Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Yanga Hoi Taabani yakubali Kichapo cha 2-1 Nyumbani Kutoka Kwa Wageni

$
0
0
Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers ya Botswana, umemalizika katika Uwanja wa Taifa kwa wenyeji kupoteza kwa jumla ya mabao 2-1.

Katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, Township Rollers ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kwanza mapema kabisa kwenye dakika ya 11 kupitia kwa Lemponye.

Baada ya bao hilo la kuongoza kwa Rollers, Yangan waliendelea kupambana ambapo katika dakika ya 30, mshambuliaji Obrey Chirwa aliweza kufunga bao la kusawazisha, kufuatia kazi nzuri ya Papy Tshishimbi aliyetoa pasi kwake.

Mpaka mwamuzi anapuliza filimbi ya kumaliza kipindi cha kwanza, matokeo yalikuwa ni 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kushambuliana kwa zamu, ambapo nyavu hazikuweza kutikisika mapema, ambapo ilichukua muda mpaka zikasalia dakika 7 zikisalia kuelekea mwishoni mwa mchezo, Sikela akafunga bao la pili kwa Rollers katika dakika ya 83.

Mpaka dakika 80 zinamalizika, Yanga walikuwa nyuma kwa mabao 2-1.

Matokeo hayo yanaipa wakati mgumu Yanga kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa huko Gaborone Botswana, ambapo watabidi washinde mabao zaidi ya mabao mawili kwa sufuri ili waweze kusonga mbele.

Dharau Zingine Huwa Hazina Faida..Ona Huyu Dada Alivyoadhirika

$
0
0

Leo Asubuhi Nikiwa Ubungo bus terminal....
Leo asubuhi nikiwa stand ya mabasi ya ubungo,mdada mmoja wakati anapanda kwenye kagari kake akadondosha simu.Mimi nikamuita ili nimweleze kilichotokea,akanisonya tena msonyo wa dharau sana na nikajuta kumgusa bega kwasababu ya kibao alichonipiga.

Alipoondoa gari nikaiokota hiyo simu na kuondoka zangu,wala sikuizima.


Nafika town simu hiyo ikaita nikapokea kwa shauku ya kujua nani,haya ndo ya kawa maongezi yetu na mpigaji.

Mimi; Hallo habari yako
Yeye; Nzuri
Mimi; nani wewe
Yeye; Mimi ndo mwenye hiyo simu ....
Mimi; Na mimi ndo nilokuita na ukanizaba kibao Pale stand ya ubungo leo na ukanisonya
Yeye; Basi kaka nisamehe naomba unambie ulipo nije tuelewane
Mimi; Nitakwambia baadaye (nikakata simu na kuzima)

Swali nimwambie napatikana wapi au nimpotezee ili liwe fundisho kwake?

Kila Wakati Anataka Nimgegede, Hataki Hata Niende Kazini...Ushauri

$
0
0
Jamani yamenikuta , nililia Mapenzi wakati sina hadi nilikuwa najiona sina bahati ya kupendwa sasa jamani nimepata msichana wa Kitanga ananipenda kufa, Sijui ni kawaida ama la huyu nilie mpata sasa anapenda sana mchezo yaani kila saa anataka tufanye hata ananikataza kwenda kazani mimi ninafanya biashara sasa huwa naenda kusimamia biashara zangu , Binti huyu nimeanza kaa nae nina week ya Pili sasa toka ahamie kwangu huwezi amani sijatoka ndani ananizuia kwa mitego ya khanga moko....Mwee mpaka naona biashara zangu zinadoda....Kweli ndio Mapenzi haya au ?

Njia 7 Za Kuwa Mafanyabiashara Mkubwa

$
0
0
Je unataka kuwa kama MO ??  Fuata hatua hizi 7 utafika alipo MO..

1. Chagua wazo bora la kibiashara.
Wazo bora la kibiashara ndilo litakalo kufanya kuwa mfanyabiashara wa mkubwa. Mara nyingi nimekuwa nikikutana na watu wakisema wanataka kuwa wafanyabiashara na kuishia kusema tu. Ila ukweli ni kwamba katika kuchagua wazo bora la kibiashara ni lazima ujiulize je unataka kuwa mzalishaji wa bidhaa au huduma? Je unataka kuwa mnunuzi na muuzaji?au  je unataka kuwa msambazaji tu ? Hayo yanaweza kuwa miongoni mwa maswali ya msingi ya kujiuliza.

2. Fanya uchunguzi juu ya washindani wako.
Hapa ndipo jicho la tatu linaposhindwa kufanya kazi mara nyingi. Tumekuwa si wachunguzaji wazuri juu ya washindani wetu ila tumekuwa wasikilizaji tu kwa watu wengine juu ya washindani wetu. Ila ikumbukwe ya kwamba fanya uchunguzi wa kutosha ili kujua washindani wako wanatumia mbinu zipi kukuza biashara zao. Hii itakusadia pia kujua ni wapi wanapokosea ili uweze kulizipa pengo hilo. Kwa kufanya hivi kutakufanya ndoto zako za kuwa mfanyabiashara wa kimataifa zitimie.

3. Tafuta mtu wa kukuongoza. (Helpful mental).
Tafuta mtu sahihi wa kukuongoza  na si mtu wa kukukwamisha. Watu wengi tunashindwa kuwa wafanyabishara wakubwa hii ni kutokana tunatafu watu ambao sio sahihi katika kutushauri. Stuka mapema juu ya jambo hili. Na anza kukaa na watu ambao tayari wamefanikiwa kwenye biashara zao watakusaidia sana kufika kule unakotaka kufika kibiashara. Siku zote ukitaka kuruka kama tai, ni lazima ujifunze kama tai wanavyoruka. Kwa maana huyo ukitaka kuwa mfanyabiashara mkubwa kubali kuchukua mwongozo wa wafanyabiashara waliofanikiwa.

4. Tambua biashara inayokua.
 Ukilijua hili ni jambo jema zaidi. Moja ya tatizo kubwa ni kwamba tumekuwa tukishuhudia biashara hazikuwi miaka nenda miaka rudi. Hii ni sababu kubwa ambayo inachangia tusiweze kujua ni kwa jinsi gani tusiwe wafanyabiashara wakubwa. Natamani kuona malengo yako yanabadilishwa kila wakati. Kwa mfano leo unauza nguo kwa kutembeza, ili kuona biashara inakuwa tunataka kuona unapata chumba kwa ajili ya kufanyia biashara hiyo napo kweli tunasema biashara inakua. Kama unafanya biashara mkoa wako mzima tunatamani kuona unaongeza mkoa mwingine na mwingine katika kusambaza huduma au bidhaa.

5. Panga malengo na mipango ya biashara yako.
Hapa inahusiana na juu ya kuuza, kununua bidhaa au huduma. Lazima malengo ya biashara yako uyapange kila robo ya mwaka ili kugundua kama biashara yako inakuwa au haikui. Na lazima pia katika kupanga malengo yako, utambue baada ya muda fulani biashara yako itakuwa imefika wapi. Kwa mfano ni muhimu kujua biashara yako itakapokuwa baada ya miaka miwili au mitatu mbeleni.

6. Tangaza biashara yako.
Wateja wako ni lazima wajue bidhaa na huduma ambayo unazalisha. Si kujua tu, lengo jingine la kutangaza bidhaa au huduma inamfanya mtumiaji aweze kujua jinsi ya kutumia kitu hicho. Kwa kutangaza biashara wateja huongezeka kwa asilimia kubwa sana na kufanya huduma au bidhaa yako kuweza kupendwa na wengi pia. Matangazo ni njia mojawapo bora ya kukufanya kuwa mfanyabiashara wa kimataifa ikiwa utaitumia vizuri.

7. Jenga mahusiano mazuri na wateja wako.
Jitahidi kulizingatia hili ya kwamba Kauli katika biashara ni mali kuliko hata  pesa. Jali wateja wako na kuwafanya wajihisi kama wanapata bidhaa bure. Kwa kadri utakavyozidi kujenga mahusiano bora na wateja hiyo itapelekea wao kupenda bidhaa zako na hiyo itakusaidia kukuza wateja wengi siku hadi siku.

Ni matumaini yangu umenielewa vizuri hizo ni baadhi ya siri chache kati nyingi zitakazokufanya kuwa mfanyabiashara mkubwa. Asante sana na usisite kumshirikisha mwingine.

Install Application ya Udaku Special Kutoka Google Play Kusoma Habari zetu Kirahisi

$
0
0
Install Application ya Udaku Special Kutoka Google Play Kusoma Habari zetu Kirahisi|

DOWNLOAD HAPA

UPDATE HAPA

Au Nenda Play Store and Search "Udaku Special" Kisha Install

Mbunge CCM Ajilipua Kwa Hoja Nane Nzito, Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 7

$
0
0

Mbunge CCM Ajilipua Kwa Hoja Nane Nzito, Soma Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 7


Advertisemen

Lema Amjibu Hussein Bashe "Ni Kweli Tunahitaji Kamati Teule Kuhusu Utekaji ?"

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema amesema kwasasa wanapita katika maumivu makali katika siasa wanazozifanya hivyo hawahitaji kuona sinema tena zikiendelea miongoni mwa wabunge wenzao.

Hiyo inakuja baada ya Mbunge Hussein Bashe kupelekea barua kwa Katibu wa Bunge kutaka iundwe kamati Teule ya kuchunguza baadhi ya mambo yanayoonesha kutishia umoja, usalama na mshikamano wa Taifa.

Lema ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram amehoji kuwa hivi ni kweli inahitajika Kamati teule kuhusu utekaji au kufifia kwa demokrasia nchini?.

==>Nina fikiri ninapaswa kusema kidogo juu ya hoja binafsi ya Mh Husein Bashe katika mkutano wa Bunge unaokuja.Hivi ni kweli tunahitaji Kamati teule kuhusu utekaji na kufifia kwa demokrasia Nchini ?

Ni maamuzi ya ccm ktk mikutano yao ya ndani ya Bunge na nje ya Bunge kuhusu hali ya demokrasia na siasa Nchini, ujenzi wa vyama vya siasa na mikutano imepigwa marufuku .

Mikutano ya Bunge live pia imepigwa marufuku , Wabunge na Madiwani wa Upinzani waneendelea kupitia mateso makubwa,vitisho vya mauaji , kuwekwa mahabusu na kufungwa.

 Wakati mambo haya yanaendelea kutokea Bunge limekataa hata kulipa matibabu ya Mh Lissu.
 Hakuna Mbunge mmoja wa ccm akiwemo Husein Bashe alishawahi kwenda kumjulia hali Mh Lissu Hospital, unajiuliza ni kwa nini ?

 Mambo haya yako wazi hayahitaji PHD kujua msimamo wa Wabunge wa ccm kuhusu haki,ukweli na nuru ya mabadiliko .
 Wabunge wa ccm wakibadili mtazamo kuhusu Nchi Bunge litakuwa imara na Bunge imara ndio msingi wa Serikali bora na Bunge imara linatokana na Wabunge majasiri, wako wapi ndani ya ccm ?
 Msingi wa kwanza wa ukomavu wenu ni kurudisha hadhi ya Bunge kwa umoja na idadi yenu , platform nyingine nje ya kujitathimini kwa masilahi ya Nchi ni unafiki.
Bashe unafikiri Kamati teule inaweza kuwa na maana kwenye Bunge hili ? hotuba za Wapinzani Bungeni zime endelea kuwa sensored ndani ya Bunge na haya ni maoni mbadala ya ushauri kwa Serikali lakini siku zote mmekaa kimya.

Chama chako ni tatizo na Viongozi wake,na wewe unafahamu mambo haya, hivi kweli tunahitaji tena kugundua kanuni ya kutengeneza gari wakati kuna magari yana tembea barabarani ?
 Tunahitaji umoja wenu kwa masilahi ya haki ndani ya Bunge kwenye mambo yote yanayo rudisha heshima ya Wabunge , wingi wenu umekuwa hasara kwa Nchi badala ya faraja.

Tunapoona maigizo yanayotaka kupotosha haki yanazingatiwa hapa ndipo tunapatwa hasira na kuondoa nidhamu katika mahusiano yasiyo na tija na Nchi , hata hivyo andiko hili sio ugomvi lakini pia limejengwa hasira na hali zetu kisiasa tunayopitia, sisi Wabunge wa upinzani karibu wote tuna kesi sehemu mbali mbali Nchini, mmoja wetu sasa ni mfungwa (Sugu) .

Tunapitia maumivu makali sana kwa sasa hatuitaji tena sinema.

Idadi ya Watanzania Ambao Huambukizwa Virus vya Ukimwi Kwa Siku

$
0
0

Takwimu zinaonesha kuwa Watanzania 225 huambukizwa Virusi Vya Ukimwi (VVU) kila siku, hiyo ikimaanisha kwamba kwa mwezi watu 6,750 huambukizwa VVU na kwa mwaka ni watu 82,125.

Takwimu hizi zimebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko leo Jumanne Machi 6, wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu uandaaji wa programu bora za Virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI.

Dk. Maboko amesema kuwa, asilimia 40 ya maambukizo mapya hutokea kwa vijana wenye umri Kati ya miaka 15 hadi 24 na kati yao wengi ni wanawake.

Hii inamaanisha kwamba katika hiyo asilimia 40 ya vijana waliopata maambukizi mapya, asilimia 80 ni wanawake, amesema Dk. Maboko.

Comments

Alichosema Dogo Janja kwa Wenye ‘Mazoea na Mke Wake

$
0
0
Msanii wa Bongofleva Dogo Janja amepost picha akiwa na mkewe Irene Uwoya katika ukurasa wake wa Instagram na kumsifia mkewe kwa kuandika Caption ambayo mwihsoni kamalizia na hashtag za kumsifia na kukataa mazoea kwa mkewe.

Dogo Janja ameandika hivi….
Ni bora umwage damu mbele ya adui yako kuliko kumwaga chozi… #MyBeautifulWife ❤️ #AtadondokaMtu#MazoeaNaMkeWangu” – Dogo Janja

Pamoja na Dogo Janja kupost na kuandika hivyo mkewe Irene Uwoya na yeye al-comment chini kwa kuandika….
“Unamkwara baba….ila usiue Utaenda Jela” – Irene Uwoya

Shaffih Dauda baada ya Yanga kupoteza mechi ya kimataifa nyumbani

$
0
0
Kumekuwa na maoni mengi na mitazamo tofauti baada ya mechi ya Caf Champions League kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers mchezo ambao umeshuhudia yanga ikipoteza nyumbani kwenye uwanja wa taifa kwa kufungwa 2-0 ikiwa ni mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza.

Wengi wao wametoa maoni kwa kuangalia matokeo ya uwanjani kwa upande wa Shaffih Dauda pia ametoa maoni yake kwa kueleza sababu kadhaa za Yanga kupoteza mechi hiyo lakini amegusia mambo mengi ikiwemo ubora wa ligi, maandalizi pamoja na vitu vingine

Wakati mwingine matokeo kama haya yanatupa mtazamo mpana wa kuangalia mambo mengine ambayo sisi tunayafanya na kuridhika nayo kutokana na mazingira ya kwetu na tunaona tupo sawa labda kutokana na mazoea.

Kwenye mechi kama hizi ili uweze kufanya vyema, ni lazima yawepo maandalizi yanayotokana na mamo mengi, kuna maandalizi ya makocha na benchi la ufundi kufanya kazi yao ya kumtambua mpinzani wanaekutana naye, hilo ni jambo la kwanza lakini wawe wanapata support kutokana na mfumo wa ligi yao na nchi yao kwa ujumla.

Yaani mpango wa maendeleo ya mpira kitaifa katika nchi yao, mamlaka husika wametekeleza majukumu yao kwa kiasi gani? Ukija kwenye ligi yao ‘Botswana’ inaendeshwa kwa utaratibu upi? Level ya ushindani kwenye ligi yao ipoje? Performance na viwango vya wachezaji kutoka katika timu tofautitofauti upoje?

Vitu vyote hivyo ni matokeo ya wadau wengi kwa maana ya vilabu vyenyewe vinamajukumu yake kuhakikisha wanaandaa mifumo mizurikutengeneza klabu zao, mamlaka zingine kwa mfano zinazosimamia ligi jukumu lao ni kuhakikisha ligi inakuwa ya ushindani ambayo itatoa bingwa ambaye atakwenda kushindana na mabingwa kutoka kwenye mataifa mengine na akawawakilishe vyema kuonesha ni namna gani ligi yao ilivyo bora na kwenda kuitangaza. Sasa kwetu, vitu vyote hivyo huwa hatuvipi kipaumbele huwa ‘tunajifanyiafanyia’.

Kilichobadilisha matokeo kwenye mechi ya Yanga na Township Rollers ni level ya performance, wenzetu level yao ilikuwa juu ukilingabisha na performance ya Yanga, Yanga walikuwa kama asilimia 50 ukilinganisha na wale Township Rollers kuanzia mchezaji mmojammoja kuja kwenye timu nzima. Naona baadhi ya watu wanazungumzia mchezaji mmojammoja kama vile Kessy, Tshishimbi, Chirwa, Yondani, lakini timu ndiyo inakupa matokeo.

Kwa mfano Kessy anafahamika kwa style yake ya uchezaji, ni ‘wing back’ anayekimbia pembeni, lakini ili upate kilicho bora kutoka kwake lazima apate ‘connection’ ya wenzake ambao wapo maeneo mengine watekeleze majukumu yao ili yeye anapokimbia na kupiga pasi ndani na anapokimbia kwenye mstari wa pembeni akutane na mpira kwenye nafasi aweze kupiga pasi ya mwisho wakati huo mshambuliaji awe amefika eneo la kufunga.

Wale Township Rollers kuanzia kwenye eneo lao la ulinzi walikuwa bora na walikuwa wanajua nawafanya kitu gani na ili waweze kutekeleza mipango aliyoizungumzia mwalimu, jambo la kwanza ni lazima wawe fit. Level ya fitness ya wachezaji wa Yanga unaweza kuiona iko chini ukilinganisha na wachezaji wa Rollers hata ukiangalia walivyokuwa wakigombea mipira ‘one against one’ walikuwa wanafanikiwa zaidi kuliko wachezaji wa Yanga. Walipokuwa wana mpira kwenye himaya zao hakuna mchezaji wa Yanga aliyekuwana uwezo wa kuuchukua.

Ukiangalia goli la pili, issue sio pasi kwa sababu unaweza ukapiga pasi hata 100 lakini upo kwenye eneo lako ambalo halimpi presha mpinzani ‘less pressure area’ mpinzani wako atakuwa anakuangalia tu unavyojifurahisha lakini unapovuka kwenda kwenye eneo la mpinzani ukiwa uanaendelea kupiga pasi maana yake wapinzani watatakiwa kuwa fit kwa kiasi kikubwa kwa sababu watatakiwa kukimbia sana kuziba ma-gape na kukaba ili kuuchukua mpira na nyinyi mcheze kwenda kwao.

Hizi Hapa Aina Mbali Mbali za Hasira za Mwanamke...Tahadhari

$
0
0

1. Kuna mwanamke ambaye akikasirika, huishia kulia tuu!

2. Lakini mwingine akichukia, anaongea saanaa muda wote hadi ikukere!

3. Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. Shavu limejaa kama Kobra!

4. Mwingine akishikwa na hasira, period ya ghafla ghafla inafuata!

5. Wako wanawake ambao, ole achukie! Atakachokishika usipokimbie anakutandika nacho, majuto baadaye! Baba mmoja alipigwa 'Pedi' ilotumika, kufuatia kung'ang'ania tendo, huku mwenzi wake yuko katika hali hiyo!

6. Mwanamke mwingine akikasirika, hasira zake zinaishia kwenye kuvunja-vunja vyombo. Au saa nyingine kugombeza-gombeza wafanyakazi na watoto! Dizaini hii, huwa ni wale waliokosa kukidhiwa haja za kihisia na waume zao!

7. Mwanamke mwingine ole akasirike. Mtajuana kitandani panapo majaaliwa! Nakwambia utaungama yote!

8. Kuna ambao wakitibuliwa, hukimbilia kufunga mabegi na kuondoka!

9. Wapo ambao wakikasirika, wanagoma kupika!

10. Wengine wakichukia, wanaamua kwenda kulala kimyaaa!!

11. Wanawake wengine wakikasirika, tumbo linakata, na pengine mpaka kuharisha!

13. Wako ambao wakishikwa na hasira, huingia maombi na kuugua kusikoweza kutamkwa. Uchungu ukiisha, wananawa uso na kwenda sokoni.

14. Yuko ambaye akishikwa na hasira, hucheka saaanaaa.... Hutajua kama amekasirika! Dizaini hii ni hatari sana, maana anaweza kukudhuru kiurahisi.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo

$
0
0

Masikini! Kumbe Mimba ya Shamsa Ford Imechoropoka

$
0
0
Masikini! Kumbe  Mimba ya Shamsa Ford Imechoropoka
KUMEKUWA na matukio mbalimbali yanayowakusanya wasanii, lakini tofauti na zamani, Shamsa Ford kwa sasa amekuwa haonekani akijichanganya na wenzake, jambo ambalo limezua minong’ono na kusababisha mwenyewe kuibuka na kudai kuwa jambo hilo lilisababisha mimba yake changa ikachoropoka.

Shamsa aliiambia Za Motomoto News kuwa, awali alikuwa akijichanganya mno kwenye ishu tofauti, lakini kwa sasa anashindwa kutokana na kupigwa marufuku na mumewe, Chid Mapenzi, baada ya kuwa na ujauzito mchanga ambao ulichoropoka kwa sababu ya kuzurura.

“Nilipigwa marufuku kutokatoka licha ya kwamba mwanzoni nilikuwa ninatoka kibishibishi tu, lakini kwa sasa imenibidi nimsikilize mume wangu zaidi maana mimba changa ilitoka kwa sababu ya kutokatoka hovyo kwenda kwenye shughuli,” alisema Shamsa.

Jeshi la Polisi Lakanusha Kupatikana kwa Masheikh Watatu Waliotoweka Zanzibar

$
0
0
Jeshi la Polisi Lakanusha Kupatikana kwa Masheikh Watatu Waliotoweka Zanzibar

Jeshi la Polisi Zanzibar limesema kuwa halina taarifa za kuonekana kwa mashekhe watatu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, ambao waliripotiwa kutoonekana tangu Januari 9, mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa jeshi hilo lilifanya kazi ya kuwatafuta mashekhe hao, lakini halikufanikiwa kuwaona.

“Zipo taarifa mitaani kuwa mashekhe hao wameonekana sasa nashangaa kwanini waliokuja kuripoti kuwa hawaonekani wameshindwa kuja kutoa taarifa kuwa wameonekana,” amesema Kamanda Ali

Aidha, Kamanda huyo ameiasa jamii kuacha kuchanganya mambo ya kihalifu na kisiasa kwa kuwa halileti taswira nzuri kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, Kamanda Ali ameongeza kuwa awali jeshi hilo lilipokea taarifa rasmi kutoka kwa familia na ndugu wa mashekhe hao, kuwa hawaonekani na wamepotea katika mazingira ya kutatanisha huku likihusishwa jeshi hilo kuwa ndio lililo wachukua

Ndoa ya Usher Raymond na Mkewe Grace Miguel Yavunjika Baada ya Wawili Hao Kuachana

$
0
0
Ndoa ya Usher Raymond na Mkewe Grace Miguel Yavunjika Baada ya Wawili Hao Kuachana
Mwaka 2018 umeonekana kuwa ni mbaya kwa wapendanao. Usher Raymond na mkewe Grace Miguel wametangaza kuachana baada ya kupita miaka miwili ya ndoa yao na kudumu kwenye mahusiano kwa miaka 10.

Kwa mujibu wa mtandao wa Us Weekly umetoa taarifa ya wawili hao ya kuachana inayosomeka, “Baada ya kufikiria sana na kuzingatia tumeamua kujitenga kama wanandoa.”

“Tunaendelea kushirikiana kwa ukaribu zaidi, marafiki wa upendo ambao wataendelea kuunga mkono kwa njia nyingine ya maisha yetu. Kiasi kikubwa cha upendo na heshima tuliyo nayo kwa kila mmoja itaongezeka tu tunapoendelea,” imeongeza taarifa hiyo.

Hata hivyo Chanzo cha karibu cha wawili hao kimeuambia mtandao huo, Usher na Grace wametengana tangu miezi michache iliyopita.

Usher na Grace wamekuwa na mahusiano kwa karibu tangu mwkaa 2009 baada ya msanii huyo kuachana na aliyekuwa mke wake, Tameka Foster ambaye walifanikiwa kupata watoto wawili kwenye ndoa yao iliyodumu kwa miaka miwili.

Hiki Hapa Kikosi Cha Simba Kitakachovaana na Al Masry ya Misri Leo

$
0
0
Hiki Hapa Kikosi Cha Simba Kitakachovaana Al Masry ya Misri Leo
KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre, tayari ameshakipanga kikosi chake ambacho kitaanza leo Jumatano kwenye mchezo wao dhidi ya Al Masry ya Misri, huku akiwapa jukumu zito la kufunga mabao washambuliaji wake, Emmanuel Okwi na John Bocco.

Mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa ni wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika na utaanza majira ya saa 12 jioni, ingawa Lechantre hakufura­hishwa na muda huo uliopangwa na viongozi.

Katika mazoezi ya juzi Jumatatu yaliyoanza majira ya saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Boko uliopo jijini Dar, Championi lilimshuhudia Lechantre akipanga kikosi chake kilichoonekana ndicho cha maan­gamizi ambacho kitatumika kum­maliza Mwarabu leo.

Katika kikosi hicho ambacho golini yupo Aishi Manula, walinzi wake ni Shomary Kapombe, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Yusuf Mlipili na James Kotei.

Kwenye kiungo wapo; Jonas Mkude, Nicholaus Gyan, Shiza Kichuya, Bocco na Okwi. Katika ma­zoezi hayo yaliyomalizika saa 1:30 usiku, kocha huyo alikuwa makini zaidi kwenye kushambulia kupitia pembeni.

Aliwapa wachezaji wake haswa wa pembeni namna ya kusham­bulia kwa kasi na kupiga krosi za maana ikiwemo kupiga pasi za mi­pira mirefu huku akiwaeleza kuwa mara nyingi Waarabu hawana kasi lakini wana uhakika na wanachoki­fanya.

Akiwazungumzia wapinzani wao hao, Lechantre alisema: “Tunak­wenda kukutana na moja kati ya timu bora Afrika ambayo inashiriki ligi bora, timu za Misri ni imara, kikweli Al Masry ni timu nzuri na tunaiheshimu.”

“Sitabadilisha mfumo, nitakuwa na washambuliaji wangu wawili, Bocco na Okwi, kwenye kiungo tutaangalia itakavyokuwa pengine nitakuja na ‘sapraizi’ baab kubwa, njooni mkaone.”

Makipa wafanya mazoezi kwa saa matatu
Katika hali ambayo haikutara­jiwa, kabla ya kuanza kwa maz­oezi hayo ya jumla, Championi liliwashuhudia makipa wanne wa kikosi hicho wakianza mazoezi mapema tu kuanzia saa 10:30 jioni wakisimamiwa na kocha wao, Muharami Mohammed.



Makipa hao ni Aishi Manula, Said Mohammed ‘Nduda’, Emmanuel Mseja na Ally Salim, walipoanza muda huo, walikuja kumaliza saa 1:30 sawa na wenzao. ambapo jumla walifanya mazoezi kwa muda wa saa tatu tofauti na siku zote.

Huu Hapa Ujumbe wa Neymar Baada ya Timu Yake Kutolewa Kwenye Mashindano

$
0
0
Huu Hapa Ujumbe wa Neymar Baada ya  Timu Yake Kutolewa Kwenye Mashindano
Nyota wa klabu ya Paris Saint-Germain Neymar Jr ameeleza masikitiko yake baada ya kukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid huku akishuhudia timu yake ikitupwa nje ya mashindano.


Neymar ambaye amefanyiwa upasuaji wa mguu wake wa kulia alikuwa nyumbani kwao Brazil akifuatilia mchezo huo ambapo PSG imekubali kichapo cha mabao 2-1 usiku wa kuamkia leo wakiwa nyumbani kwao Parc des Princess.

Baada ya mchezo Neymar alitumia ukurasa wake wa Twitter kueleza hisia zake ambapo ameandika ''Nina huzuni tumeshindwa na huzuni zaidi sikuwa uwanjani kujaribu kuisaidia timu yangu''.



Hata hivyo Neymar aliwapongeza wachezaji wenzake kwa jitihada walioonesha kwenye mchezo huo ambao mabao mawili ya Cristiano Ronaldo na Casemiro yalitosha kuipeleka Real Madrid Robo fainali kwa jumla ya ushindi wa mabao 5-2.

Katika mchezo wa jana bao la PSG lilifungwa na Endison Cavan huku vinara hao wa Ligue 1, wakimaliza 10 uwanjani baada ya kiungo wao Marco Verratti kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 66

Serikali Yapiga Marufuku Kondomu

$
0
0
Serikali Yapiga Marufuku  Kondomu
Serikali imetoa onyo kwa taasisi zisizo za Serikali kuacha kupandikiza vitanzi na kuwagawia kondomu wanafunzi shuleni kwani wanahamasisha ngono kwa umri mdogo.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 6 na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mery Tesha wakati wa maonyesho ya siku mbili ya wanawake katika viwanja vya Ghandh All.

Tesha amesema Serikali imebaini baadhi ya mashirika na taasisi zisizo za Serikali zinazunguka na kutoa huduma hizo shuleni.

“Wanafunzi hawa tuwalee katika maadili mema yanayostahili badala ya kuwapatia kondomu na vitu vingine vinavyohamasisha kufanya ngono, jambo hili halikubaliki hata kidogo,” amesema Tesha.

Mwananfunzi anayetarajia kujiunga kidato cha tano Sada Jabiri ameiomba Serikali kuifuta sheria ya mwaka 1971 ambayo inamruhusu mtoto kuolewa akiwa na miaka kuanzia 15.

“Ili kumjengea mtoto haki ya kujitambua na kutoa uamuzi sahihi ni vyema sheria ingesema hata ianzie miaka 21 ambapo mtoto anakuwa ana ufahamu mkubwa,” amesema Sada.

Mwenyekiti wa baraza la watoto Mkoa wa Mwanza, Neema Theonest alisema katika hali hii ya kuelekea uchumi wa viwanda ifikapo 2025 ni vyema kuimarisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake vijijini.

Neema amewataka wanawake waache kubweteka badala yake wajitume kufanya kazi ili kupandisha uchumi kuanzia ngazi ya familia na kutokomeza umasikini.

Akisoma risala kwa niaba ya wanawake wa Nyamagana, Grace Saiti aliiomba Serikali iendelee kutoa fursa nyingi za ajira kwa wanawake na kuwapatia nyadhifa mbalimbali kwani wanawake wana uwezo wa kuongoza na kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Pia amesema  elimu ya masuala ya uzalishaji na uanzishaji wa viwanda ifanyike zaidi kwenye maeneo yote ili mwanamke hata wa kijijini afikiwe na aweze kujiendeleza.

Wadaiwa Sugu Benki ya Wanawake Tanzania Wapewa Siku Saba

$
0
0
Wadaiwa Sugu Benki ya Wanawake Tanzania Wapewa Siku Saba

Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) imetangaza kuzipiga mnada mali za wadaiwa sugu 7,065 watakaoshindwa kulipa madeni yao ndani ya siku saba kuanzia jana.

Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo, Beng’i Issa alisema jana  Machi 6 kwamba  uamuzi huo ni sehemu ya kukabiliana na ongezeko la mikopo chechefu au isiyolipika iliayo.

“Mpaka sasa mikopo isiyolipika imefia Sh7.9 bilioni hivyo kuongeza ugumu kidogo katika kuhakikisha tunapata mtaji wa kutosha,” alisema Issa.

Ndani ya muda walioutoa, alisema wateja wanaodaiwa wanapaswa kulipa madeni yao ambayo ni ya muda mrefu.

“Wengi wameshapitiliza siku 90 za kutorejesha madeni yao kinyume na utaratibu na makubaliano na benki,” alisema

Kwa watakaoshindwa kulipa fedha hizo ndani ya muda uliotolewa wa benki kuchukua hatua za kisheria kabla ya kunadisha dhamana zao, amesema wenye dhamira ya kulipa waende kwenye tawi lolote la benki hiyo wakiwa na mpango mahususi wa jinsi watakavyofanikisha malipo yao.

Januari 4, wakati Benki Kuu Tanzania (BoT) inatangaza kufuta leseni za baadhi ya benki nchini, TWB ilipewa agizo la kuongeza mtaji ndani ya miezi sita ili kukidhi mahitaji ya ukwasi unaohitajika.

Kulingana na masharti ya taasisi za fedha na benki za biashara nchini, kila moja inatakiwa kuwa na mtaji na ukwasi wa kutosha kukidhi mahitaji ya kila siku.

Wakati TWB ikipewa onyo hilo, benki za Covenant, Efatha, Benki ya Wananchi Njombe, Kagera Farmer’s Cooperative Bank na Benki ya Wananchi Meru zilifutiwa leseni.

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania, Japhet Justine amesema  sheria inawaruhusu kuuza mali au dhamana za wateja walizoweka endapo watashindwa kurejesha mkopo kwa wakati waliokubaliana.

“Mbali na kupiga mnada mali zao, taarifa zao tutazipeleka Benki Kuu ya Tanzania wasiweze kupata mkopo katika benki nyingine yoyote nchini,” alisema Justine.

Alisema tangu kutolewa kwa taarifa ya awali kuwa benki ipo katika hali mbaya, wamekusanya zaidi ya Sh2 bilioni kutoka kwa wadaiwa walionao, hatua ambayo alisema ni nzuri.

Kwa sasa, alisema wapo katika maongezi na wadau mbalimbali kuwawezesha kupata mtaji waliowekewa na Benki Kuu na kwamba mwelekeo unaonekana kuwa mzuri.

“Baada ya benki yetu kupewa maagizo ya kuongeza mtaji na Benki Kuu tunapokea wateja na wageni wengi wanaohitaji ufafanuzi kuhusu fedha zao lakini wote wanaelewa,” aliongeza.

Edu Boy Amtolea Maneno Mazito Nay wa Mitego "Hajui Kumridhisha Mwanamke Kwenye Mapenzi Ndomana Nimemchukua Demu Wake"

$
0
0
Edu Boy Amponda Nay wa Mitego  "Hajui Kumridhisha Mwanamke Kwenye Mapenzi Ndomana Nimemchukua Demu Wake"
Msanii wa Hip Hop anayewakilisha Jiji la Mwanza, Edu Boy amefunguka na kujisifu kuwa amempokonya Nay wa Mitego anayedaiwa kwamba ni mpenzi wake Nini kutokana na kushindwa kumridhisha katika masuala mbalimbali.


Edu Boy amebainisha hayo wakati alipokuwa anapiga stori na Big Chawa kwenye kipindi cha Planet Bongo 'PB' kinachorushwa na East Africa Radio kuanzia saa 7:00 mchana hadi 10:00 alasiri Jumamatu hadi Ijumaa.

"Ujue mimi ni mtoto wa kisukuma nakula vizuri, kwa hiyo najua namna ya kumridhisha mwanamke pindi tunapokuwa katika tendo kwa sababu tunanguvu za kutosha. Kumpora mtu mpenzi wake ni jambo la kawaida",amesema Edu Boy. 
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images