Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Diamond Awa Gumzo Mlimani City Usiku wa Wasanii..Apagawisha Vilivyo

$
0
0
Diamond Usiku wa Jana aliwakonga Mioyo Mashabiki wa Mziki Pale Aliposhusha Show ya Nguvu Katika Tamasha la Usiku wa Msanii lililofanyika Pale Mlimani City ..Hii Imekata kiu kwa Wale Walio kosa Show nzuri siku ya Fiesta Baada ya Baadhi ya Mashabiki Kumzomea..

Lemutuz Aomba Kuombwa Radhi Baada ya Shabiki Wake Kuona Picha Hii na Kukoment Ndege Wenye Rangi Moja Huruka Pamoja

$
0
0
Social Network Super Star Lemutuz Aomba Kuombwa Radhi Baada ya Shabiki Wake Kuona Picha Hii na Kukoment Ndege Wenye Rangi Moja Huruka Pamoja kauli Ambayo Lemutuz Hupenda Kuitumia Katika Post zake Mbali Mbali:

Shabiki Alianza Hivi :

hariet_albert
"Dah!!huyu mbebez amekosa nguo ya heshima ya kuzuia huo mtindi daaaaah!!izi picha nyingine unazopiga @lemutuz_nation .zinaharibu au zinaleta maana nyingine ya ile slogan ndege wenye rangi moja huruka pamoja@lemutuz_nation @leahmassawe !!"

Lemutuz Akajibu Hivi:

lemutuz_nation

"@hariet_albert PLEASE UMEENDA MBALI SANA UNASEMA.MIMI NI KIRANJA WA KUSIMAMIA NGUO WANAZOVAA WANANCHI KWENYE STAREHE? I MEAN HIZO.NI NGUO MTU AMEVAA KWENYE STAREHE TENA USIKU PICHA INA TATIZO GANI SISTER PLEASE NINGEPIGA PICHA NA HUYU DADA KWENYE MKUTANO WA CCM KWELI TUMEKUTANA KWENYE STAREHE NA TUMEACHANA HAPO HAPO SASA MAMBO YA NDEGE KURUKA PAMOJA YAMETOKEA WAPI SISTER? NIOMBE RADHI PLEASE"

Uwezi Amini Watanzania Wengi Wanaipenda Miss Tanzania Kuliko Katiba ya Nchi

$
0
0
Watz saluti kwa kushika mabango.....ila ninamaswali machache...

Ivi Miss Tanzania ina faida gani kwa Maisha ya Watanzania Masikini wenye Taifa Tajiri ambalo hata rais wake hajui ni kwanini wananchi wake ni masikini???

Ivi umejaribu kufikiri Miss Tanzania inasaidiaje Kuboresha maisha yako na ya watanzania masikini walio wengi tena walioko vijijini???

Miss tz inaboreshaje huduma za Afya ili kupunguza vifo vya wanawake, watoto na watanzania masikini wenye nchi Tajiri???

Miss tz inaboreshaje Elimu nchini hasa shule za Umma ambazo wengi wanaosoma huko ni watoto wetu sisi watanzania masikini wenye Tanzania Iliyojaa Utajiri????

Miss Tz inaboreshaje huduma ya maji nchini wakina mama wengi tunabakwa kwa kufuata maji umbali mrefu???

Hii nguvu inayotumika kwa miss tz, kwa nini tusiihamishie kwenye mustabakali wa maisha yetu ya sasa na ya baadae yaani vizazi vijavyo kwenye Katiba pendekezwa???

"Katiba pendekezwa" umewahi kuifuatilia hata kwa dk 1??? Unajua kama ndo imebeba maisha yako, wajukuu wako, vitukuu na vilebwe??? Una mchango gani katika kupata Katiba Bora ya nchi yetu! umeshajiuliza na kutafakari???

Tuache kutumia fikra zetu kwenye vitu visivyo vya msingi katika maisha ya watanzania tulio wengi.... samahani lakini

Miss tz fanya yako mama...pole kwa yalokukuta.. waandaaji Wamekupa taji wenyewe kwa sababu zao wenyewe, so wasikusumbue..tena wakuache kabisa Mwanamkelive wangu, ningekuwa mimi ni wewe nisingeenda kwenye press ya kujichoresha...dhambi hii abebe Mratibu wa mashindando na team yake...

Watz tulio wengi ni Wajinga sanaaa hasa katika kuchekecha masuala yapi ya Msingi na yapi ya yasiyo ya Muhimu! na si kosa letu bali ni mikakati ya watawala wetu kuhakikisha wananchi tunajikita kuongelea Mambo ambayo hayana Msingi sana kwa wananchi wengi, badala ya kufuatilia masuala ya msingi yanayohusu hatma zetu... na wamefaulu katika hilo na wataendelea kufaulu kwa sababu ubora wa Elimu yetu inazidi kuporomoka...usitegemee mtz aanze kuongelea mfano uchakachuaji wa Katiba Pendekezwa, wala kuhoji huduma muhimu zinazotokana na kodi yake.. never!!!

Mfano rahisi angalia kwenye mitandao ya kijamii ya watanzania na ulinganishe na nchi zingine mambo wanayoyapa kipaumbele katika kuyajadili kwa nguvu kama hii tuliyoweka kwa Miss Tz...Ukilinganisha Nguvu inayotumika kwenye Katiba Pendekezwa na Nguvu ya Miss Tz kuna tofauti kubwa sana...

Pia Angalia magazeti yanayosomwa sana, kisha utawajua watz tulio wengi.. si wote.. utatujua tuliowengi ni watu wa aina gani....

Waandishi wenzangu watendeeni Haki watanzania masikini ambao Taifa lao ni Taifa Tajiri sana lakini ndo Taifa lenye watu masikini sana...waandishi ndo maana tunaitwa makanjanja!! Ivi kweli airtime na rasilimali kubwa hivi mkaziweka kwa nguvu yote hii in the name of Miss Tz???? Ebu tuwahurumie Watz na sisi wenyewe na Taifa letu hili..... sisemi kama msiandike ila mmeshupalia sana kana kwamba Miss Tz ni "Katiba pendekezwa" 
~Joyce Kiria

Jay Z na Beyonce Wakata Watu Midomo Kwa Kurudia Kiapo Cha Ndoa

$
0
0
Rapper Jay Z na mkewe Beyonce Knowles wameamua kuzama tena kwenye kina kirefu cha maisha ya ndoa baada ya siku kadhaa za misukosuko na tetesi za kuachana.

Kwa mujibu wa jarida la ‘People’, mastaa hao ambao ndoa yao imetimiza miaka sita, wamerudia kiapo cha ndoa hivi karibuni.

“Walikuwa na matatizo makubwa. Lakini wameyatatua na wamerudia kiapo chao cha ndoa.” Chanzo hicho kimeliambia jarida la People.

Katika majira ya kiangazi wakati wakiendelea na ziara yao waliyoipa jina la ‘On The Run Tour’ kulikuwa na tetesi za ugomvi na kutengana vyumba wakati wa ziara hiyo lakini walipokuwa Paris, Ufaransa, Jay Z alitoa ujumbe mzuri kwa mashabiki kuhusu uhusiano wao.

“We love Paris. It’s special to us because we got engaged here, and this is where Blue Ivy was conceived.”

Jay Z na Beyonce wameendelea kushare picha za familia yao kwenye mitandao ya kijamii na wanaelezwa kuingia studio kuandaa album yao ya pamoja inayotarajiwa kutoka mwaka 2015.

Hasheem Thabeet aongea baada ya kuachwa na Pistons

$
0
0
Baada ya kutemwa na Detroit Pistons, Hasheem Thabeet amesema hawezi kukata tamaa.

“I came way too far. and i will keep working. I will not stop,” ameandika kupitia Facebook.

Thabeet alikuwa amesaini deal lisilo na guarentee (a non-guaranteed deal) na Detroit Pristons mnamo Sept. 24, baada ya kuachwa na Philadelphia 76ers, ambao walimchukua kutoka Oklahoma City Thunder Aug. 26.

Thabeet—ambaye alishika namba 2 katika 2009 NBA Draft na kuchukuliwa na Memphis Grizzlies—alikuwa mmoja wanne waliotemwa jana Jumatatu na Pistons. Timu hiyo pia imewaacha Brian Cook, Lorenzo Brown na Josh Bostic

Jaja, Tegete Wang’ara Yanga , Waondoa Gundu la Magoli

$
0
0
Wametoa gundu’. Hicho ndicho unachoweza kusema kwa Jerryson Tegete na Genilson Santos ‘ Jaja’ walipofungia Yanga kwa mara ya kwanza, wakati Simba wameendeleza rekodi ya sare jijini Mbeya na Azam wakiambulia kipigo.

Baada ya kucheza kwa dakika 360, bila ya kuziona nyavu, Jaja aliifungia Yanga bao la kwanza kabla ya Tegete aliyetokea benchi kufunga mabao mawili katika ushindi mnono wa magoli 3-0 dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Wakati Yanga wakipata ushindi uliowaweka kileleni kwa saa 24.00 kabla ya Mtibwa kuivaa Mbeya City leo, watani zao, Simba walipata sare ya tano msimu huu baada ya kuiruhusu kirahisi Prisons kusawazisha bao kwenye Uwanja wa Sokoine 

Picha Kutoka Viwanja vya Jangwani Mkutano wa UKAWA Leo Hii

$
0
0

Hilo Ndilo Nyomi la Watu Viwanja vya Jangwani Siku ya Leo kwenye Mkutano wa Muunganiko wa Vyama vinne vya kisiasa yaani CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI NA NLD ambao umepewa Jina la Ukawa....Je Nyomi hiyo ni Dalili ya Watu Kuikubali Ukawa ? 
Toa Maoni yako!

Sakata la Shyrose Bhanji na Agenda ya Wanyarwanda Kumng'oa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki

$
0
0
Siku za nyuma tuliwahi kujadili kuhusu suala la Rwanda kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na athari zake kwa jumuiya, kutokana na tabia ya Wanyarwanda ya kujisikia kwamba wao wamezaliwa kutawala. 

Imefahamika kwamba wabunge wa Rwanda katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ndio wamekuwa wakiongoza njama za kutaka kumng'oa Spika Zziwa ili waweze kumuweka mtu atakayepitisha agenda za nchi yao kirahisi. 

Mbunge wa Tanzania, Shyrose Bhanji, ambaye aliongoza upinzani dhidi ya kung'olewa kwa Spika hivi sasa amejikuta akiwa adui wa Wanyarwanda kiasi cha kumtungia kashfa ili kumchafua. 

Hivi sasa kundi la wabunge wasiomtaka Spika Zziwa wamejipanga kuendeleza njama zao za kumng'oa kwa maelezo kwamba ameshindwa kumchukulia hatua Shyrose. 

Kama Watanzania tunapaswa kutambua njama hizi za kumchafua Mtanzania mwenzetu. Huu ni ugomvi mkubwa kuliko wengi wanavyoweza kufikiria.

Miss Tanzania ni Scandal Cover ya Mjadala wa Katiba Mpya

$
0
0
Watanzania tumefunikwa na scandal ya Miss Tanzania badala ya suala la Katiba Mpya. Pengine tufikirie upya (Rethink) hivi ni kweli tunapaswa kutumia muda na shilingi nyingi za bundle kurusha kupokea na kusambaza scandal ya Miss Tanzania badala ya Kuangalia kwa makini zaidi Suala la Katiba Mpya?? Jiulize pengine watawala wanafaidika zaidi na Miss Tanzania Scandal kwenye mitandao kuliko ambavyo Watanzania wangejikita kujadili Katiba Mpya kwenye Mitandao. Rethink Jiulize Kwa nini!

Sasa Hivi Hata Mambo ya Katiba Mpya Yamesha sahaulika......Watu ni Miss Tanzania kwa Kwenda Mbele...

Nimetembea Na ‘house Girl’ Wangu Na Sasa Ana Mimba

$
0
0
Naitwa baba Zai wa Buguruni Dar, nimeoa na tumebahatika kupata mtoto mmoja. Kutokana na mke wangu kuwa anafanya kazi, tulilazimika kutafuta mfanyakazi wa ndani. 

Mke wangu amekuwa akirudi kutoka kazini usiku sana na mimi huwa narudi nyumbani saa nane mchana. Nimejikuta muda mwingi nakuwa na mwanangu na ‘hausi geli’ tu ambapo mke wangu tumekuwa tukiwa na muda mzuri wa kuvinjari siku moja tu kwa wiki. 

Nisiwafishe ‘hausi geli’ huyu alitokea kunipagawisha kutokana na umbile lake, sijui ni tamaa au nini lakini nikajikuta nimezama katika dimbwi la mahaba kiasi cha kufikia hatua ya kumchukulia kama mke wangu kwasababu huduma nyingi alikuwa akinipatia. 

Kinachonipa wakati mgumu sasa ni kwamba, mke wangu anahisi kuwa natembea na huyu mfanyakazi wangu na kwamba ikibaini hivyo kwa ndugu jamaa na marafiki itakuwa ni aibu. Mbaya zaidi ‘hausi geli’ huyo sasa anadai ana mimba yangu. Hebu naomba unishari nifanye?

Mshiriki wa Tanzania Big Brother Afrika Atupwa Nchi ya Jumba Hilo ..Ni Yule Aliyejichua

$
0
0
Matumaini ambayo wengi wetu tulikuwa nayo kumuona mshiriki wa kutoka Afrika Mashariki ndani ya jumba la Big Brother Africa kuibuka na ushindi, yameshuka kwa kiasi kikubwa baada ya washiriki kutoka nchi mbili za Afrika Mashariki kutolewa ya jumba hilo.
Wiki moja baada ya washiriki Lillian kutoka Nigeria, Esther kutoka Uganda na Sabina kutoka Kenya kutolewa kwenye mjengo huo, Mtanzania Laveda aliyekuwa na mahusiano ya karibu na Permithias pamoja na Mkenya Alusa wamekutana na ‘rungu’ la kura lililowatupa nje ya jumba hilo.

Laveda anakuwa mshiriki wa 6 wa jinsia ya kike kutolewa nje ya jumba la BBA huku Alusa akiwa ni mshiriki wa kwanza wa kiume kutolewa #BBAHotshots

Mchezaji Nahodha wa Team ya Bafana Bafana Apigwa Risasi na Kufariki

$
0
0
Nahodha ambaye pia ni golikipa wa timu ya soka ya taifa la Afrika kusini Senzo Meyiwa amefariki dunia baada ya kupigwa risasi. Jeshi la polisi la nchi hiyo limesema.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika nyumba ya mpenzi wake iliyopo katika mji wa Vosloorus kusini mwa Johannesburg.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliichezea klabu ya Orlando Pirates na alicheza mechi nne zilizopita za timu yake ya taifa katika mechi za kufuzu za fainali ya mataifa ya Afrika.

Jumamosi alikuwepo katika tukio la timu yake pindi waliposonga mbele katika nusu fainali ya ligi ya Afrika kusini.

Katika maelezo yake Jeshi la polisi la afrika kusini limesema kwamba Meyiwa ameripotiwa kufariki wakati akiwasili hospitalini.

'Hakunaga Kama Diamond Platnumz' AwakimbizaTeam Ali Kiba Ukumbini

$
0
0
Jumamosi iliyopita, Oktoba 25, 2014 ilikuwa ni Siku ya Msanii Duniani ambayo kwa mara ya kwanza, Tanzania iliiadhimisha siku hiyo katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, mgeni rasmi akiwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Gharib Bilal.

Siku hiyo ilipambwa na matukio kibao nyuma na mbele ya pazia, ambapo kubwa lilikuwa ni la Jokate Mwegelo ambaye alikuwa miongoni mwa ma-mc wa shughuli hiyo ya kitaifa, kumfagilia waziwazi msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kwamba hakuna kama yeye, Ijumaa Wikienda lilikuwa ndani ya nyumba na kunasa matukio lukuki yaliyojiri.


JOKATE: HAKUNA KAMA DIAMOND
Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, Jokate alimfagilia waziwazi Diamond na kusema hakuna msanii anayeweza kumiliki jukwaa kama yeye.Sifa hizo alizozitoa Jokate kwa Diamond, zilisababisha ukumbi mzima ulipuke kwa kelele hasa ukizingatia kuwa wawili hao walishawahi kuwa wapenzi ila wakatengana na kile kinachodaiwa kuwa ni maneno ya watu.

Ukichanganya na kilichotokea kwenye Serengeti Fiesta 2014 ambapo Diamond ‘alikula za uso’ ukilinganisha na mpinzani wake, Ali Kiba ambaye alishangiliwa kwa nguvu, kitendo cha Jokate kumnadi Diamond jukwaani kilizidi kutengeneza vichwa vya habari.

DIAMOND ASAFISHA NYOTA
Baadaye Diamond aliangusha Number One na Mdogomdogo ambazo ziliwafanya watu wachizike hivyo kudaiwa kusafisha nyota yake iliyochafuka hivi karibuni kwenye Tamasha la Fiesta katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar alipozomewa.

Baada ya Kuachana na Mchumba Wake Rose Ndauka Hakamatiki, Pesa Zamtembelea Kama Wema na Kajala

$
0
0
Stori: Musa Mateja
Acha kabisa! Baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba’ke, Malick Bandawe kisha kurudi kwao, Kigogo jijini Dar, staa grade one wa Bongo Movies, Rose Donatus Ndauka anadaiwa hivi sasa hakamatiki hivyo hakauki viwanja.

Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda ambalo limekuwa likimnyatia kwa ukaribu Rose unaonesha kwamba tangu ametengana na mwanaume huyo amekuwa huru kupita maelezo huku akionesha jeuri ya fedha kama ilivyokuwa kwa mastaa wenzake, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja.

Pia uchunguzi huo ulibaini kwamba, mara tu baada ya kutoka ‘kifungoni’, Rose aliangusha bonge la sherehe ya ‘bethidei’ yake ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Collosseum, iliyopo Kariakoo jijini Dar na ndiko alikoanza kuonesha jeuri ya fedha.


Data zilionesha kwamba siku tishio ni ile ya Oktoba 18, mwaka huu ambapo Rose alikuwa kinara wa ushangiliaji wa timu yake ya Yanga, jambo ambalo siku za nyuma alikuwa hafanyi hivyo.
Siku hiyohiyo, baada ya kutoka uwanjani alikwenda kubadilisha mavazi yake ya njano na kijani kisha akatupia pamba za kuruka viwanja, akaibuka katika Tamasha la Fiesta kwenye Viwanja vya Leader, Kinondoni jijini Dar.

Akiwa ndani ya Leaders, Rose aliambatana na Mtangazaji wa Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ ambapo alikuwa akihaha kumnasa mwanamuziki wa Marekani, T.I aliyetimba Bongo kutumbuiza kwenye tamasha hilo.

Kama hiyo haitoshi, Alhamisi iliyopita, Rose alithibitisha kwamba kwa sasa hashikiki kwani alitimba kwenye pati ya bethidei ya shoga’ke, Dida iliyofanyika nyumbani kwake, Mwananyamala, Dar ambapo alikuwa kinara wa kujiachia kwa kusakata muziki na kumwaga ‘madolari’.

Bob Junior Apata Mchepuko Adendeka Nao Laivu Laivu

$
0
0
Stori: Imelda Mtema
Mchepuko? Baada ya kuachana na mkewe, Halima Ally, staa wa Nyota ya Chipsi Mayai na Prodyuza wa Sharobaro Records, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’ amenaswa live na mrembo anayejulikana kwa jina la Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ ambaye ni msanii wa filamu, wakiwa katika mahaba nipoteze kama ndege ya Malaysia.
Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Bob Junior ambaye hakupatikana lakini alipotafutwa Sabby ili kusikia kauli yake kuhusu uhusiano wake na Bob Junior alikiri na kusema kuwa ni mtu ambaye anampenda na ndiye anamfanya awe na furaha.
GPL

Wafanyakazi Walifanikisha Wizi wa Bank ya Stanbic - Kova

$
0
0
Watu wasiofahamika wanaosadikiwa kuwa ni Mjambazi jana walivamia Benki ya Stanbic katika tawi la Mayfair jijini Dar es Salaam nchini Tanzania na kupora kiasi cha fedha ambacho kiasi chake bado hakijafahamika.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa wa jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova ameziagiza benki zote za jijini humo kuhakikisha zinalindwa na askari polisi ili kukabiliana na uhalifu unaojitokeza mara kwa mara.
Kamanda Kova pia amesema wizi huo unaonekana ni mpango uliofanywa na baadhi ya watumishi wa banki hiyo kutokana na wezi hao kufanya tukio hilo na kuchukua fedha kwa urahisi Zaidi.
Aidha ameongeza kuwa waajiriwa wa mabenki hayo watafanyiwa uchunguzi pamoja na kuchukuliwa alama muhimu ikiwamo alama za vidole ili kukabiliana na uhalifu unaofanywa na baadhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu.
Kova amesema kuwa katika uchunguzi wa awali wamegundua wizi wa mtandao wa ndani ya banki kwa sababu hakuna nguvu iliyotumika na wakapata taarifa kuwa, kuna watu wamefungiwa chooni lakini kuna vitufe vya kubonyeza vya hatari ili kutoa taarifa lakini havikubonyezwa.

Ndoa ya Lady Jay Dee Sasa Basi Huu Ndio uthibitisho Kamili

$
0
0
Huku wakiendelea kugoma kuwa wameachana siri ya ndani ambayo inazidi kufumuka kwa mastaa wawili ambao wemetengana kinyumba ambao ni mwanamuziki Judith Wambura'Lady Jay Dee'na mtandazaji kiwango Gardner G Habash. 

Taarifa za hivi zinaeleza kuwa Jaydee ameanza kumfuta Gardner kwenye urithi wa mali mbalimbali ili baadae wasije kuleteana shida kwenye mgao.
Chanzo cha ndani kinasema kuwa tayari Jaydee ameshauza nyumba moja huko kimara na ula mgahawa wa Nyumbani Lounge ambao aliutangaza kuufunga sasa anaufungua kwa jina la Mog Bar& Reutsaurant
"Kiukweli ni kwamba hawa jamaawameachana rasmi ila hawataki hili lijulikane kwa upande wa Lady Jaydee ameanza kulihakiki mali zote walizokuwa wakishea na Gadner kwa ajili ya kuzipa umiliki wake,tayari nyumba moja wameshauza na sasa amekodi upya ule mgahawa wa Nyumbani Lounge na utaanza kazi rasmi" chanzo hicho.
na kwa upande mwingine ladyjaydee amemtimua kazi rasmi Gadner kama meneja wake na sasa kazi zote zinazimamiwa na Rapa Wakazi

Mfanyabiashara Arusha Ajiua kwa Risasi Baa Baada ya Kusababisha Ajali ya Gari

$
0
0
MFANYABIASHARA wa Arusha anayemiliki kampuni ya Tanzania Bush Camp yenye kambi za watalii katika hifadhi za Serengeti mkoani Mara na Manyara iliyopo katika mikoa ya Arusha na Manyara, Timoth Mroki (36) amejiua kwa kujipiga risasi tatu kifuani akiwa katika baa maarufu ya Arusha Raha iliyopo eneo la Shams, jijini hapa.

Kisa cha kujiua kwake kimetajwa ni kusababisha ajali, baada ya kuligonga gari lingine katika eneo la Mbauda wakati akitoka katika makazi yake yaliyopo eneo la Kwa Mrombo, jijini hapa.

Alifikwa na mauti katika tukio lililotokea kati ya saa 1:30 na saa 2:00 usiku, ndani ya baa hiyo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Mroki alifika katika baa hiyo baada ya kufanikiwa kuwatishia kwa risasi waendesha bodaboda waliokuwa wamemzingira katika eneo la ajali na kisha kuondoka kwa kasi kwa gari lake aina ya Nissan Navara.

“Alipiga risasi mbili hewani waliokuwa wamemzunguka wakanywea, akatumia mwanya huo kukimbia na moja kwa moja akafika Arusha Raha pengine kwa lengo la kujificha, na hapo akaanza kunywa…

“Ingawa inaonekana alikotoka alikunywa kidogo, alipofika Arusha Raha alikunywa haraka pombe mbili kali aina ya Valuu (Valeur) na wakati anamalizia ya tatu, akajikuta anazingirwa tena na wale waendesha bodaboda,” anasema mtoa habari huyo na kuongeza kuwa, baada ya kufyatua tena risasi mbili nyingine hewani, lakini bila ya dalili ya watu hao kutishika, ndipo akaamua kujimiminia risasi.

Habari zaidi zinasema wakati anazingirwa, naye akijihami kwa risasi wasamaria wakiwa katika harakati za kupiga simu Polisi walishtukia wakiingia katika eneo la tukio lakini tayari Mroki alikuwa ameshajitoa uhai baada ya kujimiminia risasi kifuani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatusa Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, ingawa Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi ya wilaya ya Arusha imekiri kuwepo kwa tukio hilo, lakini chanzo chetu kikikataa kutajwa jina gazetini kwa kuwa si wasemaji wa matukio ya polisi mkoani Arusha.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru.

Mwana FA, Umepiga hatua 4 mbele umerudi 8 nyuma, Disapointing

$
0
0
Alikushauri nani utoe wimbo wa pili harakaharaka ilhali 'MFALME' , ilikua bado maskioni mwa watu.

Ulikurupuka au kurupushwa.?

Huu wimbo ulofanya na KIBA si level zako,, 
kiba kabana pua ,sijui anaimbia wapi,? Kaharibu, we mwenyewe ume..! Damn.

Nilijua unarudi , ila umejipoteza., kwa hii ngoma, hata jina siijui.

Disapointed Me.

Baada ya Tatoo ya Jina, Nuhu Mziwanda achora tatoo yenye sura ya Shilole

$
0
0
Mambo ya Mahaba nipeleke West Africa nikateketee kwa Ebola yule Mpenzi wa Shilole Nuhu Mziwanda ameamua kuchora tatoo mkononi yenye sura ya Shilole kuonesha mapenzi yake kwa bidada.

Hii imekuja siku chache baada ya Shilole kuwashukia wanaomsema vibaya mpenzi wake kuwa ni mtoto, anambembenda kwasababu wapo kama mtu na mwanae,mara kijana anapenda kulelewa.Ndio Shilole alijibu kuwa huyo si mtoto kwani mapenzi anayompa chumbani ni mazito na angekuwa mtoto asingekuwa analilia mapenzi bali angekuwa analilia nyonyo kwa mama ake.

Baada siku kadhaa ndio kijana huyo akaibuka na tatoo ya hiyo kudhihirisha mapenzi kwa mwanadafada huyo. Hii ni tatoo ya pili Nuhu kujichora baada ya ile ya kwanza yenye jina la ShishiBaby. 

Btw hatuombei waachane ila siku wakiachana sijui itakuwaje?
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images