Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Alichokisema Zari Kuhusu Wasafi TV na Redio

$
0
0
Alichokisema Zari Kuhusu Wasafi TV na Redio
Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady amempongeza muimbaji huyo mara baada ya kuweka wazi ujio wa kituo chake cha redio na runinga.

Katika pongezi hizo Zari amemtaja Diamond kama mtu anayejituma zaidi katika kile anachokifanya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari ameandika;

Hongera Damond Patnumz sana kwa juhudi na bidii uliyonayo Allaah akujalie kwa mengine mazuri zaidi. Siku zote umekuwa mpiganaji wa kazi zako, kwa kuwa njia pekee ya kuijenga familia ni kupiga KAZI najua malengo yako Alhamdulillah! #wcbTV #wcbFILMSTUDIO #wcbMUSICSTUDIO #wcbRADIO #wcbHEADQUATERS.

Bila kusahau #DiamondKaranga na chibuperfume #ChibuPerfume 2018 looking good👌🙏

Hapo jana Diamond aliachia video mtandaoni ikionyesha mjengo mpya wa WCB ambao utatumika kama makao makuu ya kampuni hiyo pamoja na studio za Wasafi TV na Wasafi Redio. Pia utakumbuka hii si biashara ya kwanza kwa Diamond kwani ameshaingiza sokoni manukato yake ‘Chibu Perfume’ pamoja na Karanga.

Harmorapa Aongea Hivi Kuhusu Wema Sepetu, Dkt Shika

$
0
0
Harmorapa Aongea Hivi Kuhusu Wema Sepetu, Dkt Shika
Msanii wa muziki Harmorapa amefunguka kuhusu post aliyoweka katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuhusiana na Dk.Shika na mrembo Wema Sepetu.

Akipiga stori na Bongo5, hivi karibuni msanii huyo ameeleza kuwa wakati tukio la Dk.Shika linataokea yeye hakuwepo nchini.

“Kipindi kile wakati inatoke sikuwepo hapa nchini nilikuwa china kwa ajili ya biashara yangu, nikawa nasikia nikawa naona kinachoendelea hapa Tanzania home hapa nyumbani. Lakini kuhusu mimi kuwa baba yangu na kumpost watu wengi wanacheza na akaunti yangu wali hack one time harafu waka-post wakaandika kama walivyo andika lakini mimi sina uhusiano nao harafu sielewe kinachoendela, ukiniuliza leo hivi nashindwa hata kuelewa ,” amesema msanii huyo baada ya post yake katika mtandao wa kijamii wa Instagram kudai kuwa ana mahusiano na tajiri mtata Dk.Shika.

Akaongeza” Watu wana hack tu sometimes kuniharibia yani na wanatumia vibaya mimi mwenyewe naumia na kujiuliza sasa kwa nini nikae kwenye mitandao na kumtukana mtu na ukimtukana mitandao ni vyombo vya habari kila mmoja ataisikia hivi ni kuharibiana inakuwa sio ishu sio poa kiukweli.”

Vile vile msanii huyo akasisitiza kuwa alimtaja Wema Sepetu katika post hiyo kwa sababu ni mrembo, akaongeza “ Anamtaja mrembo huyo kwa sababu anampenda .”

Mzee Akilimali Amtetea Chirwa Baada ya Kukosa Penalti

$
0
0
Mzee Akilimali Amtetea Chirwa Baada ya Kukosa Penalti
MWENYEKITI wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali amemtetea mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa kufuatia kukosa penalti katika mechi ya juzi dhidi ya URA ya Uganda kwenye Kombe la Mapin­duzi.

Yanga iliondolewa katika nusu fainali kwa penalti 5-4 ambapo Chirwa alikosa kwa upande wa Yanga na kusaba­bisha kuwa gumzo kutokana na tukio hilo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Akilimali alisema Chirwa hakufan­ya makosa katika kupiga penalti ya mwisho kwani alidhamiria kufunga na kilichotokea ni bahati mbaya na kudai kuwa, kocha ndiye anayepaswa kulaumiwa kutokana na kumtumia licha ya kutokuwa na ma­zoezi ya pamoja na wenzake.

“Yanga tumetolewa kiume katika michuano ya Mapinduzi kwani hadi tunatoka tumefanikiwa kufanya vyema hadi dakika 90 lakini kili­chotokea hakipaswi kulaumiwa mchezaji.

“Timu ilicheza vizuri ilipamba­na na hatimaye kuweza kufikia hapo tulipofikia na ilikuwa ni lazima timu moja isonge mbele.

“Siwezi kumlaumu Chirwa, kilichotokea ni bahati mbaya kwani, hata wachezaji wa­zuri Ulaya wanakosa penalti sembuse yeye, anayepaswa kulaumiwa ni kocha kwanini amemchezesha mchezaji akiwa hana mazoezi, naona anayarudia yaleyale ya Kocha Hans Pluijm,” alisema Akilimali.

Mnasema nina Ukimwi mmenipima? .......Walionitupia Uchawi Nawaomba Msamaa Ili Nipone- Steve Nyerere

$
0
0
Walionitupia Uchawi Nawaomba Msamaa Ili Nipone- Steve Nyerere
Msanii wa filamu, Steve Nyerere amefunguka na kusema kuwa kutokana na matatizo ambayo anapitia ikiwa pamoja na maradhi yake kuna watu wengi wamekuwa wakisema kuwa ameathirika na virusi vya Ukimwi.


Muigizaji huyo amekiambia kipindi cha Enewz ya EATV kuwa anashangaa kwanini kila mtu anaongea lake kuhusu kuumwa kwake huku wengine wakifika mbali zaidi kwa kudai kwamba ameathirika.

“Watu wananifuatilia kutaka kujua hali yangu kwa sababu mimi ni mtu maarufu, ni jambo jema lakini kama kuna watu wamenitupia vitu vya ajabu naomba wanisamehe, mimi ni binadamu labda kuna namna watu nimewakosea,” alisema Steve. “Lakini nashangaa kuna watu wanadai imeathirika mmenipima, yaani kila mtu anaongea lake,”

Steve amedai kwa sasa anasumbuliwa na mbavu, miguu na tayari ameanza kupatiwa matibabu.

Ndoa Yampoteza Irene Poul Kwenye Tasnia ya Filamu

$
0
0
Ndoa Yampoteza Irene Poul Kwenye Tasnia ya Filamu
MSANII kiwango kunako soko la Bongo Muvi, Irene Paul anadaiwa kupotezwa na ndoa na kwamba kwa sasa haonekani kwenye tasnia hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo, Irene anayesifika kuzitendea haki ‘scene’ zake anazopewa hususan kwenye suala zima la ‘ung’eng’e’, tangu ameolewa amekuwa hasikiki tena kwenye filamu kama ilivyokuwa awali.

“Hii ni ndoa tu itakuwa imempoteza, zamani alikuwa tishio kwenye kila filamu anayotoa iwe ameshirikishwa au amecheza mwenyewe lakini tangu ameolewa amekuwa kimyaa,” kilibonyeza chanzo hicho.

“Ndoa si kwamba inamfanya mtu awe kimya, nipo kimya kwa sababu nina biashara zangu nyingine.”

Salamu za ACT Wazalendo Kwenye Maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar

$
0
0
Salamu za ACT Wazalendo Kwenye Maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Chama cha ACT Wazalendo kinawatakia Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla maadhimisho mema ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Taarifa kutoka kwa Chama hicho imeeleza kuwa maadhimisho haya ya Mapinduzi ya Zanzibar yawe kichocheo cha kuimarisha misingi ya undugu.

SALAMU ZA MAPINDUZI KUTOKA ACT WAZALENDO

Chama cha ACT Wazalendo kinawatakia Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla maadhimisho mema ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Maadhimisho haya ya Mapinduzi ya Zanzibar yawe kichocheo cha kuimarisha misingi ya undugu, umoja na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.

Kwa Wazazibari, Miaka 54 ya Mapinduzi iwe fursa maridhawa ya kufanya tafakari na tathmini ya kina. Ni kipindi cha kujiuliza maswali. Je malengo ya Mapinduzi ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuleta haki na usawa yamefikiwa? Vipi kuhusu ustawi wa Zanzibar? Ni kwa kiwango gani Mapinduzi ya Zanzibar yameleta maendeleo yaliyokusudiwa ya kiuchumi na kijamii kwa Wazanzibari Wote?

Ujumbe wa Chama chetu kwa Wazanzibar ni kuwa ustawi wa Zanzibar unahitaji jitihada za Wazanziabari Wote bila kujali tofauti za kisiasa. Maadhimisho ya 54 ya Mapinduzi yawakumbushe Wazanzibari umuhimu wa maridhiano ya kisiasa na kuimarisha undugu kwa ajili ya ustawi wa Zanzibar.

Juma Said Sanani, Makamo Mwenyekiti, ACT Wazalendo, Zanzibar.

12 Januari 2018

Dawa ya Kuhifadhia Maiti Zatumiwa na Wamiliki wa Bucha Kuhifadhi Nyama Isioze

$
0
0
Dawa ya Kuhifadhia Maiti Zatumiwa na Wamiliki wa Bucha Kuhifadhi Nyama Isioze
Unaambiwa ukistaajabu ya Musa basi utajionea ya Filauni! kumekuwa na taarifa kuwa kuna baadhi ya maeneo nchini Uganda watu wanaomiliki mabucha wamekuwa na desturi ya kutumia dawa ya kuhifadhia maiti kwa kuhifadhia nyama iliyobaki ili isioze.

Sasa ukweli ni serikali nchini humo jana alhamisi januari 11, 2017 imefanya msako mkali kwenye Mabucha mjini Kampala ili kubaini  baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia dawa hatari zikiwemo za kuhifadhia maiti na zile za kuulia wadudu.

Imeelezwa kuwa Wafanyabiashara hao wanadaiwa kutumia kemikali hizo ili kuhifadhi nyama zisiharibike na waweze kuuziuza kwa muda mrefu.

Katika oparesheni hiyo mabucha tisa jijini Kampala yameshafungwa kwa kutumia madawa ya aina hiyo ambapo kama itabainika kwenye upelelezi watapelekwa Mahakamani.

“Ni lazima watunze sehemu zao za kuuzia nyama (Mabucha) kuwa safi na kuacha kutumia madawa yasiyostahiki  la sivyo tutawapeleka mahakamani,“amesema Msemaji wa Mamlaka ya Uangalizi wa Jiji la Kampala (KCCA), Pater Kauju kwenye mahojiano yake na BBC.

Madhara ya kutumia nyama iliyohifadhiwa na madawa ya kuhifadhia mauti ni makubwa ikiwemo kuuwa viungo na seli mbalimbali mwilini.

Dalali Aliyemuuzia Nyumba Diamond Afunguka Kila Kitu Kuhusu Mjengo Huo Mpya

$
0
0
Dalali Aliyemuuzia Nyumba Diamond Afunguka Kila Kitu Kuhusu Mjengo Huo Mpya
Baada ya Diamond kuonesha mjengo wake mpya  dalali aliyefanikisha mjengo huo kupatikana ambapo ametaja gharama za mjengo huo na jinsi ilivyokuwa mpaka Diamond Platnumz akainunua na kusema kuwa kabla ya Diamond kununua nyumba hiyo alimuonesha sample ya nyumba kumi ndipo akaichagua hiyo.

Dalali huyo anayefahamika kwa jina la Skoba maarufu kama Dalali Mwanamke amesema kwamba nyumba hiyo Diamond alinunua kwa gharama za Tsh Billion moja na anategemea kuzindua rasmi radio yake na Tv katika mjengo huo February 2, 2018.

Rais Trump Ayatusi Mataifa ya Afrika Haiti na El Salvador

$
0
0
Rais Trump Ayatusi Mataifa ya Afrika
Rais wa Marekani amewashutumu wahamiaji wanaoingia nchini humo kwa kuwatusi katika afisi yake ndani ya Ikulu ya Whitehouse.

Ikulu ya Whitehouse haikukana tamko hilo ambalo lilithibitishwa na vyombo vyengine vya habari.

''Wanasiasa fulani wa Washington hupendelea kupigania mataifa ya kigeni, lakini rais Trump atawapigania raia wa M arekani pekee,taarifa iliotoka katika msemaji wa Ikulu Raj Sha ilisema.

Iliendelea: Kama mataifa mengine ambayo yana wahamiaji wanaofaa kuwa nchini humo, rais Trump anapigania suluhu ya kudumu inazofanya taifa hilo kuwa thabiti kwa kuwakaribisha wale ambao wana mchango katika jamii ,hukuza uchumi wetu na kuingiliana na raia wa taifa letu.

Kamwe hatakubali mkakati wa muda mfupi ulio hafifu na hatari ambao unahatarisha maisha ya raia wa Marekani, mbali na kutowaruhusu wahamiaji wanaotaka maisha mazuri Marekani ijapokuwa kupitia njia halali.

Waandamanaji wanaopinga chuki ya rais Donald Trump dhidi ya wahamiaji
Image caption
Waandamanaji wanaopinga chuki ya rais Donald Trump dhidi ya wahamiaji
Matamshi hayo ya rais Trump yanajiri huku wabunge kutika vyama vyote wakimtembelea kupendekeza mpango wa wahamaiji usiopendelea upande wowote.

Seneta wa Democrat Richard Durbin alikuwa akizungumza kuhusu vibali vya muda wa kuishi vinavyotolewa kwa raia wanaotoka katika mataifa yaliokumbwa na majanga, vita ama milipuko ya magonjwa, vilisema vyombi vya habari.

Kulingana gazeti la Washington Post , bwana Trump aliwaambia wabunge kwamba Marekani badala yake inachukua wahamiaji kutoka Norway, ambayo waziri wake mkuu alimtembelea rais Trump siku ya Jumatano.


Seneta Lindsey Graham, ambaye ni mwanachama wa chama cha Republian kutoka Carolina Kusini pia alikuwa katika mkutano huo lakini hakuweza kuzungumzia kuhusu matusi hayo yaliotolewa na rais Trum.

Gazeti la The New York Times liliripoti miaka mitatu iliopita kwamba bwana Trump alisema kuwa raia wa Haiti wote wana ''ukimwi'' wakati wa mkutano wa mwezi Juni kuhusu wahamiaji.

Na kufuatia matamshi hayo rais Trump hakusazwa katika mitandao ya kijamii.

Elijah Cummings, mbunge wa Democrat katika eneo la Maryland alichapisha ujumbe katika mtandao wa twitter akisema: Nayashutumu matamshi hayo yasiosameheka na yanayoshusha hadhi ya afisi ya rais.

Mbunge mwengine mweusi kutoka chama cha Democrat. Cedric Richmond, alisema matamshi ya bwana Trump ni dhihirisho tosha kwamba sera yake ya kuliimarisha taifa la Marekani ni sawa na kulifanya taifa la Marekani kuwa la watu weupe pekee.

Mia Love, raia wa chama cha Republican katika eneo la Utah ambaye pia ni mbunge wa pekee mwenye mizizi ya Haiti nchini Marekani amemtaka rais Trump kuomba msamaha kwa maneno hayo yalio na chuki na yenye kugawanya watu.

Muungano unaopigania haki za watu weusi NAACP ulimshutumu rais Trump kwa kuzidi kuegemea katika ubaguzi wa rangi.

Lakini Ikulu ya Whitehouse imepuuzilia mbalia shutuma hizo zinazomkabili rais.

Afisa mmoja wa Trump alinukuliwa na chombo cha habari cha CNN akisema: Ijapokuwa hili litawakasirisha watu wa Washington, wafanyikazi wanadhani kwamba matamshi hayo yanatokana na mizizi yake, sawa na matamshi yake dhidi ya wachezaji wa NFL waliopiga goti wakati wa kuimbwa kwa wimbo wa taifa.

Msemaji wa ubalozi wa El Salvador mjini Washington alikataa kuzungumzia kuhusu matamshi hayo.

Pampu za Kukama Maziwa na Kuyahifadhi Mwanamke Akiwa Safarini

$
0
0
Pampu za Kukama Maziwa na Kuyahifadhi Mwanamke Akiwa Safarini
Kampuni mbili zimetengeneza pampu ambazo zitawasaidia wanawake wanaonyonyesha kukama maziwa na kuyahifadhi wakati wakiwa safarini.

Wanawake wanaotumia pampu kawaida hukama maziwa mara kwa mara kwa siku na kati ya muda wa dakika 20.
Kampuni za Willow na Freemie Libert zimetangenezwa kwa njia ambazo zitakuwa rahisi kuvaliwa.

Mwathiriwa wa moto anayenyonyesha kuwatia moyo wengine
Willow ilishinda tuzo kutokana na kifaa hicho kwenye maonyesho ya CES mwaka 2017, kwa sababu pampu hiyo imekuwepo kwa majaribio lakini sasa inaingia rasmi sokoni kwa dola 479.

Hata hivyo imekosolewa mitandaoni kutoka kwa wale wameijaribu wengine wakesema kuwa mifuko hiyo ya maziwa ni midogo mno.


Mtandao wa Facebook Kufanya Mabadiliko Makubwa

$
0
0
Mtandao wa Facebook Kufanya Mabadiliko Makubwa
Mtandao wa kijamii wa Facebook umetangaza kufanya kile inachokiita kuwa ni mabadiliko muhimu ambayo itafawafanya watumiaji wa tovuti hiyo kuwa na mawasiliano yenye umuhimu zaidi katika maisha yao ya kila siku.

Watu watapata habari zaidi juu ya marafiki zao na familia na taarifa juu ya makampuni na taasisi zitapungua kwenye mtandao huo.Mkurugenzi mkuu wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg ameeleza kuwa maudhui ya biashara na vyombo vya habari yalikuwa yanamuondoa mtu katika nyakati muhimu ambayo watu wengi wanaithamini zaidi.

Amesema vipaumbele ambavyo Facebook imeviweka ili kuondoa changamoto iliyopo inaweza kumaanisha kuwa watu watatumia muda mfupi zaidi katika mtandao huo ,lakini muda ambao watautumia utakuwa na thamani kubwa zaidi.

Haya yakiwa mabadiliko mamkubwa katika mtandao huo wenye watumiaji zaidi ya bilioni mbili duniani kote,itaongeza mapato kutoka kwenye matangazo.

Licha ya kuwa ,Facebook imekuwa katika shinikizo kubwa la kukabiliana na watu ambao wamekuwa wanapenda mtandao huo kupita kiasi ambacho wanaweza kuatharika na afya ya akili.

Baada ya Mbowe Kupewa Mjerejesho wa Kilichompeleka Ikulu Lowasa Sasa Awatuliza Wanachadema

$
0
0
Baada ya Mbowe Kupewa Mjerejesho wa Kilichompeleka Ikulu Lowasa Sasa Awatuliza Wanachadema
Hatimaye mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametuliza mtifuano ulioibuka miongoni mwa wanachama wake baada ya waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kufanya kikao cha faragha na Rais John Magufuli.
Pia mwenyekiti huyo wa chama hicho kikuu cha upinzani amesema Chadema haitakubali kuchonganishwa kutokana na kikao hicho cha viongozi hao wawili.

Mbowe alisema hayo jana baada ya kufanya mazungumzo na Lowassa, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema kupata taarifa ya kikao chake na Rais kilichofanyika Jumanne iliyopita Ikulu, Dar es Salaam.

Tangu Ikulu itoe taarifa ya mazungumzo ya Lowassa na Rais, viongozi wa Chadema wamepokea suala hilo kwa hisia tofauti, wengi wakimkosoa mbunge huyo wa zamani wa Monduli kwa kusifia juhudi za Rais Magufuli bila ya kueleza kasoro za Serikali ya Awamu ya Tano katika kushughulikia demokrasia, uhuru wa habari, mikutano ya hadhara na masaibu wanayokabiliana nayo viongozi wa upinzani dhidi ya vyombo vya dola.

Aboubakary Liongo, ambaye ni msemaji wa Lowassa, alieleza jana kwamba waziri huyo mkuu wa zamani alifanya mazungumzo na Mbowe kwa lengo la kumpa mrejesho ya kile kilichojiri Ikulu.

Baada ya taarifa hiyo ya Liongo, Mwananchi iliwasiliana na Mbowe ambaye alithibitisha kuwapo kwa mazungumzo hayo na Lowassa.

“Ni kweli nilikutana na Mheshimiwa Lowassa na tulizungumza, lakini siwezi kutoa kila kitu. Tulichozungumza si kwa public (watu wote), lakini muda ukifika kama itahitajika tutafanya hivyo,” alisema Mbowe.

“Ieleweke kwamba, Ikulu walitoa taarifa ya dakika tano waliyoona wao inafaa. Kama wanataka watoe mazungumzo yote ya zaidi ya saa moja na nusu waliyofanya, si kuchagua kipi kiende na kipi kisiende kwa masilahi yao.

“Kama Ikulu inataka iweke full text (taarifa yote) ya mazungumzo, si kutoa vitu nusunusu kwa masilahi yao. Kama wanataka kumchonganisha (Lowassa) na wenzie wameshindwa.”

Hata hivyo, Mbowe hakueleza kama alikuwa na taarifa za kikao cha Lowassa na Rais baada ya kuulizwa na Mwananchi, badala yake alijibu swali jingine la kipi kitarajiwe. “Kama nilivyosema mwanzo, mazungumzo yalikuwa ya faragha, sidhani kama mazungumzo ya faragha unaweza kuyaweka wazi, ila muda ukifika ikihitajika tutafanya hivyo.

Tamko la Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, baada ya kukutana na Lowassa linaweza kutuliza joto ambalo lilikuwa linaonekana kuanza kupanda kutokana na kila mmoja kutoa kauli yake dhidi ya waziri huyo mkuu wa zamani.

Miongoni mwa waliotoa kauli hizo ni Mbowe mwenyewe juzi, ambaye alisema sifa alizotoa Lowassa ni maoni yake binafsi na si msimamo wa Chadema, huku akisema mtu anayemsifu Magufuli anahitaji “ujasiri wa ziada”.

Mwingine ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ambaye alihoji sababu za Lowassa kutomtaarifu Mbowe kuhusu mwaliko wake Ikulu wakati walikutana siku chache zilizopita.

Pia mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alihoji sababu za Lowassa kummwagia sifa Rais wakati hali ya kiuchumi ikiwa mbaya kutokana na biashara kufungwa; wapinzani wakikamatwa kila mara; mikutano ya hadhara ikiwa imepigwa marufuku; vyombo vya habari kufungiwa; watu kupotea na Lissu kushambuliwa kwa risasi.

Hata Umoja wa Vijana wa Chadema (Bavicha) ulimlaumu Lowassa kwa kupongeza bila ya kuzingatia masuala mengine yanayoendelea nchini.

Kauli hizo zilionekana kuanza kupandisha joto Chadema kabla ya Mbowe kukutana na mgombea huyo wa urais mwaka 2015 kupitia Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa na kuzungumza.



Viongozi Mbalimbali Waambatana na Rais Shein, Magufuli Katika Maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi

$
0
0
Viongozi Mbalimbali Waambatana na Rais Shein, Magufuli  Katika Maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi
Idadi kubwa ya viongozi mbalimbali wa Serikali na wastaafu wamejitokeza kuhudhuria katika sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika sasa katika viwanja wa Amaan vilivyopo Unguja visiwani Zanzibar.

Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein anaongoza sherehe hizo akiwa sambamba na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli sambamba na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na baadhi ya mawaziri, naibu mawaziri na wabunge mbalimbali.

Baadhi ya viongozi wastaafu waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja na marais wastaafu akiwemo, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete, Aman Abeid Karume na baadhi ya makamu wa Rais wastaafu akiwemo Mohamed Gharib Bilal.


Makonda Atoboa Siri ya Kagame Kuvutiwa na Tanzania

$
0
0
Makonda Atoboa Siri ya Kagame  Kuvutiwa na Tanzania
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amefunguka na kusema uwezo mkubwa wa Rais Magufuli na Demokrasia ya kweli ni jambo ambalo linawavutia wageni kuja Tanzania akiwepo Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame anayetarajiwa kuwasili nchini Jumapili.


Makonda amesema hayo leo akiwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam baada ya kuagana na Rais Magufuli ambaye ameelekea visiwani Zanzibar kushiriki sherehe za maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

“Amani Demokrasia ya kweli, upendo na uwezo wa mkubwa wa Rais Magufuli ndiyo msingi wa kuwavuta wageni kuja kutembelea hakuna mgeni ambaye anaweza kutembelea nchi ambayo haina upendo, amani na mshikamano. Tanzania chini ya uongozi wa Rais Magufuli inaendelea kuchanja mbuga katika nyanja za kidemokrasia hasa pia katika uwanja mwingine wa kidiplomasia na kuwafanya wageni waone sehemu nzuri ya kuja kutembelea,” alisema Makonda.

Mbali na hilo Makonda amesema kuwa Rais Paul Kagame atawasili nchini Tanzania siku ya Jumapili ya tarehe 14 ambapo atakuwa nchini kwa ziara ya siku moja na kufanya mazungumzo na Rais John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Ndoa ya Sasha Yaota Mbawa " Suala la Ndoa Halipo Tena na Mahari Sirudishi"

$
0
0
Ndoa ya Sasha Yaota Mbawa " Suala la Ndoa Halipo Tena na Mahari Sirudishi"
MWANADADA mwenye mvuto wa aina yake Bongo, Sasha Kassim ambaye alikuwa anatarajia kuolewa siku chache zijazo amesema kuwa, ishu hiyo haipo tena na mahari hairudishwi.

Akizungumza na Star Mix, Sasha alisema mwanaume huyo aliyemtaja kwa jina moja la Boniphace amejikuta akishindwa kuendelea naye sababu ya wivu, amekuwa akimuonea wivu picha anazoposti mtandaoni na kumtaka asitumie mitandao ya kijamii, jambo ambalo hayupo tayari kukubaliana nalo.

“Suala la ndoa halipo tena, yeye alinipata mtandaoni cha ajabu ananikataza kutumia mitandao nimeona sitoweza kuminywa uhuru wa maisha yangu kwa kiasi hicho, hivyo uchumba umevunjika na mpango wa kurudisha mahari haupo kabisaaa,”alisema.

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume, Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na Kuchelewa Kwa Dakika 20

$
0
0

TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za:


FULL POWER: Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.


NYAMVA: Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788/ 0715741788 -DR MAGISE 

Steve Nyerere: "Wamesema nina UKIMWI

$
0
0

Msanii wa filamu nchini Tanzania na mwanasiasa Steve Nyerere amefunguka na kusema kuwa kutokana na matatizo ambayo anapitia ikiwa pamoja na maradhi yake kuna watu wengi wamekuwa wakisema kuwa ameathirika na kukwama.


Steve amesema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha eNewz na kudai kuwa kwa sasa anasumbuliwa zaidi na miguu na kama kuna watu wamemtumia uchawi basi anawaomba msamaha wamsamehe ili aweze kupona

Kauli ya Zari kuhusu Diamond Kufungua Kituo cha Redio na TV

$
0
0

Mama watoto  wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady amempongeza muimbaji huyo mara baada ya kuweka wazi ujio wa kituo chake cha redio na runinga.


Katika pongezi hizo Zari amemtaja Diamond kama mtu anayejituma zaidi katika kile anachokifanya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari ameandika;


Hongera Damond Patnumz sana kwa juhudi na bidii uliyonayo Allaah akujalie kwa mengine mazuri zaidi. Siku zote umekuwa mpiganaji wa kazi zako, kwa kuwa njia pekee ya kuijenga familia ni kupiga KAZI najua malengo yako Alhamdulillah! #wcbTV #wcbFILMSTUDIO #wcbMUSICSTUDIO #wcbRADIO #wcbHEADQUATERS.


Bila kusahau #DiamondKaranga na chibuperfume #ChibuPerfume 2018 looking good👌🙏


Hapo jana Diamond aliachia video mtandaoni ikionyesha mjengo mpya wa WCB ambao utatumika kama makao makuu ya kampuni hiyo pamoja na studio za Wasafi TV na Wasafi Redio. 


Pia utakumbuka hii si biashara ya kwanza kwa Diamond kwani ameshaingiza sokoni manukato yake ‘Chibu Perfume’ pamoja na Karanga.

Hapa ndio itakapokuwa Radio na TV Station ya Diamond Ambayo Itaanza Kuruka Mwezi wa Pili

$
0
0

Kampuni ya Wasafi Classic (WCB), inayomilikiwa na msanii maarufu wa muziki wa Bongofleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ wanatarajia kufungua televisheni na redio Februari mwaka huu.


Haya yamebainika ikiwa ni saa chache tangu Diamond na viongozi wa kampuni hiyo watupie jumba la kifahari  ambalo linaelezwa  litakuwa ndiyo  makao makuu ya WCB ambapo mbali ya kuwa na studio za kurekodia muziki pia litakuwa na Redio na TV.


Katika mahojiano hayo, Fela amesema hatua waliofikia ni katika harakati za kampuni hiyo kuendelea kujitanua na kutoa fursa kwa vijana wengi zaidi.


Meneja wa Diamond, Said Fela  amesema pamoja na kwamba wao ni watu wanaojishughulisha na kazi za burudani, lakini TV yao na redio zitakuwa zinarusha vipindi vya aina zote vikiwemo vya kuelimisha na habari kama vilivyo vituo vingine.


“Kwetu sisi hii tunaona ni hatua nzuri kwa kuwa tunajua tukifungua vituo hivi ndivyo kadri tunavyozidi kuzalisha ajira na tumeamua kutumia wataalam ambao walikuwa kwenye fani hiyo ikiwemo wazee waliostaafu katika Shirika la Utangazaji(TBC) enzi hizo TVT kwa ajili ya kutuongoza kwa kuwa sisi wenyewe hatuwezi,”amesema Fela.


Hata hivyo, alipoulizwa kama wamejenga wenyewe mjengo huo au Fela amesema wamekodisha kama walivyokuwa wamekodisha ile ya Sinza huku sababu za kuhama akieleza ni kutokana na kuongeza huduma na pia sehemu waliyokuwepo kulikuwa na taabu ya maegesho ya magari na kujaa maji hasa mvua zinaponyesha.


Mjengo huo wa wasafi wa ghorofa moja ambao upo maeneo ya Mbezi umeonekana kuwa gumzo  katika mitandao ya kijamii na watu wengi wamempongeza Diomond na uongozi wake kwa hatua aliofikia.


Mbali na redio, tayari Diamond ameshajiingiza katika biashara nyingine ikiwemo ya manukato yanayoitwa 'Chibu', na 'Diamond karanga'

Amber Lulu: Diva Hajawahi Kuonyesha Kuchukizwa na Mapenzi Yangu na Prezzo

$
0
0
Amber Lulu: Diva Hajawahi Kuonyesha Kuchukizwa na Mapenzi Yangu na Prezzo
Msanii wa muziki Bongo na video vixen, Amber Lulu amesema Diva hana shida wala hajawai kuonyesha kuchukizwa na yeye kuwa katika mahusiano na Prezzo.

Penzi la Prezzo na Diva lilishamiri mwaka 2013 kabla ya kuja kutengana na sasa rapper huyo kutoka nchini Kenya anatoka na Amber Lulu.

Amber Lulu ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa yeye na Diva wapo sawa na mara kadhaa wamekuwa wakikutana na kuzungumza.

“Hapana hajawahi kabisa na juzi nilikuwa naye yupo fresh, nafikiri hivyo ni vitu vya zamani kwa hiyo ana maisha yake na Heri Muziki, kwa hiyo maisha ni mengine na yamebadilika hivyo hamna kumaindiana,” amesema Amber Lulu.

Uwepo wa penzi la Prezzo na Amber Lulu kulianza kuripotiwa katika vyombo vya habari na mitandao October mwaka jana, 2017.
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images