Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Nape Nhauye Awamwagia Lawama Usalama wa Taifa

$
0
0
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameibuka na kuituhumu Idara ya Usalama wa Taifa nchini haifanyi kazi zake ipasavyo inavyohitajika na badala yake wamekalia kusikiliza simu za watu wanavyoongea pamoja na kufanya mambo ambayo hayalindi uchumi wa Tanzania.

Nnape ametoa kauli hiyo  jana wakati alipokuwa akichangia bungeni taarifa ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika mkutano wa 10 kikao cha nane cha Bunge mjini Dodoma na kuishauri kamati hiyo ipeleke mapendekezo ili waweze kupitia upya sheria ya Usalama wa Taifa na kuiwezesha mikono yao iende mbali, kukumbuka jukumu lao la kuhakikisha wanalinda uchumi wa nchi katika kipindi hichi, ambacho demokrasia ya siasa inahama na kuelekea kwenye demokrasia ya uchumi ambapo muda mwingi wanapaswa kuutumia huko na sio pengine.

Kutoka na hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni George Mkuchika alimjibu Nape na wabunge wengine kwamba kazi ya Idara ya Usalama wa Taifa sio kutafuta watu waliopotea au kuumizwa kama wanavyodai na laiti wangelifahamu wanachokifanya wangekaa kimya.

"Kazi ya usalama wa Taifa nchi yeyote ni kutafuta habari na kuishauri serikali. Kwa kifupi tu mimi nasema hoja mlizozitoa kuhusu idara kwamba haishauri serikali mambo ya uchumi na mambo mengine hamna ushahidi", alisema Kapteni Mkuchika.

Pamoja na hayo, Kapteni Mkuchika aliendelea kwa kusema "sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996, kazi zilizopitishwa kwa mujibu wa Bunge kuna shughuli nne za idara kwamba ni kukusanya na kutafuta habari pamoja na kuzifanyia tathmini na wanapoyafanya hayo hawayafanyi katika mkutano wa hadhra, kushirikiana na vyombo vya idara nyingine vinashughulikana na usalama wa nchi, kuwashauri Mawaziri ili waishauri serikali na mambo yote ya kuhujumu uchumi na vingine wanayafanya kimya kimya".

Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Taifa zimehairishwa jana jioni (Ijumaa) mpaka Aprili 03 mwaka 2018.

Hatma ya Zitto Kabwe Mikononi mwa Spika

$
0
0
Kuadhibiwa  ama kutoadhibiwa na Bunge kwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) kuko chini ya Spika Job Ndugai baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kukamilisha uchunguzi wa shauri lake.

Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo anakabiliwa na tuhuma za kudharau mamlaka ya Spika kutokana na kauli yake kwamba, "Bunge limewekwa mfukoni na serikali."

Akiwasilisha bungeni mjini hapa jana taarifa ya shughuli za Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kipindi cha kuanzia Januari 2017 hadi Januari 2018, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Almas Maige, alisema tayari wameshakamilisha uchunguzi wa shauri hilo.

Pia alisema kamati yake imeshamshauri Spika hatua za kuchukua kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016.

Maige ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), alisema kuwa katika mkutano wa nane wa Bunge, baada ya Spika kupokea na kuikabidhi serikali taarifa za kamati mbili alizoziunda Julai tano kwa ajili ya kufanya uchunguzi katika sekta ya madini, Zitto aliandika kwenye mtandao wa Twitter maneno ya dharau dhidi ya Spika.

Spika aliunda kamati mbili za kuchunguza na kuishauri serikali kuhusu mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa biashara ya madini ya Tanzanite na almasi.

"Kamati ilifanya uchunguzi wa shauri hili na kukamilisha kisha kumshauri Spika kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge," Maige alisema.

Spika Ndugai hakuongoza kikao hata kimoja katika mkutano wa wiki mbili uliomalizika jana.

Serikali Yawasha Moto Bungeni Kuhusu Madanguro, Biashara ya ngono

$
0
0
Serikali imesema ina andaa mikakati itakayowezesha kudhibiti biashara ya ngono na uwepo madanguro nchini, hasa kwenye maeneo ya mijini.

Hayo yamesemwa jana Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambwe, Khalifa Mohammed Issa aliyehoji juu mpango serikali katika kudhibiti biashara ya ngono na madanguro ili kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini.

Akijibu swali la Issa, Dkt. Ndugulile alisema Serikali inaandaa mikakati mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu kuhusu madhara ya biashara ya ngono kwa jamii pamoja na kuchukua hatua za kisheria kwa wanaojihusisha na baishara hiyo, pamoja na kudhibiti uwepo wa madanguro.

Katika hatua nyingine, Dkt. Ndugulile alisema serikali inaendelea kuchukua hatua katika kudhibiti mila na desturi potofu zinazochangia maambukizi mapya ya VVU, ikiwemo ukeketaji na urithishaji wa wajane kwa ndugu wa mume, kwa kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara ya mila potofu pamoja na kutoa hamasa kwa wakunga wa jadi wanaojihusisha na ukeketaji.

Wabunge Wataka Wapewe Ulinzi, Serikali Yagoma

$
0
0

Bunge limeagiza Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ifanyiwe marekebisho ili kuweka sharti la wabunge kupatiwa ulinzi, hususan katika makazi yao wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu ya kibunge mjini Dodoma na katika maeneo yao ya uwakilishi.

Chombo hicho cha kutunga sheria pia kimeagiza kuweka utaratibu wa kutoa namba maalum za usajili wa magari ya wabunge huku kikiitaka serikali iboreshe na kuimarisha ulinzi katika maegesho ya magari bungeni.

Hayo yalisema na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu, alipowasilisha taarifa ya mwaka ya shughuli za kamati kwa kipindi cha Februari, 2017 hadi Januari, 2018.

Agizo hilo limetoka ikiwa ni takribani miezi minane tangu kushambuliwa kwa kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema).

Rais huyo wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) alipigwa risasi akiwa anajiandaa kushuka kwenye gari lake nyumbani kwake Area D mjini hapa Septemba 7, mwaka jana.

Mpaka sasa, hakuna taarifa ya kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo na Lissu anaendelea na awamu ya tatu ya matibabu yake ya kibingwa nchini Ubelgiji.

Baada ya kutokea kwa tukio hilo, Spika Job Ndugai aliiagiza kamati hiyo kulifanyia kazi na kulitolea taarifa bungeni.

Balozi Adadi alisema katika kipindi cha Novemba mwaka jana, kamati yake ilipokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu udhibiti wa usalama wa viongozi wakiwamo wabunge.

Alisema uchambuzi wao ulibaini viongozi wanaolindwa na Jeshi la Polisi kwa mujibu wa sheria ni viongozi wakuu wa nchi ambao ni Rais na Makamu wa Rais wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu na viongozi wakuu wastaafu.

Alisema wengine ni viongozi waandamizi wa serikali ambao ni mawaziri na manaibu mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na Spika na Naibu Spika wa Bunge.

"Kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi Sura ya 322, wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hupewa ulinzi wa jumla wanapokuwa katika shughuli za bungeni au kwenye safari zao za kikazi," Balozi Adadi alisema na kuongeza:

"Utaratibu huu unaliacha suala la ulinzi na usalama wa wabunge katika makazi yao wakiwa kwenye shughuli za Bunge na kwenye maeneo yao ya uwakilishi kuwa jukumu la mbunge mwenyewe."

Balozi Adadi alisema kazi za wabunge katika kuisimamia serikali zinagusa maslahi ya watu au makundi binafsi ambayo yanaweza kujenga chuki dhidi yao.

Majibu ya Serikali
Katika majibu yake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba, alisema wazo hilo ni zuri lakini nchi inatakiwa kuwekeza kwanza katika kuimarisha miundombinu kabla ya kutoa ulinzi kwa mbunge mmoja mmoja.

Aliongeza kuwa bila kuwa na miundimbinu mizuri, askari watakaopewa jukumu la kuwalinda watunga sheria hao watakuwa kwenye hatari kubwa ya kudhurika na hata kushambuliwa.

Mauaji Kibiti
Alisema kamati yake ilikutana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Septemba na Januari na ikaridhishwa na juhudi za serikali katika kushughulikia matukio mbalimbali ya uhalifu hususani matukio ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji yaliyohusisha mauaji ya viongozi, askari polisi, na raia.

"Nafurahi kutoa taarifa kuwa, kwa kazi nzuri iliyofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo hayo, hali ya usalama sasa ni shwari.

Lakini kamati inasisitiza kuwa ni wajibu wa serikali kuhakikisha kiini cha mauaji hayo kinajulikana na kudhibitiwa ili mauaji ya aina hiyo yasijirudie tena nchini," alisema.

Msongamano wa Wafungwa
Balozi Adadi pia alisema kamati yake imebaini kuna msongamano wa wafungwa na mahabusu magerezani nchini kutokana na kile ilichoona matumizi hafifu ya sheria zinazoruhusu adhabu mbadala kwa wafungwa kama vile kifungo cha nje na mahabusu kutopelekwa mahakamani kwa muda uliopangwa.

Pia kutotumika ipasavyo kwa mpango wa Parole, kasi ndogo ya kusikiliza mashauri yanayohusu mauaji na dawa za kulevya pamoja na kutokutekelezwa kwa adhabu iliyotolewa dhidi ya wafungwa waliohukumiwa kunyongwa.

"Hali hiyo inaathiri afya za wafungwa na mahabusu. Vilevile, kuiongezea serikali gharama za kuwatunza," alisema.

Ajali
Alibainisha kuwa katika kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Desemba, jumla ya ajali 1,428 ziliripotiwa na kati yake, ajali 562 zilisababisha vifo.

Alisema idadi hiyo ya vifo ni pungufu kwa vifo 91 kulinganishwa na idadi ya vifo vya aina hiyo katika kipindi kama hicho mwaka 2016.

Alisema vifo vingi vya ajali vinachangiwa hasa na mwendokasi, kutovaa kofia ngumu, kutofunga mikanda, matumizi ya vilezi, matumizi ya simu za mikononi na matumizi ya vizuizi vya watoto.

Balozi
Mkurugenzi huyo wa zamani wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) pia alisema kamati yake imebaini uchakavu wa majengo ya balozi za Tanzania kutokana na kutofanyiwa ukarabati kwa muda mrefu.

Pia alizungumzia changamoyo ya meli zenye usajili Tanzania kukamatwa nje ya nchi kwa makosa ya kihalifu ambayo ni pamoja na kubeba dawa za kulevya na vifaa vya kutengenezea silaha kali za kivita.

Alisema kamati yake inaishauri serikali kuchukua hatua za haraka kama ilivyoahidi mbele bungeni Mei 2, mwaka jana.

Utekaji na Amri za Wakuu wa Wilaya
Balozi Adadi pia alisema kamati yake ilibaini kumekuwa na ucheleweshaji wa kutoa taarifa rasmi kwa umma kuhusu hatua zilizofikiwa katika upelelezi wa matukio ya muda mrefu na yanayovuta hisia za jamii kama vile matukio ya mauaji, kutekwa na kupotea kwa viongozi na wananchi mbalimbali, unyang'anyi wa kutumia silaha na makosa makubwa ya uhujumu uchumi.

"Kamati pia ilibaini kuwa baadhi ya wakuu wa wilaya wanawaweka mahabusu wananchi na watumishi wa umma kinyume cha matakwa ya kifungu cha 15 cha Sheria ya Tawala za Mikoa ya Mwaka 1997," alisema.

"Ni wajibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Tamisemi kuendelea kuwaelimisha wakuu wa wilaya kuhusu matumizi sahihi ya sheria hiyo ingawa kwa sasa vitendo hivyo vimepungua."

Credit: Nipasher

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU.

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..
na mengi zaidi

+255 622588038au 0679119679 au +255 764318107
NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Serikali Kuwashughulikia Polisi Wanaotesa raia Wakiwa kizuizini

$
0
0
Serikali imeahidi kuwashughulikia Askari Polisi watakao bainika kutesa na kuwapiga raia wakiwa kizuizini, kwa kuwa vitendo hivyo ni kinyume na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kifungu cha 11.

Kauli hiyo imetolewa jana Februari 10, 2018 Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Eng. Hamad Masauni wakati akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Rungwe (Chadema) Sofia Mwakagenda lilohoji kama kuna sheria inayomruhusu Askari Polisi kumkamata mtuhumiwa na kumpiga na kumtesa kabla ya kufikisha kituo cha polisi.

Eng. Masauni alisema serikali kupitia wizara yake imekuwa ikiwachukulia hatua Askari Polisi wanaofanya makosa mbalimbali, ambapo  katika kipindi cha mwezi Januari hadi Disemba mwaka 2017, jumla ya askari polisi 105 waliotenda makosa mbalimbali wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa pamoja na kufukuzwa kazi.

“Kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura 20 kifungu 11 kinaeleza namna ya ukamataji, aidha kifungu hiki mahsusi cha ukamataji hakimruhusu askari kumpiga na kumtesa raia akiwa kizuizuni, kwa mujibu wa kanuni za utendaji wa jeshi la polisi askari yeyote atakayebainika kutesa, kupiga raia akiwa kizuizini huchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi au kufikishwa mahakamani,” alisema.

Mheshimiwa Temba Afunguka Kuhusu Kumfumania Mkewe Ndani ya Nyumba yake Akifanyiwa Kweli

$
0
0
Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka kundi la TMK Wanaume na kiongozi wa Mkubwa na Wanaye Mhe. Temba anadaiwa kumfumania mkewe akiwa na mwanaume na ndiyo chanzo cha kuachana na mkewe huyo Bibi Cheka ameweka wazi.


Akiongea kwenye kipindi cha eNewz Bibi Cheka amesema kuwa Mhe. Temba alimfumania mkewe akiwa na mwanaume mwingine ndani ya nyumba yake na kumfukuza kisha mwanamke huyo kuolewa na mwanaume mwingine, Bibi Cheka amemwaga mchele huo baada ya kusikia Temba akijitapa kuwa uongozi wao ulimmjengea nyumba kubwa na kudai kuwa bibi huyo hana shukrani.

Kwa upande wa Temba alifunguka na kusema kuwa hizo taarifa hazina ukweli wowote kwani yeye na familia yake wapo vizuri wala hakuna jambo kama hilo analodai Bibi Cheka

"Hapana mimi nipo na familia yangu watoto zangu wapo nyumbani na mama yao yupo likizo saizi hivyo nimetoka hapo ameniandali chai vizuri saizi ndiyo natoka kwenda kuonana na jamaa zangu tunakikao kidogo , sasa sijui yeye anaushahidi gani kusema nimeachana na mke wangu na hata kama kweli labda nimeachana naye haihusiani na mambo haya tuzungumze mambo ya muziki, sijawahi kumfumania mke wangu na sijui kwanini bibi amezungumza hayo huenda labda amekasirika"

Watazame hapa wakifunguka  zaidi

Mgombea wa Ubunge Kinondoni..Mtulia Aliagiza Jeshi la Polisi

$
0
0
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni (CCM), Maulid Mtulia amelitaka Jeshi la Polisi hasa wa usalama barabarani waache kuwafanya waendesha bodaboda kama gari lao la mshahara kwa kuwabambikia kesi zisizokuwa za kweli pindi wanapo wakamata.

 Mgombea huyo ametoa kauli hiyo akiwa kwenye muendelezo wa kuomba ridhaa huku zikiwa zimebakia takribani siku saba ili wananchi wa Jimbo la Kinondoni pamoja na Siha kushiriki zoezi la kupiga kura katika uchaguzi huo mdogo wa marudio na waweze kupata wawakilishi wao ambao kwa mara ya kwanza wataingia bungeni mjini Dodoma Aprili 03 endapo zoezi hilo litakamilika kwa amani na usalama.

"Tuna kwenda kuhakikisha tunaleta mfumo mzuri wa kuvitambua vituo vyote vya bodaboda pamoja na kuvisajili ndani ya Jimbo la Kinondoni lakini tunawambia polisi hawa vijana wamejiajiri wasibuguziwe, sio watuhumiwa wala majambazi", amesema Mtulia.

Pamoja na hayo, Mtulia ameendelea kwa kusema "naenda kupiga marufuku bodaboda kuwa gari la mshahara kwa polisi, wakamateni wanapokuwa na makosa ya kisheria na wala msibawabikize kesi".

Kwa upande mwingine, Mtulia amedai endapo atarudishwa na wananchi hao katika Jimbo la Kinondoni basi atahakikisha matatizo yote waliyokuwa nayo yatatatuliwa bila ya wasi wasi wa aina yeyote.

Mambo Yakaa Vibaya Tena kwa Mbwana Samatta..Apata Pigo Jingine

$
0
0
Nyota wa Tanzania Mbwana Ally Samatta anayekipiga kwenye klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ameumia tena kwenye mchezo wa jana wakati timu yake ilipoibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Zulte-Waregem kwenye mchezo wa ligi kuu nchini humo.


Samatta aliumia na kutolewa dakika ya 36 huku nafasi yake ikichukuliwa na mshambuliaji Dieumerci N'Dongala ambapo timu hizo zilikuwa sare ya 1-1, matokeo ambayo yalidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Genk ilifanya vizuri na  kupata mabao mawili yaliyofungwa na kiungo Thomas Buffel dakika ya 59 na kiungo Alejandro Pozuelo dakika ya 90, hivyo kufanya Genk iliyokuwa nyumbani kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3-1.

Katika mchezo huo wa jana usiku nahodha huyo wa Taifa Stars alikuwa anacheza mechi yake ya tano tangu apone maumivu ya mishipa midogo ya goti lake la mguu wa kulia iliyochanika Novemba, mwaka jana.

Mange Afichua Siri..Kumbe Diamond Karanga Sio za Diamond Bali yeye ni Balozi tu..Amtaja Mmiliki

$
0
0


Mange Kimambi Ameandika haya:


"Hili tifu la Clouds na Wasafi, siri zote zitatoka 
Mlionichambaga nilipotoa hii habari ya kuwa Karanga sio za Diamond ni za Joseph Kusaga inabidi mniombe msamaha maana mlijua kunichamba kuwa nna roho mbaya natoa habari za uwongo sijui siipendi WCB. Mtu kusema ukweli haimaanishi chuki, chuki ni kumsemea mtu uwongo!

Diamond ni balozi wa Diamond Karanga kama jinsi alivyokuwaga Balozi wa Danube. Mkisema Diamond Karanga ni za Diamond basi hata Danube ni ya kwake. Hakuna cha jina lake sijui brand yake kutumika kwa hiyo analipwa, brand yake haijatumika hapo sababu hizo karanga hazitumiii nembo wala jina la Diamond, hizo karanga zinaitwa Diamond miaka na miaka kabla hata Diamond hajawa maarufu. Tatizo wengi mmezijua hizo karanga mwaka juzi ila hizo karanga ziko sokoni miaka mingiiii.Diamond ni balozi tu wa Diamond karanga, kama jinsi wasanii wengine ni mabalozi wa Hyatt Regency na bidhaa zingine.Fullstop

Na Chibu perfume pia niliwaambia ni ya Kusaga sio ya Diamond pia mkanibishia, sijui why mnakuwaga wabishi mkiambiwa ukweli. Hata hiyo website ya mziki sio ya Diamond vile vile ni ya Kusaga.Diamond anatumika kwa kufanya promotion tu ila wamiliki ni kina Kusaga.

Na sikuongea sababu eti simpendi Diamond eti nataka kumuumbua no, niliongea sababu sio haki mnavyowanyali wasaniii wengine kama Ali Kiba eti yeye hana bidhaaa yoyote huku Diamond ana bidhaaa zote hizo, nikaona niweke rekodi sawa kuwa Diamond pia hana bidhaa yoyote ila bidhaa ni za Joseph Kusaga..... Sio haki kuwashusha wasanii wengine na kuwafanya wajione sio kitu kwa kuwatunuku wasanii wengine utajiri feki wa kutengeneza mitandaoni. Bora muwapambanishe kwa utajiri wa kweli na sio bidhaaa za kina Kusaga.....

#Repost @kamandamzeemkavu with @get_repost

Ziara Ya Mwekezaji Mr Radima Clouds Media Mikocheni, Mr Radima Ni Mmiliki wa Kiwanda Kinachozalisha #DiamondKaranga Na Clouds kupitia kwa Mkurugenzi wake ni Washirika (Partners) Katika Mradi Wa #DiamondKaranga mradi ambao msanii @diamondplatnumz ni Balozi wake.. . HONGERA SANA MZEE BABA... Mm na Bondia kikono @soudybrown tuko nyuma kuiga mfano wako wa uwekezaji @shilawadu " Mange

Snoop Dogg na Mike Tyson Waingia Ubia Kuwekeza Kwenye Kilimo cha Bangi

$
0
0
Mwanandondi msataafu ameripotiwa kufanya kazi na mwanamuziki Snoop Doggy huku akijifinza kuhusu bangi.

Mwanandondi huyo mambaye kwa sasa amefungua shamba la ukubwa wa ekari 40, kwa ajili ya kilimo cha bangi, amejiweka karibu na mwanamuziki Snoop ambaye nae tayari anafanya shughuli za uzalishaji wa bangi, ili kujifunza namna sahihi ya kuendesha kilimo hicho na kupewa ushauri wa aina sahihi ya bangi anayotakiwa kulima.

Chanzo kimoja kimeeleza kuwa Snoop amemtafuta Tyson na kumpa maelekezo ya aina ipi ya bangi anayopaswa kulima.

“Alikuwa amewekeza kiasi cha dola za marekani milioni 25 kwenye bangi hata kabla ya jimbo la Carlifonia halijaruhusu matumizi yake, kwa hiyo anajua kwa undani uzalishaji wake.”

Snoop ambaye anataka kufungua maduka ya bangi aliwahi kulieleza gazeti la “Daily Star” la nchini Marekani kuwa, anaamini kuwa uwekezaji kwenye bangi unaweza kumaliza migogoro yote duniani.

Alisema “Ninahisi kwamba watu wengi wanavyozidi kuitumia ndivyo amani inavyozidi kuongezeka”

Habari zimeeleza kuwa Snoop ameungana na mghahawa wa “Jack in the Box” kuwapa wateja wake ‘ofa’ ya bangi.

Natoa Pole kwa Mapacha Walioungana, Consolatha na Maria

$
0
0
Mapacha walioungana, Consolata na Maria bado wanaendelea kutibiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es salaam.

Pichani, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofika hospitalini hapo kuwajulia hali na kuwatakia uponyaji wa haraka.

Namuomba Mungu ili Consolata na Maria wakapate kupona na kurejea chuoni kuendelea na masomo yao.

Kwanini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.


NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.


MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA.


MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.


NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,


Je unamali yako unauza hupati wateja?

Wasiliana nami 0716-263605

Kumbe Diamond Karanga sio mali ya Diamond (Ameumbuka) Hawa Hapa Wamiliki Wenyewe

$
0
0
Kumbe ndugu yetu Naseeb is a mere ambassador a.k.a Balozi mzee Baba Joseph Kusaga Kausika Jionee video uamini. VIDEO:

Msanii AY Afunga Ndoa na Mke Wake Huko Rwanda

$
0
0
Rapper Ambwene Yessayah maarufu kama AY amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Remy.Wawili hao wamefunga ndoa jana nchini Rwanda ambako ndipo anatokea Remy. Bado AY au watu wake wa karibu hawajaposti katika mitandao ya kijamii kuelezea hilo.
July mwaka jana, 2017 ndipo AY alimvisha pete ya uchumba Remy na tukio hilo ilihudhuriwa na watu wa karibu wa wawili hao.

Baada ya Wema Kujisogeza kwa Diamond, Idris Aamua Kumuonyesha Mpenzi Wake wa Kizungu

$
0
0
Baada ya Wema kujisogeza kwa Diamond, Idris aamua kumuonyesha mpenzi wake wa kizungu

VIDEO:

Tazama 'Sendoz' Ilivyomuumbua Diamond Mahakamani, Atembea Peku

$
0
0

MSANII wa Bongo Fleva, Nasbu Abdul ‘Diamond Platinumz’ leo amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kusikiliza kesi inayomkabili ya kushindwa kumtunza mtoto wake aliyezaa na msanii mwenzake, Hamisa Mobeto.

Katika Shauri la kesi hiyo lililofunguliwa na Hamisa Mobetto akiomba Mahakama iamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto kila mwezi, litaanza kusikiliza leo katika mahakama ya watoto Kisutu.

VIDEO:

Afisa Aanguka Ghafla Baada ya Kutumbuliwa Na Makonda

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amemwagiza Mkurugenzi  kuwapangia kazi nyingine wakuu wa Idara ya mipango miji manispaa ya Ilala, Paul Mbembela na wa Ubungo, Hamis Songwe ambapo mkuu wa idara ya Ilala alianguka chini.

VIDEO:

Uamuzi wa Paul Makonda Wazua Mjadala...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya February 12

$
0
0


Uamuzi wa Paul Makonda Wazua Mjadala...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya February 12

Zitto Kabwe "Sababu za Usalama wa Taifa Kutakiwa Kufumuliwa"

$
0
0
Jana (juzi) tarehe 9/2/2018 Bunge lilikuwa linajadili Taarifa ya mwaka ya Kamati ya Bunge ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje. Kutokana na muda kutokuwa wa kutosha, wabunge wachache walipata nafasi ya kuzungumza akiwemo Mbunge wa Mtama ndugu Nape Nnauye na Mbunge wa Iringa Mjini Mheshimiwa Peter Msigwa. Katika mazungumzo yake Nape alitaka Sheria ya usalama wa Taifa irekebishwe ili kuipa nguvu Chombo cha TISS kuzuia vitendo vya uhujumu uchumi badala ya hali ya sasa ambapo matukio mengi yanayohusu uhujumu uchumi hujulikana baada ya madhara kutokea. Mifano ya kashfa kubwa kama Richmond, EPA na Escrow ilitolewa. Mchungaji Msigwa alizungumzia kitendo cha kinyama dhidi ya Mbunge mwenzetu Tundu Lissu.

Waziri wa Usalama nchini Ndugu George Huruma Mkuchika alieleza kuwa TISS hawana shida na wanaweza kuendelea na kazi zao bila kuboreshwa. Siku hiyo nilipanga kuzungumza kuhusu masuala ya usalama wa Taifa hususan Kuhusu matukio ya kusikitisha ya Watu kupotea na hata jaribio la kumwua Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu. Sikubahatika kuzungumza ndani ya Bunge, kama nilivyosema sababu ya muda. Nina machache nilitaka kuyasema Bungeni na nimeona niyaandike. Mengine nitayasema kwa kina Bungeni siku za usoni Mungu akituweka hai. Haya machache ninayoandika ni kwa sababu ya kuonyesha kuwa sheria ya usalama wa Taifa inapaswa kufumuliwa na kuandikwa upya.

Sheria ya Usalama wa Taifa, sheria namba 15 ya mwaka 1996 ina mapungufu makubwa na pia inavunjwa vunjwa na chombo kinachoitekeleza. Pungufu la msingi ni kutokuwepo kwa sehemu ya ujasusi wa kiuchumi na hasa uchumi wa kimataifa Katika sheria nzima. Iwapo sheria ingekuwa ina vifungu vya kufanya ujasusi wa kiuchumi ingeweza kufunza watumishi wake masuala hayo na kulisaidia Sana Taifa kuepuka madhara mengi.

Kwa mfano, Hivi sasa Tanzania inapoteza fedha nyingi kwa sababu ya kushindwa kuleta ndege yake iliyoshikiliwa na watu wanaotudai huko Canada. Hili lisingewezekana iwapo TISS ingekuwa inafanya uchambuzi wa masuala hatari kwa Uchumi wetu. Ujasusi wa kiuchumi ungewezesha TISS kutambua uwezekano wa ndege zetu kushikiliwa na wangetoa mapendekezo ya namna ya kuokoa jambo hilo. TISS wangeweza kumshauri Rais namna bora kununua ndege ( kwa mfano badala ya kununua kutoka kiwanda cha Bombadier Canada wangenunua kutoka kiwanda cha Bombadier Ireland ambapo pengine hakuna wanaotudai). Hivi sasa ndege 2 zaidi za Tanzania zipo hatarini kushikwa ama zimeshikiliwa na Wananchi hatujaambiwa.

Kuna kampuni kutoka Japan inayoidai Serikali USD 65 milioni kwa kukiuka mkataba wa ujenzi wa barabara, imeshapata karatasi za mahakama huko Marekani ili kushika Boeing 787 Dreamliner inayonunuliwa na Tanzania. Pia kuna kampuni huko Uingereza inatudai USD 59 milioni tayari inanyemelea ndege ya Bombadier C300 inayoundwa huko Belfast Northen Ireland. Kampuni hiyo Ina karatasi za mahakama ya UK. Iwapo Sheria ya Usalama wa Taifa ingekuwa imetoa nguvu kwa TISS kufanya uchambuzi wa mambo kama haya ingeweza kuepusha nchi na changamoto hizi na nyengine nyingi. Mathalani, Hivi sasa kuna kashfa kubwa dhidi yetu kuhusu kuweka mawe kwenye korosho zetu tulizouza huko Vietnam. Kitengo cha Ujasusi wa kiuchumi kingeshachambua na kujua kama ni hujuma za mataifa mengine dhidi yetu au ni makosa ya wakulima wetu wenyewe. Ukiwahoji haya watu wa TISS, wanasema hawana mamlaka. Ni kweli, lazima sheria irekebishwe. Lakini kuna mambo TISS wanafanya wakiwa hawana mamlaka kisheria.

Kifungu cha 5(2) cha sheria ya usalama wa Taifa kinaizuia TISS kumfuatilia mtu yeyote wala kumpekua pekua au kumfanyia ujasusi kwa sababu ya msimamo wake kisiasa au Uhuru wake wa kuipinga Serikali. TISS inavunja sheria kila wakati kwenye eneo hili.

Nina mifano michache kuthibitisha hili. Mwaka 2017 aliyekuwa Waziri wa Habari Nape Nnauye alitishiwa bastola hadharani na watu wa usalama wa Taifa. Kabla ya hapo alikuwa anafuatiliwa na gari ambayo baadaye iligundulika ndio gari iliyokuwa inamfuatilia Tundu Lissu kabla ya kupigwa risasi zaidi ya 30. Mifano hii miwili ya Nape na Lissu inaonyesha kuwa TISS inafanya kazi kinyume cha sheria inayowakataza kufuata fuata watu wala kuwapekuapekua. TISS ilikuwa inamfuatilia Nape Nnauye na pia gari iliyokuwa inamfuatilia Tundu Lissu ilikuwa ya TISS kwani ilionekana kwenye matukio yote mawili.

Mambo haya hayawezi kufanyika bila IDHINI ya Mkurugenzi Mkuu wa Usalama na au Mkuu wa Uendeshaji wa Usalama wa Taifa. Kwa sasa nafasi hizi zinashikiliwa na Bwana Kipilimba na Bwana Robert Musalika, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa ambaye ni mzaliwa Geita na amekuwa Afisa Usalama wa Mkoa wa Tabora na baadaye mwakilishi wetu huko Addis Ababa Ethiopia. Bwana Kipilimba, ambaye sasa anamaliza muda wake ni mzaliwa wa Morogoro na amekuwa Benki Kuu na NIDA kabla ya kuwa Mkuu wa Usalama.

Hakuna tukio lolote la utekaji au mauaji linalofanywa na watu wa usalama bila IDHINI ya Mkurugenzi wa Operesheni ambaye sasa ni Robert Musalika. Likitokea tukio la namna hiyo bila idhini ya Director of Operations basi ni lazima yeye atumie sheria kufanya uchunguzi na kupendekeza hatua za kuchukua.
Sheria ya usalama wa Taifa kifungu cha 14 kinatoa mamlaka kwa TISS kuchunguza jambo lolote linalookena ni tishio kwa nchi. Kifungu hiki kimeliweka jukumu hili kama WAJIBU wa chombo hiki ( duty to investigate) hivyo majibu mepesi kuwa sio kazi ya TISS kuchunguza hayana msingi kabisa.

Kuna matukio ambayo ni tishio kwa usalama wa Wananchi ambayo mpaka sasa hakuna majibu ya Serikali. Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Bwana Azory Gwanda amepotea sasa zimefika siku 85 hivi na hakuna majibu yeyote ya Serikali. Azory alikuwa anaandika Habari za kiuchunguzi kuhusu masuala ya Kibiti na kuokotwa kwa miili ya Wananchi kwenye fukwe zetu. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kibondo Bwana Simon Kanguye alitekwa na maafisa usalama wa Taifa mjini Kibondo siku moja kabla ya ziara ya Rais wa Tanzania mkoani Kigoma na mpaka leo hajulikani alipo. Matukio haya matatu ya Watu kupotea na miili kuokotwa ni matukio yanayolazimisha TISS kuyachunguza kwa kutumia kifungu cha 14 cha sheria yake ya mwaka 1996.

Kwa kuwa hawangaiki nayo ni rahisi kutafsiri kuwa kuwa TISS chini ya Mkurugenzi wa Uendeshaji Bwana Musalika wameidhinisha haya. Ni vema ifahamike kuwa kabla ya kurudi nyumbani Bwana Musalika alikuwa Mfanyakazi wa Ubalozi wetu Addis Ababa, Ethiopia nchi ambayo rekodi yake ya Watu kupotea, kutekwa, kufungwa na hata kuuwawa inatia fora. Bwana Musalika anapaswa kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Usalama ili ajieleze ni kwanini asiwajibishwe kwa kushindwa kutimiza wajibu wake wa kifungu cha 14 cha sheria ya usalama wa Taifa.

Nimetaja hapo juu suala la Mbunge Tundu Lissu. Jana Kamati Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje ya Mheshimiwa Adadi Rajabu ilionyesha kusikitishwa na tukio la Tundu kupigwa risasi na kupendekeza kuwa wabunge wapewe Ulinzi. Ni vema ieleweke kuwa mahala anapoishi Mbunge akiwa Dodoma kwenye mkutano wa Bunge ni eneo la Bungeni ( precincts of parliament). Kifungu cha 2 cha sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ( sheria namba 3 ya mwaka 1988 ) kimetafsiri kuwa eneo la Bunge ni pamoja na malazi ya Mbunge. Kwa hiyo Tundu Lissu alipigwa Risasi Katika eneo la Bunge kisheria ambalo linapaswa kulindwa na vyombo vya Serikali.
Katika mantiki ya kawaida kabisa tukio la namna hiyo haliwezi kufanyika bila idhini ya chombo kinachoshughulika na usalama na kwa maana hiyo Mkurugenzi wa Operations wa TISS. Nilisikitishwa Sana na kitendo cha Kamati ya Ulinzi na Usalama kusikitishwa tu na tukio la Kinyama dhidi ya Tundu Lissu, Kamati ilipaswa kwenda mbele na kumwajibisha Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa na Naibu wake ambaye anasimamia Operations. Kamati haikupaswa kuomba tu wabunge kupatiwa Ulinzi, bali ilipaswa kuhoji ni kwanini sheria ya Haki na Kinga za wabunge haitekelezwi na vyombo vya ulinzi na usalama.

Tunaweza kujadili mambo haya sasa hivi kwa sababu Tundu Lissu yupo kitandani Katika hospitali nchini Ubelgiji ama Ben Saanane, Azory Gwanga na Simon Kangoye wamepotezwa. Kama tusipochukua hatua mahususi na madhubuti za kuifumua TISS na kuiunda upya, watu wengi zaidi watapotea, kupigwa risasi na kuokotwa kwenye fukwe zetu. Sijui tunasubiri nini kitokee mpaka tukubali ukweli kuwa TISS inapaswa kufumuliwa na Viongozi wake wa sasa wanapaswa kuwajibishwa na kufikishwa kwenye mahakama kujibu mashtaka ya mauaji na kupoteza watu.

Vile vile kama hatutachukua hatua kuunda kitengo madhubuti cha ujasusi wa kiuchumi kwa mujibu wa sheria tutaendelea kupigwa tu kwenye mikataba ya kimataifa na kuathirika sana kiuchumi kama Taifa. Huu ni wakati mwafaka kabisa kuifumua TISS na kuiunda upya ili itumikie nchi yetu na kuhakikisha usalama wa Wananchi na usalama wa Uchumi wa Taifa. #ReformTISSnow
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images