Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Sio Rahisi Mimi Kupotea Kwenye Game kama Wengine- Ebitoke

$
0
0
Sio Rahisi Mimi Kupotea Kwenye Game kama Wengine- Ebitoke
UNAMKUMBUKA msanii wa vichekesho aliyejichukulia umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, Anna Exavery ‘ Ebitoke’, amedai kuwa bado hajapotea kwenye gemu kama wengine wanavyodhani.

Akizungumza na Full Shangwe, Ebitoke alisema kuwa, si rahisi kwa yeye kupotea kwenye gemu kwa sababu amezaliwa kuchekesha, ana madude ya hatari ingawa kwa sasa yuko kwenye majukumu mengine.

“Ha ha ha haaa! Siyo rahisi kupotea kihivyo kama watu wanavyodhani, niko na madude ya hatari sijayaachia, sema kuna majukumu mengine ya kikazi nayafanya,”alisema Ebitoke

Rais Magufuli Awapa Ujumbe Huu Nape Nnauye, Hussein Bashe

$
0
0
Rais Magufuli Awapa Ujumbe Huu Nape Nnauye, Hussein Bashe
Rais John Magufuli amewataka wabunge wawili wa CCM, Nape Nnauye na Hussein Bashe, ambao michango yao bungeni imekosoa uendeshaji uchumi, wampelekee majina ya wawekezaji wanaokwamishwa ili awape kazi.

Wabunge hao wa Mtama na Nzega Mjini waliikosoa Serikali wakati wa kujadili Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa mwaka 2018/2019.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ambaye alishutumiwa na wabunge hao kumpotosha Rais, alisema wakati akihitimisha mjadala huo kuwa alipigiwa simu na mkuu wa nchi na kuelezwa hayo.

“Naomba ninong’one na Bunge lako tukufu. Mheshimiwa Rais Magufuli aliposikia huu mjadala, alinipigia simu na aliniambia hivi,” alisema Waziri Mpango.

“Waziri, mwambie ndugu yako mheshimiwa Nape na mheshimiwa Bashe kuwa nawataka sana hao wawekezaji kwenye ujenzi wa Standard Gauge Railway.

“Wawalete hata kesho niko tayari kuwapa reli ya kutoka Kaliua –Mpanda au Isaka-Mwanza au reli ya Mtwara-Mchuchuma hadi Liganga waijenge.

“Hayo ni maneno ya mheshimiwa Rais. Natumaini waheshimiwa husika will raise up to this challenge from his excellence the president (wataifanyia kazi changamoto ya mheshimiwa Rais.”

Akijibu hoja za wabunge hao na wengine, Dk Mpango alisema si kwamba Serikali imeiweka pembeni sekta binafsi bali bado haijakaa vizuri na wakati mwingine inakuja na masharti yasiyotekelezeka.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

$
0
0

Mnunuzi Feki wa Nyumba za Lugumi Kupimwa Akili

$
0
0
Mnunuzi Feki wa Nyumba za Lugumi Kupimwa Akili
Bilionea Dkt. Luis Shika ambaye wiki iliyopita alitangaza kununua nyumba za kifahari za mfanyabiashara za Said Lugumi, zilizopo eneo la Bweni JKT jijini Dar es salaam anatarajiwa kupelekwa hospitali kupimwa afya ya akili.

Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Polisi (SACP), Benedict Kitalika, ambapo amesema uamuzi wa kumpeleka hospitali Dkt. Shika  kuchunguzwa afya ya akili yake, umetokana na uchunguzi wa awali ulioonesha anaweza kuwa na tatizo hilo huku akidai kuwa uchunguzi huo utalisaidia Jeshi la Polisi kukamilisha uchunguzi.

“Tunatarajia kumpeleka hospitali wakati wowote ili kuangalia kama kuna tatizo katika afya ya akili au la kutokana na historia yake ya maisha inavyojionyesha, hali ambayo inaweza kutupa majibu sahihi.” amesema Kamishna Kitalika.

Kamishna Kitalika amesema uchunguzi wa awali ulihusisha historia ya maisha yake inayoonyesha ni msomi aliyewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi nchini Urusi kabla ya kurudi nchini na kuishi kwenye chumba kimoja cha kukodi, huku sababu za kurudi kwake zikiwa hazijulikani.

“Na sisi tumejiuliza sana kuhusu utimamu wa akili kama upo sawa au kuna tatizo la kisaikolojia, kwa sababu ukiangalia historia yake inaonyesha wazi ni msomi mzuri ambaye ameshika nafasi za uongozi nchini Urusi, lakini maisha anayoishi nchini si ya kuridhisha. Hatujui amepatwa na nini hadi kufikia hatua ya kukodi chumba kimoja cha kuishi katika Mtaa wa Tabata, huku mwonekano wake ukiwa haupo sawa kisaikolojia.” amesema Kamishna Kitalika.

Hata hivyo, tayari jalada la kesi ya Dkt. Shika limepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ili aweze kuangalia kama kuna jinai yoyote iliyotendeka kwa mtuhumiwa huyo au la.

Akizungumzia hilo, Kamishna Kitalika amesema licha ya jalada hilo kuwa mikononi mwa AG, imebainika kuwa baadhi ya kanuni wakati wa mnada wa nyumba za Lugumi hazikufuatwa, ikiwepo ya kulipa asilimia 25 pale pale baada ya mteja kujitokeza hali ambayo inaongeza shaka kwa Dkt. Shika.

“Katika mnada ule, baadhi ya kanuni hazijafuatwa ikiwamo ya kumtaka kulipa asilimia 25 pale pale mara baada ya kununua, lakini suala hilo halijafanyika badala yake waliendelea kupiga mnada nyumba nyingine, hivyo kama taasisi za uchunguzi tunapaswa kufuatilia hatua kwa hatua,” amesema Kamishna Kitalika.

Wiki iliyopita, Dkt. Shika alijitokeza kwenye mnada wa nyumba tatu za Lugumi, mbili zipo Mtaa wa Mbweni JKT na moja ipo Upanga na kushinda minada yote.

Mnada huo ulifanywa na Kampuni ya Udalali ya Yono kwa amri ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo Dk. Shika aliahidi kununua nyumba hizo kwa thamani ya Sh bilioni 2.3 lakini alishindwa kulipia asilimia 25 ya fedha hizo ambazo ni shilingi milioni 800 kitu ambacho kilipelekea akamatwe na polisi kwa kosa la kuharibu mnada na utapeli.

Chanzo : Mtanzani

Vanessa Mdee Afunguka Kuhusu Kurudiana na Jux

$
0
0
Vanessa Mdee Afunguka Kuhusu Kurudiana na Jux
Baada ya taarifa kuwa nyingi zikidai Vanessa Mdee na Jux kurudiana, hatimaye Vanessa amejibu ukweli wa suala hilo.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Bounce’ amekiambia kipindi cha The Playlist, Times Fm kuwa hawajarudiana bali kilichopo sasa ni urafiki tu.

“Kitu ambacho nyie hamjui Jux ni mshikaji wangu ni mtu ambaye tunapatana na kufanya kazi pamoja hata vitu vingi ambavyo ni nje ya sekta ya muziki Jux anasapoti, hatuwezi kuanza kugombana na sasa hivi, tunakuwa tunaharibu biashara” amesema.

Vanessa na Jux walikuwa wapenzi na kipindi cha mahusiano yao waliweza kutoa wimbo wa pamoja uitwao Juu pamoja na kushirikishwa katika ngoma ya Nikki wa Pili ‘Safari’.

AT Atwaa Tuzo Mbili Marekani

$
0
0
Msanii wa muziki wa mduara Bongo, AT amefanikiwa kushinda tuzo mbili za B&K Music & Video Music Awards za nchini Marekani ambazo zinahusisha muziki na filamu.

Katika tuzo hizo ambazo zilifanyikakatika mji wa Washington DC, AT ameshinda tuzo hizo kupitia wimbo wake ‘Sili Feel’ ambapo alikuwa akiwania katika vipengele viwili huku kimoja kikiwa ni International Artist ambapo alikwa akiwania na wasanii wengine watatu.

Kipengele kingine ambacho alikuwa anawania msanii huyo ni Best Music Video ambapo alikuwa anawania tuzo hiyo na wasanii wengine 9.

Akiongea na Bongo5, msanii huyo amesema kwa sasa bado yupo nchini Marekani anamalizia kazi zake nyingine za muziki akiwa na uongozi wake mpya uitwao Dashiam Management ambao ndio unasimamia kazi zake kwa sasa.

Dk Cheni Awapa Makavu Wanaomsakama Lulu Kuhusu Dhamana

$
0
0
Dk Cheni Awapa Makavu Wanaomsakama Lulu Kuhusu Dhamana
MSANII mkongwe katika tasnia ya maigizo Bongo na mshereheshaji (MC), Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ ambaye ni mlezi wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa maoni yake kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuibuka maneno mengi kwenye mitandao hiyo ambapo watu wengine wanasema Lulu amepewa adhabu ndogo na wengine wakipendekeza angefungwa kwa miaka mitano na kuendelea.

Dk Cheni amewalaumu wasiomtakia mema Lulu akisema mambo yote mabaya yanaweza kumtokea yoyote, kwa hiyo kufurahia jambo baya limpatalo mtu si jambo jema.  Pia ametoa asante kwa wote wanaomwombea mema Lulu na waendeleee kufanya hivyo.

Ujumbe aliotuma msanii huyo ni huu hapa chini:

Linapokukuta jambo wapo wataokuonea huruma na wapo watakaokuwa na furaha ila niwakumbushe jambo hakuna ajuwaye kesho yake kubwa kila mapito mwambie Mungu Asante.

Watanzania walio wengi wanakuombea yaliyo mema Tunakuahidi tupo nawe kukushika mkono kwa kila hatua Maombi yao Mungu atayasikia hata kama hukumu imepita Tupo na wewe na Mungu yupo na wewe.



Kikosi cha Taifa Stars Charejea Nchini

$
0
0
Kikosi cha Taifa Stars Charejea Nchini
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kimewasili nchini leo asubuhi kikitokea nchini Benin ambako kilienda kucheza mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA.

Taifa Stars ilicheza dhidi ya Benin siku ya jumapili Novemba 12 ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya ba 1-1. Katika mchezo huo bao pekee la kusawazisha la Taifa Stars lilifungwa na Elias Maguli dakika 51 baada ya kupokea pasi ya Shiza Kichuya.

Kikosi hicho kamili kikiongozwa na benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Salum Mayanga kimewasili asubuhi ya leo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere na kupokelewa na viongozi wa shirikisho la soka nchini TFF.

Kurejea kwa Taifa Stars kunatoa mwanya kuanza kwa maandalizi ya timu za Kilimanjaro stars inayowakilisha Tanzania bara pamoja na Zanzibar Heroes ambayo inaiwakilisha Zanzibar katika michuano ya kombe la CECAFA Challenge inayoanza baadae mwezi ujao.

Yanga Yasajili Straika Mpya wa Maana

$
0
0
Yanga Yasaka Saini Ya Straika Wa Kagera
ZIKIWA zimebaki siku moja kabla ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili hapa nchini, uongozi wa Yanga unajipanga vilivyo kuhakikisha unakiimarisha kikosi chake ili kiweze kufanya vizuri katika mechi zake zijazo za Ligi Kuu Bara lakini pia katika michuano ya kimataifa.

Uongozi unahitaji kusajili wachezaji wanne katika dirisha hili dogo la usajili kwa ajili ya kuziba upungufu uliojitokeza katika kikosi hicho tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara msimu huu katika nafasi ya ulinzi, kiungo pamoja na ushambuliaji. Na tayari mazungumzo na straika mmoja wa Kagera Sugar yanaendelea.

Hata hivyo, habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga ambazo Championi Jumatatu limezipata zimedai kuwa mpaka sasa uongozi huo umeishaanza mazungumzo
na baadhi ya wachezaji ambao inawahitaji akiwemo Mtogo Vincent Bossou ambaye ilimuacha baada ya kumalizika kwa msimu uliopita lakini pia kiungo wa Mtibwa Sugar, Mohamed Issa ‘Banka’.

Ukiachana na wachezaji hao ambao taarifa zao zimekuwa zikisemwa sana hivi karibuni pia uongozi huo unadaiwa kuwa katika mazungumzo na Straika wa Kagera Sugar, Jafar Kibaya ambaye ni kati ya washambuliaji mahiri hapa nchini.

Mshambuliaji huyo ndiye aliyeivuruga ngome ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu alipoifungia timu yake bao moja wakati Yanga iliposhinda 2-1 na kuwazidi ujanja mabeki wawili matata wa timu hiyo, Kelvin Yondani na Andrew Vicent Dante ambao imekuwa adimu sana wao kufungwa msimu huu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye aliomba kutotajwa jina lake, alisema uongozi huo unajipanga kuhakikisha unamsajili Kibaya ili kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji ambayo tangu kuanza kwa ligi kuu imekuwa ikiwategemea Ibrahim Ajibu pamoja na Mzambia, Obrey Chirwa.

“Kwa hiyo kutokana na hali hiyo tumeona ni bora tupambane kuhakikisha tunamsajili Kibaya kwa ajili ya kuja kusaidiana na wachezaji hao kwani Donald Ngoma na Amissi Tambwe kwa sasa siyo wachezaji wa kuwategemea sana.

“Muda mwingi wamekuwa nje ya uwanja, jambo ambalo linatufanya tuwe na wakati mgumu pindi wanapoumia, kwa hiyo Kibaya anatufaa na tayari kocha ametuambia tuhakikishe tunamsajili kwani alimuona tulipocheza na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba na alitusumbua sana,” alisema kiongozi huyo.

Katika mchezo huo dhidi ya Yanga, Kibaya ndiye aliyefunga bao pekee la Kagera ambapo Yanga ilishinda 1-2.
Alipoulizwa suala hilo, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alisema: “Muda wa usajili bado haujafika kwa hiyo kwa sasa siwezi kuzungumzia hilo, tusubiri kwanza mpaka utakapofika muda huo.”

Hata hivyo, Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein alipoulizwa kama wapo tayari kumuachia mchezaji huyo ajiunge na Yanga alisema: “Waje tuzungumze kama watakuwa tayari kutupatia fedha ambayo tutawaambia haina shida kwani Kibaya bado ana mkataba wa miaka miwili na sisi.

“Tumemsajili msimu huu akitokea Mtibwa Sugar kwa hiyo wakikubali kutupatia fedha tutakayowaambia basi tutawapatia.”

Kibatala : Lulu Anaweza Kupata Dhamana Akisubili Rufaa Kusikilizwa

$
0
0
Kibatala Atoa Ufafanuzi Kuhusu Dhamana Ya Lulu
WAKILI wa Elizabeth Michael ‘Lulu’, Peter Kibatala, kufuatia hukumu ya miaka miwili dhidi ya Lulu jana, ametoa ufafanuzi kupitia akaunti yake ya Instagrame kuhusu kitakachofuata alipoulizwa maswali na watu wengi ambapo alitumia fursa hiyo kuwafafanulia sheria inavyosema kuhusu nini kinafuata.

Majibu yake kwa maswali hayo ni yafuatayo:

Amesema kuwa hakuna hukumu tofauti inayoweza kutolewa kabla mhukukiwa hajatumikia theluthi ya kufungo chake ambacho kwa Lulu itakuwa ni kuanzia miezi  mitano.

Ndani ya hiyo miezi mitano dhamana inaweza kuombwa wakati wakisubiria rufaaa ianze kusikilizwa.  Kwa maana hiyo anaweza kutoka kwa dhamana muda wowote mahakama ikmpatia dhamana.

Huwezi kuacha kijana wa miaka 22 mwenye maisha marefu mbele yake ahukumiwe kwa uhalifu kwa sababu ya suala la muda, kwani itaharibu maisha yake ya mbele. Kwa hiyo rufaa imelenga katika kuondoa tatizo hilo.

Kukata rufaaa na kuomba dhamana  na kufanya kazi za jamii vinaweza kufanyika kwa wakati mmoja wakati suala hili likisubiriwa kusikilizwa na mahakama ya rufaa.

Ujumbe wa Kitabala katika Instagram ni ufuatao:



Idriss Atuma Salamu za Pole kwa Mama Lulu "Mama Ndio Tunahitaji Kukuangalia Zaidi"

$
0
0
Idriss Atuma Salamu za Pole kwa Mama Lulu "Mama Ndio Tunahitaji Kukuangalia Zaidi"
MCHEKESHAJI na mshindi wa Big Brother Africa, Idris Sultan, ametoa pole kwa mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Kalugira, kwa kipindi kigumu alichokianza jana baada ya bintiye kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kutokana na kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Sultan amesema jamii impe faraja na kumtia moyo wakati akiwa katika huzuni ya kuwa mbali na binti yake.  Pia Sultan amemuelezea Lulu kuwa alikuwa ni rafiki yake wa karibu na ni mwanamke shupavu ambaye huzuni yake ikiwa jela itachukua muda mfupi kabla ya kupata marafiki na kujipa moyo wa kuhimili maisha hayo mapya ya miaka miwili.
Hayo ni maneno aliyoyatuma kwenye akaunti yake ya Instagram kama yafuatavyo:
My last piece on this, Mama Lulu tunakuombea kwa Allah upate nguvu ya kukubaliana na hii hali ambayo ni chungu kwetu sote. Tunalazimika kukubali kwasababu Mungu tu ndiye anajua kubaki na jambo kama hili moyoni kwa mda mrefu hivi linaondoaje amani. Binafsi nampenda sana Lulu na anajua, kwa mda wa miaka michache niliyojuana na Liz najua wewe mama ndio tunahitaji kukuangalia zaidi maana Lulu najua atalia wiki ya kwanza na ya pili, ya tatu atapata kazi jikoni, ya nne anajisomea, ya tano kashapata marafiki kote because your daughter is the strongest woman I have ever met maishani mwangu yani ningekua mwanamke ningekua yeye. Baby is good to go na nitajaribu kuwa positive na kusema kua ntammiss sana ila mara mbili tatu sitoacha kumtembelea na tunasubiri siku anatoka na ku-take over her throne. Hakuna aliyependa haya yatokee ila ndio yametokea we only have God and each other now. Be blessed


Wabunge Wanaotaka Pensheni Watakiwa Kuanzia Bungeni Kabla ya Kufika Serikalini

$
0
0
Wabunge Wanaotaka Pensheni Watakiwa Kuanzia Bungeni Kabla ya Kufika Serikalini
Serikali imewataka wabunge wanaotaka utaratibu wa kulipwa pensheni mara baada ya kumaliza kipindi cha ubunge urejeshwe, walipeleka jambo hilo kwanza kwenye  Tume ya Utumishi ya Bunge kabla ya kulifikisha serikalini.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amesema leo Jumanne bungeni kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Vunjo (NCCR_Mageuzi), James Mbatia.

Mbatia amesema sheria ya mwaka 1981 ilikuwa inatambua pensheni kwa wabunge wanaomaliza muda wao na kuihoji Serikali inatamka nini kuhusu kulifufua suala hilo.

Akijibu swali hilo, Mavunde amesema kwa sababu swali la mbunge huyo ni kufufua sheria ya pensheni ni vyema lianzie kwao ( Tume ya Utumishi ya Bunge) ndio lifike serikalini.

Katika swali la msingi, Mbatia ametaka kufahamu Serikali haioni busara kuifanyia marekebisho Sheria ya Maslahi na Mafao ya Majaji namba 3 ya mwaka 2007 au vinginevyo ili majaji waweze kupatiwa huduma muhimu za matibabu wakati wanapostaafu.

Akijibu Mavunde amesema masharti ya kazi na stahili za majaji ya mwaka 2013 kwa maana majaji wa Mahakama Kuu yamefafanua kuwa majaji hao wamejumuishwa katika utaratibu wa matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHF)wawapo kazini.

Amesema gharama hizo hulipwa na Serikali na hata wanapostaafu wanaendelea kupata huduma hizo kupitia mfuko huo.

"Kwa wale waliostaafu kabla ya masharti hayo kuanza kutumika hawanufaiki na mfuko huo," amesema.

Kuhusu kuangalia kulifanya suala hilo la  kiutawala, Mavunde amesema kwa sababu ni suala la kisheria na sera wanalichukua na kulifanyia kazi.

JE Wajua Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Madogo ya Kiume?

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WA NA MAUMBILE MADOGO?
Tatizo hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia ,hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wenzao,kwakawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6_8 vinginevyo mtu huyu ana matatizo.



Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo baadhi ni,upungufu wa vichocheo (hornes) za gestrojen ambapo mwanaume anapobalehe vichocheo hivi (hormones)huchochea ujuaji wa uume.chango ambalo hushambulia nerve ambapo huharibu kabisa ukuaji wa uume, Punyeto ambayo huasili misuli ya uume,pia ngiri ambayo huleta maumivu ya tumbo kuunguluma na kujaa gesi,korodani moja kuvimba,kutopata choo vizuri,sababu hizi na nyinginezo hufanya uume kulegea na kisinyaa nakuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu zakiume (hamu ya tendo landoa hupungua au kuisha kabisa).NSUMBU,Nidawa inayozalisha hormones za gestrogene na kufanya uume kukua na kuongezeka mara dufu.NZAGI,Ni dawa ya kurudisha nguvu za kiume ,hutia hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha nakuponya kabisa tatizo hilo. Pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk 15 nakuendelea kwa tendo la kwanza.kumbuka dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji.Natunatibu kisukari,bp,ngiri,miguu kuwaka moto,namengine mengi.

WASILIANA OSTADHI JUMA KWA SIMU NO,0784002216 AU 0769597778

Lukuvi Atoa Agizo kwa Jeshi la Polisi Kuwakamata Maafisa Ardhi na Wanasheria

$
0
0
Lukuvi Atoa Agizo kwa Jeshi la Polisi Kuwakamata Maafisa Ardhi na Wanasheria
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuwakamata baadhi ya maafisa ardhi na baadhi ya wanasheria ambao wamehusika katika uuzaji wa shamba kiasi cha Hekta mbili na nusu mali

ya Madina Omary Mkazi wa Bagamoyo mkoani Pwani.
Mhe Lukuvi ametoa kauli hiyo akiwa ofisi kwake mkoani Dodoma mbele ya waandishi wa habari wakati akimrejeshea mama huyo ardhi yake huku akiwataka maafisa ardhi na wanasheria kufuata taratibu zote za uuuzaji wa ardhi wakati wa kuuza.
Mhe Lukuvi amesema uuzaji wa shamba hilo ulikiuka taratibu za uuzaji wa eneo hilo ikiwemo kuwepo kwa sahihi za kufoji za wahusika wa shmba hilo huku mawikili waliofanya hivyo wakijua kuwa hilo ni kosa kisheria.
Kwa upande wake mama huyo Madina Omary amemshukuru Mhe Waziri Lukuvu kwa kumsaidia kupata ardhi hiyo ambayo alikua amedhulumiwa kwa zaidi ya miaka kumi kutoka kwa matepeli ambao alikua akishindana nao mahakamani.

Mrisho Mpoto Amvaa Afande Sele Baada ya Kutoa Lawama kwa Marehemu Kanumba

$
0
0
Mrisho Mpoto Amvaa Afande Sele Baada ya Kutoa Lawama kwa Marehemu Kanumba
Hapo jana msanii wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael (Lulu) kuhukumiwa miaka 2 jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia msanii mwenzake wa filamu, Steven Kanumba. Msanii Afande Sele aliibuka na kuandika ujumbe wa kumshtumu Kanumba kwa kitendo cha kutembea na Lulu wakati akiwa bado mdogo.

Afande sele alienda mbali zaidi kwa kueleeza kuwa aliumia zaidi baada ya matatizo aliyoyapata Lulu kupitia Kanumba, hivyo hata hakushiriki kivyovyote katika msiba wa msanii huyo ingawa alikuwepo Dar kwani hakutaka kuvaa joho la unafki.

Sasa leo hii Msanii Mrisho mpoto ameiibuka na kupinga vikali kile alichoandika Afande Sele, kupitia ukurasa wake wa Instagram Afande Sele ameandika yafuatayo;

Kaka yangu Afande Sele.. Mfalme wa maandishi…!! @afandeselekingWewe ni Kaka yangu na ni mwandishi ambae sijawahi kuacha kuheshimu maandishi yako …Leo nna mambo kadhaa kidogo kwako Kaka yangu…. Nimesoma maandishi kwenye ukurasa wako zaidi ya mara 30 Huku nikiyarudia rudia mara Kadhaa…ningependa kujua vitu Vichache kabla ya hoja yangu ya msingi kuiweka mezani…ile Barua ulimwandikia Marehemu Kanumba ulitaka imfikie? Au ulitaka wanaokwenda nyuma yake wamfikishie? ulitaka waliopo wajifunze kupitia walaka wako? Mbona nimepata kusikia Marehemu huwa halaumiwi kwakua hana uwezo wa kijitetea? Umesema ulikuwepo Sinza wakati wa msiba na hukutaka kusogea wala kuzika kwakua unasema wewe siyo mnafiki kama watanzania waliokwenda kuzika… ikiwa watu wote wangekataa ile Maiti ingekuaje? Nini Hasa lengo la Movies za Kibonge kuziita Maigizo yanayowekwa Kwenye Kanda? una ugomvi na Bongo Movies au uliandika ukiwa kwenye Jazbda kidogo….!! Mimi ndugu Mrisho Mpoto

Kigwangala na Waliopania Kuniumiza Wanahitaji Miwani ya Lenzi ya Ziada- Nyalandu

$
0
0
Kigwangala na Waliopania Kuniumiza Wanahitaji Miwani ya Lenzi ya Ziada- Nyalandu
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kuwa Waziri wa sasa wa wizara hiyo, Dkt Hamisi Kigwangalla na wale wote waliopania kumuumiza wanahitaji miwani ya lenzi ya ziada ili macho yao yaweze kuona mambo aliyoyafanya, huku akieleza kuwa baada ya kukihama chama cha Mapinduzi(CCM) amegeuzwa kuwa adui.

Mh. Nyalandu kupitia ukurasa wake wa Instagram leo ameweweka wazi baadhi ya kazi alizowahi kuzifanya ndani ya miezi 18 alipokuwa Waziri wizara hiyo.

BAADA ya kutenda mema, wakasema ASULUBIWE! Na LazaroNyalandu
NIMEINGIA Wizara ya Maliasili na Utalii kwa uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete, Mnamo Februari 10, 2014, na nimefanya kazi ya Uwaziri kwa takribani miezi 18.

Itakubukwa kwamba kipindi hiki kilikuwa ni kilele cha ujangili wa Tembo barani Afrika, huku Tanzania ikitajwa kuwa nchi kinara kwa masuala ya ujangili wa wanyamapori, hususani Tembo. Wakati huo, akiba ya meno ya Tembo katika Ghala la Taifa yalifikia takribani tani 130,000, ikiwa ni idadi kubwa ya meno ya Tembo yaliyohifadhiwa popote duniani.

Kazi yangu ya kwanza ilikuwa ni kuongozana na Rais Jakaya Kikwete kwenda London, Uingereza kuhudhuria Mkutano wa Tembo duniani ulioandaliwa na Mwana Mfalme Charles wa Uingereza, ambako pamoja na mambo mengine, Rais Jakaya Kikwete aliitaarifu dunia juu ya uamuzi wa Tanzania wa kupiga marufuku biashara ya meno ya Tembo, na kuungana na Mataifa lukuki yaliyokubali kufanya hivyo.

Aidha, kwa kushirikiana na Rais Jakaya Kikwete, tulikubali Tanzania kujiunga na Mataifa 6 barani Afrika (African Elephants Range States), ikiwepo Ethiopia, Kenya, Gabon, Chad, Botswana na mataifa mengine kwa lengo la kuongoza mapambano hayo. Mara baada ya Mkutano wa London, Tanzania na baadhi ya Mataifa ya Afrika yalikuwa washiriki wa Pound milioni 10 zilizotolewa na UINGEREZA kupambana na uhalifu huo Afrika. Niliporejea Tanzania, nilianzisha Mpango wa Kuhifadhi Vema Akiba ya Meno ya Tembo nchini kwa kuyafanyia utambuzi wa DNA (asili, umri wa Tembo, na alikotokea) na kuhakikisha hayapotei, kazi iliyofanywa kwa ushirikiano kati ya watalaamu wa Wizara na Shirika la STOP IVORY UK.

Aidha, kama Waziri, kwa idhini ya Rais, nilihojiwa na Stephen Sucker wa kipindi maarufu Cha BBC HardTalk, nikiwa Mtanzania wa Pili wakati huo kuhojiwa HardTalk, wa kwanza akiwa Rais Mstaafu Benjamin William MKAPA, na nilipata fursa ya kuielezea dunia azma ya Tanzania kuongoza mapambano dhidi ya Ujangili barani Afrika.

Kwa kuzingatia changamoto waliyokuwa nayo wahifadhi kote nchini, niliiongoza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kufanya mchakato wa kuongeza idadi ya Maaskari wa Wanyamapori kutoka 1000 hadi 4000, na kuanzisha mazoezi mahsusi kwa Maaskari wa Wanyamapori katika Pori la Akiba la Selous kwa kushiriana wa kikosi Maalum Cha US Special Forces kilichopo mjini Stuttgart, Ujerumani. Maaskari wa Wanyamapori walifundishwa umahiri na weledi katika kufanya kazi yao, na walipatiwa, kwa kushirikiana na Serikali ya Marekani, vifaa vya kuwawezesha kumudu hali yenye changamoto wanapokuwa porini. Aidha, Serikali ya Ujerumani ilikubali kutoa Uniforms na boots kwa ajili ya Askari wetu, ikiwa ni hatua za awali za kuwajengea morali na utayari wa kuitumikia nchi wanapokuwa katika mazingira tete porini.

Wakati huo huo, Taasisi ya Howard Buffet Foundation ilikubali kutoa helikopta kwa ajili ya Doria, Shirika la FZS walitoa ndege yenye kamera maalumu (infra red), Friedkin Conservation walikubali kutoa helikopta, Kilimanjaro Safari Club walitoa ndege, na Mkuju River Project walitoa ndege. Ndege ya FZS ilikuwa na kamera maalumu (infra red) zinazoweza kuwatambua majangili porini nyakati za usiku. Taasisi ya HBF, ilitoa fedha, magari, pamoja na kukikarabati Chuo Cha Maaskari wa Wanyamapori Pansiasi Mwanza na kununua vitendea kazi vingine kwa ajili ya maaskari wanafunzi.

Tukiwa tumeongeza idadi ya wapiganaji, nilishirikiana na Taasisi ya Paul Allen (mwanzishi mwenza wa Microsoft) kuidadi (kuhesabu) upya Tembo nchi nzima, ambako baada ya mwaka moja, idadi ya Tembo ikaanza kuongezeka sana kutokana na jitihada hizi shirikishi. Aidha, kupitia Paul Allen, tulianzisha mfumo mpya wa mawasiliano Selous uitwao Digital VHS, wenye lengo la kuwawezesha Maaskari kuwa na mawasiliano yasiyoingiliwa kimtandao na majangili na watu wengine wenye nia mbaya.

Halikadhalika, kwa kuzingatia hali tete ya kupotea kwa Tembo katika hifadhi ya Ruaha wakati huo, nilishirikiana na Serikali ya Marekani kupitia Taasisi ya WCS (World Conservation Society) yenye Makao yake Makuu mjini New York, ambayo ilianzisha mradi wa muda mrefu wa dola milioni 50 kuokoa Hifadhi ya Ruaha pamoja na maeneo mengine.

Mwaka huo huo, kwa kushirikiana na Shirika la International Conservation Caucus (ICCF) la Mjini Washington, DC, pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa UNDP-Tanzania na Benki ya Dunia, (ofisi ya Tanzania) niliitisha Mkutano wa Nchi 11 za Africa uliofanyika mjiini Arusha, na kukubaliana juu ya Azimio la Arusha “Arusha Declaration” kuhusu kushirikiana kuhifadhi maeneo yanayoingilina (shares ecosystems) katika nchi zetu. Washiriki wa Maendeleo ikiwepo Ujerumani, UNDP, na Marekani walishiriki nami katika kutia sahihi makubaliano kati ya Tanzania na Msumbiji (Selous-Niassa Corridor Agreement) tuliyoyafikia mjini Maputo, Msumbiji kuhusu kulinda ushoroba wa Selous-Niassa kati ya Msumbiji na Tanzania unaokadiriwa kuwa na ukubwa wa kilometa za mraba 40,000, ukiwa ni ushoroba mkubwa kuliko zote duniani.

Nilichukua hatua ya kuzishauri na kukubaliana na nchi zenye misitu ya asili ‘miombo woodland’ ambayo ndio misitu ya asili kwa Hifadhi ya Tembo barani Afrika zikubali kutia saini “Miombo Woodland Agreement”, ikiwa ni sehemu ya jitihada za mataifa haya kuhifadhi Tembo, na uoto wa asili wa Miombo, ambao unasaidia pia kuzuia mabadiliko ya tabia nchi duniani. Nchi zilizokubali ni pamoja na Zambia, Malawi, na Msumbiji, na tulianza hatua za awali za kufanya jitihadi za nchi hizi zijulikane na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa Wakati wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi, Paris, Ufaransa. Tanzania na Zambia zilikuwa nchi za kwanza kuweka sahihi Makubaliano hayo.

Nilianza mchakato na Benki ya Dunia wa kutoa dola 150, 000,000 kwa ajili ya kusaidia kuinua Utalii kusini mwa Tanzania (mikoa ya kusini mwa reli ya kati), pia tulipata Euro milioni 50 kutoka Ujerumani kwa ajili ya kusaidia Uhifadhi kupitia uanzishwaji wa TAWA, na Serikali ya China ilitoa magari mapya na pikipiki maalumu za matairi matatu kwa gharama ya zaidi ya dola milioni Moja na nusu.

Aidha, kwa ushirikiano Mkubwa na wenzangu Wizarani, Nilifanikisha kuanzisha Taasisi Mpya kabisa Tanzania ya TAWA (Tanzania Wildlife Authority), inayochukua kazi za kiuhifadhi za idara ya Wanyamapori. Nilishirikiana na wenzangu Wizarani kuandaa mfumo wa uendeshaji wa taasisi hii ili iweze kuwa kinara Cha Uhifadhi nchini kwa kumiliki na kulinda mapori yote ya Akina (Game Reserves), Mapori Tengefu, na maeneo yote ya Wanyamapori yaliyo NJE ya uangalizi wa Tanapa au Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Serikali ya Ujerumani, kama nilivyosema hapo awali, ilitoa Euro milioni 50, na Serikali ya Tanzania ilikubali Shirika hili la Umma liwe na Makao yake Makuu Mjini Morogoro.

Baada ya kuleta helikopta Wizarani, nilianzisha mpango maalumu wa kuwafundisha vijana wa Kitanzania mafunzo ya urubani wa Helikopta na ndege nchini Afrika Kusini na Marekani, na tayari kuna vijana waliofuzu vema.

Pamoja na kwamba siwezi kuyaeleza yote kwa sasa, ikumbukwe kuwa nilianzisha Tangazo la “Tanzania, the Soul of Africa”, nilianzisha Swahili Expo kwa ushirikiano na Indaba SA, na tulifanikiwa kwa ushirikiano na wadau wa Utalii nchini, kuongeza idadi ya watalii kuvuka milioni na pato la Utalii kufikia dola bilioni 1.3, huku Benki Kuu Tanzania ikiarifu kuwa Sekta ya Utalii wakati huo ilikuwa inaongoza kwa kuingiza nchini Fedha za kigeni, forex.

HIZI ni baadhi ya KAZI nilizozifanya ndani ya miezi 18 nilipokuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

Waziri Kigwangalla pamoja na wale waliopania kuniumiza wanahitaji miwani yenye lensi za ziada yamkini kwamba, macho yao yaweze kuona, na ndimi zao ziweze kukiri mema haya ambayo MUNGU alitujalia kuyafanya kwa pamoja nikiwa Waziri wa Maliasili. Iliandikwa zamani, “Kama hamniamini mimi, basi aminini kazi ninazozifanya”. Miaka zaidi ya miwili baada ya mimi kumaliza kazi yangu ya uwaziri nikiwa salama, na baada ya kuhama CCM, wamenigeuza adui. Katika Wizara ya Maliasili, Mimi Nyalandu sikuwahi kufukuzwa, kuachishwa, wala kutumbuliwa muda WOTE nikiwa Wizarani, ikiwa ni historia kubwa ikizingatiwa kuwa Mawaziri wengi hawakumaliza Salama. Mwenye masikio na ayasikie maneno haya. MUNGU awakemee wote wanaokaa vikao vya SIRI kupanga hila juu yangu, MUNGU akalikomboe Taifa letu dhidi ya roho ya HOFU inayofanya wengi kunyamaza huku wakiona Taifa linaangamia, ikawe HERI kwa wote waitamanio HAKI, na ni maombi yangu kwamba MUNGU afufue UJASIRI, na afufue KAZI yake katikati ya MIAKA. Taifa Tanzania na watu wake watasimama TENA. Tushikane MIKONO. Tuamini. Tuungane.

SIGNED
Lazaro S. Nyalandu.
Waziri Mstaafu, Maliasili na Utalii, Tanzania

Mahakama Yasikiza Kesi Inayopinga Uchaguzi wa Uhuru Kenyatta

$
0
0
Mahakama Yasikiza Kesi Inayopinga Uchaguzi wa Uhuru Kenyatta
Kwa mara ya pili katika chini ya kipindi cha miezi mitatu, macho yote sasa yanaangazia mahakama ya upeo wa juu zaidi Kenya, itakayoamua iwapo ushindi wa rais Kenyatta, ni halali au la.
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Kenya na tume ya Uchaguzi IEBC, baada ya uchaguzi wa marudio ya Oktoba 26.
Kesi tatu zimewasilishwa mbele ya majaji 6 wanaoongozwa na jaji mkuu David Maraga, mbili zikitaka ushindi wa rais Kenyatta ubatilishwe, huku moja ikitaka viongozi wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga wachukuliwe hatua kwa madai ya kuchochea wafuasi wao kususia uchaguzi, na kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.

Kesi za kubatilisha ushindi wa rais Kenyatta zimewasilishwa kwa misingi kwamba tume ya uchaguzi ilikosa kuagiza uteuzi mpya wa chama ufanyike baada ya mahakama ya upeo wa juu zaidi kufutilia mbali ushindi wa rais Kenyatta mwezi Agosti.
Mahakama ina chini ya siku saba kusikiliza na kuamua kesi hizo tatu.
Kiongozi wa upinzani nchini humo alisusia uchaguzi huo
Image caption
Kiongozi wa upinzani nchini humo alisusia uchaguzi huo

Ruge Afunguka Kuhusu Ndoa Ya Zamaradi " Sitoacha Kumuheshimu Mama wa Watoto Wangu"

$
0
0
Ruge Afunguka Kuhusu Ndoa Ya Zamaradi " Sitoacha Kumuheshimu Mama wa Watoto Wangu"
Hatimaye Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amezungumzia suala la ndoa ya mama watoto wake, Zamaradi Mketema.

Ruge amezungumzia suala hilo ikiwa ni wiki kadhaa tangu isambae sauti iliyoaminika kuwa ni ya kwake, akisikika mtu anazungumza na Zamaradi kwenye simu huku akilia kwa sauti ya mateso akilalama kuachwa.

Amesema kuwa kama mwanaume muungwana, huwa hazungumzii masuala ya ndani ya mahusiano yake ya kimapenzi, akitumia msemo wa kiingereza kuwa ‘Gentlemen don’t kiss and tell’, kwa tafrisi isiyo rasmi ‘hatubusi na kusimilia’. Msemo huu una maana ya kuwa wanandani hawasimulii kuhusu yao ya ndani.

Ruge amesema kuwa alikuwa anafahamu kila kilichokuwa kinaendelea kuhusu ndoa ya Zamaradi na kwamba alikuwa amempa baraka zote tofauti na ilivyokuwa ikizungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ameshtukizwa na kuumizwa.

“Kila kilichofanyika nilikuwa na taarifa na kilikuwa na baraka zangu. Ni sehemu ya maisha tunapitia. Kubwa kuliko yote, nina watoto wawili ambao nimezaa na Zamaradi. Nina mheshimu mno na hadi sasa naendelea kumheshimu mno,” Ruge amefunguka kupitia kipindi cha Clouds 360.

“Unajua kama kuna kitu nitakufundisha [mtangazaji] kama mdogo wangu , ‘When you are a gentleman, you don’t kiss and tell’ (Ukiwa mwanaume muungwana, haubusi na kusimulia). Vitu vingine vinabaki kuwa vyako binafsi vya ndani,” aliongeza.

Ruge ameeleza kuwa hata wikendi iliyopita alikuwa na watoto wake aliozaa na Zamaradi na kwamba anawapenda sana na hataacha kumheshimu mama yao.

Amesema amelazimika kulizungumzia hilo ili kuweka kumbukumbu sawa na sio vinginevyo.

Zamaradi alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV. Alikifanya kipindi hicho kuwa maarufu huku akishiriki kuandaa filamu zilizoshika mitaa ikiwemo filamu ya ‘Kigodolo’.

Takukuru Yaanza Kulifanyia Kazi Suala la Nyalandu

$
0
0
Takukuru Yaanza Kulifanyia Kazi Suala la Nyalandu
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), imesema kuwa suala la aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu imelisikia na imeanza kulifanyia kazi.

Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali, John Mbungo amesema kuwa wakimkuta na hatia watamfikisha kunakostahili.

Kauli hiyo ya Mbugo ameitoa leo Jumanne ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala kumlipua Nyalandu akimtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 207/2018 jana Jumatatu Dk Kigwangalla aliiagiza Takukuru na polisi kumchunguza Nyalandu.

Dk Kigwangala alisema Nyalandu aliikosesha Serikali mapato ya Sh32 bilioni kwa miaka miwili aliyohudumu katika wizara hiyo kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii.

Lulu Amefungwa Miaka Miwili Lakini Atarudi, Mwanangu Hatorudi Wanaonibeza Waniache Hakuna Mwenye Uchungu Zaidi Yangu- Mama Kanumba

$
0
0
Lulu Amefungwa Miaka Miwili Lakini Atarudi, Mwanangu Hatorudi Wanaonibeza Waniache Hakuna Mwenye Uchungu Zaidi Yangu- Mama Kanumba
Siku moja baada ya Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhukumiwa kifungo cha kutumikia jela miaka miwili kwa kosa la kuuua bila kukusudia, mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mutegoa amesema wanaombeza kwa kuishukuru Mahakama wamuache kwa hakuna mwenye uchungu zaidi yake.

Jana baada ya Mahakama Kuu kumtia hatiani mwigizaji huyo na kumpa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela, Mama Kanumba aliishukuru Mahakama akisema imetenda haki jambo ambalo lilizusha gumzo wengi wakisema hakupaswa kufurahia adhabu hiyo.

Akihojiwa na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam jana Jumatatu baada ya hukumu kutolewa alisema anashukuru kwa kuwa haki imetendeka na kwamba atakwenda kumzika rasmi mtoto wake.

Hata hivyo, Mwananchi leo Jumanne amesema asibezwe kwa kauli hiyo kwa kuwa hakuna anayeujua uchungu anaoupata kila siku.

“Mimi sijui kama ninafurahia kama wanavyodai, waulize kwamba, yeye (Lulu) alipokufa mwanangu Kanumba alifurahia? Mimi ni mkristo, sipendi kuona baya likimfika binadamu mwenzangu, lakini Lulu ameenda miaka miwili jela na atarudi, je, mwanangu atarudi lini? nitamwona wapi tena? Amehoji.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images