Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Gari Laleta Kizaazaa Laacha Njia na Kuvunja Duka na Kujeruhi

$
0
0
Gari Laleta Kizaazaa Laacha Njia na Kuvunja Duka na Kujeruhi
GARI aina ya Toyota Spacio T945 DHD limezua kizaazaa baada ya kuvunja duka la nguo la Jordan Store Collection lililopo Sinza Afrika Sana jijini Dar na kujeruhi wawili.

Mashududa wa ajali hiyo wanaeleza kuwa gari hilo lilikosea njia baada ya kudaiwa kugonga watu wawili  na baadae kuzama ndani ya duka hilo. Dereva wa gari hilo alikamatwa muda mfupi na kupelekwa kituo cha Mabatini, Kijitonyama.

Mmiliki wa duka hilo, akizungumza na Global TV Online amesema kuwa amepata hasara kubwa baada ya vitu vyake kugongwa na gari hilo na amesema anawashukuru polisi kwa kumkamata dereva na kwa sasa wanafanya hesabu kujua jumla ya hasara waliyoipata kutokana na ajali hiyo.

Mwalimu Afikishwa Mahakamani kwa Tuhuma za Kubaka Wanafunzi 9

$
0
0
Mwalimu Afikishwa Mahakamani kwa Tuhuma za  Kubaka Wanafunzi 9
Jeshi la Polisi wilayani Tarime mkoani Mara limemkamata na kumfikisha mahakamani mwalimu wa shule ya msingi Itiryo iliyopo Kata ya Ingwe,Samweli Mariba Daniel (29) kwa tuhuma za kuwabaka watoto 9 wa darasa la kwanza.

Kamishna Msaidizi wa polisi, Henry Mwaibambe amesema kuwa walishirikiana na halmashauri ya Tarime na tulifanikiwa kumkamata huyo mwalimu akijiandaa kutoroka kwenda nje ya nchi.

‘Vitendo hivyo vimefanyika katio ya tarehe 30 hadi tarehe 6 baada ya taarifa kufika kwenye vyombo vya dola mwalimu huyu alikamatwa katika mazingira magumu sana, juhudi kubwa kabisa za jeshi la polisi zilifanyika na kwakushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Tarime na tulifanikiwa kumkamata huyo mwalimu akijiandaa kutoroka kwenda nje ya nchi,’ alisema Kamanda Mwaibambe.

‘Amefikishwa mahakamani jinai 682 upepelezi wa shauri hili umekamilika na kila ushahidi umekamilika tumemfikisha mahahakamani katiki ya watoto hawa 9 watatu aliwadhalilisha kingono.’

Mwanamke Ajifungua Mapacha Wanne Mkoani Morogoro

$
0
0
Mwanamke Ajifungua Mapacha Wanne Mkoani Morogoro
Mwanamke mmoja mkazi wa Mkoa wa Morogoro amejifungua watoto mapacha wanne katika Wodi ya Wazazi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.

Mwanamke huyo aliyefahamika kwa majina ya Asha Mashaka, amepata watoto hao siku ya jana(Ijumaa)

Bi. Asha amejifungua kwa Opareshini na sasa yeye pamoja na Watoto wake hao wanaendela vyema Hospitali hapo.

Mwanajeshi wa Zamani Aliyepanga Shambulio la Krismasi Akamatwa

$
0
0
Mwanajeshi wa Zamani Aliyepanga Shambulio la Krismasi Akamatwa
Maafisa wa ujesusi nchini Marekani wamemkamata mtu anayedaiwa kupanga njama ya kufanya mashambulio siku ya Krismasi katika mojawapo ya eneo maarufu la kuwavutia watalii katika mji wa San Francisco.

Everitt Aaron Jameson, mwenye umri wa miaka 39 ambaye ni afisa wa zamani wa jeshi la majini la Marekani, ameshtakiwa kwa jaribio la kutoa usaidizi kwa shirika la kigeni linalohusishwa na visa vya ugaidi.

Bwana Jameson alifichua mpango wake kwa ajenti wa kisiri wa shirika la kijesusi la Marekani, FBI ambaye alimdhania kuwa ni mmoja wa viongozi wakuu wa kundi la Islamic State.

Anadai kumwambia ajenti huyo kwama siku ya Krismasi ni siku nzuri sana ya kutekeleza shambulizi na kwamba hakuna haja ya kutafuta kufanya mpango wa kutoweka baada ya shambulio hilo kwa sababu yuko tayari kufa.

Baada ya Kuchezea Kichapo Simba Yampokea Asante Kwasi

$
0
0
Baada ya Kuchezea Kichapo Simba Yampokea Asante Kwasi
Klabu ya soka ya Lipuli FC imetoa taarifa kuwa tayari imepokea ofa ya shilingi milioni 25 kutoka Simba kwaajili ya kumsajili beki Asante Kwasi raia wa Ghana.


Taarifa iliyotolewa leo na idara ya habari ya Lipuli FC imeeleza kuwa tayari Simba imekamilisha taratibu zote za usajili zinazohitajika na hivyo kuanzia sasa Asante Kwasi anaweza kutangazwa kuwa mchezaji halali wa Simba SC.

Tayari uongozi wa Lipuli FC umeliandikia barua shirikisho la soka nchini TFF, kuthibitisha kufikia makubaliano ya kumwachia mlinzi huyo mwenye mabao matano, akakitumikie kikosi cha vinara wa ligi Simba SC.



Simba ambayo jana jioni imeondolewa kwenye michuano ya kombe la shirikisho imekuwa ikihaha kupata saini ya Kwasi ili kuziba nafasi ya Method Mwanjali ambaye ameachwa.

Dirisha dogo la usajili linafungwa leo saa sita usiku baada ya kuwa wazi kwa takribani mwezi mmoja na nusu. Awali lilifunguliwa Novemba 15 na kufungwa Disemba 15 kabla ya kuongezwa muda hadi leo kutokana na mtambo wa usajili wa FIFA kupata hitilafu.


Utata Waibuka Uraia wa Mchungaji Zakaria Yona

$
0
0
Utata Waibuka Uraia wa Mchungaji Zakaria Yona
Mvutano umeibuka kati ya Jeshi la Uhamiaji mkoani Kilimanjaro na mchungaji wa kanisa la ‘Yesu Anaweza Centre’ Zakaria Yona pamoja na familia yake, kuhusu utata wa uraia wao.

Jeshi hilo lilimchukua mchungaji huyo na familia yake ya watu watano na kuwakabidhi Holili upande wa Kenya, lakini Serikali ya Kenya ikakataa kuwapokea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, mchungaji huyo alisema licha ya Mahakama kutoa zuio la muda kwa jeshi hilo na mwanasheria mkuu wa Serikali, bado jeshi hilo linaendelea kuwabugudhi.

Mkuu wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro, naibu kamishina wa uhamiaji (DCI), Albert Mwelamila alisema asingependa kuzungumzia malalamiko ya mchungaji huyo kwa vile ameshakwenda kortini.

“Ushahidi tuliokusanya unaonyesha si raia wa Tanzania na wamezaliwa Kenya sasa kwa sababu kuna zuio la Mahakama tunaheshimu hilo lakini tuna uhakika kuwa si raia wa Tanzania,” alisema Mwelamila.

Zuio la muda lililotokana na maombi namba 46/2017, lilitolewa Desemba 18 mwaka huu na Jaji Aishiel Sumari, ambaye aliwazuia wadaiwa kuwakamata wadai hadi shauri la msingi litakaposikilizwa.

Kwa mujibu wa amri hiyo, Jeshi la Uhamiaji na Mwanasheria mkuu wa Serikali, wamezuiwa kuwakamata mchungaji huyo na familia yake, ambayo ni pamoja na mkewe, Redempter Francis.

Hata hivyo, mchungaji huyo alidai kwamba siku moja baada ya kutolewa kwa zuio hilo, maofisa hao walikwenda nyumbani kwake eneo la Majengo kwa nia ya kuwakamata.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi?

(Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

Wasiliana nasi +255 622588038au 0679119679 au +255 764318107

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Baada ya Kufungwa Jana Timu ya Simba Yasikia Kilio cha Mashabiki na Wanachama Wake Je Omog Kutimuliwa?

$
0
0
Baada ya Kutolewa Jana Timu ya Simba Yasikia Maoni ya Mashabiki na Wanachama Wake Je Omog Kutimuliwa?
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kusema kuwa klabu ya Simba imesikia maoni ya mashabiki na wanachama wa klabu hiyo na kudai kuwa muda si mrefu watasikia matokeo.


Haji Manara amesema hayo ikiwa imepita siku moja toka klabu ya Simba iondolewe kwa mikwaju ya penati kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) na timu ya Green Warriors, kitendo ambacho kimeonyesha kuwakera na kuwaumiza sana mashabiki wa Simba na wanachama wake ambapo wengi wao walitupa lawama kwa kocha Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, raia wa Cameroon.

Baada ya Matukio ya Ubakaji na Kunajisi Kuongezeka Viongozi wa Dini, Wanaharakati Walaani

$
0
0
Baada ya Matukio ya Ubakaji na Kunajisi Kuongezeka Viongozi wa Dini, Wanaharakati Walaani
 Kuongezeka kwa matukio ya ubakaji na kunajisi mwaka 2017, yamewaibua viongozi wa dini na wanaharakati, wakisema jamii inachangia kwa sehemu kubwa huku wakitaka sheria na adhabu kali zitolewe kwa wahusika watakaobainika kutenda makosa hayo.

Taarifa ya usalama wa nchi ya Jeshi la Polisi iliyotolewa Desemba 20 na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz inaonyesha kuwa matukio hayo yameongezeka kutoka 6,985 mwaka jana hadi 7,460 mwaka huu.

Alisema makosa dhidi ya binadamu, yanayojumuisha mauaji, kubaka, kulawati, wizi wa watoto, kutupa watoto, kunajisi pamoja na usafirishaji wa binadamu, yameongezeka kutoka 11,513 mwaka jana hadi 11,620 mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la makosa 107.

Hata hivyo, DCI Boaz alibainisha kuwa makosa makubwa ya jinai yamepungua kutoka 68,204 mwaka jana hadi 61,794 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka huu.

Alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu takwimu za matukio, Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki Bukoba mkoani Kagera, Methodius Kilaini alisema inasikitisha kuona bado kuna watu wanaendelea na vitendo vya ubakaji na kunajisi licha ya kuwepo adhabu kali.

“Sisi viongozi wa dini, kisiasa na jamii tunapaswa kukemea vitendo hivi ambavyo mara nyingi vinafanywa na watu wa karibu. Lakini kunaporipotiwa watu kutenda makosa haya adhabu kali zichukuliwe kwa haraka ili iwe funzo,” alisema Askofu Kilaini na kuongeza, “Mtoto ni malaika, unapoona mtu kamnajisi halafu unamfumbia macho kisa ni ndugu yako na mnakaa ndani ili kumaliza suala hili pembeni ni hatari, mtu anapomnajisi mtoto huyo ni shetani, hivyo jamii tukemee matendo haya kwa nguvu zote.”

Askofu Kilaini aliungwa mkono na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akisema, “Ni jambo la kusikitisha. Elimu kwa jamii juu ya madhara haya ni ndogo, adhabu ni ndogo ila kubwa ni mmomonyoko wa maadili.”

“Mavazi ya baadhi ya watoto wa kike nayo yanachangia, uhuru wa watoto kuachwa wanacheza na wavulana hadi kufikia kumbaka, hivyo sheria iwe kali kwa atakayebainika lakini somo la maadili liongezwe nguvu kwani hadi mtu anafanya hayo anakuwa hana hofu ya Mungu.”

Katika taarifa yake, DCI Boaz anasema makosa dhidi ya maadili ya jamii nayo yalipungua kutoka 20,000 mwaka jana hadi kufikia 18,971 mwaka huu ikiwa ni sawa na pungufu ya makosa 1,029.

Akichambua taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Eda Sanga alisema ongezeko hilo limechangiwa na elimu inayotolewa ambayo imesaidia waathirika kutoa taarifa huku akiomba ushirikiano wa pamoja kumaliza tatizo hilo.

“Zamani watu walikuwa hawatoi taarifa, wakikutwa na tatizo wanakaa kimya lakini unapomuelimisha mtu anaelewa na anatoa taarifa lakini pia ukiielimisha jamii kuhusu madhara haya, inasaidia kupunguza tatizo,” alisema Sanga.

Sanga alisema kama kasi hiyo ya matukio ikiendelea hivyo mwaka 2018, siku za usoni kutakuwa na Taifa lisilokuwa na maadili hivyo viongozi wa dini, Serikali na jamii wanapaswa kukemea hili kwa nguvu zote na vitendo vyao vionekane kupinga hili.

Katibu mkuu mstaafu wa Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo Tanzania (CCT), Leonard Mtaita alisema “Na mimi nimesikia lakini nanichoweza kusema ni siku za mwisho zimekaribia. Watu watatenda maovu na tutayaona mengi, kikubwa wamrudie Mungu na kuacha maovu.”

Watu 22 Wahofiwa Kufa Maji Ziwa Tanganyika

$
0
0
Watu 22 Wahofiwa Kufa Maji Ziwa Tanganyika
Ikiwa ni saa 40 tangu ajali ya basi na Hiace kugongana na kuua watu saba, ajali nyingine imetokea katika Ziwa Tanganyika na watu 22 wanahofiwa kufa.

Katika ajali hiyo ziwani, watu wengine 115 wameokolewa wakiwa hai baada ya boti kugonga mtumbwi jana alfajiri.

Imeelezwa kuwa miili ya watu wanne imeopolewa na imetambuliwa na ndugu zao.

Ofisa wa Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) Mkoa wa Kigoma, Amaniel Sekulu alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea katika kitongoji cha Lubengela kijijini Msihezi, Kata ya Sunuka wilayani Uvinza.

Alisema mtumbwi uitwao Mv Pasaka uligongwa ubavuni na boti ya Atakalo Mola na kupasuka, hivyo kuzama ziwani.

Sekulu alisema mtumbwi huo ulikuwa umebeba abiria 137 waliokuwa wanakwenda kwenye mkutano wa injili katika Kijiji cha Sunuka na boti iliyokuwa ikitokea Kigoma kwenda Kalya ikiwa na abiria 65.

Sekulu alisema boti na mitumbwi inayobeba abiria hairuhusiwi kufanya safari usiku.

Akizungumzia ajali hiyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Sweetbert Njewike alisema wanaendelea kuwatafuta watu ambao hawajaonekana waliokuwa wakisafiri na vyombo hivyo.

Alisema shughuli za uokoaji zinafanywa kwa pamoja na vikosi vya Polisi, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba kulikuwa na dosari zilizosababisha ajali hiyo.

Alizitaja dosari hizo kuwa ni ukosefu wa vifaa vya uokoaji, vya kuzima moto na boti kufanya safari usiku.

Diwani wa Sunuka, Athumani Chuma alisema ajali hiyo imeacha simanzi kutokana na mazingira iliyotokea.

Alisema licha ya ajali kutokea saa tisa usiku, wanakijiji walionyesha mshikamano katika kuokoa watu wakiwa hai na hatimaye kuopoa maiti nne.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Msihezi, George Gasper alisema ajali ilitokea umbali wa mita takriban 150 kutoka ufukweni, ikiwa ni muda mfupi baada ya boti la Atakalo Mola kushusha na kupakia abiria katika Kitongoji cha Lubengela.

Desemba 20, watu saba walikufa papohapo na wengine 12 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Saratoga kugongana uso kwa uso na gari ndogo la abiria.

Ajali hiyo ilitokea saa 4:30 asubuhi katika Kijiji cha Kabeba katani Mwakizega wilaya hiyohiyo ya Uvinza.

Ndugai Apinga Mpango wa Serikali

$
0
0
 Ndugai Apinga Mpango wa Serikali
Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mpango wa Serikali wa kuwapangia vituo vya kazi moja kwa moja walimu wanaoajiriwa, akihoji ni kwa nini inapoka madaraka ya halmashauri.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Desemba 23,2017 ikiwa ni siku moja baada Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo kutangaza majina ya walimu 3,033 waliopangiwa vituo vya kazi.

Katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Dodoma leo, Spika Ndugai amehoji Tamisemi ni nani hata aweze kujua ikama ya walimu shuleni. Amesema wamekuwa wakijaza walimu maeneo yasiyo na mahitaji.

"Hili jambo linakera, yaani kila mahali sasa ni Tamisemi hadi napata shaka sasa, hivi hii zana ya D by D (ugatuaji wa madaraka) ina maana haijatafsiriwa vyema au ndiyo kupoka madaraka kwa wengine," alihoji Ndugai.

Spika ametoa mfano wa Shule ya Banyibanyi wilayani Kongwa ambayo amesema ina wanafunzi wanaoingia kidato cha tatu lakini hawajawahi kusoma masomo ya sayansi hata siku moja.

"Lakini juzi hapa mmepanga walimu na nilipita tena hapo hakuna hata mwalimu. Hawajasoma hesabu, fizikia, baiolojia, kemia na jiografia; nauliza tena wanasema Tamisemi, hivi hao walisoma wapi na ninyi mmesoma shule zipi," alihoji.

Ndugai amewatupia mzigo wabunge wa Mkoa wa Dodoma amesema wanatakiwa kuupinga mpango huo bungeni wakati yeye akiongoza vikao vya Bunge.

Pia, amepinga mpango wa utoaji fedha kwa vikundi amesema umepitwa na wakati kwa kuwa zinaliwa bure.

Amesema hakuna umuhimu wa kusema watu waunde vikundi ndipo wapewe fedha au uwezeshwaji, badala yake waangaliwe mtu mmoja mmoja ambao wanakuwa na uwezo wa kuzalisha na kisha wafuatiliwe.

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe kwa nyakati tofauti waliunga mkono hoja ya kutopeleka fedha kwa vikundi.

Lusinde amesema kumekuwa na utitiri wa vikundi baada ya kusikia kuna fedha wakati uwezo wa uzalishaji haupo.

"Namuunga mkono Spika katika hili, tunaunganisha watu hata wasiokuwa na mbinu za uzalishaji, naomba tuachane na vikundi havina tija kwa kuwa wanagawana fedha tu," amesema Lusinde.

Profesa Mwamfupe amesema Serikali inagawa vibaya rasilimali fedha kwa kauli ya kasungura kadogo tugawane lakini zinaishia kutoleta tija.

Akijibu hoja hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewaagiza wakurugenzi wa wilaya kuangalia ikama ya walimu na kuwatawanya mara moja.

Kuhusu fedha za vikundi kwa vijana na akina mama amesema jambo hilo liko kisheria. Amesema hakuna ubaya kuwasaidia watu mmoja mmoja ambao wanajiweza katika uzalishaji.

Huyu Hapa Mwanamke Tajiri Zaidi Duniani kwa Sasa, Aliyechukua Mikoba ya Liliane Bettencourt

$
0
0
Huyu Hapa Mwanamke Tajiri Zaidi Duniani kwa Sasa, Aliyechukua Mikoba ya Liliane Bettencourt
Baada ya Mfaransa Liliane Bettencourt, 94, kufariki mwezi uliopita, ambaye alikuwa mmiliki wa maduka ya bidhaa za urembo L’Oreal, ambaye ndiye aliyekuwa mwanamke tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni 39.5, sawa na takriban Tshs trilioni 94, mikoba yake imepata mrithi.

Mikoba hiyo imechukuliwa na Alice Walton, ambaye ana mali ya jumla ya Dola za Marekani bilioni 33.8. Kwa jumla, alishikilia nambari 17 katika orodha ya mabilionea wa Forbes waliotangazwa mapema mwaka huu.

Hadi kufikia mwezi November mwaka huu Alice Walton ametajwa kuwa na utajiri wa Dola bilioni 45.9 sawa na Tsh za Tanzania trilioni 108.

Watson ambaye ni binti pekee wa mwanzilishi wa maduka ya Wal-Mart Sam Walton, ndiye mwanamke tajiri zaidi Marekani na utajiri wake unatokana na hisa zake katika Wal-Mart pamoja na malipo ya mgawo wa faida.

Baada ya Malezi Linah Kuachia Ngoma na Recho Kizunguzungu

$
0
0
Baada ya Malezi Linah Kuachia Ngoma na Recho Kizunguzungu
Msanii wa muziki Bongo Linah amefunguka ujio wake mpya baada ya kujifungua.

Muimbaji huyo amesema baada ya mtoto wake kufikisha miezi mitano anaona ni wakati mzuri wa kurejea katika game.

“Mtegemee wimbo mpya mwezi huu wa 12 mwishoni nimefanya collaboration na Recho wa Kizunguzungu, nafikiri wiki ijayo tutaachia” Linah ameiambia Bongo5.

Kufanya kwa kolabo hiyo itakuwa ni mara ya pili kwa Linah na Recho kukutana katika ngoma moja baada ya kushirikishwa na kundi la Makomando katika ngoma yao inayokwenda kwa jina la Chap Chap.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

$
0
0

HARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

Basi Lililokua na Abiria 50 Limeanguka Katika Daraja Moja na Kuwaua Takriban Watu 32

$
0
0

INDIA: Basi lililokua na abiria 50 limeanguka katika daraja moja na kuwaua takriban watu 32

Gari hilo ambalo lilikuwa likiendeshwa na kijana wa miaka 16 lilipoteza uelekeo kabla ya kutumbukia katika mto Banas

Lilikuwa likiwabeba abiria kutoka eneo la Rajasthan kuelekea Ramdevji katika wilaya ya Sawai Madhopur
-
Basi hilo baadaye lilivutwa nje ya mto huo.

Rais Ali Mohammed Shein Akunwa na Zanzibar Heroes..Awapa Zawadi Kem Kem

$
0
0

Rais Ali Mohammed Shein amewapa zawadi ya Shilingi milioni tatu na kiwanja kimoja kwa kila mchezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes aliyeshiriki mashindano ya CECAFA yaliyomalizika nchini Kenya na Zanzibar kushika nafasi ya pili.


Rais huyo ametoa wito kwa Wazanzibari kuipenda timu yao kwani hakuna atakayeipenda kama wao hawaipendi na kutolea mfano wanaitwa urojo ila hawawezi kuendelea kuitwa urojo tena.

Rais Shein pia amewataka Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kuacha kupeleka masuala ya mpira mahakamani kwani ni kinyume na kanuni za FIFA na inaitia aibu Zanzibar.

Hadi Sasa Jumla ya Miili 13 imepatikana Katika Ziwa Tanganyika Baada ya Boti Mbili Kugongana

$
0
0

KIGOMA: Hadi sasa jumla ya miili 13 imepatikana katika Ziwa Tanganyika baada ya boti mbili kugongana eneo la Rubengera wilayani Uvinza hapo juzi na watu 22 kuhofiwa kufariki.

Miongoni mwa waliokuwa katika boti hizo, ni waumini wa Makanisa ya PEFA waliokuwa wakielekea kwenye mkutano wa injili eneo la Sunuka.
-

Afisa mfawidhi wa SUMATRA mkoani Kigoma amesema kupatikana kwa miili hiyo ni baada ya kuwatumia waokoaji wa majini na zoezi la kutafuta miili zaidi linaendelea.

Wolper: Sijawahi Kutambulisha Mwanaume Kwetu, Tunafanya Mapenzi Kujifurahisha tu

$
0
0
Staa wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema hajawahi kumpeleka mwanaume yeyote nyumbani kwao kumtambulisha licha ya kuwa kwenye na mahusiano na wanaume tofauti kwa nyakati tofauti tangu kuwa staa.

Wolper ameanika hayo wakati akifanya interview na Global TV Online usiku wa kuamkia leo katika shoo yake ya House of Stylish iliyofanyika katika Ukumbi wa High Spirit Lounge, jijini Dar es Salaam.

Diva huyo wa filamu ambaye amewahi kukiri mwenyewe kubanjuka na mastaa wakiwemo wa Bongo Fleva alisema mastaa wengi wanafanya mapenzi kujifurahisha tu wala si kwa ajili ya kutengeneza familia ama ndoa.

“Kwa kuwa nafanya vitu vya kijamii naepukana na baadhi ya mambo, mahusiano ya mnayoyaona kwenye mitandao ni kujifurahisha tu, ndo maana najiachia, lakini mama yangu angeuwa anatumia mitandao nisingejaribu kufanya hivyo, lazima niwaheshimu wazazi wangu.

“Sijaolewa na hamna aliyepeleka mahali nyumbani kwetu, kwa nini nimtambulshe mwanaume? Siwezi!” alisema Wolper.

Kutana na Mtabibu wa Nyota Duniani Maalim Fadhil Rashid Kutoka Comoro Kwa sasa Yupo Tanzania

$
0
0
KUTANA NA MTABIBIBU WANYOTA DUNIANIKOTE MAALIM FADHILI RASHIDI KUTOKA COMORO KWA SASA YUPO TANZANIA NI BINGWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUU KUUMA NA KUWAKA MOTO PRESHA KISUKARI VIDONDA VYA TUMBO PUMU

MAALIM FADHILI RASHIDI ANAJUWA UMEHANGAIKA SANA LAKINI HUJAFANIKIWA MUONE HARAKA AKUSAIDIE ANADAWA ZA KI COMRO DAWAZAKE HABAHATISHI MUONE HARAKA AKUSAIDIE TEZI NAUVIMBE TUMBONI ANAUWEZO WAKURUDISHA MTUALIE POTEA KIMAZINGIRA (MSUKURE) KUMFANYA MKE MUME MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA KUMUONA MBAYA WAKO LIVE KWASABABI MALUM ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA MALI BILA YA MASHARITI NAKUMILIKI MALI ZAMAJINI DAWA YAKUONGEZA UUME ZAIZI UIPENDAYO DAWA YA NGUVU ZAKIUME PIA ANAYO DAWA YAKUONGEZA HIPS SHEPU KUWA NAUMBO BOMBA KAMA UMEIBIWA AMA KUDHULUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YA MASAA (24) ANAFUNGA KESI NAKUPATA HAKIYAKO DAWA YA MVUTO WABIASHARA KUUZA MALIYAKO KWAHARAKA KUZUIYA CHUMAULETE KUSAFISHA NYOTA NAKUTOWA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI KARIBUNI WOTE TIBA NIKWADINI ZOTE UTAPATA HUDUMA POPOTE ULIPO DUNIANI

CALLING +255719362806/

WHATSAPP CALLING +255785786436

Kanisa Anglikana lapata mrithi wa Askofu Mokiwa

$
0
0
Mchungaji Jackson Sosthenes amechaguliwa kuwa askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam kwa kura 110 kati ya 185 zilizopigwa na wajumbe wa sinodi wa kanisa hilo.

Mchungaji Sosthenes amemshinda Mchungani Patrick Bendera aliyepata kura 74, huku moja ikiharibika.

Uchaguzi huo umefanyika leo Jumamosi Desemba 23,2017 katika Kanisa Kuu la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam la Mtakatifu Albano lililopo Posta wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.

Ofisa habari wa dayosisi hiyo, Yohana Sanga amesema uchaguzi umelenga kumpata askofu wa tano wa Dayosisi ya Dar es Salaam anayechukua nafasi ya Dk Valentino Mokiwa.

Amesema walioshiriki uchaguzi huo ni wajumbe wa sinodi ambao ni mapadri, mashemasi, walei, wajumbe wa vikao vya sinodi na wa idara katika dayosisi.

"Baada ya Dk Mokiwa kuamriwa kujiuzulu nafasi hii ilishikiliwa na kasisi mkuu, Jerome Napera ambaye leo amemkabidhi Canon Sosthenes,” amesema.
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images