Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Maskini!... Radio Hali Yake Bado Mbaya Baada ya Kupoteza Fahamu Kutokana na Kipigo

$
0
0
Maskini Radio Hali Yake Bado Mbaya Baada ya Kupoteza Fahamu Kutokana na Kipigo
Msanii wa muziki wa nchini Uganda Moses Nakintije Ssekibogo maarufu kama Radio, bado anaendelea kupigania uhai wake kwenye hopsitali ambayo amelazwa nchini humo, baada ya kupoteza fahamu kutokana na kipigo.

Taarifa kutoka kwa uongozi wake umesema Radio bado hajitambui ingawa ameanza kutingisha vidole, na hadi sasa ameendelea kuwa kwenye comma akipigania uhai wake

"Sasa hivi anaweza kutingisha vidole, anapigana sana sasa hivi ingawa madaktari hawataki atoke kwenye comma sasa kutokana na reaction ya mwili, inaweza ikaleta madhara kwenye dawa anazotumia, hivyo anahitajika kupumzika", umesema uongozi huo.

Radio alipata comma baada ya kupigwa na watu ambao hawajajulikana mpaka sasa kwenye ugomvi, alipokuwa akitoka kwenye hoteli moja mjini Kampala akiwa kwenye parking ya gari, na kupoteza fahamu.

Wasanii mbali mbali wa nchini humo wamekuwa wakipost kwenye mitandao yao ya kijamii, kumuombea aweze kupona haraka.


Chadema Yapeleka Mashtaka Kumshtaki Mkuu wa Wilaya ya Siha Buswelu

$
0
0
Chadema Yapeleka Mashtaka Kumshtaki Vuswelu
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga leo kupeleka mashataka yake katika Kamati ya Maadili kumshataki , Onesmo Buswelu ambaye alishiriki kufanya kampeni kumnadi mgombea wa CCM jimbo la Siha.


Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amethibitisha hilo na kusema kuwa leo majira ya saa tano asubuhi watafikisha mashtaka yao kwenye Tume ya Maadili kama ambavyo wameshautiwa na Tume ya Uchaguzi (NEC).

"Tunapeleka mashtaka leo kwenye kamati ya maadili, tulipanga kupeleka saa tano asubuhi kwa hiyo mashtaka yatakwenda muda huu kumshtaki rasmi Mkuu wa Wilaya" alisema Mrema

Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu alipanda jukwaani kumnadi mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Siha, Dk Godwin Mollel, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu kwani Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa mikoa na Wakurugenzi hawapashi kushiriki katika masuala ya siasa, na hii imetokea ikiwa tayari Tume ya Uchaguzi ilishatoa onyo kwa viongozi hao kutothubutu kushiriki katika masuala ya sias

Bushoke Akana Taarifa za Yeye Kugombana na Q-chief

$
0
0
Bushoke Akana Taarifa za Yeye Kugombana na Q-chief
Msanii Bushoke ambaye aliwahi kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Bongofleva katika kipindi cha nyuma amefunguka na kukana taarifa za yeye kugombana na Q-chief na kudai wanaweza kutofautiana lakini siyo kuzinguana kabisa.


Bushoke ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuwepo fununu kuwa wakongwe hao kwa sasa ni kama paka na panya licha ya kuwa karibu hapo awali na hata kurekodi wimbo mmoja studioni lakini mpaka sasa kazi hizo zimefungiwa studio.

"Some times' tunaweza kutofautiana lakini siyo kivile kwa hiyo namshukuru Mwenyezi Mungu yaani tupo karibu hata huko kutofautiana inawezekana mmoja wetu siku ameamka vibaya kwa hiyo ndio vitu hivyo lakini kugombana hatujawahi", alisema Bushoke. ambaye aliwahi kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Bongofleva katika kipindi cha nyuma amefunguka na kukana taarifa za yeye kugombana na Q-chief na kudai wanaweza kutofautiana lakini siyo kuzinguana kabisa.

Bushoke ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuwepo fununu kuwa wakongwe hao kwa sasa ni kama paka na panya licha ya kuwa karibu hapo awali na hata kurekodi wimbo mmoja studioni lakini mpaka sasa kazi hizo zimefungiwa studio.

"Some times' tunaweza kutofautiana lakini siyo kivile kwa hiyo namshukuru Mwenyezi Mungu yaani tupo karibu hata huko kutofautiana inawezekana mmoja wetu siku ameamka vibaya kwa hiyo ndio vitu hivyo lakini kugombana hatujawahi", alisema Bushoke.

Mwanakwaya Afariki Dunia Wakati Akiwa Anatoa Sadaka

$
0
0
Mewanakwaya Afariki Dunia Wakati Akiwa Anatoa Sadaka
Mwanakwaya wa kwaya ya Mtakatifu Secilia, Kigango cha Muze Parokia ya Zimba, Jimbo Katoliki Sumbawanga, Flora Nandi (25) ameanguka na kufariki dunia muda mfupi baada ya kutoa sadaka ya shukrani akiwa kanisani.

Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita saa nne za asubuhi wakati wa ibada ya kwanza wakati kwaya ya Mtakatifu Secilia ilipokuwa ikimsifu Mungu katika ibada hiyo.

Akizungumzia tukio hilo, mwalimu wa kanisa aliyekuwa akiongoza ibada hiyo, Katekista Philipo Lupadasi alisema wanakwaya wakiwa wanaimba na marehemu akiwa ametoka kutoa sadaka ya shukrani alirejea katika sehemu yake kwenye kwaya na kuendelea kuimba lakini ghafla alianguka chini hali iliyozua mshtuko na kusababisha ibada kusimama kwa muda.

Alisema wanakwaya wenzake walimnyanyua na kumtoa nje ya kanisa ili apate hewa wakiamini kuwa amepoteza fahamu. Katekista huyo alisema baada ya kumpepea kwa muda, waliona hapati fahamu hali iliyowalazimu kumpeleka Zahanati ya Kijiji cha Muze kwa ajili ya matibabu.

Alisema baada ya kufikishwa katika zahanati hiyo alipokewa na wahudumu wa afya ambao baada ya kumfanyia uchunguzi walibaini kuwa alikuwa ameshafariki dunia.

Baada ya kupewa taarifa za kifo hicho, wanakwaya hao waliangua kilio na hawakuweza kurudi tena kanisani kuimba katika ibada ya pili na badala yake waliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka nyumbani kwake kwa taratibu za mazishi.

Mwalimu wa kwaya hiyo, Aloyce Mwandanje alisema kuwa kifo cha mwanakwaya mwenzao ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi mitano, kimewaachia majonzi makubwa lakini hawana la kufanya kwa kuwa ni mapenzi ya Mungu.

Alisema mwili wa marehemu Nandi ulizikwa Jumatatu katika makaburi ya Kijiji cha Muze.

CUF Yajigamba Kumwangusha Mtulia Ubunge Kinondoni

$
0
0
CUF Yajigamba Kumwangusha Mtulia Ubunge Kinondoni
Mkurugenzi wa Habari Uenezi (CUF),Abdul Kambaya amesema kuwa watashinda Jimbo la kinondoni kwasababu katika Jimbo hilo Chama hicho kipo kwa muda mrefu sana.

Akizungumza na Azam News, Kambaya amesema kuwa kiasili Jimbo hilo kiasili ni la watu maskini hivyo lazima washinde katika jimbo hilo.

“Baada ya Mtulia kuhama tutashinda kwasababu Kinondoni ni Jimbo kiasili ni jimbo la watu maskini sana ni chama cha CUF kipo muda mefu sana, chama cha CUF kina madiwani katika Kata 3 kati ya Kata 10 zilizopo pale wenzetu Chadema wana Kata mbili pale na hizo wamezipata kwa hayo hayo wanayoyaita maridhiano,“ alisema Kambaya.

“Mgombea tunae mnadi ni mzaliwa wa Kinondoni Jimbo la Kinondoni mkazi wa Kinondoni mpiga kura wa Kinondoni tangu tofauti na mgombea aliyeletwa na Chadema mpiga kura w kikwajuni lakini wapiga kura wa Kinondoni wanaweza kupima kama angelikuwa anahitaji maslahi ya Kinondoni tangu 2015 angegombea Kinondoni akawa mpiga kura wa Kinondoni kwa msalahi ya wana kinondoni maslahi ya Salum Mwalimu ni ya Kikwajuni na kwa upande wa Zanzibar jambo ambalo si baya kisheria anaruhusiwa kwahiyo utashi wake wa kwanza ni Kikwajuni wa pili labda ndio Kinondoni kwahiyo wanakinondoni sio spear tairi kwamba ikiharibika hii unapachika nyingine hapana wanamjua mgombea wao wanamjua mtu ambaye watampigia kura.“

Mbowe Atua Mbeya Kusikiliza Kesi ya Sugu

$
0
0
Mbowe Atua Mbeya Kusikiliza Kesi ya Sugu
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Aikael Mbowe, leo amefika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga.

Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anakabiliwa na kesi kutoa maneno ya uchochezi.

"Nabii Tito 'Amwambia Kamanda "Mimi Ninatumia Biblia Nayosema Yanatoka Huko"

$
0
0
Jeshi la Polisi Dodoma limemkamata mtu mmoja Tito Machibya maarufu kama Nabii Tito mwenye umri wa miaka 44 kwa kosa la kueneza chuki ya kidini  dhidi ya watu wengine kinyume cha sheria. Kamanda wa Polisi Gilles Muroto amezungumza na Waandishi wa habari na kuelezea yote kwa undani

VIDEO:

Mamia ya Wanafunzi Wachomana Visu Katika Vurugu za Kidini Kenya

$
0
0
Mamia ya Wanafunzi Wachomana Visu Katika Vurugu za Kidini Kenya
Mamia ya wanafunzi nchini Kenya katika shule ya Sekondari ya Jamhuri jijini Nairobi wapo katika hali mbaya ya kiafya baada ya usiku wa jana kutokea vurugu ya kidini kwenye shule hiyo.

Taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini Kenya zinaeleza kuwa wanafunzi hao walikuwa wakizozana kati ya Waislamu na Wakristo.

Kwenye mzozo huo Wanafunzi wa dini ya Kiislamu walikuwa wanawalazimisha wenzao wakristo kubadilisha dini (Kuslimu) na ndipo vurugu zilipoanzia.

Taarifa za awali zinaelezankuwa vurugu hizo zimetoa usiku wa kuamkia leo na mamia ya Wanafunzi wamejeruhiwa kwa kuchomwa visu huku vitanda na madawati yakivunjwa kwenye vurugu hizo.

Hata hivyo tayari Jeshi la Polisi jijini Nairobi limefika shuleni hapo asubuhi hii kufuatilia tukio hilo ili kutoa taarifa rasmi idadi ya wanafunzi waliojeruhiwa.

Full Story kuhusu Nabii Tito wa Kanisa la Walevi..Mtazame Hapa Akigombana na Watu Mtaani

$
0
0
Tazama full story kuhusu mtu anayejiita Nabii Tito, wa kanisa la walevi ambaye ameibuka upya mkoani Dodoma. VIDEO:

Rais wa TFF Ametuma Salamu za Rambirambi kwa Kufuatia Msiba wa Kocha wa Mwadui

$
0
0
Rais wa TFF Ametuma Salamu za Rambirambi kwa Kufuatia Msiba wa Kocha wa Mwadui
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Jumanne Ntambi na wachezaji wa Mwadui kwa kuondokewa na kocha wao usiku wa kuamkia leo huku akiwataka wafiwa wawe na moyo wa subira


Rais Karia amesema hayo katika salamu zake zilizotolewa rasmi na Shirikisho hilo huku akisema ameshtushwa kupata taarifa hizo kwani marehemu Ntambi alikuwa na mchango mkubwa katika soka la Tanzania.

"Kifo cha Kocha Ntambi kimenishtua sana na kwa niaba ya Shirikisho natoa pole kwa wafiwa, nawaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu kwao kumpoteza mpendwa wao. Hakika alikuwa kocha aliyejitahidi kuibua vipaji na amekuwa na mchango mkubwa katika mpira wa miguu ambao bado alikuwa anautumikia mpaka kifo chake," alisema Rais Karia.

Enzi za uhai wake Jumanne Ntambi aliwahi kufundisha timu za Kahama United ya Shinyanga, Mlale JKT ya Ruvuma, Panone ya Kilimanjaro, timu ya mkoa wa Shinyanga Igembe Nsabo na mpaka mauti yanamkuta alikuwa akiifundisha Mwadui ya Shinyanga akiwa kocha msaidizi.

Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo ya Kiume ( Super Shafti)

$
0
0


DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO YA KIUME ( SUPER SHAFITI) NI DAWA YENYE UWEZO MKUBWA WAKUTIBU UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME


 (SUPER SHAFITI ni dawa ya asili yenye uwezo mkubwa wa kuogeza nguvu za kiume maradufu
(1) itakufanya uwe na nguvu za ajabu ukiwa unafanya ntedo la ndoa
(2) inaogeza hamu ya kurudia ntedo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka
( 3) itakufanya uchelewe kufika kileleni dani ya dk 30
( 4)  itaimalisha milija ya uume iliyo legea au kusinyaa
(5) lnarefusha na kunenepesha uume saizi utakavyo kuazia ichi 1-8 unene sm 2-4
 (6) itakupa nguvu za kusimamiasha uume wako barabara kama_ msumari wakati wa ntedo la ndoa
(7) inasaidia kusafisha mishipa. ya kwenye uume na hivyo kusaidia Katika kuongeza kasi ya msukumo wa damu kwenye mishipa ya uume
(8) usaidia kuurudisha nje uume ulioingia ndani
(9) inasaidia kuogeza manii nyingi ambazo vina viini vya uzazi
(10)usaidia kutibu madhara ya punyeto ,matumizi makali ya  madawa ya kizugu mirungi bangi na sigara

KWA NINI BAADHI YA WANAUME WENGI WANA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA KUWA NA MAUMBILE MADOGO YA KIUME NINI CHANZO CHAKE? 

ni kutokana na magonjwa megi kuongezeka yakiwemo kisukari presha ya kupanda na kushuka upigaji wa punyeto wa mda mrefu magonjwa ya moyo ngiri ya kuviba korondani vidonda vya tumbo
Msongo wa mawazo  tumbo kuuguruma kujaa ngesi kutopata choo vinzuri maumivu ya mgongo kiuno na tumiaji wa madawa makali ya kizungu ya kuongeza nguvu za kiume kuzaliwa na chango linaloshabulia neva za ukuwaji wa uume utumiaji wa mirungi bangi sigara na nk  tunapenda kuwatangazia wasomaji, wa makala zetu kuwa tunazo dawa nzuri za asili ambazo hazina mazala na zinazotibu na kuponyesha matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na maumbile ya kiume

NA TUNATIBU MAGONJWA YOTE SUGU KAMA KISUKARI PRESHA AINA YOTE UGONJWA WA MOYO SITRUKO KWIKWI KICHOMI MINGUU KUFA NGAZI ASIMA NK MZEE ISAYA ANAPATIKANA MAGOMENI MIKUMI KARIBU NA KANISA  TUMAINI HEBRAST CLINI NDIYO JIBU NA SULULISHO YA MATATIZO YOTE

PIGA simu 0745495181 au 0682644040

Kwa watu wa mikoa huduma utatumiwa na watu wa nje ya nchi utazipata dsm kama huna nafasi ya kufika ofisini kwetu utaletewa popote ulipo

Sanchez Amponza Henry, Mashabiki Wataka Sanamu lake livunjwe

$
0
0
Alexis Sanchez anazidi kuleta habari nyingi tangu ajiunge Manchester United, na sasa mshambuliaji huyo wa Chile amemuweka katika wakati mgumu mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thiery Henry.

Moja kati ya mambo ambayo Sanchez amesema wakati akijiunga na Manchester United ni ushauri alioupata kwa Thiery Herny ambapo Sanchez amedai kuzungumza na Henry kabla ya kuondoka.

Sanchez amesema Thiery Henry aliona ni sawa tu kwa yeye kuondoka Arsenal na Sanchez aliamua kufuata ushauri wa Thiery Henry na kuamua kuondoka Arsenal.

Mashabiki mtandaoni hii leo wengi wamekuwa wakimtupia Henry lugha chafu na wengine wakisema hawataweza kumtambua tena Thiery Henry kama legend wa timu ya Arsenal.

Mashabiki wengi wamedai kwamba Henry amekuwa akiwageuka mara nyingi na wengine wakikumbushia kwamba juzi tu aliwahi kumsifia Harry Kane wakati Tottenham ni wapinzani wao.

Sasa mashabiki wa Arsenal toka pande mbalimbali duniani wamekuwa wakiomba klabu ya Arsenal kuvunja sanamu la mchezaji huyo lililoko nje ya uwanja wa Emirates kwa kuwa Henry ni msaliti.

Idriss Sultan 'Kenya Wanatuzidi Kwa Kutengeneza Satellite yao na Tuzo za Oscar ila Kwa Umbea na Instagram Followers Hawatakaa Watukute'

$
0
0
Muigizaji wa filamu ambaye siku  zijazo anatarajia kwenda kuigiza katika filamu ya ‘The Blue Maurtius’ Idris Sultan, ametoa neno kwa Watanzania kuhusiana na majirani zetu Kenya kupata nafasi katika tuzo za filamu za Oscar.



Idris ametoa maneno katika mtandao wa Twitter na huku akionyeshwa kukerwa na baadhi ya watu wanaopenda umbea kuliko kazi.

“Kenya imepata Oscar award moja ya Lupita, imekua nominated Oscar award nyingine movie ya WATU WOTE na sasa wamefanikiwa kutengeneza satellite yao ya kwanza. Kwa kifupi watafanya yote ila hawatakaa watukute kwa instagram followers, sisi ndio noma. Satellite ndo nini ? Ina umbea ?,” ameandika Idris.

Washiriki wa tuzo za Oscar mwaka 2018 walitajwa hapo jana huku upande wa Afrika Mashariki imetoa filamu moja iitwayo iiywayo ‘Watu Wote/All of Us’ kutoka Kenya ambayo inazungumzia shambulizi la kigaidi la Al-shabaab lililotokea nchini Kenya mwaka 2014 katika eneo la Mandera ambapo watu 28 waliuawa kwenye tukio hilo.

Tabia ya Mwanamke Asiyewasjibika Kitandani

$
0
0
Inasemekana wanawake wengi wenye ndoa wanakuwa na tabia zifuatazo zinazosababisha waume zao kwenda nje ya ndoa na wale wasio na tabia ya nyumba ndogo wanaishia kubakwa na waume zao

*Mwanamke asiyemtamkia kabisa mumewe kuwa anajisikia kuwa naye.
*Mwanamke ambaye baada ya mechi huwa haonyeshi dalili yoyote kama ameridhika na tendo au hakuridhika
*Mwanamke ambaye akiwahi kulala yeye mume akija hataki kuguswa
*Mwanamke ambaye mumewe akimgusa anakubali huku analalamika .. kama ulikuwa unataka kwa nini hukuwahi kulala unangoja nilale ndo unakuja kunisumbua..
*Mwanamke huyo hatingishiki kwenye mechi kata kidogo tena amenuna... anangalia kushoto au kulia anangoja goli liingie ... kama golikipa aliyekata tamaa ya kudaka penati......
*Mwanamke haweki kabisa maandalizi kama zana za kufanyia usafi baada ya mechi kama taulo, kitambaa nk

Ziko nyingine nyingi ambazo ni kero zinazowafanya wanaume kusononeka....na mara nyingine juamua kuzira na kuwa mwanzo wa mmoja kuhama chumba..... Wanawake wenye tabia hizi jirekebisheni

Pius Msekwa: Ni Vigumu Kuzuia na Kuondoa Rushwa

$
0
0
Pius Msekwa: Ni Vigumu Kuzuia na Kuondoa Rushwa
MWANASIASA mkongwe nchini, Pius Msekwa, amesema ni vigumu kuzuia na kuondoa rushwa nyakati za uchaguzi kwa sababu za ugumu wa kimazingira ya ushahidi kwani mara nyingi vitendo hivyo hufanywa na watu waliokubaliana.



Msekwa ambaye ameshika nafasi mbalimbali za uongozi nchini ikiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameyasema hayo leo nyumbani kwake, Oyster Bay Jijini Dar katika mahojiano maalum na Global TV Habari na kuongeza kuwa zinahitajika juhudi za kipekee ili kuondoa tatizo la rushwa katika uchaguzi.

“Siyo rahisi kuizuia rushwa wakati wa uchagzui, kwanza mtoaji na mpokeaji wote wanakubaliana, utawazuiaje? Huwezi kuzuia rushwa kwa matamko, unahitaji kutunga sheria, watuhumiwa wakikamatwa uwe na ushahidi wa kuithibitishia mahakama,” alisema Mzee Msekwa.



Taifa limeshuhudia juhudi kubwa zimeoneshwa na Rais wa jamhuri ya Muunganowa Tanzania kuhakikisha anawadhibiti watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa kwakuwachukulia hatua ikiwemo kuwafikishwa mahakamani.

Hivi karibuni aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Viajana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM) Taifa, Sadifa Juma alikamatwa na TAKUKURU mjini Dodoma kwa tuhuma za rushwa na kufikishwa mahakamani wakati wa mchakato uchaguzi wa viongozi wa  UVCCM.

Ushahidi wa Sauti Dhidi ya Sugu Waruhusiwa na Mahakama

$
0
0
Ushahidi wa Sauti Dhidi ya Sugu Waruhusiwa na Mahakama
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imeamuru ushahidi kusikilizwa ushahidi wa sauti katika kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi  na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanual Masonga.

Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo baada ya mvutano uliotokea jana Jumanne ambapo upande wa utetezi ukiongozwa na mawakili Boniface Mwabukusi na Hekima Mwasipu kuiomba mahakama hiyo kutopokea ushahidi huo kwa madai kuwa  haukidhi matakwa kisheria.

Baada ya uamuzi huo wa kukubali utetezi huo uliotolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite shahidi namba tano katika kesi hiyo upande wa mashtaka Inspekta Joram Magova alitoa ushahidi wa sauti aliyowarekodi Mbilinyi na Masonga kwa kufunga Spika zilizowezesha kusikika kwa ufasaha ndani ya mahakama hiyo.

Awali kabla ya kuanza kesi hiyo ulinzi uliimarishwa katika jengo la Mahakama Kuu Mbeya ambako mahakama hiyo ipo.

Sugu na Masonga wanashtakiwa kwa kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, Desemba 30,2017 katika mkutano wa hadhara walioufanya kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge.

Asubuhi ya leo Jumatano Januari 24,2018 askari waliimarisha ulinzi, huku wakiwazuia wafuasi wa Chadema kuingia katika jengo la Mahakama kusikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Mwakagenda wameingia katika ukumbi wa Mahakama kufuatilia shauri hilo.

Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite.

Serikali Imevunja Mkataba na Wakala wa Majengo TBA

$
0
0
Serikali  Imevunja Mkataba na Wakala wa Majengo TBA

SERIKALI imevunja mkataba na Wakala wa Majengo TBA baada ya kutoa taarifa za uongo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu ujenzi wa majengo ya Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Butiama na halmashauri mpya Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Wiki iliyopita kuwa wakala huyo wa majengo alipewa onyo na Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako baada ya kusuasua kuanza mradi wa Ujenzi wa Madarasa, Ofisi za Chuo Kikuu cha Muhimbili Kampasi ya Mloganzila huku wakiwa wamepewa fedha na Serikali tayari.

Vanessa Mdee Asimulia Alichokerwa kwa Jux

$
0
0
Vanessa Mdee Asimulia Alichokerwa kwa Jux

Malkia wa Bongo Fleva anayefanya vizuri ndani na nje ya nchi, Vanessa Mdee amefunguka na kuweka bayana kwamba alikuwa anakerwa na tabia ya mpenzi wake Jux ya ku-follow wanawake ambao hawaendani nae katika mitandao ya kijamii.

Vanessa ametoa siri hiyo ambayo ilikuwa inamtafuna katika moyo wake kwa kipindi kirefu kupitia kipindi cha 'Planet Bongo ya East Afrika Radio' wakati alipokuwa akifanya mapitio ya albamu yake 'Money Monday', na kusema wimbo wa unfollow ni jambo la kweli ambalo yeye mwenyewe amelipitia katika mahusiano yake na lilikuwa linamkera kupita kiasi.

"Wimbo huu ni stori ya ukweli kabisa ambapo mpenzi wangu alikuwa ananikera na tabia ya ku-follow wasichana wengine katika 'Instagram' ambao nilikuwa siwataki, siwapendi halafu hatuendani nao. Nikawa namuuliza unawa-follow wa kazi gani ? lakini sikuwa napata majibu sahihi", alisema Vanessa.

Pamoja na hayo, Vanessa amedai ameandika wimbo huo kutoka na shida wanazipitia jinsia ya kike (wasichana na wanawake) wanayoipata kwa wapenzi wao pindi wanapotumia mitandao ya kijamii.

Msongo wa Mawazo Husababisha Unene?

$
0
0
Msongo wa Mawazo Husababisha Unene?
Sote tunafahamu nini kinatufanya tunenepe: ulaji wa vyakula vyenye kalori kupita kiasi.

Japo jibu hili ni la kweli, halijibu swali la msingi zaidi - je, ni kwanini watu hula chakula kupita kiasi?

Ni kwa nini wakati mwengine najihisi kula keki ama chokleti licha ya kwamba nafahamu nitajutia baada ya dakika chache zijazo?

Kwa mara nyingi huwa ni tamaa - ama ni kitu chengine kinachoendelea?

Licha ya kwamba nidhamu ni muhimu, kuna ushaidi mwingi kwamba msongo wa mawazo huchangia pakubwa kwa mtu kuongeza kilo za mwili.

Msongo wa mawazo kupita kiasi, huathiri jinsi mtu anavyopata usingizi na viwango vya sukari mwilini. Hali hiyo huongeza njaa na kuzidisha zaidi ulaji wa chakula kwa utaratibu.

Na hali hiyo huathiri zaidi usingizi, hata viwango vikubwa vya msongo wa mawazo huathiri zaidi viwango vya sukari. Kwa muda, huo unaweza kusababisha viwango vikubwa vya mafuta na kisukari aina ya type -2.

Na kuona kile kinachoweza kutokea, Dkt Giles Yeo, mwanachama wa Trust Me ,yeye ndiye daktari wa timu ambayo pamoja na usaidizi wa wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Leeds, aliamua kujiweka yeye mwenyewe kwenye katika hali ngumu ya msongo wa mawazo.

Wanasayansi wa Leeds walianza kwa kumuuliza Giles kufanya mambo tofauti ambayo yangemsababishia msongo wa kiakili.

Walimuweka mbele ya tarakilishi na wakamlazimisha kufanya hesabu ya kuondoa ,17 , kutoka kwa nambari kama 2,043. Na alipokuwa akikosea, waliona akipatwa na hali ya msongo wa mawazo jambo ambalo lilimpatia Giles shida.

Baada ya hapo wakamlazimu kuweka mikono yake kwenye beseni ya maji baridi kwa muda. Kabla na baada ya uchunguzi huo, kikosi hicho cha chuo kikuu cha Leeds wakampima kiwango cha sukari.

Kiwango cha sukari mwilini huongezeka wakati mtu anapokula, na kwa mwenye afya njema kama Giles, kiwango hicho cha sukari hushuka na kuwa kawaida kwa haraka.

Lakini kikosi hicho cha Leeds kilibaini kwamba siku ambayo Giles alikuwa amepitishwa kwenye shida hizo zote, bado kiwango cha sukari kilichukua muda wa saa tatu kurudi katika hali ya kawaida ambayo ni mara sita zaidi katika siku ambayo mtu ametulia bila wasiwasi wowote.

Sababu kuu ambayo husababisha hayo ni kwamba endapo mtu anapata msongo wa mawazo, mwili hujipata ''ukipigana.''

Mwili hudhani uko katika mashambulizi na hutoa glukosi kwenye damu ili kuongeza nguvu kwenye misuli.

Lakini endapo huhitaji nguvu za kukimbia kujiepusha na hatari yoyote ile, basi wengi hutoa insulini ili kuweza kurudisha kiwango cha sukari kwa kiwango cha kawaida.

Ongezeko la kiwango cha insulini na kushukwa kwa kiwango cha sukari humfanya binadamu kuhisi njaa na ndio sababu kuu kumfanya mtu kutamani kula vyakula vya sukari hasa iwapo mtu anakumbana na msongo wa mawazo.

Kitu kama hicho hutokea iwapo hujapata usingizi mzuri usiku. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na watafiti wa chuo kikuu cha King, mjini London imebaini kwamba iwapo mtu akikosa usingizi anauwezo wa kula zaidi ya kalori 385 kwa siku , ambayo ni sawa na kalori iliyoko kwenye keki ndogo.

Watoto pia hupata tamaa ya vyakula vya sukari iwapo hawajalala vizuri, kwenye utafiti mwengine,wa hivi karibuni, watafiti walichukua kikundi kidogo cha watoto wenye umri wa miaka mitatu na minne ambao hulala kila siku mchana na kuwalazimu kutolala mchana mmoja na kuhakikisha wamekaa macho saa mbili zaidi wakati wao wa kwenda kulala kila siku.

Usingizi ni muhimu kwa binadamuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Usingizi ni muhimu kwa binadamu
Siku ya pili ,watoto hao walibugia asilimia 20 ya kalori kuliko kawaida, hasa vyakula vyenye sukari nyingi na waliruhisiwa kulala kwa muda waliotaka.

Na siku ya tatu, bado watoto hao walikula kalori asilimia 14 kuliko kawaida.

Jinsi za kupunguza msongo wa mawazo kila siku?

Kitu cha kwanza, ningependa watu wanashauriwa kupata usingizi wa kutosha. Hili ni rahisi kwa kusema na si kwa vitendo, lakini mamlaka ya huduma ya afya-NHS inatupatia mbinu muhimu za kufuata.

Pia ungejaribu njia ambazo zinazofahamika zinazopunguza msongo wa mawazo kama vile mazoezi, ukulima ama kushiriki mazoezi ya yoga.

Lakini kitu muhimu tulichobaini kwenye utafiti wetu ni kwamba utafaidika iwapo ulifurahia.

Kwa hivyo jaribu kufanya vitu tofauti na uone kile kinachoweza kukufaa.

Hili Hapa Gari la Sanchez Hatari Tupu

$
0
0
Hili Hapa Gari la Sanchez Hatari Tupu
Ukitaja jina la Alexis Sanchez utakuwa unazungumzia benki inayotembe. Hilo ni kutokana na fedha atakazokuwa anapokea kama mshahara wake kwa wiki kwenye klabu yake mpya ya Manchester United.

Katika kuonyesha thamani yake hiyo kama mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika ligi ya Uingereza, Sanchez ameamua kumiliki gari la kifahari zaidi na lenye thamani kubwa.

Gari hilo ni Bentley GT yenye thamani ya paundi 150,000 ambapo ni zaidi ya shilingi milioni 475 za kitanzania.
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images