Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

ATCL Kusitisha Safari Zake

$
0
0

ATCL Kusitisha Safari Zake
Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) itasitisha safari zake kati ya miji ya Dar es Salaam na Songea kuanzia Jumamosi kutokana na ubovu wa njia ya kurukia ndege katika Uwanja wa Songea, imeelezwa.

Taarifa ya ATCL iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana ilisema safari hizo zitarudishwa mara tu baada ya kukamilika kwa matengezo makubwa ya uwanja huo "yanayotazamiwa kuanza hivi karibuni."

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Injinia Ladislaus Matindi ilisema kusitishwa kwa safari za Songea kutakuwa na athari mbili.

Ilisema ukiacha adha kwa abiria wanaokwenda Songea, hatua ya ATCL hiyo pia itaathiri safari za Mtwara "kwa kipindi kifupi kutokana na sababu za kibiashara wakati shirika likitathmini njia mbadala ya kuhudumia kituo hiki peke yake".

"ATCL inawaomba radhi wateja wake kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana na uamuzi huu," ilisema zaidi taarifa ya Injinia Matindi kwani "usalama wa wateja ni kipaumbele cha ATCL."

Wema ni Noma Hivi Ndivyo Alivyofanya Kwenye Birthday ya Martin Kadinda

$
0
0
Wema ni Noma Hivi Ndivyo Alivyofanya Kwenye Birthday ya Martin Kadinda
Kitu Wema Amemfanyia Martin Kadinda Kwenye Birthday Yake


Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumatatu

Breaking News: Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa Yamuachia Abdul Nondo kwa Dhamana

$
0
0
Breaking News: Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa Yamuachia Abdul Nondo kwa Dhamana
Leo March 26, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imemuachia kwa dhamana Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania Abdul Nondo ambaye alikuwa anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Iringa.

Nondo amepewa masharti ya dhamana  ni wadhamini wawili mmoja mtumishi wa Serikali wote wakazi wa Iringa na bondi ya kauli Tshs Milioni 5, atarudi Mahakamani April 10, 2018.

Usome Hapa Waraka Mzito wa Baraza la Maaskofu wa KKKT Unaotikisa Vichwa vya Habari Leo

$
0
0

BARAZA la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jana wametoa waraka mzito wa Sikukuu ya Pasaka ambao umesainiwa na maaskofu 27 waliokutana Machi 15, 2018 na kusomwa Jana Machi 25, 2018 katika makanisa yote ya KKKT  nchini.

Katika ujumbe huo maaskofu, wamegusia masuala makuu matatu ambayo ni jamii na uchumi, maisha na siasa na mambo mtambuka yanayohusiana na hayo ikiwemo demokrasia, huku wakisisitiza Katiba mpya ya wananchi ni suluhu ya yote. Pia, masuala ya wanasiasa kuhama chama kimoja na kwenda kingine pamoja na mabadiliko ya mara kwa mara ya mfumo wa elimu kwamba una athari kwa Taifa.

UJUMBE WA PASAKA KUTOKA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA (KKKT)

TAIFA LETU, AMANI YETU​

A. UTANGULIZI

“Fumbua Kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu wote walioachwa peke yao; Fumbuakinywa chako, uhukumu kwa haki; uwapatie maskini na wahitaji haki yao”(Mithali31:8-9).

Wapendwa wana KKKT,

Watukuka, watu wote na familia ya Mungu katika Taifa letu, “Amani iwe kwenu!; Kristo Amefufuka (Yohana 20:19).


Bwana wetu Yesu Kristo mfufuka, alipowatokea wanafunzi wake wakiwa wamejifungia ndani kwa hofu ya Wayahudi, aliwasalimu na kujifunua kwao kwa salaamu ya kuwatakia amani. Wapendwa watu wa Mungu, katika umoja wetu, sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tunawasalimuni nyote kwa kuwatakia amani. Bwana wetu Yesu Kristo Amefufuka kweli kweli – Haleluya!.


Yeye ni amani yetu, na pia ni amani kwa watu wote wenye mapenzi mema. Kwa kufufuka kwake, upendo umeishinda chuki; unyenyekevu umeushinda ubabe; nuru imelishinda giza; haki imeshinda udhalimu; msamaha umeshinda visasi; ujasiri umeshinda hofu; na kwa hiyo uzima umeshinda kifo.


Mwaka 2017, Kanisa letu limeadhimisha miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa. Tukiwa wana Matengenezo tumekumbushwa tena kuwa mwanadamu anaokolewa kwa Neema ya Mungu tu: Wokovu Hauuzwi; Mwanadamu Hauzwi walakununuliwa; na Uumbaji hauuzwi. Kanisa zima na dunia kwa ujumla tunaitwa kusimama pamoja na kuueleza ukweli huu unaoziweka huru dhamiri zetu (Yohana 8:31-32).


Matengenezo (Reforms) ni dhana ya kibiblia. Tangu zama za Agano la Kale, Mungu kwa nyakati mbalimbali aliteua wajumbe wake kuwasilisha ujumbe wake kwa jamii na kwa watawala wa dunia. Kwa Umungu wake, aliwainua wanawake na wanaume kwa makusudi ya kutoa unabii yaani, ujumbe wa Mungu kwa jamii au watawala. Wakati mwingine aliinua manabii kuwasemea wasiokuwa na sauti. Unabii na Matengenezo ni njia ya Mungu katika kusimika utawala wa haki na unaostawisha uhuru na amani.


Kwa namna ya pekee, manabii kama Daniel, walionya juu ya uongozi unaojenga uhalali wake katika wingi wa watu wanaokubaliana na uongozi huo hata kama ni katika makosa. Haikuwa rahisi kibinadamu kuukosoa mfumo kama huo lakini Mungu alitumia manabii kuzungumza na mfumo wa namna hiyo.


Unabii wa Daniel 3:7 unasema, “Kwa hiyo watu WOTE,mara waliposikia sauti za baragumu, filimbi, kinubi, zeze, santuri, zumari, na sauti za ala nyingine za muziki,walianguka kifudifudi na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebkadneza aliisimamisha”.


Hapa tunaona kosa la kiongozi kutengeneza sanamu, linasababisha kosa la watu wanaokubali kuiabudu hiyo sanamu. Tumetafakari na kusadiki kuwa, kosa la kiongozi au mfumo, haliwaondolei hatia wanaomfuata kiongozi au kuufuata mfumo, hata kama watu hao walikula kiapo cha kutii maongozi ya kiongozi huyo na mfumo wake.


Mbele ya Mungu hakuna ile kanuni ya kuwajibika kwa pamoja. Kila mtu kwa dhamiri yake anawajibika mbele za Mungu. Kwa upande mwingine, pamoja na uwajibikaji wa mtu binafsi, Nabii Ezekieli anatukumbusha na kutuonya kuwa tusipoonya na kusimama katika zamu yetu, hatia na damu ya wasio na hatia, itadaiwa mikononi mwetu (Ezekiel 33: 8-9).


Adhimisho la kufufuka kwa Yesu Kristo (Pasaka) na maadhimisho ya miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa, yanatusukuma kutafakari utume wa Kanisa katika jamii kwa nyakati zetu. Tunaalikwa kupeleka ujumbe wa amani kwa watu wote na kusimama kwa ujasiri katika kuwasemea wasio na sauti katika jamii ili kuenzi roho ya Pasaka na Matengenezo katika nyakati zetu.


Kama Kanisa na kwa nafsi zetu mmoja mmoja, tunaitwa kwa upande mmoja, kufundisha, kushauri na kutia moyo. Kwa upande mwingine, tunaitwa kuonya, kukaripia, kukemea na kuelekeza kwa uvumilivu wote na upendo (2 Timotheo 4: 1-5).


Wajibu huu kwetu sisi maaskofu ni wito na utume usiokwepeka; na kwa watu wote wa imani, wajibu huu hauna mbadala. Tunaagizwa kuchochea ujenzi wa madaraja ya maridhiano katika upendo na amani, na kuwa kinyume na mifumo yote inayoendeleza chuki na marafakano. Kwa kufanya hivyo, imetupasa kusema wazi wazi ujumbe wa amani, upendo, heshima, utu, ustahimilivu na maelewano.


Mfumo wowote unaojengwa katika utii wa sheria bila upendo; heshima bila uhuru; na amani bila haki, unajengwa katika msingi usio imara. Kupuuza wito huu kuna madhara kwa jamii yetu. Ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga (Mathayo 7: 26). Tunasihi kwa machozi mengi, tuwe wajenzi wenye akili wajengao nyumba zao juu ya mwamba (Mathayo 7:24).


Mwamba tunaotakiwa kujenga taifa letu lenye dini mbalimbali, vyama mbalimbali, na makabila mbalimbali, umetajwa katika sala kuu ya taifa letu, yaani, “DUMISHA UHURU NA UMOJA”. Bila Uhuru hakuna umoja uwezao kuleta maendeleo; na bila umoja wa kitaifa, uhuru wetu hauleti amani endelevu. Kwa sababu ya nguvu ya dhamiri safi iliyo dira ya taifa letu, tunalazimika kumtii Mungu kuliko mwanadamu (Matendo 5:29).



B. TAIFA LETU NA AMANI YETU

Tunapoadhimisha sikukuu ya kukumbuka kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, tunatambua kuwa utume wa Kanisa letu katika taifa letu, unafanyika katikati ya changamoto kadhaa. Kwa kuwa Kanisa ni sehemu ya jamii, linaguswa na changamoto hizo. Katika kukaa pamoja na kuliombea taifa letu, sisi maaskofu wa KKKT, tumetafakari na kubaini changamoto hizo. Kwa njia ya salaam za Pasaka, tunaleta kwenu changamoto tatu ili ziongeze mzigo wa kuliombea taifa letu na viongozi wake.



1. Jamii na Uchumi

Kiini cha Utume wetu katika jamii kinatuingiza kwa nia njema katika maisha ya uchumi na mshikamano wa kijamii. Neno la Mungu linatufundisha kuwa “Mwanadamu hawezi kuishi kwa mkate peke yake” (Luka 4:4). Pia neno la Mungu linatuhakikishia kuwa Bwana wetu Yesu Kristo alikuja ili tuwe na uzima tele (Yohana 10:10). Tunawiwa katika umoja wetu wa ubaba, kuipongeza serikali yetu kwa jitihada inazofanya kuboresha maisha ya wananchi.


Tumeshuhudia jitihada na nia njema kuhusu uvunaji na umilikaji wa raslimali za nchi kwa manufaa ya taifa zima. Aidha, tunapongeza jitihada za ukusanyaji wa kodi ili kuiwezesha serikali kugharamia huduma za jamii. Hata hivyo, bila kukatisha tamaa jitihada hizo, tunawiwa kushauri yafuatayo:


I. Sekta binafsi na mashirika ya dini ni wadau wa maendeleo, si washindani wa serikali katika kuchangia maendeleo ya taifa. Mazingira yasiyo rafiki kuhusu wadau hawa, ni kikwazo kisicholeta mshikamano kati ya serikali na sekta binafsi na mashirika ya dini katika kuleta maendeleo. Jitihada za makusudi na za mara kwa mara zifanyike kuondoa dhana ya ushindani kati ya serikali na wadau hawa ili kuimarisha mahusiano mema kati ya serikali na sekta binafsi.


II. Ili mfumo wa ukusanyaji wa kodi uwe endelevu; jitihada za kukusanya kodi ziendane na elimu kwa mlipa kodi. Msisitizo wa uzalendo wa kulipa kodi uende sambamba na ustawi wa walipa kodi katika shughuli zao za biashara. Mivutano isiyo na tija kati ya walipa kodi (wafanya biashara) na mamlaka ya ukusanyaji wa kodi, inastawisha uadui unaopunguza makusanyo ya kodi na kujenga ushawishi wa rushwa. Mfumo wa kodi unaowafilisi wafanya biashara, haulengi kujenga uchumi wa viwanda.



III. Kutokana na ongezeko kubwa la vijana wasio na ajira; jitihada za wazi na za makusudi zifanyike ili msukumo wa uchumi wa viwanda ufikie matumaini yanayoshikika miongoni mwa vijana wasio na ajira. Sekta binafsi, wawekezaji na wadau wengine, wahakikishiwe usalama wa mitaji yao kisheria. Hili likifanyika ni kichocheo kizuri cha ujenzi wa viwanda.



IV. Uchumi wa viwanda (vidogo na vikubwa) uendane na uwekezaji katika sekta ya kilimo maeneo ya vijijini. Kilimo na ufugaji ndizo sekta zenye wigo mpana wa viwanda vinavyogusa maisha ya watanzania walio wengi. Utozaji holela wa kodi na ushuru wa mazao unakatisha tamaa wadau wa kilimo. Migogoro kati ya wakulima na wafugaji kwa upande mmoja, na wakulima/wafugaji na wawekezaji kwa upande wa pili, si kivutio cha uwekezaji katika sekta ya kilimo.



2. Maisha ya Siasa

Kwa umoja wetu katika utume, tunatambua siasa safi na uongozi bora kuwa ni misingi iliyoongoza maisha ya siasa katika taifa letu. Ujio wa vyama vingi mnamo 1992, haukuondoa umuhimu wa misingi hii bali ulipanua matumizi ya demokrasia iliyojengwa katika uhuru wa mawazo. Taifa ni mkusanyiko wa taasisi na watu mbalimbali, wenye lengo moja lakini kwa njia mbalimbali. Kutokana na wingi huu, taifa letu daima ni juu ya vyama, taasisi na makundi.


Taifa huongozwa na katiba iliyo kiini cha sheria zote. Taifa haliongozwi na ilani za vyama. Serikali haiongozwi na ilani za vyama. Serikali huongozwa na katiba, sheria, kanuni na mapokeo mema (misingi na tunu za taifa). Serikali husimamiwa na bunge huru lililo sauti ya wananchi. Wananchi ndilo chimbuko la madaraka ya bunge. Bunge halisimamiwi na ilani, chama chochote wala mtu awaye yote. Kwa umoja wetu na kwa nyakati zetu, hivi sasa tunashuhudia matukio yaliyo kinyume na tunu na misingi iliyolilea taifa letu. Baadhi ya matukio hayo ni:



I. Hofu iliyojengwa katika matukio halisi yakiwamo utekaji, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.


II. Kupungua na hatimaye kutoweka kwa uhuru wa kujieleza, kukusanyika, na kupata habari. Kwa mwenendo huu, kuna hofu kuwa hata uhuru wa kuabudu uko mashakani.

III. Kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge, Mahakama, na Tume ya Uchaguzi. Hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa.


IV. Kukosekana kwa mazingira ya haki na uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa katika chaguzi mbalimbali. Chaguzi zote zimeghubikwa na ubabe, vurugu, hila, na vitisho.

V. Utekelezaji wa mipango ya maendeleo wenye mwelekeo wa kiitikadi. Hatua hii imeimarisha ubaguzi wa kiitikadi katika taifa letu na kukuza migawanyiko.


VI. Kushamiri kwa chuki mioyoni mwa watu ambalo ni chimbuko la visasi, kukata tamaa, na ushiriki mdogo wa wananchi katika chaguzi na maisha ya siasa.

VII. Udhalilishaji wa kauli njema isemayo “Maendeleo hayana chama“. Udhalilishaji huu unafanyika kwa njia ya kutumia fedha nyingi katika chaguzi ndogo zinazotokana na watu wanaobadili vyama ili kuleta maendeleo. Tunajiuliza, kama maendeleo hayana chama, kwa nini mtu anajiuzuru chama fulani, eti kwenda kuleta maendeleo katika chama kingine? Mchezo huu unagharimu fedha nyingi na maisha ya watu wanaokufa, kujeruhiwa na uharibifu wa mali.

Mambo haya ni tishio linalohatarisha umoja na amani ya nchi yetu.



3. Masuala Mtambuka

Kanisa ni alama ya uwepo wa utume wa kuleta na kutunza matumaini katika jamii. Ukimya wa Kanisa katika masuala yanayoigusa jamii ni ukwepaji wa wajibu wake. Lakini pia sauti ya Kanisa isiyomilikiwa na mtu isipokuwa Mungu tu, ni chachu ya amani na matumaini. Kwa dhamiri safi inayotokana na utambuzi wa “Wakati wa Mungu“(Kairos) katika taifa letu, tunawiwa kutambua masuala mtambuka yanayogusa maisha ya watu kipekee na kwa njia nyingi na kuyatolea ushauri ufuatao:


I. Kuhitimisha mabadiliko ya mara kwa mara katika mfumo wa elimu nchini ili kuondoa mwanya wa kila mtendaji mkuu wa wizara kuja na sera yake. Elimu ni kitovu cha ustawi wa taifa, kisiwe kinachokonolewa chokonolewa kila wakati. Sekta zote nchini hujenga mafanikio yake katika mafanikio ya mfumo thabiti wa elimu.


II. Uwezeshaji wa vijana kupata mikopo ya elimu ya juu uwe shirikishi na usiokuwa na “ubaguzi” kati ya wanafunzi wa vyuo binafsi na wale wa serikali; sayansi na sanaa; wazazi maskini na wenye nafasi; waliosoma shule binafsi na wale wa shule za serikali, n.k. Kwa kuwa huu ni mkopo, jitihada ziwekwe zaidi katika urejeshaji wa mkopo huo kwa kuzingatia kuwa huu ni mkopo kwa mtoto siyo kwa mzazi.

III. Vyombo vya usimamizi wa sheria na utoaji haki vionekane vinatenda haki sawa kwa watu wote na makundi yote bila kuacha ishara za fadhila au kukomoana.


IV. Wajibu wa serikali kikatiba katika kulinda uhai wa raia wake, uonekane unatekelezwa bila kuacha mwanya wa kuituhumu serikali. Ukiachwa mwanya katika ulinzi wa uhai wa raia, waweza kutumiwa na mamluki kujichukulia sheria mkononi kwa niaba ya serikali. Damu isiyo na hatia ina madhara kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo. Mpaka sasa tumeshuhudia umwagaji wa damu unaotusuta sisi sote na mamlaka zote. Mungu anatusuta watanzania kama alivyomsuta Kaini:

“Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutokakatika ardhi” (Mwanzo 4:10).



V. Uhai wa mtu una thamani isiyopimika. Ni wajibu usiokwepeka kuulinda na kuutunza uhai kwa vitendo halisi. Endapo uhai umepotea katika mazingira yoyote, uchunguzi huru na wa haki ufanyike na taarifa zitolewe kwa wakati muafaka ili kujenga jamii yenye imani kwa serikali na vyombo vyake. Matukio ya mauaji ya askari wetu, mauaji ya raia, majaribio ya kuwaua wanasiasa, utekaji, na uteswaji visipochunguzwa na kutolewa taarifa, ni shina la hofu na uchungu katika jamii. Jamii iliyojaa hofu na uchungu, haiwezi kuwa na maendeleo wala kuwa na roho ya uzalendo.



VI. Ili kulipatia taifa letu ufumbuzi wa mambo yote tuliyotaja na kushauri kwa wakati huu na ujao; tunaisihi serikali ya awamu ya tano, kurejea mchakato wa upatikanaji wa KATIBA MPYA ya wananchi, iliyopendekezwa na wananchi kupitia Tume ya Warioba. Watanzania wengi wanaona na kuamini kuwa KATIBA MPYA ina majibu ya kukidhi mahitaji ya taifa letu kwa sasa na baadaye. KATIBA MPYA ni zao la utashi wa Watanzania kupitia tume ya Warioba iliyokuwa na uwakilishi mpana wa taifa letu.

VII. Aidha, tunawashauri raia wema, kwa njia za kidemokrasia kupitia majukwaa ya kikatiba yaliyo katika maeneo yao, kudai upatikanaji wa KATIBA MPYA. Itapendeza ikiwa KATIBA MPYA itapatikana kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano yatadumu iwapo kuna KATIBA MPYA inayolinda mazuri. Kiongozi mzalendo si mbadala wa KATIBA MPYA. Tanzania yenye amani na maendeleo ni tunda la itikadi zote, dini zote, makabila yote na makundi yote chini ya KATIBA MPYA.

C. HITIMISHO

Kufufuka kwa Yesu Kristo ni kiini cha Matengenezo ya Kanisa. Kwamba, katikati ya jamii iliyokata tamaa na kutawaliwa na hofu, Kristo alifufuka na kuleta matumaini mapya. Kwamba, katikati ya wasiwasi wa Kanisa kupoteza nguvu ya utume wake, Roho Mtakatifu aliongoza Matengenezo ya Kanisa. Kwa hiyo Matengenezo ni endelevu katika jamii ya watu na taasisi zao. Muasisi wa Matengenezo Dr. Martin Luther yungali analiwajibisha Kanisa kuzingatia utume wake unaoleta matumaini mapya kila siku. Waliobatizwa wote ni wamisionari tunaotumwa na Bwana wetu Yesu Kristo (Yohana 20:21). Imetupasa kuwa nuru na chumvi ya jamii na kuwa mawakala wa uhuru, umoja na amani.


Taifa letu lilipata uhuru mwaka 1961 bila kumwaga damu. Roho ile ile ya majadiliano na maridhiano iliyokuwamo ndani ya waasisi wa taifa letu, inatakiwa kila wakati. Uhuru ulioletwa kwa majadiliano, utunzwe na kulindwa bila ulazima wa kumwaga damu ya watanzania. Uhuru na Umoja ndizo ngao zetu zilizolitunza taifa kwa zaidi ya miaka 50.


Sisi tulio maaskofu kwa neema ya Mungu, tunaleta wito kwenu wenye imani katika dini mbalimbali, kuliombea taifa letu. Kuwaombea wote wenye madaraka ili wajaliwe hekima, busara na upendo kwa taifa na watu wake. Kupitia jumuia ndogo ndogo na sharika zote, waombee viongozi wetu ili Mungu awajalie na kuwatunuku kiu ya kutenda haki, kusikiliza kuliko kusema, kuelekeza kuliko kuamrisha, kuunganisha kuliko kutawanya, kupenda watu kuliko kutamani kupendwa na watu, kutamani kutumika kuliko kutumikiwa (Marko 10:45), kuheshimu kuliko kuheshimiwa.



Ujumbe wa Pasaka unatuhimiza kuthamini uhai. Bwana wetu Yesu Kristo alikubali kufa ili kuhifadhi uhai wetu. Kwa kufa kwake na kufufuka, amekomesha kifo na mawakala wake. Tunaitwa kuthamini uhai na kutoruhusu tena watu kuteswa na kuuawa. Kwa hekima yote na unyenyekevu, tunasihi tena, kwamba ikubalike kuwa hitaji la watanzania walio wengi kwa sasa ni KATIBA MPYA. Katiba Mpya ipatikane ili kukuza na kuimarisha mfumo wa utawala utakaolinda uhai wa watu, raslimali za nchi, tunu za taifa, uhuru wa mihimili ya dola, na uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi.



Tunawatakia Pasaka njema ya mwaka 2018, na Mungu awabarikini nyote. Ni sisi

1. Askofu Dkt. Fredrick O. Shoo, Mkuu, KKKT na Dayosisi ya Kaskazini

2. Askofu Dkt. Benson K. Bagonza, Dayosisi ya Karagwe

3. Askofu Dkt. Stephen I. Munga, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki

4. Askofu Dkt. Alex S. Mkumbo, Dayosisi ya Kati

5. Askofu Blaston Gaville, Dayosisi ya Iringa

6. Askofu Dkt. Abednego N. Keshomshahara, Dayosisi ya Kaskazini Magharibi

7. Askofu Andrew P. Gulle, Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria

8. Askofu Dkt. Emmanuel Makala, Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria

9. Askofu Chediel E. Sendoro, Dayosisi ya Mwanga

10. Askofu Charles R. Mjema, Dayosisi ya Pare

11. Askofu Elias Kitoi Nassari, Dayosisi ya Meru

12. Askofu Dkt. Solomon Massangwa, Dayosisi ya Kaskazini Kati

13. Askofu Jacob Mameo Ole Paulo, Dayosisi ya Morogoro

14. Askofu Michael Adam, Dayosisi Mkoani Mara

15. Askofu Isaya Mengele, Dayosisi ya Kusini

16. Askofu Job Mbwilo, Dayosisi ya Kusini Magharibi

17. Askofu Renard Mtenji, Dayosisi ya Ulanga Kilombero

18. Askofu Ambele Mwaipopo, Dayosisi ya Ziwa Tanganyika

19. Askofu Dkt. Alex G. Malasusa, Dayosisi ya Mashariki na Pwani

20. Askofu Dkt. Edward Mwaikali, Dayosisi ya Konde

21. Askofu Levis L. Sanga, Dayosisi ya Kusini Kati

22. Askofu Amon Mwenda, Dayosisi ya Ruvuma

23. Askofu Lucas Y. Mbedule, Dayosisi ya Kusini Mashariki

24. Askofu Amon Kinyunyu, Dayosisi ya Dodoma

25. Askofu Nicolaus Nsanganzelu, Dayosisi ya Mbulu

26. Askofu Mteule Isaack Kissiri Laiser, Dayosisi Teule ya Magharibi Kati

27. Askofu Mteule Wilson Sanga, Dayosisi ya Kusini Kati

Arusha, 15 Machi 2018

Askofu Mkuu KKKT :Hatukubali Kuzibwa Mdomo na Kiongozi Yeyote wa Kisiasa au Serikali

$
0
0
Askofu Mkuu KKKT :Hatukubali Kuzibwa Mdomo na Kiongozi Yeyote wa Kisiasa au Serikali
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo ameonya kwamba asitokee kiongozi yeyote nchini wa kisiasa au serikali ambaye atajaribu kuwazuia na kuwaziba midomo viongozi wa dini kutekeleza wajibu wao wa kukemea na kuonya juu ya maovu yanayoendelea hapa nchini.

Dk. Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, pia amesema kamwe kanisa halitanyamaza kimya kwa wanasiasa wenye tabia ya kutumia nafasi zao kuligawa taifa vipande vipande.

Alizungumza hayo  jana kwenye ibada maalumu ya kusataafu kwa aliyekuwa Mchungaji wa Usharika wa Masama Kati, John Mshau wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

“Wajibu wa viongozi wa dini ni kuonya na kukemea yale mabaya yanayoendelea nchini na si vinginevyo na kwamba  asijaribu kutokea mtu yeyote kuwazuia viongozi wa dini kufanya wajibu huo kwani ni sawa na kupingana na Mungu.

“Wajibu wetu ni kuonya, kushauri, kukemea na tunatenda hivyo, asijaribu kuja mtu yeyote kutuzuia kufanya hivyo kwani neno la Mungu linasema bwana hutegemeza wenye upole na huangusha chini wenye hila, hivyo sisi kama viongozi wa dini hatutakubali kunyamaza tutasema na kukemea maovu,” amesema

Pamoja na mambo mengine, Dk. Shoo aliwaonya viongozi wote wa kisiasa nchini kuacha kutumia vyama vyao kuligawa taifa na kwamba suala hilo halitaweza kuvumiliwa na viongozi wa dini na wataendelea kusema na kuonya.

Akitolea ufafanuzi waraka ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu 27 wa KKKT, Machi 15 Jijini Arusha alisema walifunga na kuomba Mungu kwa lengo la kupata ujumbe sahihi ili wautoe kwa waumini wa kanisa hilo na Taifa kwa ujumla na kwamba hawakukurupuka kutoa ujumbe huo.

Video: Rais Magufuli Aujibu Waraka wa Maaskofu Awataka Kuhubiri Viwanda

$
0
0
Rais Magufuli Aujibu Waraka wa Maaskofu Awataka Kuhubiri Viwanda
IKIWA ni siku tatu baada Baraza la Maaskofu wa KKKT kutoa waraka kwa Taifa, Rais Dkt. John Magufuli amewaomba maaskofu wajaribu kuhubiri kwamba Tanzania inahitaji viwanda ili Watanzania wapate ajira na kuokoa Sh. Bilioni 500 zinazopotea kila mwaka kununulia madawa.


Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akizindua wa Uzinduzi wa magari 181 ya Bohari ya Dawa (Medical Store Department – MSD).

Watu 53 Wafariki Katika Mkasa wa Moto Jumba la Kemerovo, Urusi

$
0
0
Watu 53 Wafariki Katika Mkasa wa Moto Jumba la Kemerovo, Urusi
Taarifa kutoka nchini Urusi ni kwamba moto umezuka katika jumba la kibishara na kusababisha watu 53 kufariki huku wengine 64 wakiwa hawajulikani walipo.

Taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya maeneo katika jumba hilo ambalo linapatikana katika mji maarufu wa uchimbaji wa makaa ya mawe Kemerovi, Serbia, nchini humo, yako hatarini kuanguka kabisa.

Katika watu 64 ambao hawajulikani walipo, 41 kati yao inasemekana kuwa ni watoto

Inaelezwa kuwa idadi kubwa ya waliopoteza maisha walikuwa kwenye ukumbi wa sinema. Chanzo cha moto hakijajulikana lakini polisi wamekwisha anza uchunguzi wa chanzo hicho cha moto.

Baba Daimond Aongea Mazito Sakata la Waziri Shonza na Daimond "Daimond Amefanya Makosa Kama Aliyowahi Kumfanyia Mimi"

$
0
0
Baba Daimond Aongea Mazito Sakata la Waziri Shonza na Daimond "Daimond Amefanya Makosa Kama Aliyowahi Kumfanyia Mimi"
SIKU chache baada ya staa ‘grade one’ wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kutoa maneno makali dhidi ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, baba wa msanii huyo, Abdul Juma ameibuka na kukumbushia ya nyuma (kufukua makaburi) kwa kusema amefanya makosa kama aliyowahi kumfanyia yeye!



Baba Diamond alisema amesikitishwa na kauli ya mwanaye dhidi ya Shonza.“Nimesikia yale mahojiano redioni yote na niseme kama mzazi sijapendezwa hata kidogo, kitendo chakumshambulia Shonza si kizuri hata kidogo na sijui kwa nini aliamua kutoa lugha kali kiasi kile,” alisema baba Diamond.



Baba Diamond alienda mbali zaidi kwa kusema kwamba, alichokifanya mwanaye ni muendelezo wa kileambacho aliwahi kumfanyia kipindi cha nyuma.“Tabia kama hii ya kutoa lugha ya dharau hajaianza jana wala leo, nakumbuka kabisa alishawahi kunifanyia kipindi cha nyuma hadi nikakata tamaa na kujihisi sina mtotokama unakumbuka ilifi kia kipindi nikasema hata nikifa asinizike, ameendeleza tabia hiyohiyo kwa waziri.”


Diamond.

“Haya na waziri Mwakyembe ameingilia kati na kusema hakufurahishwa na kitendo hicho, naungana naye kabisa si busara Diamond kushindana na serikali na kama ana ushauri basi autoe kistaarabu.“Kama mzazi amenikwaza sana na sijafurahishwa hata kidogo, ninachomuomba kwa sasa amfuate Shonza na amuombe msamaha,atambue yeye ni sehemu ya kioo kinachoangaliwa na jamii,” alimaliza baba Diamond.



Hivi karibuni, Diamond akifanyiwa mahojiano katika Kipindi cha The Playlist cha Radio Times FM kutokana na kufungiwa kwa nyimbo zake mbili; Waka Waka na Hallelujah, alitoa maneno makali akiwa na jazba dhidi ya Naibu Waziri Shonza kuwa hajawahi kusaidiwa na waziri huyo chochote kwenye muziki wake, anashangaa kumuona anakurupuka na kumfungia nyimbo zake.


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza.

Diamond alienda mbali zaidi na kusema kuwa, haogopi hata kwenda jela atakwenda ila ataitetea Bongo Fleva kwani anaijua kuliko anavyoijua waziri huyo na kwamba kitendo cha kumfungia nyimbo zake, hakukifanyia utafi ti kwanza.



Baada ya kauli hiyo, waziri Shonza alijibu amesikia malalamiko ya Diamond lakini hawezi kumjibu kwa sababu zipo taratibu za kufuata ikiwemo kuandika barua kama anaona hajatendewa haki Februari 28, mwaka huu, TCRA iliandika barua kwa vituo vya redio na runinga ikiviagiza visitishe kucheza nyimbo 15 za wasanii zikiwemo mbili za Diamond kutokana na kuwa na maudhui ambayo ni kinyume na maadili na kanuni za Huduma za Utangazaji(mwaka 2005).

Huyu ndo Mpenzi Mpya wa Wema Sepetu Afunguka Kuhusu Uhusiano Wake

$
0
0
Huyu ndo Mpenzi Mpya wa Wema Sepetu Afunguka Kuhusu Uhusiano Wake
Hivi Karibuni zilisambaa picha na Video zianzomuonesha muigizaji Wema Sepetu akiwa na mwanaume mwingine amabaye alidaiwa kuwa ndo mpenzi wake mpya kutokana na wawili hao kuonekana wakiwa pamoja

Mwanaume huyo ambaye jina lake maarufu mtandaoni ni Rahul amesema kwamba yeye na Wema ni washikaji wakawaida anashangaa maneno yanapotoka kwani amemjua Wema sasa ni miaka 7 lakini hawana uhusiano wa kimapenzi na isitoshe kaongezea kwa kusema Wema ana mapenzi ya dhati kwa watu wake.

Nisha Azama kwenye Penzi Zito la Brown wa Wolper Wajiachia Mtandaoni Wakifanya Yao

$
0
0
Nisha Azama kwenye Penzi Zito la Brown wa Wolper Wajiachia Mtandaoni Wakifanya Yao
Msanii wa Filamu Bongo, Nisha kwa sasa ni furaha tele usoni mwake mara baada ya kuingia katika mahusiano na aliyekuwa boy friend wa Jacqueline Wolper, Brown.

Wawili hao wameonekana kuwa karibu zaidi kupitia mitandao ya kijamii na hii baada ya wote wawili mahusiano yao ya awali kuvunjika.

Utakumbuka Nisha alikuwa akidate na kijana ambaye baadaye alikuja kudai kuwa amehamishia penzi lake kwa muimbaji Snura, hata hivyo Snura alikanusha hilo, hivyo hivyo kwa Brown alitoka kuachana na Jacqueline Wolper.

March 12 mwaka huu Nisha aliposti video Instagram akionekana akiilia huku wimbo wa Diamond ‘Sikomi’, ukisikika, video hiyo ilitafsiriwa kuwa mrembo huyo ametendwa na mapenzi kutokana na maudhui ya wimbo huo ila kwa sasa kwa Brown ni kinyume cha hapo.

Rais Magufuli Amwita Waziri na Viongozi Hawa Vilaza

$
0
0
Rais Magufuli Amwita Waziri na Viongozi Hawa Vilaza
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kuwaambia viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuwa vilaza baada ya kugundua Mamlaka ya Chakula na Dawa, TFDA imekuwa kikwazo kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD).


Rais Magufuli amesema hayo leo Machi 26, 2018 wakati akizundua magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ambayo yanategemewa kuanza kusafirisha dawa mijini na vijinini, akiwa kwenye uzinduzi huo Rais Magufuli alipokea malalamiko kuwa zipo baadhi ya taasisi za serikali zimekuwa zikichangia kukwamisha ucheleweshwaji wa dawa ambazo zinaletwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

"Nimesikia saa zingine kunakuwa na ucheleweshwaji kati ya taasisi fulani fulani ndani ya serikali taasisi ya vyakula TFDA, mnaleta madawa halafu mnashindwa kupata kibali bandarini, madawa yanacheleweshwa inawezekana 'expire date' yake inafika madawa bado yamezuiliwa pale bandarini. Mimi atakae zuia madawa haya niambieni ili nijue chombo gani cha serikali, niambieni tu huyo aliyezuia nione ili na mimi nimzuie yeye moja kwa moja kuna mambo mengine ni rahisi sana wala msilalamike bali mwambie Waziri au Katibu Mkuu" alisema Rais Magufuli

Magufuli aliendelea kuweka wazi kuwa watu ambao wanakwamisha na kuchelewesha dawa kutoka ni watu ambao pia wanatoka katika wizara hiyo hiyo wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

"Hata aliyempa nguvu ya kuzuia dawa wapo chini ya wizara yenu yaani ni nyinyi wenyewe, basi nyinyi vilaza sasa mtu yupo chini yenu, yaani mtu anayezuia yupo kwako anayezuiliwa yupo kwako bado mnakaa mnaimba nini. Mimi nataka haya niyashughulikie unajua mambo mengine mnakwamishana nyinyi wenyewe kama ni TRA mwambie Katibu Mkuu, mwambie Waziri wa Afya, mwambie Waziri wa Fedha tufike mahali tusikwamishane, kwa sababu anaweza akawa amekwamisha madawa yenu lakini madawa ya mtu binafsi anayaruhusu siku hiyo hiyo sasa hili ni lenu wala halihitaji kufika kwangu" alisisitiza Magufuli

Nyosso: Najiandaa Kurudi Kuiokoa Timu Yangu

$
0
0
Nyosso: Najiandaa Kurudi Kuiokoa Timu Yangu
BEKI wa kati wa Kagera Sugar, Juma Nyosso, amefunguka kuwa, kwa sasa amebakiza mechi moja tu kati ya zile tano alizotakiwa kuzikosa baada ya kusimamishwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tan­zania (TFF), hivyo ana­jiandaa kurudi kuiokoa timu yake hiyo.

Nyosso alisimamish­wa kucheza mechi tano za Ligi Kuu Bara baada ya kukutwa na kosa la kumshambulia shabiki wakati timu yake ya Kagera Sugar ilipokubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Simba, Janu­ari 22, mwaka huu.



Mechi alizokosa Nyos­so kutokana na adhabu hiyo na matokeo yalivy­okuwa ni hizi; Kagera 1-1 Singida United, Kagera 2-1 Majimaji, Yanga 3-0 Kagera na Kagera 1-0 Mwadui. Mechi ijayo dhidi ya Ndanda, ndiyo ya mwisho.

Kagera Sugar ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 21, imebakiwa na mechi nane ambazo inatakiwa kuzitumia vizuri ili isishuke daraja mwishoni mwa msimu huu.



Akizungumza na Championi Jumatatu, Nyosso amesema: “Mechi ijayo dhidi ya Ndanda ndiyo itakuwa ya mwisho katika adhabu yangu, hivyo najiandaa kurejea kuipambania timu yangu ili tuweze kubaki ligi kuu.

“Kwa sasa hatupo kwenye nafasi nzuri, hivyo ni lazima tujipange kuhakikisha tunapam­bana katika mechi hizo nane zilizosalia tu­nakuwa salama.”

Sakata la Daimond, Waziri Shonza Lawaibua Wasanii Waomba Kukutana na Mwakyembe

$
0
0
Sakata la Daimond, Waziri Shonza Lawaibua Wasanii Waomba Kukutana na Mwakyembe

Wakati sakata la mwanamuziki Diamond Platinumz kumlalamikia Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kutowatendea haki wasanii likiendelea kuwa mjadala mitandaoni, Chama wa Wasanii wa Bongofleva (Tuma) kitakutana na waziri wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe wiki hii.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumatatu Machi 26, 2018, katibu wa chama hicho, Samuel Andrew maarufu Braton amesema sakata la Diamond na naibu waziri huyo ndio sababu kuu ya kuomba kuonana na Dk Mwakyembe.

Machi 19, 2018 Diamond wakati akihojiwa na Kituo cha Redio Times cha jijini Dar es Salaam, alilaumu hatua ya Serikali kuzifungia nyimbo 15 mwezi uliopita, zikiwamo mbili za kwake.

Diamond hakuishia katika mahojiano hayo yaliyoongozwa na mtangazaji Omary Tambwe, Machi 20, 2018 kupitia mtandao wa Twitter alimjibu naibu waziri huyo akisema ametumia njia hizo kumjibu kwa kuwa naye alitumia hizo hizo.

Katika maelezo yake Braton amebainisha kwamba awali walipanga kuonana na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kikao ambacho ilikuwa kifanyike leo.

Hata hivyo, amesema baada ya kushauriana na wenzake waliona ni vema kikao hicho akawepo na Dk Mwakyembe kwa maelezo kuwa hata Basata watapeleka taarifa za mazungumzo yao wizarani.

“Unapoongelea waziri ndio mtu wa mwisho kuongea na kutolea uamuzi wa tutakachozungumza, hivyo tukienda Basata ni kama tunazunguka tu wakati kitu tunachohitaji sasa ni utekelezaji na si taarifa,”amesema.

Alipoulizwa kama Shonza atakuwepo kwenye mkutano huo, Braton amesema hana uhakika japo vikao vingi vya wasanii huwa anakuwepo na hata hicho wangependa awepo pia.

Mwanamke Yamkuta Mazito Wakati Akitafuta Utajiri kwa Mganga wa Kienyeji

$
0
0
 Mwanamke Yamkuta Mazito Wakati Akitafuta Utajiri kwa Mganga wa Kienyeji
KUTAFUTA utajiri kwa njia za mkato hapa duniani kumewaponza wengi! Mama ambaye ni mfanyabiashara, Tabu Mwelege, mkazi wa Kijiji cha Kijiweni wilayani Sengerema jijini Mwanza, yamemkuta mazito akiwa kwa mganga wa kienyeji almaarufu sangoma, Risasi Jumamosi lina kisa na mkasa.



Tukio hilo lilijiri maeneo hayo Februari 25, mwaka huu ambapo Tabu alijikuta akiwa na majeraha kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake na kuwa katika hali mbaya baada ya kuunguzwa kwa maji ya moto alipokwenda kwa sangoma huyo ili kukuza biashara yake na kupata mali.



TABU ASIMULIA MKASA

Akilisimulia Risasi Jumamosi mkasa huo akiwa katika Hospitali ya Bugando jijini hapa huku akiwa na majeraha hayo, Tabu alieleza:“Nilikuwa nafanya biashara zangu ndogondogo pale Sengerema. “Nilifanya biashara kwa muda mrefu sana bila mafanikio.



Siku moja nilikwenda kwa mganga wa kienyeji aliyekuja pale kijijini ili nipate dawa za kukuza biashara zangu.“Kweli nilipofika kwa huyo mganga kulekule Sengerema,nilimweleza shida zangu.“Yule mganga aliniambia kama tatizo langu ni hilo nisiwe na shida kabisa na niondoe shaka kwani nilikuwa nimefika na kila kitu kitakuwa sawa.



“Nakumbuka pale kwa mganga siku ile kulikuwa na watu wengine ambao walikuwa wakihudumiwa. Ilinibidi nisubiri hadi zamu yangu ilipofi ka huku nikiwa na matumaini makubwa ya kufanikisha lengo langu la kukuza biashara zangu na kupata utajiri. “Yule mganga alikuwa mgeni pale kijijini kwetu.



Aliniambia ananitengenezea dawa nzuri itakayonisaidia kwenye kazi zangu. “Nakumbuka aliweka mawematatu kwenye maji na kuyachemsha yale maji hadi yakachemka kabisa kama mtu anayetaka kupika ugali.“Hapo yule mganga aliniambia nilale chali ambapo aliniwekea jiwe la kwanza kifuani. “Baada ya kuniwekea lile jiwe la moto sana, aliniwekea yale mawe aliyokuwa akichemshia maji.



“Aliendelea hivyo hadi mawe yote matatu yakaisha.Wakati huo nilikuwa naumia sana, lakini nilikuwa navumilia. “Baada ya lile jiwe la tatu,ndipo nikaanza kusikia maumivu makali mno ambayo sijawahi kuyapata. Wakati huo nilikuwa nimefunikwa shuka ili ule mvuke usitoke nje.



Hapo ndipo nikajikuta nimeungua mikono, kifuani, shingoni na mdomoni, nikapewa huduma ya kwanza ikiwemo kukimbizwa hospitalini kule Sengerema kabla ya kuhamishiwa hapa, lakini namshukuru Mungu naendelea vizuri na matibabu hapa Bugando,” alisimulia Tabu akiugulia maumivu makali hivyo kushindwa kuendelea na mahojiano na Gazeti la Risasi Jumamosi.



MWANAYE NAYE

Baada ya mama mtu kuishia hapo, mwanaye Tatu Kakulu aliendelea kusimulia kuwa, baada ya kupata taarifa ya mama yao kuunguzwa na mganga huyo walikwenda kumchukua kasha kumuwahisha hospitalini. Alisema baada ya kuhamishiwa Hospitali ya Bugando, mama yake anaendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.



SANGOMA ATIMKA,ASAKWA

Alipoulizwa kilichompata mganga huyo baada ya kutekeleza uhalifu huo, Tatu alisema kuwa,sangoma huyo alitimkia kusikojulikana kwani alikuwa mgeni kijijini hapo na alifi ka pale kwa ajili ya kutoa huduma ya uganga tu. Alisema kuwa, tukio hilo walikwenda kuliripoti kwenye Kituo cha Polisi cha Katunguru wilayani Sengerema ambapoanasakwa na polisi.



KAMANDA MSANGI

Risasi Jumamosi lilimtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, ACP Ahmed Msangi ili kuthibitisha tukiohilo lakini jitihada ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa

Grace Mugabe Atuhumiwa na Wizi wa Nyara za Serikali

$
0
0
Grace Mugabe Atuhumiwa na Wizi wa Nyara za Serikali
Uchunguzi umefanywa siku za hivi karibuni dhidi ya Mke wa Rais Mstaafu wa Zimbabwe, Grace Mugabe kutokana na tuhuma zinazomhusisha na biashara haramu nchni humo ya nyara za serikali.

Inaelezwa kuwa Grace amehusika katika biashara ya Pembe za Ndovu yenye thamani ya mamilioni ya dola za Kimarekani.

Anatuhumiwa kufanya biashara hiyo kipindi akiwa bado ‘First Lady’ wa nchi hiyo na kwamba alituma vipande vya nyara hizo kama zawadi kwa watu fulani wa hadhi ya juu huko Mashariki ya Kati na Asia.

Uchunguzi na taarifa hiyo imetolewa na Mamlaka ya Hifadhi za Wanyamapori wa nchini Zimbabwe na kuwasilishwa na Msemaji wake Tinashe Farawo.

"Wataandaliwa Watu Watakaofyatua Risasi"- Mwigulu

$
0
0
Wazili Nchema Atoa Onyo Kali Kuhusu Maandamano

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali inazuia kuwepo kwa maandamano ili kutoruhusu watu wachache wanaotamani Tanzania wavurugane kuharibu taswira ya nchi.

Akizungumza katika harambee iliyoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Masaka dayosisi ya Pare, wilayani Same, Mh. Nchemba amesema kuwa katika maandamano hayo wapo watu watakaofanya vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na hata kufyatua risasi ili ionekane kwamba nchi inaua watu.

"Wapo wanaotamani tuvurugane na tunapowaeleza wananchi wanaweza kujiuliza kwanini tunazuia maandamano wakati wapo watu wanaofanya mazoezi na ni kwa sababu hatutaki kuruhusu watu watuvuruge,’’ Dk Nchemba

Ameongeza kuwa wapo watu wenye mitazamo mibaya zaidi ambao wataiba na pia wataandaliwa watu watakaofyatua risasi ili ionekane watu wameuawa katika maandamano.

Amesisitiza kuwa lengo la kuzuia maandamano ni baada ya kuangalia kwa jicho la tatu maandamano hayo hivyo raia na vyama vya siasa wawaelewe kwani hawana nia ya kuminya uhuru wao ambao upo kwa mujibu wa katiba.

‘’Tunaangalia sura ambayo adui anaweza kupitia, wasione majira haya ni ya kawaida kuna mahali tumegusa hivyo hawafurahi na ndio sababu haya mambo yanatokea hivyo tunaomba msichukulie kuwa ni vitu vyepesi vyepesi bali mpanue mitazamo yenu mnapoona masuala haya yanapojitokeza,’’ ameongeza.

Irene Amvaa Wema Sepetu Amtupia Dongo Zito Kisa ni Diamond

$
0
0
Irene Amvaa Wema Sepetu Amtupia  Dongo Zito Kisa ni Diamond
Video vixen aliye jizolea umaarufu baada ya kuonekana kwenye video ya ‘Kwetu’ ya msanii Rayvanny Irene, amemtolea povu zito staa wa Bongo movie Wema Sepetu huku ikidaiwa kisa ni penzi la Diamond.

Tangu Zari aweke wazi kuwa kaachana na Diamond na kuwa single Kumekuwa na tetesi nyingi sana kwenye social media juu ya nani hasa anayechukua nafasi ya Zari na moja kati ya Wanawake waliotajwa kuwa na uhusiano na Diamond kwa sasa ni Irene na Wema.

Kuna stori ili trend sana kwenye mitandao ya kijamii siku za nyuma kidogo ambapo ilisemekana kuwa Irene na Wema wamepeana kichapo cha maana baada ya kugongana Madale nyumbani kwa Diamond.

Stori hiyo ilidai kuwa Diamond anatoka na Irene na Wema kwa wakati mmoja na wikiendi hii Irene kamtupia dongo Wema ambapo amemcheka kuwa anajiita African beauty wakati hata kiwanja hana!.

African beauty ni wimbo mpya wa Diamond na siku wimbo huo ulipotoka wasanii mbali mbali wa WCB akiwemo Harmonize alimtunuku Wema jina la African beauty jambo ambalo lilimfanya Wema ajitambe kuwa ni African beauty.

Fununu za Irene kuwa na Mahusiano na Diamond zilianza siku nyingi sana wakati bado Diamond yuko na Zari ingawa Diamond alikuwa anakataa kuwa hana Mahusiano naye.

Hii Hapa Tarehe ya Mechi ya Simba, Yanga

$
0
0
Hii Hapa Tarehe ya Mechi ya Simba, Yanga
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia Mtendaji Mkuu, Boniface Wambura leo imetangaza rasmi tarehe ambayo Watani wa Jadi (Simba SC na Yanga SC)watacheza.

Timu hizo sasa zitacheza tarehe 29 Aprili 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi ambayo Simba atakuwa mwenyeji wa pambano hilo.

Awali Bodi ya Ligi ilikuwa haijaweka tarehe hiyo wazi kutokana na mambo mbalimbali kuingiliana na kufanya ratiba ya mchezo huo kutopangwa kwa wakati.

Timu hizi zenye wafuasi wengi nchini, zilikutana Oktoba 28 2017 kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi na kwenda sare ya bao 1-1, huku wafungaji wa mabao hayo wakiwa ni Shiza Kichuya upande wa Simba na Obrey Chirwa kwa Yanga.

Video: Hivi Ndivyo Wema Alivyoonyesha Msambwanda Wake Akiwa Anaogelea

$
0
0
Video: Hivi Ndivyo Wema Alivyoonyesha Msambwanda Wake Akiwa Anaogelea
MSANII wa Bongo Movies, Wema Sepetu amezua gumzo baada ya kuachia msambwanda wake LIVE wakati akiogelea pamoja na kaka yake Diamond Platnumz, Rommy Jones.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images