Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Jaji Ahoji Wingi wa Kesi za Ponda:Nani Yuko Nyuma ya Kesi Zako?

$
0
0
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemtaka katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aeleze sababu za kuwa na kesi nyingi, huku akihusishwa na matukio mbalimbali ya uhalifu nchini.

Pia mahakama hiyo imeamuru vyombo vya dola kuacha kuwazuia wafuasi wake kuingia mahakamani kusikiliza kesi zake, na kushauri kama wana wasiwasi nao, waweke mashine za ukaguzi katika mlango wa kuingilia mahakamani hapo.

Mwenendo huo wa Sheikh Ponda ulihojiwa mahakamani hapo na Jaji Augustine Shangwa juzi kabla ya kuanza kusikiliza rufaa yake ya kupinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyomtia hatiani katika kesi ya jinai, mwaka 2012.

“Sheikh Ponda, sijui ni kwa nini una kesi nyingi kiasi hiki. Kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi (Kisutu) una kesi, Mahakama Kuu una kesi. Nani yuko nyuma ya kesi zako? Je! Serikali inakuchukia?” alihoji Jaji Shangwa.

Licha kumhoji Sheikh Ponda maswali hayo, alimweleza kuwa kama atakuwa na jambo la kuzungumza, atampa nafasi siku nyingine rufaa yake itakapotajwa. Pia Jaji Shangwa alimshauri apunguze mapambano.

“Ikiwezekana uyapunguze (mapambano) maana dunia hii si ya kupambana nayo,” alisema Jaji Shangwa na kusisitiza kuwa lazima ajiulize kwa nini ana kesi nyingi.

Jaji Shangwa aliendelea kusema: “Jambo likitokea Zanzibar, wewe umo; likitokea Morogoro umo; likitokea Dar es Salaam umo. Bahati mbaya kuna kikundi cha Uamsho kinadaiwa kulipua mabomu na kuua watu, nasikia na wewe unatajwa kuhusishwa.”

Nuh Mziwanda wa Shilole alikopi kwa Nick Cannon na Mariah Carey Kuweka Tattoo? Amepata mfano!

$
0
0
Mwimbaji wa Bongo Flava, Nuh Mziwanda aliwashitua wengi baada ya kujichora tattoo yenye jina la mpenzi wake ‘Shilole’, tattoo ambayo haifutiki daima. Kitu ambacho kiliwashitua wengi.

“Mimi nimefanya hivi kwa kupenda kwangu, sijalazimishwa na mtu. Nimejisikia kufanya hivi kwa sababu nampenda sana Shilole…tukiachana basi lakini mimi nitabaki nayo hadi nitakapoenda kaburini.” Nuh aliiambia tovuti ya Times Fm.

Hata hivyo, Shilole alisema kuwa hatajichora kwa kuwa Nuh kafanya hivyo na kwamba anashukuru kwa uamuzi wake kwa kuwa hakulazimishwa na ni ishara ya upendo wa kweli tofauti na aliowahi kukutana nao awali.

Siwezi kusema ntafanya hivyo sijui na nini basi ni mapenzi tu na mimi siku nikiamua kufanya ntafanya kama ambavyo amefanya yeye. Kiukweli ana love ya ukweli kabisa tofauti na wanaume ambao nilikuwa nao, watu walikuwa wanapenda tu wasikie wanatoka na ShiShi kwa kutaka kutafuta kick na lakini Nuh kama Nuh ana upendo wa peke yake kabisa. Yaani hadi inafikia hatua nasema alikuwa wapi. Wanasema Mungu akitaka kukupa kitu hakuandikii barua.

Uamuzi wa Nuh Mziwanda unaendana na uamuzi alioufanya Nick Cannon na Mariah Carey mwaka 2008 walipojichora tattoo za kudumu kwenye miili yao baada ya kufunga ndoa. Nick aliandika mgongoni ‘Mariah’, na Mariah alijichora kipepeo chini ya mgongo na kuandika maandishi madogo ‘Mrs Cannon’.


 “Kwangu mimi pete ni maalum na zinavutia, lakini tattoo zinamaana zaidi kitu chochote. Ni za milele na milele…” Alisema Mariah Carey.

Hivi sasa Mariah na Nick Cannon wametengana na kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika wanasubiri talaka tu.

Lakini wamebaki na alama za tattoo kwenye maisha yao ambazo hazitafutika daima hata watakapokuwa na wapenzi wengine.

Hata hivyo, tattoo inaweza isiwe kitu kama watoto wao mapacha ambapo pia ni kiunganishi kikubwa katika maisha yao.

Je, Nuh Mziwanda na Shilole wao watafikia hatua ipi? Je, watadumu kama tattoo ya Nuh Mziwanda au watayeyuka na kuachiana alama za maandishi na….!

Tunawatakia kila la kheri.

Tetesi Mpya Kuhusu Kajala Kutoka Kimapenzi na Mwanamuziki wa Bongo Flava

$
0
0
Hii ni post ya Quick Rocka wiki nne zilizopita ambapo aliandika >>> #LatePost…Paula’s graduation. @new_kajala @lamataleah
Kama zitakua ni stori za kweli inaweza ikawa ni uhusiano mwingine unaowahusu Bongo Movie na Bongo Fleva na kujiunga kwenye list ya uhusiano wa kimapenzi kutoka kwenye viwanda hivyo viwili iliyo na watu kama Wema Sepetu na Diamond, Nuh Mziwanda na Shilole na wengine waliowahi kuingia kwenye headlines Msami wa THT na Irene Uwoya.

Hii ni post aliyoiweka Quick aliyoiweka kwenye instagram yake na kuandika >>> Ma gal kay kay….#Beautiful
Gossip Cop Soudy Brown kapiga stori na meneja wa Kajala ambae alikua na wawili hawa hata wiki iliyopita Tanga ambapo kazungumzia kinachoendelea kuhusu kazi mpya ya filamu ambayo inategemewa kutoka siku si nyingi ikimuhusisha Kajala na Quick Rocker, inaitwa Mbwa Mwitu.
Meneja amekanusha stori za uhusiano huo kuwepo na kusema wawili hawa wanafanya kazi tu, kwani haiwezekani watu kufanya kazi bila kuwa wapenzi?
Soudy alimuuliza uchumba wa Quick na Kajala ukojeukoje? akajibu >>> ‘nani alikwambia wana uhusiano? hamna hicho kitu… Quick tumefanya nae movie tu, hakuna biashara nyingine yoyote zaidi ya movie’

Maskini Zitto Kabwe Azidi Kuchoreshwa na Diva Baada ya Zitto Kumakana Diva..Embu Ona Hapa

$
0
0
Kuwa uyaone mengi sio maghorofa bali ni vituko vya binaadam katika hii dunia just imagine Zitto anavyoabika sasa hivi daaah, hivi kweli kuna mwanaume aliekuwa mahabani na Diva naye akasema nina girlfriend?? baada ya Zitto kumkana Drama Queen kwamba hatoki naye sasa drama queen amtolea za uso na kutoa moja ya email aliotumiwa na zitto mmmh Diva,Diva,Diva huendani na jina lako jus take a chill n relax, sijui unafanya comedy,attention seeker but you know better ila haipendezi punguza Mama:

Email Kutoka kwa Zitoo Kwenda Kwa Diva:
Source:Sintah Blog

Utafiti: Wanawake Wanene ni Mafundi Jikoni Kuliko Wembamba

$
0
0
Duniani kuna tafiti nyingi na mara nyingi wataalamu wa masuala mabalimbali huja na tafiti tofauti tofauti...

Moja ya tafiti ambayo imenivutia kiasi cha kuja hapa jamvini ni utofauti wa ufundi wa jikoni baina ya mwanamke kimbaumbau na yule mwenye neema za allah "curvaceous" ...

Inaaminika kwamba manawake wenye nyama za nyongeza 'curvy girls' wana ujuzi mkubwa wa mapishi kuwazidi wale ambao miili yao ni vimbaumbau...

Sababu kubwa haswa inayopelekea kuwepo kwa dhana hii ni kutokana na utofauti wa tabia za ulaji baina ya mwanamke tipwatipwa na kimbaumbau...

Wataalamu wanadai eti kwa kuwa wanawake vimbaumbau ni wavivu sana kula basi hata ujuzi wao wa kuandaa madikodiko, mahanjumati na mazagazaga ni mdogo pia...(hawa nafikiri ndio wale wanaochemsha nazi bila hata kuikuna)...

Hivyo wito wangu kwetu vidume haswa wale mnaotafuta waifu matirio, kama wewe ni mtu wa kuchunuku zagazaga hebu konsida basi hiki kigezo usijekuwa walazwa na njaa au kutwa washinda kwa mama muuza...

Najuta: Nilioa Mke Kwa Kuvutiwa Sura na Umbo Lake

$
0
0
Nilidhani nimepata kumbe nimepatikana! Mwaka jana mwezi wa tatu nilifunga ndoa na mke wangu. Tumejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume. Kitu kikubwa kilichosababisha nikamuoa ni sura yake ya kuvutia, sauti yake tamu pamoja na umbile lake kwa ujumla. Kiukweli ameumbika sana.

Tatizo alilo nalo mke wangu ni kwamba kwa sasa hakamatiki! Hatulii. Anatembea hadi na marafiki zangu. Kibaya zaidi ni kwamba siku hizi kila nikitaka kufanya naye mapenzi ananiambia hajisikii kufanya hivyo. 

Ameanza kunidharau na kuniona mimi sina hadhi kwake. Inaniuma sana.

Wazazi wa pande zote mbili wamejaribu kulitatua hili bila mafanikio.

Sasa nimeona kabla ya kuchukua maamuzi mengine mazito nimeamua niwashirikishe mnipe ushauri wenu. Nisaidieni kuokoa ndoa yangu jamani.

Mbowe: Mimi ni Kisiki cha CHADEMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana alikabidhiwa fomu na makada wa chama hicho na kumtaka awanie tena kiti hicho, ombi ambalo alilikubali na kufungua milango kwa wanachama wengine ‘kupimana naye kifua’. 

“Nafasi bado ipo, anayetaka kupima kifua na mimi ajitokeze. Tena nawaomba viongozi wangu msizuie fomu kwa anayetaka,” alisema Mbowe ambaye ameongoza chama hicho kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Makada wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiongozwa na kada maarufu, Athuman Mzigo (Mapigo Saba) kutoka Kigoma, walikutana na Mbowe na kuwasilisha maombi yao ya kumtaka awanie tena nafasi hiyo.

“Kutokana na sifa za mwenyekiti wetu, tumechangishana Sh200 kila mmoja hadi zikafika Sh50,000,” alisema Mapigo Saba huku akishangiliwa na makada wenzake alioambatana nao na kuongeza:

“Tumemwomba mwenyekiti agombee nafasi hiyo kwa kuzingatia sifa; kwanza anaijua vizuri idadi ya Watanzania na matatizo yao, pili anaungwa mkono na watu wengi na amekisaidia chama kukua. Tulikuwa na madiwani 40 leo wamefika 500, wabunge watano leo 48. Halafu hana ubaguzi ndiyo maana ameunganisha vyama vya upinzani na kuunda Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi).”

Huku akichomekea maneno ya lugha ya Kiha, Mapigo Saba alisema kuwa maombi ya kumtaka Mbowe agombee pia yametolewa katika mikoa ya Rukwa, Manyara, Iringa, Njombe, Jimbo la Same Magharibi, Zanzibar, Mwanza na Kilimanjaro.


Hotuba ya Mapigo Saba ilifuatiwa na salamu kutoka kwa wazee wa wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke, Baraza la Wanawake (Bawacha) na Baraza la Vijana (Bavicha).

Akitoa salamu za Bavicha, mwenyekiti wa baraza hilo Njombe, Emmanuel Masonga alisema Mbowe ni sawa na Joshua aliyemalizia kuwaongoza wana wa Israel kuingia nchi ya Kanaani:

“Sisi Wakristo tunajua kuwa Mussa alianzisha safari ya Waisrael kwenda Kanaani, ila hakuwafikisha. Kina Mtei (Edwin), Kimesera (Victor), Bob Makani na wengineo walianzisha safari ya kwenda Ikulu, ila hawakutufikisha. Mbowe ni sawa na Joshua atakayetufikisha Ikulu,” alisema Masonga.

Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Susan Lymo alimsifu Mbowe akisema ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa katika chama hicho.

“Mwaka 2000, kulikuwa na mwanamke mmoja katika viti maalumu, mwaka 2005 waliongezeka na kufikia sita na mwaka 2010 wamefikia 26. Mwenyekiti pia ameufanya mwaka huu kuwa wa wanawake kitaifa na ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa,” alisema Lymo.

Mbali na viongozi wa chama, alikuwapo pia Sheikh Rajab Katimba kutoka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu ambaye alimsifu Mbowe na kuomba agombee tena nafasi hiyo.

Mbowe akubali
Baada ya Mratibu wa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), Nickson Tugara kummwagia sifa Mbowe, Mapigo Saba alimkabidhi fomu, huku makada wakiimba, ‘Jembe, jembe, jembe…”

Mbowe aliishukuru Kamati Kuu ya chama hicho kwa kupanga uchaguzi Septemba 14, mwaka huu ambayo ni siku yake ya kuzaliwa huku akiahidi kujenga chama imara.

“Mtaiona Chadema mpya ifikapo Septemba 14. Hiki chama hakitakufa na hatutamvumilia mtu yeyote wa kabila lolote atakayekivuruga,” alisema.

Mbowe alisema hajawahi kuomba kugombea uenyekiti wa chama hicho tangu aliponza mwaka 2000…

 “Napata wakati mgumu ninapofikia wakati huu. Chadema ina watu mbalimbali wenye taaluma na uzoefu, kwa nini mimi? Makundi haya yaliyojitokeza kunichukulia fomu yanaweza kutafsiriwa na wapenda majungu kuwa nimepanga mimi.

“Leo ni mara ya tatu naombwa kugombea uenyekiti, sijawahi kuomba. Mwaka 2004, Mzee Makani aliniomba nikamkatalia, lakini akaunda kikundi cha wazee walionichukulia fomu.

“Mwaka 2005, chama hakikuwa na mgombea urais, awali alijitokeza Profesa Mwesiga Baregu lakini akajitoa, nikaambiwa nibebe mzigo. Mwaka 2009 nikaombwa tena kugombea.”

Alisema amedhamiria kujenga chama kimtandao na kimfumo ili kuondokana na mfumo wa kienyeji… “Huko nyuma wakati wa uchaguzi watu walipeana tu nyadhifa kiundugu tukadhani chama kimeongezeka. Lakini wakati huu uchaguzi umefanyika kwa miezi tisa.

“Tulisema hatuwezi kufanya uchaguzi wa Taifa bila kupata viongozi wa mkoa, wilaya, kata, kijiji na mtaa, kitongoji na shina.

Tumefanya uchaguzi, watu wamepima na kuona mambo magumu, mara unasikia wanakimbia wakisema wameacha uenyekiti, uache wakati chama kinakua?”

Mtuhumiwa Kinara wa Mauaji ya Wanawake jijiini Arusha Anaswa na jeshi la polisi

$
0
0
Mtu mmoja ambaye inadaiwa kinara wa kuua na kujeruhi wanawake maarufu, wafanyabiashara na wenye vyeo katika ofisi mbalimbali jijini Arusha, Adamu Mussa (30) mkazi wa Majengo Juu jijini Arusha ametiwa mbaroni.

Mtuhumiwa huyo ametiwa mbaroni juzi usiku na polisi na alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bastola mbili  na risasi saba na amekiri kuhusika katika mauaji na kujeruhi wanawake jijini Arusha.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas, alizitaja bastola mbili zilizokutwa nyumbani kwa mtuhumiwa moja ni aina ya Browning  iliyotengenezwa  Jamhuri ya Czech  yenye namba A 895936 na ilikutwa na risasi saba.

Alisema bastola ya pili aliyokutwa nyumbani kwake ni aina ya Lorsin yenye namba za usajili 379126 iliyotengezwa nchini Marekani ikiwa na risasi tatu.

Sabas alisema uchunguzi wa Polisi ulibaini kuwa bastola  aina ya Browning  ilikuwa mali ya Seleman Bakari Msuya (33) mkazi wa Sombetini jijini Arusha ambaye silaha yake hiyo iliibwa baada ya  gari lake kuvunjwa kioo siku za nyuma.

Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo amewasihi wanawake kuwa na moyo wa uvumilivu na kuacha vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi zake ili kuwabaini wale wote wanaohusika na mtandao wa mauaji ya wanawake pamoja na mtoto.
Bastola iliyotumika katika shambulizi hilo. 

Mulongo aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na wanahabari wa vyombo mbalimbali ofisini kwake juu ya ujumbe uliosambazwa kwenye simu mbalimbali kupitia mtandao wa Whatsapp kuhusu kujitokeza kwa wanawake/wasichana  leo  kwa Mkuu huyo wa Mkoa  ili kujua hatma yao.
Akizungumzia suala hilo  Mulongo alitoa rai kwa akinamama wote pamoja na wasichana kuwa watulivu na kusaidia vyombo vya ulinzi na usalama kuwafichua wale wote wanaofanya mambo hayo.

Awali juzi watu  saba walikamatwa jijini Arusha  kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya unyang’anyi wa kutumia silaha kwa wanawake  pamoja na kusababisha  kifo cha mtoto, Christen  Nickos mwenye umri wa miaka mitatu na nusu  mkazi wa Olasiti jijini  hapa.

Kamanda wa Polisi Liberatus Sabas alisema watu wawili kati ya saba ambao ni Japhet  Lomnyaki (25) mkazi wa Sakina na Nehemia Kweka (34) mkazi wa Ngaramtoni walifikishwa mahakamani juzi.

Huku Adam Mussa (30) mkazi wa Majengo, Tito Loomoni (25) mkazi wa Shamsi, Joseph Loomoni (29) mkazi wa Shamsi, Abdallah Maglan (202) mkazi wa Oldadai na Emmanuel Maglan (23)  mkazi wa Oldadai wakiwa wanaendelea kuhojiwa na polisi.

Yanga na Mchezaji Okwi Hapatoshi..Hivi Huyu Mchezaji ana Matatizo Gani ?

$
0
0
Klabu ya Young Africans imemshitaki mchezaji Emmanuel Okwi kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuwasilisha nakala kwa shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) na shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa kuingia mkataba na timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga mitaa ya Twiga/Jangwani, mwenyekiti wa Yanga Bw Yusuf Manji amesema wameshangazwa na kitendo hicho kilichofanywa na viongozi wa Simba , wakala wake na mchezaji mwenyewe.
"Emmanuel Okwi awali tulishapeleka malalamiko TFF na kuwapa nakala CAF na FIFA juu ya kufanya mazungumzo na timu ya Wadi Degla FC ya nchini Misri na kufikia klabu hiyo kutuma ofa ya kutaka kumnunua bila kuwasiliana na uongozi wetu" alisema Yusuf.
Ikiwa hilo tunasubiria majibu kutoka TFF jana mchezaji huyo amesaini mkataba mwingine, hii inaonyesha ni jinsi gani mchezaji huyu kuna watu walikua wanamrubuni,kwa kusaini mkataba mwingine kitu ambacho amekiuka sheria za FIFA za usajili.
Baada ya kuona jana amesaini mkataba na Simba, Yanga tulichokifanya leo ni kuandika barua nyingine TFF juu ya suala hilo na kuomba kulipwa fidia ya US Dollar 500,000 (sawa na TZS 800,000,000/=) kutoka kwa klabu ya Simba, wakala wake na mchezaji mwenyewe aliongeza "Manji"
Aidha uongozi wa Yanga umeiomba TFF kuwa imelipatia ufumbuzi suala hilo ndani ya siku saba, na kama siku saba zikikpita basi uongozi wa Yanga utakwenda moja kwa moja FIFA na ikishindakana mahakama ya soka CAS.
Lengo sio kuikomoa timu ya Simba, bali tunachotaka ni sheria ifuatwe, Okwi alikua ameitumikia klabu ya Ynaga kwa kipindi cha miezi sita tu, na kuwa amebakiza mkataba wa miaka miwili mpaka msimu mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.
Mchezaji anayekutwa na kosa la kusaini sehem mbili adhabu yake ni kufungiwa kucheza soka kuanzia mwaka mmoja na kuendelea huku klabu husika ikifungiwa kusajili kuanzia miaka mwili na kuendela na kushushwa daraja au adhabu zote kwa pamoja.

Sababu Inayosemekana ya Babu Tale kumsimamia Shilole kikazi kwa Sasa ni Hii.

$
0
0
Manager wa Tip Top Connection na Diamond Platnumz Babu Tale inasemekana anamsimamia kwa sasa Shilole kama msanii wake kwa kile ambacho kimeelezwa na Soudy Brown kuwa deni alilokua anadaiwa Shilole.
Deni ambalo linasemwa kuwa Babu Tale alilipa ni la gari ambalo alikua akidaiwa Shilole hivyo wakakubaliana kuwa watakua wakikatana kwenye show tofauti mpaka deni hilo litakapoisha.
Soudy Brown kaongea na Shilole ambaye kasema ‘Mbona mimi sijui hayo mambo,sio kweli huo uwongo watu waongo sio kweli,gari ni langu na nina kila kitu changu watu wana donge kuona mimi Shilole naendesha Toyota Harrier Lexus nilinunua Milion 24′
‘Babu Tale ni mtu anayenisaidia kwenye kazi zangu na namheshimu kama kaka yangu nimeanza nae kazi mwaka huu na sina mkataba nae’

Pochi Yamsitiri Kajala Masanja Kukaa Nusu Utupu

$
0
0
Msanii wa filamu, Kajala Masanja, hivi karibuni alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu baada ya kukaa kwenye kiti na kuachia sehemu zake nyeti kiasi cha kuwatoa udenda baadhi ya wanaume.

Tukio hilo lilijiri mkoani Tanga wakati msanii huyo alipokwenda kwenye Tamasha la Fiesta, alipokaa kwenye kiti alijikuta akikaa vibaya mazingira yaliyomfanya ahangaike ili kuziba maeneo yake muhimu.
Kutokana na hali hiyo, alichukuwa pochi yake na kuiweka mapajani na kufanikiwa kujiziba, lakini licha kufanya hivyo alikosa raha.


Penzi la Mainda Lagombewa na Wanaume Wenye Uchu

$
0
0
Staa  wa  Filamu  za  Kibongo  aliyeamua  kumpokea  Yesu, Ruth Suka  ‘Mainda’  amesema  amekuwa  akipata  wakati  mgumu  kumjua  mwanaume  wa  kweli  ni  yupi  ambaye  anaweza  kumuoa  na  ndoa  yake  ikawa  na  raha  badala  ya  majuto  kama  ilivyo  kwa  baadhi  ya  wasanii  wenzake….

Mainda  alisema  hakuna  kipindi  kigumu  kama  kujua  yupi  ni  mwanaume  sahihi  wa  kumuoa  na  hili  limekuwa  likiutesa  moyo  wake  japo  sasa  ameamua  kumwachia Mungu  wake  ili  amsaidie  kwani  kwa  akili  zake  ameshindwa…

Hakuna  wakati  mgumu  kama  kipindi  cha  kumpata  mume  sahihi  kutoka  kwa  mungu, kwani  ukijichanganya  unaweza  kuchukua  mwanaume  ambaye  si  wako  na  kusababisha  kuwe  na  mafarakano  ndani  ya  ndoa  na  hili  ndio  linaumiza  kichwa  changu  kwani  mpaka  sasa  sijajua  ni  yupi  kati  ya  wengi  wanaohitaji  kunioa,” alisema  Mainda

Msanii  huyo  alisema  anajifunza  mambo  mengi  kupitia  ndoa  za  watu  waliomtangulia  kwani  nyingi  zimejaa  vurugu  likiwemo  suala  la  kusalitiana  na  kuambukizana  magonjwa  ya  zinaa  kama  vile  Ukimwi  na  menginenyo, hivyo  naye  hatapenda  awe  miongoni  mwa  ndoa  hizo

Ukweli Kuhusu Kifo cha Betty Ndejembi, Unyanyasaji Kwenye Mitandao ya Kijamii Yahusika

$
0
0

Ninaandika makala hii nikitambua bayana kuwa itamuudhi kila mtu anayeingia mtandaoni kwa minajili ya kuwanyanyasa watu wengine. Lakini siku zote ninaamini katika busara hii: kuuchukia ukweli hakuufanyi kuwa uongo. Ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Ukweli hauwezi kuwa uongo, na kadhalika uongo hauwezi kuwa ukweli. Kamwe asilani.

Wakati tunaomboleza kifo cha ndugu yetu Betty Ndejembi hatuwezi kukwepa ukweli kwamba siku chache kabla ya kifo chake binti huyo alinynyaswa mno kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Japo hadi muda huu hatuwezi kuhusisha moja kwa moja uhusiano kati ya unyanyasaji huo na kifo cha binti huyo, ukweli tu kwamba mtu akinyanyaswa masaa kadhaa kabla ya kifo chake, waweza kujenga picha flani.

Naomba ieleweke kuwa simlaumu mtu kwa sababu sina mamlaka ya kufanya hivyo bali dhima ya makala hii ni rambirambi zangu na kuzungumzia tatizo la unyanyasaji mtandaoni, sambamba na suala zima la unafiki kila kinapojiri kifo hususan cha mtu maarufu.

Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni. Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi, wambeya, wanafiki, wanaharamu na kila aina ya binaadamu wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza. Kwa Twitter, matusi imekuwa ni njia ya mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu wenye 'umaarufu' huko Twitter, na ukidadisi chanzo cha 'umaarufu' huo, utaambiwa 'ah huyu ana matusi si mchezo!'

Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha unyanyasaji huo. Marehemu aliitwa majina kadhaa ya kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti. Kuna waliomwita Di Maria na wanajifahamu. Japo sijui chanzo cha 'ugomvi na aliogombana nao' (na ndio maana sikujihusisha nao kwani haukunihusu), kuna wanafiki wengi tu waliokuwa katika nafasi nzuri ya kuzima moto huo hasa kwa vile baadhi yao walikuwa wakizifahamu pande zote mbili za 'ugomvi' husika.


La kukera zaidi ambalo ni wazi litajichomoza wakati wa maombolezo haya ni unafiki: baadhi ya watu walewale waliodiriki kumwandama marehemu wakati wa uhai wake watageuka kuwa wenye uchungu mkubwa baada ya kifo chake. Hii inanikumbusha suala ambalo nimeshawahi kulizungumzia mara kadhaa, katika hali ya utani japo wenye uweli, kwamba 'wakati mwafaka kabisa wa kutafuta vipaji vya uigizaji ni kwenye misiba: watu walewale waliokuwa wakikuchukia kwa nguvu zote watageuka wenye uchungu mkubwa kwa kifo chako.

Ukiangalia baadhi ya tweets za mwisho za marehemu ni wazi kuwa binti huyo alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa wanaomjali




Hata pasi uelewa wa taaluma ya saikolojia, tweets za aina hii zinaashiria tatizo, na laiti 'wenye upendo wa dhati' wangeingilia kati muda huo, huenda muda huu Betty asingekuwa marehemu. 


Na hizo tweets mbili ambazo ni miongoni mwa za mwisho kabisa za marehemu ni ushuhuda tosha wa jinsi alivyokuwa akisumbuliwa na wanyanyasaji dhidi yake mtandaoni. Ndio pengine kilichomuua ni maradhi ya kawaida ya kibinadamu lakini kila mwenye ubinadamu hatoshindwa kuhusisha unyanyasaji huu na hali mbaya ya afya aliyokuwa nayo hadi anafariki.

Kuna watakaolaumu kuwa ninatumia kifo cha binti huyo kwa 'maslahi binafsi.' Hapana, sina maslahi yoyote binafsi hasa ikizingatiwa kuwa sikuwa nikifahamiana na marehemu. Hakuna anani-follow na mie sikuwa nam-follow. Labda maslahi pekee niliyonayo ni upinzani wangu mkali dhidi ya unyanyasaji wa mtandaoni. Vyovyote ilivyo, marehemu alikuwa bullied kabla hajafariki na atakayetaka kukataa ukweli huo na akatae lakini utabaki kuwa ukweli usioweza kugeuka uongo. Na kwa hakika, kila aliyeshiriki kumnyanyasa binti huyo atakuwa anasutwa na nafsi yake, hata kama atatafuta hifadhi kwenye 'huu sio wakati wa kulaumiana' au 'we failed you Betty.' 

Mara nyingi nimekuwa nikiwalaumu watu wanaodai 'Instagram imekuwa mbaya' au Twitter imeharibika siku hizi' ambapo mara zote nimewakumbusha wahusika kuwa katika hii mitandao ya kijamii, ni muhimu kuwa makini katika nani wa kum-follow. Maana yangu ni kwamba ukim-follow mtu mwenye matusi, utashuhudia matusi katika anachoandika. Ukim-follow mtu wa busara, utashuhudia busara.

Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni kumeibuka kundi kubwa tu la watu wenye busara na elimu zao lakini wepesi wa kuvutiwa na vitu vya 'kipuuzi' - umbeya, matusi, majungu, na upuuzi mwingine, na hawasiti kushea na wanaowa-follow. Ni hivi, mtu akitweet tusi, kisha ukali-retweet, utambue kuwa unalikuza (amplify) tusi hilo. Na kimsingi, kwa kiasi kikubwa, tuna-RT vitu tunavyoviunga mkono. Uki-RT tusi maana yake unaliunga mkono. Na ni wazi mwenye kujiheshimu, na kuheshimu 'watu wa maana' wanaom-follow hawezi ku-RT upuuzi.

Tatizo kubwa sasa ni kwamba waweza kuamua kuwa-follow watu unaodhani wana busara au akili za kutosha lakini ukaishia kusoma vitu vya ajabu ajabu kwenye timeline yako kutokana na haya 'mahaba' ya ku-RT vitu vya kipuuzi. 

Binafsi, nadhani chanzo kikubwa cha mitandao ya kijamii kuwa 'sehemu za kukera, kuogopesha, kunyanyasana, nk' ni ile hali ya baadhi ya wenzetu kutokuwa na vitu muhimu vya kufanya katika maisha yao. Ni wazi kwamba ukiwa busy na maisha yako hutokuwa na muda wa kubughudhi wenzako. 

Kingine kinachopelekea social media kuwa 'dunia uwanja wa fujo' ni ugonjwa mkubwa unawasumbua baadhi ya wenzetu: kusaka sifa wasizostahili. Wanasema,. ashakum si matusi, 'lugha ya mpumbavu ni matusi,' na ndo maana baadhi ya wenzetu wasio na cha maana cha kuongea katika hadhara hukimbili matusi, unyanyasaji, maneno macha

Nitamke bayana kuwa siandiki makala hii nikitegemea kuungwa mkono na wahusika wa unyanyasaji mtandaoni. Na kwa hakika kuna uwezekano mkubwa wa makala hii kuzua 'kampeni ya chuki' dhidi yangu kutokana na makala hii. Tatizo kubwa la wenzetu hawa ni kutotaka kuambiwa kuwa 'Hapana, hili ni kosa. Na kosa ni kosa, haliwezi kuwa sahihi.' Lakini pamoja na uwezekano wa 'kuwashiwa moto' kutokana na makala hii, wito wangu kwa kila mwenye busara na akili ni kuliangalia tukio hili la kusikitisha kama 'wake up call.' Tujifunze, tujisahihishe. Tuache kusherehesha vitu vya kipuuzi mtandaoni.

Ifike mahala, ukishindwa kumkemea mtu mwenye tabia mbaya mtandaoni basi chukua option  rahisi ya kum-unfollow au ikibidi kum-block. Na ifike mahala kuwafahamisha watu wanaoendekeza utoto, majungu, umbeya, unyanyasaji na upuuzi mwingine kuwa kama hawana kitu cha maana cha kufany katika maisha yao basi isiwe sababu ya kuwasumbua wenzao wenye majukumu katika maisha yao.

Tukemee maovu badala ya kutarajia yataondoka yenyewe tu. Tuomboleze kifo cha Betty kwa kusema 'NO' kwa cyberbullies (wanyanyasaji wa mtandaoni). Tufike sehemu tuache kuwasujudia wahuni wanaodhani matusi ni sehemu ya wimbo wa taifa. Tuwakwepe waendekeza majungu, wanyanyasaji, wataka sifa za kipuuzi, na watu wasiofaa katik maisha yetu.


Wakati 'tunatafuta haki kwa marehemu Betty kutokana na unyama aliofanyiwa,' suala ambalo ni la kisheria, kilicho ndani ya uwezo wetu ni kukemea unyanyasaji mtandaoni (cyber bullying). Wakati hadi muda huu hatuwajui waliomfanyia marehemu unyama huo, takriban sote twawajua vema wanyanyasaji wa mtandaoni. Tuanze na hawa, kwani leo wamefanya kwa kwa marehemu Betty kesho itakuwa kwako.

Mwisho kabisa, ni muhimu kwetu sote kutambua kuwa tulitoka kwa udongo na tutarudi kwa udongo. Kifo ni hatma ya kila mmoja wetu.Betty ametutoka lakini nasi twaelekea huko. Visa, chuki, kunyanyasana, na vitu vingine visivyopendeza japo ni kama sehemu ya maisha yetu havipaswi kupewa nafasi katika maisha yetu haya ambayo hakuna mmoja wetu mwenye japo 'lue' ya lini yatafikia kikomo. TUPENDANE na TUHESHIMIANE.

Kwako marehemu Betty, hakuna tunaloweza kusema au kufanya sasa kurejesha uhai wako. Na hakuna neno sahihi la kuonyesha jinsi gani kifo chako kimewagusa wengi. Kubwa tunaloweza kufanya ni kukuombea kwa Mwenyezi Mungu akupatie pumziko la milele na mwanga wa milele akuangazie upumzike kwa amani. Amina.

Evarist Chahali

Model Maarufu wa Rasta za Darling Afariki Dunia Kwa Ajali ya Gari, Alimwaga Mchumba Anaenda Kwa Dada Kumbe Alikwenda kwa Mchepuko

$
0
0
Former Miss Mwanza Number Two Model na Mtangazaji wa tangazo la biashara la Nywele za Rasta za Kampuni ya Darling (Inasemekana ndio rasta maarufu zaidi Tanzania), harusi yake ilikuwa njiani kwenye matayrisho makubwa huku Mchumba wake akihaha huku na kule kutayarisha harusi yao, majuzi akamuaga anakwenda kumuona Dada yake na atalala huko huko, kesho yake yaani jana haya ndiyo yaliyotokea mbebez amefariki kwenye ajali akiwa na bwana mwingine kabisa ambaye naye amefariki so mchumba sasa haelewi na haamini kama ni kweli alichosikia na kukiona kwenye picha hizi hapa chini!!
RIP

Lady Jay Dee Adaiwa Kuopoa Ka Serengeti Boy , Picha Zanaswa

$
0
0
Na Musa Mateja
OHOOO! Siku chache baada ya ndoa ya Legendary wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ na mtangazaji mahiri nchini, Gardner Gabriel Habash ‘G Habash’ kudaiwa kuvunjika, gumzo limeibuka kufuatia kunaswa kwa picha za Jide na kijana mmoja (dogodogo) aliyetajwa kwa jina la Meddy Ahmed ‘Mtoto wa Vitoto’, Risasi Jumamosi linakupa kinaga ubaga

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Mtoto wa Vitoto huyo amekuwa na urafiki uliotukuka na Jide kwa muda mrefu kabla na baada ya mtafaruku wa ndoa ya Jide na mumewe Gardner hivyo kudaiwa kuwa ndiyo faraja ya mawazo ya mwanamuziki huyo hususan kipindi hiki cha changamoto ya mgogoro wa ndoa yake.

Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, ukaribu wa Jide na bwa’mdogo huyo ulipitiliza kiasi cha watu wa karibu na staa huyo kuanza kuhisi huenda wana uhusiano usiofaa.
“Ukaribu wao ulipitiliza hadi kila mtu wa karibu na Jide akautilia shaka, isitoshe kama unavyojua, Jide si mtu wa kuweka mambo yake hadharani. Mbaya zaidi Jide amekuwa akimposti dogo huyo kwenye mitandao yake ya kijamii,” kilisema chanzo hicho


ADAI NI MARAFIKI
Huku akiashiria sauti ya kutojiamini, dogo huyo alisema yeye na Jide ni marafiki wakubwa katika mazingira ya kawaida, pia  ni shabiki wake kama walivyo wengine ila ishu ya picha mtu yeyote anaweza kupiga.

Kuhusu kuendesha gari linalodaiwa ni la Jide, dogo alisema hajawahi ila ameshapiga nalo picha na mtu yeyote anaweza kufanya hivyo kama ana uhusiano mzuri na mwanamuziki huyo.
“Jide ni rafiki yangu na mimi ni shabiki wake wa kawaida. Kwa hiyo hilo siyo tatizo lakini pia kuhusu gari mimi sijawahi kuendesha gari la Jide lakini nimewahi kupiga nalo picha kweli kama shabiki mwingine na hakuna shida, ila siyo wapenzi, ni marafiki tu,” alisema Mtoto wa Vitoto.
GPL

Je Wewe ni Mbaya? Jua Dalili za Mdada Mwenye Shepu na Sura Mbaya

$
0
0

1.Ukiona umejipiga ‘selfie’ au hata picha yoyote ukaiweka kwenye facebook na
kutag watu mia ukapata ‘likes’ mbili tu ni dalili ya wazi kuwa we mbayaaa.

2.Ukiona wakaka wanapenda sana kampani yako lakini kila mara wanakuuliza ushauri juu ya kuwapata wadada wengine , ujue wewe ni mbaya, maana wanajiona kama vile wanaongea na mwanaume mwenzao

3.Ukiwa na wasichana wenzio halafu
mnataka kupiga picha ya pamoja ukona wanang’ang’ania wewe ndio uwapige
picha ni dalili ya wazi hawataki uwaharibie picha yao kwa sura yako mbaya.

4.Jina lako instagram na facebook pia ni dalili tosha kuwa na wewe unajijua ni mbaya, majina kama sexydiva, sweetylicious, cutebaby na kadhalika, ni nja ya kisaikolojia ya wabaya kutaka kuonekana wazuri.

5.Ukiona utafiti huu umekuudhi na una ulaani hiyo ndio dalili ya ukweli kuwa wewe mbayaaaaa

Manji: Tutapigania haki ya kusaka chetu kwa Okwi mpaka kieleweke

$
0
0
Siku moja baada ya Wekundu wa Msimbazi Simba kutangaza kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Uganda Emmanuel Arnold Okwi, hii leo uongozi wa Dar es salaam Young Africans ukiongozwa na mwenyekiti Yusuph Manji umeibuka na kukana kumpa barua mshambuliaji huyo ya kuvunja naye Mkataba na imesema mshambuliaji huyo Mganda, amewahadaa Simba SC.

Mwenyekiti huyo wa Dar es salaam Young Africans amesema tayari wameshaliandikia shirikisho la soka nchini TFF na kuomba ifanye mambo mawili, moja ni kumfungia Okwi kucheza soka na la pili ni kuifungia klabu ya Simba.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Dar es salaam Young Africans, Yusuph Manji amesema wametoa siku saba kwa TFF kufanya hivyo.

Manji amesema, iwapo TFF itashindwa kutekeleza hayo ndani ya siku hizo saba, wao watahamia Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ambako kama hawatafanikiwa pia, watahamia Mahama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS).

Manji amesema leo asubuhi wametuma malalamiko yao kimaandishi TFF na pia wanamdai Okwi fidia ya dola za Kimarekani 500,000 (Sh. Milioni 900) kutokana na kuvunja mkataba na wao.

“Tunataka Okwi afungiwe kucheza soka na Simba ifungiwe kutokana na kumsainisha Okwi. Tumeipa TFF siku saba ifanyie kazi malalamiko yetu,” amesema Manji.

Mwenyekiti huyo amesema kwamba, kabla ya jana katika malalamiko ya awali waliyotuma TFF, walitaka Okwi awalipe dola 200,000 (zaidi ya Sh. Milioni 340,000), lakini baada ya Simba kutangaza imemsajili jana, dau limepanda.

Manji amesema kwamba Yanga haina ubaya na Simba, bali watani wao hao wa jadi, wamefanya vibaya kumsainisha mchezaji huyo bila kuwasiliana nao.

“Simba SC walipaswa kuja kutuuliza kabla ya kumchukua Okwi, na wala sisi hatuna ugomvi na Simba, endapo watafungiwa au kushushwa daraja wasilie na Yussuf,”amesema.

Amesema Yanga haitatetereka kwa kuondoka kwa Okwi, shida ni kwamba taratibu hazikufuatwa. “Yanga imeachana na walimu na wachezaji mbalimbali kama Freddy Mbuna, Nsajigwa Shadrack kwa amani. Na nilisema mapema katika mkutano wa Juni, kwamba Okwi kama hatarudi, tutasajili wachezaji wengine wazuri, nimesajili Coutinho (Andrey) na Jaja (Geilson Santana),”amesema Manji.

Jana Okwi ametangaza kurejea Simba SC kwa mkataba huru wa muda, akida Yanga SC imempa barua ya kusitisha mkataba naye pamoja na kumshitaki TFF.

Okwi alisema ameamua kuomba kuichezea Simba SC kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC ili kulinda kipaji chake, kwa kuwa hata FIFA haitaki mchezaji akae bila kucheza.

“Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji.

“Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”alisema Poppe.

Okwi aliichezea Simba SC tangu mwaka 2009 kabla ya Januari mwaka jana kuuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 (Sh. Milioni 500) Etoile du Sahel ya Tunisia.

Etoile haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake kwa miezi mitatu.

Okwi akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake, ndipo akajiunga na SC Villa ya kwao.

Akiwa SC Villa ndipo aliposaini Yanga SC Desemba mwaka jana na pamoja na mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya Jangwani.

Okwi aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini kuelekea mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu uliopita akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo.

Okwi alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro wao umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu Machi, miezi minne tu baadaye tangu asajiliwe.

Vikao kadhaa vimekwishafanyika baina ya Okwi na Yanga SC tangu hapo kutafuta suluhu ya suala hilo na kikao cha mwisho jana baina ya mchezaji huyo na Manji matokeo yake ni nyota huyo kurejea Msimbazi.

Kuhusu deni lao la dola 300,000 kumuuza mchezaji huyo Etoile, Poppe amesema haihusiani kabisa na usajili wake huu wa sasa. “Ile kesi yetu ya madai ya fedha zetu kule FIFA ilikwishamalizika na vielelezo vyote vilipelekwa, bado kutolewa hukumu tu,” amesema.

Wasanii Kenya Wacharuka Waandamana Nusu Uchi Ili Nyimba zao Zipigwe Redioni

$
0
0
Siku hizi ishu ya kuvua nguo kuonyesha msisitizo au kulipigia kelele jambo flani imekua kawaida, yani wengi wameitumia hii njia kufikisha malalamiko yao na mfano mzuri ni hivi karibuni kwa Wanafunzi wa kike kwenye shule ya sekondari ya Wasichana Tabora Tanzania kubaki nusu uchi kwa nia ya kupigia kelele matatizo ya shule ikiwemo maji.
Nchi jirani ya Kenya matukio kama haya yamekua mengi pia lakini hawa ndio wamechukua headlines kwa kuwa Wanamuziki wa kwanza kuandamana kwa aina hii.
Ripota wa TZA Kenya Julius Kepkoich amesema Wasanii hawa waliandamana nje ya ofisi za Nation Media Nairobi wakiwa nusu uchi kulalamikia nyimbo zao kutochezwa na vyombo vya habari.
Wakiwa na mabango yao Wasanii hawa kutoka maeneo ya Vitongojini walisema wanaumizwa na kitendo cha nyimbo zao kutochezwa, wamekua wakitoa nyimbo mpya kila wakati lakini hazichezwi kwenye Radio wala TV badala yake zinazochezwa ni za wasanii walewale kila siku

Diva na Aunt Ezekiel Washikana Mashati kisa Ujauzito wa Aunt

$
0
0
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amemvaa prizenta wa Kipindi cha Ala za Roho cha Redio Clouds FM, Lovennes Malinzi ‘Diva’ kwa madai kwamba amemtangaza mitandaoni kuwa amepachikwa ujauzito na mume wa mtu ambaye ni densa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moses Peter ‘Moze Iyobo’, jambo ambalo ni uongo.

Akizungumza kwa masikitiko ya hali ya juu, Aunt alisema kuwa hakutegemea mtu kama Diva angetumia nafasi yake ya utangazaji kumchafua akimsingizia kuwa ni mjamzito, jambo ambalo limemsababishia matatizo kwenye ndoa yake na mumewe Sunday Demonte.

“Mwanamke kuwa mjamzito si jambo baya lakini kunichafua mbele ya jamii eti nina mimba ya Moze Iyobo, imeniuma sana.

“Hebu vuta picha wakwe, mawifi na mashemeji ambao tayari wameshasikia na kusoma kwenye ukurasa wa Diva, akisema mimi nina mimba ya yule mtoto, dah! Nimeumia sana, kwa kweli siwezi kuliacha lipite hivihivi.

“Huyo Diva lazima nitasimama naye mahakamani,” alisema Aunt.

Hivi karibuni, kwenye ukurasa wake wa Instagram, Diva aliandika: “Wakati sakata la mtoto mzuri Aunt Ezekiel ana mimba ya Moze Iyobo likipamba moto, mimba ambayo ni tangu Mwezi wa Ramadhan, sasa hesabuni miezi, hapa ni miezi miwili au mitatu.”

Uchumba wa Agness Masogange Waingia Mdudu

$
0
0
SIKU chache baada ya kupata uraia wa Afrika Kusini, uchumba wa Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ na mpenzi wake, Louis Dolnard umetibuliwa.

Hali hiyo ilijiri kutokana na madai kuwa kuna wanaume wamepeleka maneno ya kimbeya kwa mpenzi wake huyo yakiashiria kuwa mrembo huyo hajatulia.

Hata hivyo, Agnes amefunguka kuwa kamwe hawezi kuachana na mchumba wake huyo

“Wanaume wengine sijui wapoje, wanapeleka maneno ya kimbeya kwa mchumba wangu sijui wanataka nini? Kwa taarifa yao siachiki ng’o,” alisema Masogange.
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images