Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live

Hali ya Aveva si nzuri

$
0
0
Rais wa Simba, Evans Aveva.

HALI ya Rais wa Simba, Evans Aveva, si nzuri na anaendelea kutibiwa ka­tika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Jana, Aveva alishindwa kufika ma­hakamani kwa mara ya saba lakini ndugu yake akaliambia Championi, hali yake si nzuri.

“Hali yake si nzuri, anaumwa sana kwa kweli na sisi tunajisikia vibaya lakini ni kipindi cha mapito. Unajua bado ana kesi lakini kweli Aveva anaumwa sana na hata ukimuona, anaumiza sana moyo,” alisema.

Aveva amekuwa akizidi kupungua kutokana na kuugua mfululizo siku chache baada ya kuingia mahabusu akituhumiwa katika kesi ya utakatishaji fedha.

Jana, Aveva ameshindwa kuhudhuria tena mahakamani katika kesi yake ya utakatishaji fedha inayomkabili ikiwa ni mara ya saba mfululizo kutoka­na na kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia hali yake ya kiafya kutokuwa nzuri.

Aveva anakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani, akiwa na makamu wake wa rais, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

Katika kesi hiyo ambayo itakuwa ikisikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Maka­hama ya Kisutu, Thomas Simba, badala ya Victoria Nongwa ambapo wakili wa Takukuru, Nassor Katuga ameiambia mahakama hiyo kwamba kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini wameshakamilisha upelelezi, hivyo wapo tayari kuendelea kwa hatua ya kuanza kusikilizwa.

Katuga alisema kuwa wamepokea taarifa kuwa ms­hitakiwa namba moja (Aveva) ameshindwa kufika mahaka­mani kwa kuwa anaumwa na amelazwa Muhimbili, badala yake yupo Kaburu peke yake ambaye ni mshitaki­wa namba mbili.

Kwa upande wa hakimu Simba, alisema kuwa ni vyema kufuatilia hali yake kwa kuwa kesi ipo tayari kusikilizwa ili iweze kuendana na muda kutokana na kuwa ni ya muda mrefu ambapo amepanga kuanza kusikilizwa Aprili 5, mwaka huu.


Mo Music atoa povu kisa kupotea kimuziki

$
0
0
Msanii Moshi Katemi ‘Mo Music.

BAADA ya madai kuenea kuwa staa wa Bongo Fleva, Moshi Katemi ‘Mo Music’ amepotea kimuziki, ameibuka na kutoa povu si la nchi hii.

Awali, tetesi zilienea kuwa, staa huyo aliyewahi kubamba na Ngoma ya Basi Nenda kisha Skendo, kwa sasa ameamua kuupa muziki kisogo kutokana na ushindani uliopo na kwamba ameamua kujiingiza kwenye ujasiriamali wa kufuga kuku.

Ilielezwa kuwa, ngoma yake ya mwisho aliyoitoa ya Kibajaj akimshirikisha Roma Mkatoliki ndiyo ‘ilimkata maini kabisa’ baada ya kubuma sokoni.

Showbiz juzikati lilifanikiwa kumuibua Mo Music ambapo lilikutana naye uso kwa uso na kumpelekea madai hayo ya kupotea.

Showbiz: Mambo! Kuna madai yapo kuwa umepotea kimuziki na sasa umejiingiza katika ujasiriamali wa kuku?

Mo Music: Mimi? Nimepotea kivipi? Mbona ngoma zangu zinapigwa redioni? Hata nikifuga hao kuku unaosema cha ajabu kipo wapi?

Showbiz: Lakini madai yanasema Wimbo wa Kibajaj ulivyobuma ndiyo umekufanya kuachana na muziki?

Mo Music: Ninavyojua mimi Kibajaj imefanya vizuri tu, siwezi kupotea na gemu kwangu naliona changa, hao wanaoeneza maneno yote hayo waendelee na umbea wao na ole wake nije kumgundua anayesa-mbaza yote haya!

Stars yachapwa 4-1 na Algeria

$
0
0

Mechi ya kirafiki iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kati ya Algeria dhidi ya Tanzania imemalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1.

Mechi hiyo imepigwa usiku huu katika Uwanja wa Mustapha Tchaker huko Blida nchini humo.

Mabao ya Algeria katika mchezo huo ambao waliutawala kwa asilimia kubwa, yalifungwa na Baghdad Bounedjah kwenye dakika za 13 na 80, Shomari Kapombe akijifunga kwa kichwa dakika ya 43 na bao la mwisho likifungwa na Carl Medjan (52′).

Bao pekee la Taifa Stars limefungwa na Simon Msuva kufuatia kona safi ya Shiza Kichuya mnamo dakika ya 20.

Matokeo hayo yanaleta taswira mbovu kwa Tanzania haswa kuelekea kupanda kwa ubora wa viwango vya soka duniani.

Kwa mujibu wa kalenda ya FIFA, Stars itakuwa ina kibarua kingine cha mchezo wa kirafiki, dhidi ya  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mechi hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam, Machi 27 2018.

Lulu Diva Akataa Kufananishwa na Shilole "Kila mtu Anaimba Muziki Wake"

$
0
0
Lulu Diva Akataa Kufananishwa na Shilole "Kila mtu Anaimba Muziki Wake"Msanii wa BongoFleva ambaye anatamba na kibao chake cha 'amezoea', Lulu Diva amesema hapendi kuona baadhi ya watu wanashindanisha kazi zake za muziki na Shilole kwa madai kitendo hicho kinaweza kuwagombanisha jambo ambalo kwake halitaki liwe hivyo.


Lulu Diva ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya baadhi ya watu kuanza kufananisha na kushindanisha kazi za wasanii hao wawili ili mwisho wa siku apatikane aliyekuwa juu zaidi ya mwenzake.

"Hakuna hata siku moja mtu anakuja na kupotezwa, kila mtu anaimba muziki wake na mimi Shilole namuheshimu kama dada yangu na anafanya muziki wa aina yake. Ukiangalia anachokifanya Shilole na Mimi ni vitu viwili tofauti", amesema Lulu Diva.

Pamoja na hayo, Lulu Diva ameendelea kwa kusema "ni watu tu wanajaribu ku-creaty vitu ili wajaribu kutuchonganishi baina yetu ninaomba hivyo vitu visiendelee kuwepo maana ninamuheshimu sana Shilole katika muziki amenitangulia na anajua mengi zaidi yangu. Mimi sifanyi muziki wa mwanamuziki yeyote kila mtu ana muziki wake".

Vyumba vya Midoli ya Mapenzi Vinavyozua Mjadala Paris Vyanusurika Kufungwa

$
0
0
Vyumba vya Midoli ya Mapenzi Vinavyozua Mjadala Paris Vyanusurika Kufungwa
Madiwani katika jiji la Paris wametupilia mbali hoja ambayo ililenga kufunga biashara ambayo imekuwa ikihusisha watu kulipia kukaa na midoli ya mapenzi kwa saa moja.

Wateja hulipishwa €89 ($109; £78) kukaa na midoli hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya silicone.

Madiwani wa chama cha Kikomunisti pamoja na watetezi wa haki za wanawake walikuwa wameliomba Baraza la Jiji la Paris ambalo huhusika katika kusimamia jiji hilo kujadili uwezekano wa kufunga biashara hiyo ambayo imekuwa ikifahamika kama Xdolls.

Wamekuwa wakisema biashara hiyo inadhalilisha wanawake na kimsingi ni kama danguro.

Ni haramu kumiliki au kuendesha biashara ya danguro nchini Ufaransa.

Lakini polisi walifika katika biashara hiyo kabla ya mkutano wa baraza hilo la jiji kufanyika na wakatangaza kwamba hakuna sheria zozote zilizokuwa zimevunjwa.

Katika taarifa ya pamoja, madiwani wa chama cha Kikomunisti Nicolas Bonnet Oulaldj na Hervé Bégué walisema wamesikitishwa sana na uamuzi wa baraza hilo.

"Biashara hiyo, ambayo ina midoli ya ukubwa sawa na binadamu na inakaribia sana umbo la binadamu, ndio uvumbuzi wa karibuni zaidi wa kujaribu kurejesha biashara ya madanguro," walisema.

Walieleza kuwa Xdolls ni "kilele cha kuharibiwa kabisa kwa uhusiano wa wanawake na wanaume".

Midoli ya mapenzi imekuwa ikipata umaarufu nchi mbalimbali. Doli kwa jina Harmony la kampuni ya RealDoll iliyoanzishwa na Matt McMullen katika eneo la San Marcos, California huweza kutembea na hata kuzungumza
Wamesema biashara hiyo inafanyia mzaha suala la kudhalilishwa kwa wanawake na mitandao ya biashara ya ukahaba na biashara husika ya ulanguzi wa binadamu.


Jumba hilo lilifunguliwa mapema mwaka huu na kujieleza kama "kituo cha michezo".

Wateja wengi huwa ni wanaume lakini wachumba pia hutembelea kituo hicho kwa pamoja, mmiliki wa kituo hicho Joachim Lousquy, ambaye zamani alimiliki maduka ya kuuza sigara, aliambia gazeti la Le Parisien.

Jumba hilo lina vyumba vitatu ambapo kila chumba kina doli la mapenzi la urefu wa 1m 45cm (futi 4 inchi 7) vya thamani ya euro elfu kadha.


Anwani ya jumba hilo huwekwa ikiwa siri kubwa na hata majirani huwa hawafahamu ni biashara ya aina gani hufanyika humo, anasema Lousguy.

Anasema midoli hiyo ni sawa na vifaa vingine vya kujitosheleza kimapenzi na haoni ni jinsi gani vinawadhalilisha wanawake.

Midoli ya mapenzi imekuwa ikipata umaarufu nchi mbalimbali. Doli kwa jina Harmony la kampuni ya RealDoll iliyoanzishwa na Matt McMullen katika eneo la San Marcos, California huweza kutembea na hata kuzungumza.

Nchini Kenya wiki kadha zilizopita, doli la mapenzi lililobandikwa jina Samantha lilizua pia mjadala mkali.

Mama Anashikiliwa na Polisi kwa Kumvutisha Mwanae Sigara

$
0
0
Mama Anashikiliwa na Polisi kwa Kumvutisha Mwanae Sigara
Mwanamke mmoja kutoka nchini Marekani leo March 22, 2018 ameshikiliwa na polisi baada ya kusambaa kwa video kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha akimvutisha mtoto wake sigara.

Video hiyo ambayo iliangaliwa zaidi ya mara Milioni 1 ndiyo iliyofanya Polisi wajue kinachoendelea na kuanza kumtafuta mwanamke huyo anayejulikana kwa jina la Brianna Ashanti Lofton mwenye umri wa miaka 20.

Video hiyo ilimuonesha mama huyo akimpa mtoto sigara ili avute. Lofton ameshtakiwa pia na kosa na kukutwa na bangi na makosa mawili ya kunyanyasa mtoto.

Mwalimu wa Sekondari Mbaroni kwa Kumkashfu Rais Magufuli

$
0
0
Mwalimu wa Sekondari Mbaroni kwa Kumkashfu Rais Magufuli
Mwalimu wa shule ya sekondari ya Nyakisasa iliyopo mkoani Kagera aliyetambulika kwa majina ya Deogratias Simon anashikiliwa na jeshi la polisi Kagera kwa tuhuma za kumkashfu Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Augustine Ollom amesema kuwa mwalimu huyo anashikiliwa kwa kosa la kutumia ukurasa wake wa Facebook kuikashfu serikali na kumkashfu Rais Magufuli  kuwa ni Dikteta na anaminya demokrasia.

Aidha amesema kuwa kufutia hali hiyo tayari yupo mikononi mwa polisi na watakwenda naye mpaka dakika ya mwisho ili sheria iweze kutenda haki huku Kamanda amewaomba wananchi kuendelea kufichua watu wenye vitendo vya namna hiyo ili wawakabidhi polisi ili washughulikiw

Dismass Ten Amjibu Haji Manara " Maisha Ayakosi Changamoto"

$
0
0
Dismass Ten Amjibu Haji Manara " Maisha Ayakosi Changamoto"KATUBU Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, kunukuliwa akisema kuwa wamsitisha kuuza jarida lao ambalo walilianzisha likiwa ni maalum kwa kutoa habari za klabu hiyo, Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, ametamba kwa kusema kuwa zilikuwa ni mbwembwe tu.

Leo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara aliandika kuwa Yanga walianza kwa mbwembwe kuuza jarida hilo lakini hawajafika kokote, huku akiwakejeli kuwa wameuza kopi mbili pekee.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, ameweka picha inayoonesha jarida la Yanga huku akiandika maneno ambayo inawezekana ikawa ni jibu kwa Manara. 

“Maisha hayakosi changamoto! Unapomcheka mwenzio kwa sababu hajafanikiwa ni vyema ukaonyesha ulichonacho wewe” aliandika Ten.

Mapezi ya Papa Yamtia Matatani Mtaiwan

$
0
0
Mapezi ya Papa Yamtia Matatani Mtaiwan
Raia wa Taiwan, Han Chuan (61) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara kujibu mashtaka manne ya uhujumu uchumi ikiwamo kukutwa na mapezi ya samaki aina ya papa ndani ya meli ya uvuvi.

Chaun, ambaye ni nahodha wa meli ya uvuvi iitwayo Buah Naga 1, anadaiwa kukutwa na kilo 90 za mapezi hayo bila kuwapo kwa miili ya papa wenyewe.

Wakili wa Serikali, Simon Wankyo alidai mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Richard Kabate kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 26 katika Bandari ya Mtwara.

Wankyo alidai katika shtaka la kwanza, Chuan akiwa nahodha wa meli ya uvuvi yenye usajili namba FT 333489, alikutwa na kilo hizo za mapezi ya papa, huku shtaka la pili likidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya Novemba 25, 2017 na Januari 26 kati ya eneo la Magharibi la mikoa ya Lindi na Mtwara mkabala na Bahari ya Hindi akiwa nahodha wa meli alisababisha uchafuzi wa mazingira ya bahari kwa kuwatupa papa baharini baada ya kuwakata mapezi huku akijua kuwa ni kinyume cha sheria.

Katika shtaka la tatu anadaiwa kuwa Januari 26 alikutwa na bastola aina ya Bereta bila kuwa na leseni.

Wankyo alidai kuwa katika shtaka nne, siku na eneo hilo, mshtakiwa huyo alikutwa akimiliki risasi 10 za bastola hiyo bila ya kuwa na kibali kutoka mamlaka husika.

Hakimu Kabate alimtaka mshtakiwa kutosema chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 27 itakapotajwa na mshtakiwa alirudishwa rumande.

Zawadi ya Hasheem Thabeet Kwenye Birthday ya Jokate Ilikuwa Moto, Ndio Mume Mtarajiwa?

$
0
0
Zawadi ya Hasheem Thabeet Kwenye Birthday ya Jokate Ilikuwa Moto, Ndio Mume Mtarajiwa?
Licha ya Jokate Mwegelo aka Kidoti kuachana na Hasheem Thabeet kwenye mahusiano yao ambayo yalidumu kwa takribani miaka mitatu, bado wawili hao wameonyesha kutokuwa maadui na wameendelea kuwa watu wa karibu.

Jokate ameonyesha kupokea zawadi ya maua kutoka kwa mchezaji huyo wa kikapu kwa ajili ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambayo ilikuwa Jumanne ya March 20 ya mwaka huu.

Kidoti ameweka picha ya zawadi hiyo ya maua kwenye mtandao wa Instagram na kuandika ujumbe ambao unasomeka, “Still receiving birthday roses🤗☺🤩. Thank you Sheemy @hasheemthedream 🌹 @bloom_eventfully for the delivery 😊.”

Hata hivyo kwa sasa kubwa linalosubiriwa kwa mrembo huyo ni ndoa yake ambapo katika siku yake hiyo ya kuzaliwa alithibitisha kuwa yupo mbioni kuolewa japo hakumtaja mwanaume ambaye atafunga naye ndoa.

Hukumu Kesi ya Babu Seya na Mwanaye Papii Kocha Kutolewa Leo

$
0
0
Hukumu Kesi ya Babu Seya na Mwanaye Papii Kocha Kutolewa Leo
Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu (AfCHPR) inatoa hukumu katika kesi iliyowasilishwa na wanamuziki Nguza Viking maarufu Babu Seya na mwanaye, Johnson Nguza 'Papii Kocha' dhidi ya serikali ya Tanzania katika mahakama hiyo.

Wawili hao waliwasilisha rufaa katika mahakama hiyo mwaka 2015 kupinga hukumu ya kifungo cha maisha iliyokuwa imetolewa dhidi yao.

Walikuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule waliokuwa na kati ya umri wa miaka 6 na 8 mwaka 2003.

Walikuwa wametumikia kifungo cha miaka 13 kufikia wakati wa kupewa msamaha

Babu Seya ambaye ni miongoni mwa wafungwa 1,821 waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya Uhuru wa Tanganyika mnamo 9 Desemba, 2017.


Wawili hao ndio walioimba kibao maarufu cha 'Seya' na walikuwa kati ya wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kufungwa maisha au kunyonga ambao walinufaika kutokana na msamaha wa rais.

Nguza Viking na wanawe walipokutana na Magufuli
Hukumu katika kesi yao ilikuwa imepangiwa kusomwa Jumatano wiki hii lakini baadaye ikaahirishwa hadi leo.

Wafungwa waliosamehewa wamshukuru Magufuli kwa kumwimbia
Babu Seya na wanawe waachiwa huru kwa msamaha wa rais
Mahakama hiyo kupitia ujumbe Facebook imesema hukumu itaanza kusomwa mwendo wa saa tano saa za Afrika Mashariki.

Hatua ya Dkt Magufuli kuwasamehea wawili hao ilishutumiwa na watetezi wa haki za watoto na wanawake.

Kate McAlpine, mkurugenzi wa shirika la Community for Children Rights lenye makao yake Arusha aliambia BBC wakati huo kwamba alikuwa "ameshtushwa lakini hakushangazwa" na hatua ya rais huyo. Alisema hatua hiyo ilionesha 'uelewa mdogo' wa kiongozi huyo kuhusu masuala ya udhalilishaji wa watoto.

Alilinganisha hatua hiyo na tamko la Rais Magufuli kwamba wasichana wanaoshika mimba hawafai kuwa shuleni.

"Huwa hafahamu vyema mambo, hasa yanayohusu watoto kama waathiriwa. Wasichana wanaoenda shule hushika mimba kwa sababu mara nyingi ni waathiriwa wa udhalilishaji," alisema Bi McAlpine.

Wakishinda watadai fidia?
Kwa kuwa wawili hao walishasamehewa na rais, uwezekano wao kuchukuliwa hatua iwapo hukumu ya kifungo dhidi yao itadumishwa ni mdogo sana.

Hata hivyo, iwapo watapatikana bila hatia, kuna uwezekano huenda wakawasilisha kesi wakitaka walipwe fidia kwa kipindi ambacho walikaa gerezani.

Nguza Viking na Johnson Nguza ni baba na mwanaye na ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao walikuwa wanamuziki Dar es Salaam.

Wote walikamatwa 12 Oktoba, 2003 na kuzuiliwa kituo cha polisi cha Magomeni ambapo baadaye walifikishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu 16 Oktoba, 2003 na kufunguliwa mashtaka 10 ya ubakaji na 11 ya ulawiti.

Waathiriwa wao walikuwa watoto wa kati ya miaka sita na nane, na walikuwa wote kutoka darasa moja.

Waathiriwa hao walidaiwa kubakwa na kulawitiwa kwa zamu na wanaume watano.

Mnamo 25 Juni, 2004 hakimu aliwapata na hatia na kuwafunga jela Nguza na wanawe watatu. Mshtakiwa wa nne, ambaye alikuwa mwalimu, alipatikana bila hatia.
izwa na 30 Oktoba Majaji Nathalia Kimaro, akisaidiana na Mbarouk Mbarouk na Salum Masati katika Mahakama ya Rufaa wakawaachilia huru Nguza Mashine na Francis Nguza baada ya kuwapata bila hatia.

Babu Seya na mwanaye Papii Kocha walipatikana na hatia na hivyo kuendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Majaji walisema kuwa kuna uthibitisho kuwa warufani hao wawili waliwabaka watoto wa shule ya msingi mwaka 2003.

Kesi hiyo iliwashtua mashabiki wa mwanamuziki Viking nchini Tanzania, na kanda nzima ya Afrika Mashariki.

Mwanamuziki huyo mwenye kuimba nyimbo za rhumba, ambaye ni mzaliwa wa DRC, ameishi Tanzania kwa miaka mingi na kuwa na mashabiki wengi.

NACTE Yavifungia Udahili Vyuo 163

$
0
0
NACTE Yavifungia Udahili Vyuo 163
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte), imevipika marufuku takribani vyuo 163 vilivyopo nchini Tanzania kuacha kuwafanyia udahili wa masomo wanafunzi wanaotarajia kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka 2018 kutokana na kutokidhi vigezo.


Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Udahili Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Twaha Twaha leo (Machi 23, 2018) wakati walipokuwa wanazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kusema baraza linawataka waombaji wa nafasi za mafunzo kwa ngazi za Astashahada na Stashahada kwa muhula wa masomo wa Machi/Aprili, 2018 kuomba kwenye vyuo vilivyokidhi ubora ambavyo vimeorodheshwa kwenye tovuti ya baraza na sio vinginevyo.

"Baraza lilifanya uhakiki 'academic audit' kwenye vyuo vyote ambavyo vimesajiliwa na baraza ili kuweza kujiridhisha kuona kwamba vina sifa na mambo mbalimbali ambayo yanahusika na utoaji wa taaluma. Katika uhakiki huo, Baraza lilibaini kuwa baadhi ya vyuo vilikidhi viwango vya ubora kwa mujibu wa taratibu za Baraza.  Hata hivyo, baadhi ya vyuo vilibainika kuwa na changamoto mbalimbali zinazoweza kuathiri ubora wa elimu na mafunzo yanayotolewa", amesema Twaha.

Pamoja na hayo, Twaha ameendelea kwa kusema "kufuatia zoezi hilo vyuo vyote vilivyobainika kuwa na mapungufu vilitaarifiwa na kutakiwa kurekebisha mapungufu yaliyobainishwa kabla ya kuendelea na udahili wa wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo 2018/2019".

Kwa upande mwingine, Twaha amesema kuwa udahili wa muhula wa Machi/Aprili, 2018 hauhusishi programu zote za kada ya Afya na Ualimu.

Ebitoke Akanusha Kumroga Ben Pol "Sijamroga"

$
0
0
Ebitoke Akanusha Kumroga Ben Pol "Sijamroga"
Msanii wa filamu na mchekeshaji hapa bongo Ebitoke, ameweka wazi juu ya kufufuka kwa penzi lake na Ben Pol ambaye hapo awali alidai hapokei hata simu zake, na hivi karibuni kuanza kuwa pamoja tena.

Ebitoke amesema kwamba kitendo cha yeye kuonekana na Ben Pol kwenye kazi zake za comedy ni kwamba alishamuahidi kuwa atamsaidia kwenye kazi zake, na si ndumba kama baadhi ya watu wanavyodai, kutokana kwamba penzi lao lilishakufa.

“Sijamroga Ben Pol, hata hivyo kipindi cha kati kati ambacho mahusiano yetu hayakuwa sawa, sio kwamba hayakuwa sawa ni kwamba alinituliza nisiongee sana kwenye mitandao baada ya ile kusema hapokei simu zangu na kuwa niweze ku-manage mahusiano, tulikaa kama mwezi mzima tulikuwa hatuongelei chochote, lakini aliniahidi kuwa atanisaidia kazi ndo hivyo tunasaidiana”, amesema Ebitoke.

Wawili hao bado kuna sintofahamu kama ni kweli wapenzi, kwani mara nyingi Ben Pol amekuwa sio mtu wa kufurahia suala la mahusiano yake na Ebitoke kuwa wazi.

Alikiba Atambulisha Video ya Pili

$
0
0
Alikiba Atambulisha  Video ya Pili
Msanii Alikiba ambaye ni mmiliki wa label ya King'S Music Ent leo Machi 23, 2018 ametambulisha video ya pili kutoka kwenye label hiyo ambayo imefanywa na mdogo wake Abdukiba ambaye ndiyo msanii wa kwanza kutambulishwa kutoka kwenye label hiyo.


Katika video ya wimbo huo wa Abdukiba Jeraha ambao umeongozwa na Director Hanscana lakini pia msanii Alikiba naye ameonyesha uwezo wake katika kuongoza video kwa kushirikiana na director huyo kufanikisha kazi hiyo ya Abdukiba.

Mbali na hilo Alikiba aliwahi kusikika kuwa wapo wasanii wengine chini ya label yake hiyo ila anaendelea kuwapika kwani yeye anatamani kila msanii ambaye atatoka kwenye label yake hiyo ya King's Music Ent basi awe wa kufafana na yeye katika kazi hata mafanikio pia.

Novemba 29, 2017 Alikiba alimtambulisha rasmi na kuachia video ya kwanza ya Abdukiba chini ya usimamizi wake kupitia label yake na kuachia wimbo ambao yeye pia alikuwa ameshirikishwa, wimbo unaitwa 'Single'

Serikali Kuwatumia Waganga wa Kienyeji Kutibu TB

$
0
0
Serikali Kuwatumia Waganga wa Kienyeji Kutibu TB

Katika kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu (TB) nchini, serikali imesema kuwa itawatumia waganga wa kienyeji katika kuwagundua wagonjwa hao ili waweze kufikishwa kwenye vituo vya afya na kupata tiba sahihi.


Kauli hiyo imetolewa leo (Mchi 23, 2018) mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yatakayofanyika kesho (Machi 24, 2018).

Waziri Mwalimu amesema kuwa waganga wa kienyeji ni wadau muhimu katika kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuwa wagonjwa wengi hukimbilia kwao kwa kudhani kuwa wamerogwa.

Aidha, Ummy amesema kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani WHO inakadiriwa zaidi ya watu milioni 10.4 huugua kifua kikuu kila mwaka duniani huku milioni moja kati yao wakiwa ni watoto wenye umri chini ya miaka 15 na hapa nchini kila mwaka jumla ya watu 60,000 wanaambukizwa ugonjwa huo wakati mwaka 2016 watu 65,908 waliogundulika kuugua na kuanza matibabu.

Kamanda Muroto: Watakaoandamana April 20 Watajikuta Vilema

$
0
0
Kamanda Muroto: Watakaoandamana April 20 Watajikuta Vilema
Wakati vuguvugu la maandamano yanayoandaliwa kupitia mitandao ya kijamii likiendelea kupamba moto, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema watakaoandamana siku hiyo watapata matatizo makubwa na wengine watajikuta wakiwa na vilema.

Kamanda Muroto aliyasema hayo juzi alipowafikisha mbele ya wanahabari, watu wawili akiwamo dereva wa Mfuko wa Bima ya Taifa (NHIF), Amandus Manchali (31) mkazi wa Kigamboni Geti Jeusi jijini Dar es Salaam na Yuda Mbata (29) mkulima na mkazi wa Bahi.

Muroto alisema watu hao walikuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuhamasisha maandamano yenye chuki na viashiria vya kuvuruga amani ya nchi.

“Watakaoingia barabarani siku hiyo, watapata matatizo makubwa kwani wengine watajikuta wakiwa vilema na ni vizuri wakaitumia mitandao katika kuhamasisha shughuli za maendeleo badala ya kuhamasisha ujinga,” alisema Muroto

Alisema kuna watu wasiopenda amani na utulivu wa nchi, wanatumia vibaya mitandao ya mawasiliano kuvunja sheria kwa kuhamasisha chuki dhidi ya Serikali na kuhamasisha maandamano yasiyo halali.

“Hawa watu ni sawa na watu walioshiba ambao hawajui nchi imetoka wapi na mtu akishiba akavimbiwa anaweza kuhamishia choo ndani,” alisema.

Wakati hayo yakiendelea Dodoma, taarifa zilizopatikana huko Moshi zinadai kuwa mfanyabiashara mashuhuri anayemiliki maduka ya kuuza vifaa vya elektroniki ya Mekus Electronic, Ladislaus Moshi, alikamatwa Jumamosi iliyopita na kusafirishwa mpaka Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah jana alithibitisha kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo, lakini akakataa kuingia kwa undani akisema suala hilo linachunguzwa na Polisi jijini Dar es Salaam.

Kamanda Issah alifafanua kuwa mtuhumiwa huyo alisafirishwa kwenda Dar es Salaam na kumwelekeza mwandishi wetu kuwasiliana na makao makuu ya Polisi Dar es Salaam ambako uchunguzi wa tuhuma zake unafanyika.

Makamanda wazungumzia maandamano Aprili 26

Wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma akitoa onyo kali, makamanda wa Polisi katika mikoa mbalimbali nchini wamesema yeyote atakayebainika kuingia barabarani siku hiyo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Wamesema wanaendelea na uchunguzi kuwabaini watakaofanya hivyo huku wakiwatoa hofu wananchi wakiwataka waendelee na shughuli zao za kiuchumi.

Akizungumza na Mwananchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema wanaendelea kufanya upelelezi kuhusu jambo hilo.

“Kwa hiyo siwezi kukuambia kama tumewakamata au lah, jambo hili bado tunaendelea kulifanyia upelelezi lakini tu niseme, ole wake atakayekutwa anahamasisha maandamano,” alisema.

Alisema Mtanzania mwenye akili timamu na anayetanguliza uzalendo wa nchi yake mbele hawezi kuhamasisha maandamano ambayo madhara yake makubwa ni kuvuruga amani ya nchi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga alisema uhamasishaji wa maandamano hayo unafanywa kwenye mitandao pekee.

Alisema intelijensia inaendelea kuwasaka watu au vikundi vinavyojipanga kwa jambo hilo au kuendelea kuhamasisha maandamano hayo kinyume cha sheria.

“Huku Mkoa wa Mbeya hatujamkamata mtu ‘phyisically’ akihamasisha upuuzi huu wa maandamano na niwaombe wakazi wa mkoa huu waendelee na kazi zao kama kawaida, wasikubali kabisa kuandamana au kuhamasisha jambo hili,” alisema.

Alisema wengi wanaohamasisha suala hilo mitandaoni wanatumia majina bandia na wanaendelea kusakwa.

“Kwa hiyo mtu yeyote atakayeingia barabarani siku hiyo, polisi tutafanya kazi yetu kuhakikisha mkoa unaendelea kuwa wa amani na utulivu,” alisema Kamanda Mpinga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Jumanne Murilo alisema tayari viongozi mbalimbali walishazungumzia suala hilo ambalo kwa sasa hataweza kulielezea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jinathan Shanna alisema kama ilivyo kwenye mikoa mingine, polisi wa mkoa huo hawajalala.

Kamanda Shanna alisema walichobaini ni kwamba wapo wanaofanya hivyo kwa kutojua sheria ya mitandao ambao hata hivyo, hawatakuwa na msamaha kisheria.

“Kuna watu wanapokea ujumbe wa kuhamasisha maandamano halafu wanausambaza, sasa sijui wanafanya hivyo kwa sababu ya ubwege wao wa kutokujua au wana lengo la kuhamasisha hata kama wanajua kufanya hivyo ni kosa, nawasihi waache mara moja,” alisema Kamanda Shanna.

Aliwataka wakazi wa mkoa huo kutokubali kusambaza ujumbe wa aina yoyote ile wenye lengo la kuvuruga amani, badala yake wafute au kubaki nao wao wenyewe.

Kamanda wa Polisi wa Temeke, Emmanuel Lukula alisema jeshi hilo pia linaendelea kuwasaka watu hao na kwamba wakibaini uwepo wa harufu yoyote wahusika hawataachwa, watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. “Viongozi walishatoa maelekezo na sisi tunatekeleza kwa hiyo niwaambia tu wananchi kwamba, polisi hatujalala, ninachohamasisha waendelee kufanya kazi zao za kimaendeleo kama kawaida,” alisema na kuongeza;

“Waachane kabisa na jambo hili, watii sheria bila shuruti, lakini kwa atakayependa kushurutishwa, basi sheria itachukua mkondo wake.”

Ajali: Lori la Mafuta Lawaka Moto na Kuua Wawili Singida

$
0
0
Ajali: Lori la Mafuta Lawaka Moto na Kuua Wawili Singida
Taarifa kutoka mkoani Singida muda huu ni kwamba lori la mafuta limeanguka na kuwaka moto katika eneo la Mlima Sekenke na watu wawili wanaripotiwa kupoteza maisha.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Deborah Magiligimba  amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa ni kweli kuna watu wawili wamefariki, lakini bado hawajapata majina yao.

Meya wa Jiji Ataka Watu 10 Waajiliwe Kwa Kuzika Wafu Waliokosa Ndugu

$
0
0
Meya wa Jiji Ataka Watu 10 Waajiliwe Kwa Kuzika Wafu Wanaokoosa Ndugu
Kama unadhani unazo sifa za shughuli za mazishi, kuna fursa hii iliyotangazwa katika Jiji la Dar es Salaam. Wanahitajika wafanyakazi 10, kazi yao ikiwa moja tu, kuzika wafu wanaokosa ndugu.

Hayo ni maagizo yaliyotolewa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita kwa halmashauri zote za wilaya, akizitaka kila moja kuajiri watu wawili kwa kazi hiyo.

Jiji la Dar es Salaam lina halmashauri tano za wilaya hivyo kufanya wanaohitajika kwa kazi hiyo kuwa watu 10.

Halmashauri ya jiji hubeba jukumu la kuzika wafu ambao miili yao inakosa ndugu katika kipindi cha siku 21 hospitalini.

Akizungumza jana wakati wa kikao cha robo ya tatu cha Baraza la Madiwani wa Jiji, Mwita alisema amerudia agizo hilo alilotoa katika kikao kilichopita baada ya kuona halijatekelezwa.

Aliwaambia waandishi wa habari baada ya kikao cha baraza hilo kuwa katika kikao kilichopita, walifanya mgawanyo wa majukumu wa shughuli hiyo kwa halmashauri zote na jiji, “Tulikubaliana kuwa sisi kama jiji tutatoa usafiri, sanda na dawa lakini mpaka sasa bado sijaletewa hao watu (watumishi), tufanye hima wapatikane kabla ya kikao kijacho,” alisema Mwita.

Mbali ya suala hilo la maziko ya wafu wasiokuwa na ndugu zao, kikao hicho kilijadili pia suala la mkataba wa Soko la Machinga Complex na Mwita alisema wameunda kamati maalumu kujua hatua zitakazochukuliwa endapo mkataba wa soko hilo hautapatikana.

Soko hilo lilijengwa kwa mkopo kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)likiwa na jumla ya vizimba 4,200 vya kufanyia biashara na lilizinduliwa mwaka 2010 lakini Mwita alisema ofisi yake haina taarifa ulipo mkataba kati yake na shirika hilo licha ya kufanyika kwa jitihada mbalimbali.

“Kwa sasa siwezi kusema lolote kwa sababu tunasubiri ripoti kutoka kwa kamati maalumu iliyoundwa, lakini kabla ya hapo nimeshafanya vikao na NSSF na ofisi ya mkuu wa mkoa, havikuzaa matunda,” alisema.

“Muwe na subira ikifika Mei tutakuwa na jambo la kuzungumza juu ya mkataba wa eneo hilo kwani ripoti itakuwa tayari.”

Mkataba huo ‘umetoweka’ huku kukiwa na madai kwamba una kasoro kadhaa zikiwamo kutofahamika kwa gharama husika za ujenzi huo pamoja na kujengwa katika ukubwa usiostahili.

Awali, kupitia kamati iliyoundwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ikiwa ni utekelezaji wa agizo la aliyekuwa waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene lililotolewa Aprili 19, 2016, ilibainika kuwa mbali na utata wa gharama za ujenzi, Jiji la Dar es Salaam halina uwezo wa kulipa deni hilo kwa sababu hadi lilipokabidhiwa, jengo hilo lilikuwa na deni la Sh19.7 bilioni na hadi kufikia Machi 2016, lilifikia Sh32 bilioni kutokana na riba. Mkopo wa awali uliokuwa umetolewa wakati ujenzi wake ukianza ulikuwa ni Sh12 bilioni.

Kuhusu ukubwa, inadaiwa kuwa mkataba uliosaniwa ulieleza kwamba gharama za ujenzi huo zitahusisha ujenzi wa jengo la ghorofa sita likiwa na vizimba 10,000 lakini lililokabidhiwa ni jengo la ghorofa nne na vizimba 4,200

Trump Amuonya Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Obama

$
0
0
Trump Amuonya Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Obama
Rais wa Marekani, Donald Trump ameamua kuweka wazi kuwa amechoshwa na kauli za vitisho kutoka kwa aliyewahi kuwa makamu wa Rais nchini humo wakati wa utawala wa Barack Obama, Joe Biden.

Trump amesema amechoshwa na kauli za vitisho juu yake zinazotolewa na mwanasiasa huyo mkongwe nchini Marekani kutoka chama cha Democratic na kuweka wazi kuwa haogopi chochote kwani anamjua toka enzi ni mtu asiyekuwa na nguvu kimwili na kiakili.

“Mpuuzi Joe Biden anajifanya kama mtu mwenye nguvu. Ukweli ni kwamba ni mtu dhaifu kimwili na kiakili mbaya zaidi anatishia kunipiga kwa mara ya pili hii. Nadhani hanijui vizuri nitamsambaratisha mara moja na kurudi nyumbani akilia njia nzima. Usipende kutishia watu.“ameandika Trump kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Jumanne Machi 20, 2018 Joe Biden akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Masuala ya siasa cha Miami akisema kuwa kama wangekuwa wanasoma naye sekondari angemchakaza kwa masumbwi Rais Donald Trump.

“Wananiuliza ninauwezo wa kufanya mdaharo na Trump, nawajibu hapana. Natamani kama tungekuwa sekondari ningempeleka kwenye eneo la kufanyia mazoezi nimchakaze kwa makonde mazito. Haiwezekani Rais wa nchi awachezee wanawake kwa kuwatomasa halafu aje aombe radhi hadharani heti alifanya makosa, hapa chama cha Republican kilichemsha,“amesema Joe Buddeni kwenye video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa facebook wa chuo hicho.

Joe Biden anatajwa kuwa ndiye atakayekuwa mgombea wa urais mwaka 2020 kupitia tiketi ya chama cha Democratic na atashindana na Rais Trump kama atapita kwenye kura za maoni kwenye uchaguzi huo.

Mourinho: Mtu Mwenye Akili Anaelewa Hali ya Manchester United

$
0
0
Mourinho: Mtu Mwenye Akili Anaelewa Hali ya Manchester United
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema watu wenye “ubongo” na “fikira za kuelewa mambo ya msingi” wanafahamu na kuelewa kwamba klabu hiyo imo kwenye kipindi cha mpito.

Mourinho ameshutumiwa mara kwa mara kutokana na mtindo wake wa uchezaji ambao unadaiwa kutokuwa na ubunifu hata kidogo na pia kutoangazia uchezaji wa kushambulia.

Shutuma zilizidi baada ya United kuondolewa michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na klabu ya Sevilla ya Uhispania.

“Naelewa masikitiko ya kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, lakini sielewi kitu kingine chochote kamwe,” Mourinho alisema alipokuwa anahojiwa na CNN.

“Katika historia ya soka kote duniani, na si England pekee, kila wakati umekuwa na klabu kubwa zaidi zikipitia kipindi cha mpito, na unakuwa na klabu nyingine kubwa zaidi zikiwa na vipindi vinavyoendelea vya ushindi kwa muda mrefu, na hizi huwa ni kama awamu katika klabu yoyote ile.”

United, wamo nafasi ya pili Ligi Kuu ya Uingereza nyuma ya Manchester City lakini pengo kati yao ni alama 16.

City huenda wakatawazwa washindi wa ligi kwenye debi ya Manchester itakayochezewa uwanja wa Etihad mnamo 7 Aprili.

Baada ya United kufuzu kwa nusu fainali Kombe la FA kwa mara ya 29 kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Brighton Jumamosi, Mourinho aliwashutumu wachezaji wake akisema “waliogopa kucheza” na pia akatilia shaka sifa zao kama wachezaji binafsi.

Mkesha wa mechi hiyo, Mourinho, ambaye ni meneja wa zamani wa Chelsea, alitoa hotuba ya dakika 12 kutetea kazi yake United.

Mourinho alikuwa ameshinda kombe ndogo la klabu bingwa Ulaya, Europa League na pia KOmbe la Ligi msimu wake wa kwanza akiwa United.

Katika mahojiano na CNN aliongeza: “Ukiangalia Ligi ya Premia tuko na timu moja, klabu moja ambayo imejiandaa vyema sana kutushinda kwa miaka kadha iliyopita, na tuna klabu 18 nyuma yetu. Klabu moja mbele yetu, na 18 nyuma yetu.

“Bila shaka, katika siku zijazo tungependa kuwa na klabu 19 nyuma yetu lakini huu ndio uhalisia, uhalisia kwa watu wenye ubongo, walio na uwezo wa kufikiria mambo ya kimsingi, walio na ufahamu kuhusu jinsi mchezo huu ulivyo, kwamba tuko katika kipindi cha mpito.

“Na kuwa katika kipindi cha mpito na bado kufanikiwa kutimiza kwa mfano yale tuliyoyatimiza msimu uliopita, kushinda vikombe, na kufanikiwa kutimiza yale tunayojaribu kuyatimiza msimu huu, ambayo ni kujaribu bado kushinda kombe na kujaribu kumaliza wa pili … Nafikiri tuko katika nafasi nzuri.”
Viewing all 104803 articles
Browse latest View live




Latest Images