Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Jose Chameleone Amtumiaia Barua Nzito Rais Museveni Baada ya Kumkamata Bobi Wine "Kukosolewa ni Changamoto za Uongozi’'

$
0
0
Jose Chameleone Amtumiaia Barua Nzito Rais Museveni Baada ya Kumkamata Bobi Wine "Kukosolewa ni Changamoto za Uongozi’'
Msanii mkongwe wa muziki nchini Uganda, Jose Chameleone amemuandikia barua Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni wa kumuomba amsamehe rapa Bobi Wine ambaye pia ni Mbunge wa chama cha upinzani nchini humo.

Katika barua hiyo, Chameleone amesema Rais Museveni ni kama baba wa taifa hilo na anapaswa kuwa na roho ya kusamehe kama vitabu vitakatifu vinavyosema huku akisistiza kuwa masuala ya kupishana kiitikadi kwenye siasa ni  changamoto tu kwenye kazi yasijenge uadui.



Letter to His Excellency President of the republic of Uganda.
Dear President,
Seeking appointment or going through protocol will not deliver my urgent letter to you.

Right now I hope we all rather can let it be a temporary political mishap per what happened in the district of Arua on Monday. Unfortunately it left you car Vandalized,Many of us inconvenienced – A soul lost, And another Ugandan,brother, Friend,Fellow singer Honourable as appointed by Kyadondo east-Robert Kyagulanyi alias Bobi Wine and many counterparts in an unfortunate situation. Honourable Kyagulanyi has always collaborated with me and all of us society to free Uganda from
Foreign sounds,Sell our culture beyond borders through our capital ability – Music.
Bobi Wine has over time exhibited his leadership admiration. Just Like any young ambitious man, he has treaded a path of aggressiveness.
Your excellency,Our brother, Your son Bobi Wine could have gone wrong on execution of some of his ideologies. That’s a challenge .

As head of state and forefather, It’s a great one too to lead us in example of forgiveness and reconciliation as that is one of the prime problems that have hindered our society.We are so unforgiving.
I as a son of this nation on behalf of the slogan. “For God and my Country” With all honour beg you the President to symbolise forgiveness in such a time. We can all wrong but better the forgiver.Mr President, You are a Father,Parent and always forgiving one.We shall all remain calm and be hopeful that the coming developments will see us all live harmoniously and have a peaceful country henceforth.
JOHN: 8:7
Dialogue is the answer
For God and my country
🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬🇺🇬

Jose Chameleone.

Chameleone ameandika barua hiyo ikiwa ni siku chache zimepita tangu maofisa wa polisi mjini Arua wamkamate Rapa Bobi Wine kwa tuhuma za uchochezi kwenye kampeni za ubunge zinazoendelea mjini humo.

Siku ya Jumatatu Wakazi wa Arua waliupiga mawe msafara wa rais Museveni wakidai kuwa amelituma jeshi la polisi kumuua dereva wa Bobi Wine.

Mpaka sasa familia ya Bobi Wine inalalamika kwamba haijui sehemu aliyoko Mbunge huyo wa jimbo la Kyadondo Mashariki.

Jose Chameleone amemsihi Museveni kumuachilia huru Bobi Wine japo amekiri kuwa Bobi alifanya makossa, “Kwa heshima kuu nakuomba umsamehe Bobi Wine. Kila mtu anaweza akafanya kosa na hakuna kosa ambalo haliweza likasameheka”

Kulingana na taarifa za polisi ni kwamba Bobi Wine anapokea matibabu japo familia yake inadai kuwa Mbunge huyo alikuwa buheri wa afya wakati alipokamatwa.

Zamaradi Ajibu Tuhuma za Kushinikiza Dina Marious Kufukuzwa Kazi Clouds FM ‘Dina ni Mke Mwenzangu?’

$
0
0
Zamaradi Ajibu Tuhuma za Kushinikiza Dina Marious Kufukuzwa Kazi Clouds FM ‘Dina ni Mke Mwenzangu?’
Mkurugenzi wa vipindi Wasafi TV, Zamaradi Mketema amefunguka kwa mara ya kwanza tuhuma anazozushiwa kuwa kipindi anafanya kazi Clouds Media Group alihusika kushinikiza uongozi wa kampuni hiyo kumfanyia figisu figisu hadi kuachishwa kazi aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena, Dina Marious.



Zamaradi amekataa katu katu kuwa hakuwahi kuhusika na chochote ila ni watu tu wanaoeneza maneno ya uongo na hata Dina Marious mwenyewe anajua ukweli wenyewe kilichomuondoa Clouds FM.

Kesi ya Tido Mhando Yazidi Kukwama Mahakamani

$
0
0
Kesi ya Tido Mhando Yazidi Kukwama Mahakamani
Kesi inayomkabili  Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando imepigwa kalenda tena hadi Agosti 27, 2018 ambapo mashahidi wa upande wa Mashitaka wataendelea kutoa ushahidi wao.

Kesi hiyo ilipaswa kuendelea kusikilizwa leo Alhamisi Agosti 16, 2018 lakini wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai ameieleza mahakama kuwa hawana shahidi na akaomba kesi ipangiwe tarehe nyingine ili iendelee kusikilizwa.

Hata hivyo, Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Kelvin Muhina amesema Hakimu Mkazi Mkuu, Huduma Shaidi anayeiendesha kesi hiyo anaumwa na kupanga tena tarehe hiyo.

Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Aamuru Wananchi wa Kijiji Kizima Wakamatwe na Kuwekwa Ndani

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Aamuru Wananchi wa Kijiji Kizima Wakamatwe na Kuwekwa Ndani
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwasweka ndani wananchi wote wa Kijiji cha Ngole kilichopo Kata ya Ilungu wilayani Mbeya kwa kosa la kuharibu mradi wa maji wa kijiji jirani cha Msheye.

Wananchi hao wanadaiwa kuvamia na kuharibu mradi huo kwa kuvunja banio na kukata mabomba yaliyokuwa yametandazwa kuanzia kwenye chanzo cha maji kwenda kwenye makazi ya kijiji jirani wakitumia vifaa mbalimbali yakiwamo majembe na mapanga.

Ametoa agizo la kukamatwa wananchi hao jana wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya walioketi kupokea na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Aidha, amefikia uamuzi huo mara baada ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Mashesye, Osiah Mwakalila, kuwasilisha taarifa juu ya unyama waliofanyiwa na majirani zao, akidai kuwa pia walikuwa wanatishia kuwashambulia endapo wangeendelea kuhoji na kuwazuia kutekeleza uamuzi wao.

“Naagiza wananchi wote wa kijiji hicho wakamatwe wawekwe ndani bila kujali ana hali gani, watajieleza wakiwa ndani, haiwezekani sehemu zingine watu wanahangaika maji huku sehemu nyingine watu wanafyeka mabomba,” amesema Chalamila

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, amesema magari yameshatumwa yakiwa na askari wa kutosha kwa ajili ya kuwakamata wananchi hao.

Amesema kitendo kilichofanywa na wananchi wa Kijiji hicho ni uhujumu uchumi hivyo lazima washughulikiwe ipasavyo.

Lugola Kula Sahani Moja na Polisi Wala Rushwa

$
0
0
Lugola Kula Sahani Moja na Polisi Wala Rushwa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema hatawaonea huruma polisi watakaokamatwa wakichukua rushwa na wale wanaonyanyasa wenye magari, bodaboda na wananchi.

Lugola ambaye ni mbunge wa Mwibara, alisema anapokea taarifa mbalimbali zikilalamikia tabia za baadhi ya polisi kuwaonea wananchi wasio na makosa kwa kutumia nguvu na kuwalazimisha kuwaweka mahabusu hata kama kosa halistahili kuwekwa ndani.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Victoria, Mji mdogo wa Kisorya, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda mkoani Mara, jana, Lugola alisema atahakikisha anapambana na askari ambao wamechoka kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.

“Serikali ya awamu ya tano si ya mchezo mchezo, nawahakikishia wananchi wa hapa Kata ya Nansimo na pamoja na kote nchini, mimi Lugola sitamwangusha mheshimwa Rais Magufuli, sitawaangusha nyie wananchi, ninawaahidi hii tabia nawahakikishia kwa mara nyingine nitaimaliza,” alisema Lugola huku akishangiliwa.

Aliongeza kuwa magari na bodaboda ambazo hazina makosa, hazipaswi kubughudhiwa kwa sababu wamefuata taratibu zote za usalama barabarani.

“Kitendo cha askari akiwa na masilahi yake binafsi au ametumwa na mtu mwenye masilahi naye kwenda kukamata gari fulani au bodaboda kwa lengo la kujipatia rushwa tabia hiyo inapaswa kulaaniwa.

“Muda mwingine utakuta mwananchi mmoja ambaye ana masilahi na polisi anakamata gari au bodaboda yake na mmiliki wa chombo hicho cha moto huwekwa mahabusu na ukiuliza ‘nimefanya kosa gani’ wanakujibu ‘kaa ndani kwanza’, na ukiingia bure, lakini wanapokutoa unawapa rushwa, nalijua hilo vizuri sana, tabia hii haivumiliki, na nitahakikisha wananchi wa jimbo hili pamoja na Tanzania nzima mtakuwa salama,” alisema Lugola.

Alifafanua kuwa kuna baadhi ya polisi huwaweka mahabusu wananchi hovyo ili kuwatisha kwa lengo la kujipatia rushwa.

“Si kila kosa mwananchi awekwe mahabusu, yapo makosa ambayo polisi wanaweka mahabusu wananchi kwa mujibu wa sheria, lakini kitendo cha askari kumkamata mwendesha bodaboda akimlazimisha atoe rushwa au awekwe mahabusu hilo halitakubalika,” alisema.

Pia alisema wananchi wanapoonewa mara kwa mara kunatengeneza chuki dhidi ya Serikali, kwa sababu wanastahili kuishi katika mazingira ya amani na utulivu, hivyo tabia ya baadhi ya askari hao haiwezi kuvumilika.

“Hii tabia ya baadhi ya askari wanasema ‘injika ugali mke wangu mboga inakuja’ akielekea barabarani au mahali popote na kuanza kutafuta rushwa kwa nguvu zote kwa wenye magari, bodaboda au mazingira yoyote.

“Mimi Kangi Lugola naapa nitaisambaratisha haraka iwezekanavyo tabia hii, sitakuwa na huruma katika hilo na nitakuwa nafanya ziara ya kushtukiza ili niwakamate hao wenye tabia hiyo chafu katika nchi yetu,” alisema Lugola.

Hata hivyo, Lugola aliwataka polisi nchini kuwakamata waendesha magari na bodaboda ambao hawafuati sheria za barabarani.

Alitoa mfano baadhi ya waendesha bodaboda wanaovunja sheria kwa makusudi kwa kupakia abiria zaidi ya wane, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa dereva na abiria wake.

“Polisi wangu wengi wanafanya kazi kwa umakini na uaminifu mkubwa, ila wachache sana ndio wenye tabia hizo mbaya, nawataka askari hao wafuate sheria na pia kuendelea kuzikamata kama ni magari au bodaboda au wananchi wowote ambao wanavunja sheria za nchi,” alisema Lugola.

Aliyekuwa Rais Maskini Zaidi Duniani Akataa Malipo ya Uzeeni

$
0
0
Aliyekuwa Rais Maskini Zaidi Duniani Akataa Malipo ya Uzeeni
Aliyekua rais wa Uruguay, Jose Mujica ambaye alifahamika kama rais maskini zaidi duniani amesema hatachukua malipo yake ya uzeeni tangu aanze kuhudumu kama seneta.



Mujica aliacha kazi ya useneta siku ya Jumanne kiti ambacho amekua akishikilia tangu muda wake wa kuhudumu kama raisi ulipo kamilika mwaka 2015.

Kwa mujibu wa BBC rais huyo mstaafu alidai kuwa amechoka na hangeweza kuendelea na kazi hadi mwaka wa 2020. Muasi huyo wa zamani wa mlengo wa kushoto ana miaka 83.

Mujica aliwasilisha barua ya kuacha kazi kwa mkuu wa seneti. Alisema kwamba fikra ya kuacha kazi ni ya kibinasfi huku akiongeza kuwa ni uchovu wa safari ndefu.



Hata hivyo aliongeza kua ataendelea kuchangia hoja kwa sababu bado akili yake inafanya kazi. Mujica anayejulikana kwa matamshi yake ya kichesi aliomba msamaha kwa wenzake kwa uamuzi huo.

Mwaka 2016, alidai rais wa Venezuela Nicolás Maduro ni mwendazimu kama mbuzi. Umaarufu wake ulienea kutokana na maisha yake ya chini ya kukataa kuishi kwenye Ikulu ya rais.



Wakati akiwa rais na hata sasa yeye pamoja na mkewe ambaye pia alimsaidia katika vita vya msituni wamekua wakiishi katika shamba moja nje kidogo mwa mji wa Montevideo.

Alitoa mshahari wake kwa misaada na kile alichobaki nacho tu alipoingia ofisini mwaka wa 2010 ni gari aina ya Volkswagen Beetle la mwaka 1987.

Gari hilo lilipata umaarufu na mwaka 2014 alipewa dola milioni moja lakini akakataa huku akidai kuwa atashindwa kumbeba mbwa wake mwenye miguu mitatu.

Kuacha kazi kwa Mujica hakukupokelewa na mshangao kwa sababu alikua amedokeza kufanya hivyo mnano Agosti 3 alipofika mara ya mwisho seneti.

Wakati huo, mahasimu wake wa kisiasa walisema hawakua na uhakika ya kwamba atastaafu. Seneta Luis Alberto Heber alidai kuwa Mujica aliacha kazi ili ajipange kuwania kiti cha urais mwaka 2019 kwa mara ya pili.

Huku wenazke katika seneti wakimjalia mazuri wakosoaji waliendeleza mijdala kwenye mitandao ya kijamii wakidai aombe msamaha vitendo alivyofanya wakati akiwa mwanachama wa waasi wa Tupamaros miaka ya 1960 na 70.

Rosa Ree Awapa Makavu Wanaomsema Kuhusu Staili Yake ya Kubinua Mdomo

$
0
0
Rapper wa kike Tanzania ambae anafanya vizuri kwenye game la ndani na nje ya nchi Ambae ame hit na goma ya Marathon aliofanya na Billnas na siku mbili nyuma alisikika kwenye ngoma na Fid q inayoitwa Ole Chiza msanii Rosa Ree amedai kuwa Rapper wengine wa tanzania wakifanya vizuri yuko tayari kufanya nao kazi  ila hayuko Tayari kufanya kazi na mtu asiefanya poa.

Ameendelea kuwachana wale wanaomfatilia kuhusiana na kubinua midomo na kutoa ulimi wakati anaimba ambapo imekuwa kama ni style yake katika kila nyimbo anayotoa au kushirikishwa.

" Hawanilipii bili na kubinua kwangu midomo na kutoa ulimi sasa hivi nina super market, nimefanya kolabo na wasanii wa kimataifa zaid ya mmoja na bado nafanya vitu vikubwa mimi mawazo ya watu hazijiandiki usoni kwangu wala hazilipi bili zozote ingekuwa hela ningejali" Ameyatamka Rosa Ree

IGP Sirro Afunguka Kuhusu Mwandishi Aliyepigwa na Polisi

$
0
0
IGP SirroAfunguka Kuhusu Mwandishi Aliyepigwa na Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP ,Simon Sirro ametoa ufafanuzi juu ya Sakata la Mwandishi wa Habari aliyepigwa na polisi wakati akitekeleza majukumu yake katika Uwanja wa Taifa ulioko jijini Dar es Slaam na kusema kuwa upelelezi unaendelea kufanyika ili kubaini ukweli wa tukio hilo na kuchukua hatua stahiki za kisheria na  kulinda heshima ya jeshi la polisi.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akiwasili jijini Arusha kwa ziara yake ya kutembelea eneo la Mto wa Mbu ambapo yalitokea matukio ya wanawake kubakwa na kuuawa ,ziara ambayo inalenga kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo hayo ikiwa ni kuimarisha ulinzi na kuongeza idadi ya pilisi.



Sirro amesema kuwa vyombo ya usalama vinaendelea na upelelezi kujua ukiukwaji huo wa sheria iwapo ni polisi pekee ama mwandishi huyo alikiuka sheria na maagizo ya polisi ili waweze kujiridhisha na kuchukua hatua.

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi amezungumzia uchaguzi mdogo uliofanyika na dosari chache zilizosababisha na baadhi ya watu kufanya vurugu na kuwataka polisi kukamilisha upelelezi ili wafikishe mahakamani na kuchukuliwa hatua ,ikiwa ni pamoja na ziara yake katika eneo la mto wa Mbu.

Kwa Upande wake Mkazi wa Jiji la Arusha Gephrey Stephen amesema kuwa licha ya serikali kutambua mchango wa Wanahabari bado kuna changamoto kwa jeshi la polisi linapaswa kujitathmini mahusiano yake na wanahabari pamoja na wananchi kwa ujumla.


Rosa Ree "Sijali Wanaoponda Mimi Kubinua Mdomo, Maneno ya Watu Hayanilipii Bills"

$
0
0

Female Rapper, #RapGoddess @rosa_ree amesema kuwa hakuna mtu anamsumbua au kumfanya akate tamaa kuhusu muziki wake eti sababu ikiwa ni Swag zake za kubinua mdomo, au kutoa Ulimi nje

Rosa Ree amesema maoni ya watu kama hayo hayamuharibii chochote na kubinua kwake mdomo ndio kumemfanya apate Supermarket, ana Kolabo na International Artist Kibao na bado anaendelea kuzifanya na kwa sababu maoni hayo sio pesa basi wala hatakata tamaa yeye kuendelea kusonga mbele zaidi.

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume, Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na kuchelewa kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za:


FUUl POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.


NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

Hivi Ndivyo Wema Sepetu Alivyowafunika wasanii wa kike wa Tanzania

$
0
0
Muigizaji wa filamu mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu, amekuwa msanii wa kwanza kwa wanawake Tanzania kufuatiliwa na watu wengi zaidi ya milioni 3.7 kupitia mtandao wa Instagram, huku nafasi ya pili ikishikwa na Jackline Wolper ambaye ana followers milioni 3.4.

Nafasi ya tatu imeshikwa na Vanessa Mdee ambaye ana followers milioni 3.3, akifuatiwa na Shilole mwenye 'followers' 3.2 huku Linah Sanga akishika nafasi ya tano kwa 'followers' milioni 2.8.

Hayo yamebainika baada ya utafiti uliofanywa na www.eatv.tv kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram leo Agosti 16, 2018, wenye lengo la kutaka kufahamu ukubwa wa majina waliyokuwa nayo wasanii hao kama unafanana na idadi ya watu wanaofuatilia na kuwakubali mitandaoni, licha ya watu hao kuwa wanatoka maeneo mbalimbali ya miji.

Mbali na hao, muigizaji Elizabeth Michael (LULU) ameshika nafasi ya sita kwa 'followers' milioni 2.6, mkongwe wa bongo fleva, Lady Jay Dee maarufu kama 'Komando Jide' ameshika nafasi ya saba akiwa na followers milioni 2.3, nafasi nane ikichukuliwa na muigizaji Shamsa Ford akiwa na 'followers' milioni 2.2 huku nafasi ya tisa ikichukuliwa na muigizaji Irene Uwoya akiwa na 'followers' milioni 1.7.

Nafasi ya 10 ikifungwa na Snura akiwa na milioni 1.5 ya watu ambao wanafuatilia kazi zao na vitu vingine mbalimbali kutoka katika kurasa zao za Instagram.

Wengine ni Nandy akiwa na laki 930, Mwasiti laki 798, Ruby akiwa na laki 491, Maua Sama laki 465, Chemical mwana wa Lubao akiwa na laki 354, Rosa Ree laki 327

Waziri Mkuu Aagiza Kukamatwa Kwa Mtendaji....Ni baada ya upotevu wa sh milioni 141 za kijiji

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa TAKUKURU wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Bw. Francis Zuakuu kumkamata aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Bulagamilwa, Bw. Ntemi James kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa sh. milioni 141 za kijiji hicho.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Agosti 16, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tabora.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Manonga, Bw. Seif Gulamali kumuomba awasaidie katika kulipatia ufumbuzi suala hilo la upotevu wa fedha za kijiji kwa kuwa ni la muda mrefu na hakuna hatua zilizochukuliwa.

Kutokana na malalamiko hayo Waziri Mkuu amemtaka kamanda wa TAKUKURU wa wilaya hiyo ahakikishe anawatafuta watu wote waliohusika na upotevu wa fedha hizo za kijiji akiwemo na alitekuwa mtendaji wa kijiji cha Bulagamilwa, ambaye kwa sasa ni Mtendaji wa kata ya Igurubi.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma wilayani Igunga wahakikishe wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwatumikia wananchi kwa weledi na ustadi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Waziri Mkuu amesema watumishi wa umma lazima wabadilike na wafanye kazi kwa bidii, waachemazoea  na watumie utalaamu wao vizuri katika kuwahudumia wananchi na Serikali haitowavumilia wafanyakazi watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao.

"Msimamo wa  Serikali ni kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo, hivyo haitawavumilia watumishi whv atakao jihusisha navitendo vya rushwawa na matumizi mbaya ya fedha za umma."

Pia Waziri Mkuu amewataka wakuu wa idara na watumishi wengine wajiwekee utaratibu wa kuwatembelea wananchi katika maeneo yao hususan ya vijijini kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi.

Binti Aliyetaka Kujiua Apata Nafasi Nyingine ya Kuishi Baada ya Kupandikizwa Sura

$
0
0
Binti aliyetaka kujiua apata nafasi nyingine ya kuishi baada ya kupandikizwa sura
Katie Stubblefield alikuwa na umri wa miaka 18 wakati alipopata majeraha makubwa baada ya kupigwa risasi.

Aliokolewa maisha yake hospitalini ingawa majeraha aliyoyapata yalimfanya msichana huyu maisha yake yabadilike na muonekano wa uso wake ulikuwa umebadilika karibu wote.

Kwa sasa msichana huyo ana umri wa miaka 22 na ameweza kuonyesha matokeo ya upandikizaji wa uso wake ulichukua miaka kadhaa katika jarida la 'National Geographic'

Chapisho hili lilipata nafasi ya kipekee katika kilniki ya Ohio ambayo ilimfanyia upasuaji binti huyo wakati akiwa ana umri wa miaka 21.

Waandishi wa habari na wapiga picha walifuatilia upasuaji huo tangu maandalizi yanaanza mpaka wakati wa upasuaji ambao ulitumia muda wa saa 31.

Picha ya sura ya Katie ambayo ipo juu ya jarida hilo la mwezi wa septemba iliweza pia kusimuliwa katika Makala ya kwenye mtandao.

Mpaka sasa ni watu 40 tu ndio wameweza kubadilishwa muonekano wa sura zao.Mtu wa kwanza kufanyiwa upandikizaji huo ilikuwa mwaka 2010 na alifanyiwa na daktari kutoka Uhispania.

Kwa kuwa upasuaji huu bado unafahamika kama ni majaribio hivyo basi malipo yake hayapo kwenye bima nchini Marekani.

Upasuaji alioufanya Katie ulidhaminiwa na taasisi ya 'Armed Forces'ambayo inataka kuboresha matibabu ya askari ambao watakuwa wamejeruhiwa katika vita.

Katie aliaminika kuwa ni mtu sahihi kufanyiwa jaribio hilo kutokana na majeraha aliyokuwa nayo pamoja na umri wake.

Huyu ndie Mamba anaeabudiwa kama Mungu Nigeria

$
0
0
Watu huwa na imani tofauti na huabudu vitu vingi duniani. Nchini Nigeria, kuna kabila moja ambalo humuabudu mamba kama miungu.

Mamba huyo wanayemuabudu kwa sasa ana umri wa miaka 78.

Wakazi wa eneo hilo la Oje viungani mwa mji wa Ibadan kusini magharibi mwa Nigeria humuenzi mamba huyo sana na wanaamini kwamba mamba huyo anaweza kujibu maombi yao.

Huwa wanamrushia kuku kama zawadi kumshawishi kutimiza maombi yao, wengine humpa mbuzi.

 Anadaiwa kuanza kufugwa na familia hiyo kuanzia mwaka 1940 baada ya mamba mwingine aliyekuwa akifugwa kabla yake kuchukuliwa na Wazungu.

Ajabu ni kwamba familia hiyo yenyewe huwa haiamini kwamba ana nguvu zozote za kipekee.

Kiongozi wa sasa wa familia hiyo ya Delesolu, Bw Raufu Yesufu, aliambia BBC kwamba: "Kwa sababu ya Imani yetu, sisi ni Waislamu, hatuamini kwamba ana nguvu zozote."

Anasema waganga wa kienyeji na matabibu wengine huwa wanafika kwa sababu mbalimbali kutafuta msaada.

Baadhi hufika kuomba usaidizi katika kuwaponya wagonjwa au kuwasaidia watu wanaotatizika kushika mimba.

Familia hiyo huwa haiwazuii kufika kumuomba mamba huyo ambapo huwa wanampa kuku.

Watu wamekuwa wakifika kwa mamba huyo kwa muda mrefu, baadhi wakiwa na maombi ya ajabu.

Kunao wanaofika wakitaka kuchukua kinyesi chake na wengine kutaka kuchotamaji kutoka kwa kidimbwi anamoishi.

Bw Yesufu anasema kinyesi hiyo na maji hayo baadaye hutumiwa na waganga au watu binafsi kama tiba.

Tanzania yashindwa kusogea, yazidiwa na Uganda FIFA

$
0
0

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeeendelea kuganda palepale katika viwango vya soka duniani kwa mujibu wa listi ya shirikisho la soka duniani FIFA iliyotelewa leo, Agosti 16. 

Taifa Stars imeendelea kushikilia nafasi ya 140 ikiwa nafasi nne nyuma ya Rwanda inayokamata nafasi ya 136 na nafasi nane juu ya Burundi ambayo inashikilia nafasi ya 148 katika viwango hivyo. 

Uganda ‘The Cranes’ imeendelea kuongoza soka la Afrika Mashariki, ikisalia nafasi ileile ya 82 ya mwezi uliopita ikifuatiwa na Kenya iliyo katika nafasi ya 112 huku nafasi ya mwisho kwa nchi za Afrika Mashariki ikishikiliwa na Sudan Kusini ambayo ipo nafasi ya 156. 

Kwa bara la Afrika, Tunisia inaongoza ikiwa katika nafasi ya 24 baada ya kuporomoka nafasi tatu nyuma toka mwezi uliopita, ikifuatiwa na Senegal iliyopo nafsi hiyohiyo ya 24 baada ya kupanda nafasi tatu tofauti ikiwa ni katika alama ambapo Tunisia ina alama 910 huku Senegal ikiwa na alama 838. 

Bingwa wa kombe la dunia mwaka huu, timu ya taifa ya Ufaransa inaongoza katika nafasi ya kwanza ikiwa imepamda nafasi sita zaidi, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2002 ikifuatiwa na Ubelgiji katika nafasi ya pili na Brazil inayokamata nafasi ya tatu. 

Nafasi ya nne mpaka ya kumi ikishikiliwa na Croatia, Uruguay, Uingereza, Ureno, Uswisi, Hispania na Denmark kwa kufuata mpangilio wake. 

Article 3

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa Mwandishi wa habari aliyepigwa na polisi wakati akitekeleza majukumu yake katika Uwanja wa Taifa ulioko jijini Dar es Slaam alikuwa mbishi na alimkaba Askari polisi akitaka kuingia sehemu ambayo imekataliwa kuingia, ndipo askari wakawa na hasira na kuanza kuvutana ndipo ugomvi Ukaanza.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akiwasili jijini Arusha kwa ziara yake ya kutembelea eneo la Mto wa Mbu ambapo yalitokea matukio ya wanawake kubakwa na kuuawa ,ziara ambayo inalenga kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo hayo ikiwa ni kuimarisha ulinzi na kuongeza idadi ya polisi.


Sirro amesema kuwa katika tukio la kupigwa mwandishi wa habari kuna uchunguzi unafanyika ambapo baadae wataelezea ukweli baada ya kukamilisha. 


Amesema kuwa mwanzo inaonekana mwanahabari alifanya vurugu na jalada lazima lifunguliwe pamoja na askari polisi waliokuwa wanampiga upelelezi utafanyika ili kuchukua hatua kwa sababu kila jmbo linataka upelelezi. 


Amesema kuwa Mwanahabari alivua shati mwenyewe na kuanguka chini kisha kukimbia mbele kwenye kioo cha camera ili kuonekana amepigwa jambo ambalo siyo sahihi.

Meneja wa WCB, Sallam SK adai hakuna bifu kati ya Diamond na Alikiba

$
0
0

Moja ya mameneja kutoka kwa WCB, Sallam SK amefunguka kuhusu bifu la Diamond la Alikiba.


Katika mahojiano na The Playlist ya Times Fm amesema wasanii hao hawana bifu na kama lipo kuna watu wametengeneza.


"Actually hamna ugomvi, hivi vitu vilitengenezwa na actually watu waliotengeneza wanajulikana, haina haja ya kuwataja kuwa airtime sana," amesema.


"Kati ya Ali na Diamond hamna bifu hata siku moja, haijawahi kutokea na uongozi wa Ali na wetu tunakutana tunacheka na kuongea," amesema Sallam.

Meneja wa WCB, Sallam SK adai hakuna bifu kati ya Diamond na Alikiba

$
0
0

Moja ya mameneja kutoka kwa WCB, Sallam SK amefunguka kuhusu bifu la Diamond la Alikiba.


Katika mahojiano na The Playlist ya Times Fm amesema wasanii hao hawana bifu na kama lipo kuna watu wametengeneza.


"Actually hamna ugomvi, hivi vitu vilitengenezwa na actually watu waliotengeneza wanajulikana, haina haja ya kuwataja kuwa airtime sana," amesema.


"Kati ya Ali na Diamond hamna bifu hata siku moja, haijawahi kutokea na uongozi wa Ali na wetu tunakutana tunacheka na kuongea," amesema Sallam.

Naombeni Ushauri Nawezaje Kuachana na Tabia ya Kufanya Mapenzi Kinyume na Maumbile

$
0
0
Hello guys
Nimekuwa na tabia ambayo kwa kweli its not normal, coz tangu nimeanza kubalehe binti wa kwanza kufanya nae ngono alikuwa bikra (sealed kwa mbele), so nikaamua kutumia mlango wa uani kufanya nae mapenzi.

Sasa tangia hapo yani kila mwanamke ninaelala nae lazima nimuombe tigo indirectly, kwenye foreplay nashika makalio na kumtia binti vidole vya nyuma, wengine wanakataa wengine wanakubali.

Nikiona mwanamke mwenye makalio makubwa na malaini ndo nadata kabisa. Note (Im 100% straight guy, nawala wanawake tu) sasa hii tabia cjui itaisha lini?

Kama jamani kuna waliokwisha kumbana na hii hali humu, halafu wakaiacha naombeni tips, sababu hii tabia haitanipeleka mahali pema. Though its hard to get rid of this addiction but naombeni mbinu za kuiacha.

By okoyoko/JF

Serengeti Boys yaichapa za kutosha Sudan

$
0
0
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania, Serengeti Boys imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya timu ya vijana ya Sudan katika mfululizo wa michezo ya kufuzu fainali za AFCON za vijana U-17 kanda ya Afrika Mashariki zinazoendelea hapa nchini.

 Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa taifa na kuhudhuriwa na mashabiki wengi waliojitokeza kuja kuisapoti timu yao, ulianza kwa kandanda safi katika kipindi cha kwanza huku kila timu ikicheza kwa umakini mkubwa.

Serengeti Boys ndiyo walikuwa wakwanza kupata bao dakika ya 19 kupitia kwa Edson Mshirakandi aliyepiga kona ya moja kwa moja na kumshinda mlinda mlango wa Sudan, Omer Miso, bao lilidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Serengeti Boys waliamka zaidi na kucheza mpira wa kuvutia mbele ya mashabiki wao ambao waliwashangilia kwa hari zaidi, mabao mengine yalifungwa na Kelvin John dakika ya 45 na 60 pamoja na Agiri Ngoda dakika ya 72 na 79.

Kwa ushindi huo Serengeti Boys inafikisha alama 6 kwa kushinda michezo yake yote miwili, mchezo wa kwanza ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Burundi, Timu zingine zenye alama sita ni Rwanda na Ethiopia zote zikiwa baada ya kushinda michezo yake miwili.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images