Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Mapenzi ya Dogo Janja na Irene Uwoya Yapamba Moto

$
0
0
Dogo Janja Amtumia Ujumbe Mzito wa Mapenzi Irene Uwoya
Msanii wa Muziki wa Bongo Flava, Dogo Janja azidi kuyaanika mapenzi aliyonayo hadharani kwa mke wake ambaye ni Muigizaji,Irene Uwoya.



Dogo Janja kupitia ukurasa wa instagram amepost picha akiwa na mke wake huyo na kuandika caption iliyoandikwa hivi “thamani ya upendo wako ni ya maisha kama maisha yalivyo ni upendo.”

Irene Uwoya nae hakukaa kimya alimjibu Dogo Janja na kusema “Nakupenda leo jana na milele.”

Baridi Inaletwa na Mungu Inabidi Tujikinge na Ukimwi- Rais JPM

$
0
0
Baridi Inaletwa na Mungu Inabidi Tujikinge na Ukimwi- Rais JPM
Leo May 2, 2018 President Dr. John Pombe Magufuli Ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospital ya Kilolo ambapo amewataka watu wa mikoa ya Njombe na Iringa kuchukua tahadhari juu ya gonjwa la UKIMWI sababu mikoa hiyo ndio inayoongoza nchini.

“Mkoa wa Iringa na Njombe ina maambukizi mengi ya UKIMWI, Iringa una 11.2% na Njombe ni 11.6%. Inawezekana sababu ya msingi ni baridi lakini sina uhakika. Ni lazima tuwajibike katika kujikinga na UKIMWI,” amesema Rais Magufuli.

“Kwahiyo Iringa ni ya pili Njombe ni ya kwanza kwa maambukizi ya Ukimwi nilipofika hapa Kilolo inaonekana shida kubwa hapa ni baridi na kwasababu inaletwa na Mwenyezi Mungu inabidi tujikinge na kuchukua tahadhari zote kwa gonjwa hili.” -JPM

'Sikutosheka Kushiriki Ngono Mara 5 kwa Siku'

$
0
0
'Sikutosheka Kushiriki Ngono Mara 5 kwa Siku'
Shirika la wahisani la Relationship charity Relate limetoa wito kwa watu walio na uraibu wa ngono kupata usaidizi nchini Uingereza. Waathiriwa wawili wanazungumzia kuhusu athari za kuwa na pepo la ngono.

''Mara nyengine hata kushiriki ngono mara tano kwa siku haikutosha''.

Mama wa watoto 3 Rebecca Barker anasema kuwa tatizo hilo lilitawala maisha yake 2014 na kuvunja uhusiano wake

"Ilikuwa kitu cha kwanza kuja katika fikra zangu wakati nilipoamka , sikuweza kuitoa katika fikra zangu'' , alisema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37 kutoka eneo la Tadcaster Kaskazini mwa Yorkshire.

"Nilihisi kana kwamba kila kitu kilikuwa kikinikumbusha kuhusu tendo la ngono. Nadhani ilitokana na shinikizo la mawazo . Nilihisi kwamba mwili wangu wote ulikuwa ukitamani kushiriki katika shughuli hiyo.

"Ilikuwa ikinigonga na dakika tano baadaye niliitaka kushiriki tena tendo la ngono.

Nilihisi upweke, nilisalia nyumbani kwa sababu nilihisi aibu, nilikuwa nikifikiria kufanya ngono kila wakati. Hata iwapo hakuna mtu ambaye angeweza kugundua kilichokuwa katika fikra zangu , nilihisi vibaya kuwa karibu na watu wengine.

Ms Barker alivunja uhusiano wak na mpenziwe na kubadilisha maisha yake ili kutibu pepo wa ngono.
Pepo la ngono la Bi Barker lilizua matatizo makubwa katika uhusiano wake, ijapokuwa mpenziwe alipendelea hali yake kwa mara ya kwanza lakini alishindwa kuidhibiti.

"Mara ya kwanza alikuwa akifurahia lakini mwisho mwisho hakuweza kuelewa na baada ya miezi michache alianza kuuliza maswali ni wapi hisia hizo zilikuwa zikitoka .

"Alinishutumu kwa kuwa na uhusiano wa nje- alidhani kwamba nilikuwa nikihisi kufanya makosa ndiposa nikataka kushiriki naye tendo la ngono.

Uhusiaono wake ulivunjika
Mnamo mwezi Novemba 2014, bi Barker "alitaka kupumzika kutoka katika uhusiano huo na alienda kuishi na mamake.

"Nilipoondoka nilimwambia mpenzi wangu kwamba nilihitaji kuimarika kitabia na hisia. Alinikubali kuondoka na uhusiano wetu ukaisha polepole''

"Nilikuwa chini ya uangalizi wa mtaalamu wa matatizo ya kiakili wakati huo-ambaye alikuwa akinimbia kwamba atabadilisha dawa zangu , lakini hakusema kwamba kulikuwa na makundi ya usaidizi.

Bi Barker alipatikana na shinikizo la kiakili 2012 baada ya kujifungua mwanawe wa tatu. Alisema kwamba alibadilisha kazi aliyokuwa akifanya , akakosana na mpenzi wake na kuhamia Ufaransa.

''Nilifanya mabadiliko katika maisha yangu ili kukabiliana na shinikizo hilo la mawazo na pepo huyo wa ngono na ni hatua hiyo ilionisaidia'', alisema.

Relate inaelezea uraibu wa ngono kuwa kushiriki ngono isioweza kudhibitika na shirika la afya duniani WHO linatarajiwa kuweka tatizo hilo miongoni mwa matatizo ya kingono katika orodha yake ya kitaifa ya magonjwa (ICD) mnamo mwezi Mei 2019.

Graham, ambaye jina lake limebadilishwa anasema kuwa tatizo lake la kuwa na pepo wa ngono lilimlazimu kulala nje na mamia ya makahaba na kumfanya kuwa na hatia kubwa.

Wakati unapokuwa na pepo huyo unakuwa ukifikiria kitendo hicho mara kwa mara kutoka wakati unapoamka hadi wakati unapoenda kulala. Haikuwa hali nzuri, wakati unapoamka alfajiri na kutumia dawa za kukabiliana na magonjwa ya zinaa .

Bi Barker amesema kuwa ngono nio kilichokuwa kitu cha kwanza katika mafikira yake
Alikuwa na uhusiano na makahaba 3
Graham, ambaye yuko katika miaka yake ya 60 anakadiria kwamba alilipa mamia ya paundi kwa mwezi kwa miaka kadhaa ili kuimarisha uhusiano wake na baadhi ya makahaba

"Uhusiano ulioanza kama urafiki kazini ulichochea mwengine -lakini kama mahusiano ya afisi ambayo yangeanza kutokana na mhusika mmoja kutokuwa na raha katika ndoa yake tatizo langu lilikuwa pepo wa ngono ambaye nililazimika kumpatia mahitaji yake kila siku.

Una uhusiano mmoja na baadaye unataka mwengine na baadaye unajiingiza katika mwengine. Na baadaye niligundua kwamba hatua mojawapo ya haraka ya kukabiliana na tatzio langu ni kulipia huduma hiyo .

Nilikuwa nikishiriki ngono na makahaba mara tatu ama hata nne kwa wiki.

Ni sawa na kuwa mlevi , ni tatizo linalokujia katika akili yako-Unahisi na kupanda hisia unapolifikiria na unapolitenda katika mipango yako na baadaye unapomaliza unajiambia kwamba hutawahi kufanya tena.

Graham alisita kuendelea na maisha hayo ya kutisha wakati mkewe alipopata barua pepe na kumshutumu.

Alitafuta usaidizi kwa mashirika yanayowasaidia watu wa tatizo lake nchini Uingereza kama vile Sex Addicts Anonymous (SAA), shirika ambalo lina makundi 78 nchini Uingereza na kwamba amewacha kujihusisha na ngono nje ya ndoa yake kwa miaka kadhaa.

Wakati nilipohudumiwa nakumbuka kuhisi kumshukuru Mungu- na kusema kitu kitabadilika .

Nileinda kwa shirikja hilo kwa tiba ya kuwacha kushiriki katika ngono za nje ya ndoa.

Nahisi afueni kulekea katika mikutano hiyo na kuona watu ambao wako katika hali mbaya zaidi ya nilivyokuwa. Kwa watu walio katika tatizo hili nataka wajue kwamba kuna njia nyengine na unaweza kujiondoa katika tatizo hilo.

Waziri Atakiwa Kujiuzulu na Kuvunja Bunge

$
0
0
Waziri Atakiwa Kujiuzulu na Kuvunja Bunge
Mahakama ya Katiba nchini Gabon imemuamuru Waziri Mkuu wa nchi hiyo kujiuzulu na kuvunja bunge baada ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika weekend iliyopita kuchelewa.

Mahakama hiyo imeeleza kuwa Waziri Mkuu huyo Emmanuel Issoze-Ngondet na bunge la nchi hiyo halitambuliki tena kwasababu walichelewa kufanya uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

Pia mahakama hiyo imemuamuru Rais wa nchi hiyo Ali Bongo kumtangaza Waziri Mkuu wa Mpito mpaka hapo uchaguzi utakapopangwa.

Hamisa, Zari Sio Marafiki Zangu Lakini Wema Ndo Rafiki Yangu- Aunt Ezekiel

$
0
0
Hamisa, Zari Sio Marafiki Zangu Lakini Wema Ndo Rafiki Yangu- Aunt Ezekiel
Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka na kuweka wazi kuwa hana urafiki wowote na Mama watoto wa Staa Diamond, Zari na Hamisa Mobetto.

Kwa muda mrefu inajulikana kuwa Aunty Ezekiel ana urafiki na Wema Sepetu kwaiyo siku ambayo alionekana na Diamond na Zari visiwani Zanzibar wakila bata watu wengi walichukulia kama usaliti kwa rafiki yake.

Hivi sasa Tetesi zinadai kuwa Diamond yupo Kwenye Mahusiano na Hamisa Mobetto ambaye ni adui namba moja wa Wema Sepetu hivyo Kolabo mtu amekuwa akihoji Aunty atakuwa upande gani kama ni Hamisa au Wema?.

Lakini Aunty ameshaweka wazi kuhusu hilo na kudai hahitaji kuchagua upande kwa kuwa Zari na Hamisa sio marafiki zake bali Wema ndiye rafiki yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online, Aunty ameweka wazi kuwa Diamond sio bosi wake bali ni mshkaji wake wa siku nyingi kabla hata hajaanza Mahusiano na Moses Iyobo.

"Naseeb is not my boss, Naseeb mimi ni rafiki yangu na mshkaji wangu ni mtu ambaye nimejuana naye kabla ya kujuana na hawa watu wengine wote yaani tumejuana kivyetu na sio Kupitia Mahusiano yetu."

Hamisa sio rafiki yangu na wala Zari sio rafiki yangu na hata mwanamke mwingine wa Diamond sio rafiki yangu lakini Wema mimi ni rafiki yangu”.

Mniombe Nisije Kusahau Nilikotoka na Nisije Nikawa na Kiburi- Rais Magufuli

$
0
0
Mniombe Nisije Kusahau Nilikotoka na Nisije Nikawa na Kiburi- Rais Magufuli
Leo May 2, 2018 President Dr. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospital ya Kilolo ambapo amewaomba Watanzania wamuombee asije akabadilika na kuwa na kiburi.

“Niwaombe ndugu zangu mniombee, nisije kusahahu nilikotoka, ili niitumikie Tanzania kwa mafanikio makubwa, hata siku nikitoka duniani nikaenda huko, nikaishi kwa furaha kwa sababu niliwatumikia Watanzania wenzangu kwa upendo na mafanikio mazuri,” -Rais Magufuli.

“Nataka kuwahakikishia wananchi wa Kilolo, Iringa na Watanzania kwa ujumla sitawaangusha mimi siku zote nitakuwa mtumishi wenu ninajua kuongoza Kiutumishi. Naomba mniombee nisije nikabadilika nisiwe na kiburi.” -Rais Magufuli

Aliyewatumbua Wenye Elimu ya Darasa la saba Naye Atumbuliwa

$
0
0
Aliyewatumbua Wenye Elimu ya Darasa la saba Naye Atumbuliwa
Mkurugenzi mtendaji  wa halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga Peter Nyalali  amemsimamisha kazi kaimu afisa utumishi wa halmashauri hiyo Protas Dibogo kwa kosa la kukaidi kuwarudisha kazini watendaji wa vijiji 41 baada ya serikali kuagiza warejeshwe.


Nyalali ametoa kauli hiyo wakati wa kikao chake na watumishi wa halmashauri hiyo ambapo, pamoja na mambo mengine amesisitiza watendaji hao kwenda kufanya kazi kwa bidii kwenye maeneo yao mara tu watakaporejea kazini.

Hivi karibuni serikali iliagiza kurudishwa kazini kwa watumishi wote walioajiriwa 01/05/2004, ambapo  Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Bumbuli Peter Nyalali  alimwagiza kaimu afisa utumishi wa halmashauri hiyo awarudishe kazini watendaji wa vijiji 41.

Pamoja na kutolewa agizo hilo Kaimu Afisa Utumishi Protas Dibogo hakutekeleza agizo hilo jambo lililosababisha  Mkurugenzi Nyalali kumsimamisha kazi.

"Masharti yanaonyesha kwamba nyie mmeanza tarehe 1 mwezi 5. Yeye anapotosha hapa anasema kwamba mmeanza mwezi wa 6. Ninamsimamisha kazi na nafasi yake atakaa Bi Asha Majid" Nyalali.

Tarehe 01/05/2004 serikali iliwaajiri watumishi waliokuwa wakijitolea katika maeneo mbalimbali nchini,ambapo  tarehe 20/05/2004 serikali ilitoa kibali cha kuajiri watumishi wapya wenye elimu ya darasa la saba huku ikiwataka kujiendeleza wawapo kazini

Steve Nyerere na Timu ya Bongo Movie Yapeleka Fulsa Tanga ya Kuibua Vipaji

$
0
0
Steve Nyerere na Timu ya Bongo Movie Yapeleka Fulsa Tanga ya Kuibua Vipaji
TIMU  ya wasanii wa Bongo Muvi ikiongozwa na msanii wa vichekesho, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ inatarajiwa kutua Jumamosi wiki hii wilayani Pangani mkoani Tanga kwa ajili ya kutoa elimu na fursa mbalimbali za kuibua vipaji vya wasanii.



Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dares Salaam, Steve  amesema Jumamosi watakuwa wilayani humo wakiwaelimisha vijana juu ya kujitambua, kutumia fursa walizonazo mkoani humo,  kama kutumia vipaji walivyonavyo ili kufanikisha malengo yao  ya kimaisha.



Amesema kuwa vijana wengi huvunjika moyo kutokana na changamoto wanazozipitia bila ya kujua watazitatua vipi,  hivyo kupitia kampeni yao ya Amka Kijana wataweza kuwapa elimu mbalimbali.



Mbali na elimu hiyo pia amesema siku hiyo kutakuwa na mtanange wa soka baina ya mashabiki wa timu ya Simba Yanga na watatembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vilivyomo wilayani humo.



Amesema wasanii mbalimbali kama, Aunt Ezekiel, Flora Mvungi, Jaqueline Wolper, Duma, Johari, JB na wengine wengi. Tamasha hilo litakuwa la wazi na halitakuwa na kiingilio.

Rais JPM Ahoji Jambo Hili " Kwani Kusoma ndo Kujua Kingereza"

$
0
0
Rais JPM Ahoji Jambo Hili " Kwani Kusoma ndo Kujua Kingereza"
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli amehoji wanafunzi wa chuo cha Mkwawa kwamba kujua kusoma ni kujua Kiingereza.



Rais Magufuli ameyasema hayo leo, Mei 2 wakati akizungumza na wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, kilichopo mkoani Iringa wakati akitoa ufafanuzi wa shule za private na shule za Sekondari.

“Eti mtu amemaliza form 4 hajui kuandika barua ya kingereza. Kwani kusoma ni kujua kingereza? Wachina wanajua kingereza? mbona wanatengeneza mashine,” amehoji Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa “Shule za private wanafunzi wake wanachujwa, wakifika form 2 kuingia form 3 wanawachuja tena. Wanabaki na ile cream ili waonekane wanaongoza. Serikali inayowapenda wananchi wake haiwezi ikafanya hivyo.”

Abaka Mwanafunzi wa Darasa la Pili Akimhaidi Kumpa Andazi

$
0
0
Abaka Mwanafunzi wa Darasa la Pili Akimhaidi Kumpa Andazi
Jeshi  la  Polisi mkoani Shinyanga  linamshikilia Amos Meshack (36), mfanyabiashara wa udongo wa pemba, kwa tuhuma za kubaka mtoto wa umri wa miaka tisa, mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Ndala A Manispaa ya Shinyanga.

Tukio hilo lilitokea juzi  mchana nyumbani kwa mtuhumiwa huyo, Kata ya Ndala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alisema chanzo cha tukio hilo ni tamaa za  mwili.

Alisema mbinu iliyotumika ni mtuhumiwa kumwita mtoto kwa ahadi ya kumpatia Sh 200 kwa ajili ya kununulia maandazi.

“Kutokana na ahadi hiyo, mtoto aliingia katika nyumba au kibanda ambacho mtuhumiwa hukitumia kufanyia biashara ndogo ndogo za kufinyanga na kutengeneza udongo wa pemba, alimkamata na kumbaka akimsisitiza asieleze chochote kwa mtu yeyote.

“Hata hivyo, mama mzazi wa mtoto aligundua tukio la kubakwa kwa mwanaye  baada ya kumuona akiwa hana furaha na kuamua kumdadisi,” alisema.

Alisema aligundua mwanae  amebakwa baada ya kuona nguo zake za ndani  zikiwa zimefichwa nyuma ya kitanda, huku akionekana mnyonge.

Alisema baada ya kumhoji  mwanae alidai alibakwa na baba Amani ambaye ni Meshack, na kuwa huo ndiyo mchezo wake wa kila siku.

Alisema wakati akianza uchafu huo, alikuwa akimpatia pipi na safari hii alimnunulia maandazi kisha kumvutia ofisini kwake na kumbaka tena.

“Alipelekwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga kupimwa  na majibu ya daktari yalivyotoka ilibainika amebakwa…mchezo huo amekuwa akifanyiwa kila mara na siyo mara moja,”alisema.

Kamanda Haule  alisema wanamshikilia mtuhumiwa na baada ya uchunguzi   kukamilishwa atafikishwa mahakamani.

Billnass Amgeukia Alikiba

$
0
0
Billnass amgeukia Alikiba
Rapa Billnass ambaye anatamba na ngoma ya 'Tagi Ubavu' amefunguka na kuweka wazi kwa jamii kuwa Alikiba ni miongoni mwa wasanii ambaye anampa ushirikiano mkubwa kwa kila jambo ambalo huwa analifanya katika harakati zake na kudai siku zikikaribia huenda wakatoa wimbo wa pamoja.


Billnass ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana hadi 10:00 jioni baada ya kuonekana picha katika mitandao za kijamii zikiwaonesha wawili hao wakiwa studio katika siku za nyuma kidogo.

"Nina mahusiano mazuri na Alikiba na huwa ananishauri mambo mengi katika kazi zangu hata muda mwingine huwa tunataniana, naamini anakubali kazi zangu maana huwa nikiachia ngoma huwa ananiambia mdogo wangu hapo fresh au kazia buti sehemu fulani. Inshallah panapo majaliwa nitafanyakazi na Alikiba ila kwa sasa sitaki kuliweka wazi suala hili, ila watu wajue tu kuwa tunamawasiliano mazuri baina yetu", amesema Billnass.

Serikali Gabon Yajiuzulu kwa Amri ya Mahakama

$
0
0
Serikali Gabon Yajiuzulu kwa Amri ya Mahakama
Serikali ya Gabon imejiuzulu siku moja baada ya Mahakama Kuu ya Katiba kuamuru Bunge livunjwe na kuagiza uongozi wa nchi ujiuzulu kutokana na kuchelewa kuitisha uchaguzi mkuu.

Taarifa ya Serikali inasema Waziri Mkuu Emmanuel Issoze Ngondet "aliwasilisha barua ya kujiuzulu kutoka nafasi yake serikalini baada ya uamuzi wa Mahakama ya Katiba kuamuru shughuli za Bunge zisimame hatua iliyolazimisha Serikali kujiuzulu."

Kwa mujibu wa Mahakama Serikali ilipaswa kuandaa uchaguzi lakini uliahirishwa mara mbili kufikia Aprili 30.

Mahakama imesema shughuli za Bunge lililovunjwa sasa zitahamishiwa kwenye Baraza la Seneti hadi uchaguzi mpya ufanyike. Tarehe ya uchaguzi haijatangazwa.

Uchaguzi mkuu ulifanyika mwaka 2016 ambao Rais Ali Bongo alitangazwa kuwa mshindi matokeo yaliyopingwa na upinzani.

Ghasia zilizuka siku chache baada ya uchaguzi na wapinzani wanasema watu zaidi ya 50 waliuawa katika mapigano. Taarifa rasmi ya vifo ni watu watatu.

Bongo alitwaa mamlaka kutoka kwa baba yake Omar Bongo, ambaye alitawala kwa miaka 41 hadi alipofariki dunia mwaka 2009.

Wema Sepetu Afunguka Sababu Iliyomfanya Kutoudhuria Harusi ya Alikiba

$
0
0
Wema Sepetu Afunguka Sababu Iliyomfanya Kutoudhuria Harusi ya Alikiba
Msanii wa Filamu Bongo, Wema Sepetu amefunguka sababu ya kutohudhuria kwenye harusi ya msanii Alikiba.

Mrembo huyo amesema harusi ya Alikiba iligongana na birthday ya mdogo wake hivyo akashindwa kwenda kwani anaiweka familia yake mbele kwanza.

“That because ile ni siku ambayo nilimfanyia mdogo wangu birth day party, mdogo wangu alikuwa anatimiza miaka 20 mwaka huu. Kwa hiyo mwaka jana sikumfanyia chochote mwaka huu nikawa nimemuhaidi i will do the party,” amesema.

“So family first na Alikiba anajua mimi namsapoti mwisho wa siku sina kinyongo chochote namtakia kila la kheri kwenye maisha yake ya ndoa,” Wema ameiambia Bongo5.

Utakumbuka April 19, 2018 Msanii Alikiba alifunga ndoa na mpenzi wake mjini Mombasa nchini Kenya na April 29, 2018 walifanya sherehe ya pili Dar es Salaam.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya May 3

$
0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya May 3

Serikali Yasema Nondo akishinda kesi Atarejea chuoni

$
0
0
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) Abdul Nondo amesimamishwa masomo ili kulindwa, asipoteza sifa za kuwa mwanafunzi wa chuo hicho.

Kusimamishwa chuo kwa Nondo, kuliibua mjadala mkali wakati wa kuijadili bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakidai hatua hiyo ni aibu kwa chuo hicho.

Akijibu hoja hiyo leo Mei 2, 2018 bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa wizara hiyo, William Ole Nasha amesema kwa kuwa Nondo ana kesi kama akishinda anarejea chuoni na sheria inamlinda badala ya kumminya asipoteze sifa.

Rais Magufuli Anusa Ufisadi wa Bilioni 8 Ukumbi wa Chuo cha Mkwawa....Atoa Maagizo Mazito Kwa Vyombo vya Dola

$
0
0
Rais John Magufuli amefichua siri ya kukataa kuweka jiwe la msingi katika ukumbi wa jengo lililopo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa mkoani Iringa akisema limejengwa kifisadi kwa Sh 8bilioni.

Rais ameeleza hayo jana, Mei 2, 2018 wakati akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani humo.

"Muda mwingine tuambizane ukweli Chuo cha Mkwawa kimeniangusha, ndio maana nilikataa kuja kuweka jiwe la msingi katika lile jengo. Siwezi kuweka jiwe la msingi katika jengo la kifisadi.

"Nikitoka hapa nitakwenda kulikagua. Nilitegemea chuo hiki kitasimamia value of money (thamani ya fedha), kwa sababu kuna wasomi lakini tofauti."

Rais Magufuli alitumia nafasi hiyo kuviagiza vyombo vya dola kuhakikisha wanawachukulia hatua wale wote waliohusika katika mchakato huo hata kama wamestaafu, watafutwe waliko.

"Mmeshindwa kusimamia ujenzi wa lile jengo halafu leo mnaniomba mabweni? Nitaanzaje kuwakubalia wakati huku mmeshindwa, siwezi. Vyombo vya dola  na wizara vifuatilie mkishindwa nitafuatilia.

Bill Nass na Nandy Waungana Tena

$
0
0
Wiki Kadhaa baada ya Video yao ya uchi kusambaa mitandaoni, Bill Nass amefunguka kuwa tayari kuna kuna ngoma ameshafanya na Nandy muda ukifika wataachia.

Hit maker huyo wa Tagi Ubavu amesema hayo katika kipindi cha Kikaangoni cha EATV na kuongeza kuwa mrembo huyo ni rafiki yake tu kwa sasa.

“Kuna wimbo tumefanya pamoja, wimbo umefanywa chini ya S2kizzy hivyo naamini muda ukifika utatoka tu ila nachojua ni wimbo mkali, kuhusu jambo ambalo limetokea,” amesema Bill.

Rapper huyo ameongeza, “Kuhusu mimi na yeye tayari nilishaomba radhi kwa wananchi na sasa maisha ya kawaida yanaendelea, hivyo hatuna tofauti yoyote ile kwa kuwa yule ni rafiki yangu na nina iheshimu sana familia yake akiwa pamoja na mama yake kwa kuwa ni mtu ambaye amekuwa akijitoa sana kusupport kazi za mwanae.”

Wema Apata Dili Nono Kombe la Dunia Star Times Yampa Balozi

$
0
0
Wema Apata Dili Nono Kombe la Dunia Star Times Yampa Balozi
Msanii wa filamu Tanzania, Wema Sepetu, akizungumza jambo kwa niaba ya wasanii wenzake  mara baada ya kutambulishwa rasmi kuwa mabalozi wa StarTimes.


Mkurugenzi wa StarMedia Tanzania, Wang Xiaobo,  mwenye suti akiwakabidhi madishi ya televisheni mabalozi hao.


…Akijiandaa kupiga mpira ulio mbele yake kuashiria rasmi shughuli ya uzinduzi huo.


Meneja Masoko  wa StarTimes, David , akielezea namna watakavyofanikisha zoezi la urushaji matangazo yote ya kombe hilo.


Meneja Maudhui wa StarTimes, Zamaradi Nzowa (wa kwanza kushoto) akiwatambulisha rasmi wasanii hao kuwa mabalozi wao.


Wasanii wakiwa kwenye picha na baadhi ya viongozi wa StarMedia.


Baadhi ya wanahabari waliohudhuria shughuli ya uzinduzi huo wakichukua matukio mbalimbali.



KAMPUNI ya StarMedia, imetoa shavu la ubalozi kwa staa wa filamu Bongo. Wema Sepetu na wenzake, ambapo atakuwa na kazi ya kuhamasisha baadhi ya watu kuhakikisha wanafuatilia matangazo ya Kombe la Dunia, litakapoanza Juni 14 mwaka huu nchini Urusi.



Wema ataungana na baadhi ya wasanii kama Madee, Kitale, Mkaliwao, Bitoke, Manifongo na Monalisa, ambao watatumia sanaa yao kufikisha ujumbe kwa wapenda soka wote ndani na nje ya nchi.



Akizungumza kwenye uzinduzi huo Meneja Masoko  wa StarTimes, David Malisa, leo alisema uzinduzi huo unaashiria rasmi harakati za mwanzo za kuonyesha kombe hilo litakaloonyeshwa kupitia Channel zake za michezo za World Football na Sports Premium kwa muda wote wa mashindano hayo huku likitangazwa kwa lugha ya Kiswahili.



Meneja Maudhui wa StarTimes,  Zamaradi Nzowa, ametumia muda kuwatangaza mabalozi wao ambao watakuwa na jukumu la kufanya kazi hiyo ya kutoa hamasa kwa muda wote wa mashindano hayo.

Hivi Nchi ni Haimuoni Jonas Mkude Au Kwakuwa Achani Nywele?- Haji Manara

$
0
0
Hivi  Nchi ni Haimuoni Jonas Mkude Au Kwakuwa Achani Nywele?- Haji Manara
Moja kati ya mashabiki wa wakubwa wa kiungo wa Simba Jonas Mkude ni afisa habari wa Simba Haji Manara ambaye mara nyingi amekuwa akipenda kupost picha ya mchezaji huyo na kusifia uwezo na ubunifu wa mchezaji huyo awapo uwanjani, leo Haji Manara kupitia instagram account yake amempost Mkude na kuandika

“Leo nimekaa nikajiuliza swali moja gumu, kisha nikakosa majibu…hivi nchi hii haimuoni @jonasmkude20? tatizo ni nini au hilo jina Mkude limekaa kiluguru sana au kwa kuwa hachani nywele?huyu jamaa amezaliwa midfielder na kwa sasa hakuna mbadala wake kwenye nchi hii ya JPM…please tuwe serious jamani na vipawa vya watu 🙏🙏”>>>Haji Manara

Liverpool Yatinga Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya

$
0
0
Liverpool Yatinga Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya
Liverpool wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya AS Roma ya Italy.

Liverpool imetinga hatua hiyo baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-2 ugenini, lakini inasonga mbele kufuatia ushindi wa 5-2 katika mechi ya mkondo wa kwanza ikiwa nyumbani.

Liverpool imejipatia mabao yake kupitia kwa Sadio Mane pamoja na Wijnaldum, hivyo imekuwa tiketi ya kukutana na Real Madrid kwenye fainali huko Kiev.

Madrid ilikuwa ya kwanza kuingia hatua ya fainali kufuatia kuiondosha Bayern Munich kwa idaidi ya mabao 4-3.

         
ROMA XI: Alisson 6.5; Florenzi 6, Manolas 5, Fazio 5, Kolarov 6; Pellegrini 4 (Under 53, 5.5), De Rossi 6 (Gonalons 70, 5), Nainggolan 6.5; Schick 5, Dzeko 7, El Shaarawy 6 (Antonucci 75, 5).

Subs not used: Skorupski, Jesus, Peres, Gerson.

Goals: Milner(OG) 15; Dzeko 53; Nainggolan 86, 90+3(pen).

Bookings: Florenzi, Manolas, Nainggolan.

Manager: Eusebio Di Francesco.

LIVERPOOL XI: Karius 6.5; Alexander-Arnold 5 (Clyne 90), Van Dijk 7, Lovren 6, Robertson 6.5; Wijnaldum 7, Henderson 7.5, Milner 7; Salah 6.5, Firmino 7.5 (Solanke 86), Mane 8 (Klavan 83).

Subs not used: Mignolet, Moreno, Ings, Woodburn.

Goals: Mane 9, Wijnaldum 25

Bookings: Lovren, Solanke.

Manager: Jurgen Klopp.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images