Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Diamond lawamani Mombasa, adaiwa kuwafukuza Nyota Ndogo na wasanii wengine kwenye VIP Lounge

$
0
0
Kunyanyashwa kwa wasanii wa Kenya, kumemfanya Diamond na waandaji wa show yake ya Mombasa weekend iliyopita kutupiwa lawama na wapenzi wa muziki nchini humo.

Mtandao wa Standard Media wa Kenya, umeandika kuwa kwenye show hiyo iliyohudhuriwa na watu kibao, Diamond alitaka wasanii wengine wote waliokuwa watumbuize kwenye show hiyo na waliokuwa wamepangiwa kukaa naye kwenye VIP lounge, wakiwemo Susumila na Nyota Ndogo waondelewe.

Ilidaiwa pia kuwa Susumila na Nyota Ndogo walinyimwa maji ya kunywa na kwamba waliambiwa wanywe maji ya bomba kwakuwa maji ya kwenye chupa yalikuwa kwaajili ya Diamond peke yake.

Tukio hilo liliwafanya wasanii wa Mombasa waungane kuwalaani waandaji wa show hiyo ambapo VJ Delph alikataa kucheza muziki.

“Kama hili likiendelea, wapenzi wa muziki wa Mombasa watagomea show za Diamond mbeleni. Ni fedheha kwa wasanii wetu kutendewa hivyo nyumbani,” alisema Hassan Faisal wa Coastal Films.

From The Source:

 The embarrassing treatment of Kenyan artistes has Tanzanian singer Diamond and an event’s organiser receiving backlash from music lovers. During a concert held in Mombasa over the weekend in which Diamond was the showstopper, the star demanded that all other artistes who had reservations in the VIP lounge, among them Susumila and Nyota Ndogo, be moved away. There was more drama after Susumila and Nyota Ndogo were denied drinking water. They were told to look for tap water as the bottled water was only for Diamond and his crew. The act saw Mombasa artistes unite to condemn the event organiser with VJ Delph declining to deejay. 

Meseji ya Kwanza Kutoka Kwa Miss Tanzania Happiness Kwenda kwa Watanzania Wote Baada ya Shindano Hilo Kwisha Hapo Jana

$
0
0
Baada ya Miss South Africa anajulikana kwa jina la  Rolene Strauss ambaye ndie mshindi wa taji la  Miss World 2014, Aliyekuwa akiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram amefunguka baada ya kushindwa kunyakua taji hilo na hichi ndicho alichokiandika:

Nampongeza @rolenestrauss (South Africa) kwa kuibuka mshindi Miss World 2014.Watanzania wenzangu na marafiki kutoka mataifa mengine, tumepiga kura sana, mmeonyesha support kubwa kuliko matarajio ya wengi bahati mbaya kura hazikutosha. 
Natumia nafasi hii kuwashukuru wote mmoja mmoja kwa kuniunga mkono kwa kipindi chote ambacho nilikua hapa jijini #London na tokea niliposhinda mashindano ya #MissTanzania. Nisingefika hapa bila support yako. From deep inside my heart. I thank you.
Kuanzia aliyetumia muda na pesa yake kunipigia kura, aliyeandika na kutangaza habari yangu, designers mbalimbali, familia yangu, marafiki wote, wote, wote, I thank you. 
Nimejifunza vitu vingi sana kipindi chote hiki na kwakweli watanzania tumeonyesha umoja wa hali ya juu sana. Umoja wetu na udumu katika mambo yote ya kimaendeleo kwa taifa letu.
Mbarikiwe
#Happiness4MissWorld

Rolene Strauss mwenye umri wa miaka 22 akiwa ni mwanafunzi wa chuo cha  udaktari katika chuo kikuu cha Free State (University of Free State) Rolene alifuatiwa na mshindi wa pili amabye jina lake ni Miss Hungary Edina Kulcsar.

Nguvu ya Diamond inavyozidi kuongezeka Afrika na Kuwaacha Mbali Magwiji wa Musiki Africa

$
0
0
Muda uliopita ulikua ukizungumzia Wasanii wenye nguvu na waliofanikiwa kuupenyeza muziki wao kwenye nchi mbalimbali za Afrika ni lazima Wanigeria wataitawala hiyo list kama Iyanya, Davido, Wizkid, P Square na wengine ila sasa Diamond anazidi kuipa Tanzania headlines
Video mpya ya staa wa Afrika Iyanya ya Mr. Oreo iliyotajwa na kituo cha TV cha TRACE Urban kama hit iliwekwa kwenye mtandao wa YouTube September 2014 ambapo mpaka December 15 ilikua imetazamwa zaidi ya mara milioni moja na elfu 80, huku Shekini ya P Square iliyowekwa November 20 kabla ya Diamond, ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni moja laki moja lakini ya Diamond ambayo imewekwa November 20 2014 imetazamwa zaidi ya mara milioni moja na laki mbili.
Support ya Tanzania kwenye huu mwamko mpya wa kusupport vya nyumbani imechangia haya kwa kiasi kikubwa sana mpaka kumwezesha Diamond kushinda tuzo 3 za Channel O 2014, ushindi ambao ulifanya Wanigeria na wasanii wengine wa Afrika kujiuliza Diamond ni nani? kuanzia hapa ndio ikawa greenlight kwa Diamond.

Sasa hivi ni miongoni mwa mastaa wa Afrika wanaopata nafasi ya nyimbo zao kuchezwa sana kwenye TV mbalimbali za Afrika na hata kuwa kwenye level moja na mastaa wengine wakiwemo wa Nigeria ambao wametawala kwa kiasi kikubwa sana muziki wa Afrika.
Saa chache baada ya Diamond kushinda tuzo za Channel O millardayo.com ilishuhudia jinsi Wasanii wa Nigeria na nchi nyingine za South Africa walivyokua wanamfata Diamond hotelini kwake na kuzungumza kuhusu kufanya kolabo, yani ni stori iliyogeuka manake zamani Diamond ndio alikua anahangaika kuwapata ili awashirikishe lakini sasa wao ndio wanamkimbilia yeye.

Home » Ent. » Nguvu ya Diamond inavyozidi kuongezeka Afrika na kuziacha kwenda sambamba na zilizotangulia.

Nguvu ya Diamond inavyozidi kuongezeka Afrika na kuziacha kwenda sambamba na zilizotangulia.
Posted by: Millard Ayo December 15, 2014 Ent., videos
Iyanya OreoMuda uliopita ulikua ukizungumzia Wasanii wenye nguvu na waliofanikiwa kuupenyeza muziki wao kwenye nchi mbalimbali za Afrika ni lazima Wanigeria wataitawala hiyo list kama Iyanya, Davido, Wizkid, P Square na wengine ila sasa Diamond anazidi kuipa Tanzania headlines
Video mpya ya staa wa Afrika Iyanya ya Mr. Oreo iliyotajwa na kituo cha TV cha TRACE Urban kama hit iliwekwa kwenye mtandao wa YouTube September 2014 ambapo mpaka December 15 ilikua imetazamwa zaidi ya mara milioni moja na elfu 80, huku Shekini ya P Square iliyowekwa November 20 kabla ya Diamond, ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni moja laki moja lakini ya Diamond ambayo imewekwa November 20 2014 imetazamwa zaidi ya mara milioni moja na laki mbili.
Support ya Tanzania kwenye huu mwamko mpya wa kusupport vya nyumbani imechangia haya kwa kiasi kikubwa sana mpaka kumwezesha Diamond kushinda tuzo 3 za Channel O 2014, ushindi ambao ulifanya Wanigeria na wasanii wengine wa Afrika kujiuliza Diamond ni nani? kuanzia hapa ndio ikawa greenlight kwa Diamond.
Diamond 2014Sasa hivi ni miongoni mwa mastaa wa Afrika wanaopata nafasi ya nyimbo zao kuchezwa sana kwenye TV mbalimbali za Afrika na hata kuwa kwenye level moja na mastaa wengine wakiwemo wa Nigeria ambao wametawala kwa kiasi kikubwa sana muziki wa Afrika.
Saa chache baada ya Diamond kushinda tuzo za Channel O millardayo.com ilishuhudia jinsi Wasanii wa Nigeria na nchi nyingine za South Africa walivyokua wanamfata Diamond hotelini kwake na kuzungumza kuhusu kufanya kolabo, yani ni stori iliyogeuka manake zamani Diamond ndio alikua anahangaika kuwapata ili awashirikishe lakini sasa wao ndio wanamkimbilia yeye.

Video mpya ya Diamond Platnumz ‘nitampata wapi’ ndio video ya kwanza ya msanii wa Tanzania kutazamwa zaidi ya mara milioni moja kwenye mtandao wa YouTube ambapo kwenye interview na AyoTV Diamond alishawahi kusema inabidi Wasanii wengi wa Tanzania wajitokeze na waweke bidii kwenye muziki wao ili Tanzania iwe na wasanii wengi kwenye headlines za Afrika.

Kufungwa Kuna Uma Jamani..Mwigizaji wa Bongo Movies Akilia Baada ya Yanga Kupigwa Bao na Simba

$
0
0
Mwigizaji Mkongwe Katika Tasnia ya Filamu Tanzania Shamsa Ford Akilia Kwa Uchungu Baada ya Timu anayoishabikia ya Yanga Kufungwa Mabao Mawili na Timu ya Simba Jumamosi iliyopita katika uwanja wa Taifa Hapa Dar es Salaam....
Pole Shamsa

Kinachoendelea ktk Matokeo ya Serikali za Mitaa ni Mwanzo wa Mwisho wa CCM au ni Hasira tu za Escrow na Katiba?

$
0
0
Matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa yanayoendelea kutoka, yanaonyesha CCM inaendelea kushindwa vibaya!, huku upinzani ukizidi kuwapokonya mitaa na vijiji!.

Kwa matokeo haya, inawezekana huu ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa CCM?!, au ni hasira tuu ya escrow na ile "bora katiba", hii huu kuwa ni upepo tuu na utapita na hali itatulia hivyo 2015, ni kama kawa?!, CCM ni ushindi wa kishindo?!.

Japo mwisho wa siku, the overall winner atakuwa ni CCM!, lakini kwa chama kilichokuwa kimeshika mitaa 100, kikaingia kwenye uchaguzi na kupoteza mtaa mmoja, kile chama kilichoshinda mitaa 99, na kupoteza mtaa mmoja ndio the losser, na chama kilichokuwa hakina mtaa, lakini sasa kimeshinda mtaa mmoja ndio the winner!.

Japo mpira ni dakika 90, na kutangulia sii kufika, kama ulivyo mwanzo wa ngoma ni lele, na mwanzo wa safari ni hatua!, inawezekana safari sasa ndio imeanza?!, Uchaguzi huu wa serikali za mitaa, mimi nauchukulia kama ni nusu fainali tuu, fainali yenyewe ni October, 2015!, kumbe ni kweli, "you can fool some people for some times, but you can't fool all the people all the times!". Inawezekana hii ya Wana UKAWA, ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa ule ukoloni na ukiritimba wa chama kimoja?, au ni nguvu tuu ya soda kwa hasira za escrow na "bora katiba?!.

Mpaka sasa siamini hiki kinachotokea!, kwa wale watu niliowaita Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!, kumbe hata ignorants, kunawakati wanafika mahali, ignorance yao inawatoka!. This is very surprising!.

kushinda ni kushinda tuu hata kama ni mtaa mmoja!, hii ni sweet victory!.

Na kushindwa ni kushindwa tuu, hata kama ni mtaa mmoja, kunauma!.

The winner takes it all, the looser standing small!.

Hongereni Washinda!, 

Poleni Washindwa!.

Pasco.

(Sina Chama, sina Upande!)

Lulu:Napenda Zaidi Ushauri au Maoni Kuhusu Kazi Zangu Na Sio Mwili Wangu

$
0
0


Mwigizaji  wa filamu, Elizabeth Michael“Lulu”ameyasema haya akiwa “GYM” anafanya mazoezi.

“Hii ni Kwa ndugu,jamaa,marafiki na mashabiki....!
Ningependa zaidi kupokea maoni Au ushauri juu Ya kazi zangu(filamu)nifanye nn,niongeze Nn au nipunguze nn....ushauri wa Mwili WANGU ninaomba mniachie mimi na Doctor pengine....mana tunapoelekea kuna watu mtatupangia mpaka style za kulala vitandani,hamshindwi kusema kwasababu Wewe Kioo cha jamii ukilala chali haipendezi “ Lulu alimaliza.

Wengi walimuunga mkono Lulu kwa kauli  hii wakiwemo waigizaji wengine kama  Batuli. Wewe je unamaoni gani?!!

Mwanamuziki Diamond Aongelea Tuhuma za Kuwafukuza Wanamuziki Wenzake VIP Lounge na Kuwanyima Maji ya Kunywa Huko Mombasa

$
0
0
'Nimesikitishwa Sana na habari zilizoandikwa na moja ya chombo cha habari, kuwa eti nliwanyanyasa wasanii wenzangu Nyota ndogo na Susumila, kwa kuwafukuza kwenye VIP lounge na sijui eti niliwazuia wasitumie maji ya chupa hivi inaingia akilini kweli hii!!!?? Ningependa kutumia nafasi hii kuwajulisha mashabiki zangu waliokutana na story hizo kuwa sio za kweli ni zenye lengo la kudhoofisha Mahusiano yetu mazuri ya wasanii Wa Africa mashariki..kama BigEye ya Uganda ilivyowahi kuandika habari za upotoshaji Kati yangu na Jose Chameleone.. Pia Nawasihi @Bongofive ni vyema mtambue Nafasi yenu kwenye jamii kwa sasa, Kuweni makini na baadhi ya habari mnazo post ama kureport kutoka baadhi ya mitandao, zinavunja mahusiano mazuri ya wasanii wa East Africa...kumbukeni kuna watu wana tabia ya kujudge kitu kwa kusoma kichwa cha habari tu pasipo kufuatilia undani wa habari...Yawezakuwa mwaandika kwa nia njema tu, lakini ni vyema muwe mnapata na uhakika kwanza kabla ya kuripoti, hususan story za kutengeneza chuki kama hizi....kufanya hivyo ndiyo mtasaidia kukuza industry yetu ya East Africa.' Diamond Platnumz

Mtani Jembe Yazua Balaa Yanga..Waamua Kumfukuza Kumtupia Virago Kocha Maximo

$
0
0
Baada ya kuchapwa mabao 2-0 na mahasimu wao wa soka Simba SC katika mchezo wa ‘ Hisani Nani Mtani Jembe’ siku ya Jumamosi iliyopita, klabu ya Yanga SC imeamua kufikia maamuzi magumu ya kumfuta kazi kocha Marcio Maximo na ni wazi Mholanzi, Hans Van De Pluijm atachukua nafasi hiyo. Hii ni mara ya pili kwa Yanga kumfukuza kazi kocha wao mara baada ya kufungwa na Simba. Ikumbukwe mwaka uliopita, Mholanzi, Ernie Brandts aliondoshwa baada ya kufungwa mabao 3-1 katika Mtani Jembe.

Tofauti na ilivyokuwa kwa Brandts ambaye aliifundisha Yanga kwa mwaka mmoja na kuisaidia kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/13, Maximo yeye amefukuzwa baada ya kuiongoza timu hiyo katika michezo tisa ndani ya miezi mitatu. Yanga imepoteza michezo miwili kati ya saba ya ligi kuu msimu huu, Maximo ambaye alianza vizuri klabuni hapo kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii, alipoteza mchezo wa kwanza tu wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Yanga imeshinda michezo minne msimu huu, lakini hadi l,igi inasimama katika raundi ya saba hakuna mtu alikuwa na shaka kuhusu uwezo wa Maximo. Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amechokwa haraka sana na mashabiki, wapenzi, wanachama na viongozi wa klabu yake kutokana na kiwango kidogo cha uchezaji. Mifumo yake ya ufundishaji imekosa mvuto, lakini kitendo cha kufungwa kidhaifu na Simba kimeshindwa kuvumilika.

COUTINHO, JAJA, EMERSON WAMPONZA?
Ndiyo sababu kubwa, ukitoa mbinu zake, Maximo alikuwa akiwakumbatia zaidi wachezaji raia wa Brazil, Andrey Coutinho, Geilson Santos ( ambaye aliomba mwenyewe kuachwa baada ya michezo saba), kwa Emerson Oliveira siwezi kuzungumzia kwa sababu mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo alicheza katika kiwango cha kawaida wakati alipoichezea Yanga kwa mara ya kwanza.

Jaja alifunga mara mbili dhidi ya Azam, ila alikosa makali katika ligi kuu kiasi cha kufunga bao moja tu katika michezo saba ya ligi kuu. Alishindwa kumudu presha ya mashabiki wa Yanga ambao hawakuwa wakipendezwa na kiwango chake huku uchezaji wake wa taratibu ukiwaboa wengi. Maximo aliwanyima nafasi washambuaji kama Said Bahanunzi, Jerry Tegete, Saimon Msuva, Hussein Javu na Hamis Kizza hata pale wachezaji hao wa Kibrazil waliposhindwa kufanya vizuri.

Kuwang’ang’ania wachezaji hao na kuwanyima nafasi wale wenye uwezo kumewakera . Brandts aliondolewa baada ya kufungwa 3-1 licha ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili zaidi, yeye aliondolewa kwa kuwa alipingana na uamuzi wa viongozi kuwasajili baadhi ya wachezaji ambao hakuwataka wakati ule.

Brandts ndiye mwalimu aliyeifanya Yanga kucheza mchezo mzuri wa kupasiana na ndiye aliyeimarisha kiwango cha wachezaji kama, Saimon Msuva, Frank Domayo ( yuko Azam FC kwa sasa), Juma Abdul, Oscar Joshua na wengineo lakini kwa Maximo imekuwa ni tofauti, wachezaji wengi wameshuka viwango na ameshindwa kuwaimarisha wachezaji ambao ‘ wanasua-sua’. Yanga wamefanya uamuzi sahihi kwa kumuondoa Maximo na Coutinho.

Seth 'Jamani Tujifunze Kuwa na Shukrani Kwa Mungu Kwa Kila Jambo' Soma Hii Habari Uone

$
0
0
Una kazi ambayo kila asubuhi unajua Dawati lako lipo na Kiti,Ofisi yako ina AC na kiti cha kuzunguka,Una Laptop ya Ofisi na Fuel allowance kila mwezi,Vocha unawekewa na Ofisi na Simu umepewa kwa ajili ya kukuwezesha ufanye kazi Comfortably..Ukitoka kazini unarudi nyumbani,una uhakika wa kula,una kitanda kizuri,Umelipa Kodi mwaka mzima hudaiwi LAKINI BADO una Guts za Kusema "I HATE MY JOB,NACHOKA SANA"
Mshukuru sana Mungu angalau wewe una hicho kidogo...Unakaa kwenye AC asubuhi mpaka jioni unalalamika,Kuli wa Bandarini anayebeba mizigo kwenye jua kali atasemaje??
Unalalamika Una kazi mbaya just because Unakaa sana kwenye Computer na inakuumiza macho,Umewahi kujaribu kuwaza kuwa Mpiga Debe kwenye Kituo cha basi??Au kuwa Ombaomba mtaa wa Uhuru??Au kuwa Muuza Karanga anayetembea na Kapu bila kujua atapata wateja au Lah???Umewahi kujua how it feels kuwa Mmachinga kutembea Temeke hadi Mwenge unauza Nguo na hujui Mteja wako wa kwanza atakuwa wapi??
BE THANKFUL TO GOD
Angalau wewe una kazi ya kueleweka,Kuna walioGraduate miaka 3 iliyopita na kila Interview wamefeli,wewe ni nani una kazi na yeye hana wakati ukute hata GPA amekuzidi??Una undugu na Mungu akubariki wewe na yule akae miaka 2 bila kazi??
Kabla hujalaani kazi yako,Wafikirie wengine...Acha kuwa Teller ukawe Mpiga Deki wa Vyoo vya Mlimani City kama unadhani kuhesabu hela ni shida mpaka unalaani kazi yako..
Kama unakubaliana na mimi,wote na tuseme, "ASANTE MUNGU KWA BARAKA ZAKO ULIZONIBARIKI" Seth

Idris Sultan 'Sijapanga Kuwa na Mpenzi Wala Swala Hilo Halipo Katika Mipango Yangu Kabisa'

$
0
0
MSHINDI wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Rashid Sultan ameweka wazi kuwa bado hajajipanga kuwa na mpenzi na suala hilo halipo kwenye mipango yake kabisa.

Akizungumza na Global TV Online, Idris alisema sasa hivi akili yake ipo katika kubadilisha maisha ya watu ambao wamebadilisha maisha yake mpaka sasa hivi.

“Sijajipanga na sitaki kujipanga kwa sababu haipo kwenye mipango yangu, huu ni muda wa mimi kufanya kazi hayo yapo na nitayakuta tu,’ alisema Idris

Yanga Yamsajili Hamis Tambwe Na Kumuacha Mbrazil Emerson

$
0
0
YANGA SC imemuacha Mbrazil, Emerson de Oliviera Roque na kumsajili mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mrundi Amisi Tambwe.
Tambwe amesaini usiku huu Mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuachwa na klabu yake, Simba SC aliyoichezea msimu mmoja uliopita akitokea Vital’O ya Burundi.
Yanga SC imeamua kumuacha Mbrazil Emerson baada ya kushindwa kupata Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
Tambwe anaungana na Mliberia, Kpah Sherman, Wanyarwanda Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Mbrazil Andrey Coutinho kukamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni Yanga SC.
Amisi Tambwe kushoto akisaini Mkataba wa Yanga SC pembeni ya Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo, Francis Kifukwe
Wakati dirisha la usajili linafungwa Saa 6:00 usiku leo, Yanga SC imesajili jumla ya wachezaji watatu wapya baada ya kumuacha Emerson, mwingine ni Danny Mrwanda.
Katika kipindi cha msimu mmoja, Tambwe ameichezea Simba SC jumla ya mechi 43 na kuifungia mabao 26.
Maisha yake yalianza kuwa magumu Simba SC baada ya ujio wa kocha Mzambia, Patrick Phiri kuchukua mikoba ya Mcroatia, Zdravko Logarusic

Kuna Siri Gani kati ya Wachaga na Mwisho wa Mwaka?

$
0
0
Umekuwa ni utamaduni wa watu wa kasikazini hususani Wachaga kwenda mapumzikoni kila mwisho wa mwaka
Nimejaribu kufikiria ni kwanini makabila mengine hayana utamaduni huu mzuri kama wachaga?jibu sahihi bado sijapata ila nimejaribu kuhisi labda ni kwa sababu Wachaga wengi wamesoma?
Au mkoa wa Kilimanjaro upo mbali sana kiasi cha wachaga kushindwa kwenda mara kwa mara?
Lakini nimegundua hata Morogoro na Tanga sio mbali lakini Waluguru na Wasambaa hua hawaendi makwao mwisho wa mwaka so umbali na ukaribu kwangu ni vigezo vilivyokosa nguvu.
Nini siri ya Wachaga na utamaduni huu mzuri wa kwenda mapumzikoni mwisho wa mwaka?
Kwa nini makabila mengine wamekuwa wazito kutekeleza swala hili?
Mjadala upo wazi!

Tabora: Basi la kampuni ya Mohamed Trans lapata ajali na kuua watu sita

$
0
0
Watu 6 wamekufa na wengine ambao idadi yao bado haijajulikana wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Mohamed Trans lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Dar es Salaam kupinduka katika eneo la Makomero, mpakani mwa Singida na Tabora.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

Nape Nnauye atoa Tamko Maalum la CCM kuhusiana na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini.

$
0
0
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetaka watendaji wote waliosababisha kuharibika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika baadhi ya maeneo nchini wachukuliwe hatua kali.

Kimesema, watendaji hao wanastahili kuchukuliwa hatua kali kwa sababu kilichotokea ni uzembe wa hali ya juu uliofanyika huku ikifahamika wazi kwamba tukio la uchaguzi huo ni kubwa na muhimu sana kwa taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, kulingana na kosa lililojitokeza kuwa la wazi hakuna haja ya kupoteza fedha na muda kufanya uchunguzi kabla ya kuwachukulia hatua waliohusika.

"Kwa mfano, Mkurugenzi wa Halmashauri ana kila kitu na alijua mapema kuwa uchaguzi utafanyika lini kwa kuwa halikuwa jambo la dharura, inakuwaje anaruhusu karatasi ziende kwenye vituo zikiwa zimechapishwa hovyo au mahali pengine vifaa viwe vicheche?" alihoji Nape na kuongeza "Sasa hapa unahitajika uchunguzi gani tena kubaini aliyevurunda?".

"Mahali pengine zimefika karatasi za kupigia kura jina la mgombea wa CCM nembo ya CUF, au mgombea wa CUF nembo ya CCM! huu ni uzembe wa hali ya juu sana na adhabu yake haistahili kusubiri uchunguzi", alisema Nape.

Akizungumzia matokeo ya awali ya Uchaguzi huo, Nape alisema licha ya vyama vya upinzani kuwa na umri wa miaka 22 sasa, huku vikifanya harakati za kujaribu kuungana katika umoja wanaouita Ukawa, bado CCM imewagaragaraza vibaya.

Nape amesema, katika uchaguzi huo , CCM imepata zaidi ya asilimia 85 ya ushindi kwa nchi nzima, huku Dar es Salaam, ikiwa na asilimia zaidi ya 75 licha ya kwamba Chadema wanao wabunge wawili katika mkoa huo.

"Katika mazingira ya sasa ambayo vyama vya upinzani vina miaka 22, na vinafanya hata harakati za kujaribu kuungana, asilimia 85 si ndogo kwa CCM, na tunaamini huu ni mwanzo mzuri, na hatuoni namna ambavyo asilimia hii itabadilika katika uchaguzi mkuu mwakani, maana uchaguzi huu ni kama kura za maoni", alisema Nape.

"Wanaosema, asilimia ya CCM imeshuka, wajue kwamba tuliposema tunataka mfumo wa vyama vingi maana yake tulitaka ushindani katika demokrasia. Katika demokrasia ya ushindani ni vema kuruhusu vyama vya upinzani vikakua ili ushindani huo uonekane", alisema Nape.

"Hata hivyo inasikitisha kwamba licha ya vyama vya upinzani kuwa na umri wa miakaa 22 sasa, bado havijaweza kujenga imani ya kutosha kwa Watanzania hata kufikia asilimia 40 kuwa vinaweza kuongoza, lazima wapinzania wazidi kujijenga ili Watanzania wawaamini, asilimia hii 14 waliyopata karika uchaguzi huu wa serikali za mitaa bado ni ndogo sana kwa uhai wa miaka zaidi ya 22".

Nape aliwashukuru wananchi nchini kote kwa kuendelea kuiamini CCM, na kuchagua wagombea wake, huku akivipongeza vyama vya upinzani kwa maeneo waliyochaguliwa, akiwataka kuchapa kazi vinginevyo siku za baadaye wananchi watawahukumu kwa kuwatosa.

Kutimuliwa Maximo,Wachezaji Yanga kilio, Wasema Uongozi Umekosea Sana

$
0
0
Mechi ya Mtani Jembe nchini Tanzania, inayozikutanisha timu mbili za jijini Dar es Salaam zenye ushindani wa jadi, za Simba na Yanga imegeuka uwanja wa machinjio kwa makocha wa Yanga kwa mara ya pili mfululizo.
Mechi kama hiyo ilipofanyika mwaka jana, 2013, Yanga ilifungwa magoli 3-1 na kusababisha aliyekuwa kocha wake Ernie Brandts kutimuliwa pamoja na benchi lake la ufundi. Mwaka huu ni zamu ya kocha Marcio Maximo kufungashiwa virago vyake baada ya kunyukwa mabao 2-0 katika mechi ya Mtani Jembe iliyofanyika Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, na huu ukiwa ni mchezo wa nane wa ushindani baada ya michezo saba tu ya ligi kuu ya Vodacom ya nchi hiyo.
KOCHA Maximo ambaye alipokelewa kwa vifijo na nderemo na mashabiki na wanachama wa Yanga mwezi Juni mwaka huu baada ya kutangazwa kuwa kocha mpya wa timu yao, amewaaga rasmi wachezaji wa timu hiyo kwenye mazoezi uwanja wa Sekondari ya Loyola ya jijini Dar es Salaam.
Mazoezi hayo ya Jumanne asubuhi yaligeuka simanzi baada ya Maximo kuwakusanya wachezaji wake na kuwambia kuwa kuanzia hiyo jana hakuwa kocha wa timu hiyo tena na kuwatakia maisha mema ndani ya klabu hiyo ya Jangwani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji wa klabu hiyo walielezea kutoridhishwa na uamuzi wa uongozi wa klabu hiyo kumuacha kocha wao na mshambuliaji Hamis Kiiza kutoka Uganda.
Mmoja wa wachezaji hao alisema "Ni kweli kocha ametuaga asubuhi daa! ndio hivyo tumesikitika lakini hatuna jinsi."

Naye mchezaji mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema "Inaumiza sana jana (juzi) tumefanya nae mazoezi vizuri kabisa tena amechangamka kama kawaida kumbe nyuma kuna mambo yanaendelea, leo asubuhi tumeenda mazoezi kama kawaida tukijua tunafanya mazoezi matokeo yake anasema acheni kila kitu kaeni hapo nataka kuzungumza na nyinyi".
Mchezaji mwingine wa timu hiyo alisema "Hakuna mchezaji kwa kweli aliyependezwa na kitendo cha uongozi, yaani kwenye mazoezi asubuhi ilikuwa kama msiba, 'mood' ya kufanya mazoezi iilisha kabisa, yaani hakuna aliyekuwa na hamu ya kuendelea na mazoezi.
"Tumefanya kidogo mazoezi tukaondoka, ukiangalia ni sawa tumefungwa cha muhimu ilikuwa ni kukaa chini na kuzungumza na kuangalia cha kufanya, kama kuna mapungufu basi yafanyiwe kazi, mimi sijaona haja ya kumfukuza kocha hasa kipindi kama hichi."
Meneja wa timu hiyo Hafidhi Saleh alikiri Maximo kuwaaga wachezaji kabla ya mazoezi ya timu hiyo kwanza akiwapa moyo wajitume kwa kuwa ni wachezaji wazuri na timu ni nzuri na kuwataka kuongeza bidii ili wafike mbali.
"Kwa kweli inasikitisha hakuna mchezaji wala mtu aliyefurahia, kama yupo labda kimoyomoyo ila dah imetuumiza, ni mazoea cha muhimu tugange yajayo hayo mengine tuwaachie viongozi."alisema Saleh
Mchezo wa Mtani Jembe ambao ni wa kujifurahisha na kuongeza utani kati ya timu hizo, umegeuka kuwa kipimo cha ubora wa kocha hata kama kocha huyo anafanya vizuri katika michezo ya ligi kuu. Hadi wakati anafukuzwa, kocha wa Yanga Mbrazil Marcio Maximo, timu yake inashika nafasi ya pili baada ya Mtibwa inayoongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na michezo saba tu iliyochezwa.
Baadhi ya mashabiki wameunga mkono uamuzi wa kumtimua Maximo wakisema timu haikuwa na uwezo wa kupambana na timu pinzani, huku wengine wakipinga uamuzi huo kuwa haukustahili kuhukumu uwezo wa kocha huyo katika mchezo mmoja wa kirafiki na kusahau nafasi inayoshikiliwa na timu katika msimamo wa ligi kuu.

Denti Apiga Picha za Utupu Gesti House, Yadaiwa Aliyempiga Ndio Kazisambaza

$
0
0
Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela
AIBU ilioje! Denti wa chuo kimoja jijini Dar, anayefahamika kwa jina moja la Martha, amepiga picha akiwa mtupu katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Tabata, ambako alikwenda akiwa na nguo za shule, tukio linalodaiwa kutokea hivi karibuni.

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, picha hizo ziliwekwa katika mtandao mmoja wa kijamii makusudi na bwana’ke, anayedaiwa kuwa ndiye aliyempiga kwa ridhaa yake mwenyewe kabla ya kukorofishana.

Inadaiwa kuwa picha hizo ambazo zimekuwa zikisambaa kwa kasi katika blogs karibu zote nchini, hatimaye zilimfikia msichana huyo anayedaiwa kuishi Tabata, ambaye kwa aibu, alimtumia msichana mwingine.

Baada ya Martha kumtumia msichana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Lilian aliyedai kuwa ni dada yake, akimlaumu mmiliki wa mtandao kwa kuzirusha picha za mdogo wake bila kuuliza zilikotoka.
Gazeti hili linayo majibishano yaliyorekodiwa kati ya dada na mmiliki huyo, ambako Lilian alitishia kulipeleka suala hilo katika vyombo vya sheria, tishio ambalo lilikebehiwa.

“Usitutishe, hizi picha kazipiga mwenyewe kwa pozi tofauti, unataka sisi tufanyaje na aliyempiga ni bwana’ke, kwanza huu ni ulimbukeni na tunazisambaza makusudi ili liwe funzo kwa wengine wanaofanya ujinga huu,” alisema mmiliki huyo.

Kutokana na aibu aliyoipata msichana huyo, taarifa kutoka chuoni kwao, zinasema akiwa na hofu ya picha hizo kuwafikia walimu na hivyo kuharibu sifa yake, amekuwa akiwaambia marafiki zake kuwa anafikiria kuhama.

Picha zote Zipo Hapa:Global Publishers

Mwigizaji Chuchu Hans Adaiwa Kumsaliti Ray na Mfanyabiashara..Yeye Acharuka na Kusema Haya

$
0
0
Stori: Laurent Samatta
KIMENUKA! Msanii wa filamu, Chuchu Hans ambaye ni mpenzi wa wa nguli wa filamu Bongo, Vicent Kigosi ‘Ray’, amecharuka ishu ya kumsaliti mpenzi wake huyo na jamaa anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara anayeishi maeneo ya Mbezi Beach Dar.

Chanzo kinasema pamoja na Chuchu kuwa na Ray kwa muda wote, lakini inadaiwa kuwa muda fulani amekuwa akitoka na kwenda Mbezi anapoishi kijana huyo.

Hata hivyo paparazi wetu aliamua kumvutia waya Chuchu na kuzungumza naye ishu hiyo ambapo alidai stori hizo zinasambazwa na watu ambao lengo ni kutaka kumchafua kwa mpenzi wake Ray.

“Watu hawapendi kuniona natoka na Ray na ni hao ndiyo wanaotumia muda mwingi kutaka kutuvuruga. Siwezi kufanya hivi na huyo jamaa sijui wa Mbezi kwanza simfahamu na pili jamii haitanielewa nikifanya hivi,” alisema Chuchu.

Mke Aomba Talaka Kutokana na Mumewe Kuwa na Hamu ya Kufanya Ngono isiyo na Koma

$
0
0
Palikuwa na kituko cha mwaka kilichotukia katika kituo cha polisi bulenga, wakati mwanamke mmoja alipokuwa akiomba poo na huku akimtaka mumewe amsamehe na kumwachilia aende zake kutokana na mumewe kuwa na hamu ya kufanya ngono isiyo na koma.
Ruth Nakyeyune,alikuwa akilia na hanyamazishwi kwa madhila apatayo kutoka kwa mumewe huku akimuomba mumewe mwenye asili ya Nigeria bwana Sultan Ali Baba kwa pamoja ni wakaazi wa Nakuwade Bulenga,karibu na barabara ya Mityana, mwanamke anaomba poo na mwenyekusema basi yatosha na kutaka waachane kila mmoja ashike hamsini zake.

Bi Nakyeyune amesema pia kwamba amekuwa si mvumilivu kwa muda mrefu na asiyejali chochote na hataki kusikia jibu la hapana linapokuja suala la ngono.bibi huyo amesema kwamba pindi anapokuwa hajisikii vizuri na hawezi kufanya ngono,Sultan haelewi juu ya suala hilo,na humnunia.sultani alipoulizwa juu ya kununa kwake alisema kwamba hamuamini mkewe na sababu anazompa hivyo anadai anamdanganya na kumnyima haki yake bure na kusema kuwa huwa hamridhishi,mara zote mwanamke huyoa amekuwa akitafuta sababu na mara moja ameshawahi kumtishia atajiua.
Sultan alimtaka mwanamke huyo amshukuru Muumba wake kwakuwa yeye ni mume mwema asiyekunywa pombe kama wengine wafanyavyo,na kumshangaa mkewe anashindwaje kumridhisha kirahisi?

Na kumuuliza mkewe bi Nyakyeyune kwanini aliwaacha wazazi na jamaa zake kama hakuwa tayari kumridhisha kingono,na kama shangazi zake ndo walomfunda na kumpeleka kwake kwa shughuli za ndoa, vipi hayuko tayari?
Inaelezwa kuwa wake wa awali wa bwana Sultan walimkimbia mwanamume huyo kwa tabia hiyo hiyo ya kutoridhika kingono,lakini baadaye Sultani alimuomba mkewe kusalia nyumbani kwa ajili ya watoto wao ili wawalee lakini mke alikataa ushawishi huo.

Zari Ampokea Diamond Kampala kwa Mbwembwe Nyingi Huku Waandishi wa Habari wakishuhudia Tukio

$
0
0
Diamond Platnumz ametua Kampala jijini Uganda jana tayari kwaajili ya kutumbuiza leo hii kwenye show ya Zari All White Ciroc Party‬ jijini humo. Diamond alipokelewa kwenye uwanja wa ndege na mpenzi wake Zari Ttale aka The Bosslady huku waandishi wa vyomba mbali mbali maarufu wakishuhudia tukio hilo .

Wawili hao wamekutana kwa mara nyingine baada ya hivi karibuni kuwa pamoja kwenye tuzo za Channel O.
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images