Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Rais wa FIFA Apagawa na Nguo za Kimasai Alizovalishwa

$
0
0

Rais wa FIFA Apagawa na Nguo za Kimasai Alizovalishwa
Rais wa Fifa, Gianni Infantino anaongoza kikao cha siku moja kujadili masuala mbalimbali kuhusu soka la vijana na wanawake na maendeleo ya mchezo wake kwa jumla.

Mara baada ya kuwasili ukumbi hapo akiwa katika msafara wa magari manne, Infantino aliyefuatana na Rais wa CAF, Ahmad Ahmad pamoja na Rais wa TFF, Wallance Karia, Mjumbe wa CAF na mwenyekiti wa BMT, Leodegar Tenga na Kaimu Katibu wa TFF, Wilfred Kidau alivalishwa mgolole na wamasai waliokuwa akicheza ngoma nje ya ukumbi wa Mwalimu  Nyerere.

Rais huyo wa FIFA baada ya kuvalishwa mgolole pamoja na Rais wa CAF, alivalishwa bangili na alipewa kirungu kiilichotengenezwa kwa kisu.

Walipoingia ndani ya jingo hilo, walipata zawadi maalumu kutoka Bodi ya Utalii Tanzania pamoja na nakala zinazozungumzia Tanzania na hifadhi zake.

Awali wajumbe kutoka nchi 19 walitangulia wakiongozwa na Katibu mkuu wa Fifa, Fatma Samoura ambaye naye alionekana kufurahia mapambo ya kimasai kwa wamasai waliokuwa wakiuza bidhaa zao.


Mbao FC Yajipanga Kuimaliza Simba

$
0
0
Mbao Yajipanga Kuimaliza Simba

Baada ya kuondolewa katika mashindano ya Kombe la FA (ASFC), Mbao FC imesema sasa nguvu zao zote wanazihamishia kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Simba kuhakikisha wanashinda.

Timu hiyo  msimu uliopita walifanikiwa kufika fainali ya mashindano ya Kombe la ASFC, lakini msimu huu wameondolewa mapema na Njombe Mji kwa penalti 6-5 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Nahodha wa timu hiyo, Yusuph Ndikumana alisema licha ya kushindwa kusonga mbele, sasa wanageukia mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Februari 26 Jijini Dar es Salaam.

Alisema wanaamini mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na ushindani wa wapinzani wao walionao, lakini watapambana kuhakikisha wanashinda.

“Haya matokeo yametusikitisha sana, lakini ndio mambo ya mpira lazima tukubali, hapa nguvu zetu tunazielekeza kwenye mechi yetu na Simba kuhakikisha tunashinda”alisema Ndikumana.

Beki huyo Mrundi alisema licha ya Ligi kuwa ngumu, lakini hawatakata tamaa na badala yake wataendelea kusaka ushindi kwenye mechi zilizobaki iwe nyumbani au ugenini.

“Bado tunahitaji ushindi zaidi ili kujiweka nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu, pointi zetu bado hazitoshi kujihakikishia usalama, tunaenda kwa Simba kusaka ushindi tu,” alisisitiza nyota huyo.

Mbao iliyopo nafasi ya tisa ikiwa pointi 19 itawavaa Simba wanaoongoza Ligi kwa alama 42 ikiwa haijawahi kuwafunga katika mechi nne walizokutana ikiwamo ya fainali ya Kombe la FA mwaka jana.

Simba ilianza kuichapa Mbao FC bao 1-0 Jijini Dar es Salaam, kisha kuwalaza mabao 3-2 uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ikaichapa tena mabao 2-1 mechi yao ya fainali ya mashindano ya FA mkoani Dodoma na msimu huu zilitoka sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.

Wanaodaiwa Kuwa Wafuasi Chadema Waliokamatwa Siku ya Kifo cha Akwilina Warudishwa Rumande Baada ya Kukosa Dhamana

$
0
0


Watu 28 wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakituhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali na kinyume na sheria.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo mbele ya hakimu mkazi, Godfrey Mwambapa na kusomewa shtaka la kufanya mkusanyiko usiyo halali.

Washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa walitenda kosa hilo Februari 16, 2018  katika barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni.

Wamekana shtaka hilo na kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini hati ya Sh1.5milioni kwa kila mmoja.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 3, 2018 itakapotajwa.

Chirwa Afunguka Kuhusu Msimamo Wake Yanga

$
0
0
Chirwa Afunguka Kuhusu Msimamo Wake Yanga
BAADA ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali zikimhusu straika wa Yanga, Obrey Chirwa raia wa Zambia kugoma kuichezea timu hiyo, mwenyewe ameibuka na kutoa msimamo wake ndani ya timu hiyo.

Chirwa aliyejiunga na Yanga msimu uliopita akitokea FC Plati­num ya Zimbabwe, mkataba wake na Yanga unatarajiwa kumal­izika mwishoni mwa msimu huu huku kukiwa na taarifa za Simba kuinyemelea saini yake.

Hivi karibuni, taarifa zilitoka zikidai kwamba, Mzambia huyo ametaka kupewa kitita cha shilingi milioni 150 ili aongeze mkataba ndani ya timu hiyo.

Taarifa za Chirwa kugoma kuichezea Yanga, zilianza wik­iendi iliyopita baada ya jina lake kuondolewa dakika za mwisho kwenye msafara wa timu hiyo ulioelekea Shelisheli kucheza mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St Louis.

Katika mch­ezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar, Yanga iliibu­ka na ushindi wa bao 1-0, ambapo kwenye mchezo huo, Chirwa alikosa pen­alti, huku Yanga ikifunga bao lake hilo kupitia kwa Juma Mahadhi.

Kuachwa kwa Chirwa kwenye msafara huo, kulitolewa ufafanuzi na Yanga kwa kusema kuwa, mchezaJi huyo alipata majeraha kwenye mch­ezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Majimaji ambao Yanga walishinda mabao 4-1.

Baada ya kuenea taarifa za kugoma kwa Chirwa, juzi Ju­matatu klabu hiyo iliweka katika akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram sehemu ya mahojiano na Chirwa.

“Sijawahi kusema wala kumwambia mtu yeyote kuwa nataka 150M kwa ajili ya mkataba mpya, sipendezwi na namna wanavyoni­zushia, nadhani nia yao ni kunigombanisha na wapenzi wa Yanga.

“Niliumia kwenye mchezo dhidi ya Maji­maji, ajabu wanasema nimegoma, huu ni upu­uzi, mimi ni mchezaji wa Yanga, mimi na klabu ndiyo wenye kujua hati­ma yangu ya baadaye, niacheni nicheze mpira,” alisema Chirwa.

Haji Manara Amfariji Cannavaro Baada ya Kufiwa na Mwanaye

$
0
0
Haji Manara Amfariji Cannavaro Baada ya Kufiwa na Mwanaye
Afisa habari wa timu ya Simba SC, Haji Manara amekuwa miongoni mwa watu walioweza kuguswa na msiba uliomfika Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro' leo wa kufiwa na mwanae na kumtaka awe mwenye moyo wa subra.


Manara amefunguka hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kupokea taarifa hizo za msiba wa Anwar aliyefariki katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo asubuhi wakati akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua

"Pole sana Cannavaro kwa kufiwa na mtoto wako wa miezi miwili Anwar. Mimi binafsi, viongozi, wachezaji, benchi la ufundi, wanachama pamoja na mashabiki wa Simba tunaungana na Cannavaro katika kipindi hiki kigumu alichonacho yeye pamoja na familia yake kiujumla. Poleni wanayanga wote", amesema Manara.

Kwa upande mwingine, muandishi wa habari hii alipomtafuta Cannavaro kwa njia ya simu amesema japo kuwa yeye yupo njiani kurudi nchini akiwa anatokea Visiwa vya Shelisheli ameruhusu mwili wa marehemu mwanae kuzikwa leo (kuhifadhiwa).

Wanafunzi Wapoteza Fahamu Baada ya Kumuona Akwilina Ndani ya Jeneza

$
0
0
Wanafunzi Wapoteza Fahamu Baada ya Kumuona Akwilina Ndani ya Jeneza
Vilio, simanzi na kupoteza fahamu kwa baadhi ya wanafunzi ni baadhi ya matukio ya huzuni yanayojitokeza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), baada ya kuwasili mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa chuo hicho, Akwilina Akwiline.

Mwili wa mwanafunzi huyo unaagwa leo, Februari 22, 2018 katika viwanja vya chuo hicho.

Wanafunzi zaidi ya wanne aliokuwa akisoma nao Akwilina chuoni hapo ni kama hawaamini baada ya kushuhudia jeneza lenye mwili wake, huku wengine wakipoteza fahamu na kupewa huduma ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Viongozi waliofika mpaka sasa katika viwanja vya NIT ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi; Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako; Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni; Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika.

Tayari ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo imeanza.

Aliyetekeleza Mauaji ya Mwanafunzi Akwilina Aliombe Msamaha Taifa Vinginevyo Hatutofika Mbali- Father Raymond

$
0
0
 Aliyetekeleza Mauaji ya Mwanafunzi Akwilina Aliombe Msamaha Taifa Vinginevyo Hatutofika Mbali- Father Raymond
Father Raymond Mayanga wa Parokia ya Yohana Mbatizaji Ruhanga ambaye ameendesha ibada ya kuaga mwili wa marehemu Akwilina katika Chuo cha Usafirishaji (NIT) amemtaka aliyetekeleza mauaji ya mwanafunzi huyo aliombe msamaha Taifa.


Father Raymond amesema hayo leo Februari 22, 2018 na kudai kuwa jukumu hilo wameiachia serikali ya awamu ya tano na vyombo vyake vya usalama kuwa endapo watampata mtu huyo wahakikishe kuwa analiomba taifa msamaha kwani kitendo alichofanya kimewaumiza Watanzania hivyo hata akifungwa miaka 30 haitasaidia kwa kuwa tayari Akwilina ametangulia mbele ya haki na hatoweza kurudi.

"Mimi kama mtoto wa Mungu kama wengine walivyo watoto wa Mungu niwaombe tufanye kazi ya upatanishi na naomba wale ambao wana hiyo nafasi na kwa hili lililotokea kwa mwanetu Akwilina limetuumiza na kwa jinsi lilivyotuumiza nafikiri linahitaji kuponywa na namna moja tu ya kuliponya tunawaomba wale wahusika ambao wana madaraka ya kuweza kulisaidia. Huyu aliyefanya kitendo hiki baada ya kujulikana aliombe taifa hili msamaha ni hicho tu hatuna namna nyingine hata tukimfunga miaka 30 au 40 Akwilina hawezi kurudi amekwenda lakini aliyefanya huenda kwa nia nzuri ikitakoea bahati mbaya tunaomba vyombo vinavyohusika vikimaliza utaratibu wake akajulikana huyo mtu hata kwa kupitia TV awaombe wana Mungu msamaha" alisema Father Raymond


"Kheri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu vinginevyo hatutafika mbali, tumuombe Mungu kila mmoja wetu katika imani yake leo ni Akwilina huenda kesho itakuwa ni wewe sasa hatutaki hilo liendelee, na hilo halitaendelea tu kama mtu atakubali kuomba msamaha kujinyenyekeza, kuwa mnyenyekevu na kukubali nimekosa mimi, nimekosa sana nawaomba msamaha kwisha tunaendelea kama familia hakuna asiyekosea. Lakini unapojaribu kutafuta mbinu ukaliweka hivi unaliweka vile unazidi kuumiza kwa sababu mimi kama mzazi sitaelewa

"Naomba nisema hapa bila hata kigugumizi nafikiri wenye nafasi hii si wengine ni serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaiomba kama ilivyojitolea kuweka haya mazishi katika level hiyo, tunawaomba pia watusaidie kwa sababu wao ndiyo wamepewa dhamana ya maisha yetu wote hapa, na sisi kama watoto wa familia hatulingani kama vidole vyetu tunaimani kwamba serikali yetu itatusaidia katika kulipatanisha, katika kurudi kufanya kazi kama watoto wa familia moja"

Mabango Yatawala Kuaga Mwili wa Akwilina......Yakitaka Sirro, Mwigulu Kujiuzulu

$
0
0
Mabango Yatawala Kuaga Mwili wa Akwilina...... Yapo Yakitaka Sirro, Mwigulu Kujiuzulu

Baadhi ya waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, yakiwamo ya kumtaka waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kujiuzulu.

Ibada hiyo inafanyika leo Februari 22, 2018 katika viwanja vya NIT, Mabibo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu, wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali.

Waombolezaji hao walinyanyua mabango hayo baada ya waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako aliponyanyuka kutoa salamu kwa wafiwa kama walivyofanya viongozi wengine, akiwamo mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Baadhi ya ujumbe katika mabango hayo ni; “muuaji hawezi kujichunguza na Mwigulu, Sirro kwa mauaji haya bado mko ofisini.”

Juhudi za kuwataka waombolezaji hao kushusha mabango ziligonga mwamba kutokana na baadhi ya watu waliokuwa karibu yao kuja juu, wakitaka waachwe kwa maelezo kuwa wana haki ya kufanya hivyo.

Katika salamu zake za rambirambi, Profesa Ndalichako alisema: “Rais Magufuli ameshaagiza uchunguzi ufanyike na mimi kama waziri nasisitiza vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi haraka.

“Matukio ya aina hii hayapaswi kuendelea, nimehuzunika kwa msiba huu na naomba Watanzania waungane kuiombea familia.”

Soma: Padri ataka aliyempiga risasi Akwilina awekwe wazi, awaombe radhi Watanzania -VIDEO








Polepole Atoa Agizo kwa Kaya Masikini

$
0
0
Polepole Atoa Agizo kwa Kaya Masikini
Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa CCM, Humphrey Polepole ameagiza wasimamizi wa Mpango wa kunusuru kaya masikini na zenye upungufu wa chakula TASAF mkoa wa Arusha kufanya tathmini na kuongeza ruzuku kaya zinazofanya maendeleo ili kuongeza uzalishaji wenye tija.

Akiwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya TASAF ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM Polepole amesema, kuwa ni vyema kuwaongeza ruzuku kwa kaya zinazoonesha matokeo chanya katika uzalishaji ili kuweza kuwa chachu ya maendeleo katika jamii.

"Mpango wetu sisi ni kuwavusha watanzania kutoka hali waliyonayo sasa na kwenda katika hali nzuri zaidi ifikapo mwaka 2020 ndiyo maana tunalipendekeza hilo. Lakini niwapongeze watu wa Arusha kwani nimeona miradi mingi ambayo itawafanya mtoke kwenye utegemezi," Polepole

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbli mkurugenzi wa jiji la arusha Athumani Kihamia amesema asilimia kubwa ya kaya maskini hizo tayari wamesha patiwa kadi kwa ajili ya matibabu (Tika) yenye uwezo wa kuhudumia kaya sita kwa kadi moja.

Msajili wa Vyama Aijia Juu Chadema Aitaka Ijieleze

$
0
0
Msajili wa Vyama Aijia Juu Chadema Aitaka Ijieleze
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitaka kijieleza kwa nini asikichukulie hatua kwa kufanya maandamano Februari 16, 2018.

Akizungumza na Mwananchi leo Februari 22, 2018, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema barua hiyo ya msajili waliipokea jana na wanapaswa kuijibu kabla ya Februari 25, 2018.

Jaji Mutungi alipoulizwa kuhusu hilo amesema hawezi kusema lolote kwani yeye anawasiliana moja kwa moja na vyama vya siasa na si vyombo vya habari.

Chadema waliandamana Februari 16 mwaka huu wakishinikiza kupewa viapo vya mawakala wao kabla ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni.

Simba Wawasili Dar kwa Makundi

$
0
0
Simba Wawasili Dar  kwa Makundi
Huwezi kuamini! Kikosi cha Simba kimefanywa kama wafalme ndani ya ndege ya Kenya (KQ) kwa kipindi chote cha safari yao.

Iko hivi, baada ya wafanyakazi kujua msafara ule ni wa Simba, kila waipokuwa wakitoa matangazo yao ndani ya ndege walikuwa wakiwatangaza na Simba wakiwapongeza kwa ushindi na kuwatakia mafanikio mema katika mechi zijazo.

"Bila kusahau  ndani ya ndege hii tupo na Wachezaji wa Simba wanaotoka Djibouti na wamefanya vizuri katika mechi yao huko, hivyo sisi wafanyakazi wa ndege hii tunawapongeza sana, tunataka waendelee kufanya vizuri zaidi na zaidi na kuwa wawakilishi wazuri Afrika," alitangaza mfanyakazi huyo akitumia Lugha ya Kiingereza na Kiswahili.

Simba imewasili usiku wa kuamkia leo Alhamisi kwa makundi wakitumia ndege ya KQ na. wataingia kambini kesho hii Ijumaa.

Kamanda Msangi Afunguka Kuhusu Tukio la Ndugu Waliofukua Mwili wa Marehemu

$
0
0
Kamanda Msangi Afunguka Kuhusu Tukio la Ndugu Waliofukua Mwili wa Marehemu
Kamanda wa Polisi wa Mwanza Ahmed Msangi leo February 22, 2018 ametolea ufafanuzi wa tukio la kufukua mwili wa marehemu ili ndugu wajiridhishe baada ya kuwa na hofu na kifo cha ndugu yao aliyefariki akiwa anafanyiwa upasuaji katika kituo cha Afya cha Filoleli Mwanza.

Kamanda Msangi ameeleza kuwa marehemu Ashura Shaban Salum, 40, kabla ya kifo chake alifanyiwa upasuaji na baadaye kupoteza maisha na mwili wake ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, madaktari ilibidi wauchome mwili sindano ili usiharibike.

Kwenye mchakato huo wa kumchoma sindano, ilibidi madaktari wachane eneo la paja ili kupata mshipa huo wa kuchoma sindano jambo ambalo ndilo ndugu walilalamikia baada ya kukuta jeraha hilo kwenye paja la ndugu yao, wakihisi pengine kuna viungo vingine vya mwili vimetolewa.

Wakurugenzi Wanne Wafutiwa Kesi na Mahakama

$
0
0
Wakurugenzi Wanne Wafutiwa Kesi na Mahakama
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imezifuta kesi mbili zinazowakabili wakurugezi watendaji wa kampuni ya ENCC Consultants, Riziki Shemdoe na Deusdedit Kibassa wa Abshir Gure na Farhiya Warsame wa kampuni ya Lasar Logistic Limited.

Wakurugenzi hao na wenzao walifikishwa mahakamani na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Hakimu mfawidhi, Victoria Nongwa amezifuta kesi hizo kwa nyakati tofauti baada ya mawakili wa Serikali waliokuwa wakiziendesha, Dereck Mukabatunzi na Emma Msofe kuomba zifutwe.

Amesema ombi hilo ni kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea na kesi dhidi yao, hivyo mahakama imeridhia na kuwaachia.

Pia, wadhamini wao watakuwa huru na kuendelea na shughuli zao.

Father Raymond: Aliyetekeleza Mauaji ya Mwanafunzi Akwilina Awekwe Hadharani na Aombe Msamaha..... Vinginevyo Hatutafika Mbali

$
0
0
Padri Raymond Mayanga wa Parokia ya Yohane Mbatizaji Luhanga amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kumsaka mtu aliyempiga risasi mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafishaji (NIT), Akwilina Akwilini, kumweka wazi ili awaombe radhi Watanzania.

Akizungumza katika ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo inayofanyika katika viwanja vya NIT, Mabibo, Padri Mayanga amesema mtu huyo hata akifungwa miaka 30 hadi 40, Akwilina hatarudi.

“Awe amefanya kwa nia nzuri au mbaya vyombo vinavyohusika vikimaliza taratibu zake kama ni kupitia televisheni ama nini huyu mtu aombe msamaha, vinginevyo hatutafika mbali. Leo kwa Akwilina huenda kesho kwa mwingine,” amesema.

Naye mwakilishi wa familia ya Akwilina, Aloyce Shirima amesema, “Tunaomba mtufikishie salamu kwa Rais John Magufuli  kuwa wale wote waliofanya kitendo hicho wachukuliwe hatua stahiki. Taifa haliwezi kuendelea kwa kuondokewa na wasomi kizembe.”

“Akwilina ni mtoto wa sita katika familia ya watoto nane wa mzee Akwilini na ni mtoto  pekee aliyependa elimu katika familia hiyo.”

Rais wa Serikali ya wanafunzi NIT, Mchunja Othman amesema, “Alikuwa mcheshi asiyejua kununa. Tunaiomba Wizara ya Mambo ya Ndani kuhakikisha inalisimamia hili ili haki itendeke. Hii inatupa fursa ya kujifunza sisi kama binadamu maisha yetu siyo ya kudumu hivyo tutende mema.”

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo


Msajili wa Vyama vya Siasa Aiweka Kitanzini CHADEMA.....Awaandikia Barua Kuwata Wajieleze Kwa Kufanya Vurugu na Maandamano

$
0
0
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitaka kijieleza kwa nini asikichukulie hatua kwa kufanya maandamano Februari 16, 2018.

Chadema waliandamana Februari 16 mwaka huu wakishinikiza kupewa viapo vya mawakala wao kabla ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni



VIDEO: 'Sababu Za Kifo Tuna Uwezo Wa Kuzizuia' MAKONDA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Mkonda amesema hakuna mwenye uwezo wa kuzuia kifo lakini sababu zake zinaweza kuzuilika. RC Makonda ameyasema hayo wakati akitoa salamu za pole kwa waombolezaji waliojitokeza kwenye ibada ya kumuaga Mwanafunzi wa Chuo Cha Usafirishaji NIT, Akwilina Akwilini kilichotokea Februari 16, kwa kupigwa risasi.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI

JE Umehangaika na Matatizo ya Kimapenzi Kwa Muda Mrefu? Muone Shehe Chalo Atakutatulia Matatizo yako Kirahisi

$
0
0

JE umehangaika na matatizo haya kwa muda mrefu mtalamu Challo anayo dawa ya kuvuta mpenzi Je unasumbuliwa na mpenzi umeachwa na mpenzi au Mme mke na Bado unampenda na umejaribu sehemu nyingine Bila mafanikio njoo utatuliwe haraka na kundumisha ndoa yenu..

Umekimbiwa na mmeo mkeo au mpenzi na anaishi na mtu mwingine atarundi haraka kusafisha nyota mvuto wa mwili na biashara minguu kufa ngazi kuwaka moto ngiri tumbo kuunguruma na wakina Baba wasiojiweza katika tendo la uyumba kuchelewa kufika kileleni tunatibu Busha Bila oprasheni bali kwa kutumia vitabu vya dini

Tunatoa pete ya utajiri Bila mashariti mkufu wa bahati unauza Mali ya haindi unapoteza pesa kwenye biashara yako Bila kujua unataka kupandishwa cheo

Wasiliana na mtalamu Shehe Challo 0714006521 

Nyani Aiba Mamilioni Katika Nyumba ya Kiongozi wa Siasa

$
0
0

Ikiwa ni wiki chache tu zimepita tangu kutokea kwa tukio la aina yake la nyoka kumeza mamilioni ya fedha nchini Nigeria, hali hiyo ya kustajabisha imeendelea kujitokeza ambapo kwa sasa nyani anadaiwa kuiba fedha kiasi cha Naira milioni 70 (sawa na shilingi za kitanzania milioni 436), kutoka katika nyumba ya Seneta iliyoko eneo la mashambani.

Soma hapa nyoka atafuna mamilioni na kutoweka

Tukio hilo la aina yake na la kushangaza limetajwa kutokea katika nyumba ya Seneta Abdullahi Adamu aliyekuwa mwenyekiti wa Jukwaa la Maseneta wa kaskazini nchini humo, ambapo fedha zilizokuwa zimekusanywa katika awamu ya 7 wa seneti, zilitakiwa kukabidhiwa kwa mwenyekiti wa awamu ya 8 ya seneti hiyo.

Nyumba hiyo inayotajwa kuwa katika eneo la mashambani ambapo kuna wanyama mbali mbali ikiwemo nyani.

Kufuatia kutokea kwa tukio hilo, jukwaa la Seneti limemvua madaraka ya uenyekit, aliyekuwa mwenyekiti wake Seneta Abdullahi Adam, kutokana na uzembe huo huku hatua zaidi za kisheria zikifuatwa.

Wavaa Nusu Utupu Wapatiwa Kazi

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Rehema Madusa, ameliagiza Jeshi la Polisi wilayani humo kuwakamata na kuwapa adhabu ya kufyatua tofali vijana wanaovaa mavazi yasiyokuwa na staha hadharani.

Bi. Madusa ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika stendi ya mabasi wilayani humo ambapo amesema tofali hizo zitatumika kuboresha makazi ya askari.

Aidha amesema dawa imepatikana kwa  baadhi ya vijana wa kike ambao wamekuwa wanavaa nusu uchi hadharani na wanaume wanaovalia mlegezo na kuagiza wakamatwe na waoneshwe sehemu ya kufyatulia matofali yatakayotumika kwa ajili ya ujenzi wa vyoo na nyumba za polisi.

“Hawa wanaotembea barabarani nusu uchi basi wakiona vizuri basi watoe zote watembee uchi kabisa tujue moja, jeshi la polisi kamateni watu hawa pelekeni waende wakafyatue tofali kwa ajili ya kujenga nyumba za polisi,” Madusa

Hata hivyo amesema hata wanaokunywa pombe nyakati za kazi na wale wanaopiga debe bila kufuata utaratibu uliowekwa wataunganishwa pamoja kusaidia kufyatua tofali hizo.

“Wote hawa mimi nawaweka katika kundi moja kuanzia wacheza pool table, wapiga debe wanaovaa nguo zisizokuwa na staha na wale wanaovaa nguo nusu uchi, naagiza polisi na wananchi kamateni hawa wakasaidie ujenzi,”amesema.

Hata hivyo ameliagiza jeshi la polisi kushirikiana na wananchi kudhibiti  matukio ya uhalifu ikiwemo vitendo vya ujambazi na usalama barabarani.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images