Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Yanga: TFF Inavuruga Mipango Yetu

$
0
0
Yanga: TFF Inavuruga Mipango Yetu
SIKU chache baada ya uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kusema kuwa Tanzania Bara itashiriki michuano ya Chalenji itakayofanyika nchini Kenya, uongozi wa Yanga umedai kuwa michuano hiyo itawavurugia mipango yao waliyojiwekea kwa ajili ya Ligi Kuu Bara msimu huu.

Michuano ya Chalenji ambayo hushirikisha timu za taifa za nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Ce­cafa), imepangwa kuanza Novemba 25 huko nchini Kenya.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alisema wao walikuwa wamejipanga kwa kuzingatia ratiba ya awali ya ligi kuu ambayo ilikuwa haionyeshi kama kutakuwepo na mashindano ya Cha­lenji.
“Ligi inaposimama kila wakati hakika inatu­vurugia mipango yetu ambayo tulikuwa tu­mejiwekea kwa ajili ya kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu.

“Kama walijua kabisa kuwa safari hii tuta­shiriki michuano ya Chalenji walipaswa kutu­julisha mapema katika ratiba ligi kuu kabla ya kuanza kwa ligi ili tuweze kupanga mikakati yetu tukijua kuwa itakapofika tarehe fulani ku­takuwa na hiki siyo kutukurupusha namna hii.

“Wanatuvurugia mipango yetu lakini pia wanatuongezea gharama za uendeshaji wa timu, kwa sababu katika muda huo ambao ligi itakuwa imesimama tutalazimika kuiweka timu kambini kwa muda mrefu kitu ambacho hakikuwa kwenye mipango yetu,” alisema Mk­wasa.

Serikali Yazindua Ndege Itakayofanya Oparesheni Kutokomeza Uvuvi Haramu

$
0
0
Serikali Yazindua Ndege Itakayofanya Oparesheni Kutokomeza Uvuvi Haramu
Serikali imekuja na mkakati mpya unaolenga kutokomeza uvuvi haramu, baada ya kuzindua ndege maalum ambayo itakuwa inafanya oparesheni katika eneo la bahari kuu.
 Uzinduzi huo wa safari mpya ya ndege umefanywa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ambapo amebainisha kuwa lengo ni kudhibiti uvuvi haramu katika eneo la bahari kuu.
Ndege hiyo imetua hapa nchini kwa mara ya kwanza kutoka nchini Mauritius kwa ajili ya kufanya doria ya majini. Waziri amesema ujio wa safari hiyo mpya ya ndege ni matokeo ya ushirikiano na nchi za Ukanda wa Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi ili kudhibiti uvuvi haramu kwa njia zote.
“Tumeruhusu ndege ya doria, ili kuongezea nguvu katika njia za kudhibiti wavuvi haramu ambapo awali tulianza kwa njia ya majini kwa kutumia Meli  na sasa ni kwa njia ya anga kwa kutumia ndege hii kutoka Mauritius”.
Aidha Ulega ameeleza kuumizwa na namna ambavyo wavuvi haramu hutumia muda mchache ambao ni chini ya dakika tano kuharibu matumbawe kwa kupiga mabomu kisha athari zake huenda hadi miaka 100.

Kagasheki Amjia Juu Kigwangala " Naomba Athibitishe Ukaribu Wangu na OBC, Vitalu Nilivogawa Nikiwa Waziri na Rushwa Niliyopokea"

$
0
0
Kagasheki Amjia Juu Kigwangala " Naomba Athibitishe Ukaribu Wangu na OBC, Vitalu Nilivogawa Nikiwa Waziri na Rushwa Niliyopokea"
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki amemvaa Waziri wa sasa wa sasa wa wizara hiyo Mh. Hamisi Kigwangalla kwa kumtaja kuwa ana mahusiano ya karibu na Mkurugenzi wa OBC ambaye ana kashfa kubwa ya rushwa.
Kupitia mtandao wake wa Twitter Balozi Kagasheki alimtaka Mh. Kigwangalla amthibitishie kuhusu ukaribu wake na Mkurugenzi huyo na kuhusu rushwa aliyowahi kupokea ikiwa ni pamoja na kuuza vitalu.
Balozi ameandika "Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla alinukuliwa kutaja "muwekezaji OBC" alivo na kashfa za Rushwa. Alinitaja mimi kuwa karibu na OBC. Napenda athibitishe ukaribu huo, vitalu nilivogawa nikiwa Waziri na rushwa niliyopokea," Balozi Kagasheki
Hata hivyo baada ya ujumbe huo ambao ulienda moja kwa moja kwa Waziri Kigwangalla naye alijibu ujumbe huo ambao ulielekezwa kwake na kumuomba Mstaafu huyo wayazungumze nje ya mtandao
"Mhe. Balozi Kagasheki , wewe ni kaka yangu na unajua nakuheshimu sana. Tuongee kindugu nje ya hapa! Kuweka sawa ni kwamba 'sikukutaja!" Kigwangalla.
Hivi karibuni Waziri Kigwangalla aliweka wazi kwamba amewaondoa Askari wote wa kituo cha Geti la Kleins kwa kuwa wamekuwa wakitumika na mwekezaji huyo ambaye ana uhusiano wa Karibu na Prof. Songorwa (aliyemsimamisha kazi siku chache zilizopita) na alikuwa na uhusiano ya karibu na Prof. Maghembe, Lazaro Nyalandu, balozi Kagasheki na Mawaziri wa Maliasili na Utalii wa zamani.
Balozi Kagasheki aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika uongozi wa serikali ya awamu ya nne ambapo aliongoza wizara hiyo Mwaka  (2012-2013)

Ndemla Awasili Salama Sweeden

$
0
0
Ndemla  Awasili Salama Sweeden
Klabu ya soka ya Simba imethibitisha kuwa kiungo wake, Said Hamisi Juma Ndemla amewasili salama Sweden tayari kuanza  kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini nchini humo.
“Said Ndemla amewasili salama nchini Sweden tayari kuanza majaribio yake katika klabu ya AFC Eskilstima inayoshiriki ligi kuu nchini humo.” Imesema klabu ya Simba.

Picha: Bondia Iddy Mkwela Afunga Ndoa na Zawadi Mcharo

$
0
0
Picha: Bondia Iddy Mkwela Afunga Ndoa na Zawadi Mcharo
Iddi mkwela kushoto akionesha pete yake pamoja na mkewe Zawadi Mcharo
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ kulia akimpa hongera bondia Iddi Mkwela baada ya kuchukuwa jiko
Bondia IDDI Mkwela akipiga goti wakati wa kufunga ndoa

Polisi Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Mnunuzi Feki wa Nyumba za Lugumi

$
0
0
Polisi Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Mnunuzi Feki wa Nyumba za Lugumi
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamtuhumu Dk. Louis Shika, kutumiwa na mfanyabiashara Said Lugumi, ili kukwamisha uuzwaji wa nyumba zake zinazoshikiliwa na serikali.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ameeleza wanatilia shaka kuwa mtuhumiwa alitumwa na Lugumi kukwamisha mchakato wa mnada, kwani mazingira ya mnada, na namna mtuhumiwa aliyokuwa anataja bei yanawafanya kuamini kuwa aliwekwa ili wanunuzi wengine wasiweze kununua nyumba hizo.

“Aliwekwa na Lugumi mwenyewe ili mnada usifanyike ingawa sina fact za kudhibitisha hilo, ila alichokuwa anakifanya kinatufanya tuamini hivyo. Alikuwa ana-top bei kila nyumba ili washiriki wengine wasinunue,” amesema Mambosasa.

“Ila jinsi alivyo, kwa maana ya uvaaji na kuongea kwake watu walitia mashaka kama ataweza kununua ndipo akatakiwa kutoa asilimia 25 na kushindwa kulipa. Tunaendelea kumshikilia kwa mahojiano,” aliongeza na kusema jeshi hilo linaendelea kumshikilia Louis kwa mahojiano zaidi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Waziri Atoa Ufafanuzi Juu ya Tamko Alilolitoa la ‘Msichana kuolewa hadi cheti cha kidato 4’

$
0
0
Waziri Atoa Ufafanuzi Juu ya Tamko Alilolitoa la ‘Msichana kuolewa hadi cheti cha kidato 4’
Naibu waziri TAMISEMI, Joseph Kakunda ametoa ufafanuzi kuhusu kauli yake ya anaetaka kuolewa lazima awe na cheti cha kidato cha nne ndio afunge ndoa.  Mh. Kakunda amesema kuwa huo ni utekelezaji wa sera mpya ya elimu sio leo.

Akizungumza leo bungeni mjini Dodoma baada ya Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara kuihoji serikali kuhusu tamko hilo ambapo serikali imesema kuwa utakapo fika muda huo kithibitisho muhimu ni lazima awe na cheti.

“Nilisema sera mpya ya elimu ya mwaka 2014, huko tunakoelekea inabadilisha sasa mfumo wa sasa elimu ambao utahitaji mtoto aanze aanze chekechekea mwaka 1 asome shule ya msingi miaka 6 shule ya sekondari miaka minne na hii itakuwa lazima kwaatakae maliza darasa la kwanza hadi amalize form four tutakapo fika wakati huo kithibitisho muhimu ni kwamba huyu mtoto awe la living certificate wakati huo sio leo kwahiyo huo ni ufafafuzi kabisa wa sera mpya,” amesema Mh. Kakunda

Mkuu wa Mkoa Atoa Tamko 'Marufuku Kuitana Baby'

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Atoa Tamko 'Marufuku Kuitana Baby'
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amepiga marufuku tabia ya wanafunzi wa kike kuitwa “Baby” kwa madai kuwa ni chanzo cha kujiingiza kwenye mapenzi.

Tamko hilo amelitoa kwenye ziara yake ya siku moja alipotembelea shule ya sekondari Nasuli iliyopo wilayani Namtumbo, ambapo amekemea tabia hiyo kwa kusema inachochea wasichana kujihusisha na vitendo vya mapenzi wakiwa shule.
“Msikubali kuitwa “Baby” kwasababu kukubali kuitwa “Baby” ni chanzo cha kujiingiza kwenye mapenzi msikubali kuitwa “Queen” wewe ni mwanafunzi unatafuta maisha”, amesema Mndeme
Aidha RC Mndeme amewaasa wanafunzi hao kuweka bidii kwenye masomo na kujiepusha na vishawishi ambavyo vinapelekea kupata ujauzito na kulitia hasara taifa ambalo linalipa ada ili wasome bure.
Kwa upande mwingine mkuu huyo wa mkoa amewaonya wanafunzi hao wasijite wazuri kwani hiyo huwafanya wavulana wabaya wawashawishi kufanya mapenzi.


JE, Unasumbuliwa na Upungufu wa Nguvu, Hamu ya Tendo la Ndoa au Maumbile Madogo ya Uume?

$
0
0
JE, UNASUMBULIWA NA UPUNGUVU WA NGUVU, HAMU YA TENDO LA NDOA AU MAUMBILE MADOGO YA UUME?
      SOMA HAPA
    Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume au ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa limezidi kuongezeka kwa kasi duniani na limekuwa chanzo kikubwa cha ndoa nyingi na mahusiano kukosa uaminifu kutokana na wengi kutoka nje ya ndoa ili kupata mtu atakayemtosheleza na kumfikisha kileleni. Pia udogo wa maumbile ni tatizo kubwa na limekuwa likiwakosesha wanaume wengi uwezo wa kujiamini katika tendo na kusababisha tendo hilo kutokufanyika kwa usahihi. Hili pia huchangia kwa kiasi kikubwa wanawake wengi kwenda nje ya ndoa ( MAHUSIANO) kutafuta mbadala wake.

      BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa
☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni
☆Uume kusinyaa katikati ya tendo
☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.
     Kwa kutumia mimea na matunda🍅🍍🍓🌿🍉🍒🍎 @markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL:- kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 5.5 hadi 6 @150,000/=
3.VigRX CREAM:- ni gely iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile kwa wastani wa inch 6.5 hadi 8 na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200,000/=
4.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150,000/=
5.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni @130,000/=
      BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA KIAFYA NA ZIMETHIBITISHWA
🍉🍒🍓🌿🍍🍅🍀🍉
    KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WETU WA INSTAGRAM :-
      @markson_beauty_pr

Mawasiliano (+255)
           0767447444 na
              0714335378

        UTAPATA HUDUMA
    NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.

Mahakama Yatupilia Mbali Kesi ya Diamond, Hamissa Mobetto

$
0
0
Mahakama Yatupilia Mbali Kesi ya Diamond, Hamissa Mobetto
Mwanamitindo Hamisa Mobeto amekwaa kisiki mbele ya Diamond Platnumz baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto kutupilia mbali kesi aliyofunguliwa mwanamuziki huyo juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul.
Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Novemba 10 ,2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.
Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi.  Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.
Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.
Mobeto  anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.
Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto  anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.
Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto  akidai  gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Sh 5 milioni  kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.

Serikali Yaikana Taasisi ya Mikopo ya Elimu ya Juu

$
0
0
Serikali Yaikana Taasisi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
Serikali imesema haiitambui taasisi ya Tanzania Social Support Foundation (TSSF) ambayo inajihusisha na mikopo ya elimu ya juu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema hayo leo Ijumaa Novemba 10,2017 wakati akijibu mwongozo wa Spika ulioombwa na mbunge wa Mafinga Mjini (CCM), Cosato Chumi.

 “Kuna taasisi imetoa matangazo kuwa kwa wanafunzi waliokosa mikopo watapata mikopo katika hiyo taasisi na application fee (ada ya maombi) ni Sh30,000. Napenda kufahamu u-genuine (uhalali) wa hii taasisi,” aliuliza Chumi.
Amehoji ni nini kitakachotokea iwapo wanafunzi watatoa kiingilio (ada ya maombi) hicho na mwisho wa siku ikaja kutoa mikopo kwa watu wachache zaidi.

Akijibu swali hilo, Profesa Ndalichako amesema wizara yake haiitambui taasisi hiyo na kwamba imesikitika kuona tangazo katika gazeti (hakulitaja) inayaonyesha kuwa watakuwa na shughuli ambayo mgeni rasmi atakuwa ni yeye.

“Siitambui (hiyo) taasisi, hawajanikaribisha. Nitumie nafasi hii kutoa tahadhari kwa Watanzania wawe makini kwa sababu unapoona mtu anatumia jina lako kabla hata hajafika kwako ni jambo ambalo kama Serikali nimelipokea nitalifanyia kazi ili kujua uhalali wake,” amesema.

Amesema watakaoamua kutoa Sh30,000 kujiunga na taasisi hiyo wafanye wakitambua kuwa Serikali haitambui taasisi hiyo.

Siku chache zilizopita taasisi hiyo ilitoa tangazo katika baadhi ya magazeti kuwataka wanafunzi kuomba mikopo katika taasisi yao na walipe Sh30,000 za kufanya maombi.

Taasisi hiyo ilitoa taarifa nyingine kuwataka Watanzania kuupuuza taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya jamii kuwa wao ni matapeli.

Brigty Akataa Kufananishwa na Belle 9 "Kunatofauti Kubwa Kati ya Mimi Naye Nilianza Kuingia Studio Kabla Yake"

$
0
0
Brigty Akataa Kufananishwa na Belle 9 "Kunatofauti Kubwa Kati ya Mimi Naye Nilianza Kuingia Studio Kabla Yake"
Msanii wa Muziki Bongo Bright amesema kuna utofauti mkubwa kati yake na Belle 9.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri ngoma ‘Ni Wewe’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa wapo wanaowafanisha lakini kiuhalisia hawafanani na walishafanya hata ngoma pamoja ili mashabiki kuona utofauti wao.

“Hapana, mimi nimeingia studio kwa mara kwanza mwaka 2006 sidhani kama Belle 9 alikuwa amefahamika lakini kutokana amefahamika na mimi nimekuja kufahamika baadaye yeye ameshapata nafasi lazima mtu awe anaongea hivyo” amesema Bright.

Ameongeza kuwa kutokana na watu kuwafananisha ndio sababu ya kufanya kazi kwenye menejiment moja kipindi cha nyuma ambapo hata uongozi wao ulikuwa unawafanisha lakini kila mmoja ana kitu chake.

Jeshi la polisi Lamkamata Mfanyabiashara Anayeuza Risasi Mtaani

$
0
0
Jeshi la polisi Lamkamata Mfanyabiashara Anayeuza Risasi Mtaani
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam,limesema kuwa tarehe 6, Novemba mwaka huu maeneo ya Serengeti Kigamboni lilipokea taarifa ya kuwepo kwa mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Willy Peter kuwa anafanya biashara ya kuuza risasi mtaani. Polisi walifanya ufuatiliaji na hatimaye kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na risasi 69 za kivita aina ya FN G3.
Katika mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kuwa risasi hizo alipewa na mtu aliyemtaja kwa jina la Matabu William kwaajili ya kwenda kuziuza na kwamba alimpatia risasi hizo huko nyumbani kwake Kiwalani jijini Dar es salaam.

Hata hivyo polisi walifika nyumbani kwa Matabu William Matoke (52) kiwalani ambapo alikiri kufanya biashara hiyo ya risasi na alipopekuliwa katika nyumba yake hiyo alikutwa na risasi moja aliyokuwa ameifukia pembezoni mwa nyumba yake na kufanya jumla ya risasi zilizokamatwa kuwa 70.

Aidha Kamanda Mambosasa amesema kuwa watuhumiwa wote wawili wanaendelea kuhojiwa zaidi na upelelezi utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Frank Lampard Amkingia Kifua Mourinho

$
0
0
Frank Lampard Amkingia Kifua Mourinho
Nyota wa zamani na mfungaji wa muda wote wa klabu ya Chelsea Frank Lampard, amemkingia kifua kocha wa Manchester United kuwa hastahili lawama endapo hatotwaa ubingwa wa England msimu huu.
Lampard ambaye alitwaa mataji matatu ya EPL chini ya Mourinho amesema ikitokea kocha huyo hajatwaa ubingwa wa EPL msimu huu hastahili lawama bali lawama ziende kwenye ubora wa wachezaji alionao kwenye timu.
“Mourinho ni kocha anayependa kushinda na hufundisha mbinu ya kushinda tu tofauti sana na makocha wengine kama Pep Guardiola ambaye hufundisha pia kucheza mpira wa kuvutia hivyo inapokuja suala la kutopata matokeo ni ubora wa wachezaji na sio Mourinho”, amesema Lampard.
Siku za hivi karibuni Mourinho amekuwa akikosolewa kuhusu mfumo wake wa uchezaji wa kujilinda zaidi ambao awali haukuwa unatumiwa na Manchester United, ambayo ilizoeleka kwa kushambulia zaidi kuliko kujilinda.
Manchester United ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 23 nyuma ya vinara, mahasimu wao wa jiji Manchester City ambao wana alama 31 katika michezo 11 ya msimu huu.

Tanzia: Tasnia ya Habari Yapata Pigo

$
0
0
Tanzia: Tasnia ya Habari Yapata Pigo
Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Rose Athumani amefariki dunia jana usiku Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Taratibu za mazishi , zinaendelea nyumbani kwa Mjomba wake anayeitwa Pauli Mushi huko Mbezi Mpigi Magohe jijini Dar es Salaam.

Familia hiyo ilisema kuwa Rose alikuwa akisumbuliwa na homa kali iliyosababisha kifo chake kwenye Hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa.

Kwa mujibu wa Mjomba wa Marehemu, shughuli za kuaga mwili zitafanyika Jumapili na Marehemu atasafirishwa kwao Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mazishi siku ya Jumatatu.

Marehemu ameacha mtoto mmoja wa Kiume ambaye yuko kidato cha tatu.Marehemu aliwahi kufanya kazi katika Kampuni ya Mwananchi Communications LTD

Kaimu Mhariri wa Michezo, Zena Chandea alisema kuwa alimfahamu Marehemu Rose tangu mwaka 2009 alipotokea gazeti la The Citizen. Alisema kuwa Rose alikuwa ni rafiki wa kila mtu na alikuwa na tabasamu muda wote.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

Kimenuka...Mahakama yatengua Hatua Prof. Lipumba ya Kufukuzwa Wabunge 8 CUF

$
0
0
Mahakama Kuu leo imetengua kufukuzwa kwa Wabunge 8 na Madiwani 2 wa Chama cha Wananchi, CUF na kusitisha pia mchakato wa kuwafukuza uanachama mpaka shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

 Aidha Mahakama hiyo pia imemzuia Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, Magdalena Sakaya na Bodi ya Wadhamini ya CUF kujadili kuhusu uanachama wa Wabunge na Madiwani hao.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma ya CUF Taifa, imeeleza kuwa, Mahakama Kuu imekubaliana na Hoja za Wabunge 8 wa chama hicho na imeona hoja za msingi za madai yao zinazopaswa kuangaliwa kuhusu uhalali wa masuala yote yaliyowasilishwa mbele ya Mahakama hiyo.

Imefafanua kwamba, Mahakama Kuu pia imeyatupilia mbali mapingamizi mengine yote yaliyowekwa na Prof. Lipumba na Wenzake katika shauri hilo.

Shilole Amtelea Povu Barakah The Prince Baada ya Kumuhusisha Katika Mchezo Mchafu

$
0
0
Baada ya Barakah The Prince kumuhusisha Shilole katika kile anachodai kufanyiwa mchezo mchafu katika YouTube channel yake, hatimaye Shilole amejibu.

Barakah alimshtumu Mx Carter kuwa ndiye anafanya mchezo mchafu katika YouTube yake na taarifa hizo alipatiwa na Shilole kitu ambacho kimekanushwa.

Shilole amesema Barakah anataka kumgombanisha na Mx ambaye amekuwa akimsaidia katika mambo mengi ikiwemo kurudisha page yake ya Instagram ambayo ilidukuliwa.

“Lakini kwanini huyo mtoto anapenda kugombanisha watu ndio maana haelewani na watu kwa sababu ya mambo yake anayoyafanya siyo vizuri kama unataka kuongea na mtu mfuate binafsi si mpaka upitie kwa mtu mwingine” amesema.

“Sikipendi nasema ukweli halafu yule ni mdogo wangu namuheshimu, yule mtoto ajipange tunajua sometime unataka kiki lakini siyo za namna hiyo, ana dharau sana yule mtoto, ninasema haitampeleka popote, mimi kwangu hatapata kiki bali nitamuharibia, sitoe kiki kishenzi” Shilole amesisitiza.

Shilole ameongeza kuwa hajawahi kuongea na Barakah jambo kama hilo na mara ya mwisho waliongea kwenye simu ambapo Barakah alimuomba amsaidie kumpostia wimbo wake.

Vyakula Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa Kwa Haraka Kwa Mwanamke

$
0
0
Ni kweli kwamba kuna wanawake wengine huwa hata wakichezewa au kushikwashikwa kila mahali na mwanaume ili apate ashki[nyege] ya kufanya tendo la ndoa huwa ni kazi bure kwani hamu haimjii haraka au haimjii kabisa na hata akiamua kufanya anafanya tuu ili kumridhisha mwenzake.

Japokuwa hisia za mwanamke zipo mbali mno lakini kama mwanaume atamshikashika pande tofautitofauti za mwili wake na kumletea utundu wa hapa na pale basi hisia huja na akajiskia ni mwenye kuhitaji tendo hilo la kiutu uzima na akaweza ipasavyo.

Kama na wewe ni mmojawapo kati ya wahanga wa tatizo hilo nakushauri tumia dawa hizi zenye kupatikana kiurahisi kabisa katika mazingira yetu kwani ni zenye kusaidia kutibu kabisa matatizo ya kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa wanawake kwa haraka zaidi.



MBEGU ZA FENESI
Mbegu za fenesi zinafahamika na kila mmoja,ni zile ambazo zinapatikana ndani ya tunda la fenesi,kama mwanamke anapendelea kula tunda hizo kuanzia kumi au zaidi kila baada ya siku 4 baada ya kuzichemsha na kuiva vizuri basi hamu ya kufanya tendo la ndoa zitamzidia na atakuwa ni mwenye kutamani kufanya mchezo huo kwa matamanio makubwa sana....hii ni tiba nzuri kwa wanawake wenye tatizo hili.



UJI WA ULEZI
Wanawake wanashauriwa kunywa uji wa ulezi kila siku asubuhi kwani uji huu una uwezo wa kuamsha hisia za mapenzi.



MUHOGO MBICHI
Imethibitishwa kwamaba kama muhogo mbichi kama utapendelewa kuliwa na mwanamke kiasi cha vipande5 pia vina uwezo wa kuamsha hisia za mapenzi au tendo la ndoa kwa wanawake.


KOROSHO
Nazo zinatajwa ni nzuri sana kwa kumuongezea mwanamke hamu ya kufanya tendo la ndoa akiwa ni mwenye kuzila mara kwa mara.


Tazama Msanii Rosa Ree Alivyofanya Maajabu Kwenye Video Hii Hapa Chini:


Rosa Ree Aishangaza Dunia Kwa Kuachia Video yake Hii Mpya Usiku wa Leo...Itazame Hapa

$
0
0

Rapper wa kike kutoka Tanzania Aitwaye Rosa Ree usiku wa Jana ameendelea kuonyesha kuwa yeye ndio mkali wa Kurap kwa upande wa wadada Afrika baada ya kuachia Video kali ya wimbo wake unaitwa Dow...Itazame Hapa Chini Mtu Wangu....

 Press Play
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images