Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Kitwanga aikosoa Serikali ujenzi wa Reli

$
0
0

Mbunge wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga ameikosoa Serikali ya awamu ya tano na kuitaka iwe na mipango inayoeleweka na si kufanya maamuzi au mipango ya zimamoto.


Kitwanga amesema hayo bungeni na kudai kuwa Serikali haina haja ya kujenga reli nusu nusu ikiwa inaona haina mpango endelevu wenye tija na kuleta matumaini kwa wafanyabiashara na watu wa viwanda.


"Tunahangaika kutengeneza reli na reli inajengwa kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro inawekwa reli ya umeme ila ukishafika Morogoro kuja Dodoma utofauti wa reli kati ya hiyo standard gauge na ya kawaida unatofautiana, sijui sasa unaanza kupakua hiyo mizigo uanze kupakua kwenye ile reli nyingine ya zamani? Mimi nadhani kuwe na mipango ambao unakuwa ni wa jumla utachukua muda lakini unajua tunajenga reli kutoka Dar es Salaam mpaka Kigoma au Dar es Salaam mpaka Mwanza" alisema Kitwanga


Kitwanga aliendelea kusema kuwa; "Lazima kuwa na mipango thabiti tunasema kwamba hicho ni kipindi cha mpito ambacho kitakuwa kinaeleweka kwa wafanyabiashara na watu wenye viwanda nchini ambapo watakuwa na matarajio yanaoeleweka na mipango hii ifuatwe 


"Hakuna sababu ya kuanza kujenga nusu nusu wakati hujui kinachofuatia na huna mpango wa kupata hela, ni vyema ukawa umejipanga kwamba nikitoka Dar es Salaam kufika Morogoro nitakuwa nimepata fedha kutoka Morogoro kwenda Dodoma, Tabora tusiwe na mipango ya zima moto" alisisitiza Kitwanga

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Al Haji Mussa Salimu Ampa ONYO Kali Mange Kimambi

$
0
0

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Al Haji Mussa Salimu amemjibu mwanadada mkosoaji wa mtandaoni Mange Kimambi kwa kudai kuwa huu ndiyo mwaka wake wa mwisho kutumia mikono pamoja na ulimi wake kutukana watu.


Sheikh huyo amesema kwamba kutokana na kitendo hicho cha Mwanadada huyo kumuanika mtandaoni na kumtolea maneno machafu yeye kama kiongozi wa dini atarudi kwenda kushtaki katika mahakama ya mbinguni ambayo haina rushwa.


Kauli hiyo ya Sheikh Mkuu imekuja ikiwa ni siku moja tangu ianze kusambaa picha yake mitandaoni na kuanza kutuhumiwa kuwa anashiriki katika kampeni za uchaguzi mdogo kukisaidia Chama Cha Mapinduzi


"Tutarejea katika mahakama ya mbinguni kwani mahakama ya Mwenyezi Mungu haina rushwa na tutamuuliza  Mwenyezi Mungu kama alimpa Huyu Mange Kimambi mikono kwa ajilli ya kudhalilisha na kuvunja heshma za watu. Amekuwa akiwatukana viongozi wa serikali lakini kwa hekima zao wamemnyamazia kimya.


"Tunamuonya acheze na namba nyingine lakini siyo viongozi wa dini kwani wao wana mahakama ya kushatakia. Huu utakuwa mwaka wake wa mwisho kutumia ulimi au mikono yake kudhalilisha watu".-Al Haji Mussa Salimu .


Hata hivyo Sheikh huyo amesema kwamba wapo watu wengi waliompa rai ya kutomjibu Mange Kimambi  na kwamba kumjibu kwake kutamfanya atukanwe sana lakini amesema kwamba mwanadada huyo aendelee kutukana kwani dua ya mwenye kudhulumiwa haina kizuizi na kama anaishi hapa duniani basi afahamu kwamba hataendelea kuwa salama na amejihalalishia mwenyewe kwa ulimi wake na mikono yake.

Wananchi Watakiwa Kutoa Taarifa Hospitali Zinazotoza Mama Wajawazito

$
0
0

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

Serikali imewataka wananchi kutoa taarifa kuhusu hospitali zinazotoza fedha kwa ajili ya matibabu kwa akina mama wajawazito ili kuweza kuchukua hatua muhimu kukomesha hali hiyo.


Kauli hiyo imetolewa jana Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu  Hawa Chakoma lililohusu matibabu bure kwa mama wajawazito.


Dkt. Ngugulile alisema kuwa mama wajawazito ni moja ya makundi maalumu wanaostahili kupata huduma za matibabu bure kama ilivyooneshwa katika mwongozo na uchangiaji wa huduma za afya wa mwaka 1997.


“Mwongozo umeweka bayana kuwa kina mama wajawazito ni haki yao kupewa huduma zote bila malipo na sio zile tuu zinazohusu huduma za ujauzito katika mwongozo uliopitiwa mwaka 2009/2010 imetamkwa bayana kuwa huduma za afya kwa mama wajawazito ni bure, ikiwa na maana kwamba mara tu mwanamke anapokuwa na ujauzito huduma zote kuanzia kliniki ya wajawazito, pale anapogundulika maradhi yoyote, pamoja na huduma ya kujifungua sanjali na kumuona daktari, kupatiwa vipimo, kupewa dawa na kufanyiwa upasuaji pale inapohitajika kufanya hivyo” alifafanua Dkt. Ndugulile.


Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa Wizara imeanzisha utaratibu wa kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vinavyohitajika wakati wa kujifungua ambapo watapewa akina mama wajawazito wanapokaribia kujifungua.


Hata hivyo, Dkt Ndugulile alisema kuwa kwa sasa kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa akina mama kujifungua katika vituo vya afya ambapo zaidi ya asilimia 60 ya akinamama wanajifungulia kwenye vituo vya afya.


Mbali na hayo, Serikali imezitaka Halmashauri zote nchini kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sera hiyo ili akina mama wajawazito wapate huduma za matibabu bure kama Mwongozo wa Uchangiaji wa mwaka 1997 na Sera ya Afya ya mwaka 2007 inavyoelekeza.

Mgombea udiwani Chadema apatikana akiwa hajitambui

$
0
0

Mgombea udiwani (Chadema) Kata ya Buhangaza, Mchungaji Athanasio Makoti (28) aliyepotea Februari 2,2018 katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hajitambui.


Makoti amepatikana leo Februari 5,2018 saa moja asubuhi, Katibu wa Chadema wilayani Muleba, Elisha Kabombo alisema alitelekezwa na watu wasiojulikana jirani na Hospitali ya Kagondo.


Amesema wananchi waliokuwa wakipita eneo hilo usiku wa kuamkia leo walimuona akiwa kando mwa  barabara ya kuelekea Bukoba, hivyo kumpeleka hospitali.


“Hali yake si nzuri kwa sababu hawezi kuzungumza vyema wala kuketi. Kawekewa dripu za maji. Tuzidi kumuombea,” amesema.


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Isack Msangi amethibitisha kupokea taarifa za kupatikana mgombea huyo. Amesema vyombo vya dola vinamhoji ili kuendelea na uchunguzi.


Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kagondo, Dk Humphrey Batungi alipoulizwa afya ya mgombea huyo amesema ni mapema kuzungumza.


“Ninaelekea kwenye kikao nitafute mchana baada ya dawa anazotumia mgonjwa kufanya kazi na huenda akawa na mabadiliko,” amesema Dk Batungi.


Katibu wa uenezi wa Chadema jimbo la Muleba Kusini na mratibu wa chama hicho jimbo la Muleba Kaskazini, Hamisi Yusufu amesema baada ya kufikishwa hospitali alikutwa na majeraha, huku akizungumza kwa shida.


Amesema mgombea huyo wa udiwani aliwaeleza amenyang’anywa fedha, waliomteka walimfunga kitambaa cheusi usoni na kumtaka asigombee uchaguzi utakaofanyika Februari 17,2018 na amekiri  kuwafahamu baadhi ya waliomteka.


Katika uchaguzi huo anachuana na mgombea wa CCM, Jenitha Tibeyenda na wa NCCR-Mageuzi, Grason Anaseti.

Soma Nafasi Nyingi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo Katika Magazeti

$
0
0

Wasiliana na Mtaalam Chief Sultan Makata...Kumaliza Shida zako zilizoshindikana

$
0
0

CHIEF SULTAN MAKATA
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
CHIEF SULTAN MAKATA ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)

CHIEF SULTAN MAKATA ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..)

Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?
Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda
Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio?
Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo..
Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.
Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.

Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Maalim Hussein Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi..

CHIEF SULTAN MAKATA Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..
Anatibu Kutumia QUR_AN DAWA ZA ASILI YA AFRICA, Dawa za KIARABU NA MAJINI..
ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.

ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI.. HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA. HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..
MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..

Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu..
Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti..

+255 677 805 105 WhatsAPP.
+255 746 426 604 Kupiga.

Fid Q Amuweka Wazi Mpenzi Wake Awapiga Stop Wanawake Wanaomsumbua

$
0
0
Fid Q Amuweka Wazi Mpenzi Wake Awapiga Stop Wanawake Wanaomsumbua
Mkali wa HipHop Bongo Fid Q ameonekana kukamatika kimahaba kwa  mrembo ambaye amemtambulisha nyumbani kwao Mwanza na ameiambia eNEWZ kuwa kwa sasa yupo kwenye mahusiano rasmi.


Fid Q amesema ameamua kupost picha kwenye mitandao yake  ya kijamii ili kupunguza wasichana wengine kumtumia meseji za kumsumbua lakini pia kuwaonyesha mashabiki zake kwamba kwa sasa yupo katika mahusiano rasmi kwani umri wake unaruhusu.

''Nimeamua kuweka mahusiano yangu wazi ili kuzuia usumbufu wa kina dada wanaonisumbua katika mitandao ya kijamii na hata ninapokuwa kwenye viwanja vya starehe na mda wowote kuanzia sasa ninaweza kutangaza ndoa'', amefunguka.

Kwa upande wake mrembo huyo wa Fid amesema hawashangai sana wanawake wanaomtongoza Fid kwenye 'Social network' kwa kuwa mpenzi wake anamuonekano mzuri na ni mwanaume ambaye ameshapitia mambo mengi duniani hivyo anaamini kwamba atakuwa mwanaume bora kwake.

Hii Hapa Orodha ya Majeruhi 11 ya Wachezaji wa Yanga

$
0
0
Hii Hapa Orodha ya Majeruhi 11 ya Wachezaji wa Yanga
Tatizo la majeruhi ndani ya klabu ya Yanga yazidi kuongezeka baada ya sasa kufikia 11 hali ambayo inatishia harakati za kuwania ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu huu.



Kwa mujibu wa taarifa ya daktari wa timu hiyio Edward Bavu amekiri kufikia 11 mpaka sasa.

Wachezaji wetu 11 bado ni majeruhi, ni wazi hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho- Dr Bavu.
@yangasc VS @njombemjifcofficial
1.YOUTHE ROSTAND
2.JUMA ABDUL
3.HAJI MWINYI
4.ABDALLAH SHAIBU
5.ANDREW VICENT
6.PATO NGONYANI
7.YOHANA NKOMOLA
8.THABAN KAMUSOKO
9.HAMIS TAMBWE
10.DONALD NGOMA
11.IBRAHIM AJIB

Lissu Atembelewa na Maofisa wa EU

$
0
0

Lissu Atembelewa na Maofisa wa EU
Maofisa watatu wa Jumuiya ya Ulaya (EU) leo Februari 5,2018 wamemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayeendelea na matibabu nchini Ubelgiji.

Lissu alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30, Septemba 7 mwaka jana na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi alilazwa hadi Januari 6,2018  alipohamishiwa Ubelgiji katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, anakoendelea na matibabu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Februari 5,2018 Lissu amewataja maofisa hao kuwa ni Mkuu wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki katika Wizara ya Nje ya EU, Patrick Simonnet.

Wengine ni Mkuu wa Dawati la Tanzania katika EU, Marta Szilagyi, Vania Bonalbert ambaye ni ofisa wa ubalozi wa EU Tanzania anayeshughulikia masuala ya utawala bora na haki za binadamu na Hortensia May Lyatuu.

Amesema ujumbe wa maofisa hao mbali ya kumjulia hali walifanya mazungumzo ya masuala mbali mbali yanayohusu Tanzania.

Dada Yake Mowzey Radio Akamatwa na Polisi Uganda

$
0
0
Dada Yake Mowzey Radio Akamatwa na Polisi Uganda
Polisi nchini Uganda wamemkamata mtuhumiwa anayehusishwa na mauaji ya mwanamuziki maarufu Mowzey Radio, aliyefariki kutokana majeraha aliyoyapata baada ya mzozo uliotokea kwenye kilabu moja ya usiku '' De Bar'', iliyopo katika mji wa Entebbe.

Wakati wa mazishi yake, mama yake Jane Kasumba aliwalaani wauaji wake imeripotiwa katika magazeti ya Daily Monitor.

Amenukuliwa akisema:

Nimeumizwa sana, sana. Lakini kinachoniumiza zaidi ni kwamba sikuwaona waliomuua mwanangu. Ninawalaani waliomuua mwana wangu. "

"Utawala wa hospitali ya Case wanasikitika kutangaza kifo cha Moses Ssekibogo maarufu kama Mowzey Radio leo tarehe 1 Februari 2018 saa kumi na mbili asubuhi," ilisoma sehemu ya taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Case kuhusiana na kifo chake.

Radio, ambaye jina lake halisi Moses Ssekibogo, alifariki kutokana na majeraha yaliyotokana na kupigwa na mlinzi wa kilabu hiyo ya usiku majuma mawili yaliyopita

Daily Monitor inaripoti kuwa polisi wamewakamata mameneja wa kilabu hiyo kwa mahojiano.

Gazeti la serikali, New Vision imeripot kuwa mamlaka imeifunga kilabu hiyo ili kupisha uchunguzi ufanyike.

Njombe FC Yaionya Yanga "Msitegemee Mteremko Taifa Leo"

$
0
0
 Njombe FC  Yaionya  Yanga  "Msitegemee Mteremko Taifa Leo"
LICHA ya kuhamasika kusaka ushindi kwa udi na uvumba ili kupunguza wigo wa pointi saba inazozidiwa na watani zao Simba, mabingwa watetezi, Yanga, wameambiwa na wapinzani wao Njombe Mji kuwa wasitarajie mteremko katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa mkoani Njombe, mabingwa hao walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji hao ambao walipanda daraja msimu huu sambamba na Singida United na Lipuli FC.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, alisema kuwa huu ni wakati wa lala salama na kilichoko katika mipango yao ni kushinda kila mchezo.

Nsajisgwa alisema kuwa kama watashinda mechi zao zote zilizosalia ikiwamo dhidi ya vinara Simba na Azam FC, anaamini nafasi ya kutetea ubingwa wanaoushikilia itawezekana.

Beki na nahodha huyo wa zamani wa Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, alisema mechi zote za ligi ni ngumu na wamejiandaa kukabiliana na ushindani kutoka kwa timu zote 16 zinazoshiriki ligi hiyo.

"Wachezaji wetu wanafahamu ugumu na ushindani uliopo katika ligi, tunawakumbusha kupambana katika dakika zote 90 kwa sababu tunaamini hakuna mechi nyepesi, kuhusu majeruhi, tunajua tutakavyoipanga timu na kila mchezaji aliyesajiliwa ana uwezo wa kuitumikia Yanga," alisema kocha huyo.

Kwa upande wa Kaimu Kocha Mkuu wa Njombe Mji, Mrage Kabange, alisema jana kuwa wamekuja Dar es Salaam kushindana na kuondoka na pointi.

"Haijalishi tunacheza ugenini, mpira hauna hivyo siku hizi, kikubwa tunaifahamu Yanga na tumejipanga kupambana nao uwanjani na si kuangalia ukubwa wa jina la klabu yao," alisema Kabange.

Baada ya mechi ya leo, Yanga itaendelea na maandalizi ya kuwakabili St Louise kutoka Shelisheli katika mchezo wa raundi ya awali ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mzigo wa Madeni Yaiandama Tanesco

$
0
0
Mzigo wa Madeni Yaiandama Tanesco
BUNGE limeitaka serikali kulisaidia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kulipa madeni ya mabilioni ya shilingi yanayolikabili kiasi cha kulifanya lishindwe kujiendesha kwa ufanisi.

Agizo hilo lilitolewa bungeni mjini hapa jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Deogratius Ngalawa, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya shughuli za kamati yake kwa kipindi cha Januari 2017 hadi Januari, 2018.

Alibainisha kuwa hadi Desemba 31, shirika lilikuwa linawadai wateja wake ambao ni serikali na taasisi zake pamoja na wateja binafsi Sh. bilioni 277.4. Wateja binafsi wanadaiwa Sh. bilioni 83.8 wakati serikali na taasisi zake likiwamo Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) wanadaiwa Sh. bilioni 193.7.

Alisema pamoja na Tanesco kudai kiasi hicho cha fedha kwa wateja wake, kufikia Desemba 31, yenyewe ilikuwa inadaiwa na wazabuni Sh. bilioni 913.

"Kwa mwaka wa fedha uliopita, serikali ilitenga Sh. bilioni 293.41 kwa ajili ya maendeleo ya Tanesco, lakini hadi Desemba 31 (nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18), shirika lilikuwa limepokea Sh. bilioni 42.1, sawa na asilimia 14 ya fedha zilizotengwa," alisema.

Ngalawa alisema kamati yake imebaini madeni ya Tanesco yanasababisha kuzorota kwa utendaji wa shirika na yamekuwa yakiongezeka na hakuna jitihada za serikali kusaidia kumaliza madeni hayo.

Alisema kamati yake pia imebaini Tanesco inaingia gharama kubwa za uzalishaji wa umeme kutokana na kutumia mafuta hasa kwenye maeneo ambayo hayajaunganishwa na gridi ya taifa.

Alisema hali ya upatikanaji wa umeme nchini bado ni changamoto katika baadhi ya maeneo hasa Mkoa wa Dar es Salaam ambako nishati hiyo imekuwa si ya uhakika na kuathiri uchumi wa wananchi, akibainisha kuwa tatizo la miundombinu chakavu limechangia hali duni ya upatikanaji umeme wa uhakika nchini.

"Bunge linaishauri serikali kutenga na kupeleka fedha za kutosha kwa Tanesco kuiwezesha kuifanya matengenezo mitambo ya kufua umeme na miundombinu ya umeme nchini, hivyo kuepusha adha ya ukosefu wa umeme na kusababisha hasara kwa taifa," alisema.

Mahakama Yaagiza Nabii Titto Apime Upya Akili

$
0
0
 Mahakama Yaagiza Nabii Titto Apime Upya Akili
MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma imeagiza mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya Dodoma Tito Machibya, maarufu kama ‘Nabii Tito’ (45) kupimwa akili upya katika Taasisi ya Afya ya Akili ya Mirembe Isanga mkoani Dodoma ili kuriridhisha kama ana matatizo ya akili.


Licha ya kuagizwa mtuhumiwa huyo kufanyiwa vipimo upya, mahakama pia imetaka kuwasilishwa kwa vielelezo kama kweli ana tatizo hilo kama alivyoieleza mahakama.

Nabii Tito anashtakiwa kwa kosa la kujaribu kujiua kwa kutumia wembe.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha, alisema jana kuwa kutokana na mshtakiwa kuieleza mahakama kuwa ana matatizo ya akili na alifanya tukio hilo kutokana na kusikia vitu ambavyo vilikuwa vinamwamuru akate, mahakama itabidi  ipate vielelezo ambavyo vitathibitisha anachokisema.

Karayemaha alisema kutokana na kifungu namba 219 (2) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, kama mshtakiwa atabainika kweli ana matatizo ya afya ya akili, mahakama itaamua kuwa alivyofanya tukio hilo hakuwa na akili timamu, hivyo hana hatia.

“Mshitakiwa anadai kuwa ana matatizo ya akili na amekuwa akitibiwa katika hospitali mbalimbli ikiwemo ya Maweni.  Mahakama hii inaagiza vielelezo vyake vyote viletwe hapa lakini pia apelekwe kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya ya akili Mirembe Isanga,” alisema Karayemaha.

Pia alisema kama mshtakiwa atabainika kuwa hana tatizo lolote la afya ya akili kwa mujibu wa vielelezo vyake pamoja na vipimo atakavyofanyiwa, atakuwa na kesi ya kujibu.

“Kutokana na hili aliloiambia mahakama kuwa ana matatizo ya akili hata suala la dhamana tunaliweka pembeni kwanza kwa sababu hawezi kujieleza lakini kama itabainika kuwa hana matatizo ya akili kutokana na vielelezo vitakavyoletwa pamoja na vipimo vitakavyofanyika, suala la dhamana litafanyiwa kazi,"alisema.

Hata hivyo alisema mshtakiwa huyo anarudi rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa  Februari 19,  mwaka huu.

Wakati kesi itakapotajwa vielelezo vyote pamoja na vipimo vinatakiwa kuwa tayari vimeshawasilishwa mbele ya mahakama hiyo.

Nabii Tito anashtakiwa kwa tuhuma za kutaka kujiua kwa kujikata na wembe na kujijeruhi kwenye maeneo ya tumbo Januari 25, mwaka huu, katika mtaa huo wa Ng’ong’ona alipokuwa akikaguliwa na polisi.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Madogo?

$
0
0
Matatizo haya yame kuwa yakiwaathiri watu wengi sana kisaikolijia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wenzao kwa kawaida mwanaume ana takiwa awe na uume kuanzia inch(6_8)vinginevyo mtu huyo atakuwa na matatizo.

Zipo sababu nyingi zinazo sababisha tatizo hilo baadhi ni upungufu wa vichocheo (Hormones za Getrogen) Ambazo mwanaume akisha balehe vichocheo hivi huchochea ukuaji wa uume, chango husababisha NEVA ambayo huathiri misuri ya uume. Ngiri ambayo Huleta maumivu ya tumbo kuunguruma na kujaa guess, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri , miguu kufa ganzi, maumivu ya kiuno,upigaji wa punyeto sababu hizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembaba na mara kwa mara hipelekea kupunguka kwa nguvu za kiume na ham ya tendo la ndoa hukosekana na kuisha kabisa

NSUMBU:__Ni dawa dawa inayo zalisha hormones za Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka mara dufu.

NZAGI :--Ni dawa bora ya kurudisha nguvu za kiume na kukupa hamu ya kurudia tendo la ndoa mara dufu utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara nne
(4)bila hamu kuisha (kuchoka) dawa hii ni tiba kamili kwa matatizo hayo. Dawa hii pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk(15_30)kwa tendo moja la ndoa dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji kuanzia miaka(18_90)wana ruhusiwa kuzitumia Pia tunatibu KISUKARI, PRESHA, PUMU, MALARIA SUGU, MIMBA KUHARIBIKA(Chango)

POWER :__Ni dawa ya mitishamba inaongeza hips, (makalio), miguu, ina punguza maziwa (chuchu). Ina toa harufu mbaya sehem za siri Nk.

Pia anazo dawa za mvuto wa mapenzi,biashara, kurudishwa kazini, kumuita aliye mbali kwa mda mfupi tu

OSTADH JUMA ANAPATIKANA MBANGALA ZAKHIEM SIMU: 0769-597778 au 0784-002216 au 0627457957 Wote mnakaribishwa

“Sishangai Kuona John Bocco Anapata Matokeo Mazuri”-Shaffih Dauda

$
0
0
Nahodha wa  Simba John Raphael Bocco ‘Adebayor’ jana Januari 4, 2018 alifunga magoli mawili dhidi ya Ruvu Shooting na kufikisha jumla ya mabao tisa kwenye ligi msimu huu akiwa nyuma kwa magoli matatu dhidi mshambuliaji mwezake Emanuel okwi anaeongoza orodha ya wafungaji akiwa na magoli 12 hadi sasa.

Shaffih Dauda amesema kutokana na anavyomfahamu Bocco hashangazwi kuona mchezaji huyo wa zamani wa azam akipata matokeo mazuri akiwa fit kwa sababu ni miongoni mwa wachezaji wachache wazawa wanaothamini kazi yao.

“Bocco ni moja ya wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu, ni mchezaji ambaye kwa kumfuatilia kwangu na ninavyomfahamu, anaithamini kazi yake. Ni mchezaji anayejua anatakiwa kufanya nini uwanjani na nje ya uwanja.”

“Wakati yupo azam, inatokea wachezaji wamemaliza mazoezi na kupewa mapumziko ya siku mbili nyumbani kabla ya kurejea tena azam complex kuweka kambi kujiandaa na mechi, bocco alikuwa anabaki azam complex anaendelea kujifua mwenyewe, anaungana na vijana wa u20 kufanya mazoezi wachezaji wenzake wakirui baada ya siku mbili wanamkuta anaungana nao.”

“Ubora wa bocco sio kitu kinachokuja kwa bahati mbaya, anawekeza muda na ananidhamu ya juu, ni nahodha ambaye anakuwa wa kwanza katika tukio lolote linalohusu timu. Basi la timu likiwa linaondoka kwenda mazoezini bocco atakuwa ameshakaa kwenye siti zamani, mazoezini na kwenye chakula cha pamoja mara nyingi anakuwa wa kwanza, kwa hiyo sishangai kuona anapata matokeo mazuri  anapokuwa fiti.”

Bocco amekuwa na mwendelezo mzuri wa kufunga mfululizo katika mechi za hivi karibuni, alifunga magoli mawili vs Ndanda, alifunga goli moja vs Kagera Sugar, alifunga magoli mawili vs Majimaji, alifunga magoli mawili vs Ruvu Shooting.

Julius Mtatiro "Taifa Lilimpoteza Nyerere, Limemzika Kingunge

$
0
0
Taifa lilimpoteza Julius Nyerere, taifa limempoteza Kingunge! Kama unafuatilia historia ya taifa letu lazima utakuwa unajua kuwa ni mara chache sana taifa lolote linakuwa na wanasiasa wa haiba hiyo.

Taifa limekuwa na mamia na maelfu ya wanasiasa, lakini Nyerere na Kingunge ni EXCEPTIONAL! Na ukitafuta hao wanasiasa mahsusi na wa kipekee kwa sasa, ni kwa tochi!

Kingunge hakuwa mwanasiasa tu, alikuwa ni STRATEGIST wa hali ya juu. Nakumbuka siku niliyokutana naye ana kwa ana kwa mara ya kwanza nyumbani kwake, ilikuwa miaka 10 iliyopita.

Mimi na wenzangu tulikuwa kwake kumshawishi azungumze na Rais ili serikali ione haja ya kuongeza pesa za kujikimu za wanafunzi. Kikao kile kilikwenda jioni nzima na akakihamisha kesho yake asubuhi.

Mara ya pili kwenda kwake ilikuwa ni kuzungumza naye juu ya namna serikali ilivyokosea kutatua mgogoro baina yake na wanafunzi wa UDSM. Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga anaikumbuka ziara hii vizuri sana.

Mzee Kingunge anakusikiliza dakika 15 au ukipenda dakika 30, unazungumza wewe tu, ukimaliza, anaanza kupitia hoja zako zote na anazigeuzageuza anavyotaka.

Anakuonesha makosa ya serikali, anakueleza makosa ya wanafunzi, anakidadavulia uchuro wa uongozi wa chuo kisha anakwambia atakwenda kuzungumza jambo gani na Rais!

Leo hii hakuna BRAINS kama za Nyerere na Kingunge. Leo kuna hizi BRAINS zetu, za kawaida kabisa, za COPYING and PASTING, za kufoka na kutukana na kupiga risasi na kutisha na kuzuia na kutweza na kuumiza, kunyima dhamana na kufunga, kutafuta ukuu na kutafuta sifa.

Nitakuwa na fursa ya kueleza mengi kwa kina kuhusu ziara mbili ambazo nilishiriki na kuzungumza na mzee huyu muhimu kwa kirefu, nitafanya hivyo kwa njia maalum sana.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Mungu atusaidie tujenge hata robo tu ya uwezo aliokuwa nao Mzee wa taifa.

#Mtatiro J

Kutana na Mchezaji Ambae Ndani ya Misimu Miwili Mchezaji Amepandisha Timu Mbili Ligi Kuu

$
0
0
Songa Betheli ni mshambuliaji aliyeweka rekodi ya kupandisha ligi kuu timu mbili kwa misimu miwili tofauti, msimu uliopita aliisaidia Singida United kupanda daraja kitu ambacho amekifanya tena akiwa na Biashara United ya Musoma mkoani Mara.

Betheli ni miongoni mwa wachezaji walioisaidia singida kupada ligi kuu kwa kufungia magoli mengi timu hiyo lakini baada ya minziro kuondoka Singida United betheli aliondoka pia.

“Kwa sasa ni mchezaji wa Biashara United ambayo tumefanikiwa kuipandisha ligi kuu baada ya kazi ngumu lakini napenda kumshukuru Mungu kwa hilo. Nikilinganisha furaha niliyokuwanayo nikiwa Singida United ni tofauti na hapa Biashara kwa sababu nikiwa hapa nimeweza kuwa na mahusiano mazuri na wachezaji wenzangu, benchi la ufundi pamoja na uongozi mzima hiyo ndiyo tofauti na nilivyokuwa Singida United.”

“Nina uwezo ndio maana nakuwa kwenye timu na ninakuwa na mchango wa kufanikisha timu kupanda daraja, malengo yangu kwa sasa ni kucheza ligi kuu kwa kwa mafanikio kwa sababu umri haunisubiri.”

“Niliamua kutoka Singida United nikaenda Stand United lakini nikajiunga na Biashara katika dirisha dogo ili nije nijifue nifanye vizuri lakini pia nipate ‘title’, malengo yangu niliyojiwekea katika michezo mitano nikiwa Biashara nimeyatimiza, nimefunga magoli manne katika mechi tano nilizocheza, mchezo wa mwisho dhidi ya Transit Camp nimehusika katika magoli yote matatu tuliyofunga. Nimesababisha penati tukafunga goli la kwanza, nikafunga mwenyewe goli la pili nikatoa assist ya goli la tatu.”

“Mipango yangu ilikuwa kuja biashara kwa ajili ya kujifua lakini kwa sasa nitaipa kipaumbele Bishara kwa maana timu nitakayoichezea ligi kuu kama watakuwa tayari kukaa na mimi na kunipa mkataba.”

Songa anaungana na aliyekuwa kocha wake Singida United Fred Felix Minziro ambaye pia ameweka rekodi ya kupandisha ligi guu timu mbili tofauti katika misimu miwili mfululizo.

Mkoa wa Mara utashudia michezo ya ligi kuu Tanzania bara baada ya Biashara United kupanda ligi kuu kutokana na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya transit camp kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi C uliochezwa uwanja wa Karume mjini Musoma.

Breaking news: Joshua Nassari Afikishwa Mahakamani

$
0
0
Breaking news: Joshua Nassari Afikishwa Mahakamani
Taarifa kutoka Arusha zilizotufikia hivi karibuni ni kuhusu  Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru.

Nassari anakabiliwa na tuhuma za shambulio analodaiwa kulifanya kwa aliyekuwa Mtendaji wa Kata ya Makiba mwaka 2014. Mtendaji huyo bado hajatajwa jina lake.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

$
0
0

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

Chadema Yalaani Tukio la Kutekwa kwa Mgombea Wake wa Udiwani

$
0
0
Chadema Yalaani Tukio la Kutekwa kwa Mgombea Wake wa Udiwani
Chadema imelaani tukio waliloliita la kutekwa kwa mgombea wake wa udiwani Kata ya Guhangaza wilayani Muleba mkoani Kagera, Mchungaji Athanas Makoti (28) aliyepatikana jana alfajiri akiwa hajitambui.

Wakati Chadema ikilaani tukio hilo lililotokea Februari 2, aliyekuwa mgombea udiwani wa chama hicho Kata ya Manzase wilayani Chamwino mkoani Dodoma, Mashaka Chalo amejiunga na CCM pamoja na wanachama wengine 131 wa chama hicho cha upinzani.

Wakati Chadema ikisema Makoti alitekwa, polisi juzi ilieleza kuwa taarifa zilizowasilishwa kwao ni kwamba alitoweka baada ya kuondoka nyumbani na kutorejea.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene chama hicho kimelitaka Jeshi la Polisi kuchunguza tukio la kutoweka Makoti ambaye anatibiwa katika Hospitali ya Kagondo, baada ya kuokotwa kando mwa barabara ya kuelekea Bukoba.

“Tangu Makoti alipotoweka Polisi haikufungua jalada la uchunguzi. Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi makao makuu kuingilia kati ili uchunguzi wa haraka kuhusu suala hilo ufanyike,” alisema Makene.

Chama hicho pia kimeiomba Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBU) kutumia mamlaka yake kuhakikisha tukio hilo linafanyiwa uchunguzi wa haraka kuwabaini wahusika na kuchukua hatua.

“Pia tunaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kukemea vitendo kama hivyo ambavyo vinatia doa mfumo wa uchaguzi na demokrasia nchini, ukimya wao unaashiria wanakubaliana na tabia hii mpya ya utekaji ambayo tuliilalamikia hata wakati wa uchaguzi wa marudio wa kata 43, Novemba mwaka jana,” alisema Makene.

Akizungumza na Mwananchi jana, katibu wa Chadema wilayani Muleba, Elisha Kabombo alisema Makoti alitelekezwa na watu wasiojulikana jirani na Hospitali ya Kagondo.

Alisema wananchi waliokuwa wakipita eneo hilo usiku wa kuamkia jana walimuona akiwa kando mwa barabara ya kuelekea Bukoba, hivyo kumpeleka hospitali.

“Hali yake si nzuri kwa sababu hawezi kuzungumza vyema wala kuketi. Kawekewa dripu za maji. Tuzidi kumuombea,” alisema.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Isack Msangi alithibitisha kupokea taarifa za kupatikana mgombea huyo. Alisema vyombo vya dola vinamhoji ili kuendelea na uchunguzi.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kagondo, Dk Humphrey Batungi alipoulizwa afya ya mgombea huyo alisema ni mapema kuizungumzia.

Katibu wa uenezi wa Chadema Jimbo la Muleba Kusini na mratibu wa chama hicho Jimbo la Muleba Kaskazini, Hamisi Yusufu alisema baada ya kufikishwa hospitali alikutwa akiwa na majeraha, huku akizungumza kwa shida.

Alisema Makoti aliwaeleza amenyang’anywa fedha, waliomteka walimfunga kitambaa cheusi usoni na kumtaka asigombee uchaguzi utakaofanyika Februari 17 na amekiri kuwafahamu baadhi ya waliomteka.

Juzi, katika Kata ya Manzase wilayani Chamwino, naibu katibu mkuu wa CCM (Bara), Rodrick Mpogolo alimpokea mgombea udiwani wa Chadema, Chalo alipozindua kampeni za udiwani katika Kijiji cha Manzase.

Chalo amehamia Chadema ikiwa ni siku ya tatu tangu chama hicho kikuu cha upinzani nchini kuzindua kampeni katika kata hiyo, akinadiwa na mbunge wa viti maalumu, Kunti Majala.

Katika mkutano huo, mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde alisema uamuzi wa Chalo kujiuzulu ni ushindi kwa chama tawala.

“Mpogolo unaweza kufungua kampeni hizi na kisha kuzifunga maana kazi imekwisha. Tulikuwa na wagombea watatu, lakini kuondoka kwa huyu, CCM tunaona kazi imekwisha. Wagombea wengine waliobaki hata tukilala usingizi hakuna kitu ushindi ni wetu,” alisema.

Akizungumza katika mkutano huo, Chalo alisema amerejea CCM kwa sababu ni chama chake na kimemlea.

Imeandikwa na Shaaban Ndyamukama (Muleba), Burhan Yakubu (Tanga), na Habel Chidawali (Dodoma).

Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images