Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Halima Mdee Yupo Hospitali Afrika Kusini Kesi Yake Yakwama

$
0
0
Halima Mdee Yupo Hospitali Afrika Kusini Kesi Yake Yakwama
Kesi ya kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili mbunge wa Kawe, Halima Mdee leo March 29, 2018 imeshindwa kuendelea baada ya mshtakiwa kuwa mgonjwa.

Kesi hiyo imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na mshtakiwa huyo kuwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu.

Mdee anakabiliwa na shtaka moja la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais,  kwa kusema, “anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afungwe breki” kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

“Kesi hii imekuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi na tayari upande wa mashtaka tunaye shahidi hapa mahakamani, lakini nimepata taarifa kuwa mshtakiwa ni magonjwa na ameshindwa kufika mahakamani hapa,” -Wakili Mwita.

Baada ya kueleza hayo, wadhamini wa Mdee, Fares Robison ambaye ni Diwani wa Mbezi Juu na Martha Mtiko Diwani wa viti maalumu, wameieleza mahakama hiyo kuwa Mdee yupo Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu. Baada ya maelezo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi May 3, 2018 itakapoendelea na ushahidi.

Mkwasa Atangaza Rasmi Mkutano Mkuu wa Yanga

$
0
0
Mkwasa Atangaza Rasmi Mkutano Mkuu wa Yanga
Katibu Mkuu wa Young Africans  Sports Club, Charles Boniface Mkwasa ametangaza rasmi siku maalumu ambayo itafanya mkutano mkuu wa wanachama wote wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali muhimu ya maendeleo.

Muda mfupi uliopita Mkwasa ameiambia tovuti ya klabu hiyo kuwa wanachama wa Yanga wanapaswa kufanya maandalizi ya kuhudhuria mkutano huo sasa kwa kulipa ada zao mapema kwa sababu kwenye mkutano huo ukaguzi mkubwa utafanyika kabla ya watu kuingia ndani ya ukumbi.



Mkwasa ameongeza kuwa kupitia kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika jumapili iliyopita imeridhia kufanyika kwa Mkutano huo na kuomba wanachama kujindaa kwa ajenda ambazo zitatangazwa baaadae.

Mkutano huo umepangwa kufanyika Mei 5 mwaka 2018 jijini Dar es Salaam huku wanachama wenye kadi za aina zote mbili za zamani na zile zinazotolewa kupitia benki ya posta wataruhusiwa kuingia ukumbuni.

Rapper DMX Ahukumiwa Kifungo cha Mwaka Mmoja Jela

$
0
0
Rapper DMX Ahukumiwa Kifungo cha Mwaka Mmoja Jela
Rapper kutoka nchini Marekani anayeunda kundi la Ruff Ryders, DMX amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.

 DMX alikamatwa July mwaka jana, kwa mujibu wa CBS rapper huyo anadaiwa kiasi cha dola milioni 1.7 ambapo inasemekana alifungua akauti benki nyingine na kutumia jina jingine ili kukwepa kodi.

DXM alikuwa akikabiliwa na mashtaka 14 ya ukwepaji kodi, hata hivyo alilipa faini ya dola 5000,000 za Kimarekani kinyume na hapo angetumikia kifungo cha miaka 44 jela.

Imeripotiwa kuwa DMX ameingiza zaidi ya dola milioni 2.3 kwa mwaka 2010 hadi 2015 lakini msanii huyo alikwepa kulipa kodi. Rapper huyo ni baba wa watoto 15.

Wafuasi wa Chadema Waliamsha Dude Mahakamani

$
0
0
Wafuasi wa Chadema Waliamsha Dude Mahakamani
IKIWA ni saa 48 zimepita tangu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wenzake watano wa chama hicho kupelekwa katika mahabusu ya Segerea baada ya kunyimwa dhamana katika kesi yao waliyosomewa juzi Machi 27, Katika Mahakama ya Kisutu Dar, wafuasi wa chama hicho waliofurika mahakamani hapo wamezua sintofahamu baada ya kufanya vurugu wakipiga makelele na kuimba wakitaka haki.

Wafuasi hao waliokuwa nje ya geti la mahakama hiyo wakiwa wamekusanyika baada ya Jeshi la Polisi kuwazuia kuingia mahakamani kusikiliza kesi ya viongozi hao walianza kupiga makelele wakiimba ‘hatupoi hatupoi, tunataka haki tunataka haki’, hali iliyowalazimu polisi kutia kambi eneo hilo na kuimarisha ulinzi kuhakikisha hakuna uvunjifu wowote wa amani unafanyika.

Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea tena leo Machi 29, ili kufanya jitihada za kupata dhamani. Viongozi wengine waandamizi wa Chadema wanaoshtakiwa katika kesi hiyo ni: Vicent Mashinji, John Mnyika, Peter Msigwa, Ester Matiko na Salum Mwalimu, watapandishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa masharti ya dhamana kama ipo au haipo.

Haya Hapa Ndio Makosa ya Mwanaume Yanayosababisha Mke au Mchumba Amsaliti

$
0
0
Kuna sababu anuai zinazomfanya mwanamke amsaliti mumewe. Ni muhimu kutambua kuwa mwanamke ni kiumbe mwenye hisia kali na daima ahisi raha na amani. Baadhi ya nyakati hufanya usaliti ili kuziba pengo la upungufu unaotokea katika maisha yake. Zifuatazo ni sababu kubwa ambazo zinamfanya amsaliti mumewe:

1. KUTOMPA KIPAUMBELE NA KUTOMTHAMINI

Tunatambua kuwa mke anafanya kazi kubwa sana ambayo lau kama ingekuwa ni kampuni basi pangehitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya. Atamtunza mume, watoto, nyumba na familia kwa ujumla.

Wakati fulani mume anaweza akampuuza na asimthamini, licha ya kujitoa kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia. Hivyo, kutotoa kipaumble kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu mume, mke akipata mtu anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hataacha kuitumia hiyo fursa.

2. UKOSEFU WA MAHABA

Kwa asili mwanamke ana silika ya hitajio la kupendwa, mwanamke anahitaji kupendwa, mwanaume yeye ana silika ya kupenda ngono, ukimpa ngono tu basi anaridhika.

Mwanamke anahitaji kupetiwapetiwa, anahitaji kudekezwa, anahitaji aambiwe maneno yenye ladha adimu yaliyochanganywa na vionjo vya ndimu, mwanamke anataka hivyo, anataka aone kama anapendwa, anataka aone mtu anamwambia vile alivyo, alivyo maridhawa, amueleze hisia zake, ampe lugha ya kimajnun, mwanamke anamtaka Majnun. Sasa akimpata mtu wa aina hiyo, tofauti na mumewe, huwa ni balaa tupu, mnanipata hapo?

3. USALITI WA MUME

Miongoni mwa mambo ambayo huibadilisha roho ya mwanamke ni pale anapogundua kuwa mumewe kipenzi anamsaliti. Hapo mwanamke anaweza akabadilika kabisa. Wapo wanaosamehe, lakini wapo wanaolipiza kisasi.

4. KUTOJIAMINI

Mwanamke anahitaji mwanaume anayemfanya ajiamini iwapo mumewe hatekelezi jukumu hilo, akimpata mtu anayemfanya ajiamini, yanaweza kutokea mengine kabisa. Hivyo, nasaha zangu kwa kaka zangu kuyaangalia kwa makini mambo haya.

Jux Afunguka Sakata la Ujauzito wa Vannessa

$
0
0
Jux afunguka sakata la ujauzito wa Vannessa
Msanii wa muziki BongoFleva Juma Jux ambaye yuko kwenye mahusiano ya kimapenzi na Vanessa Mdee, amekanusha taarifa za mpenzi wake huyo kuwa mjamzito na kudai kwa sasa hawajajipanga kufanya hivyo ila endapo watakuwa tayari kwa hilo watasema.


Jux ameeleza hayo wakati alipokuwa anahojiwa na moja wapo ya chombo cha habari nchini Tanzania baada ya kuenea picha ya mpenzi wake Vanessa mitandaoni ikiwa inamuonesha tumbo lake limeja jaa mithiri ya ujauzito.

"Kiukweli Vanessa hana ujauzito ile ni picha tu, labda siku hiyo alikuwa ametoka kula 'ameshiba' na kupigwa picha vibaya ndio ikatokea hivyo. Lakini hakuna kitu kama hicho, hivyo vitu inabidi viende kwa mipango pia lazima mwenzako umshirikishe endapo unataka kufanya hivyo na mkubaliane ili mambo yaweze kwenda sawa", amesema Jux.

Pamoja na hayo, Jux ameendelea kwa kusema "ikifika 'time' watu watajua kwasababu sisi hatuwezi kuficha mambo hata kama sisi hatuto-post lakini inaweza akaja ku-post mtu mwingine kwa kutuona sehemu fulani".

Jux kwa sasa anafanya vizuri kibao chake kipya kilichopewa jina la 'fimbo' aliyoachia siku za hivi karibuni.

Makonda Atoa Zawadi ya Vifaa vya Kujifungulia kwa Wajawazito Watakaojifungua Pasaka

$
0
0
Makonda Atoa Zawadi  ya Vifaa vya Kujifungulia kwa Wajawazito Watakaojifungua Pasaka
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo ametoa zawadi ya vifaa tiba vya Mama mzazi kwaajili ya kujifungulia (Delivery Packs) 200 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi million 20 Kama zawadi yake ya sikukuu ya pasaka kwa kinamama watakaojifungua kwenye msimu huu wa pasaka.

Gharama ya mfuko mmoja (package) ya Vifaa hivyo vya kisasa ni Shilingi laki Moja ambapo ndani yake kuna Mashuka, Vitambaa, Dawa, Mabomba ya Sindano, Pamba, Kibanio cha kitovu, Nyuzi, pedi za kinamama, Dawa ya kuzuia upotevu wa damu, Nyembe na Gloves ambapo vitatolewa Bure kwa Mama mzazi atakaejifungua msimu huu wa pasaka kwenye vituo vya Afya na zahanati zilizopo kwenye Wilaya Tano za Mkoa huo.

Makonda ametoa vifaa hivyo baada ya kubaini changamoto ya baadhi ya kinamama kushindwa kumudu gharama ya vifaa vya kujifungulia na kujikuta wanatumia kanga au nguo jambo ambalo ni hatari kiafya kwa mama na mtoto.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Makonda kwa waganga wakuu wa halmashauri na wasimamizi wa vituo na Zahanati, Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Grace Maghembe amesema vifaa hivyo vitasaidia pia kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Vifaa hivi vinapatikana Bure kwenye Hospitali zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwa Msimu huu wa Pasaka hivyo kwa wewe Mama unaetaka kujifungua fika Hospitalini vifaa vyako utavikuta.

Kimenuka! Dili la Zali Lawagombanisha Shamsa Ford na Faiza

$
0
0
Kimenuka! Dili la Zali Lawagombanisha Shamsa Ford na  Faiza
Baada ya hapo jana aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady kupata dili la kuwa balozi wa bidhaa za Softcare Diapers, mjadala umekuwa mkubwa ni kwanii mastaa wa kike Bongo hawapati fursa kama hizo.

Muigizaji Faiza Ally alihoji ni kwa nini mastaa wa Bongo hawajapata dili hilo badala yake akapewa mtu mwingine, Faiza alienda mbali zaidi kwa kusema Wakenya na Waganda hawezi kufanya kitu kama hicho.

Sasa Shamsa Ford amepigana na mtazamo wa Faiza kwa kueleza kuwa mastaa wa kike Bongo wamejiharibia wenyewe ingawa wanajulikana lakini si kwa upande ambao unavutia kibiashara. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

Naona tu watu wanalalamika kwanini madili yanawapita mastar wa bongo na wageni ndo wanapata nafasi hiyo. Mimi nina mtazamo tofauti kabisaa, kabla ya kuanza kumtafuta mchawi ni nani ni bora kwanza tukajikagua wenyewe kwanza, nina uhakika kila biashara ina condition zake na kila biashara inahitaji faida.

Hakuna mfanyabiashara atayekubali kumchukua STAR wa bongo kisa uzalendo tu halafu apate hasara, tusipinge ukweli sisi wenyewe baadhi ya wasanii tumevunja uaminifu kwa wafanyabiashara wakubwa kutokana na matendo yetu. Unapozungumzia kuwa ambassador unazungumzia kubeba brand ya mtu, sasa ni nani anaetaka kuchafua brand yake ibebwe na mtu asieeleweka, swala sio kujulikana tu ila unajulikana vipi!?

Maana kama jamii inakudharau hata hiyo bidhaa unayoibeba itadharaulika.kikubwa tujifunze, swala sio kujulikana ila swala ni kuwa unajulikana vipi!? Watu wanakutambua kwa lipi kisha akili kichwani mwako .Ni vizuri tumeumia sasa tujipange na kufukiaa mashimo yaliyotoboka ili na sisi tueshimike na kuthaminika…Niliowakera mnisamehe tu lazima tuishi kwa kuambiana ukweli.

Soma Pia; Zari awanyoosha mastaa wa kike Tanzania, alamba dili nono Dar

Utakumbuka February 14 mwaka huu (Valentine’s Day) Zari The Boss Lady alitangaza rasmi kuachana na Diamond kutokana na kuchoshwa na habari za kusalitiwa ambazo husikika kila siku katika vyombo vya habari. Katika mahusiano yao Diamond na Zari wamefanikiwa kupata watoto wawili ‘Tiffah na Nillan’.

Twaweza:Asilimia 80 Wataka Uhuru Kumkosoa Rais

$
0
0
Twaweza:Asilimia 80 Wataka Uhuru Kumkosoa Rais
Utafiti uliofanywa na taasisi ya TWAWEZA na kuripotiwa leo Machi 29, 2018 umedai kuwa asilimia 80 ya wananchi wanataka wawe huru kumkosoa Rais katika mambo ambayo anafanya ndani ya nchi.


Katika utafiti huo ambao umeonyesha kuwa asilimia 70 ya Watanzania wamekuwa wakiamini zaidi kauli zinazotolewa na Rais John Pombe Magufuli wamehitaji kuwa huru pia kukosoa kauli hizo, asilimia 60 wanasema hawako huru kukosoa kauli zinazotolewa na Rais wakati asilimia 54 wanasema hivyo kuhusu kauli zinazotolewa na Makamu wa Rais na asilimi 51 kwa kauli za Waziri Mkuu.

Aidha utafiti huo umekwenda mbali zaidi na kuonyesha kuwa wananchi wanajisikia huru kuwakosoa Wenyeviti wa Vijiji, mitaaa na viongozi wa upinzani pamoja na madiwani

"Wananchi 8 kati ya 10 wanasema wanajisikia huru kuwakosoa mwenyeviti wa vijiji/mitaa (83%), viongozi wa vyama vya upinzani (77%), madiwani (76%)." alisema taarifa ya TWAWEZA

Mbali na hilo Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amefunguka juu ya utafiti huo na kusema kuwa yeye amekuwa akimshauri Rais John Pombe Magufuli na amekuwa akishaurika hivyo anashangaa kuona watu wanasema Rais hashauriki na kudai kuwa kuna njia ya kumkosoa Rais.

"Rais ni mtu mkubwa sana hata kumkosoa kunahitaji taratibu fulani. Kwenye familia unaweza kumkosoa kaka lakini baba huwezi kumwambia 'umebugi' mimi huwa namshauri Rais na ananisikia, wanaosema hashauriki wanamshauri wapi? alihoji Dkt. Abbas 

Naombeni Msaada Kila Nikifanya Mapenzi Bila Zana Napata Ujauzito

$
0
0
Mimi ni Msichana wa Miaka 25 , Tatizo langu ni kuwa kila nikifanya mapenzi na mvulana bila kutumia zana lazima nipate mimba, nilianza kuwajua wanaume toka nikiwa na miaka 21 siku niliyotolewa bikira nilipata mimba pia ikanibidi niitoe kwa vile nilikuwa nasoma ..sasa kuanzia kipindi hicho nikifanya tu lazima nipate mimba nimeshatoa mimba kumi na tano mpaka sasa, Nimejaribu kufuata Calender lakini wapi...Je hili ni Tatizo ama nimelogwa ? Nimekuwa mtu wa kufanya abortion kila wakati mpaka naogopa sasa nisije haribu kizazi changu nikashindwa kuzaa muda muafaka wa kuwa na mtoto....................

Help pliz
Mimi Mdau ..Msinitukane jamani

Askari Amuua Raia kwa Risasi kwa Sababu ya Mlegezo

$
0
0
Askari Amuua Raia kwa Risasi kwa Sababu ya Mlegezo
Kutoka Houston, Texas, nchini Marekani, inaripotiwa kuwa askari mmoja amempiga risasi mwanaume mmoja asiye na silaha hadi kufariki ambaye alikuwa anatembea barabarani huku suruali yake ikiwa miguuni.

Kamera iliyonasa tukio hilo imemuonesha kijana huyo Danny Ray Thomas mwenye miaka 34, akitembea na polisi huyo kuanza kupiga kelele akimwambia lala chini na kisha akafyatua risasi na kumpiga.

Inaelezwa kuwa askari na mhanga huyo wa ‘ukatili wa polisi’ wote ni weusi wa Asili ya Afrika.

Familia ya marehemu, imeeleza kuwa ndugu yao alikuwa akitembea na suruali ikiwa miguuni kwasababu alikuwa anapitia msongo wa mawazo ‘depression‘ baada ya watoto wake kufariki.

Mwanaume Agundulika na Kisonono Kisichotibika

$
0
0
Mwanaume Agundulika na Kisonono Kisichotibika
Mwanaume mmoja nchini Uingereza amezua gumzo baada ya kupimwa na madaktari na kukutwa na ugonjwa wa kisonono katika kiwango cha juu na kibaya zaidi kuwahi kutokea duniani.

Inaelezwa kuwa mwanaume huyo alikuwa na mpenzi mmoja akiwa nchini Uingereza lakini aliupata ugonjwa huo baada ya kukutana kimwili na mwanamke kutoka Kusini Mashariki mwa bara la Asia.

Madaktari wameeleza kuwa mwanaume huyo alipata maambukizi hayo tangu mwanzoni mwa mwaka huu na hadi sasa ugonjwa huo umeshindwa kutibika.

Maafisa afya tayari wameshaanza kutafuta wanawake wengine ambao yawezekana wamekuwa na uhusiano na mwanaume huyo ili pia waanze kusaidiwa.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 622588038au 0679119679 au +255 764318107

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Video:Steve Nyerere “Wenye Akili Tupo Wachache, Wajinga Wengi Wanatuchafua”

$
0
0
Video:Steve Nyerere “Wenye Akili Tupo Wachache, Wajinga Wengi Wanatuchafua”
Baada ya Kusambaa Picha inayoonesha waigizaji wakiwa gerezani huku mlangoni kufuli  likiwa limeachwa na ufunguo ukiwa umebaki palepale kitu kilichozua gumzo kwenye mitandao ya kijamii watu wakijadili Bongo Movie kuwa inazidi kupotea.

Steve Nyerere amesema kuwa hiyo ni kwa sababu wenye akili kama yeye wapo wachache kuliko wajinga walio wengi ambao wamekuwa wakichafua tasnia hiyo ila yeye anaamini kuwa ile ilikuwa behind the scene ila hajui aliyeisambaza ile alikuwa nani.

Zifahamu Hatari Kuu Zilizojificha Ndani ya Bafu Lako

$
0
0
Zifahamu Hatari Kuu Zilizojificha Ndani ya Bafu Lako
Watafiti katika nchini Uingereza wanasema kuwa usafi wa bafuni ni jambo linalofaa kuzingatiwa kuliko wengi wanavyodhania.

 "Bafu ni mahali ambapo usafi wake huwa ni mgumu''

"Watu hutumia muda wao katika kusafisha vyoo vyao lakini ingelikuwa vyema kama kila mtu angezingatia zaidi usafi wa bafu kwa kutumia madawa ya kuuwa bakteria."

1.Kuoga kwa kutumia kifaa cha kukumwagia maji mwilini kwenye bafu za manyunyu

Wataalamu wanasema unapotumia kifaa hiki kwenye bafu za manyunyu hunabudi kuwa makini sana, kwani kinapotumika baada ya kuzimwa kwa muda mrefu na kutumiwa tena hugeuka kuwa makao ya vimelea vya bakteria.

Hatari nyingine kwa watu wazima na watoto itokanayo na kifaa hicho (shower) ni uwezekano wa kuunguzwa na maji yanayotoka kwenye kifaa hiki ambacho kinaweza kuwa moto sana na kuuchoma mwili.

Msemaji wa kituo cha utafiti Rospa ameiambia BBC: " Tunawaomba watu kuweka maji baridi kwanza ndani ya beseni/ vidimbwi vya maji ya kuoga kwa ajili ya watoto . Kwa kufanya hivyo unawaepusha watoto na hatari ya kuungua kwao wanapojaribu kujifungulia maji ya moto.

Mimea sita ya kushangaza zaidi duniani
"Kuna uwezekano mkubwa kwamba pale unapoweka maji moto kwenye beseni/ama kidimbwi cha maji ya kuoga watoto wanaweza kuyanawa na kuungua, lakini unapoweka maji ya baridi kwanza ndani ya beseni na baadae kuyachanganya na ya moto, uwezekano watoto kuungua utakuwa ni mdogo ".

2. Sabuni ya kuoga huenda ikawa si salama

Mkono ulioshikilia sabuni ya kuogeaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kwa kawaida unapotumia kipande cha sabuni cha kuoga unatarajia kitasafisha mikono yako kwa hivyo si rahisi kufikiria kwamba kinaweza kuwa kitovu cha vimelea vya maambukizi.

Hata hivyo unaweza kuwa unajidanganya, kulingana na wataalam wa masuala ya afya.

Profesa wa Oxford anasema: "Bakteria wanaweza kukaa kwenye sabuni ya kuogea na kuhama kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine - mfano bakteria aina ya E.coli ambao huishi maeneo hayo.

" Ikiwa mtu atatoka nje ya kikundi cha familia akiwa na bakteria ama mmoja wa familia akipata bakteria hao , basi bafu litakuwa mahala salama kwa bakteria hao kuishi na kusambaa kwa familia nzima."

Mambo muhimu kuhusu sayari ya Mars
Profesa wa Oxford anashauri kuwa matumizi ya sabuni ya maji ni bora kuliko kipande cha sabuni kwa matumizi ya kifamilia .

Na taasisi ya kitaifa ya afya na ushauri bora wa kiafya nchini Uingereza iliwashauri maafisa wa afya nchini humo kutumia sabuni za maji ama zilizowekwa kwenye chupa kunawa mikono .

3. Taulo pia si salama zisipotumiwa kwa makini


'' Usiwahi kamwe kutumia taulo moja na mtu mwingine'' wanashauri wataalam wa masuala ya afya
Taulo iliyokaushwa vizuri na pengine ukaipiga pasi , ni bora kwa kukausha mikono ama uso wako unapokuwa na maji nyakati za mchana.

Lakini usiruhusu kwa namna yoyote ile mtu mwingine aitumie, anashauri Profesa Oxford.

"Taulo ni kitu chenye utata," alisema Profesa Oxford. "Usiwahi kutumia kamwe taulo moja na mtu mwingine - Sishauri hilo."

Asali ''inaweza kukabili maambukizi ya mkojo''
Ni jambo la kawaida kwa watu kutumia taulo moja katika maeneo ya sinki za bafuni/chooni ambayo hutumiwa na wanafamilia na hata marafiki wanaotembelea familia.

Hata hivyo , Profesa Oxford anasema: "Ni heri kuepukika'' . Vimelea vya magonjwa /bakteria vinaweza kukaa kwenye taulo kwa saa nne. Kusema ukweli taulo ni mahala pazuli kwao kukaa kwa sababu hewa imefunikwa na kuwa nzito

"Ningeshauri karatasi laini zitumiwe kama kukausha mikono badala ya taulo na kutupwa kwenye debe la taka au kila mtu awe na taulo yake"

4. Hatari ya kuwaogesha watoto wakiwa na doli zao za plastiki bafuni

Utafiti kuhusu athari za kuingia katika bafu lako na vifaa vingine mfano doli za plastiki unapoenda kuwaogesha watoto wadogo kunaweza kusababisha hatari kubwa.


Gazeti la Times limeripoti juu ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Uswiss ya Sayansi na Teknolojia ambapo watafiti walifanyia uchunguzi doli zinazochezewa na watoto wakati wa kuoga na kubaini kuwa asilimia 58 ya doli hizo zilikuwa na bakteria hatari aina ya fangasi.

Mkuu wa utafiti huo alionya watu wasiwarushie watoto wao maji usoni kwa kutumia doli za kuchezea kwani anasema inaweza kusababisha "maambukizi ya macho, maskio au hata ya tumbo".


Doli la plastiki la bata ambalo hutumiwa sana na wazazi kuwapumbaza watoto wakati wanapooshwa ambalo ni mojawapo ya doli zinazoweza kutunza vimelea/bakteria wa maambukizi
5. Kuteleza kwa sakafu ya bafu pia ni hatari nyingine ya bafuni

Ni dhahiri kwamba kuanguka bafuni kuna madhara yake makubwa , sabuni na maji kwa pamoja huifanya sakafu kuwa ya kuteleza.

Mtoto mchanga akiwa ameketi kwenye kiti cha kuogea bafuni. Wataalam wa afya wanasema kifaa kama hiki si salama kwani kinaweza kutunza bakteria wa maambukizi na kumuambukiza mtoto
Watu hupata majeraha ya mara kwa mara kwa kuvunjika mifupa , majeraha ya mwili, na vidonda wanapoingia ama kutoka bafuni , ama wakati mwingine huanguka kwenye sakafu yenye unyevunyevu

Kujaribu kupunguza matatizo haya, watu wanashauriwa kutumia mazulia ya bafuni kwenye sakafu ,mazulia ya kuzuwia kuteleza ndani ya vidimbwi vya maji na kusafisha mabomba na sakafu za bafu mara baada ya kulitumia hususan pale wanapotumia sabundi za mafuta (jeli) ama mafuta ya mwili.

Ireland Kuhalalisha ‘Utoaji Mimba’ kwa Kura

$
0
0
Ireland Kuhalalisha ‘Utoaji Mimba’ kwa Kura
Nchi ya Ireland ambayo ni ya misingi ya kidini hususani kwa dhehebu za Kikatoliki, suala la utoaji mimba kwa miaka mingi limekuwa haramu hata kama ni kwa kesi za kidaktari.

Kutokana na marufuku hiyo ya kisheria wanawake wamelazimika kwa kipindi chote kwenda kutibiwa nchi za nje endapo madaktari watasema inabidi watolewe mimba hizo kutokana na kuhatarisha maisha yao .

Hali hii imeanza kubadilika ambapo wanaharakati kwa miaka wameshinikiza kufutwa kwa sheria hii na kuhalaisha utoaji wa mimba kwa wanawake, na jana March 28, 2018 Waziri wa Afya nchini humo Simon Harris amezungumza.

Waziri huyo ameeleza kuwa May 25, 2018 itapigwa kura ambayo ndiyo itatoa hatima ya kuhalalishwa kwa sheria mpya ya utoaji wa mimba nchini humo baada ya miaka 35 au la.

CAG Aomba Radhi Wananchi Juu ya Taarifa ya Deni la Taifa Aliyompa Rais Magufuli "Yalikuwa Makosa ya Kimatamshi Deni ni Himilivu"

$
0
0
CAG Aomba Radhi Wananchi Juu ya Taarifa ya Deni la Taifa Aliyompa Rais Magufuli  "Yalikuwa Makosa ya Kimatamshi Deni ni Himilivu"
Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Profesa. Mussa Assad ameomba radhi wananchi na serikali juu ya taarifa ya deni la taifa na kusema kuwa yalifanyika makosa ya kimatamshi deni hilo ni himilivu.


Profesa Assad ametoa taarifa hiyo mjini Dodoma ambapo amesema deni halisi ni shilingi trillion 46.08 na ni himilivu hivyo anaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa wananchi na taasisi za serikali.

"CAG anapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kauli yake aliyotoa kuhusiana na mwenendo wa na ukuaji wa deni la taifa kama alivyonukuliwa wakati akitoa ripoti hizo kwa Mhe. Rais Magufuli taarifa sahihi kuhusu mwenendo wa deni ni kwamba kwa kujibu wa taarifa ya maandishi wa CAG hadi kufikia tarehe 30 Juni 2017 deni la taifa lilikuwa ni trilioni 46.08 katika deni hilo deni la ndani ya trilioni 13.34 sawa na asilimia 16 na deni la nje nu trilioni 37.75 ambayo ni sawa na asilima 71, kwa hivyo utafiti umebaini kuwa deni la taifa kwa sasa ni himilivu"

CAG wakati akitoa ripoti hiyo kwa Rais John Pombe Magufuli kuhusu suala la muenendo wa deni la taifa alidai kuwa deni la taifa si himilivu lakini kwa mujibu wa utafiti ambao wamefanya wao CAG ameibuka na kuomba radhi na kusisitiza kuwa ripoti ya CAG ni siri hadi itakapowasilishwa bungeni.

Mahakama ya Kenya Yawahukumu Waziri, IGP na Mkuu wa Uhamiaji Kisa Mugina

$
0
0
Mahakama ya Kenya Yawahukumu Waziri, IGP na Mkuu wa Uhamiaji Kisa Mugina

Mahakama nchini Kenya imewahukumu Waziri Fred Matiang'i, Mkuu wa Uhamiaji Gordon Kihalangwa na IGP Joseph Boinnet kulipa faini KSh200,000 (Sh4.4m) kwa kosa la kuidharau mahakama

Jaji wa Mahakama Kuu George Odunga Jumatano alisema waziri wa usalama nchini humo, mkuu wa polisi na mkuu wa idara ya uhamiaji watakuwa wamekaidi maagizo ya mahakama iwapo wangekataa kumwachilia huru.

Alikuwa ametoa ilani kwa watatu hao kufika mahakamani baadaye Jumatano lakini baada yao kukosa kufika akawapata na hatia ya kukaidi agizo la mahakama.

Wizara haina ugomvi na msanii yeyote wa Tanzania – Waziri Shonza

$
0
0
Wizara haina ugomvi na msanii yeyote wa Tanzania – Waziri Shonza
Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) leo tarehe 29 Machi, 2018 akimbatana na Naibu Waziri, Juliana D. Shonza (Mb), Katibu Mtendaji wa BASATA, Mwakilishi wa Bodi ya Filamu Tanzania na Katibu wa Chama cha Muziki wa Kizazi (TUMA) wamekutana na wasanii Roma Mkatoliki na Suzan Michael (Pretty Kind) kujadili maombi yao ya kusamehewa adhabu zao za kufungiwa kujishughulisha kwenye Sanaa kwa kipindi cha miezi 6.



Baada ya majadiliano yaliyochukua zaidi ya masaa 4 Waziri na Naibu Waziri walitoa uamuzi wa kuwafungulia wasanii hao ili waendelee kujishughilisha na kazi za sanaa. Aidha, Msanii Roma alitangaza kuufuta wimbo wake wa “kibamia” na kuomba vyombo vyote vya matagazo nchini kutourusha wimbo huo, ili usiendelee kuleta ukakakasi nchini.

FA,JDee Kupanda Jukwaa Moja

$
0
0
FA,JDee Kupanda Jukwaa Moja
BAADA ya kutofautiana kwa takribani miaka mitano, wakongwe kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ pamoja na Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ wanatarajia kukutana jukwaa moja, Jumamosi hii (Machi 31) ndani ya Ukumbi wa Golden Tulip, Oysterbay.



Akizungumza na Showbiz, Jide alisema shoo hiyo itakuwa ya kihistoria kwake na kuwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia vibao watakavyoimba yeye na MwanaFA kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka zaidi ya mitano.


“Sina mengi ya kusema zaidi ya vitendo jukwaani. Nitapiga live band jimbo zangu karibu zote,” alisema Jide.



Miongoni mwa nyimbo zilizotamba ambazo wataimba kwa pamoja mwanaFA na Jide usiku huo ni Hawajui, Msiache Kuongea, Wanaume Kama Mabinti pamoja na Sikiliza.

ANDREW CARLOS.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images