Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Diamond Platnumz Amvaaa na Kumjibu Waziri Shonza Kwa Mara nyingine

$
0
0

Diamond Platnumz Amvaaa na Kumjibu Waziri Shonza Kwa Mara nyingine kupitia Mtandao wa Twitter ..Vita Hii ni Balaaa

Massage za Wadada Saluni Zinatutega na Tunashawishika

$
0
0
MASSAGE katika saloon ni mtindo wa kusugusugua mwili kwa kuupaka kwanza na dawa maalumu ili kuondoa uchafu na kuufanya mwili uwe safi,pale pale MASK nayo hupakwa usoni kwa lengo la kuinadhifisha sura.

TATIZO SIYO MASSAGE AMA MASK,
tatizo ni hao wadada kwanza WANAVAA NGUO ZA KUTEGA NA WAKATI MWINGINE ni wazuri sana, mbaya zaidi wakianza kukusuguasugua, mara waguse masikioni tena taraatibu hadi stimu zinapanda na unafumba macho na kausingizi kwa mbali kanasogea.

JAMANI MNATUTEGA na mwisho tunashawishika na tunaamua KUWAOMBA moja kwa moja.

Pamoja na Umaarufu Alionao Wema Sepetu Kwanini Hana Maendeleo Yoyote, Anakwama Wapi?

$
0
0
Pamoja na umaarufu alionao wema , ni wapi alipokwama hadi anashindwa kuwa na maendeleo?., Amekosa washauri au tatizo ni nini

Baadhi ya watu wanadai kuwa wema ameshindwa kutumia umaarufu wake kujitajirisha, wengine wanadai kuwa Wema amekuwa akitumika kwa maslahi ya watu wengine bila kujitambua, wakitolea mfano Wcb jinsi wanavyo mtumiaga kwa ajili ya maslahi yao na kumtema

Wema amebahatika kuwa na watu milioni 3.4 wanaomfollow instagram lakini ameshindwa kutumia hiyo nafasi kujitangaza kibiashara kama wanavyofanya wenzie akina Wolper, Esma, Aunt Ezekiel

Wema hadi now hana hata kibanda cha mbao alichojenga, tofauti na umaarufu anaojipa, maisha yake yamekuwa ni ya maigizo kila kukicha

Anakwama wapi , ili tumshauri?

By Mtotomtamuu/JF

Sikiliza Sauti ya Naibu Waziri Juliana Shonza Akimjibu Diamond Platnumz, Ingiwa Alisema Hawezi Mjibu

$
0
0

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, amesema amesikia malalamiko ya mwanamuziki Diamond lakini hawezi kumjibu kwa sababu zipo taratibu za kufuata kama anaona hajatendewa haki.

Shonza analijibu hilo ikiwa ni siku moja tangu mwanamuziki 'Diamond' amtaje waziri huyo katika malalamiko yake, akidai amekuwa akikurupuka na kutolea mfano wa kufungia nyimbo na wasanii wakati akihojiwa na kituo cha redio cha Times.

Waziri huyo amesema hayupo tayari kumjibu Diamond ingawa wasanii wanapaswa kuelewa kuwa hakuna aliye juu ya sheria hata kama msanii mkubwa namna gani.


Msikilize Sauti Hapa Chini:

Wema Sepetu, Zari Hapatoshi Mitandaoni, Maua Yazua Gumzo Balaa

$
0
0

WEMA SEPETU NA ZARI THE BOSS LADY KUMEKUCHA,HAPATOSHI,DJ WA DIAMOND JORMY JONES AFANYA YAKE
Wema, Zari Hapatoshi Mitandaoni, Maua Yazua Gumzo Balaa! Siku chache baada ya mzazi mwenza wa Mbongo Fleva, Diamond Platnumz, Mwanamama Zari The Boss Lady, kupost picha ya ua jeusi katika ukurasa wake wa Instagram, akiashiria kupigana kibuti na mzazi mwenziye huyo.

Queen wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, ambaye hivi karibuni ameibua minongo’no kuwa amerudiana na x- wake ambaye ni mzazi mwenza wa Zari, Diamond, ambapo leo amewashangaza mashabiki mitandaoni kwa kuposti picha ya Ua jekundu kwenye ukurasa wake wa Instagram, linaloashiria Mapenzi ya dhati, na kuwaachama mashabiki njia panda wasijue kuwa ua hilo ni kijembe cha kumuonyeshea Zari kuwa ni kweli amerudiana na mbongo Fleva huyo au lah!

Baada ya posti hiyo ya Wema, .mashabiki wamekuwa na maoni tofauti tofauti, huku wengine wakidai hakutakiwa kupost ua hilo, wengine wamempongeza na kuonyesha kutamani kuona wawili hao wakirudiana....

Mchungaji Awalambisha Viatu Waumini Wake Ili Wapate Baraka za Miujiza

$
0
0
Mchungaji mmoja kutoka Nigeria (39), Andrew Ejimadu wa kanisa la Christ Freedom Ministries amezua gumzo mtandaoni baada ya ku-post picha zake katika mtandao wa Facebook wakati wa kuabudu mitandaoni.

Nabii huyo ameshangaza maelfu ya watu baada ya kuonyesha picha za waumini wa kanisa lake wakibusu na kulamba viatu vyake akidai kuwa kwa kufanya hivyo watapata baraka na miujiza.

Nabii huyo aliweka picha hizo katika ukurasa wake na kuandika.“Nimebariki miguu yako, nimeosha nyayo zako.”

“Kitu cha kwanza kesho asubuhi, ikiwa utaandika Amen na ushirikishe ujumbe huu, kuna mtu atakupigia simu na miguu yako itakubeba hadi huko kuchukua zawadi maalum. Watu wengi watakosa hilo, jaribu,” Andrew Ejimadu.

Mwaka 2016, Mchungaji Ejimadu alipamba vichwa vya habari na kushikiliwa na polisi nchini Zambia yeye na kaka yake, Cleopasa Ejimadu kwa kosa la kumbaka binti mdogo mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikwenda kwenye makazi yao kwa ajili ya uponyaji na kupata ushauri wa kiroho.


Mpekuzi

Mmiliki wa Facebook Kikaangoni....Aitwa Rasmi na Bunge Kujitetea

$
0
0
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa mtandao maarufu wa Facebook Mark Zuckerberg ameitwa kwa barua rasmi na Kamati ya Bunge la nchini Uingereza ili kutoa ushahidi kuhusu kutumia data binafsi za watumiaji wa Facebook kupitia Cambridge Analytica.

Cambridge Analytica  ni kampuni ambayo iko nchini Uingereza ambayo inatuhumiwa kutumia taarifa za wanachama Milioni 50 ili kuweka ushawishi katika Uchaguzi Mkuu wa Urais nchini Marekani uliofanyika mwaka 2016.

Kampuni ya Facebook inatuhumiwa kwa kosa la kushindwa kuwapa taarifa watumiaji wa mtandao huo kuwa, taarifa zao zinaweza kuwa zilipatikana na kutunzwa na kampuni hiyo ya Cambridge Analytica, kampuni ambayo inasemekana kumsaidia Donald Trump kushinda Urais 2016 Marekani.

Hatahivyo Facebook imeeleza kuwa iliifungia kampuni hiyo kupata taarifa za mtandao huo, japokuwa iliweza kupata taarifa hizo kwa njia za udanganyifu na kuvunja sera za mtandao huo.

Serikali Yafunguka Kushambuliwa Afisa wa Ubalozi wa Syria Tanzania

$
0
0
Baada ya kuwepo kwa taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu kushambuliwa kwa afisa wa ubalozi wa Syria nchini Tanzania na watu watatu wasiojulikana na kupigwa ikiwa pamoja na kuporwa pesa, simu na gari aliyokuwa akiitumia kwa shughuli za ubalozi.


Kufuatia taarifa hizo Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abasi amefunguka na kukiri kupata taarifa hizo na kudai kuwa serikali inafuatilia suala hilo na itatoa taarifa kamili kuhusu jambo hilo.

"Umma unaarifiwa kuwa vyombo vya dola vinafuatilia taarifa za Afisa Ubalozi wa Syria nchini kushambuliwa, kuporwa. Taarifa kamili itatolewa" alisema Abasi 

Aidha katika taarifa za awali zinadai kuwa afisa huyo amelazwa katika hospitali ya Agha Khan akipatiwa matibabu kufuatia shambulio hilo


Mtoto Aliyezaliwa na Miguu 3 Afanyiwa Upasuaji na Kuondolewa Mguu Mmoja

$
0
0
Mtoto wa mdogo wa miezi 10 kutoka China ambaye alizaliwa na miguu mitatu umefanyiwa upasuaji wa masaa kumi na kuondolewa mguu mmoja. Madaktari nchini China wamefanikiwa kuutoa mguu huo watatu na sasa amebakiwa na miguu miwili kama binadamu wengine.

Madaktari waliomfanyia upasuaji wamesema kujitokeza kwa mguu wa tatu kwa mtoto huyo ilikuwa changamoto ya kiafya iliyotokea wakati akiwa tumboni mwa mama yake.

Kocha Jose Mourinho Ambiwa Amepitwa na Wakati si Kitu si Lolote Katika Ufundishaji wa Soka

$
0
0
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anaonekana kupitwa na wakati na tabia zake zimebadilika , kulingana na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Chris Sutton.

Mourinho amekosolewa na baadhji ya mashabiki wa United pamoja na wachanganuzi wa kandanda kwa mtindo wake wa kucheza kandanda unaoonekana kutokuwa na mbinu mpya.

United iko katika nafasi ya pili katika ligi ya Uingereza na wako katika nusu fainali katika kombe la FA lakini walibanduliwa katika kombe la vilabu bingwa wiki iliopita.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright aliambia BBC Radio 5 live asingependelea kucheza chini ya Mourinho hivi sasa.

United wako pointi 16 nyuma ya Manchester City katika ligi huku kukiwa imesalia mechi nane na itachuana na Tottenham mwezi ujao ili kufika fainali ya kombe la FA.

Lakini huku City ikiwa imefanikiwa kufunga mabao 85 katika ligi ya Uingereza msimu huu , United imefunga mabao 58 pekee, ikiwa ndio machache zaidi miongoni mwa timu nne bora katika ligi hiyo kulingana na jedwali.

Red Devils walibanduliwa katika kombe la Ulaya na Sevilla, walioshinda 2-1 katika uwanja wa Old Trafford huku City na Liverpool zikisonga mbele katika robo fainali.

Sutton akizumnguza siku ya Jumatatu alisema: Mourinho amebadilika yeye binafsi kutoka alivyokuwa 2004. Anaangazia maswala madogo ya kijinga. Je ni janga kwa Man United kwa sasa? Hapana.

Lakini hilo ndio lililokuwa lengo la Mourinho kuja Man United na kumaliza nyuma ya City na kutokuwa na ari ya kuwania mataji makubwa? amepitwa na wakati.

Anaangalia City na mtindo wa soka wao na Liverpool .Huyu ni mtu ambaye alisajiliwa na Man United kwa kuwa alikuwa anaonekana kuwa na kipaji , Sasa anaonekana amepitwa na wakati kutokana na mtindo wa mchezo wake na vile timu nyengine zinavyocheza.

Mourinho mwenye umri wa miaka 55 alishinda ligi ya Uingereza mara tatu , mara mbili akiwa mkufunzi wa Chelsea.

Alimrithi Louis van Gaal kama mkufunzi wa United mnamo mwezi Mei 2016 na ameshinda kombe la EFL pamoja na lile la Yuropa katika msimu wake wa kwanza .

Wright anamlaumu mkufunzi huyo kwa kuleta kiza katika klabu hiyo .

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Uingereza alisema: Sijui amefanywa nini. Klabu hiyo ilimleta Mourino ili kuleta ubora ,ametumia fedha nyingi lakini anazozana na kila mtu.

Manchester City inacheza mtindo wa kandanda ambao ni mzuri na unaonekana .

Baada ya United kufunga huku mashambulio yao yote yakilenga goli wakati walipoishinda Brighton 2-0 katika raundi ya sita kombe la FA siku ya Jumamosi, Mourinho alisema kwamba kikosi chake kiliogopa kucheza.

Beki wa kushoto Luke Shaw alikuwa mmoja ya wachezaji waliotajwa na kukosolewa na mkufunzi huyo baada ya kusema kwamba hakufurahishwa na kiwango cha mchezaji huyo.

Mchezaji huyo wa UIngereza ambaye ameichezea United mara 15 msimu huu alikuwa akianzishwa tangu Februari.

Je Ananyanyaswa? aliuliza Sutton. Sipendelei neno 'kunyanyaswa' katika soka kwa sababu huwa kuna hisia kali katika chumba cha maandilizi hususan kutoka kwa mkufunzi.

Huwa kuna maneneo yanayotumiwa na mkufunzi kuwakosoa wachezaji.

Swala hilo limekuwa likifanyika tangu soka ianze. Kila mtu yuko tofauti. Kwa upande wa ukufunzi wana haki ya kuhakikisha kuwa wanafahamiana na kila mchezaji kitabia.

Wright alisema kuwa Mourinho anafaa kufanya kila kitu ili kuhakikisha kuwa kiwango cha mchezo wa Luke Shaw kinaimarika baada ya mchezaji huyo kuvunjika mguu wake wa kulia mara mbili mwezi Septemba 2015.

Alisema: Alivunjika mguu na sasa anaonekana mzito lakini hilo halimaanishi kwamba hawezi kupanda juu na kushuka chini katika wingi yake.

Sijui maisha yake ya kibinafsi lakini haiwezekani kwamba kila mara mkufunzi anarudi kumkumbusha. Mourinho anafaa kumuimarisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye huenda atashiriki katika kombe la dunia na kikosi cha Uingereza.

Ukosoaji wa Mourinho umemuudhi Shaw. Amekasirishwa na hatu hiyo . Siwezi kusema sana kuhusu vile watu wake walivyokasirishwa.

Ni hivi juzi alikuwa akiuguza jeraha la mguu na sio mara ya kwanza kwamba Mourinho amemkosoa , wengine huweka vichwa vyao chini lakini inadaiwa kuwa ilikuwa kibinafsi.

Michael Carrick amekuwa United kwa takriban miaka 12-13 na anatarajiwa kujiunga na idara ya ukufunzi ya timu hiyo. Iwpao kuna mtu anayefaa kumteta Shaw basi inafaa kuwa Carrick.

Ni vyema kuona mabao yatakavyokuwa. Sio chumba cha maandilizi cha miaka minne ama mitano iliopita wakati kulikuwa na wachezaji kama vile Patrice Evra, Nemanja Vidic na Rio Ferdinand ambao wangeweka kikao na Furgusson na kumwambia kuna swala tata.

Amuua Mkewe na Kuificha Maiti Kwenye Mbuyu kwa Miaka 8

$
0
0
Mwanaume  mmoja aliyejulikana kwa jina Bernard Shumba mkazi wa Singida anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa kumuua mke wake miaka minane iliyopita kisha kuuficha mwili wa marehemu kwenye mbuyu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Deborah Magiligimba, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa baada ya kukamatwa alikiri kutenda kosa hilo na kwenda kuonyesha mwili wa marehemu aliokuwa ameuhifadhi ndani ya mbuyu ambapo jeshi hilo kushirikiana na wananchi limefanikiwa kupata mabaki yake.

Inadaiwa kuwa mnamo Julai 10, 2010 katika Kijiji cha Yulansoni Kata na Tarafa ya Kinyangiri Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Tabu Robert (28) ambaye kwa kabila ni Mnyiramba, mkulima wa Yulansoni, aliuawa na mume wake aitwae Bernard Shumba Siza (47), Mnyiramba na mkulima wa Yulansoni.

Baada ya Mmuhumiwa kufanya tukio hilo aliuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuuficha kwenye mti wa mbuyu ambao una tundu kubwa na kisha aliripoti polisi kituo kidogo cha Kinampanda Mkalama kuwa mke wake ametoroka na alianza kumtafuta hadi tarehe Machi 17, 2018 ambapo taarifa zilipopatikana kuwa alimuua.

Baada ya mtuhumiwa kukamatwa na kuhojiwa alikiri kufanya kitendo hicho na kuonyesha sehemu alipouficha mwili huo Machi 18, mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni.

Mkuu wa polisi kituo cha  Mkalama na timu yake ya makachero walifika eneo la tukio na kufanikiwa kupata mabaki ya mifupa yakiwa ndani ya mti huo. Baadhi ya mifupa imechukuliwa kwa ajili ya kupelekwa kwa mkemia wa serikali na iliyobakia ndugu wamekabidhiwa kwa ajili ya mazishi.


Mrembo Jokate Atangaza Kuolewa

$
0
0

Mwanamitindo na Mjasiliamali Jokate Mwegelo ambaye pia ni Kaimu Katibu Hamasa wa Jumuiya ya Vijana wa CCM, ameibuka na kudai anatarajia kuolewa 'kuwa mke wa mtu siku za hivi karibuni' licha ya kumficha mwanaume ambaye atamuoa.


Jokate ametoa kauli hiyo mchana wa leo (Machi 20, 2018) kupitia ukurasa wake wa kijamii akiwa wahabarisha wadau wake wakae mkao wa kula kusherehekea tukio hilo ambalo amelipanga kulifanya katika siku za usoni.

"March Quen, karibu nitakuwa mke wa mtu fulani na mama watoto wake. 'God is great and faithful, grown but forever a baby girl'. Ni kwa neema tu na rehema zake Mungu. Thank you loves for dragging me out to take these", amesema Jokate.

Jokate Mwegelo ameweza kuweka uwazi wa maisha yake ndani ya siku aliyoweza kuletwa duniani 'kuzaliwa' miaka kadhaa iliyopita tarehe na mwezi kama wa leo.

Mwanafunzi UDSM Ngoma Bado Nzito Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 21

$
0
0


Mwanafunzi UDSM Ngoma Bado Nzito Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 21

Huku Sakata la Waziri na Diamond Platnumz Likishika Kasi, Diamond Aweka Rekodi YouTube Barani Afrika

$
0
0
Diamond Platnumz kila kukicha anaendelea kuweka rekodi kwenye muziki wake na awamu hii sio views wa kwenye mtandao wa YouTube bali ni Subscribers.

Diamond kwenye akaunti yake ya YouTube tayari amefikisha Subscribers milioni 1+ na kuwa msanii wa muziki wa 8 barani Afrika kuwa na Subscribers zaidi ya milioni 1.

Kwa sasa Diamond Platnumz ameungana na wasanii kama Amr Diab kutoka Misri mwenye Subscribers milioni 1.6, Kundi la muziki la Die Antiwoord kutoka Afrika Kusini subscribers milioni 1.8, Dzjoker Chemsou milioni 1.6, Lartiste milioni 2.2, Ilias Tiiw milioni 1.8, Sofia Carlsberg milioni 1.8 .

Wengine ni Tamar Hosny milioni 2.8, shady Srour milioni 2.8 wote kutoka Misri na Saad Lamjarred kutoka Morocco ambaye ndiye msanii wa muziki anayeongoza kwa bara la Afrika kuwa na Subscribers wengi milioni 4.4 .

Kwa upande wa wasanii wengine kutoka Afrika kama Davido, Wizkid, Yemi Alade, Tiwa Savage, Sarkodie, Alikiba na Cassper Nyovest wote bado hawajafikisha Subscribers milioni 1 ingawaje hao wanatumia mtandao wa VEVO, na akaunti inayoongoza kuwa na Subscribers wengi ni ile ya kundi la PSquare ina subscribers laki 7.

Wiki iliyopita Diamond Platnumz aliachia album yake ya ‘A BOY FROM TANDALE’ na tayari imepokelewa vizuri na mashabiki wa muziki barani Afrika ambapo imeanza kutrend kwenye mitandao ya kununulia nyimbo kwenye baadhi ya nchi kama Burkina Faso, Oman, Namibia, Kenya, na Malaysia na kwenye mitandao mikubwa ya kimuziki kama SPOTIFY

Mwakyembe Amshukia Diamond, Asema Umarufu Utamkosti, Awezi Bishana na Shonza na Atapotea Kubishana na Serikali

$
0
0
Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kukerwa na mwanamuziki Diamond Platnumz kutokana na kumdharirisha naibu wake Juliana Shonza wakati akihojiwa katika kipindi cha The Play List cha Times FM na mitandaoni.

Katika maelezo yake Mwakyembe amesema inaelekea sasa Diamond ameanza kulewa umaarufu sasa. Kuhusu hoja ya vikao anavyodai mwanamuziki huyo Mwakyembe amesema kuwa “kama ni vikao na wasanii, tumefanya vingi sana, lakini Diamond hahudhurii vikao hivyo na si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, haijalishi nibmaarufu kiasi gani."

"Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea wenzake," amesema Mwakyembe.

Aidha Waziri Mwakuembe amemalizia kwa kumshauri mwanamuziki huyo kuwa "si busara kwake kushindana na Serikali, na kama ana ushauri basi autoe kistaarabu utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi alivyofanya. Sijafurahishwa hata kidogo."

BREAKING: Rais Magufuli Katengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)

$
0
0
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Blandina Nyoni na kuivunja bodi hiyo. Uteuzi wa Mwenyekiti na bodi nyingine utafanyika baadaye.

Mambo ni Mtoo..Lemutuz Naye Aibuka na Kumkosoa Naibu Waziri Shonza, Adai Anatumiwa Bila Kujijua

$
0
0

Lemutuz ameandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram:

From @lemutuz_superbrand -
Dear Mheshimiwa Naibu Waziri Mh. J. Shonza we have always been kool kwa sababu wote tupo Chama kimoja yaani Chama Tawala I have always respected your views lakini kwenye hili la kushirikiana na huyo "MUNGU MTU" wa hicho kituo cha Radio anayetaka Wasanii wampigie magoti ninaomba kutofautiana na wewe ...hua sio rahisi kwangu kusimama against Kiongozi yoyote wa Serikali na Chama changu in the Public lakini kwenye hili la wewe kushindana na Msanii maarufu kioo chetu cha Taifa Duniani on a serious note umeshauriwa vibaya sana na naona kama unataka kurudia makosa ya waliokutangulia ya Kiongozi kuchukua side za mabifu ya kijinga na kitoto baina ya Wanajamii hasa katika our Entertainment industry ...in the first place Kiongozi wa Taifa of your level badala ya kwenda kwenye neutral ground like TBC kuongelea Wasanii uliowafungia wewe ukaenda kwa "MUNGU MTU" mwenye mabifu na Msanii maarufu Duniani Mtanzania kama wewe na mimi ambaye na yeye umefungia miziki yake huku ukijua wazi kua yule "MUNGU MTU" ana mabifu ya kufikia kufungia miziki yake kutopigwa kwenye Radio anayoifanyia kazi what was that? ni nani aliyekupa huu ushauri so shallow minded na so low? na ulikua unajaribu kutuambia nini Wanachi ambao some of us tunao uwezo wa kuona na kujua kila kitu kinachoendelea behind the scene? ..I mean WaTanzania tumeaibika sana kwenye music industry Duniani na kwa muda mrefu sana leo finally Mungu amesikia kilio chetu tuna Msanii anayetuweka kwenye ramani ya Dunia ni majuzi amechaguliwa kutengeneza Wimbo na Show ya ufunguzi katika Mashindano ya Kombe la Dunia leo wewe upo busy kupigana naye kwenye Social Media hivi sisi Wabongo what has gone wrong na our thinking? ..halafu naomba kuuliza Naibu Waziri hivi kweli ndiye anayetakiwa kufungia miziki au Basata? hivi ni kweli Naibu Waziri ndiye uliyetakiwa kuwaita kina Gigi Money na Sanchi kweli seriously kuhusu mavazi na tabia zao kama wasanii? ..I mean something is wrong mheshimiwa aidha unatumiwa bila kujijua au you are missing something but kitendo cha wewe kuungana na "MUNGU MTU" against Diamond HAKIKUBALIKI CHANGE NOW! - @lemutuz_superbrand

Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayub Rioba apata Ajali Kigoma

$
0
0
Watu wawili wamefariki Dunia wilayani Kasulu mkoani Kigoma kufuatia ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba, lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu.

Kamanda  Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni watembea kwa miguu wawili, waliofahamika kwa majina ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto, Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na Majeruhi mmoja aliefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto, ambae hali yake ilielezwa kuwa mbaya huku akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.

Amesmea Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

Kamanda Otieno aliongeza kwwa kutoa tahadhari kufuatia  Chanzo cha ajali hiyo kuwa ni utelezi unaotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo,hivyo amewaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani.

Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.


Pichani kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba baada ya kunusurika kifo akiwa eneo la tukio pamoja na Polisi waliofika

Maboresho Katika Application ya Udaku Special.... Download Upya Kwenye Simu yako Kupata Habari Zetu Haraka

Rais Magufuli Amteua Ernest Mangu Kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda

$
0
0
Rais Magufuli Amteua Ernest Mangu Kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda
Rais Magufuli amewateua aliyekuwa IGP, Ernest Mangu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda na Meja Jenerali Mstaafu, Simon Mumwi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi.

Wateule wote wataapishwa Machi 21 Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5:00 asubuhi.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images