Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Baada Simba Kushinda Kwa Kishindo Sasa Kutua Dar Kibabe

$
0
0
Baada Simba Kushinda Kwa Kishindo Sasa Kutua Dar Kibabe
Kikosi cha klabu ya Simba kinatarajia kurejea kikitokea nchini Djibouti katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Simba SC ilikuwa nchini humo kwaajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika CAF dhidi ya Gendarmerie na kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 1 – 0 bao likifungwa na mshambuliaji wao raia wa Uganda, Emmanuel Okwi katika kipindi cha pili.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo umeseme kuwa Simba itaondoka Djibouti majira ya saa 12:05 jioni.

Kikosi cha Simba kurejea leo nchini.
Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka nchini Djibouti saa 12:05 jioni ya leo kurejea nchini kwa kutumia usafiri wa ndege kupitia Shirika la KQ.

Simba SC imefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu baada ya kuifungashia Gendarmerie kwa jumla ya mabao 5 – 0.

Ben Pol Ashindwa Kuvumilia Afunguka Kuhusu Nywele za Vanessa Mdee

$
0
0
Ben Pol Ashindwa Kuvumilia Afunguka Kuhusu Nywele za Vanessa Mdee
Trend ya rangi za nywele kwa baadhi ya wasanii ndio inayochukua headlines katika mitandao ya kijamii kwa sasa ambapo Ben Pol alianza kuja na nywele za kijani kibichi na comments zikawa nyingi kutoka kwa mashabiki

AliKiba na Ommy Dimpoz ni baadhi ya wasanii ambao wamebeba headlines kutokana na muonekano mpya wa nywele zao baada ya kuzipaka rangi na kwa sasa Vanessa Mdee anabeba headlines hizo akiwa ana muonekano mpya kichwani wa rangi ya orange.

Kupitia mtandao wa instagram wa Ben Pol ameonekana kufarijika na kile ambacho Vanessa Mdee amefanya kichwani kwake kwa kupaka rangi ya orange

Inasikitisha! Mtoto wa Miaka Sita Afariki Baada ya Kupelekwa Mlimani Kutolewa Mapepo

$
0
0
Inasikitisha!  Mtoto wa Miaka Sita Afariki Baada ya Kupelekwa Mlimani Kutolewa Mapepo
 Mtoto wa miaka sita amefariki dunia akiombewa mlimani alikopelekwa kutolewa mapepo, huku mama yake mzazi akishikiliwa polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo akizungumzia tukio hilo amesema lilitokea Februari 18,2018 saa tano asubuhi katika mlima Gambiwe.

Amesema mama wa mtoto Neema Petro (25) na mke mwenzake Raheli Musa (25) walikwenda mlimani na mtoto huyo kwa ajili ya maombi na kufunga.

Kamanda amesema wanawake hao wakazi wa kijiji cha Bukulu wilayani Nyang'hwale wanashikiliwa kutokana na kifo cha mtoto Frank Bariki (6), ambaye mwili wake umekutwa na majeraha shingoni na kwenye mbavu.

Akatwa Sehemu za Siri na Mkewe Baada ya Kukutwa na Picha za Ngono Kwenye Simu

$
0
0
Akatwa Sehemu za Siri na Mkewe Baada ya Kukutwa na Picha za Ngono Kwenye Simu
Wataalamu wa mambo wanasema wivu ni kitovu cha kuimarisha penzi kwa watu walio kwenye ndoa lakini endapo ukizidi unakuwa ni kero na sumu kwa wanandoa, na hilo limethibitishwa kwenye familia ya Azad Singh huko Joginder Nagar mjini Jalandhar nchini India ambapo mzee huyo amejikuta katika hali mbaya kiafya baada ya kukatwa sehemu za siri na mkewe.

Singh (53) alishambuliwa na mkewe kwa kuhisiwa kuchepuka baada ya simu yake kukutwa ikiwa na picha za ngono ambapo mkewe alihisi kuwa picha hizo ni za michepuko yake.

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Sukhwant Kaur  (37) amedai kuwa, mumewe usiku wa tukio  alikuwa anaongea na simu na watu ambao hakuwatambua, na baadaye aliposhika simu hiyo wakati mumewe akiwa amelala alikuta kuna meseji za mapenzi kutoka kwenye namba ngeni na picha za ngono ambapo alihisi tayari ameshasalitiwa na ndipo alipoamua kumjeruhi kwa kumkata sehemu zake za siri.

Kwa ripoti iliyotolewa na Jeshi la polisi mjini Jalanddhar imeeleza kuwa mwanamke huyo alichukua hatua baada ya kuripoti kwa muda mrefu kwa ndugu zake kutaka suluhu juu ya tabia ya mumewe ya kumsaliti kwenye ndoa.

“Tulimkamata mwanamke mmoja aliyekuja kuripoti kituoni tarehe 19 Februari 2018 kwa kosa la kumjeruhi mumewe kwa kumkata sehemu zake za siri kwa kisu na kisha kuzidumbukiza chooni, baada ya tukio hilo majirani walisikia kelele na ndipo walipochukua maamuzi ya kumpeleka hospitali ambapo yupo hadi sasa anapatiwa matibabu nahali yake bado ni tete. Sababu kubwa ya Mama huyo kufanya hivyo ni amedai ni wivu wa kimapenzi,  bado jeshi tunaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo,“amesema Kamanda msaidizi wa kituo cha polisi mjini Jalandhar aitwaye Satinder Kumar.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail Mama huyo wa watoto wawili amesema alimvizia mumewe akiwa amelala na kumkata sehemu za siri kisha kuzitumbukiza chooni.

Sakata la Kumfukuza Miguna Lachukua Sura Mpya ....... Serikali, Mahakama Zavutana

$
0
0
Sakata la Kumfukuza Miguna Lachukua Sura Mpya ....... Serikali, Mahakama Zavutana
Sakata la kumfukuza nchini mwanasheria maarufu wa kenya Miguna Miguna linazidi kuchukua sura mpya baada ya mahaka Kuu kuamuru arudishwe nchini mara moja.


Jaji Luka Kimaru ameamuru Dkt Miguna arudishwe Kenya kwa kuwa Serikali ilikaidi agizo la mahakama, la kutakiwa kufikishwa mahakamani kwa mwanasheria huyo baada ya tukio la kumuapisha Raila Odinga.

Jaji Kimaru amesema hatua ya serikali kumfukuza Miguna ni kinyume cha katiba na sheria za kimataifa na kwamba mtu moja hawezi kupokonywa uraia wake.

Miguna ni mzaliwa wa eneo la Nyando, kaunti ya Kisumu lakini alipata uraia wa Canada alipoenda kusoma elimu ya juu na kuanza kufanya kazi za sheria.

Kwa upande wa serikali imesema ilipasa kumchukulia hatua hiyo Miguna baada ya kupata taarifa kutoka kwa usalama wa Taifa, kuwa mtu huyo ni hatari kwa usalama wa nchi.

Feza Kessy Afunguka Alivyomtongoza Msanii Mwenzake

$
0
0
Feza Kessy Afunguka Alivyomtongoza Msanii Mwenzake
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ametokea kwenye tasnia ya urembo, Feza Kessy, amekiri kuwahi kumtongoza mwanaume ambaye alitokea kumpenda, kitu ambacho ni kigumu kwa mabinti wengi.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Feza amesema alipoachana na mpenzi wake aliyepita alikaa na upweke kwa muda mrefu, lakini alikuwa na hisia za mapenzi kwa msanii Cyril kwa muda mrefu tangu akiwa kwenye mahusiano ya awali, na kuamua kumwambia ukweli.

“Nilikuwa nam-like sana, yeye alikuwa anan-ilike kidogo, ye alitakiwa aje kunibembeleza kiukweli maana kipindi kile nilikuwa naupweke plus kuumizwa, nilikuwa natangaza nia kwakweli lakini akawa ananiambia ooh sijui nina mtu, sasa na mimi nikawa siamini nilidhani ananipima kwanza, lakini ndio ikawa hivyo hata mtu wake akanifuata inbox kunitaka niachane naye”, amesema Feza Kessy.

Pamoja na kutoswa huko kutoka kwa Singida Boy mwenye Six Pack Zake, Feza amesema wamebaki kuwa marafiki wazuri, lakini bado ana hisia za kweli kwa Cyril na sio kumzingua.



Mwenyekiti, Mwanasheria wa Halmashauri ya Misungwi Wakamatwa na Polisi

$
0
0
Mwenyekiti,  Mwanasheria wa Halmashauri ya Misungwi Wakamatwa na Polisi
JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana  na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoani hapa  imemkamata Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Anthony Bahebe.

Pia Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Alphonce Sebukoto naye amekamatwa na Jeshi hilo. Viongozi wote hao wanakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu wa fedha za umma.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

Kamanda Msangi alisema, Bw. Sebukoto alikamatwa Februari 19, 2017 na Bw. Bahebe amekamatwa leo na wote wanaendelea kuhojiwa na Polisi kwa kushirikiana na TAKUKURU.

Naye Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Ernest Makale alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Bahebe.

Alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo hayo kwa Bw. Bahebe Novemba 2017 wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya ukurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi ambapo jumla sh. milioni 138 ziliingizwa katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti huyo. Alisema kiasi kingine cha fedha kinachunguzwa kubaini kilipo.

Kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na juhudi za Serikali katika mapambado dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka pamoja na fedha za umma.

Februari 19, 2019 akiwa katika ziara yake wilayani Misungwi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimsimamisha kazi Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Sebukoto na kuagiza achungunzwe na vyombo husika.

Alichukua hatua hiyo baada Mwanasheria huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushindwa kuishauri vyema halmashauri hiyo na kuisababishia hasara ya sh. milioni 278.

Amesema Mwanasheria huyo Novemba 2017 wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya ukurugenzi aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Anthony Bahebe.

Waziri Mkuu alisema Bw. Bahebe aliishtaki halmashauri hiyo akidai kulipwa fedha kwa ajili ya kazi ya ukandarasi wa mradi wa maji Igenge uliojengwa na kampuni ya ukandarasi ya Seekevim.

Alisema mradi huo ulianza 2014 na ulitakiwa ukamilike 2015. Mwanasheria huyo aliidhinisha malipo hayo wakati ambao tayari hati maalumu ya uwakilishi ilikuwa imekwisha tangu Desemba 2015.

Alisema Mwanasheria alimlipa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kufanya kazi na Halmashauri jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma.

Hivyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi wa umma kuzingatia maadili ya utumishi na matakwa ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yao.

  (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 21, 2018.

Asasi za Kiraia Zapaza Sauti Zimetaka Tume Huru ya Uchanguzi Kuundwa Kuchunguza Mauaji

$
0
0
Asasi za Kiraia Zapaza Sauti  Zimetaka Tume Huru ya Uchanguzi Kuundwa Kuchunguza Mauaji
Asasi za Kiraia nchini zimetaka iundwe Tume huru ya uchunguzi wa kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Akwilina Akwiline itakayoundwa na Taasisi za Dini, Vyombo vya Habari, Majaji, Mahakimu, Polisi na Baraza la Vyama vya Siasa.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Equality for Growth, Jane Magigita amesema kuwa Asasi za kiraia zimesikitishwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

“Tunapendekeza iundwe Tume huru ya uchunguzi itakayohusisha Azaki, Taasisi za dini, vyombo vya Habari, Baraza la vyama vya siasa, wanahabari, Majaji, Polisi, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora kufanya uchunguzi juu ya vifo na vitendo vya utekwaji na utesaji,”-Magigita

“Pia ni kosa kubwa kuwaachia Polisi kujichunguza wenyewe katika matukio yanayowahusu,” -Magigita

Mbali na hilo, pia ameiomba Serikali itazame upya suala la upatikanaji wa Katiba mpya na mchakato wake uanze mwaka huu kwani ndiyo suluhisho la matatizo mbalimbali yanayotokea katika Jamii kwa sasa.

Hii Hapa Ratiba ya Viporo vya Simba na Yanga

$
0
0
Hii Hapa Ratiba ya Viporo vya Simba na Yanga
Bodi ya ligi imetangaza tarehe ya michezo ya kiporo ya timu za Simba na Yanga ambazo zinawakiklisha taifa kwenye michuano ya kimatifa barani Afrika ambapo Simba itacheza na Mbao FC huku Yanga ikicheza na Ndanda FC.

Mchezo wa Simba SC dhidi ya Mbao FC utafanyika Jumatatu ya Februari 26 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam wakati mchezo kati ya Ndanda FC dhidi ya Yanga SC utapigwa Februari 28.

Mechi hizo za raundi ya 19 hazikuchezwa kutokana na Simba kuwa nchini Djibouti kucheza na Gendarmerie kwenye mchezo uliochezwa jana na Simba SC kushinda bao 1-0. Yanga yenyewe itakuwa dimbani kucheza na St. Louis ya nchini Shelisheli.

Simba SC inarejea leo Dar es Salaam baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Gendarmerie Tnare mjini Djibouti City katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba SC inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 42, huku Yanga ikiwa na alama 37 katika nafasi ya pili ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 35 katika nafasi ya tatu.

Viongozi wa MDC-T Wavurugana Mazikoni kwa Tsvangirai

$
0
0
Viongozi wa MDC-T Wavurugana Mazikoni kwa Tsvangirai

Makamu wa Rais wa MDC-T Thokozani Khuphe, Katibu Mkuu Douglas Mwonzora na mratibu wa kitaifa, Abednico Bhebhe Jumanne walilazimika kujificha kwenye kibanda cha Waziri Mkuu wa zamani, Morgan Tsvangirai kukimbia vita vya madaraka ya chama.

Khuphe na Mwonzora wako upande ambao unapingana na upande wa kaimu kiongozi wa MDC-T Nelson Chamisa ambaye alitwaa madaraka saa chache baada ya kutangazwa kuwa Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa kansa ya utumbo.

Washambuliaji walimsakama Khuphe mara alipofika kwa ajili ya mazishi. Alipoonekana tu akishuka kwenye gari lake huku akiwa ameongozana na walinzi wawili na kuanza kutembea kuelekea nyumbani kwa Tsvangirai, kundi la watu lilimfuata mwanamama huyo na kuanza kumsakama.

Naibu waziri mkuu wa zamani alikimbia kuokoa maisha yake kwa kuingia nyumba ya jirani huku akifuatwa na kundi la watu. Baadaye aliokolewa na walinzi wa ZRP.

Khuphe alionekana akitetemeka na akitokwa machozi muda wote wakati Mwonzora alionekana dhahiri amefura kwa hasira. Bhebhe alichukua jukumu la kuwa mratibu na alionekana kuikubali hali hiyo.

Shuhuda mmoja alieleza hali ya kutisha wakati Khuphe na Mwonzora wakishambuliwa kwa maneno kabla ya kuingia ndani ya nyumba ya mmoja wa majirani wa Tsvangirai.

"Kundi la zaidi ya watu mia moja lilitumia mawe na fimbo kuwashambulia. Mwanamke mmoja (Lwazi Sibanda) alipigwa na chupa tupu ya bia na akawa anavuja damu.

"Walitishia kuchoma nyumba hiyo na wakatupa mawe kupitia dirisha kwa jitihada za kumpiga Khuphe," shuhuda aliliambia New Zimbabwe.

Mwonzora alithibitisha kuwa walishambuliwa, akimshutumu Chamisa kuwa nyuma ya vurugu.

"Mwanzoni watu 10 walitushambulia, lakini maofisa usalama waliwamudu. Wakaenda kuongeza nguvu na kurudi wakiwa zaidi ya 100," alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Amshauri Mumewe Kuoa Mke wa Pili ...... Amuandalia Mavazi ya Kuolea

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Pangani Amshauri Mumewe Kuoa Mke wa Pili ...... Amuandalia Mavazi ya Kuolea
Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah, ameushangaza umma baada ya kumpongeza mume wake kwa kuongeza mke wa pili, kwani ni kitendo cha nadra sana kwa wanawake kufanya hivyo licha ya kuwa misingi ya dini inaruhusu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mkuu wa wilaya huyo ameandika ujumbe huku akiujulisha umma kuwa wazo la mume wake kuongeza mke wa pili lilitoka kwake, baada ya kuona majukumu ya kazi yanambana na kushindwa kutekeleza majukumu ya ndoa.

“Assalaam Alaykum, nichukue nafasi hii kumpongeza Mume wangu  kwa kuongeza mke wa pili. Kwa kuwa dini yetu ya Kiislam inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu, kulingana na uzito wa majukumu yangu nalazimika mda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo mume wangu kukosa huduma za msingi”, ameandika Bi. Zainab Abdallah.

Mheshimiwa huyo wa serikali ya wamu ya tano aliendelea kuandika kuwa ...”Namshkuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi ombi langu, hatimaye nimempata mwenzangu wa kusaidiana naye majukumu mazito ya ulezi wa mume. Alhamdulillah, M/Mungu ametupa riziki na uwezo, hivyo tunapaswa kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa rabb atupe stara inshaaAllah.


VIDEO: Aliyekua Mgombea Chadema Kupinga Matokeo Uchaguzi Siha Mahakamani

$
0
0
Na Ferdinand Shayo
Aliyekuwa Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CDM) jimbo la Siha Mkoani Kilimanjaro Bw elvis Mosi amesema kuwa ana mpango wa kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo  ya uchaguzi yaliyompa ushindi Dr Godwin Mollel wa CCM kwa madai kuwa taratibu na kanuni za uchaguzi zilikiukwa hivyo  anatarajia kulifikisha suala hilo mahakamani.

Bw Mosi ambaye alipata kura 5905 dhidi ya kura 25611 za Dr Mollel amesema, wanakusanya ushahidi wa kutosha ambao utaiwezesha mahakama kutengua matokeo hayo na uchaguzi kurudiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake sanya juu bw mosi amezitaja baadhi ya taratibu hizo kuwa ni pamoja na kubadilisha matokeo ya kura zake katika vituo na kupewa dr mollel jambo ambalo lilimfanya asisaini fomu za matokeo..insert ya bw elvis mosi mgombea ubunge wa ccm jimbo la siha.

Afisa 0ganizesheni wa Halmashauri na serikali za mitaa wa cdm kanda ya kaskazini Bw Ndonde Totinan amesema, matokeo ya kata 11 kati ya 17 ya jimbo hilo yana utata mkubwa ambao hawaridhiki nao na idadi ya kura zilizopigwa ziliongezwa katika baadhi ya vituo....insert ya bw ndonde totinan afisa ognizesheni wa CMD kanda ya Kaskazini.

Naye Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CUF Bw .Tumsifuel Mwanri ambaye hakusaini fomu za matokeo amesema, uchaguzi huo haukuwa huru na ulijaa ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadam.

VIDEO:

JE Umehangaika na Matatizo ya Kimapenzi Kwa Muda Mrefu? Muone Shehe Chalo Atakutatulia Matatizo yako Kirahisi

$
0
0
JE umehangaika na matatizo haya kwa muda mrefu mtalamu Challo anayo dawa ya kuvuta mpenzi Je unasumbuliwa na mpenzi umeachwa na mpenzi au Mme mke na Bado unampenda na umejaribu sehemu nyingine Bila mafanikio njoo utatuliwe haraka na kundumisha ndoa yenu..

Umekimbiwa na mmeo mkeo au mpenzi na anaishi na mtu mwingine atarundi haraka kusafisha nyota mvuto wa mwili na biashara minguu kufa ngazi kuwaka moto ngiri tumbo kuunguruma na wakina Baba wasiojiweza katika tendo la uyumba kuchelewa kufika kileleni tunatibu Busha Bila oprasheni bali kwa kutumia vitabu vya dini

Tunatoa pete ya utajiri Bila mashariti mkufu wa bahati unauza Mali ya haindi unapoteza pesa kwenye biashara yako Bila kujua unataka kupandishwa cheo

Wasiliana na mtalamu Shehe Challo 0714006521

Timu ya Yanga Nayo Yafuata Nyayo za Mnyama Simba Kimataifa....

$
0
0
YANGA SC imefanikiwa kwenda Raundi ya Kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya sare ya 1-1 na wenyeji, Saint Louis Suns United jioni ya leo katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali Uwanja wa Linite mjini Victoria, Shelisheli.

Mabingwa wa Tanzania wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya Februari 10 kushinda 1-0 pia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bao pekee la kiungo Juma Mahadhi aliyekosekana uwanjani leo kwa sababu ya homa.

Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na marefa Madagascar, Andofetra Avombitana Rakotojaona aliyesaidiwa na Lionel Hasinjarasoa Andrianantenaina na Pierre Jean Eric Andrivoavonjy, hadi maopumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Bao hilo lilifungwa na kiungo mshambuliaji mjuzi wa kuuchezea mpira, Ibrahim Ajib Migomba dakika ya 45 akimalizia krosi nzuri ya beki wa kulia, Hassan Ramadhan Hamisi ‘Kessy’.

Kabla ya bao hilo, timu hizo zilikuwa zikishambuliana kwa zamu, ingawa hayakuwa mashambulizi ya kusisimua na ilikuwa kazi rahisi kwa safu zote za ulinzi kuokoa.

Katika kipindi hicho, ilishuhudiwa kila timu ikionywa kwa kadi ya njano, Herve Rakotoarison kwa upande wa Saint Louis dakika ya 16 na Nahodha, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwa upande wa Yanga dakika ya 29.

Kipindi cha pili, Yanga iliendelea kusukuma mashambulizi langoni mwa wenyeji kujaribu kuunenepesha ushindi wao, lakini wakaishia kukosa mabao ya wazi.

Saint Louis wakasawazisha bao hilo dakika ya pili kati ya nne za nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida kupitia kwa Nahodha wake, Betrand Esther aliyefunga kwa kichwa baada ya mabeki wa Yanga kuzembea kuokoa mpira wa juu.

Katika kipindi hicho, refa Andofetra Avombitana Rakotojaona aliwaonyesha kadi za njano Elijah Tamboo wa Saint Louis na Kessy wa Yanga kwa makosa tofauti.

Kwa matokeo hayo, Yanga itakutana na mshindi kati ya El Merreikh ya Sudan na Township Rollers ya Botswana. Township Rollers ilishinda 3-0 nyumbani pia.

Saint Louis; Michael Ramandimius, Jean Paul Algae, Steve Henriette, Damien Maria, Betrand Esther, Travis Laurence, Herve Rakotoarison/Jude Nancy dk58, Tahiry Andriamandimby, Mervin Mathiot/Roddy Melanie dk58, Elijah Tamboo, na Karl Hall.

Yanga SC; Youthe Rostand, Hassan Kessy, Gardiel Michael/Mwinyi Mngwali dk77, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Said Juma ‘Makapu’/Raphael Daudi dk59, Pato Ngonyani, Papy Kabamba Tshishimbi, Pius Buswita, Ibrahim Ajib na Emmanuel Martin.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhhamisi ya February 22

$
0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhhamisi ya February 22

Godbless Lema: Nawatakia Kila la Heri Madiwani Waliohama na Kujiunga na CCM

$
0
0
Ninawatakia kila la kheri Madiwani waliojiunga na CCM leo katika nchi yenye mfumo wa siasa za vyama vingi uamuzi kama huu unaweza kuwa sawa kama utashi wa maamuzi haya ungewezwa kujengwa katika maadili na ukweli.

Safari hii ya mageuzi ya kujenga demokrasia ni safari ngumu sana wengi wameamua kuuza haki na utu wao na wengine wataendelea, bila shaka ni dhahiri kuwa Taifa letu linapita katika changamoto nyingi kwa sasa kushambuliwa kwa demokrasia kwa njia yoyote Ile sio hasara ya CHADEMA bali ni hasara ya nchi yetu.

Kwa mtu mwenye akili timamu hata ndani ya CCM huwezi kuruhusu kuuawa kwa demokrasi ya Nchi kwa sababu tu ya faida mfu ya chama chako madhara makubwa kichama hayako kwetu bali zaidi yatakuja kuonekana huko CCM kwani hatuna muda mrefu biashara kama hii italeta shida ndani kubwa ndani yao na chama tawala kinapokosa busara ya kutawala sio faida kwa upinzani bali ni hasara kwa Taifa.

Hata hivyo nafikiri tuko kwenye wakati mzuri sana wa mageuzi ya nchi yetu tunapaswa kujipa muda kidogo, haikuwa kazi rahisi Israel kutoka Misri na na kufika Kanaani lakini walifika.

Nchi hii itafikia kilele muhimu cha haki mara nyingi mambo mengi katika Dunia yana amuliwa na muda, tafadhali msiwaze chuki dhidi yao kwani watu wa hii wanaendelea kuwa msaada wa utafiti kwetu wa fikra ndani ya nchi yetu nakufanya tathimini ya kweli ya safari hii muhimu ambayo sijui tutafika lini lakini lazima kuwepo kwenye lengo bila kuyumba ili uhuru wetu uonekane kesho.

Arusha MSIOGOPE.

Yajue Madhara yatokanayo na Matumizi ya Bangi

$
0
0
Kwanz kabisa bangi ni neno ambalo hutumika kuelelezea sehemu iliyokaushwa ya maua, mbegu, mche na majani ya mmea ujulikanao kama Indian hemp. Mmea huu huko mitaani una majina mengi, majina hayo ni kama: dope, nyasi, majani, mche, ganja, magugu, kitu, sigara kali, blanti na mboga.

Kwa kitaalam “cannabis” huelezea aina mbali mbali za dawa za kulevya zitokanazo na mmea wa Indian hemp ambazo ni bangi (marijuana) na hashish.

Aina hizi za dawa zitokanazo na mmea huu ziko katika kundi la dawa za kulevya ziletazo maruweruwe (hallucinogen) au dawa zinazoathiri ubongo na kubadili jinsi tunavyotazama mambo katika uhalisia wake, nan do maana mtu akitumia bangi mara nyingi hufanya vitui vya ajabu sana.

Kuna zaidi ya aina 400 za kemikali katika mmea huu na kemikali ya kulaumiwa inayohusika na mabadiliko haya katika ubongo hujulikana kama tetrahydrocannabinol (THC). Kiasi cha THC hutofautiana kulingana na eneo ulikolimwa mmea wa Indian hemp.

Kama tulivyoona bangi ni sehemu iliyokaushwa ya majani, mbegu, maua, na mche na huwa na rangi ya kijani, kijivu au brauni, lakini bangi ni dawa ya kulevya ambayo hutumika kinyume cha sheria katika sehemu nyingi duniani.

Bangi hutumika kwa kuvuta moshi kutoka katika msokoto, sigara iliyoungwa au bomba maalum ya kuvutia moshi wake. Wakati mwingine watumiaji hupukutisha sigara na kujaza bomba la sigara bangi au bangi iliyochanganywa na dawa nyingine za kulevya kama cocaine na aina hii hujulikana na watumiaji kama “blunt”

Mtumiaji anapovuta msokoto wa bangi, huanza kufanya kazi baada ya dakika chache na mvutaji huanza kuhisi mapigo ya moyo yakienda mbio, mapokeo ya uhalisia huanza kubadilika na kuona vitu visivyo katika uhalisia (ndoto za  mchana/ maruweruwe). Matokeo haya ya muda mfupi baada kuvuta moshi wa bangi, huweza kudumu kwa muda wa saa mbili hadi nne au kuendelea kwa muda mrefu zaidi ikitegemea na kiasi cha THC kilichovutwa na ukali wake.

Mara nyingi wavutaji wa bangi huvuta moshi kwa nguvu ndani ya mapafu na kuushikilia kwa muda mrefu ili kuongeza ufanyaji kazi wa THC ukilinganisha na anayevuta sigara na hii husababisha madhara makubwa katika mapafu ya mvutaji. Mbali na maudhi kama kukohoa na koo kuwasha, imeonekana kuwa uvutaji wa aina hii wa moshi unamweka mvutaji katika hatari mara tano zaidi ya kupata saratani ukilinganisha na mvutaji sigara.

Matatizo ya ubongo yanayopelekea kuathiri afya ya akili ni ugonjwa mbaya uwapatao wavutaji wa bangi. Anayevuta bangi huwa na uwezo mdogo wa kumbukumbu na pia humuondolea uwezo wa asili wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi ukilinganisha na mtu asiyevuta bangi.

 Hivyo kila wakati kwa ulinzi na usalama wa afya epuka matumizi ya bangi.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

$
0
0

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN na Nyota

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

 ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO   HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, NA KUPONYA MAGONJWA SUGU ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp 0622766715

Hii Hapa Ratiba ya Kuuaga Mwili wa Akwilina Katika Chuo cha NIT

$
0
0
Hii Hapa Ratiba ya Kuuaga Mwili wa Akwilina Katika Chuo cha NIT
Ratiba ya kuaga mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline leo katika viwanja vya chuo cha NIT.


Hatimaye Rais wa FIFA Atua Bongo Alfajiri ya Leo

$
0
0
Hatimaye Rais wa FIFA Atua Bongo Alfajiri ya Leo
Hatimaye rais wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani fifa, Gianni Infantino amewasili nchini majira ya saa 10 : 30 alfajiri ya kuamkia leo na kupokelewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere.



Infantino atakuwa hapa nchini kwaajili ya mkutano mkuu wa mwaka wa FIFA unaotarajiwa kuanza leo Februari 22 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere huku ukitegemewa kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa Shirikisho hilo.


Baada ya kuwa hapa nchini, Infantino ataonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli.

Mkutano huu wa viongozi wa FIFA na CAF umebeba ajenda mbalimbali  ikiwemo kujadili Maendeleo ya Soka la Wanawake, Maendeleo ya Soka la Vijana, Utaratibu wa kusaidia Vilabu vya soka pamoja na vipaumbele mbalimbali vya kukuza soka kwa nchi za Afrika.

Infantino anatarajiwa kuondoka nchini mara baada ya kumaliza mkutano wake na kushiriki chakula cha jioni.

Picha zikionyesha Rais huyo wa FIFA, Infantino akiwa sambamba na rais wa CAF pamoja na wajumbe

Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>