Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Aunty Ezekiel: Jamani niacheni ni maisha yangu

$
0
0
NYOTA wa filamu za Kibongo, Aunty Ezekiel amesema hapendelei kuwaona watu wakimsumbua kwa kumtaka afanye wanavyotaka wao, ilhali yeye ana maisha yake binafsi.

Mwigizaji huyo aliyefanya sherehe ya kuzaliwa siku chache zilizopita, alisema licha ya kwamba yeye ni kioo cha jamii, lakini kuna wakati anapaswa aachwe ili aishi maisha yake binafsi, kwani anaamini umaarufu siyo mzigo.

“Nikiwa kama msanii ninapaswa kuishi maisha ya aina fulani ili niwe mfano kwa jamii, kinachonishinda ni watu wanaotaka niishi vile wanavyotaka wao, jambo ambalo si sahihi, ni vizuri wakakumbuka kwamba na mimi ni binadamu na nina maisha yangu binafsi,” alisema na kuongeza:

“Mfano katika akaunti zangu za mitandao ya kijamii, watu wananichagulia picha za ‘kupost’ kila siku kioo kioo, mnatuita vioo vya jamii wakati mnatutukana kila siku, kioo changu kimevunjika mjue hivyo nitafanya vile ninavyotaka na si mtakavyo ninyi,” alijigamba mwigizaji huyo.

‘Mchezaji Mkude wa Simba Akitua Yanga tu Kazi imekwisha’

$
0
0
KOCHA wa Simba, Patrick Phiri amefichua siri moja kwamba kiungo mkabaji wake, Jonas Mkude, hana muda mrefu atasaini mkataba wa miaka miwili Msimbazi lakini endapo akishawishika na kukimbilia Yanga au Azam kazi yake itakuwa imekwisha kisoka kwani atakuwa amejimaliza.

Mkude ambaye amebakiza mkataba wa miezi sita na Simba amewaambia Yanga wanaomnyemelea wampe Sh80 milioni ahame Simba ingawa viongozi wa Mnyama wameanza mazungumzo naye na wameshamkabidhi gari jipya ili kumshawishi atulie.

 Akizungumza na Mwanaspoti Phiri ambaye ni raia wa Zambia, alisema hakuna shaka kwamba kwa sasa nchini hakuna kiungo aliye katika kiwango bora cha kuweza kukaba na kuchezesha timu kama alivyo Mkude lakini anatakiwa kuwa makini na uamuzi wake.

“Nafahamu soka ni kazi yake hilo halina ubishi, kwa uwezo wake sasa ni wakati wa kupata mafanikio makubwa kupitia kipaji chake, nafikiri hatakiwi kufanya kosa kuondoka Simba,  atulie hapa ajijenge kiakili kuhimili soka la ushindani,”alisema Phiri.

“Bado anahitaji kucheza Simba labda afikirie hivyo baada ya miaka miwili mbele atakuwa na akili ya kuweza kuhimili presha kubwa kama hiyo akihama sasa sawa lakini kuna uwezekano mkubwa wa kumaliza kipaji chake.”

Phiri alisema mara baada ya kusikia taarifa za kiungo huyo kutaka kuondoka alimwita na kuzungumza naye juu ya uwezekano wa kuendelea kubaki Simba na juu ya maisha halisi ya klabu hiyo.

“Akiondoka Mkude hali ya kikosi chetu itakuwa mbaya zaidi, kwa sasa ni kama lulu ndani ya kikosi, ni mchezaji wa kiwango cha juu ambaye kila klabu ingependa kuwa na huduma yake,” aliongeza.

“Baada ya kupata habari kuwa anamaliza mkataba wake nilimwita na kuongea naye, nilimwuliza juu ya maisha ya Simba kwa kipindi alichokuwa pale, nilimwuliza pia juu ya changamoto na kama anayafurahia maisha pamoja na sisi,” alisema Phiri na kuongeza

“Ameniambia hana shida na maisha ya Simba, ana furaha ya kuendelea kuwa pamoja na sisi hivyo nimeuomba uongozi ujitahidi kumalizana naye mapema, najua viongozi wangu ni watendaji hivyo mambo yatakwenda sawa.”

Wakati huohuo Phiri alisema kikosi chake kinaendelea vizuri na maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya Ruvu Shooting ambapo ameweka nguvu kubwa katika kuhakikisha washambuliaji wake wanafunga mabao mengi pamoja na kuimarisha ulinzi.

“Wachezaji wapo kwenye hali nzuri, kila mmoja anajitahidi kutimiza majukumu yake, wiki hii nimeweka nguvu kubwa kwenye mbinu za ushindi, tutakata kushinda mechi ijayo,” alisema Phiri.

Baba Diamond Amsaka Wema Sepetu, Ataka Kujua Kisa cha Kuachana

$
0
0
Stori: Musa Mateja na Gladness Mallya

Baada ya Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’ kummwaga mwanaye, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, baba mzazi wa jamaa huyo, Abdul Jumaa ‘Baba Diamond’, amenaswa akimsaka mrembo huyo ili kujua mbichi na mbivu.

‘UBUYU’ KUTOKA KWA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya kusikia habari za mwanaye kumwagwa na Wema aliumia roho kwani anamkubali Wema kuliko warembo wengine wote ambao walishatembea na mwanaye huyo.

“Hakuna habari mbaya kwa baba Diamond katika kipindi hiki kama ishu ya Wema kumwaga.

MAUMIVU
“Unaambiwa ‘mdingi’ aliumia sana kwani huwa anampenda mkwe wake Wema.
“Baba Diamond anaamini kabisa kwamba Wema ana nyota ndiyo maana Diamond akiwa naye huwa anang’ara sana,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
TATIZO NI NINI?
“Amekuwa akimsaka Wema ili ajue tatizo ni nini na kama kuna uwezekano wakae wayamalize.”
Habari zilieleza kwamba, kwa wiki nzima, baba Diamond amekuwa akimfuata Wema nyumbani kwake, Mtaa wa Bwawani-Kijitonyama jijini Dar lakini amekuwa akimkosa.

RISASI JUMAMOSI MZIGONI
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili (Risasi Jumamosi) lilipiga kambi kwa siku kadhaa getini kwa Wema huku likiweka mtego ambao juzikati ulimnasa mzee huyo.Baba Diamond alishuhudiwa akigonga geti kwenye nyumba hiyo anayoishi mkwe wake na kuzungumza na mlinzi ambaye alimwambia kuwa mwanadada huyo hayupo.

Kwa mujibu wa mlinzi wa getini hapo mzee huyo alikuwa akiomba kumuona Wema ili amuulize sababu ya kumwacha Diamond ambaye walikuwa na mapenzi kama ya njiwa.Baada ya kumkosa mzee huyo alisema anaendelea kumsaka hadi atakapompata ili wazungumzie ishu hiyo kiundani.

WAZO LA KWENDA KWA DIAMOND
Baada ya kuondoka nyumbani hapo kwa Wema, mzee huyo alisema huenda yupo kwa Diamond na hata kama hatakuwepo itabidi azungumze naye juu ya ishu hiyo ya kuachwa na Wema.
Ilisemekana kwamba mzee huyo anafanya jitihada zote hizo kwani kwa upande wake Wema ndiye mwanamke pekee anayemkubali.

Ilielezwa kwamba baba Diamond anataka kuwasikiliza kila mmoja na kuhakikisha anawaunganisha upya ili waendelee na safari yao ya kimapenzi hadi watakapooana.

TUJIUNGE NYUMBANI KWA DIAMOND
Huku wanahabari wetu wakipeana ishara kuwa wawahi getini kwa Diamond au Dangote, walipofika mahali hapo, dakika chache baadaye mzee huyo alinaswa getini kwa mwanaye maeneo ya Sinza-Mori, Dar akigonga mlango.

GETI LAFUNGULIWA
Baada ya kugonga kwa muda mrefu huku akiwa amefura, alitokea msichana ambaye alimfungulia mlango mdogo wa getini ambapo alikuwa akizungumza naye akiomba kuonana na Diamond bila mafanikio.

MAMA DIAMOND KWA MBALI
Wakati mzee huyo akiomba kuingia ndani, kwa mbali alionekana mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kwa mbali akiwa amekaa barazani bila kutambua sauti ya baba Diamond aliyekuwa akizungumza nje ya geti.

MADANSA WA DIAMOND
Hata hivyo, baadhi ya madansa wa Diamond walikuwa wakiingia na kutoka bila kumjali mzee huyo huku mmojawao akimfananisha bila kuwa na uhakika.Baba Diamond alipoona imeshindikana kumuona mwanaye huku mlango ukifungwa, aliondoka kwa huzuni akiamini ipo siku atawakutanisha Wema na Diamond ili kumaliza tofauti zao.

Gazeti hili liliwatafuta zilipendwa hao kwa nyakati tofauti lakini hawakupatikana hivyo jitihada za kuwafikia zinaendelea au hata wao wenyewe wakisoma habari hii watatupigia simu zetu kwani wanazo namba.

TULIKOTOKA
Huko nyuma, Diamond aliwahi kudai kwamba baba yake alimtelekeza yeye na mama yake ambapo waliishi maisha ya tabu na kushindwa kusoma kwa kukosa ada lakini hivi karibuni alitangaza kumsamehe.

Wakati Diamond akifanya kufuru kila kukicha na kugawa magari, baba yake anaishi peke yake,  maeneo ya Magomeni-Kagera, Dar.
Credits:Global Publishers

Baby Madaha na Isabela Ambae ni Mke Mtarajiwa Wafanya Ufuska

$
0
0

Stori: Imelda Mtema

HAMNAZO? Mastaa wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda ‘Bella’ na Baby Madaha  wamenaswa wakifanya vitendo vichafu maeneo ya Tabata jijini Dar baada ya kupiga masanga ya kutosha mwilini.

Kwa mujibu wa chanzo, Baby na Bella walifika maeneo hayo juzikati wakiwa wazima kabisa lakini baada ya kufakamia pombe kwa kasi ndipo walipoanza kufanya madudu huku mchumba wa Bella, Luteni Kalama, akiwakimbia na kuwaacha wenyewe.

“Walianza kushikanashikana kama wanasagana, wakapakatana huku wakiwa na chupa za pombe wakicheza kwa hisia za kimahaba kama mtu na mtuwe, yani Kalama anatakiwa ajiongeze vinginevyo mkewe mtarajiwa ataharibikiwa,” kilisema chanzo.
Credits:Global Publishers

Diamond Atanua na Boss Lady Zari Tajiri East Africa Nzima

$
0
0
Ni baada ya huyu mdada kutoka uganda ZARI a.k.a The boss lady binti tajiri East afica nzima mwenye gari na nyumba za kifahari kuwa karibu awali na "sukari ya warembo"
licha ya kupanda ndege moja wakija Tanzania na kupost picha zao instagram chanzo kimesema binti huyu na chibu walifika wote airport ili kujiandaa na safarit ya kuja tz. awali inasemekana wawili hao walikua karibu kitu kilichofanya wapeane kampani waje na ndege tarehe moja, ratiba moja, kwa siti moja, Hii imekuja wakati ambao kuna tetesi kuwa Dai Ameachana na Mpenzi wake Wema Sepetu.

Kuhusu Miss Tanzania 2014, Ndiyo Tumeshasahau au inakuwaje Hasa?

$
0
0
Iliripotiwa kuwa Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni ililikabidhi suala la utata wa Miss Tanzania 2014 kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ili kufanyiwa uchunguzi.

Pia ilidaiwa kuwa BASATA lina siku 7 za kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli wa utata uliojitokeza. Habari hizi za uchunguzi zilijulikana takribani wiki mbili zilizopita.

Lakini mpaka sasa hakuna taarifa zozote zile juu ya kilichojulikana kutokana na uchunguzi huo. Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni alinukuliwa akisema kwamba "Tayari tumeshalikabidhi kwa BASATA na tumewapa muda wa wiki moja kisha watatupa majibu na ushauri juu ya walichogundua, baada ya hapo sisi tutajua nini kifanyike na kutoa tamko rasmi"

Sasa huu ukosefu wa tamko rasmi tuutafsiri vipi? Ndo yale yale ya 'huu ni upepo tu, utapita' au...? Manake hii habari ndo imeshajifia zake na ni kama vile hakuna tena mwenye raghba ya kutaka kujua au hata kufuatilia ili kuweza kujua hatma yake!

Je, ndo Watanzania ndivyo tulivyo - wepesi sana wa kusahau mambo na hatuna hulka ya kufuatilia mambo mpaka tukajua mwisho wake? Au tunasumbuliwa na maradhi ya ukosefu wa nadhari?

Breaking News:Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu Amejivua Taji Kwa Hiari Yake

$
0
0

Sitti Mtemvu 2014 kajivua taji rasmi ndani ya hoteli ya JB BELMONTE Posta - Dar es Salaam.

Mshindi namba 2, Lilian Kamazima kakabidhiwa rasmi taji hilo.
Hapo mwanzo alikua anashutumiwa Kwamba amegushi vyeti na umri ili ashide umiss ambapo ilizua mjadala mkubwa  Hata hivyo alikanusha habari hizo kwamba sio za kweli ambapo hata Hashimu Lundenga alithibitisha kwamba hajagushi umri kwenye huu uzi Lundenga: Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu ni miss halali mwenye vigezo vyote.

Huyu Ndio Miss Tanzania 2014 Mpya Baada ya Sitti Mtemvu Kujivua Taji kwa Kashfa ya Umri

$
0
0
Baada ya Sitti Mtemvu 2014 kujivua taji rasmi ndani ya hoteli ya JB BELMONTE Posta - Dar es Salaam leo Mshindi namba 2, Lilian Kamazima kakabidhiwa rasmi taji hilo.
Sitti alikuwa anashutumiwa kwa kugushi vyeti na umri ili ashide u-miss ambapo ilizua mjadala mkubwa 

Zito atuhumiwa kuomba msaada wa kifedha kutoka iptl ili afifishe suala la escrow

$
0
0
Mwenyekiti wa PAC,Zitto Kabwe, atuhumiwa kuomba rushwa kutoka kwa mmiliki wa mtambo wa IPTL ili azime sakata hilo kupitia kamati yake.

Tuhuma hizo zimetolewa na katibu mkuu wa chama cha kijamii ambae amedai message ya Zitto kwenda kwa singasinga huyo ilinaswa.

Hata hivyo,mh.Zitto amekana tuhuma hizo na kudai kuwa maamuzi hafanyi peke yake na kwamba kashifa hiyo ni kubwa inayoweza kuangusha tembo mkubwa na hiki kinachoendelea hivi sasa kuhusu sakata hilo ni kishindo cha tembo huyo anaetaka kuanguka.

MY TAKE:
Pamoja na mapungufu ya Zitto, lakini kwa hili, sidhani kama ni kweli.

Amini Usiamini Wema Sepetu na Penny Wamaliza Tofauti zao

$
0
0
Good news iliyonifikia usiku huu kuwa Mtangazaji wa TV Penny Mungila aka VJ Penny na staa wa Bongo Movie Wema Sepetu wamemaliza tofauti zao baada ya kutoelewana takribani miezi kadhaa iliyopita.Upatanisho huo umefanywa na Junaitha ambaye aliandaa chakula cha usiku katika hoteli ya Sea Cliff Hotel Dar es Salaam.
Mastaa hao wawili walitengana baada ya kila mmoja kuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo Fleva Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platinumz huku wakiacha gumzo katika mitandao ya kijamii.

Diamond Platnumz na Zari Katika Mapozi Tofauti ..Movie Ndo Limeanza Au?

$
0
0

Thank you @diamondplatnumz for this opportunity. Africa get ready for our new project #uganda #Tanzania
Baada ya zari Kupost hiyo Picha insta hizi ni Baadhi ya message kutoka kwa Fans wao:

 maulidmlangwa
Kwanza walitoka wote south afrika Pamoja,walipanda ndege moja,walikaa siti pamoja,walishuka dar pamoja,wanakutana sehemu mbalimbali za starehe pamoja,wanafanya project Pamoja! Mimi nahisi kizungu zungu mwenzenu!

who_iz_the_boss
Who else was talking?? Abi next tym u should learn how to watch n keep calm. My boss is too smart to play around. Thanks for ur time

dalalmwanamke
Diamond ukirudi kwa wema umelogwa tena alokuloga mifupa saiv loh! Huyu ndo wife sio material tuu bali materialization ana kila kitu kashulishuli anajitambua husemi ana shida ya pesa mmh mmmh kikubwa na point yng ya msingi ilipo ni #Hardworkerwoman soo pleeeez @zarithebosslady naomba utuokoleee huyu star wetu hope mkiwa nae atafikia anapowaza kila siku plz i berg you @zarithebosslady ntaliaaaaaaa

fruiternest
I am waiting to see this episode. Its ridiculous u never even post your husband .... ur rich , u lost my respect! No project ... this is scandal

Video ikionyesha Jinsi Lundenga Alipokuwa Akitangaza Kuvuliwa kwa Sitti Mtemvu Taji la Miss Tanzania

$
0
0
Kamati ya Miss Tanzania ilikutana na Waandishi wa habari kutangaza maamuzi mapya November 8 2014 baada ya taarifa nyingi na mitandao ya kijamii kujaa stori za mshindi wa Miss Tanzania Sitti Mtemvu kudaiwa kudanganya umri taarifa ambazo hata hivyo alishawahi kuzikanusha.
Kama maamuzi mapya yalikupita unaweza kubonyeza hii video hapa chini…

Gardner Amkana Lady Jay dee Mchana Kweupe

$
0
0
Hii imetokea jana katika tamasha maalum la kituo kipya cha kazi cha Gardner E.FM ambapo Gardner alipanda jukwaani kujitambulisha mashabiki waliokuwepo wakamuuliza shemeji Jaydee yuko wapi? Akawajibu i am single boy now kisha akaomba awekewe nyimbo ya Single boy ya Ali Kiba na kuicheza jukwaani huku akimpandisha jukwaani shabiki wa kike na kumwambia amvue tishet yake kimahaba kuthibitisha usingo boy wake ambapo demu huyo alimvua kwa staili hiyo gardner huku ukumbi ukilipuka kwa shangwe.

Angalia Video Jinsi Diamond Alivyomuimbisha Mdogo Mdogo Yemi Alade Ndani ya Coke Studio

$
0
0
Diamond (Tanzania) brings his latest track to Coke Studio Africa for a fusion performance with Yemi Alade (Nigeria). The energetic dance gets the audience on their feet, with Yemi bringing in her dancing prowess.

Rais Jakaya Kikwete Afanyiwa Upasuaji Nchini Marekani

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja
unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa.
Hali ya MheshimiwaRais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.

Nuhu Mziwanda Aongelea Habari ya Kupigwa na Shilole..'Asema ni Mapenzi'

$
0
0
Stori: Imelda Mtema

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amefunguka kuwa  watu wanaomsema vibaya kuhusu yeye kupewa kichapo na mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wanakosea kwani anaamini kufanywa hivyo ni mahaba.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Mziwanda alisema kuna taarifa zimeenea kuwa huwa anapigwa na Shilole pindi anapokosea lakini ukweli si kupigwa ‘live’ bali ni kupigwa kimahaba.
“Jamani kupigwa wanakozungumzia watu sielewi lakini mimi ananipiga kimahaba, wanaosema kuwa mpenzi wangu ananipiga washindwe, watuache kwa raha zetu,” alisema Shilole.

Mwigizaji Jack Pentzel na Mumewe Kimenuka

$
0
0
NDOA ndoano! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Steven Pentzel ‘Jack Pentzel’ na mumewe Gardner Dibibi wanadaiwa kukinukisha na kuingia kwenye gogoro la kila siku hadi mwanaume kutaka kuondoka nyumbani wanakoishi Mbezi-Shamba jijini Dar.

Kikizungumza na Ijumaa Wikienda, chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wanandoa hao, kilisema kwamba, kila kukicha wawili hao wamekuwa wakigombana na sababu kubwa ni Jack kuchelewa kurudi nyumbani.

Ilidaiwa kwamba, tangu Jack awe na ushosti na staa mwenzake wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka amekuwa ni mtu wa kujiachia na kujisahau kwamba ni mke wa mtu. “Yaani ndoa ya Jack inashikiliwa na uzi kwani kila siku wanapigana na hivi karibuni mumewe alikusanya nguo na kuweka kwenye begi akitaka kuondoka nyumbani.

“Tatizo mwanamke anachelewa kurudi nyumbani, mumewe akimuuliza ndiyo mgogoro unaanzia hapo,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilimsaka mume wa Jack, Dibibi ili kueleza ukweli juu ya suala hilo.
Credits:Global Publishers

Hata uwe mrembo vipi Ukipenda Taarabu Maksi Zinashuka

$
0
0
Inaitaji roho ngumu kama paka kuingia kwenye beef na waamini wa taarabu lakini kwa sababu ni kweli acha nisimamie kweli yangu hata kama wakimind poa tu....maana maisha yangu ni yangu na ninaamini sana kwenye ukweli...hili swala nalijuwa vema. Kuwa kila mtu anahaki kupenda kile anachoona kinafaa kwake.

Huwezi kumlazimisha mtu kupenda aina ya muziki ila kuna wadada hapa mjini wanajifanya wanajua kukariri taarabu, watu mpo bar au kwenye daladala taarabu ikipigwa mtu anafuataisha maneno mwanzo mwisho bila kukosea na taarab zilivyo ndefu, Wengi wa Aina Hiyo ni Washari sana, Hata Ndoa zao nyingi zina matatizo.

Haki ya nani hata kama ungekuwa mzuri kama cleopatra kwangu nakushusha maksi kama ni mwanafunzini yule unayestahili SAP

Team Wema Wamweka Kati Diamond Baada ya Tetesi za Kutoka na Zari the Lady Boss

$
0
0
Kinara wa Team Wema Dougiemasta15 huku instagram amefunguka haya kuhusu Diamond:

kiroho safi kaka shemej wala hatugombani..ujue dai ss sote ni waafrica ndio wepesi kuja na conclusion na tunaudhaifu wa kuchunguza ujue shemej wengi tunataman kuamin kuwa hii ni project na surely we will b so proud ila shemej kinamna flan ww huaminiki huwa unakuwa na project nying sana lkn zinaend up kuwa coming soon...mfano JOKATE ukisema mnashot video sawa lkn matokeo yake unashot hadi behind de scene, penny pia ilikuwa project mwisho wasiku ukamprojectisha, wema nae movie matokeo yake mpaka leo producer sion location mmh kwa style hii kwel shemej kukuamin inakuwa ngumu sana cz hiz coming soon afu zinaend up kuwa coming forever zinatuchosha...inshu ya zari mbona kama umetuchakachua kaka shemej kwanz mlituambia mmekutana kweny ndege which its okey mkakaa siti moja means waliwaandalia siti zenu nyie watu mkijua mtapanda ndege moja still fea labda ndege ilikuwa empty so uka move..then katika kupoteza muda labda ndo mkaona mfanye something together still okey haya mkarud bongo muanze project kama project shemej ww unaimba zari designer na pia nimeskia anaimba not sure ss shemej hizi picha mala upo nyuma ya zari mmekumbatiana mala unamkiss shingoni ndio project yenyewe ss MLIENDA STUDIO LINI NA MKAREKODI LINI NA NYIMBO MLIANDIKA LINI MPAKA FASTA MUANZE KUSHOT VIDEO NA HIYO VIDEO HAINA DIRECTOR n mm ckuwahi kuambiwa kama sintah ni mtengeneza video mmmh shemej so you know zari ni mtu mzima ana watoto ana ameachwa na mumewe ana history ya kupenda ndogo ndogo na kuwaaribia maisha...if you lov ur career stick to it ila ukisema ufanye vitu kumkomoa mtu end of time ss ni mashabiki kama tunaweza kukupandisha naiman hata kukushusha tunawez sio kwa ubaya lkn ila his fake promises zako za something big is coming plz ur a business man try to keep ur promic......nitaendelea

Mwanamuziki Amin Naye Ajitoa THT Rasmi kama Alivyofanya Linah Sanga

$
0
0
THT jana imemuaga rasmi Amini ambaye  miongoni mwa mastar wanaotokea kwenye jumba hilo la vipaji Tanzania baada ya kuishi ndani yake kwa zaidi ya miaka 9 mpaka sasa.
Amini ambaye anakua msanii wa pili kutoka kwenye uongozi wa THT baada ya Linah ambaye aliagwa Mwezi July mwaka huu anasema ameishukuru sana THT kwa muda wote aliokuwa nayo kuanzia kama mwanafunzi hadi baadae kuwa mwanamuziki kamili.
Baada ya kukamilika kwa shughuli ya kutoa vyeti kwa walimu na uongozi wa THT akiwemo Mkurugenzi Ruge Mutahaba,Amini pia aliwapa nafasi waandishi na waalikwa kushuhudia kipande cha video ya wimbo wake mpya uitwao Mbeleko.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images