Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Simba Kiboko Wamchomoa Dida Yanga Wampa Mkataba wa Miaka Miwili

$
0
0
Simba Kiboko Wamchomoa Dida Yanga Wampa Mkataba wa Miaka Miwili
HII ni habari njema kwa mashabiki wa Simba, ni kwamba leo kipa wa zamani wa Yanga, Deogratius Muni­shi ‘Dida’ anasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba.



Dida awali aliwahi kuwa kipa wa Simba, akaondoka na kwen­da Yanga na baadaye akakimbil­ia Afrika Kusini ambapo alijiunga na timu ya Tucks ya nchi hiyo, ambapo taarifa zilisema kuwa hakuwa anapata nafasi ya kuto­sha ya kucheza.



Hata hivyo, hivi karibuni kipa huyo alitua hapa nchini na taari­fa kusema kuwa anajiunga na timu ya Yanga, Championi likamtafu­ta na ku­zungumza naye ambapo aligoma katakata, lakini habari ambazo tumezi­pata ni kwamba anasaini kuichezea Simba leo.



Chanzo cha ndani cha uhakika kutoka kwenye uon­gozi wa Simba, kimese­ma kuwa Dida atasaini mkataba wa miaka miwili leo ikiwa ni siku moja tu baada ya Meddie Kagere na Pascal Wawa kutua kwenye kikosi hicho cha Msim­bazi.



“Taarifa ni kwamba saa chache zijazo au kesho asubuhi Dida atasaini mkataba wa kuitu­mikia Simba, bado haijafahami­ka ni miaka mingapi kwa kuwa inafanywa siri lakini haiwezi kuwa chini ya miwili kwa kuwa mwenyewe alitaka hivyo.



‘’Analetwa ili kumpa upinzani Aishi Manula na inaonekana kuwa Said Mohammed ‘Nduda’ atapelekwa kwa mkopo kwa msimu ujao kwa kuwa Simba wanaamini kuwa ni kipa mzuri lakini majeraha ndiyo yalimsum­bua msimu uliopita,” kilisema chanzo hicho ambacho kipa karibu na benchi la ufundi la timu hiyo.



Zipo Kampuni Nimefanya Kazi, Mikataba Ninayo Wamekimbia na Hela Zangu- Mzee Majuto

$
0
0
Zipo Kampuni Nimefanya Kazi, Mikataba Ninayo Wamekimbia na Hela Zangu- Mzee Majuto
 Staa mkongwe kwenye tasnia ya uigizaji nchini Mzee Majuto ambaye alikuwa nchini India kwaajili ya matibabu na amerejea nchini baada ya kumaliza matibabu.

Moja ya jambo ambalo ameliongelea King Majuto ni kuhusiana na kampuni ambazo aliwahi kufanya nazo kazi za matangazo na hawakumlipa anavyostahili au walivyokubaliana.

Mzee majuto amesema kuwa japo ana hela nyingi ambazo amezulumiwa kwa baadhi ya watu aliofanya nao kazi yeye ameawasamehe japo kuna hela nyingi zipo mikononi mwa watu na hawana mpango wa kulipa.

"Nimeletwa duniani kwaajili ya kuwachekesha watu na sio kuwapa laana watu kwahiyo nimewasamehe wote ambao wamenidhulumu pesa zangu mungu atawaonyesha hapa hapa duniani" Mzee Majuto.

Mahakama Yafuta Hukumu ya Mwanamke Aliyemuua Mumewe

$
0
0
Mahakama Yafuta Hukumu ya Mwanamke Aliyemuua Mumewe
Mahakama ya rufaa nchini Sudan imefutilia mbali hukumu ya kifo dhidi ya mwanamke ambaye alimuua mumewe baada ya madai kwamba alimbaka , wakili wake amesema.

Noura Hussein mwenye umri wa miaka 19 badala yake alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela , wakili wake Abdelaha Mohamad alisema.

Mamake, Zainab Ahmed, aliambia BBC kwamba anafurahia kwamba maisha ya mwanawe yaliokolewa.

Watu maarufu wa kimataifa waliunga mkono kampeni ya mtandaoni, #JusticeforNoura,{ haki kwa Noura} iliotaka aachiliwe huru.

Mwezi uliopita, mahakama ya Kiislamu ilikuwa imemuhukumu kifo kwa kumnyonga , baada ya kukiri kumuua mumewe Abdulrahman Mohamed Hammad.

Bi Hussein alisema kuwa mumewe aliwatumia binamu zake ambao anadai walimshikilia kwa nguvu huku akimbaka.

Alipojaribu kurejelea kitendo hicho siku iliofuata alimdunga kisu hadi kufa.

Bi Hussein alilazimishwa kufunga ndoa akiwa na umri wa miaka 16. Mumewe ambaye alikuwa binamu yake alikuwa mkubwa wake kwa miaka 16 .

Kulingana na ripoti ya 2017 ya Umoja wa Mataifa kuhusu shirika la watoto Unicef, thuluthi moja ya watoto wa Sudan huolewa kabla ya kufikisha miaka 18.

Congo na Somalia ni miongoni mwa nchi kumi hatari kwa wanawake
Katika taarifa yake, shirika la haki za kibinaadamu la Amnesty International, lilitaja uamuzi huo kuwa habari nzuri, lakini likasema kuwa kifungo cha miaka mitano jela ni adhabu isiostahili.

Limeitaka nchi hiyo kufanyia marekebisho sheria zake kuhusu ndoa, ubakaji katika ndoa ili waathiriwa wasiadhibiwe.


Watanzania Wawili Wanyakua Tuzo za Malikia Elizabeth

$
0
0
Watanzania Wawili Wanyakua Tuzo za Malikia Elizabeth
Vijana wawili kutoka Tanzania wametwaa tuzo ya Malkia Elizabeth ya viongozi vijana, ambayo hutolewa kwa vijana wenye uwezo wa kubadilisha jamii katika nyanja za kijamii, kielimu na utamaduni na kuleta maendeleo kupitia kazi zao.

Alice Magaka na Isaya Yunge, wameiwakilisha Tanzania katika tuzo hizo ambazo hafla yake imefanyika jijini, London nchini Uingereza, huku lengo lake likiwa ni kuona na kutambua namna vijana wanavyofanya kazi za kuzibadili jamii wanazotoka katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii na utamaduni.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyokutanisha vijana kutoka mataifa 38 yaliyo katika jumuiya ya madola, Malkia Elizabeth amesema kuwa tuzo hizo ni kwa ajili ya kutambua na kuthamini uwezo wa vijana wanaoweza kufanya vitu vikubwa katika jamii, wakiwa na umri mdogo.

“Vijana hawa tunawapa tuzo hizi ili kuamsha hamasa kwa vijana wengine kujitolea katika jamii, kubadili mitazamo hasi, kuleta mafanikio chanya na kukuza uchumi usiokuwa tegemezi katika mataifa yao”, amesema Malkia Elizabeth.

Alice amepokea tuzo hiyo kupitia  kwa kazi anayofanya ya kuelimisha wasichana kuhusu usafi wakati wa hedhi na kutoa huduma ya kugawa taulo za kike kupitia kampeni anazofanya ili kupata michango kutoka kwa jamii, huku Isaya amepokea kwa ugunduzi wa  programu ya simu, SomaApp, programu ya simu ambayo inasaidia kurahisiaha usomaji kwa wanafunzi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

AS ROMA Yashindwa Kuficha Hisia Zake kwa Nigeria

$
0
0
AS ROMA Yashindwa Kuficha Hisia Zake kwa Nigeria
Hapo jana usiku timu ya taifa ya Nigeria iliyaaga mashindano ya michuano ya kombe la dunia nchini Urusi baada ya kutolewa na Argentina kwa jumla ya mabao 2 – 1 matokeo yaliyoacha simanzi kwa Waafrika na hata wasiyo wa bara hilo waliyokuwa na mapenzi mema na The Super Eagles.



Kabla hata ya michuano hiiyo kuanza klabu ya AS ROMA ya Italia ilionyesha mapenzi yake ya wazi dhidi ya miamba hiyo ya Afrika na kuitabiria makubwa kwenye kombe hilo.

Baada ya kutolewa na Argentina klabu ya AS ROMA kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter imeandika ujumbe kuwa inajiskia vibaya kupata matokeo mabaya Super Eagles.

Ni huzuni, hii ni kwa wote Super Eagle na mashabiki wake wenye hisia, ilikuwa na jezi nzuri zaidi, kupitia Nigeria tumetengeneza marafiki wengi zaidi wapo watakao baki nasi na wapo ambao wataondoka lakini tunaimani ipo siku moja tutaonana Roma ama kuwatembelea Lagosi.



Kabla ya mechi ya Nigeria dhidi ya Argentina AS Roma iliibashiria The Super Eagle kushinda kwa asilimia 44.

Najuana na Daimond Muda Mrefu Kabla ya Zari- Huddah

$
0
0
Najuana na Daimond Muda Mrefu Kabla ya Zari- Huddah
Mrembo kutokea pande za  Nairobi nchini Kenya, Huddah Monroe amesema hakuna chochote kinachoendelea kati yake na Diamond Platnumz.

Mrembo huyo amelazimika kuzungumzia hilo mara baada ya kuonekana kutokuwa karibu zaidi na aliyekuwa mpenzi wa Diamond, Zari The Boss Lady kama hapo awali.

“Lakini yote yanapita , watu wanaongea sana, ooh! Huddah ana kitu na Diamond, kitu ambacho wanadanganya mwisho wa siku. Mimi na Diamond tumekutana muda mrefu kabla ya kukutana na Zari,” Huddah ameiambia Wasafi TV.

Huddah ameendelea kwa kusema kuwa yeye na Zari walikuwa karibu sana na alikuwa akimueleza vitu vingi sana vya vyake na endeapo angetaka kuvieka kwenye mitandao angeweza lakini hawezi kutokana ni rafiki nzuri.

Nuh Mziwanda Bado Alikupuka Penzi la Shilole "Mwanamke Pekee Aliyenifundisha Maisha Sitofuta Tatoo Yake"

$
0
0
Nuh Mziwanda Bado Alikupuka Penzi la Shilole "Mwanamke Pekee Aliyenifundisha Maisha Sitofuta Tatoo Yake"
Msanii wa muziki wa Bongo fleva, Nuhu Mziwanda amefunguka kuwa aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Shilole ni mwanamke pekee aliyemfundisha maisha na majukumu akiwa kama mtoto wa kiume.

Nuh amefunguka hayo kupitia DADAZ ya East Africa Television, ambapo amesema kuwa mwanadada huyo ndiye aliyekuwa mpenzi wake wa kwanza aliyemzidi  umri na tayari alikuta akiwa mwenye familia.

“Shilole ndio mwanamke wangu wa kwanza aliyekuwa kanizidi umri, na amenifundisha majukumu na maisha pia baba anatakiwa kuwa vipi ndio chanzo cha mimi kuchora ‘tatoo’ ya jina lake mkononi kwangu hata tulipoachana sikuwahi kuifuta kwakuwa itabaki kuwa sehemu ya maisha yangu”, amesema Nuh.

Nuh na Shilole waliachana na baada ya muda msanii huyo alifanikiwa kufunga ndoa na mwanadada Nawal aliyefanikiwa kupata nae mtoto mmoja na baadaye waliachana pia.

Kumbe Zari Hana Namba ya Simu ya Daimond Mwenye Atoboa Siri

$
0
0
Kumbe Zari Hana Namba ya Simu ya Daimond Mwenye Atoboa Siri
Ni takribani miezi mitano sasa tangu Zari The Boss Lady aachane na Diamond Platnumz, je, mrembo huyo anam-miss mazazi mwenzie?.

Jibu ni hapana, Zari ameeleza kuwa si kum-miss pekee, bali hata namba ya Diamond hana kwa sasa. Katika ukurasa wa Instagram wa mwanae, Tiffah Zari ndipo ameeleza hilo alipomjibu shabiki.

Shabiki huyo alieleza; Believe that Zari is missing his ex-hubby. Hii ni baada ya caption iliyokuwepo kwenye picha ya Tiffa iliyosema; How i wait for my papa to call.

Ndipo Zari The Boss Lady akaamua kujibu hilo.

“But I don’t have his number incase I missed him, I don’t have to express it through my daughter’s account. Don’t project your behavior on me” alieleza Zari.

Utakumbuka February 24, 2018 ndipo Zari alitangaza kuachana na Diamond Platnumz. May 31, 2018 ambapo Diamond alitoa wimbo wake ‘Iyena’, Babu Tale alifunga safari hadi Afrika Kusini kuhakikisha wawili hao wanarudiana. Hata hivyo June 11, 2018 Zari alieleza kuwa wamekubaliana watashirikiana kama wazazi katika kulea watoto wao na si vinginevyo.

Kutana na Maalim Fadhili Rashid ni Mtaalam wa Tiba za Asili

$
0
0

KUTANA NA MAALIM FADHILI RASHIDI NI MTAALAM WATIBA ZA ASILI JE? UMEACHWA NAMPENZI WAKO? JE? NA HAUJUI NAMNA YA KUMRUSHA?

MAALIM FADHILI RASHIDI HURUDISHA MAHUSINO NA MPENZI WAKO ALIE KUACHA NDANI YA MASAA (72) TU MUONE HARAKA AKUSAIDIE, ACHA KUTESEKA NA MAPENZI

MAALIM FADHILI RASHIDI NI BINGWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUUKUUMA NAKUWAKA MOTO, PRESHA, KISUKARI, VIDONDA VYATUMBO, PUMU,

TEZI NA UVIMBE TUMBONI, ANA UWEZO WAKURUDISHA MTU ALE POTEA KIMAZINGIRA (MSUKURE), KUMFANYA MKE/ MUME/ MPENZI ASIKUSALITI, DAWA YA ( LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA,

KUMUONA MBAYAWAKO LIVE KWA SABABU MAALUMU, ANATOWA PETE YA BAHATI NA KUMILIKI MALI ZA MAJINI, DAWA YA UZAZI, KUSHIKA UJAUZITO NDANI YA SIKU (14) TU

DAWA YA KUONGEZA UUME SAIZI UPENDAYO, DAWA YA NGUVU ZA KIUME, PIA ANAYO DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEPU KUWA NA UMBO BOMBA,
KAMA UMEIBIWA AMA KUDHULIMIWA UTARUDISHIWA MALI YAKO NDANI YA MASAA (72) TU, ANAFUNGA KESI NAKUPATA HAKI YAKO, MVUTO WA MAPENZI NA BIASHARA, KUUZA MALIYAKO KWA HARAKA

KUZUIYA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, KUSAFISHA NYOTA NA KUTOWA MIKOSI, KUPANDISHWA CHEO KAZINI, ACHAKUHANGAIKA MAALIM FADHILI RASHIDI NDIO MKOMBOZI WAKO

CALLING +255 7193628 06/ +255 763276239/
WHATSAPP IMO +255 785786436

Huddah Monroe Ataja Kinachowafanya Wanaume Wasibanduke Kwake

$
0
0

Mrembo kutokea nchini Kenya, Huddah Monroe  amefunguka kitu ambacho kinavutia wanaume kutoka kwake.


Mrembo huyo ambaye alikuwa hapa nchini hivi karibuni, katika mahojiano na Wasafi TV amesema tabasamu lake ndilo linavutia wanaume wengi.


“Which part on my body wanaume wengi wapo attractive is….., I think is my smile,” amesema Huddah.


June 17, 2018 katika show ya Harmonize ‘Kusi Night’, Huddah ni miongoni mwa wale waliotoa burudani ya aina yake. Alipanda jukwaani na kucheza ngoma ya Diamond ‘ African Beauty’ kitu kilichoibua shangwe la aina yake.

JeWajua - Wajerumani hawajawahi kutolewa kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Dunia, Je leo?

$
0
0

Germany 🇩🇪 vs South Korea 🇰🇷 .
South Korea 🇰🇷 watakuwa bila ya nahodha wao Ki Sung-yueng, ambaye amepata majeruhi kwenye misuli ya nyuma ya mguu.
Coach Shin Tae-yong anafahami timu yake inahitaji ushindi na hivyo lazima achague timu ambayo itacheza mchezo wa kushambulia zaidi.
.
Germany watakuwa wanamkosa Jerome Boateng ambaye ana kadi nyekundu aliyoipata vs Sweden, lakini beki mwenzie wa Bayern Mars Hummels yupo fiti kurejea kikosini baada ya kuukosa mchezo uliopita.
.
Midfielder Sebastian Rudy hatocheza leo baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa pua baada ya kuumizwa katika mtanange vs Sweden.
.
Nini wanahitaji Ujerumani ili kufuzu
.
Joachim Low na vijana wake wanahitaji ushindi ili kutimiza pointi 6 huku wakiiombea Sweden ipate matokeo yoyote ambayo hayatowazidi kitakwimu zozote.
:
#Takwimu: Mechi mbili kati ya 3 baina ya timu hizi zimechezwa katika World Cup - Wajerumani wakishinda zote mbili (3-2 mwaka 1994 & 1-0 mwaka 2002). Ushindi pekee wa South Korea dhidi ya Ujerumani ulikuwa katika mchezo wa kirafiki mwaka 2004.

Habari Njema Kwa Wanaume Wote Wenye Matatizo ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0

Je unawahi hufika mapema kileleni? Je uume wako hausimami imara ipasavyo? Je hupati hamu ya kurudia tendo la ndoa? Je unamaumbile madogo ya uume?

Sasa ipo tiba sahihi inayomaliza kabisa tatizo la nguvu za kiume na maumbile madogo kwa wakati.

- NGAKWA ni dawa bora ya asili inayotibu tatizo la nguvu za kiume nakulimaliza kabisa bila tatizo tena kujirudia.

- NKOMA ni dawa ya asili inayokuza na kunenepesha maumbile ya uume yaliyo madogo au kusinyaa kabisa wastani (Inch 6-7)

- Pia tunatibu matatizo mengine ya mfumo wa uzazi kwa mwanaume na mwanamke kama Ngiri, Kuvimba Korodani, Kushika au Kutia mbimba, Fangasi Sugu, Uvimbe kwenye kizazi Nk.

Dr FARU anapatikana Buguruni Dar es salaam, Piga Namba - 0755996494

HUDUMA ITAKUFIKIA POPOTE PALE ULIPO.

Tarimba Aishtumu Simba "Wanasubiri Tutaje Wao Wasajili"

$
0
0
Tarimba Aishtumu Simba "Wanasubiri Tutaje Wao Wasajili"
Mwenyekiti wa kamati ya kuisaidia klabu ya Yanga kuvuka katika kipindi hiki cha mpito, Abbas Tarimba amesema kuwa watani wao wa kihistoria Simba hawana uwezo wa kung’amua vipaji vipya katika Soka na kuvisajili

Huo ni mfululizo wa kauli mbalimbali za viongozi wa klabu hiyo kuhusu namna ambavyo watani wao wanavyosajili wachezaji wenye majina makubwa ambao awali walikuwa wanawaniwa na klabu yao, ambapo Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa aliwahi kukaririwa akisema baadhi ya vilabu vya ligi kuu vinatumia listi ya wachezaji ambao wao wamewaorodhesha kuwahitaji kwa kupitia mlango wa uwani na kuwasajili.

“Simba wamekuwa wakisubiri sisi tutaje wachezaji ambao tunawahitaji kuwasajili ili wao waje na kuwasajili kupitia mlango wa uwani jambo ambalo mimi naliona ni kukosa watu wazuri wa kusaka vipaji “.Alisema Tarimba.

Tarimba ameyasema hayo baada ya watani wao kumsajili mshambuliaji wa Gor Mahia, Meddie Kagere ambaye awali Yanga ilihusishwa kutaka kumsajili ili kuimarisha kikosi chake kuelekea katika michuano ya kombe la Shirikisho la Afrika na msimu mpya wa Ligi Kuu.

Mchezaji huyo aliyesajiliwa na Simba aling’ara katika michuano ya SportPesa Super Cup akiwa na klabu ya Gor Mahia ambapo aliibuka mfungaji bora wa michuano hiyo na kuzivutia klabu kadhaa Tanzania zikiwemo Simba na Yanga.

Katika siku za hivi karibuni, Abbas Tarimba aliwahi kuzungumza kuwa yeye na kamati yake watakuwa wanafanya usajili wao kimyakimya ili kuwaficha watani wao wasiweze kujua ni wachezaji gani wamewasajili.

15 Mbaloni kwa Wizi kwa Njia ya Ujumbe Kwenye Simu

$
0
0
15 Mbaloni kwa Wizi kwa Njia ya Ujumbe Kwenye Simu
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limeawakamata watu 15 akiwemo Lule Lusale (35) mkazi wa Rgani Ng’ambo na wenzake kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa mitandaoni kwa njia ya kuwatumia watu mbalimbali ujumbe mfupi wa simu wakitaka wawatumie pesa haraka, simu 45, kadi 352 za simu, vitambulisho na komputer mpakato (laptops) zipatazo 5.

Akizungumza na wanahabari, Kamanda wa Oparesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi, Liberatus Sabas amesema watuhumiwa hao wamekamatwa jijini Dar es Salaam na wengine mkoani Rukwa ambapo baada ya kufanyiwa upelelezi wamekiri kuhusika na matukio ya wizi huo ambao kwa sasa umesambaa mitandaoniu na kusema wamekuwa wakitumia mfumo wa Bulk SMS ambao unawawezesha kutuma jumbe zaidi ya 10,000 kwa wakati mmoja.

“Baada ya lkupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, jeshi letu lilianza uchunguzi na kuwabaini watuhumiwa hao ambao wamekamatwa, walikuwa wakituma jumbe zinazosomeka kama ifuatavyo.

Ujumbe wa kwanza; “Nitumie hiyo hela katika namba hii”, ujumbe wa pili; “Namba ile ya awali ina matatizo, nitumie sasa hiyo hela katika namba hii,” Ujumbe wa tatu; “Namba ile ya wawai ina matatizo, sasa nitumie hivi”, ujumbe wa nne; ” Mganga wa jadi, msamalia, Je, unasumbuliwa na magonjwa sugu, ndoa, pesa na majini? Pete, kusafisha nyota wasiliana na namba 074213……. huduma itakufata popote ulipo” hawa wote walikuwa ni matapeli,” amesema Sabas.

Rais wa Zanzibar Kutua Nchini Kesho kwa Dhiara ya Siku Mbili

$
0
0
Rais wa Zanzibar Kutua Nchini Kesho kwa Dhiara ya Siku Mbili
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangangwa ambaye anatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Hii ni ziara ya kwanza kwa Rais Mnangangwa kuja nchini tangu aingie madarakani mwezi November mwaka jana.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inasema lengo la ziara hiyo ni kujitambulisha kwa Rais John Magufuli na wananchi wa Tanzania.

Rais Mnangangwa atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais John Magufuli na pia kutembelea chuo cha sanaa cha Kaole Bagamoyo ambacho awali kilitumika kutoa mafunzo kwa wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa bara la Afrika na yeye akiwa ni mmoja wapo aliyepata mafunzo katika chuo hicho.

Mbowe na Wenzake Wawasilisha Maombi Mahakamani Kusitisha Kesi Yao

$
0
0
Mbowe na Wenzake Wawasilisha Maombi Mahakamani Kusitisha Kesi Yao
Viongozi 9 wa CHADEMA, akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe kupitia wakili wao wamewasilisha maombi chini ya hati ya dharura ya kutaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu isitishe usikilizaji wa kesi yao ya kufanya maandamano.

Maombi hayo yanayotarajiwa kusikilizwa June 28, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri yamewasilishwa na wakili utetezi, Peter Kibatala.

Katika maombi hayo namba 15/2018 upande wa utetezi umedai kuwa wanaomba usikilizwaji wa kesi hiyo usitishwe hadi pale Mahakama Kuu itakapoyapitia maamuzi yote yaliyotolewa na Mahakama ya Kisutu kuhusu kesi hiyo.

Naye Wakili wa serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ameiambia mahakama kuwa wamepokea nakala ya maombi hayo, hivyo wanaomba kuwasilisha majibu yao ya hati kinzani kesho June 28, 2018.

Awali wakili Nchimbi alieeleza mahakama kuwa kesi hiyo imeitishwa ili washtakiwa wasomewe maelezo ya awali (Ph).

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri ameiahirisha kesi ya msingi hadi July 2,2018.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.

Katibu wa chama hicho Dk.  Vicenti  Mashinji, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Tarime mjini Esther  Matiko na  mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

Katika kesi hiyo namba 112 ya mwaka 2018 Mbowe na wenzake hao wanaokabiliwa na mashtaka 13 ikiwamo ya kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi wa uasi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai.

Makosa hayo  yanadaiwa kutendeka Februari 16,2018 katika maeneo ya viwanja vya buibui, Mwananyamala na  barabara ya Kawawa kinondoni mkwajuni

Watanzania Waliokamatwa kwa Uvuvi Haramu Kenya Waachiwa

$
0
0
Serikali imesema Watanzania 109 waliokamatwa hivi karibuni kwa madai ya kufanya uvuvi haramu Bahari ya Hindi, upande wa Kenya wamepata dhamana na kurejea nchini.

Hata hivyo, bado Serikali za pande zote mbili zinaendelea kufanya mawasiliano jinsi ya kulishughulikia suala hilo.

Wavuvi hao walikamatwa eneo la Shimoni, linalomilikiwa na bandari Kusini Mashariki mwa Kenya karibu na mpaka wa Tanzania na kufikishwa mahakama ya Kaunti ya Kwale mwanzoni wa mwezi huu.

Walizuiliwa baada ya kushindwa kulipa dhamana ya Ksh20,000 (sawa na zaidi ya Tsh 450000) kila mmoja.

Tangu wakati huo Serikali ya Tanzania imesema imeanza harakati za kuhakikisha kuwa raia hao wanaachiwa huru.

Akizungumza na gazeti hili leo Juni 27, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Susan Kolimba amesema raia hao waliachiwa na kurejea nyumbani.

“Tayari waliachiliwa baada ya kupewa dhamana wakati mawasiliano ya kiserikali yakiendelea,” amesema naibu waziri huyo kifupi.

Hata hivyo, hakuwa tayari kutaja tarehe waliyoachiwa  zaidi ya kusisitiza kuwa Serikali inaendelea kujadiliana na Kenya.

Kiir na Machar Kutiliana Mkataba wa Makubaliano ya Amani

$
0
0
 Kiir na Machar Kutiliana Mkataba wa Makubaliano ya Amani
Rais wa Sudan kusini Salva Kiir na Kiongozi wa waasi Riek Machar wanatarajiwa kutia saini makubaliano waliyoyafanya siku ya Jumatatu, kufikisha mwisho miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenye nchini humo.

Wawili hao walikutana siku ya Jumatatu mjini Khartoum ambapo walifanya mazungumzo na kukubaliana baadhi ya maeneo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Sudan Al-Dirdiri Mohamed Ahmed amesema maeneo yaliyofikiwa makubaliano yatatangazwa baadaye leo, viongozi hao watakapokutana.

Mchezaji wa Swansea City Avutiwa na Wimbo wa Chura wa Snura

$
0
0
Mshambuliaji wa klabu ya Swansea City, Wilfried Bony amefunguka kuwa anaupenda wimbo wa Chura wa Snura huku akisifia baadhi ya waigizaji filamu hapa Bongo.

Bony ambaye yupo nchini Tanzania akizungumza na Waandishi wa Habari leo Juni 27, 2018 jijini Dar es salaam, amesema kuwa wimbo wa Chura ni wimbo mzuri kusikiliza na video yake inavutia kuitazama hususani kwa wanaume kwani ina wanawake wanaocheza vizuri wimbo huo.

Hata hivyo, wimbo wa Chura mwaka 2016 ulifungiwa na serikali kwa kosa la kukiuka maadili ya Mtanzania rejea kwenye hii link na video hapo chini (Serikali yaufungia wimbo wa Snura ‘Chura’).

Alichokisema Casto Endapo Tunda Naye Atachora Tatoo

$
0
0
Alichokisema Casto Eandapo Tunda   Naye Atachora Tatoo
Mara baada ya kuchora tattoo ya mpenzi wake Tunda, Mtangazaji wa kipindi cha Siz Kitaa kinachoruka Clouds TV, Casto Dickson amefunguka iwapo Tunda naye atafanya hivyo.

Casto amesema hadi kufikia hatua hiyo kuna jambo la tofauti baina yao na iwapo Tunda atafanya hivyo watu wataona.

“Utamuona akichora, kama akichora utamuona akichora, ana maamuzi yake, yeah!. Kwa sababu kuchora tattoo si pete sisi tumeanza hivi tuna sababu zetu,” amesema.

“Tuna maana yetu ambayo itakuja kuwa tofauti kabisa, for the first time in Africa tuseme, mtakuja kuona, yeah!,” Casto ameiambia Bongo5.

Mtangazaji huyo ameongeza kuwa hataki kuliweka suala hilo kuwa siku wakiachana atafuta hiyo tattoo na kueleza kwa upande wake hamna kitu kama hicho. Casto Dickson na Tunda mapenzi yao yalianza kugonga vichwa habari March 2018 pale walipoyaweka wazi.
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images