Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Kiwanda cha Dangote Chatoa Msaada ya Mifuko 2,400 ya Seruji Kwaajili ya Kuboresha Miundombinu ya Shule

$
0
0
Kiwanda cha Dangote Chatoa Msaada ya Mifuko 2,400 ya Seruji Kwaajili ya Kuboresha Miundombinu ya Shule
Wakati baadhi ya wanafunzi wa shule 10 za Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara wakisoma katika madarasa ya nyasi na chini ya miti,  kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo mjini hapa kimekabidhi mifuko 2,400 ya saruji kusaidia kuboresha miundombinu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa mkoa, Gelasius Byakanwa kufanya ziara katika halmashauri hiyo na kuzibaini shule hizo.

Ziara hiyo ilifanyika siku chache baada ya MCL Digital kuripoti wanafunzi wa Shule ya Msingi Mitambo kusomea chini ya miti ambapo kiliitishwa kikao cha wadau wa elimu na kutoa ahadi mbalimbali ukiwemo uongozi wa kiwanda hicho.

Akikabidhi saruji hiyo kwa halmashauri, Kaimu Katibu Tawala wa wilaya, Francis Mkuti amesema mkuu wa mkoa wa Mtwara aliitisha kikao cha wadau wa elimu na watu kuahidi vitu mbalimbali pamoja na nguvu kazi ili kuwaondolea wanafunzi adha wanayokumbana nayo na kuwawezesha kupata elimu bora.

“Nishukuru uongozi wa kiwanda cha Dangote, lengo la mkuu wa mkoa ni kuboresha miundombinu ili (wanafunzi) wapate elimu bora na kutuwezesha kutoka katika zile nafasi za mwisho na sisi tuweze kusogea juu, niwakumbushe wengine walioahidi na wao kutimiza ahadi ili kufikia azma tuliyokusudia,” alisema.

“Kila kitu tunafanya kwa hatua, naamini tukimaliza suala la madarasa itafuata miundombinu mingine ikiwemo nyumba za walimu.”

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri, Fundikira Masamalo amesema saruji hiyo itatumika kujenga madarasa 48 ya shule 10 zilizoonekana kuwa na hali mbaya.

Amesema halmashauri imeshaandaa vikundi vya vijana kwa ajili ya kufyatua matofali yatakayosambazwa katika maeneo yaliyoonekana kuwa na uhaba wa madarasa.

   

Rosa Ree Afunguka Kuhusu Mahaba Yake kwa Khaligraph Jones

$
0
0
Rosa Ree Afunguka Kuhusu Mahaba Yake kwa Khaligraph Jones
Msanii wa muziki Bongo, Rosa Ree amefunguka jinsi anavyovutiwa na uwezo wa kimuziki wa rapper kutoka nchini Kenya, Khaligraph Jones.

Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa amekuwa karibu na Khaligraph Jones kutokana anamshawishi kufanya vitu vikubwa katika muziki wake.

“Khaligraph Jones is also brother of mind, ni mtu ambaye nina ukaribu sana naye, pia yeye anani-inspire sana kutokana na issue zake ambazo anazifanya,” amesema.

“Ni mpambanaji sana, hustler sana atahakikisha anafikia lile lengo ambalo analo na ni kitu ambacho kinani-inspire mimi kama female rapper, Kaligraph pia ni mtu ambaye ana moyo wa pekee yake,” ameongeza.

Mwaka jana Rosa Ree alimshirikisha Khaligraph Jones katika remix ya ngoma yake inayokwenda kwa jina la One Time. Rosa Ree kwa sasa anatamba na ngoma ‘Marathon’ aliyomshirikisha Bill Nass.

Chege: Nitakuwa wa Mwisho Kuoa

$
0
0
Chege: Nitakuwa wa Mwisho Kuoa
Msanii wa muziki Bongo, Chege amengufuka kuhusu mipango yake ya kuoa.

Chege ambaye leo ameachia ngoma mpya ‘Kaitaba’ aliyomshirikisha Saida Karoli ameiambia Clouds Fm kuwa atakuwa wa mwisho kuoa kwani hapendi kushauriwa kitu baada ya watu wengine kufanya kitu kama hicho.

“Huwa sipendi kuambiwa nifanye kitu ambacho mwingine amekifanya, nina mpenzi ninayempenda kabisa na tunaishi pamoja, muda ukifika nitaoa, nilichogundua nitakuwa wa mwisho kuoa” amesema Chege.

September mwaka jana Chege aliiambia Bongo5 kuwa kitendo cha kuoa ni kujifunga milele, hivyo mtu anatakiwa achague mwenza sahihi ambaye anaweza kuishi naye kwa muda wote huo na isiwe kuoa kwa sababu ya trending za watu kitu ambacho hawezi kukipa nafasi katika maisha yake.

Maneno ya Izzo B, Rama Dee na Niki wa Pili Muda Mchache Baada ya Sugu Kuhukumiwa Miezi 5

$
0
0
Izzo B, Rama Dee na Niki wa Pili Waguswa na Kifungo cha Sugu Waandika Ujumbe Huu
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na mwenzake Emmanuel Masonga wamehukumiwa kwenda jela miezi mitano na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mbeya leo Februari 26, 2018 baada ya kukutwa na hatia kutumia lugha ya fedhea dhidi ya Rais Magufuli.


Baada ya kuhukumiwa kwenda jela baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva wamefunguka yao ya moyoni kuhusu tukio hilo huku wengine wakimtia moyo kuwa gerezani siyo kaburini hivyo atamaliza muda wake na kurudi uraiani kuwapigania wananchi wa Mbeya.

"Nguvu ya Mungu ikapate kuwa nawe pamoja na familia yako, gerezani sio kaburini 'stay strong' Jongwe" aliandika Niki wa Pili

Kwa upande wake msanii Rama Dee yeye amesema kuwa ameumizwa sana na bahari ya Sugu kufungwa jela miezi mitano na kudai si picha nzuri katika nchi yetu kwa mambo kama haya.

"Nasikitika sana kwa hii habari kama msanii pia kama rafiki wa Sugu, hii si picha nzuri" Rama Dee

Aidha msanii Izzo Bizness ambaye anaiwakilisha Mbeya vizuri katika muziki wa Hip hop pia ameonyesha hisia zake na kumtaka Mbunge huyo kuwa mvumilivu na kusimama imara katika kipindi hiki.

Mbali na huyo Rapa Roma Mkatoliki alikuwa na haya ya kusema juu ya kifungo cha Sugu "Hata hili lipatita' stay strong Joseph Zaburi 35: 1-28 "

Askari Polisi: Wema Kaniambia Anatumia Bangi Kama Starehe

$
0
0
Askari Polisi: Wema Kaniambia Anatumia Bangi Kama Starehe
Kesi inayomkabili Muigizaji Wema Sepetu  imeendelea ambapo Ofisa wa Polisi WP Marry ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Wema alimwambia anatumia Dawa za kulevya aina ya Bangi kama starehe na sio kuuza.

WP Marry ambaye ni shahidi wa tatu ameyaeleza hayo wakati akiongozwa na Wakili wa serikali Costantine Kakula, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

WP Marry amedai kuwa Wema alimueleza maneno hayo hayo wakati walipokuwa njiani kuelekea nyumbani kwake kumkagua.

Amedai kuwa February 4, 2017 aliagizwa kumtoa Wema mahabusu na kwenda kumfanyia upekuzi nyumbani kwake akiwa na OC CID na Maofisa wengine wa Polisi.

Amedai kuwa wakiwa wanajiandaa kuondoka Central Polisi kuelekea kwa Wema Bunju Basihaya, wakiwa kwenye gari kuelekea huko alimuuliza Wema kuhusu tuhuma zinazomkabili kwamba anahusika na Dawa za kulevya au kutumia.

Amedai kuwa Wema alijibu “Sijishughulishi na kuuza ila ila natumia bangi kama starehe”.

WP Marry amedai kuwa baada ya kumuuliza Wema alimwambia mara yake ya mwisho kuvuta Bangi ilikuwa Jumatatu ambapo swali hilo aliulizwa February 4,2017.

Alieleza kuwa walipofika nyumbani kwa Wema waligonga geti na kufunguliwa na mdada wa kazi ambapo walivyoingia ndani walikuta kuna mdada mwingine wa kazi.

WP Marry amedai kuwa kabla ya kuingia ndani Wema aliomba kumpigia simu dada yake ili awepo wakati wa kufanya ukaguzi ambapo dada ake alifika na kujitambulisha kwa jina la Nuru Sepetu.

WP Marry ameeleza kuwa wakati Wema anampigia simu dada yake alitoka dada mmoja wa kazi kumfuata mjumbe ambapo alikuja naye na kujitambulisha kwa jina la Steven Ndaho.

Amedai baada ya dada yake Wema kufika alitaka kuwapekua kabla ya kuingia ndani ambapo Nuru aliwapekuwa wote kabla ya kuingia ndani.

Amedai baada ya kumaliza upekuzi walirudi Central polis, February 8,2017 saa nne asubuhi alipewa maelekezo na Inspeta Wille kwamba aende na Wema kwa mkemia kuu wa serikali kwa ajili ya kuchukuliwa sampuli ya mkojo.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi March 12 na 13, 2018 kwaajili ya kuendelea na ushahidi.

Mahakama Yaamuru Miguna Arejeshwe Kutoka Canada

$
0
0
Mahakama Yaamuru Miguna Arejeshwe Kutoka Canada
Mahakama Kuu imesimamisha uamuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang'i wa kumtangaza mwanasheria machachari Miguna Miguna kuwa ni mhamiaji aliyepigwa marufuku.
Jaji Enoch Chacha Mwita Jumatatu kadhalika alisimamisha kufutwa kwa pasipoti ya Dk Miguna kulikofanywa na bosi wa uhamiaji Gordon Kihalangwa. Jaji huyo pia aliiamuru Idara ya Uhamiaji kusaidia kurudi kwa Dk Miguna kutoka Canada.
Aidha, Jaji ameliacha kama lilivyo tangazo la kwenye gazeti la serikali lililotolewa na Dk Matiang'i la kutangaza Vuguvugu la Taifa la Upinzani (NRM) ambalo ni tawi la muungano wa chama cha National Super Alliance (Nasa) kuwa kikundi cha uhalifu.
Jaji Mwita aliamua kwamba haki za Dk Miguna zilikiukwa kwa kufukuzwa kwake, na kwamba madai yaliyotolewa dhidi yake yanahitaji awepo yeye binafsi kujitetea.
Akisisitiza kuwa ushahidi kama huo hauwezi kutolewa kupitia hati ya kiapo, jaji aliamuru maofisa wa uhamiaji kumtumia Dk Miguna nyaraka za kumwezesha kusafiri.
Jaji aliamuru ikiwa zitakosekana nyaraka hizo kwamba anaweza kutumia pasipoti yake ya Canada, na kwamba anaweza kuja tarehe atakayoamua.
Jaji pia ameamuru pande husika katika kesi hiyo kuharakisha usikilizwaji akitaja kuwa ni kutokana na uharaka wa jambo hilo.

Polisi Yamkamata Mtekaji wa Watu na Mporaji Mali

$
0
0
Polisi Yamkamata Mtekaji wa Watu na Mporaji Mali
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amefunguka na kusema kuwa wamefanikiwa kumkamata Rajabu Muhamed maarufu kwa jina la Rajeshi mwenye umri wa miaka 25  ambaye anatuhumiwa kwa kuteka wamama, kuwabaka na kuwapora mali.


Kamanda Mambosasa amesema kuwa mtu huyo hutumia gari aina ya Fun Cargo akikutana na wanawake huwalazimisha kuingia kwenye gari hiyo na kisha kuwatisha yeye ni Freemason hivyo watoe mali zao wasipofanya hivyo huwatishia kuwakata sehemu zao za siri.

"Hutumia gari namba T 172 BLH aina ya Fun Cargo rangi ya Silver huwakamata wanawake, huwanyang'anya wafanyabishara wanaoendelea kufanya shughuli zao na akishawakamata huwaingiza kwenye gari yake kwa nguvu kisha kudai vitu mbalimbali ikiwa pamoja na kuchukua mabegi na baadaye huzunguka nao mtaani huku akiwatisha kuwa yeye ni Freemason na kuwa atawauwa na kuwanyonya damu, kitendo hicho hupelekea wa kina mama hao kukabidhi kila walichokuwa nacho lakini pia huwatishia wakatoa password  za benki chini ya tishio kubwa la kuwatoa uhai na kuwakata sehemu za siri, huyu ni mnyama wa kutosha ana sura za binadamu lakini ni mnyama" alisema Mambosasa

Kamanda Mambosasa aliendelea kusema kuwa Rajabu Muhamed ameshawafanyia vitendo vya kinyama wanawake wengi sana hapa mjini ikiwa pamoja na kuwabaka na kuwadhalilisha

"Anafanya vitendo vya unyang'anyi kwa kutumia nguvu na hasa kwa wanawake, ubakaji na unyanyasaji wa kila aina, amefanya vitendo vingi sana mjini hapa vya unyanyasaji wa kina mama anawateka anajifanya ni Freemason anawapeleka mahali anapowapeleka na kuwafanyia vitendo vyote vya kinyama. Huyu muhumi huyu na anachoniambia mimi kwamba ameacha lakini amewadhuru wanawake wengi sana hapa mjini na wachache wenye ujasiri walifika kuripoti na ndiyo tukafuatilia na kufanikiwa kumtia mbaroni jana usiku maeneo ya Kinondoni".

Tanzania Yatunukiwa Tuzo ya Mapambano Dhidi ya Ugonjwa wa Malaria

$
0
0
Tanzania Yatunukiwa Tuzo na WHO Dhidi ya Mapambano
Shirika la Afya Duniani (WHO) imeitunukia nchi ya Tanzania imetunukiwa tuzo ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria kwa kutambua juhudi zake za kupambana na ugonjwa huo.


Tuzo hiyo imekabidhiwa leo kwa Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Kambi na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkaazi wa WHO, Ritha Njau, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Profesa Kambi amesema kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali kiwango cha maambukizi ya malaria nchini kimepungua kutoka kesi milioni 18 mwaka 2008 hadi kufikia milioni 5.5. huku idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano vikiwa vimepungua kutoka vifo 102 kwa kila vizazi hai 1,000 hadi kufikia vifo 67 kwa kila vizazi hai 1,000.

“Ugonjwa wa malaria ni miongoni mwa magonjwa yaliyochangia idadi kubwa ya vifo hivyo lakini kwa kuwa tumeudhibiti imesaidia kupungua vifo hivyo,” amesema Profesa Kambi.

JE Umehangaika na Matatizo ya Kimapenzi Kwa Muda Mrefu? Muone Shehe Chalo Atakutatulia Matatizo yako Kirahisi

$
0
0

JE umehangaika na matatizo haya kwa muda mrefu mtalamu Challo anayo dawa ya kuvuta mpenzi Je unasumbuliwa na mpenzi umeachwa na mpenzi au Mme mke na Bado unampenda na umejaribu sehemu nyingine Bila mafanikio njoo utatuliwe haraka na kundumisha ndoa yenu..

Umekimbiwa na mmeo mkeo au mpenzi na anaishi na mtu mwingine atarundi haraka kusafisha nyota mvuto wa mwili na biashara minguu kufa ngazi kuwaka moto ngiri tumbo kuunguruma na wakina Baba wasiojiweza katika tendo la uyumba kuchelewa kufika kileleni tunatibu Busha Bila oprasheni bali kwa kutumia vitabu vya dini

Tunatoa pete ya utajiri Bila mashariti mkufu wa bahati unauza Mali ya haindi unapoteza pesa kwenye biashara yako Bila kujua unataka kupandishwa cheo

Wasiliana na mtalamu Shehe Challo 0714006521

VIDEO: 'Serikali Inafurahia Viongozi Wa Upinzani Wanavyouwa?' Mtatiro Afunguka

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi CUF,  Julius Mtatiro amesema kukaa kimya kwa Serikali pindi wanapouawa Viongozi wa Vyama vya Upinzani kunaashiria kuwa Serikali inafurahia vifo hivyo hali ambayo inawafanya wauaji waendelee kufanya mauaji hayo kwa kuwa hawakemewi na Serikali.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI:

Kamanda Mambosasa Ajibu Kuhusu Watu Hatari kwa Taifa

$
0
0
Kamanda Mambosasa Ajibu Kuhusu Watu Hatari kwa Taifa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amefunguka na kujibu juu ya tuhuma alizotoa Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian Majura Musiba kuhusu watu 10 aliodai ni hatari kwa usalama wa taifa.


Kamanda Mambosasa akiongea na waandishi wa habari leo Februari 26, 2018 amewataka Watanzania kutoshabikia habari kwenye mitandao ya kijamii na kudai kuwa habari zingine zinaandikwa na watu wenye upungufu wa akili lakini amedai kuwa wao taarifa hizo wamezipokea na kuzifanyia kazi kwani jeshi la polisi huwa linafanyia kazi kila aina ya taarifa kutoka kwa kila mtu.

"Niseme tu hao wanaodaiwa ni tishio kwa usalama wa taifa hizo ni taarifa sisi tukipokea huwa kwa kawaida hatupuuzii taarifa yoyote hata ingetolewa na kichaa, wapo vichaa wengi wanaendelea kuongea na kuposti mambo tunaendelea kuyapokea na kuyashugulikia mpaka tutakapogundua hili limeandikwa na kichaa tunaachana nalo, lakini niendelee kuwaomba Watanzania muendelee kulipa ushirikiano jeshi la polisi kwani tupo imara" alisema Mambosasa

Mbali na hilo Kamanda Mambosasa aliwashauri watu ambao wanakuwa na taarifa yoyote wahakikishe wanawafikishie wao jeshi la polisi ili waweze kuzifanyia uchunguzi zaidi

"Niwaombe pale ambapo wanasikia kwamba kuna tishio lolote lile waendelee kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama tupo sisi polisi na wapo wenzetu wa usalama wa taifa lakini pia wapo viongozi mbalimbali katika ngazi tofauti hata serikali za mtaa wakiona ni vigumu kunifikia waendelee kutoa taarifa kwa watu hao kwani lengo taarifa hizo zifike sehemu ambayo taarifa hizo haziwezi kupotoshwa "


Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian Majura Musiba jana alitaja orodha ya watu 10 ambao kwa mtazamo wake anasema kuwa ni watu hatari kwa usalama wa taifa na kusema kuwa watu hao wanapaswa kudhibitiwa, watu hao ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mange Kimambi, Tundu Lissu, Zitto Kabwe, Julius Mtatiro, John Heche, Maria Sarungi, John Marwa, Evalist Chahari.

Wahamiaji 83 wa Ethiopia Wapandishwa Kizimbani

$
0
0
Wahamiaji 83 wa Ethiopia Wapandishwa Kizimbani
Wahamiaji 83 raia wa Ethiopia na Mtanzania mmoja mkazi wa Tukuyu wamefikishwa Mahakama ya Mkoa Iringa huku wahamiaji hao wakituhumiwa kuingia nchini bila kibali.

Akisoma mashtaka hayo leo Februari 26, 2018, wakili wa Serikali, Godfrey Ngwijo amesema raia hao wanakabiliwa na shtaka la kuingia nchini kinyume na kifungu cha sheria namba 45(i) kifungu (1) ,(2) kilichofanyiwa marekebisho 2016.

Ngwijo amesema Februari 23, 2018 saa moja jioni katika kijiji cha Mazombe wilayani Kilolo, wahamiaji 83 wasio na vibali walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi kwa kuingia nchini kinyume na sheria ambapo dereva wa lori walilopanda  hakupatikana baada ya kukimbia.

Amesema wahamiaji hao walikamatwa wakiwa katika hali mbaya kutokana na kukaa sehemu ya nyuma ya lori hilo ambako hakuna hewa ya kutosha, joto kali na kutokula chakula kwa muda mrefu.

Baadhi ya wahamiaji hao leo wamefikishwa hospitali ya mkoa kupata matibabu.

Wakili huyo amesema kati ya waliofika mahakamani kusomewa mashtaka yao, watatu  walishindwa kufika kwa sababu bado wako hospitali wanaendelea na matibabu.

Mtanzania aliyekutwa katika gari hiyo, Hassan Mwalusanjo akituhumiwa kusafirisha wahamiaji hao kwa kutumia lori mali ya Gabriel Mwakyambiki mkazi wa Tukuyu kinyume na sheria, alikana kosa hilo.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, David Ngonyani ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 2, 2018.

Tanesco Yawasaka Wezi wa Umeme

$
0
0
Tanesco Yawasaka Wezi wa Umeme
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Kupitia kikosi kazi maalum limeendesha kampeni kabambe ya kubaini na kutokomeza matukio ya wizi wa umeme pamoja na uhujumu miundombinu ya Shirika Mkoani Njombe ikiwa ni mwendelezo wa jitihada endelevu za TANESCO katika kudhibiti upotevu wa mapato ya Shirika.



Akiongea katika kampeni hiyo, Kaimu Meneja wa TANESCO Makao Makuu anayesimamia Wateja Wakubwa Mhandisi Fredrick Njavike ambaye pia ameongoza Zoezi hilo alisema kuwa, ndani ya siku tano kupitia kampeni hiyo tayari wamekagua takribani wateja 2000 katika Wilaya ya makambako pekee huku Njombe Mjini wakitarajia kukagua wateja 1000.

Njavike ameongeza kuwa katika idadi ya wateja waliokaguliwa, wateja kadhaa walibainika kujihusisha na vitendo vya wizi wa Umeme. Kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Njombe wahalifu hao walichukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kulipa gharama za kiasi chote cha umeme walichokuwa wakiliibia Shirika baada ya kupigiwa mahesabu.

"Zoezi hili la ukaguzi na msako wa wezi wa umeme ni zoezi endelevu linalofanyika Nchi nzima na niwatahadharishe wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja, kwani ni lazma watagundulika na hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na malipo ya fidia ya kiasi cha umeme walicholiibia Shirika.

Hivyo niwaombe Wananchi kuendelea kutupa ushirikiano kwa kufichua watu wenye viashiria vya Wizi wa Umeme. Lakini pia niwaombe wateja wetu kutoa taarifa TANESCO pale wanapona hitilafu zozote katika mita zao pamoja na kuepukana na vishoka wanaowashawishi waibe umeme kwani kupitia msako huu hakuna atakayeiba Umeme na akasalimika bila kukuamatwa na kuchukuliwa hatua" Alisema Mhandisi Njavike
Naye Meneja wa TANESCO Mkoa wa Njombe, Mhandisi Emmanuel Kachewa ametoa Wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Njombe kuendelea kushirikiana na TANESCO katika kuwafichua wezi wa Umeme popote walipo ili waweze kuchukuliwa hatua na kuokoa upotevu wa mapato ya Shirika kwa ujumla.

Kwa upande wa baadhi ya wananchi walioshuhudia msako huu ukifanyika mitaani waliipongeza TANESCO kwa kuanza kutambua thamani ya mali zao na kulinda umeme wao ambapo mwanchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Mponzi alisema kuwa Matukio ya wizi wa umeme yapo mtaani na wakati mwingine yamekuwa yakisababisha hata vifo kwa wahusika kunaswa na umeme wakati wakijaribu kuiba umeme hivyo ni vyema TANESCO pia Wakatoa na Elimu juu ya madhara ya Wizi wa umeme kwa wananchi wote wafahamu.

Aidha TANESCO imekuwa ikiingia hasara kutokana na vitendo vya wateja wachache ambao kwa makusudi kabisa wamekuwa wakiliibia Shirika umeme kwa katika maeneo mbalimbali na hivyo kulikosesha Shirika mapato stahiki na kurudisha nyuma jitihada za TANESCO na Serikali Katika kusambaza Umeme Nchi nzima na hivyo kufifisha kasi ya Uimarishaji wa Miundombinu ya Uzalishaji, Ufuaji na Usambazaji umeme Nchini.

Majariwa Atoa Agizo la Kukamatwa Mkurugenzi wa Halmashauri

$
0
0
Majariwa Atoa Agizo la Kukamatwa Mkurugenzi wa Halmashauri
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mtwara, Stephen Mafipa kumtafuta popote alipo na kumkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi, Fortunatus Kagoro kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.

Mbali na Kagoro pia kaimu mweka hazina, Heri Hamad, ofisa mipango,  Teresia Nsumba  nao ameagiza wakamatwe na baada ya uchunguzi watakaobainika kwamba hawajahusika na ubadhilifu huo watarudishwa kazini,  "Lazima fedha za Serikali zitumike kama ilivyokusudiwa."

Taarifa iliyotolewa leo Februari 26, 2018 na ofisi ya Waziri Mkuu inaeleza kuwa watendaji hao wanadaiwa kutumia Sh1.8bilioni zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halmashauri ya mji wa Masasi kwa kuchora mchoro na kujenga msingi katika maeneo mawili tofauti.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa halmashauri ya mji wa Masasi na halmashauri ya wilaya ya Masasi akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.

Amesema mwaka 2014 Serikali ilipeleka Sh575milioni wilayani Masasi kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halmashauri hiyo na fedha hizo ziliishia kutumika  katika hatua za maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja na kutengeneza michoro ya jengo.

Amesema 2016/2017 Serikali ilipeleka tena Sh1.25 bilioni kwa ajili ya ujenzi huo, ambapo halmashauri hiyo ilienda kutafuta eneo lingine na kufanya tena shughuli zilizokuwa zimefanyika na kuanza ujenzi ambao umeishia katika msingi na fedha zimeisha.

Pia amewataka watendaji hao kutotumia fedha za makusanyo ya ndani kwa ajili ya kuziba pengo la fedha za mradi huo ambazo baadhi yake hazijulikani zilipo na amewaagiza madiwani kutoruhusu jambo hilo.

Waliomkimbia Waziri Alipofanya Ziara ya Kushtukiza Watakiwa Kujisalimisha Polisi Saa 10

$
0
0
Waliomkimbia Waziri Alipofanya Ziara ya Kushtukiza Watakiwa Kujisalimisha Polisi Saa 10
Baada ya viongozi wa Kampuni ya  Ujenzi ya Jesco ya jijini Mwanza kumkacha ‘kiana’ alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za kampuni hiyo, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amewaamuru kuripoti ofisini kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza kabla au ifikapo saa 10:00 jioni leo..

Mavunde ametoa agizo hilo leo Februari 26 baada ya kuwasubiri viongozi hao ofisini kwao kwa zaidi ya saa nzima bila mafanikio.

Pamoja nao, naibu waziri pia ameuagiza uongozi wa kampuni hiyo kuwasalimisha kwenye mamlaka husika wafanyakazi wawili raia wa kigeni walioajiriwa kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari na wafanyakazi wa ngazi ya chini aliowakuta eneo la ofisi hizo alipofanya ziara ya kushtukiza, Mavunde amesema uongozi wa kampuni hiyo unatuhumiwa kutowalipa mishahara wafanyakazi kwa muda mrefu pamoja na kuajiri raia wa kigeni bila kufuata taratibu za kisheria.

“Kosa lingine ni kutojisajili kwenye mfuko wa wafanyakazi (CWF), licha wizara kutoa maagizo ya kufanya hivyo mwaka mmoja uliopita,” amesema Mavunde.

Amesema iwapo tuhuma dhidi ya uongozi huo zitathibitishwa, wahusika wanakabiliwa na hatari ya kufingo cha miaka sita jela au faini ya Sh50 milioni au adhabu zote kwa pamoja.

Baada ya kutoa maagizo hayo, Mavunde ameamua kuondoka katika ofisi za kampuni hiyo kuendelea na ziara katika maeneo mengine.

Awali, baadhi ya wafanyakazi waliozungumza na naibu waziri wakiomba kutotajwa majina gazetini wamesema mkurugenzi na meneja uajiri wa kampuni hiyo wameamua kuingia mitini kukwepa kujibu tuhuma dhidi yao za kutowalipa mishahara wafanyakazi kwa muda mrefu.

“Inawezekana taarifa za ziara ya kushtukiza ya waziri zimevuja ndio maana wamekimbia,” amesema mmoja wa wafanyakazi hao

Akizungumzia ziara yake ofisini hapo, Mavunde amesema imetokana na taarifa za siri alizopata kuhusu ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za kazi ikiwemo kutowalipa wafanyakazi mishahara, ajira kwa wageni kinyume cha sheria na kutojisajili CWF.

   

Polisi Wavamia Mkutano wa ACT-Wazalendo

$
0
0
Polisi Wavamia Mkutano wa ACT-Wazalendo
Mkutano wa ndani wa Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe uliokuwa unafanyika katika Kata ya Nambisi,wilayani Mbulu umevamiwa na Polisi wakiwa katika magari ya Defender.

Taarifa iliyotolewa leo na Afisa Habari wa Chama hicho, imeeleza kuwa polisi baada ya kuzungumza na Mwenyekiti wa Mkoa Manyara na kuelezwa kuwa kikao ni cha ndani hakihitaji taarifa Polisi wameondoka na kuagiza diwani wa kata huyo kuripoti kituo cha Polisi.

Taarifa kwa waandishi

MKUTANO wa ndani wa Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo,ndugu Zitto Kabwe uliokuwa unafanyika katika Kata ya Nambisi,wilayani Mbulu umevamiwa na Polisi wakiwa katika magari ya defender

.Baada ya kuzungumza na Mwenyekiti wa Mkoa Manyara na kuelezwa kuwa kikao ni cha ndani hakihitaji Taarifa Polisi wameondoka na kuagiza diwani Wa kata huyo kuripoti kituo cha Polisi

Abdallah Khamis

Afisa Habari

ACT Wazalendo

26/02/2018

Zitto yupo katika ziara ya mikoa 8 kutembelea Kata mbalimbali ambazo wananchi walichagua Madiwani kutoka chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Watu Wawili Wakamatwa Kwa Tuhuma za Mauaji ya Kiongozi wa Chadema

$
0
0
Watu Wawili Wakamatwa Kwa Tuhuma za Mauaji ya Kiongozi wa Chadema
Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata watu wawili wanaotuhumiwa kuhusika kwenye mauaji ya aliyekuwa Katibu wa CHADEMA kata ya Hananasif, aliyeuawa kwa kukatwa na mapanga na mwili wake kutupwa Coco Beach.

Tokeo la picha la kamanda mambosasa
Kamanda Mambosasa

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Februari 26, 2018. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema watu hao ni mwanamke na mwanaume huku akikataa kuwataja majina yao ili kutoharibu ushahidi.

“Mnamo tarehe 23 Februari 2018 majira ya saa 5:30 usiku huko katika maeneno ya Hananasif, Kinondoni kufuatia uchunguzi unaoendelea juu ya mauaji yaliyokuwa yameripotiwa wamekamatwa watu wawili mmoja wa kike na mwingine mwanaume kwa tuhuma zinazohusiana na mauaji haya,“amesema Kamanda Mambosasa na kutolea maelezo juu ya majina yao.

“Nimeshindwa kuwataja majina hapa kwa sababu za kiupelelezi katika wale ambao wanafuatiliwa hapa bado wengine hatujawakamata, kwa hiyo tutaendelea kuwafuatilia ili tuweze kuwatia mbaroni,“amesema Mambosasa.

Soma zaidi – Marekani yalaani mauaji ya kiongozi wa CHADEMA

Wiki mbili zilizopita mwili wa marehemu Daniel John uliokotwa katika fukwe za Coco Beach ukiwa umejeruhiwa vibaya na mabanga sehemu za mwili wake.

Dogo Janja Adaiwa Ameolewa..

$
0
0
Mkali wa Bongofleva Edu Boy ameamua kumjibu Dogo Janja ile kauli aliyomuambia kuwa yeye ni mtoto na kumuambia kwa kusema Janja ameolewa na ndo maana anaona wenzake wadogo hivyo apambane na ndoa yake.

Akiongea na eNEWZ amesema kinachomsumbua Dogo Janja ni kwamba ameolewa na hajaoa, huenda baada ya yeye kufunga ndoa anahisi kwamba kila kitu kipo sawa kwake na kuwaona wasanii wenzake wadogo kiumri na hata kimaisha.

''Dogo Janja ni mdogo sana kwangu kiumri nina uwezo wa kumshika na kumpiga vibao kama mdogo wangu na akatulia asiniambie chochote, kumuoa Irene asione kama amemaliza kila kitu'', amesema.

Edu Boy pia amefunguka kuwa anasikia Stamina anamtafuta hivyo aende tu kwenye maeneo ambayo anapatikana kama studio za Mona Ganster atamkuta wamalizane.
Zaidi fuatilia ENEWZ ya EATV saa 12:00 jioni.

Tundu Lissu Afunguka Kuhusu Hukuma ya Sugu na Masonga...Adai ni Heshima

$
0
0
Salaam kutoka Belgium

Waheshimiwa wangu salaam kutoka Ubelgiji. Nawapeni pole nyingi kwa yaliyomkuta Mh. Sugu na Goddie Masonga siku ya leo.

Naomba kuzungumzia suala hili kwa kirefu kidogo.

Kwanza, hukumu ya leo sio mwisho wa mjadala mahakamani. Bado kuna fursa, nay haki, ya rufaa High Court na, ikibidi, Court of Appeal.

Pili, hukumu ya leo haina maana Sugu atakaa gerezani muda wote huo. Kuna haki ya dhamana pending appeal. Ndivyo ambavyo tumefanya kwa viongozi na wanachama wetu wengi in the past.

Tatu, hukumu ya leo haina athari yoyote kwa ubunge wa Sugu. Katiba inaweka masharti ya kifungo cha miezi sita au zaidi, na kwa makosa ya 'utovu wa uaminifu.' Uchochezi au kutoa lugha ya matusi sio makosa ya utovu wa uaminifu.

Nne, pamoja na kwamba sijaona nakala ya hukumu, adhabu ya kifungo bila faini kwa kosa la kwanza ni kinyume na sentencing principles. Hii ni mojawapo ya hoja zetu zilizoshinda katika kesi ya Mh. Juakali High Court mwaka jana.

Tano, hata kama atakaa gerezani muda wote huo, hukumu za kesi za kisiasa kama hii hazijawahi kuwapunguzia heshima wapigania haki popote pale duniani.

On the contrary, kifungo cha aina hii ni beji ya heshima kwa kila mpigania haki na uhuru. Orodha ya mifano ni ndefu sana: Nyerere (ijapokuwa yeye alilipa faini), Kenyatta, Mandela, Mugabe, Fidel Castro, etc.

Alichokifanya hakimu leo ni kuwaongeza Sugu na Masonga kwenye orodha hii ya heshima. They'll come out even bigger and stronger than when they went in.

Sita, naunga mkono pendekezo la Mh. Zitto kwamba wabunge wetu wote warekodi maneno aliyofungiwa nayo Sugu na kuyaweka mitandaoni ili watukamate na sisi pia.

Instead of agonising, let's organise and make this issue bigger and bigger mpaka wakimbie wenyewe au watukamate na kutufunga wote.

Na sio wabunge tu, tuhamasishe kila mwanachama wetu na kila anayechukizwa na uonevu huu ayarudie maneno haya ili nao wakamatwe na kufungwa.

Tumlazimishe Magufuli na watu wake waamue: waigeuze nchi nzima kuwa gereza moja kubwa, au akubali kusemwa kwa maneno na lugha asiyoipenda. Hiyo ndio maana pekee ya freedom of speech in a democracy.

Nawatakieni kila la kheri katika hii safari ndefu ya kuelekea kwenye haki.

Tundu Lissu

Nuh Mziwanda Akiri Hana Kifua Cha Kuficha Mambo yake ya Ndani

$
0
0
Msanii wa Bongofleva Nuh Mziwanda amekiri kushindwa kuwa na kifua cha kuficha mambo yake ya ndani na ndo maana imekuwa rahisi kwake kuandika nyimbo zinazohusiana na historia yake ya kweli.

Akiongea na eNEWZ Nuh amesema kwamba ''Si mara ya kwanza kuimba juu ya mahusiano yangu yaliyopita ukiacha wimbo wa Jike Shupa na sasa nimeimba wimbo mwingine unaoitwa 'Upofu' ambao ndani ya wimbo huo nimeimba yaliyonitokea kwa aliyekuwa mke wangu na mama mtoto wangu Nawal'', amesema.

Nuh amefunguka zaidi kuwa yeye sio msiri na hawezi kukaa na kitu ambacho kinamuumiza moyo lazima akiweke wazi ili abaki na amani lakini pia hutumia nafasi hiyo kuelimisha wale ambao wanamuangalia yeye kama mfano waweze kujifunza kitu kutoka kwake.

Mkali huyo pia amewaomba mashabiki zake kuendelea kumpatia sapoti katika mziki wake na kufuatilia nyimbo zake huku akisisitiza kwamba nyimbo zake zote ameimba historia yake ya kweli na ni mambo tu ambayo  yanaweza kumtokea mtu yeyote.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images