha kwanza ndio niendelee na kazi aliyonipa mheshimiwa rais”, ameongeza.

Tanzia: Gavana wa Nyeri Nchini Kenya, Wahome Gakuru Afariki kwa Ajali

$
0
0
Gavana wa Nyeri Nchini Kenya, Wahome Gakuru Afariki kwa Ajali
Gavana wa kaunti ya Nyeri nchini Kenya, Wahome Gakuru amefariki mapema siku ya Jumanne kufuatia ajali mbaya ya barabarani katika eneo la Kabati katika barabara kuu ya Thika-Sagana katika kaunti ya Murang’a.
Alikimbizwa katika Hospitali ya Thika Level 5 kwa matibabu ya dharura lakini akaaga dunia.
Kaunti kamishna wa Murang’a John Elungata alithibitisha kifo hicho.
Bwana Elungata alisema kuwa kabati ni eneo hatari na madereva hukosa mwelekeo kila kunaponyesha.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa gari la gavana huyo lilikuwa na abiria wanne wakati wa ajali hiyo ,akiwemo msaidizi wake wa kibinafsi, mlinzi wake na Dereva.
Mkono na mguu wa msaidizi wake wa kibinafsi ilivunjika huku miguu ya mlinzi wake ikijeruhiwa vibaya huku Dereva akidaiwa kuwa katika hali nzuri.
Polisi wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya gurudumo moja la gari hilo kupasuka wakati mvua kali ilipokuwa ikinyesha.

Mwili wa Gavana huyo umesafirishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Lee mjini Nairobi.
Inadaiwa kuwa Gavana huyo alikuwa akielekea kuhudhuria kipindi kimoja cha radio na runinga wakati gari lake lilipokumbwa na ajali hiyo.
Daktari Gakuru ni Gavana wa pili wa Nyeri kufariki afisini baada ya Gavana Nderitu Gachagua kufariki mwezi Februari mwaka huu.

Watu Wenye Silaha Wavamia Kituo cha Runinga

$
0
0
Watu Wenye Silaha Wavamia Kituo cha Runinga
Watu wenye silaha wamevamia kituo kimoja cha Runinga mjini Kabul Afghanistan na kumuuwa mtu mmoja.
Washambuliaji watatu, waliingia kwa nguvu ndani ya jumba ambalo mna kituo cha Runinga cha Shamshad, baada ya kulipua vilipuzi.
Mlinzi na mmoja wa washambuliaji wanasemekana kuuwawa, huku operesheni ya kiusalama ingali ikiendelea.
Idadi kamili ya majeruhi bado haijajulikana.
Inaaminika kuwa kundi linalojiita Islamic State, ndilo lililohusika na uvamizi huo, hayo ni kwa mjibu wa shirika moja la habari Nchini Afghanistan, Amaq.
Mwaandishi wa BBC katika eneo hilo anasema kuwa hadi sasa anasikia milio ya risasi, kwani mshambuliaji mmoja aliyesalia anaendelea kukabiliana na walinda usalama.
Shamshad TV ilizima mara tu baada ya shambulio hilo kuanza.
"Badhi ya wafanyikazi wenzangu wameuwawa na wengine kujeruhiwa. Nilifaulu kuhepa," Hashmat Istankzai, ripota wan kituo kimoja kinacjhotangaza kwa lugha ya Pashto, ameiambia BBC.
Shamshad TV, ina vipindi vingi vinavyotangazwa kwa lugha nyingi nchini Afghanistan, ikiwemo taarifa ya Habari kwa lugha ya Pashto.
Ni mojawepo ya vituo vinavyoshirikiana na BBC.
Mji mkuu, Kabul umekuwa ukilengwa mara kwa mara hasa katika miezi ya hivi karibuni, mashambulio ambayo yanateklezwa na wanamgambo wa Taliban na wapiganaji wanaojiita Islamic State.
Afghanistan ni mojawepo ya mataifa hatari zaidi kwa waandishi habari na wafanyikazi wengine wa vyombo vya habari.
Mwezi Mei mwaka huu, Dereva mmoja wa BBC alikuwa miongoni mwa zaidi ya watu 150 waliouwawa, katika shambulio baya na kubwa zaidi la kujitoa mhanga, lililofanyika katika mji mkuu Kabul.
Mwaka jana, wafanyikazi 7 wakituo kimoja cha kibinafsi cha runinga, cha Tolo TV waliuwawa na mhanga wa kujitoa kufa wa kundi la Taliban Mjini Kabul.

Kesi Inayomkabili Mfanyakazi wa TRA ya Kumiliki Mali na Kuishi Kifahari Kinyume na Mshahara Wake Imeahirishwa

$
0
0
 MfKesi Inayomkabilianyakazi wa TRA ya Kumiliki Mali na Kuishi Kifahari Kinyume na Mshahara Wake Imeahirishwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya kumiliki mali na kuishi kifahari kinyume na mshahara wake inayomkabili Ofisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi hadi December 12, 2017 kwa sababu upande wa mashtaka haujamaliza kuandaa maelezo ya awali (PH).

Wakili wa Serikali, Vitalis Peter amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (PH) lakini bado hawajamaliza kuandaa.

“Tunaomba tupangiwe tarehe nyingine ili tuje kumsomea mshtakiwa maelezo yake,” alieleza Peter.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shahidi ameahirisha kesi hiyo hadi December 12,2017.

Mshtakiwa ana makosa mawili, inadaiwa kati ya March 21, 2016 na June 30, 2016 katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam,akiwa mwajiriwa wa TRA, kama Ofisa msaidizi wa forodha alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume na sheria.

Inadaiwa alikutwa akimiliki magari 19 ambayo ni Toyota ra4,Toyota dyna truck, Toyota viz, Suzuki carry,Toyota ipsum,toyosha wish,Toyota mark ll,Toyota regiusage,Toyota estima,Toyota Alex,Toyota Noah,Toyota crown,Toyota hiace,Toyota estima,Toyota lasso,Suzuki carry, ambayo yana thamani ya Tsh.197.6.

Kosa la pili, anadaiwa kuwa kati ya March 21, 2012 na March 30, 2016 jijini Dar es salaam akiwa mwajiri wa TRA aliishi maisha ya kipato cha juu tofauti na kipato chake yenye thamani ya Tsh. 333,255,556.24 tofauti na kipato chake.

Mshtakiwa yupo nje kwa masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya Tsh. milioni 20

Steve Nyerere Afunguka Sakata Lake na Mzazi Mwenzie Joti

$
0
0
Steve Nyerere Afunguka Kuhusu Mzazi Mwenzie Joti
Muigizaji wa filamu nchini, Steven Nyerere ameto majibu ya post zilizosambaa mtandaoni zinazodai kuwa ni amepewa onyo kali na mzazi mwenzake na Joti. Ni baada ya kumuigiza mtoto wake katika masuala ya ndoa ya Joti.

Akiongea na Bongo5, Steve amedai kuwa hakuna mtu mdogo anayetukanwa bali mtu mkubwa ndiye anayetukanwa.

“Unapokuwa baba unapokuwa kiongozi, kutukanwa ni moja ya kuwa mpana hakuna mdogo ambaye anatukanwa mkubwa ndiye anayetukanwa kwa sababu matusi ndiyo yanayomuingia na anatanua wigo,” amesema Steve.

Pia akaongeza kuwa “Kiongozi bora ni yule anayetukana na nataka kuwa ambia kuwa yale ni mambo ya kifamilia hatutakiwi kuyaongelea hayapo kwenye uzalendo.”

Safari ya Ndemla Kwenda Sweeden Yasogezwa Mbele

$
0
0
Safari ya Ndemla Kwenda Sweeden  Yasogezwa Mbele
Klabu ya soka ya Simba imetoa taarifa ya kusogezwa mbele kwa safari ya mchezaji wao Hamis Said Juma Ndemla iliyopaswa kufanyika leo.
Ndemla ambaye amepata nafasi ya kufanya majaribio ya soka la kulipwa katika klabu ya AFC Eskilstuna nchini Sweden sasa anatarajiwa kusafiri Novemba 9 mwaka huu.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tunapenda kuwafahamisha kuwa safari ya mchezaji wetu Hamis Said Juma Ndemla iliyokuwa ifanyike leo Jumanne imesogezwa mbele.

Ndemla ambaye amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini Sweden, sasa ataondoka nchini siku ya Alhamis ya tarehe 9 ya mwezi huu.

Mabadiliko haya ya safari hayataathiri muda wake wa majaribio katika klabu hiyo,ambapo atakuwa huko kwa siku 14.

Imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,

Simba Sports Club.

Haji S.Manara.

Watinga Mahakamani Kupinga Ushindi wa Marudio wa Rais Uhuru Kenyatta

$
0
0
Watinga Mahakamani Kupinga Ushindi wa Marudio wa Rais Uhuru Kenyatta
Mbunge wa zamani na mfanyabiashara maarufu John Mwau na muungano wa wanaharakati uitwao Kura Yangu Sauti Yangu, Jumatatu walifungua kesi Mahakama ya Juu kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta alioupata kwenye uchaguzi wa marudio Oktoba 26.

Aliyekuwa wa kwanza kufungua kesi alikuwa Mwau anayetaka Mahakama ya Juu kubatilisha uchaguzi huo wa marudio ulioitishwa baada ya mahakama hiyo hiyo kuweka historia kwa kuufuta ule wa Agosti 8 na kuamuru ufanyike mwingine katika muda wa siku 60.

Mbunge huyo wa zamani anapinga katika kesi hiyo kujumuishwa kwenye uchaguzi huo mgombea ambaye ametangazwa na mahakama kuwa amefilisika na kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) ilipaswa kusimamia upya mchakato wa uteuzi wa kupitisha wagombea urais, kama hukumu ilivyosema.

Baadaye wanaharakati wa Kura Yangu Sauti Yangu walifungua pia kesi kupinga ushindi wa Kenyatta katika uchaguzi ambao mpinzani wake mkuu wa National Super Alliance (Nasa) Raila Odinga alisusia.

Odinga alikuwa kiini cha ushindi wa Kenyatta kufutwa baada ya kufungua kesi Mahakama ya Juu akilalamikia dosari kadhaa na ukiukwaji wa Katiba uliofanywa na IEBC. Katika uchaguzi wa awali Kenyatta alishinda kwa asilimia 54 lakini wa marudio alijikusanyia asilimia 98 huku walioshiriki wakipungua hadi kuwa asilimia 38.8.

Polisi Watinga Makao Makuu ya ACT Wazalendo Chama Hicho Chagoma Kupekuliwa

$
0
0
Polisi Watinga Makao Makuu ya ACT Wazalendo Kwaajili ya Kupekua Chama Hicho Chagoma Kupekuliwa
Polisi wamefika Makao Makuu ya ACT, wamekutana na Katibu wa Uenezi, Itikadi na Mawasiliano ya Umma, Ado Shaibu, ambaye baada ya kuwapokea amewaeleza kuwa mwenye Ofisi ni Katibu Mkuu ambaye hayupo ofisini.

Amewaeleza pia kuwa kama Jeshi la Polisi lilitaka kufanya Upekuzi kwenye Ofisi za ACT Wazalendo, nafasi nzuri kwao ilikuwa ni jana kwa kuwa walimhoji Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo kwa Masaa 7.

Polisi wamesisitiza kufanya upekuzi leo, hivyo wameamua kumfuata Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ndugu Dorothy Semu, nyumbani kwake ili awepo wakati wa upekuzi husika.

Hili Hapa Jibu la Rosa Ree kwa Gigy Money

$
0
0
Hili Hapa Jibu la Rosa Ree kwa Gigy Money
Msanii wa muziki wa rap Bongo, Rosa Ree amejibu iwapo alishazipata taarifa za Gigy Money kuhitaji kufanya naye kolabo.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya Dow amesema uwezekano wa kufanya kolabo upo kwani Gigy ni msanii mzuri na ameshasikiliza kazi zake.

“Kweli naona kazi zake zinafanya vizuri, hatujawahi kukaa na kuongea kuhusu kufanya kazi lakini itatokea ni kitu ambacho hakina shida, tufanya tu” Rosa Ree ameiambia Bongo5.

June mwaka huu Rosa Ree alisema hana mpango wa kufanya kolabo na Shilole kwa sasa kwa sababu yeye siyo shabiki wake ila kwa upande wa Rosa Ree sawa.

“Sina hata mpango wala sitaki, sio fun wake (Shilole), labda Rosa Ree, tatizo la watu walio up wanasumbua, so hip hop its better, mimi ningepata mtu wa kuniandikia niwe nachana ningependa, I don’t love this kind of music ambayo nafanya, nafanya ili nipate hela, mimi napenda hip hop,” alisema Gigy.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..


JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU.

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.

Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi +255 622588038au 0679119679 au +255 764318107

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Picha: Nyalandu Afanya Maamuzi Ajitosa Kumtembelea Lowasa Ofisini Kwake kwa Mazungumzo

$
0
0
Nyalandu Afanya Maamuzi Ahamua Kumtembelea  Lowasa Ofisini Kwake
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu amemtembelea Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Nyalandu aliyejiondoa CCM wiki iliyopita leo Jumanne Novemba 7,2017 amemshukuru Lowassa kwa kuonyesha njia kwa wengine kuwa kuna maisha nje ya CCM.

“Mzee wangu nimekuja kujitambulisha na kusema asante kutufungulia mlango,” amesema Nyalandu katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Lowassa.

Watanzania Wawili Waliokuwa Wakienda Somalia Kujiunga na Al-Shabaab Wakamatwa Kenya

$
0
0
Watanzania Wawili Waliokuwa Wakienda Somalia Kujiunga na Al-Shabaab Wakamatwa Kenya
Watanzania wawili wamekamatwa na polisi wa kupambana na ugaidi katika eneo la isiolo nchini Kenya, wakienda Somalia ambako wanahisiwa wakienda kujiunga na Al- Shabaab

Mkuu wa polisi kituo cha Isiolo Charles Ontita amesema Watanzania hao walikamatwa na maaskari katika bara bara ya Isiolo – Moyale karibu na njia panda inayoelekea Garba, na baada ya kuwapekua ndipo walibaini walikuwa Watanzania na hawakuwa na vibali vya kusafiria.
“Maaskari waliokuwa doria walisimamisha basi na kuanza kukagua, ndipo walipowakuta wageni wawili ambao hawakuwa na vibali, waliwaambia askari kuwa walikuwa wanaenda Moyale kufanya kazi ambayo wameitiwa, na baada ya kupekua simu zao walikuta baadhi ya namba za Somalia ambazo walikuwa wakiwasiliana nazo, na kusema ndio watu waliowaitia kazi”, amesema Kamanda Ontita.
Watanzania hao wametajwa kuwa ni Juma Abbas Zuberi mwenye miaka 28 na Ali Juma Kaondo wa miaka 17, wamepelekwa katika kituo cha polisi cha Isiolo, huku wakiendelea kuchunguzwa na Akskari hao wa kupambana na ugaidi kutoka Nairobi.


TRA Kuwaburuza Mahakamani Walioshindwa Kulipa Kodi

$
0
0
TRA  Kuwaburuza Mahakamani Walioshindwa Kulipa Kodi
Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga inatarajia kuwaburuza mahakamani wawekezaji wakubwa kwenye migodi ya Madini ya almasi baada ya kushindwa kulipa kodi ya huduma ya jamii zaidi ya shilingi milioni 480 zilizotakiwa kulipwa tangu mwaka 2011 hadi mwaka huu wa 2017.

Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Steven Magoiga katika baraza la Madiwani baada ya kutokea sintofahamu katika taarifa ya fedha katika kipindi cha robo mwaka hali iliyomlazimu mkurugenzi kutamka wazi wazi juu ya mgogoro kati ya mgodi wa alimasi wa Mwadui na serikali kuwa umekuwa chanzo cha kuikosesha halmashauri ya Kishapu mapato na kuchangia kudidimiza miradi ya Maendeleo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu, Steven Magoiga amesema wawekezaji wa madini ya almasi na dhahabu wamekuwa wakikwepa kulipa kodi ya serikali hali iliyoilazimu TMAA kuchunguza na kubaini udanganyifu wa zaidi ya shilingi milioni 111 na kutoa taarifa kwa halmashauri kuwa fedha hizo ni lazima zilipwe kama kodi halali ya huduma.

Kwa upande mwingine mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu Bw. Boniface Butondo amesema wawekezaji wanaotuhumiwa wana nafasi moja ya kuketi pamoja na uongozi wa halmashauri kuweka mikakati ya kulipa deni hilo kabla ya kesi kufika mahakamani.

HESLB: Hakuna Mwanafunzi Atakayepata Mkopo Wakati Hana Vigezo Staiki

$
0
0
HESLB: Hakuna Mwanafunzi Atakayepata Mkopo Wakati Hana Vigezo Staiki
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu HESLB imesema hakuna mwanafunzi ambaye atapata mkopo wakati hana vigezo stahiki ambavyo vimeainishwa.

Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi wa bodi hiyo Abdul Razaq Badru baada ya kuwepo kwa mkanganyiko wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliokosa mkopo.

“Waombaji waliofika ofisini na wale ambao hawajafika tumesikia malalamiko yao na tunayafanyia kazi lakini mikopo watapata wenye sifa pekee kama huna sifa huwezi kupata mkopo”, amesema Badru.

Aidha Mkurugenzi amesema bajeti ya fedha za mikopo kwa mwaka wa masomo wa 2017/18 ni bilioni 427, kwaajili ya wanafunzi 122,000 wakiwemo wa mwaka wa pili na watatu, huku zaidi ya wanafunzi elfu 30 wa mwaka wa kwanza wakiwa kwenye bajeti ya kupata mkopo.

Badru amesema hadi saa wanafunzi 29,578 tayari wameshapata mikopo kiasi cha shilingi bilioni 96 na wameshaaanza masomo kwasababu walitimiza sifa za kupata mkopo. Amesisitiza kuwa hakuna mwanafunzi atakayekosa mkopo wakati amekidhi vigezo na sifa za kupata mkopo.

Mzee Majuto Afunguka Kuwa Kuna Watu Wasiojulikana Wanataka Kumuua

$
0
0
Mzee Majuto Afunguka Kuwa Kuna Watu Wasiojulikana Wanataka Kumuua
TAKRIBAN siku 10 baada ya kudai kutapeliwa milioni 25 na kampuni moja ya filamu (jina linahifadhiwa) mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, staa wa filamu za vichekesho Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ amefunguka kuwa, kuna watu wasiojulikana wanaotala kumuua, Ijumaa Wikienda limedokezwa.

Chanzo makini kililieleza Ijumaa Wikienda kuwa, staa huyo tangu atoe malalamiko ya kutapeliwa fedha zake hizo kwa Waziri Mwakyembe, amekuwa akiishi kwa wasiwasi huku akihisi kwamba anaweza kuuawa na watu wasiojulikana  kwa kuwa tu amedai haki yake.

“Yaani Mzee Majuto hana amani kabisa, amekuwa akilalamika kwamba kuna watu wanataka kumuua kwa kuwa tu alidai haki yake na mpaka sasa hajapata hata shilingi moja yupo tu, anahofia kuendelea kudai tena baada ya kumweleza waziri siku zilizopita na alipoteza namba yake ya simu kwenye ndege hivyo ameamua kunyamaza tu sasa,” kilieleza chanzo kutoka Tanga anapoishi Mzee Majuto.

Ijumaa Wikienda liliingia mzigoni ili kuujua ukweli ambapo lilimtafuta Mzee Majuto akiwa nyumbani kwake, Tanga ambapo alikiri kweli kwamba kwa sasa anaogopa kuendelea kudai kwani anatishiwa kunyongwa au kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

“Licha ya kumweleza Waziri Mwakyembe, lakini mpaka sasa sijalipwa chochote na ninaogopa kuendelea kudai kwani natishiwa kuuawa, si unajua siku hizi mtu ukidai haki yako unaweza kunyongwa au ukiwa barazani kwako ukashtukia unapigwa risasi na watu wasiojulikana.

“Nilikuwa na namba ya Waziri Mwakyembe, nilimpigia mara moja baada ya siku zile kuniahidi atalishughulikia suala langu, lakini aliniambia yupo kwenye kikao nimtafute wakati mwingine.

“Siku chache baadaye nikiwa ninasafiri kwenye ndege nilipoteza simu na namba
ikapotelea hukohuko hivyo imebidi sasa nitulie nimwachie tu Mungu atanilipia hizo fedha ninazodai maana naogopa kunyongwa jamani,” alisema Mzee Majuto.

AMKUMBUSHA WAZIRI
Hata hivyo, Mzee Majuto alimkumbusha Wazi Mwakyembe kuhusiana na suala hilo ili amsaidie kwani peke yake ameshindwa kuendelea kudai kwa kuwa ana hofu kwamba anaweza kufanyiwa kitu mbaya.

TUJIKUMBUSHE
Oktoba 27, mwaka huu, Waziri Mwakyembe alikutana na wasanii mbalimbali kujadili changamoto za kazi ya sanaa nchini na kusema katika vitu ambavyo atapambana navyo ni pamoja na watu wanaowadhulumu wasanii haki yao na kuwaibia kazi zao za sanaa.

Waziri Mwakyembe alisema: “Mzee Majuto akaniomba kitu kimoja na kuniambia anaumwa anahitaji pesa, lakini ameshafanya kazi na kampuni (akaitaja) na ameshatengeneza filamu zaidi ya 100 kwa mkataba wa kulipwa fedha ndogo tu, shilingi milioni 25, lakini huu ni mwaka wa pili hajalipwa hata senti tano na nilimuahidi kulishughulikia.”

Waziri Mwakyembe aliendelea kufafanua kuwa kwa sasa yupo tayari kutumia fedha zake mfukoni kuhakikisha Mzee Majuto anapata haki yake kwa kazi mbalimbali alizofanya na kampuni hiyo.

Source: Global Publisher


Mimi Wakwanza Kumuona Uwoya Kabla ya Dogo Janja Sikuvutiwa Kumuoa Siwezi Kuwa na Wivu- Ray

$
0
0
 Mimi Wakwanza Kumuona Uwoya Kabla ya Dogo Janja Sikuvutiwa Kumuoa Siwezi Kuwa na Wivu- Ray
Msanii Vicent Kigosi maarufu kama Ray ambaye ndiye aliyemfungulia milango ya kuingia kwenye sanaa muigizaji Irene Uwoya, amesema hawezi kuwa na wivu kwa kuolewa na Dogo Janja.

Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Ray amesema yeye alianza kumuona Irene kabla ya Dogo Janja, lakini hakuvutiwa kumuoa, hivyo hawezi kuwa na hisia za wivu kwa yeye kumuoa muigizaji huyo mwenye mvuto wa kipekee.
“Mimi siwezi kuwa na wivu nilianza kumuona Irene kabla ya Dogo Janja, Dogo Janja ni mdogo wangu na namuheshimu kwa maamuzi ya kumuoa Irene Uwoya, mimi yule ni dada yangu ambaye nimetoka naye mbali kwenye sanaa, na mimi ndiye nilimu-introduce kwenye sanaa na marehemu Kanumba, kama ningekuwa nimemuona ningetamani kuwa naye basi ningekuwa nae lakini niliamua kufanya naye kazi tu, wengine wamemuona wamemchukua, ni jambo zuri hata Mungu anafurahia”, amesema Ray.
Ray ameendelea kusema kwamba yuko tayari kumuita Dogo Janja shemeji kwa sababu ameshamuoa dada yao Irene Uwoya, na kuhusu suala la umri halijalishi sana kwani kikubwa ni upendo.
“Mapenzi ni kipenda roho, na kipenda roho hula nyama mbichi, kama wamependana wenyewe inatosha, niko tayari kumuita shemeji kwa kuwa kashamuoa dada yangu”, amesema Ray.
Hivi karibuni Dogo Janja na Irene Uwoya wamefunga ndoa jambo ambalo limewashtua watu wengi, kwa kuwa kuna tofauti kubwa ya umri kati ya wawili hao.

Kutana na Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed Kutoka Bagamoyo...Ana Dawa za Kurudisha Mapenzi na Zingine Nyingi

$
0
0
MIUJIZA YA SHARIFU SEIF MOHAMED KUTOKA BAGAMOYO.

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,
(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:
Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

USHAURI: kama unahitaji msaada ni  bora kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate  msaada kwa haraka.

Dogo Janja Yamfika Hapaaaa! Amtolea Povu la Kufa Mtu Mtangazani Mmbea Mmbea Soudy Brown na Kumwanika

$
0
0
Yule Kijana mdogo kwenye Tasnia ya Bongo fleva Abdulazizi Chande 'Dogo janja' ambaye wiki kazaa zilizopita amejikaza ubongo na kuamua kufunga ndoa na Diva kwenye tasnia ya BongoMovie mwanadada Irene 'Sheila' Uwoya ,

Juzi ameamua kumtolea povu mtangazaji 'Mmbea' Wa Tv na Radio Clouds Soudy brown ambaye amekuwa akimuandama mara kwa mara dogojanja kwa suala la ndoa yake na Mwanadada Uwoya kwakile kinachoonekana Tofauti ya umri kati ya wanandoa hao,

Baada ya kuona Soudy brown anavuka mipaka Dogojanja ameamua kumtolea povu la wiki Soudy huku akipost picha inayomuonesha Soudy brown sura yake halisi bila ya mask, Naona Badamu banazidi Kumwagikaaaaa.

Azam FC Wagutuka...Wampiga Chini Mchezaji wa nje Baada ya Kutokuonyesha Kiwango

$
0
0
Klabu ya soka ya Azam FC imetangaza kuachana na nyota wake wa kimataifa Yahaya Mohamed kutoka nchini Ghana baada ya kushindwa kuonesha kiwango cha kuridhisha.

Taarifa ya klabu hiyo imesema kuwa viongozi wamekaa na mchezaji huyo na kumalizana vyema kwasababu pande zote mbili zinatambua changamoto za mchezo wa soka kuwa kuna mazingira kugoma lakini pia falsafa kutoendana na mchezaji.

Aidha klabu hiyo imesema itaendelea kukumbuka mchango mkubwa wa Yahaya alioutoa kwenye timu hiyo hususani kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi ambapo aliisadia klabu kuibuka mabingwa.

Yahaya ataondoka nchini kesho kurejea kwao Ghana. Azam FC imesema itaanza mapema mchakato wa kumpata mrithi wa Yahaya ambaye atasajiliwa wakati wa dirisha dogo kwa kufuata mapendekezo ya mwalimu.

Azam FC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa na alama 19 nyuma ya Simba SC ambayo pia ina alama 19 zikitofautiana kwa magoli ya kufunga na kufungwa.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images