Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Derby Hazijaisha, Leo ni Vita ya Nafasi ya Pili Pale Madrid

$
0
0
Baada ya jana kushuhudia derby kali zadi katika msimu wa ligi kati ya Manchester City vs Manchester United, hii leo tunakwenda kuona derby nyingine ambapo Real Madrid wataikaribisha Athletico Madrid.

Tofauti na derby kati ya Man City na Man United, derby ya Madrid haina bingwa na wote hawa wawili wanapambana kwa ajili ya kutafuta nafasi ya pili katika msimu huu wa La Liga.

Athletico Madrid hawajawahi shinda hapa Bernabeu tangu 1999, lakini Athletico wamewahi kushinda michezo mitatu kati ya michezo 11 ambayo wamecheza katika uwanja huu wa Santiago Bernabeu

Katika michezo yao 4 iliyopita katika ligi, Athletico Madrid wamepoteza michezo miwili lakini ushindi wa 2-0 dhidi ya Sportinh katikati ya wiki unawapa hamasa kubwa kuweza kushinda mchezo wao wa leo.

Pamoja na kuuanza msimu kwa kusuasua, sasa vijana wa Zinedine Zidane wanaonekana kukaa vizuri katika La Liga, michezo yao 14 iliyopita, Real Madrid wamefanikiwa kushinda michezo 12.

Kumaliza nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kwa kiasi fulani itaweka ajira ya Zinedine Zidane sehemu nzuri, ushindi wa leo utawapa alama 66 ikiwa ni alama 1 nyuma ya Athletico Madrid walioko nafasi ya pili.

Akina Dada, Sio Kila Ex Wako Anayeomba Mrudiane Anamaanisha...

$
0
0
Sio Kila EX wako anayeomba Mrudiane anamaanisha! Wengine huomba kurudi ili wakutesti tu jinsi ulivyo Mbulula,jinsi usivyo na msimamo na jinsi ulivyo CHEAP na huna Misimamo wala Future.
Jitu mmeachana miezi 6,leo linakutesti lirudishe majeshi,na wewe ulivyo kiazi,upo-upo tu,ina maana miezi yote hii ulikuwa umeganda unasubiria rehema zake ama??

Kurudia Matapishi ya EX ukitegemea Amebadilika ni Sawa na Kupika Sufuria la Makande kwa Mshumaa,Utaambulia Masizi tu..
Kipi kipya kakiona kwako hadi arudi??Nini Kilimshinda huko nyuma ambacho leo anakiweza anataka kurudi??Akafie Mbele huko.

KUWA NA MSIMAMO,Ukisema Its Over umaanishe,sio unakuwa na hisia zinapepea tu kama Bendera ya Katibu Kata wa Kishumundu...Mtu kama Hajielewi achana nae,siku akijirudisha mwambie kwanza akapimwe Minyoo ya Kinyarwanda.
Umekazana kuwaambia marafiki zako 'Siku hizi hakuna Mapenzi ya dhati watu wote Majanga tu',nani amekwambia hayapo??Yapo sana ila wewe unatumia mbinu tofauti..Huwezi kusoma Degree ya Law halafu u-apply kazi ya Chief Accountant wa Bodi ya Tumbaku...Kila siku utasingizia Balance Sheet haina Jurisprudence..Lawyers mmenielewa!

Acha kudate watu wasiojielewa,Usidate kwa sababu uko lonely,Usiwe desperate kuingia Mahusiano kwa sababu shosti zako wanakusimulia walivyopelekwa Ruwenzori Waterfalls..Ingia kwenye Mahusiano pale Moyo wako ukiwa tayari na mtu uliyemfia kihisia na amekuwa approved na Veins,Auricles,na Aorta za Moyo wako kwamba He/She is really the One..
Unadate na mtu ambaye mustakabali wake mwenyewe haujui,ukimuuliza anataka kuwa wapi ndani ya miaka 5 ijayo anakwambia Mungu anajua dont worry,halafu BBM na Instagram unajiita Baby Ake Mie Iam in Love..Utaishia kufua boxer hadi kucha zinukie gololi!

Mbwa kamwe hashughuliki na kesi za Paka kufungiwa kabatini.Date the Right Person,With Right reasons,in a Right Time uone kama Mapenzi hayapo...

Je Wajua Kujamiaana na Mtu Hata Kwa Dakika Moja Unaweka Agano la Damu..Je Wajua Madhara yake?

$
0
0
Unapohusiana na mtu kimapenzi unafanya naye agano la damu. Agano hilo maana yake ni kwamba wewe unakubaliana na kufungamana na sifa na tabia pamoja na vifungo vingine vyote kama vile laana, mizimu, matatizo na majanga mbalimbali yanayomhusu huyo uliyefanya naye mapenzi, kadhalika na yeye anafungamana na wewe katika mambo hayo. Agano la namna hiyo humtaka aliyeingia katika hayo mapatano kukubaliana nayo "consistently". Iwapo mhusika hatatii au ataenda kinyume na agano, ndipo agano hilo "hutrigger malice" na kusababisha kutokuelewana, vurumai, kutokupendana na hata kuuana katika mahusiano na mara nyingi kupelekea kuachana!

Kimsingi, unapojamiana na mtu unakubaliana naye kuchangia kila kilicho chake, na yeye pia anakubaliana kuchangia na wewe kila kilicho chako, hasa laana na matatizo kama vile magonjwa na mizimu kwa sababu hivi vitu vimejengwa katika maagano ya damu.

Ndio maana wakati mnaoana na mwenzio mlipendana sana, lakini kwa sababu wewe au mwenzi wako alichepuka na kufanya maagano: ugomvi, mapigano, kutishiana, chuki na hata kutaka kuuana hakuishi kila leo! Swala sio wivu kwamba unahisi mwenzi wako anakusaliti au kuhitilafiana katika mambo tu ya kawaida, issue ni yale maagano ya damu ambayo "hudemand price"!

Mara nyingi unasikia watu wanalalamika kuhusu tabia za watoto "huyu mtoto tabia kaichukua wapi, mbona baba na mama yake au ukoo wao hawako hivyo?". Chanzo cha tabia za ajabuajabu za watoto ni matokeo ya michepuko iliyofanya maagano na watu/koo zingine zenye laana. Laana na matatizo yanayoletwa na agano la damu katika familia havihitaji mtu kuchepuka na kuzaa nje ya ndoa, bali tu kuhusiana katika mapenzi!

Mimi nilipoingia kwenye mahusiano na mke wangu nilivunja maagano yote kwa jina la Yesu. Lakini kumbuka kuwa huwezi kuvunja maagano kama vile ya michepuko kwa jina la Yesu ili "kufavor your own evil deeds"!

Maagano yanayofanywa na watu kwa njia ya mapenzi huenda vizazi hadi vizazi. Hii ni sawa kabisa kwa mjibu wa sayansi kwani "hereditary information" kutoka kizazi hadi kizazi hubebwa na viasili vilivyopo katika damu, mfano DNA.

Pasco anaweza kuendeleza hii mada kwa uchambuzi zaidi.

Mie na mke wangu tuna furaha fulltime kwa sababu mapenzi yetu yananawiri kila kukicha, na huwa hatuelewi kabisa matatizo katika ndoa za watu yanatokana na nini! "We are the happiest couple" kwa sababu "we posses several life secrets" mojawapo ni siri kuhusu agano la damu!

Tambueni ya kwamba one of the great decisions a person can make in his/her life ni kuwa na uhusiano wa kimapenzi (hata kwa dakika moja) na mtu kwa sababu anafanya naye life covenant "blood covenant"!
We teach you things that matter most!

- LifeHacker

Wanaume Watoa Wake zao Kama BET ya Mpira Man United Vs Man City...Idriss Sultan Afunguka

$
0
0

From @idrissultan - Zamani nikiona hii ningecheka sanaaaa nisema “Na mvua hii mke wa mtu anafanywa hamna” ila leo nimemaindi na nakupa sababu. Kuna kitu kwa kiingereza kinaitwa “OBJECTIFY” ambacho ni kum-treat mtu au mnyama kama kifaa au kitu.

Kwa Africa naona tumezidisha kidogo hili na maybe ni wakati tukajikagua vizuri. Kwa mfano huu tumemfanya mke wa Amani kama kifaa au kitu, hana usemi katika huu ufala wetu wa mechi za mpira, yeye ni kukaa asubiri Man City ashinde ili apelekwe kwa mawanaume mwingine baada ya wiki arudi. I repeat “Utani tufanye sana ila tukiwa hili tunalijua”. Sijawahi sikia mwanamke anashindwa kwenye bahati nasibu na kusema anamtoa mhanga mmewe

Mahari ni kusema “Nawashukuru wazazi kwa kumtunza mkwe wangu mpaka sasa mnanikabidhi nimpende na kumjali kuliko ninyi” . Haimaanishi “Sasa nimemnunua mtoto wenu na risiti ni cheti cha ndoa”..

Mtume Muhammad (SAW) alikua anaoa mwanamke kwasababu yupo lonely au mumewe kafariki na sio kujionyesha kuwa ana uwezo wa kuoa tu kuonyesha mabavu. We should respect the woman that gives you kids and feeds you hata kama wote mnaamka kwenda kazini ila yeye anafanya extra. DO NOT OBJECTIFY HER 😒.

Mwanaume wa kweli, anayejiamini, anayekubali uwanaume wake, anayejiheshimu hawezi fanya ujinga kama huu. Mkeo ni siri yako wanatakiwa wanaume wakimuona wamuogopeeee balaaa. Acheni siku nikiona mtaona, unamshika hata mkono nakupiga risasi 😒

Watu 3 Kati ya 6 Waliotoweka Siku 5 Zilizopita Wapatikana Wakiwa hai

$
0
0

PEMBA: Watu 3 kati ya 6 waliotoweka siku 5 zilizopita wapatikana wakiwa hai. Jeshi la Polisi linaendelea na utaratibu wa kuwahoji.

Waliopatikana ni Juma Kombo Fimbo (17), Said Shanani Mohamed (16) na Abdallah Khamis Abdallah (19)

Imeelezwa vijana hao walionekana alfajiri, wawili kati yao mikononi wakiwa na kamba.

Taarifa kamili kuhusu tukio zima la kutekwa nyara kwa vijana hao itatolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini walikotoweka vijana hao siku 5 zilizopita

Askofu Kakobe Afunguka Sababu za Kutokwenda Uhamiaji

$
0
0

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amefunguka na kukiri wazi kuwa hakuweza kwenda ofisi za uhamiaji kwa mara ya kwanza alipoitwa kutokana na kuwa busy na shughuli za pasaka.

Mchungaji Kakobe amesema hayo baada ya kupata wito wa pili kufika katika ofisi za uhamiaji siku ya Jumatatu April 9, 2018 ambapo amesema kuwa atakwenda ili kuitika wito huo kama ambavyo amehitajika kufika majira ya saa nne asubuhi.

"Ni kweli tumepata barua ndiyo tunajipanga kwenda kesho Jumatatu majira ya saa nne asubuhi kama ambavyo barua imedai, ni kweli niliitwa kwa mara ya kwanza ila yalikuwa ni majira ya pasaka na kipindi hicho kidogo tulikuwa na shuguli nzito kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka ambayo ndiyo sikuu kubwa sana kwa wakristo, kwa hiyo kutokana na kutofika ndiyo maana wameleta hii barua nyingine ya kukumbushia hivyo tutafika hiyo kesho kutokana na wito wao" alisisitiza Kakobe

Kwa upande wa Naibu Kamishna wa Uhamiaji Crispin Crispin Ngonyani alikiri kumwita kwa mara ya pili mchungaji huyo lakini hajaweza wazi sababu kubwa za wao kumwita mchungaji huyo katika ofisi zao, ingawa watu wanahusisha kuitwa kwa Kakobe kuwa huenda ofisi hizo zina mashaka na uraia wake kama zilivyo onyesha mashaka juu ya uraia wa Mwanafunzi wa UDSM Abdul Nondo ambaye amehitajika kufika ofisi za uhamiaji tarehe 20 April akiwa na vyeti vya kuzaliwa vya wazazi wake wote, pamoja na vyeti vya babu na bibi zake wa pande zote za wazazi wake.

Msimamo wa Rais Magufuli Kuhusu Serikali Kugawa Ng'ombe Longido

$
0
0

"Nimewaita Wabunge wa Arusha hapa waje waeleze shida zao. Shida hizo nimezipokea, lakini ni shida moja tu nataka niijibu hapa, ile ya kugawa ng'ombe. Sigawi Ng'ombe Mimi

Ninafahamu Mzee wangu Kikwete alienda kuwagawia ng'ombe kule Longido. Hilo Mimi siliwezi!

Tukianza na utaratibu huu; Ng'ombe wanakufa halafu Serikali inagawa, Pamba zikikauka Serikali inagawa, Korosho zikiharibika Serikali inagawa, hilo Mimi siliwezi nataka nizungumze wazi

Kwahiyo sitopeleka Ng'ombe Longido nataka niwaeleze hivyo. Zilizogawiwa wakati ule ni hizo hizo. Sijawahi kuahidi kugawa ng'ombe. Huyo ndio Magufuli!"

Okoa Ndoa yako Sasa...Umepungukiwa na Nguvu za Kiume na Unashindwa Kupanda Mlima Vizuri

$
0
0

OKOA NDOA YAKO SASA : JE UMEPUNGUKIWA NA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO AU MPENZI WAKO HAKUTIMIZII UTAKACHO:


Acha kujiona mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kwa sababu ya kutokuwa na nguvu za kiume au Uume wako mdogo

Dawa YA MAPRO POWERA ndio dawa sahihi na tiba tosha kwa sasa Kutibu tatizo na kuponesha kabisa tatizo LA KUWAI KUFIKA KILELENI KABLA MWENZI WAKO BADO AJAKOJOA

KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA NA MWILI KUCHOKA

UUME KUSINYAA NA KUWA LEGELEGE

KUUMWA NA TUMBO WAKATI UNAPOMALIZA KUFANYA TENDO

Dawa hii utumiwa ata na wazee wenye umri mkubwa na haina madhara yoyote

MAKAKANUA HII NI dawa ya maumbili madogo urefusha na kunenepesha saizi upendayo saiz 5-6-7-8 na unene sm 3-4-5 kwa mini huabiki kwa kuwa na UUME mdogo wai sasa upate tiba sahihi kabisa na ni tofauti na ulizowai kutumia :

Tunarudisha mke au mpenzi ndani ya masaa matatu tu zipo dawa za presha kisukali vidonda vya tumbo korodani iliyovimba dawa za uzazi tunapunguza matiti makubwa kitambi na mwili mkubwa dawa zipo FIKA OFISINI KWANGU MBAGALA ZAKHEMU KWA WATEJA AMBAO AMTAKUWA NA NAFASI YA KUJA OFISINI AU MLIO MKOANI MTALETEWA p

Piga simu 0743362017 au 0789234653

DR AGU

Polepole Ataka Rais Magufuli Apewe Muda Kwanza wa Kunyoosha

$
0
0

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM , Ndg Humphrey Polepole ametaka Rais Magufuli apewe muda kwanza wa kunyoosha na kurejesha misingi ya utaifa kabla hajagusa kwenye suala la mchakato wa Katiba Mpya.

Polepole ametoa kauli wakati alipokuwa akifanya majibizano katika ukurasa wake
ahi kusema Katiba inayopendekezwa ni nzuri hivyo rais anapaswa kupewa muda wa kuimarisha nchi na Ukatiba.

"Aliyesema Katiba Inayopendekezwa nzuri nani? Ilipatikana bila muafaka, maridhiano na uelewa wa pamoja. Tumpe nafasi Ndg. Magufuli atunyooshe, aturejeshee misingi ya Utaifa, hasa nidhamu ya sisi viongozi na umuhimu wa kuheshimu watu. Saizi tujenge nchi na kuimarisha UKATIBA", Polepole.

Oktoba, 20014 Bunge maalumu la Katiba nchini Tanzania lilipitisha rasimu ya katiba iliyopendekezwa ambapo kabla ya kupitishwa kwa rasimu hiyo, bunge hilo maalum lilikaa kama kamati kujadili mapendekezo katika Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na tume hiyo ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya uongozi wa Jaji Joseph Warioba.

Zoezi hilo la upigaji kura ambalo lilianza Septemba 29 mpaka Oktoba 2, siku matokeo yalipotangazwa, lilisusiwa na wabunge wengi wa upinzani, kwa madai kuwa baadhi ya vipengele vya awali vilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyopewa kazi ya kukusanya maoni kutoka kwa mwananchi, vilikuwa vimeondolewa.

Kampuni ya Simu ya Apple Yaamua Kuingia Kwenye Biashara ya Magari

$
0
0

Kampuni ya Apple maarufu kwa utengenezaji wa simu za iPhone inatarajia kuzindua gari lake la kwanza mwaka 2020. Pichani ni moja ya mfano mmojawapo.

Meya Aliyesifiwa na Rais Afunguka Kuhusu Kuhama

$
0
0
Meya, Wajiji la Arusha, Kalista Lazaro (CHADEMA) amefunguka na kusema kitendo cha Rais kumsifia mbele ya hadhara ni heshima kwake na viongozi wa Arusha na kusema hakuna sababu kiongozi aliyechaguliwa na wananchi kuhama chama kwa kumuunga mkono Rais.


Kalista Lazaro alisema hayo April 7, 2018 baada ya Rais Magufuli kumsifia kuwa ni kati ya watu ambao wanapenda maendeleo na kufanya maendeleo katika jiji la Arusha Mjini licha ya kiongozi huyo kutokea katika chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

"Hii pongezi la Rais ni kwa sababu alipokea taarifa ya utendaji ya jiji la Arusha na tangu alipoingia nilimweleza mambo ambayo tumefanya kwa mfano amepongeza jitihada kubwa ya ujenzi wa madarasa tangu mwaka 2016 ambapo tumejenga madarasa 105, 2017 tumejenga madarasa 61, tunapandisha vituo vya afya mara moja na dispensary kwa ujumla tano, hospitali ya wilaya, barabara za lami, barabara za vumbi na juzi tumetangaza tenda ya kilometa 10 za lami katika jiji la Arusha ambapo barabara ya Njiro, Kwa Mlombo, Sombetini zinaenda kujengwa lami pamoja na barabara ya Ngarenalo kwangu mimi ni heshima na hii heshima nimeipokea kwa niamba ya wananchi wa jiji la Arusha" alisema Kalista Lazaro 

Aidha Kalista Lazaro amedai kupongezwa kwake kuwe funzo kwa viongozi wengine ambao wamekuwa wakihama kutoka CHADEMA na kwenda CCM kwa kigezo cha kuunga mkono serikali na kudai kuwa ukitaka kufanya hivyo unachotakiwa kutekeleza tu yale uliyoahidi kwa wananchi wako na si kwa kigezo cha kuhama chama.

"Wale ambao walikuwa wanabeza na hawatambui sasa wametambua kuwa Meya wao anapongezwa na Rais Magufuli mbele ya halaiki ya watu, mbele ya polisi, mbele ya Mkuu wa Majeshi hivyo Rais anaona kazi tunayofanya na niwaambie wananchi hakuna sababu ya kiongozi wa kuchaguliwa kuhama, ukitaka kutekeleza wajibu wako na kuunga mkono serikali unatakiwa ufanye kazi ambayo umeahidi wananchi wako. Mimi leo napongezwa nikiwa ndani ya CHADEMA, nikiwa Meya wa CHADEMA na diwani wa CHADEMA kwangu mimi ni heshima" alisisitiza

SOMA PIA: Nafasi 200 za Kazi Zilizotangazwa Leo 

Ali Choki aikacha Twanga Pepeta na kujiunga na The Mafik Band (Video)

$
0
0
Msanii wa muziki wa dansi, Ali Choki amefunguka kwa kusema kwamba kwasasa ameachana na bendi ya Twanga Pepeta na kujiunga na bendi mpya ya The Mafik Band ambayo inasimamiwa na msanii wa muziki, Shetta. Muimbaji huyo mkongwe amedai hawezi tena kurudi katika bendi hiyo ya zamani kwa kuwa haina mvuto kama zamani.

VIDEO:


SOMA PIA: Government Job Opportunities, Application Deadline 11 April 2018

Faida za Mti wa Mlonge kwa Mama Anayenyonyesha

$
0
0
Maziwa ya mama ndiyo yanakubalika na jamii kama chakula bora zaidi cha mtoto kwani  yana kinga ya mwili na viinilishe muhimu kwa ajili ya mtoto na yana kila kitu kinachohitajika katika kumlinda mtoto dhidi ya maambukizi, aleji na kumpa mtoto kinga ya mwili na afya kwa ujumla.

 Kuhusu Mti wa mlonge:-

Majani ya mti wa mlonge yana kiasi cha kutosha cha vitamini na madini matano mhimu zaidi kama madini ya chuma, kalsiamu, Vitamini A, E na K.

Mti wa mlonge una Madini chuma yanahitajika katika kuzuia uchovu . Mara baada ya kujifungua mama wengi wanatokewa kuwa na upungufu wa madini ya chuma kama matokeo ya kupotea kwa damu nyingi wakati wa kujifungua jambo ambalo linaweza kupelekea hali ya uchovu sugu na udhaifu wa mwili kwa ujumla.

Kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa majani ya mlonge kina zaidi ya asilimia 46.8 cha mahitaji yako ya madini chuma kwa siku.

Matumizi ya mlonge kwa mama anayenyonyesha yatapelekea kumuondolea uchovu na kumuongezea kiasi kingi cha maziwa kwa ajili ya mtoto.

Mlonge una madini chuma (iron) mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach

Mti wa mlonge una Kalsiamu  ambayo ni mhimu katika kuimarisha mifupa na meno kwa wote mama na mtoto. Mlonge una Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe

Mlonge una Vitamini K husaidia damu isigande na ni mhimu hali hii kwa mama anayenyonyesha na kwa mtoto pia.

Vitamini K kwa kawaida hutolewa kwa watoto kwa njia ya sindano au vidonge mara tu wanapozaliwa. Ni vitamini mhimu kwa wamama ambao wanaweza kupatwa na tatizo la kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua.



Chanzo na: Fadhili Paulo

Nakua Chizi Kwa Wivu wa Mke Wangu...

$
0
0
Nina mke mmoja ambae tunapendana sana, tatizo ana WIVU kupindukia.

1.Ninapoingia tu home ananidaka na kuninusa nguo, akisikia pafyum kwa mbali MATATIZO,
Mim situmii pafyum ila usafiri wa daladala kwetu ni shida, mnabana hadi kupumua shida. Matokeo yake sipendi watu waniguse kitu ambacho ni kigumu kwenye usafiri wa jumuiya!

2.Kila ninapoenda anataka nitume picha kwa Whatsap, hata kama kwenye daladala nimesimama, anataka nipenye dirishan nipige hilo eneo,au nijipige kitu ambacho watu hawakubali maana wanaona unawapiga wao!

Yaani nimekuwa mtu wa kupiga piga picha mpaka ofisini wananishangaa

Je Hii ni sawa Kwa Wenzangu?

JE NIFANYEJE MAANA TUNAPENDANA SANA.

SOMA PIA: Nampenda Kwasababu Ananigusa Penyewe Kwenye Kipele..

Download Upya Application Yetu ya UDAKU SPECIAL .....Ile Ya Zamani Tutaifuta

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya UDAKU SPECIAL Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Marekebisho Makubwa tumeyafanya ikiwa na tatizo la Notification kutatuliwa

NB: App mpya ina Icon Nyekundu

 Bonyeza Hapa Chini

==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>  

Endapo Yanga SC itafanikiwa kuwatoa Dicha itaingiza kiasi hiki cha fedha kutoka CAF

$
0
0
Jana Aprili 08, 2018 klabu ya Yanga imefanikiwa kupata matokeo ya goli 2-0 dhidi ya Waethiopia ‘Welaytta Dicha’ kwenye mchezo wa kombe la shirikisho Afrika, ambapo kwa sasa Yanga watahitaji ushindi au sare ya namna yoyote ili iweze kusonga mbele.


Endapo Yanga watafanikiwa kusonga mbele watajishindia kitita cha dola $150,000 sawa na tsh milioni 339 zinazotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa kila klabu inayofanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Hata hivyo, Yanga SC wanaonekana kuwa imara zaidi na kutoa matumaini kwa Watanzania kwani licha ya mchezo wa jana kukosekana kwa wachezaji wao muhimu kama Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa na Said Juma ‘Makapu’ wanaotumikia adhabu ya kadi mbili za njano, bado Yanga wanaonekana kuwazidi uwezo Waethiopia hao.

klabu ya Yanga mchezo wa jana umekuwa mchezo wake wa kwanza kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika, baada ya kungolewaa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na klabu ya Township Rollers ya Botswana.

SOMA PIA: Mama Mwenye Nyumba Ananitega Sana.

Je Wajua Kwanini Mziki wa Dance Umekufa Bongo? Ali Choki Awatupia Lawama Watangazaji Wenye Umri Mdogo

$
0
0
Msanii Mkongwe wa muziki wa dansi nchini Tanzania, Ali Choki ametaja sababu zilizoupoteza kwenye ramani muziki wa dansi nchini Tanzania.

Ali Choki akiongea na Waandishi wa Habari jana Aprili 07, 2018 kwenye uzinduzi wa Respect Barber Shop amesema kuwa sababu kubwa ni umri wa watangazaji wengi kwenye vipindi vya burudani kuwa mdogo na wengi wao wanapendelea kucheza muziki wa Bongo Fleva sana kwani kipindi muziki wa dansi unatamba wengi wao walikuwa ni wadogo.

Akitoa sababu nyingine ya kupotea kwa muziki wa dansi ni uwezo wa kifedha wa kutengeneza video kali ambazo zingewafanya watu wengi wavutiwe kuangalia kazi za muziki huo.

Ali Choki amesema kuwa amejipanga kuurejesha muziki huo kwa upande wake ameahidi kufanya kolabo na msanii mkubwa wa Bongo Fleva na kutengeneza video nzuri ili kuvutia kizazi kipya cha Bongo Fleva

Najuta: Mchepuko Anataka Kunipeleka Kwa Makonda

$
0
0
Ilikuwa kama utani mwaka 2013 tukiwa kwenye daladala za Kimara - Posta. Nilimtongoza akanitunuku na mimba ya mtoto wa kike ikapatika na akajifungua salama salmini.

Kifupi nimekuwa nikitoa huduma zote kwa huyu mchepuko tokea akiwa mjamzito na nahudumia kwa kutoa kama laki mbili na nusu kila mwezi, lakini haridhiki kabisa anasema fedha haitoshi sababu mtoto anaugua mara kwa mara na mimi nilishamwambia siwezi toa zaidi ya hapo coz hata wife hamjui na nina watoto wengine kwa wife.

Tatizo ni tokea Makonda atangaze kuwa wanawake waliotelekezewa watoto wakatoe taarifa, aisee the whole week am at high risk... nalala kwa shida ni mawazo tu hadi wife kanistukia.. Ni ananitishia kila siku simu haziishi kuwa jumatatu atakuwa wa kwanza kunireport kwa Makonda, na mzaramo huyu kichwa chake antena haipo sawa najua hatanii ataenda tu. Nimejaribu kumtumia rafiki yake amshauri imeshindika.

Jana jioni nimemtumia laki moja, asubuhi hii kanitumia sms... "Unajua kulea wewe? Umenitumia vihela vya mboga hivi huoni wanaume wenzio wanavyotoa? Unajua Mobetto anapewa sh ngapi kwa siku? Kwa taarifa yako hii ni nauli ya tax kesho kwenda kwa Makonda"...

Wakuu hapa nakaribia kuwa chizi sometime najikuta naongea alone. Ushauri tafadhali.

By Pius

Rais Magufuli awataka viongozi wa dini kuhubiri amani

$
0
0
Rais John Magufuli amewataka viongozi wa madhehebu ya dini kuhubiri na kusisitiza amani ambayo ni msingi wa maendeleo.

Amesema hayo leo Aprili 8 katika misa ya kusimikwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Isaac Amani iliyofanyika katika parokia ya mtakatifu Theresia mjini humo.

Amenukuu maandiko matakatifu kutoka kwenye vitabu mbalimbali vya biblia yanayosisitiza  amani.

Kuhusu maombi matatu yaliyotolewa na Padri Aloyce juu ya kuhamishwa Shule ya Msingi Naura ambayo ilianzishwa mwaka 1950 ikiitwa St Theresa School mali ya Kanisa hilo ambayo ilitaifishwa na Serikali mwaka 1967 alisema suala hilo lina changamoto kulipatia majibu ya haraka.

"Nikitoa tamko la kurejesha shule hii leo litasumbua sana kila mali zilizotaifishwa mwaka 1967 zitatakiwa kurejeshwa nami sitaki mgogoro huu," alisema Rais Magufuli

Alisema anaamini kila jambo lina wakati wake na waendelee kumuombea  ili apate amani ya kutoa uamuzi sahihi.

Amesema hata suala la Shule ya Saint Jude inayotoa elimu bure kwa watoto wanaotoka kwenye Kaya zisizo na uwezo inayodaiwa kodi ya Sh6bilioni alisema hawezi kuingilia suala hilo kwakua lipo mahakamani na hataki kuonekana anavunja sheria.

Akizungumzia shughuli za maendeleo katika jiji la Arusha alisema kumekua na mafanikio makubwa katika huduma za elimu na afya.

Kwa upande wake Askofu Mkuu na  Balozi wa Papa nchini, Maleck Schosist alitoa salamu zake na kumtaka Askofu Mkuu ,Amani kufanya kazi ya utume.

Rais wa zamani wa Brazil Lula da Silva awasili jela kuanza kutumikia kifungo chake

$
0
0
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amewasili katika jela la Curibita kuanza kutumikia kifungo cha miaka 12 jela baada ya siku ya Ijumaa, mahakama kumhukumu kwa mashitaka ya ufisadi.

Matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vya Brazil yameonesha akiwasili kwa helikopta katika makao makuu ya polisi katika mji wa Curibita ulioko kusini mwa Brazil.

Hayo yanajiri baada ya Lula da Silva kujisalimisha kwa polisi ambapo mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 72 aliondoka Sao Paoli akiwa amezingirwa na walinzi kwenye jengo la muungano wa wafuasi vyama mjini humo.

Lula alikutwa na hatia ya kupokea rushwa kutoka kwenye kampuni kubwa ya ujenzi, ili iweze kupata mikataba ya serikali.

Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images