Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

JWTZ itoe Tamko Juu ya Diamond na Ney wa Mitego Kuvaa Sare za Jeshi na Kukata Mauno

$
0
0
Kama wiki mbili zimepita toka jeshi letu pendwa litupige mkwara juu ya matumizi ya sare zake au zinazofanana na hizo kwa mtu ambae si askari.. Kwamba ukivaa tu basi umevunja sheria na inapaswa uadhibiwe mara moja, either mahakamani au 'wapigwe tu'.. Hilo linapewa nguvu na taarifa ya juzi kati jamaa kulazimishwa kuoga maji ya barabarani maeneo ya kariakoo baada ya mjeda mmoja kumnyaka na nguo zinazofanana na zao.. 

Sasa cha ajabu mbona juzi katika tamasha la Fiesta mwanamziki Diamond na timu yake pamoja na Ney anayewatega, wameonekana wazi wakiwa na sare hizo tena wamezivaa hovyo hovyo kata K wakinengua jukwaani.??? Au hiyo sheria inamgusa nani?

Huyu kijana akiwa na ufahamu kuwa television ya taifa inaonyesha hili tamasha lao kavaa SARE ZA JESHI tena full kuanzia viatu mpaka kofia.

Wasanii ni Mfano wa Kuiga, Sasa hawa wanafundisha nini watu wengine?

Hii ni Dharau

Martin Kadinda Amfuata Jackline Patrick Gerezani China

$
0
0
Stori: Mayasa Mariwata
Imekaa poa sana! Ubuyu kutoka Hong Kong, China unadai kwamba mbunifu wa mavazi Bongo, Martin Kadinda hivi karibuni alimfuata Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ gerezani aliyefungwa nchini humo kwa msala wa kukamatwa na madawa ya kulevya

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Kadinda ambaye ni meneja wa Wema Isaac Sepetu zilidai kwamba katika safari yake nchini humo, alifuatana na Wema na Petit Man.

“Kadinda amepongezwa sana kwa hatua yake hiyo, kuhusu kama alionana naye au alichoongea naye, tusubiri arudi maana bado yupo China,” alisema rafiki wa mmiliki huyo wa lebo za mavazi za Single Button na Kwachukwachu.
GPL

Baada ya Kuachana na Edzen, Dida Azifuta Ndoto za Kuolewa Tena

$
0
0
Stori: Imelda Mtema
NDOA basi! Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amezima ndoto za kuishi maisha ya mke na mume kwa kudai kuwa, amebaini kujiingiza kwenye ulimwengu huo ni kujipa ‘stress’ za kujitakia.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda juzi, Dida alisema baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake, Edzen Jumanne, amebaini wanaume wote lao ni moja hivyo kama atakubali kuingia kwenye ndoa na mwanaume mwingine, itakuwa ni yaleyale.

“Yani sasa hivi hata aje mwanaume na gia gani siwezi kukubali kuolewa tena, kwa kifupi sina ndoto za kuitwa mke wa mtu tena, bora nibaki peke yangu nifanye mambo yangu,” alisema Dida.

MTU Aliyesadikiwa Kuwa na Ugonjwa wa Ebola Sengerema Mwanza, Azikwa kwa Taadhari Kubwa

$
0
0
MTU aliyesadikiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola Wilaya Sengerema mkoani Mwanza, amezikwa kwa hadhari kubwa na wataalamu wa afya.

Wakati mtu huyo akizikwa jana, hofu kubwa imetanda  mikoa ya Kanda ya ziwa, huku watu wakiogopa kugusana katika vyombo vya usafiri na kutumiana ujumbe mfupi wa simu za mikononi (SMS) juu ya kuchukua hadhari ya ugonjwa huo.

Mgonjwa anayedaiwa kufariki dunia kwa ugonjwa huo, ametajwa kuwa ni Salome Richad (17), mkazi wa Kahunda Wilaya ya Sengerema.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mganga Mkuu wa Hospitali Teule ya Sengerema, Mary Jose alisema mwili huo umezikwa na wataalamu ikiwa ni hatua ya kuchukua hadhari.

“Hakuna Ebola Sengerema, kilichofanyika ni hadhari tu, hii ni hadhari..narudia hakuna ebola Sengereama, kilichofanyika ni hadhari tu,” alisema.

Hata hivyo, Jose hakutaka kuzungumza zaidi kwa kile alichodai mwenye mamlaka ya kuzungumzia suala hilo ni Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO).

Wakimbiana kwenye daladala

Kutokana na hofu ya ugonjwa huo, jana wananchi walihaha katika vyombo vya usafiri hususan daladala, wakikataa kugusana.

Hali hiyo, ilisababisha wengi kuanza kutuma ujumbe mfupi kwa ndugu na jamaa kupitia simu za kiganjani kuwataarifu kutopeana mikono na mtu yeyote kwa kuwa Ebola imeingia Mwanza.

Imeelezwa hofu kubwa ipo katika Wilaya ya Sengerema ambayo inaonekana kuathirika zaidi.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Caren Yunus amewataka wananchi kuwa watulivu  kwa sababu ugonjwa huo bado haujathibitishwa rasmi.

Alisema sampuli zimechukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

Yunus aliliambia gazeti  hili kuwa, amesikitishwa na taarifa zinazodai Richard amekufa kwa ugonjwa wa Ebola baada ya kufikishwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema.

“Binafsi nasikitishwa na aliyetoa taarifa za Richard kwamba amefariki dunia kwa ugonjwa wa ebola… amepata wapi mamlaka ya kuzungumzia suala hili katika vyombo vya habari, uchunguzi kuhusu kifo cha binti huyo unaendelea na kwa taarifa za awali nilizonazo hakufariki kwa ugonjwa huo.

“Hivi sasa wananchi wamekuwa na hofu kubwa, sasa kama mkuu wa wilaya tunawahoji wale wote waliozungumza kwenye taarifa zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari tujue wapi walithibitisha wakati sampuli bado zipo Muhimbili,” alihoji.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Valentino Bangi, hajatoa kauli yoyote licha ya kutafutwa na waandishi bila mafanikio huku simu yake ikiita bila kupokelewa.

Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dk. Rutachunzibwa Thomas alisema amesikia taarifa ambazo si rasmi za kifo cha mtu mmoja anayedaiwa kuwa na dalili za Ebola na kuwataka wananchi mkoani humo kuchukua hadhari kutokana na ugonjwa huo hatari.

Alisema wananchi wote bila ya kujali mtu yuko kwenye nafasi gani, anapaswa kuchukua tahadhari na kuwaelimisha wananchi juu ya dalili za ugonjwa huo, ambao haujapata dawa.

“Ninaloweza kusema ni kwamba, ugonjwa huu tusiwaachie watu wanaofanya shughuli za sekta ya afya, bali kila mtu atoe ushirikiano kuanzia ngazi ya kaya kwa kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono na kukumbatiana, pia ikiwa kuna mtu atabainika kuwa nao ni vema tahadhari ikachukuliwa maana ukigusa damu yake, jasho na mambo mengine unaupata.

“Mpaka sasa ugonjwa huo umetajwa katika wilaya iliyopo jirani na mpaka wa Uganda na Tanzania, ila sina taarifa za ugonjwa kuingia mkoani Kagera,tunachukua hadhari zote,” alisema Dk. Thomas.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Afya Duniani (WHO), idadi ya watu waliofariki na ugonjwa wa Ebola imefikia 1,350 na idadi hiyo inaweza kuongezeka katika siku za hivi karibuni kutokana na kuendelea kuenea kwa ugonjwa huo katika maeneo mbalimbali duniani.

Taarifa hii imeandaliwa na Benjamin Masese, John Maduhu (Mwanza), Shomari Binda (Mara) na Renata Kipaka (Kagera).

Alama za Ufaulu wa Show ya Fiesta 2014 Kwa Wanamuziki Walioimba

$
0
0
Mdau mmoja wa Muziki Aliyekuwepo kwenye Show ya Fiesta Jumamosi Usiku Ametoa Tasmini yake kwa Wanamuziki Walioimba Siku hiyo na kuwapa Maksi kama ifuatavyo:

Ali Kiba 97%
Mwana Fa 94%
Weusi 91%
Mr blue & B.O.B 83%
Stamina 71%
Diamond Platnumz 65%
Ommy Diampoz 62%
madee &Tip Top 58%
Young Killer 50%
Yamoto band 47%
Chege &Temba 42%
Ney wa Mitego 30%

International 
T.I 88%
Davido 70%
Victoria Kimani 50%
Waje 43%

HAWA AKINA
Recho 
Barnaba
Shaa
Linah
Makomandoo
Vanesa Mdee
Next time msiwalete wanatuibia hela zetu tu bado hawajakizi viwango.
Ruhusu kufanya masahihisho kwa alama anazoona zina makosa.

By Mzanzibar Halisi

Big Brother Africa: Washiriki wa Kenya, Uganda, na Nigeria watolewa Mchezoni, Mtanzania Aponea Chupuchupu

$
0
0
Mtanzania Laveda Jumapili October 19 aliponea chupuchupu kwa kubaki kwenye jumba la Big Brother Africa, huku akiwashuhudia washiriki wenzake watatu wa kike wakitoka mchezoni.

Esther (Uganda) , Lilian (Nigeria) pamoja na Sabina (Kenya) ndio washiriki walioondolewa katika shindano hilo usiku wa jana ikiwa ni ‘eviction’ ya pili toka shindano lianze.

Hadi sasa washiriki watano wa kike wametoka katika shindano hilo na kufanya idadi ya washiriki wa jinsia ya kike kubaki 8 huku wanaume wakiwa 13.

Nchi za Zambia, Mozambique, Kenya, Uganda and Nigeria kila moja imeshapoteza muwakilishi mmoja hivyo zote zimebaki na muwakilishi mmoja mmoja tu mjengoni.

Eti The King is Back ! Kwani Alikuwa Ameenda Wapi na Kutuwakilisha Katika Jukwaa Gani Tangu Amekuwa King?

$
0
0
Kuna watu mnakera kwakweli..na nimeanza kuamini hizi team team hizi zinaua mziki..hivi unaambiwa eti king iz back cjui izi rudi..wat ???????alikua ameenda wapi??huyu king mziki wetu kaupeleka wapi?? huyu king katuwakilisha kwenye jukwaa gani kubwa tangu amekua king???simchukii mtu ila na nyie mnao jiita mastar vumbi nyie ndo wachonganishi kuliko hata hizo Team..star na wewe unaandika caption imekaa kimafumbo tuuu ili iweje?mie ni fans wa chibu na kiba...ila wat i see ni kwamba watu wana take advantage ya kiba kurud kwenye game ili kumshusha diamond na ni kitu ambacho akiwezekani..whether u believe o not..chibu atabaki kuwa chibu na tukubali tukatae dogo mziki wetu kautangaza ila hata kama mnamchukia kwa roho zenu mbaya kiba ataki kuwa star ki kwenu kwenu wakati diamond atakua star wa Tz yote..hizo vumbi na mikwala ni kawaida tu..by the way wote wamefanya show nzuri..sasa hizo king king iz back iz wat ndo nini??king ninae mjua ni majuto tu..wengine wasanii..tuufikishe mziki mbali ila sio kwa majumgu..Tanzania bila majungu inawezekana.....
KWAN UYO AL K ALIKUA KASAFIRI MPAKA ARUDI ALIENDA WAPI ? LEO NINA HASIRA LEO JICHANGANYE UONE !!!!!
By Malkia wa Insta

Kwa Nini Wanawake wa Kiislamu Hawautaki Tena Ukewenza?

$
0
0
Ndugu zanguni Qur'an ni kitabu kitakatifu pekee kinachoruhusu mwanaume kuwa na wanawake zaidi ya mmoja yaani mwanaume anaweza akaoa mpaka wanawake wanne so long as anaweza kuwahandle. 

Lakini katika miaka ya hivi karibuni wanawake wa kiislamu wamekuwa hawataki kuwa mke wa pili, watatu ama hata wa nne. Pia hata yule mwanamke ambae tayari yupo kwenye ndoa akisikia kuwa mume wake ana plan ya kuoa mke wa pili nakuambia nyumbani hapatakalika.

Swali langu ni kwamba, je ina maana wanawake wa kiislamu wameamua kupingana na maandiko yanayoruhusu hicho kitu ama je siku hizi kitabu hicho siyo mwongozo tena?
 ~By Bornagain

Wanachama Wanaopinga Katiba Waondoke CCM - Wassira

$
0
0
Chama  Cha Mapinduzi  kimewataka  wanachama   wake   wanaopingana  na msimamo   wa chama  hicho  kuhusu  katiba  inayopendekezwa kurudisha kadi  na kuondoka  mara  moja ndani   ya  chama  hicho.

Chama  Cha Mapinduzi  kimewataka  wanachama   wake   wanaopingana  na msimamo   wa chama  hicho  kuhusu  katiba  inayopendekezwa kurudisha kadi  na kuondoka  mara  moja ndani   ya  chama  hicho, badala  ya  kutumia mgongo  ya  CCM kuwapotosha   watanzania.

Kauli  hiyo  imetolewa  na  mjumbe  wa  kamati  kuu   wa  halmashauri  kuu  ya  taifa  ya Chama  Cha Mapinduzi  Mh Stephen  Wassira,  muda  mfupi  baada   ya  kupokelewa  na wawakilishi  wa wananchi  wa  mkoa  wa Mara, ikiwa ni siku  chache  tu  baada  ya  kumalizika  kwa  Bunge  Maalum  la  Katiba, ambapo amesema  kuna  baadhi  ya  wana CCM   wamekuwa  wakitumia  mgongo  wa  chama  hicho  kuwapotosha  wananchi kuhusu katiba  hiyo  inayopendekezwa.

Hata  hivyo  Mh. Wassira  ambaye  ni waziri  wa  nchi  ofisi  ya Rais  mahusiano na uratibu, amesema katiba  inayopendekezwa endapo   itapitishwa  na  wananchi  itajibu kilio  cha  miaka  mingi  kuhusu ukiukwaji   wa  maadili   vikiwemo  vitendo  vya  rushwa ndani  ya  jamiii.

Nuh Mziwanda: Najifunza 'Ubaba wa Familia ' Kwa Shilole

$
0
0
Nuh Mziwanda a.k.a Babby wa Shilole, amesema kuwa kuzama katika penzi la bibie huyu na kuingia katika maisha yake kumemfundisha kitu kikubwa kabisa na kila siku anaendelea kujifunza namna ya kuishi katika familia akiwa kama baba katika umri mdogo.

Mkali huyu ambaye anashine na Ngoma ambayo pia ina bonge moja ya chupa, Msondongoma, amesema kuwa katika hatua ya mwanzo maisha haya mapya ndani ya familia ya shilole, yalikuwa yanampatia changamoto lakini sasa amengundua kuwa hili ni darasa poa kabisa la maisha yake ya baadae ya ubaba.

Maskini Mchezaji wa Mpira Afariki Akipiga Sarakasi Kusherehekea Bao

$
0
0
Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake.
Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kw atimu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC.
Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki.
Mechi hiyo ambapo alipata jerehe la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo.
Taarifa kutoka kwa ligi hiyo kpitia kwa mtandao wa Facebook, ilisema : ''imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa soka na mashabiki wa Mizoram. ''
"Peter alikuwa mchezaji mzuri na milizni mzuri sana, na pia alikuwa mchapa kazi.''

Kamati ya Miss Tanzania Kutolea Ufafanuzi wa Miss Tanzania Mwenye Utata wa Umri Siku ya leo

$
0
0
Mara baada ya kutwaa taji hilo kumeibuka utata juu ya umri wa Miss Tanzania 2014.
Habari zimezagaa katika mitandao ya kijamii, ambapo anatuhumiwa kudanganya umri wake. Kuna taarifa zinasema Bi Sitti alitaja kuwa ana umri wa miaka 18, jambo linalobishaniwa.
Lakini ukweli utajulikana leo 21 Oktoba 2014, ambapo waandaji rasmi wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, Lino International wameahidi kulitolea ufafanuzi suala hilo.
Binafsi ninayasubiri kwa hamu kubwa maelezo ya kina yatakayo wanyamazisha Watanzania

Ommy Dimpoz Atoboa Siri ya Picha Anayoonekana Akishuka Kwenye Treni ‘Tusiamini kila Tukionacho Mtandaoni’

$
0
0
Baada ya kusambaa kwa picha ya Ommy Dimpoz anayoonekana akiwa kama kijana wa kijijini aliyetua mjini Dar es Salaam na watu wengi kuhisi ni picha yake ya zamani aliyopigwa wakati anatua Dar (kitu ambacho si kweli), ameamua kuelezea hisia zake.

Akiweka picha nyingine kwenye Instagram lakini awamu hii akiwa na Vanessa Mdee (ambayo inaonesha kuwa ni moja ya kazi zake zitakazokuja), Ommy amesema amejifunza mengi kutokana na jinsi watu walivyoiongelea picha hiyo.

“Wiki iliyopita nimejifunza mambo mengi sana baada ya ile picha niliyodandia treni kusambaa kwenye mitandao kuna watu waliongelea km utani,kuna watu walinikebehi,wengine waliweka kwenye mitandao na kunitusi kabisa,”ameandika Ommy.

“Ila nilichogundua Sio kila tunachokiona kwenye mitandao kina ukweli tujaribu kuwa wachunguzi,tuache mambo ya kucopy na kupaste jambo la mwisho kabisa siri ya Maisha anaijua mungu usimdharau mtu kwa muonekano unayemuona mshamba eti amekukuta mjini kesho ndo huyo huyo atakayekupa ajira tupendane tusidharauliane……Asante @vanessamdee kwa kupokea na fuko langu.”
~Bongo5

Mwanamuziki T.I. awawakia Waliomwambia Kuja Tanzania Kutampa Ugonjwa wa Ebola!

$
0
0
Mfalme wa Kusini, T.I. amemind. Tangia weekend iliyoishia alipokuwa akipost picha za ujio wake nchini Tanzania, baadhi ya followers wake wajinga wa Marekani wamekuwa wakimkejeli kuwa anaweza kurudi Marekani akiwa ameambukizwa ugonjwa wa Ebola. 

Katika kuthibitisha kuwa amekuwa akisoma comments zao, T.I. ameonekana kutofurahishwa na kauli hizo za kipuuzi na ameamua kumtolea uvivu mmoja wao aliyemtelea habari hizo za Ebola.


~Bongo5

Mbowe Atolea Ufafanuzi Picha Iliyosambaa Mitandaoni Akibusiana Laivu Laivu

$
0
0
Week iliyopita Picha hiyo hapo juu ilienea mitandaoni ukimuonesha Freeman Mbowe na Mkewe Wakibusiana Live ....Mbowe Ameongea haya Kuhusu Picha hiyo :

“Kwanza mke wangu alikuwa anatimiza umri wa miaka 50 ya kuzaliwa, vilevile firstborn wetu Dudley alikuwa amemaliza shahada yake ya kwanza Chuo Kikuu cha Sussex, Uingereza, kwa mambo hayo mawili, tuliona ipo haja ya kufanya sherehe, ukizingatia watoto wetu wengine wawili Nicole na Denis walikuwa wamerejea nchini kwa sababu nao wanasoma nje ya nchi.

Siku hiyo ya tukio ilikuwa Jumapili, tulianza kwa kwenda kanisani Azania Front tukatoa sadaka, baada ya hapo tulikwenda Serena Hotel kwenye Ukumbi wa Kivukoni ambako chakula cha mchana kilikuwa kimeandaliwa, tukajumuika na ndugu wengine pamoja na marafiki.

“Haikuwa sherehe tu kusema labda nilikurupuka kumbusu mke wangu, ilikuwa sherehe ya kifamilia, kumpongeza mke wangu na mtoto wetu,” alisema Mbowe.

Divido Aishukuru Clouds FM Kumkutanisha na T.I, Pia Amshukuru Diamond Kwa Kumkaribisha Vizuri Bongo

$
0
0
Davido ametumia Instagram kutoa shukrani zake baada ya kuwa sehemu ya wasanii waliotumbuiza Jumamosi iliyopita.

“Kwaheri TANZANIA 26464 ! It was great sharing the stage with @troubleman31 … Thank you clouds Fm for making it possible! And bless my brother @diamondplatnumz for welcoming me well.” 

Sitti Mtemvu Kuvuliwa Au Kutokuvuliwa Taji leo ?

$
0
0
Kamati ya Miss Tanzania leo inatarajiwa kuelezea ukweli juu ya sakata la kudanganya umri la mshindi wa taji hilo mwaka huu, Sitti Mtemvu.
Mratibu wa shindano hilo Hashim Lundenga amesema kamati yake itaelelezea taarifa ambazo walikuwa nazo kuhusiana na mrembo huyo na matokeo ya uchunguzi baada ya taarifa nyingi zilizoibuka.
"Yamesemwa mengi na yameandikwa mengi, hivyo leo itajulikana kama atavuliwa taji ama la" maneno hayo amesema Lundenga
Je, wewe mtazamo wako ni upi, unapenda abaki na taji au avuliwe?


Lundenga Amtetea Sitti Mtemvu mbele ya Waandishi wa Habari, Sitti Asema Mnamuandama kwa Vitu vya Uongo

$
0
0
Mwaka 2005 kulikua na ushindani kidogo, mwaka 2006 kulikua na ushindani  wa Wema na Jokate na upinzani huu umeendelea kuwepo kwenye mashindano yetu lakini ya mwaka huu imezidi mno, kumekua na matusi… kashfa na hata naona wamevuka mpaka na kuingiza mambo ya kisiasa ambayo sisi hatuyapendi, huu ni mchezo kama mchezo mwingine wowote… yani taji la mwaka mmoja limefunika mpaka katiba na Simba na Yanga?
Hayo ni maelezo aliyoyatoa Mr. Hasheem Lundenga mbele ya Waandishi wa habari Dar es salaam October 21 2014 kuhusu ishu ya Miss Tanzania ambae aliandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mrembo huyu kudanganya umri, elimu na mambo mengine.

Yafuatayo ni mambo waliyoyasema Hasheem Lundenga na Miss Tanzania Sitti.
‘Walidai kwamba Miss Tanzania ana mtoto baada ya kutoka picha moja akiwa na mtoto, nasema katika utafiti wetu sisi Miss Tanzania hana mtoto na mwenye vithibitisho halali kwamba ana mtoto atuletee, kama kuna uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa cha mtoto….. leta hicho cheti’ – Lundenga
‘Hili la sisi kuchukua rushwa kutoka kwa baba wa Sitti, Abbas Mtemvu…. jamani hii ni stori ya kijingajinga, ni mambo ya kipumbavu sana kuandika haya mambo, hamjui taratibu zetu tunavyowapata majaji na wanavyofanya kazi…Majaji huwa wanatafutwa siku nne za mwisho na huwa hakuna mtu anajua atakua Jaji na huwa tupeleka majina 15 BASATA na wao ndio wanaturudishia majina tisa ya Majaji waliopitishwa’ – Lundenga

‘Magazeti mbalimbali yameripoti kwamba Sitti alikua na Masters, ukweli ni kwamba katika fomu tulizonazo sisi Sitti hajaandika hata sehemu moja kwamba amesoma mpaka Masters, swala la Masters limetoka wapi? ni uongo huo’ - Lundenga
‘Kuhusu swala la yeye kuzungumza kifaransa, mtu anajua lugha ya kimataifa mbona kwenye mashindano ya dunia wanazungumza Kifaransa na lugha nyingine? lakini mbona hata kwenye fainali alijibu kwa Kiingereza pia? Kifaransa zilikua ni mbwembwe kuwashawishi Majaji, na kweli walishawishika na ndio maana akashinda’ – Lundenga
‘Jingine ambalo ni kubwa zaidi ni swala la umri lililozungumzwa sana, katika mashindano yetu washiriki wote hujaza fomu na kuandika tarehe ya kuzaliwa, fomu ya Sitti hii hapa na inaonyesha amezaliwa May 31 1991 kwa hiyo alitimiza masharti ya kushiriki kwa kuwa ana umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 24′ – Lundenga

‘Wote walioshiriki Miss Tanzania 2014 akiwemo Sitti walituletea vyeti vyao Original vya kuzaliwa tarehe 13 na kisha tukatoa nakala kupitia hivyo vyeti vyao Original’ – Lundenga
‘Sisi kazi yetu sio kupeleleza sana, tukipata information chache zinatutosha… kama mtu anatatizo na hiki cheti cha Sitti cha kuzaliwa akafanye utafiti, ukipata ukweli tuletee sisi lakini kazi ya uchunguzi sio ya kwetu’ – Lundenga


Baada ya Lundenga kuongea, Miss Tanzania 2014 Sitti nae aliongea machache kwamba ni kweli ana umri wa miaka 23 vilevile cheti chake cha kuzaliwa kilipotea sababu amekua akisafiri mara kwa mara’ -Sitti
Waandishi wa habari walipotaka awaambie na uthibitisho kama aliripoti Polisi kuhusu kupotea kwa cheti chake, Sitti alisema ‘sikutegemea haya maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo, kama mtakua mnahitaji kunihoji mnaweza kupanga siku yenu na mkanihoji’ – Sitti

Kuhusu yeye kuwa na mtoto Sitti amejibu kwa ufupi kwa kusema >>> ‘Nadhani inajieleza kama Muheshimiwa alivyosema kwamba sina mtoto na mkitaka tunaweza kwenda Hospitali kwa sababu naona kama mnaniandama kwa vitu ambavyo sio vya kweli’

Kuhusu ukweli kama hati ya kusafiria pamoja na leseni ya gari vilivyosambazwa mitandaoni ni kweli vikionyesha kwamba amezaliwa mwaka 1989, Sitti amesema ‘Sitogusia hilo swala sababu nilivyokua nakuja kuomba Miss Tanzania niliomba cheti cha kuzaliwa, hivyo vitu vingine ni maisha binafsi…. kwahiyo sidhani kama na nyie mngependa kuona mtu anachukua leseni ya gari au Passport iwe ya kweli ama feki na kuiweka kwenye mtandao’
Hayo ndio maelezo yaliyotolewa leo kwenye mkutano na Waandishi wa habari…. kama una comment yoyote iandike hapa chini na itatufikia.

Video Ikionyesha jinsi Sitti Mtemvu Alivyokuwa Akijitetea Mbele kwa Kujibu Maswali ya Waandishi wa Habari

$
0
0
Sitti Mtemvu Miss Tanzania Akijibu Maswali ya Waandishi wa Habari leo kuhusu utata wa Umri na Mambo mengine. Video hii Hapa chini:

Hasheem Thabeet Majanga Matupu, Atemwa na Team ya Pistons Baada ya Kuichezea Mwezi Mmoja

$
0
0
Timu ya Kikapu ya Pistons imemtema Mchezaji wake kutoka nchini Tanzania, Hasheem Thabeet ambaye amejiunga na Pistons mwezi septemba akitokea klabu ya Philadelphia iliyokuwa imemchukua kutoka Oklahoma City Thunder.
Alicheza dakika tano tu katika mchezo mmoja wa pre season na katika mwezi huu amecheza dakika tano tu dhidi ya Washington Wizard huku akikosa jaribio lake moja na kufunga. Pamoja na Hasheem Thabeet wengine waliofungasha virago ni Brian Cook, Lorenzo Brown na Josh Bostic.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images