Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Diamond Azungumzia Matatizo Yanayompata Kwenye Maisha Yake ya Mapenzi Kwa Namna Hii

$
0
0
Diamond  Azungumzia Matatizo Yanayompata  Kwenye Maisha Yake ya Mapenzi
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz ameachia wimbo mpya wenye simulizi ya kinachomshinda katika kuishi maisha ya mahusiano ambapo hakuacha kusimuliza juu ya tukio lililotokea mpaka kupata mtoto wake wa tatu ‘Prince Abdul’ kwa mrembo Hamisa Mobetto.

Diamond Platnumz kama ilivyo kawaida yake kuyazungumzia mapenzi kwa malalamiko hakuacha kuwahusisha mtayarishaji wa kazi hiyo Lizer na dada yake Esma jinsi walivyomshauri juaa ya patashika alizokutana nazo katika mapenzi ya wapenzi aliowapenda mpaka kufikia hatua ya kutia nanga nzito kwa mama wa watito wake Zarinah Hassan ‘Zari The BossLady’

Marufuku Kumuweka Mwanangu Kwenye Mitandao ya Kijamii- Masogange

$
0
0
Marufuku Kumuweka Mwanangu Kwenye Mitandao ya Kijamii- Masogange
MREMBO aliyejipatia jina kubwa kutokana na kazi yake ya kuuza nyago kwenye video za wanamuziki Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ amesema kuwa, kwa upande wake ni marufuku kumuweka mtoto wake kwenye mitandao ya kijamii.

Masogange aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, ni bora yeye akiwa anatukanwa na kuambiwa maneno machafu kuliko mwanaye kwa sababu kwenye mitandao watu hawaangalii kama ni mtoto, bali wao ni kutukana tu.

“Siwezi kumnadi mwanangu, ni jambo ambalo nimejiwekea, kama atapenda mambo ya mtandaoni, akija kuwa mkubwa, atajiachia mwenyewe,” alisema Masogange ambaye mtoto mwanaye huyo wa kike ana umri miaka nane sasa.

IGP Siro Afanya Ziara Bandari Dar Kufanya Ukaguzi wa Magari Yaliyoibuliwa Rais Magufuli

$
0
0
IGP Siro Afanya Ziara Bandari Dar  Kufanya Ukaguzi wa Magari Yaliyoibuliwa Rais Magufuli
MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro, amefanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam, ili kufanya ukaguzi wa magari 31 ya Jeshi hilo ambayo Rais John Magufuli, alielekeza kukabidhiwa kwa Jeshi hilo ili kurahisisha utendaji wao wa kazi.

Akiwa Bandarini hapo IGP Sirro amekutana na kufanya mazungumzo na askari wa Jeshi hilo Kikosi cha Bandari ambapo amewataka kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ipasavyo pamoja na kutenda haki ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wateja.
Hata hivyo IGP amewataka Polisi wasaidizi wanaofanya kazi bandarini hapo kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuendelea kudhibiti vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.

Rais Alikubali Goli la Messi Lililokataliwa na Refa

$
0
0
Rais wa La Liga Javier Tebas Amesema Goli la Messi Lililokataliwa na Refa ni Halali
Rais wa La Liga Javier Tebas amesema goli alilofunga Messi dhidi ya Valencia jumapili, likakataliwa na refarii lilikuwa ni goli halali ila kutokuwa na teknolojia ya mwamuzi wa video ndio kumesababisha utata huo.

“Nikisema sio goli nitakuwa nadanganya na dunia itaniona muongo na kuniambia labda nimekuwa kipofu, lilikuwa ni goli halali lakini kukosa VAR ndio sababu ya bao hilo kutokukubaliwa”, amesema Tebas.
Tebas amesema msimu ujao matumizi ya Video Assistant Referee (VAR) yataanza bila kuchelewa ili kuepusha makosa kama hayo yaliyotokea kwenye bao la Messi.

Messi alifunga bao halali dakika ya 30 baada ya mkwaju wake kumpita mlinda mlango Neto wa Valencia kabla ya kipa huyo kufanya jitihada za kuuokoa lakini tayari ulikuwa umevuka mstari ila mwamuzi hakuona hivyo kuamuru mechi iendelee.
Barcelona wanaongoza msimamo wa La Liga kwa alama 35 wakifuatiwa na Valencia yenye alama 31. Atletico Madrid ipo nafasi ya 3 ikiwa na alama 27 sawa na mabingwa watetezi Real Madrid wenye alama 27 katika nafasi ya 4.

Viwanja Vinauzwa Kwa Bei Nafuuu Kabisa Bunju Mapinga Dar/ Magamoyo

$
0
0

Sale! Sale! Viwanja Mapinga. Nauza viwanja bei sawa na bure kama ifuatavyo: 20/30 mil 7, 30/30 mil 10, 30/40 mil 13, nusu eka mil 20, ekari moja mil 40
Call / whatsap 0757489709
Email: menejadar@yahoo.com

Edward Lowassa Afika Sherehe ya Kuapishwa kwa Kenyatta

$
0
0

Lowassa afika sherehe ya kuapishwa kwa Kenyatta

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Edward Lowassa ni miongoni mwa wageni waliofika Kasarani sherehe ya kuapishwa kwa Bw Kenyatta.

Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0
MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.


Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na Nasi kwa Namba; 0783140065

Tupo Mbagala Rangi Tat

Polisi Watumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya Mamia ya Watu Kenya

$
0
0
Polisi Watumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya Mamia ya Watu Karasani
Polisi wametumia mabomu ya machozi kudhibiti mamia ya watu waliokuwa wanataka kuingia kwa nguvu kwenye uwanja wa Kasarani ambako zinafanyika sherehe za kuapishwa Rais Uhuru Kenyatta.

"Haki yetu, Haki Yetu," walipiga kelele watu hao ambao wengi wao walikuwa wamevalia nguo za rangi za chama tawala cha Jubilee walipokuwa wakisukumana kutaka kuwapita polisi.

Maofisa wa polisi waliwazuia watu hao wakawapiga baadhi na kuwaacha wakiwa majeruhi. Baadhi walipata tiba ya huduma ya kwanza wakati walioumia zaidi walisafirishwa hadi Hospitali ya Taifa ya Kenyatta.

Polisi walionekana wakiwakimbiza baadhi ya watu wakati wengine walipita kwa nguvu kwenye milango.

Kulikuwa na farasi na magari ya kubeba wagonjwa. Ulinzi ni mkali na wahudhuriaji wote lazima wapekuliwe kuingia ndani ya uwanja huo ambamo wageni kutoka nchi 20 – wakuu wa nchi au mawaziri – wamehudhuria.

Hata hivyo, kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga, aliyesusia uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26 amesusia sherehe hizo na badala yake alikuwa amepanga kuhutubia mkusanyiko mwingine mkubwa eneo la Jacaranda kwa ajili ya kuwakumbuka wafuasi wao waliouawa wakati wa maandamano hivi karibuni.

Kikwete Asikitishwa Kukoza Sherehe za Kuapishwa Kenyatta

$
0
0
Kikwete Asikitishwa Kukoza Sherehe za Kuapishwa Kenyatta
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete amesikitika kutohudhuria kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya na kusema alipata mwaliko kuhudhuria sherehe za kuapishwa Kenyatta lakini ameshindwa kutokana na kuingiliana kwa majukumu.

Leo baadhi ya mitandao ya kijamii nchini Kenya alidai kuwa Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete ni mmoja wa wageni ambao wamehudhuria sherehe za kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta jambo ambalo Jakaya Kikwete amelipinga kwa kusema ameshindwa kwenda Kenya kutokana na majukumu kuingiliana.
Jakaya Kikwete ametumia mtandao wake wa Twitter kufikisha ujumbe wake wa pongezi kwa Kenyatta kuchaguliwa tena kuongoza nchi ya Kenya ambayo ni nchi rafiki na Tanzania kwa miaka mingi sasa.
"Nakupongeza Rais UKenyatta kwa kuchaguliwa tena kuongoza nchi rafiki ya Kenya. Nakushukuru kwa mwaliko wa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwako. Nasikitika sitaweza kuhudhuria kutokana na kuingiliana kwa majukumu. Nakutakia kila la kheri katika awamu yako ijayo" alindika Kikwete

Rais Uhuru Kenyatta alichaguliwa kuwa Rais kwa Kenya katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26, 2017

Ratiba ya Michuano ya Kombe la Mapinduzi Hii Hapa Yanga Yabebwa

$
0
0
Ratiba ya Michuano ya Kombe la Mapinduzi Hii Hapa
Ratiba ya michuano ya kombe la Mapinduzi imetolewa ambapo mabingwa watetezi, Azam FC wataanza na Jamhuri katika mchezo utakaofanyika uwanja wa Amaan  Januari 2 mwaka 2018, kuanzia saa 10:15 jioni.

Simba SC ambayo ilicheza fainali na Azam FC mashindano yaliyopita itafungua dimba na URA ya Uganda katika michuano hiyo Januari 2, mwaka 2018 uwanja wa Amaan, Zanzibar mchezo ambao utaanza saa 2:15 usiku.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara Yanga, wataanza na JKU ya Zanzibar Januari 1, uwanja wa Amaan, mchezo huo utaanza saa 2:15 usiku.
Ufunguzi rasmi wa Kombe la Mapinduzi 2018 utafanyika Desemba 30, mwaka huu kwa mechi mbili kuchezwa Uwanja wa Amaan, kwanza Zimamoto na Mlandege Saa 10:17 jioni na baadaye JKU na Shaba Saa 2:15 usiku.

Pesa ya Kumsaidia Dudu Baya Ninayo, Najua Hayuko Vizuri- Mr Nice

$
0
0
Pesa ya Kumsaidia Dudu Baya Ninayo, Najua Hayuko Vizuri- Mr Nice
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Mr. Nice amesema anajua kwa sasa Dudu Baya ana hali mbaya ila kama msanii huyo anatajitokeza yeye yupo tayari kumsaidia ili aweze kuendelea na muziki wake.

Muimbaji huyo ambaye kipindi cha nyuma alikuwa na ugomvi mkubwa na Dudu Baya, ameiambia E-Newz ya EATV kuwa anapoishi nchini Kenya amekuwa akisaidia watu wengi hivyo hataona tabu kufanya hivyo kwa Dudu Baya.

“Napenda kumpa salamu nyingi, napenda kumuombea kwa Mungu abadilike amekua mtu mzima sasa fanye muziki. Ajitokeze afanye muziki na mimi nipo tayari kumsapoti kwa sababu hata pesa ya kumsaidia Dudu Baya ninayo, najua hayuko vizuri, hivyo naweza kumsaidia” amesema Mr. Nice.

Hata hivyo amesema kuwa msaada huo ni hadi pale atakapokidhi vigezo na masharti na kuongeza kuwa kitendo cha Dudu Baya kumfuata jukwaani kipindi cha nyuma na kumpiga kimefanya watu wengi kumuogopa na kushindwa hata kumsaidia pindi anapokuwa na shida.

Yanga Yamsajili Mshambuliaji Yohana Mkomolwa Kutoka Serengeti Boys

$
0
0
Yanga Yamsajili Mshambuliaji  Yohana Mkomolwa Kutoka Serengeti Boys
SIKU moja baada ya kumsainisha mkataba wa miaka miwili beki wa kati raia wa Kongo, Fiston Kayembe, Yanga jana ilimnasa mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Vijana 'Serengeti Boys' Yohana Mkomolwa.

Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, imemsainisha nyota huyo mkataba wa miaka miwili na ataanza kuitumikia timu hiyo pale ligi itakapoendelea baada ya kupisha michuano ya Kombe la Chalenji.

Mkomolwa ambaye alifanya vizuri na Serengeti Boys kwenye michuano ya Afrika iliyofanyika, Gabon mwaka huu,anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Yanga kwenye dirisha hili dogo.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, akizungumza na gazeti hili jana, alithibitisha 'kinda' huyo kusajiliwa na Yanga.'Ni kweli Mkomolwa amejiunga na sisi..., na hii ni katika kuboresha kikosi chetu," alisema Saleh.

Katika hatua nyingine, Saleh, aliema kuwa kocha wa timu hiyo, George Lwandamina, ametoa mapumziko ya wiki moja kwa wachezji wake.

Alisema wachezaji wa timu hiyo wataendelea na mazoezi Jumatatu ijayo kwenye Uwanja wa Uhuru.

"Unajua baada ya ligi kusimama, kocha ameamua kuwapa wachezaji ambao hawamo kwenye vikosi vya timu za Taifa mapumziko ya wiki moja, tutaanza mazoezi Jumatatu ijayo,"alisema Saleh.

Yanga inawachezaji kwenye vikosi vya timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' na ile ya zanzibar 'Zanzibar Heroes' ambazo zote zitashiriki michuano ya Chalenji inayoanza Desemba 5, mwaka huu nchini Kenya.

Mama Samia, Lowasa Kushuhudia Kuapishwa kwa Kenyatta

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa na Makamu wa Rais Samia Suluhu ni miongoni mwa viongozi waliofika nchini Kenya kuiwakilisha Tanzania kwenye sherehe za kuapishwa rais wa nchi hiyo.

Kiongozi mwingine wa Tanzania ambaye  amehudhuria sherehe hizo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki Dk Suzan Kolimba

Sherehe za kuapishwa Uhuru Kenyatta zinafanyika leo mjini Nairobi huku viongozi wa mataifa mbalimbali  wakiwa wanatarajiwa kushuhudia.

Taifa la Kenya leo linatekeleza shughuli muhimu ya kikatiba ya kumuapishwa kiongozi wa taifa hilo kufuatia ushindi wake wa marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 uliosusiwa na upinzani.

Uhuru Kenyatta leo anaapishwa rasmi kuwa rais wa nchi hiyo kwa muhula wa pili baada ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu.

Uchaguzi uliofanyika Agosti ulifutwa  na mahakama kutokana na kile kilichotajwa kuwa uchaguzi usio huru na haki.

Marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 ulimpatia Kenyatta asilimia 98 ya kura huku waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo wakiwa  na asilimia 39.

Eti Unashangilia Ushindi! Huu ni uporaji- Msigwa

$
0
0
Eti Unashangilia Ushindi! Huu ni uporaji- Msigwa
Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa ametupa jiwe gizani kwa wapinzani wao wea kisiasa kwamba wamewashinda kwa hoja zote za kisiasa na wameshindwa kuzijibu hicyo anawashangaa kushangilia ushindi.

Msigwa amesema kwamba wapinzani  wao lazima watawashinda kama watatumia vyombo vya usalama na siyo kwa hoja na kwamba wao Chadema wakitoa hoja wao wamekuwa wakishindwa kuzijibu.
Msigwa kupitia ukurasa wake wa Twiter ameandika kwamba "Hatuna mafunzo ya kipolisi wala kijeshi! Mkitumia vyombo vya usalama lazima mtatushinda , lakini tumewashinda HOJA zote za kisiasa! Mmeshindwa kuzijibu! Eti unashangilia Ushindi! Huu ni uporaji" Msigwa
Chama cha upinzani CHADEMA kimekuwa kikilalamikia chama tawala kutumia vyombo vya dola katika kuwakandamiza.

Alichokisema Zitto Kabwe Baada ya Rais Magufuli Kutohudhuria Sherehe za Kuapishwa kwa Rais Kenyatta

$
0
0
Alichokisema Zitto Kabwe Baada ya Rais Magufuli Kutohudhuria Kuapishwa kwa Rais Kenyatta
Zitto Kabwe amefunguka na kusema kitendo cha Makamu wa Rais Mhe. Samia kupokelewa na Balozi Kenya ni ishara kuwa mahusiano ya Tanzania na Kenya hayapo vizuri na kudai Rais Magufuli kutokwenda kwenye sherehe za kuapishwa Kenyatta inaweza kueleweka.

Zitto Kabwe amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter na kusema kitendo cha Rais Magufuli kutohudhuria kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta inaweza kueleweka kwani kiongozi huyo hakuweza kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame.
"Makamu wetu wa Rais kupokelewa na Balozi ( sio hata Waziri wa Mashauri ya Kigeni au Waziri mwengine) ni dalili kuwa mahusiano yetu yanalega lega. Rais kutokwenda Kenya inaweza kueleweka maana hata Rwanda hakwenda kwenye uapishaji wa Paul Kagame" aliandika Zitto Kabwe.


Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi +255 622588038au 0679119679 au +255 764318107
NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE..

Mmiliki wa Shule Apandishwa Kizimbani na Kusomewa Shitaka la Mauaji ya Mwanafunzi Moshi

$
0
0
Mmiliki wa Shule Apandishwa Kizimbani na Kusomewa Shitaka la Mauaji ya Mwanafunzi Moshi
Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi imewasomea shitaka la mauaji watu watatu wanaotuhumiwa kumuua kijana Humphrey Makundi aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo Moshi.

Watuhumiwa hao ni mmiliki wa shule ya Scolastica, Edward Shayo mwenye miaka 63, mlinzi wa shule hiyo Hamis Chacha mwenye miaka 28 na Laban Nabiswa mwenye miaka 37.
Upande wa Jamhuri katika shitaka hilo lililofika mbele ya Hakimu Mkazi, Julieti Mawore umewakilishwa na Mwanasheria Kassim Nassiri akisaidiana na Wakili wa kujitegemea, Faygrace Sadallah.
Akisoma maelezo ya hati ya mashitaka mbele ya mahakama hiyo, Nassiri alieleza kuwa mnamo Novemba 6 mwaka huu mshitakiwa wa kwanza, Hamis Chacha wa pili Edward Shayo na wa tatu Laban Nabiswa, walimuua kwa kukusudia mtu aitwaye Humphrey Makundi.

Aidha washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikliza shitaka la mauaji huku akiwataka kusubiri kufanya hivyo pindi watakapofikishwa mahakama kuu ambapo watapata nafasi ya kuwasilisha mashahidi wao pamoja na kujitetea.
Hakimu Mkazi Mawore, ameahairisha shitaka hadi Desemba 8 mwaka huu litakapotajwa tena na  kwamba washitakiwa wote watarudishwa rumande kutokana na  kesi hiyo kutokuwa na dhamana.

Setlait ya Urusi Yapoteza Mawasiliano Yake Baada ya Kuizindua

$
0
0
Urusi Yapoteza Mawasiliano na Setlait Yake Baada ya Kuizindu
Urusi imepoteza mawasiliano na setlait yake ya hali ya hewa saa chache baada ya kuizindua.
Mawasiliano yamepotea kwa sababu haiko katika obit yake , kulingana na shirika la angani la Roscoms.
Setlait hiyo kwa jina Meteor-M ilibebwa katika roketi ya Soyuz.
Uzinduzi huo ulifanyika kutoka eneo la Vostochny cosmodrome mashariki mwa Urusi.
Ni uzinduzi wa pili kutoka kambi hiyo ambayo ilifunguliwa mwaka uliopita.

Biblia Iliyotumika Kumuapisha Rais wa Kwanza wa Kenya Yatumika Kumuapisha Uhuru Kenyatta na Makamo Wake

$
0
0
Biblia Iliyotumika Kumuapisha Rais wa Kwanza wa Kenya Yatumika Kumuapisha Uhuru Kenyatta na Makamo Wake
KATIKA hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Kenya na Makamu wake, imeelezwa kuwa, nakala ya Biblia iliyotumiwa kumwapisha Rais Uhuru Kenyatta ni ile iliyotumiwa kumwapisha kwa Rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta ambaye ni baba’ke rais wa sasa wakati nakala ya Katiba ni iliyotiwa saini wakati wa kurasmishwa kwa Katiba ya sasa mwaka 2010 uwanjani Uhuru Park.
Biblia hiyo ilitumika mwaka 1964 kumwapisha Jomo Kenyatta, 2013 kumwapisha Uhuru kenyatta na leo Novemba 28, 2017 kumwapisha Uhuru Kenyatta katika Uwanja wa Kasarani.

Uhuru Kenyatta akiapishwa kuwa Rais wa Kenya mwaka 2013.
Msajili Mkuu wa Mahakama, Anne Amadi amemwapisha Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Kenya kwa mhula wa miaka mingine mitano ijayo na William Ruto kuwa Makamu wake.
Rais Kenyatta: “Nitatekeleza majukumu yangu, na wajibu wangu katika Ofisi ya rais wa Kenya, na kwamba nitatenda haki kwa wote kwa mujibu wa Katiba hii kama ilivyo kwenye sheria, na sheria za Kenya bila woga, mapendeleo au ubaguzi au nia mbaya. Ewe mwenyezi Mungu nisaidie.”

Uhuru Kenyatta akiapishwa kuwa Rais wa Kenya, leo Novemba 28,  2017.
Rais Kenyatta ala kiapo cha utiifu.
Rais Kenyatta: “Naapa kwamba nitakuwa mwaminifu, kikamilifu, kwa Jamhuri ya Kenya, kwamba nitatii, nitahifadhi, kulinda na kutetea Katiba ya Kenya kama ilivyo kwenye sheria, na sheria nyingine zote za Jamhuri. Na kwamba nitalinda mipaka na heshima ya watu wa Kenya. Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.”
Baadaye, alitia saini viapo vyote viwili, kisha cheti cha kuapishwa, kuthibitisha kwamba sherehe ya leo imefanyika ambapo pia Jaji Mkuu David Maraga pia aliweka saini yake kwenye stakabadhi zote tatu (vipao viwili) na cheti cha kuapishwa kwa Rais ikifuatiwa na Jeshi la nchi hiyo kupiga Mizinga 21 ikiwa ni heshima kwa Rais mpya, Uhuru Kenyatta.

Tanesco Yaanza Kuhamisha Mali Zake Kwenye Jengo Lao Lililowekwa X

$
0
0
Tanesco Yaanza Kuhamisha Mali Zake Kwenye Jengo Lao Lililowekwa X
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linahamisha mali zake kwenye jengo linalopaswa kubomolewa eneo la Ubungo lililo ndani ya hifadhi ya barabara.

Pilikapilika za wafanyakazi wa shirika hilo kuhamisha mali zinaendelea leo Jumanne Novemba 28,2017.

Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji amesema wanahamia katika ofisi zingine za shirika hilo zilizoko jijini Dar es Salaam.

Uongozi wa Tanesco katika taarifa kwa umma iliyotolewa jana Jumatatu Novemba 27,2017 ulisema umeanza utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu kubomolewa jengo hilo.

Novemba 15,2017 akitokea Chato alipokwenda kwa mapumziko baada ya ziara ya Uganda, Rais Magufuli aliagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuweka alama ya X katika jengo lenye ofisi za Tanesco sehemu zilizo katika hifadhi ya barabara.

Tanesco imeanza kubomoa ukuta wa mbele ya jengo hilo na kuhamisha watumishi kupisha shughuli za ubomoaji kufanyika kwa usalama.

Uongozi wa shirika hilo na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) unaendelea kufanya utaratibu utakaowezesha ubomoaji wa jengo hilo la ghorofa kufanyika bila kuathiri huduma kwa wateja wa Tanesco.

“Katika kipindi hiki cha utekelezaji wa agizo la Rais. Tunapenda kuwahakikishia wateja  na Watanzania kwa jumla kuwa, huduma za umeme zitaendelea kupatikana kama kawaida ikiwemo huduma ya ununuzi wa Luku,” imesema taarifa hiyo.
Chanzo: Mwananchi
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images