Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Watu 9 wakamatwa na Jeshi la Polisi

$
0
0
Watu tisa wanaodhaniwa kuwa ni wahamiaji haramu wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kwa tuhuma za kuingia nchini Kinyume cha sheria.

Watuhumiwa hao wamekamatwa katika eneo na Nyashishi Wilayani Msingwi Mkoani humo wakiwa wamejificha katika vichaka kwa ajili ya kwenda kuchukuliwa kwa ajili ya kuendelea na safari yao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa kukamatwa kwa raia hao kunafuatia taarifa za raia mwema aliewatilia shaka na kisha kutoa taarifa kwa jeshi la polisi juu ya watu hao waliojificha katika kichaka hicho.

Katika hatua nyingine Kamanda Ahmed Msangi amewataka wananchi kutanguliza uzalendo kwa kuwafichua watu wanaoshi nchini bila ya kuwa na vibali maalumu na kinyume cha sheria.

Shule ya Wasichana Korogwe Yateketea kwa Moto

$
0
0
Shule ya Wasichana Korogwe Yateketea kwa Moto
Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe  iliyoko wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga, inaungua moto usiku huu, huku chanzo cha ajali ya moto huo kikiwa hakijajulikana.


Inadaiwa watu kadhaa wamejeruhiwa kutokana na moto huo. Hakuna vifo vilivyoripotiwa ama kuthibitishwa hadi sasa.


Tunaendelea kufuatilia kwa kina, taarifa zaidi tutakuletea baadaye.

Mabweni mawili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia.

Moto huo ulianza majira ya saa 3 usiku, huku wanafunzi wote walikuwa madarasani (preparation) maarufu kama prepo.


Majeruhi takribani 15 wa tukio hilo hiyo walitokana mshtuko wa moyo lakini walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Magunga na wanaendelea vizuri.

RC Dodoma Ampa Mkandarasi Wiki Mbili

$
0
0
RC Dodoma Ampa Mkandarasi Wiki Mbili
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge ametoa muda wa wiki mbili kukamilishwa kwa mkandarasi wa mradi wa Umwagiliaji unaofadhiliwa na Mpango wa Chakula Duniani WFP, ambao ulitarajiwa kukamilika mwaka 2017 wilayani Chamwino.


Maelekezo hayo ameyatoa katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya Kilimo inayotekelezwa wilayani Chamwino itakayogharimu zaidi ya shilingi milioni 800 ambapo vijiji vitatu vinatarajia kunufaika na mradi huo.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa muda uliobaki mkandarasi huyo hana budi kupelekea mafundi wote katika eneo la mradi ili kuukamilisha kwa wakati licha ya changamot zilizokuwepo hapo awali.

"Jitahidini kuanzia leo mtakuwa mmebakisha wiki mbili tu. Yaani piga ua nataka mradi ukamilike haraka iwezekanavyo. Wewe tafuta hata mafundi wako msiangalie kwamba mtapata nini sidianeni,  mafundi washirikiane na Injinia huu mradi ukamilike," Mahenge.

Kenya Yaigaragaza Tanzania Kili Marathon 2018..Haya Hapa Majina ya Washindi

$
0
0

Leo Jumapili Machi, 4 2018 yamefanyika mashindano ya riadha mkoani Kilimanjaro ambayo ni maarufu kwa Kili Marathon ambayo hufanyika kila mwaka.

Mashindano haya hushirikisha watu kutoka mataifa mbalimbali, ambapo wale wote ambao hufanya vizuri hupewa zawadi, wakati wengine hupewa medali ikiwa ni ishara kwa walishiriki mbio hizo.

Mashindano haya yalianza mwaka 2003 yakiwa na washiriki waliokadiriwa kuwa kati ya 300-400 lakini sasa yamekuwa yakishirikisha maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali.

Katika mashindano hayo, raia kutoka Kenya wamekuwa wakifanya vizuri zaidi, na hata mwaka huu wamedhihirisha hilo baada ya kuongoza kwa kuwa na washindi wengi zaidi katika kilomita 21 na kilomita 42.

Hapa chini ni orodha ya washindi wa kilomita 21.

Geofry Torotich- Kenya
Simon Muthoni- Kenya
Shadrack Korir- Kenya
Daniel Kemoi- Kenya
Stephen Mwendwa- Kenya
Nicolas Kosgei- Kenya
Tom Mutie- Tanzania
Vincent Kimutai- Kenya
George Njoroge- Tanzania
Alex Bartilol- Kenya

Walioongoza katika kilomita 42, wote ni wawakilishi kutoka Kenya.

Cosmas Muteti- Kenya
Elkana Yego- Kenya
George Onyancha- Kenya
William Koskei- Kenya
Kipngetich Timbwol- Kenya
Francis Nzyoki- Kenya
Stephen Kimbomet- Kenya
Stephen Cimemin Njogu- Kenya
Evans Taiget- Kenya
Mark Lukuya- Kenya
Kwa mwaka 2019, mbio hizo zinatarajiwa kutimua vumbi Jumapili Machi 3, 2019.

Museveni, Amfuta Kazi Inspekta Mkuu wa Polisi,

$
0
0
Museveni, amfuta kazi Kayihura na Tumukunde
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amemfuta kazi Inspekta mkuu wa polisi, Kale Kayihura na waziri wa Ulinzi, Henry Tumukunde.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Museveni amesema: ” Kwa uwezo wa mamlaka niliyopewa kikatiba, nimemteua Jenerali Elly Tumwiine kama waziri wa usalama. Nimemteua pia bwana Okoth Ochola kama afisa mkuu wa polisi. Niabu wake atakuwa ni Brigedia Sabiiti Muzeei.”



Generali Kayihura, alishiriki katika vita vilivyomsaidia rais Museveni kuingia madarakani mwaka 1986, lakini amekabiliwa na shinikizo kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa hali ya usalama.

Zaidi ya wanawake 20 wameuawa katika visa vya mauaji ambavyo havijatatuliwa katika maenoe yanayouzunguka mji mkuu wa Kampala, na katika miezi mitatu iliyopita raia watatu wa kigeni pia wameuawa.

Chadema Yafunguka Kuhusu Mbowe Kulazwa KCMC

$
0
0
Chadema Yafunguka Kuhusu Mbowe Kulazwa KCMC
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Moshi Kilimanjaro.


Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amethibitisha juu ya taarifa hiyo na kusema kuwa Mbowe amelazwa toka jana Machi 4, 2018 na mpaka sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

“Ni kweli Mbowe amelazwa toka jana yupo pale KCMC na anaendelea kupatiwa matibabu, siwezi kuzungumzia kinachomsumbua kwa kuwa ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari labda hivyo tutambue tu anaumwa amelazwa KCMC” alisema Mrema

Mbowe siku za karibuni alikuwa na mizunguko mingi mno kuanzia kwenye kampeni za uchaguzi wa Kinondoni na Siha lakini pia safari za Mbeya mara kadhaa kwenye kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini na Katibu wa CHADEMA Nyanda za Juu Kusini.

WCB Watoa Tamko Baada ya Diamond Kufungiwa Nyimbo Mbili

$
0
0
WCB Watoa Tamko Baada ya Diamond Kufungiwa Nyimbo Mbili
Mara baada ya kufungiwa kwa ngoma mbili za Diamond ‘Waka na Hallelujah’, uongozi wa WCB umetoa tamko.

Meneja wa WCB, Sallam SK amesema kabla ya kutoa ngoma zao huwa zinakaguliwa na mlezi wao ambao ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda.

Ameendelea kwa kusema bado hawaelewi sababu ya kufungiwa kwa ngoma hizo, hivyo mlevi wao ataweza kuliongelea hilo zaidi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Sallam SK ameandika;

Tumepigiwa simu na vyombo vya habari kila sehemu kuulizwa juu ya nyimbo mbili za Diamond kufungiwa, nimeona tukiwa kama taasisi huwaga tunafanya vitu kwa kutokukurupuka sie kamaWCB Wasafi tulipoona taasisi yetu inakuwa kubwa tukaomba ulezi kwa Mhe. Paul Makonda ambae ni kiongozi wa serikali mwenye kupenda maendeleo ya vijana.

Kwa hiyo nyimbo zote za WCB kabla ya kutoka lazima mlezi wetu azipitie, kuna nyimbo nyingi ameshazizuia na zinazotoka basi ameridhia yeye binafsi zitoke, kwahiyo sioni sababu ya nyimbo ya Hallelujah na Waka kufungiwa kama inavyosemekana maana sisi hatujapata barua ya kuwa nyimbo hizo zimefungiwa na kwa sababu ipi.

Kama kweli zimefungiwa basi mlezi wetu ataweza kuongea mengi zaidi yangu mimi.

Wiki iliyopita Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) ilitangaza kufungia baadhi ya nyimbo zilizooneka kutokuwa na maadili, miongoni mwa ngoma hizo ni Hallelujah ambayo Diamond ameshirikiana na Morgan Heritage na ile ya Waka aliyoshirikiana na Rick Ross.

Vigogo wa Chadema Waripoti Polisi

$
0
0
Vigogo wa Chadema Waripoti Polisi
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji na viongozi wengine wa chama hicho wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi leo asubuhi Machi 5, 2018.

Februari 27, 2018 viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye leo hayupo kwa maelezo kuwa ni mgonjwa, walifika kituoni hapo na kuhojiwa kwa takribani saa tano, kisha kuachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti tena leo.

Viongozi hao wakiongozwa na Dk Mashinji ambaye Februari 27, 2018 hakufika kuhojiwa kutokana na kuwa nje ya nchi, mpaka saa 2:15 asubuhi walikuwa wamewasili wote kituoni hapo.

Mbali na Mashinji, viongozi wengine waliofika kituoni ni naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).

Pia, wamo mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee; mwenyekiti wa kanda ya Serengeti, John Heche na Esther Matiko ambaye ni mweka hazina wa Bawacha.

Viongozi hao wameambatana na wakili Frederick Kihwelo na Alex Massaba pamoja na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya.

Massaba ameieleza MCL Digital kuwa Mbowe hatoweza kufika kwa kuwa ni mgonjwa.

Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema akiwamo Mbowe.

Wito huo ulikuja siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo kwa mawakala wao.

Julius Mtatiro "Nimeona Tangazo la Wahuni la Kunifuta Uanachama...Mimi Nipo Ofisini na Naendelea na Kazi"

$
0
0
Ndugu zangu. Nimeona taarifa kwenye mitandao kuwa kuna watu wanajiita viongozi wa CUF wilaya ya Ubungo na kwamba ati wamenivua uanachama wa CUF. Bila shaka hawa ni vijana wa Bwana yule na wanatumika kututoa kwenye ajenda kubwa za kitaifa.

Mwezi Disemba mwaka jana pia wahuni hao walitangaza ati wamenivua uanachama, tangazo lao la jana si jipya! Mimi naendelea na majukumu yangu kama kiongozi wa juu wa chama anayetambuliwa na chama na vikao vya chama, na vitangazo hivyo vya wahuni haviwezi kunishughulisha wala kuwashughulisha wenzangu.

Nasubiri tangazo lingine la wahuni hao, la kunifukuza uanachama mara ya 3, ya 4, ya 5 na ya 6. Hawatushughulishi kabisa maana dawa ya mgonjwa ni kumpa dawa tu.

#Mtatiro J,
#Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi Taifa,
#The Civic United Front (CUF),
#05 Machi 2018.

Simba Yasema Wanasubiria Ubingwa Toka kwa Yanga

$
0
0
Simba Yasema Wanasubiria Ubingwa Toka kwa Yanga
SARE ya Simba dhidi ya Stand United ni kama imewaamsha Yanga kutetea ubingwa wao lakini uongozi wa timu hiyo, umeweka wazi kuwa Yanga hawapaswi kuchekelea matokeo hayo kwani ubingwa wa msimu huu wataupata kutokea kwao.



Simba ilitoka sare ya bao 3-3 na Stand katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa huku matokeo hayo yakiibakiza kileleni ikiwa na pointi 46 baada kucheza michezo 20 huku Yanga wakiwa nafasi ya pili na pointi 40 na ikiwa na mchezo mmoja mkononi kufuatia kucheza mechi 19.



Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema kuwa matokeo waliyopata katika mchezo dhidi ya Stand ni kama yamewatoa usingizini kwani wameshapanga mkakati mzito utakaoweza kuwapa ubingwa wa msimu huu.



“Kiukweli matokeo ya sare dhidi ya Stand kwanza hatukuyategemea kabisa lakini imetokea, mashabiki hawapaswi kulalamika na watambue haiwezekani kila siku tushinde sisi, ila kitu kizuri ni kwamba hatujafungwa, sasa hao wanaoshangilia sijui wanashangilia kitu gani.



“Stand wametuamsha sasa tunaelewa na tumeweka mkakaki mzito wa kuhakikisha tunachukua ubingwa wa msimu huu na hatutaki yajirudie ya msimu uliopita lakini hao wanaoshangilia sare yetu wakumbuke tuna mechi nao ambayo tutawafunga na kuweza kuchukua ubingwa wa msimu huu,” alisema Manara.



Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana Aprili 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa ligi kuu.

Rick Ross Yupo Mahututi Alazwa Hospitali

$
0
0
Rick Ross Yupo Mahututi Alazwa Hospitali
Missy Elliot na Snoop Dogg ni miongoni mwa nyota wanaomuombea rappa Rick Ross aliyelazwa hospitalini Marekani.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 42 amelazwa katika hospitali moja huko Miami, huku taarifa zisizoweza kuthibitishwa kutoka vyombo vya habari nchini humo zikiashiria kwamba yuko katika hali mahututi.

Katika matandao wa kijamii Twitter Snoop aliandika "Maombi kwa wingi kwa rafiki yangu Rick Ross", "Tunatumai utapona ndugu yangu."

Missy Elliot amesema yeye pia anamuombea muimbaji huyo wa mtindo wa rap ambaye pia ni mfanyabiashara.

Nyimbo za Diamond na wengine zafungiwa Tanzania

Miongoni mwa marafiki wake Ross mashuhuri P Diddy alituma ujumbe katika mtandao wake wakijamii akitaka kila mtu amuombee Rick Ross.

Fat Joe na LL Cool J wameelezea wasiwasi wao, huko LL Cool J akimuambia Rick "Vumilia".

Familia ya Rick Ross imekana taarifa kwamba mwanamuziki huyo amewekwa kwenye mashine ya kumsaidia kupumua kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.

Na rappa Fat Trel, aliyesajiliwa na kampuni ya muziki ya Ross amesema "hajambo" na hakuekwa katika mashine hiyo ya kusmaidia kupumua.

Ruka ujumbe wa Instagram wa fat_gleeshMwisho wa ujumbe wa Instagram wa fat_gleesh
Rick Ross, ambaye jina lake halisi ni William Leonard Roberts II, alifafatika mara mbili katika muda wa saa 6 mnamo 2011.

Wakati huo alisema alifafatika kutokana na ukosefu kupumzika.

"Nitalala saa mbili alafu nishughulike - Kwasababu ya kutafuta riziki - u hustler," alisema.

Serikali Yakiri Uwepo wa Changamoto ya Usafishaji Umeme Nchini

$
0
0
Serikali Yakiri Uwepo wa Changamoto ya Usafishaji Umeme Nchini
Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari – Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amekiri uwepo wa changamoto ya usafishaji wa umeme nchini baada ya kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Dkt. Abbas ameyasema hayo leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, ambapo ameeleza kuwa kwenye umeme kuna mambo makubwa mawili ambayo ni uzalishaji na usafirishaji.

“Ndugu yangu kwenye umeme, umeme kuna mambo makubwa mawili, kuna uzalishaji na kuna usafirishaji kwa kweli tunazochangamoto za kuuzalisha umeme na ndizo ambapo nimeeleza kwa kweli kwa kiasi kikubwa tunaangalia kwa namna gani tunazitatua kwa maana ya kuazalisha umeme mwingi lakini lazima tukiri kwenye nchi yetu kuna changamoto kubwa sana ya kuusafirisha sasa, ukishauingiza kwenye gridi ya Taifa unafikaje kwako unafikaje kwenye viwanda? kwahiyo kuna changamoto kwenye mifumo kama hizi transfomer zinaungua mara kwa mara kutokana na hali mbalimbali za hewa na kipindi hiki cha mvua changamoto ndio zinaongezeka,“ amesema Dkt. Abbas wakati akijibu swali la mwandishi aliyehoji kukatika katika kwa umeme.

Ameongeza “Sasa kwa ambapo ninachoweza kukuhakikishia kwa mujibu wa uzalishaji wa umeme Tanzania na mahitaji bado tuna umeme mwingi sana kuliko mahitaji na kama tulivyoonyesha hapa miaka kadhaa ijayo tutakuwa na umeme mwingi zaidi“.

KCMC Yafunguka Kuhusu Maendeleo ya Hali ya Mbowe

$
0
0
KCMC Yafunguka Kuhusu Maendeleo ya  Hali ya Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC anasumbuliwa na maumivu makali ya kichwa, ameekeza Afisa Habari wa KCMC.


Ofisa habari wa KCMC, Gabriel Chisseo amesema hayo leo Machi 5,2018 alipozungumza na waandishi wa habari.

Chisseo amesema walimpokea Mbowe jana jioni Machi 4, 2018 akiwa na maumivu makali ya kichwa.

Amesema hali ya Mbowe inaendelea vizuri na amepumzishwa hospitalini hapo.

“Jana jioni tulimpokea Mbowe, taarifa zinaonyesha alikuwa na maumivu ya kichwa. Taarifa za kitabibu zinaonyesha ni uchovu,” amesema Chisseo.

Amesema madaktari wanaendelea kumhudumia kwa ukaribu na baadaye atafanyiwa vipimo vingine.

Nabii Tito Ashindwa Kufika Mahakamani Kesi Yake Yaairishwa

$
0
0
 Nabii Tito Ashindwa Kufika Mahakamani Kesi Yake YaairishwaMahakama ya Wilaya ya Dodoma kesi inayomkabili Onesmo Machibya anaefahamika kwa jina  ‘Nabii Tito ‘ya kujaribu kujiua imeahirishwa hadi March 19, 2018.

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, James Karayemaha aliagiza mtuhumiwa huyo kuchukuliwa vipimo vya akili yake ili kujua kama ana matatizo ya akili katika taasisi ya magonjwa ya akili ya Isanga mjini Dodoma.

Leo ‘Nabii Tito’ hakuweza kufika mahakamani ambapo kesi yake iliahirishwa na Hakimu Mwajuma Lukindo.

‘Nabii Tito’ anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kujiua kwa kujikata na wembe na anadaiwa kufanya hivyo Januari 25, 2018 akiwa mahabusu.

Zaidi ya Madaktari 500 Wagoma Nchini Kenya

$
0
0
Zaidi ya madaktari 500 katika hospitali kuu ya Kenyatta nchini Kenya wamesusia kazi wakitaka kurejeshwa kwa mwenzao aliyesimamishwa kazi baada ya kumfanyia kimakosa mgonjwa upasuaji wa kichwa.

Mwenyekiti wa Muungano wa Madaktari nchini, Samuel Oroko, amesema kumsimamisha kazi daktari huyo ilikuwa ni uamuzi ambao hauwezi kutatatua shida zinazoikumba hospitali hiyo.

Muungano huo unataka mfumo mzima wa hospitali kuchunguzwa, ikiwemo kuboresha mfumo wa kunakili data ya wagonjwa na pia kuongezwa kwa idadi ya maeneo ya upasuaji.

Wagonjwa wanavyoteseka kutokana na mgomo wa madaktari Kenya
Oroko alitetea uamuzi wa madaktari kususia kazi, akisema 'huu ndio wakati bora wa kuangalia kwa undani hali ya hospitali ya Kenyatta'.

Wiki iliyopita, Afisa mkuu mtendaji wa hospitali ya taifa ya Kenyatta mjini Nairobi - Lily Koros - alipewa likizo ya lazima huku Daktari na wahudumu katika hospitali hiyo wakisimamishwa kazi baada ya mgonjwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa kimakosa.

Mkasa huo ulitokana na mchanganyiko wa majina ya wagonjwa wawili wote waliokuwa wana matatizo ya kichwa, na kosa halikujulikana hadi mgonjwa mmoja alipopasuliwa kichwa ndani ya chumba cha upasuaji.

Muungano huo pia unadai marupurupu ya madaktari wakuu, ambayo wanasema hawajalipwa licha ya makubaliano na serikali mwaka jana.

Ni mwaka jana tu ambapo madaktari nchini Kenya waligoma kwa miezi mitatu wakidai kuboreshwa kwa hali za maeneo yao ya kazi sawa na mishahara.

Hospitali ya Kenyatta ndio hospitali kubwa zaidi ya umma nchini Kenya, na kusimamishwa kwa shughuli za matibabu huenda kukaathiri shughuli katika hopsitali nyingine nchini.

Takwimu zinaonyesha kuwa hospitali ya Kenyatta huwapokea wagonjwa wasiopungua 3,000 kwa siku.

Ndege za Tanzania Kuwasili Nchini Julai Mwaka Huu

$
0
0
Ndege za Tanzania Kuwasili Nchini Julai Mwaka Huu

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas, amefunguka na kuweka wazi rasmi mwezi ambao ndege za Tanzania zitawasili nchini na kusema kuwa Julai mwaka huu ndege hizo zitaingia nchini.


Akiongea na waandishi wa habari leo Machi 5, 2018 Dkt. Abbas amesema kuwa ndege hizo zinategemewa kuingia nchini mwezi Julai na kudai kuwa ndiyo maana kumekuwa na nguvu kubwa ya kuendelea kufanya upanuzi wa viwanja vya ndege nchini ili kuruhusu ndege hizo kuweza kutua katika viwanja mbalimbali.

"Julai mwaka huu nchi yetu itapokea ndege kadhaa mpya ikiwemo 'Boeing Dreamliner' hivyo ukarabati wa viwanja vya ndege vya Kitaifa/ Kimataifa na Kimkoa unaendelea kwa kasi nchini" alisema Dkt. Hassan Abbasi.

Mbali na hilo Dkt. Hassan Abbas amedai kuwa Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi kuwaondolea adha ya usafiri wananchi wa maziwa makuu ya nchi yetu likiwemo Ziwa Nyasa, Tanganyika na Victoria hivyo serikali imeanza mchakato wa kupata meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 1200.

"Meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria  1200 na mizigo tani 400 Ziwa Victoria, mkandarasi amepatikana na majadiliano ya mwisho na kusaini mkataba na kampuni ya STX ya Jamhuri ya Korea vitafanyika mwaka huu" Dkt. Hassan Abbas

Hiki Hapa Kilichojili Kwenye Kesi ya Rugemarila

$
0
0
Hiki Hapa Kilichojili Kwenye Kesi ya Rugemarila
Mahakama ya Rufani imesikiliza maombi ya mfanyabiashara James Rugemarila kuhusu kurekebisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa ya kupinga kunyimwa dhamana na Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ‘Mahakama ya Mafisadi’.

Maombi hayo yamesikilizwa mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Bernad Luanda, ambapo wengine ni Batuel Mmilla na Gerald Ndika.

Katika maombi hayo ambapo Rugemarila amejiwakilisha mwenyewe anaomba mahakama imruhusu kufanya mabadiliko ya kusudio la kukata rufaa kuhusu dhamana yake.

Pia imruhusu amuingize mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi kama mtu muhimu katika maombi hayo.

Pia mahakama hiyo impatie dhamana wakati maombi hayo yakiendelea kusikilizwa.

Katika maombi hayo upande wa Jamhuri umewakilishwa na Mawakili wanne, akiwemo Zainabu Mambo na Tumain Kweka ambao wamepinga kupokelewa kwa maombi ya Rugemarila.

Akitoa hoja za kupinga kupokelewa kwa maombi hayo, Wakili Kweka ameomba maombu hayo yatupiliwe mbali kwa sababu yamefunguliwa kupitia kifungu kisicho sahihi ambacho kinaichanganya mahakama kujua kama yamefunguliwa kama kesi ya jinai ama madai.

Pia mfanyaniashara Seth ameingizwa kimakosa katika maombi hayo, hivyo hausiki kwa sababu maombi yake dhamana Mahakama Kuu yalitupiliwa mbali, hivyo alipaswa kufungua maombi mengine katika Mahakama ya Rufaa na sio kujumuishwa katika maombi ya Rugemarila.

Kutokana na hoja hizo, Rugemarila naye ametoa hoja zake akidai kuwa maombi yake yapo sahihi na anaiomba mahakama iyapokee.

“Pingamizi la Jamhuri halipo sahihi kwa sababu hawajafafanua ipasavyo kwa kile wanachokipinga, pia walipaswa kutoa pingamizi hilo kwa njia ya maandishi,”.

Kuhusu suala la kumuingiza Sethi, Rugemarila ameiomba mahakama iyapokee kwanza maombi yake kisha wakati wa kusikilizwa ndipo ataeleza sababu za kumuunganisha.

Baada ya kueleza hayo, Jaji Luanda amesema wanaahirisha maombi hayo na watapanga tarehe kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Kwa pamoja washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309.

Zari Airudisha Upya Vita Yake na Mobetto..... Amshushia Maneno Mazito Kisa Hiki Hapa

$
0
0
Zari Airudisha Upya Vita Yake na  Mobetto.....  Amshushia Maneno Mazito  Kisa Hiki Hapa
Baada ya kuchuniana kwa muda, vita ya maneno kati ya Zari The Boss Lady na Hamisa Mobetto inaonekana kuibuka upya.

Safari hii Zari ametumia mtandao wa Snapchart kutupa madogo kwa Hamisa akielezwa kuchangazwa kwake na Hamisa kujiona mdogo na mrembo lakini hawezi kuwa na mwanaume (mpenzi) wa kwake pekee yake na hata akiwa naye hawekwi hadharani.

Pia katika post hizo za Zari anaoneka kuitangaza TV Show yake ambayo ipo mbioni. Hivi karibuni katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Zari alisema show yake hiyo itatambulika kwa jina la Life Of Zari The Boss Lady.

Pia katika posti nyingine Zari anaoneka kujibu kauli ya Hamisa ambayo alidai alikuwa katika mahusiano kwa kipindi cha miaka tisa na Diamond, Zari amechukulia jambo hilo kama ni upumbavu wa Hamisa.


Beef kati ya Zari na Hamisa lilianza pale ilipogundulika kuwa Hamisa amezaa na Diamond wakati akijua muimbaji huyo yupo katika mahusiano na Zari na tayari walikuwa wameshajaliwa watoto wawili, Tiffah na Nillan.

Polisi Wamvuruga Faiza Atamani Kuwa Mzungu Ataka Wamrudishie Simu Yake ya Milioni Tatu "Inaniuma Sana Nataka Simu Yangu"

$
0
0
Jeshi la Polisi Lamvuruga Faiza Atamani Kuwa M zungu Ataka Polisi Wamrudishie Simu Yake ya Milioni Tatu "Inaniuma Sana Nataka Simu Yangu"
Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Faiza Ally amefunguka kuwa kama angekuwa na uwezo wa kubadili utaifa wake basi angefanya hivyo na kuchangua nchi za Ulaya, kwani anaona maisha ya Tanzania yanamuwia magumu kwa upande wa uhuru wa mtu binafsi na haki za kibinadamu.

Faiza amesema hayo baada ya kudai kuwa jeshi la polisi nchini limeshikilia simu yake ya mkononi kwa miezi mitatu sasa tangu aposti picha yake akiwa leba kwenye mitandao ya kijamii.

“Kama kuna siku nimeamka na maumivu makali ni leo , leo ni siku ambayo natamani ningekua mzungu niishi katika nchi zenye haki za kibinaadamu , maana kuna wkt unahisi unaonewa kwenye nchi yako! Huu ni mwezi wa 3 toka police wachukue simu yangu I phone 7+ yenye thamani ya shilingi M.3 , inaniuma sana , kila wiki naripoti police sasa nimeanza kupewa wiki mbili, mbili, kisa ni picha yangu ya leba wao wana hesabu kama phonographs,“ameandika Faiza Ally kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kwa upande mwingine mrembo huyo amesema juzi Jumamosi alilitaarifu jeshi hilo kuwa amechoka kuripoti polisi akiwataka ajue mwisho ni lini lakini polisi walimwambia aendelee kuripoti hadi mwanasheria atakaporudisha jalada la uchunguzi.

“Juzi nimwaambia nimechoka jamani naombeni sasa nijue kuripoti huku mwisho lini? wanasema hawajui mpaka mwanasheria arudishe Jalada, nimewaomba nimuone mwanasheria wamesema siruhusiwi wao ndio wanatakiwa wafatilie ndio wa nipe majibu,“ameandika Faiza Ally.

Soma na Hii – Faiza Ally baada ya kuposti picha akiwa leba ‘Nimepongezwa sana’

Mwishoni mwa mwaka jana mrembo Faiza aliposti picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa leba, picha ambayo ilizua taharuki kwenye jamii na ndiyo iliyopelekea simu yake kushukuliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi.

SOMA WARAKA ALIOANDIKA FAIZA ALLY KUHUSU MALALAMIKO YAKE JUU YA JESHI LA POLISI

Kama kuna siku nimeamka na maumivu makali ni leo , leo ni siku ambayo natamani ningekua mzungu niishi katika nchi zenye haki za kibinaadamu , maana kuna wkt unahisi unaonewa kwenye nchi yako! Huu ni mwezi wa 3 toka police wachukue simu yangu I phone 7+ yenye thamani ya shilingi M.3 , inaniuma sana , kila wiki naripoti police.

Sasa nimeanza kupewa wiki mbili, mbili, kisa ni picha yangu ya leba wao wana hesabu kama phonographs, juzi nimwaambia nimechoka jamani naombeni sasa nijue kuripoti huku mwisho lini? wanasema hawajui mpaka mwanasheria arudishe Jalada, nimewaomba nimuone mwanasheria wamesema siruhusiwi wao ndio wanatakiwa wafatilie ndio wa nipe majibu, nimwaambia changamoto ninazo pitia kuhusu kukosa simu, kwanza mm nimfanya biashara kwenye mitandao contact zangu zote , mails , number za cm , picha zipo humo napata wakati mgumu kwenye kazi zangu.

Naombeni simu yangu, na kumbukumbu zangu na wanangu muhimu sana zote zipo humu maisha yangu bila hiyo simu ni magumu mno, mm ni mama wa watoto wawili, ugali wangu, ada ya mwanangu , kodi ya nyumba na duka zote nategemea kupitia humu , kiufupi cm yangu ndio maisha yangu jamani naombeni mnirudishie , ndio kwanza nimepewa wiki mbili zingine na sina mategemeo, nikiuliza simu yangu ya nn wanasema wana ichunguza , najiuliza mnaichunguza nini mpaka leo miezi mitatu sielewi, jamani sijawahi kuwa muuza bangi wala Unga wala jambazi au muhujumu wa serekali au mtuhumiwa wa aina yoyote mnaichunguza nini???😭😭😭😭

Nimewaza mpaka nimetamani ningekua na mabwana kama sita hivi mmoja aninunulie simu niendelee na maisha yangu, najitahidi nisimame bila mabwana lkn mwisho wa siku wanawake tukizidiwa hakuna namna ! Sasa hivi sio sawa ni kama mnarudisha juhudi za maisha yangu nyuma ! Naombeni mtoe hukumu yangu nimechoka kuzungushwa, kama mnanipeleka mahakamani nipelekeni, nijue moja .mimi jamani siwezi kuacha au kusamehe simu ya millioni 3 jamani hali ya maisha ni ngumu na lzm niwe na simu yenye viwango kutokana na kazi yangu , sasa nalazimika kulipia camera kwa ajili ya kushuti video ya matangazo ya biashara zangu ktkna na nilio nayo haina uwezo, na lzm kupata garama zaidi SEREKALI NAOMBA MSAMAHA KWA KOSA LANGU , MAISHA YANGU YAMESIMAMA😭

Video: Wema Amtolea Uvivu Zari, Kuhusu Yeye na Diamond

$
0
0
Video: Wema Amtolea Uvivu Zari, Kuhusu Yeye na Diamond

Baada yataarifa zinazozagaa kuwa wema sepetu ndo Chanzo cha Kuachanisha penzi la diamond na Zari Wema afunguka na kukataa tuhuma hizo huku wema akikataa kuwa mshauri wa Zari.



Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images