Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104796 articles
Browse latest View live

Zari Awakalisha Mastaa wa Bongo Asaini Mkataba Mnono

$
0
0
Baada ya Kutua Bongo Zari Asaini Mkataba Mnono
Mpenzi wa zamani wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zarinah Hassan maarufu Zari The Boss Lady ametua nchini kwa ajili ya kusaini mkataba wa ubalozi wa kampuni ya Kedz Tanzania inayojihusisha na utengenezaji wa pampasi.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo Jumatano Machi 28, 2018 katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam, Zari ambaye ni mama wa watoto watano amesema anashukuru kupata mkataba na kampuni hiyo.

Hata hivyo, kiu ya wanahabari ilikuwa kusikia akizungumzia uhusiano wake uliovunjika lakini alikwepa swali hilo akidai kuwa si  kilichomleta.

“Unajua hii ni kazi na haihusiani kabisa na masuala ya familia, hivyo nisingependa kulizungumzia hilo leo,” alifafanua.

Zari alitangaza kuachana na mwanamuziki Diamond Platnumz Februari 14, 2018  kupitia mtandao wa Instagram.

Wiki mbili baadaye akihojiwa na Kituo cha BBC Swahili, Zari amesema ameamua kuachana na Diamond kutokana na sababu mbalimbali moja ikiwa ni kushikana hadharani na mwigizaji Wema Sepetu.



Jux Kupata Mtoto Hivi Karibuni

$
0
0
Jux Kupata Mtoto Hivi Karibuni
Msanii wa RnB Jux amesema anatamani kupata mtoto na Mungu akijali hivi karibuni atafanikisha hilo.

Muimbaji huyo ambaye amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Vanessa Mdee kwa muda sasa, amekiambia kipindi cha Uhondo, E Fm kuwa kulingana na umri wake wa miaka 28 anatarajia hadi atakapofikisha 30 atakuwa na mtoto.

“Yeah sina mtoto lakini Mwenyenzi Mungu akipenda siwezi nikasema siku gani lakini soon tu, Mwenyenzi Mungu akinijalia ninavyotaka mimi itakuwa (na mtoto) lakini ni kitu natamani sana kuwa nacho,” amesema.

“Sio kuzaa tu mtoto, je unazaa na nani na huyu mtu unazaa naye yeye mwenyewe yupo vipi, siwezi nikawa na mtoto na msichana yeyote kwanza, japo sometime huwa inatokea ila nakuwa makini sana sana,” amesema.

Inafahamika fika mpenzi wa Jux ni muimbaji Vanessa Mdee ambaye siku za hivi karibuni zilizuka taarifa kuwa ni mjamzito, hata hivyo Vanessa alikanusha taarifa hizo kwa kueleza kuwa hazikuwa na ukweli wowote. Jux kwa sasa anafanya vizuri ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Fimbo.

Mahakama Yawafutia Kesi na Kuwaacha Huru 44 wa Chadema Kimwaga, Lijuakali Kusomewa Maelezo ya Awali April 24

$
0
0
Mahakama Yawafutia Kesi na Kuwaacha Huru 44 wa Chadema  Kimwaga, Lijuakali Kusomewa Maelezo ya Awali April 24
Washtakiwa 44 kati ya 57 wa kesi ya kuchoma moto ofisi ya Serikali ya kijiji cha Sofi wilayani Malinyi mkoani Morogoro wamefutiwa mashtaka na kuwa huru, huku wabunge wa Chadema Suzan Kiwanga (Mlimba) na Peter Lijualikali wa Kilombero na wenzao 11, ikielezwa watasomewa maelezo ya awali Aprili 24, 2018.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali, Sunday Hyera uliwasilisha ombi la kuwafutia mashtaka washtakiwa hao 44 kwa kile walichodai kuwa hawana ushahidi wa nguvu utakaowatia hatiani washtakiwa hao.

Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo, Ivan Msack ameridhia ombi la kuwafutia mashtaka washtakiwa hao na hivyo kuhairisha kesi hadi Aprili 24 ambako washtakiwa 13, wakiwemo wabunge hao kesi yao itaanza kusikilizwa kwa maelezo ya awali.

Nje ya mahakama mmoja wa mawakili wanaowatetea washtakiwa hao, Fredy Kalonga amedai kuwa kwa sasa wanajiandaa kukabiliana na ushahidi utakaotolewa na upande wa mashtaka dhidi ya wabunge hao na wengine 11.

Miongoni mwa waliofutiwa mashtaka ni pamoja na diwani wa Mkula, Clement Mjami aliyedai Jamhuri imeonyesha udhaifu mkubwa kwa kukosa ushahidi dhidi yake.

RC Makalla Amtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kufanya Uchunguzi Kifo cha Kijana Alen

$
0
0
RC Makalla Amtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  Kufanya Uchunguzi Kifo cha Kijana Alen
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amefunguka na kumtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga kuunda kamati maalumu kuchunguza juu ya kifo cha utata cha kijana, Alen Achiles (20), aliyefariki muda mfupi baada ya kutoka mikononi mwa Polisi


Mkuu wa mkoa wa Mbeya alisema hayo kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, William Ntinika ambaye alimuwakilisha kwenye msiba huo baada ya RC kupata dharura.

"Kutokana na tukio hilo RC amemuagiza RPC aunde kikosi kazi kitakachochunguza tukio hili toka lilipoanza mpaka tukio lilipofika mwisho na taarifa amkabidhi na wale watakaobanika kama mjuavyo nchi yetu inaongozwa kwa sheria hatua zitachukuliwa mara moja, hayo maagizo nimepewa kwa hiyo RPC naomba nifikishe ujumbe huu nilikuwa sijakwambia kwamba unaunda timu itakayochunguza ikiwashirikisha pia wanafamilia na jamii kwa ujumla ambayo inafahamu" alisema Ntinika

Hata hivyo wananchi mbalimbali ambao walikuwepo eneo la msiba wameendelea kulinyooshea mkono jeshi la polisi kuhusika na kifo cha kijana huyo licha ya kuwa RPC mkoa wa Mbey alisema jeshi la polisi haliusiki na kofo cha kijana huyo na kudai kuwa aliondoka katika mikono yao akiwa salama.

Mugina: Nateseka Katika Mahabusu ya Uwanja wa Ndege Naishi Kama Mbwa

$
0
0
Mugina: Nateseka Katika Mahabusu ya Uwanja wa Ndege Naishi Kama Mbwa
Mwanasheria aliyejitangaza kuwa jenerali wa vuguvugu la NRM, Miguna Miguna amesema anaishi kama mbwa katika mahabusu ya polisi iliyoko kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Wakili huyo, aliyewasili Jumatatu mchana akitokea Uingereza, amekataliwa kuingia nchini licha ya amri mbili za mahakama kuelekeza arudishwe nchini baada ya kusafirishwa kwa nguvu ikidaiwa anarejeshwa kwao Canada.

Chooni

Katika taarifa yake, Miguna amesema Jumatano kwamba polisi wanamshikilia “ndani ya choo finyu na kichafu bila kupewa mahitaji ya msingi ya afya na muhimu kwa maisha”.

Gazeti la Nation halikuweza kuthibitisha madai yake kwa sababu polisi wamezuia waandishi wa habari na wanasheria kumwona.

 “Wajibu maombi hawajaniletea chakula, maji na huduma ya afya na zaidi sijapewa haki ya kupata ushauri,” alisema.

Chumba kilichopo karibu na Uwanja Na 2, anadai hakifai kuishi mtu. “Sina uwezo kwenda bafuni na sijaoga tangu Jumapili ya Machi 25. Choo kilichopo hapa ninaposhikiliwa hakina maji ya bomba,” amesema katika taarifa.

“Maji yaliyopo chooni ni ya moto tu, hivyo siwezi hata kuosha uso wala kupiga mswaki.”

Mwanasheria huyo alilaani kuendelea kushikiliwa na watu aliowaita “wadhalimu”.

Miguna Miguna arejea Kenya na makeke yake



Amri ya mahakama

Jaji Roselyn Aburili Jumanne aliamuru Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’i, Mkurugenzi wa Idara ya Uhamiaji Gordon Kihalangwa na Inspekta Jenerali wa Polisi, Joseph Boinett kumwachia mwanasheria huyo na wampeleke mahakamani Jumatano asubuhi.

Maofisa wengine waliolengwa na amri ya mahakama ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai George Kinoti, mkuu wa kikosi cha matukio ya dharura Said Kiprotich, OCPD wa JKIA na Mwanasheria Mkuu.

“Licha ya amri ya mahakama, na kama ambavyo wamekuwa wakifanya awali, wajibu maombi hawajaniachia,” alisema Miguna.

Jaji alitoa amri hiyo baada ya Miguna kupitia wanasheria wake kuwashtaki viongozi hao kwamba wanamshikilia isivyo halali.

China na Korea Kaskazini Zathibitisha Kim Jong-un Ndiye Aliyezuru China

$
0
0
China na Korea Kaskazini Zathibitisha Kim Jong-un Ndiye Aliyezuru China
Baada ya siku ya uvumi wa siku nyingi, imethibitishwa kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amezuru China.

Ziara hiyo, ambayo ilithibitishwa na China na Korea Kaskazini, ndiyo ya kwanza inayofahamika ya Bw Kim nje ya taifa lake tangu alipochukua mamlaka mwaka 2011.

Bw Kim alifanya "mazungumzo ya kufana" na kiongozi wa China Xi Jinping mjini Beijing, shirika la habari la China, Xinhua liliripoti.

China ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kiuchumi na baadhi ya wachambuzi wanasema uwezekano wa wawili hao kabla ya mkutano mkuu wa Bw Kim na viongozi wa Korea Kusini na Marekani ulitarajiwa.

Bw Kim amepangiwa kukutana na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in mwezi Aprili na Rais wa Marekani Donald Trump mwezi Mei.

Ziara hiyo ya Beijing inatazamwa na wengi kama hatua muhimu katika maandalizi ya Korea Kaskazini kuhusu mazungumzo hayo.

Wakati wa ziara hiyo, Bw Kim alimhakikishia mwenzake wa China kwamba amejitolea kuacha kustawisha silaha za nyuklia, kwa mujibu wa shirika la habari la Xinhua.

"Suala la kumalizwa kwa silaha za nyuklia katika Rais ya Korea linaweza kutatuliwa, lakini iwapo tu Korea Kusini na Marekani watajibu juhudi zetu kwa nia njema, kuunda mazingira ya amani na uthabiti na pia kwa kuchukua hatua za kusonga mbele kwa pamoja kutoka kwa wadau wote kuhakikisha amani inapatikana," Bw Kim alinukuliwa akisema.

Shirika la habari la Korea Kaskazini, KCNA, lilieleza ziara hiyo kama yenye umuhimu mkubwa katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na China.

"Ina maana kwa Korea Kaskazini kufafanua msimamo wake na kushirikiana na China, mshirika wake muhimu zaidi," msomu katika Pacific Forum CSIS Andray Abrahamian ameambia BBC.

"Uhusiano huo umekuwa ukidhoofika katika miaka mitano iliyopita na China imekuwa imetengwa kidiplomasia katika miezi kadha iliyopita," amesema.

"Kutoka kwa mtazamo wa Beijing, hii ni ziara ambayo ilifaa kufanyika kitambo sana."

Vyombo vya habari vya Japan vilikuwa vya kwanza kuandika taarifa kuhusu ziara hiyo mapema wiki hii
Kwa sehemu kubwa, hii ni ziara yenye maana kubwa kwa urafiki wa Korea Kaskazini na China, na ni ishara ya heshima pia, Fyodor Tertitskiy wa shirika la habari la NK News linaloangazia sana taarifa kuhusu Korea Kaskazini alisema.

"Wana mikutano miwili mikubwa kati ya kiongozi wao na mataifa mengine - mmoja na Seoul na mwingine na Washington - na pengine wanataka kuusikia msimamo wa China pia.

Waandamanaji Seoul 5 Novemba, 2017 wakiitisha amani kati ya Marekani na Korea Kaskazini
KCNA wamesema Bw Xi pia amekubali mwaliko wa kuzuru Korea Kaskazini.


Bw Kim aliwasili akiandamana na mkewe, Ri Sol Ju, Jumapili na wawili hao waliondoka Beijing Jumanne alasiri, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari.

Ziara hiyo ni ya karibuni kwenye msururu wa shughuli nyingi za kidiplomasia tangu Korea Kaskazini na Kusini zilipoanza kuimarisha uhusiano wao wakati wa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi iliyoandaliwa Korea Kusini.

China iliwasiliana na utawala wa Trump na kuwafahamisha yaliyotokea katika mkutano huo Jumanne, serikali ya Trump ilithibitisha.

"Tunatazama hili kama ishara nyingine kwamba kampeni yetu ya kuweka shinikizo kali ndiyo inayozaa matunda na kufanikisha mazingira mwafaka ya mazungumzo na Korea Kaskazini," msemaji wa ikulu ya White House Sarah Huckabee Sanders amesema.

Polisi wa China wakiwa wamefunga barabara kuruhusu msafara wa magari ya Korea Kaskazini kupita karibu na ikulu ndogo ya rais ya Diaoyutai, Beijing
Mwezi uliopita, Bw Trump alichukua hatua isiyo ya kawaida na kukubali mwaliko wa kukutana na Bw Kim baada ya miezi mingi ya uhasama na majibizano pamoja na Korea Kaskazini kufanyia majaribio makombora.

Mkutano huo wa Bw Kim na Bw Trump ukifanyika, basi Bw Trump atakuwa rais wa kwanza kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini akiwa bado uongozini.

Vituo vya Redio 23 Vyafungiwa kwa 'Kutangaza Uganga wa Kienyeji

$
0
0
Vituo vya Redio 23 Vyafungiwa kwa 'Kuchochea Ushirikina'
Tume ya mawasiliano nchini Uganda, UCC, imefungia zaidi ya vituo 20 vya redio vya FM.

Vituo hivyo vinashutumiwa kutangaza 'uganga wa kienyeji na kuwatapeli wananchi.'

Hatua hii inafuata onyo la tangu zamani viache kuwaweka hewani waganga wa kienyeji.

Tangazo hilo la kufungiwa vituo vya redio 23 limetolewa jana jioni na mwenyekiti wa Tume ya Mawasiliano Godfrey Mutabazi.

Bwana Mutabazi ameshutumu redio hizo kutumiwa na waganga wa kienyeji kuwatapeli wananchi na kuvunja sheria ya uchawi ya kifungu cha pili.

Redio hizo zimekuwa zikiwapa vipindi waganga hao wa kienyeji kutangaza uganga wao, huku wakiwaambia wananchi kutuma fedha kupitia njia ya simu za mikononi.

Msemaji wa tume ya mawasiliano Pamela Ankunda ameielezea BBC kuwa, "Kwa kuwaweka hewani matapeli wanaojiita waganga wa kinyeji, wakitumia mbinu mbali mbali wakiwa hewani ili kuwatepeli wananchi."

"Kwa mfano kwa kuwalaghia wananchI kwamba ukituma fedha hizo kwa njia ya simu ya mkononi utapata utajiri, baada ya kutuma kesho yake utapata mamilioni ya fedha chini ya kitanda chako.Hivyo tumetumia sheria ya kuwajibisha radio hizo na kufunga FM Radio 23 baada ya kusikiliza matangazo hayo." amesema Bi Ankunda

Baadhi ya vituo hivyo 23 ni kutoka wilaya mbalimbali zikiwemo redio mbili za jiji Kamapla ambazo ni Metro FM, Dembe FM inayomilikiwa na gazeti la Monitor, nyingine ni kutoka sehemu mbalimbali za nchi mashariki , kaskazini na magaharibi mwa Uganda.

Tume imewataka wamiliki wa redio zote zilizofungiwa kufika katika tume ya mamlaka ya mawasiliano ya kieloktroniki, inayohusika na kutoa leseni ya matangazo.

Bi Ankunda amesema vituo hivyo vina nafasi ya kufunguliwa wakifuata sheria.

"Bado wananafasi ya kuzungumza na tume, kama wakiandika barua ya kuomba msamaha na kuthibitisha kwamba hawatatangaza tena matangazo hayo na kufuata kanuni na sheria ya utangazaji, tutawarudisha tena hewani.

Hii siyo mara ya kwanza tume ya mamlaka ya mawasiliano kufungia redio za FM kwa kuvunja kanuni na sheria ya utangazaji nchini Uganda.

Miaka ya nyuma Rais Museveni amewahi kutishia kufungia vituo vya redio na pia kumekuwa na matukio ya polisi kuvamia baadhi ya vituo vya habari.

Tutaanzisha Mitihani Ili Uwe Mtumishi wa Kinondoni Unafanya Ukifaulu Ndio Utaruhusiwa- DC Hapi

$
0
0
Tutaanzisha Mitihani Ili Uwe Mtumishi wa Kinondoni Unafanya Ukifaulu Ndio Utaruhusiwa- DC Hapi
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amesema kuwa “Ili ufanye kazi Kinondoni lazima uwe na akili na kasi ya kuendana na Kinondoni, huko mbele ili uwe mtumishi Kinondoni tutaanzisha mitihani unafanya mtihani ukifaulu ndio utaruhusiwa, ukifeli tutakurudisha huko huko ulikotoka hatutaki watu wasioendana na kasi yetu” – DC Ally Hapi.

DC Hapi ameyasema hayo leo katika Mkutano wa Wajasiliamali wote wa wilaya ya Kinondoni uliofanyika katika Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es salaam.

Kenya, Tanzania Wahakiki Mpaka wa Kimataifa

$
0
0
Kenya, Tanzania Wahakiki Mpaka wa Kimataifa
Timu za watalaamu wa upimaji ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Tanzania na taasisi za usimamizi wa Ardhi nchini Kenya zimekutana wilayani Tarime mkoani Mara kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa kazi ya kuhakiki na kuimarisha mpaka wa Kimataifa baina ya nchi hizi mbili.

Mapema mwezi Machi, Naibu Waziri wa Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula alitangaza azma ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza kuimarisha mipaka yake kwa nchi jirani za Kenya na Uganda baada ya ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya katika Mbuga ya Wanyama ya Taifa ya Serengeti iliyopo mkoani Mara.

Hatua ya uhakiki na uimarishaji wa alama za mipaka ya mikataifa inatokana na mpaka huu kuwa wa siku nyingi na haukuwa wazi katika maeneo mengi pia baadhi ya alama hizo kuharibiwa, kung’olewa au kuchakaa na hivyo kusababisha Serikali pande zote kushindwa kusimamia kwa ufanisi shughuli za mipakani, rasilimali za nchi pamoja na ulinzi na usalama.

Katika uimarishaji wa alama hizo za mipaka hivi sasa, kutaongezwa alama mpya ndogo zinazoonana kwa umbali wa mita 100 pamoja na kubainisha eneo la ardhi huru kwa kila upande wa nchi (buffer zone).

Wataalam wa masuala ya upimaji ardhi pamoja na maafisa mbalimbali kutoka katika ofisi za Serikali za nchi zote mbili waliojumuika pamoja wilayani Tarime mkoani Mara kupanga namna ya kutekeleza kazi ya uhakiki na uimarishaji wa mipaka ya kimataifa kwa pamoja. Wa tatu kutoka kulia (walioketi) ni Mkuu wa Msafara wa wataalam kutoka Tanzania Bw. Huruma Lugala na kulia kwake ni Mkuu wa Msafara kutoka Kenya Bw. Julius Rotich.

Mkuu wa zoezi la Uhamasihaji katika kazi ya kuhakiki na kuimarisha mipaka ya Kimataifa kati ya Tanzania na Kenya Bw. Raymond Bagenda kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza wakati wa kikao cha pamoja cha wataalam wa masuala ya upimaji ardhi kutoka katika ofisi za Serikali za nchi zote mbili. Kikao hiko kilichofanyika wilayani Tarime mkoani Mara kinapanga namna ya kutekeleza kazi hiyo kwa pamoja. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais nchini Kenya inayohusika na Usimamizi wa Mipaka ya Kimataifa (KIBO) Bw. Joseph Rotich.

Baadhi ya Wataalam wa masuala ya upimaji ardhi pamoja na maafisa mbalimbali kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na katika ofisi zingine za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia mazungumzo kuhusu namna ya kutekeleza kazi ya uhakiki na uimarishaji wa mipaka ya kimataifa kati ya Kenya na Tanzania.

Aliyekuwa Kamishna Madini Kusomewa Maelezo ya Awali Aprili 2

$
0
0
Aliyekuwa Kamishna Madini Kusomewa Maelezo ya Awali Aprili 2
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Aprili 2, 2018 kumsomea maelezo ya awali (PH), aliyekuwa Kaimu Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ally Samaje.

Mwendesha Mashtaka kutoka Takukuru, Leonard Swai ameyasema hayo leo Machi 28, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusomewa mshtakiwa maelezo yake.

Kwa mara ya kwanza, Samaje alifikishwa mahakamani hapo, Februari 9 mwaka huu kujibu mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka yanayomkabili.

Swai alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuwa inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa ila kwa sasa imehamishiwa kwa Hakimu Mwambapa.

"Kesi hii ilikuwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa, ila kwa sasa imehamishiwa kwako, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali, " amedai Swai.

Baada ya Swai kutoa maelezo hayo, Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi April 2, mwaka huu, ambapo upande wa mashtaka utamsomea maelezo hayo.

Katika kesi ya msingi, Swai alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda makosa hayo kati Aprili 9 na Juni 21, 2013 Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa Yanga Waliokua Kambini ya Taifa Waelekea Morogoro Kuungana na Wenzao

$
0
0
Wachezaji wa Yanga Waliokua Kambini ya Taifa Waelekea Morogoro Kuungana na Wenzao
Wachezaji wa Yanga waliokuwa kambini na timu ya taifa, Taifa Stars, leo wanatarajia kusafiri kuelekea mkoani Morogoro kujiunga na kikosi chao kinachojiandaa na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Singida United.

Yanga imeweka kambi Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United utakaopigwa Aprili Mosi 2018 kwenye Uwanja wa Namfua, mjini Singida.

Ibrahim Ajib, Hassan Kessy, Kelvin Yondan na Gadiel Michael wataondoka mchana wa leo kwenda Morogoro kuungana na wachezaji wenzao ambao wameweka kambi maalum mjini humo.

Golipika Ramadhan Kabwili, hatoweza kusafiri kutokana na majukumu mengine ya kuitumikia timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, inayojiandaa na mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON U20.


Ngorongoro inajiandaa kucheza mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON U20 dhidi ya DR Congo Machi 31 2018 utakaopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Rais Shein Awaapisha Viongozi Leo

$
0
0
Rais Shein Awaapisha Viongozi LeoRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Viongozi walioapishwa na Rais Dk. Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Fatma Gharib Bilal ambaye ameapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto.

Mwengine aliyeapishwa ni Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais.

Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said pamoja na Mawaziri.

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Sabuni Hizi Zinaongoza Kuachanisha Ndoa

$
0
0

Ukienda guest au hoteli yoyote hapa TZ unakuta sabuni hizi za EVA zimewekwa kwenye bafu la choo cha chumba ulichopanga..

Kwa kawaida ni adimu sana kuikuta inatumika nyumbani,hivo nadhani hata watengenezaji wa hizi sabuni wanajua kuwa soko lao kubwa ni nyumba za wageni..

SABUNI HIZI ZINA HARUFU SANA..
Wanawake wanazijua sana harufu za sabuni hizi na ikitokea umerud nyumbani na harufu yake una maswali magumu ya kujibu,.

Inavosemekana baadhi ya ndoa zimevunjika kwasababu ya harufu ya hizi sabuni..

Ni wakati mwafaka wa kampuni inayozitengeneza kuangalia kama kuna umuhimu wa kuweka harufu kali kwenye bidhaa yao hii..

Wasiozijua kwa jina picha hiyo hapo..

Huyu Dereva Tax Atanivunjia Ndoa Yangu, Nifanyeje?

$
0
0
Nimekuja kwenu nahitaji ushauri, ni urgent.

Hapo katikati niligundua kuwa Mr wangu ana kimada, tukasumbuana na kugombana sana juu ya hilo, ingawa sikumshika live ila ni wazi kwamba alikua nae, mbali na hilo pia ni mlevi kupindukia.

Nilipoona suala hilo linaendelea nikaona isiwe tabu, nikatafuta suluhisho.

Na mimi nikatafuta mtu pembeni aniliwaze, kuna dereva tax huwa tunamtumia sana kwa shughuli za kifamilia,
Nikaamua kumzawadia penzi huyo jamaa, sio kwamba nilimuanza mimi, bali alikua akinisumbua siku nyingi, hivyo nikaona nimkubali.

Katika mara zote nilizokutana nae (6) niligundua kwamba hajiwezi kabisa, nikaona this relationship is not worth it, nikampiga chini, pia mtu mwenyewe hana hata Chumba cha kulala, Mara zote anaazima Chumba kwa mwenzie, ingawa ukimuona kwa nje ubrazamen alionao huwezi amini, ni type ya wale wanaume wenye kuongea sana na mbwembwe nyingi lakini hamna lolote.

Nikakata mawasiliano nae na kumwambia asinitafute tena, akaanza kunililia nisimwache, anapiga simu muda wote kunibembeleza, kila akiniona hata na watu wengine Mtaani, labda Dukani n.k atakimbia haraka kuja na kuomba tuongee pembeni hadi kero.

Hivi karibuni nimepata mtu mwingine mahali nakoabudu, he is so caring, ni mtu mwenye Upendo sana, hanywi pombe na ananipenda kwa dhati, he is god fearing and above all his performance is much better than my husband and the tax driver's.

Juzi kumetokea shida kubwa baada ya Mr kushika sms ya yule tax driver akiendelea kunibembeleza, Nikalazimika kusema kuwa jamaa ndio ananifuatilia, ananitaka kimapenzi, akasema kama ni kweli na ili aniamini Basi tufanye fumanizi la kutengeneza, kwamba nikubaliane na yule kijana wa tax kwenda nae guest na yeye aje atufumanie na kundi la mabaunsa wamwoe wote.

Nikikataa mpango huo basi atajua nilishatembea nae, na mimi najua yule tax driver kwa vyovyote vile atauvaa huo mtego, namuonea huruma sitaki apate aibu hiyo wakati tulishaachana nae.

Nipo njia panda naombeni ushauri nifanyeje?

Pata Huduma za Matibabu ya Asili na Nyota Pamoja na Pete za Bahati

$
0
0

Mtabibu Mongwa husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwawale walio sumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa chochote sasa njoo ujionee miujiza hapo kwahapo bila malipo yoyote malipo baada yakazi napia humpa mtu jini la mali kwayule anaye taka kumiliki bila mashariti yoyote
Tunatibu magonjwa mbalimbali yaliyo shindikana mpenzi aliye kukimbia nakumrudisha kwa masaa 24 tu napia natoa dawa za nguvu za kiume kuurefusha uume paka pale unapotaka .

Natoa dawa za biashara na mvuto ==tunatoa dawa zauzazi kwa wale kina mama wenye matatizoya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote njoo umalize tatizo lako sasa
Natoa mazindiko yanyumba na mwili biashara na mvuto kazini

Kupandisha nyota ili kungaa kupandishwa cheo kazini kurudisha mali zilizo pote zilizo ibiwa kuzulumiwa
Kesi zilizo shindikana uzimaliza mara moja namengine mengi ya siri piga simu

+255 764291657

Mjane Aliyemlilia Magufuli Afungwa Jela Miezi Mitatu...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya March 29

Times FM Waomba Radhi kwa Kauli za Msanii Diamond

$
0
0

Kituo cha Redio Times cha jijini Dar es Salaam kilichorusha mahojiano ya  mwanamuziki Diamond Platnumz kimeomba radhi kwa kauli tata zilizozua mjadala nchini.

Taarifa hiyo iliyowekwa  katika mtandao wa kijamii wa Instagram, ilisema imeamua kuomba radhi kutokana na kauli tata alizotumia msanii huyo wakati akihojiwa katika kipindi cha Play List kinachoongozwa na mtangazaji Omary Tambwe.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba siku hiyo Diamond alialikwa katika kipindi hicho  kwa ajili ya kupongezwa kwa kumpa tuzo maalumu nyota wa mchezo kwa mchango wake kwenye muziki na  kutoa ajira kwa vijana.

Jingine ni kutangaza lugha ya Kiswahili kupitia muziki na kupeperusha bendera ya Tanzania kupitia sanaa ya muziki na kutoa albamu yake mpya ya ‘A Boy From Tandale ‘  ambapo kituo hicho kilimtaja kama msanii bora wa kiume, msanii bora wa kimataifa kwa kuvunja rekodi na  msanii mwenye ushawishi zaidi na pia kumpatia tuzo maalum (Plaque).

“Kwa namna ambayo haikutarajiwa , mwanamuziki huyo alitumia kauli  tata dhidi ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Juliana Shonza katika mahojiano hayo.

“Uongozi wa Times unaomba radhi kwa Wizara, Naibu Waziri, TCRA, Basata pamoja na umma kutokana na kauli hiyo ya Diamond kwani Times haikuwa dhamira yetu kwa sintofahamu hiyo na tumekuwa tunafanya jazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za utangazaji,” imesema taarifa hiyo.


Tamko la CHADEMA Kuhusu Viongozi wao Kulazwa Mahabusu

$
0
0

Kamati Kuu ya chama hicho jana Jumatano, Mach 28 ilikutana  na  kutoa  msimamo wake  ambapo walidai kuwa hawapo tayari kuendelea  kuonewa. 

Juzi Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wenzake  walifikishwa mahakamani na kuswekwa rumande baada ya kunyimwa dhamana,

Baadhi ya viongozi wa Chadema waliozungumza ni pamoja na Makamu mwenyekiti wa Chadema, Profesa Safari, Godbless Lema na John Mrema, ambapo mkutano huo pia ulihudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Kuu akiwemo Edward Lowassa, Fredrick Sumaye na Meya Boniface Jacob.

Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Abdallah Safari alisema tukio la kunyimwa dhamana na kupelekwa rumande kwa viongozi hao ni uonevu kwani dhamana ni haki ya mtuhumiwa anapokamatwa.

“Licha yaa jitihada za mawakili wetu kuwatetea viongozi wetu lakini wamewanyima dhamana. Tumemwandikia barua Jaji Mkuu kumwambia mbona kila tunapokamatwa linapofika swala la dhamana tunakataliwa? Jaji Mkuu kajibu kirahisi sana eti kateni rufaa,” alisema Prof. Abdallah Safari.

Kwa upande wake, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema kwamba anafahamu kuwa upo mkakati wa kuwafunga Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine waliowekwa mahabusu tangu jana.

“Huo mchezo wanaotaka kufanya waendelee nao, wamewanyima dhamana ili kesi iendeshwe haraka na wawafunge kama alivyofanyiwa Sugu. Tunajua vikao vyao na nia yao. Wakitaka tusema, ukiogopa kufa utakufa.

“Sisi tutaweka mambo mengi hadharani, sina uhakika kama Mwenyekiti wetu kesho(leo) atapewa dhamana. Hapa tulipofika hatuwezi kuendelea kuishi kwa hofu. Hii vita si ya Chadema, hii ni vita ya demokrasia, Akwilina hakuwa mwanachama wa Chadema lakini aliawa, sasa nafikiri inatosha.

“Baada ya kutoka mahakamani kesho(leo) tutakutana na kuamua iwapo tufungulie maji na tuanike kila kitu kwa sababu hatuna namna. Yeyote aliyehusika tutamuanika,” alisema Lema.

Kituo cha redio cha Times FM kimeomba radhi Wizara ya Habari Kwa Kumuhoji Diamond Platnumz

$
0
0

Kituo cha redio cha Times FM kimeomba radhi Wizara ya Habari, Naibu Waziri Juliana Shonza, TCRA,
BASATA pamoja na umma kutokana na kauli tata zilizotolewa na mwanamuziki Diamond Platnumz katika moja ya mahojiano yake hivi karibuni.

Times FM imesema kuwa, hiyo haikuwa dhamira yao.

Jeshi la Polisi Lakanusha Kuhusika na Kifo cha Kijana Allen Mapunda Huko Mbeya

$
0
0

MBEYA: Jeshi la Polisi limeutaarifu umma wa Watanzania kuwa halihusiki kwa namna yoyote na kifo cha kijana Allen Mapunda(20) anayedaiwa kufariki saa chache baada ya kutoka Kituo cha Polisi.
-
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga amewaambia Wanahabari kuwa, Jeshi hilo limeanza kufanya uchunguzi wa kina kuhusu kifo cha kijana huyo
-
Kamanda Mpinga amesema kijana huyo aliachiwa na Jeshi la Polisi muda wa saa nne asubuhi baada ya kudhaminiwa na ndugu zake na ilipofika saa 12 jioni zilipatikana taarifa kuwa mtuhumiwa huyo amefariki dunia
-
Jeshi la Polisi linatuhumiwa na Wananchi pamoja ndugu kuhusika katika kifo hicho kwani inadaiwa kuwa kijana Allen alidhoofika sana kwa kupigwa na kuteswa akiwa mikononi mwa Jeshi hilo.
Viewing all 104796 articles
Browse latest View live




Latest Images