Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Watu 12 Wafariki Kwenye Ajali ya Gari Mkoani Kagera

$
0
0
Watu 12 Wafariki Kwenye Ajali ya Gari Mkoani Kagera
AJALI mbaya ya gari dogo aina ya Nissan Caravan (Hiace) lenye namba za usajili T 542 DKE ambalo limegonga magari makubwa mawili ya mizigo imesababisha vifo vya watu 11 na wengine watano kujeruhiwa katika eneo la Nyangozi kata ya Nyantakara wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera jana Jumapili, Jan. 14, 2017.

Kamanda waPolisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambap ameeleza kuwa gari hilo dogo la abiria lilikuwa linatokea Kakonko mkoani Kigoma kuelekea Kahama huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva ambaye aligonga magari mawili ya mizigo yenye namba za usajili T694 COX lililokuwa likivuta tela namba T 103 DKJ mali ya kampuni ya Mruruma Enterprises ya Dar es Salaam.

Ollomi amesema kuwa watu 9 wamefariki papo hapo eneo la ajali, mmoja alifariki njiani akiwahishwa hospitali na mwingine amepoteza maisha leo asubuhi. Majeruhi watano wanaendelea kupata matibabu katika hospitali teule ya Wilaya ya Biharamulo.

Gari hilo dogo lilikuwa na abiria wapatao 17 ambapo 11 wamefariki akiwemo dereva wake na watano wamejeruhiwa huku mmpoja akitoka salama.

Kichanga Kilichopotea Kwenye Mazingira ya Kutatanisha Chapatikana Kiutata

$
0
0
Kichanga Kilichopotea Kwenye Mazingira ya Kutatanisha Chapatikana Kiutata
Hekaheka ya leo January 15, 2018 nimuendelezo wa Hekaheka ya mtoto mchanga wa miezi miwili aliyepotea kwenye mazingira ya kutatanisha ambapo ilidaiwa kuwa hakuna mtu aliyefika kwenye nyumba hiyo wala mtu aliyetoka, kitu kilichosababisha wahusika kuhusisha na imani za kishirikina huku wakimtuhumu jirani yao kuhusika.

Sasa mtoto huyo amepatikana ni baaada ya mwanamke kumpeleka kwa siri na kumuweka karibu na nyumba ambayo alikuwa akiishi mtoto huyo huku akiwa amevalishwa nguo nyingine tofauti na zile ambazo alipotea nazo na mpaka mtoto huyo anarudishwa alikuwa katimiza siku nne.

Uchebe: Hii ni Stata Bado Sherehe ya Tatu..... Hakuna Mwenye Mwanamke Mzuri Kuliko Mimi

$
0
0
Uchebe: Hii ni Stata Bado Sherehe ya Tatu..... Hakuna Mwenye Mwanamke Mzuri Kuliko Mimi
Baada ya kufunga ndoa Uchebe kupitia ukrasa wake wa instagram ameandika mambo mbalimbali  ikiwa kutupa vijembe na  kumsifia mke wake Shilole ambaye kwa sasa ni mama kijacho kwamba hakuna mwenye mwanamke mzuri kama yeye.

Uchebe ambaye amelichukua jana ilikuwa sherehe ya ndoa yake amesema shere ya jana ni stata sherehe ingine kubwa inatarajia kufanyika na kutupa vijembe kwa wale wanaomsema kuhusu penzi lake na mkewe.


Haya ni baadhi ya maneno na  vijembe alivyoandika uchebe mitandaoni;1. mke wangu peke yangu bado sherehe ya tatu ngoja mke wangu akapige shoo ulaya tutafanya party funga kazi hii ni stata
2.sina kinyaa na mke wangu nina mnyonya ata kama katoka kupiga show na majasho
3.Wenye wake wotw mikono juu Ilove u zuu watu vichwa vinawauma!..Oooh umalizi mwaka nawacheka kwa zarau
4.Uchebe usijimalize acha na ya kesho! hahaa najimaliza ili niwape la kusema nyie si mnajua kuchonga
5.Hakuna mwenye mwanamke mzuri kama mimi

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume, Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na Kuchelewa Kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za:


FULL POWER: Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.


NYAMVA: Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788/ 0715741788 -DR MAGISE

Lowassa: "Ujumbe wa Magufuli ni kunitaka nirejee CCM, ila nilikataa"

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amesema ujumbe wa Rais Magufuli kwake alipofanya nae mazungumzo Ikulu, ulikuwa ni kumshawishi arejee CCM suala ambalo hakukubaliana nalo na alimueleza Rais kwamba uamuzi wake wa kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA haukua wakubahatisha.

Siri ya Mapenzi ya Wizi Kuwa Matamu Kuliko ya Halali

$
0
0
Ni swali ambalo wengine pia inawezekana wamekuwa wakijiuliza. Inakuaje mapenzi ya kuiba, mapenzi ya juu juu yanakuwa matamu sana kuliko mapenzi ambayo yamehalalishwa.

Mapenzi kiufupi kuwa mazuri yanabebwa na mambo mengi sana.moja kuu katika hayo ni adventures(matukio) binafsi nilishawah kuwa na mpenzi wa toka miaka ya late 90 ambaye kuna matukio mengi sana yashawahi kutukuta sote.tushawah mpaka kukamatwa na polisi tuki make love, tumeshawah kukamatawa tena jumba bovu.tumeshawah kupelekana polisi mpaka ameolewa yule dada amekuwa aki miss matukio tena makubwa makubwa.tushapelekana sana polisi na mumewe sometime akihusika lakini mwishone naendelea ku mgegeda yule dada.adventures na sisi wengine adventures zinatusisimua zaidi.

Mapenzi ya namna hii yananikumbusha kisa cha wapenzi wawili ambao walianzia mapenzi yao chuo.ikafika wakamaliza masomo.wakarudi kwa wazaz wao.ikawa hali ni ngumu sana kiuchumi.bas wanapitiana wanaenda kutafuta kazi.wakiwa wanarud late sometime wanakuwa hawana naul wanalazimika kupita njia short cuts na wakiwa huko wakati mwingine wanajiwa na hamu ya mapenzi wanatafuta sehem ya giza wanafanya mapenzi.

Wakawa wakati mwingine wanafanya mapenzi hadi kwenye majumba mabovu au dampo. Sehem ambayo tu watapata privacy.wakawa waki enjoy sana maisha hayo.

Siku zikaenda wakapata kazi wakaoana wakawa na nyumba nzuri.wakaona tofaut.hawa enjoy maisha.no fire burning inside them,no passion.ingawa sasa wana kitanda kikubwa na nyumba nzuri n.k

Iliwachukua muda sana kuweza kugundua tatizo ni nini na mwishowe waliamua kuweka ustaarabu pembeni.wakaanza kuishi maisha ya no care na kuweka ustaarabu pembeni.wakajikuta wana enjoy tena mapenzi.

Inatokea unakuwa na mpenzi ambaye mnapenda sana.unapokuwa naye mnakuwa kwa kificho. Unaenda kumchukua anakaa nyuma ya gari amelala kwenye seat ili asionekane.mnaenda hotel ambayo inabidi kwnza uka check usalama then anachomoka kuingia room.ndani mnaenjoy sana.trust me.halaf anatoka tena kigaidi amevaa ushungi au kofia kubwa na miwani.

Fikiria huyu mpenzi ambaye pengine ni married.ametoroka kazini kaja ukamgegede mara moja alijawa na hamu au katoka jioni kazin mnaonana mnaenda bar flani nmnapark gari mnagegedana kwenye gari.halafu mnaagana.akirudi anachat nawe alivyo enjoy n.k

Fikiria mpenz ambaye kaaga ameenda kwenye msiba kumbe kaja ukamgegede sehemu au kwako kwa masaa kadhaa. Huwa ni mapenzi real na yenye mashamushamu sana.yana raha yake.

Mapenzi anayokwambia now baby usipigie usitume text ndo nafika home.ntakutafuta kesho.kesho yake anakupigia akiongea kwa sauti ya chini kuwa yupo chooni ametamani tu asikie sauti yako.halaf ana kata.jion anakuuliza upo wapi.anakwambia anakuja angalau umpige kimoja.huwa yanakuwa ya ajabu sana na yenye hisia kali.

By GuDume

Sumaye:Kuzuiwa Kikutano ya Hadhara ni Uonevu kwa Wananchi

$
0
0
Waziri Mkuu wa mstaafu, Frederick Sumaye amesema zuio la kufanya mikutano ya hadhara hadi mwaka 2020, linaminya uhuru wa wananchi wenye nia ya kuanzisha vyama vipya ya siasa.

Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini ametoa kauli hiyo jana Januari 14, 2018 katika mahojiano na kituo cha Televisheni cha Azam.

Amesema zuio la kufanya mikutano liko kinyume na sheria iliyoanzisha vyama vya siasa.

“Jambo jingine ambalo ni gumu zaidi, nikisema leo si mwana CCM sitaki kwenda CCM, CUF wala Chadema, kwa utaratibu ulipo sasa siwezi kuanzisha chama kwani huwezi kufanya mkutano wowote kwa sababu tunafunga kabisa mtu kuanzisha chama,” amesema Sumaye na kuongeza,

 “…, CCM wao wanaonekana hawana wa kuwazuia, Mwenyekiti wao (Rais John Magufuli) anakwenda popote, wakati wowote ingawa unashindwa kumtofautisha na ziara za kiserikali.”

Kuhusu hamahama ya wanachama amesema, “ “Wanacheza na fedha za wananchi,  mfano mbunge wa Kinondoni (Maulid Mtulia aliyehamia CCM) alikuwa CUF, anakwenda CCM halafu wanamrudisha tena kugombea.”

“Sawa na yule wa Siha (Dk Godwin Mollel amehamia CCM) naye karejeshwa kugombea. Hii ni sawa na kuwatukana watu.”
Chanzo Mwananchi

Lissu Kushtakiwa Mahakama ya Kimataifa (The Heque)

$
0
0
Lissu Kushtakiwa Mahakama ya Kimataifa (The Heque)
CYPRIAN Mujura ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa CZ Information & Media Consulotant LTD, leo kautaarifu umma kuwa kupitia wanasheria na mawakili maarufu hapa nchini wanakusudia kumfungulia mashtaka katika mahakama ya ndani na ya Kimataifa (The Heque) Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissukwa kauli zake dhidi ya serikali.



Majura amesema hayo leo Jumatatu, Jan. 15, 2017 akizungumza na wanahabari na kusema kuwa, katika Kipindi cha Focus on Africa kinachorushwa na BBC wakati akihojiwa na mwandishi Victor Kenani wiki mbili zilizopita, Tundu Lissu anadaiwa kusema Tanzania kwa sasa ni nchi hatarishi kwa siasa pamoja na pamoja na wote wanaohoji utendaji wa Serikali.



“Alisema watu wanauawa hovyo wanatupwa baharini kwenye viroba, tunataka atupe uthibitisho wa madai yake hayo ndani ya siku mbili zijazo kuanzia leo,” alisema Majura.

Majura amedai kauli hizo ni hatarishi kwa usalama wa nchi, na kwamba inaondoa amani ya nchi iliyoachwa na waasisi wa Taifa hili huku akieleza kuwa mawakili wamejipanga kumfungulia Lissu mahakama za hapa ndani ya Tanzania na wengine wanajiandaa kwenda Mahakama ya Kimataifa (The Heque).

Lissu yupo nchini Ubelgiji tangu wiki iliyopita, Jan. 6 ambako amelekwa ili kuendelea kupatiwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma mnamo Septemba 7, mwaka jana.

Afrika Kusini Yamuita Balozi wa Marekani Kufuatia Matamshi ya Trump Kuhusu Afrika

$
0
0
Afrika Kusini Yamuita Balozi wa Marekani Kufuatia Matamshi ya Trump Kuhusu Afrika
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Afrika Kusini imemuita naibu balozi wa Marekani mjini Pretoria kufuatia matamshi ya Trump kuhusu nchi za Afrika.

Bwana Trump anaripitiwa kuyataja mataifa ya Afrika kuwa machafu wakati wa mahojiano kuhusu sera za uhamiaji.

Amewaambia waandishi wa habari kuwa yeye sio mbaguzi.

Taarifa kutoka ofisi ya nchi za kigeni ya Afrika Kusini inasema kuwa inaunga mkono taarifa iliyotolewa na Muunganoa wa Afrika.

AU ilieezea mshangao wake kutokana na matamsh hayo na kumtaka Trump kuomba msamaha.

Afrika Kusini inasema kuwa uhusiano wake na Mareknia unastahili kuwa katika misingi ya heshima.

Namibia, Botswana na Ghana ni baadhi ya nchi ambazo zimetoa taarifa za kumshutumu vikali Bw. Trump.

Mzee Akilimali Aweka Msimamo Wake Asema Atapinga Mambo ya Mo Dewji Hadi Atakapoingia Kabulini

$
0
0
Mzee Akilimali Aweka Msimamo Wake Asema Atapinga Mambo ya Mo Dewji Hadi Atakapoingia Kabulini
Mmoja wa wanachama wakongwe wa klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema kuwa ataendelea kupinga suala la ukodishwaji wa klabu hiyo hadi atakapoingia kaburini na kudai kuwa wanachama waache kumsakama kwa kuwa Serikali ndivyo ilivyoamua.

Hivi karibuni Klabu ya Yanga ilitangaza kuanza mchakato wa mabadiliko kama ilivyo kwa watani wao Simba ambao wamemkabidhi timu Mohamed Dewji ‘Mo’ kwa ajili ya kuingia katika mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu kwa njia ya hisa.

Akilimali amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwa miongoni mwa wanachama ambao wanapinga mabadiliko ndani ya klabu hiyo jambo ambalo limekuwa likiwachukiza baadhi ya wanachama.

Akilimali alisema kuwa, amekuwa na bahati mbaya kwa baadhi ya wanachama na viongozi wa Yanga kutokana na kupinga suala la Yanga kumilikiwa na mtu mmoja na kudai kuwa ataendelea kufanya hivyo hadi atakapoingia kaburini.

“Nimekuwa na bahati mbaya kwa baadhi ya wanachama na viongozi, ni kutokana na kukataa katu suala la Yanga kumilikishwa mtu mmoja hilo haliwezekani na nitapinga hadi naingia kaburini.

“Nipo tayari uanzishwe mfumo wa kampuni kama inaavyotajwa katika katiba ya Yanga ibara ya 56 ambayo inasema Yanga itaanzisha kampuni ya umma ambapo wanachama wanamiliki hisa asilimia 51 na wanahisa asilimia 41.

“Lakini kwa kuwa nilikataa ndiyo naambiwa napinga mabadiliko, Yanga haikodishwi kama masufuria na kwa bahati nzuri serikali ikatusikiliza sisi watu wachache tuliopinga ukodishwaji ndipo wanaposema kuwa mimi napinga maendeleo.


“Mimi nahitaji maendeleo ya Yanga hadi kiama lakini utaratibu ufuatwe sio kumpa mtu mmoja, kwa kuwa viongozi wangu walitaka kukodisha na mimi pamoja na serikali kupinga, ndiyo wameniambia mimi napinga maendeleo, jambo hilo si sawa,” alisema Akilimali.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni Dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi?

Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Waziri Mkuu: “Tutakamilisha ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Musoma”

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inakamilisha ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara iliyoanza kujengwa mwaka 1980.

Alitoa kauli hiyo wakati alipokagua ujenzi wa hospitali hiyo baada ya kuwasili mkoani Mara kwa ajili ya ziara yake ya kikazi.

Waziri Mkuu amesema Serikali itakamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa awamu, ambapo wataanza na eneo la mapokezi na vyumba vya madaktari.

Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya nchini, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuiamini na kushirikiana nayo.

Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 ili ujenzi uendelee. Ujenzi huo ulianza mwaka 1980, ulisimama mwaka 1987 kuanza tena 2010.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amekagua uwanja wa ndege wa Musoma mkoani Mara ambao unatarajiwa kukarabatiwa na kuwekwa lami.

Amesema kukamilika kwa ukarabati huo wa kiwanja hicho kutafungua fursa za utalii ndani ya mkoa huo ambao umezungukwa na vivutio vingi.

Amesema Serikali imedhamilria kukarabati viwanja mbalimbali vya ndege nchini kikiwemo cha Musoma ili kuboresha huduma za usafiri wa anga.

Viwanja vingine vinavyotarajiwa kukarabatiwa ni Iringa, Kilwa Masoko, Lake Manyara, Lindi, Moshi, Njombe, Tanga, Simiyu, Singida na Songea.

Waziri Mkuu amesema viwanja hivyo kwa sasa vinakarabatiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), ambao wanajenga kwa gharama nafuu na kwa viwango vinavyostahili.

Awali, Meneja wa TANROADS, mkoa wa Mara Mhandisi Mlima Ngaila alisema ukarabati huo utafanyika kwa awamu tatu ambapo ya kwanza itahusisha upanuzi wa uwanja na ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege.

Alisema barabara ya kuruka na kutua ndege ina urefu wa km. 1.6 na upana wa mita 33 ni ya changarawe, hivyo kusababisha baadhi ya ndege kushindwa kutua.

Pia, Waziri Mkuu alikagua ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Musoma na kwamba ameridhishwa na ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo.

“Shule hii ilipewa sh bilioni 1.28 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu. Nimekagua jengo la utawala, madarasa, mabweni, jiko, maabara na bwalo, nimeridhika na kazi iliyofanyika.”

Shule hiyo ni miongoni mwa shule 10 kongwe ambazo Serikali iliamua kuzikarabati ili ziweze kurudi kama zamani na kuendelea kutumika.

Hata hivyo Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Manispaa ya Musoma kushirikiana na uongozi wa shule hiyo katika kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili.

Miongoni mwa changamoto hizo ni malipo ya watumishi wasaidizi wakiwemo wapishi, walinzi na madereva, ambapo aliitaka kuchukua jukumu la kuwalipa watumishi hao badala ya kuacha jukumu hilo kwa Mkuu wa Shule.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Uamuzi wa serikali dhidi ya gazeti la Nipashe kwa taarifa ya kupotosha kuhusu Rais

RC Makonda amfuta machozi mjane ambaye nyumba yake iliuzwa na matapeli

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemsaidia mama mjane Benadetha Rwendela aliedhulumiwa nyumba yake Plot No. 239 Block B Kunduchi Beach kwa kupigwa mnada na madalali kutoka kampuni ya Nkanya Ltd kinyume na taratibu kisha kuamrishwa kuondoka ndani ya siku 30.

Baada ya RC Makonda kuona taarifa hizo kwenye baadhi ya vyombo vya vabari na mitandao alimuita mjane huyo ofisini kwake kisha kumkutanisha na wanasheria wa mkoa na kubaini utapeli mkubwa uliotumika kuuza nyumba hiyo kutokana na watu kufoji nyaraka ikiwemo sahihi ya mwenyekiti wa mtaa huku nyumba hiyo ikiwa na zuio la Mahakama.

Aidha imebainika kuwa hati za nyumba hiyo zilifojiwa kisha kutumika kuchukuwa mkopo wa shilingi bilioni moja pasipo mmiliki wa nyumba kujua kinachoendelea.

Kutokana na hilo RC Makonda ameagiza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kuwakamata matapeli waliohusika pamoja na kuagiza kusimamishwa mnada huo kwakuwa ni batili huku akimsihi mama mjane kuishi kwa amani kwenye nyumba yake.

Aidha RC Makonda amesema Jumatatu ya wiki ijayo atakutana na Bank ya KCB kwa ajili ya mazungumzo huku akiwaagiza madalali wote wanaotaka kufanya minada kwenye mkoa huu kuhakikisha wanapata ruhusa kutoka kwa wakuu wa wilaya.

Kwa upande wake mjane huyo Benadetha Rwendela ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwajali wananchi wake na kuwasaidia pale wanapopata matatizo huku akimpongeza Rais Magufuli kwa kumteua RC Makonda.

Shilole Atoboa Siri ya Pete Aliyovishwa na Uchebe " Pete Niliyovishwa Imetoka Marekani"

$
0
0
Shilole Atoboa Siri ya Pete Aliyovishwa na Uchebe " Pete Niliyovishwa Imetoka Marekani"
MSANII wa muziki wa Mduara Bongo, Zuwena Mohammed, ‘Shilole’ au Shishi Baby mefunguka kuwa pete ya ndoa aliyovishwa na mume wake, Ashrafu Uchebe katika usiku wa harusi yao kuwa ni zawadi ya pekee aliyopewa na mjomba wake kutoka nchini Marekani

Shilole ameanika hayo kupitia ukurasa waske wa Instagram na kusema;


Wanyamwezi tumefundwa bana 😂😂 pete nzuri tumezawadiwa na unlce wangu kutoka marekani @gift_jeweleries @gift_jeweleries kiboko ya gold original 🙏. Ameandika Shilole.







Zari Kimyaa!... Sasa ni Vita Mpya ya Tunda na Mobetto

$
0
0
Zari Kimyaa!... Sasa ni Vita Mpya ya Tunda na Mobetto
Ubuyu wa mjini kwa sasa ni vita mpya kati ya mwanamitindo, Hamisa Mobeto na mwanadada anayeuza nyago kwenye video mbalimbali za wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Tunda Sebastian, kisa kikitajwa kuwa ni msanii wa Bongo Fleva ambaye ni baba watoto wa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Ijumaa Wikienda lina undani kamili.

Chanzo makini cha ubuyu huo kilicho karibu na mastaa hao kilimwaga ubuyu kuwa, wawili kwenye gogoro zito huku Tunda akidaiwa kufanya chokochoko kwa kumrushia vijembe Mobeto ambaye amezaa na msanii huyo ambaye kwa sasa anadaiwa kutoka kimapenzi na Tunda.

Chanzo hicho kilifunguka kuwa, siyo siri tena kwamba Tunda anatoka kimapenzi na msanii huyo anayedaiwa kumpangishia bonge la jumba la kifahari maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar.

TUNDA ADAIWA KUAPA

Ubuyu wa motomoto ulidai kuwa, Tunda ameapa kuwa, lazima mwaka huu amzalie

msanii huyo kama ilivyokuwa kwa Mobeto mwaka jana.

“Mobeto anajua kila kitu kuhusu Tunda kutoka kimapenzi na mzazi mwenziye kwa hiyo kwa sasa ni paka na panya, hawapendani kabisa.

“Hivi karibuni walikutana kwenye sherehe ya mdada f’lani hivi hawakusalimiana, kiukweli huyo msanii wa Bongo Fleva anawachanganya sana wanawake,” kilisema chanzo hicho.


Hamisa Mobeto.

UKWELI NI UPI?

Ili kuujua ukweli wa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Tunda na kufanya naye mahojiano ambapo mambo yalikuwa hivi;

Ijumaa Wikienda: Habari yako Tunda?

Tunda: Nzuri, karibu.

Ijumaa Wikienda: Kuna habari kwamba kwa sasa unatoka na msanii wa Bongo Fleva, unazungumziaje?

Tunda: Natoka naye tunaelekea wapi?

Ijumaa Wikienda: Yaani unatoka naye kimapenzi na juzikati ulionekana ukila Elements, Masaki.

Tunda: Mtu anawezaje kutoka kimapenzi na kaka yake? Huyo msanii ni kaka yangu na inajulikana na kila mtu, sasa sijui mtu anawezaje kutoka kimapenzi na mtu anayemheshimu kama kaka yake?

Ijumaa Wikienda: Lakini kuna habari kwamba, wewe kuna bifu kubwa kati yako na Mobeto, kisa kutoka na mzazi mwenzake huyo, hilo likoje?

Tunda: Sijawahi kuwa na bifu na Hamisa (Mobeto) ninamheshimu kama dada yangu.

Ijumaa Wikienda: Hivi karibuni kulikuwa na sherehe ya rafiki yenu na mlipokuta wewe na Mobeto mlichuniana, unasemaje?

Tunda: Hilo ndo’ nasikia kutoka kwako.

Ijumaa Wikienda: Je, ni kweli ujauzito ulionao kwa sasa ni wa msanii huyo au unazaa na nani?

Tunda: Nazaa na kaka yangu.

Ijumaa Wikienda: Kaka yako huyo msanii wa Bongo Fleva?

Tunda: (kimya).



TEAM MOBETO NA TUNDA

Kwa upande wa Mobeto alipotafutwa ili atoe neno kuhusiana na ubuyu huo, simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa SMS hakujibu hivyo jitihada za kumpata ili afunguke anachokijua kwani timu yake imekuwa ikimshambulia Tunda.



ZARI KIMYAAA…

Hata hivyo, tofauti na wengi walivyotarajia kuwa baada ya kuzuka kwa ishu hiyo Zari angekuja juu, yeye amekuwa kimya hadi sasa.



Diamond Kuishi Nje ya Tanzania?....“Natafuta Nyumba ya Kununa Kigali Nyumba Yangu ya Baadae kwa Ajili ya Simbas !! "

$
0
0
Diamond Kuishi Nje ya Dar?....“Natafuta Nyumba ya Kununa Kigali Nyumba Yangu ya Baadae kwa Ajili ya Simbas !! "
Bongofleva Diamond Platnumz ni miongoni mwa mastaa ambao wameahidi mwaka 2018 tutarajie vitu vingi kutoka kwao, Diamond akiwa ameanza na kutuonyesha headquarters mpya za WCB .

Ukitaja  nyumba anazomiliki Diamond Platnumz kiukwelihuwezi kuacha kutaja nyumba yake ya Afrika Kusini na Tanzania lakini inatajwa kuwa ana nyumba raidi ya moja na kwa sasa anafikiria kununua nyumba nyingine Kigali Rwanda.

Kupitia ukurasa wake wa instagram ameonyesha kutaka kuishi Kigali Rwanda tofauti na kuwa na nyumba Afrika Kusini na Tanzania Diamond amepost picha ya mji fulani na kuandika “natafuta nyumba ya kununa Kigali nyumba yangu ya baadae kwa ajili ya simbas !! familia yangu ya Rwanda mna mchango wowote??

Utovu wa Nidhamu Wamponza Chirwa Afungiwa na Kupigwa Faini na TFF

$
0
0
 Makosa ya Utovu wa Nidhamu Yamponza Afungiwa na Kupigwa Faini na TFF
Kamati ya nidhamu iliyokutana  Jumapili, Januari 14, 2018 imepitia kesi ya mshambuliaji wa Yanga SC, Obrey Chirwa iliyowasilishwa na Bodi ya Ligi iliyohusu mchezo namba 83 kati ya Yanga na Tanzania Prisons ya mbeya iliyochezwa Novemba 25, 2017 Uwanja wa Azam Complex imemfungia michezo mitatu mchezaji huyo kwa makosa ya utovu wa nidhamu.

Chirwa alishtakiwa kwa kosa la kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons kwenye mchezo huo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1. Chirwa ambaye alifika kusikiliza kesi hiyo akiwa na mwakilishi wake alikiri kutenda kosa hilo.

Kamati baada ya kumsikiliza Chirwa na kupitia Video za mchezo huo pamoja na taarifa ya kamishna  na Muamuzi imetoa adhabu kwa mchezaji huyo kupitia Kanuni za Ligi Kuu kanuni ya 37 (7b) na kanuni za nidhamu za TFF kifungu cha 48(1d) na 48(2).

Chirwa amefungiwa mechi tatu na anatakiwa kulipa faina ya Tsh. 500,000 kutokana na kosa la kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Novemba 25, 2017 kwenye uwanja wa Azam Complex.

kwa mujibu wa taarifa iliyotelewa na TFF, adhabu hiyo imetolewa baada Chirwa kukiri kufanya kosa hilo la kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons.

Michezo mitatu ambayo Chirwa ataikosi ni Yanga vs Mwadui (Januari 17, 2018), Yanga vs Njombe Mji (Januari 21, 2018) na Yanga vs Majimaji (Januri 28, 2018) mechi zote Yanga itacheza kwenye uwanja wake wa nyumbani (Uhuru).

Shilawadu Watibua Harusi ya Shilole ....Ahaidi Kupeleka Ubuyu kwa Shilole na Uchebe Ili Kukuza Kibamia

$
0
0
Shilawadu Watibua Harusi ya Shilole ....Ahaidi Kupeleka Ubuyu kwa  Shilole na Uchebe Ili Kukuza Kibamia
KUFUATIA sherehe ya harusi ya msanii wa muziki Biongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ na Ashraf Uchebe iliyofanyika Hekima Garden, Mikocheni jijini Dar, Mtangazaji wa Kipindi cha Shilawadu cha Clouds TV, Soudy Brown aliyekuwa miongoni mwa waliofika katika hafla hiyo, kama kawaida yake hakuacha kutia mbwembwe zake kwa maharusi huku akiwaacha waalikwa wakiangua vicheko kila alipozungumza.

Katika sherehe hiyo iliyofurika wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva na Bongo Movies, Soudy alitamba kumnunulia suti bwana harusi (Uchebe) huku akiahipi pia kupeleka ubuyu kwa wanandoa hao kila siku kwa muda wa mwaka mmoja huku akieleza kuwa ubuyu huo hukuza vibamia kuwa bilinganya jambo ambalo kila mtu alilipokea kwa hisia tofauti ukumbini hapo.



Muswada wa Umri wa Kustaafu Kujadiliwa Bungeni

$
0
0
Muswada wa Umri wa Kustaafu Kujadiliwa Bungeni
Vikao vya kamati za Bunge vimeanza huku miongoni mwa miswada itakayojadiliwa ikiwa ni ule utakaoongeza umri wa kustaafu kwa lazima kutoka miaka 60 hadi 65 kwa maprofesa, wahadhiri waandamizi na madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu wa umma.

Marekebisho hayo yapo katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba Tano wa Mwaka 2017 ambao utazihusisha sheria tano ikiwamo ya Utumishi wa Umma sura namba 298 ambapo kifungu kipya cha 25A kitaongezwa.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria inayoongozwa na Mohamed Mchengerwa ndio itakayojadili muswada huo ambao utahusisha pia sheria nyingine tano.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju lengo la kuongezwa kwa kifungu hicho ni kuweka kwenye masharti ya umri wa kustaafu kwa watumishi wa umma ambayo hayapo kwenye sheria ya sasa.

“Mapendekezo ya kuongeza kifungu kipya yanalenga kuweka utaratibu mpya wa umri wa kustaafu kwa maprofesa na wahadhiri waandamizi wa vyuo vikuu vya umma na madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu wa hospitali za umma,” alisema.

Alisema mfumo huo mpya unalenga kuongeza umri wa kustaafu wa utumishi wa umma kwa ridhaa kwa maprofesa na wahadhiri waandamizi wa vyuo vikuu vya umma na madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu wa hospitali za umma ili uwe 60 kwa wale wanaostaafu kwa hiari badala ya 55 wa sasa.

Pia, mfumo huo unalenga kuongeza umri wa kustaafu kwa lazima uwe miaka 65 badala ya sasa wa miaka 60 ya sasa.

“Marekebisho haya yanalenga kutekeleza maamuzi ya Serikali yanayolenga kuongeza umri wa kustaafu kwa maprofesa, wahadhiri waandamizi wa madaktari bingwa wa binadamu kutoka vyuo vikuu vya umma na hospitali za umma,” alisema.

Masaju alisema katika maelezo ya muswada huo kuwa kuongeza umri kwa kada hizo kutapunguza gharama kwa Serikali ya kuingia mikataba na wataalamu hao mara wanapostaafu.

Alisema pia uamuzi huo utaongeza muda kwa wataalamu wengine kulitumikia Taifa kwa muda mrefu zaidi na pia kufundisha na kukuza wataalamu wachanga walioko chini.   


Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>