Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Newcastle United yaipa Kichapo Manchester United

$
0
0
Klabu ya soka ya Manchester United leo imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa klabu ya Newcastle United.

Bao pekee katika mchezo huo wa ligi kuu ya soka nchini England uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Saint James Park limefungwa na Matt Ritchie dakika ya 65.

Kwa upande wa kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameendelea kuwa na rekodi mbaya kwenye uwanja huo akiwa hajawahi kushinda mchezo wowote wa ligi.

Mourinho akiwa na Chelsea na Manchester United kwa sasa amefanikiwa kushinda mechi mbili tu kati ya tisa kwenye uwanja wa St. James Park huku mechi hizo mbili zikiwa ni za kombe la ligi (EFL CUP).

Matokeo ya leo yanaiacha Manchester United katika nafasi ya pili ikiwa na alama 56 ikiwaacha vinara manchester City wakiwa kileleni kwa alama 72.

Hatua za Kufahamu Kama Hati ya Nyumba au Kiwanja ni Halali au Feki

$
0
0

NA  BASHIR  YAKUB

Ni  wangapi  wamefanyiwa  utapeli  katika  harakati  za  kununua  viwanja  au  nyumba.  Ni  wangapi  wamepata  hasara  kubwa  kutokana  na  michezo  ya  utapeli  iliyotamalaki  katika  ardhi  nchini.  Ni  kesi  ngapi  ziko  mahakamani  zinazohusisha  utapeli   katika  mauzo na  manunuzi  ya  ardhi.  Idadi  ni kubwa  mno  na huu  ndio  ukweli.

Siku  zote  huwa tunasema  ni  vigumu  kujua   ukubwa  na  hatari  ya  jambo   hili  mpaka  likukute  au  limkute  mtu  wako  wa  karibu. Lakini  swali  ni  ikiwa  watu   wamekuwa  wakijifunza  kupitia  wenzao  ambao  wamekutwa  na  haya. Kama  na wewe  bado  hujajifunza  basi ni  muhimu  sasa  kujifunza.

Mtu   anauza  ardhi  moja  kwa  watu hata   zaidi  ya  wanne tofauti, mtu  anauza  ardhi  asiyokuwa  yake  huku  akijua  kabisa  sio  ya kwake, mtu  anaghushi  hati  au  leseni  ya  makazi  kisha  anauza  kiwanja  au  nyumba ya  mtu, kiongozi  wa  serikali  ya  mtaa   anashiriki  kuuza  ardhi  ya mtu   huku akijua  kuwa  juzi  mtu  mwingine  alinunua  ardhi  hiyohiyo, kwa  ufupi  hali  ni  mbaya  na  ni  vema  kusema  ili  watu  wachukue  tahadhari.

Wizara  ya  ardhi  imeshasema mara  nyingi  kuwa  moja  ya  sababu  kubwa  inayopelekea  watu   kutapeliwa  katika  manunuzi  ya  ardhi  ni  wanunuzi  wenyewe  kutozingatia  taratibu  za  kisheria  za  manunuzi. Migogoro  mingi  imezalika  hapa.

Mara  kadhaa  tumewahi  kueleza  kwenye  makala mbalimbali  namna  salama  ya  kununua  ardhi  kwa  kuepuka  utapeli.  Zipo  makala nyingi  ambazo  zimeeleza  hatua  za  kufuata  ili  uwe  salama.  Hata  hivyo  leo  kitaelezwa  kitu  kingine  ambacho  hakikuwahi  kuelezwa.  Ni  namna  ya kuhakiki  hati  au  leseni  ya  makazi   ili  kujua  ikiwa ni  halisi (original)  au  feki kabla  ya  kununua  kiwanja  au  nyumba.

1.UHAKIKI  ULIOWAHI  KUSHAURIWA.

Kabla  ya  kueleza  njia  nyingine  ya uhakiki  inayotakiwa  kuelezwa  leo hebu  tujikumbushe  njia iliyowahi  kuelezwa  katika  makala  zilizopita. Ni  uhakiki  wa  hati  kwa  njia  ya   upekuzi  rasmi( official  search).  Tulisema  kuwa  kupitia  njia  hii  utaandaa  maombi  kwenda  kwa   msajili  wa  hati(Registrar of Title)   ukitaka  kujua  ikiwa  nyumba /kiwan ja  unachotaka  kununua  kama kina  mgogoro  au  ikiwa kuna  mtu  mwingine  mwenye  maslahi  juu  yake.

Mgogoro  ni  kama  kuna  zuio  la  kifamilia( caveat), zuio  kutoka  mahakamani  na  mengine  yanayofanana  na  hayo.  Na  kuwapo  mtu  mwingine  mwenye  maslahi  ni  kama  kiwanja  au  nyumba hiyo kuwa   imesimama  kama  dhamana   ya  mkopo n.k.  Majibu  ya  vitu  vyote  hivi  utayapata utakapojibiwa   maombi  yako  ya  upekuzi  rasmi ( official  search).

2. UHAKIKI   WA  KUIJUA  HATI  ORIGINAL.                                         

Hili  ndilo  linaloshauriwa   leo.  Ni uhakiki  wa  kujua  ikiwa  hati  ni  halisi  au  feki.  Upekuzi  rasmi(official  search) ulioelezwa  hapo  juu  kazi  yake  sio  kuonesha  uhalisi  au  ubatili  wa  hati  bali  husaidia  katika kujua  taarifa/maudhui( contents)  za  hati.  Na hii  ni  kwasababu  unapopeleka  maombi  haya hairuhusiwi kuambatanishi  hati.

Ni  kupitia  njia  hii  ya  kuwasilisha hati  halisi  kwa  msajili  unapoweza  kujua  uhalisi  au  ubatili  wa  hati. Basi unachotakiwa  kufanya  ni  kuchukua  hati  ya  kiwanja  au  nyumba unayotaka  kununua  na  kuipeleka  kwa  msajili  wa  hati.  Kama  muuzaji  hatokubali  kukupa  hati  ili  ukaihakiki  basi  muombe  uongozane  naye  akiwa  ameishika  yeye  mpaka  kwa  msajili.

Lakini  hautaenda  hivyo  bali  utafanya  maombi  maalum  ambapo  siku  utakapokuwa  unapeleka  hiyo  hati  utakuwa  tayari  umepeleka  maombi  kwanza  au  iwe siku  hiyo  ndio   unapeleka  maombi  pamoja  na  hati kwa  uhakiki. Pia  unaweza  kuwatumia  wanasheria  katika  hili.

Msajili  wa  hati  anachokifanya  ni  kuchukua  hiyo  hati  mliyoileta  na kuikagua  kwa  kutumia  mfumo(system) ikiwa  ni  halali  na  ikiwa   kweli  ilitolewa na  ofisi  yake.  Ikiwa  iko  sawa  atathibitisha  na  kubariki  muamala  wenu  na  ikiwa  si  sawa  pia  atasema.  Hakuna  namna  ambavyo  unaweza  kupewa  hati  feki  ikiwa  ulipitia  utaratibu  huu. Hata  mabenki  yanayokopesha  kwa  kukubali  dhamana  za  hati  hujiridhisha  kwa  njia  hii ili  kukwepa  dhamana  feki.

Simba imerudi Anga za Kimataifa..Yamchapa Mtu 4 Bila

$
0
0
Simba wamerejea kwenye anga za kimataifa kwa ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Gendarmerie National ya Djibouti katika mchezo wa Caf Confederation Cup.

Wekundu wa Msimbazi wamesubiri kwa miaka mitano (5) mfululizo tangu waliposhiriki kwa mara ya mwisho mwaka 2012 na kuondolewa Al Ahly Shendi kwenye michuano ya vilabu bingwa Afrika.

Magoli ya Simba katika mchezo wa leo yamefungwa na Said Hamisi Ndemla, John Bocco ambaye amefunga magoli mawili huku goli la mwisho likifungwa na Emanuel Okwi.

Pacha ya ushambuliaji inayoundwa na John Bocco na Emanuel Okwi imeendeleza makali yake hadi kwenye michuano ya Afrika baada ya wawili hao kufunga magoli matatu kwa pamoja. (Bocco amefunga magoli mawili, Okwi amefunga goli moja na kumtengeneza goli moja lililofungwa na Bocco.

Kocha Simba Kawajibu Wanaobeza 4G Kimataifa

$
0
0
Baada ya Simba kushinda kwa magoli 4-0 kwenye mcheO wao wa kwanza wa kimataifa dhidi ya Gendarmerie, mashabiki wa wekundu wa Msimbazi wanasema Simba ilikuwa na uwezo wa kupata ushindi mkubwa zaidi ya walioupata kutokana na udhaifu wa wapinzani wao.

Kocha msaidizi wa Sima Masoud Djuma amesema waliwataka wachezaji wasitumie nguvu kubwa kwenye mchezo mmoja kutokana na kukabiliwa na michezo miwili ya VPL hivi karibuni.

“Nimemsikia mwalimu wao anasema zamani walikuwa wanafungwa hadi magoli tisa au 10, huo ni mpira wa zamani, mpira wa kisasa kitu cha muhimu ni kwamba hatukuruhusu kufungwa goli.”

“Halafu sisi tuna mechi mbili za ligi zimeongozana hapa karibu kwa hiyo ilikuwa lazima tucheze kwa mpangilio kwa sababu ni lazima tushinde zote kwa hiyo hatukutumia nguvu nyingi kwenye mchezo mmoja.”

“Tunashukuru tulipata magoli ya mapema nafas

Kiwanja Kinauzwa Bei Rahisi Kabisa

$
0
0

Kiwanja Kinauzwa Bei Rahisi Kabisa
Ukubwa mita 52 × mita 20
Kipo nyuma ya shule ya BAOBAB Eneo la Mapings
Bei mil 18 inapungua kidogo

Piga Namba 0762 614 079

Chura Anatafuta ‘Mchumba’ Nchini Bolivia

$
0
0
Wataalam wa kuhifadhi wanyama nchini Bolivia wameanza kutembea katika Taifa hilo zima wakimtafuta chura wa ‘kike’ atakayejamiana na chura mmoja asiye wa kawaida ambaye wanahofia kizazi chake huenda kikapotea kutokana na yeye kuwa peke yake.

Chura huyo aliyepewa jina la ‘Romeo’ mwenye umri wa miaka 10, anaishi katika maji na amekuwa akimtafuta mwenzake kwa kipindi cha miaka tisa. Tayari amewekwa katika mtandao wa kuwakutanisha wapendanao akisema ‘Namtafuta mpenzi juliet.’

Wanasayansi kwa sasa wanatafuta chura wa kike atakaye jamiana na Romeo katika madimbwi ya maji na mito ili kuhifadhi kizazi hicho.

Moja ya wanaomtunza amesema ”Hatutaki yeye apoteze matumaini. lakini wahifadhi hao watalazimika kuongeza kasi ya kumsaka chura huyo wa kike kwa kuwa hawezi kuishi zaidi ya miaka 15”.

Chura huyo anaishi katika pipa katika kumbukumbu ya Cochabamba amebakiza miaka mitano ya kuishi.

”Namtafuta Juliet wangu kwa sababu mimi ni kizazi cha mwisho cha familia yangu, Namtufuta chura wa kizazi changu, la sivyo kizazi changu chote kitaangamia”.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

$
0
0
SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

Riyama na Mume Wake Mahaba Niue

$
0
0
Riyama na Mume Wake Mahaba Niue
MWANAMAMA mwenye sifa zote awepo mbele ya kamera za Bongo Movies, Riyama Ally anamuomba Mungu yeye na mumewe, Leo Mysterio waishi miaka mingi ili kila mmoja aje kumzika mwenzake wafikapo uzeeni.

Riyama aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, siyo watu wote wanapenda kuombeana dua waishi miaka mingi kama mke na mume, bali huwa wanahesabu tu siku za kuachana, lakini kwa upande wake yeye ni tofauti.

“Kila siku ninaomba dua ili mimi na mume wangu tuishi miaka mingi kwa kuziepuka husda za watu ambazo zipo kila kona,” alisema Riyama ambaye ni mkali wa kuigiza sinema za majonzi.

Mzee Akilimali Amkataa Chirwa

$
0
0
Mzee Akilimali Amkataa Chirwa
KATIBU wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Ak­ilimali, amelitaka benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Mzam­bia, George Lwandamina, kuhakikisha wanatafuta mbadala wa mchezaji atakayekuwa anapiga pen­alti badala ya Mzambia, Obrey Chirwa.

Mzee Akilimali ameyasema hayo kufuatia mshambuliaji huyo kuwa na mfululizo wa kukosa penalti ambapo juzi Jumamosi alikosa tena wakati Yanga iliposhinda bao 1-0 dhidi ya St Louis katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Kwa mwaka huu, Chirwa amepiga jumla ya penalti tano ambapo kati ya hizo kakosa nne dhidi ya URA kwenye Kombe la Mapinduzi, Ihefu katika Kombe la FA, Njombe Mji kwenye Ligi Kuu Bara na St Louis. Aliyopata ni dhidi ya Ihefu ambapo kwenye mch­ezo huo alipiga penalti mbili.

Akizungumza na Champio­ni Jumatatu, Mzee Akilimali alisema kuwa kwa upande wake analitupia lawama benchi la ufundi la timu hiyo kwa kuendelea kumpa penalti mchezaji huyo licha ya kuto­kuwa na bahati nazo hali inay­owafanya kupata wakati mgumu kupata matokeo.

“Kwangu siwezi kumlaumu Chirwa hata kidogo, wa kulaumiwa ni benchi zima la ufundi likion­gozwa na Lwan­damina kwa sababu sioni haja ya kuendelea kumtumia penalti aendelee kupiga mchezaji huyo maana hana bahati nazo hata kidogo.

“Siku zote amekuwa akikosa penalti katika michezo muhimu na hii ni (mechi) ya tatu kwake lakini bado amekuwa akikosa, sasa kwa nini wasibadilishe na ukiangalia katika mchezo wa jana (juzi) yeye ndiyo ameighar­imu timu kwa kiasi kikubwa lakini walimu sijui hawakuliona hilo au vipi,” alisema Mzee Akili­mali.

ANC Kufanya Uamuzi wa Mwisho wa Kumng'oa Zuma Leo

$
0
0
ANC Kufanya Uamuzi wa Mwisho wa Kumng'oa Zuma Leo
Kiongozi wa Chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa chama kitafanya uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya Rais Jacob Zuma.

Akizungumza kaika mkutano wa hadhara mjini Cape Town, Ramaphosa amedokeza kuwa Rais Zuma atatakiwa kujiuzulu.

Amesisitiza kuwa wala rushwa wote wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho anasema Nelson Mandela, baba wa taifa hilo angekitaka.

Bwana Ramaphosa alikuwa akizungumza katika kumbukumbu ya miaka 28 toka Rais wa kwanza mzalendo nnchini humo Nelson Mandela alipolihutubia taifa, mara tu baada ya kuachiwa gerezani.

Irene Uwoya Aumbuka ... Mabaa Medi Wamuumbua

$
0
0
Irene Uwoya Aumbuka ... Mabaa Medi Wamuumbua
UBUYU wa leo hatujauvukia maji kutoka Zanzibar, bali tumeupata maeneo ya Magomeni-Kwa Fundikira, Dar, unaitwa ubuyu wa vimto ambapo unamung’unywa kuwa, ile baa maarufu ya staa mkali wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya ijulikanayo kwa jina la Last Minutes imefungwa kwa madai kuwa mabaamedi wake wamegoma kwa kutolipwa mishahara miezi mitatu



MMOJA WA WAFANYAKAZI AFUNGUKA

Msambaza ubuyu huo ambaye alikuwa ni mmoja wa mabaamedi katika baa hiyo aliyeomba hifadhi ya jina kwa sababu ya kutotaka kuonekana mmbaya, alidai kuwa, yeye na wenzake watano waliamua kuchukua uamuzi wa kugoma kwa sababu hawajalipwa mishahara ya miezi mitatu, jambo ambalo wamelivumilia kwa kipindi chote hicho.



“Ukweli ni kwamba kama mtu anafahamu ubinadamu, huwezi kumwacha mwenzako akiteseka wakati amekufanyia kazi kwa kipindi hata cha mwezi mmoja bila kumlipa chochote, ukizingatia maisha ya sasa ni magumu sana mtu, mtu unavumilia hadi unachoka,” alisema mfanyakazi huyo.

Taarifa hizo zilizidi kueleza kuwa, mara kwa mara wafanyakazi hao walikuwa wakimkumbushia Uwoya juu ya madai ya stahiki zao, lakini waliishia kuambiwa kuwa watalipwa kesho ambayo haikufika.



WADAI KUPIGWA KALENDA

Mhudumu huyo alilieleza Ijumaa Wikienda kuwa, wamekuwa wakipigwa kalenda kila siku, jambo ambalo limekuwa likiwaumiza siku hadi siku hadi kufikia hatua ya kuamua kugoma wote.

“Siku hizi kazi hakuna, lakini hadi mtu anaamua kuacha kazi, ujue kuna tatizo kubwa,” alisema mwanadada huyo.



IJUMAA WIKIENDA NA MAMA KUBWA

Baada ya kupata ubuyu huo, Ijumaa Wikienda liliwatafuta wahusika ambapo wa kwanza alikuwa ni Mariam Ismail ‘Mama Kubwa’ Uchunguzi wa gazeti hili kwenye baa hiyo ulibaini kuwa, Mama Kubwa ndiye meneja ambapo alipoulizwa kuhusiana na hilo, mambo yalikuwa hivi;



Ijumaa Wikienda: Vipi Mariam, mzima? Siku hizi hizi baa mmeifunga?

Mariam: Kwa nini?

Ijumaa Wikienda: Nimeona kama wiki hamjafungua, lakini pia kuna malalamiko kuwa hamjawalipi wafanyakazi wenu mshahara ni miezi mitatu sasa, hilo likoje?

Mariam: Nani amekuambia? Hilo siyo kweli kabisa.



Ijumaa Wikienda: Ukweli ni upi sasa?

Mariam: Ni kwamba pale tumefunga kwa sababu kuna matengenezo tunafanya ya kupaongeza maana kulikuwa kumebana sana hivyo wateja wengine walikuwa wanakosa nafasi.

Ijumaa Wikienda: Mbona kuna madai kuwa mmefunga kwa sababu wafanyakazi wamegoma kwa kuwa hamjawalipa mishahara yao ya miezi mitatu?



Mariam: Hiyo siyo kweli kabisa itakuwa ni mfanyakazi mmoja ambaye alikuwa ana matatizo na sisi. Huyo ndiye anasambaza hizo habari za uzushi, lakini sisi tuko kwenye matengenezo.



UWOYA ANASEMAJE?

Baada ya kumsikia Mariam, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Uwoya ambapo alisema kuwa yeye hana cha zaidi cha kuzungumza na kwamba maelezo ya meneja wake yanajitosheleza.

NEC: Maandalizi ya Uchaguzi Yanaendelea Vizuri

$
0
0
NEC: Maandalizi ya Uchaguzi Yanaendelea Vizuri
Zikiwa zimebaki siku 6 kabla ya uchaguzi mdogo wa ubunge Siha na Kinondoni na kata nane kufanyika, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema maandalizi yanaendelea vizuri.

NEC imesema maandalizi hayo ni pamoja na ufumbuzi wa changamoto ndogondogo zinazojitokeza.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima amesema hayo baada ya mkutano wa watendaji wa Tume na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumujuri.

Kailima amesema Tume inafuatilia kwa karibu maandalizi ya uchaguzi huo utakaofanyika Jumamosi Februari 17,2018.

Katika taarifa ya NEC iliyotolewa leo Februari 11,2018 Kailima amepongeza jitihada zinazofanywa na msimamizi wa uchaguzi  na wasaidizi wake katika kuhakikisha changamoto zinazojitokeza zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Amewashauri wasimamizi wa uchaguzi kuendelea kukutana na wawakilishi wa vyama vya siasa kwa ajili ya kutoa taarifa katika kila hatua.

Kailima amesema Tume imejipanga kuanza kutoa vipindi vya elimu ya mpiga kura mfululizo hadi siku ya uchaguzi.

Amesema elimu itahusu mada kadhaa zikiwemo haki na wajibu wa mpiga kura, wakala wa vyama vya siasa na msimamizi wa uchaguzi pamoja na taratibu zote za upigaji kura.

Man U Yakubali Kichapo Kutoka kwa Newcastle United

$
0
0
Man U Yakubali Kichapo  Kutoka kwa Newcastle United
Klabu ya soka ya Manchester United leo imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa klabu ya Newcastle United.

Bao pekee katika mchezo huo wa ligi kuu ya soka nchini England uliomalizika jana jioni kwenye uwanja wa Saint James Park limefungwa na Matt Ritchie dakika ya 65.

Kwa upande wa kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameendelea kuwa na rekodi mbaya kwenye uwanja huo akiwa hajawahi kushinda mchezo wowote wa ligi.

Mourinho akiwa na Chelsea na Manchester United kwa sasa amefanikiwa kushinda mechi mbili tu kati ya tisa kwenye uwanja wa St. James Park huku mechi hizo mbili zikiwa ni za kombe la ligi (EFL CUP).

Matokeo ya yanaiacha Manchester United katika nafasi ya pili ikiwa na alama 56 ikiwaacha vinara manchester City wakiwa kileleni kwa alama 72.

Mwanaume Ajiua kwa Kunywa Sumu Kisa Wivu wa Mapenzi

$
0
0

Mwanaume Ajiua kwa Kunywa Sumu Kisa Wivu wa Mapenzi
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 43, Nicholas Wambua anayeishi katika eneo la Pipe Line Mjini Nairobi nchini Kenya, amejiua kwa kunywa sumu baada ya kumuhisi mkewe akimsaliti.


Mwanaume huyo ambaye alikuwa akifanya biashara ya mitumba katika eneo hilo, amefanya tukio hilo asubuhi ya Jumapili hii huku akiaacha ujumbe kwa watu wake wa karibu wamwambie mke wake huyo awaangalie watoto.

“Aliniambia ankwenda mbali na kuniomba nimwambie mama Sharon awaangalie watoto wake kwa ajili yake, ahtukujua akimaanisha kifo”, amesema Bi. Tabitha Bernad ambaye ni mkwe wa marehemu Wambua.

Mkwe wake huyo ameendelea kwa kusema kwamba mara nyingi marehemu alikuwa akimlalamikia kuwa mke wake ana tabia ya kuleta wanaume tofauti tofauti nyumbani kwao na kulala nao, iliniumiza kwa kweli lakini hatukupata muda wakuzungumza zaidi”, amesema Bi. Tabitha ambaye pia ni mkwe wa marehemu.

Mama Samia Kuzindua Mradi wa Kusimamia Maliasili

$
0
0
Mama Samia Kuzindua Mradi wa Kusimamia Maliasili
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo anatarajiwa kuzindua mradi wa kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa kanda ya kusini ujulikanao kama REGROW (Resilient Natural Resource for Tourism and Growth).


Mh. Suluhu anazindua mradi huo wenye lengo la kuongeza mchango wa sekta ya maliasili na utalii katika uchumi wa taifa kwa kuboresha vivutio vya utalii, miundombinu, usimamizi wa vivutio na kuongeza faida za kiuchumi kwa jamii zinazoishi jirani na maeneo ya hifadhi.

Mradi huu ambao maandalizi yake yalianza mwezi Novemba 2014 utazinduliwa rasmi katika viwanja vya Kihesa Kilolo Mjini Iringa ambapo Kauli Mbiu ya uzinduzi huo ni “Utalii kwa Maendeleo Endelevu- Karibu Kusini”.

Taasisi zitakazohusika na utekelezaji wa mradi huo ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Ofisi ya Bonde la Mto Rufiji, Bodi ya Utalii Tanzania, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya mbalimbali nchini.


Video: Baunsa wa Diambond Atosahau Unyama Huu Aliofanyiwa

$
0
0
Mpango mzima wa ‘Birthday Party’ ya baunsa wa Mfalme wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, anayefahamika zaidi kwa jina la Mwarabu Fighter, ulifanyika katika fukwe za Sea Breeze zilizopo Mbezi Beach – Dar, jana Februari 11, 2018.


Mashabiki wa Mwarabu Fighter na wageni waalikwa wote walipata fursa ya kukata keki pamoja na baunsa huyo kisha kupiga stori mbili tatu, na mwisho wa yote wakaamua kumfanyizia kitu mbaya ambayo hata yeye hatosahau maishani mwake……

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo Jumatatu

$
0
0

KERO za Michango ya Sherehe Katika Jamii ya Watanzania

$
0
0

Wakuu hii kitu bado bongo ipo tena siku hizi ni project kubwa na za garama ya juu.

Watu wanakutana kila wiki mara moja kwenye baadhi ya bar, wanakunywa na kusaza katika hivyo vikao vya maandalizi, vikao hivyo huchukua miezi miwili hadi mitatu. Na katika vikao hivyo watu hutoa ahadi ya kiasi cha fedha watakachotoa kwa ajili ya harasi, wanaume hutoa michango ya bachela parti na harusi kuu, na kina dada hutoa michango ya sendi off, bridoshawa, kichenipati, na harusi kuu.

Kwa kifupi zoezi hili linakula hela nyingi sana, nimeambiwa sometimes you can be asked to contribute to more than 10 wedding a year, na ukitoa chini ya laki moja unaonekana mtu wa hovyo hovyo.

Jamani ndugu zangu naombeni mwongozo mimi naona kama hii ni too much.

Badala ya michango ya vikao vya harusi basi tuihamishie kwenye Elimu na Matibabu.

AINA 10 za Wanawake Zitakazofanya Maisha yako Kuwa Magumu

$
0
0

Katika kuangalia tabia za wanawake, nakuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.

1. Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.

2. Mwanamke asieomba msamaha
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.

3. Mlalamishi
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.

4. Asiyejielewa
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.

5. Anayetawala na kutotosheka
Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.

6. Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.

7. Nusa Nusa
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye mara moja.

8. Asie na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.

9. Mcheza ndondi
Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.

10. Mtoto wa mama
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla kuwauliza wazazi wake.

Hatua 10 za Kumchagua Mchumba

$
0
0

Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.

Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na dazeni ya wapenzi.

Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.

Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli.

Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.

Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake. Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake.

Mwanamnke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Suzzy aliwahi kuniomba ushauri, akasema amechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo lake. Lakini kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari ameshafanya mapenzi na wanaume hao.

Nia ya swali lake ilikuwa ni kuniomba njia za kumtambua mwanaume mkweli bila kufanya naye mapenzi? Aliuliza hivyo huku akiwa na hoja kuwa wanaume wengi hawako tayari kuwa na uhusiano na msichana bila kufanya naye mapenzi na wakati huo huo huficha tabia zao chafu wakilenga kumnasa wamtakaye.

Binafsi nafahamu kuwa kuna wanawake/wanawake wengi ambao hujiingiza katika mapenzi kwa kutekwa na hadaa za mwili na kujikuta wanacheza mchezo wa kitoto wa pata potea.

Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya.

Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.

KWANZA- Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.

Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure.

PILI- Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.

TATU- Anza kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka.

NNE - Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.

Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.

TANO - Ajipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.

Ikibainika mwanaume aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa.

Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.

SITA - Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda.

Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.

SABA - Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana

NANE - Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.

TISA - Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.

KUMI - Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake.

Mwisho ni kwamba kanuni hizi huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na maradhi.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live


Latest Images