Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Mbowe, Mnyika. Mashinji na Viongozi Wengine Chadema Wang'ang'aniwa na Polisi Wapelekwa Rumande

$
0
0
Mbowe, Mnyika. Mashinji na Viongozi Wengine Chadema Wang'ang'aniwa na Polisi Wapelekwa Rumande
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe na baadhi ya viongozi wengine waandamizi wa chama hicho akiwepo Katibu Mkuu Dkt Vincent Mashinji, John Mnyika, Salum Mwalimu na Ester Matiko wamewekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha polisi Dar es Salaam.


Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha hilo na kusema kuwa viongozi hao wamewekwa mahabusu leo Machi 27, 2018 baada ya kuripoti Kituo Kikuu Cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao.

“Viongozi Wakuu wa Chama pamoja na wabunge waliokuwa wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao, wamewekwa mahabusu. Polisi hawajaeleza sababu ya kufanya hivyo. Mawakili wetu wanashughulikia. Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi,” alisema Makene.

Mwakyembe Atangaza Kanuni za Mitandao, Radio na TV

$
0
0
Mwakyembe Atangaza Kanuni za Mitandao, Radio na TV
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametangaza kanuni mmbalimbali za sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.


Kanuni hizo ni zile za sheria ya Mawasilinao ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Habari za Mtandaoni) ya mwaka 2018 ijulikanayo kama The Electronic and Postal Communications (Online Content) Regulations, 2018.

Kanuni nyingine ni zile za sheria ya Mawasilinao ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Utangazji katika Redio na Runinga) ya mwaka 2018, ijulikanayo kama The Electronic and Postal Communications (Radio and Television Broadcasting Content) Regulations 2018.

Kanuni hizo ambazo zimetengenezwa chini ya kifungu cha 103 cha sheria ya EPOCA zimesainiwa na Waziri Mwakyembe ambaye ndiye mwenye dhamana ya maudhui ya Habari na Utangazaji.

Video: Siko Vizuri Kiakili, Barua Nimeona Kwenye Mitandao- Abdul Nondo

$
0
0
Video: Siko Vizuri Kiakili, Barua Nimeona Kwenye Mitandao- Abdul  Nondo
Leo March 27, 2018 Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo ameongea na waandishi wa habari baada ya kufika Jijini Dar es salaam akiwa natokea mkoani Iringa ambapo alikuwa anakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Hakimu mkazi Wilaya ya Iringa.


Wakili Aliyeidhinisha Kiapo cha Odinga Azuiliwa Uwanja wa Ndege Nairobi

$
0
0
Wakili Aliyeidhinisha Kiapo cha Odinga Azuiliwa Uwanja wa Ndege Nairobi
Wakili wa upinzani aliyeidhinisha kiapo cha Bw Raila Odinga alipokuwa anajiapisha kuwa 'Rais wa Wananchi' mwezi Januari bado amekwama katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi.

Bw Miguna Miguna alijaribu kurejea Kenya Jumatatu lakini akazuiwa kuingia baada yake kudaiwa kutowasilisha pasipoti ya Canada ambayo ilitumiwa kumsafirisha kwa nguvu hadi Canada.

Taarifa zinasema Bw Miguna, ambaye pasipoti yake ya Kenya ilitwaliwa na polisi kabla ya kuondolewa kwake Kenya mwezi jana, alikuwa ametakiwa kuwasilisha ombi la kupata visa ya kukaa Kenya kwa miezi sita kwa kutumia pasipoti hiyo yake ya Canada.

Alikataa jaribio hilo na badala yake kutoa kitambulisho chake cha taifa kuonesha kwamba yeye ni Mkenya na kutaka aruhusiwe kuingia.

Bw Miguna, aliyekuwa amewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa nane adhuhuri, alikesha kwenye uwanja huo.

Maafisa walijaribu kumsafirisha kutoka uwanja huo kwa kutumia ndege ya shirika la Emirates ambayo ilikuwa inaelekea Canada kupitia Dubai.

Wakili wa upinzani James Orengo, seneta ambaye majuzi alichaguliwa kuwa kiongozi wa upinzani Bunge la Seneti, ameambia Reuters kwamba maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia ndio waliojaribu kumlazimisha Bw Miguna kupanda ndege hiyo iliyokuwa inaondoka.

Video iliyopeperushwa moja kwa moja na runinga ya kibinafsi ya Citizen ilimuonesha Bw Miguna akiwa kwenye lango la ndege akiwaambia wahudumu: "Siendi popote, hamuwezi kuniondoa kutoka kwa nchi yangu kwa nguvu."

Bw Orengo ameambia Reuters kwamba maafisa hao wa polisi baadaye walimuondoa mwanasiasa huyo kutoka kwenye ndege hiyo na kumzuilia kwa muda katika afisi za uhamiaji katika uwanja huo wa JKIA.

Baadaye asubuhi, walimhamishia kituo cha polisi cha uwanja huo na kuendelea kumzuilia.

Odinga kufika uwanja wa ndege
Bw Odinga alikuwa amefika uwanjani humo Jumatatu usiku kujaribu kutatua mzozo huo.

Kwa mujibu wa Bw Orengo, Bw Odinga alikuwa ametoa wito kwa serikali kumrejeshea Miguna pasipoti yake ya Kenya.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Uhamiaji mapema Jumanne ilisema Bw Miguna alianza "kuzua fujo na kulalamika" uwanja wa ndege na kwamba alikuwa anataka kuruhusiwa kuingia Kenya bila kuidhinishwa na maafisa wa uhamiaji.

Wizara hiyo imesema inafanikisha utaratibu wa kumuwezesha Bw Miguna kuwasilisha tena ombi la kuwa raia wa Kenya.

Mkurugenzi wa Idara ya Uhamiaji Joseph Munywoki kwenye taarifa alisema: "Badala ya kuonesha hati za kusafiria alizotumia kwenda Canada, Miguna alianza kuzua fujo na kulalamika akisema kwamba yeye ni Mkenya na anafaa kuruhusiwa kuingia Kenya bila kupitia kwa meza ya idara ya uhamiaji kama inavyotakiwa kwa abiria wote wanaowasili bila kujali uraia wao."

"Hatujamzuia kuingia Kenya, tunamtaka tu afuate utaratibu kama watu wengine wote," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani

Idara ya uhamiaji ya Kenya imekariri kuwa Miguna alipoteza uraia wa Kenya mwaka 1988 alipopewa uraia wa Canada wakati alipokuwa ni kinyume cha sheria kuwa na uraia wa nchi mbili nchini Kenya.

Kuzuiliwa kwa Bw Miguna kumejadiliwa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii Kenya, baadhi wakiunga mkono hatua hiyo lakini wengine wakiwashutumu maafisa wa uwanja wa ndege na serikali.

Bw Miguna alikamatwa na polisi kwa mchango wake katika kuapishwa kwa Bw Odinga kuwa "rais wa wananchi", hafla iliyofanyika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi mnamo 30 Januari.

Bw Miguna, ambaye pia ni wakili, ndiye aliyetia saini hati ya kiapo ya Bw Odinga.

Serikali ilikuwa imeeleza hatua hiyo ya kiongozi huyo wa upinzani kuwa uhaini wa hali ya juu.

Bw Odinga anadai kwamba alimshinda Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu wa 8 Agosti ambao matokeo yake yalifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu kwa sababu ya kutokea kwa kasoro nyingi.

Mahakama iliamuru uchaguzi mpya ufanyike lakini Bw Odinga akasusia uchaguzi huo mnamo 26 Oktoba.
Polisi nchini Kenya wamejipata tena wakishutumiwa kwa kuwapiga na kuwajeruhi waandishi wa habari wakiwa kazini.

Polisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia waliwashambulia waandishi wa habari wa magazeti na televisheni na wapiga picha Jumatatu usiku walipokuwa wakifuatilia taarifa kuhusu kurejea Kenya kwa Bw Miguna.

Maafisa hao, ambao hawakufurahishwa na ufuatiliaji wa vyombo vya habari wa taarifa ya kurejea kwa mwanasiasa huyo waligeuza hasira zao kwa waandishi wa habari na kuwaumiza baadhi yao.

Mpigapicha wa televisheni ya NTV aliachwa akiwa na majeraha yaliyokuwa yanavuja damu huku kamera na vifaa vyake vya matangazo ya moja kwa moja vikiharibiwa na maafisa hao wa usalama.

Alikuwa akitangaza tukio hilo moja kwa moja alipovamiwa na polisi

Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Citizen Steven Letoo pia alijeruhiwa na vifaa vyake vikachukuliwa.


Amevitolea wito vyombo vya habari kuchukua hatua za kisheria dhidi ya maafisa husika na makamanda wao.

Taifa Stars Kuvaana na DR Congo Leo

$
0
0
Taifa Stars Kuvaana na DR Congo Leo
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti Premium Lager, ya Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), inatarajia kucheza mchezo wake wa pili wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Jamhuri ya Demokrasia Congo hii leo siku ya Jumanne Machi 27, 2018, kwenye uwanja wa Taifa.

Huu ni mchezo muhimu katika tarehe zilizopo kwenye kalenda ya FIFA ambapo kocha msaidizi, Hemed Morocco tayari amesema wanauchukulia kwa uzito mkubwa na nia ni kufanya vizuri.

Katika mwezi huu wa Machi, Taifa Stars ilipanga kucheza mechi mbili za kirafiki, kwanza ikiwa tayari imechezwa nchini Algeria dhidi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo.

Kikosi hicho cha Taifa Stars kitaongozwa na nahodha wake Mbwana Samatta anayecheza katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Mbali na Samatta, wachezaji wengine waliyoitwa kwenye kikosi na kocha Salum Mayanga ni pamoja na Aishi Manula, Ramadhan Kabwili, Mohamed Abdulrahman, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Abdi Banda, Kelvin Yondan, Himid Mao Simon Msuva, Mudathir Yahya, Mbwana Samatta, Said Ndemla na Shiza Kichuya.

Wengine ni Hassan Kessy, Erasto Nyoni, Shaban Chilunda, Ibrahim Ajib, Yahaya Zayd, Mohamed Issa, Rashid Mandawa na Faisal Salum.

RC Makonda Awakalia Kooni Wanaume Wanaotelekeza Watoto "Ukimpa Mimba Mwanamke Dar Ujipange kwa Matunzo"

$
0
0
RC Makonda Awakalia Kooni Wanaotelekeza Watoto "Ukimpa Mimba Mwanamke Dar Ujipange kwa Matunzo"
Jopo la Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Maafisa Ustawi wa Jamii, Wanasheria pamoja na Askari Polisi kutoka Dawati la Jinsia  wamemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kuwa wamejidhatiti vyema kuwasikiliza kinamama waliotelekezwa na hawapatiwi pesa ya matunzo ya mtoto kwenye zoezi la siku tano za kuwapatia msaada wa kisheria kinamama hao linalotaraji kuanza April 09 Mwaka huu.
Akizungumza na wataalamu hao RC Makonda amesema tatizo la wamama waliotelekezwa ni kubwa na limekuwa likisababisha kinamama na watoto kuishi maisha ya tabu na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani na vizazi vya watoto wenye chuki na Baba zao.
RC Makonda amesema lengo la Zoezi hilo sio ugomvi bali ni kumwezesha Mtoto kupata mahitaji ili aweze kuitumia vyema fursa ya elimu bure chini ya serikali ya awamu ya tano.
Aidha RC Makonda amewahimiza wataalamu hao kuhakikisha wanawasikiliza kinamama kwa umakini na kusimamia haki pasipo upendeleo.
Pamoja na hayo RC Makonda amesema wapo kinababa ambao wameanza kutoa fedha ya matunzo ya Mtoto baana ya kusikia tangazo ambapo amewasihi kinamama hao kufika April 09 kwaajili ya kuonana na wataalamu ili waweke makubaliano kwenye mfumo rasmi wa kimaandishi.
IFIKE HATUA MWANAUME UKIMPA MWANAMKE UJAUZITO BILA MPANGILIO AOGOPE KAMA ILIVYO KWENYE UBAKAJI

Nileteeni Mapendekezo ya Kutumbua Wasiofaa- Rais Magufuli

$
0
0
Nileteeni mapendekezo ya kutumbua wasiofaa- Rais Magufuli
Rais Dkt. John Magufuli amuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aitishe kikao cha Mawaziri wote ili wajadili na kutafuta majawabu hoja zilizomo katika ripoti ya CAG aliyokabidhiwa hii leo, pia na kumtaka apeleke mapendekezo ya watu anaotaka watumbuliwe.


Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo (Machi 27, 2018) wakati alipokuwa anapokea ripoti kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Profesa Musa Assad hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

"Kwa ujumla Waziri Mkuu nimekupa hizi 'document' kakae kikao na Mawaziri wako wote, Makatibu wakuu, Wakuu wa Taasisi mbalimbali katika kila maeneo, kila eneo likazungumziwe wazi ili hayo maeneo yasije yakajirudia tena. Ninafahamu kuna zingine utakuta zaidi miaka hata ya 20, nina uhakika mtatengeneza utaratibu wa kuzifuta ili kusudi zisije kujirudia",amesema Dkt. Magufuli.

Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli ameendelea kwa kusema "kuna hoja nyingine za watu ni kutokana na uzembe tu wakutokujali, watendaji wetu hawataki kuzishughulikia basi waambiwe wazishughulikie. Lakini kama kutakuwepo na watu ambao ni sugu kila mwaka wanaambiwa wao, hilo nalo mlete mapendekezo kupitia kikao chako hicho kwamba ni nani tumtoe, nani akapumzike, nani akafanye shughuli nyingine".

Kwa upande mwingine, Dkt. Magufuli amewaahidi Wabunge walioshiriki katika hafla hiyo kwa kusema ataifanyia kazi orodha ambayo huwa anapelekewa kwaajili ya kupitisha uteuzi wa wenyeviti kama walivyoomba.

Christian Bella Afunguka Kuhusu Muziki wa Hip Hop

$
0
0
Christian Bella Afunguka Kuhusu Muziki wa Hip Hop
Muimbaji Christiana Bella amefunguka kuhusu mipango yake ya kuanza kufanya muziki wa rap/hip hop.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Lamba Lamba’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio hadi sasa tayari kuna ngoma ameandikiwa na Nikki wa Pili, hivyo muda wowote atasikika akirap.

“Walijua mimi Bella naimba muziki wa Bolingo tu, no!, nani ngoma tayari nimeandikiwa na Nikki wa Pili ambayo nitachana
mimi napenda kufanya vitu ambavyo sijafanya ambacho watu hawajajua kama Bela anaweza kufanya hicho kitu,” amesema.

“Napenda sana hip hop hata kama Naimba, napenda sana kusikiliza watu anaochana si Weusi tu nawasikiliza,” ameongeza.

Christiana Bella amekuwa akishirikishwa na wasanii kadhaa ambao wanafanya vizuri katika muziki wa hip hop Bongo, miongoni mwao ni Weusi na Fid Q, pia ameweza kuwashirikisha Joh Makini na Khaligraph Jones kutoka nchini Kenya.

Mama Samia Awapa Somo Mashirika ya Umma, Sekta Binafsi

$
0
0
Mama Samia Awapa Somo Mashirika ya Umma, Sekta Binafsi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi kuwaruhusu wafanyakazi kushiriki michezo katika maeneo yao ya kazi lakini pia kuwaruhusu wafanyakazi hao kushiriki Michezo ya SHIMMUTA.


Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) mjini Dodoma.

Makamu wa Rais amesema michezo ni muhimu sana kwenye Tanzania ya Viwanda kwani michezo husaidia mwili kuwa wenye afya bora na utendaji wao wa kazi unakuwa mzuri zaidi.

Makamu wa Rais amesema yeye alikuwa mwanamichezo mzuri wa mpira wa pete (Netball) lakini kwa sasa anafanya mazoezi kidogo kidogo asubuhi na jioni.

“Najua Umuhimu wa kufanya mazoezi kwa sababu nikiacha kufanya mazoezi nadorora na katika nafasi hii ukidorora unadorora mpaka akili na kazi zitakushinda,” amesema Mama Samia.

Makamu wa Rais aliwasihi Viongozi wa Michezo kusimamia masuala ya michezo katika maeneo ya kazi na kuwataka Viongozi wa Taasisi kuweka bajeti ya michezo kwa ajili ya kushiriki michezo ya SHIMMUTA.

Makamu wa Rais amesema ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015- 2020 imeleekeza kuendeleza michezo sehemu za kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa SHIMMUTA, Ndugu Hamis Mkanachi alimpongeza Makamu wa Rais kwa juhudi anazozifanya katika kukuza michezo nchini.

Rayvanny Afunguka Utendaji wa Kazi wa Daimond Ndani ya WCB

$
0
0
Rayvanny Afunguka Utendaji wa Kazi wa Daimond Ndani ya WCB
Msanii Rayvanny kutoka WCB amesema katika utendaji kazi wake na Diamond ndani ya label hiyo hawajawahi kufikia hatua ya kupishana kauli katika kazi.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Makulusa’ ameiambia Funiko Base ya Radio Five mara nyingi mambo yanayotokea ni ya kawaida ingawa kuna mengine huonyesha kutopendezwa nayo.

“Nikikosea lazima anikoromee lakini kunikoromea hajawahi kwa sababu yeye siyo mtu wa kufokafoka lakini kitu akikukataza unajua hiki kitu hajakipenda, kwa hiyo unajua wewe hapo inabidi ujiongeze,” amesema Rayvanny.

Soma Pia; Ujumbe wa Rayvanny kwa Diamond, ‘Hakuna anayefanikiwa akakosa maadui’

Rayvanny na Diamond wameshafanya ngoma pamoja inayokwenda kwa jina la Salome, pia wamekutana katika ngoma ‘Zilipendwa’ ambayo iliwakutanisha wasanii wote walio chini ya WCB.

Serikali Kugharamia Mazishi ya Kijana Aliyekufa Muda Mfupi Baada ya Kutoka Polisi Mbeya

$
0
0
Serikali Kugharamia Mazishi ya Kijana Aliyekufa Muda Mfupi Baada ya Kutoka Polisi Mbeya
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, William Ntinika amefunguka na kuweka wazi kuwa serikali itagharamia mazishi ya kijana Alen Achiles (20), aliyefariki muda mfupi baada ya kutoka polisi.


Mkuu wa wilaya huyo ambaye alifika nyumbani kwa wazazi wa marehemu na kutoa rambirambi ya laki mbili na kuahidi kuwa serikali itagharamia mazishi ya kijana huyo ikiwa pamoja na kukodi gari la matangazo pamoja na chakula.

Hata hivyo jeshi la polisi mkoani Mbeya limekana kuhusika na kifo cha kijana huyo na kusema kuwa kijana huyo alitoka mikononi mwa Jeshi hilo na kuondoka na ndugu zake baada ya kudhaminiwa akiwa salama.

Mbali na hilo kwa mujibu wa ripoti kutoka hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya iliyotolewa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya, Dk. Godlove Mbwanji, amesema kijana huyo alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo na kueleza kuwa taarifa zilizoandikwa kwenye kitabu cha taarifa za wagonjwa cha hospitali hiyo, zilionyesha kuwa alikuwa amepigwa na kuumia ndani kwa ndani.

Kwa upande wake mama mlezi wa marehemu Alen, Alice Mapunda, ameeleza kuwa  wakati wanamchukua kijana wao hospitalini alikuwa analalamika kuwa anajisikia maumivu makali sehemu za tumbo huku akiwa na majeraha mikononi na kichwani, huku mama mdogo wa marehemu, Justina Kilasa, akidai kuwa  kijana huyo hakuwa mzurulaji kama inavyodaiwa na Jeshi la polisi na badala yake alikuwa anafanya biashara zake za machungwa na jioni kwenda kanisani.

Nondo Hajakosea Ndani ya Chuo- Haki za Binadamu

$
0
0
Nondo Hajakosea Ndani ya Chuo- Haki za Binadamu
Shirika la Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) wamesema uamuzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) kumsimamisha masomo Mwenyekiti wa TSN Abdul Nondo kabla ya kumalizika kwa kesi inayomkabili mahakamani, ni sawa na kumhukumu kabla ya kesi hiyo kumalizika.

Akizungumza na waandishi wa habari Onesmo Olengurumwa ambae ni Mratibu THRDC amesema uamuzi wa UDSM unakwenda kinyume na haki za binadamu na Katiba ya nchi.

” Nondo hata kesi yake ukiangalia aliripoti kama mlalamikaji lakini kilichotokea ndiyo hicho sasa kabla ya ukweli haujajulikana chuo nao wanatoa uamuzi huo kwa kweli hawajamtendea haki mwanafunzi huyu,” -Olengurumwa

Jacob Zuma Amriwa Kufika Mahakamani

$
0
0
Jacob Zuma Amriwa Kufika Mahakamani
Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameamriwa kufika mahakamani wiki ijayo kukabiliana na mshtaka mbalimbali ya rushwa ambayo yana thamani ya mabilioni ya Dola za Marekani.

Mwanasheria wa Zuma ameeleza kuwa Zuma alipewa jana taarifa rasmi ya kufika kwenye Mahakama Kuu ya mji wa Durban April 6, 2018. Taarifa hii pia imethibitishwa na kitengo cha upelelezi polisi.

Kesi hiyo inahusiana na jukumu lake katika mpango wa silaha za miaka ya 1990. Waendesha mashtaka mara ya kwanza walimshtaki Zuma kuhusu kesi hiyo mwaka 2005 kipindi akiwa Makamu wa Rais.

Lakini mashtaka haya yalifutwa wiki chache baada ya kuwa Rais wa nchi hiyo kwa madai kwamba, mashtaka hayo yalikuwa yana shinikizo la kisiasa.

Mbowe na Viongozi Wengine wa Chadema Washtakiwa kwa Makosa Nane Ikiwamo Uasi, Maandamano na Kuamasisha Chuki

$
0
0
Mbowe na Viongozi Wengine wa Chadema Washtakiwa kwa Makosa Nane Ikiwamo Uasi, Maandamano na Kuamasisha Chuki
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wengine watano wa chama hicho wamefikishwa katika Mahakama ya Kisutu na kusomewa mashtaka manane ikiwemo kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha Mwanafunzi wa Chuo cha NIT, Akwilina Akwiline, Feb 16 mwaka huu.



Watuhumiwa hao wamesomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo Nchimbi amedai kuwa kosa la kwanza ni kufanya mkusanyiko ama maandamano yasiyo na uhalali.



Washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa Februari 16, 2018 wakiwa barabara ya Mkwajuni walikusanyika kwa lengo la kutekeleza mkusanyiko ili watu waliokuwepo eneo hilo waogope kuona maandamano ya kuvunja amani.



Kosa la pili ni kufanya mkusanyiko usio halali; washtakiwa wote wanadaiwa kutenda kosa hilo Februari 16, 2018 Barabara ya Kawawa maeneo ya Kinondoni Mkwajuni ambapo kwa pamoja wakiwa na watu wengine 12 ambao hawajafikishwa mahakamani wanadaiwa wakiwa katika maandamano na mkusanyiko wa vurugu waligoma kutii amri ya kusambaratika na kuvunja mkusanyiko huo uliosababisha kifo cha Akwilana Akwilini na majeraha kwa maofisa wa Polisi.



Kosa la tatu ni kuhamasisha chuki kwa wanajamii isivyo halali, ambalo linamkabili Mbowe, ambapo wanadaiwa Februari 16, 2018 akiwa Viwanja vya Buibui Kinondoni DSM akihutubia wakazi wa maeneo hayo na DSM alitoa matamshi ambayo yangesababisha chuki kwa Jamii.






Kosa la nne linalomkabili Mbowe ni uchochezi na kusababisha chuki katika jamii, ambapo inadaiwa alitenda Februari 16,2018. Inadaiwa akiwa Uwanja wa Buibui Kinondoni DSM akihutubia wakazi wa Dar alitoa matamshi  ambayo yangepelekea chuki katika Jamii huku kosa jingine likiwa ni la uchochezi wa uasi, ambapo inadaiwa Mbowe amelitenda Februari 16, 2018 katika viwanja vya Buibui Kinondoni DSM.



Inadaiwa akiwa na nia ya kupandikiza chuki na dharau dhidi ya uongozi uliopo madarakani alitoa maneno ambayo ni wazi yangesababisha uasi. Pia kosa jingine linalomkabili Mbowe ni uchochezi wa uasi, ambapo inadaiwa amelitenda Februari 16,2018 katika viwanja vya Buibui, Kinondoni DSM.

Inadaiwa akihutubia mkutano wa hadhara alitoa matamshi ambayo yangepandikiza chuki na dharau kwa wananchi wa Tanzania dhidi ya uongozi uliopo madarakani. Kosa la saba linamkabili Mbowe ambalo ni ushawishi wa utendekaji wa kosa la jinai, ambalo amelitenda Februari 16, 2018 maeneo ya Buibui Kinondoni DSM.

Inadaiwa Mbowe akiwa amejumuika na watu wengine aliwashawishi wakazi wa maeneo hayo na DSM kutenda kosa. Katika kosa la 8, Wakili Nchimbi amedai linamkabili Msigwa ambalo ni kushawishi raia kutenda kosa la jinai.

Msigwa anadaiwa ametenda kosa hilo Februari 16, 2018 katika viwanja vya Buibui Kinondoni DSM, ambapo aliwashawishi wakazi wa maeneo hayo na DSM kutembea mbele ya umma wakiwa na silaha.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa wote walikana ambapo Wakili Nchimbi amedai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na anaomba tarehe kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali. Hata hivyo, Wakili Nchimbi aliwasilisha maombi kwa mahakama hiyo ili washtakiwa wanyimwe dhamana kwa sababu ya usalama wa umma wa Watanzania.

Dar es Salaam Fahamu Siri Kubwa ya Utajiri Ambayo Matajiri Hawataki Uijue

$
0
0

Hope wengi wetu tupo tuna jishughulisha na biashara  kama kilimo na biashara zingine tofauti tofauti

But tukumbuke Technology inaenda fasta sana hope mmeshasikia about Bitcoin , Ripple na Cryptocurrency zingine kwa ujumla. Ni decentralized digital money ambazo zinakuwa kwa kasi sana
Chini ya its innovative blockchain technology huku soko lake Duniani likifika zaidi ya billion 700 Jan 2018.

Juzi tu mlisikia mmiliki wa Ripple  Chris Larsen kawa tajiri namba 5 duniani kutokana na crypto.... Pia msanii 50 cent baada ya kufilisika juzi katangazwa ni millionea  mpya just because alikuwa ana hold bitcoin za kutosha.

Binafsi  I have been investing and trading katika hilo soko na ningependa na ndugu zangu wa mbeya mkalijua hilo soko vizuri.

Bado mapema ni muda wako muafaka upate elimu sahihi ili uweze kuendeleza safari ya mafanikio

Angalia coin ya Ripple january 2017 ilikuwa inauzwa 0.002 but leo inauzwa dola 1.

Kama unge invest dola 100 ungepata coin elfu 20.

Ambazo leo ungekuwa na dola elfu 20,000 sawa na zaidi ya million 40 za kitanzania.

Zipo coin nyingine very smart

Hakuna mtu aliyezaliwa na utajiri au umaskini.

ELIMU KWANZA, MENGINE BAADAE

Gamy
# CMC Co- Founder



Jiunge na group la whatsapp uwepo katika watu 200 wa mwazo kwa ajili ya free training class April 2018

bonyeza hapa chini kuweza kujiunga na group

https://chat.whatsapp.com/invite/22OShPJ2Xh63HR02KCEttJ

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Bila Mtaji

$
0
0

Wengi huamini kuwa lazima uwe na fedha ndiyo uanzishe biashara na ndiyo sababu yao kuu ya kukaa bila kujishughulisha. Ukweli ni kwamba mtaji ni moja ya kitu muhimu katika kuanzisha biashara, lakini kuna aina ya biashara ambazo zinahitaji gharama ndogo kuanzisha na kukupelekea kupata faida kubwa.

Kama mfanyabiashara unaweza kutoka kwa kishindo kwa kuanza ukiwa huna kitu na kufanya kazi kwa juhudi ukiwa upande wa huduma na kufanikiwa kutengeneza faida kubwa na kutokea hapo na kuanza kufikiria kuanza kukodi ofisi yako, kuajiri watu wengine na kadhalika.

Ingawa ni rahisi kutoka ukiwa upande wa huduma lakini inahitaji ujuzi au weledi fulani hivi ili uweze kufika kilele cha mafanikio. Hapa simaanishi lazima uwe umesoma chuo kikuu maana ujuzi au utaalamu wa jambo halihusiani na digrii ya chuo kikuu.

Unaweza pata ujuzi kwa kuhudhuria semina na warsha mbalimbali au kufundishwa na mtu mwenye ujuzi husika na baada ya kupata ujuzi kuanza kuufanyia kazi katika maisha yako ya kawaida kila siku na kuwa bora kwa upande huo.

Nimejaribu kuorodhesha aina zaidi ya biashara 14 unazoweza kuanzisha pasipo kuwa na mtaji kabisa au mtaji kidogo sana. Hizi ni aina ya biashara ambazo nimezifanya kwa muda sasa na kuona matunda yake na nyingine nimeshuhudia watu wakifanya na kufanikiwa.

Kama kweli una shauku ya kweli kuanza leo biashara soma kwa umakini sana na kuona je, ni wapi pa kuanzia ili uweze kutimiza lengo lako la maisha.

Zifuatazo ni baadhi ya biashara unazoweza kuanzisha kwa mtaji mdogo au pasipo mtaji kabisa. Hizi ni kama vile huduma za kuandika miradi biashara, mshauri wa mambo ya biashara, huduma za kuandaa vitabu vya hesabu, kutoa huduma ya kuandaa nakuendesha matukio, kuanzisha tovuti kwa huduma mbalimbali, mshauri wa masoko, mtafasiri wa maandiko mbalimbali kwenda lugha ya wazawa, kutafiti fursa mpya za biashara, kutoa huduma za kuchapisha, kutoa huduma za kuajiri, mshauri wa mitandao ya kijamii na kutoa huduma za kuandikisha majina ya kampuni.

Ukweli ni kuwa wajasiriamali wengi hawajui hata kuandika ‘business plan’ katika uwezo wa kuwashawishi wawekezaji kuja kuwekeza na huwa hawawekezi muda wa kutosha kujifunza kwa hilo. Kama unaweza timiza hitaji hili biashara ipo mikononi kwako.

1. Mshauri wa mambo ya biashara: Wewe ni una uzoefu wa ujasiriamali au umiliki wa biashara? Unajua nini kinahitajika ili uanzishe biashara, kujenga biashara, kuongeza biashara na kukua? Sasa unaweza kuanza kazi ya ushauri wa biashara. Unaweza kusaidia kampuni au biashara mbalimbali kutoka chini ya uvungu na kwa kutoa ushauri na maelekezo muhimu. Unaweza kuwasaidia watu walioajiriwa kuanza kutoka kwenye ajira na kuingia kwa ujasiriamali kwa malipo.

2. Huduma za kuandaa vitabu vya mahesabu. Wewe ni mzuri katika kuandaa vitabu vya uhasibu vya kampuni au biashara mbalimbali? Unaweza kuweka ulingano kwa vitabu vya uhasibu. (Hili ni jambo huwa na shauku kulipata). Sasa hamna kitu kinaweza kukuzuia wewe kuanza huduma za kuandaa vitabu vya mahesabu. Anza sasa.

3. Kutoa huduma ya kuandaa na kuendesha matukio (Event management), kampuni nyingi kila mara huwa na matukio mbalimbali mfano semina, siku ya familia, sherehe mbalimbali. Mara nyingi kampuni kama kampuni haiwezi kufanikisha kwa ufanisi uandaaji wa matukio haya na hivi ndivyo ilivyo kutokana na wafanya kazi wao kuwa na majukumu.

Hivyo ili kuwa na ufanisi hapa inabidi kampuni zikodi watu wanye ujuzi wa kuandaa shughuli husika kwa uhakika. Wewe kama una ujuzi na uzoefu wa kuandaa shughuli kama hizo; mwanzo mpaka mwisho, uwanja ni wako. Mfano kuna matukio kama siku ya familia, semina kwa wafanyakazi, maonyesho ya biashara ndani na nje ya nchi.

4. Kuanzisha tovuti kwa huduma mbalimbali. Kwa Afrika watu kunufaika na tovuti ndio kwanza ipo hatua za mwanzoni. Unaweza kuanzisha tovuti na kutoa huduma ya taarifa. Watu wengi wanaotembelea tovuti yako wanaweza kuongea na kampuni kadhaa kuja kutangaza na wewe na kutengeneza fedha za kutosha.

Kama hujui jinsi ya kutengeneza tovuti usijali kuna tovuti za bure kabisa ambazo zimetengenezwa tayari kinachohitajika ni wewe kujaza fomu zao na ndani ya dakika moja unakuwa na wewe tovuti yako na kama unahitaji nunua domain, unaweza ukawa moja kwa moja tovuti yako. Tovuti unazoweza ingia na kutengeneza tovuti yako bure ni www.weebly.com,www.webs.com au pia unaweza tengeneza blog ikawa unaweka taarifa watu wanatafuta na kisha kutafuta wadhamini wa hiyo blog.

5. Mshauri wa masoko. Je wewe unaweza ukanionyesha njia ya gharama ndogo ya kuongeza wateja kuanzia asilimia 30 hadi 70 au zaidi? Kama ndio biashara ipo mikononi mwako. Unaweza ukajiweka wewe mwenyewe katika ushauri wa masoko kwa wamiliki biashara ndogo na kati hata kubwa jinsi ya kuteka na kuwavuta wateja na kuongeza mauzo ya bidhaa kwa ada fulani, kutokana huduma husika.

6. Mtafasiri wa maandiko mbalimbali kwenda lugha ya wazawa; Kampuni nyingi za nje zinazokuja hapa nchini, huwa wanahitaji kutafsiri taarifa zao kwenda lugha ya wazawa, mfano mradi fulani, tovuti zao, mfano kama ni kampuni ya vitabu mwandishi mmiliki angependa ili auze kwa wazawa inabidi atafasiri kwenda lugha ya wazawa. Mfano kuna hata miradi mbalimbali ambayo inatakiwa iangaliwe na wazawa.

7. Kutafiti fursa mpya za biashara: Nina marafiki zangu ambao walianza kutoa huduma ya kutafiti fursa mpya na wanafanya vyema kwenye hii biashara. Wanachofanya kutupia jicho kwa mambo yajayo, mwelekeo, mahitaji aua fursa za biashara na kuandaa mradi au mpango kuhusiana hilo na kuuza hilo wazo kwa kampuni makubwa.

8. Kutoa huduma za kuchapisha. Biashara hii inafahamika na wengi lakini bado inalipa. Unaweza kuanza kutoa huduma ya kuchapisha business, banner sposters card, viperushi na catalogues kwa biashara ndogo na za kati.

9. Kutoa huduma za kuajiri. Siku hizi kazi za managementi za rasilimali watu kwa kampuni nyingi hutolewa na tenda kwa kampuni za nje ya kampuni husika kufanya hiyo kazi ili kuongeza ufanisi kwa kampuni husika na hivyo kupelekea kampuni husika kuweka umakini wake wa kutimiza lengo lake mahususi.

Kama una uelewa na ujuzi wa kutosha wa kushughulika na maswala ya rasiliamali watu uwanja ni wako. Kwa sasa hapa Tanzania kujisajili kuwa wakala wa kuajiri ni bure unatakiwa uende pale wizara ya ajira na vijana kujisajili.

10. Mshauri wa mitandao ya kijamii (social media consultancy). Kwa hii dunia mitandao ya kijamii imechukua asilimia kubwa. Je wewe unajua jinsi ya kutengeneza foleni kwa mitandao ya kijamii? Unajua jinsi ya kuboresha na kuelimisha umma juu ya chapa (brand) za makampuni ndani ya mitandao ya kijamii kama facebook, twitter na linked in? Basi unaweza kuwa mashauri wa mitandao ya kijamii na kutengeneza fedha zako.

11. Kutoa huduma za kuandikisha majina ya kampuni. Je wewe ni mzuri katika kuandika katiba za kampuni? Unajua jinsi ya kuchagua jina sahihi la kampuni? Unajua hatua zinazohitajika ili ukamilishe uandikishe jina la biashara? Anza sasa fungua biashara yako ya kutoa huduma za kuandikisha majina ya kampuni.

Huduma nyingine unazoweza kuzifanya ili kutengeneza fedha ni kutoa huduma za kuandikisha haki miliki za bidhaa au huduma huduma za ushauri kwa biashara ndogo au kuandika vitabu vya uelimishaji.

Matatizo Yatokanayo na Matumizi ya Simu Gizani

$
0
0

Daktari justice Authur, ambae ni daktari kule africa kusini ameniomba kuwagawia hii na nyie pia. Amesema ni muhimu sana.

Hivyo usiidharau au kusita kuisoma hii.

Pale taa zinapokuwa zimezimwa usiku, usiitumie simu yako ya mkononi (smart phone)

Tafadhali sambaza kwa familia na marafiki haraka ujumbe huu…..

tabia za kutumia simu muda ule kabla ya kulala huku taa zinapokuwa zimezimwa inaweza pelekea matatizo makubwa sana.

Kwa sasa, idadi ya wagonjwa kuanzia miaka 30-40 wanatafuta matibabu makubwa. kutokana na matumizi ya simu za mkononi (smart phone) gizani.

Profesa Li Li, kiongozi wa hospitali ya macho huko singapore amesema: anasema mionzi ya moja kwa moja kwa zaidi ya dk 30 na kuendelea inaweza kusababisha mpangilio na mbadiliko wa seli macho na hivyo kusababisha saratani na kushindwa kuona kabisa.

Kupata saratani ya macho inamaanisha unasubiri kupoteza kuona kwa sababu utaalamu wa afya kwa sasa hautibu saratani hivyo ni bora tuache kutumia simu za mikononi gizani ili tujikinge.
Simu za mikononi(smartphone) zenye mwanga mweupe sana karibu na macho gizani, unabadili mfumo wa seli macho na kupelekea matatizo ya saratani ya macho.

Proffessor Li Li amesema dalili za mbadiliko wa seli macho mara nyingi wanazigundua watu wenye umri mkubwa (wazee), ila kwa hivi sasa zinagunduliwa hata na kwa vijana wadogo. Hasa kwa wenye umri wa kuanzia miaka 30-40 wanaongezeka kwa asilimia 3% na wote hawa ni watumiaji wa simu za mikononi (smartphone) kupitiliza.

Hata hivyo, kutumia simu (smartphone) gizani sio sababu ya tatizo la kupelekea saratani ya macho. Na pia kidogo inaweza sababishwa na ugonjwa wa macho makavu, mtoto wa jicho na mwisho kupelekea kupoteza kuona.

Dalili za mwanzo kama vile vipele vidogo vidogo huwa zinatibiwa kwa mionzi, sindano na madawa.

Madaktari bingwa wa macho 254 kutoka mahosipitalini profesa Li Li atoa hoja kwamba kikubwa cha muhimu ni kwamba ni kuwa mbali na tabia za kutumia simu gizani. Sababu tabia hizi za kutumia simu (smartphone) kabla ya kulala zitakusababishia matatizo ya maisha yako kwa ujumla.

Marafiki: ili kujiangalia sisi wenyewe na familia zetu, kwamba hakuna kuzima taa endapo unatumia simu ya mkononi. Wape taarifa haraka wote watumiaji wa simu za mikononi gizani wanaweza kupoteza kwa urahisi sana uwezo wa kuona.

Epuka Kuvaa Chupi, Faida za Kutokuvaa Chupi Zipo Nyingi Sana na Pia Muhimu.

$
0
0


Leo naomba nikukumbushe somo la Afya ya uzazi. Somo hili litafafanua faida na hasara au madhara yatokanayo na uvaaji wa nguo za ndani hasa Chupi. Uvaaji wa chupi kihistoria ulianza karne ya 19 baada ya uvumbuzi wa viwanda na mapinduzi yake yaliyoambatana na mapinduzi ya teknolojia.

Enzi za mama zetu na babu zetu uvaaji wa chupi haukuwepo hapa Tanzania. Uvaaji wa chupi uliletwa na wamisionari na wakoloni wakati wanaleta dini Africa. Kabla ya hapo waafrica hatukuwa na utamaduni wa KUVAA chupi.

Mtoto akizaliwa hakuvalishwa chupi kamwe kama ilivyo Leo. Mwanamke pia enzi hizo alikuwa havai chupi. Mwanaume naye pia alikuwa havai chupi? Watu wote walikuwa hawavai chupi. Mwanamke alikuwa hachuchumai chini pindi akijisaidia kutokana na kwamba hawakuwa wanavaa chupi hivyo wakitaka kujisaidia haja ndogo walikuwa wanasimama tu na kupanua miguu na kuanza kukojoa.

Nyakati za leo ambapo uvaaji chupi kwa wanaume na wanawake uko juu sana kuanzia watu tunapokuwa watoto wadogo hali ya Afya ya viungo vya uzazi imeendelea kuwa mbaya sana. Yafuatayo ni baadhi ya madhara ya kuvaa chupi :

1. Magonjwa ya "Urinary tract infection" au UTI hayataisha kwako. 

Hii hasa ni kwa wanawake wanavaa nguo nyingi kwa wakati mmoja na kwa muda mrefu zaidi ya saa kumi. Unavaa chupi, lakini tight, suruali ya jinzi, nk halafu unashinda na hizo nguo kuanzia asubuhi unapoenda kazini hadi saa mbili usiku unaporudi home. Hiyo ni hatari sana.

Mwanamke anayefanya kazi zinazompasa kuwepo kazini zaidi ya masaa 8 namshauri asiwe anavaa chupi kabisa. Chupi ivaliwe nyakati za hedhi tu. Kama hauko kwenye siku zako vaa suruali tu bila chupi. Au vaa underskirt pekee yake kwa ndani na ndoo uvae nguo yako ya kawaida. Hii itakuepusha na kuugua UTI. Ukiacha sababu za ngono UTI husababishwa na bacteria wanaopendelea mahali penye unyevu na joto. Kwa hiyo mwanamke akivaa nguo nyingi bacteria hao hujipatia joto la kutosha kuzaana.
Mwanamke ni vyema ukaepuka kuvaa nguo za kubana mwili sana ili kuepukana na uwezekano wa kupafanya ukeni pawe na joto sana na ikitokea bacteria mmoja tu akaingia humo atazaa haraka sana na kujikuta UTI inakuwa rafiki yako. Vaa sketi bila chupi au kama kuvaa suruali ni lazima hakikisha unavaa suruali peke yake. Jizoeze tu utazoea. Na ukizoea kuvaa nguo bila chupi utainjoi sana.

2. Magonjwa ya kuvu au fungus hayatakoma kwako.

Bado niko kwa wanawake, kama nilivyoeleza mwanzo hapo magonjwa ya fungus yanasababishwa pia na kuvaa chupi kwa muda mrefu. Chupi inayovaliwa kwa zaidi ya saa 8 lazima italeta ukungu au uvundo sehemu nyeti. Huo uvundo waweza kuleta fungus ukeni. Fungus za ukeni hazina tofauti na zile za miguuni kwa wanaume wanaovaa viatu kwa muda mrefu bila usafi miguuni wa kutosha.

Chupi inakuwa kama socks za wanaume. Mwanamke avaae chupi muda mrefu bila kuruhusu upepo upite ndani ni watapata fungus ukeni sawa na mwanaume anayevaa socksi zisizofaa kiafya. Chupi au socks zinazofaa ni zile za pamba au cotton.

Of course sababu za kupata ugonjwa wa fungus kwa mwanamke siyo tu kuvaa chupi inayobanaaaa kwa muda mrefu ni pamoja na kutawadha kwa kutumia maji.

Wanawake wengi hawajui kutawadha kwa kutumia maji. Wengi wamalizapo kujitawadha haja kubwa ndipo hurudi kujisafisha ukeni. Hii ni hatari sana kwani bacteria watokanao na kinyesi unawahamisha kutoka nyuma na kuwaleta mbele.

Mwanamke unapaswa kutawadha kwanza mbele kisha umalizie nyuma.

Yaani hakikisha kuwa uchafu wa nyuma unaoweza kuwa umebakia kwenye vidole vyako usiuingize ukeni kwa namna yoyote. Tawadha pande zote lakini uhakikishe kuwa haviingiliani mbele na nyuma. Sawa dada yangu? Uko poa hapo?

Kikubwa hapa ni usafi wa mbele na nyuma. Usafi wa chupi zetu. Uvaaji chupi wetu.

Kwa mfano uwapo safarini tena safari ndefu ya zaidi ya saa 8 ni vyema ukasafiri bila kuvaa chupi isipokuwa tu kama uko kwenye siku zile za adabu. Hata kama uko kwenye siku za adabu ni vyema ukasafiri bila kuvaa manguo mengi sana yanayobana mwili. Vaa chupi na sketi au suruali isiyoubana sana mwili wako.


3. Chupi husababisha ugumba kwa wanaume. 

Sababu nyingi za ugumba tunaweza ukizipata kutoka kwa madaktari wetu wa hospitali zetu. Lakini ukija kwangu mimi Daktari wa magonjwa ya tabia (Lifestyle Based Diseases Doctor) nitakuongezea sababu nyingine ya ugumba wa wanaume kuwa ni kuvaa chupi zinazobana sana.

Mwanaume shujaa havai chupi. Anavaa kaptura badala ya chupi. Tena havai kaptura inayobana sana. Anavaa isiyobana viungo muhimu kwa uzalishaji wa watoto. Mbegu za kiume huzalishwa kwa wingi wakati wa baridi. Kuvaa chupi inayobana kwa muda mrefu husababisha pumbu kuchemka sana na kushindwa kuzalisha mbegu nyingi. Mwanaume mwenye mbegu chache hushindwa kutungisha mimba kwani mbegu zake zinakwenda ukeni kwa uchache na kushindwa kuogelea ukeni.


4. Chupi husababisha miwasho sana kwenye mapaja ya mwanaume na mwanamke.

Epuka kuvaa chupi zinazobana ili kuepukana na miwasho.

5. Chupi husababisha michubuko ya mapaja. 

Ukivaa chupi kwa muda mrefu utajikuta umepata michubuko mapajani karibu na uume au uke .

6. Uvaaji chupi usiku huchelewesha tendo la ndoa.

Mwanaume anapohitaji vitu adimu usiku wakatimwingine anapaswa kujichotea tu kirahisi kwani ni mke wake halali lakini akikutana na chupi inakuwa kikwazo. Mwanamke usilale na chupi usiku. Unaogopa nini? Hakuna majambazi wala moto. Nani alikwambia ulale na chupi eti unajihami na ajali za moto usiku.? Mbona tangu umelala na chupi usiku hakuna ajali ya moto iliyokwishatokea.

Acheni kuvaa chupi enyi wanawake ili ikitokea waume zenu tunahitaji naniii usiku tujipatie kwa wepesi! Au Siyo?

Tangu niache kuvaa chupi sijawahi tena kuwashwa mapajani wala mke wangu hajawa na taarifa za fungus na UTI kama zamani alipokea hajalielewa somo hili. Na wewe pia nakushauri uache kuvaa chupi kuanzia leo Uwe na afya bora maeneo yote nyeti.

Mahakama Kuu Kenya Yaagiza Miguna Aachiliwe

$
0
0

Jaji wa mahakama kuu Roseline Aburili ameagiza wakili wa upande wa upinzani Miguna Miguna kuachiliwa kutoka kwa uwanja wa ndege wa kimataifa Jomo Kenyatta.

Miguna ameagizwa kutokea mahakamani kesho Jumatano sasa tatu saa za Afrika Mashariki.

Bw Miguna Miguna alijaribu kurejea Kenya Jumatatu lakini akazuiwa kuingia baada yake kudaiwa kutowasilisha pasipoti ya Canada ambayo ilitumiwa kumsafirisha kwa nguvu hadi Canada.

Wakili huyo alisisitiza kwamba ni raia wa Kenya na hafai kuzuiwa kurejea.

Bw Miguna, aliyekuwa amewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa nane adhuhuri, alikesha kwenye uwanja huo.

Maafisa walijaribu kumsafirisha kutoka uwanja huo kwa kutumia ndege ya shirika la Emirates ambayo ilikuwa inaelekea Canada kupitia Dubai.


Watumishi Watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Wafikishwa Mahakamani

$
0
0

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imewafikisha mahakamani Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro  kwa kosa la kuisababishia hasara serikali  dola za Kimarekani 35,500.

Watuhumiwa ni pamoja na Joseph Mtwala{36},John Mlambo{42},Mwahu Yunus {38},Mery Njau{38} na Catherini Edward {33}.

Watuhumiwa hao wote kwa pamoja walisomewa shitaka moja na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa{TAKUKURU} ,Adamu Kilongozi akiwa na Hamidu Simbano na Richard Jacopiyo kuwa walitenda kosa hilo kati ya desemba 25 mwaka 2013 na juni 6 mwaka 2014.

Kilongozi alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao wakiwa katika lango la Nabi Mkoani Mara na lango kuu la Loduare Mkoani Arusha watuhumiwa hao walisababishia serikali hasara ya fedha za Kimarekani kiasi hicho wakiwa watumishi wa NCAA.

Mwendesha mashitaka huyo alisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha,Bernad Nganga na kueleza kuwa walifanya kosa hilo huku wakijua ni kinyume na sheria.

Watuhumiwa wote walikana shitaka hilo na walipewa dhamana ya fedha taslimu shilingi milioni 7.9 au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo na taratibu za dhamana zilikuwa zikiendelea .

Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU alisema kuwa ushahidi wa kesi hiyo umekamilika na aliiomba mahakama hiyo kupanga Tarehe ya kuanza usikilzwaji wa awali.

Watuhumiwa wote watano wamepelekwa rumande kwakushindwa kukidhi masharti ya dhamani ,ambapo watasomewa hoja za  awali April 10 mwaka huu.

Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images