Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Suala la Upotevu wa Trilioni 1.5 Latua kwa Magufuli "Hakuna Trilioni 1.5 Iliyoibiwa na Serikali"

$
0
0
Suala la Upotevu wa Trilioni 1.5 Latua kwa Magufuli "Hakuna Trilioni 1.5 Iliyoibiwa na Serikali"
Rais John Magufuli amesema katika ripoti aliyopokea kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad haikuwa na upotevu wa fedha Tsh. Trilioni 1.5 kama inavyodaiwa.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akiwaapisha majaji Ikulu Dar es Salaam na kueleza watu wanatumia uhuru wao vibaya na kupotosha kitu kilicholeta taharuki.

Rais Magufuli amesema mara baada ya kusikia kuna fedha zilizopotea alipiga simu kwa CAG kuhoji;.

“Mbona kwenye ripoti yako uliyonisomea hapa Ikulu hukunieleza juu wizi wa Trilioni 1.5 kwa sababu ungenisomea hapo siku hiyo hiyo ningefukuza watu , kama nimefukuza wakurugenzi watatu siku hiyo kwa kupata hati chafu hawa na Trilioni 1.5 uliwaficha wapi nimejaribu kusoma ripoti yako nimeperuzi kila kona sioni mahali zimeandikwa zimepotea trilioni 1.5 na Profesa Assad akaniambia hakuna kitu kama hicho na Katibu Mkuu akasema hakuna trilioni 1.5 iliyoibiwa na serikali” amesema Rais Magufuli

“Kwa sababu ya uhuru wa mtu kuandika chochote kwenye mitandao kwani hata ndege walisema mbovu hivyo ni kawaida ya uhuru huu, bahati nzuri Controller and Auditor General yupo hapa eti Controller and Auditor General kwenye ripoti yako tumeibiwa Trilioni 1.5? Sema hapa hapa watu wajue”

Baada ya kauli hiyo ya Rais Magufuli CAG alisema hakuna kitu kama hicho, pia katibu Mkuu alisema hakuna jambo kama hilo na kusisitiza kuwa Hazina wapo vizuri na wapo salama.

Wenger Afanya Uamuzi Mgumu ... Atangaza Kujiuzulu Nafasi ya Ukocha

$
0
0
Wenger Afanya Uamuzi Mgumu ... Atangaza Kujiuzulu Nafasi ya Ukocha
Kocha wa club ya Arsenal ya England Arsene Wenger leo Ijumaa ya April 20 2018 ametangaza maamuzi ambayo yamewashitua wengi kutokana na kudumu na club ya Arsenal kwa miaka mingi.



Leo kocha Arsene Wenger baada ya kuifundisha club hiyo kwa miaka 22 toka alipojiunga nayo mwaka 1996 akitokea Nagoya Grampus ya Japan, ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi ya ukocha wa timu hiyo na kuwa ataondoka katika club hiyo baada ya msimu kumalizika.



Wenger ametangaza kufikia maamuzi hayo baada ya kukaa kwa kina na kujadiliana na viongozi wa Arsenal licha ya kuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Arsenal ili umalizike.

“Baada ya majadiliano ya kina na club, nahisi sasa ni wakati sahihi kwa mimi kuachia ngazi mwisho wa msimu huu”>>>> Wenger

Wanafunzi Walishwa Kinyesi na Mkojo Katika Hafla ya Kuwakaribisha Chuoni

$
0
0
Wanafunzi Walishwa Kinyesi na Mkojo Katika Hafla ya Kuwakaribisha Chuoni
Sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wapya katika chuo kikuu cha Msumbiji imezua hisia kali baada ya picha kusambazwa katika mitandao ya kijamii zikioinyesha wanafunzi hao wanavyolazimishwa kunywa na kuoga mikojo na kinyesi.

Kulingana na mwandishi wa BBC Jose tembe mjini Maputo, baadhi ya wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho cha kilimo, misitu na uhandisi cha Unizambeze katikati ya mkoa wa Zambezi pia walinyolewa.


''Waandalizi wa sherehe hiyo walitukata nywele zetu .Ilikuwa inatisha, ilikuwa haiwezi kuvumilika.Walitulazimisha kula mikojo na kinyesi . Tuliogeshwa na mikojo huku wakifuta pua zetu na vinyesi''.

Mwanafunzi mwengine Quiteria Jorge, alisema kuwa mwanafunzi ambaye alikuwa katika mwaka wa pili aliwatoa katika darasa lao ili kuwafanyia sherehe hiyo ya kukera.

''Walitukata nywele zetu kwa sababu wao wanahisi ni ndefu mno, lakini hatukuweza kufanya chochote, Nililia nikalia hadi nilipofika nyumbani''.

Kisa hicho hakikuwafurahisha wazazi wa wanafunzi hao ambao wamewataka wasimamizi wa chuo hicho kuwachukulia hatua hali wahusika.

Cardoso Miguel ambaye ni mkurugenzi wa elimu ya juu mkoani humo alisema kuwa uchunguzi unaendelea , ''kama tunavyoweza kuona picha katika mitandao ya kijamii ni wazi kwamba tabia hiyo haifai''

Kamati iliobuniwa itachunguza kiwango cha mateso hayo kwa kila mwanafunzi, huku wengine wakirudishwa nyumbani na wengine kufutiliwa mbali .

Sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya sio rasmi lakini hufanyika sana katika vyuo vikuu nchini humo zikiandaliwa na wanafunzi waliopo katika mwaka wa pili.

Rais Magufuli Achukizwa na Mitandao ya Kijamii " Uhuru Nchini Unasababisha Kila Kupost Anachojisikia"

$
0
0
Rais Magufuli Achukizwa na Mitandao ya Kijamii " Uhuru Nchini Unasababisha Kila Kupost Anachojisikia"
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kudai kuna ugonjwa umewaingia watanzania wa kupenda kuamini kila kitu kitakachokuwa kinaandikiwa na kuwekwa katika mitandao ya kijamii hata kama sio za kweli.


Dkt. Magufuli amesema hayo leo April 20, 2018 wakati akiwaapisha Majaji, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka, Ikulu jijini Dar es Salaam na kusema kuwa watu wanatumia uhuru wao vibaya na kupotosha watu kuhusu upotevu wa fedha hizo na kuleta taharuki katika nchi.

"Kuna ugonjwa tumeupata sisi watanzania wa kuamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ni cha kweli, sasa sijui huu ugonjwa umetoka wapi lakini ni kwasababu hii mitandao hatui-control sisi. Wako huko wenye mitandao yao ambao wenyewe wako busy na kutengeneza bussiness na hawajali na matatizo mtakayopata na ndio maana mkienda katika nchi kama China sina uhakika kama wana Google na WhatsApp kama tulizonazo sisi ndio maana kila mmoja anapojifikiria ana-post chochote", amesema Dkt. Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amesema uwepo wa uhuru nchini ndio unasababisha kila mtu ku-post kile anachojisikia katika mitandao ya jamii na kuwaaminisha watu.

Odinga Akutana na Mwai Kibaki kwa Mazungumzo

$
0
0
Odinga Akutana na Mwai Kibaki kwa Mazungumzo
Kiongozi wa chama cha upinzani cha ODM Raila Odinga Ijumaa amekutana na kufanya mazungumzo na rais mstaafu Mwai Kibaki ambaye alishirikiana naye kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Ajenda ya kikao chao cha dharura, ambacho kimekuja mwezi mmoja tangu Odinga ashikane mkono na Rais Uhuru Kenyatta, haikuwekwa wazi.

Odinga aliongozana na Paul Mwangi mshauri wake wa masuala ya kisheria na mwenyekiti mwenza wa timu iliyoandaa mpango wa kiongozi huyo kushikana mkono na Kenyatta.

“Raila anakwenda kukutana na rais mstaafu,” Mwangi aliliambia kwa simu gazeti la Nation bila kutoa maelezo zaidi.

Hata hivyo, gazeti hilo, lilifahamishwa kwamba Odinga alitarajiwa kumfahamisha rais mstaafu juu ya mpango huo mpya na Kenyatta.

“Ni kuhusu suala la kushikana mkono, mambo mengine yanapita hivyo anataka kumweleza Mzee Kibaki kilichojiri,” kilisema chanzo kingine.

Kikao hicho pia kinafanyika wiki moja tangu Odinga awe na mazungumzo kama hayo na mrithi wa Mzee Kibaki, rais mstaafu Daniel Moi, nyumbani kwake Kabarak katika Kaunti ya Nakuru.

Mapema asuhubi leo Ijumaa, Odinga alikuwa na kikao na gavana wa Nairobi, Mike Sonko katika ofisi za Capitol Hill.



DPP Afunga Rasmi Jalada la Kesi ya Mauaji ya Akwilina

$
0
0
DPP Afunga Rasmi Jalada la Kesi ya Mauaji ya Akwilina
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga amesema, jalada la kesi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini amelifunga rasmi.

Hayo ameyasema leo Aprili 20, 2018; Ikulu jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari huku akionya watu wanaovunjua amani kutofumbiwa macho wakiwamo waandishi wa habari.

Amesema jeshi la polisi linapotumia nguvu kuzuia maandamano, haliwezi kushtakiwa au hata kukitokea vurugu na kusababisha mauaji huwezi kulishtaki jeshi.

”Katika maandamano yale ya watu zaidi ya 200, huwezi kubaini nani amehusika na kumpiga risasi Akwilina na mwili wake haukutolewa risasi yoyote.”

Alipoulizwa kuhusu askari waliokamatwa baada ya kutokea kwa tukio hilo, Biswalo amesema, “kama jalada nimelifunga, kwa hiyo askari wale nao wameachiwa huru hawana hatia.”

Mkurugenzi huyo amesema moja ya jukumu lake ni kuhakikisha amani inakuwapo,”na niseme tu kuwa, mimi sina chama cha siasa, si mwanasiasa, kwa hiyo sitamvumilia mtu awe mkubwa wala mdogo, nitamshughulikia.”

“Na wanaosema wataandamana, waambieni wasifanye hivyo kwani wakiandamana watakwenda kuwasilimulia familia yake,” amesisitiza Biswalo

Pia, amevionya vyombo vya habari ambavyo vinavyoweza kuchangia uvunjifu wa amani, hatua zitachukuliwa hivyo kuvitaka kuwa makini na kutimiza wajibu wao kwa kufuata misingi ya taaluma yao.

Kilichotokea Kwenye Sherehe ya Ali Kiba Acha tu!

$
0
0

Kilichotokea Kwenye Sherehe ya Ali Kiba Acha tu!
KIMASOMASO mwanangu usimwone, ni wimbo ambao Ali Kiba alimwimba mkewe, Amina Khalef mara tu baada ya kumkumbatia wakati wa sherehe yao iliyofanyika jana Alhamisi kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee mjini Mombasa.

Kiba ambaye alivalia nguo aina ya Joho na kilemba cheupe alimwimbia mrembo wake huyo ambaye

usiku huo alikuwa kama malaika kutokana na namna alivyopendeza na gauni lake refu lililokuwa na rangi ya krimu na limejimwaga kama manyoya ya ndege Tausi.

Baada ya hapo, alianza kucheza naye muziki laini aina ya bluzi taratibu na nderemo na vifijo vikasikika watu wakishangilia si unajua kelele za akina mama tena wanapokuwa na yao na mambo yakaendelea.

Ikafika wakati wa kumtafuta baba unajua ilikuwaje, si akatajwa Gavana Hassan Joho 'Sultan' ambaye aliwasili ukumbini hapo mapema.

Katika sherehe hizo, Kiba aliingia ukumbini hapo na ndugu yake, Abdu Kiba aliyekuwa amevalia pia nguo aina ya joho pamoja na rafiki yake Ommy Dimpoz wote ni wasanii  wa Bongo Freva lakini yeye alipiga suti kali ya rangi nyekundu na nyeusi.

Witness Awatolea Povu Wanawake wa Bongo Mmezidi Kufeki ndio maana Wasanii Wakubwa Wanaenda Kuoa Nje ya Bongo"

$
0
0
Witness Awatolea Povu Wanawake wa Bongo Mmezidi Kufeki ndio maana  Wasanii Wakubwa Wanaenda Kuoa Nje ya Bongo"
Kwa sasa wasanii wakubwa Bongo wanapooa au wanapotaka kuoa lazima suala la kuoa mrembo kutoka nje ya nchi lichukue headlines zake.

Sasa msanii wa muziki Bongo, Witness a.k.a Kibonge Mwepesi amefunguka sababu za wasanii maarufu kuanzisha tread ya kuoa warembo kutoka nje ya Bongo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Witness ameandika;

Hivi ni nani aliwaroga wanawake wa kibongo? Wamekazana kweli witnesz hununui wigi la gharama, sijui hushonei,wanja wako siyo wa kisasa, witness haupo kama wasanii wenzio walivyo weeell (am unique thats why silinganishwi na yeyote yule) Witness haufanyi make up za gharama, haupaki lipstick za gharama etc halafu watu wakienda kuoa #KENYA mnalalamika kwa ufeki wenu.

Seriously kwa kweli bongo tunaongoza kwa fake bi***es, fake hair, fake nails, fake eye lashes, fake Chinese asses yaani its too much these bitches are even fake in bed why would you expect a real husband when everything else you own is fake? You gonna get fake boyfriends,fake husbands who are going to marry other ladies who arent fake since you attracted more fakeness in your life, indeed fake things are what your going to get!.

Makaka wanalalamika mnapenda vitu vya gharama sana, #shameonyou na kazi zenyewe hamfanyi kazi kuwageuza wenzenu swapping machines, watu wanataka wanawake wa kujenga nao maisha,wenye akili,wachapakazi na kufanya nao vitu vikubwa vya kujenga familia na kuacha legacy, mwanamke anayeona what is peruvian hair? #douaaaa bora tusave mume wangu tununue private jet, a yatch tuwekeze somewhere but all you want is show off, nikasuke hiki insta nzima na shoga zangu watanikoma hahahhahaaahah it’s too late bi***es.

Utakumbuka February 24, 2018 msanii AY alifunga ndoa  na mpenzi wake wa muda mrefu Remy kutokea nchini Rwanda, na hapo jana Alikiba alimuoa mrembo kutoka nchini Kenya. Pia mara baada ya msanii Alikiba kutangaza angeoa nchini Kenya hapo awali, Dully Sykes naye alisema kuna uwezekano wa kufanya kitu kama hicho.

Chadema: Si Trilioni 1.5 tu Kuna Pesa Kibao Zimepigwa

$
0
0
Chadema: Si Trilioni 1.5 tu Kuna Pesa Kibao Zimepigwa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimefanya mkutano na waandishi wa habari na kuudai kwamba ukiachilia mbali kiwango za zaidi ya shilingi trilioni 1.5 ambazo zilidaiwa na Zitto Kabwe kwamba hazifahamiki zimekwenda wapi katika ripoti ya CAG, kuna kiwango kingine kikubwa cha fedha pia kimetumika hovyo.



Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Uenezi wa Chadema, John Mrema, leo Aprili 18, 2018 katika makao makuu ya Chama hicho, Kinondoni Dar, na kudai kuwa fedha nyingine zilizopotea ni za kwenye mashirika ya umma yakiwemo ya mifuko ya hifadhi za jamii, ununuzi wa ndege na Shirika la Ndege kwa ujumla. Amedai chama chao kitatoa ufafanuzi wa kifungu kwa kifungu kuhusu ripoti hiyo ya CAG.



“Baada ya sakata hili la trilioni 1.5, kuna wanasiasa hasa wa ccm wanataka kubadilisha mjadala huu na kuanza kusema eti Chadema kuna ufisadi,” alisema John Mrema.



Hata hivyo, Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema hakuna fedha taslimu kiasi cha shilingi trilioni 1.51 iliyopotea au kutumika kwa matumizi ambayo hayakuidhinishwa na Bunge.



Pia, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa katika ripoti ambayo alipokea kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad haikuonyesha upotevu wa fedha hizo na kueleza endapo kungebainika kitu kama hicho, basi aliyehusika angechukua hatua kali siku hiyo hiyo.

Diamond Umaarufu Umekulevya, Sasa Jitasmini Upya

$
0
0
KWA kila mtu anayemfahamu Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, msanii wa kizazi kipya ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akiipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa katika muziki, hawezi kuacha kushangazwa na kitendo cha msanii huyo kuposti video chafu, alichokifanya siku chache zilizopita.



Kwa ambao hawakupa­ta nafasi ya kuzitazama video hizo, kwa nyakati tofauti Diamond al­ionekana akifanya hadharani mambo ya kikubwa, yanayopaswa kufanywa chumbani, tena kwa kifi­cho, taa zikiwa zimezimwa, kibaya ni kwamba alikuwa pia akijire­kodi.Ya kwanza alionekana akiwa na mwanamke mwenye asili ya kigeni, ambayo walikuwa wakiyafanya hay­awezi kuandikika kwa lugha nyepesi, kwa kifupi ulikuwa ni uchafu ambao ni kinyume kabisa na mila za Kitanzania.



Hakuishia hapo, muda mfupi baadaye ikaonekana video nyingine akiwa na mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto, wakifanya mambo yasiyofaa kuonekana hadharani, huku staa huyo wa ngoma ya African Beauty aliyomshirikisha msanii wa kimataifa, Omarion akionekana kugida pombe kwa fujo. Ukichunguza vizuri, inaonesha video zote mbili zilipigwa katika chumba kimoja, tena katika muda ambao haukupishana sana.

SOMA PIA: Nafasi za ajira zilizotangazwa Leo

Unajaribu kujiuliza, lengo la Diamond kurekodi video hizo kisha baadaye kuziposti mitandaoni lilikuwa ni nini? Kutafuta kiki? Ina maana mpaka leo Diamond kwa levo alizofikia anaweza kuwa anatege­mea kiki kuendelea kubaki kwenye chati na kusahau kuna mamilioni ya vijana wanaomtazama kama ‘kioo’ chao? Alifanya kwa lengo la kumuumiza mzazi mwenzake, Zarina Hassan ‘Zari’ kwa lengo la kulipiza maumivu ya kuachwa? Unawezaje kumlipiza mwanamke aliyekuzalia watoto kwa utoto wa kiasi hiki?



Anataka kesho wanaye wakikua waje wajifunze nini kutoka kwa baba yao? Amesahau kwamba intaneti inao uwezo wa kuhifadhi mambo kwa miaka chungu mbovu kiasi kwamba hata wanaye wa­takuja kuona uchafu wa baba yao? Come on!

Namfahamu Diamond tangu akiwa anahangaika kutafuta njia ya kutokea katika gemu la Muziki wa Bongo Fleva na nilikuwa miongoni mwa waandishi wa mwanzomwanzo kuan­dika habari zake, Hemed Kisanda ambaye naye kwa kipindi hicho alikuwa mwandishi wa habari za burudani, anaweza kuwa shahidi mzuri wa hili.



Diamond wa kipindi hicho, siyo Diamond wa sasa, nakubali kwamba mafanikio hulevya lakini ulevi huu anaouonesha Dia­mond sasa ni ‘too much’, ni zaidi ya ulevi wa pombe haramu ya gongo. Mara kadhaa nakumbuka Diamond alikuwa akikatisha ‘intavyuu’ kwa lengo la kwen­da kuswali baada ya kusikia adhana kwa sababu huyu ni muumini wa dini ya Kiislam, ziko wapi nyakati zile? Uko wapi unyenyekevu ule?



Sikia ‘A boy from Tandale’, hakuna hali ambayo huwa ni ya kudumu katika maisha, kama ule msoto wa enzi hizo ukiwa Tandale, ukisaga lami kutafuta promo ya kazi zako za muziki haukuweza kuwa wa kudumu maishani mwako baadaye ukatoboa, hata huu umaarufu ulionao sasa, wa kuruka na ndege kila kukicha, leo upo Ujerumani, kesho Marekani ukifanya shoo kubwa na kula bata, siyo kitu cha kudumu.



Mambo yote yatakapopita, matendo yako, utu wako na yale uliyowafanyia wengine ndiyo vitu vitakavyosalia, Waingereza wanasema ‘karma will hunt you’. Haya unayoyafanya leo, ipo siku yatakurudia, machozi ya wanawake unaowadhalili­sha na kuwatumia kingono utakavyo, ipo siku yatakuru­dia na sijui kama utakuwa umejiandaa kukabiliana nayo, yanaweza yasikurudie wewe lakini yakaurudia uzao wako.



Matendo yako lazima yaendane na heshima unay­opewa na mashabiki wako na watu wote wanaokutakia mema, wakiwemo viongozi wa nchi yetu! Umesahau ni siku chache tu zilizopita Rais Magufuli alikupa heshima kubwa kwenye uzinduzi wa Bombadier? Ukijikweza sana mbele za watu, ipo siku utashushwa mbele za watu na kila mmoja atakudharau! Na huu mchezo uliouanza hivi karibuni wa ku­tunishiana misuli na serikali, hauwezi kukuacha salama.

Adios Amigo.



HASH POWER, +255 719 401 968

mu Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, msanii wa kizazi kipya ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akiipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa katika muziki, hawezi kuacha kushangazwa na kitendo cha msanii huyo kuposti video chafu, alichokifanya siku chache zilizopita.Kwa ambao hawakupa­ta nafasi ya kuzitazama video hizo, kwa nyakati tofauti Diamond al­ionekana akifanya hadharani mambo ya kikubwa, yanayopaswa kufanywa chumbani, tena kwa kifi­cho, taa zikiwa zimezimwa, kibaya ni kwamba alikuwa pia akijire­kodi.Ya kwanza alionekana akiwa na mwanamke mwenye asili ya kigeni, ambayo walikuwa wakiyafanya hay­awezi kuandikika kwa lugha nyepesi, kwa kifupi ulikuwa ni uchafu ambao ni kinyume kabisa na mila za Kitanzania.

Hakuishia hapo, muda mfupi baadaye ikaonekana video nyingine akiwa na mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto, wakifanya mambo yasiyofaa kuonekana hadharani, huku staa huyo wa ngoma ya African Beauty aliyomshirikisha msanii wa kimataifa, Omarion akionekana kugida pombe kwa fujo. Ukichunguza vizuri, inaonesha video zote mbili zilipigwa katika chumba kimoja, tena katika muda ambao haukupishana sana.

Unajaribu kujiuliza, lengo la Diamond kurekodi video hizo kisha baadaye kuziposti mitandaoni lilikuwa ni nini? Kutafuta kiki? Ina maana mpaka leo Diamond kwa levo alizofikia anaweza kuwa anatege­mea kiki kuendelea kubaki kwenye chati na kusahau kuna mamilioni ya vijana wanaomtazama kama ‘kioo’ chao? Alifanya kwa lengo la kumuumiza mzazi mwenzake, Zarina Hassan ‘Zari’ kwa lengo la kulipiza maumivu ya kuachwa? Unawezaje kumlipiza mwanamke aliyekuzalia watoto kwa utoto wa kiasi hiki?

Anataka kesho wanaye wakikua waje wajifunze nini kutoka kwa baba yao? Amesahau kwamba intaneti inao uwezo wa kuhifadhi mambo kwa miaka chungu mbovu kiasi kwamba hata wanaye wa­takuja kuona uchafu wa baba yao? Come on!

Namfahamu Diamond tangu akiwa anahangaika kutafuta njia ya kutokea katika gemu la Muziki wa Bongo Fleva na nilikuwa miongoni mwa waandishi wa mwanzomwanzo kuan­dika habari zake, Hemed Kisanda ambaye naye kwa kipindi hicho alikuwa mwandishi wa habari za burudani, anaweza kuwa shahidi mzuri wa hili.

Diamond wa kipindi hicho, siyo Diamond wa sasa, nakubali kwamba mafanikio hulevya lakini ulevi huu anaouonesha Dia­mond sasa ni ‘too much’, ni zaidi ya ulevi wa pombe haramu ya gongo. Mara kadhaa nakumbuka Diamond alikuwa akikatisha ‘intavyuu’ kwa lengo la kwen­da kuswali baada ya kusikia adhana kwa sababu huyu ni muumini wa dini ya Kiislam, ziko wapi nyakati zile? Uko wapi unyenyekevu ule?

Sikia ‘A boy from Tandale’, hakuna hali ambayo huwa ni ya kudumu katika maisha, kama ule msoto wa enzi hizo ukiwa Tandale, ukisaga lami kutafuta promo ya kazi zako za muziki haukuweza kuwa wa kudumu maishani mwako baadaye ukatoboa, hata huu umaarufu ulionao sasa, wa kuruka na ndege kila kukicha, leo upo Ujerumani, kesho Marekani ukifanya shoo kubwa na kula bata, siyo kitu cha kudumu.

Mambo yote yatakapopita, matendo yako, utu wako na yale uliyowafanyia wengine ndiyo vitu vitakavyosalia, Waingereza wanasema ‘karma will hunt you’. Haya unayoyafanya leo, ipo siku yatakurudia, machozi ya wanawake unaowadhalili­sha na kuwatumia kingono utakavyo, ipo siku yatakuru­dia na sijui kama utakuwa umejiandaa kukabiliana nayo, yanaweza yasikurudie wewe lakini yakaurudia uzao wako.

Matendo yako lazima yaendane na heshima unay­opewa na mashabiki wako na watu wote wanaokutakia mema, wakiwemo viongozi wa nchi yetu! Umesahau ni siku chache tu zilizopita Rais Magufuli alikupa heshima kubwa kwenye uzinduzi wa Bombadier? Ukijikweza sana mbele za watu, ipo siku utashushwa mbele za watu na kila mmoja atakudharau! Na huu mchezo uliouanza hivi karibuni wa ku­tunishiana misuli na serikali, hauwezi kukuacha salama.

SOMA PIA: Job Opportunities at Precision Air Services

Adios Amigo.



HASH POWER, +255 719 401 968

Kauli Rasmi Ya Serikali Kuhusu Hoja Ya Kutoonekana Kwenye Matumizi Ya Serikali Shilingi Trilioni 1.51

$
0
0
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
KAULI YA SERIKALI KUHUSU HOJA YA KUTOONEKANA KWENYE MATUMIZI YA SERIKALI SHILINGI TRILIONI 1.51


UTANGULIZI

1.   Mheshimiwa Spikakwa mujibu wa Kanuni ya 49 ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari 2016, naomba kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Kauli ya Serikali juu ya madai ya kutoonekana kwa matumizi ya shilingi trilioni 1.51 kwenye matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

2.   Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2012/13 hadi 2016/17, Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango ilikuwa kwenye kipindi cha mpito cha miaka mitano ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kuandaa hesabu za Serikali kwa kutumia mfumo wa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (International Public-Sector Accounting Standards - IPSAS Accrual). Katika kipindi hicho, Serikali iliendelea kukusanya taarifa mbalimbali kwa kutumia mfumo huu ili kutuwezesha kutambua kikamilifu hesabu za mali, madeni pamoja na mapato yanayotokana na kodi. IPSAS Accrual ni mfumo wa kiuhasibu ambapo mapato yanatambuliwa baada ya muamala husika kukamilika na sio wakati fedha taslimu inapopokelewa; na matumizi yanatambuliwa wakati muamala wa matumizi umekamilika na sio wakati fedha inalipwa. Mfumo huu ni mzuri na una faida nyingi ikiwa ni pamoja na miamala ya Mapato na Matumizi kutambuliwa wakati husika na siyo wakati wa fedha taslimu inapopokelewa au kulipwa.

3.   Mheshimiwa Spika, matokeo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa uandaaji wa hesabu kwa mfumo wa IPSAS Accrual umeiwezesha Serikali na taasisi zake kutoa taarifa za kina na zinazoonesha uwazi na uwajibikaji wa taasisi husika, hususan katika usimamizi wa mali na madeni ya taasisi. Kuongezeka kwa uwazi, kumewawezesha watumiaji wa hesabu kupata taarifa zinazowasaidia kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati.

4.   Mheshimiwa Spika, kutokana na matumizi ya mfumo huu wa viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika sekta ya umma, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu na Watanzania kwa ujumla kwamba hakuna fedha taslimu ya shilingi trilioni 1.51 iliyopotea au kutumika kwenye matumizi ambayo hayakuidhinishwa na Bunge. Hivyo basi, madai ya baadhi ya watu wasiolitakia mema Taifa letu na Serikali yetu ya Awamu ya Tano hayana msingi wowote wenye mantiki. Haya yanadhihirishwa na aya zifuatazo kwenye tamko hili la Serikali.

5.   Mheshimiwa Spikataarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeeleza jumla ya mapato yote ya Serikali kwa mwaka 2016/17, yalikuwa shilingi trilioni 25.3 ambapo fedha hizi zinajumuisha mapato ya kodi, mapato yasiyo ya kodi, mikopo ya ndani na nje pamoja na misaada na mikopo nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo.

6.   Mheshimiwa Spikanapenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba, kuanzia mwaka 2016/17, Mamlaka ya Mapato Tanzania ilianza rasmi kuyatambua mapato kwa mfumo wa Accrual. Hivyo basi, kati ya mapato haya ya shilingi trilioni 25.3, yalikuwemo pia mapato tarajiwa (receivables) kama mapato ya kodi yenye jumla ya shilingi bilioni 687.3 pamoja na mapato ya kodi yaliyokusanywa kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya jumla ya shilingi bilioni 203.92 (transfer to Zanzibar).

7.   Mheshimiwa Spikakatika uandishi wa taarifa ya ukaguzi, CAG alitumia taarifa za hesabu na nyaraka mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti (Budget Execution Report) ambapo hadi kufikia tarehe 30 Juni 2017, mapato yalikuwa jumla ya shilingi trilioni 25.3 na matumizi yalikuwa shilingi trilioni 23.79. Matumizi haya hayakujumuisha shilingi bilioni 697.85 zilizotumika kulipa dhamana na hati fungani za Serikali zilizoiva. Matumizi haya yalikuwa hayajafanyiwa uhamisho (re-allocation) wakati ukaguzi unakamilika. Hivyo basi, baada ya kufanya uhamisho jumla ya matumizi yote kwa kutumia Ridhaa za Matumizi (Exchequer issues) yalikuwa shilingi trilioni 24.4.


8.   Mheshimiwa Spika, kutokana na ufafanuzi huo, shilingi trilioni 1.51 zilizodaiwa kutoonekana kwenye matumizi ya Serikali zilitokana na mchanganuo ufuatao;

Maelezo
Shilingi Trilioni
Matumizi ya dhamana na hati fungani zilizoiva
0.6979
Mapato tarajiwa (Receivables)
         0.6873
Mapato ya kodi yaliyokusanywa kwa niaba ya Serikali ya Zanzibar
0.2039
Jumla
1.5891
Fedha iliyotolewa zaidi ya mapato (Bank Overdraft)
(0.0791)
Fedha zilizodaiwa kutoonekana kwenye matumizi
1.51
                                                                                       
9.   Mheshimiwa Spikahii inamaanisha kwamba, baada ya kupunguza mapato ya Zanzibar ya shilingi bilioni 203.92 na kupunguza mapato tarajiwa ya shilingi bilioni 687.3, mapato halisi kwa mwaka 2016/17 yalikuwa shilingi trilioni 24.41. Aidha, baada ya kujumlisha matumizi ya dhamana na hati fungani zilizoiva za kiasi cha shilingi bilioni 697.85kwenye matumizi ya shilingi trilioni 23.79 yaliyooneshwa katika Taarifa ya CAG, ridhaa za matumizi zilizotolewa zilikuwa shilingi trilioni 24.49 na kuleta ziada ya matumizi ya shilingi bilioni 79.07 ikilinganishwa na mapato. Kwa mchanganuo huu, ni dhahiri kwamba kwa mwaka 2016/2017 matumizi ya Serikali yalikuwa makubwa kuliko mapato kwa shilingi bilioni 79.09 ambazo ni Overdraft kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Utaratibu wa kutoa fedha zaidi ya mapato (Overdraft facility) uko kwa mujibu wa kifungu cha 34 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.

Hitimisho

10.              Mheshimiwa SpikaSerikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imepata mafanikio makubwa katika uandaaji wa Hesabu za Serikali kwa kutumia mfumo huo wa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS Accrual). Itakumbukwa kwamba, katika Afrika, Tanzania ndio nchi pekee iliyofanikiwa kwa kiwango kikubwa kuandaa hesabu kwa kuzingatia matakwa ya IPSAS na kufanikisha kuandaa hesabu za Majumuisho kwa kuzingatia mfumo huo.

11.               Mheshimiwa Spikakutokana na maelezo haya ya Serikali, napenda kulitaarifa Bunge lako Tukufu na wananchi kwa ujumla kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ipo makini na haiwezi kuruhusu upotevu wa aina yoyote wa fedha za umma.  Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuona kwamba, kila mapato yanayokusanywa yanatumika ipasavyo na kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania.

12.              Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii, na naomba kuwasilisha.

Wachina Kushusha Bei ya Simu Nchini...Ni Baada ya Kuahidi Kuanzisha Kiwanda Hapahapa Nchini

$
0
0
Bei za simu za kisasa nchini zinatarajia kushuka baada ya Tanzania na China kuingia makubaliano ya ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza simu za mkononi hapa nchini.

Mbali na ujenzi wa kiwanda hicho, pia China itajenga kituo cha kutengeneza program za mawasiliano kwa ajili ya soko la Afrika na Mashariki ya Kati.

Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki alitoa taarifa hiyo jana kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Tweeter ya Ubalozi wa Tanzania nchini humo; ambayo ilithibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga.

SOMA PIA: Job Opportunities at JKT Tanzania

Aliitaja kampuni itakayotengeneza simu janja (smartphones) kuwa ni Shenzen-Qingchuan Technology (SQTL).

Licha ya kutokutaja lini uwekezaji huo utaanza na sehemu utakakofanyika, Balozi Kairuki alieleza kuwa ujio wa kiwanda hicho utafanya bei ya simu nchini, hususani simu janja kuwa nafuu.

"Kampuni hiyo imepanga kuwekeza nchini Tanzania kwa kujenga mtambo wa kutengeneza simu za mkononi pamoja na kituo cha kutengeneza simu za kisasa za mawasiliano kwa ajili ya soko la Afrika na Mashariki ya Kati," alisema balozi Kairuki.

Balozi Kairuki alisema kampuni hiyo ilieleza kuwa itazalisha simu zenye ubora na viwango vya soko la kimataifa.

Alieleza kuwa Kampuni hiyo pia imepanga kuajiri vijana 100 watakaopelekwa nchini China katika mji wa Shezen kupata mafunzo kwa muda wa miezi sita.

Breaking News: Mrembo Agness Masogange Amefariki Dunia

$
0
0

Video queen wa muda mrefu Agness Gerald  maarufu kama Masogange amefariki Dunia leo katika Hospitali ya Mama ngoma Mwenge,
CMG inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

Okwi, Manura Kukosekana Mechi ya Yanga?

$
0
0
Okwi, Manura Kukosekana Mechi ya Yanga?
Benchi la ufundi la klabu ya Simba kesho litaingia kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Lupili FC likiwa na tahadhari kubwa kwa wachezaji wake wawili, mshambuliaji Emmanuel Okwi na kipa Aishi Manula kutoka na nyota hao kuwa na kadi mbili za njano.


Wawili hao tayari wameshaoneshwa kadi mbili za njano katika michezo miwili iliyopita na endapo wataoneshwa kadi nyingine ya njano katika mchezo wa kesho moja kwa moja watakuwa wamekosa mchezo ujao ambao ni dhidi ya Yanga April 29.

Benchi la ufundi la Simba huenda likachukua maamuzi magumu kuepusha nyota hao kupata kadi ambapo golini anaweza kuanza golikipa namba mbili Said Mohammed ambaye hajadaka mchezo hata mmoja msimu huu.



Kwa upande wa Okwi, makocha Pierre Lechantre na Masoud Djuma wanaweza kuamua kumwacha nje Okwi ambaye hana rekodi nzuri kwenye viwanja vya mikoani akiwa amefunga mabao matatu tu kati ya 19 ambayo amefunga msimu huu.

Simba kwasasa inaongoza ligi ikiwa na alama 58 kwenye michezo 24 ikifuatiwa na Yanga yenye alama 47 kwenye michezo 22. Lipuli FC ipo katika nafasi ya 8 ikiwa na alama 31 baada ya michezo 25.

Alikiba, AY na Daimond Waziunganisha Tanzania na Kenya, Rwanda Pamoja na Uganda

$
0
0

Alikiba, AY na Daimond Waziunganisha Tanzania na  Kenya, Rwanda Pamoja na Uganda
Siku moja baada ya msanii Ali Kiba kufunga ndoa na Amina Khalef, raia kutoka nchini Kenya, sasa atakuwa msanii wa tatu kuunganisha familia katika nchi zinaoziunganisha Afrika Mashariki.

Jumuiya ya Afrika Mashariki inaunganishwa na nchi sita ambazo ni Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudani Kusini, Burundi na Kenya.

Awali aliyeanza kuunganisha undugu ni msanii Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz ambaye alikuwa na mahusiano na mwanama raia wa Uganda , Zarina Hassan ‘Zari’ na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili, Tiffah na Nillan.

Japokuwa kwa sasa Zari na Diamond hawapo pamoja, lakini kitendo cha kuzaa watoto kinawaunganisha kama familia.

Baadaye msanii wa siku nyingi wa Bongo Fleva, Ambwene Yessayah 'AY ' alifunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Remy ambaye ni raia wa nchini Rwanda.

Wawili hao waalianza kufunga ndoa ya kimila Feb 11 mwaka huu na kufanya sherehe nyingine nchini Tanzania, Februari 24 katika Hoteli ya Golden Tulip na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Lady Jaydee, Mwana FA, Salama Jabir, Profesa Jay (Joseph Haule-Mbunge wa Mikumi), Fid Q na wengineo wengi.

Kama vile haitoshi jana Kiba naye alifuata nyayo za Diamond na AY, baada ya kufunga ndoa na Amina Khalef mjini Mombasa kutokana na mwanamke huyo kuwa raia wa Kenya.

Shughuli za harusi zilianza majira ya asubuhi kwa Kiba kufungishwa ndoa msikitini majira ya asubuhi na jioni kufuatiwa na sherehe kubwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo nchini humo.

Diamond ampongeza Kiba

Hata hivyo,  jana katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram, Diamond alimpongeza Kiba kwa hatua yake hiyo kwa kuandika “Wadau nimeambiwa King Kiba kaoa leo...mfikishieni Salam zangu za ndoa njema, na maisha yenye furaha, amani na baraka tele.”

Hii ni mara ya pili kwa Diamond kutaka kuonyesha hadharani kwamba hana bifu na msanii huyo kama watu ambavyo wamekuwa wakiwachukulia, ambapo mara ya kwanza ikiwa ni muda mfupi tangu kituo chao cha TV cha Wasafi kuanza kurusha matangazo walicheza na nyimbo za Kiba jambo ambalo lilizua gumzo mitandaoni.

Polisi Yaua Majambazi Wanne Mkoani Pwani

$
0
0
Polisi Yaua Majambazi Wanne Mkoani Pwani
Majambazi wanne wameuawa  na polisi asubuhi ya leo Ijumaa Aprili 20, wakati wakijaribu kupora Kisarawe mkoani Pwani.

Kabla ya kuuawa yalitokea majibizano ya risasi kati yao na askari Polisi.

Imedaiwa majambazi hao wametokea jijini Dar es Salaam na walikuwa wanatumia gari lenye namba za kibalozi hatua iliyosababisha askari wa usalama barabarani kutowahisi chochote kwani gari hizo sio rahisi kusimamishwa ovyo.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, ambaye pia ni Mwenyekiti Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Pwani, Evarist Ndikilo amethibitisha tukio hilo.

Yanga Kukwea Pipa kesho Kuwaguata Mbeya City

$
0
0
Yanga Kukwea Pipa kesho  Kuwaguata Mbeya City
Siku moja baada ya kuwasili nchini wakitokea Ethipia kwenye mchezo wa kombe la shirikisho la CAF dhidi ya Welayta Dicha,mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga, wanakwea ‘pipa’ kesho mchana kulekea jijini Mbeya tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya wenyeji Mbeya City uliopangwa kuchezwa jumapili kwenye uwanja wa Sokoine.

Kaimu kocha mkuu Noel Mwandilla amesema kuwa hali ya kikosi chake  si mbaya licha ya safari na mchezo mgumu  wa kombe la shirikisho na wako tayari kwa ajili ya kupambana kuhakikisha  timu inapata pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo wa ugenini.

Watu wote wanafahamu kazi ngumu tuliyifanya juzi kule Ethiopia,tuko sawa na tayari kwa mchezo wa jumapili, mpira wa miguu unatuongoza kuwa tayari kwa mapambano muda wowote, nia yetu ni kushinda na kupata poiti tatu muhimu ambazo zitatusongeza zaidi kwenye mbio za ubingwa, amesema Mwandilla.

Kwa upande wake daktari wa kikosi cha Yanga, kiungo Papy Kambamba hatakuwa sehemu ya mchezo huo wa jumapili, kupisha majeraha ya mguu wa kulia aliyopata kwenye mchezo  wa kombe la shirikisho dhidi ya Welayta Dicha,huku mshambuliaji Ibrahim Ajib akitarajia kurejea rasmi kikosi baada ya kupona Maralia.

Papy hatakuwepo, aliumia Ethiopia, tukiwa kule tulimpatia matibabu ya awali,kesho atakuwa hospital kwa vipimo zaidi, Ibrahim Ajib atarejea  kikosini kwa sababu amepona Maralia,kuhusu Andrew Vicent  hakuna shaka  juu yake yuko vizuri anaweza kucheza ila itategema na waalimu kama wataona inafaa, alisema Dr Bavu.

Yanga imefuzu hatua ya makundi baada ya kufanikiwa kuitoa Welayta Dicha kwa ushindi wa jumla wa magoli 2-1.

Mambo ni Hivi Zari Afunguka 'Siwezi Kudate Mtanzania Tena', Adai Mwanaye Sio wa Tandale

$
0
0
Mambo ni Hivi Zari Afunguka 'Siwezi Kudate Mtanzania Tena', Adai Mwanaye Sio wa Tandale
Mfanyabiashara maarufu na baby mama wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady ameibuka na kuapa kuwa hataweza kutembea na mwanaume wa Kitanzania tena.

Zari ameyasema hayo baada ya Kupitia kipindi Kigumu na Ex wake Diamond ambaye alichepuka sana kipindi cha Mahusiano yao ya miaka minne hadi kufikia hatua ya kuzaa nje.

Zari alimmwaga Diamond mapema mwaka huu siku ya wapendanao baada ya kuchoshwa na tabia zake za kupenda michepuko.

Lakini pia Zari ameibuka na kudai kuwa mtoto wake Tiffah sio wa Tandale hii iliyokea siku chache zilizopita wakati Zari na marafiki zake walipokuwa kwenye Instagram live.

Zari alifunguka na kusema mtoto wake Tiffah anashindwa kutofautisha kati ya R na L tabia ambayo ameirithi kutoka kwa Upande wa Baba yake kwani Watanzania wengi hawawezi kutofautisha R na L na wengi wao wanamuita Zali badala ya Zari.

Ndipo mmoja kati ya marafiki wa Zari alisema Tiffah ni wa Tandale Lakini mara moja Zari alikataa na kusema mwanaye sio wa Tandale.

Tandale ndipo Diamond na familia yake walipokulia na hajawahi hata mara moja kukataa asili yake na hata albamu yake inaitwa ‘A boy From Tandale’.

Baada ya Kusameheana, Romy Jons na Baraka Kutambulisha Ngoma ya Pamoja

$
0
0
Baada ya Kusameheana, Romy Jons na Baraka Kutambulisha Ngoma ya Pamoja
Ikiwa hawana muda mrefu tangu walipokuwa katika mgogoro baada ya Romy Jons kusemekana kuwa amemtongoza Najma ambae ni mpenzi wake na Baraka hivyo kuwa fanya wawili hao kuingia katika headlines kuwa wamgombana,

Lakini siku ya April 19 ,Romy Jons aliamua kuomba msamaha na kusema kuwa amekubali kosa lake na amaeona haina haja ya yeye na barak kuendelea kugombana wakati wanauwezo wa kukaa pamoja na kufanya kazi ili kutokemeza umaskini kwa vijana.

Leo tena katika ukurasa wake wa instagram, Romy Jons amendika caption iliwaacha mashabiki wakishangaa kidogo kuhusu uhusiano wao kwa sababu Romy anasema kuwa ili kuwaonyesha mashabiki kuwa hawana bifu tena wameamua kufanya ngoma yao ya pamoja lakini mashabiki wameanza ku-judge kuwa inawezekana wawili hawa walikuwa wametengeneza kiki ili kuupa wimbo huo umaarufu.

"KESHO IFIKAPO SAA KUMI NA MBILI JION PANAPO MAJALIWA NITAACHIA NGOMA YANGU YA KWANZA NILIYOMSHIRIKISHA BARAKA THE PRINCE ITAKAYO PATIKANA KATIKA ALBUM YANGU INAYOITWA CHANGED.NIMEONA NIANZE NA HII NILIYOMSHIRIKISHA BARAKA ILI KUWAONYESHA WATU KUWA TLISHAMALIZA TOFAUTI ZETU.TUSUBIRI ZAWADI YETU IFIKAPO HIYO KESHO SAA 12.ASANTENI SANA , IJUMAA KAREEM"

Kifo cha Agness Masogange...Mwanasheria Wake Afunguka Hali yake Kiafya Ilivyokuwa Wakati wa Kesi

$
0
0
Msanii anayepamba video za muziki (video queen), Agnes Gerald ‘Masogange’ amefariki dunia leo.

Taarifa hizo zimethibitishwa na mwanasheria wake, Reuben Simwanza

Simwanza amesema taarifa za kifo chake amezipata kupitia dada yake, saa chache zilizopita.

Kwa maelezo ya Simwanza, dada wa Masogange, Emma Gerald, ndiye aliyetoa taarifa hizo baada tu ya kutoka kumuona alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mwanasheria huyo ambaye amedai yeye si msemaji zaidi, kuhusu nini chanzo cha kifo chake, alidai mara ya mwisho waliwasiliana naye siku mbili zilizopita kwa ujumbe wa simu ya mkononi.

 “Unajua kuumwa kweli alikuwa anaumwa, kipindi cha kesi yake magonjwa ya hapa na pale ikiwamo presha, si unajua tena mambo ya kesi hayana mwenyewe, lakini baada ya kwisha tulikuwa tunataniana kwamba sasa nina imani utakuwa powa kwani kila kitu kipo sawa,”amesema Simwanza.

Hata hivyo amesema yupo njiani kuelekea hospitali kwa kuwa hakuweza kupata maelezo zaidi kutoka kwa dada yake huyo ambaye amemsikia akiwa analia tu.

Hivi karibuni, Masogange alihukumiwa kulipa faini ya Sh 1.5 milioni  na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin.

Alibainika kutumia dawa hizo kati ya Februari 7 na 14, 2017
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images