Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Lukuvi Atoa Onyo kwa Vishoka wa Ardhi

$
0
0
Serikali imekemea baadhi ya wawekezaji wanaotumia vibaya jina la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuwatoa wananchi katika maeneo yao kwa kisingizio cha kupewa kibali na wizara hiyo wakati sio kweli.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Ardhi William Lukuvi ambapo amewaonya baadhi ya wawekezaji ambao wameonekana kushirikiana na baadhi ya watumishi wa serikali katika kunyang'anya haki za wananchi kitendo ambacho amesema kwa utawala wa serikali hii ya awamu ya tano hakina nafasi.

Ameongeza kwamba, kwa sasa serikali inaendelea na zoezi la kurudisha ardhi ya wananchi mikononi mwao bila ya gharama yeyote na kwa yale maeneo ambayo yatabainika kuwa na ukiukwaji wa umiliki watayarudisha kwa wenyewe ili kuendelezwa.

Mh. Lukuvi amesema zoezi la utambuzi wa umiliki wa maeneo na urasimishaji ni endelevu kwa mikoa yote nchini lengo ni kujua maeneo yanayomilikiwa kihalali na kumaliza migogoro ya ardhi ambayo imeonekana bado ni changamoto kwa maeneo mengi mijini na vijijini.


Kuelekea 2018:Barua Yangu Kwa Rais Wangu Dr John Pombe Magufuli

$
0
0
Mheshimiwa Rais,

Pongezi kwa kumaliza miaka miwili na zaidi madarakani na pongezi za dhati kwa vita dhidi ya rushwa ambayo umepigina nayo toka siku ulipoapishwa na kuonyesha mwelekeo mwema.

Mheshimiwa Rais, tukiwa tunaelekea kufunga mwaka 2018, mimi kama mwananchi na mpiga kura ningependa kuona serikali ikiwaangalia kwa jicho la karibu matajiri wa Tanzania wanaomiliki biashara mbalimbali ambao utajiri wao wameuficha nje ya nchi.

Mheshimiwa Rais, ni lazima kila Mtanzania afahamu, hata kama wengine watafahamu kwa shingo upande kwamba tunaimini nchi yetu na taasisi zake kiasi kwamba tunaweza kuwekeza maisha yetu, mali na fedha zetu hapa nyumbani. Hii ndio njia pekee ya kuipelekea nchi mbele pamoja na jitihada za kupambana na rushwa ambazo zinatekelezwa.

Mheshimiwa Rais, hali ilivyo sasa bado ni tofauti. Wapo baadhi ya raia ambao hawaijali nchi wala hawajali kuhusu mafanikio yake. Raia hawa wanatengeneza mabilioni ya fedha wakiwa Tanzania lakini baada ya hapo wanakwenda kuwekeza katika vitu vikubwa nje ya nchi. Tanzania haipati faida yoyote na hii ni moja ya mambo ambayo yamechangia kudorora kwa kiwango cha maisha ya Mtanzania wa kawaida.

Mheshimiwa Rais, najua unafahamu kuwa wafanyabiashara wengi wakubwa walitajwa katika sakata la Panama wakiwa ni miongoni mwa watu wenye akaunti katika taasisi za kifedha za nje ya nchi ili kuficha utajiri wao, utajiri ambao umepatikana hapa nchini, kwa rasimali zetu, miundombinu yetu, nguvu kazi yetu, na wakati mwingine hata mitaji toka taasisi zetu za fedha au taasisi za nje za fedha kupitia jina la nchi yetu.

Mheshimiwa Rais, ni vigumu sana kuwaamini hawa watu. Wanapambana kwa mbinu yoyote ili kujikusanyia mali kutoka kwa watanzania wanyonge wanaofanyakazi kwa bidii na kutoa faida kidogo sana wanayopata kurejesha kwa jamii.

Mheshimiwa Rais, nakumbuka kupitia gazeti la The Citizen lilivyoripoti jinsi Watanzania wengi walivyokamatwa katika sakata la Panama Papers mwaka 2016. Nimekuwa nikiwaza ni kiasi gani taifa limekuwa likipoteza. Sakata la kuvuja nyaraka la hivi karibuni la Paradise Paper limeibua tena hasira zangu juu ya suala hili.

Mheshimiwa Rais, juma lililopita niliona taarifa iliyoandikwa kwa kina namna Yusuf Manji (mmoja wa Watanzania 45 wanaotumia akaunti za nje kuficha utajiri wao) alivyojikusanyia fedha kutoka TANESCO ndani ya mwaka mmoja kupitia zabuni, zaidi ya shilingi bilioni 100.

Mheshimiwa Rais, najiuliza kuna mtu yeyote amefanya uchunguzi kujua kama hizi fedha zilitumika kwa njia sahihi? Au huduma aliyoitoa kama sehemu ya zabuni ilikidhi vigezo vilivyotakiwa? Kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, hata ndugu zake pia walitajwa katika sakata la Panama.

Mheshimiwa Rais, wala huhitaji intelijensia kubwa kujua baadhi ya mambo, mfano ukipekua kupitia Google utaona ana mali mbalimbali nchini Marekani. Hili, ukiongeza na kwamba alitajwa katika sakata la Panama, linanifanya mimi kuwa na mashaka na malengo ya biashara yake yoyte nchini Tanzania. Huyu ni mtu mmoja tu, wako mamia hapa nchini.

Mheshimiwa Rais, TAKUKURU na TRA wanajukumu la kuhakikisha kama fedha za umma walizopewa watu hawa kufanya kazi za umma zilitumika katika namna inayokubalika, kuanzia huduma iliyokusudiwa, kodi, namna zabuni ilivyopatikana, faida ilivyotumika na kadhalika.



Mheshimiwa Rais, 2018 pia nakuombea uwe mwaka ambao utaacha kuteua watu ambao lazima uwe unarudi tena kuwakumbusha kufanya kazi zao. Najiuliza mara nyingi kwamba umeteua mtu, umempa majukumu lakini bado inabidi urudi tena kumkumbusha cha kufanya na bado yuko pale pale. Mfano hili jambo la video zisizo na maadili, Waziri hatazami TV hadi urudi tena umkumbushe? Mbona ana wasaidizi lukuki na kodi zetu tunawalipa? Mbona anakuchosha na una mengi ya kufanya? Ishu ya Bandari na zile flow meters? Kweli hadi Rais urudi tena bandarini kukagua personally? Hii si fair kwako Mheshimiwa na kwa nchi. If people can’t deliver they need to quit. Tunahitaji muda wako utusaidie mambo mengi. Hawa watu wanakuchosha kwa kila wakati kuwakumbusha ya kufanya.

Mheshimiwa Rais, ningependa kuandika zaidi lakini naomba nikuache na hili kwanza. Nitaandika tena wakati mwingine.



Wako katika ujenzi wa Taifa

Uhuru Wanzagi,

Musoma, Mara, Tanzania

Wakfu wa Nelson Mandela Umekanusha Kuandaa wala Kutoa tuzo za "Nelson Mandela" Zilizoripotiwa Desemba 27.

$
0
0
Wakfu wa Nelson Mandela umebainisha kuwa haukuandaa, kusimamia wala kutoa tuzo za “Nelson Mandela”, ambazo zimeripotiwa katika vyombo mbalimbali ya habari Tanzania, Kenya na Burundi Disemba 27, 2017. Habari hiyo pia haikutajwa na vyombo vya habari nchini Afrika Kusini. Swahili Times on Twitter

Source:Swahili Times Twitter

Ushauri wangu:Vyombo vya habari nchini viwe vinajiridhisha kama habari ina ukweli wasikimbilie kuwa wa kwanza kuripoti,kuna media kubwa tunazoziamini nazo ziliingia ktk mkumbo huo wa kutoa fake news.

Mwanaume Auwa Watoto Wake Wawili na Yeye Kunywa Sumu Ambayo iligoma Kumuua...Akamatwa

$
0
0

KIAMBU, KENYA: Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanaume mmoja aliyewaua Watoto wake wawil 2 na yeye kunywa sumu ambayo haikumuua.

Watoto hao waliouawa mmoja alikuwa na miaka 7 na mwingine miaka 3

Inadaiwa kuwa siku moja kabla ya Sherehe ya Christmas familia hiyo ilisafiri hadi Narumoru ambako Mama wa Watoto hao alibakia huko kwasababu ambazo hazijajulikana.

Ondoa Nyama Uzembe na Kupunguza Mwili Kwa Kutumia Virutubisho vya Edmark

$
0
0
NI VIRUTUBISHO AU CHAKULA MBADALA
ZIMEHAKIKIWA NA TFDA
Ni uhakika kwa afya yako,👉 kupunguza uzito na sumu mwilini,mafuta/lehemu mbaya, Kitambi na nyama uzembe na kutibu MAGONJWA Mbali mbali
@looseweight_trainer ni msaada wako text WhatsApp 0713 777 470 upate suluhisho la afya yako KARIBU
@looseweight_trainer

Jeshi la Polisi linamshikilia Mfanyakazi wa PPF Baada ya Kukutwa Akisafirisha Dawa za Kulevya

$
0
0

KILIMANJARO: Jeshi la Polisi linamshikilia Mfanyakazi wa PPF, Anitha Oswald(32) kwa kukamatwa akisafirisha Dawa za Kulevya(Mirungi).

Mwanamke huyo alikuwa akisafirisha bidhaa hiyo haramu kwa kutumia gari lake dogo.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Siri ya Dr Kimei Kung'oka CRDB.....Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Disemba 29

$
0
0


Siri ya Dr Kimei Kung'oka CRDB.....Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Disemba 29

Taarifa ya Serikali kuhusu viongozi wanaotumia mahubiri yao kuchambua masuala ya kisiasa

$
0
0

Taarifa ya Serikali kuhusu viongozi wanaotumia mahubiri yao kuchambua masuala ya kisiasa

Benki Kuu ya Tanzania (BOT ) yatoa gawio la Tsh. 300 bilioni kwa Serikali

$
0
0

Benki Kuu ya Tanzania (BOT ) yatoa gawio la Tsh. 300 bilioni kwa Serikali

Mkurugenzi Mtendaji CRDB Atangaza Kung'atuka

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei amesema hatoongeza muda wa kuiongoza taasisi hiyo baada ya mkataba wake kukamilika Mei, 2019.

Mkurugenzi huyo atakayekuwa ameiongoza CRDB kwa miaka 21 atakapostaafu, amesema uamuzi huo anaufanya kupisha damu mpya kuendeleza mafanikio ya benki hiyo kubwa nchini.

“Si vizuri kung’ang’ania madaraka. Tunao wakurugenzi tuliowaandaa kwa muda mrefu ambao wanaweza kuendeleza nitakapoishia. Ninapisha damu changa nami nitaendelea kuwa mwanahisa wa kawaida,” amesema Dk Kimei leo Alhamisi Desemba 28,2017.

Kwa utaratibu wa benki hiyo, mchakato wa kumpata mkurugenzi mtendaji huchukua miezi 18 lakini Dk Kimei ameongeza mwezi mmoja na kuifanya 19 ili kuipa bodi ya wakurugenzi nafasi zaidi ya kukamilisha hatua hizo.

Amesema ingawa upo mfumo mzuri wa kurithishana madaraka ndani ya benki hiyo, lakini mwenyekiti na bodi wana uhuru wa kumchagua mtu mwenye sifa za ziada kutoka nje na kushirikiana na familia ya benki kuendeleza mafanikio.

“Katiba yetu inataka Mtanzania ndiye aiongoze CRDB. Ninaiamini timu niliyoshirikiana nayo tangu niingie hapa. Hata benki nyingine zinazotafuta wakurugenzi watendaji, ningezishauri zije CRDB,” amesema.

Ndani ya muda uliobaki kabla mkurugenzi mpya hajakaribishwa, Dk Kimei amesema angependa kuona inapata faida kama ya mwaka 2015 ilipotengeneza Sh187 bilioni ikiongezeka kutoka Sh148 mwaka 2014.

Rais Magufuli awasilisha fomu inayotaja mali na madeni yake

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Desemba, 2017 amewasilisha fomu yake ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Mtaa wa Ohio, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuwasilisha fomu hiyo Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kazi inazofanya na amemtaka Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye atakuwa hajawasilisha tamko lake ifikapo tarehe 31 Desemba, 2017.

“Mhe. Jaji Nsekela ikifika tarehe 31 Desemba, ambayo ni siku ya mwisho kwa Mujibu wa Sheria, weka mstari na usipokee fomu zingine, halafu tuone sheria itafanyaje, nakutakia kazi njema” amesisistiza Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wake Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela amemshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kutekeleza matakwa ya kisheria yanayomlazimu kujaza fomu hizo na amesisitiza kuwa ujazaji wa fomu hizo kwa viongozi wa umma sio ombi.

“Viongozi hawaombwi kujaza fomu hizi, kuna baadhi wanadhani labda kutuletea hilo tamko ni fadhila, hapana, sheria ya nchi inahitaji hivyo na kuna sababu zake za msingi” amesema Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela.

Aidha, Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuwasilisha taarifa ya akaunti yake ya benki sambamba na tamko hilo, na amekiri kuwa ameonesha mfano wa kuigwa na viongozi wengine.

Tamko la viongozi wa umma kuhusu rasilimali na madeni linatolewa kwa mujibu wa kifungu cha 9 na cha 11 cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Desemba, 2017

Kutana na Sharifu Juma Mohamedi Mtabiri Wa Nyota Za Binadamu Duniani

$
0
0
KUTANA NA SHARIFU JUMA MOHAMEDI NIMTABIBU WANYOTA ZA BINANADAM DUNIANIKOTE RUDISHA MAHUSIANO NA MPEZIWAKO NDANI YA MASAA (72) TU SHARIFU JUMA MOHAMED ANATIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUU KUUMA NA KUWAKAMOTO PRESHA KISUKARI VIDONDA VYATUMBO PUMU NA TEZI NA UVIMBETUMBONI

ANAUWEZO WAKURUDISHA MTUALIE A KIMAZINGIRA (MSUKURE) KUMFANYA MUME MKE MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALAMPENZIWAKO UNAVYOTAKA KUMUONA MBAYAWAKO LIV KWASABABU MAALUM ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA YA MASHARITI NA ITAKUONGOZA KATIKA SHUGURI ZAKO NAKUMILIKI PESA ZAMAJINI DAWA YA UZAZI KWAKINAMAMA KUSHIKA UJAUZITO NDANI YASIKU 14 UWELEWA WAMASOMO DARASANI PAMOJA NAKUFAULU MITIHANI DAWA YA NGUVU ZAKIUME NAKUREFUSHA UUME SAIZI UIPENDAYO KAMA UMEIBIWA AMA KUDHULUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YAMASAA(24) ANAFUNGAKESI NAKUPATA HAKIYAKO DAWA YA MVUTO WABIASHARA KUUZA MALI YAKO KWA HARAKA PIA ANAWEKA KINGA KWENYE SHAMBA NYUMBA KIWANJA NA KWENYE VYOMBO VYAUSAFIRI

KUZUIYA CHUMA ULETE KUSAFISHA NYOTA NAKUONDOWA MIKOSI PIA ANA PUNGA MARUHANI ANATOWA MAJINI MACHAFU DAWA YA KUACHAPOMBE NASIGARA UTAPATA HUDUMAHII POPOTE ULIPO DUNIANI


CALL OR WHATSAPP+255713679496 

Serikali Yawaonya Viongozi wa Dini Kupiga Siasa......Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Disemba 29

Wananchi wa Liberia Wamchagua Nyota wa Soka Kwenye Uchaguzi wa Marudio wa Urais Uliofanyika Nchini Humo .

$
0
0

Aliyekuwa nyota wa soka, George Weah, ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa marudio wa urais uliofanyika nchini Liberia.

Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ilisema kwamba Weah alipata asili mia 61.5 ya kura zote zilizopigwa na kupata ushindi kwenye kaunti 14 kati ya 15.

Weah, mwenye umri wa miaka 51, alikuwa anashindana na makamu wa rais Joseph Boakai, kila mmoja akitaka kujaza nafasi ya rais Ellen Johnson Sirleaf, ambaye anaondoka mamlakani baada ya mihula miwili inayoruhusiwa na katiba ya Liberia.

Sirleaf alimshinda Weah kwenye uchaguzi wa mwaka  2005, baada ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi kuibuka kutoka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Tume ya uchaguzi ilisema asilimia 56 ya wapiga kura walijitokeza, ambao ni wachache kuliko waliojitokeza tarehe 10 mwezi Oktoba, wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi huo.

Waangalizi walisema kwamba vituo vya kupigia kura wiki hii vilikuwa na utaratibu mzuri kuliko uchaguzi wa oktoba.

Mgombea mwenza wa Weah, Jewel Howard Taylor, ni mke wa zamani wa aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor, aliyeanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo na ambaye anatumikia kifungo cha miaka 50 nchini Uingereza kwa majukumu yake katika ukatili uliotokea nchini Sierra Leone.

Weah alikuwa mwanasoka mwenye umaarufu mkubwa mnamo miaka ya 90. Alichezea timu kama vile Chelsea, Manchester City na AC milan.

Mwaka Mpya Kuwakuta Mahabusu Malinzi na Wenzake.

$
0
0

Kesi  ya  kutakatisha Dola za Marekani 375,418 inayomkabili aliyekuwa Rais wa shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake, imepigwa kalenda hadi Januari 11, 2018 baada ya upande wa Jamhuri kudai bado haujakamilika.

Hata hivyo,  upande wa utetezi uliiomba  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  Dar es Salaam, kuuamuru upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo.

Kesi hiyo ilitajwa jana na  Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Leonard Swai, alidai kuwa  upelelezi bado haujakamilika, hivyo akaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko, alidai kuwa kesi hiyo ni ya muda mrefu na kila siku wanaambiwa jalada bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Hakimu Mashauri alisema mahakama hiyo inafanya kazi ya kutafsiri sheria na kama itafanya vinginevyo itakuwa nje ya sheria.

Alisema kesi hiyo itatajwa Januari 11, 2018 na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga ambao wanakabiliwa na mashtaka 28, ikiwamo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.

UVCCM:Huu Sio Wakati Wakuabudu Cheo Cha Mtu

$
0
0

Mwenyekiti wa Umoja wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kheir James, amesema wakati wa kufanya kazi kwa woga ndani ya umoja huo umepitwa na wakati.

Akizungumza na wanachama wa CCM na jumuiya zake visiwani Zanzibar, alisema huu ni wakati wa kufanya kazi kwa ushirikiano badala ya kumuabudu mtu kutokana na cheo chake.

Alisema kiongozi anayejitambua ni yule anayefanya kazi kwa maslahi ya vijana wenzake na kilichobaki kwa sasa ni kupambana ili jumuiya hiyo ya vijana iweze kufika mbali kwa maslahi ya vijana na taifa kwa ujumla.

Aidha, alisema wakati wa vijana wanaopenda kulalamika umefika mwisho hivyo ni vyema wakajitahidi kufanya kazi bila ya upendeleo na woga.

Aliwataka viongozi wenzake katika jumuiya hiyo kuanza kuhakiki mali za chama na aliyekuwa haendani na kasi ya chama hicho awapishe wanaoweza.

"Umegombania nafasi na tumekupa, sasa tufanyeni kazi ili vijana wajue thamani ya uongozi," alisema.

Kheir alisema uhakiki wa mali za chama hicho kwa upande wa Zanzibar utafanywa na Wazanzibari wenyewe na atahakikisha anapatiwa ripoti ya uhakika kwenye taarifa watakazozipeleka kwa uongozi wa juu na uhakiki wa watumishi hewa pia utaangaliwa.

Makamo Mwenyekiti wa Umoja huo, Tabia Maulid Mwita, alisema yupo tayari kufanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu na vijana wote na kuwashukuru kwa kumchagua kushika nafasi hiyo na kuendeleza ahadi zake alizoziahidi kipindi cha kampeni.

Aidha, aliwataka vijana kuacha makundi kwa kuwa uchaguzi umekwisha hivyo atahakikisha haki inatendeka bila ya kumuonea mtu wala kujali cheo chake na kufanya maamuzi kwa matakwa yake bila ya kumshauri mtu.

"Vijana ndio jeuri ya chama ila kwa anayejitambua na sio kukaa kutukana katika majukwaa kijana mzuri ni yule anayependa kusikiliza ushauri wa wakubwa wake," alisema.

Mapema akitoa utambulisho kwa viongozi, Kaimu Katibu wa Umoja huo Zanzibar, Abdulghafar Idirissa Juma, alisema Umoja huo utaangalia upya vitega uchumi vyake ili viweze kuleta tija kwa wanachama na kuiendeleza jumuiya yao.

Akizungumzia mradi wa Darajani alisema kuwa ulihodhiwa na baadhi ya viongozi wa serikali hivyo alimtaka Mwenyekiti wa Umoja huo kulifuatilia suala hilo ili mipango iendelee na mradi huo uweze kuleta tija kwa vijana na taifa kwa ujumla.

Hiki Ndicho Walichosema TAKUKURU Mahakamani kuhusu nyaraka walizoomba kutoka kwa Aveva

$
0
0

Upande wa Jamhuri katika kesi ya tuhuma za utakatishaji fedha inayowakabili waliokuwa vigogo wa Klabu ya Simba, Evance Aveva na Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu, umedai mahakamani kwamba bado haujapokea nyaraka kutoka kwa rais huyo.

Madai hayo yalitolewa na Wakili wa Serikali, Leonard Swai, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa, anayesikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa jana  kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi bado haujakamilika na kwamba bado wanasubiri nyaraka kutoka kwa Aveva.

"Mheshimiwa Hakimu, upande wa Jamhuri bado hatujakabidhiwa nyaraka tulizoomba kutoka  ofisi ya Aveva ili wakamilishe upelelezi," alidai Swai.

Hata hivyo, upande wa utetezi alidai kuwa wameipokea barua ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (Takukuru) kuhusu maombi hayo na wanayafanyia kazi.

Hakimu Nongwa alisema kesi hiyo itatajwa  Januari 11, 2018 na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.

Awali, upande wa Jamhuri  uliomba ufunguo kutoka kwa Aveva ili kuwawezesha kupata nyaraka hizo ikiwa ni sehemu ya kukamilisha upelelezi.

Katika kesi ya msingi, Aveva na makamu wake Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha dola za Marekani 300,000.

Washtakiwa hao wanadaiwa kula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa  dola 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.

Papii Kocha na Babu Seya kwenda Congo kwa shughuli ya Kimila

$
0
0
Wasanii wa muziki wa dansi, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ wanatarajia kwenda kwao nchini Congo kwa ajili ya shughuli ya kimila.

Msanii Kikumba Mpango ‘King Kikii’ ambaye ni mtu wa karibu wa wasanii hao amekiambia kituo cha Runinga cha Azam kuwa Babu Seya na Papii Kocha wataenda nyumbani kwa ajili kutembelea kaburi la mama yao mzazi.

“Hawa watu, Nguza na mwanawe inatakiwa kwanza baada ya mapumziko inatakiwa wafunge safari waendee nyumbani (Congo), unajua mama Nguza alikuwepo hapa wakati alikuwa hai alikuwa anamuona mwanaye lakini alikuwa ameshakata tamaa kwa bahati mbaya akaenda nyumbani kufika na yeye akafariki,” amesema.

“Sasa kimila inatakiwa wafike kwanza, wafike mpaka kwenye kaburi ya mama mzazi, kabla ya yeye kufanya kitu chochote halafu baada hapo ndio mambo mengine yatafuata,” ameongeza.

Babu Seya na Papii Kocha walitoka gerezani December 9 mwaka huu walipokuwa wakitumikia kifungo cha maisha mara baada ya kupata msamaha wa Rais Dkt. John Magufuli.

Mbowe asita kuweka bayana mikakati ya Vyama kuhofia uchochezi

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kamatakamata ya viongozi wa upinzani na kufunguliwa kesi za uchochezi ni moja ya kikwazo cha vyama vinavyounda Ukawa kutoweka hadharani mikakati yake ya kufanya siasa mwakani.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mbowe alisema anasita kuweka bayana mikakati ya vyama vya Chadema, CUF, NLD na NCCR-Mageuzi vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa hofu ya kuitwa mchochezi.

Kwa mantiki hiyo ni kama Ukawa itaingia katika aina nyingine ya kufanya siasa baada ya ile iliyozoeleka kuwa ngumu kutokana na misukosuko wanayoipata.

Miongoni mwa viongozi wa upinzani wanaokabiliwa na kesi za uchochezi ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ambaye ana kesi zaidi ya tano. Lissu kwa sasa yuko Nairobi nchini Kenya akitibiwa baada ya kushambuliwa kwa risasi Septemba 7 mjini Dodoma.

Upinzani umekuwa na wakati mgumu tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 baada ya Rais John Magufuli kuzuia mikutano ya hadhara na viongozi wake kukamatwa mara kwa mara wakituhumiwa kwa uchochezi na wengine kufunguliwa kesi.

Mbowe alitoa kauli hiyo juzi baada ya gazeti hili kutaka kujua mwelekeo wa vyama hivyo baada ya kuwa kimya na kususia uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Longido, Singida Kaskazini na Songea Mjini utakaofanyika Januari 13 mwakani.

“Siwezi kutoa silaha zote hadharani maana nikisema watasema Mbowe mchochezi,” alisema kiongozi huyo wa upinzani bungeni.

“Na mtu anayefikiri haya tunayofanyiwa kuwa wanaoumia ni Chadema, anajidanganya. Upinzani makini unajenga Taifa imara.

“Kufanya kazi katika upinzani kwa awamu hii ni mateso. Haturuhusiwi kufanya mikutano ya kisiasa, haturuhusiwi kuendesha mijadala yaani unamfunga mikono nyuma halafu unamwambia njoo upigane.”

Wabunge wengine wanaokabiliwa na makosa ya uchochezi na baadhi kesi zao zimemalizika ni Halima Mdee (Kawe), Peter Lijualikali (Kilombelo), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), Godbless Lema (Arusha Mjini), Susan Kiwanga (Mlimba), Ester Bulaya (Bunda Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Saed Kubenea (Ubungo).

Kwa upande wa viongozi waliohojiwa au kufungulkiwa kesi wakihusishwa na uchochezi ni Dk Vincent Mashinji ambaye ni katibu mkuu wa Chadema, Edward Lowassa (waziri mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema) Patrick ole Sosopi (mwenyekiti wa Baraza la Vijana, Chadema), Salim Mwalimu (naibu katibu mkuu-Zanzibar) na viongozi wa ngazi ya mikoa, wilaya na kata.

Akitoa ufafanuzi kuhusu kosa la uchochezi, wakili wa kujitegemea, Harold Sungusia alisema wanasiasa watakuwa waathirika wakubwa kwa kuwa ni kosa la kisiasa.

“Ili kumaliza tatizo hili la uchochezi ni lazima tukubali uwepo wa mfumo wa vyama vingi vya siasa, lazima tuwe na Katiba Mpya,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu kutoweka wazi mikakati yao na ushiriki wa vyama hivyo katika uchaguzi wa marudio wa ubunge katika majimbo matatu utakaofanyika Januari 13, Mbowe alisema uamuzi huo hauwaumizi Chadema wala wapinzani, bali Taifa.

Vyama hivyo vimesusia uchaguzi vikidai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ifanyie kazi changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43 uliofanyika Novemba 26.

Katika uchaguzi huo uliotokana na baadhi ya madiwani kujiuzulu uanachama na kujivua nyadhifa zao kwa maelezo kuwa wanamuunga mkono Rais Magufuli, upinzani ulishinda kiti kimoja.

“Upinzani hautakufa ila utabadili operesheni. Hatuna sababu za kwenda kushiriki uchaguzi ambao watawala wameonyesha watashinda,” alisema Mbowe.

Alisema ni vigumu kuingia katika uchaguzi wakati tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, vyama vya upinzani vinabanwa na kuzuiwa kufanya siasa.

“CCM inatumia wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na mawaziri pamoja na vyombo vya umma huku sisi tukizuiwa. Wenzetu wanafanya mikutano, wanatumia vyombo vya habari vya umma, wanatumia ma- RC, DC, DED na mawaziri,” alisema.

“Wanasema tuje katika uchaguzi ambao imesikika kiongozi akisema ‘inawezekanaje unamtangaza mpinzani wakati nimekupa gari na nyumba’. Sasa watu wanataka ushahidi gani wa kuonyesha tunakandamizwa.”

Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images