Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Taharuki Yatanda Baada ya Kuamka na Kukuta Jeneza Tupu Nje ya Nyumba Yake

$
0
0
Taharuki Yatanda Baada ya Kuamka na Kukuta Jeneza Tupu Nje ya Nyumba Yake
NELSON Edson, mkazi wa Mtaa wa Nsalaga Kata ya Nsalaga jijini hapa amejikuta kwenye taharuki kubwa baada ya kuamka na kukuta jeneza tupu dogo nje ya mlango wa nyumba yake.

Tukio hilo lililoibua hekaheka mtaani hapo lilijiri asubuhi ya Machi 27, mwaka huu.



Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Nsalaga, Paul Ngonde, alipokea taarifa kutoka kwa Edson na kuamua kwenda eneo la tukio ili kushuhudia.

Alisema kuwa, baada ya kuwashirikisha wazee wa mila juu ya jambo hilo, walilifungua jeneza hilo na kukuta likiwa tupu, lakini likiwa na sanda nyeupe iliyoviringishwa ndani yake.



“Nimeshangaa asubuhi kuamka na kukuta jeneza nje ya mlango wa nyumba yangu, sijaelewa ni nini madhumuni ya kuwekewa jeneza hilo,” alisema Edson huku akionesha kustaajabishwa na tukio hilo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, mtaa huo umekuwa na matukio ya ajabuajabu yakiwemo ya kutupa watoto, lakini tukio hilo la jeneza limekuwa ni tukio la kwanza kutokea mtaani kwake.



Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, DCP Mohammed Mpinga alikiri kutokea kwa tukio na kwamba jeshi lake linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo huku akiwataka wanachi kutulia.

Punguza Unene Unaokusumbua Katika Mwili Kwa Kutumia Bidhaa za Edmark

$
0
0
"Tumia Dawa za Edmark za Kupunguza uzito uliozidi Mwilini Mwako, Edmark ni Vurutubisho na Chakula Mbadala na Zimehakikiwa na TFDA...

Ni uhakika kwa afya yako,👉 kupunguza uzito na sumu mwilini, Mafuta Sehemu Mbaya, Kitambi na nyama uzembe na kutibu MAGONJWA Mbalimbali kwa msaada wako mfuate instagram: @my_health_my_wealth @my_health_my_wealth


Au Mtafute WhatsApp Huyu Dada kwa kutumia Namba +255783 566844

Pia Dawa za Edmark Zinaweza kupa Fursa ya Biashara Uweze pata Kipato Kirahisi kwa Kuwasaidia watu Kuimarisha Afya zao

Wolper: Hakuna Mwanaume Anayehonga

$
0
0
Wolper: Hakuna Mwanaume Anayehonga
MKALI wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe amesarenda na kufunguka kuwa, mwanamke yeyote ni vyema akajituma kwa sababu hakuna mwanaume anayehonga kwa sasa.

Akipiga stori na Ijumaa Wikienda, Wolper alisema kuwa, zamani mwanamke alikuwa anashindwa kujitegemea kwa sababu alijua kuna hela atapewa na mwanaume fulani, lakini kwa sasa hiyo haipo kwani wanaume nao wamebana hivyo ni bora wakajituma na kujisimamia mwenyewe kwenye kazi wanazozifanya.



“Mambo ya kusubiria hela ya kuhongwa nilishafuta kwenye kichwa changu ndipo nikapata nguvu ya kufanya kazi zangu maana hela za kuhongwa sizitaki kabisa,” alisema Wolper.

Staa huyo aliongeza kuwa, kwa sasa kazi yake ya ushonaji imemfanya kuanza kujulikana hadi nje ya nchi huku akiwandaa wasichana wadogo ili waweze kujitegemea.

Singida United Yawaonyesha Ubabe Yanga

$
0
0
Singida Unitedi Yawaonyesha Ubabe Yanga
Timu ya Yanga SC imeshindwa kusonga mbele katika michuano ya kombe la Shirikisho baada ya kuchapwa na wapinzani wao Siginda United kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kutoka sare ya mabao 1-1 kwenye dakika 90 za mchezo mzima.


Katika dakika 45 za kipindi cha kwanza katika mchezo huo timu ya Yanga ilifanikiwa kupata bao lake la kwanza kupitia mchezaji wake Yusuf Mhilu kwa kutumia mpira wa kichwa akiunganisha kona ya Ibrahim Ajib Kayika kwenye dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza cha mchezo na kupelekea timu yake kuongoza kipindi chote cha kwanza mpaka kuisha licha Singida United kuonesha jitihada za kutaka kusawazisha bao hilo lakini kwa bahati mbaya juhudi zao hazikuweza kuzaaa matunda.

Dakika 45 za pili za mchezo huo, Singida United walifanikiwa kusawazilisha bao la wapinzani wao kupitia mchezaji wao Kenny Ally na mpaka kipinga cha mwisho kinapulizwa timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 1-1 na kusababisha kupigwa mikwaju ya matuta na kuifanya Singida United kutoka kifua mbele baada ya kupata mikwaju 4-2 dhidi ya wapinzani wao Yanga SC.

Kutokana na ushindi huo, timu ya Singida United imejikatia tiketi ya moja kwa moja ya kuchuana na JKT Tanzania katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho.

Timu ya Yanga kwa sasa itakuwa imebakia na taji moja mkononi inalowania katika msimu huu wa mwaka 2018/2019 baada ya kutolewa leo katika michuano ya kombe la Shirikisho na Singida United kwenye dimba la Namfua mkoani Singida.

Esma Atoa ya Moyoni ''Nitafurahi Sana Daimond Akimuoa Wema Sepetu''

$
0
0
Esma Atoa ya Moyoni ''Nitafurai Sana  Daimond Akimuoa Wema Sepetu''
MWANADA-SHOSTI ambaye ni dada wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Esma Khan ‘Esma Platnumz’ amefunguka kuwa, kama kaka yake ataamua kurusha karata yake kwa mkali wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na kufunga naye ndoa itakuwa poa tu.

Akipiga stori na Over Ze Weekend, Esma alitoa la moyoni kuwa kwa upande wake, hawezi kumchagulia kaka yake mke, lakini kama ataamua kurudisha majeshi kwa mpenzi wake wa zamani, Wema atafurahi zaidi.



“Unajua Nasibu (Diamond) ndiye anajua zaidi mke anayemfaa, lakini kama pia ataamua kurudi kwa Wema, mimi nitafurahi tu kwa sababu ni mtu ambaye tunapatana sana na ninampenda pia,” alisema Esma.



Kumekuwa na sintofahamu ya nani atakayeolewa na Diamond baada ya kutengana na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na kutangaza kuwa atafunga ndoa mwezi Juni, mwaka huu.

Tuzo za Sinema Zetu: Gabo Anyakua Tano, Wema Sepetu Mbili Waacha Historia

$
0
0
Tuzo za Sinema Zetu: Gabo Anyakua Tuzo Tano, Wema Sepetu Mbili  Waacha uacha historia
Usiku wa leo katika ukumbi wa Mlimani City macho ya Watanzania yamepata kushuhudia zoezi la ugawaji wa tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF) zenye jumla ya vipengele 18 huku kimoja kikiwa cha People Choice na kukamilisha vipengele 19 ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Mstaafu wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni mualikwa akiwa muigizaji kutoka India aitwaye Pritika Rao maarufu kama Aliyah ambaye amejizolea umaarufu kupitia tamthilia ya ‘Beitehaa’.

Katika usiki huu uliopambwa na muziki tofauti kutoka ndani ya Tanzania, mastaa mbalimbali katika sekta ya burudani wamepata kushuduhia tuzo hizo zilizoweka na kuandika historia kwa wasanii kama vile Gabo Zigamba aliyenyakuwa jumla ya tuzo tano huku malkia wa filamu nchini Wema Sepetu aliondoka na tuzo mbili na filamu ya ‘Binti Zanibar’ ikiondoka na tuzo.

Waziri Mkuu Israel Alipongeza Jeshi kwa Kuwaua Wapalestina

$
0
0
Waziri Mkuu Israel Alipongeza Jeshi kwa Kuwaua Wapalestina
Serikali ya Marekani imeweka kipingamizi juu ya muswada ulioletwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) Jumamosi ukitaka uchunguzi ufanyike juu ya Israeli kutumia risasi za moto dhidi ya Wapalestina walioshiriki katika maandamano katika Ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa maelezo ya mwanadiplomasia wa Baraza hilo ambaye alilifahamisha shirika la habari la Ufaransa.

Vyombo vya usalama vya Palestina vimesema kwamba sio chini ya watu 15 waliuwawa Ijumaa na majeshi ya Israeli na zaidi ya watu 750 walitupiwa risasi za moto.

Wapalestina walizika maiti za watu wao Jumamosi, huku waombolezaji wakitangaza kulipiza kisasi.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamini Netanyahu aliyapongeza majeshi ya Israeli ambayo yalitupa risasi dhidi ya Wapalestina.

“Hongereni askari wetu,” waziri mkuu alisema katika tamko la serikali. “Israel inachukua hatua thabiti na kwa azma ya kulinda uhuru wake na usalama wa wananchi wake.”

Wapalestina walikuwa katika siku ya maombolezo ya kitaifa Jumamosi.

Shirika la habari la Associated Press (AP) limeripoti Jumamosi kuwa mmoja wa waandishi wake walishuhudia Wapalestina wawili, katika matukio mawili tofauti, ambao walikuwa wakitembea karibu na mpaka wa eneo lenye uzio la Ukanda wa Gaza linalotenganisha Israeli kutoka kwa Wapalestina. Wanajeshi wa Israeli waliwatupia risasi na kuwapata Wapalestina hao miguuni.

Katika tukio jingine, kijana wa miaka 16 ameiambia AP yeye alitupa mawe kuelekea katika mpaka huo siku ya Ijumaa na kutupiwa risasi zilizolenga miguu yote miwili. Kijana huyo alikuwa hospitali akitibiwa wakati mguu mmoja umefungwa bendeji na mwengine umetiwa vyuma, wakala wa habari wameripoti.

Waziri Majaliwa Kuwasha Mwenge wa Uhuru Leo

$
0
0
Wazili Majaliwa Kuwasha Mwenge wa Uhuru Leo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Aprili 2,2018 atawasha Mwenge wa Uhuru mkoani Geita.

Sherehe za kuwashwa Mwenge zinatarajiwa kuanza saa moja asubuhi hadi saa tano asubuhi katika kiwanja cha Magogo mjini Geita.

Mwenge wa Uhuru ambao utakimbizwa mkoani Geita kwa siku sita  utakabidhiwa mkoani Kagera Aprili 7,2018.

Mbio za Mwenge ambazo kauli mbiu kwa mwaka huu ni ‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa zitahitimishwa Oktoba 14,2018 mkoani Tanga.

Muziki wa Bongo Wamnyima Raha Ray C '' Kuna Muda Natamani Nibebe Mimba Nizae''

$
0
0
Muimbaji Ray C amefunguka mazito kwa kile anachoona kinaenda ndivyo sivyo katika muziki wa Bongo Flava kwa sasa.

Muziki wa Bongo Wamnyima Raha Ray C '' Kuna Muda Natamani Nibebe Mimba Nizae''
Ray C amefikia hata hatua ya kutumia maneno makali kueleza hisia zake kwa yale ambavyo hakubaliani nayo kwenye tasnia hiyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

Kuna muda huwa nafikiria mambo mengi sana! kuna muda najiskia kuamua kutiwa mimba, nizae niwe tu mama wa nyumbani! maana kuna muda nikiangalia wasanii wenye maendeleo kwenye Bongo Flava ni wachache saaaaana! na sijiongelei mimi maana mimi mwenyewe kuna wakati nilivurunda mwenyewe!

Nakubali nilibugi na nikagundua nimebugi haswa na ndio maana nimepambana mpaka hapa niliko baada ya kugundua baraka tele nilizozawadiwa na Mungu ni kubwa mno kuliko starehe za muda za ndogo na za kibwege!!! Ila huwa nakaa najiuliza miaka kama sita ambayo nilipotea kwenye industry! kuna wasanii nilianza nao na wana vipaji vya ajabu maskini lakini wengi wao wamezimwa kama taa!!!

Namkumbuka Nature, Joseline, Bushoke, Z Anto, Matonya, Makamua, Marlow, Domokaya n.k😢 majina ni mengi siwezi maliza!!!!!Wengi sana ni wasanii wakubwa sana na wana uwezo mkubwa mno. Najiuliza kitu gani kinachowakatisha tamaa hadi leo wamekuwa hadimu!!!???Mi nilikuwa kimya kutokana na sehemu.niliyokuwepo!!NAMAANISHA!? Jehanam!! na hawa niliowaacha je??? Kuna nini kwenye bongo flava???

Wasanii wapya ni wengi yes nalijua hilo lakini ukweli ni kuwa nchi yoyote hapa Afrika Mashariki nikienda naskia tu nyimbo za zamani nyingi na mpya pia!! mimi mwenyewe pamoja na mahanjumat ya pepo ya ahera yote lakini bado sauti ipo na nyie je???Nahisi kuna jini mmoja kwenye hii industry anaesababisha wasanii wengi wajione kama ndo basi tena! point yake ni moja! Na uwezo wa kukujenga na kukumaliza mara moja!!!maana yake nini sasa???.

Mungu anisamehe nianze kwenda kabla ya huyu jini!Pesa!! pesa!Pesa!Pesa!Ingekuwa pesa ndo uhai wallah hata Michael Jaclson asingekufa!!!!.

Nimeitumia hiyo picha sababu roho imeniuma siku ya mwisho kabisa ndo venue inabadilishwa!!!!Kuna karoho tu kamenikasirisha nimehisi kama kuna upuuzi wa kisengwile umefanywa ili mradi tu waharibu shughuli ya dada wa watu! Roho ya ndani huongea ukweli na ndo ninachohisi siku ya leo.

Wasanii mna kazi kubwa ya kuanza kujiamini kwanza kabla ya kuamini mtu mwingine! Mkishajua aliewapa vipaji naamini Mtasimama tena, Mtaingia studio tena! Maana mashabiki wenu bado wapo!!! Kinachohitajika ni kipaji sio promota anaefikiria tumbo lake na mpaka leo anazidi kukondeana!! ziba lakini tutakutana kaburini!.

Napenda Kulala Bila Nguo Hata Kama Cjaolewa- Kajala

$
0
0
Napenda Kulala Bila Nguo Hata Kama Cjaolewa- Kajala
STAA mwenye mvuto wa kipekee kwenye kiwanda cha filamu Bongo, Kajala Masanja ametoa kali baada ya kusema kuwa katika vitu ambavyo havipendi ni kulala na nguo usiku japokuwa bado hajaolewa.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Kajala alisema kuwa, jambo la kwanza ambalo mtu akimwingilia usiku wa manane, atakiona ni mwili wake maana kuvaa nguo yeye usiku ni mwiko hata kuwe na baridi kiasi gani analala hivyohivyo.

“Jamani ukiniambia nivae nguo usiku, unaweza kunichapa fimbo maana siwezi hata kidogo yaani siku mtu akiniingilia usiku kuniibia, anaweza kuachana na zoezi hilo akaanza kunikodolea macho,” alisema Kajala huku akicheka.

Mpenzi Wangu Anakosa Ute Wakati wa Tendo Ushauri Wako Tafadhali

$
0
0
Mpenzi Wangu Anakosa Ute Wakati wa Tendo Ushauri Wako Tafadhali
Tuna mwaka na miezi 3 toka tuanze uhusiano. Mwanzo nilikua namuandaa anatoa ute wakutosha kabisa ,ila kadri siku zinapozidi kusonga hata nimuandae vipi ute unatoka lakini wakulazimisha mno!!

Hali hiyo ilivyoanza tulijua labda ni hali ya mpito lakini hakuna mabadiliko yoyote... nikimuuliza anadai yeye mwenyewe haelewi na inamuumiza kuwa hivyo na hajui tatizo nini..

Soma Nafasi za Ajira zilizotangazwa Leo Jumatatu

$
0
0

Download Upya Application Yetu Ya Udaku Special .....Ile Ya Zamani Tutaifuta

Kinachowaponza Wanawake Wengi ni Maamuzi Duni Kwenye Mambo ya Msingi..Soma Hii

$
0
0

LABDA HII ITAWASAIDIA:
Kinachowaponza Wanawake ni POOR DECISION MAKING IN CRITICAL ISSUES.
Unakuta mtu anajua kabisa ana Boyfriend Levi la Kutupwa,analala mtaroni kila siku,anafikishwa nyumbani hajitambui kafikaje,yeye yupo tu amekazana na Fanta yake..Unachumbiwa na kuolewa na hilihili levi,unasota nalo miaka 2 ya ndoa inakuwa kero...Ulimvumilia kwenye Uchumba coz hamkuwa mnalala pamoja,analewa na kutapika akiwa kwake na wewe uko kwenu..Sasa Mzigo ni wako,mko SAME BED..Anatapika hapo..Harudi home siku 4..Na hata akirudi yuko Njwii,hata 'kazi hawezi kupiga'

Unaenda kulalamika kwa Mchungaji kuhusu Tabia mbaya ya mmeo...YOU KNEW IT..Ukapuuzia na ukakubali kuolewa na JANGA...Mtabaki kusumbua Wachungaji na Wakwe kuwapatanisha wakati mlikuwa na Muda wa kujuana kabla hamjaamua kuishi pamoja

Kipindi cha Uchumba kitumie KUMFAHAMU VIZURI..Sio ukitumie KUMCHUNA,KULA BATA,OFA ZA KITIMOTO,TRIP ZA BAGAMOYO,KUMPIGA MIZINGA YA PERUVIAN HAIR..Ukasahau KEY ISSUES...Mmekaa miaka 6 ana watoto 2 na Wanawake wengine..Analewa na kulala mtaroni..Halafu analeta Posa unasema kuolewa ni Bahati.

Yakikushinda Usitusumbue...Sio kila POSA ni bahati,Posa nyingine ni kichaka tu cha kutua majanga yao...Your Decision TODAY will affect your TOMORROW...Think twice before you say YES to a Problem.

By Seth De Jesus

Maneno ya Zitto Kabwe Baada ya Yanga Kuondolewa Katika Michuano Kombe la Shirikisho

$
0
0
Maneno ya Zitto Kabwe Baada ya Yanga Kuondolewa Katika Michuano Kombe la Shirikisho
Masaa kadhaa baada ya klabu ya soka ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la shirikisho nchini ASFC, Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye ni shabiki mkubwa wa Simba ametupa kijembe kwa watani wao Yanga.


Yanga jana jioni iliondolewa katika michuano hiyo na Singida United kwa jumla ya penalti 4-2 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Katika mikwaju ya Penalti kiungo wa Yanga Papy Tshishimbi alipaisha juu kitendo ambacho kimemfanya Mh. Zitto kutoa tahadhari hiyo.


''Tahadhari kwenu wananchi wa kondoa na vijiji vyake.. lile shuti la penalti ya shishimbi bado lipo hewani hivyo muwe makini na utuaji wake usijeleta madhara makubwa'', umesomeka ujumbe wa Zitto kupitia mtandao wa Twitter.
Mbali na Tshishimbi mchezaji mwingine ambaye alikosa penalti ni Emmanuel Martin huku Singida United wakipata Penalti zao 4 kati ya 5 na kuwafanya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo hutoa mwakilishi wa Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Timu 4 ambazo zimefuzu hatua ya nusu fainali ni Stand United iliyoitoa Njombe Mji, JKT Tanzania iliyoitoa Tanzania Prison, Mtibwa Sugar iliyoitoa Azam FC na Singida United iliyoitoa Yanga SC.

Maaskofu wa KKKT Wasikitishwa na Wanaopinga Waraka Wao

$
0
0
Maaskofu wa KKKT Wasikitishwa na Wanaopinga Waraka Wao
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa wao kama Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamesikitishwa na watu ambao wanapinga waraka wao na kusema ni wajinga


Askofu Shoo ametoa kauli hiyo April 1,2018  katika Usharika wa Moshi Mjini Dayosisi ya kaskazini, mkoani Kilimanjaro na kusema kuwa wao wataendelea kusema ukweli siku zote

"Sisi tunasikitika sana tunaposema jambo la kweli, jambo linalohusu maisha ya watanzania wote katika waraka ule tuliotoa kama waraka wa maaskofu halafu kuna watu wachache wajinga mimi nimesema wamesema maaskofu wamesema sababu sadaka zimepungua kanisani, sisi sadaka haijapungua kwani wakristo wameendelea kujitoa sana na hatujapungukiwa na kitu napenda kuwashukuru na Mungu awabariki sana, na sisi tutaendelea kusema ukweli na wanaotaka kuharibu ukweli huo waendelee kuharibu lakini watanzania walio wengi, watanzania wenye hekima wanaelewa maneno tuliyozungumza siyo maneno ya kujibu tu haraka haraka bali maneno ya kututafakarisha"

Askofu Shoo aliendelea kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hilo na kusema kuwa

"Tutaitwa majina mengi lakini tunajua ni jitihada za ule upotoshaji wa ule ukweli uliopo katika ule waraka, siyo jambo la hivi hivi tu kwa wakati mmoja maaskofu wa makanisa mawili makubwa hapa nchini kukaa na kutoa waraka, hatukukaa na kusema tutatoa waraka lakini Baraza la Maaskofu wa Katoliki wakakaa na kuja na ule waraka sisi wa KKKT tutakaa tukaja na waraka ukilinganisha ujumbe ni ule ule mimi nasema tena kuna kitu Mungu anataka kutuambia kama Watanzania kupitia ujumbe ule. Mungu awaguse hao wanaotumia nguvu nyingi kutaka kupotosha waraka ule, wanatumia nguvu nyingi kupaka matope"

Chombo cha Anga za Juu cha China Chaanguka Pacific

$
0
0
Chombo cha anga za juu cha China chaanguka Pacific
Chombo cha anga za juu cha China kilichoacha kutumika Tiangong-1 kimemeguka vipande vingi kikiingia anga ya dunia na kuanguka maeneo ya bahari kusini mwa Pacific.

Chombo hicho kiliingia anga ya dunia saa 00:15 GMT Jumatatu, idara ya anga za juu ya China imetangaza.

Tiangong-1 ilirushwa angani mwaka 2011 kufanyia majaribio teknolojia ya kuunganisha vyombo mbalimbali anga za juu na pia vyombo vya kuzunguka kwenye mzingo wa dunia.

Chombo hicho ni sehemu ya juhudi za China za kuunda kituo cha anga za juu kitakachokuwa kinadhibitiwa na binadamu katika anga za juu kufikia mwaka 2022.

Kiliacha kufanya kazi Machi 2016.

Tunayoyafahamu kuhusu eneo ambalo kilianguka?

Maafisa wanasema tu kwamba kilianguka "juu ya Pacific Kusini".

Wataalamu wa anga za juu wa Marekani wamesema wametumia teknolojia ya kufuatilia mzingo wa dunia kuthibitisha kuingia ardhini kwa Tiangong-1.

Mtaalamu wa anga za juu Jonathan McDowell kutoka Harvard ameandika kwenye Twitter kwamba huenda chombo hicho kimeanguka kaskazini magharibi mwa Tahiti.

Wataalamu walitatizika kubaini hasa ni wapi chombo hicho kingeanguka.

Idara ya anga za juu ya China ilikuwa awali imekadiria kimakosa kwamba chombo hicho kingeanguka karibu na Sao Paulo, Brazil muda mfupi kabla ya chombo hicho kuingia anga ya dunia.

Shirika la Anga za Juu la Ulaya lilisema mapema kwamba uwezekano mkubwa ni kwamba chombo hicho cha Tiangong-1 kingeanguka baharini.


ESA walisisitiza kwamba uwezekano wa mtu kugongwa na vifusi vhya vyombo hicho ulikuwa "chini ya mara milioni kumi ya uwezekano wa mtu kupigwa na radi."

Haijabainika ni kiasi gani cha vifusi hivyo kimeanguka ardhini.

Mbona chombo hiki kikaanguka hivi?
Tiangong kilifaa kusitisha shughuli yake ya kuizunguka dunia kwa utaratibu na mpangilio fulani.

Ni chombo kilichokuwa na urefu wa mita 10 (futi 32) na uzani wa zaidi ya tani 8 na ni kikubwa zaidi ya vyombo vyote vilivyoundwa na binadamu ambavyo vimewahi kuanguka kutoka anga za juu.

Lengo lilikuwa kutumia vifaa vinavyokipa chombo hicho msukumo kukielekeza hadi maeneo ya mbali yasiyo na watu maeneo ya Bahari ya Kusini.

Lakini kabla ya hilo kufanyika, ghafla mfumo wa kukidhibiti ulikumbwa na hitilafu na wataalamu wa China wakapoteza udhibiti.

Mashirika 13 ya anga za juu ya mataifa mbalimbali, yakiongozwa na Shirika la Anga za Juu la Ulaya (ESA), yalifuatilia njia ya Tiangong na kujaribu kuiga tabia yake kadiri kilivyokaribia kuingia ndani ya anga ya dunia huku kikiendelea kuizunguka.

Mwanananga Wang Yaping alitoa mhadhara unaokumbukwa sana kwa watoto akiwa moja kwa moja kutoka chombo cha Tiangong-1 kikiwa anga za juu
Chombo hiki kirirushwa mwaka 2011 kufanyia majaribio utaratibu wa kutuma vyombo vingine na kuviunganisha vikiwa anga za juu
Makundi mawili ya wanaanga yalizuru chombo hicho wakitumia vyombo vidogo kwa jina Shenzhou - mwaka 2012 na 2013
Walijumuisha wanaanga wa kwanza wa kike kutoka China Liu Yang na Wang Yaping
China inapanga kutuma chombo cha anga za juu cha kudumu katika mwongo mmoja ujao
Imeunga roketi inayobeba kuinua vitu vya uzani wa juu sana kwa jina Long March 5 kwa ajili ya kazi hiyo
Ndicho chombo kikubwa zaidi kuwahi kuanguka kutoka angani?

Tiangong ni miongoni mwa vyombo vingine vikubwa vilivyowahi kuanguka bila kudhibitiwa, lakini bado kineachwa nyuma na vyombo vingine.

Chombo cha Skylab cha Marekani kilikuwa na uzani wa tani 80 kilipoanguka, ingawa kiliweza kudhibitiwa kwa kiasi fulani, mwaka 1979.

Kilianguka Australia Magharibi ardhini lakini hakuna aliyejeruhiwa.

Chimbuko la Illuminati na dhana kuhusu nguvu zao
Chombo cha Nasa cha Columbia nacho kilikuwa na uzani wa tani 100 kilipoanguka mwaka 2003.

Tena, ardhini hakuna aliyegongwa na vifusi vyake ambavyo vilitapakaa majimbo ya Texas na Louisiana.

Mtaalamu Jonathan McDowell kutoka Kituo cha Fizikia ya Anga za Juu cha Harvard-Smithsonian anasema kwa kukadiria, 50 ni chombo cha 50 kwa ukubwa.

Mnamo 2001, Uchina ilizindua vyombo vyake vya anga kwa kujaribu kuwatuma wanyama mwaka 2003 kwenye chombo cha anga za mbali kwenye mzingo wa dunia, na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa ni ya tatu kufanya hivyobaada ya Muungano wa Usovieti na Marekani.

Mpango wa vituo vya safari za anga za mbali ulianza kwa kukituma chombo cha Tiangong-1 ama "Kasri la Mbinguni", mwaka 2011.

Kituo hicho kidogo kiliweza kuwahifadhi wataalam wa masuala ya anga za mbali lakini kwa muda mfupi wa siku kadhaa. Mchina wa kwanza mwanamke mtaalamu wa anga za juu Liu Yang alitembelea kituo hicho mwaka 2012.

Kilikamilisha huduma zake mwezi Machi 2016, miaka miwili zaidi ya muda kiliopangiwa.

Mamba Apatikana Katika Bwawa la Kuogelea Florida, Marekani

$
0
0
Mamba apatikana katika bwawa la kuogelea Florida, Marekani
Polisi katika jimbo la Florida, Marekani wamesema mamba wa urefu wa futi 11 alipatikana kwenye bwawa la kuogelea la familia moja katika jumba hilo.

Polisi wamepakia picha za mamba huyo mtandaoni.

Wakazi wa Nokomis waliwapigia simu polisi na kuomba usaidizi baada ya kumgundua mnyama huyo.

Afisa wa polisi wa eneo la Sarasota alipakia mtandaoni picha ya afisa wa wanyama aliyeitwa kumnasa akiwa anamburuta mnyama huyo kutoka kwenye maji Jumamosi.


Mamba nchini Marekani kwa kawaida hukua hadi kuwa na futi kati ya 11 na 15 na wanaweza kuwa na uzani wa kilo 454.

Mamba wa Marekani hupatikana mashariki mwa Marekani katika majimbo ya Florida na Louisiana, kila jimbo likiwa na zaidi ya mamba milioni moja.

Eneo la kusini mwa Florida ndilo pekee ambalo mamba wa Marekani na mamba wa kawaida huishi kwa pamoja.

Ingawa awali walikuwa wameorodheshwa kama wanyama walio hatarini chini ya sheria za mwaka 1973, idadi yao iliongezeka sana kwa haraka na kufikia mwaka 1987 wakaondolewa kutoka kwenye orodha hiyo.

Inakadiriwa kwamba kuna mamba milioni moja hivi Florida, na wengine milioni moja Louisiana.

Masiki Mama Kanumba Maisha Yazidi Kumchachia Aomba Msaada kwa Mzungu

$
0
0
Masiki Mama Kanumba Maisha Yazidi Kumchachia  Aomba Msaada kwa Mzungu
KUTOKANA na hali ngumu ya maisha hivi sasa, mama mzazi wa aliyekuwa mwigizaji mahiri wa Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amemwangukia mwanadada mwenye asili ya kizungu aitwaye Mouna ili amsaidia kwenye shughuli ya kumbukumbu ya mwanaye inayofanyika kila Aprili 7.

Akizungumza na Over Ze Weekend, mama Kanumba aliweka wazi kuwa, amezunguka huku na kule, lakini hajapata msaada wowote hivyo anamuomba Mouna asimtupe kwenye hilo.

“Nimeona nimuombe tena Mouna kwa sababu alikuja Tanzania kuniona na kufika kaburini kwa Kanumba hivyo anaonekana wazi ana mapenzi kiasi gani na mimi na sasa ninamuona kama mwanangu,” alisema mama Kanumba.

Hivi karibuni, Mouna alitinga Bongo akitokea nchini Ujerumani na kufika kaburini kwa Kanumba kisha kwenda nyumbani kwa mama wa jamaa huyo, Kimara- Temboni jijini Dar na kuahidi kumchukua akapumzike kidogo kwenye nchi hiyo iliyo barani Ulaya.

Simba Yamalizana na Wanairinga

$
0
0
Simba yamalizana na Wanairinga
Kikosi cha vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba, kimeanza safari asubuhi ya leo kutoka mkoani Iringa kuelekea mkoani Njombe, kwaajili ya mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Njombe Mji.


Kikosi cha Simba kiliondoka jijini Dar es salaam Ijumaa iliyopita na kutua Mkoani Iringa ambako kiliweka kambi ya muda ambapo jana kilifanya mazoezi katika uwanja wa Samora mkoani humo.

Mchezo huo wa raundi ya 21 kwa Simba na 22 kwa Njombe Mji utapigwa kesho April 3 kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Njombe kuanzia saa 10:00 jioni.

Simba kwasasa ipo kileleni ikiwa na alama 46 sawa na Yanga yenye alama 46 zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa. Njombe Mji ipo nafasi ya 15 ikiwa na alama 21 katika michezo 18.
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images