Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Mabasi 18 Yakamatwa kwa Kosa la Kuzidisha Nauli

$
0
0
Mabasi 18 Yakamatwa kwa Kosa la Kuzidisha Nauli
Jumla ya mabasi 18 yamekamatwa kwa siku mbili mkoani Tanga  kwa makosa  ya kuzidisha nauli kwa abiria katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya baada ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa nchi Kavu na Majini  (Sumatra)  kwa kushirikiana na jeshi la polisi kuendesha msako maalumu.

Ofisa wa Sumatra mkoa wa Tanga Dk Walukani Luhamba alisema jana kuwa idadi hiyo ya mabasi ilikamatwa kufuatia kufanyika oparesheni iliendeshwa kwa siku mbili kwa lengo la kudhibiti vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wenye mabasi kupandisha nauli katika kipindi hiki cha siku kuu za Krismasi na mwaka mpya.

Amesema  mabasi yaliyokamatwa katika oparesheni hiyo  ni yale  yaliyokuwa yakitokea Tanga kuelekea   Dar es salaam , Mbeya, Moshi, Arusha, Dodoma na Morogoro na nchi jirani ya Kenya ambapo mbali ya kuongeza nauli, mengine yalikutwa na makosa ya abiria kutofunga mikanda, mikanda mibovu, na kuzidisha idadi ya abiria kama kulingana na maelekezo ya leseni husika.

“Tumeweka kambi katika barabara kuu eneo la Mkata, Segera, Korogwe na Mombo, hakuna basi litakaloruhusiwa kuendelea na safari, tutawashusha abiria na dereva tutamfikisha mahakamani lakini mmiliki atatozwa faini ya Sh300,000”alisema Dk Walukani.

Ofisa huyo amesema  operesheni hiyo pia itahusisha ukaguzi wa mabasi yanayoondoka jijini Tanga kabla ya saa 12.00 alfajiri kwa sababu ni kinyume cha sheria ya usafirishaji wa abiria.

Hatua hiyo ya Sumatra, imepongezwa na wasafiri waliozungumza na Mwananchi katika kituo kikuu cha mabasi cha Kange Jijini Tanga waliosema kwa kipindi hiki kuna haja ya kuwadhibiti wenye mabasi kwani wanadai ni kipindi chao cha mavuno.

Flora Jonathani  aliyesafiri  kutoka  Dar es salaam hadi Tanga jana  amesema  ameshuhudia  abiria  waliokuwa wakielekea Mkoani Kilimanjaro wakitozwa Sh40,000 kila mmoja ili kuweza kupata nafasi kwenye mabasi.

“Kwenye tiketi wanaandika nauli inayoruhusiwa na Sumatra lakini fedha halisi wanazotoa abiria ni kubwa mno na wanakubali ili waweze kupata usafiri kwenda kwao”amesema Flora.

Mtulia Apingwa Kila Kona Baada ya Kutangaza Nia ya Kugombea Ubunge Kinondoni

$
0
0
Mtulia Apingwa Kila Kona Baada ya Kutangaza Nia ya Kugombea Ubunge Kinondoni
Uamuzi wa aliyekuwa mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia kuhamia CCM na kutangaza nia ya kutaka kuomba ridhaa ya kuwania tena ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chama tawala umepokewa kwa hisia tofauti huku wengi wakimponda katika mitandao ya kijamii.

Japokuwa wapo waliompongeza kwa hatua hiyo na pia uamuzi wake huobaada ya kueleza nia yake hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, wengi wameonekana kukerwa huku wakisema hataweza kushinda tena.

Desemba 2, Mtulia alijiuzulu ubunge baada ya kubaini kuwa Serikali ya CCM inafanya kazi kubwa ya kutekeleza ilani yake na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo upinzani uliahidi kuyatekeleza.

Kupitia ujumbe wake Facebook, Mtulia aliwapa pole wananchi wa jimbo hilo kwa maumivu waliyoyapata kwa uamuzi wake wa kujiuzulu ubunge.

“Nawahakikishia bado ninawapenda nipo tayari kuwatumikia tena kwa lengo la kuleta maendeleo kwenye jimbo letu. Nichukie fursa hii kutangaza nia kwa wana Kinondoni wote na Watanzania kwa ujumla kuwa nitachukua fomu ya kuomba ridhaa kwenye chama changu cha CCM,” alisema.

“Endapo chama changu kitaridhia, basi nitakuja mbele yenu kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya ubunge wa jimbo letu Kinondoni.” Baada ya andiko hilo, mwananchi aliyejitaja kwa jina moja la Benson katika ukurasa wa Facebook ameandika, “...Naamini unaposoma ujumbe wa watu moyo unakusuta, najua unagombana na nafsi yako ukiwa umekaa peke yako.”

Pia, kupitia ukurasa wa mbunge huyo wa zamani, mmoja wa wafuasi wake, Dulla wa Mzumbe aliandika, “Watu walikuwa wakipigwa ili washinikize utangazwe nafasi ya ubunge, leo umekuwa kibaraka wa CCM huna lolote na ubunge hupati tena maishani mwako.”

Adam Nigangwa alisema, “... Kwanza CCM wenyewe wataanza kukugwaya, sasa hivi wanakuona kama karatasi la kufungia vitumbua.”

Bosco Mfundo amesema, “... Laana ya wana Kinondoni haitakuacha salama.”

Abdallah Kayela ameandika, “Jamani si ndio huyu aliyeapa kupitia kitabu cha Mungu pale kwenye ukumbi wa sokoni Tandale kuwa yeye si CCM na hawezi kuwa CCM mpaka kufa, Braza akili ya kuambiwa changanya na zako hela ulizopata tafuta biashara ufanye.”

Katika maoni yake, John Mazanda alisema Mtulia alichaguliwa kwa gharama kubwa, ikiwa ni pamoja na wananchi kukesha kulinda kura zake zisiibiwe na kwamba ni vyema angehama karibu na Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Deus Mandara amesema, “Yaani umetuona wana Kinondoni ni malofa kiasi hicho! Ulikuwa hujulikani lakini Ukawa walikufanya watu wakujue... Rudi tena uone.”

Mohamed Lamimu ameandika, “...Kama moja ya ahadi ilikuwa kukufanya uwe mgombea tena wamekutapeli. Kama utakuwa mgombea basi labda watumie mabavu ili uwe mbunge.”

Mbali na kumshukia, wafuasi wake hao nao walikuwa wakitupiana vijembe hasa katika ujumbe unaomuunga mkono mbunge huyo wa zamani wa Kinondoni, huku baadhi wakimpongeza kwa hatua yake.

Mwandishi wetu alipopitia ukurasa huo wa Facebook jana saa 11:30 jioni, wananchi waliokuwa wamejitokeza kumjibu walikuwa wamefikia 63 na wote wakimponda isipokuwa watatu.

Waliompongeza ni Kashinde Kalungwana akisema, “Kwa mujibu wa Katiba watu wako yuko huru kwenda watakako na kuishi popote ilimladi havunji Sheria. Kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine ni haki yake ya kikatiba.”

Othuman Sefu alimuunga mkono akiandika kuwa wananchi wa Kinondoni watarajie maendeleo maana Mtulia anakwenda kukaa na wapanga bajeti, “Ukiwa mpishi basi watoto wako hawalali njaa.

Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Bunju Cityfc alisema, “Fikra sahihi huja kwa lugha sahihi. CCM ndiyo lugha sahihi kwa fikra sahihi za maendeleo ya Watanzania.”

Mwimbaji wa Korea Kusini Kim Jong-hyun Kuzikwa Leo

$
0
0
Mwimbaji wa Korea Kusini Kim Jong-hyun Kuzikwa Leo
Mazishi ya mwimbaji mashuhuri wa Korea Kusini Kim Jong-hyun, yanafanyika leo hii mjini Seoul.

Mwanamuziki huyo ambaye pia alikua mtangazaji wa radio, mwandishi wa vitabu na mtunzi wa nyimbo, alikutwa amekufa katika tukio linalotajwa kuwa la kujiua.

Umati mkubwa wa watu umekusanyika kumsindikiza katika safari yake ya mwisho, huku mwili wake ukibebwa na gari aina ya limousine nyeusi kutoka hospitalini alipohifadhiwa kwa takriban siku tatu.

Ibada ya kumuaga kifamilia ilifanyika mapema pia mjini Seoul.

Mwanamuziki huyo aliyekua na miaka 27 akiimbia bendi ya Shinee,alikutwa ameanguka kutoka ghorofa moja refu la kupangisha siku ya Jumatatu.

Catalonia Kufanya Uchaguzi Wake Mkuu Leo

$
0
0
Catalonia Kufanya Uchaguzi Wake Mkuu Leo
Raia wa Catalonia leo hii watachagua viongozi wao wapya, katika uchaguzi ambao serikali kuu ya Uhispania inaamini utamaliza msuguano wa kisiasa unaoendelea.

Serikali kuu ya Madrid iliuvunja utawala uliokuwepo awali, baada ya kuandaa kura ya maoni iliyotajwa kuwa haikufuata kanuni, iliyotaka uhuru wa eneo hilo.


Rais wa Catalonia aliyeondolewa madarakani, Carles Puigdemont, amekuwa akiendeleza kampeni zake za kujitenga na Madrid akiwa uhamishoni chini Ubelgiji kwa kupitia mitandao ya kijamii.

Mwezi Oktoba yalifanyika maandamano makubwa ya Catalonia kutaka kujitenga na Hispania

Mwezi Oktoba yalifanyika maandamano makubwa ya Catalonia kutaka kujitenga na Hispania
Takwimu zinaonyesha kuwa vyama vinavyotaka kujitenga na vile vinavyotaka kusalia kwenye serikali ya Madrid vinalingana katika kura za maoni.

Kuna kila dalili uchaguzi huu ukaibua tena hisia za kutaka kujitenga kuliko kutatua matatizo.

Method Mwanjali Abebeshwa Virago Simba

$
0
0
Method Mwanjali Abebeshwa Virago Simba
Klabu ya soka ya Simba SC imethibitisha kuachana na beki wao kisiki ambaye pia alikuwa kepteni wa timu hiyo kutoka nchini Zimbabwe, Method Mwanjali.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, Zakaria Hanspoppe amethibitisha taarifa hiyo kwa kusema kuwa mchezaji pekee aliyeachwa katika dirisha hili dogo la usajili ni Mwanjali.

“Mchezaji aliyeachwa Simba ni Mwanjali peke yake, hakuna mchezaji mwingine aliyeachwa au aliyeongezwa Simba,” amesema Hanspope.

Wakati huo huo Mwenyekiti huyo wa usajili ameongezas kuwa tayari wamewasilisha barua kwa Lipuli FC kwa ajili ya maombi ya kumsajili mchezaji Asante Kwasi ambaye usajili wake umezua utata na kuteka vichwa vya habari hivi karibuni.

Waziri Mkuu wa Uingereza Amfukuza Kazi Naibu Wake

$
0
0
Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May amefukuza kazi Naibu wake, Damian Green baada ya kugundulika alidanganya kuhusu kwa video za ngono zilizokutwa kwenye komputa yake ya bungeni

Uchunguzi kwenye ofisi ya baraza la mawaziri ulisema alitoa taarifa ambazo sio sahihi na za kupotosha akikataa kuwa alijua kuhusu kugundulika kwa video hizo kwenye uvamizi wa polisi kwenye ofisi za bunge mwaka 2008

Green alilazimishwa kujiuzulu baada ya washauri kwenye masuala ya mawaziri kusema alivunja maadili ya uwaziri

Green alikuwa mshirika mkubwa wa waziri mkuu, na kuondoka kwake kutakuwa ni pigo kubwa kipindi hiki ambacho Uingereza inapitia kwenye majadiliano ya kujitoa Umoja wa Ulaya

Uongozi wa Kiwanda cha Urafiki Kuwabebesha Virago Wapangaji Wake Wenye Madeni Watoa Siku 14

$
0
0
Uongozi wa Kiwanda cha Urafiki Kuwaondoa Wapangaji Wenye Madeni Watoa Siku 14
Uongozi wa Kiwanda cha Urafiki umetangaza kiama kwa wapangaji zaidi ya 160 ukiwataka kulipa kodi la sivyo watawaondoa pasipo kuangalia hadhi ya mtu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 21,2017 naibu meneja wa kiwanda hicho, Shadrack Nsekela amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya wapangaji kushindwa kulipa madeni wanayodaiwa tangu mwaka 2015.

"Hakuna msalie mtume katika hili, tutawatoa wote bila kujali nani ni nani. Tumeanza kuwapa notisi tangu mwaka 2015 lakini hawalipi sasa tunawatoa," amesema Nsekela.

Amesema wapangaji waliopo katika kota za Urafiki jijini Dar es Salaam wanadaiwa kati ya Sh600 milioni na Sh1 bilioni.

Nsekela amesema wameanza kuwatoa wapangaji wa ofisi, huku wale wa makazi wakitakiwa kujiandaa wakati wowote nao watatolewa.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono, Scholastika Kevela amesema baada ya siku 14 watapiga mnada mali walizokamata ili kufidia deni.

Amesema mbali ya ofisi, kuna yadi ya magari ambayo imefungwa na wahusika wakishindwa kulipa mnada utafanyika bila kumwonea haya mtu yoyote.

Breaking News: Mbunge Lijuakali Akamatwa Tena na Polisi

$
0
0
Breaking News: Mbunge Lijuakali Akamatwa Tena na Polisi
Polisi Mkoani Morogoro  wamemkamata mbunge wa kilombero Peter Lijuakali muda mfupi baada ya mahakama mkazi Morogoro kuahirisha kesi inayomkabili

Ondoa Nyama Uzembe na Kupunguza Mwili Kwa Kutumia Virutubisho vya Edmark

$
0
0
NI VIRUTUBISHO AU CHAKULA MBADALA
ZIMEHAKIKIWA NA TFDA
Ni uhakika kwa afya yako,👉 kupunguza uzito na sumu mwilini,mafuta/lehemu mbaya, Kitambi na nyama uzembe na kutibu MAGONJWA Mbali mbali
@looseweight_trainer ni msaada wako text WhatsApp 0713 777 470 upate suluhisho la afya yako KARIBU
@looseweight_trainer

Izzo B , Amwaga Machozi Live Kwenye XXL na Hiki Ndichokilichomliza

$
0
0
Izzo B , Amwaga Machozi Live Kwenye XXL na Hiki Ndichokilichomliza

Tazama Hapa Video:

Alichosema Baba Diamond Baada ya Mama Diamond Kuolewa

$
0
0
Alichosema baba Diamond baada ya mama Diamond Kuolewa Msikilize hapa Baba Diamond Akifunguka Baada ya Kusikia Mama Diamond Kaolewa na Mwanaume Mwingine:

Breaking News: Meya wa Zamani wa Kinondoni Alhaji Londa Atakiwa Kulipa Milioni 18 Leo Ili Asitolewe Vitu Nje na Urafiki

$
0
0
Meya wa Zamani wa  Kinondoni Alhaji  Londa Atakiwa Kulipa Milioni 18 Leo Ili Asitolewe Vitu Nje na Urafiki
Meya wa zamani wa Manispaa ya Kinondoni Alhaji Salum Londa amepewa muda hadi saa tisa alasiri leo awe amelipa kodi ya nyumba anayodaiwa na Kiwanda cha Urafiki kiasi cha Sh. 18 milioni, iwapo atashindwa, vitu vyake vitatolewa nje.

Kutana na Mtabibu wa Nyota Duniani Maalim Fadhil Rashid Kutoka Comoro Kwa sasa Yupo Tanzania

$
0
0
KUTANA NA MTABIBIBU WANYOTA DUNIANIKOTE MAALIM FADHILI RASHIDI KUTOKA COMORO KWA SASA YUPO TANZANIA NI BINGWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUU KUUMA NA KUWAKA MOTO PRESHA KISUKARI VIDONDA VYA TUMBO PUMU

MAALIM FADHILI RASHIDI ANAJUWA UMEHANGAIKA SANA LAKINI HUJAFANIKIWA MUONE HARAKA AKUSAIDIE ANADAWA ZA KI COMRO DAWAZAKE HABAHATISHI MUONE HARAKA AKUSAIDIE TEZI NAUVIMBE TUMBONI ANAUWEZO WAKURUDISHA MTUALIE POTEA KIMAZINGIRA (MSUKURE) KUMFANYA MKE MUME MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA KUMUONA MBAYA WAKO LIVE KWASABABI MALUM ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA MALI BILA YA MASHARITI NAKUMILIKI MALI ZAMAJINI DAWA YAKUONGEZA UUME ZAIZI UIPENDAYO DAWA YA NGUVU ZAKIUME PIA ANAYO DAWA YAKUONGEZA HIPS SHEPU KUWA NAUMBO BOMBA KAMA UMEIBIWA AMA KUDHULUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YA MASAA (24) ANAFUNGA KESI NAKUPATA HAKIYAKO DAWA YA MVUTO WABIASHARA KUUZA MALIYAKO KWAHARAKA KUZUIYA CHUMAULETE KUSAFISHA NYOTA NAKUTOWA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI KARIBUNI WOTE TIBA NIKWADINI ZOTE UTAPATA HUDUMA POPOTE ULIPO DUNIANI

CALLING +255719362806/

WHATSAPP CALLING +255785786436

Lukuvi Amaliza Mgogoro wa Muda Mrefu Vingunguti Ataka Kampuni ya PPM Kurejesha Nyaraka za Wananchi

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameumaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya wakazi wa Mtaa wa Mtambani Vingunguti na mwekezaji kampuni ya PPM.

Waziri Lukuvi amesema Serikali haitambui uwekezaji uliokuwa ufanyike na kwamba, mwekezaji hakufuata utaratibu hivyo kusababisha mgogoro huo.

Eneo hilo la eka 228 lina jumla ya nyumba 4,000 na wakazi 70,000.

"Hatuzuii mtu kuuza mali yake, tunachosimamia haki itendeke na utaratibu ufuatwe lakini katika mchakato huu mambo yamekwenda ndivyo sivyo," amesema Lukuvi leo Alhamisi Desemba 21,2017.

Amesema, "Kuanzia leo nasema haya maeneo ni mali ya wananchi kama anataka kununua aanze upya kufuata utaratibu uliowekwa, haiwezekani mtu anakuja kuwanunua watu 70,000 kienyeji."

Inadaiwa mwekezaji huyo alitaka kununua eneo hilo kwa ajili ya kujenga bandari kavu.

Kwa mujibu wa wananchi wa eneo hilo tangu mwaka 2012 mwekezaji huyo aliwazuia kufanya shughuli zozote za uendelezaji kwa kile alichodai ameshafanya tathmini.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna kinachoendelea na malipo hayajafanyika.

Alipoulizwa kinachoendelea katika uwekezaji huo, meneja mradi wa PPM, Deogratius Chacha amesema wapo katika hatua za mwisho na malipo yangefanyika ndani ya siku 90.

Wakazi wa eneo hilo wamemwambia waziri Lukuvi kuwa mwekezaji amechukua pia leseni zao za makazi na picha.

Kauli hiyo imemfanya waziri Lukuvi kutoa agizo kwa meneja huyo kuwarudishia nyaraka wakazi wote hadi ifikapo kesho saa tano asubuhi.

"OCD chukua vielelezo vya meneja, hakikisha hadi kufikia kesho saa tano awe amewarudishia wananchi nyaraka zao, kinyume cha hapo mkamate mweke ndani," amesema.

Wanaharakati wa Haki za Binadamu Wakosoa Hatua ya Bunge Kuondoa Ukomo wa Umri wa Urais

$
0
0
Wanaharakati wa Haki za Binadamu Wamekosoa Hatua ya Bunge Kuondoa Ukomo wa Umri wa Urais
Wanaharakati wa haki za binadamu wamekosoa hatua ya Bunge kuifanyia marekebisho Katiba ili kumwezesha kiongozi wa nchi hiyo mwenye miaka 73, Yoweri Museveni kurefusha muda wa uongozi.

Wanaharakati wamesema hatua hiyo inarudisha nyuma demokrasia na uamuzi wa wananchi.

Hata hivyo, msemaji wa chama tawala cha NRM, Rogers Mulindwa amekanusha madai kuwa kubadilishwa kipengele cha umri kwenye Katiba kulilenga kumnufaisha Rais Museveni.

Kipengele cha Katiba ya sasa kinaweka ukomo wa umri wa mgombea urais kuwa miaka 75, hali ambayo ingemzuia Museveni kugombea katika uchaguzi ujao wa mwaka 2021 kwa muhula wa sita.

Wabunge 315 walipiga kura kuunga mkono marekebisho hayo, huku 62 wakiyapinga. Wabunge wa chama tawala waliopiga kura ya Hapana walizomewa na wenzao.

Awali, kulizuka mvutano katika jengo la Bunge, wakati baadhi ya wabunge walipokabiliana na watu wa usalama ambao waliwazuia kuingia bungeni ambako kulikuwa kukiendelea mjadala.

Wabunge pia wamerejesha ukomo wa vipindi viwili vya kuwa madarakani kutoka miaka saba hadi miaka mitano, hivyo wabunge wa sasa wataendelea kuongoza hadi mwaka 2023.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya siku tatu za wabunge kujadiliana, huku kukishuhudiwa ulinzi mkali ndani na nje ya Bunge ambapo wakati fulani hata wabunge wenyewe walivutana mashati.

Muswada wa sasa utakuwa sheria baada ya Rais Museveni kuutia saini.

Muswada mpya pia umerejesha ukomo wa mihula ya Rais kuwa madarakani, sheria ambayo iliondolewa ilipofanyiwa marekebisho wakati wa kuingizwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 2005.

Hii inamaanisha kuwa katika uchaguzi ujao Rais Museveni ataweza kuwania urais kwa mihula miwili ambapo akichaguliwa atakaa madarakani mpaka mwaka 2031.

Alichokisema Makamo wa Rais Katika Uzinduzi wa Kuifanya Dododma Iwe ya Kijani

$
0
0
Alichokisema Makamo wa Rais Katika Uzinduzi wa Kuifanya Dododma Iwe ya Kijani
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu leo amezungumza mambo mengi katika uzinduzi wa programu ya kuifanya Dodoma iwe ya kijani.



Haya ni baadhi ya mambo 9 aliyoyazungumza mjini Dodoma;

-Tupunguze ukataji miti na uvunaji wa miti uzingatie sheria zilizopo.

-Taasisi za serikali zitunge sheria ndogo za kusimamia shughuli za mazingira.

-Wananchi tuitikie na kutekeleza programu mbalimbali zinazoanzishwa kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.

-Hii ni awamu ya kwanza tutaratibu awamu ya pili ya program hii.

-TANROADS iandae utaratibu wa kupanda miti pembezoni mwa barabara.

-Wananchi tuanze kutumia nishati mbadala ili kunusuru mazingira yetu.

-Naagiza kampeni hii isiishie Dodoma Mjini bali ienee katika Wilaya zote za Mkoa huu na hatimaye nchi nzima.

-Upandaji wa miti si kwa ajili ya hifadhi tu bali ni fursa ya kiuchumi pia.

-Kampeni hii ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa kijani ni kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu Dkt. Magufuli wa kuhamishia Makao Makuu hapa Dodoma.

Kristmass Kitaifa Kuadhimishwa Zanzibar

$
0
0
Kristmass Kitaifa KufanyikaKuadhimishwa Zanzibar
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limesema misa ya Krismasi kitaifa itaadhimishwa katika Jimbo Katoliki Zanzibar katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Minara Miwili.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Desemba 21,2017 na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Jamii ya baraza hilo, Bernard James imesema misa hiyo itaongozwa na Askofu wa jimbo hilo, Mhashamu Augustino Shao.

Katika sikukuu hiyo inayoadhimishwa Desemba 25 ya kila mwaka, Wakristo duniani huadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Awali, mratibu wa matukio ya kanisa Tumaini Media, John Leveti amesema Kardinali Polycarp Pengo ataongoza misa ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Maurus, Kurasini jijini Dar es Salaam.

"Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa yeye siku hiyo ya mkesha, Desemba 24 ataongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Joseph," alisema Leveti.

"Siku ya sikukuu Kardinali Pengo atafanya ibada katika Kanisa la Mtakatifu Joseph na Nzigilwa atakuwa St Peters," amesema.

Kajala Azua Balaa Barabarani

$
0
0
Kajala Azua Balaa Barabarani
Muigizaji mwenye ‘taito’ kubwa Bongo, Kajala Masanja amenaswa akipiga misele barabarani na kuzua gumzo la aina yake kutokana na nguo aliyovaa kumbana mwili kiasi cha kuonesha laivu ukubwa wa kalio lake.

Tukio hilo lilishuhudiwa na paparazi wetu mapema wiki hii ambapo mrembo huyo alinaswa akikatiza mitaa ya Bamaga-Mwenge kuelekea Sayansi akiwa ameongozana na bwa’mdogo mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja.

 Watu waliokuwa kwenye magari yao binafsi walionekana kupunguza mwendo na kumfuatilia Kajala kwa karibu huku wale makondakta wakipiga miluzi kutokana na jinsi walivyopagawa na mrembo huyo.

“Oyooo dah hawa watu nilidhani ni mambo ya kwenye TV kumbe ukiwaona laivu pia ni balaa,” alisikika konda mmoja aliyekuwa kituoni Bamaga.

Paparazi wetu alimfuatilia hatua kwa hatua Kajala ambapo baadhi ya wenye magari binafsi walionekana wanataka kusimama kabisa, lakini walionekana kushindwa kufanya hivyo wakimhofia kijana ambaye aliongozana na Kajala.

“Unaweza kukuta huyo mshikaji japo anaonekana mdogomdogo lakini anatoka na Kajala. Hawa mastaa hawashindwi hawa,” alisikika jamaa mmoja aliyekuwa akimkodolea macho Kajala.

Njemba mwingine alisikika akisema kuwa; “Mh! Kajala huyu si yule wa mwanzo. Amebongeka sana. Kwa kweli hili umbo lake kwa sasa hastahili kutembea kwa miguu kama hivi. Huyu ni mtu wa kukaa kwenye gari muda wote.”

Mwanahabari wetu aliendelea kumfuatilia Kajala kwa muda mrefu, lakini baadaye alibaini kuwa yupo mazoezini kwani alikuwa akienda na kurudi na hata alivyomshtukia paparazi wetu akimfotoa picha, hakutaka kuzungumzia lolote.
Chanzo: Global Publishers

Kipimo cha Ukubwa wa Mwanamuziki ni Idadi ya Albamu Alizonazo Sokoni- Soggy Doggy

$
0
0
Kipimo cha Ukubwa wa Mwanamuziki ni Idadi ya Albamu Alizonazo Sokoni- Soggy Doggy
Msanii wa mkongwe muziki Bongo, Soggy Doggy amesema kipimo cha ukubwa wa mwanamuziki ni idadi ya albamu alizonazo sokoni.

Soggy ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kwa sasa wanapaswa kulijua hilo na kutumia fursa ya kimtandao pamoja na idadi ya mashabiki wanaokutana nao katika show ili kuuza albamu.

“Bado kuna umuhimu mkubwa sana, hata duniani tu huwezi ukajiita mwanamuziki mkubwa kama albamu huna, yaani mimi nashangaa naendelea tena kushangaa Diamond alifanya show Mlimani City kiingilio elfu 50 alishindwaje kuwa na albamu ya kuwagawia wale watu waliotoa kiingilio” amesema.

Soggy Doggy ameongeza kuwa moja ya vitu anavyojivunia katika maisha yake ya muziki ni albamu, “mimi navimba nilitoa albamu tano na zilienda sokoni, juzi niliwaambia watu ni Sugu na Lady Jaydee ndio walionivuka,”.

Baba Mzazi wa Diamond Afunguka Kuhusu Zari, Wema na Mobetto

$
0
0
Baba Mzazi wa Diamond Afunguka Kuhusu Zari, Wema na Mobetto
Baba mzazi wa staa kutokea Bongoflevani Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz, Mzee Abdul amezungumza kuhusu kuwahi kukutana na Zari ambaye ni mkwe wake aliyezaa na mtoto wake Diamond ambapo amesema hajawahi kuzungumza na ZARI toka amemsikia,  ila Wema Sepetu na Hamisa Mobetto ameshawahi kuongea nao.

Baba wa Diamond amesema kwamba aliwai kuzungumza na Wema Sepetu kwani alishawai kwenda kumtembelea kipindi alipokuwa na Diamond lakini pia amezungumza na Hamissa kipindi alipoenda  kuhudhuria kwenye 40 ya mjukuu wake kwa Hamissa.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>