Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Mchepuko wa Zari The Boss Lady (Farouque) Abwaga Manyanga na Kusema Haya

$
0
0
Ninaripoti kutoka Uganda kama ifuatavyo: 

Baada ya Diamond kujisevia Zari kiulaini bila kutumia nguvu boyfriend wa Zari aamua kujiweka kando kwa madai kwamba ni bora awe single kuliko kuwa na Mwanamke asiyejiheshimu. Ameorodhesha tuhuma 5 ikiwemo kupasha kiporo na baba watoto wake, kuwa na mitafaruku ya mara kwa mara kuhusu mali za exhusband Ivan, kukutana na Diamond kwenye Ndege kisha kumalizana kiutu uzima na nyingine 3 Kama alivyoziorodhesha. 


Hata hivyo mchepuko mwingine wa Zari (basketballer LK4 BBA season 7 ambaye alikuwa anachepuka na Zari wakati Zari yuko ndoani) alimlaumu farouque kwa kumuuliza "are you mad"? 


Pamoja na lawama za LK4 bado jamaa anaonekana kuchoshwa na uchepukaji wa bidada kwani genye zake ziko karibu. 


Farouk Sempala is hurting following cozy pics of his ex-lover Zari and Tanzania's Diamond Platnumz that went viral. Diamond Platnumz and Zari at a Beach in Dar. Using his facebook profile, he made this post;

"I would rather remain single than have a beautiful wife that does not respect herself and turns out to justify her wrongs as rights, it's just a waste of time and calories." The post was followed by five other points and one of them was tagged to Zari and Diamond Platnumz - You bump into a singer on a plane and you call that a project!

Dully Sykes na Maunda Zorro Watoa Wimbo wa Matusi Mwanzo Mwisho..Download Hapa

$
0
0
Dully Sykes na Maunda Zoro Wameachia Wimbo wenye Mahadhi ya Matusi Ambapo Dully anasikika akiimba mambo ya chumbani huku Maunda Zorro Akilia kwa Mahaba..
Unaweza Kuudownload wimbo huo Hapa chini usikie mwenyewe...

It’s All Love: Wema Sepetu na Penny Wafanya Shopping Pamoja

$
0
0
Walikuwa marafiki wa damu, wakaja kuwa maadui.. na sasa ni marafiki tena. Baada ya kupatanishwa kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Junaithar siku kadhaa zilizopita, Wema Sepetu na Penny Mungilwa wameendelea kuuimarisha zaidi urafiki wao.

Penny ameshare picha kwenye Instagram akiwa pamoja na Miss Tanzania huyo wa zamani ambayo Wema pia ameirepost kwenye akaunti yake. Hiyo ni picha ya kwanza ya warembo hao wakiwa pamoja kuwahi kuweka kwenye akaunti zao katika kipindi kirefu.

Wakiongea kwa pamoja na Bongo5 leo wakifanya shopping ya nguo, warembo hao wamedai kuwa wana mipango ya kufanya filamu pamoja na wanatarajia kuingia kambini mwakani.

Picha hiyo imepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wao wanaopenda kuwaona wakiwa pamoja.

Wema Sepetu Aanika Kisa cha Kumwaga Diamond Platnumz

$
0
0
Na Musa Mateja
MISS Tanzania 2006/07 ambaye ni staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, amevunja ukimya kwa kuamua kuanika kisa cha yeye kummwaga aliyekuwa mwandani wake, nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Akizungumza na Amani katika mahojiano maalum jijini Dar, juzikati, Wema alianza kwa kufunguka kwamba, kuna watu wamekuwa wakizungumzia ishu ya yeye kumtema Diamond huku kisa wakiwa hawakijui na wengine wamehamishia sababu kwa nyota wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’, jambo ambalo si kweli.

Wema alimwaga ‘ubuyu’ kwamba, yeye ameamua kumpa likizo ndefu Diamond ili kila mmoja aweze kufanya mambo yake ya maana kwa uhuru mkubwa hasa baada ya jamaa huyo kunukuliwa na magazeti pendwa akisema hana mpango wa kuoa jambo ambalo lilimkatisha tamaa na kumwacha njia panda.

SAFARI YAKE CHINA NAYO TATIZO
Kuhusu suala la kusema amempa likizo ndefu ili kila mtu afanye mambo yake,
Wema alirejea safari yake ya China hivi karibuni ambapo Diamond hakutaka asafiri ila akalazimisha. Hapo aliona anatakiwa kuwa huru zaidi.

MWISHO WA LIKIZO
Wema alipotakiwa kutaja mwisho wa likizo hiyo endapo ni ya siku 28  kama ilivyo
kwa sheria ya kazi ya Tanzania, aligoma kusema chochote huku akisisitiza amempa likizo Diamond.

AMZUNGUMZIA ZARI
Staa huyo asiyekaukiwa na matukio, alikwenda mbele zaidi kwa kumzungumzia Zari ambapo alisema kuna wanaodai mwanamuziki huyo tajiri yuko kimapenzi na Diamond, lakini yeye haoni ukweli wowote kwani anajua wawili hao wana ‘projekti’ ambayo ni mawazo ya muda mrefu.

BOFYA HAPA KUMSIKIA WEMA
“Kwanza naomba watu wajue kuwa, projekti ya Diamond na Zari ninaijua na bahati nzuri Zari ni shoga‘ngu tangu kitambo hivyo yote yanayofanyika mimi nayatambua hatua kwa hatua pamoja na kwamba sijaongea na Diamond siku nyingi,” alisema Wema.

DIAMOND AULIZWA KAMA ANAITAMBUA LIKIZO NDEFU
Baada ya mazungumzo na Wema, mwanahabari wetu alimtafuta Diamond kwa lengo la kutaka kumfahamisha kama anafahamu kwamba amepewa likizo ndefu.
“Dah! Nashindwa niseme nini hapo! Lakini ujue maisha kila mfa maji siku zote haishi kutapatapa, kiukweli mimi hapo naona Wema anatoa majibu ya kisiasa tu.

“Nashindwa kujibu kila linalosemwa na watu ila kuna kipindi mtu hutakiwi kujibu kila kitu. Kuna mambo mengine yanatakiwa uyaache yapite tu.
“Mimi nimeachwa na Wema, Zari ni rafiki yangu tu, acheni projekti iendelee,” alisema Diamond huku akichekacheka kwa ishara ya furaha akijiandaa kuachia ngoma kali mpya iitwayo ‘Nitampata Wapi’ leo.

KWENYE WHATSAPP
Wakati Diamond akisema hayo, baadaye kwenye maelezo yake mafupi (profile) ya WhatsApp aliweka picha ya Zari huku akiambatanisha na maneno yaliyosomeka:
“Unapokosa usisikitike, Mwenyezi Mungu kakuandalia kizuri zaidi.”

Wema na Diamond wamekuwa na kasumba ya kuachana na kurudiana hivyo kuna kila dalili wawili hao wakarudiana tena.

Halima Kimwana Akana Kuhusika na Uhusiano wa Diamond na Zari

$
0
0
Mdada wa mjini ambaye ni dada wa hiyari wa msanii, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Halima Kimwana amedai kuwa hahusiki na uhusiano unaoendelea kati ya kaka yake huyo na mrembo kutoka Uganda, Zari.

Akizungumza na waandishi wetu, Halima alisema kuwa hawezi kuzungumzia suala lolote la Diamond na uhusiano wake na Zari kwa kuwa hahusiki na jambo lolote kati yao.

“Jamani mimi sifahamu chochote na siwezi kuzungumzia kwa kuwa sijui na sihusiki,” alisema Halima anayedaiwa kumuunganishia Diamond kwa mademu kibao japo tuhuma hizo anazipinga.

CUF Kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

$
0
0
Chama cha Wananchi CUF kimesema kitasusia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwaka huu kama serikali (TAMISEMI) haitabadilisha kanuni za uchaguzi huo ambazo anadai kuwa zina lengo la kuvikandamiza vyama vya upinzani.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha CUF Tanzania bara Magdalena Sakaya amesema serikali ya Tanzania imekurupuka kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu kwani haikuwa na mpango kamili kuendesha uchaguzi huo.
Sakaya amesema viongozi wa serikali wamekuwa wakitoa taarifa zinazokinzana juu ya uchaguzi huo kati ya Rais na Waziri Mkuu, ambapo Rais alisema katika kikao cha mashauriano ya vyama vya siasa kilichoandaliwa na TCD kuwa uchaguzi huo ungefanyika mwezi Februari mwakani na Waziri Mkuu kutangaza kuwa uchaguzi huo utafanyika
Desemba 14.
Kwa upande wa kiongozi wa CHADEMA bwana Fulgency Mapunda ambaye ni Afisa uhamasishaji Chadema amewataka viongozi wa halimashaurui zote kuacha kuwakandamiza wagombea wa upinzani kwa mashinikizo ya viongozi wa kisiasa.
Naye Diwani wa Kigogo kupitia CCM Richard Chegula amewataka viongozi wa upinzani wkuacha lawama kabla ya uchaguzi kwani waamuzi ni wapiga kura wenyewe.
Kwa upande wa Tamisemi kupitia Mkurugenzi wake wa serikali za mitaa bwana Calist Luanda amefafanua juu ya swala zima la uchaguzi huo, na kusema kuwa tuhuma zinazotolewa siyo za kweli

Navio Awakubali Wakali Bongo Flava Tanzania..Ataja Msanii Anaye Taka Kufanya Nae Wimbo

$
0
0
Rapa mkali kabisa kutoka Uganda, Navio ambaye kwa sasa yupo hapa nchini Tanzania kwa shughuli za kimuziki, amewataja wasanii Shaa, Diamond, Joh Makini, Izzo Business, Vanessa Mdee na AY kama wasanii kutoka hapa Bongo ambao anawakubali zaidi.

Navio ameiambia eNewz kuwa, kazi za wasanii hawa pamoja na moyo wao katika kazi ni kati ya vitu vinavyomfanya kuwaelewa zaidi pamoja na kufurahia kazi zao.
Rapa huyo pia ameweka wazi uwezekano wa kufanya kolabo na wasanii kutoka hapa Tanzania, akiwa tayari katika maongezi ya awali na msanii Izzo Business.

Zitto na Kafulila Walibezwa na Kudhallilishwa je Waliowadhalilisha leo Wanajisikiaje?

$
0
0
Kiukweli nilisikitika sana pindi nilipoangalia bunge na kumsikia AG akimdhalilisha Kafulila kwa kumuita tumbili ulikuwa ni ubaguzi wa hali ya juu mwafrika kumuita mwafrika mwenzake tumbili tunayaona ulaya tu tena kwenye mchezo wa kandanda.AG huyu hakuishia hapo akamtisha na kukiondoa kichwa chake.Siku zikifuata tukamsikia katibu mkuu mwenye jeuri ambaye kafukuzisha mawaziri wengi kazi sababu ya upigaji wake akaibuka na kuwabeza Zitto na Kafulila kuwaita wala rushwa na kukazia hawa ni tumbili na wana makaratasi ya kufungia maandazi wanajidaia kinga ya bunge watoke nje kama ni wanaume kweli niwaoneshe na kutoa vitisho vingi na kujinasibu yeye ni msafi.Sasa wazee ripoti ipo mezani tunasubiri tuone usafi wenu sasa bwana katibu na AG

Kaka Yangu Anataka Kumuoa Mchumba Wangu, Ameamua Kwelikweli

$
0
0
Ndugu zangu kuna mchumba wangu mpaka sasa tuna mahusiano yenye umri wa miezi 5. 

Kaka yangu wa damu amekomaa kumchukua na kibaya jana kaniwahi kwenda kumtolea mahari(kiukweli kimapato ameniacha gepu sana), ndugu wa binti wamempokea tena vizuri. 

Nikimuuliza mchumba wangu kuna nini tena? Anadai naye hailewi kinachoendelea na ananishauri niwaishe mahari ndani mwezi huu.

Nikimuliza unamtaka nani ? Anadai amechanganyikiwa katika hili swala ila anadai kuwa bado ananipenda.

Ndugu zangu nifanyeje katika hili?

Sina Mahusiano na Sitti Mtemvu- Lundenga

$
0
0
Mkurugenzi wa Lino Agency ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na aliyekuwa mshindi wa kwanza wa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu.

Lundenga amefunguka hayo leo alipokuwa akichata Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa sita mchana mpka saa nane mchana.
Mbali na mahusiano Watu wengi walitaka kujua ni sifa zipi zilizompelekea mrembo Sitti Mtevu kutwaa taji hilo kama si upendeleo kutoka katika kamati na crew inayohusika kuandaa mashindano hayo kwani watu wengi wamekuwa wakisema kuwa mrembo huyo alikuwa hastahili kushinda taji hilo ukilinganisha na warembo wengine ambao walikuwa wakichuana nae,kufuatia hali Ludenga ikabidi aweke wazi sifa tano amabzo zinamfanya mtu kushinda taji la Miss Tanzania kuwa ni lazima awe na sura nzuri, umbo zuri, mvuto, haiba, ufahamu wa kutosha wa mambo mbali mbali.

SITI HANA SIFA YA KUWA MISS TEMEKE
Kutokana na maamuzi ambayo Sitti Mtevu aliamua kujivua taji la Miss Tanzania 2014 hivyo mrembo huyo amejifutia sifa zake zote alizopata katika kusaka taji la Miss Tanzania hivyo si Miss Chang'ombe wala si Miss Temeke tena.
Hashim Lundenga amesema kuwa kitendo cha Sitti kujivua taji hivyo automaticaly amevua mataji yake yote aliyopata katika ngazi ya wilaya mkoa na hata Taifa kama ambavyo ilivyotangazwa.
"Hashim Lundenga: Automatimacally anakuwa amejivua na mataji mengine pia...."
Kufuatia sakata la Mrembo Sitti Mtevu kudanganya UMMA juu ya umri wake na kumgharimu kulivua taji hilo la Miss Tanzania 2014.Ludenga amesema kuwa hali ya udanganyifu wa umri wa warembo hao huwa ni suala la kawaida na lipo kila mwaka ila kwa kuwa huwa wako makini ndiyo maana wangundua hivyo haoni sababu ya yeye na kampuni yake kuwajibika kisa Sitti Mtevu alidanganya umri.
"Hashim Lundenga: sio sahihi, tupo makini na ndio maana tumegundua, fahamu ya kwamba kila mwaka washiriki wengi tu hutudanganya kuhusu umri wao na ndio maana tupo makini...... tuwajibike kwa kosa gani?????"

NIPO TAYARI KUKABIDHI KIJITI KWA MWINGINE
Kufuatia kuzuka kwa kashfa mbalimbali zinazohushisha mashindano ya Miss Tanzania na waandaaji wake mashabiki wa Eatv walitaka kujua kama Mkurugenzi huyo wa Lino Agency Hashim Lundenga yupo tayari kuachia nafasi hiyo ili watu wengine waweze kuendeleza pale wao walipohishia lakini Ludenga aliweka wazi kuwa yeye kama Mkurugenzi yupo tayari kuchagua mtu mwingine ili asimamie nafasi yake lakini si kuwaachia watu wengine kuendesha shindano hilo.
"Hashim Lundenga :Lino International Agency ni Kampuni ya mtu binafsi na inayo Directors wake, hivyo tunaweza kuteua Mkurugenzi mwingine wa kufanya kazi hiyo........"

MISS TANZANIA HAIWEZI KUFUTWA
Kutokana na baadhi ya watu kutooana umuhimu wa uwepo wa mashindano ya Miss Tanzania na kuyahusisha na kumomonyoka kwa maadili hususani kwa warembo wa Tanzania watu wamependekeza mashindano hayo yafutwe kwani yamekuwa hayana tija na hayana haki kwani kumekuwa na upendeleo na udanganyifu na vitendo vya rushwa ambavyo hupelekea wasichana wengi kuvunja utu wao kwa sababu ya kutaka kushinda au kufikia hatua fulani katika mashindano hayo.
"Hashim Lundenga:Sitty bado ni msichana mrembo na ataendelea kuwa mrembo....haya mashindano hayawezi kufutwa kwa sababu wananchi wanaelewa faida zake, wewe usiyejua faida zake, baki hivyo hivyo..."

MISS TANZANIA HAKUNA FAIDA YOYOTE
Hashim Lundenga ameweka wazi kuwa katika mashindano hayo hakuna faida yoyote anayopata zaidi ya yeye mwenyewe kufahamika na kutembea nchi nyingi duniani,watu walitaka kujua kwanini miaka yoye amekuwa aking'ang'ana yeye tu katika kuandaa na kusimamia mashindano hayo na je anafanya kwa masilahi ya nani na hayo ndiyo yalikuwa majibu ya Lundenga
"Hashim Lundenga hakuna faida yeyote, zaidi ya kufahamika, kutembea nchi nyingi duniani, n.k."

KASHFA YA NGONO KWANGU FITINA TU
Hashim Lundenga amekana leo wakati akichat Live na mashabiki wa ukurawa wa EATV kuwa hana kashfa ya kuomba ngono au kuwa lazimisha warembo hao kutoka na yeye kingono ili waweze kushinda au kushiriki mashindano hayo,Ludenga anasema hizo ni fitina tu za watu fulani wenye lengo la kumchafua na kuchafua mashindano hayo.
"Hashim Lundenga hakuna kashfa kama hiyo..........hiyo ni fitna.............."
Lakini pia Lundenga aliwaambia watanzania kuwa kutokana na Sitti kujivua taji na kumpa nafasi mshindi wa pili kuchukua taji hilo hivyo wasitegemee tena sherehe za kumkabidhi taji hilo Miss Tanzania namba mbili kwani shehere watafanya wazazi wake pamoja na wakala wake wa mkoa alipotokea
"Hashim Lundenga hakuna sherehe yeyote, sherehe huandaliwa na wazazi wake na wakala wake wa mkoa alipotokea"
Hashim Lundenga alimaliza kwa kusema kuwa tunaoomba radhi sana kwa wale wote ambao hatukuweza kujibu maswali yenu yote kutoka na ufinyu wa muda.

Angalio Video ya Wimbo Mpya wa Diamond-Ntampata Wapi

$
0
0
Alhamisi ya Nov 20 Diamond Platnumz  ameibariki siku hii kwa kuachia video na audio ya wimbo wake mpya unaoitwa Nitampata wapi,kwenye radio station,tv na kwenye mitandao.
Video hii ambayo kwa mara ya kwanza ilianza kuonyeshwa Nov 19 kupitia kituo cha MTV BASE,kama hukufanikiwa kuiona unaweza kuiona kwa kubonyeza play hapo chini.

Maruhani Yamsumbua Penny, Apiga Makelele Barabarani Ovyo

$
0
0
Prizenta wa Kituo cha Radio E-FM cha jijini Dar, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ anadaiwa kukumbwa na mauzauza yaliyodaiwa ni mapepo na kujikuta akipiga makelele barabarani.

Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilidai kwamba, ishu hiyo ilijiri maeneo ya Makongo jijini Dar es Salaam, juzikati wakati staa huyo akielekea msibani ambapo rafiki yake kipenzi aitwaye Skitter alifariki dunia.

Chanzo hicho kilidai kwamba Penny alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kawaida, alipofika maeneo hayo aliegesha gari pembeni na kuanza kupiga kelele akilia kwa uchungu hivyo kuwaacha watu waliomshuhudia wakiwa midomo wazi wakitaka kujua kilichompata mtangazaji huyo. Mpashaji wetu huyo alizidi kueleza kwamba baada ya kama  dakika kumi, Penny aliondoa gari na kuendelea na safari.

Paparazi wetu aliponyetishiwa ishu hiyo alimtafuta Penny na kumuuliza kuhusu tukio hilo ambapo alisema alikuwa akienda kwenye msiba wa rafiki yake, alipokaribia kufika alipata uchungu ndiyo akatokewa na hali hiyo.

Unaweza Kuudownload Wimbo Mpya wa Diamond Uliotoka Leo Hapa

$
0
0
Diamond Ametoa Wimbo Mpya Siku ya leo Unaitwa Ntampata Wapi , Kama Unataka Kudownload basi Hapa ndio Mahala Pake..

Martin Kadinda 'Kama Wameachana Basi Wamechokana Wenyewe Mimi Sio Chanzo cha Kuachana Kwao'

$
0
0
'Oyooooooo...naona now tunaanza kupangiana maisha aiseee... This is my personal page i post about myself and kazi zangu za ushonaji na ubunifu.... Ukiona post about @diamondplatnumz @wemasepetu @officiallulumichael @petitman_wakuache or any other person.. Its because those are my people niko nao mara nyingi ila sio lazima to post anything about them.... So if i post am having sex... Am naked.. Am eating or anything its my page.... GET That.... back to BMW and mahusiano ya hao watu wawili sihusiki na sina taarifa about kuachana kwao... Na kama wameachana watakuwa wamechokana wenyewe.... Mimi niwe chanzo cha kuachana kwao kwakuwa nilikuwa kuwadi wa kuwakutanisha?? Kawa walivyotongozana ndo watakavyoachana.... Tatizo lenu mmekariri maisha na akili za matope kulainika kila mkimwagiwa maji..... Ukijiona ni bingwa wa matusi fungua page yako tukana...... Nasemajeeeeeeee #NdoIshakuwa na mkae mkijua FARASI UMPANDAE AKUTISHI KWA MBIO ZAKE........' Kadinda

Safari Hii Watuhumiwa wa Wizi wa Mabilioni ya Escrow Kuzikwa Bongo Ama Gate of Heaven?

$
0
0
Ni kwa takribani miezi 5 sasa imepita tangu kuibuliwa kwa sakata la ufisadi wa mabilioni ya ESCROW account,kashfa iliyoibuliwa na mbunge wa Kigoma Kusini Davidi Kafulila,kashfa iliyoibua mzozomkubwa bungeni kiasi cha mwanasheria mkuu jaji Fredrick Werema kudaiwa kutoa kauli za kumtishia maisha mh Kafulila ikiwa ni pamoja na kumwita Tumbili,huku akikanusha kwa nguvu zote kwamba fedha hizo za ESCROW zilizotokana na mzozo wa kibiashara kati ya IPTL na TANESCO si za umma bali ni za IPTL na wadau wenzake wa kibiashara.

Sasa kashfa hiyo imeibuka upya na kwa nguvu zote,hasa ikichagizwa na mbinyo wa kibajeti,ambapo nchi wahisani wamegoma kuchangia bajeti yetu ya maendeleo mpaka pale ripoti hiyo itakapowekwa wazi,kinachochangia skendo hiyo kusambaa nchi nzima kama moto wa petrol ni ripoti za mkaguzi na mzibiti mkuu wa serikali na ile ya PCCB ambazo zimekwenda mbali zaidi kwa kutaja kiwango kilichochotwa kwamba ni zaidi y ash Bilioni 320,huku Bohari kuu ya madawa ikiwa haina dawa wala uwezo wa kununua dawa kutokanana kudaiwa zaidi ya bilioni 102

Nikiendelea kukumbuka mwanzoni mwa sakata la EPA, Namkumbuka aliekuwa gavana wa benki kuu Ballali akiumwa gafla na kusafirishwa gafla kwenda nchini Marekani kutibiwa, ambapo hakikupita kipindi kirefu tukatangaziwa kwamba amefariki dunia, ikumbukwe kwamba Ballali ndo aliyekuwa anajua ni nani na nani walichota mabilioni ya EPA; kwa idhini ya nani na kwa matumizi yapi,lakini ndivyo hivyo alikufa na majibu yote hayo ingawa kifo chake kilizua utata mwingi na sintofahamu, huku wakiwepo watu ambao kamwe usingewaambia Ballali amekufa wakakusikia na kukuamini.

Ni mwaka huu mwandishi wa gazeti la mwananchi Meena ndie alietutegulia kitendawili cha wapi alipozikiwa Ballali,pale alipoibuka na story hiyo ya Ballali kwa kututajia mahala alipozikwa ,akituambia kwamba mtanzania mwenzetu huyo Ballali alizikwa nchini Marekani katika eneo maarufu la makaburi nchini humo linaofahamika kama “Gate of Heaven”mwandishi huyo ama kwa kutumwa ama kujituma alienda mbali zaidi kwa kutuonesha mpaka picha za kaburi la Ballali na makaburi mengine,japo alichofeli ni kushindwa kutuwekea walau picha moja ya mwili wa Ballali ukiwa kwenye jeneza.

Kutoka EPA sasa tuna TEGETA ESCROW, yaani msitu mpya, lakini nyani wakiwa walewale,nikiwa kama mtanzania ninaeguswa na kuumizwa na athari za ufisadi na rushwa za aina yeyote kama wizi wa Richmond, EPA, ESCROW, RADA. Ninaliona zengwe lilioko mbele yetu kama taifa, hapa tutarajie kudanganywa sana, tutarajie kuhamishiwa ajenda na mwisho tutarajie propaganda nyingi kutoka serikalini kuliko ukweli. Lakini naomba nimalizie kwa kuwauliza wahusika wakuu na wahusika wadogo wa sakata la wizi wa fedha za umma kwenye account ya ESCROW na serikali kwa ujumla. Kwamba safari hii je, wezi wa pesa zetu watapelekwa mahakamani? Ama wataumwa gafla na kukimbilia kutibiwa ughaibuni kama alivyofanya Balali? Je, watuhumiwa wakijifisha ama kufishwa watazikwa safari hii nyumbani Tanzania ili nami nipande treni kutoka kwetu Kigoma walau niwahi matanga? Ama ni kama kawaida watazikiwa ughaibuni (Marekani)mnijibu kiungwana tafadhari, watazikwa Bongo ama kwenye makaburi ya Gate of Heaven kama Ballali?

Hataki Massage, Romance, Gogo on Bed kwa Ufupi Nimeuziwa Mbuzi Guniani

$
0
0
Nimetoka kuoa kabila moja kubwa kaskazini huko hasara tupu kwa kweli
tulikua kwenye uchumba zaidi ya miaka miwili na nusu aliniambia yeye bado bikra kwahiyo nimvumilie hadi ndoa ndo tuta duu nikamkubalia
kweli tumefunga ndoa miezi sita sasa imepita
sijakuta cha bikra wala birika nimeambulia kopo la kufa mtu , pili gogo hajigusi hata kutoa mguno wa uongo kitandani kama nimenunua s3x dolly vile,
hataki kufanyiwa love play , hataki massage kwa ufupi Nimeula
wenye uzoefu hivi atakuja kubadilika? Wadada wa kichaga ndo mlivyo au ananiigizia?

The All White Party Night 'Tarehe 22/11/2014, Yamoto Band, Fm Academia and Barnaba Watakuwepo at Escape 1

$
0
0

Tickets za Jamamosi The All White Party at Escape One sasa zinapatikana qt:- 1. Samaki Samaki Mliman City 2. Clouds FM Mikochen 3. Samaki Samaki at Samora Avenue and 4. City Sports Lounge jengo la Azania Bank karibu na sanamu. Kiingilio 10,000 na VIP 20,000 .....!

Wazazi wa Miss Tanzania Mpya Wacharuka..Wahoji Zawadi za Mtoto wao Zipo Wapi

$
0
0
 Wazazi wa Miss Tanzania mpya, Lilian Kamazima wameitaka Kamati ya Miss Tanzania  iwape maelezo ya uhakika kuhusu zawadi na taji la binti yao kwa kuwa hadi sasa wako njiapanda.

Kauli hiyo ya  Eva na Deus Kamazima imekuja siku chache baada ya mrembo huyo kuwasili jijini Arusha akitokea Dar es Salaam.

Wakizungumza nyumbani kwao, Majengo Juu jijini Arusha jana, wazazi hao walionyeshwa kushangazwa na hatua ya kumpokea binti yao akiwa hana taji, pamoja na fedha ambazo alistahili kupatiwa kama mshindi.

Walisema kuwa walimpokea binti yao kama ‘yatima’, hata tiketi ya ndege alilazimika kulipiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwandago Investment Ltd, aliyemuibua katika ngazi ya Kanda ya Kaskazini.

“Tunaiomba Kamati ya Miss Tanzania itupe maelezo ya kina kuhusu zawadi, taji pamoja na vitu vingine kwa kuwa tumempokea binti yetu kama bila zawadi wala taji,” walieleza wazazi hao kwa nyakati tofauti.

Awali, mrembo huyo alisema kuwa pamoja na kwamba bado hajakabidhiwa taji wala zawadi yoyote na Kamati ya Miss Tanzania, lakini kitendo cha kupewa kiti hicho ameridhika.

“Sijapewa taji wala zawadi , lakini kitendo cha kupewa kiti cha umalkia nimeridhika,” alisema  Lilian.

Mkurugenzi wa  Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga alipoulizwa kuhusu madai hayo alisema kuwa ni kweli bado hawajamkabidhi fedha na zawadi  kwa kuwa kuna taratibu za kiofisi bado zinafanyika.

“Ni kweli, tulimwambia atuachie akaunti yake kwa kuwa kuna taratibu zinafanyika, tutamwekea pesa na kuhusu zawadi huyo alirithi taji, hakuwa mshindi wa kwanza, lazima mwelewe,” alisema Lundega.

Baada ya Shy-Rose Bhanji Kudaiwa Kumpiga Mbunge Mwenzake, Hiki Kimesemwa ungeni

$
0
0
Kumekuwa na taarifa kuhusu kuwepo migogoro mbalimbali inayohusisha Wabunge wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki ambapo Mbunge Shy-Rose Bhanji amehusishwa sana kwenye vichwa vya habari.
Kwenye kikao cha Bunge November 20 2014 Dodoma Hatibu ambae ni mbunge wa Zanzibar aliuliza 
 “… Sisi wabunge wa bunge hili ndiyo wapiga kura wa kuwachagua wawakilishi wetu wa kutuwakilisha katika bunge la Afrika Mashariki, kumekuwa na taarifa za kulipaka Taifa hili matope kulitia aibu kutokana na  baadhi ya wawakilishi wetu, Wabunge wetu wa Afrika Mashariki kutokana na matendo wanayoyafanya kule..”

“…Ni lini hasa kinachoendelea pale na hatua gani zilizochukuliwa kuhusu ukosefu wa nidhamu uliojitokeza kwa mbunge Shyrose Banji wazi wazi na bili hali hakuna taarifa yoyote, Mheshimiwa Naibu Spika naomba mwongozo wako…”– Hatibu.

Baada ya swali waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akawasha kipaza sauti na kutoa haya majibu “…Naomba nitoe taarifa kwamba kinachotokea katika Bunge la Afrika Mashariki kwa kiasi kikubwa kinahusu mgogoro wa  spika mwenyewe, hilo ndiyo chanzo cha matatizo mengi, kwa hiyo  wabunge  wa Bunge la  Afrika Mashariki wamegawika kataka makundi mawili, kuna kundi linalotaka Spika lazma aondolewe, na wengine wanadai wanamtetea abaki…”

Sasa katika kundi ambalo wanataka  abaki imeonekana Tanzania ndio kikwazo, kwa sababu ili upate uamuzi ndani la Bunge la Afrika Mashariki  katika suala lolote lazima upate akidi inayotosheleza kutoka  kila nchi, sasa wabunge wa Tanzania ambao mwanzoni waliunga mkono hoja ya kumuondoa yule Spika wamefuta hilo na wamekubaliana aendelee kwa hiyo imeleta chuku kiasi Fulani…“– Sitta.

 “…Katika tukio ambalo limetokea juzi na nasema hivi kwa sababu  Naibu Waziri wangu yuko kule kwa hiyo ni jambo halisi, kilichotokea sio kama kinavyoelezwa Mheshimiwa Shyrose Banji ambaye anahesabika ni mfuasi mkubwa wa Yule Spika kiasi kwamba wenzie wanamuona kama kibaraka vile, alikuwa anapita katikati ya Wabunge wengine kuwahi usafiri kwa bahati mbaya akamgonga Mheshimiwa Ndelakindo Kessy, Mheshimiwa Ndelakindo akahamaki na kwa kusaidiwa na  baadhi ya Wabunge  wengine wa Uganda akaenda kituo cha Polisi kutoa taarifa kwa madai kwamba amefanyiwa makosa ya jinai wanaita ‘assaults’…“– Sitta.

Penny Ataja Mahari Yake Kwa Mtu Atakae Taka Kumuoa

$
0
0
Jina la Penny limo katika orodha ya mastaa waliowahi kuwa na uhusiano na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. Jina lake kamili ni Penniel Mwingilwa. Huyu ni Mtangazaji wa Radio Efm ya jijini Dar.


Wiki hii yuko hapa kujibu maswali ambayo waandishi wetu Imelda Mtema na Hamida Hassan walimuweka mtu kati.Ijumaa: Mambo Penny, naona sasa hivi una gari nyingine, ile Toyota Brevis ambayo mpenzi wako wa zamani Diamond alikununulia iko wapi?

Penny: (Kicheko)...kwa kweli namshukuru kwa kuninunulia ile gari ila sasa hivi siko nayo, nimeamua kubadilisha, si unajua mtu lazima uende na wakati?
Ijumaa: Mara ya mwisho kupanda daladala ilikuwa lini?

Penny: Nakumbuka ilikuwa mwaka 2008. Nilipoanza tu kazi ya utangazaji, nilipopanda daladala watu walikuwa wananishangaa sana nikaona hiyo siyo poa, nikawa napanda teksi.

Ijumaa: Ulikuwa na Diamond mkaachana, hebu tuambie kwenye maisha yako ungependa umpate mwanaume wa aina gani?Penny: Kwanza awe mchamungu, pili anithamini lakini pia awe mtu muelewa. Yaani ajue ni wakati gani wa kufanya maamuzi sahihi na awe tayari kunisikiliza.

Ijumaa: Nini ambacho kinakukwaza sana na hukipendi kabisa?
Penny: Ni watu kuniongelea tena kwa mambo ambayo hawayajui kuhusu mimi. Nakerwa sana na wanaofanya hivyo.Ijumaa: Ukiwa katika ‘stress’ au mtu kakukwza na kukukosesha amani, kipi ambacho huwa unakifanya kurudisha amani yako?

Penny: Nikiwa katika hali hiyo breki ya kwanza ni kanisani. Pale kwenye Kanisa la St. Joseph pembeni kuna kakanisa kadogo.Kwa hiyo nakwenda pale, nasoma Biblia na kusali kwa muda wa saa sita hivi kisha nikiondoka hapo nakuwa sawa.

Ijumaa: Muda wa kuolewa ukifika na mwanaume akaja kwenu na ukatakiwa utamke mwenyewe mahari yako, ungetaka mahari ya shilingi ngapi?Penny: Sina makuu, nitamtaka mwanaume huyo ampe baba yangu juzuu na msahafu halafu mama yangu apewe Biblia. Kama kutakuwa na pesa kidogo tutaipeleka kwa watoto yatima.

Ijumaa: Mastaa wengi wa kike wanadaiwa kutojua kupika, wewe hili likoje kwako?
Penny: Kitu ambacho nitamshukuru mama yangu siku zote ni kunifundisha kupika. Najua kupika vitu vingi sana tena vinakuwa vitamu mno, kasoro ugali ndiyo unanishinda ila najitahidi kujifunza.

Ijumaa: Umeanza kujitegemea ukiwa na umri mdogo, vipi unajilindaje na vishawishi vya wanaume?
Penny: Wakati naanza kupanga tulikaa kama familia, tukajadili ikaonekana naweza kukaa peke yangu japo bado nipo chini ya wazazi wangu. Kuhusu vishawishi havinisumbui kwani najitambua.

Ijumaa: Kilichowasukuma mkaamua kupatana na Wema Sepetu ni kipi?
Penny: Sisi ni watu wazima, tuliona haileti picha nzuri kuwa maadui. Sasa hivi tuko na amani na hatutaruhusu watu watugombanishe tena.

Ijumaa: Ni kwa nini unapenda kuvaa nguo fupi?
Penny: Vimini siwezi kuacha ndugu yangu kwa sababu nina mguu mzuri wa kuvaa hivyo, au wewe unanionaje?

GPL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images