Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Winnie Mandela Kuzikwa April 14 kwa Heshima Zote za Serikali

$
0
0
Winnie Mandela Kuzikwa April 14 kwa Heshima Zote za Serikali
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametoa taarifa rasmi juu ya mazishi ya Winnie Mandela ambaye Taifa hilo linamtambua kama mama wa Taifa, aliyefariki April 1, mwaka huu.


Akizungumza mara baada ya kuwasili nyumbani kwa familia ya marehemu, Rais Ramaphosa amesema Winnie Mandela atazikwa kwa heshima zote za serikali na utamaduni wa Afrika Kusini hapo April 14, huku zikitanguliwa na shughuli zingine za mazishi kuanzia April 11.

Rais Ramaphosa ameendelea kwa kusema kwamba kama Taifa linatambua mchango wa Winnie Mandela, hivyo watampa heshima zote pamoja na watu wote wanaowatakia mema taifa la Afrika Kusini.

“Kwa ngazi ya serikali ya kitaifa, tumetangaza kuwa Winnie Mandela atakuwa na mazishi ya kitaifa rasmi. Tungependa kutoa shukrani zetu na shukrani zetu kwa wengi nchini kote na ulimwengu ambao wanatutaka sisi vizuri, "amesema Rais Ramaphosa.

Winnie Mandela alikuwa mke wa pili wa aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, na alikuwa ni mmoja wa wapigania uhuru wa watu weusi na kuendeleza harakati hata wakati viongozi wa ANC akiwemo Nelson Mandela wakiwa wamefungwa jela, kwa muda wa miaka 27.




Wema Sepetu: Kuna Kundi la Watu Linamfanyia Fitna

$
0
0
Wema Sepetu: Kuna Kundi la Watu Linamfanyia Fitna
Baada ya malkia wa filamu Wema Sepetu kuchukua tuzo mbili za SZIFF 2018, amefunguka kwa kudai kuwa kuna kundi la watu linamfanyia fitna aonekane hakuna anachokifanya katika tasnia ya filamu.

Baada ya malkia wa filamu Wema Sepetu kuchukua tuzo mbili za SZIFF 2018, amefunguka kwa kudai kuwa kuna kundi la watu linamfanyia fitna aonekane hakuna anachokifanya katika tasnia ya filamu.

Muigizaji huyo ameyasema hayo leo hii wakati akiwashukuru wadau mbalimbali waliofanyika kuchukua tuzo hizo mbili. Kupitia Instagma Wema ameandika.

Napenda kuchukua nafasi hii Kumshukuru kwanza Allah Sub’hannah wata’Allah kwa kunifkisha hapa nilipo sasa… Najua ni mambo mengi sana yanafanyika kwa ubaya juu yangu ila yeye ndo amekuwa Tumaini langu kubwa… Nimshukuru Mama angu mzazi pamoja na familia yangu yote kwa ujumla kwa kusimama na mimi bega kwa bega katika kila kitu.

Nitoe n shukran zangu za dhati kabisa kwa Azam Tv kwa kutupa wasanii wote wa Tasnia ya Filamu fursa hii kubwa ya kuweza kujua nani zaidi… Hakika ni Changamoto nzuri sana na naiona inakuja kuleta mabadiliko makubwa kwenye Tasnia yetu.

Napenda kutoa Special thanks to my Love, The Woman behind The Best Actress 2018, My Tyler Perry, wanamuita Neema Ndepanya kwa kuniamini na kuniongoza vyema katika kazi… Najua upo very proud na nakuahidi kuendelea kuku make proud… We have so much to do mamy… @neema_ndepanya
Wema Sepetu Empire, Nawapenda sana watoto wangu… Nyinyi ni zaidi ya Ndugu sasa… Na tunaenda kufanya mapinduzi makubwa sana .. Maana sio kwa hasira nilizonazo sasahivi… .

Last But Not Least…. Wema Lovers… Hizi tuzo ni zenu… Nawashukuru kwa kunipa endless support kila ninapohitaji… Bila nyinyi siwezi… Ntaendelea kuwapenda na kuwathamini mpaka siku nakata kauli… .

Pia nichukue nafasi hii kuwashkuru wasanii wenzangu wote tulioshiriki kwenye tuzo hizi na kuwapa hongera maana hata kuwa nominated tu ni hatua kubwa sana… .

Mwisho kabisa nawashkuru wasanii WOTE wa Tasnia ya Filamu kwa ujumla… Tutakutana mwakani tena kwenye TUZO… Inshallah…

The Weeknd Awaonya Wasanii wa Muziki dunia

$
0
0
The Weeknd Awaonya Wasanii wa Muziki dunia
Msanii wa muziki kutoka Canada, The Weeknd amewaonya wasanii wa muziki dunia akiwemo Wizkid kuacha mara moja kutumia neno ‘StarBoy’ kwa madai kuwa neno hilo ameshalilipia (TradeMark) kwa matumizi yake ya kibiashara.

The Weekend amesema kuwa yeye ndiye muanzilishi wa neno hilo ‘StarBoy’ na yeyote atakayetumia atachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Tayari wanasheria wa The Weeknd wameshaandaa nyaraka za kumburuza Eymun Talasazan mahakamani kwa kutumia neno ‘StarBoy’ kwenye vipindi vyake vya TV baada ya The Weeknd kuachia album yake ya ‘StarBoy’ mwaka 2016.

Wimbo wa ‘StarBoy’ ni moja ya nyimbo zilizopo kwenye album hiyo na ulifanikiwa kushika namba moja kwenye chati za Billboard top 100.

Kwa The Weeknd wimbo wa StarBoy ni wimbo wa tatu kushika namba moja kwenye chati hizo maarufu zaidi duniani.

Nukuu Sita Maarufu za Winnie Mandela

$
0
0
Nukuu sita maarufu za Winnie Mandela
Mwanasiasa na mwanaharakati aliyepigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini Winnie Madikizela-Mandela alifariki dunia Jumatatu akiwa na miaka 81.

Alikuwa mke wa zamani wa rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini Nelson Mandela lakini alikuwa na msimamo mkali zaidi kumshinda hata Bw Mandela mwenyewe.

Winnie alifahamika sana na wengi kama Mama wa Taifa.

Alikuwa nembo kuu ya vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, na ingawa sifa zake ziliingia doa miaka ya baadaye, lakini bado alitambuliwa kama mtetezi wa wanyonge.

Alisalia kuwa mwanachama wa chama tawala cha African National Congress (ANC) ingawa nyakati za karibuni alikuwa akikosoa uongozi wa chama hicho.

Hapa, tunaangazia nukuu sita maarufu ambazo alwiahi kuzitoa.

"Miaka niliyofungwa gerezani ilinifanya kuwa mkakamavu... Huwa sina tena hisia za woga ... Hakuna chochote ambacho naweza kukiogopa. Hakuna kitu ambacho sijatendewa na serikali. Hakuna uchungu ambao zijakumbana nao."

Nukuu hii katika kitabu chake cha Lives of Courage: Women for a New South Africa(Maisha ya Ujasiri: Wanawake wa Afrika Kusini Mpya), inaashiria jinsi Bi Madikizela-Mandela alivyofanyiwa ukatili na serikali ya utawala wa ubaguzi wa rangi.

Alifungwa jela mara nyingi kuanzia 1969 na muda mwingi alikuwa amefungwa bila kuwa na ruhusa ya kukutana na wafungwa wengine.

Mwaka 1976, mwaka wa maandamano ya Soweto, alifukuzwa kutoka mji wake na kulazimishwa kuishi maeneo ya mashambani.

Bi Madikizela-Mandela alikuwa mwanasiasa kivyake, na alipinga hatua ya mumewe ya kushauriana na watawala wa ubaguzi wa rangi.

Alidai hilo lingesababisha "usaliti" wa watu weusi.

Licha ya tofauti zao, Bi Mandela alimteua kuwa waziri msaidizi serikali yake ya kwanza 1994.

Alimfuta kazi mwaka mmoja baadaye, lakini Bi Mandela alipinga hilo mahakamani na kufanikiwa. Lakini alifutwa kazi tena.

"Kwa viberiti vyetu na mikufu yetu tutaikomboa nchi hii."

Tamko hilo, katika mkutano wa siasa mjini Johannesburg, aliashiria kwamba Bi Mandikizela-Mandela alikuwa ameidhinisha na kuunga mkono njia katili ya "kuweka mikufu" - njia ya kuweka matairi shingoni washukiwa wa usaliti na kuwachoma moto wakiwa hai.

Hilo lilishangaza dunia na kutia doa sifa za ANC. Tamko hilo lilishutumiwa na wengi, akiwemo mshindi wa tuzo ya Nobel Askofu Mkuu Desmond Tutu (pichani juu).

"Nilikuwa na wakati mdogo sana kumpenda. Na upendo huo umedumu miaka hii yote ambayo tulitenganishwa... pengine kama ningepewa muda wa kutosha wa kumfahamu vyema zaidi pengine ningegundua kasoro nyingi, lakini nilikuwa tu na wakati wa kumpenda na kumkosa sana wakati wote."

Nelson na Winnie Mandela walikuwa wanandoa waliokuwa maarufu zaidi Afrika Kusini.

Alitambuliwa na wengi kama "mama wa taifa" na aliweka hai jina la mumewe miaka 27 aliyokuwa gerezani.

Alikuwa mfanyakazi wa kutoa huduma kwa jamii alipoolewa na Bw Mandela ambaye tayari alikuwa mmoja wa viongozi wa ANC mwaka 1958. Bw Mandela alihukumiwa jela maisha mwaka 1961 kwa mchango wake katika kupigana na utawala wa makaburu.
"Mimi ni mazao ya wananchi wa taifa hili. Mimi ni mazao ya adui wangu mkuu."

Wawili hao walitalikiana mwaka 1996, miaka miwili baada ya Bw Mandela kuwa rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini. Miaka ambayo walikaa bila kuonana yamkini iliathiri uhusiano wao. Bi Madikizela-Mandela alituhumiwa kuwa na uhusiano nje ya ndoa.

Alidumisha jina la mumewe wa kwanza jambo ambalo wakosoaji walilitazama kama mpango wake wa kuendelea kufaidi kutokana na nembo ya Mandela.
"Wengi wa wanawake huupokea mfumo dume bila kuuliza maswali na hata huutetea, kwa kuelekeza mahangaiko yao sio kwa wanaume bali dhidi yao wenyewe wakishindania wanaume walio wana wao wa kiume, wapenzi wao na waume zao. Kitamaduni, mke ambaye amedhalilishwa hujituliza na kuelekeza ghadhabu zake kwa wakwe. Kwa hivyo, wanaume huishia kuwatawala wanawake kupitia juhudi za wanawake wenyewe."

Bi Madikizela-Mandela alisifiwa na wafuasi wake kama mtetezi wa haki za wanawake.

Winnie Mandela afariki dunia Afrika Kusini
Alikuwa kiongozi wa vuguvugu la wanawake katika ANC baada ya chama hicho kuruhusiwa kuendelea na shughuli zake tena mwaka 1990.

Aliamini kwamba wanawake weusi walitatizwa na nira aina tatu za ukandamizaji - jinsia yao, rangi na tabaka.


Former wife of the late South African President Nelson Mandela, Winnie Mandela (C) holds the hands of South African President Jacob Zuma (L) and South African Deputy President Cyril Ramaphosa (R) during the opening session of the South African ruling party African National Congress policy conference on June 30, 2017 in Johannesburg.Haki miliki ya pichaAFP
"Ninaamini kuna kitu ambacho ni kibaya sana katika historia ya taifa letu, na jinsi ambavyo tumeiharibu African National Congress."

Katika miaka yake ya baadaye, Bi Madikizela-Mandela alivunjwa moyo na ANC - chama cha zamani cha ukombozi ambayo kiliingia madarakani mwaka 1994 - hii ni kwa sababu ya ufisadi na unga'ng'aniaji wa mamlaka miongoni mwa viongozi wake.

Aliendelea kukiunga mkono lakini alionekana kumuunga mkono Cyril Ramaphosa alipochukua uongozi kutoka kwa Jacob Zuma mapema mwezi huu.

Serikali Yaeleza Mkakati Mpya wa Kupambana na Dawa za Kulevya

$
0
0
Serikali Yaeleza Mkakati Mpya wa Kupambana na Dawa za Kulevya
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde ni miongoni mwa Mawaziri waliosimama Bungeni leo ambapo alielezea mikakati ya Serikali katika kupambana na madhara ya dawa za kulevya nchini.

Mavunde amesema.>>>“Katika mikakati ambayo tumejiwekea katika kudhibiti dawa za kulevya ni pamoja na kupunguza madhara kwa kuwa na madirisha maalum katika hospitali zetu za mikoa ambayo yatakuwa yakiwahudumia waathirika”

Cannavaro Aituliza Yanga

$
0
0
Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amewaambia wanachama na wapenzi wa Yanga wasife moyo baada ya timu yao kutolewa na Singida United kwenye mashindano ya Azam Sports Federation Cup.

“Tunamsukuru Mungu tumefika salama Morogoro, tunawaomba mashabiki wa Yanga wasife moyo kutokana na kupoteza mchezo wetu dhidi ya Singida United japo tulijitahidi lakini tukafungwa kwa penati.”

“Tuna mechi ya kimataifa siku ya Jumamosi, tunaomba mashabiki waje kwa wingi kutupa sapoti ili tuweze kufanya vizuri.”

“Nafasi ya ubingwa wa ligi bado ipo kwa sababu sisi na Simba tuna pointi sawa lakini tumewazidi kwa mchezo mmoja, kwa upande wetu bado tuna nafasi ya kuwa mabingwa na bado tuna nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika.

Kwa sasa Yanga imeweka kambi mjini Morogoro kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo wao wa kimataifa dhidi ya waethiopia, Yanga ilipoteza nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo hivyo nafasi iliyobaki kwao ni kutwaa ubingwa wa ligi ili kuwa wawakilishi katika mashindano ya vilabu bingwa Afrika.

Nafasi ya kuwakilisha Tanzania bara katika mashindano ya kombe la shirikisho Afrika ipo mikononi mwa timu nne zilizofuzu hatua ya nusu fainali ya ASFC ambazo ni stand united, JKT Tanzania, Mtibwa Sugar na Singida United.

Comments

Edo Kumwembe Auponda Uwanja wa Sabasaba

$
0
0
Mwandishi na Mchambuzi wa Soka, Edo Kumwembe, ametoa maoni yake kuhusiana na ubowa wa Uwanja wa Sabasaba ambao una kibarua hivi sasa kati ya Njombe Mji FC dhidi ya Simba SC.

Edo ameeleza kuwa Uwanja huo hauna ubora wa kuridhisha kwa kusema kuwa haustahili kupewa hadhi ya kuchezea mechi za ligi.

"Simuoni Okwi. Well Watanzania tusiwe wajinga...tuna ushabiki wa kijinga sana wa Mpira...tuwageukie wanaotuongoza... Huu uwanja hauwezi kuwa wa Ligi kuu... Pitch bovu na halitoi matokeo halali...mchezaji Kama Okwi hawezi kudrible hata hatua sita...Mechi inazungumzwa saaana katika media lakini ukienda uwanjani ni upuuzi tu... Nakerwa na pitch mbovu.. Hazitupi hadhi za mechi ya Ligi kuu" ameandika Edo kupitia Facebook.

John Bocco Aunguruma Njombe..Aitoa Simba Kimaso Maso

$
0
0
Magoli mawili ya mshambulia John Bocco wa Simba yameipa ushindi timu yake dhidi ya Njombe Mji kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara na kufikisha pointi 49 pointi tatu mbele ya Yanga ambayo ipo nafasi ya pili.

Bocco alifunga goli la kwanza dakika ya 17 na dakika ya 64 na kuizima kabisa Njombe Mji ambayo ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 18 kwenye msimamo wa ligi inapambana isishuke daraja.

Baada ya mchezo, Bocco amesema pamoja na wachezaji wengine watapambana kuhakikisha wanapata pointi tatu katika kila mchezo.

“Ushindani bado mkubwa, kuna timu zinapambana kwenda juu na nyingine zinapambana zisiende chini. Mimi na wenzangu tutapambana kwa kila hali na kila uwanja iwe nyumbani au ugenini kuhakikisha tunapata pointi tatu kwa kila mchezo”-John Raphael Bocco mwamuzi wa mchezo wa leo.

Spika Job Ndugai Arejea Nyumbani Toka Kwenye Matibabu India

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamburi ya Muungano wa Tanzania,Mh Job Ndugai akipokelewa na Mama Salma Kikwete (MB) na Wabunge wengine mara baada ya kuwasili leo akitokea nchini India kwa matibabu.

Hapa ni eneo la wageni maarufu (VIP) katika uwanja wa ndege Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).Mh.Spika amewasili alasiri ya leo,akitumia ndege ya Shirika la "Fly Emirates" # EK725.

Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai alisema Februari mwaka huu kuwa Spika Ndugai yupo India kwa ajili ya kuangalia afya yake (check-up).

Mbowe Atoka na Msimamo Mkali Segerea..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya April 4

$
0
0


Mbowe Atoka na Msimamo Mkali Segerea..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya April 4

Pata Habari Masaa 24......Pakua Upya Application Yetu Tukuhabarishe Usiku na Mchana

Madhara ya Kutofanya Tendo la Ndoa Muda Mrefu.

$
0
0
Habari zenu, nimeona niwaletee hili nina imani mtajifunza hasa kwa wale wasiofahamu,Ukikaa Muda Mrefu bila Kufanya tendo la Ndoa madhara yake ni kama haya:

• Hasira za mara kwa mara katika mambo madogo,
• kupendelea sana kuangalia picha za uchi,
• Kusahausahau,
• Kupendelea story za mapenzi,
• Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (Mke),
• Kupenda kurukiarukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo
yasiyokuhusu),
• Kuumwa na kichwa,
• Kukakamaa mgongo (wanaume),
• Kuingiliwa kirahisi na jini mahaba,
• Kupoteza umakini ktk kazi (efficiency),
• Siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno,
• Waweza ku-develop tabia mpya ambayo hukuwahi kuwa nayo ili iwe mbadala

kama ulevi n.k. Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

Mbunge Ashauri Wanaume Kuoa Wake Wengi

$
0
0
Mbunge mmoja nchini Kenya ameibua hoja kuwataka wanaume kuoa wanawake wengi, ili kuweza kusaidia malezi ya familia na kupunguza watoto wa mitaani.

Mbunge huyo anayejulikana kwa jina la Gathoni wa Muchomba kutoka kaunti ya Kiambu, amesema ameona ni vyema iwapo wanaume wataoa wanawake wengi kwani watoto wengi nchini humo wamekuwa wakilelewa na mzazi mmoja, jambo ambalo linasababisha malezi mabaya na watoto kuangukia kwenye matatizo.

“Nimetoa haya matamshi kama kiongozi wa Kiambu kwa sababu ya matatizo ambayo tunayo ya watoto kulelewa na 'single mother', nadhani hilo linaweza likawa suluhisho litasaidia kwenye malezi ya familia, kama uko na uwezo wa kutunza na kutumikia kwa mahitaji yake yote, naona tumekuwa tunaacha yale ambayo tulikuwa tunafuatilia miaka iliyopita”, amesema Mbunge huyo.

Mbunge huyo amedai tangu jamii hiyo ilipotupilia mbali utamaduni huo, matatizo mengi yametokea ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaorandaranda mitaani.

Mwaka 2014, Rais Uhuru Kenyatta aliidhinisha Sheria ya ndoa ambayo inawaruhusu wanaume kuoa wanawake wengi kisheria iwapo watasajili ndoa zao kama za kitamaduni au za Kiislamu.

Punguza Unene Unaokusumbua Katika Mwili Kwa Kutumia Bidhaa za Edmark

$
0
0


"Tumia Dawa za Edmark za Kupunguza uzito uliozidi Mwilini Mwako, Edmark ni Vurutubisho na Chakula Mbadala na Zimehakikiwa na TFDA...

Ni uhakika kwa afya yako,👉 kupunguza uzito na sumu mwilini, Mafuta Sehemu Mbaya, Kitambi na nyama uzembe na kutibu MAGONJWA Mbalimbali kwa msaada wako mfuate instagram: @my_health_my_wealth @my_health_my_wealth


Au Mtafute WhatsApp Huyu Dada kwa kutumia Namba +255783 566844

Pia Dawa za Edmark Zinaweza kupa Fursa ya Biashara Uweze pata Kipato Kirahisi kwa Kuwasaidia watu Kuimarisha Afya zao

Rais Magufuli Amteua Dk Fidelice Mafumiko Kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali

$
0
0
Rais Magufuli Amteua Dk Fidelice Mafumiko  Kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali
Rais John Magufuli amemteua Dk Fidelice Mafumiko  kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Uteuzi huo wa Dk Mafumiko umeanza leo Jumanne Aprili 3, 2018.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,  Gerson Msigwa imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Dk Mafumiko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).

Dk Mafumiko anachukua nafasi ya Profesa Samuel Manyele ambaye amemaliza muda wake

Mbunge Awahimiza Wanaume Kuoa Wake Wengi

$
0
0
Mbunge Awahimiza Wanaume Kuoa Wake Wengi
Mbunge mmoja nchini Kenya amefufua tena mjadala wa iwapo wanaume wanafaa kuwaoa wanawake wengi.

Gathoni wa Muchomba, ambaye ni mwakilishi wa wanawake kutoka kaunti ya Kiambu, amesema wanauem wakiwaoa wanawake wengi mengi ya matatizo ya kijamii yatafikia kikomo.

Video yake akitoa wito kwa watu wa jamii ya Wakikuyu kurejelea utamaduni wa kuwaoa wake wengi imesambaa sana katika mitandao ya kijamii nchini humo.

Amedai tangu jamii hiyo ilipotupilia mbali utamaduni huo, matatizo mengi yametokea ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaorandaranda mitaani.

Mwaka 2014, Rais Uhuru Kenyatta aliidhinisha Sheria ya Ndoa ambayo inawaruhusu wanaume kuoa wanawake wengi kisheria iwapo watasajili ndoa zao kama za kitamaduni au za Kiislamu.

Wakristo hata hivyo hawaruhusiwi kuoa wake wengi chini ya sheria hiyo.

Bi Muchomba alisema wengi wa wabunge tayari wamewaoa wake wengi na “wanajivunia” jambo hilo.

Nimemiss Kwenda Kula Bata Kama Zamani- Maimatha

$
0
0
Nimemiss Kwenda Kula Bata Kama Zamani- Maimatha
MTANGAZAJI maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’ ambaye alijifungua hivi karibuni, ameibuka na kueleza kwamba katika kipindi hiki, hakuna kitu kinachomuumiza roho kama kushindwa kutoka ‘out’ kwenda kula bata kama zamani.


Akipiga stori na Za Motomoto News, Mai alisema kuwa, kwa siku kadhaa alizokaa ndani kwa ajili ya uzazi na kumlea mwanaye amekuwa akitamani kwenda kula bata, lakini inashindikana kutokana na kichanga hicho. Hata hivyo, alisema akitimiza siku arobaini tu anamwacha na kuanza kujiachia kama awali.

“Huyu mwanangu ambaye anajulikana kwa jina la Tajiri Mtoto, nitamlea kidijitali kwani nikishamtoa tu arobaini, naanza kujiachia kwa kula bata kama zamani pamoja na kufanya kazi zangu, huyu sitamlea kama yule wa kwanza, kwamba nikae miaka miwili bila kufanya kazi, nikifanya hivyo itakula kwangu maana maisha ya sasa yamebadilika sana, ni lazima mtu ufanye kazi,” alisema.

Jeshi la Polisi Lamshikilia John Heche

$
0
0
Jeshi la Polisi Lamshikilia John Heche
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya DSM, linamshikilia Mbunge wa Tarime Vijini, John Heche (CHADEMA), kwa tuhuma za kushindwa kuripoti polisi kama alivyotakiwa jeshi hilo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu DSM, Lazaro Mambosasa amethibitisha kushikiliwa kwa mbunge huyo.

“Ni kama alivyoshikiliwa mwenzake Mdee naye hakuripoti, walikuja wakatakiwa kurudi wote wao hawakurudi, hakuna kosa jipya kosa lake ni kutorudi hadi wenzake wanapelekwa mahakamani,” -Mambosasa.

Serikali Yataka Kesi ya Kina Mbowe Kusikilizwa Mfululizo

$
0
0
Serikali yataka kesi ya kina Mbowe kusikilizwa mfululizo
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine sita wa chama hicho wamerejea uraiani jana baada ya kutimiza masharti ya dhamana, huku Jamhuri ikiomba kesi ya uchochezi inayowakabili isikilizwe haraka kwa kuwa ushahidi umekamilika.

Wengine waliopata dhamana baada ya kusota mahabusu kwa siku tano ni Katibu Mkuu, Dk Vincent Mashinji; manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar); Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; na mhazini wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Esther Matiko.

Kiongozi mwingine aliyeachiwa kwa dhamana baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuunganishwa na wenzake ni mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee aliyekamatwa na Polisi Jumapili usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Afrika Kusini.

Baada ya kusomewa mashtaka ya uchochezi na uasi, Jamhuri ilipinga dhamana ya Mdee ombi lililokataliwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Machi 27, viongozi hao isipokuwa Mdee, walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka manane yakiwamo ya kuhamasisha uasi, chuki na maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Kati ya makosa hayo, mawili yanawakabili wote sita ambayo ni kufanya mkusanyiko au maandamano yasiyo halali Februari 16 wakiwa Barabara ya Kawawa, Kinondoni Mkwajuni.

Masharti ya dhamana waliyotimizwa ni kila mshtakiwa kusaini hati ya dhamana ya Sh20 milioni; kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka uongozi wa mtaa au kijiji; nakala za vitambulisho vyao; na kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi kila Ijumaa.

Walifikishwa Kisutu jana saa mbili asubuhi na walisubiri hadi saa 5:47 asubuhi Hakimu Mashauri alipoingia mahakamani.

Wakati kesi ikiendelea, idadi kubwa ya wanachama wa Chadema waliojitokeza nje ya uzio wa Mahakama wakiimba nyimbo kutaka viongozi hao waachiwe, walitawanywa na polisi kwa kumwagiwa maji ya kuwasha na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema 26 wanashikiliwa akiwamo mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Baada ya Hakimu Mashauri kuingia mahakamani, upande wa mashtaka uliomba kurekebisha hati ya mashtaka ili kumwongeza Mdee katika kesi hiyo. Pia, uliomba kuwasomea washtakiwa makosa upya lakini mawakili wa utetezi wakiongozwa na Peter Kibatala walipinga wakiomba Mahakama itekeleze kwanza amri ya masharti ya dhamana kwa washtakiwa wa awali. Mahakama ilikubali ombi hilo, hivyo wadhamini wa washtakiwa waliwasilisha vielelezo vyao vya dhamana ambavyo baada ya kukaguliwa na kujiridhisha walidhaminiwa.

Dhamana ya Mdee yapingwa

Baada ya hilo, Mdee alipandishwa kizimbani na washtakiwa wote walisomewa upya mashtaka ambayo walikana kuyatenda.

Kibatala aliiomba Mdee apewe dhamana kwa masharti kama yaliyotolewa kwa washtakiwa wengine kwa kuzingatia msingi wa kisheria wa uamuzi wa mashauri yanayofanana lakini Jamhuri ilipinga ikidai alishindwa kutekeleza masharti ya dhamana ya polisi.

Wakili wa Serikali Mkuu, Dk Zainabu Mango alisema kabla ya kufikishwa mahakamani, Mdee alipewa dhamana polisi ambayo hakukidhi masharti yake yaliyomtaka kuripoti mara moja kwa wiki lakini hakuhudhuria mara tatu mfululizo Machi 15, 22 na 29.

Wakili mwingine wa Serikali Faraja Nchimbi aliiomba Mahakama kama itaona ni lazima kumpa dhamana, izingatie vigezo vya kisheria ikiwa ni pamoja na kuwa na wadhamini, kuwasilisha polisi hati za kusafiria na kutotoka nje ya Dar es Salaam bila kibali.

Kibatala akijibu hoja hizo za Jamhuri alisema ni za kufikirika, kwamba mawakili si maofisa wapelelezi, wakamataji wala waliompa dhamana hivyo wanayoyasema ni uvumi.

Hakimu Mashauri alitupilia mbali pingamizi la dhamana dhidi ya Mdee akisema hakuna sheria inayoeleza kuwa mshtakiwa akiruka dhamana ya polisi na mahakamani anyimwe dhamana kwa kuwa hizo ni taasisi mbili tofauti.

Ombi kesi kusikilizwa mfululizo

Baada ya uamuzi huo, Nchimbi aliwasilisha ombi kuwa Mahakama iruhusu kesi isikilizwe haraka akisema upelelezi umekamilika.

Aliomba usikilizwaji wa awali ufanyike leo mchana ili washtakiwa wasomewe maelezo ya awali ya kesi na Mahakama ipange tarehe ya kuanza usikilizwaji rasmi wa ushahidi. Alisema msingi wa ombi hilo ni kutokana na ukweli kwamba washtakiwa wengi ni wabunge na kwa nafasi zao kesi hiyo inavuta hisia za watu wengi.

Kibatala alipinga ombi hilo akisema yeye ndiye kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi na kwamba leo atakuwa na kesi nyingine Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi na kesho atakuwa na kesi nyingine.

Alisema pia atakuwa na vikao na mkutano wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) jijini Arusha, hivyo aliomba usikilizwaji wa awali ufanyike Aprili 16 ombi ambalo lilikubaliwa na Hakimu Mashauri.

Baada ya kutoka mahakamani, Mbowe alisema ameona mengi mahabusu na atapanga siku ya kuyaeleza na kutoa taarifa ya kesi inayowakabili.

Tuzo Alizopata Wema Zawatoa Povu Bongo Movie Wasema Amependelewa

$
0
0
Tuzo Alizopata Wema Zawatoa Povu Bongo Movie  Wasema Amependelewa
Tuzo ya mwigizaji bora wa filamu wa kike nchini ya SZIFF aliyoipata Wema Sepetu juzi, imeonekana kuwagawa mastaa wa Bongo Movie wengine wakimbeza na baadhi wakimpongeza.

Mpasuko huo umekuja kufuatia kuwepo baadhi ya mastaa wanaoona Wema amestahili tuzo hiyo huku wengine wakiamini amepewa kwa upendeleo.

Maneno yalianza kwenye mitandao muda mfupi baada ya Wema kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo aliyokuwa akiwania na Riyama Ally na wasanii wengine wa kike chipukizi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwigizaji Irene Uwoya aliweka picha ya Gabo na kuandika, "Hapa hawajapepesa umestahili."

Mwigizaji Youbnesh maarufu Batuli akaweka picha hiyo hiyo na kuandika," Ukisikia mtu kutenda haki na kutendewa haki ndio hii. Gabo wangu Mwenyezi Mungu aendelee kukunyanyua juu Inshallah, endelea kutunza heshima na tamaduni zetu, keep working hard baba hongera sana."

Kauli hizo zimeonekana kuwakera mashabiki wengi wa Wema na kujikuta wakiwashambulia mastaa hao kwamba kumpongeza Gabo peke yake kunaashiria kuwa hawakubaliani na ushindi wa mwigizaji huyo wa kike aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006.

Pamona na mashabiki kuja juu, mwigizaji  Eshe Buheti alikuwa na maoni tofauti na wenzake akionyesha kuamini kuwa Wema alistahili tuzo hiyo.

Hakuishia hapo Eshe aliwatupia lawama mastaa wa Bongo Movie kwa kudharau walipotakiwa kuwasilisha filamu ili zishindanishwe kwenye tuzo hizo.

"Mlitegemea nini wakati tulipoambiwa tupeleke filamu tulilegeza kamba, wenzetu wakatumia fursa. Hili ni funzo tumelipata nadhani mwakani kila mtu ataamka alipolala. Tuache maneno jamani, tupongezane kwa waliostahili.”

Mwingine aliyemtetea Wema ni mwigizaji Faiza Ally akisema waigizaji wana roho mbaya kwamba hawapendi kuona mwenzao akifanikiwa.

Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images