Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Simba aunguruma uwanja wa Taifa autawala msitu wa Mbao

$
0
0

Wekundu wa msimbazi Simba SC hii leo wameweza kuifunga timu ya Mbao FC kwa jumla ya mabao 5 – 0  bila huruma mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara uliyopigwa uwanja wa Taifa.

Mashujaa waliyo ifundisha Mbao FC somo la soka hii loe ni Shiza Ramadhani Kichuya huku Mshambuliaji wake rai wa Uganda, Emmanuel Okwi akitakata uwanjani baada ya kutupia mawili yanayomfanya kutimiza idadi ya magoli 16 katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu.

Nikki wa Pili, Roma, Nay wa Mitego na Kala Jeremiah baada ya hukumu ya Sugu

$
0
0
Ikiwa leo February 24, 2018 Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela, wasanii mbali mbali wameonyeshwa kuguswa na hilo lilomfika Sugu.

Wasanii wao wameguswa kutokana Sugu ni miongoni mwa wasanii wa mwanzo waliyoipa heshima kubwa Bongo Flava na kuifanya kukubalika zaidi. Nikki wa Pili, Izzo Bizness, Kala Jeremiah, Nay wa Mitego na Rama Dee watumia mitandao ya kijamii kuandika haya;

nikkwapili :Nguvu ya Mungu ikapate kuwa nawe pamoja na familia yako, gerezani sio kaburini stay strong Jongwe

izzo_biznesss: Stay strong Big Brother JONGWE.

kalajeremiahs: TAY STRONG JONGWE

naytrueboytz: Stay Strong Brother Sugu

legendeeofficial: Nasikitika sana kwa hii habari kama Msanii pia kama Rafiki Wa Sugu,hii si picha nzuri!

professorjaytz :#This Too Shall Pass Mungu Sio KIZIWI wala Sio KIPOFU..

Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wamehukumu kifungo cha miezi mitano jela. Sugu anakabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais Magufuli ambayo wanadaiwa kuitoa December 30, 2017 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge mkoani Mbeya.

Mkutano wa Mh. Zitto Wavamiwa na Polisi

$
0
0
Mkutano wa ndani wa Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe uliokuwa unafanyika katika Kata ya Nambisi,wilayani Mbulu umevamiwa na Polisi wakiwa katika magari ya Defender.


Taarifa iliyotolewa leo na Afisa Habari wa Chama hicho, imeeleza kuwa polisi baada ya kuzungumza na Mwenyekiti wa Mkoa Manyara na kuelezwa kuwa kikao ni cha ndani hakihitaji taarifa Polisi wameondoka na kuagiza diwani wa kata huyo kuripoti kituo cha Polisi.

Taarifa kwa waandishi

MKUTANO wa ndani wa Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo,ndugu Zitto Kabwe uliokuwa unafanyika katika Kata ya Nambisi,wilayani Mbulu umevamiwa na Polisi wakiwa katika magari ya defender

.Baada ya kuzungumza na Mwenyekiti wa Mkoa Manyara na kuelezwa kuwa kikao ni cha ndani hakihitaji Taarifa Polisi wameondoka na kuagiza diwani Wa kata huyo kuripoti kituo cha Polisi

Abdallah Khamis

Afisa Habari

ACT Wazalendo

26/02/2018

Zitto yupo katika ziara ya mikoa 8 kutembelea Kata mbalimbali ambazo wananchi walichagua Madiwani kutoka chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Mabasi ya Utalii Kuanza Kuzunguka Dar es Salaam

$
0
0

Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam imepitisha silingi bilioni 75 za bajeti kwa mwaka 2018/2019 huku kipaumbele kikiwekwa kwenye utalii.

Ndani ya bajeti hiyo zimetengwa fedha kwa ajili ya kununua mabasi makubwa ya kitalii ambayo yatakuwa yakizunguka katika viunga mbalimbali vya Jiji la Dar es Salaam kuwazungusha watalii.

Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita alisema tayari mabasi mawili yameshawasili na yanasubiriwa mengine ili biashara ya utalii ndani ya jiji ianze mapema iwezekanavyo.

“Nadhani madiwani kwa pamoja tumeona imefika wakati kuweka nguvu kubwa kwenye utalii katika jiji letu kama ilivyo katika miji mingine mikubwa barani Afrika mfano majirani zetu Mombasa na Lamu,” alisema.

Mjumbe wa baraza la madiwani la halmashauri hiyo na mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea alisema ni hatua kubwa kwa jiji na ilipaswa kuwa hivyo muda mrefu.

“Ukitembea katika nchi mbalimbali wenzetu wamezingatia mno suala la utalii wa ndani ya mji, naweza kusema tumechelewa ilitakiwa tufike huko muda mrefu ndiyo sababu suala hili lilipokuja kwetu tumeliridhia,” alisema.

Wahamiaji 83 wa Ethiopia Wapandishwa Kizimbani

$
0
0
Wahamiaji 83 raia wa Ethiopia na Mtanzania mmoja mkazi wa Tukuyu wamefikishwa Mahakama ya Mkoa Iringa huku wahamiaji hao wakituhumiwa kuingia nchini bila kibali.

Akisoma mashtaka hayo leo Februari 26, 2018, wakili wa Serikali, Godfrey Ngwijo amesema raia hao wanakabiliwa na shtaka la kuingia nchini kinyume na kifungu cha sheria namba 45(i) kifungu (1) ,(2) kilichofanyiwa marekebisho 2016.

Ngwijo amesema Februari 23, 2018 saa moja jioni katika kijiji cha Mazombe wilayani Kilolo, wahamiaji 83 wasio na vibali walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi kwa kuingia nchini kinyume na sheria ambapo dereva wa lori walilopanda  hakupatikana baada ya kukimbia.

Amesema wahamiaji hao walikamatwa wakiwa katika hali mbaya kutokana na kukaa sehemu ya nyuma ya lori hilo ambako hakuna hewa ya kutosha, joto kali na kutokula chakula kwa muda mrefu.

Baadhi ya wahamiaji hao leo wamefikishwa hospitali ya mkoa kupata matibabu.

Wakili huyo amesema kati ya waliofika mahakamani kusomewa mashtaka yao, watatu  walishindwa kufika kwa sababu bado wako hospitali wanaendelea na matibabu.

Mtanzania aliyekutwa katika gari hiyo, Hassan Mwalusanjo akituhumiwa kusafirisha wahamiaji hao kwa kutumia lori mali ya Gabriel Mwakyambiki mkazi wa Tukuyu kinyume na sheria, alikana kosa hilo.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, David Ngonyani ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 2, 2018.

Waziri Mkuu Aiagiza TAKUKURU Kuwakamata Aliiyekuwa Mkugenzi wa Halimashauri Masasi na Mweka Hazina

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mtwara Bw. Stephen Mafipa  kumtafuta popote alipo na kumkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Bw. Fortunatus  Kagoro  kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.

Mbali na Bw. Kagoro pia Kaimu Mweka Hazina Bw. Heri Hamad Afisa Mipango Bi Teresia Nsumba  nao ameagiza wakamatwe na baada ya uchunguzi watakaobainika kwamba hawajahusika na ubadhilifu huo watarudishwa kazini. "Lazima fedha za Serikali zitumike kama ilivyokusudiwa."

Watendaji hao wanadaiwa kutumia sh. bilioni 1.8 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Mji wa Masasi kwa kuchora mchoro na kujenga msingi katika maeneo mawili tofauti.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Februari 26, 2018) wakati akizungumza na watumishi na Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Masasi na Halmashauri ya wilaya ya Masasi akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.

Amesema mwaka 2014  Serikali ilipeleka sh milioni 575 wilaya Masasi kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Halmashauri hiyo na fedha hizo ziliishia kutumika  katika hatua za maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja na kutengeneza michoro ya jengo.

Waziri Mkuu amesema 2016/2017 Serikali ilipeleka tena sh. bilioni 1.25 kwa ajili ya ujenzi huo, ambapo Halmashauri hiyo ilienda kutafuta eneo lingine na kufanya tena shughuli zilizokuwa zimefanyika na kuanza ujenzi ambao umeishia katika msingi na fedha zimeisha.

Pia amewataka watendaji hao kutotumia fedha za makusanyo ya ndani kwa ajili ya kuziba pengo la fedha za mradi huo ambazo baadhi yake hazijulikani zilipo na amewaagiza Madiwani kutoruhusu jambo hilo.

"Madiwani msikubali kutumia fedha za makusanyo ya ndani kupeleka kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo ambayo tayari Serikali ilishatoa fedha ya ujenzi wake.

Amesema Serikali inahitaji kuona fedha za maendeleo zinazopelekwa katika Halmashauri mbalimbali nchini zinatumika kama ilivyoelekeza na si vinginevyo na Serikai haitakuwa na mzaha kwa mtumishi atakayezitumia vibaya.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 26, 2018.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

$
0
0
SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN na Nyota

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

 ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO   HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, NA KUPONYA MAGONJWA SUGU ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp 0622766715

Mahakama Yatupilia Mbali Kesi ya Mchungaji Mwingila

$
0
0
Mahakama Yatupilia Mbali Kesi ya Mchungaji Mwingila
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia  mbali kesi ya madai iliyofunguliwa na Dkt. William Morris, raia wa Marekani dhidi ya mkewe Phills Nyimbi na Mchungaji Josephat Mwingira na kutaka alipe gharama alizotumia mdaiwa.

Dkt. William Morris aliwasilisha maombi mahakamani hapo akiomba mkewe, Mwingira na mtoto wake (9) wafanyiwe kipimo cha kujua vinasaba  vya mtoto (DNA).

Dkt. Morris ambaye ni mume wa (mdaiwa wa pili, Phills Nyimbi) aliiomba mahakama itoe amri ya mkewe, Mwingira na mtoto wakafanyiwe kipimo hicho cha DNA ili aweze kujua wazazi  halisi wa mtoto aliyezaa na mkewe.

Alidai mchungaji Mwingira alizini na mkewe na hatimaye kuzaa naye mtoto wa huyo wa kiume.

Akisoma hukumu hiyo leo Februari 26,  Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, amesema Dkt.  Morris katika kesi hiyo ameshindwa kuonyesha mahusiano ya kimapenzi  kati ya Phills na Mchungaji Mwingira.

Pia ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa na mke wa  Morris ni matokeo ya  mahusiano ya kimapenzi  kati ya Phills na Mchungaji Mwingira.

Hivyo mahakama imeitupilia mbali kesi hiyo na kusema mdai ameshindwa kuthibitisha madai yake  katika kiwango kinachotakiwa katika mashauri ya madai na alipe gharama.

Desemba 28, 2011,  Morris na Phills  walifunga  ndoa  ya kanisani  na wakati wa mahusiano yao, Phills  na Mchungaji Mwingira wanadaiwa  kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na kupata  mtoto wa kiume.


Daina Nyange Atoa la Moyoni Kuhusu Aliyemtundika Mimba "Muda si Mrefu Nitamtambulisha Baba Kijacho Wangu"

$
0
0
Daina Nyange Atoa la Moyoni Kuhusu Aliyemtundika Mimba "Muda si Mrefu Nitamtambulisha Baba Kijacho Wangu"
KUTOKANA na gumzo ambalo linaendelea kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii, juu ya mtu aliyemtundika ujauzito mwanadada Dayna Nyange, kuzidi kushika kasi, mwenyewe ameibuka na kutoa la moyoni.

Akichonga na Full Shangwe, Dayna aliyetoa Wimbo wa Sale Sale, alisema kuwa, watu kubashiri mara kwa mara juu ya baba wa kijacho wake ni kwa sababu wana hamu sana ya kumfahamu na kiu yao anakwenda kuikata hivi karibuni.

“Muda si mrefu ninakwenda kumtambulisha baba kijacho wangu, nakwenda kufanya hili kwa sababu watu wanaonekana wana kiu sana ya kumfahamu kiasi kwamba wanakuwa wanabashiri mpaka kuwagusa wasionihusu kabisa,” alisema Dayna.

Alipoulizwa lini hasa anakwenda kufanya hivyo alisema ni surprise lakini ni katika kipindi kifupi kuanzia sasa!

Hatimaye Diamond Akabidhiwa Leseni ya Wasafi Redio,TV

$
0
0
Hatimaye Diamond Akabidhiwa Leseni ya Wasafi Redio,TV

Msanii wa muziki, Diamond Platnumz Jumatatu hii amekabidhiwa leseni ya kurusha matangazo ya vituo vyake vya Wasafi Redio na Wasafi TV na Mhe. Waziri wa Habari, Tamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar, Rashid Ali Juma.

Hatua hiyo inaonyesha huwenda vituo hivyo vikaanza kurusha matangazo hivi karibuni kutokana na maandalizi mengi kufanywa.


Diamond amepost ujembe huu instagram.. Leo tulikabidhiwa Rasmi Leseni ya @wasafitv na @wasafifm na Mh Waziri wa Habari, Tamaduni , Utalii na Michezo Zanzibar mh Rashid Ali Juma…..Shukran Nyingi ziifikie Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jamuhuri nzima ya Muungano wa Tanzania… Ma raisi zetu pendwa Dr John Pombe Magufuli & Dr Ali Mohammed Shein pamoja na Mawaziri wa Habari Tamaduni na Michezo Mh Rashid Ali Juma & Harrison Mwakiyembe….Tamanio letu ni kutengeneza nyanja za Ajira kwa nduguzetu wenye Taaluma za Habari na Utangazaji ambao pengine hawajapata nafasi bado….kwa kuthamini kuwa, bila wao leo hii sisi tusingekuwepo….lakini pia Pamoja kushirikiana na Media zetu nchi Kuendeleza kunyanyua Vipaji toka mitaani na Tasnia nzima ya Sanaa, Michezo na Tamaduni…. #HiiNiYetuSote

Mbowe Aitaka Serikali Kudhibiti Matukio ya Mauaji ya Kikatili

$
0
0
Mbowe Aitaka Serikali Kudhibiti Matukio ya Mauaji ya Kikatili

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Tanzania haitakuwa salama kama haki haitatendeka kwa Serikali kutafuta ufumbuzi na kudhibiti matukio ya watu kuuawa kikatili.

Akizungumza jana wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Diwani wa Namwawala wilayani Kilombero, Godfrey Luena aliyeuawa Februari 22 kwa kukatwa mapanga, Mbowe alisema Watanzania wasikubali kuingia katika uadui wa kisiasa.

Mbowe alisema matukio yanayotokea sasa ya mauaji yanatia shaka na Serikali isipoyadhibiti itasababisha wananchi wanaopotelewa na ndugu kukaa na manung’uniko.

Alimuomba Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, James Ihunyo aliyehudhuria mazishi hayo kuwatuliza vijana wenye jazba kuhusu matukio yanayoendelea nchini. Mkuu wa Wilaya, Ihunyo aliposimama kuzungumza alisema wameshaunda timu maalumu kuwasaka waliohusika na tukio hilo.

Awali, Mbowe alisema matukio ya mauaji ya kikatili dhidi ya viongozi wa Chadema hayatairudisha nyuma badala yake wataendelea kuimarika.

Alisema kwa kuwa Polisi imetoa tamko kuwa kushambuliwa Luena kunatokana na kisasi, hivyo inawajua watuhumiwa, ana imani watakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya dola.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu alisema ndani ya mwezi mmoja chama hicho kimepoteza viongozi wawili katika matukio yanayofanana. Alimtaja mwingine kuwa ni Katibu wa Chadema Kata ya Hananasif jijini Dar es Salaam, Daniel John ambaye mwili wake uliokotwa katika ufukwe wa Coco.

Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na wabunge wa Kilombero Peter Lijuakali, Susan Kiwanga wa Mlimba na Devotha Minja wa Viti Maalumu.

Rais wa Afrika Kusini Atangaza Baraza Jipya la Mawaziri

$
0
0
Rais wa Afrika Kusini Atangaza Baraza Jipya la Mawaziri
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza baraza lake jipya la mawaziri.

Waziri wa zamani wa fedha Nhlanhla Nene amerejeshwa tena katika nafasi hiyo.

Nene alifukuzwa Disemba 2015 na Rais wa zamani Jacob Zuma na nafasi yake ikachukuliwa na Des van Rooyen.

Palipotokea anguko la thamani ya randi alilazimika kumfukuza Rooyen na kumchagua Pravin Gordhan, siku nne baadae ambaye pia alimfukuza kazi siku za mbeleni.

Katika baraza la Ramaphosa, Gordhan amerejea kama waziri wa masuala la biashara.
Aliyekuwa mke wake Zuma, Nkosazana Dlamini-Zuma, ameteuliwa kuwa waziri wa ofisi wa rais.

Bw Ramaphosa, ambaye ni mfanya biashara wa umri wa miaka 65, katika hotuba yake ya taifa awali mwezi huu, aliahidi kupambana na rushwa na kuboresha uchumi wa nchi hio.

Aliingia madarkani baada ya mtangulizi wake kuondoka katika hali tete, akikataa shinikizo kubwa ya yeye kujiuzulu.

Utawala wa miaka tisa ya Bw Zuma ulikumbwa na misukosuko ya shutuma za ufisadi wakati nchi ilikuwa ikipambana na madeni ya ndani pamoja na viwango vya juu vya ukosaji ajira.

Mke wa Sugu Afunguka Haya Baada ya Sugu Kuhukumiwa Miezi Mitano

$
0
0
Mchumba wa Sugu Afunguka Haya Baada ya Sugu Kuhukumiwa Miezi Mitano
Mchumba wa Mhe. Joseph Mbilinyi “Sugu', Happyness Msonga amefunguka na kusema kuwa kitendo cha kufungwa jela miezi mitano kwa mchumba wake huyo kinaweza kuleta athari kidogo kwenye familia lakini amedai alishajipanga kukabiliana na hali hiyo.


Happyness amesema hayo leo Februari 26, 2018 baada ya Sugu kukutwa na hatia na kushtakiwa kwenda jela miezi mitano na kusema kuwa tayari alianza kupambana na changamoto hizo hivyo haitakuwa na tatizo.

"Pengo ni kubwa kwa sababu Joseph ana familia lakini pia mbali na kuwa Mbunge pia ni mfanyabiashara kwa hiyo utaona changamoto ambazo nitabaki nazo lakini si changamoto kwa sababu nimeshazikabili kipindi ambacho alikuwa ndani kwa mwezi mzima, nilikuwa tayari na familia na kuweza kusimamia kila kitu bila tatizo lolote" alisema Happyness

Mbali na mchumba wa Sugu mke wa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga, Grace Malya naye amedai kuwa kifungo hicho cha mumewe kitaathiri familia yake na kudai kuwa lakini wao walikuwa wameshajiandaa kwa jambo hilo.

"Hata leo pia hukumu hii sikuipokea sawa sawa na bado ni changamoto lakini hatuna jinsi kwa kuwa tayari wameshaamua japokuwa tulikuwa tunaona dalili zote kwamba hili litatokea" alisema Mke wa Masonga

Ofisa Ardhi Amwaga Chozi Mbele ya Waziri

$
0
0
Ofisa Ardhi Amwaga Chozi Mbele ya Waziri
MPIMA Ardhi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Thobias Patrick, jana alimwaga machozi mbele ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, wakati akijitetea kuhusu tuhuma za kupima eneo la serikali na kujimilikisha kisha kuliuza.

Patrick alikumbana na kadhia hiyo wakati wa ziara ya Waziri Lukuvi katika kampeni yake ya ‘Funguka kwa Waziri’ baada ya wakazi wa mji huo kumfikishia Waziri tuhuma zinazomkabili ofisa huyo.

Baada ya kupata tuhuma hizo, Lukuvi alitembelea eneo hilo na kumhoji ofisa huyo kwa nini alipima eneo la serikali na kumilikisha watu binafsi na yeye akiwa mmiliki wa kiwanja kimojawapo na kisha kukiuza.

Kutokana na swali hilo, Patrick alipata wakati mgumu kujibu tuhuma hizo ambazo zimekuwa zikimkabili kwa muda mrefu, hivyo kujikuta akitokwa machozi huku akijitetea kuwa eneo linalohusishwa na tuhuma hizo si lake kwa kuwa yeye aliuza kiwanja namba 590 Block N na si hicho anachotuhumiwa kukiuza.

Waziri Lukuvi alimwonya ofisa huyo kutojihusisha na ununuzi wa maeneo yenye utata wakati akijua yeye ni mtumishi wa serikali tena akiwa ofisa anayehusika na upimaji wa maeneo hayo.

Waziri Lukuvi yuko katika ziara zake za kukutana na wananchi walio na migogoro ya ardhi na kuitatua ana kwa ana.

Kwa sasa anaendelea na ziara yake kutatua migogoro ya ardhi katika kampeni yake ya ‘Funguka kwa Waziri’.

Hadi sasa ameshasikiliza na kutatua zaidi ya kero na migogoro 2,000 katika mkoa wa Dar es Salaam na wilaya zake za Ilala, Kinondoni na Temeke, mkoa wa Kagera katika Wilaya za Karagwe, Kyerwa na Ngara na kwa upande wa Shinyanga wilaya ya Kahama.

Baada ya Shinyanga, Lukuvi anataraji kufanya ziara katika mkoa wa Pwani ambako kuna migogoro mingi ya ardhi ya muda mrefu kabla ya kwenda maeneo mengine Tanzania Bara.

John Bocco Ajishindia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi January

$
0
0
 John Bocco Anajishindia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi January

Wakati Simba SC ikitawala vema msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara kwa kujikusanyia jumla ya alama 44 mpaka sasa wakati huo huo mshambuliaji wake, John Bocco anajishindia tuzo ya mchezaji bora.

Bocco amejishindia tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari hii leo wakati wa mchezo wa timu yake ya Simba SC dhidi ya Mbao FC ya jijini Mwanza.

Wakati mshambuliaji huyo akitwaa tuzo hiyo ya mwezi, timu yake ya Simba SC hii leo wameweza kuifunga timu ya Mbao FC kwa jumla ya mabao 5 – 0  bila huruma mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara uliyopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Stamina Hana Uwezo wa Kunipiga- Edu Boy

$
0
0
Stamina Hana Uwezo wa Kunipiga- Edu Boy
Msanii Edu Boy amedai kuna taarifa kuwa Stamina anamtafuta ili kumpiga baada ya kumchana kwenye ngoma yake ‘Tunasafisha’ ila ni kitu ambacho hakimuumizi kichwa.

Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa haishi kwa sheria za mtu yeyote na iwepo Stamina anamtafuta yeye sehemu yoyote anapatikana.

“Siishi chini ya sheria ya mtu, naishi chini ya sheria za nchi ila siishi kwamba nikimchana Stamina nitakutana naye anipige, kwanza hana uwezo wa kukutana na mimi anipige naamini kwa asilimia mia,” amesema.

Ameongeza kuwa anajua fika kwa sasa wasanii wengi hawampendi kutokana amekuwa na tabia ya kuwachana kila mara ila jambo hilo halitomzuia kufanya muziki wake.

Yanga Yapewa Nafasi ya Kujiandaa Ligi ya Mabingwa Afrika

$
0
0
Yanga Yapewa Nafasi ya Kujiandaa Ligi ya Mabingwa Afrika

Mechi ya Yanga na Mtibwa iliyokuwa ipigwe hivi karibuni imeahirishwa ili kuipa nafasi Yanga kujiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ilikuwa na kibarua hicho cha kucheza na Mtibwa baada ya kukutana na Ndanda FC hata hivyo kwa mujibu wa mabadiliko hayo sasa mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine ili kuwapa nafasi wawakilishi hao kujiandaa vyema.
Yanga itakutana na Ndanda kesho Jumatatno kwenye mechi ya Ligi Kuu na baada ya hapo itapata muda wa kujiandaa mechi ya  Ligi ya Mabingwa Africa dhidi ya Township Rollers ya Botswana.
Mchezo huo dhidi ya Rollers ambayo wapo kileleni mwa Ligi Kuu ya Botswana ikiwa na pointi 45 msimu huu, utachezwa Machi 6, 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Afisa Ataka Kufanya Vitendo vya Ulawiti Bungeni

$
0
0
Afisa Ataka Kufanya Vitendo vya Ulawiti Bungeni

Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya amemfungulia mashtaka mfanyakazi wa Bunge la nchi hiyo, kwa kutaka kumlawiti

Mfanyakazi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya usalama wake, ametajwa kutaka kumfanyia kitendo hiko kiovu mwanafunzi wa kiume, kwenye maeneo ya ofisi za bunge.

Kwenye maelezo yake mwanafunzi huyo amesema kwamba afisa huyo alimfuata na kumwambia yeye ni Afisa wa Polisi, na kumchukua mpaka ndani ya majengo ya bunge, na kuanza kumfanyia vitendo hivyo viovu.

“Aliniafuata na kunikamata akiniambia yeye ni polis, akanipeleka ndani ya jengo la bunge, na kuanza kugusa na kuniingiza uum* wake sehemu zangu za nyuma za siri..”, alikuwa akielezea mwanafunzi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa pia.

Hata hivyo tetesi zinasemekana kuwa muhanga wa tukio hilo alikubali kufuta kesi mahakamani, baada ya kupewa rushwa ya shilingi elfu 5 ya Kenya, amabyo ni sawa na shilingi laki moja ya Tanzania. Source Citizen

IGP Sirro Awatumia Salamu Wanaoandaa Kufanya Maandamano

$
0
0
IGP Sirro Awatumia Salamu Wanaoandaa Kufanya Maandamano
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro amefunguka na kuwaonya watu wanaohamasisha kufanyika kwa maandamano nchini Tanzania bila kufuata utaratibu na kusema jeshi la polisi limejipanga kuwakabili watu hao kwani watakuwa wakivunja sheria za nchi.


Sirro amesema hayo Februari 26, 2018 akiwa Bariadi Mkoani Simiyu wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ambapo amedai kuwa amekuwa akiona kuna watu kupitia mitandao ya kijamii wamekuwa wakihamasisha watu kufanya maandamano.

"Wote tunajua kwamba maandamano Katiba imetamka na sheria za vyama vya siasa imetamka kwamba maandamano ni haki kwa raia lakini kuna utaratibu wa maandamano, sasa kuna maandamano ambayo ni halali na ambayo si halali. Maandamano ambayo si halali maanake yanaashilia uvunjifu wa amani ni maandamano ambayo yanaelekea kutenda uhalifu sasa kama ni maandamano yanakuja kwa njia ya uhalifu na jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kuzuia uhalifu maanake ni lazima tuhakikishe maandamano hayo hayafanyiki hivyo ni lazima juhudi ifanyike kabla ya hayo maandamano kufanyika"

"Maandamano yakifanyika ambayo si halali uwezo wa kuudhibiti tunao sasa natoa ti salamu kwa wale ambao wanafikiri wataweza kufanya maandamano ambayo si halali ya kutaka kuleta vurugu ndani ya nchi ambao ni watu wachache wenye maanake ni lazima watapamba na jeshi la polisi ambalo linasimamia usalama wa nchi hii, lakini niwambie na wale vijana wadogo na wazazi, wazazi wajitahidi sana kulea watoto zao wajaribu kuwaambia watoto zao wasiingie kwenye kuvunja sheria kwani unaweza kuvunja sheria kirahisi ila madhara yake ni makubwa. Unaweza kuingia kwenye maandamano ambayo si ya halali halafu ukileta shida kubwa kwako na familia yako"

Mbali na hilo Kamanda Sirro alisema kuwa wananchi wengi ndani ya Tanzania wanataka kufanya maendeleo na hawapendi kabisa usumbufu na kusema watu ambao wanataka kuleta usumbufu wanacheza tu kwani watapamba naye.

"Wanacheza na hiyo mitandao sijui tumefika mia moja, mia mbili siju elfu moja wajaze wanachosema lakini nasema nafasi hiyo hawataipata" alisisitiza Sirro

Mfalme wa Saudi Arabia Amewafuta Kazi Mkuu wa Majeshi, Makamanda wa Vyeo vya Juu Jeshini

$
0
0
Mfalme wa Saudi Arabia Amewafuta Kazi  Mkuu wa Majeshi, Makamanda wa Vyeo vya Juu Jeshini
Leo February 27, 2018 habari kutoka nchini Saudi Arabia ni kwamba Mfalme wa nchi hiyo King Salman amefanya mabadiliko katika jeshi la nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwafuta kazi Makamanda wa Vyeo vya juu jeshini akiwemo Mkuu wa majeshi.

Taarifa hiyo imetolewa na shirika rasmi la habari la Saudi Arabia la SPA ambapo limeeleza kuwa Mfalme Salman pia amefanya mabadiliko kwa Makamanda wa vikosi vya nchi kavu na vile vya angani.

Hadi sasa hakuna sababu yoyote ya mabadiliko hayo iliyowekwa wazi lakini inasemekana mabadiliko hayo kiasi flani yameshawishiwa na Mrithi wa Mfalme Mohammed bin Salman.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images