Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Familia 208 za watoto waliotelekezwa na baba zao, zaanza kupata huduma

$
0
0
Zaidi ya familia 208 za watoto waliotelekezwa na baba zao, zimepatanishwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Paul Makonda.

Hayo yamebainishwa jana Aprili 27 na Makonda wakati akitoa majumuisho ya zoezi la kuwasikiliza wanawake waliotelekezwa na wenza wao wakiwa na watoto.

Kadhalika Makonda, hakuacha kuwashukuru waandishi wa habari kwa kufanya kazi kubwa katika kuhabarisha umma kuhusu kampeni yake.

“Kwanza niwashukuru waandishi wa habari kwa kazi nzuri mliyofanya, lakini pia niwashukuru wote walionitukana kwa kuanzisha zoezi hili wakiwamo wabunge,"alisema.

Alisema zoezi hilo limefanikiwa kwani  familia 208 zimeanza kupata huduma kutoka kwa baba zao.

Kadhalika amesema, kati ya watu 17,000 waliofika ofisini kwake, 90 wamefanikiwa kupimwa uhalali wa baba kwa mtoto ( DNA) na watoto 2971 wakifanikiwa kupata  bima ya afya.

"Tumeunda tume ya watu 15 watakaofuatilia kwa kina matatizo ya kiutawala katika kushughulikia masuala  yanayohusu jamii kwani imeonekana kuna shida kubwa kwa watu wanaoshughulika na ustawi wa jamii," alisema.

Serikali: Haiwezekani Majuto Kuomba Sh 500,000

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema inaudhi kuona msanii wa filamu, Amri Athuman maarufu King Majuto anaomba msaada wa Sh 500,000 kwa ajili ya matibabu wakati kuna makampuni yalifaidika naye kwa kuingia mikataba aliyodai ya dhuluma.

Kutokana na hali hiyo, amesema serikali imechoka kusikia vilio vya wasanii wa filamu kudhulumiwa haki zao na sasa imeunda kamati maalumu ya wanasheria kukagua mikataba yote ya mashirika na makampuni waliyoingia wasanii akiwamo  King Majuto na marehemu Seteven Kanumba ‘Kanumba’.

Pia imeagiza wasanii wote ambao wanaona wameingia mikataba ya kipumbavu na makampuni au mashirika hayo wawasilishe taarifa zao kwa serikali.

Dk. Mwakyembe amesema hayo jana  Aprili 27, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge katika kuhitimisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo.

“Kwa kweli dhuluma kwa wasanii ilikuwapo kubwa sana kwa kutumia ‘middle men’ (watu wa kati), watu wenye fedha wamechezea sana Watanzania wetu. Hili limeanza kubadilika tumeanza kuwa- empower (kuwezesha) wasanii wetu kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wasitumie middle men.

“Kwa mfano vijana wetu wazuri kama kina Kanumba, amefariki kila mtu anajua ni milionea, hapana.. waliotajirika ni wengine. Leo hii mwanasanaa mzuri mzee majuto anaumwa, anaomba fedha, mimi nachanga kutoka mfuko kwangu,” alisema Dk. Mwakyembe.

Alisema licha ya kwamba nusu ya mabango ya biashara na matangazo ya biashara ni ya  Mzee Majuto inashangaza kuona anaomba fedha ya matibabu.

CCM yakomba safu nzima ya uongozi Chadema

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ediwn Sanda amesema kuwa safu ya uongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye jimbo hilo wamehamia CCM kutokana na kazi nzuri anazozifanya Rais Dkt. Magufuli

Ameyasema hayo leo April 27, 2018 alipopata nafasi ya kuwasalimu viongozi mbalimbali akiwemo Rais Dkt. Magufuli kwenye sherehe za ufunguzi wa barabara ya Kondoa, Babati yenye urefu wa kilomita 251

“Rais safu ya uongozi mzima ya CHADEMA imehamia CCM, Mwenyekiti wa Jimbo, Katibu wa Jimbo, na viongozi wengine kwa uchache wao, kwa kweli nashukuru sana ila tunakwenda kubomoa moja kwa moja dhana ya upinzani Kondoa kwani viongozi wao wote wamehamia CCM tayari kutokana na kazi ambazo unafanya,”amesema Sanda

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa upinzani wamekuwa wakihama kutoka katika vyama vyao vya siasa na kujiunga na chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile wanachodai kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Kim Jong-un Akubali Kuondoa Silaha za Nyukilia

$
0
0
Mkutano wa kihistoria baina ya Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in umeanza Ijumaa kaitka kijiji cha truce village huko Panmunjom.

Kim Jong-un alivuka eneo la mpakani lisilokuwa na harakati za kijeshi ambalo limeyagawanya mataifa hayo mawili kwa zaidi ya miaka 60.

Hatimaye viongozi hao kutoka upande wa utawala wa kikomunisti (kaskazini) na upande wa utawala wa kidemokrasia (kusini) walikaribiana kabla ya kutangaza azma yao ya kuondoa silaha za nyuklia na kuendeleza amani.

“Leo, Mwenyikiti Kim Jong Un na mimi tumethibitisha ile azma yetu ya kufikia hali ya kutokuwepo silaha za nyuklia katika eneo la rasi ya Korea katika hatua ya kuondosha kabisa silaha za nyuklia ikiwa ni lengo letu la pamoja,” amesema Rais Moon Jae katika sherehe za kutangaza makubaliano ambayo wameyaita tamko la Panmunjom.

Kiongozi wa Korea Kaskazini kwa upande wake amesema kuwa amekubaliana na Tangazo hilo la pamoja na mikataba iliyotangulia baina ya nchi hizo mbili bila ya kufafanua au kuthibitisha matokeo ya makubaliano hayo ya kuondosha vitisho vya programu ya silaha za nyuklia za nchi hiyo

“Tumeamua kufungua awamu hii ya kuboresha mahusiano na maendeleo kwa kutekeleza kikamilifu Tangazo la Kaskazini- Kusini na mikataba yote iliyotangulia ambayo ilikubalika.,” amesema Kim.

Bunge Lafunguka Kuhusu Taarifa za Cyprian Musiba Kufukuzwa Bungeni Jana

$
0
0

Bunge limesema, picha zinazosambaa mitandao zikidai Mkurugenzi wa CZI, Cyprian Musiba amefukuzwa bungeni si za kweli. Musiba amekidhi vigezo vya kusajiliwa kuripoti habari za Bunge na kwamba alikuwa akihamishwa kwenda jukwaa mahsusi ambalo Waandishi hukaa wawapo Bungeni.

Gigy Money “Huwezi Kumuona Mwanangu Hata Kwa Milioni 90”

$
0
0
Msanii wa bongofleva Gigy Money amethibitisha kupata mtoto wa kike ambaye amempa jina la Myra ambapo awali alimpatia jina la Candy lakini kasema kabadili hilo jina kwakuwa baadhi ya watu wenye majina ya Candy wamekuwa hawana sifa nzuri.

Gigy Money amethibitisha hilo baada ya kuzungumza na millardayo.com na Ayo Tv na kusema kuwa hawezi kuitoa sura ya mtoto wake mpaka arobaini ifike na mpaka sasa mwanae kashapata u-ambassodor lakini hawezi kuionesha sura ya mwanae kwa sasa..

Bonyeza PLAY hapa chini kusikiliza FULL STORY…

Ridhiwani Kikwete Afunguka Kuhusu Kifo cha Mdogo wa Mbunge John Heche Kilichosababishwa na Polisi

$
0
0

Ridhiwani Kikwete Afunguka Kuhusu Kifo cha Mdogo wa Mbunge John Heche Kilichosababishwa na Polisi

Regrann from @ridhiwani_kikwete - Kitendo kilichotokea sio tu kimesikitisha ukoo wa Bwana Heche lakini kwangu Binafsi. Jeshi letu limetengenezwa kulinda Watu na Mali zao sio kuumiza wasio na hatia. Ni imani yangu Serikali itasimamia haki kwa familia ya Heche. Poleni sana kwa Msiba.Mungu awape subira @HecheJohn

Kocha Mourinho Anajutia Kauli hii Aliyowahi Kumwambia Wenger

$
0
0
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger Jumapili ya April 29 2018 ataingia katika uwanja wa Old Trafford kwa mara ya mwisho akiwa kama kocha wa Arsenal kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu, imezoeleka mara nyingi Wenger akikaribia kucheza na timu inayofundishwa na Jose Mourinho huwa kuna kauli za vijembe zinatawala.



Leo April 27 kuelekea mchezo huo Jose Mourinho akiongea na waandishi wa habari ameongea kauli tofauti na kuonesha kusikitishwa kwake na kauli mbaya na kejeli alizowahi kumtolea kocha Arsene Wenger kipindi cha nyuma, Wenger alikuwa na upinzani mkubwa na Man United kipindi inafundishwa na Sir Alex Ferguson lakini mara nyingi yeye na Mourinho wameonekana kuwa upinzani zaidi timu zao zinapokutana.



Jose Mourinho aliwahi kutoa kauli mbalimbali kwa Wenger zinazoonesha kejeli kama ‘mtaalam wa kufeli’ lakini October 2014 waliwahi kuzozana uso kwa uso kiasi cha kusukumana kutokana na kupishana kauli alipoulizwa na waandishi kuhusu hilo Mourinho>>>“Ndio najutia kwa kauli mbovu nilizowahi kutoa kama ambavyo yeye alifanya”

Kutana na Mabingwa wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala Wakutatulie Tatizo lako Popote Ulipo

$
0
0

KUTANA NA MABINGWA HAWA WA TIBA ASILIA NA TIBA MBADALA WAKUTATULIE TATIZO LAKO POPOTE ULIPO AFRICA,ASIA, AMERICA, FALUME ZAKIARABU HUDUMA ZETU ZITAKUFIKIA..... Bi khajat ni mtaalamu wa mambo yamahusiano (MAPENZI) kama umeachwa namume, mpenzi, mchumba, mke, au hajatulia unataka kumtuliza mpenzi wako akupende asikusaliti asitoke nje ya ndoa.... Bi khajati atakurudishia mahusiano yako yaliyo vunjika nakuyafunga yasiteteleke tena... Bi khajati anauwezo wakukupandishia nyota zako hata kama huna bahati yakupendwa kusaminiwa, utaanza kupendwa nawatu wenye pesa matajiri nawatakujali nakukupenda nakutimiziwa ndoto zako.... MAALIMU JUMAA NIBINGWA WA TIBA ASILIA,,, acha kuusononesha moyo wako kw sababu ya ugumu wa maisha.... Jipatie dawa za ngekewa kwenye biashara yako, pete za bahati mvuto wa biashara.. Kupata kazi, ajira nk.... Kama unahisi nyota yako haiko sawa maalimu jumaa atakupandisha nyota yako itang'ala na itafanikisha mambo yako....

PIA TUNATOA UTAJIRI WA MAJINI KWA YEYOTE ANAEHITAJI, Kama unataka utajiri wa pete, au wamajini bila masharti wasiliana nasi kw simu hizo muda wowote popote ulipo ,usisite kupiga simu hata Kama unamambo yako binafsi shida binafsi, maradh, kesi, kazi, biashara, nk. Piga simu ushauli ni bure karibuni sna.... +255 678 857 642 na +255 754 661 565 ...

yote yanawekena inn shaa laaah......

Shilole Atoa Shart Zito la Kifo Chake "Sitaki Mniage"

$
0
0
Shilole Atoa Shart Zito la Kifo Chake "Sitaki Mniage"
MWANAMUZIKI maarufu, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ametoa sharti zito kuwa, siku akifa hatataka mwili wake ufanyiwe mbwembwe kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kama wanavyofanyiwa mastaa wakifariki na badala yake mambo yote yamalizike msikitini.

Akizungumza na Risasi Jumamosi ikiwa ni siku chache baada ya video queen, Agness Gerald ‘Masogange’ kufariki dunia kisha kuagwa viwanjani hapo, Shilole alisema yeye anatoa agizo kuwa, ikiwa ametokea amefariki dunia leo au kesho, kama siyo kuagwa nyumbani kwake Gongo la Mboto, basi aagwe msikitini.
“Mimi sitapenda kabisa taratibu za mazishi yangu zifanyike katika Viwanja vya Leaders, ni bora kama nyumba yangu itakuwa haijamalizika basi watu wakafanyie taratibu hizo msikitini kwa sababu mimi ni mtoto wa kiislam, siwezi kuagwa kwenye viwanja ambavyo watu wanakunywa na kuuza pombe,” alisema Shilole.

SOMA Pia: Job Opportunity at Brighter Monday Tanzania, Marketing Intern

Vyeti vya Vipimo vya Masogange Vyavuja Huu Hapa Ugonjwa Uliomuua

$
0
0
Vyeti vya Vipimo vya Masogange Vyavuja Huu Hapa Ugonjwa Uliomuua
WAKATI akitimiza siku tatu kaburini, kijijini kwao, Utengule-Usongwe, Mbalizi jijini Mbeya, vipimo vya afya ya aliyekuwa video queen na msanii wa sinema za Kibongo, Agness Gerald Waya almaarufu Masogange, vimevuja, Ijumaa limedokezwa.

Masogange alifariki dunia Aprili 20, mwaka huu katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar kwa kile kilichoelezwa na daktari kuwa alilazwa hospitalini hapo kwa siku nne akisumbuliwa na Nimonia na upungufu wa damu mwilini.

MAMBO MENGI YAIBUKA

Mara baada ya kuaga dunia, kuliibuka mambo mengi kwenye mitandao ya kijamii juu ya kifo chake huku magonjwa mbalimbali yakitajwa, lakini kwa waliomjua Masogange vizuri Masogange ndiyo wamemwaga ushahidi wa vipimo vya vyeti vyake vya Ugonjwa wa Ukimwi.


CHETI CHA KWANZA

Kwa mujibu wa vipimo hivyo ambavyo inaonekana alifanya mara mbili kwa nyakati na hospitali tofauti, cha kwanza kinaonesha kwamba, alifanya zoezi hilo, Septemba, 2016 kisha kuyaanika majibu yake kuwa alikuwa HIV-Negative, yaani hakuwa na Ukimwi.

Cheti hicho kilionesha kwamba, Masogange alifanya zoezi hilo la upimaji kwenye Hospitali ya TMJ-Mikocheni jijini Dar. Kwa mujibu wa watu hao wa karibu, Masogange alichukua uamuzi huo kufuatia kuwepo kwa maneno mengi mitandaoni yaliyomhusisha na ugonjwa huo hivyo alitaka kuwakata ngebe waliokuwa wakichonga na kumharibia michongo yake ya mjini.

Taarifa hizo zilionesha kuwa, Masogange alichukua hatua hiyo siku chache baada ya video queen mwingine wa Bongo, Tunda Sebastian kufanya hivyo na kuweza kumaliza kabisa uvumi huo baada ya kubainika kuwa hawana Ukimwi.

CHETI CHA PILI

Kama hiyo haitoshi, ili kumaliza kabisa uvumi huo, Masogange alipima kwa mara nyingine kwenye Hospitali ya Mama Ngoma na kuanika vyeti vya majibu yake kuwa alikuwa HIV-Negative kwa mara nyingine. Duru za kihabari zilionesha kuwa, baada ya kuaga dunia hivi karibuni, madai hayo yaliibuka kwa mara nyingine hivyo kuwapa jukumu watu wake wa karibu kumtetea kuwa alikuwa salama.

MASOGANGE ALIKUWA SALAMA

Katika kumtetea huko ndipo walipojikuta wakianika vyeti hivyo vyote vilivyoonesha kuwa, Masogange alikuwa salama.

“Kiukweli nimeviona vyeti vyake vyote viwili, alikuwa salama kabisa hivyo watu waache maneno kwani kila kitu kinapangwa na Mungu, tumwache Aggy (Masogange) apumzike,” alisema mmoja wa waliokuwa marafiki wakubwa wa mwanadada huyo.

Masogange alianza kupata umaarufu baada ya kuonekana kwenye video ya kwanza ya My Lady ya msanii wa Bongo Fleva, Suma Rider.

UMAARUFU

Baadaye alipata jina zaidi kufuatia kuonekana kwenye video ya Masogange (Macho Yangu) ya Mwanamuziki, Abednego Damian ‘Belle 9’ kisha Msambinungwa ya Tunda Man.

Masogange ameacha mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 11 aliyezaa na jamaa aitwaye Sabri Shaban, mkazi wa Magomeni jijini Dar.

SOMA Pia: Job Opportunity at Duma Works, Customer Development Manager

GPL

Mnamsumbua Diamond Hapa, Kenya Wamempokea na Nyumba Wamempangia – Musukuma

$
0
0
Mnamsumbua Diamond hapa, Kenya wamempokea na nyumba wamempangia – Musukuma
Mbunge wa Jimbo la Geita vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma) ameuponda utaratibu wa serikali kufungia nyimbo za wasanii pindi zinapoonekana kukiuka maadili.

Akizungumza leo Bungeni April 27, 2018 wakati akichangia bajeti ya wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaaa na Michezo, Musukuma amesema serikali inatakiwa kutoa elimu zaidi kuliko kufungia.

“Msitumie muda mwingi kufungia, ni bora ukatumia muda mwingi kuwafundisha na kukemea yale mambo madogo madogo ili hii tasnia iendelee,” amesema.

“Mnamsumbua Diamond hapa masikini ya Mungu, mnaona yaliyofanyika Kenya, wenzenu wamempokea wanamuambia imba kila kitu ambacho umezuiliwa, wamempa kiwanja, wamempangia nyumba, tutapoteza hizi bahati,” amesisitiza.

Utakumbuka February 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuamuru kutopigwa katika vyombo vya habari.

SOMA Pia: Job Opportunity at Uchumi Commercial Bank Ltd, Head of Internal Audit

Viboko Vyawakimbiza Wanafunzi Shuleni

$
0
0
Viboko Vyawakimbiza Wanafunzi Shuleni
Wanafunzi wanne kati ya watano wa Shule ya Msingi Ndolage, Kata ya Kamachumu, Kagera wamekamatwa wakidaiwa kutoroka shule na kwenda kutafuta kazi za ndani mjini Bukoba.

Wanafunzi hao wenye miaka 11 hadi 14 walitoroka Aprili 25 wakiwa na sare za shule.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ndolage, Frederick Byarugaba alisema wanafunzi hao (majina tunayahifadhi) walitoka nyumbani kwao Kitongoji cha Buganda B, Kamachumu na walipata usafiri wa kuelekea Bukoba Mjini.

“Baada ya taarifa hizo kusambaa kuwa wanafunzi wametoroka, uongozi wa shule ulitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, Kituo cha Kamachumu, Muleba,” alisema Byarugaba.

Alisema watoto hao walionekana kwa mara ya kwanza, Manispaa ya Bukoba wakitembea pamoja na baadhi ya watu wakiwamo abiria waliwakamata na kutoa taarifa polisi na kwa uongozi wa shule.

“Walikuwa na utoro wa rejareja na mara kadhaa wamekuwa wakikanywa kuhusu tabia mbaya ya utoro, hivyo baada ya wazazi kutoa taarifa ya kutoonekana nyumbani tulianza kusambaza ujumbe wa kuwatafuta,” alisema Byarugaba.

Mmoja wa walezi wa watoto hao, Christopher Kalumuna alisema kuwa baada ya mwalimu wa zamu kudai hawakuonekana shuleni hapo alisambaza taarifa kwenye miji midogo ya Kemondo, Kyetema na Bukoba Mjini hadi kwenye vituo vya magari ili kubaini kama wanaweza kusafiri.

“Huyu ni mtoto wa marehemu kaka yangu (jina tunalihifadhi) na mama yake naye ni marehemu, alikuwa akinifanyia kazi za nyumbani baada ya kutoka shule,” alisema Kalumuna.

Akizungumza kuhusu kilichowafanya kutoroka, mtoto huyo alisema walirubuniwa na mwenzao, ambaye aliiwambia kuwa shuleni kumeandaliwa adhabu ya watoto watoro hivyo watoroke kuepuka viboko au nyaya za umeme.

“Tuliogopa adhabu na ni kweli tumekuwa watoro kila mara na tunachelewa shule. Tulipoondoka tulilala kichakani bila kula huko Kemondo na tulitembea kwa miguu.

“Baada ya kufika Bukoba mjini kiongozi wetu (mwanafunzi mwenzao) alitutoroka na tuliokotwa baada ya kuanza kulia, ndipo tukamweleza aliyetuokota akatupandisha kwenye gari hadi Kamachumu,” alisema mtoto huyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Agustino Olomi alithibi

Baada ya Kifo cha Masogange Irene Uwoya, Dogo Janja Waikimbia Nyumba Waliokuwa Wakiishi na Marehemu

$
0
0
Baada ya Kifo cha Masogange Irene Uwoya, Dogo Janja Waikimbia Nyumba Waliokuwa Wakiishi na Marehemu
STAA mkali wa filamu Bongo, Irene Uwoya na baby wake Abdul Chende ‘Dogo Janja’ wamefungukia dhamira yao ya kuihama nyumba waliyokuwa wakiishi na marehemu Agness Gerald ‘Masogange’ iliyopo Makongo Juu jijini Dar wakidai kuwa, hawatakuwa na amani.


Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa niaba ya mkewe, Dogo Janja alisema kuwa hawawezi kuendelea kuishi hapo tena kwa sababu kwao itakuwa ni majonzi kila siku na hiyo ni kutokana na ukaribu waliokuwa nao kwa Masogange.


“Kwa kweli mimi na mke wangu hatuwezi tena kuendelea kuishi Makongo Juu kwenye ile nyumba maana kwetu itakuwa ni simanzi tuu, Masogange alikuwa ni mtu wetu wa karibu sana na tulikuwa tukifanya vitu vingi pamoja, pia mke wangu atakuwa na huzuni sana akiendelea kuishi pale,” alisema Dogo Janja.

Mama Kanumba Amjibu Wema Baada ya Kukataa Kuigiza Nae "Wema Alitaka Nishike Bakuli Nikaombe Barabarani?"

$
0
0
Mama Kanumba Amjibu Wema Baada ya Kukataa Kuigiza Nae "Je Wema Alitaka Nishike Bakuri Nikaombe Barabarani?"
BAADA ya hivi karibuni staa wa filamu, Wema Sepetu kueleza maneno aliyoelezwa na aliyekuwa msanii wa filamu, marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake kwamba hataki kabisa mama yake mzazi, Flora Mtegoa aigize, mzazi huyo ameibuka na kufungukia ishu hiyo.



Akipiga stori na Za Motomoto News, mama Kanumba alisema mwanaye huyo alisema hayo kwa sababu alikuwa akimtunza na kumlipa mshahara kama mfanyakazi lakini kwa sasa hayupo hivyo ndiyo maana ameingia kwenye sanaa ya uigizaji kwa kuwa bila hivyo angegeuka ombaomba jambo ambalo halipendezi.


“Kanumba alisema hayo kwa kuwa alikuwa ananitunza yaani ananinunulia vyakula na kunilipa mshahara kila mwezi kama mfanyakazi lakini sasa hayupo, je Wema alitaka nishike bakuli nikaombe barabarani au? Maana kulima siwezi hivyo naona tu bora niigize ili niweze kujikimu kimaisha,” alisema mama Kanumba

Kibadeni Awapa Mbinu Simba, Yanga

$
0
0
Kibadeni Awapa Mbinu Simba, Yanga
Kuelekea mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga, kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni amewataka wachezaji kila mmoja kucheza kwa uwezo wake ili kuonyesha kipaji alichonacho na mwisho wa siku aisaidie timu.


“Naziomba hizi timu mbili Simba na Yanga wajue kwamba jumapili wanaenda kuonyesha vipaji vyao na walichofundishwa na makocha wao, pia wanatakiwa kutulia na sio kucheza kwa kukamiana bali soka safi kama ilivyo kwa wachezaji wa nje,” amesema Kibadeni.

Aidha Kibadeni pia amewataka viongozi wa vilabu hivyo kuweza kuwalinda wachezaji ili kutunza vipaji vyao ambavyo vitawasaidia sio kwenye soka la Simba na Yanga bali hata nje ya mipaka ya Tanzania.

Mchezo ambao unaweza kuamua mbio za ubingwa utapigwa siku ya jumapili April 29 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Tayari tiketi za pambano hilo zimeshaanza kuuzwa na shirikisho la soka nchini TFF.

Simba kwasasa ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 59 baada ya michezo 25. Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 48 baada ya mechi 23. Baada ya pambano la jumapili Simba itabakiwa na mechi 4 huku Yanga ikibakiwa na mechi 6.

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Secta Binafasi na Serikalini

$
0
0

Download Hapa Application Mpya ya Udaku Special Uweze Soma Vimbwanga na Udaku Mtaani Kila Siku

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya UDAKU SPECIAL Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Marekebisho Makubwa tumeyafanya ikiwa na tatizo la Notification kutatuliwa

NB: App mpya ina Icon Nyekundu

 Bonyeza Hapa Chini Kuinstall Upya:


==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>    

Okoa Ndoa yako Sasa...Umepungukiwa na Nguvu za Kiume na Unashindwa Kupanda Mlima Vizuri

$
0
0
OKOA NDOA YAKO SASA : JE UMEPUNGUKIWA NA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO AU MPENZI WAKO HAKUTIMIZII UTAKACHO:


Acha kujiona mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kwa sababu ya kutokuwa na nguvu za kiume au Uume wako mdogo

Dawa YA MAPRO POWERA ndio dawa sahihi na tiba tosha kwa sasa Kutibu tatizo na kuponesha kabisa tatizo LA KUWAI KUFIKA KILELENI KABLA MWENZI WAKO BADO AJAKOJOA

KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA NA MWILI KUCHOKA

UUME KUSINYAA NA KUWA LEGELEGE

KUUMWA NA TUMBO WAKATI UNAPOMALIZA KUFANYA TENDO

Dawa hii utumiwa ata na wazee wenye umri mkubwa na haina madhara yoyote

MAKAKANUA HII NI dawa ya maumbili madogo urefusha na kunenepesha saizi upendayo saiz 5-6-7-8 na unene sm 3-4-5 kwa mini huabiki kwa kuwa na UUME mdogo wai sasa upate tiba sahihi kabisa na ni tofauti na ulizowai kutumia :

Tunarudisha mke au mpenzi ndani ya masaa matatu tu zipo dawa za presha kisukali vidonda vya tumbo korodani iliyovimba dawa za uzazi tunapunguza matiti makubwa kitambi na mwili mkubwa dawa zipo FIKA OFISINI KWANGU MBAGALA ZAKHEMU KWA WATEJA AMBAO AMTAKUWA NA NAFASI YA KUJA OFISINI AU MLIO MKOANI MTALETEWA p

Piga simu 0743362017 au 0789234653

DR AGU

Asante Kwasi Kuhusubiri kwa Hamu Mchezo wa Simba, Yanga

$
0
0
Asante Kwasi Kuhusubiri kwa Hamu Mchezo wa Simba, Yanga
WAKATI Simba na Yanga zikitarajiwa kuvaana siku ya Jumapili ya Aprili 29, beki Mghana wa Simba, Asante Kwasi, amefunguka anajisikia furaha kucheza mchezo huo ambao ni mara yake ya kwanza na anaamini watapata matokeo.

Simba na Yanga zitashuka dimbani keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati mchezo wa awali uliozikutanisha timu hizo zilitoa sare ya 1-1.

Akizungumza na Championi Ijumaa, beki huyo alisema ni mchezo wake wa kwanza akiwa Simba lakini anajisikia furaha kuwa sehemu ya mchezo huo na lengo ni kupata matokeo.

“Najisikia furaha sababu ni mchezo mkubwa kwa timu zetu hapa nyumbani na kwa upande wangu, ni mara ya kwanza kucheza mchezo huo tangu nijiunge na Simba.

“Ingawa si mgeni kwa hizi timu sababu tayari awali niliwahi kukutana nazo nje ya hapa Simba, lakini kikubwa na sisi kupambana na kuweza kupata matokeo na kusonga mbele,” alisema Kwasi.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images