Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Lissu Yupo Tayari Kutaja Waliomshambulia...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Novemba 24

$
0
0


Lissu Yupo Tayari Kutaja Waliomshambulia...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Novemba 24

Kafulila: "Ndoa Yangu Haihusiani na Siasa ilifungwa Kanisani na Sio kwa Mwenyekiti wa Chama"

$
0
0
Daudi Kafulila ambaye hapo jana amekihama chama cha CHADEMA, amesema suala la mke wake kuridhia au kutoridhia kwa yeye kuhama chama wakati yeye ni Mbunge wa chama hiko, ni suala ambalo halihusiani na ndoa yao.

Kafulila ameyasema hayo leo na kueleza kwamba linapokuja suala la ndoa hapo ndio huwa lazima wafikie makubaliano, lakini ikija suala la kisiasa kila mtu ana uamuzi wake ambao hawaingiliani kwani ndoa yao ilifngwa kanisani na sio kwenye chama.

“Haya ni maamuzi ya kisisasa, sisi ndoa yetu ilifungwa kanisani haikufungwa kwa mwenyekiti wa chama au kwenye chama, kwa hiyo ndoa ni jambo jingine na harakati ni mjambo jingine, yeye ni mke wangu lakini haimaanishi tunakubaliana kwenye kila kitu, tunakubaliana kwenye mambo ya ndoa, kwenye siasa kila mtu anaweza akatazama jinsi anavyotazama yeye na sio shida”, amesema Kafulila.

Hivi sasa kumekuwa na mvutano kati ya wanandoa hao baada ya Kafulila kuhama CHADEMA, huku mke wake akisema hakuwa na taarifa zozote, na hata hizo sababu zake za kuhama hazina ukweli na kumtaka aweke wazi sababu rasmi za kufanya hivyo

Mke wa Kafulila Atoa ya Moyoni Uamuzi wa Mumewe Kuikimbia CHADEMA

$
0
0
Mke wa aliyewahi kuwa mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, Jesca Kishoa, amemtaja mumewe kuwa ni mtu aliyeingia kundi la wanasiasa wasio na msimamo.

Kishoya amesema wakati wote mumewe amekuwa na msimamo usioyumba lakini anashangazwa kaingia katika mtego mbovu.

"Bado naamini kuwa Chadema ni mahali sahihi kabisa ambapo siwezi kufikiri siku moja nitatoka,  hivyo siyumbi kwa hilo na wanaonipigia  simu watambue hilo," amesema  Kishoya

Amesema  taarifa za mumewe kujiondoa Chadema amezipata kupitia vyombo vya habari akiwa Dodoma kwenye kampeni za udiwani lakini alimpigia wakazungumza sana na bado hakumpa sababu zilizoshiba za kuondoka kwake.

Hata hivyo amepinga madai ya Kafulila kuwa anaondoka upinzani kwa sababu ya upinzani kushindwa kusimamia ajenda ya ufisadi badala yake akasema ana mambo yake.

"Wanasiasa ambao hawana misimamo ndiyo husingizia vitu hivyo, siamini kama maneno yale yalitoka rohoni mwake, CCM siyo mahali sahihi kwa kuzungumzia mambo ya ufisadi hata kidogo, "

Mbuge huyo amesema wakati wote katika maisha yao mumewe amekuwa ni muumini mzuri wa kuhubiri habari za ufisadi ikiwemo pale alipotoa maisha yake kuhusu sakata la Escrow.

Tundu Lissu kusafirishwa kwa matibabu nje ya Afrika......Familia yataka Lissu akahojiwe Nairobi

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anatarajiwa  kusafirishwa nje ya nchi kwa matibabu mwezi mmoja kuanzia sasa.

Familia yake imesema Lissu baada ya kupata matibabu nje ya nchi amepanga kufanya mambo matano akirejea salama .

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Novemba 23, kaka wa Tundu Lissu, Wakili Alute Mughwai alisema taratibu za kumsafirisha  nje ya nchi zimeanza.

Lissu, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu na mwanasheria mkuu wa chadema amelazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 alipokuwa akirejea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma Septemba7.

"Awamu ya tatu ya matibabu yake ni maalumu sana kwani itahusu pia mazoezi ambayo kama haitafanyika vyema ataweza kupata ulemavu wa kudumu,"alisema.

Hata hivyo, alisema  Lissu atapelekwa nje kwa ndege ya kawaida tofauti na hali yake ya awali alipotakiwa kusafirishwa  na ndege maalumu za wagonjwa.

"Itatolewa taarifa ni lini ataondoka kwa matibabu na atakwenda nchi gani, hasa baada ya kupata ushauri wa mwisho wa madaktari katika hospitali Nairobi," alisema.

Mughwai alisema amezungumza na Lissu akiwa Hospitali Nairobi na amemueleza kuwa  akirejea tu nchini, kuna mambo makubwa matano ambayo atafanya.

Alisema jambo la kwanza, ambalo atafanya ni kwenda katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kuwashukuru madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo kwa kuokoa maisha yake siku aliyopigwa risasi.

Wakili Mughwai alisema Lissu amemwambia baada ya hapo atakwenda kanisani na msikitini kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya ibada maalumu.

"Baada ya ibada, tutaangalia utaratibu kifamilia kama itawezekana  kwenda kufanya matambiko  kwenye makaburi ya wahenga wetu 76 waliofariki katika vita miaka 200 iliyopita," alisema.

Alisema  baada ya hapo, anatarajia kuendelea kufanya kazi zake za siasa na uwakili pale alipoishia kwa ari kubwa .

Wakili Mughwai alisema  jambo la tano atahakikisha  anasimama na kupambana kisheria na watu waliotaka kukatisha maisha yake baada ya kumpiga risasi.

"Amesema atahakikisha anasimamia jambo hili kwa uwezo wake wote ili kuhakikisha wanafikishwa katika vyombo vya sheria waliohusika na uovu huo," alisema.

Familia yataka Lissu akahojiwe Nairobi
Akizungumzia juu ya upelelezi wa shauri la Lissu, Mughwai alisema bado msimamo wao upo palepale wanaomba wapelelezi kutoka nje ya nchi washirikiane na wapelelezi wa ndani kuwakamata watuhumiwa.

Alisema ingawa familia ya Lissu iliandika barua tangu Septemba 16, kutaka wapelelezi wa kimataifa na kujibiwa na mwanasheria mkuu Septemba 20  kuwa jukumu la upelelezi ni la polisi.

 "Tunataka wapelelezi wa nje kushirikiana na wa ndani kwa sababu hatuna imani na upelelezi kutokana na kasi ndogo kwani hadi sasa wamekuwa wakieleza kukwama upelelezi kutokana na kutomuhoji dereva wa Lissu,"alisema.

Hata hivyo, alisema kwa sasa Lissu anaweza kuongea mwenyewe hivyo, jeshi la polisi linaweza kwenda Nairobi kumuhoji na atawapa maelezo yote ikiwepo watu ambao aliwatambua.

"Bila shaka Lissu atawaeleza watu hao, walimshambulia kwa sababu gani,"alisema.

Familia yaelezea gharama
Katika hatua nyingine, Mughwai alisema Oktoba 2, familia ya Lissu ilikutana na viongozi wa bunge kujadili matibabu yake ambayo ni haki yake kisheria.

Alisema baada ya mazungumzo hayo, Oktoba 8, familia iliandika barua rasmi kwa katibu wa bunge kwa kuzingatia sheria ya bunge namba 14 kifungu cha 24 kuhusu stahiki za mbunge.

Alisema barua hiyo, ilipelekwa bungeni kwa kutumia shirika la kubeba mizigo na vifurushi la DHL na kupokelewa Oktoba 19 na baadaye aliwasiliana na Spika Job Ndugai na kumweleza juu ya barua hiyo na aliahidiwa kuwa suala hilo litashughuliwa.

Hata hivyo, alisema familia haijapata mrejesho tangu wakati huo hadi Novomba 11, alipoamua kumpigia katibu mpya wa bunge baada ya kushauriwa na Spika Ndugai ambaye aliahidi kufuatilia.

"Hivyo hadi sasa bado Bunge halijaanza kugharamia matibabu ya Lissu kama sheria inavyosema na Lissu amekuwa akitibiwa kwa michango ya watu mbali mbali," alisema

Alisema michango hiyo ambayo inakusanywa katika akaunti maalumu ya Chadema  na pia kupitia chama cha mawakili(TLS) ndio hadi sasa inatumika.

"Tutaendelea kulitaka Bunge kugharamia matibabu kwani sio suala la hiari, ni haki ya mbunge lakini pia tunaomba wananchi waendelee kuchangia matibabu ya Lissu kupitia akaunti iliyotolewa na Chadema, chama cha TLS na kwa familia"alisema

Akanusha mgawanyiko juu ya matibabu
Katika hatua nyingine, Mughwai alisema, familia ya Lissu, Chadema na chama cha Mawakili wa Tanganyika(TLS), hawana mgawanyiko wowote juu ya matibabu ama hatua zinazoendelea za kumtibu Lissu.

Wakili Mughwai alisema wanasikitishwa na taarifa kuwa familia imegawanyika juu ya uamuzi wa kuliomba bunge kugharamia matibabu ya Lissu.

"Tupo kitu kimoja wote familia yetu tupo pamoja kwa yote na Lissu anajua hatua zote kwani hata makamishna wa bunge walipomtembelea Oktoba 23 aliwauliza kuhusu stahiki zake kama mbunge,"alisema.

Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nje ya nyumba yake akirejea kutoka vikao vya bunge Dodoma, Septemba 7 na kukimbizwa hospitali ya Nairobi kwa matibabu ambapo hadi sasa anapatiwa matibabu.

Breaking News: TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia

$
0
0
Mchambuzi Huru imepata uthibitisho wa taarifa za kifo cha Mhe. Gama ambacho kinadaiwa kutokea muda wa Saa 6 kuelekea Saa 7 usiku wa kuamkia leo.

Amefariki akiwa mbunge wa Songea Mjini na amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii Songea katika Hospitali ya Peramiho.

Gama amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Inadaiwa marehemu Gama alianguka nyumbani kwake saa saba usiku juzi huko Likuyu; akapooza upande wa kushoto akawa hajitambui kabisa na akapelekwa Hospitali ya Peramiho ambako aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi

Dkt Slaa Apata Shavu Rais Magufuli Amteua Kuwa Balozi

$
0
0
Dkt Slaa Apata Shavu Rais Magufuli Amteua Kuwa Balozi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua aliyewahi kuwa Katibu mkuu wa Chama cha Chadema Dr. Wilborad Slaa kuwa balozi.

Moto Wateketeza Ofisi ya Ofisa Mtendaji Ubungo

$
0
0
Moto Wateketeza Ofisi ya Ofisa Mtendaji Ubungo
Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Saranga, Ubungo, jijini Dar es Salaam,  imeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo, huku baadhi ya mali na nyaraka za serikali zilizokuwemo zikiteketea.

Kwa mujibu wa wahusika, chanzo  cha moto huo hakijajulikana lakini juhudi zinaendelea kumpata mtendaji wa kata hiyo ili kujua hasara iliyotokana na moto huo na ni vitu au mali gani zilizokuwemo katika ofisi hiyo.

Muonekano wa ofisi ya Mtendaji Kata ya Saranga Ubungo iliyotekelezwa kwa moto usiku wa kuamkia leo.



Tanzia: Mbunge wa Songea Mjini Gama Kuzikwa Kijijini Kwao Likuyufusi

$
0
0
Tanzia: Mbunge wa Songea Mjini Gama Kuzikwa Kijijini Kwao Likuyufusi
Aliyekua mbunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama anatarajiwa kuzikwa Jumatatu katika makaburi ya familia yaliyopo Kijiji cha Likuyufusi mkoani Ruvuma.

Gama aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Novemba 24,2017 atazikwa Jumatatu Novemba 27,2017 katika makaburi hayo yaliyopo umbali wa kilomita 25 kutoka Songea mjini.

Akizungumza na Mwananchi Issa Fussi ambaye ni msemaji wa familia na mdogo wa Gama amesema amefariki usiku wa kuamkia leo akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Peramiho.

Amesema Gama alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na alipelekwa hospitalini hapo Jumatano Novemba 22,2017 usiku na kulazwa hospitalini hapo .

Fussi amesema msiba huo ni pigo kwa familia kwa kuwa Gama alikuwa nguzo akitegemewa katika masuala mbalimbali ya maendeleo na kifamilia.

Amesema mwili wa marehemu Gama umehifadhiwa katika Hospitali ya Peramiho na utaratibu wa mazishi unaendelea.

Wolper Alia na Mastaa Kutomsapoti Katika Biashara Yake

$
0
0
Wolper Alia na Mastaa Kutomsapoti Katika Biashara Yake
STAA wa Bongo Movies, Jacquline Wolper amesema kuwa mastaa wengi hawapendi kupeana ‘sapoti’, kiasi kwamba hata kama staa mwenzao akiwa na biashara yake wapo radhi kununua kwingine lakini si kwake, ili tu wamkomoe.

Akichonga na gazeti hili, Wolper alijitolea mfano kwa kusema kuwa tangu amejiingiza kwenye biashara ya ushonaji, watu wengi ambao wamekuwa wateja wa biashara zake ni wa kawaida tu na wasanii wenzike hawazidi hata watatu. “Unapofanya maendeleo kwa sisi mastaa wenzako si kwamba wanapenda.
 Wananuna ndiyo maana huwezi kuwaona wakikusapoti,” alisema Wolper.

Mama Kanumba Aumizwa na Kifungo cha Lulu Ajipanga Kumtembelea Gerezani

$
0
0
Mama Kanumba Aumizwa na Kifungo cha Lulu Ajipanga Kumtembelea Gerezani
MAMA wa staa wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Frola Mtegoa amesema kuwa, kutokana na matatizo yaliyompata staa wa filamu Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili, amekuwa akimuonea huruma na anajipanga kumtembelea gerezani.

Akipiga stori na Ijumaa, Mtegoa alisema watu wengi wamekuwa wakihisi kuwa ana chuki na Lulu, lakini moyo wake unampenda na kama isingekuwa sheria kuhitaji Lulu kufungwa basi yeye asingekuwa na tatizo naye.

Staa wa filamu Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’
“Sina chuki na Lulu, tulikuwa karibu lakini nafikiri watu wake wanaozunguka ndiyo waliosababisha ukaribu wetu kuparanganyika. “Lakini moyoni ninampenda na kiimani mimi ni Mkristo.

Kwa hiyo siwezi kufurahi kuona mwenzangu anapata matatizo, ipo siku nitamtembelea gerezani!” alisema mama huyo.

Emmerson Mnangagwa Kuapishwa Kumrithi Mugabe Kama Rais

$
0
0
Emmerson Mnangagwa Kuapishwa Kumrithi Mugabe Kama Rais
Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla.
Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano -ataapishwa kaka uwanja wa ndege wa Harare.
Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke .
Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza "utamaduni wa ufisadi".
Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 hapo siku ya Jumanne iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe
Ilitolewa kwa njia ya barua bungeni na kikao cha kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae kikakatizwa.
Katika barua hiyo Bwana Mugabe alisema anajiuzulu ili kuruhusu mchakato rahisi na wa amani wa ukabidhianaji mamlaka na kwamba uamuzi wake ulikuwa wa hiari.
Robert Mugabe na mkewe Grace tarehe 8 Novemba 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image caption
Rais Mugabe alishutumiwa kwa kumuandaa mkewe Grace kuchukua wadhfa wa urais
Bwana Mugabe na mkewe Grace hawajaonekana hadharani tangu Jumapili, na haifahamiki wako wapi .
Alhamis , taarifa zilielezea kuwa Bwana Mugabe amepewa kinga ya kutoshtakiwa.
Televisheni ya taifa imesema kuwa atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Bwana Munangagwa.
Sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa michezo mjini Harare wenye viti 60,000- huku waandalizi wakiwataka waZimbabwe kuhudhuria kwa wingi sherehe hizo.
Alhamisi Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini (MDC ) alitoa wito wa kufanyika kwa mageuzi makubwa ya kisiasa ili kuondoa masuala yaliyoweka madarakani kwa muda mrefu utawala wa Bwana.
Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai
Image caption
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement fo Democratic Change (MDC) Morgan Tsvangirai
Bwana Munangagwa alikimbilia nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita- na kurejea nchini Jumatano wiki hii ambapo alipokelewa kama shujaa.
Bwana Mnangagwa aliahidi kubuni ajira ambapo baadhi wanakadiria kuwa 90% ya watu hawana ajira.
"Tunataka kukuza uchumi wetu, tunataka amani, tunataka kazi, kazi, kazi ," aliuambia umati wa watu uliomshangilia mjini Harare.
Jumatano chama tawala cha ZANU PF kilisema kitafanya mageuzi kuondoa sheria zilizomfanya Mugabe kuwepo madarakani kwa muda mrefu.

Mugabe Kuhudhuria Kuapishwa kwa Emmerson Mnangagwa

$
0
0
Mugabe kuhudhuria kuapishwa kwa Emmerson Mnangagwa
Robert Mugabe anatarajiwa kuhudhuria kuapishwa kwa rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kulingana na runinga ya habari ya taifa hilo ZBC .
Maandalizi yameanza katika uwanja wa kitaifa wa michezo katika mji mkuu wa Harare ambapo hafla hiyo itafanyika.
Mwandishi wa maswala ya kidiplomasia Judith Makwanya amesema kuwa kiongozi anayeondoka anatarajiwa kukagua gwaride akitoa kwaheri huku kiongozi mpya akilijulisha jeshi katika sherehe hiyo ya gwaride.
Tayari waziri wa Uingereza barani Afrika Rory Stewart amewasili nchini Zimbabwe mapema kulinga na chombo cha habari cha AFP.
Mugabe: ''Naombewa nife''
Mugabe atakumbukwa kwa mabaya
Rais Robert Mugabe amejiuzulu
Afisa huyo amewasili tayari kuhudhuria kuapishwa kwa rais mpya siku ya Ijumaa.
Bwana Sterwart anatarajiwa kukutana na viongozi wa kisiasa na wale wa kibiashara pamoja na makundi ya haki za kibinaadamu na mashirika yasiokuwa ya kiserikali kulingana na waziri wa maswala ya kigeni nchini Uingereza.
Ametaja mabadiliko hayo ya kihistoria kuwa wakati muhimu baada ya utawala mbaya wa rais wa zamani Robert Mugabe.
Uingereza inataka kuwa mshirika wa kweli wa raia wa Zimbabwe wakati huu ambao wanaanza mwanzo mpya, bwana Stewart aliambia AFP

Washawasha la Polisi Lililokuwa Katika Msafara wa Kusindikiza Mahabusu Lapinduka Kiajabu

$
0
0
Washawasha la Polisi Lililokuwa Katika Msafara wa Kusindikiza Mahabusu Lapinduka kiajab
GARI la Jeshi la Polisi linalobeba maji ya kuwasha maarufu kama ‘washawasha’ lililokuwa kwenye msafara wa kusindikiza mahabusu, lilipinduka barabarani na kusababisha msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam jana.

PICHA HII HAIHUSIANI NA HABARI HII.
Washawasha hilo lenye namba PT 0887 aina ya Mercedes Benz, ambalo ndani yake kulikuwa na dereva na askari mmoja, lilipata ajali Barabara ya Bibi Titi, baada ya tairi moja la mbele kupasuka.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alithibitisha kuwapo kwa ajali hiyo iliyotokea saa 4:00 asubuhi na kutaja chanzo chake kuwa ni kupasuka kwa tairi.

“Baada ya ajali ilifanyika juhudi za kuliinua na kuliondoa eneo la barabara ili lisiendelee kusababisha foleni zaidi katikati ya mji,” alisema.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni alisema gari hilo lilikuwa likitokea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuelekea Kambi ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Ukonga.

“Gari hili la washawasha lilikuwa kwenye mwelekeo mmoja na magari mengine ambayo yalikuwa yamebeba mahabusu wakitoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuelekea Ukonga,” alisema.

Alisema baada ya kufika eneo hilo ndipo lilipopinduka na kusababisha barabara hiyo isipitike pamoja na kuwajeruhi askari waliokuwa ndani.

Alisema waliojeruhiwa ni dereva na askari mmoja aliyekuwa ndani ya gari hilo ambalo nalo limeharibika.

“Ajali ilitokea saa 4:00 asubuhi na hadi saa 5:15 lilikuwa limeshaondolewa eneo la tukio, ilichukua muda kidogo kuliondoa kama unavyojua uzito wa gari hili,” alisema.


JE Wajua Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Madogo ya Kiume? 07:55

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WA NA MAUMBILE MADOGO?
Tatizo hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia ,hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wenzao,kwakawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6_8 vinginevyo mtu huyu ana matatizo.


Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo baadhi ni,upungufu wa vichocheo (hornes) za gestrojen ambapo mwanaume anapobalehe vichocheo hivi (hormones)huchochea ujuaji wa uume.chango ambalo hushambulia nerve ambapo huharibu kabisa ukuaji wa uume, Punyeto ambayo huasili misuli ya uume,pia ngiri ambayo huleta maumivu ya tumbo kuunguluma na kujaa gesi,korodani moja kuvimba,kutopata choo vizuri,sababu hizi na nyinginezo hufanya uume kulegea na kisinyaa nakuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu zakiume (hamu ya tendo landoa hupungua au kuisha kabisa).NSUMBU,Nidawa inayozalisha hormones za gestrogene na kufanya uume kukua na kuongezeka mara dufu.NZAGI,Ni dawa ya kurudisha nguvu za kiume ,hutia hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha nakuponya kabisa tatizo hilo. Pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk 15 nakuendelea kwa tendo la kwanza.kumbuka dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji.Natunatibu kisukari,bp,ngiri,miguu kuwaka moto,namengine mengi.

WASILIANA OSTADHI JUMA KWA SIMU NO,0784002216 AU 0769597778

Dr. Luis Shika Natoa Milioni 1.5$ Za Kimarekani Kila Mwaka Shinyanga Wilayani Kahama

$
0
0
Dr. Luis Shika Natoa Milioni 1.5$ Za Kimarekani Kila Mwaka Shinyanga Wilayani Kahama
VIDEO:

Uteuzi wa Dr. W.P.Slaa kuwa Balozi: Rais Magufuli Anaendelea Kujieleza na Kujipambanua Kisiasa

$
0
0
Mwanzo mwanzoni nikiri kuwa nimefarijika sana kwa uteuzi wa Dr. Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi. Uteuzi huo umefanywa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli. Nimefurahi kwakuwa Dr. Slaa, kwa weledi wake, usomi wake, kwa sifa zake uzoefu wake na ubobezi anastahili uteuzi huo au wowote kwa ajili ya kuitumikia nchi.

Kwa uteuzi wa Dr. Slaa kuwa Balozi, Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM anaendelea kujieleza na kujipambanua. Anajipambanua kuwa anasimamia kauli zake. Mara kwa mara hutamka kuwa 'maendeleo hayana chama'. Na akawahi kukaririwa akisema kuwa anaweza kumteua hata asiye mwanaCCM kama tu ana sifa. Akafanya hivyo kwa Mama Mghwira na kwa Prof. Kitila Mkumbo.

Teuzi zake nje ya CCM, pamoja na kwamba zinaweza kuzua malalamiko, manung'uniko na maumivu kwa wanaCCM, zinajieleza na kujipambanua kuwa uwezo, uzalendo na uchapakazi ndiyo vigezo pekee vilivyobaki katika teuzi za Rais Magufuli. Kwake yeye, hakuna tofauti kati ya mwanaCCM au mwanachama wa chama kingine au asiye na chama kama Dr. Slaa. Ipso facto,Mr. President depicts himself.

Ndiyo maana, katika moja ya michango yangu humu, nimewahi kusema kuwa Rais Magufuli ni 'Jenerali wa Kisiasa'. Anachofanya ni kukusanya na kushambulia tu katika kusimamia ajenda zake alizoahidi na anazoziahidi.

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo Ijumaa

$
0
0

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi +255 622588038au 0679119679 au +255 764318107
NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Wema Sepetu Afiwa Ashindwa Kutinga Mahakamani Kesi Yake Yaahirishwa

$
0
0
Wema Sepetu Ashindwa Kutinga Mahakamani Kesi  Yake Yaahirishwa
Kesi ya kutumia madawa ya kulevya inayomkabili Malkia wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu imeahirishwa leo katika Mahakama ya Mkazi Kisutu hadi Desemba 14 mwaka huu.

Akieleza sababu za kuahirishwa kwa kesi hiyo Wakili anayemsimamia Wema Sepetu, Peter Kibatala amesema mteja wake amefiwa hivyo asingeliweza kufika Mahakamani leo.

Wema Sepetu anakabiliwa na kesi ya kutumia madawa ya kulevya aina ya Bangi na tayari pande zote mbili zimesha wasilishaushahidi mahakamani.

Shamsa Ford Akoshwa na Ya Dkt Shika Awataka Wasanii Kuiga Mfano Wake

$
0
0
Shamsa Ford Akoshwa na Ya Dkt Shika Awataka  Wasanii Kuiga Mfano Wake
Msanii wa Filamu Bongo, Shamsa Ford ameonyesha kufurahishwa kwa namna Dkt.  Louis Shika alivyokuwa maarufu kwa kipindi kifupi bila kutumia nguvu kubwa.

Katika hilo Shamsa amewataka wasanii wenzake kuinga mfano huo kwa kufanya kazi kwa bidii na zenye ubora na wakati wao ukifika watatoka tu na si vinginevyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shamsa ameandika;

Nilichojifunza kutoka kwa Dk. SHIKA Wasanii wengi hutumia nguvu kubwa ili wawe midomoni mwa watu, hufikia hatua ya kutengeneza skendo, kuunda mabifu, kuloga, kutukanana n.k.

Kuibuka kwa Dr. Shika kumefanya nijue kama umepangiwa kuwa maarufu utakuwa tu. Unadhani kusema tu ‘900 itapendeza’ ndio kunaweza kumfanya mtu awe maarufu? Hapana!, ni wakati wake tu ulikuwa umefika, hata wewe na yule zamu yako ikifika utakuwa tu juu.

Nachowashauri wenzangu haina haja ya kulazimisha umaarufu jitahidi ufanye kazi kwa bidii na uwe mbunifu kwa kile ukifanyacho kazi yako itakupandisha juu na kamwe hutoshuka ila ukilazimisha umaarufu utasikika kwa muda tu na kisha kupotea kabisa.

Kwa kina dada wale wanaopiga picture za utupu ili wapate umaarufu mwisho wa siku utaambulia umaarufu wa kudharauliwa na unakwisha kwa muda mfupi.

Umaarufu wa Dkt. Shika umekuja baada ya kujitokeza katika mnada wa  kuuza nyumba za Lugumi ambapo Dk. Shika aliahidi kununua nyumba hizo kwa thamani ya Sh bilioni 2.3 lakini alishindwa kulipia asilimia 25 ya fedha hizo ambazo ni shilingi milioni 800.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images