Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Zimebaki siku 30 Diamond Platinumz na Zari Kulitikisa Jiji la Dar-es-Salaam na Nchi Nzima, Mashabiki Muandae Viingilio.

$
0
0
Wachumba wa Zamani Diamond Platinumz na Zari wanatarajia kuandika historia nyingine kama ilivyo kawaida yao pale uwanja wa uhuru ambapo kutakuwa na matukio mengi sana ikiwemo album ya mwanamuzi Diamond Platinumz " A boy from Tandale" ambayo kwa tukio la kuzindua inataraji kuuza nakala 30,000 za mwanzo huku kukiwa na kiingilio kuwaona wasafi wote wakiongozwa na Diamond Platinumz.

Hata hivyo waandaaji wa tukio hili walishaomba uwanja wa taifa lakini wameambiwa utakuwa na matumizi hivyo wamepewa uwanja wa uhuru kwani kwa makisio yao waliona uwanja wa uhuru hautotosha kabisa lakini Plan imekuwa ni kufanya tukio hilo kila mkoa kwa kiingilio ambacho hakitasababisha watu kushindwa kupumua uwanjani.....

Katika siku hiyo kutakuwa na tukio lingine kubwa zaidi ambalo sitaliweka hapa kwa sababu za kibiashara lakini joto la tukio hilo litapanda zaidi ikifika march kwani kuna mengi zaidi yatatangazwa kuhusu Diamond na kuwaacha wengi midomo wazi....

Kikubwa zaidi ni kuwa tamasha hili hadi sasa linagombewa na kampuni kubwa mbili ambazo zinataka kuweka matangazo mule ndani ya uwanja siku ya tamasha ambalo bila shaka litaweka historia......

Wana jamvi kwa leo nawajuza haya tuu lakini mkumbuke kuwaona Diamond na Zari safari hii ni kwa pesa si bure tena.....

Ray Kigosi Atetea Uamuzi wa Kumvisha Hereni Mtoto wake Ambaye ni wa Kiume

$
0
0
Msanii wa filamu, Vincent Kigosi maarufu ‘Ray’ amesema kitendo cha kumvisha mtoto wake hereni ni kutokana na kuwa nyota kama yeye.

Ray amesema hayo alipozungumza na MCL Digital baada ya kuweka hadharani picha za mtoto huyo wa kiume aliyevishwa hereni hivyo kuzua gumzo. Maoni kadhaa yamekuwa yakitolewa kuhusu kitendo hicho pamoja na kunyolewa nywele staili ya kiduku.

Akizungumzia uamuzi wa kufanya hivyo kwa mtoto wake wa pekee aitwaye Jaden, msanii huyu aliyewahi kutamba na filamu za Oprah, Waves of Sorrow na Pretty amesema yeye ni nyota maarufu hivyo mtoto wake lazima afuate nyayo zake.

“Mbona mimi baba yake nimetoboa masikio watu hawasemi, si kwa kuwa wanajua mimi ni mtu maarufu, hivyo umaarufu huu nilionao hata mtoto lazima awe nao japo sijamtoboa sikio atakuja kufanya hivyo mwenyewe kama ataamua atakapokuwa mkubwa,” amesema.

Ray amesema, “Hao wanaosema waendelee tu kusema kwa kuwa kusema ni haki yao, na huyu ni mwanangu hakuna mtu wa kunipangia nini cha kumfanyia.”


Mwananchi

Steve Nyerere "Siyo Siri Hata Mimi Nimewachoka Bongo Movies"

$
0
0
KOMEDIANI wa Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ anaamini kuwa, soko la sinema za Kibongo haliwezi kubadilika kama sura za waigizaji ni zilezile za kila siku ambazo hata yeye amezichoka.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Steve alisema kuwa, kama kila mtu anapotazama sinema anakutana na sura ya Kajala Masanja, Shamsa Ford, Aunt Ezekiel na wengine, watu wanachoka na mwisho wa siku ndipo linatokea anguko la sinema kama lilivyotokea.

Steve alisema kuwa, inatakiwa ufike wakati wale mastaa wakubwa waachie ngazi na kuwapa nafasi wengine ili watu waone ladha tofauti maana sura zao zimechosha mashabiki.

“Ninachokipigania ni kwamba waigizaji wakubwa wabaki na haki miliki zao, lakini sura za mastaa haohao zinachosha maana hata mimi nimezichoka,” alisema Steve.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya February 19

$
0
0

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya February 19

Sajenti Aapa Kumzalia Mtoto Dullah Makabila

$
0
0
Sajenti Aapa Kumzalia Mtoto Dullah Makabila
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Husna Idd ‘Sajenti’ ameapa kuwa lazima ampatie japo mtoto mmoja staa wa Singeli, Abdallah Makabila ‘Dullah Makabila’.

Sajenti aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, pamoja na kwamba miezi michache iliyopita alipata balaa baada ya ujauzito wake kutoka, lakini bado anaamini Mungu atamsaidia, atapata mwingine.

“Ninamuomba sana Mungu anifanikishe tena kwani nimepanga lazima nimzalie Dullah (Makabila),” alisema Sajenti.

Sajenti aliongeza kuwa, Dullah anapenda watoto na hilo ndilo lililomhamasisha zaidi kutamani kumpatia mtoto.

Mama Samia Awasili Mwanza kwa Ziara

$
0
0
Mama Samia Awasili Mwanza kwa Ziara
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini Mwanza jana jioni na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka.

Makamu wa Rais anategemewa kuanza ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo kesho mkoani Simiyu.

Katika ziara hiyo itakayoanza leo tarehe 19/2/2018 na kumalizika tarehe 22/2/2018, Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Kiloleli na kuweka jiwe la msingi na baada ya hapo atazungumza na wanachi Lamadi .

Pia Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za viongozi wa mkoa katika eneo la Nyaumata.

Miradi mingine ambayo Makamu wa Rais ataitembelea ni Kukagua Ujenzi wa Barabara za Lami Bariadi mjini chini ya Programu ya uimarishaji wa Serikali za Mitaa za Mjini.

Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa la Mwanjoro na kusalimia wananchi siku ya tarehe 20, pia atasalimia wananchi wa Mwanhuzi Mjini, Mwandoya (Meatu)

Tarehe 21, Makamu wa Rais atafungua Kongamano la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda Tanzania kasha atafungua jengo la Utawala la halmashauri ya Itilima na kusalimia wananchi, kufungua jingo la upasuaji la Samia Suluhu Hassan katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa na kuzungumza na wananchi katika viwanja vya nguzo nane.

Siku ya tarehe 22, Makamu wa Rais ataongoza Mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria .

Mtulia Achaguliwa kwa Kukosa Kura za Watu 40,000 wa Mwaka 2015 Kinondoni

$
0
0
Mtulia Achaguliwa kwa Kukosa Kura za Watu 40,000 wa Mwaka 2015 Kinondoni
Wakati Maulid Mtulia wa CCM akitangazwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Kinondoni, takwimu zinaonyesha kuwa amechaguliwa na chini ya nusu ya wapiga kura waliomchagua mwaka 2015.

Hali hii ni tofauti kwa Dk Godwin Mollel wa CCM, ambaye alitangazwa mshindi katika Jimbo la Siha kwa kupata kura 25,611 ikiwa ni zaidi kwa kura 2,865 ya zile alizopata mwaka 2015 ambazo ni 22,746.

Katika matokeo yaliyotangazwa jana na msimamizi wa uchaguzi wa Kinondoni, Aaron Kagurumjuli, Mtulia ameibuka mshindi kwa kupata kura 30,247 huku Salum Mwalimu wa Chadema akipata kura 12,353.

Kagurumjuli ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kinondoni alisema idadi ya wapiga kura walioandikishwa walikuwa 264,055, waliopiga kura ni 45,454 sawa na asilimia 17.2, kura halali ni 44,867 na zilizoharibika ni 587.

Idadi hiyo ya kura za Mtulia ni nusu ya zile alizopata mwaka 2015 katika Uchaguzi Mkuu akiwa CUF na kuungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa Ukawa kwani alipata kura 70,337 dhidi ya mpinzani wake wa CCM, Idd Azzan aliyepata kura 65,964.

Bila kujali sababu nyingine, hii ina maana kuwa watu 40,000 ambao walimchagua Mtulia mwaka 2015 hawakujitokeza au hawakumchagua juzi.

Matokeo ya Mtulia ni tofauti na yale ya Siha ambako msimamizi wa uchaguzi, Valerian Juwal alimtangaza Dk Mollel mshindi kwa kupata kura 25,611 huku Elvis Mosi wa Chadema akipata kura 5,905.

Kwa matokeo hayo, Dk Mollel aliyehama Chadema na kujiunga na CCM amepata kura zaidi ya zile za mwaka 2015 ambazo ni 22,746 zilizompa ushindi dhidi ya Aggrey Mwanri wa CCM aliyekuwa akitetea jimbo hilo aliyepata kura 18,584.

Akizungumzia matokeo hayo, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (Ruco), Profesa Gaundence Mpangala alisema chaguzi ndogo za ubunge hujitokeza kwa mtu kufariki dunia au mahakama kutengua ushindi lakini hili la watu kujiuzulu na kugombea tena ni kitu kipya.

“Wananchi wamechoka na siasa za aina hii mpya ya mtu kujiuzulu na huyohuyo anagombea tena, huu ni mgomo baridi ambao ili kuumaliza tuondokane na siasa za aina hii,” alisema Profesa Mpangala.

Alisema mwanasiasa kuwa upinzani au chama tawala si kosa; kubwa ni kuleta maendeleo kwa wananchi na kila upande haupaswi kuuona mwingine ni adui.

“Rais wa sasa wa Zimbabwe (Emmerson Mnangagwa) ameamua kukutana na vyama vyote vya upinzani ili kujadili jinsi ya kuendesha uchaguzi huru na haki ujao, sijui hapa Rais (John) Magufuli anaweza kukutana na wapinzani, sioni hilo,” alisema.

Akichambua matokeo hayo kwa jumla, Profesa Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema, “Unajua chaguzi ndogo hazijalishi zinasababishwa na kifo au mahakama lakini zimekuwa hazina mvuto na kwa mfumo wetu wengi wape ndicho kinachojitokeza.”

Alisema hakuna sababu za msingi zinazomlazimisha mtu kwenda kupiga kura na wengine wanaona hata wasipokwenda kupiga kura hakuna tatizo au wanajiuliza mbunge atamsaidia kitu gani.

   

Undani Kifo cha Mwanafunzi Aliyeuawa kwa Kupigwa Risasi

$
0
0
   Undani Kifo cha Mwanafunzi Aliyeuawa kwa Kupigwa Risasi
SIKU tatu zikiwa zimepita tangu kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Maftah (22), imeelezwa alipanda daladala ambalo mauti yalimfika humo akipeleka barua ya kuomba kufanya mazoezi kwa vitendo aliyokuwa akitarajia kuanza Jumatatu ijayo mkoani Pwani.


Akwilina alipigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni na polisi waliokuwa wakijaribu kutawanya maandamano ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ijumaa jioni.

Rais John Magufuli jana alisema katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya Twitter kuwa "Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili."

Rais Magufuli pia alielezea kusikitishwa "sana" na kifo cha Akwilina, na kutoa pole kwa familia, ndugu, wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huo. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako alisema marehemu alikuwa ni miongoni mwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

Aidha, Prof. Ndalichako alisema siku ya Ijumaa Akwilina alikuwa njiani kupeleka barua ya kuomba kufanya kazi kwa vitendo katika moja ya kampuni zilizopo Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Marehemu alipanda daladala linalofanya safari kati ya Mabibo na Makumbusho katika kituo cha NIT na kufuatia maelezo ya waziri kwamba alikuwa akielekea Bagamoyo, ilikuwa ashuke mwisho wa safari kabla ya kuunganisha daladala nyingine kwenda Bunju Sokoni au Tegeta Nyuki zilizo stendi za Bagamoyo. 

Taarifa za kipolisi zilizotolewa jana zilisema mwili wa marehemu aliyekuwa amekaa kiti cha nyuma katika daladala hiyo yenye namba T558 CSX aina ya Nissan Civilian, ulikutwa ukiwa na jeraha kubwa kichwani lililooneka kutokana na kupigwa na kitu chenye ncha kali, kilichoingia upande wa kulia na kutoka upande wa kushoto.

Prof. Ndalichako alisema Akwilina alikuwa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Ununuzi na Ugavi katika chuo hicho.

"Wizara yangu itagharamia mazishi yake hadi hapo atakapopumzishwa katika makao yake ya milele," alisema Prof. Ndalichako. "Tutasimamia shughuli zote za msiba huo.

"Tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki... kwa uongozi wa NIT, kwa wanafunzi na wananchi wote.

"Serikali imepata pigo kubwa kwa sababu inawekeza pesa nyingi katika kuwasomesha wanafunzi kuanzia elimu ya msingi hadi elimu ya juu kwa kuwapa mikopo."

FUNDISHO KWA MTUAkirejea agizo la Rais Magufuli la vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni alisema:

Uchunguzi utakapokamilika serikali itatoa taarifa ambayo itakuwa fundisho kwa mtu mwingine kusababisha hali kama hiyo kutokea tena. Aidha, Masauni alisema siasa isiwe chanzo cha watu kufariki au kuwa walemavu.

Alisema serikali kwa sasa inataka kujiridhisha undani wa tukio hilo lilivyotokea bila ya kumuonea mtu yoyote, na kwamba uchunguzi hautachukua muda mrefu.

"Nani anajua ile risasi ilitoka kwa nani? Kama yupo anayejua aje atuambie, kwa sasa maiti ipo hospitali tunasubiri taarifa, hatuwezi kukurupuka tu," alisema Masauni.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilishasema mapema jana linawashikilia askari wake sita kufuatia tukio hilo na silaha zao zinachunguzwa, ikiwa ni pamoja na kuzipeleka kwa wataalamu wa milipuko kwa uchunguzi wa kina.

Aidha, jeshi hilo lilisema limeunda timu ya upelelezi ili kuchunguza chanzo cha kifo cha binti huyo.

Mzee Majuto Afunguka Baada ya Kufanyiwa Upasuaji " Mungu Mkubwa

$
0
0
Mzee Majuto Afunguka Baada ya Kufanyiwa Upasuaji " Mungu Mkubwa
MUNGU mkubwa! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kusikia habari njema kuwa, mchekeshaji Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ au ‘King Majuto’ mwenye umri wa miaka 60 kufanyiwa upasuaji na sasa anaendelea vizuri, Ijumaa Wikienda limedokezwa.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda akiwa katika Hospitali ya Tumaini, Upanga jijini Dar, wikiendi iliyopita, mke wa Mzee Majuto, Aisha Yusuf alisema kuwa, mumewe huyo ambaye alikuwa akisumbuliwa na saratani ya tezi dume alifanyiwa upasuaji huo Februari 12, mwaka huu na hali yake inaendelea vizuri.

“Tunamshukuru sana Mungu, Mzee Majuto anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji japokuwa tupo hospitali bado hatujajua ataruhusiwa kutoka lini ndiyo tunawasikilizia madaktari ila hana tatizo, anaendelea vizuri kabisa kwa sasa,” alisema Asha.

Kwa upande wa wasanii, Afisa Habari, Uenezi, Uhusiano na Umma wa Chama cha Waigizaji wa Kinondoni, Dar, Masoud Kaftany alithibitisha kwamba hali ya mzee huyo inaendelea vyema hivyo kuwataka wasanii kwenda kumjulia hali.

“Mzee Majuto ameshafanyiwa upasuaji na sasa ni ruksa kwa wasanii wenzake kwenda kumuona na kumjulia hali kwa utaratibu watakaoukuta kwa wauguzi, tunamshukuru sana Mungu kwa hili,” alisema Kaftany.

Mzee Majuto aliyezaliwa mwaka 1958 alianza kusumbuliwa na ugonjwa ambao hakugundulika mapema kabla ya kubainika kuwa na saratani ya tezi kisha kufanyiwa upasuaji. Ijumaa Wikienda linamuombea Mzee Majuto apone mapema!

Wafungwa Waliteka Gereza Wawaweka Chini ya Ulinzi Wafanyakazi wa Gereza Hilo

$
0
0
Wafungwa Waliteka Gereza Wawaweka Chini ya Ulinzi Wafanyakazi wa Gereza Hilo
Wafungwa wamechukua udhibiti wa gereza kwenyr mji wa Rio de Janeiro nchini Brazil na wanawashika mateka baadhi ya wafanyakazi wa gereza hilo.

Polisi waliojihami wanalizunguka gereza hilo lenye msongamano wa wafungwa la Japari ambalo liko chini ya udhibiti wa genge moja la wahalifu lenye guvu nyingi mjini humo.

Wafungwa watatu ambao walihusika katika kulidhibiti gereza hilo wamepigwa risasi lakini hawajapa majeraha ya kuwatishia maisha.

Ghasia hizo zinatokea siku mbili baada ya Rais wa Brazil Michel Temer, kusaini sheria ya kuwapa wanajeshi ruhusa ya kusimamia usalama wa mji wa Rio de Janeiro.

Maafisa wa gereza wanasema ghasia hizo huenda zimechangiwa na hatua mpya za ulinzi.

Dk Mollel apita kushukuru wapiga kura wa

$
0
0
Dk Mollel apita kushukuru wapiga kura wa
February 17 ni siku ambayo jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro kulifanyika uchaguzi mdogo na mgombea Ubunge kupitia tiketi ya CCM Dr Godwin Mollel alifanikiwa kuibuka mshindi wa Ubunge kwa kupata jumla ya kura 25611.

Leo baada ya ushindi huo ameamua kupita kwenye kata nne kwa ajili ya kushukuru na kusema kuwa hatofanya sherehe kama wabunge wengine wanavyofanya baada ya kutangazwa washindi, bali atafanya shughuli za maendeleo kama sehemu ya sherehe yake.

Dr Mollel katika kata ya Nduimet ameahidi kutoa mabati 200 yatakayosaidia kukamilisha ujenzi wa darasa la shule ya Lemushu, akiwa anaendelea na zoezi hilo amepita pia kwa viongozi wa dini na kuahidi kushirikiana nao baada ya kutembelea kata za Nduimet, Engaranairobi, Sanya Juu na kata ya Lawate.

Nafasi za Ajira zilizotangazwa Siku ya Leo

$
0
0

Zari Hataki Kusikia Kuhusu Diamond Wala Michepuko Yake

$
0
0
Zari Hataki Kusikia Kuhusu Diamond Wala Michepuko Yake
Drama kati ya Zari The Boss Lady na Diamond Platnumz bado zipo pale tena katika kiwango cha juu.

Safari hii Zari amewajia juu wale ambao wanamfuata mtandaoni na kumuuliza kuhusu kuachana kwake na Diamond. Zari akiwa Insta Live ameonyesha kuchukizwa na hilo.

Zari amesikika akisema hii nafasi, hili jukwaa ni kusuhu Zari pekee, sio Diamond, sio mama yake wala michepuke yake na kuongeza maneno makali kidogo, kisha kurudia tena hapa ni kuhusiana na Zari tu.

Utakumbuka Jumatano ya wiki iliyopita katika siku ya wapendanao (Valentine’s Day) Zari The Boss Lady alitangaza rasmi kuachana na Diamond kutokana na kuchoshwa na habari za kusalitiwa ambazo husikika kila siku katika vyombo vya habari. Katika mahusiano yao Diamond na Zari wamefanikiwa kupata watoto wawili ‘Tiffah na Nillan’.

Maskini Mwanamke Achomwa Moto na Waganga wa Jadi Akitafuta Uzazi

$
0
0
Maskini Mwanamke Achomwa Moto na Waganga wa Jadi Akitafuta Uzazi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, linawashikilia waganga wa jadi wawili ambapo mmoja ni mkazi wa Kijiji cha Obwere na Michael Jacob wa Omuga kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumuunguza moto, Emiliana Thomas anayeishi Kijiji cha Omuga wilayani Rorya.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Henry Mwaibambe alisema jana kuwa, majeruhi huyo ambaye ni mwanamke anayesumbuliwa na tatizo la kutopata ujauzito, waganga hao walimwaminisha kuwa ataupata.

Alisema walimwambia ili apate mtoto ni mpaka kuku imwagiwe mafuta ya taa na iteketezwe moto huku mama huyo akiwa ameishikilia mikononi.

Kamanda alisema baada ya waganga hao kuwasha moto ulimunguza na kumsababishia majeraha.

Mwaibambe alisema, awali waganga hao walimweleza mwanamke huyo kuwa anasumbuliwa na mashetani ndani ya tumbo na ndio yanayomfanya asizae.

Alisema walimweleza kwamba kuku ikiteketea ikiwa mikononi mwake atakuwa ameondokana na mashetani, hivyo ni lazima iteketezwe.

Kamanda huyo alisema baada ya waganga hao ‘kumsomesha’ mwanamke huyo alikubali na ndipo walipoimwagia mafuta ya taa kuku hiyo na kuwasha moto kwa kibiriti uliolipuka na kumjeruhi kifuani na mikononi.

Mwaibambe aliongeza kuwa, hali ya mama huyo ni mbaya na anaendelea na matibabu katika Hospital ya Kowak wilayani humo.

Mmoja wa waganga hao wa jadi, Jacob alisema tukio hilo ni ‘bahati mbaya’.

“Alikuja akiomba tiba, sasa kwa bahati mbaya mafuta yalikuwa yamemumwagikia mikononi na mikono ya nguo aliyokuwa amevaa ilikuwa hadi mikononi, wakati tumewasha moto ndipo ukamuunguza,” alisema Jacob.

Akizungumza na gazeti hili, mwakilishi wa Chama cha Tiba Asili mkoani Mara, Jacob Matiko alilaani kitendo hicho kuwa hakiendani na taratibu za tiba na kinakiuka sheria inayozuia vitendo hivyo huku akiwataka waganga kutofanya utapeli iwapo hawawezi kufanya tiba kama matabibu asili.

Wakati huohuo, polisi inawashikilia watu wawili kutoka Ethiopia kwa kuingia nchini bila vibali.

Mwaibambe alisema katika tukio hilo waliwakamata pia Watanzania wawili ambao walikuwa wakiwasafirisha raia hao wa kigeni akiwamo na Pasaka Meng’anyi mkazi wa Buhemba mjini Sirari wilayani Tarime.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Meng’anyi alieleza kuwa alipewa kazi ya kuwapokea raia hao kutoka Stendi ya Tarime hadi Mwanza na wakifika mjini humo kuna mtu atakayewapokea.

Alisema ili kufanikisha kazi hiyo alilipwa Sh300,000 huku mwenzake akiahidiwa kulipwa 100,000 ambazo bado hajalipwa baada ya kuwatoa Sirari hadi Stendi ya Tarime.

Edu Boy Amuwashia Moto Dogo Janja " Kuoa Kusikufanye Uwe na Hharau kwa Wengine"

$
0
0
Edu Boy Amuwashia Moto Dogo Janja " Kuoa Kusikufanye Uwe na Hharau kwa Wengine"
Msanii wa Hip Hop anayewakilisha Mwanza, Edu Boy amefunguka na kudai amekerwa na kitendo cha Dogo Janja kumuita yeye mtoto mdogo na kumtaka atengue kauli yake hiyo kwani kuoa kwake kusimfanye awe na dharau kwa wengine.

Edu Boy amebainisha hayo wakati akizungumza na Bill Sepenga kwenye kipindi cha 'FRIDAY NIGHT LIVE' (FNL) inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya kupita takribani 'week' moja tokea Dogo Janja kuzungumza kupitia eNewz na kudai anamchukulia Edu ni mtoto ambae anahitaji kuisoma vizuri 'game' ya muziki ili aweze kukua nayo hivyo hawezi kubishana nae.

"Hii tabia ya Dongo janja ya kuwa anahojiwa kwenye vyombo vya habari aniita mimi mtoto wakati inabidi atengue kauli yake. Kufunga ndoa kusisababishe kuita watu watoto, kuna ndoa nyingine unakuwa unajitwisha mabomu ujue. 'so' inabidi awe makini sana, mabomu yasije yakarupuka hadharani akafa na watu", amesema Edu Boy.

Kwa upande mwingine, Edu Boy amemtaka Dogo Janja awe makini na ndoa yake ili mabomu yakija kurupuka afe mwenyewe.


Mahakama ya Ufisadi Kuamua Hatima ya Majalada 106 ya Makontena Yaliyotoroshwa Bila Kulipa Kodi

$
0
0
Mahakama ya Ufisadi Kuamua Hatima ya Majalada 106 ya Makontena Yaliyotoroshwa Bila Kulipa Kodi
Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu Mahakama ya Ufisadi, leo inatarajia kutoa uamuzi wa kuyapokea au kutoyapokea majalada 106 yanayohusu makontena 329 yaliyotoroshwa katika Bandari Kavu ya Azam (AICD), bila kulipiwa kodi.

Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayotokana na utoroshaji wa makontena hayo, uliomba kuwasilisha mahakamani majadala hayo kupitia kwa shahidi wake wa kwanza, Ashrafu Khan, yapokewe kama vielelezo ya ushahidi.

Hata hivyo, mawakili wa utetezi Kung’e Wabeya na Nehemia Nkoko waliweka pingamizi dhidi ya shahidi huyo kuwa si mtu sahihi, hivyo hana mamlaka kisheria kuyawasilisha mahakamani majalada hayo kama vilelezo kwa kuwa si yeye aliyeyaandaa wala hayakuwa mikononi mwake.

Nkoko alipinga kuwa majalada hayo si sehemu ya nyaraka au vielelezo vilivyotajwa na upande wa mashtaka katika hatua ya ufungaji wa kesi hiyo katika mahakama ya chini.

Kiongozi wa jopo la mawakili wa Serikali, Vitalis Peter aliiomba mahakama ilitupilie mbali pingamizi hilo akidai kuwa shahidi huyo ni sahihi kuwasilisha vielelezo hivyo, kwani hakuna kifungu cha sheria kinachoeleza kuwa kama shahidi si mtunzaji wa vielelezo hawezi kuviwasilisha maakamani.

Kuhusu hoja kwamba vielelezo hivyo havikutajwa katika hatua ya ufungaji na uhamishaji shauri hilo katika mahakama ya chini, Vitalis alidai yalitajwa kwa jina la jumla kama Azam custom clearence files na nakala zake mawakili hao walipewa.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Winfrida Korosso anayesikiliza kesi hiyo aliahirisha kwa ajili ya kuandika uamuzi ambao alipanga kuutoa leo.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Raymond Louis (39) ambaye ni meneja wa operesheni za ulinzi na usalama, AICD; Hamis Omary (48), mchambuzi mwandamizi wa masuala ya biashara TRA, Haroun Mpande (28) wa Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta (ICT), Khalid Yusuph Hassan na Benson Vitalis Malembo.

   

Daimond Kufanya Ziara Kwenye Majiji 12 Nchini Marekani

$
0
0
Daimond Kufanya Ziara Kwenye Majiji 12 Nchini Marekani
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametangaza ziara yake ya muziki nchini Marekani ambapo atatumbuiza kwenye majiji 12 nchini humo.

Ziara hiyo inayoanza tarehe 22 June hadi 23 July 2018, Diamond atawapagawisha kwa burudani wakazi wa Majiji ya New York, Los Angeles, Minnesota, Houston, Seattle, Kansas City, Washington DC, Boston, Atlanta, Columbus, Philadephia, Dallas.

“Kuelekea kwenye Kuachiwa Rasmi kwa Albam ya #AboyFromTandale Ndugu zangu Mlio Marekani Jiandaeni kwa Ziara ya #AboyFromTandaleUSATour mdani ya State hizo 12 kuanzia tareh 22/06 hadi 23/07 Mwaka 2018!!“amesema Diamond Platnumz.


Ziara hiyo ya ‘A Boy From Tandale’ itakuja baada ya kuachiwa kwa album yake ya ‘A Boy From Tandale’ mwezi Machi 14, 2018.

Soma zaidi – Diamond Platnumz asogeza mbele tarehe ya kuachia album yake ‘A Boy From Tandale’

Zitto Kabwe Kufanya Ziara ya Kutembelea Maeneo Yanayoongozwa na ACT Wazalendo

$
0
0
Zitto Kabwe Kufanya Ziara ya Kutembelea Maeneo Yanayoongozwa na ACT Wazalendo
Chama cha ACT- Wazalendo kupitia Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe pamoja na viongozi wengine wa chama hicho wameanza ziara ya mikoa 8 kutembelea Kata mbalimbali ambazo wananchi walichagua Madiwani kutoka chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Zitto kupitia taarifa yake aliyoitoa leo, imeeleza kuwa lengo la ziara ni kuwashukuru wananchi na kushiriki kazi za maendeleo katika Kata hizo.

Leo, nikiwa pamoja Na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa, Mama Annamarrystella Mallack, Katibu wa Kamati hiyo, ndugu Janeth Joel Rithe, pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Sera na Utafiti, ndugu Emmanuel Mvula tumeanza ziara ya mikoa 8 kutembelea Kata mbalimbali ambazo wananchi walichagua Madiwani kutoka chama chetu cha ACT Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Lengo la ziara ni kuwashukuru wananchi, kushiriki kazi za maendeleo katika kata, kuzungumza na kamati ya maendeleo ya kata, kuzungumza na wananchi wa kata husika, kuangalia utendaji wa madiwani kutokana na matarajio ya wananchi, kuona vikwazo na changamoto za Madiwani wetu, kusisitiza Uwazi, Uwajibikaji na Ushirikishwaji wa wananchi kwenye masuala yote ya Kata, pamoja na kufanya tafiti juu ya masuala ya kisera pamoja na miradi ya maendeleo ambayo ACT Wazalendo Taifa tunaweza kuyabeba kusaidia madiwani wetu.

Ziara itafanyika kwa siku 19 katika mikoa 8 husika, ambako leo tumeanzia Kata ya Kiparang’anda, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Kiparang’anda
Mkuranga
Pwani
Februari 19, 2018

Nabii Tito Kupelekwa Mirembe na Mahakama

$
0
0
Mahakama Yaamuru Nabii Tito Apelekwe Mirembe Akapimwe Tena Akili
Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imemuamuru Mkuu wa Gereza la Isanga kumpeleka hospitali kuu ya magonjwa ya akili (Mirembe), mkazi wa kijiji cha Nong'ona Tito Onesmo Machibya maarufu kama (Nabii Tito), ili kuchunguzwa kama ana ugonjwa wa akili au la.


Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo James Karayemaha amesema anahitaji majibu hayo mnamo Marchi 5 mwaka 2018 siku ambayo mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani ikiwa ni baada ya agizo la mtuhumiwa huyo kupimwa akili kutotekelezwa hapo awali.

Nabii Tito Machibya alifikishwa Mahakamani hapo akituhumiwa kufanya uchochezi wa kidini kupitia mafundisho anayo yatoa na amekuwa akiieleza Mahakama kuwa amekuwa akifanya hivyo kwa sababu ana matatizo ya akili na kutoa vithibitisho toka hospitali ya Taifa Muhimbili.

Picha ya Bastola Yamwingiza Matatani Mbunge

$
0
0
Picha ya Bastola Yamwingiza Matatani Mbunge
Mbunge wa Australia George Robert Christensen amejikuta akikabiliwa na wakati mgumu pamoja na shutuma baada ya kutuma picha kwenye ukurasa wake wa Facebook akiwa na bastola huku akidaiwa kutoa maneno ya kejeli kwa wafuasi wa Chama cha Green.


Maneno yanayodaiwa kuambatanishwa na picha hiyo yamesomeka "mnahisi mna bahati,ninyi watu msio na thamani" (“Do you feel lucky, greenie punks?”)

Chama cha Green kimesema kwamba kauli iliyotolewa na mbunge huyo wa Chama cha Conservative ni ya kusikitisha sana na kuainisha kwamba ameitoa kipindi ambacho watu 17 wameuwawa nchini Marekani katika shambulio la bunduki katika shule moja jimboni Florida..

Polisi katika mji huo imesema kwamba inaangalia uwezekano wa ikiwa uchunguzi unaweza kufanyika au la ingawa mbunge huyo amekaririwa akisema kwamba kauli hiyo aliyoituma ilikuwa utani.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo  Malcolm Turnbull amesema kauli hiyo iliyotumwa katika ukurasa wa facebook wa mbunge huyo haikuwa sahihi.

Taarifa nyingine kutoka makao makuu ya jeshi la polisi nchini humo imesema inapima kauli hiyo kabla ya kuchukua hatuahuku Wapinzani wa kisiasa wakimshutumu  Christensen kwa kuchochea vurugu.

Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>