Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Kwa Matokeo ya Utafiti wa TWAWEZA...Hata Diamond Platinum Aweza Kuwa Rais

$
0
0
Nimekuwa nafuatilia kipindi cha asubuhi hii katika kituo cha TV cha StarTV. Nimewasikiliza wote. Huko Dar es salaam Dr. Kitila Mkumbo kaonesha upeo wake katika hili na Mwanaharakati Lenatus Mkinga ameonesha uwezo wake.

Kilicho nishangaza leo Kitila amepwaya sana kwa kutoa hoja zisizo na mashiko kwa kuegemea kumponda Dr. W. P. Slaa kwa kumwita hana adabu kwa kutokubaliana na matokeo hayo ambayo yamempa ushindi Edward Lowasa.

Kitila ameonesha kutokuegemea upande wowote pale alipotamka wazi kuwa utafiti huu una lengo la kumshafisha mtu fulani na ndiyo maaana watu walifanya sherehe ya kupongezana. Kaenda mbali na kutaja kuwa kundi hilo lililosherehekea ndilo hilo hilo lililompatia Dora 2500 cash ili aandae kipindi kwenye TV kwa lengo la kumsafisha mtu wao. Alizichukua fedha hizo na kuziwasilisha kwa viongozi wa CCM na kusema nimepewa fedha hizi kwa lengo la kumsafisha EL. Ameongeza na kusema kuwa utafiti huu umelenga kwenye muonekano wa mtu na sio utendaji au uadilifu katika taifa. Anasema unawezaje kumpa mtu ushindi MWIZI WA MABILIONI YA WATANZANIA kwa kuandaa kampuni fake ya RICHMOND isiyokuwa na usajili wala leseni!!!!!

Ameongea mengi lakini kubwa kuliko ni pale aliposema kwenye orodha ya washindanishwaji kama angewekwa DIAMOND PLATINUM nae angepata kura za kutosha kama vile walivyopata wengine ambao hata kutangaza nia hawajatangaza mf. Tundu Lissu na Magufuri achilia mbali Zitto na wengineo waliotangaza.

My Take:

Dr. Kitila Mkumbo usimlaumu Dr. Slaa kwa wewe kujiita msomi na kumdharau Dr. Slaa kwa kumuita hana adabu. TWAWEZA ninaijua haswa chimbuko lake na sio kama unavyotaka watu tuamini kuwa ni asasi ya kikanda. Pia unanipa mashaka na U-Dr wako kwani kwa sasa unavyoonekana huna tofauti na Prof. wa Kichina....... Jirekebisha Brother unapotea....

By Alfred Daud Pigangoma

Mastaa kumfanyia Edward Lowassa sherehe ya kumpongeza

$
0
0
SIKU chache baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kutangazwa kuwa anaongoza katika kinyang’anyiro cha urais 2015, mastaa mbalimbali wanaomuunga mkono wameandaa mkakati wa kumfanyia sherehe ya kumpongeza.

Chanzo makini kilichopo ndani ya kamati ya wasanii hao wa Bongo Movies, kitendo cha Taasisi ya Twaweza kutangaza kuwa Lowassa anaongoza na kuwagaragaza makada wenzake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kwao ni ishara tosha ya ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao.

“Mastaa wa Bongo Movies wanaomuunga mkono Lowassa wameandaa bonge la pati la kumpongeza Lowassa na siku hiyo watakula, watakunywa maana mipango yao tayari wanaona inakwenda vizuri na hakuna mtu ambaye anaweza kumuangusha katika chama hicho,” kilisema chanzo bila kutaja lini na wapi watakapofanyia sherehe hiyo.
Mbali na sherehe hiyo kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali, chanzo hicho kimeeleza kuwa wanatarajiwa pia kualikwa wananchi mbalimbali wanaomuunga mkono Lowassa.

“Safari ya kuelekea uchaguzi mkuu ndiyo imeanza rasmi, Twaweza wametafiti na kubaini kile ambacho sisi tulikuwa tunakiamini, Lowassa hana mpinzani CCM, ushindi ni lazima,” kilisema chanzo hicho.

Wasanii ambao wanatajwa kuwa upande wa Lowassa ni Jacqueline Wolper, Esha Buheti, Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’, Wema Sepetu ‘Madam’ na wengine kibao.

Taasisi ya Twaweza iliyofanya utafiti kwa mwezi Septemba, ilitangaza matokeo hayo Jumatano iliyopita na mtafiti wake, Elvis Mushi ambapo alisema wananchi 1,445 walihojiwa kwa njia ya simu ambapo Lowassa alipata asilimia 13 huku waziri mkuu wa sasa, Mizengo Pinda akimfuatia kwa kupata asilimia 12.

Wengine waliopigiwa kura katika utafiti huo ni Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbrod Slaa aliyepata asilimia 11, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akipata asilimia 6 huku Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe akiondoka na asilimia 5.

Chanzo: GPL

Mgao wa Mali wa Gadner na Jide Utata

$
0
0
HALI tete! Bado vuguvugu la madai ya kuvunjika kwa ndoa ya mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteni’ na Mbongo Fleva, Judith Daines Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee au Jide’, sasa lingine limeibuka ambapo mali za wawili hao zinatajwa kuzua utata, Risasi Jumamosi  linachambua

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani, Gardner ameshapeleka hati ya kesi kwa mwanasheria wake kwa kusudio la kumpandisha kizimbani mtalaka wake huyo ili mgawo wa mali ujulikane na kila mmoja apate haki yake.

KILICHOZINGATIWA
Kilichozingatiwa katika mgawo huo ni uhalali wa ndoa yao iliyofungwa Mei 14, 2005 ambapo mali zote zilizopatikana ndani ya ndoa ni za wote kwa mujibu wa sheria ya Ndoa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Gardner anataka mgawo wake, lakini sasa utata ulioibuka ni kwamba, inaonekana kama mali zote ni za Jide kwa vile zimeandikwa majina yake hivyo jamaa ana wasiwasi kwamba Jide anaweza kusema mahakamani kuwa alizichuma mali hizo kabla ya ndoa,” kilisema chanzo hicho kilicho jirani na familia hiyo.

Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, utata huo umemfanya Gardner kuwa bize ili kuhakikisha anaumaliza hususan kwenye nyumba yao iliyopo Mbezi ambapo wengi wanaamini ilijengwa kwa kutumia fedha ya Jide kabla hawajafunga ndoa.

MALI ZINAZOTAJWA
Mali zinazotajwa kuibua utata ni Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Kinondoni, Dar ambao hivi karibuni Jide aliubadili jina na kuuita M.O.G Restaurant. Mgahawa huo walipangishwa na mtu.

Kuna madai kwamba, Jide na Gardner kabla ya ndoa yao kuparaganyika walikwenda kwa mmiliki huyo na kusema wameamua kuuacha baada ya mkataba wao kumalizika. Lakini kilichoonekana baadaye, Jide alirudi kwa njia ya uani na kuanzisha mkataba mpya bila Gardner na kuuita M.O.G.

Mali nyingine mbali na nyumba na mgahawa ni mabasi madogo mawili aina ya Toyota Hiace, moja la Machozi Band na la M.O.G Restaurant. Mabasi hayo yameandikwa Lady Jaydee & Machozi Band. Hata hivyo, yapo madai kwamba Machozi Band nayo imebadilishwa jina, sasa inaitwa Lady Jaydee & The Band.

Mali nyingine ni Albamu zote za Jide alizotoa tangu mwaka 2005 wakiwa tayari kwenye ndoa ambapo kwa kawaida mauzo yake ni endelevu na gari la kutembelea aina ya Range Rover Vogue.
Albamu hizo ni  Moto (2005),  Shukrani, The Best of Lady Jaydee (2006) na Nothing But the Truth (2014).

KAMA NI KUPATA
Chanzo kinabainisha kuwa, uhakika wa mali anazoweza kupata Gardner ni mgawo wa pesa kwa mauzo ya gari hilo la kutembelea na nyumba ambapo inaaminika ndiyo mali ya kifamilia zaidi. 

SHERIA YA TALAKA 
Risasi Jumamosi lilitembea ofisi za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (Rita) jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujua sheria za talaka zinasemaje!

1. Mwenza mwenye nia ya kuomba ndoa ivunjwe anatakiwa kupeleka malalamiko yake  Baraza la Usuluhishi la Ndoa linalotambuliwa kisheria ambapo ni Ofisi ya Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Baraza la Kata, Mabaraza ya Ndoa ya Kidini katika Misikiti
na Makanisa.

2. Baraza litasikiliza malalamiko na likishindwa kusuluhisha, hati maalumu itaandikwa kwenda mahakamani ikielezea mgogoro kwa kifupi na baraza kutoa maoni yake kwa suala husika.
4. Mahakama itasikiliza shauri husika na ikiridhia itatoa tamko la kuvunjika kwa ndoa (decree).

Tamko la kuvunjika ndoa litawasilishwa Rita kwa ajili ya kusajiliwa na kuingizwa katika daftari la talaka. Baada ya hapo msajili atatoa hati ya talaka ambayo ni uthibitisho wa kuvunjika kwa ndoa na utaratibu wa mgawanyo wa mali utafuata kwa kila kilichochumwa (hata kijiko) wakati watalaka hao wakiwa ndani ya ndoa.

JIDE AFICHA MAWASILIANO YAKE
Risasi Jumamosi lilimsaka Jide kwa njia mbalimbali lakini hakupatikana. Baadhi ya watu wamesema kwa sasa mwanamuziki huyo ameficha mawasiliano yake.

ALICHOSEMA GARDNER
Gardner alipotafutwa na mwandishi wetu kwanza alianza kwa kukana madai kwa mtindo huu.
Mwandishi: (anajitambulisha kwa jina na kampuni anayofanyia kazi), najua uko kwenye mgogoro wa mali na shemeji (Jide).

Gardner: Kwanza huo mgogoro unaniambia wewe, mimi siujui. Lakini kwa hayo unayotaka kuniuliza nasema no comment (sina cha kusema).
GPL

Wanawake Wanaovaa Nguo Fupi Kenya Wakiona Cha Moto ..Angalia Video Huyu Anavyovuliwa Hadharani

$
0
0
Kenya Kimenuka kwa Wanawake Wanaovaa Nguo Fupi ama Suruali za Kubana na Kuachia Makalio , Mpaka sasa yameripotiwa matukio kadhaa ya wanawake waliovaa min Skirts  kushambuliwa na kuvuliwa nguo hadharani mbele za watu ..Hili Hapa chini ni tukio mojawapo ...


Wapitiwa na Usingizi Mpaka Asubuhi Baada ya Kujipa Raha Ndani ya Gari

$
0
0
Watu wawili Mvulana na msichana Ambao hawakuweza Kutambulika kwa haraka Wamekutwa Asubuhi kweupe wakiwa kwenye usingizi mzito ndani ya Gari lililopaki Pembeni ya Barabara Maeneo ya Sinza wakiwa uchi Sehemu za chini, Kwa haraka haraka inaonyesha watu hawa walikuwa wakifanya mapenzi ndani ya gari na kisha kupitiwa na Usingizi ambao inaonekana umesababishwa na pombe kupita kiasi walizokunywa usiku.
Watu walijazana na kuanza kuchukua picha kupitia madirisha mpaka wawili hao waliposhtuka na kutokomea pasipojulikana..

Pale Ambapo Muathirika wa UKIMWI Anapoamua Kuyakatili Maisha ya Watoto Wake.

$
0
0
Watoto wadogo wamekuwa katika hatari ambapo mara nyingi tumesikia taarifa za watoto kufanyiwa vitendo mbalimbali vya kikatili na watu wazima.
Taarifa kutoka katika mitandao ya Nigeria imesema watoto wadogo wawili ndugu, mmoja mwenye umri wa miaka sita na mwingine miaka nane wamebakwa na mwanaume ambaye amewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mama yao.
Mtu huyo, Terkula Iorpuur mwenye miaka 32 aliyekuwa akijishughulisha na kazi za ujenzi, aliripotiwa kituo cha Polisi cha ‘B’ Division Police Station na mjomba wa watoto hao ambapo alikamatwa.
Mama wa watoto hao aligundua hali ya utofauti kwa watoto hao ambapo walikuwa hawatembei vizuri.
Mwendesha mashtaka Terzungwe Kajo amesema uchunguzi umeonyesha mshtakiwa huyo ana maamukizi ya VVU.
Kesi hiyo imesogezwa mbele mpaka tarehe 4 Desemba ambapo itatajwa tena na mshtakiwa amerudishwa gerezani.

Mwanamke Amnyoa Nnywele Mke wa Mtu Kwa Kutumia Kisu Baada ya Kuhisi Anatembea na Mume Wake

$
0
0

Kutoka Insta: Mwanamke mmoja mke wa mtu huko arusha Amemkata Nywele Mwanamke Mwenzake Ambae na mke wa mtu kwa kutumia Kisu Baada ya kuhisi anatembea na mume wake ..

Video ipo Hapa: Kwa hisani ya @teamukwelinauwazi


Raia Mwingine wa Marekani Akatwa Shingo na Wanamgambo wa Kiislam wa IS

$
0
0
Kanda moja ya video iliowekwa mtandaoni inaonyesha mauaji ya mtu wa kutoa huduma za misaada raia wa Marekani Abdul Rahman Kassig ambaye alikuwa anajulikana kama Peter Kassig kabla ya kutekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State nchini Syria mwaka uliopita
Video hiyo inamuonyesha mawanamume mmoja anayeonekana kuwa mwanachama wa Islamic State akiwa na kisu mkononi na maandishi yanayosema kuwa Peter Kassig ameuawa.
Kanda hiyo pia ina picha za watu kadha waliouawa ambao wanasemekana kuwa wanajeshi wa Syria waliokuwa wametekwa nyara.
Marekani imesema kuwa inafanya juhudi za kubaini chimbuko la kanda hiyo.
Bwana Kassig ambaye anajulikana kama Peter alitekwa nyara mwaka uliopita.
Mnamo mwezi Octoba kanda nyengine ya video ya kifo cha mfanyikazi mwengine wa misaada kutoka Uingereza Alan Henning iliisha huku Kassig akitishiwa

Udaku Specially Presents The All White Party At Escape 1, Tarehe 22 Nov 2014

$
0
0
The all White Party si ya kukosa Mdau wangu wa Udaku, Party itafanyika Escape 1 Tarehe 22 Mwezi Huu, Yamoto Band, Barnaba na FM Academia ndio watakuwa waburudishaji wakubwa ..
Entry: 
Normal: 10,000 Tsh
VIP:20,000 Tsh

Pia Lile gari la Gharama Kuliko Yote Bongo Aina ya Lamborgin litakuwepo kwa wale Watakao Hitaji kupiga Nalo Picha 

Masai Ajitosa Kwa Wema Sepetu, Apeleka Barua ya Kuomba Uchumba kwa Mama Wema

$
0
0
GOOD news? Habari mpya kutoka kwa mlimbwende asiyechuja Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam au Beautiful Onyinye’ ni kwamba, Mmasai wa Kigoma, Ayoub Nyembo ‘Masai’ ameibuka na kupeleka barua ya uchumba nyumbani kwa wazazi wa mrembo huyo, Sinza-Mori jijini Dar, Ijumaa Wikienda lina mkanda mzima.

WAZO LILIVYOIBUKA
Mtu wa karibu na Masai alilipenyezea gazeti hili habari kuwa, baada ya habari za Wema kummwaga mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuandikwa magazetini hivi karibuni, fasta Masai aliiona fursa ‘u-single’ kwa Wema, akatangaza nia ya kumposa kwani alikuwa akimzimia muda mrefu.
“Masai ametumia fursa, hakutaka kuchelewa maana wazo alikuwa nalo kitambo lakini alishindwa kufanya hivyo kwa kumhofia Diamond,” alisema mtu huyo.

AKUTANISHWA NA IJUMAA WIKIENDA
Baada ya mtu huyo wa karibu na Masai kupata mawasiliano ya Ijumaa Wikienda kisha alikutanishwa nalo maeneo ya Mwenge jijini Dar akiwa tayari ‘amejikoki’, mkononi akiwa na barua ya uchumba sambamba na bahasha yenye shilingi elfu hamsini kama posa.

Ijumaa Wikienda: Unataka kumuoa Wema kweli au unazingua?
Masai: Nipo ‘serious’ ndiyo maana unaona nimekuja kwako nikiwa kamili na mshenga wangu nipeleke kwa mama Wema.

SAFARI KWA MAMA WEMA
Huku mwanahabari wetu akigonga picha za kumwaga kwa kila hatua, alimwelekeza Masai huyo ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva nyumbani kwa mama Wema, Mariam Sepetu ‘Mkwe’ ambapo waliambatana na mshenga wake lakini walipokaribia, Masai alikaa sehemu na kumtuma mshenga azame ndani.

NDANI KWA MZAA CHEMA
Mshenga alipozama ndani, alikutana na mfanyakazi wa ndani (house girl) ambaye alipokea barua hiyo ya uchumba na kumpelekea moja kwa moja mama Wema.

BARUA YASOMWA
Baada ya kutua mikononi mwa mama Wema, aliisoma barua ya uchumba kisha akamuomba mshenga kuingia ndani huku akiwa na furaha hususan pale alipogundua kuwa mkwewe mtarajiwa (Masai) ni mtu wa Kigoma.

MAZUNGUMZO YA FURAHA 
“Kwa hiyo Wema wangu anatakiwa aolewe Kigoma akale migebuka eeh?,” mama alimuuliza mshenga.

Bila hiyana mshenga akajibu: “Ndiyo mama, Masai anaishi Kigoma ila ana nyumba zake Dar, huwa anakuja mara kwa mara kwenye biashara zake na pia ana mji Singida katika Kijiji cha Ikungi na ni mfugaji mzuri, ng’ombe anao wa kutosha.”


Shangwe zaidi iliongezeka kwa mama Wema baada ya kusikia Masai huyo ana mji Singida tena kwenye kijiji ambacho yeye anatokea akatoa masharti kuwa afuate taratibu za Kitanzania kwa kumtaka Masai azungumze na Wema kisha ampigie simu ndiyo apokee barua kwa amani.

HUYU HAPA MAMA WEMA
“Hili ni jambo la kheri jamani, nimekuelewa lakini uchukue barua hii sambamba na posa urudi kwanza ukamwambie huyo mkwe mtarajiwa azungumze na Wema wakikubaliana, Wema yeye ndiye aniambie siku ya ninyi kuja kutoa posa ili na mimi nijiandae,” alisema mama Wema.
Credits:Globalpublishers

Joyce Kiria Akwaa Skendo ya Utapeli ya ile ya Biashara ya Telexfree

$
0
0
Why Joyce? Hosti wa Kipindi cha Wanawake Live kupita Televisheni ya EATV, Joyce Kiria yupo kwenye wakati mgumu baada ya kukwaa skendo ya utapeli kwa marafiki zake (majina yanahifadhiwa kwa sasa) akidaiwa kuwashawishi kuingia kwenye biashara ya Mtandao ya Telexfree Network Marketing.

Kwa mujibu wa sosi makini, ishu hiyo imeibuka juzikati ambapo Joyce alikuwa akishushiwa zigo la lawama na marafiki zake hao huku baadhi wakitishia kumshitaki kwa kuwatapeli kwani wamepoteza fedha nyingi kwenye mpango huo wakidai hawajaona chochote.

“Dada Joyce aliwashawishi marafiki zake wengi, wakaingia na kila watu walipomshtua na kumwambia kuwa ni utapeli mtupu alikuwa akiwatolea lugha za kuudhi. Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Joyce na kumuuliza juu ya ishu hiyo ambapo alifunguka: “Ni kweli niliwashawishi marafiki zangu kwa sababu nilijua biashara hiyo inalipa na hata mimi nimeumia sana kuona imekufa kwani sikupenda.

“Nimepoteza fedha nyingi. Ilikuwa ni kama desi ilivyokufa, hakuna wa kulaumiwa.”
Joyce aliongeza kwamba, kama kuna watu ambao wanadai amewatapeli waende mahakamani kwa sababu hakuwalazimisha kuingia wala hakuwashikia panga.

Telexfree Network Marketing ni kampuni iliyokuwa ikijihusisha na biashara ya mtandao ambapo mhusika hutoa kiasi cha fedha huku akiunganisha watu wengine ambapo kipato chake kwa maana ya faida itaongezeka mara kwa mara kwa kadiri anavyounganisha watu wengi.
Credits:Globalpublishers

Nimegundua Baba Mwenye Nyumba Hunipiga Chabo Nikiwa na Mpenzi Sita Kitandani?

$
0
0
Ni Miez Mitatu Sasa Toka Nihamie, Lakin Kuna Jambo Moja Nimeligundua, Milango Yote Ina Kitobo Kidogo Kinachohitaji Umakini Kukigundua.

Cha Ajabu Nilipojaribu Kumtaarifu Baba Mwenye Nyumba Wangu Kukiziba...Alikuja Juu Na Kusema ,Niiache Nyumba Yake Kama Ilivyo. Nikaona Ngoja Niwadodose Wapangaji Wenzangu.

Walinishangaza Waliponiambia Hilo Tundu Ni Kazi Maalum Kwa Baba Huyu. Nimegundua Analitumia Kutupiga Chabo Na Ndio Maana Anataka Vijana Waliooa Ndio Wapange Hii Nyumba!

Ripoti ya CAG Kuhusu IPTL ya Kisiasa Kuliko Kisheria CAG Aburuzwe Mahakamani

$
0
0
Nimesoma magazeti kuhusu inayohisiwa kuwa ripoti ya CAG kuhusu IPTL.Nilichokiona ni bla bla za kisiasa zaidi kuliko kisheria.Mfano imeandika kuwa Tanesco wali-overpay IPTL kwa bilioni 321.Mkataba wa kisheria upo uliosainiwa na kila upande kuwa utalipa hiki na hiki hiyo overpayment inatokeaje? Ina maana TANESCO walikiuka mkataba na ku-overpay?

Halafu kituko kingine eti wali-overpay kwa muda wa miaka 10 mfululizo kutoka 2002 hadi 2012.Yaani mwaka wa kwanza u-overpay,wa pili uoverpay,wa tatu u-overpay hadi ifike 10 ndio uje ugundue leo? Tanesco kwa nini hawakuchukua hatua yeyote wakaamua wawe wana-overpay mwaka hadi mwaka? Hadi ikafika 10?

Jambo moja serious kisheria ni nani aliyekuwa mkaguzi wa hesabu wa TANESCO kwa miaka hiyo yote 10? Si ni CAG huyu huyu au yuko mwingine?.Je kila mwaka alipokagua hakuona hilo tatizo? Ripoti zake za auditing ziko wapi? Je ameliona tatizo hilo la overpaynment mwaka huu baada ya shinikizo la wabunge?

Kama ni kweli CAG ndie alikuwa mkaguzi wa mahesabu ya TANESCO inabidi aburuzwe mahakamani pia kwa kutoa ripoti zisizo kweli za Tanesco miaka 10 mfululizo kuanzia 2002 hadi 2012.

Download Wimbo Mpya Kutoka Kwa Mwasiti Akimshirikisha Kingzilla. Wimbo Unaitwa Leo.

$
0
0
Download Wimbo Mpya Kutoka Kwa Mwasiti Akimshirikisha Kingzilla. Wimbo Unaitwa Leo.

Mtoto Mwingine Atekwa, Auawa na Kukatwa Nyeti

$
0
0
WIMBI la utekaji na mauaji ya watoto katika Jiji la Dar bado ni tishio kufuatia wiki iliyopita, maiti ya mtoto Nuru Mohamed (7) mkazi wa Majohe Kichangani Wilaya ya Ilala, kuokotwa ikiwa imeharibika vibaya, tena baadhi ya viungo vyake vikiwa vimenyofolewa.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Novemba 6, mwaka huu, majira ya saa 12 jioni, baada ya watoto wenzake aliokuwa akicheza nao kudai kuwa Nuru alichukuliwa na mtu aliyekuwa amevalia mavazi ya Kininja na kutokomea naye.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwa eneo la tukio, walisema mwili wa mtoto huyo ulikutwa ukiwa hauna sehemu za siri, matiti, nyama ya kisogoni na makalio kukatwa na kuzibwa na gundi hali iliyoashiria ushirikina.

BABA MZAZI PICHANI ASIMULIA ILIVYOKUWA
“Nakumbuka siku ya kutoweka kwake, nilikua kazini nikapigiwa simu saa 12.45 jioni na kuelezwa Nuru ametekwa na mtu aliyevaa kininja, aliyemrubuni kwenda kumnunulia biskuti. “Nilielezwa kwamba muda mfupi baada ya kutoweka, watoto wenzake walipatwa na hofu na kumwambia mama yake kwamba kuna mtu kaondoka na marehemu hali iliyomfanya kuinuka na kuanza kufuatilia bila mafanikio.

“Niliungana na mke wangu pamoja na ndugu wengine kumtafuta hadi asubuhi bila mafanikio, nikiwa nipo maeneo ya Chamazi saa 2 asubuhi nilipigiwa simu na kuambiwa mwili wa mwanangu umepatikana maeneo ya lwa Mkandawile ukiwa umeharibika, nilienda na kukuta kuwa ni yeye.

“Tulitoa taarifa polisi ambao walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili hadi Hospitali ya Amana na muda mfupi baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari tuliuchukua na kuuzika makaburi yaliyopo maeneo ya ninakoishi,” alisema

Mjunbe wa Shina namba 15 Tawi la Majohe, Matanzira Thomas maarufu kwa jina la Kobra alisema kwamba matukio hayo ya utekaji watoto, kuwaua na kuondoka na sehemu ya viungo ni hatari hasa katika nchi ya amani kama Tanzania, hivyo ameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini na kuwakamata watu hao hatari.


Hatimaye Kivuko Kipya cha Safari za Dar es Salaam Kwenda Bagamayo Chawasili

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli leo amepokea kivuko kipya cha MV Dar es Salaam chenye uwezo wa kubeba abiria 306.

Kivuko hiki kipya kitatoa huduma ya usafiri kati ya Jiji la Dar es Salaam na mwambao wa Bahari ya Hindi hadi Bagamoyo. Kivuko cha MV Dar es Salaam kitakuwa na kasi kuliko kivuko chochote Afrika ya Mashariki na hasa mwambao wa bahari ya Hindi ukiacha Afrika ya Kusini.

Itakumbukwa waziri Magufuli amekuwa akiahidi kufanya jitihada za kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kununua kivuko kitakachofanya safari zake katika mwambao wa bahari ya Hindi mpaka Bagamoyo.

Kivuko hiki mkombozi wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kimejengwa na kampuni kutoka Denmark kwa gharama ya shilingi (Tanzania) bilioni 7.9.

Sifa kubwa ya kivuko cha MV DAR ES SALAAM:

1. Kina uwezo wa kubeba abiria kati ya 306 waliokaa hadi 400,

2. Kina spidi (speed) kubwa kuliko vivuko vyote Tanzania na hata Afrika ya Mashariki

3. Kina ghorofa mbili (Two Floors)

4. Kwa ndani kina makochi mazuri kabisa ya kisasa ikiwa pmoja na life jacket

5.Kina tekinorojia ya kisasa kabisa ya Nivigation.

Ripoti Maalumu ya CAG Kuhusu Akaunti ya Escrow Yakabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Pac Zitto Kabwe

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akikabidhi Ripoti maalumu ya CAG Kuhusu akaunti ya ESCROW kwa Mwenyekiti…

Tujikumbushe:

Ripoti ya sakata la uchotaji wa Dola za Marekani 200 milioni katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyotua bungeni wiki iliyopita, imeibua mambo mazito baada ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kugundua kuwa fedha zilizochotwa kwenye akaunti hiyo zilikuwa mali ya Tanesco.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza kuwa fedha zilizokuwa kwenye akaunti hiyo ni Sh306 bilioni wakati madai ya Tanesco kwa IPTL ni Sh321 bilioni, hivyo fedha zote za Escrow zilipaswa kwenda Tanesco na bado ingekuwa inadai.

Ukaguzi wa akaunti hiyo uliamuliwa na Serikali baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila kudai kuna ufisadi katika uchotaji wa fedha hizo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Akaunti hiyo ilifunguliwa baada ya kutokea mgogoro wa kibiashara baina ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Mama Yangu Amenionyesha Baba Yangu Halisi Baada ya Miaka 38, Nimemkataa Laivu

$
0
0
Mimi nina miaka 38 sasa, msomi wa elimu ya juu na nina kazi nzuri pia, nilikuwa naishi vizuri na wazazi wangu wawili I mean baba na mama, sasa hapa juzi baada ya ugomvi, mama ameondoka nyumbani na kuniambia eti baba nilienae sio baba yangu biological na baada ya kikao kirefu nimeonyeshwa baba mwingine wanaomsema ndio baba biological ila mbele ya watu wote nilimkana na kumwambia asinijue kabisa na wala sitaki kuharibiwa maisha yangu. 

Mimi nina baba yangu ambae amenilea na ndio naamini ni baba halisi kwangu, sasa wanakazania DNA mimi nikasema sitaki chochote na nisiingizwe kwenye ugomvi wa wazazi wangu na ninampenda sana baba yangu alienilea kwasababu amenisomesha shule za gharama na amenitembeza duniani na kunipa kila nilichotaka mpaka hapa nilipo namwona kama mtu namba moja muhimu kwangu hapa duniani.

Je waungwana nilichofanya ni makosa?

Wanawake Kenya Waandamana Kupinga Kuvuliwa Nguo Hadharani Kwa Wanao Vaa Nguo Fupi

$
0
0
Wanawake mjini Nairobi, Kenya leo wameandamana kupinga kitendo cha mwanamke mmoja kuvuliwa nguo wiki jana kwa madai kuwa alikuwa amevalia sketi fupi sana.
Wanawake wengi walikerwa na kitendo hicho wakisema kuwa kila mwanamke ana haki ya kuvalia mavazi yanayomfurahisha.
Hiyo wiki jana kanda ya video ilisambazwa kwa mitandao ya kijamii ikionyesha mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina hadi sasa akivuliwa nguo zake na wanaume katika kituo cha magari ya abiria kati kati mwa Nairobi.

Wanawake mashuhuri wakiwemo wasanii, wanasiasa na wanaharakati walilaani kitendo hicho wakihoji kwani mavazi ya mwanamke yanamhusu nini mwanamume ambaye sio mumewe wala jamaa yake.
Baadhi walikitaja kitendo hicho kuwa cha kinyama na kinachokiuka haki za wanawake.
Msanii mmoja mashuhuri Nyota Ndogo alinukuliwa akisema ikiwa wanaume wanawavua nguo wanawake kwa kile wanachosema ni mavazi yasiyo ya kiheshima, basi na wanaume wanaolegeza long'i zao na wao basi pia wavuliwe nguzo zao.

Lundenga Kikaangoni Tena Baada ya Sitti Kushindwa Kurudisha Zawadi Zote Alizopewa

$
0
0

Lundenga na Kampuni yake ya Urembo matatani tena baada ya Basata kuhoji kwanini Sitti Mtemvu Bado Hajarudisha zawadi zote alizoshinda Katika Mashindano hayo ya Urembo..
Basata Imesema Sitti inaitajika kurudisha zawadi zote alizoshinda kuanzia Miss Temeke, Miss Changombe na Miss Tanzania 2014 kwa vile huko pote alishiriki huku amedanganya Umri ..
Kazi Ipo .....

Je Unafikiri Hapo Haki Inatendeka Kweli ?

Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images